CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Simulizi : Kikomo
Sehemu Ya Pili (2)
"Mipango ya operesheni yote naigeuza. Nikijipeleka kama nilivyopanga basi najichimbia kaburi. Inanibidi sasa nijihadhari. Nitahitaji msaada fulani fulani zaidi kutoka ofisi kuu.
"Vizuri, endelea unavyoona ni sawa, maana opereshani yote iko mikononi mwako. Kila unachohitaji utapata, kwaheri".
"Kwaheri, asante".
Nilipomaliza kupiga simu nilionelea huu ndiyo muda wa kwenda kumuona Buluba. Nambari ya nyumba ilikuwa 32 Kirumba. Niliondoka moja kwa moja kwa miguu kuelekea Kirumba na huku mawazo yangu yakinizunguka sana. Nilitafuta hiyo nyumba kwa bidii sana lakini kwa sababu nambari zenyewe hazikuwa na mpango ilinibidi niulize. Nilikwenda kwenye duka moja la Mwarabu kuuliza.
"Habari ndugu".
"Nzuri".
"Nyumba nambari 32 inaweza kuwa wapi?"
"Nasunguka pande ile takuta nambari 32".
"Asante".
Nilifuata maelezo ya Mwarabu na mara moja nikaiona. Nilibisha hodi mlangoni lakini hakukuwa na jibu. Taa ilikuwa ikiwaka ndani. Nilizungusha kitasa mlango ukafunguka, kumbe ulikuwa wazi. Huenda alikuwa ameenda dukani, nikaingia nimsubiri.
Nyumba ilikuwa na sebule nzuri yenye saa kubwa sana ukutani. Nayo ilionyesha saa moja usiku, wakati nilipokuwa naingia. Taa ya chumba cha karibu nayo ilikuwa inawaka. Katika hali hii nikafikiria huenda amejilaza kitandani na usingizi ukamzidi. Nikaamua nimwangalie humo chumbani.
Lo! Nilipofungua chumba nilipata tishio jingine Matayo Buluba alikuwa ananing'inia darini amekufa! Jasho lilinitoka. nikashikwa na bumbuwazi kubwa. Jack Mbwileamekufa, Majulanaye! Sasa Buluba.
Wakati nakata shauri kuondoka nikasikia mtu anafungua mlango wa sebuleni. Nilijibanza kwenye ukuta karibu na mlango wa chumba cha kulala.
"Lazima utakuwa umeangusha humo chumbani", sauti moja ilisema.
"Huenda, lakini sidhani", alijibu mwingine.
"Fanya haraka, tafuta haraka haraka, anaweza akaja mtu akatukuta humu," sauti ya kwanza ilionya.
"Hapa sebuleni hakuna. Lo, sijui nisipoiona hiyo karatasi nitakwenda wapi!"
Kumbe walikuwa wanatafuta karatasi. Mara moja nami nikatazama huku na huku nikakiona kijikaratasi chini ya uvungu wa kitanda. Mara mlango wa sebuleni ukafunguliwa. Pandikizi la mtu likaingia, lakini bado lilikuwa halijaniona. Macho yake yalienda moja kwa moja kwenye hicho kikaratasi chini ya uvungu. Alipotaka kuinama ili akiokote kufumba na kufumbua alikuwa amelala chini kwa vile nilimpiga teke la uso bila ya yeye kutegemea.
Bastola aliyokuwa ameshika ilimtoka mikononi nami nikaruka kasi kuikota na kumwelekezea mwenzake ambaye alikuwa amepigwa butwaa. Kwa wepesi wangu nilifyatua risasi na kumpiga mwenziwe mkono wa kulia ambao ulikuwa umeshikilia bastola. Nayo ikadondoka bila ya yeye kutaka. Mwenziwe alipojaribu kujitahidi kunyanyuka hakua na la kufanya isipokuwa kusalimu amri yangu sasa.
"Kwanini mmemuua Matayo?" Niliwauliza.
"Sijui", hilo pandikizi lilijibu kwa hofu.
Hasira zikanipanda huku nimeshikilia bastola.
"Naona tunataniana. Mumemuua rafiki yangu na halafu mnafanya masihara, mtanitambua sasa".
Kabla sijafanya chochote nikakikumbuka kile kikaratasi ambacho nilikuwa nacho mikononi. Huku nimeshikilia bastola tayari, nilikisoma hicho kikaratasi. Kiliandikwa.
Ndugu Busy, fika Songwe klabu kabla ya saa sita usiku bila ya kukosa. Ukikosa usije ukanilaumu. Lonely.
"Huyu Busy ni nani?" Nilimuuliza yule pandikizi.
"Simjui, Tom ndiye alikuwa akimjua. Mimi huwa namsikia tu".
"Mwongo, sema ukweli la sivyo utamfuata mwenzio sasa hivi".
Wakati huo mwenzake niliyempiga risasi alikuwa akitapatapa kwa maumivu ya mkono.
"Kweli mimi simjui ila namsikia tu, ndiye anafanya mipango yote ya magendo ya almasi yeye ni kama wakala na.
Kabla hajamaliza mlango ulifunguliwa. Mimi mara moja nikaruka upande kama umeme. Kisu kilichokuwa kimetumwa kuniua kwa bahati nikamwingia pandikizi kifuani na mtu aliyekitupa akakimbia. Nilipomwangalia pandikizi alikuwa ameanguka chini huku damu ikimtoka kasi kifuani. Hakuonyesha matumaini ya kuepa kifo iwapo angebakia muda mfupi ufuatao.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ingawa nilijikaza sana lakini nilianza kuona mahali pale hapakuwa na usalama wowotw kwangu. niliamua mara moja kuwapiga wote risasi mbili na kuondoka upesi iwezenavyo kabla jeshi la maharamia halijanivamia. Kisha nikakimbilia nje ili nirudi hotelini nilikofikia.
Sijui ni muda gani nilitumia lakini nilikuwa nikienda kasi mno. Sikuwa na haja yoyote ya kutafuta gari. Nilifika hotelini huku nikitweta na kutoa jasho jingi. Nilipotulia kidogo nikaoga na kubadilisha mavazi. Niliongeza risasi zaidi za bastola yangu kwa vile nilijua sasa maadui zangu ni wengi mno na itanilazimu mara kwa mara kupambana bila ya kutegemea. Funguo za chumba nilizichukua kwani nilikuwa wasije wakajua ni wapi nalala.
Sehemu hii ya mji wa Mwanza kuna kampuni ambayo unaweza muda wowote kukodi gari na ukaliendesha mwenyewe. Nikafanya hivyo na nikaamua kwenda Songwa Club kadri ya hicho kikaratasi kilivyosema.
Songwa Club iko kilomita kama kumi kutoka Maganzo, ama ni kama kilomita nne kutoka njiapanda iendayo Mwadui.
Nilitaka kuwahi kabla ya saa sita. Niliingia ndani ya gari nikafunga mkanda tayari kwa kuendesha mwendo wa kasi sana. Mnamo saa tano na dakika ishirini nilikuwa nimefika kwenye njia panda ya kwenda Mwadui na Songwa, lakini sababu nilifikiria kwamba sitaweza kurudi na kulala Mwanza nilikata shauri kwenda Maganzo nikalipie mapema chumba cha kulala katika nyumba ya wageni.
Nilipoingia Maganzo nikazungukazunguka kidogo halafu nikakata shauri kupanga chumba katika nyumba na baa iliyokuwa ikiitwa MASWA. Nilipoingia hapo baa ilikuwa imejaa hivi hata nafasi ya kukaa haikupatikana ingawa nilikuwa na kiu sana ya bia nilijikaza nisitamani.
"Halo," nilimwita mwanamke mmoja wa baa.
"Unasemaje?".
"Nataka chumba cha kulala".
"Subiri".
Baada ya muda mfupi akarudi.
"Kipo chumba kimoja tu, kina vitanda viwili kwa shilingi sitini tu".
"Sawa tu".
"Haya kalipe pale kaunta kwa yule mama mnene. Una mzigo?"
"Ndiyo, ni mfuko mdogo tu".
"Lipa halafu nitakuonyesha mahali pa kulala".
Nililipa na huyo mama akanionyesha chumba.
"Vyumba vyetu vizuri sana. Vitanda havipigi kelele", alieleza kwa tabasamu.
"Safi sana".
"Wewe unatoka wapi?"
"Mwanza".
"Unashughuli hapa?"
"Bila ya shaka, mtu haendi mahali bila ya shughuli. Lakini nataka kwanza kwenda kumuona rafiki yangu katika Baa ya Bantu".
"Tutaonana ukirudi".
"Asante".
Baada ya kupata chumba nilikifunga nikaondoka na kuingia ndani ya gari. Nilipoingia Songwa Clab ilikuwa saa sita kasoro robo. Kulikuwa na watu wengi, lakini kulikuwa na nafasi. Sikutaka kukaa chini kwenye meza maana ningeonekana mgeni na ningeweza kufahamika upesi.
"Halo, nipe bia baridi", niliagiza.
Bia yangu ilikuja nikaendelea kunywa. Niliangaza macho kwa chati baa nzima ili niweze kumuona mtu ambaye ana hali ya kumsubiri mtu lakini sikuweza kufanikiwa. Ilikuwa inafika saa sita na bado sikuwa nimeona kitu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Wewe ni mgeni hapa siyo?" Mtu aliyekuwa karibu yangu aliniuliza.
"Si sana, kwanini unauliza?"
"Nyuso za hapa tunazijua, au umeletwa Mwanza kwa uhamisho?"
"Hapana, kwani wewe unafanya kazi Mwadui?"
"Hapana, mimi nafanya hapo Songwe Stesheni ya Reli."
"Mbona maelezo yako ni kama karibu kila mtu wa Mwadui unamfahamu?"
"Si hivyo, maafisa wengi wa Mwadui huja kunywa na kutembea huku, tuseme maafisa wote wa Kiafrika wenye magari. Kule Mwadui hakuna wanawake, lakini hapa na Maganzo ndiko kwenye soko la watoto wa kike.
"Umekaa hapa Songwa kwa muda gani?"
"Lo, miaka kumi na miwili sasa. Toka nimemaliza darasa la nane nikajiunga na Reli ya Afrika Mashariki. Baada ya kutoka kwenye shule yao huko Nairobi nikaletwa hapa kama karani wa stesheni na leo niko hapa naitwa kama Stesheni Masta. Kwa hiyo Songwa, Mwadui na Maganzo nazijua kama kiganja changu".
"Miaka kumi na miwili, kweli umekaa."
Niliagiza bia zingine mbili, moja kwa huyu mtu. Bia zilipokuja huyu mtu akanishukuru sana.
"Asante sana, hapa watu hawanunuliani bia. Asante sana".
"Usijali".
"Ulisema unaitwa nani?".
"Mimi naitwa Mark, na wewe?"
"Abdul".
"Umetokea wapi?"
"Mimi nakaa Mwanza".
"Aisee".
"Ilikuwa sasa saa sita na robo na kulikuwa hakuna mabadiliko ya hali.
"Wanafunga saa ngapi siku hizi?"
"Kwa kawaida ni saa sita lakini wakati mwingine mpaka lyamba
Mara simu ikaanza kulia hapo kaunta. Akaipokea mfanyakazi wa kaunta. Baada ya kuzungumza kidogo akaita.
"We Mwenentumba kamwite Mzee Reuben kule ndani simu yake toka Mwanza.
Nilijisikia moyo wangu unapiga haraka haraka. Muda si mrefu kabisa. Alizungumza kwa muda mfupi akaweka simu chini huku amekunja uso akarudi huko ndani.
Huyu sehemu yote hii huitwa Pweke. Ni mtu hatari sana kuna tetesi kuwa anafanya magendo ya almasi ya hali ya juu. Polisi inasemekana wanamtafuta wameshindwa. Na ukitaka kumjua sana maisha yako hayawi marefu sana. Ni tajiri sana ana malori sana huko Shinyanga, Maganzo, Dar es Salaam na Mwanza. Vile vile watu humwita Pweke kwa sababu ni mara chache unamwona katika kikundi cha watu wengine", alinieleza taratibu.
"Yeye hukaa wapi?"
"Anakaa Maganzo, Shinyanga, Mwanza na Dar es Salaam, huko kote anakaa ana majumba lakini mara nyingi yuko Maganzo.
"Huenda basi nimemwona Mwanza".
"Bila shaka," Abdul alijibu. Hali yake ilionekana ni ya kulewa. "Tena nasikia yeye huwa anatumia dawa kuingia na kutoka Mwadui kuchukua almasi", aliendelea kueleza.
"Watu toka Afrika Mashariki nzima wanaoshughulika na magendo ya almasi nasikia wanamfahamu sana. Lo, ngoja ninyamaze nisije nikasikika nasema juu yake, maana nasikia ana masikio zaidi ya serikali. Polisi wenyewe tu hawathubutu kumgusa".
Niliagiza pombe zingine.
"Lete pombe".
"Loo, hakika nimefurahi sana, kaka wewe ni mtu mkarimu sana. Bahati mbaya mwezi umeniendea vibaya, miye ningekualika uje tunywe tena kesho, lakini nilikuwa na shilingi ishirini tu na nimeshamaliza. Hawa watu wa hapa hawathubutu kukopesha hata sisi wanywaji wa kila siku".
"Usijali, siku nyingine utajaaliwa."
Maelezo ya Abdul yalikuwa yamenisaidia sana.
"Mtu huyu ni wa ajabu sana. Ana dawa zinazoweza kusababisha kifo ana kujua mtu yeyote anavyomuwaza", alinieleza. Polisi akimfuatafuata anaweza kupata ajali akafa, au akafukuzwa kazi. Huenda hivi ninavyosema anasikia."
"Hawezi. Mbona una woga hivi".
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Wewe siyo mwoga? Sema baya lolote juu yake hapa Maganzo kama hatutakusikia umekufa kesho asubuhi. Wanawake wote Maganzo anawajua. Inasemekana anawaajiri wampe habari za wageni wote wanaoingia. Yeye huwalipa ujira wa kuwaridhisha hivi kwamba wasieleze habari hizi kwa mtu yeyote, ila Reuben. Askari kanzu wote wanaokuja kupeleleza habari za hapa hufa. Nimekaa hapa miaka kumi na nimeshuhudia wakifa. Wanawake wote sehemu hii ni wapelelezi wake. Lolote utakalosema litafika kwake. Sisi tunamwogopa mno," alimalizia na kisha akanywa matone ya mwisho ya bia yake katika glasi.
"Kunywa nyingine".
"Hapana, nimelewa anaenda".
"Unakaa wapi?. Nitakupeleka."
"Usijali, nakaa hapo mbele kama kilomita mbili tu kuelekea njia panda, lakini kwanza napita kwa rafiki yangu hapo karibu.
"Haya kwaheri nikipata muda nitakuja nikuone hapo stesheni kesho.
"Bila ya shaka karibu. Mara kwa mara urafiki huanzia kwenye tungi".
"Na kweli, basi tutaonana kesho".
Tulipeana mikono Abdul akaondoka. Ilikuwa saa saba kasoro robo hivi nikaagiza bia nyingine ya haraka haraka nielekee zangu Maganzo. Niliyokuwa nimeyapata yalinitosha kabisa ilinibidi kuzicheuacheua habari hizi kulingana na kazi niliyopewa kuwafichua na kuwakamata maharamia wa magendo ya almasi.
Wakati namalizia bia yangu ya mwisho. Mzee Reuben kama anavyoitwa alitoka ndani akamuaga mfanyakazi wa kaunta. Akaondoka kwenda zake. Nilipogeuka nikaona watu wamebaki wachache sana na kwenye kaunta tulikuwa tumebaki wawili tu.
Nilimaliza bia yangu nikamuaga mfanyakazi wa kaunta. Nikaenda zangu. Reuben alikuwa keshakwenda, maana hakukuwa na gari hapo nje.
Mawazo yangu yalikuwa mengi sana juu ya Reuben, Busy na kundi lao, nilitia gari moto kuelekea Maganzo. Nilipokaribia njia panda kwa mbele niliona kitu kimelala barabarani. Kwanza nilifikiri kwamba ni mbwa amekanyagwa lakini niliposogea karibu nikaona ni mtu. Niliposegea karibu zaidi nywele zangu zikasimama. Ni Abdul! Nikafunga breki bastola yangu ndogo nikaibana kwenye kiganja nikiwa tayari kwa lolote. Nilitelemka kwenye gari. Nilipomfikia nilikuta bado hajakata roho. Moyo wake ulikuwa unagonga kasi. Alionekana kama mtu aliyepigwapigwa sana au kugogwa na gari. Sikuweza kuona damu mahali alipolala.
"Hapo hapo! Nyama we!" sauti ilisikika mara tu nilipoinama ili nimwinue.
"Huyu mtu anakufa, niacheni nimpeleke hospitali", niliwajibu kwa ghadhabu.
"Wewe je? Hujihurumii mwenyewe kwanza?"
"Mniue basi mnangoja nini?" niliwajibu kwa hasira.
Niliamini kwamba saa yangu nami ilikuwa imefika, kwa hiyo kuomboleza kusingenifaa. Ilikuwa kufa na kupona. Bila ya kukawia nilifyatua bastola yangu na risasi zikawapata wawili barabara. Mwenzao wa watatu akakimbia na hamsini zake. Ndipo nikapata nafasi ya kumnyanyua Abdul na kumweka garini.
Maharamia hao wawili walikuwa wakitweta chini - mmoja wao alikuwa na bastola nayo ilidondoka kando. Niliiokona sikuwa na haja ya kuwachunguza bali niliwaburura hadi kando ya barabara na kuwaacha wafe huko. Kama kuna mtu atakayewaona bahati yao kwani palikuwa na majani marefu sana.
Abdul alikuwa hajakata roho. Niling'oa gari kutoka hapo kuelekea Shinyanga umbali wa kilomita thelathini hivi. Nilienda kasi sana hadi hospitali.
"Ndugu, nimemleta mgonjwa mmoja mahututi ndani ya gari", nilimweleza muuguzi.
Yeye haraka haraka akisaidiwa na mfanyakazi mwenzake walichukua machela na kumbeba Abdul. Machela ilisukumwa mpaka kwenye chumba ambacho kilikuwa na daktari ambaye alionekana kama alikuwa akisinziasinzia.
"Vipi? Ajali ya gari?" Daktari aliuliza huku akisogea kwenye machela.
"Hapana nimemkuta amelala kwenye njia panda ya Mwadui na Shinyanga. Nikatoka garini nikakuta amepigwa na bado anapumua kwa hiyo nikakata shauri kumkimbiza hapa hospitalini haraka iwezekanavyo".
"Lydia tafadhali mpeleke chumba cha uchunguzi, tayarisha vifaa vyote haraka mimi najaza cheti chake".
Lydia na John walisukuma machela kuelekea kwenye hicho chumba.
"Unafikiri atapona?" Nilimuuliza daktari kama mtoto mdogo.
"Sijui, inategemea amepigwa kiasi gani. Ukifika asubuhi tutafahamu, kwani unamfahamu?"
"Hapana. Nimemwokota tu. Hata hivyo ni mgonjwa wangu sasa".
"Sawa, umepiga ripoti polisi?"
"Bado. Nilikuwa sina budi kwanza kumleta huku maana mtu mwenyewe taabani sana"
"Sawa, jina lako nani?"
"Mark Buhulula".
"Unakaa wapi?"
"Mwanza".
"Kabila".
"Msukuma".CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Wa wapi?"
"Ntuzu".
"Haya asante sana. Utakuwa hapa Shinyanga muda?"
"Hapana, niko Maganzo".
Daktari akamtupia jicho na kurudisha mara.
"Haya asante. Ukiweza kufika asubuhi tafadhali njoo unione nitakueleza hali ya mgonjwa wako. Mimi ninamaliza kazi saa tatu asubuhi".
"Nitajaribu kuwahi daktari".
"Haya kwaheri, asante sana".
"Kwaheri na nyinyi, asanteni sana".
Niliondoka moja kwa moja hadi Maganzo. Nilitaka kumpigia simu Chifu usiku huo, lakini nikata shauri nimpigie asubuhi. Mawazo ya visa vya usiku yalinisumbua sana. Nilifikiri kuu ya majambazi hawa pamoja na vifo vyote. Kule Abdul kunong'onezana nami tu tayari ilikuwa imeshafahamika kuwa amesema mambo mengi, na wakawa tayari kumwadhibu kiasi kile cha kumuua.
Ilionekana kweli kuwapo kwangu Maganzo kulifahamika na nilikwisha kuwa mashakani. Na lile jambazi lililokimbia huenda limepeleka habari za kufa wenzi wao kwa Pweke.
Nilipokuwa nakaribia Maganzo nikakumbuka maneno ya Abdul kwamba hilo jambazi Pweke limenunua wanawake wote wa mji kwa kuwafanya macho na masikio yake katika kupata habari zozote zile.
Maganzo ilikuwa tayari kimya. Mji mzima ulikuwa tayari umeshatulia sana. Mabaa yote yalikuwa yamefungwa kwa hiyo niliendesha moja kwa moja kuelekea Bantu. Nilipofika Bantu Bar nikaegesha gari langu vizuri nikaanza kufunga milango kama kawaida. Baada ya hapo nikatembea kuelekea mlango ambao nilikuwa nimeonyeshwa nipite nikikuta baa imefungwa. Huu mlango niliukuta wazi, nikaingia ndani.
Nilienda moja kwa moja mpaka kwenye mlango wa chumbani kwangu. Niliangalia vizuri kuona kama umewahi kufunguliwa, lakini haukuonyesha wasiwasi. Nilifungua mlango bastola mkononi na kuingia ndani. Nilipoingia tu nikasikia sauti.
"Karibu ndani ndugu. Funga mlango na uwashe taa. Usilelte matata, kama hutaki kiadhirika".
Kwa kuwa kulikuwa na giza sikujua huyo mtu alikuwa peke yake au wengi. Nilikata shauri nifanye kama nilivyoagizwa. Nilirudisha bastola yangu mfukoni. Nikarudisha mlango na kuusingika. Nikawasha taa.
Ndani mlikuwa na watu watano. Mmoja wao alikuwa ameshika bastola imara na imeelekezwa usoni kwangu. Nilipowaangalia vizuri hao wengine kumbe nao walikuwa na bastola, wameelekeza kwangu.
"Kaa chini ndugu, usiwe na wasiwasi. Tungetaka kukuua usingefanya lolote, ungekufa tu".
Kulikuwa na meza ndogo na kiti. Nikakivuta nikaketi.
"Abdul ana hali gani?"
"Sijui, nilimwacha bado amezirai".
Nikamwangalia vizuri huyu mtu aliyeniuliza. Alikuwa kijana mwenye umri wa miaka ishirini na mitano hivi. Alionekana jasiri sana.
"Mimi nakuona wewe ni mtu jasiri sana, na ingawa nimeamriwa kukuua, nimeonelea kwanza nikupe onyo kama kawaida yangu niwaonyavyo kwanza wote waingiliao mipango yetu. Wengi nimewaonya, hawakusikia na wote wamefifia duniani. Ningependa na wewe uwe kwenye kundi hilo, kwa hiyo nakuomba uondoke sasa hivi baada ya sisi kuondoka, urudi zako Dar es Salaam. Mambo yaliyokuleta tunayajua. Mark Buhulula, na una bahati sana. Sasa hivi ungekuwa ulimwengu wa marehemu. Usipoondoka sidhani hiyo bahati itaendelea. Tatizo unalotaka kulitatua ni gumu mno. Linataka jeshi zima na si mtu mmoja. Saa tisa na nusu uwe umeshaondoka hapa mjini la sivyo usilalamike yakikupata".
"Nikikataa kuondoka je?"
"Kama wewe una akili naamini utaondoka, lakini kama umechoka na maisha baki. Tuone kama jua ya kesho litakukuta hai. Yaliyompata Mathayo umesahau, kwaheri ya kuonana kama umesahau. Twendeni zetu".
"Kwaheri, nitafikiria".
Bila kunijibu huyo kijana aliondoka huku akifuatwa na watu wake. Alinishangaza sana kwa utulivu wake na akaniogopesha vile vile. Nilibana mlango nikazima taa. Nilikaa kwenye kitanda nikifikiri. Nilifikiri kutimka niende zangu Mwanza halafu Dar es Salaam, lakini nikakumbuka kwamba nimetumwa kuja kufanya kazi. Nilikuwa nimekuja kuinua uchumi wa wananchi. Kwa hiyo nilikuwa sina budi kujitoa mhanga kama wenzangu walivyokuwa wamejitoa mhanga waliotangulia kabla yangu.
Baada ya mafikira haya nilikata shauri nisiondoke na nikae nione kutatokea nini. Kuja kunitisha nilijua lazima na wao CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wana wasiwasi. Hivyo nilichukua mfuko wangu nikavua nguo nikatengeneza kitanda kama vile mtu amelala. Nikavuta kiti nikaa karibu na mlango. Nilitoa bastola yangu tayari kwa matatizo yoyote. Nikasinzia kidogo kwa sababu ya uchovu.
Nilikuwa nimelala kama nusu saa hivi, niliposhtuka kuangalia saa yangu ilikuwa karibu saa kumi asubuhi. Kilichonishtua sikukijua ni nini.
Baada ya kitambo kifupi nikaona mtu ananyemelea kitanda. Alivyoingia sijui. Alikuwa na kisu mkononi. na wakati huo huo kwenye kona nyingine ya chumba niliona mtu amesimama na bastola mkononi. Wakati huo walikuwa bado hawajaniona maana waliamini nimelala hapo kama kitanda kilivyokuwa kinadanganya. Hivyo mtu alipofika karibu na kitanda mahali alipofikiria ni kifua, akainua kisu. Wakati anatelemsha kuchoma nami nikaachia risasi kwanza kwa huyo aliyeshika bastola na kisha kwa huyo aliyeshika kisu. Kukawa patashika katika chumba. Kisha nikawasha taa. Aliyeshika bastola alitapatapa na alipomuona mwenzake akipiga makambi ya mwisho akahudhunika na kumsemesha.
"Haa Deus unakufa?"
"Na wewe je mbona hujihurumii", nilimkebehi.
Nilimsogelea nikamchoma na kisu chao wenyewe. Nilichukua kamba mfukoni mwangu nikamfunga.
"Mliingiaje humu?"
"Kwa kupitia hapo juu".
Nilipoangalia nikaona kuna kipande kimoja cha ubao kwenye pembe moja ya dari kilichokuwa kimekatwa na kurudishwa.
"Wakati gani mambo haya yalifanyika?"
"Kati ya saa saba na saa nane".
"Ndipo kundi lile lote lilipopita mara ya kwanza?"
"Ndiyo".
"Mbona nyinyi mlipoingia sikuwasikia?".
"Angalia hivyo viatu chini".
Nilipoangalia nikaona soli zake zimetengenezwa laini nene zenye kufanana na matakia ya paka au chui. Kwa bahati nzuri risasi haikumpiga pabaya ni mkono tu ulioumia, alitapatapa tu kwa sababu ya hofu. Na kwa hivyo niliamini hii ni nafasi ya kumtumia mmoja wao. Huyo mwingine hakuonyesha matumaini ya kuishi kwani risasi nyingi zilimchakaza kifua.
"Twende".
"Wapi unanipeleka? Siendi popote iwapo wataka kunia uniue tu".
"Usinicheleweshe".
"Nimesema uniue, siendi popote".
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hasira zikanipanda na nikampiga mkono huu uliolemaa na risasi. Akalia sana kwa uchungu. Kisha nikambeba mgongoni na kumweka garini. Nilimpekua kuona kama ana chochote cha kunidhuru, nikaona hana. Bastola yake nilikwisha ipora.
Niliwasha gari moto na kuelekea Shinyanga. Niliondoka kwa mwendo mdogo sana sababu ya mawazo mengi niliyokuwa nayo baada ya haya yote kutokea ilinishangaza kuona wakati wote wa patashika katika chumba hicho hakuna mpangaji wa vyumba vya jirani aliyejitokeza. Imekuwaje? Mbona niliambiwa vyumba vyote vimejaa wageni! Nyumba hii haina budi kuchunguzwa. Nilikumbuka pia maneno ya Abdul ya kwamba jambazi Pweke amenunua wanawake wote wa baa wapeleleze kila mgeni aingiaye.
Jambazi nililokuwa nimelibeba ndani ya gari lilikuwa limeishazirai na mkono wake kufura vibaya. Hata hivyo nilikuwa nalisukasuka mara kwa mara na likapata maumivu makali. Wakati huo ndiyo nilipata nafasi ya kulihoji maswali kadhaa. Niliendesha gari mpaka karibu na hospitali ya Kolandoto, lakini porini kwa kufuata njia waliyokuwa wakipita ng'ombe.
Niliegesha gari huko mbali na barabara, ilikuwa yapata saa kumi na nusu hivi usiku na ilinibidi nifanye haraka shughuli yangu watu wasije nikuta waendapo shambani mapema asubuhi. Nilimtoa huyu mtu kutoka ndani ya gari nikamweka kwenye majani, nikisaidiwa na mbalamwezi. Nilitoa aina ya dawa kali mfukoni mwangu nikaiweka kwenye pamba kidogo nikamwekea puani. Haikupita hata dakika akapiga chafya na kuzinduka.
"Niko wapi hapa. Tunafanya nini?"
"Tulia, wewe ulikuja kuniua Maganzo, sasa ni zamu yako. Tuko porini wawili tu, na leo utanikoma.
"Nilikwambia uniue mbona hujaniua? Hata ufanye nini sikwambii lolote wewe niue tu".
"Mimi sikuui ila kuniambia utaniambia tu. Vua suruali upesi".
"Nitavyaje na wewe umenifunga?"
Nilimsogelea nikamsukuma kwa nguvu, akaanguka chini. Nilichukua kamba nyingine nikamfunga miguu. Halafu nikaanza kumvua suruali haraka haraka.
"Unataka kunifanya nini we?"
"Tulia, Nikikwambia kwa ustaarabu hutaki, sasa utanitambua".
"Niue tu, maana hata ufanye nini sisemi lolote".
Baada ya kushusha suruali na chupi nikazishika korodani zake.
"Jina lako nani?"
"Nimekwambia sisemi, husikii? Niue tu kama ulivyomuua Deus".
Nilipoona hivi nikazishika vizuri korodani zake, nikazivuta na kuziminya kwa nguvu. Punde akapiga kelele.
"Aaaa, aaa, niache sitaki".
"Jina lako nani?"
"Nicodemas."
"Unamfanyia nani kazi?"
"Sijui?"
Hasira ilinipanda, maana alikuwa ananichelewesha. Nilichukua koleo nikavuta korodani moja sasa. Nikaiweka katikati ya koleo nikaanza kuibana.
"Aaa, aaa, aaa ngoja niseme, tafadhali niachie nitasema yote, aaa, aaa, aaa".
"Unamfanyia nani kazi?"
"Ole".
Ole ni nani?"
"Ni yule tuliyekuja naye kwako usiku".
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Yeye Ole anamfanyia nani kazi?"
"Pweke".
"Pweke ni nani?"
"Yeye sisi hatumuoni mara kwa mara ila tunajua tu kuwa ndiye anaongoza hili kundi".
"Ni yeye pekee yake?" Niliuliza huku nikibana kidogo koleo".
"Ee hapana siku moja nilimsikia anasema na Ole juu ya mzee alisema mzee amekasirika sana huko Dar es Salaam. Ni hayo tu".
Nikabana kidogo tena.
"Nafikiri huyo ndiye mkubwa, lakini ana wenzake Shinyanga, Arusha, Mwanza, Musoma, Nairobi na Kampala. Hawa tumewahi kuwaona wanapokuja kwenye mkutano na sisi huwa tunaizunguka kulinda nyumba wanamofanyia mikutano".
"Shughuli yenu kubwa ni nini?".
Alishtuka kidogo juu ya swali hili, kisha akajibu, "Hujui ni almasi bila shaka wizi wote mkubwa wa almasi toka Mwadui lazima uhusike na kundi letu".
"Je, umewahi mwenyewe kuiba?".
"Sijui kuiba mimi ni mlinzi na nimeajiriwa kuua tu wako wanajua wameajiriwa kuiba".
"Kama nani?".
Nikabana koleo.
"Sijui hata jina moja nasema kweli tafadhali nasema kweli nasikia tu wengi wanafanyakazi huku Mwadui lakini kweli aaaa sijui jina hata moja".
"Mnalipwa kiasi gani?"
"Aaaa nalipwa shilingi elfu kumi kwa mwezi"
"Elfu kumi wewe mlinzi tu?"
"Ndiyo, kama akina Ole nasikia wanalipwa shilingi elfu ishirini kwa mwezi".
"Kwa mbali niliona mtu anakuja nikamtwanga Nicodemus na kitako cha bastola kisha nikambeba hadi garini, nikatia gari moto kabla huyu mtu hajatufikia. Nilipofika barabara kuu nikakata shauri nielekee Shinyanga. Ilikuwa yapata saa kumi na moja ya asubuhi sasa nilikwishajua kwamba ni wakati wa mapambano na kundi ambalo limejiandaa hasa na lenye kufurahia kazi yake kwa sababu ya ujira mkubwa bila shaka wana nidhamu kubwa. Ole na wenzie walijuaje kuja kwangu kabla hata sijaondoka Dar es Salaam watu waliojua ni Chifu, Mkuu wa Polisi, Maselina, Lwiza, George na Didi. Lakini Didi hakuniona jinsi nilivyovaa au kuonekana wakati naondoka na wala hakujua jina langu lilikuwa Mark Buhulula. Nikakata shauri kupiga simu Dar es Salaam nijue kama kulikuwa na mtu mwingine aliyejua ambaye angeweza kuwajulisha juu yangu bila ya kujua yote haya. Ingekuwa vigumu sana kunitambua baada tu ya kuingia Mwanza.
Wakati nikifikiria hivi nikawa naingia Shinyanga mjini. Niliendesha moja kwa moja mpaka kituo cha usalama Shinyanga ambako nilimkuta askari wa zamu.
"Mkuu wa kituo yupo?" Nilimuuliza.
"Yupo".
"Naomba kumuona".
"Wewe nani na shida yako nini?"
"Nina mtu ndani ya gari mahututi, hivi tunavyozidi kubishana akifa mimi simo">
Nilipomwambia hivi akagutuka na kuchukua simu na kupiga.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mzee kuna mtu anataka kukuona... Sijui hajaniambia lolote" Kisha akanigeukia, "Nenda chumba nambari sita".
"ASante, angalia hiyo gari asitoke mtu au weka mlinzi kabisa shauri yako akikimbia". Kabla hajajibu mimi nikaelekea chumba namba sita. Nilibisha na kuingia ndani. Mkuu wa kituo kwa kufuatana na mavazi na tepe alizovaa alikuwa na cheo cha Inspekta.
"Habari Inspekta?"
"Salama, nikusaidie nini?"
Nilishika mfukoni mwangu nikatoa kitambulisho changu aliposoma akatoa macho ya woga huku akisimama kidogo alibabaika aseme nini.
"Nikusaidie nini mzee?"
"Nina mtu kwenye gari sasa amezirai lakini kwa muda tu wekeni rumande mpaka atakapopata maagizo zaidi na angalia asitoroke. Akitoroka bahati yako mbaya, utajua wewe mwenyewe. Habari hii isielezwe kwa mtu yeyote iwe siri yako mpaka hapo baadaye. Kwaheri, tutaonana tena ikibidi.
"Bila ya shaka mzee, mimi mwenyewe nitahakikisha maagizo yako yatatekelezwa," alisema huku akiondoka kunisindikiza.
Tulipofika kaunta akamwambia askari wa zamu. "Nenda ukamtoe mtu ndani ya hilo gari, mlete chumbani kwangu".
Baada ya kumtoa nikaingia ndani ya gari na kuondoka, nilitafuta mahali pazuri nikaegesha gari ili nilale kidogo. Nilipoamka ilikuwa saa mbili kamili, niliinua kiti cha gari nikawasha gari kuelekea kituo cha petroli. Baada ya kuweka mafuta nilikata shauri niende Hoteli ya Shinyanga nikapate kifungua kinywa. Nilipoingia hotelini nikaelekea msalani ambako nilikuta beseni. Nilipiga mswaki na kunawa sawasawa. Kisha nikarudi hotelini nikatafuta meza nikakaa. Mfanyakazi wa hoteli akanijia.
"Utakula nini mzee?".
"Nipe kahawa, mayai mawili ya kukaanga na maziwa.
Nikakaa kungoja chakula. Chakula kilipokuwa tayari kikaletwa nikaanza kula. Wakati nilipokuwa karibu kumaliza kula, nikashtuka watu wawili wanavuta viti na kukaa katika meza hiyo hiyo. Nilipoinua macho kuwaangalia nikatambua kuwa mmoja ni Ole na mwingine ni kati ya hao watu wake. Kijasho chembamba nikakihisi kutekenya maungo.
"Chakula chako kimeshalipiwa, inuka taratibu twende la sivyo angalia ubavuni".
Nilipoangalia ubavuni ndani ya kila koti la kila mmoja walikuwa washikilia bastola zenye viwambo vya kuziba sauti.
"Ok", nilijibu.
Nikaweka uma na kisu chinim, nikachukua kitambaa, nikajifuta.
"Hakuna ujanja, hatutaki kuua mbele ya watu, lakini ukitulazimisha tutafanya hivyo", nikaacha kitambaa changu na funguo moja juu ya meza nikainuka, wakanitanguliza huyo kijana aliyekuwa ameniletea chakula akanisemesha.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mzee, rafiki zako wameshalipa, asante sana".
"Asante kijana".
Mbele usawa na mlango nikamuona mtu wa tatu, nae mara moja nikaona kitu kinatokeza, nikajua alikuwa na bastola na nje kama mita kumi kutoka kwenye gari langu nikaona kuna gari aina ya Benz na watu wawili mara moja nikajua ndilo gari walilokuja nalo nilipokuwa usawa na huyo mtu wa tatu mlangoni, na huku hawa wawili wakiwa nyuma, kijana wa hoteli akaita.
"Mzee kitambaa umesahau".
Wote wakashituka na kugeuka hapo hapo nikapata nafasi kufumba na kufumbua ngumi mbili za nguvu kushoto na kulia shingoni mwa hao wawili wa nyuma yangu na wakati huo huo nikamtandika teke la tumbo watatu wote chini na bastola zao kabla hawajaamka mimi nilitimka na kurukia ndani ya gari langu wakati naweka gia ya kwanza ndipo Ole akaamka na kupiga risasi na huku mimi naondoka kasi risasi zake zote zilinikosa wakati naweka gia ya pili halafu ya tatu, nikamuona anarukia ndani ya hiyo Benz yao iliyokuwa na watu wawili wakanifukuza wawili waliachwa nyuma kwa hiyo gari likawa na watu watatu tulifukuzana barabarani na wakati nafika gereji moja katikati ya mji likatokea lori kubwa likakata barabara nzima nikakanyaga breki mara moja nikarudi gia namba moja nikazungusha usukani nikaweza kupita nyuma yake kabla halijanibana. nilipoona ninaweza kupita likaendelea mbele kuipa Benz nafasi.
Nilijaribu kuongeza moto zaidi, mara kukatokea trekta ambalo sikuweza kulikwepa, lakini nilipata kuruka kabla gari halijagongwa na kwisha kabisa nikaanza kukimbia nao walionifuata waliponiona wakatoka ndani ya gari na kuanza kunifukuza bastola mkononi huku Benz nayo ikikatisha kunifuata.
Nilikimbia mpaka kwenye jumba la shirika la usagaji ndani ya ghala la magunia ya mahindi ambayo hayajasagwa nilipandia dirishani na kujibwaga chini karibu na mlinzi nilimpiga ngumi ya shingo ili nipenye kumbe walikuwa wameniona nao wakaingia hapo hapo dirishani mimi nilijificha kwenye magunia nilipotulia ndipo nikasikia sauti zingine za wananchi zikisema, "mwizi mwizi mwizi".
Tulianza kutafutana kwenye magunia, nikamsikia mmoja karibu yangu akijisemea, "Yuko wapi?" Alikuwa karibu sana nami, nilipomwangalia yeye alikuwa bado hajaniona nikafundua kwamba ndiye yule aliyekuwa dereva ya hiyo gari alikuwa ameliacha nje, nilimpiga karate moja ya shingo na kumshindilia katikati ya magunia nilipompokonya bastoka yake na haraka haraka nikaelekea dirishani kusudi niwahi gari lao, nilipokuwa naruka dirishani wakaniona lakini risasi zilikuwa zimechelewa wakaanza kunifuata kupitia hapo hapo dirishani.
Nilipofika nje, bastola mkoni, nikaangaza huku na huku Benz lao lilikuwa na watu wawili ndani mara karibu yangu nikaona gari moja lenye msichana mmoja wa Kihindi naye anataka kuwasha nililikimbilia bastola mkononi nikapitia upande wa dereva nikafungua mlango na kumwekea bastola sikioni pale na huku nikimsukuma kwenye kiti cha abiria.
"Wewe sogea huko tafadhali".
"We fanya nini mimi pana kosa wewe miji".
"Sogea nitakueleza baadaye".
Majambazi yakatuona yakatupa risasi zikaipiga gari nayo ikayumba mimi nilishikilia usukani bila ya wasiwasi nikamuonya huyo msichana wa Kihindi.
"Wewe lala chini utauawa".
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mungu mimi nafanya nini wewe, ua mimi pama kosa".
"Nyamaza!"
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment