Simulizi : Dili Tata
Sehemu Ya Tatu (3)
Akarudi katika mawazo yakeCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwanza akampima bwana wake kwa kujiuliza ni vipi anaweza kumsaidia iwapo balaa likitokea? Akaona pale msaada hakuna. Akamfikiria mwanaume Kijogobwire. Mtu yule anavyoonekana mzoefu na mipango mingi na kujuana na wengi kama alivyodai mwenyewe, basi kuhusu suala hili kuharibika asiwe na wasiwasi nalo kabisa. Mchezo wote uliotendeka umepangwa na mwanaume Kijo na hata suala la ukusanyaji wa madai pia mwanaume atausimamia yeye na kwa hakika hakuna kitakacho haribika. Hivyo asiwe na shaka ya kwenda jela, na wala hata polisi hatogusa. Kumfikiria Kijogobwire kukamfanya nywele kumsisimka ‘Mwanaume yule mjanja, mzuri kisura na mzuri kimwili, hivi kitandani anakuwaje?’ akajiuliza swali ‘Inakuwa vipi atakapokuwa amekushika vizuri akikupa starehe ya kimwili na kukuliwaza kiakili?’ Mawazo yake yakatoka katika mtazamo wa hatari na kuingia katika mtazamo wa kingono. Akatabasamu kwa mawazo hayo
Kutabasamu kwake kukamfanya kuzidi kuzama katika mawazo hayo. Akajikuta sasa mawazo yake yamempeleka na anajiona yuko katika kitandana na mwanaume huyo akionyeshwa ufundi katika uwanja wa fundi seremala, katika namna ambayo hawajawahi kuhisi kwamba ipo.
‘Anti vipi unageuka nayo?’ akashituka konda akimuuliza swali hilo. Akachungulia dirishani na kujikuta akiwa ameshafika mwisho wa safari akageuka kuangalia katika gari, akaona gari ni nyeupe abiria wote wameshateremka amebabi peke yake na mawazo yake.
Huku akijihisi aibu kama vile konda amejua anachokiwaza, akateremka
Kama kawaida yake tokea lilipotokea tukipo hili, akageuka kwa tahadhari na kwa kujifanya kama vile kuna mtu anamuangalia ili kujipa uhakika kua hakuna anayemfuatilia. Japo alikuwa na uthibitisho kuwa hakuna mwenye kumfatilia lakini alijipa angalizo kwamba ni muhimu kuhahikisha kila tendo lake ili asijejitia katika mkenge kwa uzembe wake
Aliporidhika kwamba hakuna mtu anayefuatilia nyendo zake akarudi mpaka kwa Mama Zakaria mwanzo na
kukodi bodaboda
Ilipo kambi yao ni mtaa wa Bondeni lakini ilibidi azungukie mitaa ya Makumbusho na hata alipofika Bondeni ilimbidi ateremke mtaa wa pili kabla ya hapo. Matendo haya ameyaoa sana katika filamu alizokuwa akiziangalia, leo akaona hana budi kuyaigiza ili kutokuuweka usalama wake shakani
Akakata mtaa huo alioshuka Bodaboda na kupita kichochoro kimoja na kutokea katika nyumba moja iliyokuwa na ukuta wa rangi ya manjano na ukimya wa hali ya juu kana kwamba haina wakazi ndani yake. Nyumba hiyo kwa wakati huo ilikuwa katika ukarabati ambao umekamilika kwa asilimia tisini. Ilikuwa bado matengenezo madogo madogo tu ili kuwa imekamilika rasmi
Badaa ya kufika getini akaangalia kulia na kushoto. Akagonga mlango huku moyo ukimuenda mbio. Kote alikotoka ni mawazo tu yaliokuwa yamemsonga lakini hapa akahisi mapigo ya moyo wake sasa yakianza kwenda kasi na mwili kwa mbali kuanza kumtetemeka. Alikuwa na sababu mbili zilizozalisha hali hiyo. Kwanza kabisa ni kule kutaka kujua kwamba kila kitu kiko sawa. Lakini jambo la pili ambalo ndio kubwa zaidi ni hamu ya kukutana na bwana kijogobwire. Alikuwa anatamani kumuona tena mwanaume huyo mzuri. Kila akiifikiria sura yake, sauti yake na utanashati wake, akajikuta mapigo ya moyo wake yakizidi kushika kasi. Kitu pekee ambacho kilitibua hamu hii ni kule kuona kwamba Chan’duu yupo na hatopata nafasi ya kuweza kukaa na Kijo faragha na kuongea nae kwa kujiachia. Kwa jinsi alivyokuwa anajihisi kulegea kabla hata hajakutana na mwanaume Kj ni dhahiri kwamba leo hii kama angelikamatwa mkono tu angelijikuta kitandani bila kuhoji wala kujitambua. Yaani ingekuwa ni sawa na kidume Kijo kujiokotea dodo lililodondoka mtini
Akagonga mara ya nne kisha akaona kama kuna mtu anamchungulia. Halafu mlango wa geti ukafunguliwa kisha mlango wa kawaida. Aliyefungua mlango alikuwa ni kijana mdogo tu ambaye umri wake hauvuki miaka kumi na nane.
‘Karibu’ kijana akamkaribisha kwa uchangamfu
‘Asante’ akajibu na kupitiliza ndani bila kutaka kuhojiana na kijana huyu aliyekutana naye mara moja tu katika siku ya kupanga mipango na kufahamishwa kwamba huyo ndio mlinzi wa nyumba watakayo hifadhi mzigo wao wenye thamani ya milioni za njuruku
Akapiga hatua tatu na kusimama akitishwa na ukimya uliotawala ndani kwani nyumba ilikuwa shwari kama haina mtu ndani yake
‘Wako uani?’ akauliza akimaanisha Kijo na Chan’duu
‘Ndio, ila yupo braza tu bwana wako ametoka’
‘Ametoka?’ akahoji moyo ukizidi kumdunda. Hii ni nafasi aliyokuwa akiitaka kwa udi na uvumba. Kukutana na Kijo wakiwa wawili tu ndio kitu alichokuwa akikitaka kwani leo atapata nafasi ya kujilengesha kwa mtu huyo na kuangalia bahati yake. Leo ndio siku ya kuunga urafiki rasmi na kupima je huko mbele ataweza kuwa mwanamke wake au anajipa matumaini ya bure tu
‘Amekwenda wapi?’ akataka uhakika
‘Nilisikia anakwenda Tanga’
‘Tanga’ akauliza kwa kushangaa
‘Ndio’
‘Tanga kufanya nini?’ akahoji akiwa anahisi labda dogo amesikia vibaya. ‘Huenda labda amekwenda mtaa wa Tanga pale ilala’ akafikiria
‘Kwa kweli sijui labda umuulize braza mana yeye ndio aliyemuagiza aende’
‘Ok. Kijo yuko na nani?’ akauliza kwa kujichanganya. Alishaambiwa yuko peke yake na anajua kwamba humu ndani kuna watu watatu tu, so ukiacha Chan’duu ambaye hayupo na huyu dogo anayeongea naye inamaana yuko na nani?
Hata yeye akaona kwamba ameuliza swali la kijinga
‘Ok. Sasa usije kwanza huku tunamaongezi kidogo. Sawa?’ akasema ili kusahihisha makosa yake. Alikuwa anajua kwamba kijana huyu kazi yake hapa ndani ni usafi na kumshuhulikia mtoto tu
Akanza kupiga hatua huku mapigo ya moyo wake akiyasikia yanavyodunda huku koo likianza kumkauka na kijasho kikianza kumtoka
Akapitiliza mpaka mabanda ya uani. akaangalia nyuma kama dogo naye anakuja maeneo haya kwa minajili ya kwenda chooni na kuhakikisha kwamba Kijo yupo chumbani. Alipoona yuko peke yake kama alivyokuwa anajua kuwa hakuna mwingine zaidi yake hapo alipo, akalivua dera na kulitia katika mkoba. Akatoa vipodozi na kujipodoa haraka haraka. Akajiweka safi na kujihakikisha binafsi kwamba amependeza na nguo zake ziko sawa. Aliporidhika na muonekano wake wa kirembo, akajipulizia pafyumu, kisha akarudisha vitu katika mkoba na kuweka kila kitu vizuri. Akasimama kama dakika moja hivi ili kutuliza pumzi zilizokuwa zimeanza kumtoka kwa fujo. Alipoona yuko sawa akaogonga mlango katika chumba alichopo KijoCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Pita’ akasikia sauti ikimuambia
Sauti iliyomfanya mwili mzima kumzizima
Akafungua mlango na kuingia
Alipoingia ndani akamuona mwanaume Kijogobwire akiwa anafanya mazoezi ya kupiga push-up
Sofi alipoingia wala Kijo hakuacha alichokuwa anakifanya, akawa anaendelea na mazoezi yake tu
Chini alikuwa amevaa penc juu akiwa tumbo wazi. Alikuwa amewasha feni lililokuwa likilifanya jasho lake lisitoke kwa wingi. Japo kama katika chumba hicho kulikuwa na sofa na kitanda lakini Sofi alijikuta akiwa amesimama bila kukaa akiwa hajui afanye nini. Hakutegemea kukutana na Kijogobwire na kutokupokelewa kwa bashasha. Alikuwa amefikiria akiingia hapa, mwanaume huyo ataonyesha hamu ya kutaka kumkumbatia na kuuliza habari za siku mbili tatu zilizopita huku akionyesha uchangamfu wa hali ya juu. Akawa bado amesimama na mkoba wake mkononi
Kijo alipomaliza kusema hamsini akimaanisha Push-up ya mwisho aliyopiga akanyanyuka na kuanza kujinyoosha
Kifua chake kilivyo kipana kiasi na kilivyokuwa kimeroa jasho kwa mbali kilimfanya Sofi kuzidi kuchanganyikiwa. Mapigo ya moyo yakazidi kumbana na baridi kumshika ghafla
‘Niambie patna’ Kijo akamsalimia huku akimsogelea
‘Po..’ akataka kujibu lakini sauti ikakwama. Akakohoa kidogo kuiweka sawa
‘Poa patna. Mambo?’ akajikaza kujibu huku sauti yake ikiwa ya mbali na iliyojaa udhaifu
Kama kuna kitu ambacho Sofi angekijua basi angeruka kwa furaha na kushangilia ni ukweli kwamba kumbe hata Kijo alikuwa muda mrefu anamsubiri Sofi kwa hamu kubwa sana, hasa katika kipindi hichi ambacho amemuondoa Chan’duu kwa makusudi
Ilivyokuwa ni kwamba, suala la kwenda Tanga ilikuwa ni lake yeye lakini aliona ni bora hata kumtuma mtu asiye mzoefu ili apate nafasi ya kuwa na Sofi peke yake apate kuongea naye mambo mawili. La kwanza, kwa vile Sofi ndio mwenye kazi basi ndio mtu ambaye anatakiwa kumueleza kwanza kwamba kwa vile yeye ni patna kamili basi mgao unatakiwa kuwa mafungu matatu na si kumpa robo ya mgao kama walivyosema awali. Na jambo la pili, alikuwa anataka kuona je anaweza kumtongoza mwanamke huyu kisha huko mbele akaweza kumpindua Chan’duu?. Kijo alikuwa anapenda sana wasichana wa watu kwani alikuwa huru sana kuwafanya atakavyo kitandani kuliko mwanamke wake ambaye ana masharti si haba katika uwanja wa seremela
Hivyo nafasi hii ilikuwa ameamua kuicheza kukamilifu ili akamilishe mambo hayo
Alipoona mwanake huyu anavyobabaika akajua mambo yote hayo mawili yatakuwa mepesi sana kwake hasa ukizingatia ana masaa manne ya kukamilisha zoezi hili
Akamsoghelea Sofi na kumuambia ‘Karibu sana patna. Karibu rasmi kambini. Karibu rasmi katika kuunyemelea utajiri’ kipindi akimuambia hayo alikuwa ameshamsogelea karibu kabisa. Akapeleka uso wake katika uso wa Sofi na kumbusu mdomoni ikiwa kama kumkaribisha, lakini akitumia mitego ya kimapenzi
Busu hili lilimfanya Sofi kuganda kama sanamu akajikuta bado kidogo pumzi zimkate
Kijo akiwa anajua kwamba hapa ameshamaliza kazi na sasa ni yeye tu na taimingi zake, akautoa uso wake katika uso wa Sofi na kumkaribisha kuketi
‘Karibu ukae mpenzi’
‘Asante’ Sofi akajibu akiwa hajielewi
‘Tuna mengi ya kuongea, au sio swety?’ akamuuliza tena kimtego
‘Sana’ sofi akakiri lakini akili yake ikiwa juu ya mwili wa Kijo zaidi ya mipango
‘Subiri kwanza nikakuchukulie kinywaji’ Kijo akasema na bila kusubiri jibu akatoka na kumuacha Sofi akiwa amelegea akionyesha hamu ya kuingia msambweni
Dakika tatu ziliyofuata Kijo akarudi na chupa mbili za bia zilizokwisha funguliwa. Moja akamkabidhi Sofi na moja akaanza kunywa mwenyewe
‘Unajua patna, we mwenyewe unaona shuhuli ninayoifanya. Kwanza vipi umeuonaje mziki wangu?’ akataka kutoa maelezo lakini akaona kwanza aulize swali ili lipate kurahisishia mambo
‘Mh, yani bila wewe hii kazi isingefanyika’ Sofi akakiri ‘unajua kipindi tulipokuwa na hili wazo sisi tulichukulia simpo tu lakini tokea umeanza kupanga mambo ndio mimi nimejua kwamba hili suala linatakiwa umakini mkubwa na kwa kweli uko makini zaidi ya inavyotakiwa. Kwanza ile staili ya kumteka mtoto hakuna ambaye angeliweza kuibuni kati yetu. Hahaha’ hapa kwanza Sofi akacheka ‘unajua mimi kwanza nilipokuona nilidhani mwanamke kweli! Hee ulipendeza kama mwanamke. Alikutengeneza nani?’
‘Mhu, unajua kazi zetu pia zina wanawake wanaozifanya kama wewe, so kama nataka kuwa kama mwanamke kuna dada mmoja huwa anakuja kunitengeneza nakuwa kama vile ulivyoniona. Pale si namuibia mwanaume yoyote?’
‘Sana. Hasa sauti yako. Uliwahi kuwa muigizaji nini?’
‘Hapana, mazoezi tu, si unajua kipindi kingine kuna shuhuli zinatokea unatakiwa umpigie simu mtu kwa sauti ya kike! Nilichukua muda mrefu sana kufanya mazoezi ndio nikaweza kama ulivyoniona’ akamalizia kwa sauti ya kike maneno yafuatayo ‘Mimi naitwa Hanifa mwenyeji wa Zanzibar nataka ulielekeze kwa ndugu zangu..’ sauti hii ilimcheksha Sofi akajikuta akicheka na kucheka. Alikuwa anajihisi furaha na raha ya hali ya juu hapa mbele ya mwanaume aliyeanza kumzuzua roho yake. Katika akili ya Kijo kulikuwa na sauti moja tu iliyokuwa ikimuambia ‘Amekwisha huyu, wewe tu’
‘Na sio hilo tu patna, na kama unavyoona, nimetafuta chimbo hili ambalo hakuna mtu anayeweza kulitilia shaka na nimemuweka mtu wa kutusaidia ambaye hii ni kazi zake na hawezi kubabaika kwa chochote na hatolipwa pesa nyingi. Na kama unavyojua kama tunatumia simu nilazima tutumie laini iliyosajiliwa na ndio mana nikamtuma Chan’duu aende Tanga akanunue laini nne za mitandao tofauti kisha amuombe mtu wa kusajili amsajilie kwa msaada wake hivyo hata laini ikishitukiwa wakati tumeshamaliza mchezo msala utadondokea Tanga na ushahidi utapotea. Na si hivyo tu kuna kazi ya kukusanya pesa ambayo si ndogo na inatakiwa umakini katika kuipata.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hayo yete nitayasimamia mimi, so patna, ninataka mgao uwe sawa kwa sawa. sijui umenielewa?’ baada ya kumchekesha akamalizia alichotaka kusema
‘Hilo halina tatizo hata Chan’duu majuzi kabla hatujaifanya kazi ya kumteka mtoto nilimwambia kwamba huwezi kukubali mgao tuliokwambia. Japo kama alikuwa mbishi lakini naona kwamba ameelewa. Hivi kwani hasa huenda tukapata kama milioni ngapi?’ akataka kujua kwamba je ni ile ile tano aliyodhani yeye au mwanaume huyu wa mipango itakuwa ameshaongeza kidau
‘Tutadai milioni Mia mbili’ mwanaume akajibu kwa uhakika
‘Mili.. mi.. Milio.. Mili..’ Sofi akashindwa kuuliza kutokana na mshituko uliompata
‘Hizo hela atakuwa nazo za kulipa?’ akajikuta akiuliza swali la kipumbavu
‘Aah patna! Bilionea mzima ashindwe kulipa vijisenti kama hivyo?’
Wakati Sofi akiwa bado ameshangaa Kijo akanyanyuka na kumsogelea alipo. Alikuwa ameshamaliza suala la kwanza sasa mwanaume anapiga hatua ya pili
‘Unajua patna! Unaishi na mlugaluga ndio mana hata vitu vidogo kama hivi vinakushitua. Yaani kama hili dili tungekuwa mimi na wewe tu tungepiga hela zaidi ya hiyo na mgao ungekuwa nusu kwa nusu’ akasema huku akiwa amemshika mkono
‘Kweli ee?’ sofi akauliza akiwa amelegea
Kijo akaona hapa amesharahisishiwa kazi
‘Kabisa. Kwanza mtoto mzuri mjanja kama wewe ulitakiwa kuwa na mtu kama mimi’ akamuambia huku akianza kumpapasa
‘Kwani mi mzuri?’ Sofi akauliza akiwa anamuangalia usoni huku macho yamemlegea
‘Kwani hujioni?’
‘Ata, mi nasikia tu watu wananisifia’ akajibu akiwa anazidi kulegea
Kijo akaupeleka mkono wake katika uso na kumvuta karibu ‘Wewe ni mtoto mzuri mjanja na karibuni utakuwa tajiri’ akasema na kumbusu mdomoni
Sofi akajikuta akiwa hana cha kufanya zaidi kulala vizuri
………
Masaa manne yakakatika na watu kufanya walichotaka kufanya kwa kujinafasi wapendavyo. Chanduu aliporudi alimkuta Kijo akiwa yuko uwani akifanya mazoezi
‘Vipi kila kitu kimeenda fresh?’ akamuuliza
‘Kama ulivyopanga. Sofi yuko wapi?’ akauliza akimuangalia usoni
‘Yuko geto amelala’ akajibu akimuangalia usoni moja kwa moja akiwa anajua Chan’duu alichomaanisha
‘Amekuja saa ngapi?’ akauliza tena
‘Muda kidogo. Alipoingia alikuulizia nikamwambia umeenda Tanga akasema anaomba mahala apumzike kwani anajihi kichwa kinamuuma kwani siku mbili hizi hajapata usingizi kwa wasiwasi’
‘Kwa hiyo toka alipokuja amelala tu?’
‘Ndio. Na kwa vile umerudi itakuwa vizuri ukamuamsha tupange kuhusu jinsi ya kuanza kazi’
‘Poa’ akaitikia na kuelekea chumbani bado mawazo yakiwa yamemsonga. Tokea juzi kipindi wako hapa kambini na teka lao, Kijo alimuambia kwamba awasiliane na Sofi kwa ajili ya kumsalimia tu. Leo hii wakati ambapo ilitakiwa Sofi aje, mara ghafla safari ambayo ilikuwa aende Kijo ikabadilika na kutakiwa aende yeye. Kikubwa kilichokuwa kikimtisha ni kwamba, watu hawa watapata muda mrefu wa kuwa pamoja kipindi yeye yupo safari na hilo litasababisha waongee mengi asiyoyajua. Kwanza kabisa alikuwa ana wasiwasi na Sofi kwa kuegemea sana upande wa Kijo zaidi ya upande wake kwani kwanza mapatano yameshapita lakini juzi amebadilika na kutaka Kijo alipwe sawa na wao kitu ambacho sio mapatano ya awali yalivyokuwa. Sawa na ni kweli mwanaume huyu atafanya kazi kubwa kuliko wao, lakini si wamekubaliana na elfu themanini ya advansi amechukua? Lakini la pili lililokuwa linamfanya asitake watu hawa kupata muda wa kuwa peke yao -kitu ambacho kimeshindikana- ni kule kupata muda wa kuweza kubageni bei watakayouza teka lao bila yeye kuchangia. Toka juzi anamuambia Kj kuwa wapange kima lakini mwanaume ameng’ang’ania mpaka awepo Sofi. Kuna nini hapa? Watu wanasema ‘Pesa ni shetani’ sasa kama kauli hiyo ipo na ni ya kweli ni vipi shetani huyo atakaye kuwa upande wa mwanaume Kijogobwire ashindwe kumshawishi Sofi kumgeuka yeye Chan’duu? Au hata kama hakumgeuka, je hawawezi kupanga kumchezea shere? Watu hawa watakapokuwa wawili tu watapanga mipango ya kuweza kumminya katika mgao, kitu ambacho abadani hataki kitokee. Jinsi Kijo alivyo mjanja kuwa na Sofi pekee wakipanga mambo basi Chan’duu itakula kwake.
Wakati huo akiwaza haya alikuwa katika Gari maeneo ya Kihaba akisonga safari ya Tanga. Katika hilo aliapa kwamba atakaporudi Tanga tu atahakikisha anairudisha nafasi aliyopokonywa bila kujua na mwanaume Kijo, nafasi yake ya kuwa yeye ndio kiongozi badala ya mfuasi kama ilivyo sasa. Atakaporejesha nafasi yake basi hatua kwa hatua ataanza kuutawala mchezo mzima na kuhakikisha kila kitu kinaenda kama anavyotaka na si kama anavyotaka mvamizi Kijogobwire
Baada ya hilo sasa likaja suala kubwa zaidi linalomsumbua kichwa mara baada ya kulifikiri. Hilo ni suala la Sofi na Kijo kuonekana kila mmoja kukumkubali mwenzake. Pale alipokuwa akizungumza na Kijo katika namna ya upekenyuzi kujua ni vipi anamchukulia Sofi, majibu ya mwanaume huyo yalimtisha sana, kwani mwanaume hakujivunga kumsifia shemeji yake alivyo mrembo na mwenye mipango inayoongozwa na akili nyingi zenye kufanya kazi haraka, huku akiwa hasiti kuonyesha kwamba anatamani kama vile angelikuwa mtu wake. Upande wa pili nao hakukuwa na nafuu kwani Sofi alipokuwa akimzungumzia mwanaume Kijogobwire, alikuwa anamzungumzia kama vile anamjua miaka na miaka. Huu ulikuwa mtihani maji ya shingo kwa Chan’duu. Watu hawa wawili wakiwa pamoja kwa hata nusu saa si watatongozana? Na wakitongozana si wataishia siku moja kuwa wapenzi wa siri? Kila Chan’duu anavyofikiria akili za Sofi jinsi alivyomuongoza katika mambo mengi, hakuwa tayari kuona kuna mtu anamnyanganya mwanamke wake. Akili za Chan’duu katika maisha yake zilikuwa hazivuki katika kuvaa na kula, lakini Sofi alipoingia katika maisha yake alimbadilisha na kumfanya kuwa mtu wa malengo na kujua anachokifanya. Sasa mtu huyu kung’oka si itakuwa anarudishwa maisha yake ya kutojitambua?CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lakini pia kuna maneno aliwahi kuyasikia sana katika maisha yake toka yuko mtoto lakini hakuyazingatia mpaka Sofi alipoibuka katika maisha yake. ‘Mapenzi yako Tanga’ hii ni kauli aliyoisikia sana lakini hakuwa anajua maana yake mpaka pale alipokuwa mpenzi wa Sofi. Mtoto ni fundi kitandani usiambiwe na mtu, na ni mjuzi wa mahaba usihadithiwe. Uhondo anaoupata kwa msichana huyu, milele hatoacha nafasi ya kuona mtu mwingine anaupata. Chan’duu alikuwa na wivu mkali sana mpaka watu walikuwa wakimuambia hivyo na hata Sofi alikuwa akimuambia aache wivu huo, lakini siku zote alikuwa anajitetea kwamba analinda mzigo wake katika gari ambayo ina vibaka wengi kuliko abiria wa kawaida. Na wivu huo haukuja tu bali ulitokana na mahaba ya ndani anayopewa, na mapenzi motomoto anayofanyiwa.
Ni ukweli uliowazi kabisa kwamba mzigo wako ni dhamana yako hivyo ukiuacha upotee itakula kwako kwa ujinga wako na yeye hakuwa tayari kuona mambo yanamuharibikia kwa uzembe wake
Hivyo akawa makini sana kwani leo kukutana watu hawa wanaoonekana kuendana, peke yao, sirini, ndani ya masaa matatu ama sita atakayokuwa yuko Tanga, aliona ni balaa zito. Hapo alipowaza mambo hayo ni wakati akiwa kwenye gari, safarini, sasa wakati huu ambao amesharudi na kusikia kwamba mwanamke wake amelala kwa vile kichwa kinamuua, kulimfariji sana, sana, kwani anajua kwamba mwanamke wake ana matatizo ya kichwa na mara nyingi huwa analalamika hasa pale anapokunywa pombe nyingi au kukosa usingizi ama kuchoka sana. Kujua kwamba mwanamke wake amelala muda mrefu uliopita na vile siku tatu hizi hajamgusa, kukamfanya sehemu zake za siri kupata mshituko na mshawasha wa kuona anafanya kitendo cha kumpa raha na liwazo. Akajipa mawazo kwamba akifika ndani kilichopo ni kwenda kitandani moja kwa moja kumsalimia mwandani wake na kuanza mambo. Mara nyingi tu mpenzi wake huwa wanakutana katika hali hiyo na kuufanya uwanja kuwaka moto
Mwanaume akafungua mlango taratibu na kwa kunyata akaingia ndani
Kabla hajapiga hatua za kumfikisha kitandani alipolala Sofi akasimama na kumuangalia Sofi ambaye alikuwa amelala huku mgongo ukiwa juu. Akamkagua mwanamke wake kama vile ndio kwanza anamuona. Mate ya uchu yakataka kumtoka. Akajiona ni mwenye bahati kubwa kuwa na msichana huyu mwenye umbo la kuvutia na akiwa anammiliki peke yake tu. Bila kujua kwamba mlalo huo uliolalwa umetokana na mambo makubwa yaliyofanywa kwa fujo na kidume Kijogobwire muda mchache tu uliopita na kumuacha Sofi akiwa amechoka huku nafsi yake ikiwa imesuuzika na kijihisi kama yuko peponi
Chan’duu akamsogelea kwa kumnyatia mpaka alipofika kitandani akakaa kwenye kitanda karibu kabisa na mwili wa sofi
Akanyanyua mkono huku anatetemeka kama vile ndio kwanza ni siku ya kwanza ya kukutana naye. Akataka kumkamata makalio lakini akasita ghafla ikiwa anajua kwamba katika vitu ambavyo ukitaka kumtibua Sofi na msiongee kwa muda wa juma zima basi umguse sehemu zake za nyuma
Akasitisha jambo hilo na kuupeleka mkono wake sehemu za mgongoni na kuanza kumpapasa. Kitendo cha kupapaswa ni kama kilimgutusha Sofi lakini hakugeuka kumuangalia ni nani anyemchezea maungo, kikubwa alichokifanya ni kusikilizia kuchezewa huko na kuanza kutoa mguno flani wa mahaba wenye kushawishi. Kitendo hiki kikaamsha mashetani ya Chan’duu na tamaa ya mwili kumjaa. Akajikuta akiwa na hamu kubwa ya kuona anavua nguo zake na kujitupa msambweni lakini kama vile ambavyo ameshazoeshwa na mwanamke wake kwamba kuwepo na mahaba ya muda mrefu kwanza kabla ya msambwe mwanaume akajikuta akikaa sawa na kwa mikono yake yote miwili kuanza kumpapasa Sofi mauongo yote kuanzia maeneo ya shingo mabega kwapa na mgongo. Sasa Sofi akawa anatoa sauti ya kuanza kuzidiwa na ashki. Chan’duu ni kama shetani tu alimpitia, akajikuta leo bila woga akiiteremsha mikono yake na kuanza kumshika maeneo ya makalio taratibu katika kumpapasa. Katika kitu ambacho Chan’duu kilimshangaza na hatimaye kumfurahisha ni kitendo cha Sofi kuonekana kukifurahia kitendo hicho tofauti na ugomvi anaouanzisha mara anapoona muelekeo wa mikono kushika huko. Chan’duu akaanza kutoa nguo zake mauongoni huku akimuona na Sofi naye akianza kuzitoa nguo zake mbili zilizobaki maungoni mwake wakati huu. Kitu hiki kilimfanya Chan’duu kuzidi kuchanganyikiwa. Akaupeleka mkono wake katika mahala ambako palimsisimua sana Sofi kiasi cha mwanamke huyo kujikunja huku uso wake ukimuangalia Chan’duu mdomo wake ukitaka kutoa kauli. Lakini ni kama vile tu shetani aliepusha balaa zito ambalo lingetokea kama Sofi asingejizuia alichotaka kukitamka mara tu alipoona kwamba aliyetaka kumuambia sio aliyemkusudia. Sofi wakati ambao mashetani ya mahaba yameshamshika alikuwa anataka kusema ‘Aa jamani Kijooo’ lakini wakati anasema ‘Aa jamani K..’ ndipo hapo hapo macho yake yalipoona kwamba kumbe aliyekuwa anamshika maungo kwa nia ya kurudia tena mchezo hakuwa bwana wake mpya mwanaume Kijogobwire bali mwanaume wake halisi bwana Chan’duu
‘Aha Chan’duu umerudi?’ ikabidi kuuliza huku akibabaika
Japo kama neno K, Sofi alivyolitoa halikuishia kusikilikana, lakini Chanduu kuna kitu kilimjia ghafla kuwa mwanamke wake alitaka kusema Kijogobwire. Akabaki kuduaa na mshituko kumshika. Lakini kila alivyokuwa anazama katika mawazo akawa haoni picha kwamba mwanamke wake ni kweli alikusudia Kj. Huyu alitaka kusema nini? Kama angelisema kitu kama S ingemaanisha Swetty, B kwa Babii, M kwa My, H kwa maana ya Honey, D iko Dear, M kwa Mr, L ni Love, O itakuwa Oo My God kwa maana ya kupagawa na T ni The One, huku G ikiwakilisha Gud.. hii K alimaanisha nini? Itakuwa K ni kwa Kijogobwire tu
Mwanaume akanyong’onyea akaona kabisa hapa ameshazidiwa ujanja kama vile alivyodhani
Zile Push-up alizokuwa anapiga kidume K pale nje ni za kuchekelea ushindi? Akajiuliza. Au ni za kujipongeza? Ama ni za kurudisha nguvu alizozipoteza hapa kitandani wakati yeye amekwenda kufuatilia laini za simu?
Oo masikini! Chan’duu sasa anataabika. Anakiona cha mtema kuni. Kufa hafi lakini cha moto anakionaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika wakati wa neema yeye kwake ndio imekuwa kipindi cha mateso?
Mawazo yakamjaa pima
Hapa anajiona kabisa kuwa anaondoshwa mchana kweupee na hakuna jinsi
Sofi ni kama vile alijua kwamba hapa ameropoka bila kujiuliza. Akajilaumu kwa kutokuwa makini. Kwanini hakugeuka kwanza kisha ndio akamtaja aliyetaka? Sawa alizidiwa na mahanjamu kiasi cha kujikuta yuko tayari kuropoka chochote kwa mtu ambaye amemuingia moyoni kiasi cha kuwa yuko tayari kumuachia anachotaka, lakini si alikuwa anajua kwamba mtu huyu atarudi muda si mrefu? Kwanini hakuwa makini?
Akaona hapa ameshamwaga mboga na asipoucheza huu mchezo katika namna ya uigizaji basi huenda aliyebaki akamwaga mboga
‘Mbona umeacha mpenzi? Mimi nilikuwa na hamu na wewe tokea majuzi. Umerudi, najihisi faraja sana’ akalegeza sauti na macho
Ulaghai ambao haukumuingia Chan’duu hata chembe
‘Ulitaka kusemaje?’ akauliza akiwa amekaza macho
‘Saa ngapi honey?’ naye akauliza
‘Kipindi unageuka?’
‘Nilitaka kusema, jamani mbona unanitesa babii’ akaingiza gia nzito
Gia ambayo bado kidogo imlegeze Chan’duu, lakini mwanaume akachekecha kichwa akaona haya ni maelezo mepesi
‘Sasa mbona uliponiona ulisita na kushituka?’ akauliza akijua hapo amemkamata
‘Nimeshituka kwasababu nilipokuangalia niliona jasho linakuvuja uso umekuiva na kama unatetemeka, nikadhani labda unajihisi kuumwa’ hapa Sofi alimshika mtu pabaya kwani ni kweli uchu aliokuwa nao Chan’duu na kitendo cha kumpapasa sofi kwenye makalio bila kukaripiwa kulimfanya ajihisi kutetemeka kwa kutoamini. Jasho kweli lilikuwa linamvuja. Sasa kukiri kwamba nimebanwa na mahanjamu mpaka sijiwezi, haiwezekani, na kusema kwamba nilisikia kama unataka kutaja jina la Kijo ataonekana analeta wivu wa kitoto. Kubabaika kwake kukamfanya Sofi sasa kuutawala mchezo
‘Kama unajisia vibaya nenda kaoge upate dawa tupange vitu vingine’ akasema sasa akinyanyuka akijihisi kuumaliza machezo huku akishukuru mungu kwamba ni vipi angeweza kufanya mapenzi na Chan’duu muda mfupi baada ya kuridhishwa nafsi yake na Kj. Kwake sasa hivi Chan’duu ni kama takataka tu hana hadhi hata ya kumgusa
Chan’duu kuona Sofi ananyanyuka akamdaka mkono, moyoni akiona hapa tayari huenda akakosa penzi
‘Hapana babii ni uchovu tu lakini niko sawa’ akasema na kumteremsha Sofi kitandani akimnyanganya nguo alizokuwa sasa anazivaa
‘Basi kama umechoka nenda kaoge then utatukuta hapo nje tunakusubiri na Kj ili tuje tupange’ akasema huku akizivaa nguo zake zilizokuwa zimeanza kuvuliwa
‘Usijali kwanza tunanii halafu nitaenda kuoga kwani hata mimi nina hamu nawe mpenzi’ akasema sasa akimshusha kitandani kinguvu
‘Eh Chan’duu! Vipi huelewi mtu akikuambia kitu? Wewe kushakuwa mtu mzima bwana, nimekwambia nenda kaoge kwani mimi si nipo au nitakufa’ akauliza akinyanyuka kwa nguvu akiwa amekunja sura
Kitendo hiki kimkamkera mno Chan’duu
‘Unasemaje?’ akauliza kwa ukali
‘Inamaana hujasikia au?’ Sofia akauliza kwa jeuri
Maneno haya yalimfanya Chan’duu awe mwekundu kwa hasira mishipa ikaanza kumnyanyuka kiasi cha kujikuta akianza kuhema kwa tabu. Ilikuwa bado hajapata uamuzi sahihi wa kuchukua kati ya kuanza kutoa kichapo au matusi au kuuliza ninini hasa kinaendelea. Wakati bado akiwa anababaika mara ghafla mlango ukafunguliwa na mwanaume Kijo akaingia
Akawakuta watu wawili wakiwa wamesimama kama majogoo yanayoviziana katika ugomvi
Sofi akaikamata kanga aliyovaa na kuifunga vizuri kiunoni
‘Naomba muje nje basi tukae tuanze kupanga’ Kijo akasema akiwaangalia akijua wazi hapa hakuna usalama
‘Sio lazima nje hata hapa tunaweza kuongea’ Chan’duu akajibu kwa hasira
Maneno haya yalivyotoka Kijo akajua kwamba Chan’duu kuna kitu amekishitukia na alipokuwa anakihoji hakupata majibu yenye kuridhisha hivyo hapa akimjibu tofauti huenda kikawaka. Ilikuwa ni kutokana na mshipa wa ashki kumnyanyuka mwanaume Chan’duu tu ndio uliozima uwezo wake wa kuona na kujiuliza kwani kama hapa ndani angeliangalia kwa umakini mara moja angegundua kwamba mwanamke wake ameshaliwa mambo. Hapa ndani kulikuwa na fulana ambayo asubuhi wakati anatoka ilikuwa imevaliwa na Kijo na hata kitanda kilikuwa kiko ovyo kuashiria kwamba kuna milalo ya ajabu ililalwa na pia kulikuwa na chupa za pombe kadhaa ambazo zilikwisha tumika na kwa vyovyote jinsi Sofi asivyokuwa mnywaji mzuri basi walitumia wawili. Hali ya chumba ilikuwa dhahiri kuwa Chan’duu ameshazidiwa ujanja.
‘Ok kama unataka tupange humu humu ndani pia ni sawa.’ Kijo akasema kumridhisha Chan’duu
Akavuta stuli na kukaa. Sofi akakaa pembe moja ya kitanda mbali na wote. Chan’duu mwenyewe akakaa pembe ya pili na hasira zake
‘Ok. Nahisi suala la laini liko sawa?’ akauliza Kj kumuuliza Chan’duu
‘Ndio’ mwanaume akajibu kwa kifupi
‘Sasa cha kwanza, Sofi tupatie namba za mama wa mtoto ili tumpigie simu tumueleze kwamba mtoto tuko naye na tutahitaji fedha kesho na mapema ili tumpatie mwanawe’
Sofi hakugigisa akazitaja namba hizo haraka harakaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Sofi alisema kwamba tajiri ni baba mtoto wala sio mama mtoto. Kwa hiyo namba za mama yake hazina kazi atutajie namba za baba yake ili tumpigie kwani yeye ndio mwenye hela’ Chan’duu akaingilia kati kwa sauti kavu ya kiuongozi
Neno hilo likamchekesha Kj. Akacheka kidogo kisha akasema ‘Chan’duu haya mambo ya kupanga niachie mimi mzoefu. Wewe ulishasikia kwamba baba mtu ni bahili sana na mtoto anapendwa sana na mama yake. Unadhani katika hao wawili ni nani atatoa hela kwa ajili ya kumkomboa mtoto wake?’
‘Hata ukimpigia mama, atakaye toa hela ni baba mtu kwani ndio mwenye mtoto na ndio mwenye hela’ akang’ang’ania msimamo wake katika hali ile ile ya kuonyesha kwamba sasa yeye ndio kiongozi na mpangaji wa mambo haya kama ilivyokuwa mwanzo alipotoa dili hili
‘Chanduu acha ubishi, anachosema Kijo ni ukweli kwani ukiacha uzoefu wake lakini mimi ninayeishi na ile familia najua kuwa yule mzee hawezi kutoa hata milioni tano achilia mbali milioni mia mbili’ Sofi akaingilia kati
Neno milioni mia mbili lilimshitua Chan’duu akanyanyua uso na kumuangalia Sofi. Mawazo yake siku zote ni kwamba wakidai fidia basi itakuwa milioni ishirini na tano lakini kumbe dili hili ni zito namna hii? Mara akajihisi kusahau hasira zake za mapenzi na kujikuta tamaa ya fedha imemuingia ghafla zaidi ya mwanzo na hapa sasa akajipa mamlaka kamili ya kuwa kiongozi wa mchezo huu bila kujali wenzake watachukulia vipi
Japo kama alishituka kuona kwamba wenzake kumbe walishapanga bila ya yeye kujua lakini hela iliyotajwa ilikuwa nyingi kiasi ambacho zengwe halina nafasi
‘Mimi kama kiongozi wa hili dili nimeshasema tunampigia baba wa mtoto, kama mnanikatalia itakuwa labda mna yenu, kwanza Sofi, Kijo aniliniambia unaumwa kichwa na umelala na nilipokuwa karibu yako nilisikia harufu ya pombe kwa hiyo ulikunywa ili iwe dawa au kuna kitu kinaendelea hapa?’ akauliza kimikwara
Sofi kama kawaida yake hili lilikuwa jepesi sana kulikabili
‘Ndio nilikunywa bia ambazo nilimuomba Kijo anipe kwani nahisi kuchanganyikiwa tokea tukio hili lilivyotokea. Kwanza sijui usalama wangu ukoje na nahisi huko mbele huenda tukaishia jela iwapo wewe utang’ang’ania kupanga mambo usiyoyajua’ akamrushia mpira mwenyewe
Hapa ikawa nafasi ya Kijogobwi kuingilia kusawazisha mambo
‘Mnakumbuka mara ya kwanza nilisemaje? Nilisema kwamba katika Dili tata kama hili ugomvi kwa patnas ni mbaya kuliko usaliti. Naomba tupange mambo na hasira zetu binafsi tuziweke pembeni. Sikia Chan’duu, tele simu nimpigie mama tupange namna ya kushika pesa ambazo kila mmoja kesho itamkuta akiwa tajiri’
‘Mimi ndio mwenye dili na pia najua kuwa mwenye hela ni baba hivyo naomba namba zake nimpigie tusicheleweshe muda kwa kitu ambacho mimi nimeshakitolea uamuzi’ akajibu kwa sauti kali kidogo kuonyesha kwamba ameshaamua
‘Chan’duu acha ubishi wewe humjui yule muhindi na mimi pia kabla sijaja hapa nilikuwa huko. Kwa taarifa yako kulikuja maaskari kufanya mahojiano na kwa namna yoyote ukimpigia yule muhindi basi ni lazima atawataarifu’ Sofi akanasihi
‘Ivi nyinyi mnataka kunigeuka au? Mbona inaonekana kama vile lenu moja?’ akauliza kwa hamaki akiwa hataki kusikia mtu akipinga neno lake
Kitu hiki kilimuudhi mno Kijogobwire. Akakaa kwa muda akifikiria suluhisho la tatizo hili, alipolipata akanyanyua uso na kumuambia Sofi
‘Mpe namba za baba mtu’
Sofi akamuangalia Kijo kwa muda ili kuona kwamba yuko sirias. Mwishowe akamtajia
Chanduu akaziandika katika simu kisha akapiga
Simu ikaita mara ya kwanza bila kupokelewa. Akapiga tena. Ilipokuwa katikati ya muito sauti ya kihindi ikasikika
‘Hellow’
‘Habari’ Chan’duu akaanzisha maongezi
‘Muzuri’
‘Natumaini naongea na ndugu Mazarkhan’
‘Aa yes, wewe ni nani?’
‘Mimi naitwa Poul, kifupi nikwamba mimi ndio nimemteka mwanao na nataka shilingi milioni mia mbili ili niweze kumuachia huru’
‘Iko taka??’
‘Milioni mia mbili’
‘Iko taka? Milioni mia bili??’
‘Ndio. Tena kesho muda ambao nitakupigia simu ili umpate mwanao’ akasema akidhani labda Mazarkhan alishituka kwa furaha
‘Wewe iko pandwa na wazimu? Iko taka Milioni mia bili? Iko jua wewe iyo ela iko vipi? Wewe iko changanyikiwa? Milioni mia bili iko ona wewe na familia yako? Iko taka kwenda jela wewe? Iko taka chezea mimi?’ muhindi akawa sasa anakuja juu maneno yanamtoka kama amechanganyikia
Maneno haya yakamchanganya Chan’duu akajikuta akipagawa na ghafla akaikata simu na kuganda kama sanamu
Mduao aliokuwa nao Chan’duu ulimfanya Kijo kujua dhahiri kilichotokea
‘Si nilikuambia kuwa mtu bahili huwa haelewi? Unaona sasa umeshaanza kuharibu mambo?’ akasema kama kutoa tahadhari akijua kwamba maamuzi aliyoyafikiria mwanzo ndio sasa yakuyachukua. Kipindi Kijo hajampa ruhusa Chan’duu ya kupiga simu alikuwa anawaza kwamba mtu huyu huko mbele atamletea tabu na cha msingi ni kuangalia namna ya kumtoa katika dili hili na namna ya kumdhibiti huko mbele asije kutoa siri. Kwa vile namna ya kumkata alikuwa ameshaipata na namna ya kumdhibiti huko mbele ikiwa hajaifikia muafaka akaamua kutokuleta zengwe hapa
Chan’duu akawa hana cha kujibu zaidi ya kuganda na simu yake kama vile imepigiwa gundi katika mikono yakeCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Imekuwaje?’ Sofi akauliza macho yamemtoka
‘Muulize mwenyewe’ Kj akatupa mpira
‘Vipi! Umeharibu? We si uliambiwa halafu ukaleta ubishi? Lione kwanza juso lake. Unataka kutuingiza katika matatizo kwa upumbavu wako’ Sofi akaja juu
Chan’duu ikawa bado hajui nini cha kufanya
Sofi akasonya na kusema ‘Mijitu mingie bwana. Lione kwanza’ na kutoka nje kwa hasira
Hapa Kijo akatafakari jinsi ya kumaliza kilichobaki
‘Sikiza best. Haina tatizo kwa sasa kwani hakuna kilichoharibika. Cha msingi acha tusubiri siku tatu zipite kisha tutachukua hatua nyingine ambayo itamshawishi muhindi kufanya tunavyotaka. Wala usijali jembe’ akasema na kumshika begani ili kumpoza
Maneno aliyoyasema Kj na kumshika bega vilimfariji sana kiasi cha kujikuta akishusha pumzi na kufikiria kwamba ni kweli jambo hii liko juu sana ya uwezo wake na anatakiwa kulifanya kama kiongozi mkuu anavyosema na si kama anavyotaka. Iwapo kama aking’ang’ania msimamo wake huu uliotokana na wivu anaweza kujikuta akiozea gerezani na Sofi pia kumkosa. Kwani kweli Sofi na Kijo wanaweza kumgeuka? ‘Hapana’ akajipa moyo ili kujitoa katika hali aliyonayo
‘Mm, kuna watu duniani wabahili’ akasema Chan’duu kumuambia Kijo ili lawama imkumbe muhindi na kumuepuka yeye
…….
Kweli kuna watu duniani ni wa bahili lakini inataka moyo kutoa mamilioni ya shilingi kumkomboa mtoto ambaye kama utafanya taratibu nyingine unaweza kumkomboa. Mazarkhan aliona haina haja hata ya kutoa milioni moja wakati kuna askari ambao wanalifuatilia jambo hili. Japo kama mkewe alikuja juu akitaka mawasiliano na watekaji ili apatane nao awalipe wamuachie mwanawe lakini Mazarkhan hakukubali. Aliwapigia simu maaskari na kuwataarifu kwamba kuna mtu amepiga simu kutaka apewe pesa kwa ajili ya mtoto aliyemteka
‘Hili ni jambo tulilokuwa tunalitegemea’ mmoja wa maaskari akamwambia Mazar kipindi tayari wameshafika na kujadili nini cha kufanya
‘Tokea mwanzo tulipokuhoji na ukasema huna adui yoyote na familia yako pia iko hivyo tulijua kwamba mwanao atakuwa ametekwa na utadaiwa fidia. Hii nchi saa wajanja wameshakuwa wengi na haya mambo yapo sana sasa hivi, lakini usiwe na shaka tutawatia mikononi na mwanao utampata akiwa mzima kabisa bila kutoa hata shilingi tano’ akaahidi
‘Kama baba iko fanya ivyo basi iko mimi toa zawadi kubwa kupa nyinyi’ mama mtu akaahidi
‘Usijali mama hilo ni jukumu letu hali hitaji changamoto isiyo rasmi’ inspekta akasema ili asionekane kwamba kazi hii ataifanya kwa nguvu kubwa ili azawadiwe pesa kutoka kwa muhindi
‘Sasa hebu mpigie simu mwambie kwamba umekubali kulipa hiyo fidia ili aseme wapi mkutane ili mfanye mabadilishano’ inspekta akashauri
Mazarkhan akatoa simu na kuitafuta namba iliyompigia. Wakati akifanya hivyo mmoja wa askari akamuuliza
‘Huyo bwana anaitwa nani?’
‘Anaita Poul Ngemba’
‘Usihadaike na jina wala namba huyu jamaa anaweza kuwa mzoefu akatumia namba ya bandia na inaweza kuwa ni mtandao mkubwa uliofanya hili tukio ndio mana ukataka hela nyingi kama hizo’
Simu ikaanza kuita
‘Ongea na kwa taratibu’ afande akaamrisha
…………..
Wakati simu ilipokuwa inaita Chan’duu bado alikuwa yuko chumbani amelala juu ya kitanda mawazo yamemtawala, Sofi akiwa yuko nje na Kijogobwire wakijadili hili na lile juu ya mpango huu unaotaka kukwama
‘Unajua Sofi mpenzi, hili ni bonge la dili lakini lina udhaifu mmoja mkubwa ndani yake na tusipokuwa makini tunaweza kujikuta tukiishia jela. Na isitoshe.. Nahisi kama vile mia mbili ukiigawanya kwa mbili inagawanyika vizuri zaidi kuliko ukiigawanya kwa tatu’ akasema Kijo akimuangalia Sofi usoni kuona analipokea vipi neno lake la mwisho
Hapa haikuwa na ufisho. Mia mbili kugawanya kwa mbili maana yake ni kumtoa nje ya mpango Chan’duu. Na kwa vile sasa Sofi ameshaanza kumuona Chan’duu si chochote si lolote hivyo hakuna cha kumfikiria..
‘Lakini yule bege anajua mengi, tukimchezea si itakuwa balaa?’ akauliza, wazo lake likiwa na maana ya kumdhibiti Chan’duu na si kumuonea huruma kwa kazi aliyoifanya
‘Hapana. Yule ni mtoto mdogo tu hawezi kutuzidi ujanja na isitoshe kuna njia nyingi sana za kumnyamazisha mtu anayetaka kukukatiza kuikamata milioni mia moja’ akasema akiwaza kumnyamazisha Chan’duu moja kwa moja huku Sofi akiwa hajui kabisa Kj anawaza nini
Kabla Sofi hajajibu neno hili la Kijo mara Chan’duu aliyekuwa anakuja mbio na simu mkononi akawafikia walipo
‘Vipi?’ Kijo akauliza akimshangaa jinsi anavyohema
‘Muhindi anapiga’ akajibu akiwa anatetemeka
Kj na Sofi wakaangaliana
Kipindi walikuwa wanaangaliana simu ikaanza kuita tena
‘Lete’ Kj akasema na kuichukua simu kutoka katika mikono ya Chan
‘Hallow’ akaitikia taratibu
‘Mimi iko tayari toa milioni mia bili kama iko wewe taka lakini taka manangu iko salama’ Mazarkhan akasema kwa kutumia sauti ya kawaida
Kijogobwire akafikiria kwa nukta kadhaaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Vizuri. Sasa fanya hivi.. Kesho saa tano asubuhi shukua hiyo hela njoo nayo mpaka Kigamboni lakini pitia njia ya Posta na kabla hujapanda Panton nipigie simu nikuambie wapi tukutane unipe changu ili nikupe mwanao’ akamaliza na kukata simu
‘Vipi kasemaje?’ Chan’duu akauliza kama vile hajasikia kilichokuwa kikiongelewa
‘Usijali alichosema hapa cha kufanya ni hivi, mimi nitatoka kwa ajili ya kwenda kutayarisha mambo mawili matatu ili kesho saa tano tukakutane naye, sasa hapa nitaawacha lakini sitaki mlumbane kwani itaharibu mambo’ alipokwisha kusema hivyo akachomoka na kuingia ndani. Kj kuondoka tu Chan’duu akataka kumuambia kitu Sofi lakini msichana akanyanyuka na kwenda pembeni kujitenga mbali naye.
Chan’duu akabaki hapo hapo akiwa hajui nini cha kuanya
…………..
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment