Search This Blog

Friday, 20 May 2022

FARIDA - 2

 







    Simulizi : Farida

    Sehemu Ya Pili (2)



    Alinifurahisha sana Farida

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Bravo smart girl" Tuligonga mikono yetu kwa furaha.



    Tukaondoka pwani tukiwa tumeshikana mikono. Hatukuwa tofauti na wapenzi. Wapenzi wa muda mrefu.

    Nilimsindikiza Farida mpaka nyumbani kwake. Kisha nami nilirejea nyumbani kwangu.



    Usiku wa siku hiyo sikulala. Niliwaza mambo mengi sana. Maneno ya Farida yalijirudia mara kwa mara kichwani mwangu mithili ya mkanda wa sinema niupendao.



    Nilikili, Farida aliongea ukweli mtupu. Na kilihitajika kitu kimoja tu kama kweli nilikuwa nataka kuishi na Farida. Kumuoa Farida. Yalihitajika niwe na mapenzi. Mapenzi ya dhati. Mapenzi ambayo hayataweza kutenganishwa hata kitokee chochote kile.



    Hilo halikunipa shida. Nilijua jinsi ya nilivyokuwa na mapenzi ya dhati kwa Farida. Mapenzi ya kweli, lakini nilipomfikiria Nassoro. Mume wa zamani wa Farida. Nilikosa raha kabisa. Niliikumbuka sura ya Nassoro siku ile ya fumanizi. Taswira ya mwili wake ilirejea kichwani kwangu. Nassoro alikuwa na kitu....



    Nassoro alikuwa mwanaume mweusi, mrefu na mnene wastani. Alikuwa na sura pana, sura iliyonakshiwa na ndevu lukuki kidevuni hadi katika mdomo wake wa juu. Ndevu nyingi sana zilizotengeneza mtindo wa duara. Kichwani alikuwa amenyoa nywele zote, mtindo wa upara. Alikuwa na kifua kipana. Kifua cha mazoezi. Hakufanana hata kidogo na msomi wa sheria wa chuo kikuu. Alifanana na 'ma'bodyguard' ama walinzi wa mlangoni katika kumbi mbalimbali za starehe.



    Nilikumbuka jinsi nilivyokuwa namfatilia kipindi kile, baada ya kuambiwa na majirani zangu zaidi ya wanne kwamba mchumba wangu Fatma alikuwa ananisaliti.

    Anatembea na mtu mnene mwenye Range Rover nyeusi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwanzoni sikuamini hata kidogo. Nilikuwa namuamini sana Fatma wangu.

    Fatma alikuwa ni kila kitu katika maisha yangu. Hadi inafikia wiki ile ambayo ijumaa ilibidi tuoane, tulikuwa tumeishi na Fatma kama wapenzi takribani miaka mitano.

    Nilikuwa naamini kwamba namjua vizuri Fatma. Namjua nje-ndani.



    Fatma alikuwa sio mtu wa kubabaishwa katika mapenzi. Alikuwa na msimamo. Msimamo thabiti. Msimamo imara. Hakuyumbishwa kabisa katika misimamo yake, iwe katika maisha ama katika mapenzi.



    Ingawa nilianza nae uhusiano miaka mitano iliyopita, lakini nilimfahamu Fatma zamani sana. Tangu enzi anasoma shule ya sekondari Jitegemee. Ndio maana nilijiridhisha kwamba Fatma anastahili kuwa mke wangu. Mwenza wangu wa maisha. Mama wa watoto wangu. Mkwe wa mama yangu. Wifi wa dada yangu. Shemeji wa kaka zangu na marafiki zangu.

    Kumbe sikujua. Nilikuwa najua kidogo sana kuhusu Fatma. Nilikuwa siujui undani wa Fatma. Uchunguzi wangu wa awali uligonga mwamba. Niliamini sivyo kutokana na upole wa Fatma. Nilisahau ile methali maarufu ya wahenga, kwamba 'Simba mpole ndio hula nyama'.



    Nilipoambiwa kwamba Fatma anatembea na mwanaume mnene mwenye Range Rover nyeusi sikuamini kabisa. Lakini pamoja na kutoamini sikuzipuuza taarifa zile. Nipo hivyo, huwa nina tabia ya kufanya uchunguzi kabla ya kuamua. Sina pupa katika kufanya maamuzi yangu.

    Siku zote pupa haijengi, pupa hufanya ufanye maamuzi yasiyo sahihi. Nilikuwa siamui nikiwa na pupa ama hasira.



    Nilianza kufatilia nyendo za mchumba wangu Fatma kimyakimya. Mara kadhaa nilikuwa namfatilia mwenyewe. Mara nyingine nilimpa kazi hiyo rafiki yangu Saidi. Tukawa tunamfatilia Fatma bila yeye mwenyewe kujua.



    Siku tatu tu za kumfatilia tuligundua mambo mengi sana. Mambo ambayo sikuwahi kuyajua kabisa kuhusu Fatma.



    Kumbe Fatma alikuwa mwanamke mlevi sana. Alikuwa mwanamke malaya na mpenda starehe hadi pa'mwisho.



    Siku zile tatu za uchunguzi ilinifunukia kwamba Fatma alikuwa na wanaume wanne tofauti. Lakini mwanaume wake mkuu alikuwa jamaa mnene mwenye Range rover nyeusi kama nilivyoambiwa awali.



    Lakini cha ajabu pamoja na kukaa na Fatma miaka yote hiyo sikutaka kuamini kuwa Fatma alikuwa mwanamke mlevi. Mara kadhaa nilikuwa natoka nae usiku Fatma hakuwahi kutia hata tone la pombe katika mdomo wake. Siku zote alikuwa ananiambia kwamba anachukia sana pombe. Anawachukia sana walevi wa pombe. Leo hii namuona Fatma anakunywa pombe, hata wewe usingeamini.



    Niliamua kughairisha suala la kumuoa Fatma. Nakumbuka wakati nafikia uamuzi huo zilibaki siku tano tu ili tufunge ndoa. Hapo nikawa natafuta mbinu sahihi ili jamii yote ielewe kwamba tatizo sio mimi mpaka ndoa ile inafutika. Tatizo alikuwa ni Fatma...





    Ikafika siku mbaya kabisa. Siku ambayo sitokuja kuisahau katika maisha yangu. Siku ile, nilikuwa nishajua kila kitu kuhusu Fatma. Umalaya, ulevi, kupenda starehe yalikuwa ndio maisha yake.



    Nakumbuka nilimpigia simu Fatma saa tatu asubuhi, nikimtaarifu kuwa nina safari ya kwenda Bagamoyo. Hakutaka kuhoji sana lengo la safari hiyo. Aliniruhusu bila kinyongo. Kumbe sikuwa na safari yoyote. Nilipanga fumanizi !



    Saa tano usiku nilikuwa Magomeni. Tena nagonga mlango wa chumba changu. Nikiwa na uhakika kabisa Fatma yupo ndani na jamaa mwenye madevu anayeendesha Range nyeusi.



    Niligonga mara ya kwanza. Ukimya ukachukua nafasi, nikagonga tena. Kwa mbali, nilisikia watu wakiongea kwa sauti ndogo sana.



    Dakika saba baadae sijui hata watu walitokea wapi, wahuni wa Magomeni, wambea wa Magomeni, walikuwa wamejaa mlangoni kwangu. Wote wakiwa na hamu ya kushuhudia fumanizi.



    Sikuwa na jinsi, nilikaa pembeni huku nikistaajabu. Sasa walikuwa wanagonga wao mlango, tena kwa fujo. Lakini mlango haukufunguliwa.



    Jinsi walivyokuwa wanapiga makelele na mayowe ndipo ummati wa watu ulikuwa unaongezeka. Niliiona hali ya hatari. Lakini sikuwa na jinsi, sikuwa na namna ya kuzuia.



    Mlango wa chumba changu ulivunjwa. Tulimkuta Fatma na jamaa mwenye madevu wakiwa wamejikunyata ndani ya shuka. Ilikuwa ni picha mbaya sana ambayo sitoisahau kamwe katika maisha yangu. Mimi nilibaki shuhuda. Shughuli ilivaliwa njuga na majirani zangu wakishirikiana na watoto wa Magomeni.

    Waliamua. Wakawafanyia yote waliyowafanyia. Ambayo yaliwekwa mbele ya gazeti Risasi, na kuweka historia ndani ya Magomeni na jiji zima la Dar es salaam.



    *****



    Ilikuwa ni saa kumi jioni. Nilikuwa ndani ya gari yangu nikitoka kazini. Nilikuwa naendesha taratibu huku nikitafakari mambo kadhaa. Kati ya mambo hayo suala la Farida lilichukua nafasi kubwa sana katika kichwa changu.



    Niliamini kwamba kuingia katika uhusiano na Farida ni kuingia katika vita. Vita vya mapenzi. Vita ngumu kuliko vita zote. Niliamini kwamba Nassoro hatokubali, Fatma hatokubali. Wote wataungana kwa pamoja kupambana na sisi. Hawatokubali.



    Nilikuwa najua kwamba pamoja kwamba Fatma alinisaliti lakini bado alikuwa ananipenda. Hata baada ya tukio lile mara kadhaa alikuwa ananitumia meseji za kuomba nimsamehe, kuomba turudiane tena. Tuoane.

    Alionesha kujutia kwa yote aliyoyafanya. Lakini mimi sikuwa tayari kumsamehe.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nakumbuka siku moja tulikutana getini pale Mlimani City. Mimi nilikuwa naenda kutoa fedha katika benki ya CRDB, yeye alikuwa anatoka nje. Tulikutana uso kwa uso. Yeye akiwa peke yake. Mimi nikiwa peke yangu. Yaani mimi na yeye...



    Fatma hakusita kuonesha hisia zake kwangu. Neno lake la kwanza lilikuwa ni kuniomba msamaha.

    Nilijifanya sijamsikia. Nilimpita kwa kasi nikiingia ndani. Alinishika mkono wangu wa kushoto kwa nguvu.



    Alisema " Naomba unisamehe Nassibu. Binadamu gani usiyeweza kusamehe wenzio. Mungu anasema samehe saba mara sabini. Tumeumbiwa makosa Nassib. Tumeumbiwa msamaha. Kukosea kwa binadamu ni moja ya sifa yao. Naomba unisamehe please. Amini bado nakupenda, nakupenda sana Nassib"



    Sikuwa na muda wa kujibu ngonjera zake. Nilikaa kimya. Ukimya wangu ulimuumiza sana Fatma.

    Niliona machozi yakitiririka katika macho yake yote mawili. Fatma alikuwa analia. Nilitamani kumsamehe, lakini nilivyofikiria vitendo vyake niligairi mara moja.



    Nilikumbuka siku niliyomshuhudia Fatma akifanya mapenzi mtaroni pale Hongera bar. Tena aliyekuwa anafanya nae alikuwa ni mlinzi wa chuo cha Ustawi wa jamii. Hiyo ilikuwa siku ya kwanza tu ya kumfatilia Fatma na nyendo zake.



    Nilishikwa na uchungu.



    Nikampigia simu. Kwa sauti ya upole alinambia kwamba muda huo yuko nyumbani kwake kalala. Wakati nilikuwa namuona. Alikuwa mtaroni na mlinzi. Niliingalia simu yangu. Mpaka tone la machozi lilipodondoka katika kioo cha simu yangu ndipo nilipogundua kama nilikuwa ninalia. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nililia kwa sababu ya mapenzi. Fatma aliniliza mithili ya mtoto mdogo.



    Mtu wa aina hiyo anastahili kusamehewa kweli? Tufanye msamaha unaweza kwenda kwa yeyote yule lakini je Fatma anastahili kuolewa?.



    Nilivyokumbuka hayo, chozi lake halikuwa na thamani tena kwangu. Nilijitoa kwa nguvu mkono wangu na kuanza kuondoka. Fatma alinifata huku akiwa kapiga magoti. Akilia kama mimi nilivyolia siku ile. Akilia kwa sababu ya mapenzi. Akinililia mimi.



    Watu walitushangaa sana.



    Nikiwa katikati ya mawazo nilistuka ghafla. Gari nililopishana nalo ndilo lililonistua, lilinitoa katika mawazo yangu juu ya Fatma.



    Lilikuwa ni Range Rover nyeusi!



    Sasa nikawa makini. Nikawa naendesha gari kwa tahadhari zote. Nikiangalia kwenye 'sight mirror' mara kwa mara. Kengele ya hatari ilikuwa inagonga kwa nguvu sana kichwani mwangu.



    Nilijisemea kimoyomoyo "Ile itakuwa Range Rover ya Nassoro tu"



    Hadi nafika katika baa ya Masoko by Night sikuwa naiona ile gari katika 'sight mirror'. Nikajipa moyo labda hakuwa Nassoro.



    Nilikunja mkono wa kulia njia iliyokuwa inaelekea katika nyumba ya kulala wageni ya kisasa ya Hilton. Nilipofika Hilton nikakata kushoto kuelekea katika mtaa ilipokuwa nyumba yangu.

    Nilifika.



    Wakati nahangaika kupaki gari yangu barazani kwangu.

    Simu yangu iliita.

    Alikuwa Farida.



    "Nass kuwa makini mpenzi wangu. Nassoro anakusaka kama shilingi ya rupia" Farida alisema mara tu baada ya kupokea simu yake.



    Ilikuwa ni kauli ya hatari sana na pengine ilinipasa kuogopa hasa baada ya kupishana na Range rover nyeusi hivi punde.

    Lakini sikuogopa.

    Akili yangu ilizama katika neno lake moja tu 'Mpenzi wangu'



    "Farida leo kaniita mpenzi wangu" Niliwaza.



    "Nass unanielewa jamani" Farida alilalama simuni.



    Nilishuka garini simu ikiwa sikuoni. Nikiwa siamini masikio yangu. Nilibaki kimya.



    Nilipogeuka pembeni. Nilistuka sana!.



    Range Rover nyeusi ilikuwa nd'o inapaki pembeni ya nyumba yangu.



    "Nassorooo!" Niliropoka kwa nguvu.

    Simu ikanidondoka chini bila kupenda.



    Kwa kutumia kioo cha gari, jamaa aliniona vizuri jinsi ya nilivyopatwa na mstuko. Alitabasamu kwa mbali.



    Kisha, alishusha taratibu mguu wake wa kulia toka katika Range Rover nyeusi. Kiatu safi cheusi 'mkuki moyoni' kiligusa ardhi.

    Nassoro, alishusha na mguu wake wa kushoto. Kiatu safi cha kahawia kiligusa ardhi, nacho kilikuwa mkuki moyoni. Aina sawa na cha awali. Rangi ni tofauti ya awali. Mguu wa kushoto nao ukakanyaga ardhi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kisha ilifuata suruali ya kitambaa cheusi, niliuona mkanda safi wa ngozi ukiwa umetulia kiunoni. Kisha shati safi jekundu lilifuata, likiwa limechomekewa juu ya suruali nyeusi. Sasa nilimuona usoni.

    Alikuwa na madevu yaliyomtapakaa hovyo usoni. Kichwani alikuwa na bonge la upara. Likiwa linang'aa vizuri sana. Nilijisemea kimoyomoyo



    "Hakika huyu ndio Nassoro"



    Alisimama wima. Akaingiza mkono wake wa kulia katika mfuko wa suruali yake. Alitoa sigara ndevu, aina ya sigara nilizozoea kuziona katika 'movie', akaiweka mdomoni kimadaha, akaingiza mkono wake wa kushoto mfukoni, akatoa kibiriti cha gesi. Akawasha.

    Alivuta funda refu. Akatoa moshi puani na mdomoni. Moshi mwingi.

    Akaanza kunisogelea.



    Nilitetemeka vibaya sana!



    Akanikaribia " Eti anakwiita Nass. Unaitwa Nass na mke wa mtu we' unafurahia? Akanyamaza, aliniangalia, aliiweka tena sigara yake mdomoni. Akaivuta. Safari hii hakutoa hata chembe ya moshi. Alimeza kila kitu.



    Aliongea tena "Nass chagua moja kati ya haya, Farida ama Kifo?"



    Nilijitutumua " Sijakuelewa kaka, kwanza wewe ni nani? Na huyo Farida ni nani?" Niliuliza kama bwege vile.



    "Mi sio muongeaji sana. Mimi sio muimba taarabu mimi. Sijui u'Hadija Kopa. Mimi ni mtu wa kutenda. Answer this question kisha nitende..Kati ya Farida na Kifo unachagua nini?" Alivyotaja neno Kifo macho aliyatoa pima.



    Akanisogezea sura yake mbaya sana kwangu. Sura zetu zikakaribiana sana. Harufu ya moshi wa sigara nilikuwa nausikia moja kwa moja.Toka kwa Nassoro, kuja kwangu.. Nassib.



    Kichwani mwangu yalipita haya



    " Maisha ni mapambano tangu siku ya kutungwa mimba yako. Fikiria mbegu zaidi ya milioni moja zilivyopambana ili kulifikia yai la mama yako. Mbegu ya kwanza kufika ndio wewe. Ulipambana na kushinda mpambano. Mpambano wa mbegu. Unajifunza nini hapo..Dunia ni uwanja wa mapambano. Na furaha yetu ni kushinda mpambano. Hatuna budi kushinda mapambano mbalimbali ili kufikia kilele cha mafanikio..." Yalikuwa maneno aliyonambia rafiki yangu Joel kipindi tuko chuo. Lakini sikuwahi kumaliza kufikiria.



    "Nakuuliza kwa mara ya tatu, na ya mwisho.

    Chagua moja kati ya haya mambo mawili, kuwa na Farida kisha ufe, ama kuendelea kuwa hai bila ya kuwa na Farida?" Aliongea huku akiwa kakunja ndita haijawahi kutokea katika sayari hii.



    Sasa nilimuelewa.





    "Namchagua Farida!" Nilijibu kwa kujiamini.



    "Ok, I will see you later" Alitembea harakaharaka aliingia katika gari lake, Range Rover nyeusi na kuondoka kwa kasi.



    Nilibaki nikiwa nimeegemea boneti la gari, jasho likinitoka vibaya sana, nikiingalia simu yangu iliyokuwa kila kitu kwake.



    Nikiwa bado natafakari, nikasikia sauti nyororo. Sauti ya mpenzi wangu. Sauti ya mke wangu mtarajiwa. Sauti ya mwanamke ninayempenda zaidi hapa duniani. Sauti ya Farida ilisema" Pole sana Nass na leo nimeamini kweli unanipenda"



    Nilinyanyua sura yangu na kumuangalia Farida.



    "Ulikuwa wapi Farida?" Nilimuuliza Farida huku nikiiokota simu yangu chini.



    "Nilikuwa sokoni wakati nakupigia simu. Simu Ilivyokatika ghafla nikajua kuna tatizo. Nikaja mbio si unajua hapa sio mbali na sokoni. Nimesikia kila mlichoongea nikiwa upande wa pili wa gari lako. Nimesikia kila kitu yaani..Nassib your a man!" Farida alisema huku akinipigapiga kifuani. Nilijisikia faraja sana.



    " OK, hapo nimekuelewa"



    "Hebu tuingie ndani kwanza tukaongee vizuri" Farida alishauri.



    "Sidhani kama humu ndani ni sehemu salama. Kama umesikia kila kitu bila shaka umesikia na onyo la Nassoro. Umesikia chagua langu. Nimekuchagua wewe Farida. Nimekuchagua wewe kwasababu nakupenda Farida. Nakupenda zaidi ya neno nakupenda linavyomaanisha. Nakupenda kwa maana sahihi ya upendo, upendo wa kweli. Kwa hiyo dakika yoyote atakayokuja Nassoro hatokuja na maswali tena, ni vitendo tu. Bila shaka atataka kuniua kwa kuwa nimekuchagua wewe. Twende sehemu nyingine ya siri ili tukaongee, na kujipanga kwa vita!"



    "Uko smart sana Nass. Naunga mkono hoja. Wapi unahisi sehemu sahihi ya kupanga haya mambo?" Aliniuliza huku akiniangalia usoni.



    Nilimjibu harakaharaka " Ingia kwenye gari twende"



    Tukaingia kwenye gari, nikawasha gari na kuondoka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****



    Ilikuwa imepita wiki moja tangu nipigwe mikwara na Nassoro. Tangu siku ile hakutokea tena Nassoro. Tulikuwa tumejadiliana mambo mengi sana na Farida katika kumkabili Nassoro. Tulibakisha jambo moja ambalo tulikubaliana tujadiliane siku nyingine. Ni kuhusu suala la mahusiano yangu na Farida. Farida bado alikuwa na hofu kunikubalia. Alikuwa anahofia maisha yangu. Alikuwa anaogopa kuniingiza katika matatizo. Pamoja na mimi mwenyewe kukubali kwamba nipo tayari kufa ila niwe na Farida lakini bado haokuondoa hofu kwangu. Alinambia tusubiri baada ya wiki moja ndipo tujadili kwa kina jambo hilo.



    Leo, tulikuwa tumekaa katika meza ya pembeni. Katika hoteli ya kitalii ya Kimbilio. Tulikuwa tumekaa mkabala na Farida. Tukiangaliana.



    Meza yetu kulikuwa na sahani mbili, zilizojaa vyakula. Mimi niliagiza ugali kwa nyama ya mbuzi. Wakati Farida aliagiza chips na kuku nusu. Vyupa vya soda vilijaza nafasi katika meza yetu. Upande wake kulikuwa na Fanta orange. Kwangu Sprite.



    Nilimwangalia usoni. Farida alikuwa amependeza sana. Alivaa blauzi ya bluu, yenye nakshi ya rangi ya dhahabu kifuani. Hereni za bluu. Na kidani cha thamani cha bluu, chenye herufi N katikati iliyowekwa kwa nakshi ya dhahabu. Usoni alikuwa amevaa miwani aliyoiweka juu kidogo ya macho yake. Chini, alikuwa amevaa suruali ya jeansi nyeusi iliyomkaa vyema sana, iliyoruhusu kuionesha vyema shepu yake nzuri mno. Na chini alivaa viatu vya wazi vyenye nakshi ya bluu.

    Meza yetu ilikuwa inanukia harufu nzuri sana ya uturi toka kwa Farida.



    Wakati namwangalia. Farida alikuwa akitabasamu huku anahangaika kukata nyama ya kuku. Niliyaona meno yake meupe yaliyo kwenye mpangilio nzuri huku yakiacha nafasi katikati...mwanya wa kufa mtu.



    Alivyoniona namwangalia alitabasamu zaidi. Akanambia kwa sauti yake nyororo " Umependeza sana Nass. Hiyo suti nyeusi imekukaa vizuri sana. Ni kali sana, halafu wewe mwili wako ulivyo kila nguo mwake. Najiona niko na mwanaume, mwanaume shaba' bi".



    "Hahaha daah hizo sifa. Thank you Farida. Sina haja ya kusema kuhusu wewe. Unafunika kila sekunde. Najivunia kupata nafasi ya kuwa karibu na wewe. Najiona kama nimekaa na wale wanawake wazuri wa peponi, mahru'rain"



    "Hahaha yapasa kunisifia tu Nass, its your responsibility. Asiponisifia wewe unafikiri atanisifia nani? Aliniuliza swali huku akinipiga kofi dogo shavuni.



    Nilimwangalia Farida, alikuwa na furaha tele usoni mwake. Hakuwa na hofu kabisa ya vitisho vya Nassoro..



    Nilisema kwa sauti ya upole " Lengo la kikao hiki kidogo ni kukusisitizia Farida kile nikwambiacho kila siku. Kuendelea kulia kilio changu cha kila siku. Kilio cha kukubembeleza Farida.

    Amini nakupenda sana. Ni mwezi huu sasa nimekuwa nikikuimbia katika ngoma za masikio yako wimbo huu, wimbo wa mapenzi. Nakupenda sana. Na sitochoka hata siku moja kukuimbia wimbo huu, ni wimbo niupendao sana, hasa nikikuimbia wewe. Mwanamke nikupendae kuliko kitu chochote kile chini ya jua. Nilikupenda Farida katika sekunde yangu ya kwanza tu kukuona. Ninakupenda Farida kwa namna ileile hadi leo. Sijapunguza upendo wangu kwako. Upendo wa dhati. Na ninaahidi nitaongeza. Wallah nitakupenda milele Farida. Naomba unipe moyo wako. Nikupe moyo wangu. Tupendane. Uwe furaha yangu. Niwe furaha yako. Furaha nitakayoitunza siku zote katika maisha yangu yote. Farid....."



    Alinyoosha mkono wake na kuuziba mdomo wangu. " Usiseme mengi sana Nass. Nakupenda pia Nass. Nilikupenda tangu siku ya kwanza. Ni hofu tu ndio iliyonifanya nichelewe kukwambia kama Nakupenda sana. Umenionesha kwa vitendo kama unanipenda. Nami nakuahidi nitakupenda kwa vitendo"



    Nilipatwa na furaha isiyomithilika, niliongea "Nashukuru sana Farida. Am very happy yaani kwa kunikabidhi moyo wako. Nakupromise that nitakupenda siku zote za maisha yangu. Sitokutesa. Sitokuumiza kamwe. Am proud to be with you Farida"



    "Nass, usimalize maneno. Weka na akiba ya maneno" Alisema huku akicheka.



    Tuligonga glasi na kuanza kunywa. Tulikuwa na furaha sana. Tulikuwa wapendao tuliopendeza sana

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hivi Farida, vipi Nassoro hajakutafuta hivi karibuni?" Nilijaribu kumuuliza kiutani.



    "Achana na Rick Ross yule, tule bata hahaha" Farida alijibu huku akicheka.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog