Search This Blog

Friday, 20 May 2022

FARIDA - 3

 







    Simulizi : Farida

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Hivyo ndivyo penzi langu na Farida lilivyoanza. Lilianza ndani ya hoteli ya kitalii. Na kukua kila siku. Langu likawa la Farida, la Farida likawa langu. Nilijua mengi sana kuhusu Farida, ambayo sikuwa nayajua awali. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Penzi letu lilikomaa kila baada ya siku. Likawa penzi la mfano ndani ya Kilwa. Likawa penzi zuri sana. Likawa penzi tamu mno. Lilikuwa penzi tamu mithili ya wewe na mpenzi wako. Ndio, wewe hapo na mpenzi wako. Tulikuwa pamoja na Farida kama kumbikumbi. Tulisahau kabisa kuhusu Nassoro na tuliamini Nassoro alisahau kuhusu sisi.



    *****



    ILIKUWA siku ya jumatano. Miezi zaidi ya mitatu toka tuingie katika uhusiano na Farida. Uhusiano bora sana wa mapenzi. Tulibakisha miezi sita tu mbele ili mimi na Farida tuoane.



    Siku hiyo nilikuwa ofisini kwangu nikisahili wagonjwa na kuwatibu kama ilivyokuwa majukumu ya kazi yangu. Ilikuwa inakaribia kufika saa nne asubuhi. Muda wa kwenda kunywa chai.



    Nilikuwa nimehudumia wagonjwa takribani tisa, kati ya wagonjwa wengi waliokuwa wamepanga foleni ndefu nje ya ofisi yangu.



    Mgonjwa wa kumi alizua kizazaa.



    Alikuwa mwanamke mrembo sana. Kwa kumkadiria kiumri alikuwa hajatimiza hata miaka ishirini na tano. Alikuwa amevaa baibui katika mwili wake mzuri, baibui lililoruhusu sura yake kuonekana vyema. Alikuwa na sura nzuri nyeupe iliyohifadhi pua ndefu.



    "Naitwa Farida" Alijitambulisha huku akitabasamu.



    Niliposikia jina hilo nami nilitabasamu. Nilimkumbuka Farida wangu.



    "Dokta, umemkumbuka mchumba'ko Farida nini?" Aliniuliza kitu ambacho nilikuwa nakiwaza.



    Nilizidi kutabasamu.



    "Dokta mimi nimekuja hapa kwa kujua hii ni nafasi pekee ambayo ninaweza kuongea na wewe, maana nje ya hapa muda wote upo na Farida tu" Mgonjwa Farida aliongea huku akisimama.



    Nilishangaa. Nilikuwa makini kusikiliza anapotaka kuelekea yule msichana.



    Alivua baibui lake huku nikimwangalia. Alibaki na pensi fupi ya kaki na t.shirt nyeupe. Alikuwa na mapaja mapana yaliyotengeneza vyema shepu yake ya kupendeza sana.

    Juu chuchu za maziwa yake zilikuwa zinaonekana dhahiri katika ile fulana yake. Ishara kwamba alikuwa hajavaa sidiria kwa ndani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Narudia tena, naitwa Farida. Hakuna haja ya kusema nimetoka wapi ila kuna mambo kadhaa nataka kujua toka kwako" Alisema akiwa katika harakati za kukaa chini.



    "Mambo gani hayo? Unajua nipo kazini Farida. Tungetafuta sehemu nyingine tofauti na hapa kama mambo yenyewe si ya kikazi. Si umewaona kuna wagonjwa wengi sana nje wanasubiri huduma" Nilisema huku nikimwangalia usoni Farida.



    "Acha kuchonga sana Nassib. Nami pia nipo kazini" Aliongea huku akiwa anaiweka bastola yake juu ya meza yangu.



    Moyo ulinirupuka. Sikuwa nimewahi kuiona bastola 'live' tangu nizaliwe.



    "Usiogope dokta. Sijaja kuitumia hii, ila ukinilazimisha kuitumia I will do that" Sasa akawa anaongea huku akiiangalia bastola "Halafu uzuri wa hii bomba ina kiwambo cha kuzuia sauti. Nina kupasua kichwa chako na ninaondoka kimyakimya". Sasa akawa anaongea huku ananiangalia usoni "Maiti yako itakuja onwa na wagonjwa wako. Nani atajua kama Farida nd'o kakupasua kichwa chako? Ili nisikupasue hilo libichwa lako unatakiwa kunijibu kwa usahihi kila nitakachokuuliza.

    Narudia tena na unatakiwa kunijibu kwa usahihi." Farida aliongea huku akinitazama usoni.



    Jasho lilikuwa linanitoka vibaya sana. Farida aliongea kwa kumaanisha. Niliogopa sana. Nilihofia mno. Nilitetereka kwa kweli.



    "Bila shaka unamtambua Farida?" Aliniuliza.



    Niliitikia kwa kutumia kichwa.



    "Dokta, huwa tunatumia mdomo kama huu kujibu" Alisema huku akiupapasa mdomo wa bastola yake.



    "Ndio namfahamu" Nilijibu harakaharaka huku sauti yangu ikiwa imejaa uwoga.



    "Farida amewahi kulitaja jina la Rick Ross mbele yako?" Aliniuliza.



    Nililielewa swali. Nilikuwa na jibu. Lakini sikujua mantiki ya swali hivyo sikujua kabisa nijibu nini.



    "Hujalisikia swali Nass?" Farida aliniuliza huku akilitumia jina alipendalo Farida.



    "Nimelisikia" Nilijibu.



    "Nataka jibu" Aliniuliza.



    "Sijawahi kumsikia" Nilijibu.



    "Nilikwambia ukisema uwongo nakufanyaje?" Aliniuliza tena.



    " Unanipasua kichwa changu"



    "Mbona umesema uwongo sasa?" Aliongea huku akinioneshea bastola usoni.



    "Amewahi kulitumia..." Nilijibu huku midomo ikitetemeka.



    Niliushuhudia mstuko mkubwa sana katika uso wa Farida.



    "Unasema?" Aliuliza kwa nguvu.



    "Farida amewahi kumuita Nassoro Rick Ross mbele yangu" Nilijibu tena kwa sauti ndogo.



    "Alimtaja Nass kama Rick Ross wakati mkizungumzia nini?" Farida aliniuliza huku akinikazia macho. Nikaelewa kwamba yule dada alikuwa anaelewa kama nadanganya ama la kwa kuniangalia usoni, macho yangu. Nikakumbuka hata mimi ninavyowafanyia wagonjwa wakati nawasahili.



    "Huyu mwanamke atakuwa mtu mbaya sana. Atakuwa kasomea saikolojia ya uhalifu, crime psychology. Lazima nitumie akili za ziada kunusurika hapa" Niliwaza kimoyomoyo.



    "Alikuwa analitaja hilo jina katika mazungumzo yetu ya kawaida tu" Nilijibu hivyo kwa kujiamini huku nikimwangalia usoni Farida.



    "Usijaribu kunidanganya..." Hakumaliza kauli yake. Mlango ulisukumwa kwa nguvu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuwa Farida wangu!



    Alipoingia tu ndani ya ofisi yangu jicho lake lilituwa kwa mteja wangu aliyekuwa kitini. Alimtambua.



    Alitamka kwa nguvu, macho kayatoa pima "Vampire!"



    Niliuona mstuko toka kwa yule dada aliyejitambulisha awali kwa jina la Farida. Na sasa Farida wangu kumtambua kwa jina la Vampire.



    Ilikuwa hali ya hatari!



    Mlango ulikuwa wazi, Farida wangu hakuufunga. Wagonjwa waliokuwa nje walikuwa wanashuhudia kila kitu mle ndani. Niliona hali ya hatari iliyokuwepo pale, nikafikiria itakuwaje endapo wagonjwa wakiiona bastola pale mezani. Ile ilikuwa hospitali, sio Polisi, sio jeshini.

    Niliangalia mkononi kwa Farida. Bastola haikuwepo! Niliangalia juu ya meza. Patupu!



    Sikuelewa Vampire aliificha muda gani ile bastola. Kwa hakika mwanamke yule alikuwa ni Mzuka kweli.



    Zilipita dakika mbili za taharuki na mishangao. Hakuna neno lengine lililoongelewa zaidi na Vampire wala Farida wangu. Yalikuwa yanatembea macho ya chuki tu. Toka kwa Vampire kwenda kwa Farida, kutoka kwa Farida kwenda kwa Vampire.



    "Kuna kitu" Nilijimbia mwenyewe.



    Muda uleule aliingia Dokta Martin. Mkuu wangu wa kazi pale hospitali.



    "Kuna nini Dokta Nassib?" Aliingia na swali kuelekea kwangu.



    Nilibabaika sana.



    "Hamna kitu bosi" Nilianza kuelezea "Nilikuwa namhudumia huyu mgonjwa. Sasa kutokana na ugonjwa wake nilichukua muda mrefu kidogo, kuona hivyo huyu dada" Niliongea huku nikimuonesha kidole Farida wangu "aliingia nae kwa kuona nachelewa" Niliongea maneno hata sijui yalikuwa yametokea wapi.



    "Yuko wapi huyo dada aliyeingia awali?" Dokta Martin aliniuliza.



    Niliangalia kitini.



    Vampire hakuwepo!



    E bwana wee...



    Nilibabaika sana. Ni kweli Vampire hakuwepo. Farida wangu alikuwa kasimama wima mdomo wazi. Haongei kitu, labda alikuwa na hasikii kitu pia.



    "Hudumia wagonjwa, kisha tuonane ofisini baadae" Dokta Martin alisema kwa hasira huku akiondoka. Nilijua ameghadhibika hasa.



    Ndani ya ofisi yangu tulibaki wawili tu, mimi na Farida. Farida akiwa mdomo wazi. Bila shaka alistushwa sana na ujio wa yule mwanamke mle ndani.



    "Keti chini mpenzi wangu" Nilimuambia huku nikimuonesha kiti.

    Hakunisikia.

    Hakunielewa.

    Bado Farida alikuwa amesimama wima. Mdomo wazi.



    Nilimpigia nesi Rehema. Akaja. Nikamuambia amuongoze Farida hadi wodini.



    Farida alikuwa anaenda, kashikwa begani na nesi Rehema huku machozi yakimtoka.



    Mimi nilibaki nikiwa nimepigwa na butwaa. Nikiwa sielewi Farida amepatwa na nini. Sielewi mwanamke yule nimpendae amekumbwa na nini.



    Lakini sikuwa na jinsi, ilinipasa kuhudumia wagonjwa wengine.



    Saa nane kamili mchana nilimaliza kazi ya kuhudumia wagonjwa. Nilienda moja kwa moja ofisini kwa Dokta Martin. Kuitikia wito. Nilipigwa na butwaa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dokta Martin alikuwa amelala akiwa ameegemea kiti huku Vampire akimpepea kwa kutumia gazeti la Mwanachi...





    Nilisimama wima mlangoni nikiwa nahema kwa fujo. Pumzi zinakuja kwa kasi, zinarudi taratibu. Nilikuwa nashuhudia na sikuitaji kufanya uchunguzi wowote kujua kwamba dokta Martin alikuwa maiti. Vampire alikuwa anaipepea maiti ya Dokta Martin kwa gazeti. Dokta Martin akiwa ametulia tuli kitini. Kwakuwa nilikuwa ni daktari tu ndio maana niligundua kwamba Dokta Martin alikuwa ameuwawa kwa umbali ule. Harakaharaka, nilizungusha macho yangu katika chumba cha Dokta Martin.



    Ndipo nilipoona.



    Ukutani, karibu na dirisha kulikuwa na herufi 'V' iliyochorwa kwa kutumia damu. Damu iliyotumika ya nani? Alama 'V' ilikuwa inamaanisha nini? Sikuweza kutambua kwa harakaharaka. Maana Vampire alifunua mdomo wake



    "Karibu sana Nass tuendelee na mjadala wetu. Naona tuliingiliwa na watu wasiohusika kule, sasa hapa naomba ufunge mlango kabisa wasitusumbue" Vampire aliongea kwa kujiamini. Sauti ya kikike iliyorindima vizuri kwangu. Lakini ndani ya sauti hiyo yalibebwa maneno ambayo yalinifanya nihofie sana.



    Nilikuwa palepale mlangoni. Nimesimama sijielewi. Vampire anataka nifunge mlango. Je nitabaki salama kweli tukibaki wawili tu na mwanamke yule wa ajabu. Mwanamke hatari sana!



    Aliyakatisha mawazo yangu kwa kuongea "Nass, hatuna mwezi mzima humu wa kusubiri ufanye nisemacho. Funga mlango tumalizie mjadala wetu, niondoke" Alisema kwa sauti laini sana, ya kipole, ya kisichana. Alisema yote hayo akiwa bado anaipepea maiti ya Dokta Martin kwa kutumia gazeti. Kwa hakika Vampire alikuwa mtu wa ajabu sana.



    Bila kujielewa nilitekeleza agizo lake. Nilifunga mlango. Niliushuhudia mkono wangu mwenyewe ulivyokuwa unatetemeka wakati nimeushika funguo nikiuzungusha ndani ya kitasa.



    Aliongea "Napenda watu watiifu kama wewe. Sipendi kabisa watu wabishiwabishi. Wewe nahisi tutaelewana" Vampire aliongea maneno hayo nikiwa nimemgeuzia mgongo, nafunga mlango.



    Niligeuka. Aliniita kwa kutumia mkono wa kushoto. Huku mkono wa kulia safari hii akiupigapiga mwili wa Dokta Martin kwa kutumia gazeti. Nilienda taratibu. Vampire alionesha kidole chake katika kiti. Nilimuelewa. Nilikaa katika kiti mbele ya Vampire. Tukawa tunatazamana. Nikiwa na sura ya huruma sana. Nilikuwa mithili ya mwanafunzi mtukutu, aliyekamatwa na kupelekwa mbele ya mkuu wa shule na baba yake.



    Aliongea tena "Farida, hulitaja jina la Rick Ross akiwa katika mazingira gani, ama mukiwa mnazungumzia kitu gani?" Moja kwa moja Vampire alinirushia swali. Swali nisilolipenda hata kulisikia.



    Nilitoa jibu lilelile "Hulitaja katika mazingira ya kawaida tu" Nilijibu nikiwa simuangalii usoni.



    "Unayapenda maisha yako Nass?" Aliniuliza.



    "Ndio" Nilimjibu.



    "Kama kweli unayapenda maisha yako. Na kama bado una ndoto za kuendelea kuishi maisha matamu, wewe na Farida wako...Basi usirudie kusema uwongo. Hili ni onyo la pili na la mwisho. Ukinidanganya tena sikuonyi. Nakupasua kichwa kwa bastola hizi" Vampire alisema huku akiitoa bastola mbili, moja upande wa kushoto wa kiuno chake, nyingine upande wa kulia wa kiuno chake.



    "Farida, hulitaja jina la Rick Ross katika mazingira gani?" Aliniuliza tena.



    Sasa niliamua kumjibu.



    "Mara nyingi hulitaja jina hilo katika mazingira ya kunionya" Nilimjibu.



    "Mazingira ya kukuonya kivipi?" Vampire aliniuliza huku akikaa vizuri kitini.



    Nilikumbuka harakaharaka. Niliisikia sauti ya Farida katika fikra zangu ikijirudia mithili ya mwangu "Nass, Nassoro ni Rick Ross wewe"



    "Nass!" Vampire aliniita kwa ukali.



    " Alikuwa analitaja wakati akinitahadharisha kuhusu Nassoro?" Nilijibu harakaharaka bila ya swali kurudiwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    " Hebu toa mfano wa jinsi akivyokuhadharisha" Vampire alizidi kunibana.



    "Nass, Nassoro ni Rick Ross wewe" Nilisema bila kufikiria.



    Niliuona mstuko kidogo toka usoni kwa Vampire. Nikajua katika kauli hiyo katambua kitu.



    Alinyanyuka kitini. "Nashukuru sana kwa ushirikiano wako". Alisema huku akipiga hatua kutoka nje. Na bastola zake mkononi.



    Nilikuwa siamini macho yangu. Yaani Vampire aniache hai? Alitembea hadi mlangoni. Akasimama.



    Aliongea "Dokta Martin kafa kwa shinikizo la damu. Mimi na wewe hatujawahi kuonana katika maisha yetu. Tuliyoyaongea hapa yasifike katika sikio la Farida. Ukifanya kinyume na hivyo nitarudi tena kwako. Na nitakuua (Akamalizia na tusi zito la nguoni) huku akiipitisha bastola yake shingoni mwake." Vampire alimalizia kuongea akiwa nje ya mlango.



    Nilipumua kwa nguvu. Pumzi ya kuhemwa sana. Kwa pupa nikitoka nje ya ofisi kichwa chini. Nikiwa sina raha hata chembe. Nilienda kukaa katika benchi la mapokezi. Nikiwa na uwoga wa kiwango cha juu.



    "Kwani vipi Dokta Nassib, mbona kama hauko sawa?" Nilistuliwa na sauti ya Nesi Rehema.



    Sikujua nesi Rehema alikuwa amefika pale kwa muda gani. Nilikuwa nimezama katika mawazo kweli. Ilifikia hatua mtu kukaa pembeni yangu bila mimi mwenyewe kumtambua.



    "Nina kahoma kidogo Ray, ila soon i will be ok" Nilimjibu na wasiwasi tele.



    "Twende nikusindikize ofisini kwako basi. Ni heri ukae kule kuliko hapa". Alinishauri.



    Niliukubali ushauri wa Nesi Rehema. Alinishika mkono na kuanza kunikokota taratibu. Tukiwa njiani tulisikia mayowe yasiyo na mfano. Nesi Rehema alibabaika. Aniongoze mimi ama aende huko yalikokuwa yanapigwa mayowe.



    Mimi nilielewa. Bila shaka maiti ya Dokta Martin ilikuwa imeonwa na mtu ofisini kwake.



    Na sasa alikuwa anapiga mayowe..



    Nesi Rehema alinikokota hadi ofisini kwangu. Aliniacha kitini na kutoka nje kwa kasi.



    "Nakuja Dokta Nassib!" Niliisikia sauti ya Nesi Rehema akiwa anatokomea nje.



    Nikiwa peke yangu ofisini, niliwaza harakaharaka. Kubwa lililoganda katika kichwa changu nilikuwa nimeingia katika mkasa. Mkasa mkubwa. Nilihitaji kuongozwa na busara ili niepuke mkosi mkubwa uliokuwa unanikimbilia kwa kasi. Kasi kubwa sana.



    Nilimkumbuka Farida.



    Nilijipekua katika koti langu jeupe kutoa simu. Nilizitafuta namba za Farida na kuzipiga.



    Simu ilianza kuongea kwa pupa " Kuanzia sasa tumia akili Nass. Tupo katika hali ya hatari. Uwepo wa Vampire Kilwa ni ishara kwamba tupo karibu na kifo. Yule ni Vampire! Na kumbuka kwamba Nassoro ni Rick Ross! "



    "Unajua sikuelewi Farida. Uko wapi nije tuongee. Bado upo mapumziko ama? Niliuliza harakaharaka.



    " Tukutane beach, pale tulipokutana siku ile" Alijibu.

    Akakata simu.



    *****



    Farida alikuwa amevaa suruali ya jeans ya bluu. Koti kubwa lililofika hadi magotini. Begani alikuwa na mkoba mkubwa kiasi. Nywele zake ndefu alikuwa amezilaza kwa nyuma.



    Ni saa moja ilikuwa imepita tangu nilivyokutana na Farida pwani. Sehemu yetu ileile tuliyoizoea. Hadi muda huo alikuwa amenieleza mambo mengi sana kuhusu mume wake wa zamani, Nassoro. Alinisimulia pia habari za kuogofya kuhusu yule mwanamke katili, Vampire.



    Nilikumbuka alivyonisimulia kwa hisia baada ya kumuuliza kwanini anamuita Nassoro Rick Ross.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alianza kwa kusema " Nakusimulia haya kwa sababu moja tu. Nakupenda sana Nass. Na nimeamua kukukabidhi moyo wangu kwako. Nimeridhia kukukabidhi furaha yangu. Nimeamua kukukabidhi maumivu yangu. Na kubwa nimekukabidhi maisha yangu. Maisha yangu mimi Farida. Na hiyo yote kwa sababu Nakupenda. Kwa sababu ya usalama wa maisha yetu lazima nikueleze kila kitu ili ujue tunapambana na watu wa aina gani"



    Farida alinyanyuka. Alisogea baharini. Kulikuwa na mti utupao kivuli, akauegemea. Mimi nilibaki nimekaa chini palepale. Alianza kuongea huku akiangalia maji ya bahari.



    "Wakina Nassoro ni watu hatari sana. Ni hatari zaidi ya neno hatari lenyewe" Alitulia kidogo. Nilisikia sauti yake ikiwa imejaa woga lukuki wakati akiongea. Nikaamini Farida alikuwa anamaanisha akiongeacho.



    Aliendelea " Wakina Nassoro wana genge la kihalifu. Genge la siri sana. Kazi yao kuu ni kuua, kuwaficha na kuwasafirisha watu wenye ulemavu wa ngozi, maalbino!" Aligeuka nyuma Farida. Alinikuta nami nikiwa nimesimama wima. Nikiwa katika harakati za kumsogelea pale alipokuwa.



    Aliongea huku akinifata "Katika hilo genge lao la uhalifu washiriki wote wana majina ya siri. Katika majina hayo jina la siri la Nassoro ni Rick Ross. Na yeye kama Rick Ross, jukumu lake kuu ni kuua ama kukata viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi" Farida alinifikia, alinishika mikono yangu yote miwili. Tukawa tunaangaliana.



    " Na yule mwanamke niliyemtambua kwa jina la Vampire. Kazi yake kuu, ni kusimamia usalama wakati viungo vya maalbino vikiwa vinasafarishwa.



    " Umeyajuaje yote hayo Farida?" Nilithubutu kumuuliza.



    "Nimeyajua hayo kwa bahati mbaya tu. Kuna siku nilikuwa nataka niangalie video ya mkanda wetu wa harusi na Nassoro. Katika laptop yake ndo niliyakuta mambo hayo katika 'file' la siri"



    "Kina Nassoro wanajua kama unayajua mambo yao?" Nilimuuliza tena.



    Alijibu " Walikuwa hawana uhakika. Ila bila shaka leo watakuwa wamepata uhakika"



    "Kwani umekutana nao leo?" Nilimuuliza nikiwa na kihoro.



    "Ni baada ya wewe kuwaambia nishalitaja jina la Rick Ross mbele yako. Hilo ni jina lake la siri, wanayajua wao wenyewe tu wakiwa katika mambo yao ya siri. Kukili kwako kwamba nimelitaja jina la Rick Ross mbele yako ni sawa na kukili kwamba mimi ninazijua siri zao"



    " Mh, mambo mazito sana" Nilisema nikiwa nimekata tamaa.



    "Na ya hatari zaidi ya unavyoyafikiria" Farida alimalizia.



    " Sasa Farida, kwanini tusiyaripoti haya mambo katika vyombo vya sheria?"



    "Usithubutu hata kuwaza hivyo Nass. Kama unahamu kwenda kuzimu jaribu.." Alisema huku akiniangalia kwa huruma.



    "Kwanini tusithubutu?" Niliuliza kwa sauti isiyo na nguvu.



    "Wana mtandao mpana sana wale. Polisi utakayemkuta kaunta anaweza kuwa yumo katika mpango wao. Mkuu wa kituo anaweza kuwa katika mipango wao..wanafanya mambo yao kiakili sana, wanafanya mambo kimkakati na mbinu za uhakika"



    Nilimkatisha " Sasa wanawezaje kuwashawishi watu wote hao?"



    "Pesa inaongea. Ni kitu gani ambacho pesa inashindwa kununua? Pesa inanunua haki, pesa inanunua ukweli. Kutokana na nguvu ya pesa hadi leo sijajua yupi ni mtu sahihi zaidi yako kumtwisha mambo haya katika kichwa chako"



    Nilikubali kwa kichwa.



    Saa moja ilikuwa imepita tangu tulijadili mambo hayo na Farida. Hadi sasa tulikuwa hatujapata muafaka.

    Tuliwaza na kuwazua.

    Bado hatukupata njia sahihi ya kuwakabili wakina Nassoro. Bado tuliona hatari ilikuwa inatunyemelea mbele yetu. Inatunyemelea kwa kasi kubwa sana.



    "Sasa tunafanyaje ili kuepuka kisanga hiki Farida?. Maana tupo katika hali ya hatari sana. Kosa moja tu litasababisha vifo vyetu, lazima tutumie akili za ziada kuikwepa mikono haramu ya wale jamaa. Na lazima tufanye juu chini kumtafuta mtu ambaye tutamuelezea haya ili aweze kutusaidia.."



    Alinikatisha " Nakubaliana na wewe Nass hundred percent, but the issue is... mtu huyo ni nani? Mtu tutakayeamini kwa asilimia zote kwamba yuko upande wetu" Aliniangalia usoni kwa macho yale laini yakiyomlenga machozi, akaendelea. "Na wale jamaa kwakuwa washajua kuwa niliyaona mambo yao waliyokuwa wanayafanya, lazima waongeze nguvu katika msako wao. Watusake. Watukamate. Watuue" Farida aliongea huku machozi yakiwa yanamtiririka.



    "Usilie Farida. Amini hatotukufa, I will use my effort to ensure that jamaa tunawamaliza sisi, na mipango yao hasi tunaiweka hadharani. Amini tuko pamoja katika hali zote Farida. Nitakuwa na wewe bega kwa bega kuhakikisha haudhuriki. Hauumii. Hauteseki. Na nafanya haya yote kwakuwa nakupenda kwa moyo wangu wote Farida"



    Farida aliniangalia. Alitabasamu huku akiwa analia. Alinikumbatia kwa nguvu. Mdomo wake ukiwa karibu na sikio langu la kulia.



    Alisema " Wewe ni mwanaume Nass. Mwanaume shababi. Mwanaume niliyekuwa namsaka usiku na mchana. Na leo nimempata. Ninajivunia sana kuwa na wewe Nass. Nakupenda Nass. Nakupenda mno" Alimaliza huku akinipiga busu la nguvu katika shavu langu. Busu lililonifanya nisahau hatari iliyokuwa inatukaribia kwa muda.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara simu ya Farida iliita. Aliangalia simu yake.



    "Namba ngeni" Alisema kwa sauti ndogo.



    "Pokea" Nilimwambia.



    Aliniangalia usoni huku akitikisa kichwa kukataa.



    Simu iliita mpaka ikakata.



    Baada ya dakika mbili simu yake iliita tena. Namba ileile.



    "Pokea Farida" Nilimshauri tena.



    "Hapana Nass, ni hatari kupokea simu kwa wakati hatari kama huu" Farida aliongea kwa sauti ndogo.



    Nilikuwa sijamuelewa Farida. Lakini niliamua kusikiliza hisia zake. Nilitulia tuli nikimwangalia Farida akivyoiangalia simu yake.



    Simu ilivyokata.

    Farida aliifungua nyuma ya simu yake. Aliitoa 'line' yake ya simu na kuivunjavunja.



    "Ni very easy waka'detect tulipo kwa kutumia hizi simu" Farida alisema huku akiiweka mfukoni simu yake isiyo na 'line'.



    Nilikubali kwa kichwa. Nilikumbuka jinsi ya filamu kadhaa za kimarekani wakivyotumia njia hizo. Lakini sikuwa naamini kama hiyo teknolojia itakuwa imefika hadi Tanzania.



    Dakika tatu baadae simu yangu ilianza kuita. Ilikuwa namba ileile. Namba iliyotoka kumpigia Farida hivi punde.

    Nilichukua simu na kumuonesha Farida.

    Alicheka.



    "Si unaona, nilikwambia, huyo ni Vampire!" Alisema kwa hamasa.



    "Kaipataje sasa namba yangu?" Nilimuuliza Farida swali la kizembe.



    "Nimekwambia huyo ni Vampire!" Farida alisema kwa nguvu.



    Aliendelea " Yaani usishangae Vampire kujua namba yako. Its small thing kwake"



    Nilikubali kwa kichwa kama zezeta.



    Mara ya tatu sasa simu yangu ilikuwa inaita.

    Ilivyokata.

    Nikaizima.

    Nikaitia mfukoni.



    "Sasa tutatokaje hapa. Yatupasa kuwa nje ya mji huu. Mji ushachafuka huu, bila shaka kutakuwa maadui wengi sana"



    "Ni kweli yatupasa tuondoke lakini sio sasa. Bila shaka kina Vampire watahisi sisi tunataka kutoroka. Bila shaka wataweka watu katika njia zote zitakazotuwezesha kutoka katika mji huu. Hapa la msingi tutafute sehemu tutakayoweka kambi yetu ya muda mfupi. Mambo yakitulia ndipo tutaondoka" Farida alinieleza.



    Nilikubaliana na mawazo ya Farida. Ni kweli ilitupasa kujificha sehemu kwa muda. Ni sehemu gani salama? Ndipo nilipomkumbuka nesi Rehema.



    "Nesi Rehema anaweza kutuficha nyumbani kwake kwa muda" Niliwaza kimoyomoyo.



    "Sasa tutajificha wapi kwa muda huu wa kusubiri huu upepo mbaya upite?" Farida aliniuliza.



    "Kuna rafiki yangu mmoja. Ni nesi katika hospitali yetu pale, anaweza kutuhifadhi nyumbani kwake kwa muda" Nilimwambia.



    "Unamuamini huyo rafiki yako?. Tuko katika wakati mbaya sana, lazima uwe na imani kuu kwa kila mtu utakayemshirikisha katika jambo hili" Farida alinionya.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nesi Rehema alikuwa ni zaidi ya rafiki kwangu. Tulikuwa tunashirikiana katika mambo mengi sana. Alinipa siri zake,nilimpa siri zangu. Tulishauriana katika mambo mbalimbali. Tulipeana moyo katika matatizo mbalimbali.



    "Namwamini sana nesi Rehema. She is my best friend" Nilijibu kwa kujiamini.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog