Search This Blog

Friday, 20 May 2022

FARIDA - 1

 







    IMEANDIKWA NA : HALFANI SUDY



    *********************************************************************************



    Simulizi : Farida

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kilwa Masoko...mwaka 2014



    Alikuwa ni mwanamke mzuri sana. Mwanamke mrefu, urefu usiochukiza. Alikuwa na sura ya duara. Nywele zake alikuwa amezikata vizuri ndogondogo. Alikuwa na umbo zuri lililotenganeshwa na kiuno chembamba. Kifuani, alibeba maziwa madogo ya duara. Tumbo dogo, yale wayabebayo walimbwende. Chini, alikuwa na mapaja ya haja. Mapaja manene yanayojaa vyema katika suruali. Alikuwa na miguu minene. Miguu iitwayo ya bia. Alikuwa anatembea kwa mwendo wa madaha. Huku akiacha mwili wake unatikisika vizuri sana kwa nyuma.



    Hizo ni sifa chache sana za mwanamke niliyokuwa namsubiri. Sikuwa na miadi nae. Nilikuwa namsubiri apite tu ili nimuone.

    Hakuwa mpenzi wangu.

    Sikuwa namjua kwa jina.

    Sikuwa najua anapokaa.



    Sikwenda kazini ili nimuone mwanamke ambaye nilitokea kumhusudu sana. Mwanamke aliyetokea kuuteka moyo wangu ghafla. Kuzimeza fikra zangu.

    Cha ajabu. Saa saba sasa hakuwa amepita. Alikuwa na kawaida ya kupita kila siku, saa tatu asubuhi, leo hii saa saba alikuwa bado hajatokea.



    "Amepatwa na nini? Mbona mpaka sasahivi hapiti? Au anaumwa? Au amesafiri?

    Au leo amepita asubuhi sana..



    Siku yoyote atakayopita lazima nimueleze jinsi ninavyoumia juu yake. Nimueleze nia yangu ya dhati ya kutaka kuwa nae. Awe wangu. Nimueleze kama ninampenda kuliko mwanamke yeyote yule hapa duniani. Nimueleze kuwa nataka kuishi na yeye milele. Nataka kuwa sehemu ya maisha yake, awe sehemu ya maisha yangu. Nataka anikaribishe katika moyo wake, niweke kambi. Tena kambi ya kudumu..."



    Nikiwa katikati ya mawazo mara nilimuona akija. Moyo uliniripuka kwa furaha.

    Alikuwa amependeza kuliko siku zote.



    Alikuwa amevaa suruali ya jinsi ya pinki. Blauzi nzuri yenye mistari meupe na meusi, rangi iliyofanana na mnyama pundamilia. Mkononi alikuwa amebeba kibegi kidogo cheupe. Alikuwa anatembea kwa madaha kuja pale nilipokuwa nimekaa.



    Nilinyanyuka huku nikisema "Samahani dada"



    Alisimama huku akiuliza kwa sauti ndogo " Unaniita mimi?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilianza kumsogelea taratibu huku nikijibu "Ndio"



    Leo ndio nilipata nafasi ya kuisikia sauti yake. Alikuwa na sauti nzuri mno. Sauti isiyo kera masikioni. Ilikuwa mithili ya sauti ya ndege chiriku.



    Alisimama akiwa ananisubiri. Nilimsogelea taratibu. Kichwani mawazo mengi yakishindana kichwani kwangu.



    "Samahani tena dada. Kabla sijakwambia sababu ya kukusimamisha hapa, naomba tufahamiane, mimi naitwa Nassib Omary"



    Aliniangalia kwa tuo. Alinipandisha chini-juu. Kama alikuwa anathaminisha thamani ya kila kitu nilichovaa. Akabinua mdomo kidogo kwa juu. Akasema " Naitwa Farida.."

    Akaanza kuondoka.



    Nilimshika mkono. " Sasa mbona unaondoka Farida. Nilisema tutambuane kisha ndo nikueleze sababu ya kukusimamisha. Samahani sana lakini"



    Farida alisema huku akifanya harakati wa kutoa mkono wake nilioushika imara "Nimechelewa sana leo. Naomba nitafute muda mwengine"



    Niliendelea kumshika " kwani unaenda wapi? Unajua kila siku nakuona unapita hapa, unaenda wapi?"



    "Subiri nikupe business card yangu. Nimechelewa sana yaani kaka. Tutawasiliana."



    Aliutoa mkono wake niliokuwa nimeushika. Akafungua zipu ya pembeni ya mkoba wake. Akatoa 'business card'. Alinikabidhi.

    "Tutawasiliana Nass" alisema kwa lafudhi tamu sana. Sauti itokayo puani. Zaidi, nilifurahia sana kwa jinsi alivyofupisha jina langu.



    Alianza kuondoka kwa maringo. Niligeuka kumwangalia jinsi alivyokuwa anaondoka.



    Nilikili kimoyomoyo " Farida alikuwa ni bonge la mwanamke"

    Nilitabasamu.



    Nilirudi kukaa kitini. Nilianza kuisoma 'business card' aliyoniachia Farida.



    Kulikuwa na majina yake kamili. Namba yake ya simu. Barua pepe. Jina la sehemu anayofanyia kazi na mambo mengine kadhaa.



    Nikaichukua ile namba ya simu na kuinakili katika simu yangu.

    Niliiangalia jinsi namba ya Farida ilivyotulia katika simu yangu. Nilitabasamu tena.



    Nilienda kazini. Mimi nilikuwa ni daktari katika hospitali binafsi ya Bakwata. Mwaka wa pili sasa tangu nihitimu masomo yangu ya fani ya utabibu katika Chuo kikuu cha Muhimbili.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipomaliza masomo mwaka 2012 niliamua kurudi nyumbani ili kuwasaidia watu wa nyumbani kwetu. Nilifika ofisini na kuegemeza kichwa changu katika meza. Nikimuwaza Farida.



    Nikiwa katikati ya mawazo. Ghafla nilistuka baada ya mlango wa ofisi yangu kusukumwa kwa nguvu.

    Alikuwa ni nesi Rehema.



    Kwa sauti kubwa alisema " Ajari! Dokta kuna mgonjwa kapata ajari ya bodaboda. Yaani ameumia sana Doktaa"



    Sikumjibu. Nilibeba vifaa vyangu vya kazi harakaharaka. Nikaelekea chumba cha mapumziko. Nesi Rehema alikuwa mbele akikimbilia huko. Nami nilikuwa namfuata nyuma kwa kasi.



    Tulipofika tu chumba cha mapumziko. Nilimuona.



    Nilichanganyikiwa hasa.



    Nilianza kuiona suruali ya pinki. Kisha nikaiona blauzi ya Pundamilia. Sikumtaka mtabiri kunitabiria. Alikuwa Farida. Farida ndiye alikuwa mgonjwa.



    Nilisogea taratibu pale kitandani. Farida alikuwa analia kwa sauti. Analia, anataka kunyanyuka, nesi Hasna alimdhibiti.



    Nesi Hasna alisema baada ya kuniona " Amevunjika Dokta. Amevunjika mguu"



    Sauti ya nesi Hasna ilikuwa inasikika kwa mbali sana. Sauti yake ilimezwa na kilio cha Farida. Kilio cha maumivu.



    Nilimsogelea. Alinitambua. Alilia kwa nguvu "Nass nakufaaa, Nass nakufa mimi mwenzio. Nimevunjika mguu. Nimeumia mgongoni. Nakufa mimi. Naomba unisaidie"



    Niliongea taratibu, huku nikimpa huduma ya kwanza " Pole sana Farida. Utapona."



    Nesi Hasna na Nesi Rehema walibaki midomo wazi. Walishangaa kujua kwamba nilikuwa nafahamiana na Farida.



    *****



    Wiki moja baadae. Farida alikuwa na plasta gumu katika mguu wake wa kulia. Nilijitahidi kwa kadri niwezavyo kuhakikisha nampa huduma kwa kiwango cha juu. Hadhi inayostahili.



    Hakuumia sana kama nesi Rehema alivyonitaarifu awali. Alivunjika mguu. Lakini dereva wa bodaboda aliyekuwa kampakia alikuwa kaumia vibaya sana. Alipewa rufaa na kupelekwa hospitali ya mkoa wa Lindi. Hospitali ya Sokoine.



    Nilikuwa daktari wa Farida. Nilikuwa muuguzi wa Farida. Nilikuwa ndugu wa Farida. Tangu kaumia hakuja ndugu yake yeyote kumwangalia. Mara zote nilipomuuliza kuhusu ndugu zake hakutaka kabisa kuongelea. Alikuwa anasononeka tu.



    Nilikuwa ni mtu wa karibu sana wa Farida. Alinizoea. Nilimzoea. Tulizoeana. Ukaribu wangu na Farida ulikuwa ni kitu nilichokuwa nakihitaji sana, nakipenda. Muda mwingi nilikuwa nashinda katika wodi namba mbili. Wodi aliyokuwa amelazwa Farida. Ukaribu wangu kwa Farida ulinifanya nizidi kumpenda. Nilikuwa naisubiri kwa hamu siku ambayo nitapata nafasi ya kumueleza Farida kuwa nilikuwa nampenda sana.



    Nakumbuka ilikuwa siku ya jumapili. Mwezi wa tatu tangu ile ajari ya pikipiki aliyoipata Farida. Sasa alikuwa ametolewa plasta ngumu mguuni. Alikuwa anatembea ingawa kwa kuchechemea kwa mbali.



    Jumapili hiyo ilitukuta tukiwa katika ufukwe pwani ya Jimbiza. Farida alikuwa amevaa pensi fupi ya kaki, yenye mifuko pembeni, na tisheti nyeupe ikiwa na maandishi mawili yaliyoandikwa kwa rangi nyeusi..CK. Chini alivaa raba safi nyeupe, nazo zilikuwa na maandishi meusi ya CK pembeni. Kichwani alikuwa amevaa kapelo nyeupe iliyomkaa vema. CK ni maandishi yaliyosomeka mbele ya kofia hiyo. Farida alikuwa amependeza sana.



    Mimi, nilikuwa nimevaa traki nyeusi ikiwa na ufito mweupe pembeni. Juu, nilivaa fulana nyeupe yenye maandishi meupe mbele ya fulana hiyo. Yalisomeka..Reebok. Chini nilivaa viatu vya wazi vya kimasai.



    Tulikuwa tumeshikana mikono na Farida. Tukitembea ufukweni kwa furaha. Ilikuwa mithili ya mtu na mchumbawe.



    Tulifika sehemu safi. Tulikaa chini. Nilipanga kuitumia siku hiyo, muda huo, kumueleza Farida juu ya hisia zangu za moyoni.



    Niliianza kwa kumuita "Farida"



    Farida aliitika kwa sauti laini. Ya kudeka. "Abee Nass.."



    "Hivi ni rangi gani uipendayo hapa duniani?" Nilimuuliza taratibu.



    Alijibu bila ya kufikiria "Pinki"



    Nilimuuliza tena " Tunda gani ulipendalo hapa duniani?"



    Harakaharaka alisema " Apple"



    Niliingiza mkono wangu mfukoni. Nilitoa zawadi. Nikampa. Alilifungua akiwa na furaha tele. Ilikuwa ni zawadi aipendayo ikiwa katika kitambaa chenye rangi aipendayo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nass jamani. Ulijuaje? Ahsante sanaa" Alisema huku akinikumbatia.



    Nilimpa zawadi ya apple. Ikiwa nimeiviringisha katika kitambaa safi cha pinki.



    "Farida" Nilimuita tena.



    "Abee" Aliitika huku akiniangalia usoni kwa macho yake mazuri.



    Nilimwambia " Kuna kitu ninataka kukwambia"



    "Kitu gani hiko Nass?" Alisema huku akinifuta mchanga shavuni.



    Nikamtoa mkono shavuni kwangu. Nikainuka. Nikainyoosha mikono yangu. Akaishika imara. Nilimnyanyua. Tukawa tumesimama wima tunaangaliana. Macho yetu yaligongana. Aliona aibu. Akainama chini.



    Nikamgeuza nyuma. Ikawa yeye mbele, mimi nyuma. Tukawa tunatembea taratibu kuelekea majini. Tulienda hadi katika maji. Miguu yetu ilizama kidogo majini. Nikamsogelea kabisa. Kifua changu kiligusana na mgongo wake. Niliinama kidogo, mdomo wangu niliusogeza sikioni kwake. Nilinong'ona kwa sauti ndogo sana.



    "Farida, samahani sana kwa ninachotaka kukwambia. Ni jambo nililokaa nalo moyoni mwangu siku nyingi sana. Ni jambo linaloutesa sana moyo wangu"



    Farida alikuwa amefumba macho. Akisikiliza kwa makini sana sauti yangu, huku akihisi vizuri pumzi zangu "ni Jambo gani hilo Nass likusumbualo?



    Niliendelea " Ukweli ni kwamba nimetokea kukupenda sana Farida. Umbo lako, sauti yako, tabia yako, kwa pamoja vimejenga huba kwangu. Moyo wangu umekutunuku. Farida umetamalaki katika moyo wangu, katika fikra zangu. Nakupenda Farida. Nakupenda kwa maana sahihi ya upendo. Upendo wa dhati. Nipe moyo wako niuhifadhi, niutunze, niulee. Naomba uwe wangu Farida, niwe wako. Nikupende, unipende, tupendane. Tupendane kwa dhati. Nakuomba Farida, kubali uwe wangu..."



    Farida aligeuka taratibu kuniangalia. Aliitazama sura yangu. Nilimwangalia. Nilikuwa natokwa na machozi. Nalia. Machozi ya upendo.



    "Sasa Nass kwanini unalia? "



    "Nalia kwa sababu NAKUPENDA SANA FARIDA"



    Nilijiona nimeutua mzigo, mzito sana. Mzigo nilioubeba katika moyo wangu takribani miezi minne. Mzigo uliokuwa unanitesa usiku. Unanitesa mchana.



    Macho yangu yalionesha kuwa nilikuwa nampenda sana Farida. Nilikuwa namwangalia Farida kwa jicho la upendo, jicho la huba, jicho la nihurumie mwenzio, jicho la Wallah nakupenda sana.

    Sitanii.

    Sidanganyi.

    Siongopi.



    Baada ya sekunde kadhaa za ukimya. Niliisikia sauti niipendayo. Sauti ya Farida. " Napenda sana nikupende. Lakini siko tayari kukupenda. Naomba, tuendelee kuwa marafiki. Tuendelee kuwa mtu na daktari wake. Mtu na mgonjwa wake..."



    Hakumaliza. Nilikiweka kidole changu cha shahada juu ya midomo yake. Aliacha kuongea.

    Kwa sauti ya kwikwi nilisema " Unapenda unipende lakini hauko tayari kunipenda? Unamaanisha nini? Kwanini usikipende kitu ukipendacho? Kwanini upende kunipenda? Lakini usipende kunipenda?"



    Alikitoa kidole changu cha shahada juu ya mdomo wake, aliongea kwa sauti ya taratibu



    "Nass, ipo siku utaelewa maana ya maneno yangu. Bado mapema sana kwa sasa"



    Nilibaki nimekodoa macho. Nikiwa siamini kama Farida alikuwa amenikataa. Siku zote niliamini katu Farida hawezi kunikataa, kwa ukarimu niliomfanyia.



    Pamoja na kumuuguza mimi pindi alivyoumia. Kumtibia mimi tena kwa gharama zangu. Kumpa mazoezi hadi kuhakikisha anakuwa sawa kiafya na kiakili, kwa muda wangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilifanya vitu zaidi ya hapo. Farida akawa rafiki yangu wa pekee. Tulishirikiana mambo mengi sana. Tulitoka 'out' pamoja mara kadhaa. Tulienda disco. Tulienda sinema tulivyojisikia.

    Tuliwasiliana sana.



    Sikuamka bila kumtakia asubuhi njema. Sikula bila kumkaribisha chakula. Sikulala bila kumtakia usiku mwema. Mara kadhaa nilimchokoza kwa kumuita baby katika meseji, naye bila kusita alijibu honey. Nikajua nimemteka. Nikajua nimemlevya. Nimelamba dume. Hawezi kunikataa.

    Lakini haikuwa hivyo.

    Farida alikataa, tena katakata.



    Siku ile tuliachana saa kumi na mbili jioni. Huku jibu la Farida likiwa lilelile. Hataki kuwa na mimi.



    *****



    Zilipita wiki zipatazo mbili. Baada ya jumapili ya kumueleza hisia zangu Farida. Tulikuwa tumeonana mara mbili tu baada ya siku ile. Nilijaribu kumkumbushia Farida mara kadhaa kwa meseji na wakati mwengine kwa kumpigia simu, lakini bado alibaki na msimamo wake.

    Mwishowe nikakubali kuwa nilikuwa nimekataliwa.



    Ilifika jumapili nyingine. Niliamua kwenda ufukweni mwa bahari peke yangu. Nilikaa ufukweni mwa bahari. Upepo mwanana ukinipuliza. Mkononi nilishika kitabu cha riwaya mzuri ya mapenzi, inaitwa MKASA. Kitabu makini kilichoandikwa na nguli wa riwaya za mapenzi Tanzania, Fadhy Mtanga.



    Nilisisimka sana na mkasa wa mapenzi uliomkuta Jane katika riwaya hiyo. Niliusifu umahiri wa Jane, niliukubali ujasiri wa Jane. Nilifurahia upendo wa dhati aliokuwa nao Abdul. Nilikuwa nasoma meseji ya Abdul aliyomtumia Jane katika riwaya hiyo...



    "..... Jane mpenzi wangu, katika hali yoyote ile. Ninakuahidi, sitompenda mwanamke mwingine yeyote kwa nafasi yako. Mapenzi yangu kwako hayana kifani. Hayapimiki. Hayana mbadala. Nimebahatika duniani kupendwa nawe. Nitalienzi penzi lako siku zote za maisha yan......”



    Sikumaliza kusoma ujumbe ule, mbele yangu alikuwa amesimama mtu...





    Niliinua sura yangu. Nilikuwa natazamana na Farida.



    Aliongea huku akiwa kaniinamia " Nass una tabia mbaya sana, siku hizi unakuja beach peke yako. Hupokei simu zangu. Hujibu sms zangu. Mbona umebadirika hivi Nass?"



    Nilifunika kitabu changu, nikasema. " Sina tabia mbaya Farida. Natamani sana kutoka na wewe ila nilihisi labda huienjoy kampani yangu. Hufurahii kuwa karibu na mimi. Kuhusu simu zako mbona napokea siku zote. Lini sijapokea simu yako Farida?"



    " Nimekupigia zaidi ya mara tatu nusu saa tu iliyopita. Hujapokea.



    Alirembua kidogo. Akang'ata papi zake za midomo kisha akasema "Nass, lini nilikwambia siienjoy kampani yako? Wewe ndiye rafiki yangu pekee hapa Kilwa, na bila shaka rafiki yangu wa pekee hapa duniani. Napenda sana kampani yako. Napenda sana kuwa karibu na wewe. Na sitoacha kupenda..."



    "Kuhusu simu, kumbe ulinipigia sahivi. Nimemute simu ili nipate wasaa wa kusoma hiki kitabu. Nimevutika sana na hii riwaya ya Mkasa."



    Farida alionekana kunielewa. Alikaa ubavuni mwangu na kuanza kuongea mambo mengine.



    Alichukua kitabu mapajani mwangu huku akiongea " Kaandika nani hiki kitabu?"



    "Fadhy Mtanga" Nilimjibu.



    "Si nd'o yule aliyeandika riwaya ya Huba?" Aliuliza.



    "Ndio. Huba, Kizungumkuti, na hii Mkasa, zote kaandika yeye" Nilimjibu.



    "He is my favorite writer. Nilimpenda sana katika Simulizi yake ya moja ya kuitwa Fungate. Yaani alinitaharuki mwanzo mwisho"



    Simu ya Farida iliita.



    Alikiweka chini kitabu cha riwaya ya Mkasa, akaipokea.



    "Mimi niko poa"



    "Umempata wakili gani sasa?"



    "Wakili Hamidu yuko vizuri"



    "Sawa, tutaongea vizuri jioni"



    Baada ya mazungumzo ya simu nilidhani Farida atanambia habari kumhusu wakili. Lakini Farida hakuzungumzia kabisa.



    " Eeeh Nass leo weekend ratiba yako ipoje usiku?"



    Kiunyonge nilijibu "Nitakuwa home tu. Si unajua jumapili. Tomorrow job"



    Alinipigapiga mgongoni huku akiongea " Basi naomba unisindikize sehemu Nass"



    " Sehemu gani Farida? " Nilimuuliza.



    "Nataka kwenda kumuua mtu leo usiku!" Farida aliongea kwa sauti kavu. Ya kujiamini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilistuka. Nilimuangalia usoni. Aliniangalia bila ya kupepesa macho.



    "Kuua?" Nilimuuliza.



    "Kumuua mtu!" Alirudia.



    Nilituliza akili. Nikakaa sawa. Nikamuuliza " Unataka kwenda kumuua nani? Na kwanini umuue?"



    Farida aliangalia baharini dakika kadhaa, akaongea " Nataka nikamuue mjomba wangu"



    "Sababu?" Nilimuuliza.



    "Kabla sijakwambia sababu niahidi utanisaidia"



    Niliwaza. Alikuwa amenipa mtihani mkubwa sana. Sikuwa msomi wa sheria lakini nilikuwa nafahamu kwamba kushiriki kumuua mtu ni kosa la jinai.

    "Nikubali. Nikatae" Nilijiuliza kimoyomoyo.



    Niliongea kwa sauti ya utaratibu

    " Farida naweza kukusaidia usiue"



    "Nimeomba unisaidie kuua. Sijakuomba unisaidie nisiue" Alinijibu kwa kujiamini.



    "Kwanini unataka kumuua mjomba wako?" Nilimuuliza.



    "Kwasababu kanifundisha chuki. Siku zote nilizokaa nae alikuwa ananifundisha chuki badala ya kunifundisha upendo. Tangu mtoto amekuwa na kazi ya kunijaza chuki moyoni mwangu. Amenifanyia vitendo vingi vya chuki. Na mimi nataka nikamuoneshe kwamba nimekubuhu katika elimu ya chuki aliyonifundisha. NATAKA NIKAMUONESHE!"



    "Amekufundisha chuki badala ya upendo? Kivipi?" Nilijitutumua kumuuliza. Sauti yangu ilijaa woga.



    "Unaijua chuki Nass? Ngoja nikusimulie kisa hiki utaelewa maana sahihi ya neno chuki....



    Ni hivi, miaka kumi na moja iliyopita, katika mji wa Gairo mkoani Morogoro kulikuwa na familia moja. Ilikuwa ni familia ya watu watatu. Baba, mama na mtoto wao mmoja.



    Familia hiyo, ilikuwa ni miongoni mwa familia zinazojiweza huko Gairo. Baba wa familia alikuwa ni mhasibu katika benki ya makabwela ya NMB. Mama wa familia alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa mwenye kumiliki maduka makubwa ya nguo na saluni kadhaa za kike.



    Mtoto wao wa pekee alikuwa anasoma kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kilakala.



    Ilikuwa ni familia yenye ukwasi. Ukwasi ulioifanya familia hiyo iwe na furaha wakati wote. Furaha siku zote.



    Unawajua binadamu Nass? Farida aliniuliza.



    " Nawajua" Nilijibu kwa mkato.



    Aliendelea " Nahisi huwajui binadamu Nass. Ngoja nikwambie kitu kuhusu binadamu...



    Binadamu ni viumbe wa ajabu sana. Wanaweza kukuchekea hadi jino lao la mwisho. Kumbe moyoni mwao wana hasira na wewe. Wana chuki na wewe. Wana wivu na wewe. Wana husda na wewe. Wana kinyongo. Wana hasira. Hawakupendi. Hawapendi mafanikio yako. Wanapenda usifanikiwe. Hawapendi familia yako. Tena bahati mbaya zaidi binadamu hao wanaopenda uwe na balaa wanaweza kuwa ndugu zako. Ndugu wa damu.



    Na katika familia hiyo ya Gairo iliingiliwa na chuki za binadamu. Tena mjomba wa familia. Kaka wa mama wa familia. Ndiye alikuwa mwiba. Mwiba mkali.



    Alimuua kwa kisu baba wa familia hiyo huku mwanawe akimshuhudia, alimuua mtu ambaye ni shemeji yake. Alimuua kwa sumu mama wa familia hiyo, ambaye ni dada yake. Baba mmoja, mama mmoja. Sababu kuu, tamaa ya mali.



    Yule mtoto alipotimiza siku ya saba ya uyatima, alibakwa, alilawitiwa na kufukuzwa ndani ya nyumba ya wazazi wake. Alifanyiwa hayo na yuleyule mjomba wake. Tena mchana wa saa saba. Jua la utosi.

    Yule mtoto mdogo toka katika familia iliyo bora akageuka kuwa mtoto wa mtaani.



    Nikuulize swali Nass, hivi unadhani mtoto huyo atakuwa na nini juu ya mjomba wake? Upendo ama Chuki?"



    Nilikaa kimya. Sikujibu.



    Farida aliniangalia usoni.." Dokta unashindwa kujibu swali dogo kama hilo?"



    "Obvious atatengeneza chuki, lakini..." Nilikuwa najibu, alinikatisha.



    " Hakuna cha lakini Nass. Chuki ni chuki haina cha lakini. Halafu nikwambie sifa mojawapo ya chuki, chuki hudumu milele moyoni. Hukua kama mtoto mdogo akuavyo. Mateso yanapoongezeka na chuki hukomaa na hasira hushamiri kwa yule chanzo cha yote. Chanzo cha chuki. Kwa maana hiyo yule mtoto wa Gairo chuki yake ilikomaa dhidi ya mjomba wake".



    Nilimwita " Farida"



    Hakunisikiliza. Hakuitika " Ngoja nikwambie matokeo ya chuki Nass. Siku zote chuki hutengeneza roho mbaya ambayo huzalisha kisasi. Chuki na kisasi ni ndugu. Ndugu wa damu. Ndugu wa baba mmoja, mama mmoja. Alianza kuzaliwa chuki, uzao wa pili akafata kisasi. Kwa yeyote aliyekusababishia chuki huzaliwa kisasi dhidi yake.



    Ukiwa na kisasi na mtu hakitoki haraka. Labda umsababishie huyo mtu maumivu sawa na aliyokusababishia wewe, au zaidi.



    Sasa Nass, huyo mtoto aliyeuliwa wazazi wake wote wawili akishuhudia, aliyebakwa na mjomba wake na kufukuzwa nyumbani kwao saa saba ya mchana. NI MIMI, FARIDA. Na huyo mjomba mbakaji nd'o huyo ninayeomba msaada wako twende tukamuue leo!"



    "Pole sana Farida lakini ukishamuua huyo aliyekusababishia chuki unadhani ndio chuki yako kwake itakwisha?" Nilimuuliza.



    "Chuki haitokwisha. Najua nitaichukia maiti yake, nitalichukia kaburi lake, nitakichukia kizazi chake. Lakini itakuwa nimelipa kisasi. Nitajisikia furaha kwa kumuua aliyenisababishia chuki ndani ya moyo wangu"



    "Farida, kwani shida yako hasa ni nini? Kuiendeleza chuki kizazi kwa kizazi ama kulipa kisasi ambacho kitaendeleza visasi? Ulisema chuki hudumu milele, basi nikwambie kisasi hakina kikomo, unalijua hilo" Nilimuuliza.





    " Shida yangu nina chuki, hivyo nataka kulipa kisasi!". Alijibu kwa hasira.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Ila umekubali kwamba kisasi hakiondoi chuki?"



    "Kinapunguza…." Alijibu kwa mkato.



    "Sasa ukimuua mjomba wako, unajua vyombo vya dola vitakuhusu?"



    "Usihofu. Nimeshaandaa wakili, waakili mahiri, wakili Shaweji Faki atatutetea". Alijibu kwa kujiamini.



    “Unafahamu kwamba kuua ni dhambi?. Dini zote duniani zinakataza kuua. Ila kitu kingine kibaya ni hiki, sasahivi wewe una kisasi na mjomba wako, ila utakapomuua lazima watoto wa mjomba wako watakuwa na kisasi na wewe na kizazi chako. Kisasi hakijawahi kufika mwisho. Kisasi hakina mwisho. Sumu ya kisasi ni mbaya sana pengine kuliko sumu ya chuki. Sumu ya kisasi hutembea kizazi hadi kizazi. Njia sahihi ya kukimaliza kisasi ni kusamehe. Kwa maana hata ukimuua mjomba wako haifuti ukweli kwamba aliwaua wazazi wako. Alikubaka. Alikufukuza. Zaidi utakuwa umejitafutia matatizo na vyombo vya dola na kisasi kipya kitakufuata popote uendapo" Nilimueleza kwa kirefu.



    Alinigeukia, akatabasamu huku ananiuliza "Hivi umewahi kuwa na mpenzi Nass?" Nilibabaika. Sikumuelewa. Swali lake halikuwa katika yale tuliyokuwa tunayoongea awali.



    Baada ya kufikiria kwa muda kidogo nilimjibu "Nimewahi kuwa na mpenzi…".



    "Kwanini mliachana?. Hivi mwanamke anawezaje kumuacha mwanaume smart kama wewe?"



    "Alinisaliti" Nilimjibu kwa mkato.



    "Pole sana Nass, ilikuwaje?"



    "Ni kumbukumbu mbaya kabisa ku’experience katika maisha yangu. Sipendi hata kuikumbuka. Sipendi kuisimulia. Huwa inaniumiza sana"



    "Pole sana Nass. Kila kitu duniani hutokea kwa sababu. Kwangu, usaliti wa mapenzi ni miongoni mwa mambo madogo sana yaliyonitokea. Nakumbuka niliapa sitokuja penda tena…"



    Nilimkatisha kwa swali "Kwani sasahivi umependa?"



    "Swali gumu hilo Nass. Hebu nisimulie jinsi ulivyosalitiwa bwana, au unaona aibu?" Farida aliniuliza huku akicheka.



    "Mwenzio nililia Farida. Nilimkuta jamaa juu ya kifua cha mke wangu. Katika nyumba yangu. Katika chumba changu. Katika kitanda changu. Ndani ya shuka langu. Daaah nililia kama mtoto mdogo"



    "Ilikuwa lini? Na wapi? Ni nani huyo mwanamke" Farida maswali yalimtoka mfululizo.



    "Miaka mitano sasa imepita, kipindi kile nipo mwaka wa mwisho chuo. Ilikuwa Magomeni Dar es salaam"



    "Mlikuwa mnakaa karibu na shule ya msingi Magome..."



    Nilimkatisha "ndio..ulisikia nini hiyo story?"



    "Kumbe mchumba’o nd'o alifumaniwa na Nassoro?" Aliniuliza macho yamemtoka pima.



    "Nipo tayari kuchagua kifo ikibidi, kuliko kukuacha wewe Farida. Nakupenda kwa maana sahihi ya neno nakupenda linavyomaanisha….”.



    Na hii ni sehemu ya nne..



    Miaka mitano sasa imepita, kipindi kile nipo mwaka wa mwisho chuo. Ilikuwa Magomeni Dar es salaam"



    "Mlikuwa mnakaa karibu na shule ya msingi Magome..."



    Nilimkatisha "ndio..ulisikia nini hiyo story?"



    "Kumbe mchumba’o nd'o alifumaniwa na Nassoro?" Aliniuliza macho yamemtoka pima.



    "Farida, unamfahamu yule mwanaharamu? Nilipokaa nae mchumba’ngu alinambia yule jamaa alikuwa anaitwa Nassoro. Halafu zilibaki siku tatu tu ujue ili tuoane na Fatma?" Nilimwambia.



    "Nass, Nassoro alikuwa mume wangu wa ndoa…" Farida aliongea huku macho yake yakilengwa na machozi.



    "Unasema kweli Farida?" Nilimuuliza kwa wahka.



    "Baba yake Nassoro ndiye aliyenitoa katika uchokoraa hadi kuwa mtu. Ni yeye aliyenitoa toka katika uchangudoa na kunileta kuwa mtu, mtu safi. Mtu mwenye heshima. Alinitoa jalalani na kunipeleka hekaluni, kwenye maisha bora. Hakunipenda bure mzee yule. Nilimuonesha uaminifu mdogo tu, ambao yeye aliuthamini sana.



    Nilimsaidia kuipata laptop yake baada ya kuibiwa na vibaka sokoni Kariakoo. Niliwashuhudia vibaka wakati wanavunja kioo cha gari yake. Niliwajua wale vijana. Nikaongea nao. Walikubali kurejesha laptop kwa malipo. Baba yake Nassoro alilia kama mtoto mdogo siku niliyomkabidhi laptop yake. Hakuamini. Bila shaka ilikuwa ni kila kitu kwake.



    Siku tatu baadae alikuja tena Kariakoo. Alinitafuta hadi akanipata. Akanichukua. Toka siku hiyo nikahamia kwake. Nikawa naishi kwake. Huko ndiko nilipokutana na Nassoro. Mtoto wake wa kwanza wa kiume. Kipindi hiko Nassoro alikuwa anasoma sheria pale chuo kikuu cha Dar es salaam. Alikuwa anaenda chuo na kurudi nyumbani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Miezi mitatu baadae tuliingia katika uhusiano wa siri wa kimapenzi na Nassoro. Ukweli ni kwamba nilimpenda, alinipenda. Na kwa bahati nzuri baba hata alipofahamu aliubariki uhusiano wetu. Aliupenda.



    Upenzi ukakomaa, ukaja uchumba, miaka miwili baadae, tulioana.



    Nakumbuka nilikaa saba, kama ilivyo desturi za kiafrika. Nassoro alinipa mapenzi yote ndani ya siku saba za awali za ndoa yetu. Nilipotoka saba tu na vituko vilianzia hapo. Nass, nakwambia nili’enjoy ndoa yangu siku saba tu za awali. Siku ya nane vilianza vipigo tena bila sababu za msingi. Hakunipenda toka siku ile ya nane. Nilishangaa hata kwanini alinioa. Yaani hadi leo bado najiuliza. Kuanzia hapo ndipo nikaijua tabia sahihi ya Nasoro. Alikuwa malaya. Alikuwa mpigaji. Alikuwa mlevi. Hajali. Jeuri. Nilimvumilia hadi siku niliyosikia alikamatwa baada ya kufumaniwa na mwanamke huko Magomeni shule. Na yeye akalawitiwa...



    Hivi ilikuwaje kwani Nass?" Farida aliniuliza.



    "Hadithi ndefu sana. Lakini la umuhimu nikwambie kwamba hivi sasa Fatma ameolewa na Nassoro"



    "Nalijua hilo…" Farida alijibu kwa upole.



    "Sasa unataka kujua nini hasa?"



    "Ilikuwaje mpaka Nassoro akalawitiwa?"



    "Ni vijana tu wa Magomeni ndio walimfanyia hivyo. Hawakuridhika na vitendo alivyokuwa ananifanyia. Nilikuwa naishi nao vizuri sana. So’ wakamfanyia hivyo ili kupunguza hasira zao"



    "Maajabu, hii ni simulizi ya mapenzi. Simulizi ya mapenzi ya pande mbili zilizokuwa na mahusiano kabla, kisha kubadilishana. Wahusika wa simulizi hii ni wenye mfanano wa herufi za mwanzo za majina yao. Nassib na Farida. Nassoro na Fatma. Yaani wao wameoana na sisi tumekutana, tu marafiki. Marafiki wa kweli. Watu wenye mfanano wa historia. Historia zetu ni sawa Nass. Na tumeumizwa na watu ambao sasa wameoana."



    Nilipendezwa sana na maneno ya Farida. Nikamuuliza "Nikuulize kitu Farida?"



    "Niulize Nass" Alijibu huku akiniangalia usoni. Nami nilimwangalia. Ingawa giza lilikuwa limeanza kushamiri lakini niliuona vizuri uso wa Farida. Ulikuwa uso wa kipole. Uso uliobeba mashavu yenye kubonyea achekapo. Uso mzuri sana. Uso wa mwanamke nimpendae. Mwanamke wa ndoto yangu. Mwanamke wa maisha yangu. Roho yangu. Kila kitu kwangu. Nilizidi kumpenda Farida kila sekunde nimtazamayo.



    "Can u marry me Farida?" Nilimuuliza kwa sauti ndogo aliyoisikia vyema.





    Farida alistuka kidogo kwa swali langu. Akaniangalia usoni. Tukaangaliana " Nass, sio rahisi kama unavyofikiria"



    "Kwanini Farida?" Nilimuuliza.



    "Nass, humfahamu Nassoro wewe. Sio mtu yule..Nassoro ni Rick Ross"



    "Sio muda wa kumfikiria Nassoro huu. Yeye kashaoa. Kwanini nawe usiangalie mbele. Unataka usisonge mbele kisa Nassoro. Give me a chance in your heart Farida. Na hakika nitakufuta kumbukumbu zote mbaya ulizowahi kuzipitia katika maisha yako. Nikabidhi mimi shida zako Farida, hakika nitakufanya mwanamke mwenye raha kuliko wote chini ya jua. Nitakupenda pasi na kifani, nitakujari, nitakuheshimu, nitakutunza, nitakulinda, nitakulea mithili ya mtoto mchanga. Nitahakikisha unakuwa na furaha siku zote za maisha yako. Nipe moyo wako Farida, niuoneshe jinsi ninavyojua kupenda. Hutosikia msamiati wa usaliti kwangu. Nakupromise Farida"



    Farida aliangalia juu. Alikuwa anafikiria. Aliongea huku akiingalia mbingu " Nassoro hakuniacha. Nilimuacha. Hadi kesho Nassoro bado anataka turudiane. Alinisumbua sana nilipokuwa Dar na hiyo ni miongoni mwa sababu ya kuamua kuhamia huku, sababu nyingine ni kuwa karibu na mjomba wangu muuaji. Ambaye alihama Gairo na kuhamia huku. Ilinipasa nami nije huku ili nisipate shida siku nitakayoamua kumuua.



    Pamoja kwamba nipo huku lakini bado Nassoro ananifatilia. Sijui hata nani alimwambia kama nipo huku. Siku ileeee, siku ya kwanza kukutana na wewe, unakumbuka? ile siku ya kupata ajari ya pikipiki. Ile ajari sababu alikuwa ni Nassoro" Alishusha sura yake chini.



    Nilistuka sana. Katika yote hili sikulitegemea " Sijakuelewa Farida"



    Aliendelea " Unajua siku ile nilichelewa sana kuamka. Nilikuwa najisikia vibaya. Mida ile nilikuwa naelekea saluni kwangu. Njiani nilikutana na Nassoro akiwa ndani ya gari jeusi. Aliniita kwa mkono akiwa garini. Nilipuuza.



    Nilivyoondoka alianza kunikimbiza kwa gari yake, Range Rover Nyeusi. Nilikimbia hadi stendi. Nikakodi pikipiki na kuendelea kukimbia. Aliendelea kunifukuza na gari yake.



    Tulivyofika Kisangi dereva wangu aliyumba.

    Tukaanguka.

    Nassoro alikuja kwa kasi na kutaka kutugonga. Mimi nilimuona. Nilijirusha pembeni ya barabara na kutua vibaya kwa kutumia mgongo. Dereva pikipiki alichelewa, aligongwa mguuni, na Rick Ross aliondoka moja kwa moja"



    "E bwana wee. Kumbe nd'o chanzo cha ile ajari yako?"



    "Ilikuwa hivyo Nass. Na tangu siku ile Nassoro hajaacha kunifatilia. Lengo lake kuu likiwa ni kuniua. Mimi kwasasa ni adui wa Nassoro, tena adui mkubwa sana. Siku tukiingia katika mahusiano na wewe, na akijua kwamba wewe ulikuwa mchumba wa Fatma, halafu ajue kwamba we ni mtu uliyesababisha alawitiwe. Vita ya Nassoro kamwe hutoweza kuimudu Nass. Itakuwa ni vita vya tatu vya dunia nakwambia. Nassoro ni Rick Ross.

    Ataniua. Atakuua. Atatuua!"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nilipumua kwa nguvu. Niliuona ukweli katika maneno ya Farida. Kumbe mambo yalikuwa magumu tofauti kabisa na nikivyofikiria awali, nilisema "Sasa, naona giza linaingia. Tutafute wakati mwengine wa kuyaongelea haya. Kwasasa naona turejee nyumbani"



    "Sawa Nass" Alijibu kwa mkato.



    Tukiwa tunanyanyuka nilimuuliza " Na vipi kuhusu kisasi kwa mjomba wako?"



    "Nimemsamehe" Alijibu huku akijifuta mchanga wa pwani katika nguo zake.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog