Search This Blog

Friday, 20 May 2022

DILI TATA - 2

 







    Simulizi : Dili Tata

    Sehemu Ya Pili (2)



    Kijogobwire alipoondoka tu Sofi akaanza kuleta zengwe ‘Sasa ndio nini kuleta maneno ya kutaka kukwamisha mpango?’CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Wewe, usiniulize maswali ya kipuuzi, kwani huoni kama yule mtu ni mjanja sana?’

    ‘Sasa ulitaka tupate mtu mjinga?’ akauliza kizengwe

    ‘Sio tupate mtu mjinga, ila tulitaka mtu ambaye atatusaidia katika utekaji na si mtu anayejua kila kitu’

    ‘Kwa hiyo ulitaka tupate baunsa tu na sio mtu anayejua mipango?’

    ‘Wewe, ebu naomba tuelewane, au una lako jambo juu ya yule jamaa’ Chan’duu akauliza akiwa amekaza macho

    Neno hili likambabaisha Sofi kwani bwana wake alikuwa amezungumza ukweli. Hapa asipojifanya mjinga huenda akaharibu kila kitu

    Akarudi chini

    ‘Hamna baby, ila mimi nafikiri Kijogobwire ni mtu sahihi kwani anaweza kupanga vitu mwanzo mwisho, wewe muamini na huko mbele naamini hatutajuta kwanini tuko naye’ akasawazisha

    Chan’duu akapunguza hasira ‘Sawa. Ila nitamuamini nusu nusu, ila akileta ujanja.. Tukigeukana..’ hakumalizia kauli yake ya kuonya akanyanyuka na kwenda msalani. Aliporudi akaketi kimya

    Kilichobakia hapo ilikuwa ni kunywa na kula tu

    Wakatoka hapo baa saa saba kwani Chan’duu aling’ang’ania kuangalia mpira uliokuwa ukionyeshwa live katika ligi moja ya ulaya

    Waliporudi nyumbani wakaingia kuoga na kuingia kitandani

    Hiyo ilikuwa yapata saa nane na nusu za usiku sasa. Pamoja na kwamba usiku likuwa umeshasogea na Chan’duu alikuwa kidogo ulevi umeshaanza kumpata baada ya bia kadhaa alizokunywa huko walikokuwa lakini usingizi ulimgomea. Kitu hiki anachotarajia kukifanya ni kipya katika maisha yake na si chepesi hata chembe. Pamoja na kwamba jambo hili analotaka kulifanya linaweza kufanikiwa na liwaweza lisifanikiwe pia lakini uzito wake uko kuanzia mwanzo mpaka mwisho iwe ni katika kukwama au katika kufanikiwa. Linaweza kukwama kwa yeye kuishia pabaya na linaweza kufanikiwa lakini akawa mkimbizi maisha yake yote iwapo kama siri itavuja. Hilo ni la kwanza. Kikubwa ambacho kilikuwa kinamnyima raha zaidi na kuweza kuupoteza usingizi wake ni pale alipokuwa akifikiria hatua ambazo Kijogobwire anapiga tokea alipokutana naye na kumuelezea suala zima la kazi hiyo. Unajua! Unapokutana na mtu anayejua, utajua tu kwamba huyu mtu anajua

    Utajua kwa kumtazama matendo yake yalivyo sahihi na ya haraka katika wakati sahihi na wa haraka

    Bila wivu kijicho ama zengwe inabidi tu akubali kwamba jamaa ni mkali

    Katika huo ukali wake sasa ndipo ilipo kasheshe. Iwapo kama jambo hili likija kubumburuka na wao kuwa watafutwa baada ya tuhuma za kutaka kuteka kuwekwa wazi, mtu huyu aitwaye Kijogobwire katika kuokoa nafsi yake anaweza kupanga mbinu za kutoroka. Na katika hali ya kushangaza hata atapokamatwa unaweza kukuta yeye Chan’duu na mwanamke wake wanaishia pabaya na kijana kudunda mtaani akiwa amepangua tuhuma kama vile ana baba mwanasheria

    Wakati wao watakapokuwa jela kijana ama atakuwa maili nyingi akiokoa nafsi yake au atakuwa mitaani akidunda baada ya kesi kuwadondoshea wahusika wake, ambao hakuna mwingine zaidi yake yeye na Sofi. Mtu huyu ni sawa na jeshi la mtu mmoja na ni mtu hatari kushirikiana naye

    Lakini kali kuliko zote ni kwamba, hana ujanja sasa wa kumtosa na kumchagua mtu mwingine. Pale mwanzo kama angecheza karata zake vizuri ‘atleast’ angefanikiwa lakini sasa ‘no’ hamna namna

    Kama angekuwa mjuzi na mzoefu wa walau dili za kijambazi basi angekuwa na mtandao mpana ambao ungetoa wigo mpana wa uteuzi na hata kuwa na uwezo wa kumzima mtu huyu pale atakapojifanya kidampa wa kutaka kufichua siri, lakini hana mtandao wala wigo

    Akaona mawazo hayo ya kumuumiza na kumkatisha tamaa ayaweke pembeni na kuwaza mambo yenye nafuu. Mambo ya faraja na kuliwaza moyo. Hapo akawaza jinsi siku nyingi alivyokuwa akifanya jitihada ili aweze kupata dili likalomfanya kuukata kimaisha na kuanza kutanua akivaa vizuri na kustarehe atakavyo kama anavyowaona vijawa wenzake wa Magomeni wanavyotanua na magari ya baba zao na mama zao na kwenda viwanja vyote wapendavyo. Alikuwa amechoka kula kwa macho sasa anataka kula kwa matendo na dili hili litamfanikishia hicho. Mwanaume akatabasamu CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dili hili anategemea ndio kitalu chake cha kuvuna na kutanulia. Hapo atatisha kuliko njaa. Akacheka kwa mbali ili Sofi asimshitukie. Lakini pale alipowaza kwamba kuna Sofi upande wake wa kushoto, furaha yake ikayayuka tena ghafla na mawazo hasi kumrejea jumla

    Hivi ni kwa nini tokea mwanzo hajafikiria kuhusu huyu mwanamke wake? Kwa kweli hamuelewi elewi

    Toka amekutana na Kijo pale bar mwanamke wake amekuwa sio yule aliyekuwa hababaishwi wala kupelekeshwa kwa maneno na mwanaume mwengine zaidi yake. Mbele ya yule jamaa, Sofi amekuwa mtu wa hewallwa na hata kuweza kumtingishia kibiriti yeye, kitu ambacho hajawahi kukifanya toka wakutane. Siku zote katika uhusiano wao mwanamke yuko chini, yeye anaamua na kufanya kila kitu, isipokuwa leo tu. Kikubwa ni pale alipokuwa akipima maneno ya mwanamke wake pale anapozungumza mbele ya mtu huyo. Kila kauli aliyokuwa anaitoa, alikuwa akiitoa kwa njia ya sauti laini na ya kubembeleza. Akajiuliza maana ya kitu hicho. Je ni kwasababu anataka kazi ifanyike? Au kuna la ziada? Kufikiri hivyo kukaupeperusha moja kwa moja usingizi uliotaka kuja. Akabaki akigaragara kitandani mara ageuke kushoto mara ageuke kulia. Sasa ana mlima mrefu wa kupanda. Amefikia ukomo wa ujuzi wake. Anaona dalili za kupelekeshwa na kuburuzwa zikianza kujitokeza..

    Katika suala la mawazo na kukosa usingizi hakuwa peke yake

    Upande wa pili pia Sofi uzingizi ulimkimbia

    Chan’duu usingizi ulimruka kutokana na kunyimwa raha na fikira zake, lakini kwa Sofi hali ilikuwa tofauti

    Yeye alikuwa na mengi juu ya suala hili. Mengi yakiegemea katika masuala ya kiuchumi na mengi yakiegamia katika masuala ya kimapenzi

    Msichana alikuwa na mawazo mchanganyiko yaliomnyima usingizi wa haraka, naye kujikuta akigaragara kama vile bwana wake alivyokuwa akifanya

    Kwanza kabisa katika maisha yake hajawahi kutenda kosa la kisheria. Hakumbuki kwamba kuna siku alishawahi kupigana hata na mtu. Achilia mbali kupigana, hata kumtukana mtu ilikuwa ngumu kwake. Alikuwa mpole asiye na matatizo na mtu. Sasa mtu kama yeye kuweza kushiriki kitendo cha kuteka mtu! Sijui hata itakuwaje?

    Hivi wahalifu huwa wanawaza nini? Au huu ni kama mchezo anaouona tu katika filamu?

    Sula la pili, ni lazima ajue ni kipi kitamfikia kama suala hili litakwama? Je atafukuzwa kazi? Au atakamatwa na kupelekwa polisi na kisha mahakamani kama vile anavyoona katika sinema? Hapana, kabla mambo kufika huko, atatoroka na kurudi kijijini kwako mara tu atakapoona anaanza kutiliwa mashaka, kwa hiyo hilo la kukamatwa wala asiwe na wasiwasi nalo

    Suala la tatu, ni zile hisia za kukamata hela nyingi kwa wakati mmoja. Je watadai shilingi ngapi baada ya kumteka mtoto? Mmh, huenda ikawa shilingi milioni tano. Hapo ndipo akili zake zilipogota. Hajawahi kukamata laki nane za pamoja katika maisha yake. Siku aliyokamata laki saba kamili pale alipopokea upatu -aliousotea mwaka mzima- alijihi kutetemeka kiasi cha mtu aliyempatia hela hiyo kumuona bonge la mshamba. Sasa milioni mbili je akiipata itakuwaje? Kwa vile yeye ndie aliyetoa dili, na huwa anasikia kwamba ukitoa dili basi huwa unazidi katika mgao, basi yeye atachukua mbili na wenzake moja na nusu moja na nusu

    Ataifanyia nini hela hii? Atakwenda kijijini kwao na kujenga jumba, atanunua shamba kubwa atalimisha, atanunua na ng’ombe na kumuachia baba yake aendeleze mambo, kisha atarudi mjini na kufungua biashara ya mgahawa

    Akatabasamu kwa kuona atakavyotesa na hela zake akiwa msichana mdogo tu





    Hilo akaliacha

    Akaja katika upande wa nne.

    Chan’duu ni mwanaume wake wa kwanza, lakini hivi, pale alipomtongoza alimkubali kwasababu alimpenda au ilitokana na akili za kitoto na ugeni wa mapenzi? Leo hii amekutana na mtu aliyemfanya mapigo ya moyo wake kwenda mbio na kwa hakika amempenda

    Kule kumfikiria tu mwanaume Kijogobwire akajihisi raha ya hali ya juu sana

    Yalikuwa nimawazo mazuri mno kwake. Akageuka huku akitabasamu ili aendelee na burudani yake ya mawazo

    Akakutana macho kwa macho na Chan’duu aliyekunja uso mawazo yamemjaa tele kichwani

    ‘Unacheka nini’ Chan’duu akauliza akiwa kakaza uso bila kujali kwamba mwanamke wake naye mpaka sasa hajapata usingizi

    ‘Nawaza tukifanikiwa hii dili tutaishi maisha gani! Si utanioa ee?’ akadanganya akiwa ameshituka baada ya kuhisi sasa anaweza kushitukiwa

    ‘Hata mimi nilikuwa na mawazo hayo hayo baby’ naye akaunganisha mchezo huo

    Sofi akaupeleka mkono wake na kumkamata usoni

    ‘Chan’duu naomba nikuulize’

    Jambo hili lilimshangaza mno Chan’duu. Sofi hana kawaida ya kumuita kwa jina lake toka walipokuwa wapenzi. Jina ni baby mpenzi au mume wangu, lakini toka walipokuwa pale bar hii ni mara ya tatu sasa anamuita kwa jina lake tena bila wasiwasi. Hili likazidi kumuonyesha kwamba huenda mwanamke wake sasa anaanza kujiona wako sawa hasa baada ya kutoa dili hili wanalolitegemea. Kumbe hakujua kuwa kuna mabaya zaidi ya hilo alilolifikiria. Ameshapata mpinzani katika suala la penzi lake na anakaribia kuzidiwa ujanja

    ‘Niulize mke wangu’ ikabili kupotezea

    ‘Hivi umeshawahi kushiriki katika tukio kama hili?’ akataka kujua

    ‘La kuteka? Bado. Lakini ujambazi nishawahi kushiriki’ akanyamaza kidogo ‘Na nishawahi hata kuua’ akamalizia kwa kudanganya ili kumtisha CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Nini??’ Sofi akauliza kwa mshituko macho yamemtoka

    ‘Nadhani umenisikia.. Na nataka ujue kuwa, iwapo kama tukigeukana…’ kama kawaida hakumalizia kauli yake akageuka upande wa pili na kusingizia kulala



    Katika hili la mawazo, kulikuwepo na upande wa tatu pia. Nao ni upande wa mwanaume Kijogobwire. Yeye baada ya kukutana na mtu wake aliyekuwa na ahadi naye, alichukua mzigo alioletewa na kukutana na mnunuzi na kuingiza zaidi ya shilingi laki tano. Baada ya kuingiza hela hiyo leo akaiacha ile kawaida yake ya kwenda viwanja kutumia na msichana mpya atakaye mpigia simu -baada ya kukutana naye siku moja kwa bahati tu na kuchukua namba yake- au mmoja kati ya mademu zake anaowafagilia, akarudi nyumbani kuja kulala mawazo yakiwa yamemzonga juu ya kupiga hela nzito ya kumfanya kuhama mji ama ikiwezekana nchi kabisa na kukimbia nchi jirani na kuishi maisha ya raha na starehe huku akifanya shuhuli halali atakazozifungua kutokana na hela atakayoiingiza.

    Hela hizo alizokuwa akiziota kuziingiza si kwamba ilikuwa tayari ana mtego nazo! Ila kilichomtia kiwewe matumaini na matarajio ni hili dili ya kumteka mtoto wa kihindi mwenye baba bilionea asiyejitambua

    Tofauti na wazo la Sofi -na Chan’duu pia kwamba- eti suala la utekaji wa watoto huishia katika filamu au nchi za nje, kwake yeye matukio hayo hata hapa nchini yashawahi kutokea na moja wapo yeye aliwahi kushiriki, japo alikuwa kama kidampa tu. Lakini alipopata mgao aliona kwamba kazi waliyopiga ilikuwa na hela ndefu na ni ya maana

    Pale mwazo watu hawa walipompa hii dili alijua itakuwa ya utekaji wa kitoto, katika mitaa wanayoishi, lakini alipokuja kuambiwa kwamba mtarajiwa ni mtoto wa mtu mwenye mabilioni ya shilingi benki, tena mtoto mdogo anayependwa sana na mama yeke, tena mtu mwenyewe hana uhusiano na vigogo, akajua hapo panaweza kumzalishia si chini ya shilingi za kitanzania milioni hamsini. Si mgeni wa kukamata hela inayofikia milioni moja lakini hajawahi kumiliki milioni tatu kwa pamoja. Siku zote alikuwa akijiambia kwamba hela kuanzia elfu kumi mpaka milioni moja zipo kwa ajili ya matumizi ya kimaisha anasa na starehe tu, ataanza kujakutafuta utajiri rasmi siku atakayo kamata milioni kumi na kuendelea. Sasa nafasi hiyo imejitela yenyewe. Katika watu wale wawili watakao kuwa patna zake hakuna hata mmoja atakaye msumbua. Kama walipanga kumpa robo ya mgao basi wamejidanganya sana, yeye ni mshiriki kamili na atataka mgao kamili, so wakidai fidia ya milioni mia moja na hamsini basi tayari ana milioni zake hamsini kibindoni

    Mwanamume akanyanyuka kitandani na kwenda varandani. Akatoka bia katika friji lake. Akakaa katika sofa. Akaifungua na kuanza kunywa taratibu bila kujali kwamba ni saa kumi za alfajiri

    Akarudisha mawazo yake katika suala la utajiri unaomnyemelea

    Sasa akawa anasoma alama za nyakati. Ghafla tu akijifanya yeye ni mganga wa kienyeji kujua ghaib kabla ya mambo kumkumba. Hapa akajipa moyo kwamba wala haihitajiki ramli kujua kwamba kile kitakachoingia, kwanza kitaishia kupumua benki mpaka vuguvugu likapapoisha na yeye kusonga mbele akujuako.

    Wazo hili akalifikiri mara mbili. Kwani kuna sababu ya kukimbia mji? Ni nani atamuona wakati akifanya matanuzi kama ataamua kukimbilia Kenya? Hakuna. Basi atakomaa na jiji

    Watu wanamjua kwamba yeye ni sharobaro, ana kawaida ya kutembea na magari ya kukodi na kuvaa nguo za bei, hivyo watakapomuona anatanua na gari lake mwenyewe mtaani huku akiwa amenunua nyumba sehemu, hakuna atakaye mshangaa kwani wote wanajua kwamba yeye anakazi nyingi zinazomuingizia pesa lakini matanuzi tu ndio yanamfanya kutokutulia. Hivyo wakati huu watu wakimuona na gari yake mwenyewe na nyumba juu, watajua kuwa ameamua tu sasa kufanya mambo ya maana na wataishia hata kumpongeza

    Mwanaume akatabasamu na kukiri kwamba amejitengenezea nafasi. Amejitengenezea mipango ya kuukata kimaisha bila kuingia hata darasa moja la elimu ya juu

    Hapa akaona kuna kila sababu ya kulipanga jambo hili kwa utulivu sana ili liishie juu kwa juu na lisifike kwenye hadhira na polisi kulishupalia

    Suala la kukamata mshiko likitiki tu, atalazimika kujifanya bize katika kila dili ili watu wamuone jinsi anavyohaha juani kwa minajili ya kuja kula kivulini, na baada ya miezi kadhaa tu ataitoa mijihela benki na kuifanya atakavyo bila watu kutia mushkeli

    Wakati huo wa kuzuga kwa mishemishe za bandia itakuwa sawa na kwenda likizo ya kutafuta posho ya kumkimu wakati hali halisi ni kwamba ana bingo ya maana ikihema mahala fulani paitwapo benk

    Akili yake ikamuunga mkono moja kwa moja juu ya maamuzi atakayoyabeba

    Hakuna ambaye anaweza kulipua bomu alilolitega yeye na kulitegua sawia. Kama ni filamu basi yeye ndie steringi na yeye ndie adui mwenyewe

    Sijui kama kuna busara inamfaa zaidi ya kujifanya mtu wa mishe sana wakati huu, kumbe kiundani kabisa ni kwamba anawaramba watu vichogo

    Mfuko wake hautapwaya daima dumu atakuwa tajiri mtoto popote takapotia kwato..

    Kwa wastani watu watatu hawa kila mmoja alikuwa na mawazo yake na hakuna ambaye alipata usingizi katika siku hii ya kwanza ya kukutana kwao kupanga mipango.



    ………….



    Japo kama Sofi alipata usingizi mara baada ya kusikia adhana ya kwanza ya swala ya alfajiri lakini pale watu walipokuwa wakifanya ibada hiyo ya kiislamu usingizi ulimruka kabisa akabaki macho mawazo yake yakiwa yamerudi upya akiwaza juu ya shilingi milioni kadhaa atakazo zikamata huku pengine akiwa sasa ni mwanamke wa Kijogobwire na si kimada wa Chan’duu

    Mwanamke akanyanyuka kitandani akaisogelea dressingtable yake na kuchukua vifaa vya kwenda kufanyia usafi

    Akaingia maliwatoni akaoga na kurudi ndani kuvaa mawazoni mwake kukiwa na maneno ya Kijo kwamba kazi hii ili ifanikiwe basi ni lazima kapteni atulie kimwili na kiakili. Hivyo, anatakiwa kuwa mtulivu na wa kawaida muda wote wa kutenda suala hili, huku akiigiza kitendo sahihi katika wakati muafaka. Kuigiza tu? Hilo ni jambo dogo sana kwake. Na kutenda vitu katika wakati muafaka pia haliwezi kuwa tatizo kubwaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Japo kama kulikuwa hakujacha sawasawa akaamua kutoka hivyo hivyo na kuelekea kibaruani kwake akimuacha Chan’duu aliyepitiwa na usingizi muda huo akikoroma kama chatu

    Akamuangalia bwana wake kumfananisha na Kijogobwire akaona ni sawa na kufananisha nyani na binaadamu. Akajihisi ghafla akianza kumchukia bwana wake huku akiilani bahati yake. Kijo alikuwepo wapi muda wote huo kabla ya kukutana na mwanaume huyu asiye na mbele wala nyuma? Akajiuliza na kujiona mazonge ya kimapenzi kumkumba

    Akachomoka kuelekea kazini

    Kwa vile alifika kituoni mapema sana tofauti na kawaida yake, akaona asipande gari na kuwahi kwani akionekana anaanza kuwahi sana inaweza kuwapa watu kujiuliza maswali mara tukio litakapo tokea. Akabaki hapo kituoni kama vile kuna mtu anamsubiri akiiacha dalalala hii ikiondoka hii ikija na kupakia abiria. Ilipotimu muda wake wa kawaida akapanda gari na kuelekea Msasani kuanza kazi yake rasmi aliyojipa jana. Kazi ya upelelezi wa kukamilisha mipango na si kazi ya kutumika kama kibarua wa mdosi

    Akaingia kazini na kufanya taratibu zake za kawaida, akamchulua mtoto na kuelekea naye sehemu wanayokodi Taxi na kueleka shule. Aliporudi akaendelea na mambo yake ya kawaida huku kwa siri sana akijaribu kumchokonoa mfanyakazi mwenzake ili apate kujua mengi juu ya bosi wake. Mfanyakazi huyu mama mtu mzima kiasi, ameshafanya kazi katika nyumba hii kwa muda wa miaka kumi na tisa sasa, hivyo familia hii inayomuamini na kuishi nao kama familia yake alikuwa anaijua vizuri sana. Kitu ambacho mama huyu kila siku alikuwa analalamika kwa Sofi ni kule kutokuthaminika kwake na watu hawa aliowaona toka ndio kwanza wanatoka kwao India na wanaanza maisha rasmi mpaka kufikia kuwa matajiri wakubwa

    ‘Usione hivi mdogo wangu mimi nimeanza kufanya kazi katika nyumba hii tokea huyu bwana hata hajawa tajiri mpaka sasa ana mabilioni ya shilingi benki. Nimeanza kufanya kazi hapa tokea nikiwa msichana mpaka sasa nazeeka. Napika nafanya usafi na kila kitu lakini mshahara wangu haupandi, nikiwa na matatizo wahanisaidii na kama unavyoona mama alivyo na mdomo mchafu na baba alivyo na mkono wa birika. Yani nafanya kwa sababu sina jinsi. Sikusoma, nitafanya nini? Kama si kuwa na watoto wanaosoma na kutaka mahitaji ya lazima basi ningelishaacha muda mrefu na kukaa nyumbani tu’ maneno haya mama huyu alikuwa akiyasema muda mwingi katika namna ya kulalamika na kushitaki. Maneno haya aliyoyasema na leo hapa mbele ya Sofi mpekenyuzi, yalimfanya mtu huyu aliyeichoka familia hii siku za kwanza tu za kuanza kazi kwake, kuzidi kuihalalisha mipango yake ya kumteka mtoto wa familia hii ili tu si kudai fidia mzito bali pia kuiadabisha kwa kunyanyasa watu

    Ilipofika mchana, akapigiwa simu na Chan’duu akifahamishwa kwa kifupi tu kwamba watakutana na Kijogobwire katika baa moja iitwayo ‘Sisi kiboko yao’ maeneo ya Mwananyamala kwa Kopa muda wa saa kumi na mbili na nusu kwa ajili ya kupanga rasmi mikakati, hivyo akitoka kazini apitilize tu mpaka mahala hapo alipoelekezwa

    Akafanya taratibu zilizobaki za kikazi na muda wake wa kutoka ulipofika saa kumi na moja akachukua mkoba wake na kuaga na kuelekea Mwananyamala

    Alichelewa kwa muda wa dakika arobaini na tano kutokana na foleni za magari, alifika na kuwakuta wanaume zake -mwanaume wake anayetaka kumpa talaka na mwanaume wake mtarajiwa- wakiwa tayari wanachupa mbili mbili za bia na maongezi yakiendelea.

    Alipofika cha kwanza alikwenda mpaka kwa Chan’duu na kumkumbatia huku akimkisi lakini macho yake yote yakiwa kwa Kijogobwire aliyekuwa akitabasamu. Kitendo hiki pia kilikuwa kufikisha ujumbe kwa mtu mwingine kwa kupitia matendo kwa mtu mwingine, ujumbe uliopokelewa sawia, ukiwa umeeleweka vizuri sana na mwanaume Kj

    ‘Mambo K’ akamsalimia Kijo kwa sauti laini na mapozi tele

    ‘Niko fresh patna, vipi huko mipango iko poa?’ akajibu kikazi zaidi ili asimgutushe Chan’duu kwamba hapa anataka kuibiwa

    ‘Upelelezi wangu uko full na nahisi utalipa maradufu’ akajibu kikazi akiwa na maana nyingine tofauti pia

    ‘Ok. Sasa tunapanga nini?’ Chan’duu akauliza ili mazungumzo yazungumzwe kila mtu atimke kwake ili watu hawa wasije kuzoeana kisha ikawa balaa kwake

    ‘Kwa upande wangu nimepanga mambo vizuri kabisa ninachohitaji ni maelezo kutoka kwa patna ili nijue jinsi ya kuunga mambo haya ili kazi ifanikishe’ akajibu Kijo kwa kujiamini kama vile yeye ndio mwenye kazi

    ‘Sofi tuambie’ ikabidi Chan’duu amtupie mpira mwanamke wake

    ‘Kwanza leo nimeongea kwa muda mrefu kuhusu wale watu na mtu mmoja anayewajua kiundani zaidi ili kupata hakika ya mambo yalivyo. So nimepewa uhakika kwamba hawana uhusiano na mtu yoyote mzito na utajiri wao umekuja kwa kuhangaika sana na kama nilivyosema awali hata polisi wanawaogopa. Hivyo upande huo hakuna tatizo. Upande wa pili ni kwamba saa moja kasoro mimi huwa nampeleka yule mtoto shule kwa kutumia taxi ya kukodi..’

    ‘Taxi maalumu?’ Kijo akataka ufafanuzi

    ‘Hapana. Yule mzee huwa anaacha hela tofauti tofauti ili nipatane kwani anasema ukimzoea mtu atakuwa ana uhakika wa kumlipa hela hiyo hiyo kila siku. Hivyo huwa tunatoka na saa moja kasoro kumi namfikisha shule. Ikifika saa saba napanda daladala nikifika shule huwa nakodi tena taxi na kurudi naye nyumbani. Tukirudi huwa ninamuogesha, anakula, anaenda kulala mpaka saa kumi na moja mama yake anaporudi kazini mimi huwa ninatoka na kurudi nyumbani’ hayo ndio yakawa maelezo ya Sofi. Maeleozo mafupi, mepesi, lakini yenye maana kubwa

    Chan’duu hakuwa na cha kuuliza

    ‘Hamna mizunguko mingine mnayofanya?’ Kijo akauliza

    ‘Kuna baadhi ya siku za Jumamosi au Jumapili huwa tunatoka kifamilia na kwenda bichi au supamarket kufanya manunuzi. Zaidi ya hapo huwa siruhusiwi kutoka nae kwenda popote

    ‘Sasa kama ikibidi hivyo mambo yako hivi.. Kuna maeneo mawili ya kumtekea, moja shule na jingine bichi, lakini hii bichi ni ngumu kwani haujui ratiba zake zikoje. So nafasi pekee iliyobaki ni kumteka hapo shule..’

    ‘Kitu ambacho kitakuwa kugumu’ Chan’duu akadakia

    Wote wakamuangalia



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Kitakuwa kigumu kwanini?’ Sofi akauliza

    ‘Kuweza kuvamia shule na kumteka mtu tunaweza kuuawa’ akajibu kwa uhakika

    Jambo hili Sofi akaliona ni kweli na linaweza kuwa hatari

    ‘Ndio mana mimi nakuona wewe kama imature’ Kijo akamuamia Chan’duu

    ‘Kivipi?’ Chan’duu akauliza akiwa amekaza sura

    ‘Aliyekwambia kama tutavamia eneo nani? Kwani sisi ni majambazi? Majambazi ndio huwa wanavamia lakini sio watekaji’ mwanaume akajibu katika namna ya kumzodoa

    ‘Kwa hiyo tutafanyake?’ akuliza akihisi kudhalilika huku akimuangalia Sofi macho yalivyong’aa kwa kuhisi kuwa Bwana kijogobwire ni bonge la bwana mipango dazani

    Akachukua bia na kuigubia ili kupoza machungu

    ‘Ok mipango iko hivi..’ mwanaume akaanza kutoa darasa la kipi kitafanyika ili kazi ikamilike huku akitumia fursa hiyo kumuonyesha Chan’duu kuwa yeye ni mtoto mdogo sana hapa na kumuonyesha Sofi kwamba yeye ni bonge la mwanaume



    iii

    Jua lilikuwa kali, na kama lilivyo jiji la Dar-es-salaam mihangaiko ya watu ilikuwa ikiendelea kama kawaida kila mtu akikimbizana na siku ili aweze kuwa na maisha mazuri zaidi ya mwingine. Ndoto hii ya kila mkazi wa jiji la Dar ilimfanya Chanduu kuwa wa kwanza kufika mahala pa tukio zaidi hata ya muda aliopangiwa kufanya hivyo na planmaster mwenyewe bwana Kijogobwire.

    Alikuwa amevaa kinadhifu kama afisa fulani wa masoko kutoka kampuni inayosaka jina kwa nguvu zote. Chini four angle nyeusi sawa na suruali yake ya kitambaa iliyokolea pasi ipaswavyo huku juu akiwa na shati jeupe la bei kubwa lililofungashiwa na tai nyeusi iliyomkaa sawasawa. Ilikuwa ni siku ya tatu baada ya mipango kupangwa, kila mmoja kwa wakati wake akifanya kama alivyopangiwa, na kila mmoja akajaribu kwa kila hali kucheza nafasi yake kwa umakini wa hali ya juu

    Muda ulikuwa saa saba kasoro dakika kumi, siku ya Jumatano, maeneo, shule ya Upanga nuser school. Chan’duu akaangalia kushoto na kulia na kuvuka barabara inayotenganisha shule na majumba ya shirika la taifa. Watu walikuwa wako katika shuhuli zao, kila mtu na mambo yake

    Akaangalia kulia na kumuona kwa mbali Sofi akija kwa mguu taratibu kwa ajili ya kumfuata mtoto wa bosi wake ambaye leo atakuwa mtaji wa watu kutajirika

    Akatupa macho upande wa pili na kuiona Taxi bubu moja ikitoka katika moja ya nyumba za hapo mtaani ikiwa kama vile imetoka kuchukua abiria iliyomkosa

    Wakati Taxi hii ilipopiga hatua kadhaa tu akamuona Sofi akiisimamisha Taxi hiyo

    Taxi ilipojitenga mbali na barabara Sofi akaifuata na kuanza kuongea na dereva wa gari hiyo ikiwa kama vile wanapatana kuhusu kumpeleka mahala fulani

    Aliporidhika na alichokiona, akatupa macho upande mwingine. Akamuona dada mmoja aliyevalia dera akiwa ameweka wigi kubwa lililofunika sehemu yote ya kichwa chake na sehemu kubwa ya uso wake. Dada huyu mwembamba alikuwa na kiuno kipana na matako makubwa tofauti na umbile lake. Pamoja na kuvaa dera lakini makalio yake yalionekana vyema na kutokana na alivyopendeza hasa sura yake ya kuvutia wengi wa watu walikuwa wakimsalimia na kujaribu kumsimamisha. Dada huyo ambaye hakujali watu wanavyo msemesha au kumsimamisha alikwenda moja kwa moja mpaka katika mahala fulani palipokuwa na kijana mmoja muuza kioski na kuanza kumuuliza maneno mawili matatu akiwa kama anataka kufahamishwa jambo. Chan’duu aliporidhika kumuona dada huyo akatupa macho katika mlango wa shule na kuwaona watu sasa wakitoka na watoto wao wanaosoma hapo wakiwa wamesharuhusiwa kurudi majumbani baada ya muda wa masomo kwisha

    Akaliona basi la kwanza linalobeba wanafunzi kuwarejesha majumbani likiruhusiwa na walinzi wa getini waliokuwa makini na kila nyendo za wanafunzi na watu zao. Lilipopita akatoka taratibu alipokuwa na kwenda moja kwa moja kwa walinzi wa shule hiyo na kuanza kuwauliza maswali kadhaa kuhusiana na shule hiyo na ubora wake

    Hii haikuwa kazi ya walinzi, wakamuelekeza ofisi zilipo ili akapate maelezo kamili ya jinsi ya kumleta mtoto wake kujiunga na shule hiyo kama anavyotaka, lakini akatoa udhuru kwamba anamsubiri mtu katika mambo ya kiofisi hivyo hatakuwa na muda wa kuingia ndani. Akawaomba wamuelekeze utaratibu wanaojua. Hili la Chanduu ilikuwa ni kuwapoteza malengo walinzi hao ili wasione tukio linalotaka kutokea

    Wakati mazungumzo hayo yakiendelea, kwa jicho pembe, akamuona Sofi akitoka na mwanafunzi wake na kuelekea ilipo Taxi. Alipoifikia taxi na kutaka kuipanda mara yule dada mwenye mvuto na makalio matata akatoka alipokuwa na kuanza kumuita Sofi kwa jina la anti na kuanza kuongea naye katika namna ya kumuuliza jambo.

    Jambo hili likamfanya Chan’duu kutabasamu nafsini mwake akiwa na hakika sasa suala limefikia mahala pazuri

    ‘Asanteni’ akaambia walinzi na kuanza kuondoka huku macho yake yote juu ya dereva, sofi na dada wa wigi

    Chan’du akijua kinachoendelea na kitakachotokea akamuona yule dereva wa taxi akishuka na kuja kumfungulia mtoto mlango.

    Mtoto akapanda.

    Dereva akaingia na kutia gari moto

    ‘Anti fanya twende’ Dereva akamuambia Sofi kwa sauti. Sofi alipotaka kunyanyua mguu, mwanamke aliyevaa dera na wigi akamshika mkono na kumuuliza tena kitu huku akitoa karatasi iliyokuwa na kitu kama ramani. Sofi mawazo yake yote yakawa yako katika kumuelekeza huyo dada kile alichouliza. Mara akaona Taxi ikitoka mahala hapo taratibu kama vile inapaki pembeni kumsubiri. Ghafla gari hiyo ikatoka katika mwendo wa wastani na kisha mwendo kasi na kukomea. Kama vile ameshituka na kugundua kwamba taxi imemkimbia, Sofi akaanza kupiga kelele za kusema ‘Mtoto wa bosi wangu ameibiwa. Mtoto wa bosi wangu ametekwa’. Yule dada aliyekuwa pamoja naye pia akaanza kupiga kelele za kuomba msaada ili watu wamsaidie Sofi kutokana na mkasa huu wa ghafla na mzito uliomtokea. Kitu hiki kikamfanya Sofi kuzidi kupiga kelele. Kelele zilizo wafikia walinzi na watu wa jirani na kuanza kujaa kuja kujua kipi kimetokea. Kwa kadiri watu walivyokuwa wakijaa hapo ndipo Chan’duu alipopata nafasi ya kuchomoka mahala hapo na kutoweka ikifuatiwa na yule dada mvaa dera

    Kila mtu akaongea analojua mwenyewe katika kulizungumzia tukio hili lililotokea na jinsi ya kumsaidia mtu aliyetokewa na jambo hilo

    Dakika kadhaa zilipokatika polisi wakawa wameshafika katika kutaka kujua ni kipi kilichojiri

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ********

    Miaka miwili nyuma wakati Sofi bado yupo kwa mama aliyemtoa kijijini na kuwa na muda kidogo wa uhuru hasa baada ya kumaliza kazi zake za ndani alikuwa amevutiwa sana na sanaa ya uigizaji na akatamani kwa kila namma kuwa msanii

    Magomeni alipokuwa anaishi katika ukumbi mmoja wa ccm kulikuwa na kundi la sanaa. Akaomba ruhusa ya kushiriki mazoezi ili walau siku moja apate kucheza muvi, na kwa vile mtu aliyekuwa akiishi naye alikuwa akimchukulia kama mwanawe akampa ruhusa kwa masharti kwamba ajichunge kwani jiji hili lina mambo na hatavumilia mimba isiyo na mwenyewe. Sharti hili Sofi akalikubali. Akaanza mazoezi na kubahatika kushiriki filamu mbili ambazo hazikuwahi kutoka. Katika kundi hilo Sofi alikuwa muigizaji hodari sana na mwenye kuelewa mara moja. Ndoto za Sofi zilikufa mara tu baada ya kupata kibarua hiki cha kwa mdosi. Lakini pamoja na ndoto kufa kipaji kilibaki kama kilivyo. Leo hii kipaji cha uigizaji cha Sofi kilikuwa katika msitari wa mbele katika kuhakikisha anaucheza mchezo wa kutekwa kwa mtoto katika namna ya kutoshitukiwa labla tu na malaika





    Tokea maaskari walipofika shule baada ya kutaarifiwa tukio hilo mpaka alipofikishwa kituoni ili kutoa maelezo kamili hadi wazazi wa mtoto wanafika, yeye alikuwa anajifanya kuchanganyikiwa kupindukia huku akilia mfululizo na kwa kuonyesha machungu yake kuna wakati akajifanya kuzimia kabisa

    Kila mmoja alimuonea huruma

    Ilipofika saa kumi na moja ikawa mahojiano na polisi yamekwisha na kwa jinsi hali yake ilivyo ikabidi kukodiwa taxi na kurejeshwa nyumbani

    Alipofikishwa nyumbani, kilichotokea hakumsimulia yoyote, na pamoja na kuwa hakukuwa na mtu anayemfuatilia, lakini hata hivyo alijifungia ndani na hakuwasiliana na yoyote

    Na siku ya pili pia hakutoka ndani kwa minajili ya kwenda popote, kikubwa alipiga simu kazini kwake ili kuhoji kama kuna taarifa zozote za kupatikana kwa mtoto. Mfanyakazi mwenzake akamuhabarisha kwa kifupi kwamba mpaka sasa hakuna lolote zaidi ya ndugu wa wadosi kuja kuwapa pole kwa jambo hili lililowakumba na ahadi ya polisi kuwa mtoto atapatika tu. ‘Je kuna jambo lolote polisi walilolipata kuonyesha kwamba huenda wakamkamata dereva aliyetokomea na mtoto’ akataka kujua jibu alilopewa ni kwamba ‘Hapana. Mpaka sasa polisi bado hawajaweza kujua kwa undani kabisa ni nani alifanya hivyo? Kwa madhumuni gani? Na gari aliyotumia namba zake ni zipi? Kwa wastani wengi wa waliokuwepo hakuna ambaye alipata kuisoma gari namba’

    Sofi hapo akachomekea ‘Na kwanini jambo hili halipo katika vyombo vya habari’ jibu likawa kwamba ‘Shule imekubaliana na familia na jeshi la polisi, jambo hili kuwa siri wakati taratibu nyingine zikifuata’ hayo yalitosha kumuonyesha kwamba kila kitu kwa wakati huo bado kiko sawa, kiko upande wao

    Kwa vile Kijogobwire alipanga kusiwepo mawasiliano ya aina yoyote kati ya washirika hawa watatu katika siku mbili za awali za tukio, basi Sofi akaishia kushinda ndani akijifanya kuugulia maumivu ya nafsi huku kumbe akisubiri wakati muafaka kukutana na washirika wenzake na kuanza mchakato rasmi wa kuzisaka shilingi milioni tano zitakazo mfanya kuwa tajiri kijijini kwao

    Siku ya Jumapili akaamka saa moja kamili za asubuhi na kuingia zake maliwatoni kufanya usafi. Alipotoka msalani akaingia chumbani kwake na kulifungua kabati la nguo na kutoa dera akalivaa na kulishushia na mtandio. Alikuwa amevaa katika namna ya heshima na taadhima. Leo ikiwa ni siku ya kwenda kwa waajiri wake kuangalia ni kipi kipya kilichojiri huku akijifanya kujuta kwa kusababisha hali hiyo, kabla ya kwenda kambini kwa washirika wake kupanga mambo. Lakini pamoja na kuvaa hivyo hayo yalikuwa ni mavazi ya juu ya mwili tu kwani ndani ya mavazi hayo alikuwa amevaa kimini kifupi kilichomkaa ipasavyo pamoja na fulana nyepesi iliyomtoa vizuri sana. Lengo la mavazi yake ya ndani ni kwenda kumfanya Kijogobwire achanganyikiwe kwa ajili yake huku hayo akiyafanya ni mavazi ya kushindia katika siku yake ya kwanza kambini. Alipokwisha kuvaa akachukua mkoba wake akaingiza vipodozi na nguo kadhaa kwa ajili ya kuvaa katika siku mbili zijazo atakazo kaa kambini kwa ajili ya kusubiri mambo kutiki. Akajiangalia katika kioo na kujiona yuko sawa. Akafunga mlango wake na kutoka. Akawaaga wananyumba wenzake kwamba hatakuwepo kwa muda wa siku mbili kwani anaenda kwa shangazi yake maeneo ya Mbagala kupumzisha akili. Akafika kituoni na kuchukua gari ielekeayo Msasani. Saa mbili na robo akaingia kwa wadosi. Alipoingia tu kabla hata hajasalimia alitupa macho katika ukuta uliokuwa na picha ya mama mwenye nyumba na mtoto wake aliyetekwa. Akaanza kudondosha machozi. Kitendo cha yeye kutokwa na machozi kiliamsha hisia nzito za waliokuwepo kiasi cha kujikuta nao wakiangua kilio. Kama si baba mwenye nyumba kuwa mkali na kuwataka wote kutokulia kwani mtoto atarudi basi ndani hapo pangelikuwa kama kuna msiba

    Wakati sasa kilio kimeshaisha na ameshasalimiana na waajiri wake Mr na Msr Mazarkhan, akakaa pembeni na mfanyakazi mwenzake ili kuuliza mawili matatu apate kujua kinachoendelea. Ni kama vile siku hii ilikuwa ya bahati kwake kwani akiwa katikati ya upekenyuzi huo mara nyumba ikapata ugeni. Walikuwa ni askari waliokuwa katika upelelezi wa tukio hilo wakiwa wamefika hapo kwa ajili ya kuuliza mambo mawili matatu yatakayo warahisishia upelelezi wao

    Maaskari hawa kwanza walifanya mahojiano na baba wa mtoto katika kutaka kujua ni kipi hasa kinaweza kuwa chimbuko la watekaji kufanya walichofanya

    Kwa vile Sofi alikuwa ni mmoja wa wahusika wa tukio hili naye alishirikishwa katika kikao hiki ili kama kuna lolote la kuulizwa basi apate kuwasaidia askari hawa katika upelelezi wao

    Masikio ya Sofi yalikuwa makini kudaka kila neno huku akili yake ikiwa inajaribu kutafakari matendo anayofanya yasije kumuonyesha kama mtu mwenye hofu na hatimaye kushtukiwa

    ‘Ndugu Mazarkhan, kama ambavyo nilisema mara ya mwisho tulipokutana kwamba ili tufanikiwe kumpata mwanao nilazima kwanza tujue mambo kadhaa kutoka kwako ili tupate kuunga matukio. Kwa hiyo kwanza tunachotaka kufahamu kutoka kwako ni je una maadui wa kibiashara ambao umekwazana nao au hata kuwa wana kijicho juu ya biashara zako?’ akauliza mmoja wa maaskari kwa utulivu huku mwenzake wa upande wa pili akiwa anaandika kila kinachoulizwa na kujibiwa

    ‘Kwa kweli katika biashara ya mimi hakuna kitu kama iyo. Biashara ni muzuri tu na kila mitu napatana na mimi na kila mutu penda mimi kwa ile kitu nafanya na kila kitu iko sawa sawa’ bwana Mazar akajibu kwa lafudhi ya kihindi

    ‘Kwa hiyo katika eneo hilo hakuna tatizo. Je unadhani kwamba kuna mtu yoyote ana ugomvi binafsi na familia yako ikiwemo mkeo na mwanao? Hakuna tatizo lolote katika upende huo?’ likawa swali la pili

    Katika hili Mr Mazar kwanza alimuangalia mkewe ambaye alitingisha kichwa kuonyesha kwamba kwa upande wake hana tatizo na mtu yoyote na kisha akamuangalia mtoto wake wa kiume ambaye naye alitoa ishara kama aliyoitoa mama yake, hapo akapata nguvu ya kujibu

    ‘Kama navyoona kwa pande ya bibi aina tatizo na pande ya toto pia iko sawa kwa kweli hapana adui na mutu katika famili ya mimi’

    ‘Aha!’ afande akasema ‘sasa kama hakuna kitu ambacho kinaweza kusababisha mtu kutenda hili alilolifanya kwako basi kuna kitu kimoja tu ndio kilichosababisha hilo kutokea, lakini kwa sasa hatuwezi kuliweka wazi kwasababu hatuna hakika nalo ila tunakuomba kitu kimoja, kama kuna chcochote kitatokea juu ya suala hili hata kama kitatokea usiku wa manane naomba umfahamishe mmoja kati ya sisi watatu tuliopo hapa. Tutakuachia namba zetu binafsi za simu ili ufanye hivyo. Kama mtu aliyemchukua mwanao atakupigia na kusema lolote basi naomba kwanza uwasiliane na sisi kabla ya kuchua hatua yoyote. Tumeelewana?’

    ‘Ndio bana kuba’

    Kipindi chote kicho cha mahojiano Sofi alikuwa anajiweka katika hali ya huzuni na masikitiko akijua kwamba hapa ndio pale anapotakiwa aigize zaidi katika uhalisia wa mtu anayejutia kilichotokea huku ikiwa anaonyesha dhahiri kwamba kilichotokea kilitokea kwa bahati mbaya, akijua kwamba maaskari hawa pamoja na kwamba maswali yao wanayauliza kwa mzee lakini umakini wao pia uko kwa kila mmoja wakiwa wanajua baadae watachambua katika kupata mbumba na mchele, na ni hapo kama wakati huu asipokuwa makini anapoweza kushitukiwa kabla ya mambo kuiva



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini pia kwake ilikuwa muda huu ni wa kujua ni kipi kinaendelea ili apate kuwafikishia na wenzake waelewe kilichopo na kupanga mambo vizuri zaidi. Hapa yeye ni sawa na mpelelezi katika kambi ya adui huku akiwa anajifanya mwenzao. Yeye hapa ni sawa na Chui mkali kati mwili laini ya Kondoo

    ‘Ok, na kabla hatujaondoka naomba niulize swali la mwisho’ akaendelea kusikiliza mahojiano yaliokuwa yakikaribia kufikia tamati, moyoni akiwa tayari ana majibu ya maswali ambayo aliona huenda akaulizwa yeye baada ya zamu ya Mr Mazar kwisha

    ‘Ndio bana kuba’

    ‘Hakuna mfanyakazi wako yoyote au hata ndugu yako ambaye huwa haridhiki na maamuzi yako au kuwa na donge na wewe?’

    Swali hili lilifanya moyo wa Sofi kukaribia kupasuka kwa mshituko kama si kujikaza kike basi hapa angemwaga mtama hadharani. Akajikaza kutulia ili kusikiliza swali hili jibu lake litatoka lipi

    ‘Bana kuba mimi iko ishi na kila mutu kwa vizuri haina matatizo kila kitu iko muzuri’ ndio jibu lililofuatia

    ‘Ok tunashukuru’ akasema kiongozi wa askari hao lakini kipindi anataka kunyanyuka ili kuaga akasita na kumuangalia Sofi

    ‘Aaa samahani mdogo wangu. Najua kwamba una maumivu makali na unajiona kama mzembe kwa tukio hili kutokea mikononi mwako ila usijali mambo haya hutokea sana’

    Sofi akaitikia kwa kutingisha kichwa

    ‘Vipi hujaweza kukumbuka sura labda ya dereva au hata aina ya rangi ya gari mtoto iliyopotea nayo?’

    ‘Hapana’ akajibu kwa kifupi na kwa sauti ya chini iliyoambatana na sauti ya kutaka kulia

    ‘Ok, basi sisi tunaenda na tunaahidi kurudi muda wowote kama kuna jipya, ila ndio hivyo kama kutakuwa na lolote kwa upande wenu msichelewe kutufahamisha’

    Huo ukawa mwisho wa mahojiano na askari kuondoka

    Baada ya hayo, ilimlazimu kukaa kwa kitambo kidogo ili kuonyesha kwamba hapo amekuja kwa ajili ya kujiunga na familia katika suala hili lililotokea kupitia mikononi mwake kwa bahati mbaya, na alicheza nafasi yake ipaswavyo kwani kila mtu alikuwa anampoza na kumtaka asijali kwani ni mipango ya muumba

    Mtu ambaye alitawaliwa na huzuni na kukataa tamaa kiasi cha kuwa kama mgonjwa ni mama wa mtoto. Alikuwa amekonda na kuwa kama sio yeye mwenye maneno na jeuri kama vile amekatwa ulimi na mikono

    Pamoja na kuona huzuni na hali mbaya aliyokuwa nayo mama huyo wa mtoto, Sofi huruma haikumuingia bali alikuwa akijihisi raha nafsi mwake kila alipokuwa akifikiria matusi mazito -na vibao viwili vitatu alivyowahi kupigwa au kurushiwa vitu huku akidhihakiwa na kutolewa maneno ya kashfa kama vile kuitwa nyani au mniga- aliyokuwa akiyapata kwa mama huyu mara pale anapokawia kufanya kitu. Japo kama kilichopo hakipo kwa ajili ya kulipia kisasi lakini manyanyaso hayo aliyokuwa akiyapata, hapa alijihisi faraja mno kumuona mtu anayejiona kwa rangi na mali zake alivyokuwa mnyonge akitia huruma kwa kila mtu. ‘Leo hii ameuona umuhimu wa kila mmoja ee? Pumbavu zake’ akajisemea mnoyoni ‘Muangalie vile, nyooo’ akaongeza huku moyoni akijuta kwanini hana uwezo wa kumuambia bayana kwamba yeye ndio amefanya hivyo na ikiwezekana hata kumtemea mate.

    Baada ya muda akatoa pendekezo la kubaki hapa, akijua wazi kwamba hawezi kukubali. Na kama vile alivyojua ni hivyo hivyo ndivyo ilivyokuwa. Kwani baba mwenye nyumba alikataa wazo hilo kwa madai kwamba hakuna kazi ya kufanya ‘Kama toto ipo rudi basi na wewe ipo rudi kazini’ ndicho alichoambiwa

    Ilipotimu saa tisa akaaga ili kurudi nyumbani akiahidi kurudi kila mara kuja kuulizia kinachoendelea.

    Akatoka na kuelekea kituo cha daladala na kuchukua usafiri kuelekea Mwananyamala ambako ndipo sasa ilipo kambi ya kukutania na washirika wenzake

    Huko ndiko mahala mwanaume Kj alikopata nyumba ya kuhifadhi teka kabla ya madai kuanza

    Japo kama alikuwa na hakika ya kutokufuatiliwa lakini kila mara alikuwa akigeuka nyuma au hata pembeni kuhakikisha kuwa hakuna askari yoyote aliyeunganisha safari hiyo katika kumfuatilia nyendo zake

    Wakati akiwa katika daladala alikuwa mbali kimawazo akifikiri hili na lile hapa na pale. Kikubwa zaidi kilichokuwa kinayasumbua mawazo yake ni jinsi polisi wanavyoonyesha kuwa makini na kesi hii. Kwa mfano.. Maswali waliyouliza pale yalikuwa yanaonyesha wazi kwamba wanajua sasa kinachoendelea. Kama familia ile ya mdosi ingekuwa na ugomvi na mtu, ingekuwa kesi imeshapata muelekeo wa kuifanya kuwa ngumu kwani wazo la polisi lingekuwa kwamba kuna mtu analipiza kisasi, lakini mdosi kukanusha kwamba hana adui imefanya kesi kuchukua muelekeo wa pili wa kumfanya mtu kukimbia na mtoto, nalo ni lile walilotaka kujua kwamba je familia ina mtu wanayehisi ana kijicho nayo bila sababu za maana?. Jibu kwamba hakuna limewafanya askari wale kuhisi kwamba tayari wameshaanza kupata mwangaza sahihi wa kilichotokea. Na bila kujipa moyo, mwanga huo Sofi alikuwa anaujua. Hakutaka kujidanganya kuwa askari wale walishindwa kusema pale kwasababu hawana uhakika. Walishindwa kuweka hadharani wanachokifahamu kwa sababu tu haukuwa muda muafaka kwao. Ni dhahiri kwamba, hata kama huna mafunzo ya kitelejensia, kuwa mjanja tu inatosha kuhisi kuwa, palipobaki ni nafasi ya mtoto kutekwa kwa ajili ya wazazi kulipishwa fidia ili aachiwe huru. Sofi hakuona sababu ya kujidanganya. Aliliona hili katika uso wa askari aliyekuwa anaongoza mahojiano. Na aliliona hili kwa sikio la tatu alilo nalo. Kuwaza hivyo kukaanza kumnyong’onyesha. Awali alidhani kwamba suala hili litakuwa laini kama unanawa -kama vile wanavyopenda kusema watoto wa mjini- lakini kuona kwamba ghafla tu hata hawajatoa madai ya fidia tayari maaskari wameshajua kinachoendelea, kulimtisha. Akaona jela hiyoo ikimwita. Alikuwa hajawahi kujiuliza kuhusu jela wala kuwaza kuhusu siku moja kufikishwa polisi kwani hakuwa muhalifu. Leo anajihisi milango ya jela ikiwa wazi na manyapara kumsubiri

    ‘Dada inamana husikii au unafanya makusudi?’ akaona mtu akimshika begani kumuambia maneno hayoCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kitendo hiki kilimshitua akabaki akiwa ametumbua macho akimuangalia mwanamke mmoja wa makamo akiwa amesimama pembeni yake akimuangalia kwa hasira

    ‘Sasa utasogea na mimi nikae au utanipisha nipite?’ mwanamke huyo akarudia

    Sofi akashituka kwamba alipotea sana kimawazo kiasi kwamba alikuwa wala hajui alipo

    Kipindi anapanda alikuwa amekuta daladala ilikuwa imekaribia kujaa na akapata kiti kilichokuwa na mtu tayari akiwa dirishani. Hapa alipo mtu aliyekuwa amekaa pembeni yake ameshateremka bila hata yeye kujua, inamaana ameruka au? Hivi ameambiwa mangapi ambayo hakuyasikia? Akasogea pembeni na kumpisha dada wa watu apite. Kama ingelikuwa haendi Mwananyamala mwisho basi alikuwa na hakika angepitishwa kituo. Akaangalia nje kujua yuko wapi

    Akakuta gari ndio kwanza iko Kinondoni





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog