Simulizi :
Njama
Sehemu Ya Pili (2)
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wote walitingisha vichwa kuonesha kuwa wamenielewa.
Kutokana na mipango yangu ilivyokuwa
nilionelea
tokea wakati huo tuanze kazi bila kupoteza muda.
Nilitoa
onyo tena "Kukubali kwenu kushiriki na mimi katika upelelezi wa tukio hili
mjue
kabisa mmejiwekea sahihi ya kifo. Natoa natoa muda wa
mwisho kama kuna mtu anaona wasiwasi
katika
moyo wake nampa nafasi aache shughuli hii", niliwaasa na kuwaangalia kwa makini
sana.
Mwisho Veronika akasema
"Unajuwa
Willy dakika ile mtu anapozaliwa pale pale anapewa huku ya kifo. Nina maana
ya
kusema kuwa binadamu hata aishi vipi kufa lazima
atakufa. Kule kuishi baada ya kuzaliwa ina
maana kuwa
ile hukumu ya kifo inaahirishwa kutekelezwa. ..
"Unajuwa
Willy dakika ile mtu anapozaliwa pale pale anapewa huku ya kifo. Nina maana ya
kusema
kuwa binadamu hata aishi vipi kufa lazima atakufa. Kule
kuishi baada ya kuzaliwa ina maana
kuwa ile
hukumu ya kifo inaahirishwa kutekelezwa.Wengine huahirishwa kwa mwezi mmoja.
Hivyo
mtoto anazaliwa na baada ya mwezi mmoja anakufa. Hii si
ajabu maana hukumu yake ya kifo
imetekelezwa baada ya mwezi mmoja. Wengine huishi hata
miaka mia moja. Hii ina maana kuwa
hukumu
yake aliyopewa dakika alipozaliwa imetekelezwa baada ya miaka mia.Hivyo kila mtu
na
sehemu yake ya kuishi. Kwa hiyo kuogopa kufa ni
ujinga."
"Mimi sina wasiwasi, maana kifo cha namna hii, nitakuwa
nimekufa kifo cha heshima", alisema
Sherriff.
"Okke,
sasa naamini nina watu. Tokea sasa nyinyi si ndugu tena ila ni makomredi",
niliwaeleza.
"Kwani komredi ina maana kubwa zaidi ya ndugu?",
Veronika aliuliza.
"Hasa, ina maana kali zaidi. Komredi ina maana mwenzi
katika harakati".
"Asante komredi Willy, naona tunywe maji haya katika
jina la komredi", Veronika aliomba. Wote
tukagonganisha glasi zetu.
"Sasa mimi
naonelea itabidi tuanze upelelezi wetu bandarini. Itabidi tukamuone
ofisa
aliyehusina ili na sisi tupate habari toka kwake ana
kwa ana ingawaje atakuwa amekwisha
sumbuliwa
sana na polisi na maafisa usalama kwa maswali. Huenda sisi tukapata jambo
ambalo
huenda wao wameliruka. Halafu tukaendelea hivyo hivyo
katika ofisi zote zilizohusika kabla
hatujachukua hatua kali zaidi", mnaonaje.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sawa", walijibu kwa pamoja.
Tulinyanyuka na kuelekea kwenye gari langu,
nikawafungulia milango. Veronika alikaa mbele na
mimi.
Sherriff akakaa nyuma. Nilipotaka kuwasha gari moto niliona kijikaratasi
chini,
nikakiokota taratibu nikakisoma. Eddy alikuwa
ameniandikia namba zote za magari aliyokodi.
Akionesha
namba za magari aliyoacha kwenye maegesho ya New Afrika na Kilimanjaro Hoteli
kama
nilivyokuwa nimeamru. Nilianza kusikia msisimko wa damu
ikionyesha kuwa kazi imeanza. Nilipiga
gari moto
tukaelekea bandarini.
MIWSHO WA SURA YA TATU
NJAMA
FUNUNU
SURA YA
NNE
"Samahani binti tunaomba kumuona Meneja",
nilimwambia mwandishi mahsusi wa Meneja wa Bandari.
"Sijui
nyinyi ni akina nani?", aliuliza msichana huyu aliyeonekana amechoka
choka.
"Mwambie ni Willy Gamba na wateja wake kutoka gazeti la
Afrika".
Meneja wa Bandari tulikuwa tunafahamiana kikazi, hasa
kutokana na shughuli zingine tulizokuwa
tunazifanya katika kampuni yetu ya Afrika Internation
Agencies.
Yule msichana alizungumza na bosi wake kwa simu,
alipomaliza alinyanyuka na kutufungulia
mlango
tukaingia ndani. Tulimkuta Issack Mlingi ambaye ndiye Meneja wa Bandari
aliyehusika na
tukio hili akionyesha hali ya kuchoka sana. Nafikiri
hii ilitokana na bughudha alizopata toka
kwa polisi
na watu wengine wanaohusika na upelelezi wa tukio hili. Macho yake yalikuwa
mekundu
na yamevimba.
"Karibuni
ndani", alisema huku akinyanyuka ili tusalimiane.
"Samahani
ndugu Mlingi, naamini una shughuli nyingi sana", nilimuomba radhi.
"Si kitu
Gamba, karibuni".
"Hawa ni wateja wangu Sherriff na Veronika kutoka
gazeti la Afrika ambalo kampuni yangu ni
wakala
wake, na jamani huyu ni Issack Mlingi, Meneja wa Bandari", walipeana mikono
kisha wote
tukavuta viti tukakaa.
"Ndugu
Mlingi ni imani yangu kuwa umeisha ulizwa maswali mengi juu ya tukio hili
lililotokea
hapa bandarini. Lakini naamini hatutakuwa
tumekuhangaisha kama tutakuuliza maswali. Kama
nilivyokwisha kwambia hawa waandishi wa gazeti la
Afrika na ni waandishi pekee walioruhusiwa
kuingia
hapa nchini kuandika juu ya tukio hili, naamini unajua msimamo wa gazeti la
Afrika.
Hata hivyo tutakuuliza maswali kidogo tu kusudi
tusikuchoshe sana".
"Hebu nipeni vitambulisho vyenu niviangalie",
aliomba.
Sherriff na Veronika walimpa vitambulisho, akaviangalia
na aliporidhika akavirudisha.
"Haya
ulizeni maswali yenu, maana ikiendelea hivi naweza kupata wazimu", alisema huku
akitoa
tabasamu la uchovu.
"Tumesoma
maelezo yako uliyotoa polisi, ila tumekuja hapa kukuuliza maswali machache juu
ya
mambo ambayo hatukuwa tumeyaelewa vizuri", alisema
Sherriff.
"Ulieleza kuwa ulipata simu kutoka kwa Jones Mantare
ambaye umezoea sana sauti yake, kiasi
kwamba
huwezi kuikosea ukiisikia. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba, Mantare anasema
hakuwa
amekupigia simu kwani alikuwa na mkutano na Mwenyekiti
wa Kamati na Mwenyekiti amethibitisha
kuwa ni
kweli walikuwa wote toka saa tisa hadi saa kumi na moja. Baada ya kupata maelezo
hayo
bado unaweza kusema kuwa sauti ile ni sawa kabisa na ya
Mantare?".
"Kwa sababu wakati ule nilikuwa sina wasiwasi kuwa kuna
jambo baya roho yangu iliridhika kuwa
ni
Mantare. Lakini sasa kwa sababu Mantare anasema hakupiga simu, ndipo nakumbuka
kuwa
nilimwuliza kama ana mafua, maana kwa mbali alikuwa
akizungumzia puani, na yeye alijibu kweli
mafua
yalikuwa yamemkaba sana. Lakini maelezo mengine, mathalani ambayo huwa
tunataniana na
Jonas, yalikuwa yote sawa. Kusema kweli inawezekana
kabisa alikuwa mtu mwingine anayemfahamu
sana,
lazima niseme sana maana isingekuwa hili jambo la mafua bado ningeendelea
kung'ang'ania
alikuwa Jones. Lakini Jones amekuja hapa hana mafua
hata kidogo kwa siku nyingi".
"Hebu
fikiria tena kidogo juu ya sura na sauti au umbile na tabia ya huyu mtu
aliyekuwa
akijiita Meja Paul Liboi, unaweza kuwa na uhakika
kabisa kuwa mtu huyu ni mzalendo wa
Tanzania?", Veronika aliuliza.
Ndugu
Mlingi alisita kidogo kujibu swali hili na uso wake ukakunjamana kidogo. Baada
ya
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kufikiri sana akasema.
"Nafikiri
anaweza asiwe mzalendo".
Wote tukamwangalia.
"Kwanini
unafikiri hivyo?", mimi nilimuuliza.
"Wazo hili
lilikuwa halijaingia kichwani mwangu, lakini sasa baada ya kuuliza swali
hili
inawezekana mtu huyu asiwe mtanzania maana kwanza
kiswahili chake hakikuwa kimenyooka na
alipenda
sana kuchanganya na kiingereza. Mimi nilimfikiria kuwa huenda ni Mjaruo,
lakini
alikuwa hajang'oa meno. Vile vile alikuwa na haraka
haraka na maneno ya mkato mkato. Nikifiri
sana
hakuna na ile hali ya kirafiki waliyonayo watanzania wengine wengi. Lakini kwa
sababu
nilijuwa ni mwanajeshi nikafikiri ndio sababu aikuwa na
tabia ya namna hiyo".
"Una jambo jingine ambalo huenda sasa unafikiri
halikuwa lakawaida juu ya tukio lolote baada
ya kujuwa
watu hawa walikuwa majahiri?".
"Nafikiri
nimeshasema yote, ila tu huenda kitu kimoja, sijui kama kinahusika ama
vipi".
"Ehe, kitu gani".
"Baada ya
kuzungumza na huyo anayejiita Jones Mantare, simu za jengo hili hazikufanya
kazi
tena. Tulipowaeleza Posta kesho yake, walikuja mafundi
na kusema waya inayounganisha jengo
hili na
waya zinazokwenda Posta ilikuwa imekatika kwa kuangukiwa na mti. Sasa nilianza
kuona
picha kidogo ya tukio hili. Nilijua mara moja kuwa watu
waliokuwa wameshughulikia tukio hili
ni watu
wenye kujua ujasusi wa hali ya juu; kwani walihakikisha kuwa kila hatua
wanayoichukua
na nyayo zake wanazifuta ili asiwepo mtu wa
kuzifuatiia".
TUjikuta tumeridhishwa sana na safari yetu ya bandarini
hivyo tukaona tuondoke.
"Asante sana ndugu Mlingi, kama tukihitaji mambo zaidi
tutakuona tena, na kama utakumbuka kitu
cochote
kinachoweza kutusaidia nipigie simu. Nafikiri simu yangu unayo?",
nilimuuliza.
"Ndio ninayo", alijibu.
"Na
tahadhali usizungumze ovyo juu ya tukio hili, maana si tukio zuri",
nilimwonya.
"Bila shaka nitajitahidi".
Tuliagana
nae, tukaondoka kuelekea mjini.
FUNUNU
"Samahani binti tunaomba kumuona Meneja",
nilimwambia mwandishi mahsusi wa Meneja wa Bandari.
"Sijui
nyinyi ni akina nani?", aliuliza msichana huyu aliyeonekana amechoka
choka.
"Mwambie ni Willy Gamba na wateja wake kutoka gazeti la
Afrika".
Meneja wa Bandari tulikuwa tunafahamiana kikazi, hasa
kutokana na shughuli zingine tulizokuwa tunazifanya katika kampuni yetu ya
Afrika Internation Agencies.
Yule
msichana alizungumza na bosi wake kwa simu, alipomaliza alinyanyuka na
kutufungulia mlango tukaingia ndani. Tulimkuta Issack Mlingi ambaye ndiye Meneja
wa Bandari aliyehusika na tukio hili akionyesha hali ya kuchoka sana. Nafikiri
hii ilitokana na bughudha alizopata toka kwa polisi na watu wengine wanaohusika
na upelelezi wa tukio hili. Macho yake yalikuwa mekundu na yamevimba.
"Karibuni
ndani", alisema huku akinyanyuka ili tusalimiane.
"Samahani
ndugu Mlingi, naamini una shughuli nyingi sana", nilimuomba radhi.
"Si kitu
Gamba, karibuni".
"Hawa ni wateja wangu Sherriff na Veronika kutoka
gazeti la Afrika ambalo kampuni yangu ni wakala wake, na jamani huyu ni Issack
Mlingi, Meneja wa Bandari", walipeana mikono kisha wote tukavuta viti
tukakaa.
"Ndugu Mlingi ni imani yangu kuwa umeisha ulizwa
maswali mengi juu ya tukio hili lililotokea hapa bandarini. Lakini naamini
hatutakuwa tumekuhangaisha kama tutakuuliza maswali. Kama nilivyokwisha kwambia
hawa waandishi wa gazeti la Afrika na ni waandishi pekee walioruhusiwa kuingia
hapa nchini kuandika juu ya tukio hili, naamini unajua msimamo wa gazeti la
Afrika. Hata hivyo tutakuuliza maswali kidogo tu kusudi tusikuchoshe
sana".
"Hebu nipeni vitambulisho vyenu niviangalie",
aliomba.
Sherriff na Veronika walimpa vitambulisho, akaviangalia
na aliporidhika akavirudisha.
"Haya
ulizeni maswali yenu, maana ikiendelea hivi naweza kupata wazimu", alisema huku
akitoa tabasamu la uchovu.
"Tumesoma
maelezo yako uliyotoa polisi, ila tumekuja hapa kukuuliza maswali machache juu
ya mambo ambayo hatukuwa tumeyaelewa vizuri", alisema Sherriff.
"Ulieleza
kuwa ulipata simu kutoka kwa Jones Mantare ambaye umezoea sana sauti yake, kiasi
kwamba huwezi kuikosea ukiisikia. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba, Mantare
anasema hakuwa amekupigia simu kwani alikuwa na mkutano na Mwenyekiti wa Kamati
na Mwenyekiti amethibitisha kuwa ni kweli walikuwa wote toka saa tisa hadi saa
kumi na moja. Baada ya kupata maelezo hayo bado unaweza kusema kuwa sauti ile ni
sawa kabisa na ya Mantare?".
"Kwa
sababu wakati ule nilikuwa sina wasiwasi kuwa kuna jambo baya roho yangu
iliridhika kuwa ni Mantare. Lakini sasa kwa sababu Mantare anasema hakupiga
simu, ndipo nakumbuka kuwa nilimwuliza kama ana mafua, maana kwa mbali alikuwa
akizungumzia puani, na yeye alijibu kweli mafua yalikuwa yamemkaba sana. Lakini
maelezo mengine, mathalani ambayo huwa tunataniana na Jonas, yalikuwa yote sawa.
Kusema kweli inawezekana kabisa alikuwa mtu mwingine anayemfahamu sana, lazima
niseme sana maana isingekuwa hili jambo la mafua bado ningeendelea kung'ang'ania
alikuwa Jones. Lakini Jones amekuja hapa hana mafua hata kidogo kwa siku
nyingi".
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hebu fikiria tena kidogo juu ya sura na sauti au
umbile na tabia ya huyu mtu aliyekuwa akijiita Meja Paul Liboi, unaweza kuwa na
uhakika kabisa kuwa mtu huyu ni mzalendo wa Tanzania?", Veronika
aliuliza.
Ndugu Mlingi alisita kidogo kujibu swali hili na uso
wake ukakunjamana kidogo. Baada ya kufikiri sana akasema.
"Nafikiri
anaweza asiwe mzalendo".
Wote tukamwangalia.
"Kwanini
unafikiri hivyo?", mimi nilimuuliza.
"Wazo hili
lilikuwa halijaingia kichwani mwangu, lakini sasa baada ya kuuliza swali hili
inawezekana mtu huyu asiwe mtanzania maana kwanza kiswahili chake hakikuwa
kimenyooka na alipenda sana kuchanganya na kiingereza. Mimi nilimfikiria kuwa
huenda ni Mjaruo, lakini alikuwa hajang'oa meno. Vile vile alikuwa na haraka
haraka na maneno ya mkato mkato. Nikifiri sana hakuna na ile hali ya kirafiki
waliyonayo watanzania wengine wengi. Lakini kwa sababu nilijuwa ni mwanajeshi
nikafikiri ndio sababu aikuwa na tabia ya namna hiyo".
"Una jambo
jingine ambalo huenda sasa unafikiri halikuwa lakawaida juu ya tukio lolote
baada ya kujuwa watu hawa walikuwa majahiri?".
"Nafikiri
nimeshasema yote, ila tu huenda kitu kimoja, sijui kama kinahusika ama
vipi".
"Ehe, kitu gani".
"Baada ya
kuzungumza na huyo anayejiita Jones Mantare, simu za jengo hili hazikufanya kazi
tena. Tulipowaeleza Posta kesho yake, walikuja mafundi na kusema waya
inayounganisha jengo hili na waya zinazokwenda Posta ilikuwa imekatika kwa
kuangukiwa na mti. Sasa nilianza kuona picha kidogo ya tukio hili. Nilijua mara
moja kuwa watu waliokuwa wameshughulikia tukio hili ni watu wenye kujua ujasusi
wa hali ya juu; kwani walihakikisha kuwa kila hatua wanayoichukua na nyayo zake
wanazifuta ili asiwepo mtu wa kuzifuatiia".
TUjikuta
tumeridhishwa sana na safari yetu ya bandarini hivyo tukaona tuondoke.
"Asante
sana ndugu Mlingi, kama tukihitaji mambo zaidi tutakuona tena, na kama
utakumbuka kitu cochote kinachoweza kutusaidia nipigie simu. Nafikiri simu yangu
unayo?", nilimuuliza.
"Ndio ninayo", alijibu.
"Na
tahadhali usizungumze ovyo juu ya tukio hili, maana si tukio zuri",
nilimwonya.
"Bila shaka nitajitahidi".
Tuliagana
nae, tukaondoka kuelekea mjini.
Nilijaribu
nilivyoweza kuangalia kama naweza kumwona Eddy na mwenzake, lakini wapi hakika
vijana walikuwa wanafanya kazi nzuri sana, maana kama mimi Willy sikuweza
kuwatambua basi hakuna mtu mwingine tena, si kama najisifu ila huo ndio ukweli,
mtu akitaka kunitafuta mimi basi ajiweke sawa, la sivyo shauri lake.
"Kamara
kama ulivyomjua alikuwa mtu wa namna gani, unafiri anaweza kwa njia yoyote akawa
kajiingiza katika jambo hili?", nilimuuliza Sherriff huku tukiwa tumesimama
kungojea kuingia barabara ya site drive, tukutokea bandarini.
"Mimi
nakuhakikishia komredi kuwa Kamara alikuwa hawezi kufanya jambo kama hilo, ni
lazima tu iko namna ambayo alishambuliwa na kunyang'anywa karatasi hizo,
alinihakikishia Sherriff.
"Oke, naona sasa twende kwenye ofisi ya kamati ya
Ukombozi ya OAU", nilimweleza huku nageuza gari kuingia site drive na kuelekea
kwenye ofisi ya kamati.
Tulipofika kwenye mapokezi ya ofisi hii ya kamati na
kumkuta msichana mmoja akizungumza kwenye simu, ikatubidi tumsubiri kidogo
amalize kuzungumza, niliangalia saa yangu ilikuwa yapata saa sita na dakika
tano.
"Samani jamani, sijui niwasaidie nini", msichana
alituuliza.
"Bila samahani binti, sisi tunaomba kumwona Jones
Mantare", nilijibu.
"Mna ahadi naye?", binti aliuliza.
"Hapa,
lakini nafikiri ukimwambia Willy Gamba wa AIA na wageni toka gazeti la Afrika,
ambao wanataka kumwona, anaweza kutuona", nilimweleza.
"Msubiri
basi", huyo msichana alijibu kisha akainua simu na kuanza kuzungumza na ofisi ya
Mantare. Jones Mantare alikuwa ananifahamu, maana nilikuwa nimehakikisha kuwa
nafahamiana karibu na kila mtu katika ofisi hii ya kamati, yeye alikuwa
akinifahamu kama mfanyabiashara, maana ndivyo nilivyojulishwa kwake. Tokea hapo
tulikuwa tunaonana mara kwa mara sehemu za starehe na kujenga uelewano wa
kutosha, hivyo nilihisi kuwa asingeweza kunikatalia nisimuone, ingawa nilijuwa
atakuwa katika hali isiyokuwa ya kawaida. Baada ya kuzungumza kwa muda kwenye
simu msichana alitwambia.
"Mnaweza kwenda kumwona, ofisi yake ipo mwisho wa ujia
mkono wa kulia".
"Asante sana binti", nilimjibu.
Tulimwacha
tukaelekea alikotuelekeza. Tulibisha mlango pale tulipokuwa
tumeelekezwa.
"Karibu", tulisikia sauti ya msichana ikitoka ndani.
Nilifungua mlango tukaingia na tujikuta katika ofisi kubwa ya mwandishi mahsusi
wa Mantare.
"Habari zako bibie", nilimsalimia kwa niaba ya
mwenzangu.
"Nzuri, ni Gamba na wenzake nafikiri?",
aliuliza.
"Hasa", nilijibu.
"Ingieni
moja kwa moja anawasubiri", alisema huku akisimama na kutufungulia mlango wa
bosi wake. Tulipoingia tu Mantare alisimama.
"Ahaa
ndugu Willy, karibuni".
"Asante, asante Jones".
"Nafikiri
niwajulishe, huyu ni ndugu Jones Mantare, ofisa katika kamati hii ya ukombozi,
na hawa ni komredi Ahmedi Sherriff na komredi Veronika Amadu. Ni waandishi wa
habari wa gazeti la "AFRIKA".
Walipeana
mikono kwa mara nyingine.
"Ehe, mlitaka kuniona, sijui niwasaidie nini?",
aliuliza.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hawa makomredi ni wateja wangu, kampuni yangu ndio
wakala wa gazeti la Afrika hapa nchini. Hasa kitu kilichotueta hapa ni kutokana
na tukio hili la juzi. Nafikiri unaelewa msimamo wa gazeti la Afrika katika
ukombozi, na kutokana na msimamo huo wameiomba serikali kama wanaweza kuandika
habari za kuaminika juu ya tukio hili. Ni wasiwasi wao kuwa magazeti mengi ya
kibeberu yataandika habari za kupotosha, na wao wako hapa ili waweze kueleza
jumuia ya ulimwengu ukweli mtupu. Kwa hiyo tutashukuru sana ukiweza kutusaidia
katika kujibu maswali machache. Hatutataka kupoteza muda wako kutueleza mengi,
maana nakala ya maelezo yako tumeipata toka polisi. Hivi ni nia yetu uweze
kutufafanulia katika sehemu ambazo hazieleweki katika tukio hili".
Niliona
kule kutaja nakala ya maelezo yake kutoka polisi kulimtoa wasiwasi aliokuwa
ameuonyesha usoni mwake. Niliona macho ya Veronika yakiwaka kuonyesha kuwa
nilivyoeleza nimeeleza vizuri sana na Sherriff alitingisha kichwa kuonyesha kuwa
niliyoyasema ni sawa kabisa.
"Sawa
ndugu Willy, nitakuwa tayari kuwajibu mwaswali yenu, kusema kweli kama
ulivyosema, radio za kibeberu zimekwisha tangaza uongo ili kuridhisha maslahi
yao. Kwa jinsi hii tutakuwa radhi kuona ukweli unaandikwa na gazeti hili. Haya
sijui mna maswali gani?".
"Inasemekana kuwa hayati Kamara Franki ndiye alikuwa
anashughulikia suala hili la silaha. Na amekutwa ameuawa. Nafikiria hizi
karatasi zilitokatokaje mikononi mwa marehemu na kuingia mikononi mwa hawa
majahiri?. Maana kutokana na maelezo ya Polisi ofisi yenu hii haikuvunjwa mahali
popote", Sherriff aliuliza.
"Sawa
kabisa?, kutokana na maelezo ya mwandishi mahsusi wa marehemu, anasema ya
kwamba?, wakati marehemu anatoka ofisini alimweleza aweke zile karatasi za
kuchukulia silaha ndani ya mkoba wake, kwa sababu alikuwa anategemea kwenda
kwenye kikosi cha Jeshi kinachoshughulikia silaha za wapigania uhuru kesho yake,
kabla hajaja ofisini. Kwa hiyo, jibu kwa swali lako ni kwamba watu hawa
walimnyang'anya marehemu karatasi hizo na ndio sababu wamemuua."
"Watu hawa
unafikiri walijuajuaje kuwa marehemu atakuwa na karatasi hizi ndani ya mkoba
wake?", Veronika aliuliza.
"Hapo
ndipo hata sisi tumekwama".
"Huyu
mwandishi mahsusi wa marehemu yupo", nilimuuliza.
"Ndio
yupo".
"Unaweza kumwita tukazungumza nae kidogo?".
"Hali yake
si nzuri sana, bado ana mshituko kwa ajili ya marehemu. Unajua mnapofanya kazi
kwa uhusiano ulio karibu na mtu mnakuwa na urafiki wa hali ya juu sana. Hata
hivyo nitajaribu kuwaitieni".
Alishika
simu na kuzungumza na mwandishi wake. Wakati tukimsubiri Veronika alimuuliza
tena. "Ofisa wa kule bandarini Ndugu Mlingi anasema mtu aliyempigia simu alikuwa
na sauti kama yako, mathalani mambo mnayotaniana yalikuwa vile vile, unaweza
kufikiri mtu yeyote hapa ofisini au hata nje anayeweza kuigiza sauti yako kiasi
hicho?".
"Ni imani yangu kuwa mtu kukuigiza kiasi hicho lazima
awe mtu aliyekuzoea, na mtu aliyekusikia ukizungumza mara kwa mara, hasa na huyu
ndugu Mlingi".
"Kuesema kweli, nimefikiria kweli juu ya mtu huyu mpaka
nimechoka, nitazidi kumfikiria kama wazo likinijia nitakupigia simu."
Mara
mlango ulifunguliwa akaingia msichana mrefu mwembamba mwenye nywele nyingi. Kama
unapenda wasichana warefu na wembamba, basi hapa pana msichana wa namna hiyo,
jina lake Margreth. Ni mzuri kiasi chake.
"Karibu
Margreth", Mantare alimkaribisha, wote tukasimama akatujulisha kwake. Mwandishi
mahsusi alileta kiti kingine na Margreth akaketi.
"Samahani
Margreth", hawa ndugu wana maswali kidogo ya kukuuliza," Mantare
alimwambia.
Margreth hakujibu kiti bali alituangalia tu.
"Samahani
sana binti, sisi wote yunaelewa hali uliyonayo, ila imetubidi tukuone tuweze
kuzungumza nawe huenda utatusaidia kutatua huu mkasa uliompata bosi wako",
nilimwelezea.
"Niko tayari kuwaelezea chochote kama kitasidia
kuwapata watu waliomuua bosi wangu." Magreth alijibu huku machozi
yakimlengalenga.
"Jaribu kukumbuka, nilimwambia, "wakati marehemu
anakueleza uweke zile karatasi za kuchukulia silaha kulikuwa na mtu mwingine
yeyote?".
Alikaa kimya kwa muda kisha akajibu, "Hapana", harafu
kama amegutuka akasema, "Ndio nakumbuka sasa, alikuwepo tarishi wetu wa hapa
ofisini".
Nikasikia kengere ya tahadhari inalia kichwani mwangu.
Wote tulitazamana.
"Tarishi huyu yuko hapa?", niliuliza.
"Hapana,
ni mgonjwa anaumwa na ameandikiwa kulala siku tano', Margreth alijibu.
"Toka
lini?".
"Toka tarehe nne".
"Yaani
siku ambayo ilibainika kuwa silaha zimeibiwa na bosi wako ameuawa?".
"Ndio".
"Yaani
atakuwa kazini tarehe tisa".
"Ndio".
"Una
uhakika kabisa alikuwepo?".
"Ndio".
Habari
kama hizi mimi ndizo huwa zinanitibua, maana wakati kifo kinatokea haafu
kinatokea kitu kingine chenye uhusiano wa karibu namna hii, basi hapo ndipo huwa
naanza kujumulisha moja kwa moja na kupata mbili.
Nilimgeukia Mantare na kumwuliza, "Huyu tarishi ndiye
alikuwa tarishi wa ofisi nzima?".
"Ndio'.
"Anaitwa
nani?".
"Anaitwa George Kiki".
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mmekuwa naye muda gari?".
"Yapata
miezi sita sasa".
"Ni MTANZANIA!".
"Hapana ni
mkimbizi kutoka Afrika Kusini, aliletwa kwenye ofisi yetu na chama cha wapigania
uhuru cha Afrika Kusini kilichopo hapa mjini cha SANP. Ili tumsaidie. Alipokuja
hapa alitupa maelezo yake na kuonekana ni kati ya vijana walioanzisha maandamano
ya kitongoji cha Soweto huko Afrika Kusini. Alieleza kuwa yeye alipata mwanya wa
kutoroka gerezani ndipo akakimbia na kuweza kufika hapa baada ya safari ndefu ya
taabu. Kwa vile alikuwa hana kisomo cha kutosha jinsi yeye alivyojieleza
tuliamua kumpa kazi ya utarishi ili kumsaidia. Kusema kweli amekuwa kijana
mwenye bidii sana, na anapendwa na kila mfanyakazi wa hapa, hasa kwa nidhamu
yake, na utekelezaji wa kazi yake".
"Kwa hivi
alikuwa na fursa ya kuingia ndani ya ofisi ya mtu yeyote wakati waowote ili
kuchukua mafaili na mambo kama hayo?".
"Hasa
ndivyo ilivyokuwa".
"Anaishi wapi?".
"Anaishi
huko Kinondoni sehemu za Hananasifu Estate katika nyumba za shirika la
nyumba".
"Nyumba yenyewe unaijuwa?".
"Mimi
nimewahi kufika kwake; tumewahi kumpeleka na marehemu", alisema Margret huku
tena machozi yakimlengalenga.
"Samahani
Mantare, sijui unaweza kumruhusu Margret akatuelekeza kwa Ndugu
Kiki?".
"Bila wasiwasi mnaweza kwenda nae".
Niliwaangalia wenzangu nikaona wameridhika na maswali
na majibu ya hapa, hivyo kwa niaba yao nikamshukuru ndugu Mantare.
"Ikiwa
tutahitaji jambo lolote tutarudi tena au tutapiga simu. Na wewe ukipata jambo
lolote usisite kutufahamisha".
"Hamna
tabu, nitafurahi kuwasaidia".
Tuliagana
tukaondoka kuelekea Kinondoni.
"Mimi
naona tukapate chakula cha mchana kwanza", Sherriff alishauri.
"Sawa",
walijibu kwa pamoja. Sherriff alikaa nyuma pamoja na Margret na wakati huo mimi
naendesha nikiwa katika mafikara mengi, Sherriff alichukua jukumu la kumtuliza
Margret akimweleza mambo mengi juu ya matatizo ya binadamu na kumwambia kuwa
asihuzunike sana maana ndiyo binadamu. Kadiri Sherriff alivyozidi kusema ndivyo
Margret uso wake ulizidi kutokwa na huzuni kwani mimi nilikuwa nawaangalia
katika kioo cha kuendeshea. Hata Sherriff alipofika kusema yeye huwa anaamini
kuwa kwa kila linalotendeka linatendeka kwa ajili ya uzuri, nilimwona Margret
anamwemwesa kwa mara ya kwanza, na ndipo sura yake ilionyesha uzuri aliokuwa
nao. Niliona hata Sherriff aligundua uzuri huo, kwani uso wake ulibadilika kiasi
cha kwamba moyo wake uliguswa.
Tulifika
New Afrika Hoteli, nikaegesha gari wote tukatoka nje. Basi, moja kwa moja
tulifuliza kwenda kwenye lifti ya kutupeleka orofa ya kwanza ambapo ndipo
Bandari Grill ilipo. Mbele yangu nilimwona Eddy anavuka sehemu ya mapokezi,
halafu akazungusha kichwa akaingia kwenye choo kilichopo hapa chini. Hii ilikuwa
ishara kuwa alitaka kuniona.
"Samahani
jamani nasikia nimebanwa haja ndogo, tangulieni nakuja sasa hivi. Margret, we
ndiye mwenyeji washughulikie wagaeni".
"Bila
wasiwasi", alijibu akiwa anaanza kupona kutoka katika mshituko
alioupata.
Niliingia maliwatoni nikamkuta Eddy
ananisubiri.
"Mpaka dakika hii hakuna chochote", aliniambia bila
kuniangalia.
"Sawa, nendeni mkale halafu nenda ofisini nitakukuta
huko kiasi cha saa kumi hivi".
"Oke",
alisema huku akielekea kwenye mlango wa kutokea.
Mimi
nilimaliZa haja yangu ya uongo na kweli nikaondoka kujiunga na wenzangu.
Tulipata muro safi sana hapa Bandari Grill, na kwa sababu kila mtu alikuwa na
njaa tulikula kimya kimya.
"Nasikia
kichwa kinaniuma", Veronika alilalamika.
"Nafikiri
kwa ajili ya hali ya hewa. Joto jingi sana kuliko ulilozoea",
nilimjibu.
"Kama ni hivyo afadhali ukameze dawa upumzike, sisi
tutakwenda kumwona Kiki halafu tutakuja kukuona", Sherriff alishauri.
"Naona
hivyo ni sawa", alijibu.
Basi tulikubaliana Veronika apumzike sisi tuendelee na
shughuli. Tuliondoka New Afrika na kumtelemsha Veronika Kilimanajaro.
"Vero
mpenzi, kuna gari lile pale unaweza kulitumia wakati wowote. swichi iko chini ya
zulia", nilimuonyesha gari ambalo Eddy alikuwa ameliacha hapo. Sisi tuliondoka
na kuendelea na safari yetu ya Kinondoni.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Twende kupitia barabara ya Upanga moja kwa moja,
halafu tukivuka Salendar briji mbele kuna barabara ya Kinondoni hivyo tutaingia
kushoto. Sehemu iko mbele ya makaburi. Baada ya makaburi kuna barabara la vumbi,
linakatisha barabara hii. Tukiacha hilo na kuendelea mbele tukakuta barabara
nyingine ya vumbi inaingia kushoto na kuna kibao kimeandikwa Bamboo Baa and
Restauranti, basi hapo ndipo tutakapoingia", alieleza Margret kwa ufasaha
kabisa.
Mimi hupenda maelezo ya namna hii, siyo mtu amefika
mahali pa kukata kona ndipo anasema, kata hapa kushoto. Maelekezo hayo ni ya
kihuni na ndiyo anayosababisha ajali nyingi.
Nilifuata
maelezo ya Margret vizuri kabisa, nilipotaka kuingia kushoto pale kwenye bao la
tangazo la Bamboo Baa and Restauranti, Margret alisema, 'Njia hapa si nzuri
twende pole pole, halafu mbele kidogo utakata kushoto tena tuelekee kwenye
nyumba hizo pale", alinielekeza na kuonyesha kwa kidole.
Niliendesha pole pole nikaikuta njia na kuifuata
kuelekea kwenye nyumba hizi za shirika la nyumba.
"Baada ya
nyumba hiyo yenye bendera ya CCM, ambayo ndiyo ya mjumbe, ya pili
yake".
"Hapa?".
"Ndio,
mlango huu huu".
Nyumba hizi zinakaa familia mbili mbili, lakini
zimetengwa katikati kiasi kwamba kila familia ina sehemu yake kamili. Tulitoka
ndani ya gari, Margret akatangulia na kibisha hodi. Lakini hatukupata jibu.
Nilisikia moyo wangu unapiga haraka haraka, hii ni sirika niliyozaliwa nayo, na
ilikuwa ni ishara kuwa kuna hatari.
"Hebu
ngoja Margret", nilimwambia nikimrudisha nyuma.
Niliujaribu mlango ukafunguka nikamwita Sherriff na
kumwambia hakuna mtu, tulifungua mlango mwingine uliokuwa unaelekea jikoni,
bafuni na chumba cha kulala. Tukiwa wote na wasiwasi tukibisha hodi kwenye
mlango wa chumba cha kulala. Lakini hatukupata jibu. Nilitoa Bastola yangu, na
kusukuma mlango wazi.
Tulimkuta mtu ambaye tuliamini ni Kiki amechomwa kisu
kifuani!, nilipomshika nikajua alikuwa amekwisha kufa saa nyingi sana. Kisu
kilikuwa kimeachwa pale kifuani. Kilikuwa kisu kikubwa na mpini wake mwekundu.
Tulimwita Margret aje atuhakikishie.
Akiwa
anatetemeka kwa woga alikuja na kusema, "Ndiye yeye masikini", akaanza kulia
tena tulimbembeleza na kumvuta na kuondoka haraka haraka ndani ya nyumba hiyo.
Tuliingia katika gari langu na kuelekea mjini. Sasa nilianza kuongeza hesabu
kwamba mbili na mbili na kupata nne. Na vile vile majahiri hawa walianza
kunitisha kwani mbinu zao zilikuwa kubwa. Lakini hata hivyo mbinu za Willy ni
kubwa zaidi.
"Mapambano yameanza Sherriff", nilisema kwa sauti
ambayo sikuamini ilikuwa yangu.
"Na kweli
yameanza", Sherriff alijibu.
Wakati huo
tulikuwa tumesimama kwenye taa za usalama barabarani za salendar briji
tukuelekea New Afrika. Saa yangu ilisema ni saa kumi na dakika mbili.
"Naona
mimi mnifikishe nyumbani", Margret aliomba.
"Unakaa
wapi".
"Ninakaa kwenye orofa pale nyuma ya Rex
Hoteli".
"Nazijua orofa hizo, uko orofa ya ngapi, maana tunaweza
kukuhitaji ama kikazi ama katika hali ya kustarehe, unasemaje?".
"Karibu
mimi niko orofa ya pili chumba namba kumi na nane. Simu yangu ni
22221".
Basi wakati huo tulikuwa tumefika Posta ya Azikiwe,
tulipofika kwenye sanamu ya Bisimini, tukaingia Independent Evenue.
"Unajua",
Margret alitugutusha.
"Ehee", nilijibu na kumwangalia ndani ya kioo cha
kuendeshea, maana yeye alikuwa amekaa nyuma.
"Sijui ni
mafikara yangu, ila tu limekuja kama wazo la kunishangaza, maana baada ya
kutokea mambo haya kila kitu nakiona si cha kawaida kinanigutusha".
"Nini
kimekugutuusha?", Sherriff aliuliza akionesha msisimko.
"Unajua
pale kwenye lango la kuingia ndani ya ofisi yetu kumekuwa na mwendawazimu ambaye
amekaa pale zaidi ya mwezi mzima. Amekuwa amevaa matambalatambala tu na amebeba
makopo mengi, sijui mmemuona?".
"Mimi
nilimwona", Sherriff alijibu.
"Mimi
sikumwona".
"Polisi walikuja kumchukua siku moja, na kumpeleka
kunakohusika lakini hazikupita saa tatu akarudi. Alikuwa hatoki pale hata dakika
moja, usiku na mchana kutokana na walinzi wa usiku wanavyosema. Leo mlipokuja
alikuwepo maana mimi niliona gari lenu linaingia wakati natoka kunywa chai. Gari
lenu lilipoingia na yeye alivuka lango akaingia ndani. Hii ni kawaida yake,
kwani huwa anaombaomba kwa kila mgeni anayefika pale ofisini na ndio sababu
aliitiwa polisi kwa sababu anawafadhaisha wageni wetu. Gari lenu mliliegesha
mbele kabisa ya mlango wa kuingia mapokezi na kutoka ndani ya gari haraka hivyo
hakuwahi. Mimi nilipoingia pale mapokezi nilikuta nyinyi mmekwisha kwenda
ofisini kwa Mantare ila nilimkuta yule kichaa anamuuliza yule msichana wa
mapokezi. Hawa watu wanasema wanatoka katika gazeti la Afrika. Yule msichana wa
mapokezi alikasirika na kumfokea, Toka hapa! kama wanatoka gazeti la Afrika
watakufaa nini wewe?, wana kazi ya maana kuliko kuonana na mwendawazimu kama
wewe. Toka!".
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kitu cha kushangaza ni kwamba wakati tunaondoka pale
ofisini kwetu nakumbuka sikumuona wala makopo yake na kilago chake hakikuwepo,
sijui jambo hili lina maana yoyote au mnaonaje nyinyi wenyewe?", alimalizia
Margret.
"Unasema alikuja hajawahi kutoka pale hata dakika moja,
ila tu siku ile aliyochukuliwa na polisi kwa muda wa masaa matatu?",
nilimuuliza.
"Nina uhakika kabisa maana mimi damu yangu ilikuwa
haipatani na yule mtu kabisa, na ni mimi niliyefanya kampeni ya kumuitia polisi
lakini aliporudi alionekana kuwa maafisa wote walidharau kumchukulia hatua
tena".
"Ukimwangalia alikuwa anaonekana kichaa au unafikiri
anajifanya tu?", nilimuuliza.
"Kitu
kilichonikosanisha naye ni kwa sababu siku moja aliniambia yeye si kichaa ila
anajifanya tu ili kujipatia pesa bila jasho. maana ilikuwa ukimwangalia sana
wakati yeye hana habari anakuwa kama si mtu kichaa, ila huwa anapoona watu
anakuwa kichaa kabisa".
"Asante sana, kumbuka jambo hili linaweza likawa na
msingi tutaliangalia".
"Asante".
Niliegesha
gari mbele ya Rex Hoteli.
"Wakati wowote tutegemee", nilimweleza huku
akitelemka.
"Mnakaribishwa", akiwa zaidi anamwangalia Sherriff.
Sherriff alitoa mkono wake wakapeana mikono. Tayari kulikuwa na kitu kinapita
kati yao, maana nyuso zilikuwa wakati wanapeana mikono, mimi ndiye najua, maana
hata mimi hali hii inanitokea. Walikuwa wameanguka katika penzi.
"Mimi
naona turudi pale ofisi ya kamati tukahakikishe kama kweli hayupo pale yule
kichaa", nikimwambia Sherriff.
"Sawa".
Tulikwenda
kimya kimya kila mtu akichambua mambo, tuliyokuwa tumeyapata na kuyaona,
tulipofika pale ofisini tulimkuta mlinzi wa jioni anayeingia kazini saa tisa
wanapofunga kazi mpaka saa kumi na mbili asubuhi, ilionekana alikuwa
anafanyakazi masaa mengi sana, lakini yeye alipenda kazi yake na kuridhika na
kipato alichokuwa anakipata, baada ya kutusalimia na kutueleza hizo saa zake za
kazi, nilimuuliza.
"Unajua kulikuwa na mzee mmoja kichaa hapa sijui
amehamia wapi?'.
"Hata mimi nashangaa, kichaa huyu alikuwa hatoki hapa
hata dakika moja. Hata haja zake alikuwa akiifanya hapa hapa karibu. Polisi
walimchukua hapa akawachenga akarudi mwishowe wakamwachia akae tu. sasa leo
nafika nakuta kiisha ondoka na wala harufu yake hakuna. Nimeshangaa sana. Amekaa
karibu mwezi mzima".
"Ulikuwa unapata fursa ya kuzungumza nae?".
"Si mara
nyingi, ila tu siku moja nilikuja na ..........akasita kusema.
"Sema tu
usiogope, hata kama ni siri, sisi tutakufichia".
"Lakini
nyinyi ni akina nani?".
"Sisi tunashughulikia wagonjwa wa akili, tumepata
habari toka polisi kuwa kuna mwendawazimu hapa, hivyo unaweza kutueleza tabia
yake ili tuweze kumtafuta. Kwa hiyo usisite kutueleza", nilidanganya.
Baada ya
kutafakari mambo haya aliendelea, "Siku moja kulikuwa na tafrija hapa ofisini
jioni. Mimi niliweza kwa mbinu zangu kujipatia mzinga mzima wa whiski aina ya
'Dimple' nikauficha wagaeni wote walipoondoka, nilitoka nje ya lango na kuanza
kunywa huu mzinga wa whiski. yeye alipoona ninakunywa hii whiski alikuja na kopo
lake akaniomba kwa vile nilikuwa najuwa siwezi kumaliza chupa nzima nilimgawia
nusu basi alikunywa ile pombe kama maji. Basi ilipomkolea akaanza kuzungumza
Kiingereza ila mara kwa mara alisema neno sijui 'Sazafrika' neno hili alilirudia
mara nyingi. Na nyinyi mnajua vichaa mimi niliachana nae nikaendelea na shughuli
zangu. Sasa sielewi kama kilikuwa Kiingereza sawa sawa. Lakini kitu
kilichonivutia ni kule kutamka hicho Kiingereza chake kama mzungu. Lakini husema
kichaa ana mashetani saba, anaweza kuzungumza lugha saba tofauti."
"Asante
sana, na samahani sana kwa kukubugudhi", Sherriff alitoa mfukoni shilingi
arobaini akampa. Yule Mzee alifurahi sana.
"Mungu
awaongezee wanangu".
Tuliingia ndani ya gari tukaondoka zetu.
"Unaona
mambo yalivyo Sherriff?, hii inaonyesha wazi kuwa George Kiki alikuwa ni jasusi
aliyepachikwa hapa na mabeberu na wakafanikiwa. Mimi simulaumu mtu yeyote, hata
mimi huenda ningemsaidia kupata kazi. Baada ya mabeberu kujua mkataba wa silaha
kati ya PLF na Urusi miezi sita iliyopita walichukua hatua ya kuhakikisha hizo
silaha haziwafikii wapigania uhuru wa PLF maana inasemekana ni silaha za kisasa
kabisa. Tutakapoonana na kiongozi wa PLF atatueleza zaidi, kuajiliwa kwa kiki
miezi sita iliyopita kunaoana kabisa na nyakati za mkataba huo. Inaonekana kazi
ya jasusi huyo ni kujua mambo yote yanayotendeka juu ya huo ili mwishowe aweze
kuiba hizo karatasi za kuchukulia silaha, jambo hili amefanikiwa", nilinyamazi
kidogo.
"Kwanini wamwue?", Sherriff aliuliza.
"Kwa
sababu hawakuwa na haja nae tena, asije akashikwa na kutoa siri. Hii
inanionyesha jinsi watu hawa walivyo wajuzi katika kazi yao, hawataki kufanya
makosa".
Wakati huu tukizungumza tulikuwa tukielekea
mjini.
"Juu ya huyu kichaa unasemaje?".
"Huyu
kichaa nae ni jasusi. Ninavyoona mimi huyu aliwekwa pale ofisini kusudi aweze
kuona nini kitatokea hapo ofisini baada ya silaha kuibwa. Aliwekwa mwezi mmoja
ili kuondoa mashaka. Hivyo alikuwa anangoja kuona baada ya polisi na maofisa wa
usalama ni nani mwingine aliyekuwa na dukuduku juu ya jambo hili. Aliposikia
waandishi wa habari wa gazeti la Afrika nao wamejiingiza akawa amemaliza kazi,
akaondoka kwenda kupeleka ujumbe, ni wazi kabisa wao walijuwa polisi na maofisa
wa usalama watalishughulikia jambo hili na ninafikiri walishapima uzito na kuona
wanaweza kukabiliana nao. Hivyo walingoja wajue kama kuna kundi jingine
litakalojiingiza katika katika upelelezi wa tukio hili. Sasa wamejua; kwa hivyo
waandishi wa gazeti lazima muwe macho. Tokea sasa kaeni katika tahadhari; lolote
linaweza kutokea. Unaonaje maoni yangu?'.
"Lo Willy,
ndio maana wewe ni mpelelezi maarufu katika Afrika. Maelezo yako yanaeleza hali
halisi kabisa. Na swali ulilomuuliza Margret kama kuna mtu mwingine aliyeweza
kuona akiweka karatasi ndani ya mkoba, mimi nilikuwa silifikilii kabisa na ndilo
swali lililotupa mwanga. Kweli kila mtu na kazi yake", alisifu
Sherriff.
"Lakini maswali mliyouliza ninyi vile vile ni ya maana
sana, nafikiri kuliko waliyoulizwa na Polisi. Sidhani Polisi wameishafikia hii
tuliyofikia kwa muda huu mfupi".
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara wazo likanijia.
"Lile
jambo lililokuwa linakutatanisha nimepata jibu lake. Swali la nani aliyepiga
simu kwa Mlingi akiiga sauti ya Mantare na maneno ya Mantare aliyozoea
kuzungumza na Mlingi".
"George kiki", alijibu Sharriff.
"Kabisa,
unajuwa Kiki alikuwa anaingia ndani ya kila ofisi ya ofisa akiwa kama tarishi.
Swali hili nilimuuliza Mantare akakubali. Hivyo Kiki akiwa jasusi
aliyefundishwa, ninavyofikilia, haikuwa kazi kumsiliza Mantare katika simu zake
nyingi na ninafikiri alifanya kila njia kusikiliza simu kati ya Mantare na
Mlingi. Hii inaonekana wazi kabisa".
"Lo
tunaanza kuona mwanga sasa", Sherriff alisema.
"Kweli
tumeona mwanga, lakini ni mwanga unaotufikisha kwenye giza nene. Maana Kiki
ambaye angetupa fununu ya watu hawa amekufa, yule kichaa lazima ameshapotea
hewani, gtumerudi pale pale".
"Watu hawa
ni akina nani na silaha hizi ziko wapi?", niliuliza swali hili wakati naegesha
gari New Afrika.
"Hilo ndio swali gumu lakini afadhali tunajua Afrika
Kusini inahusika, maana Kiki katokea huko. Na yule kichaa alipolewa alizungumzia
Sozafrika ambayo nasadiki ni South Afrika".
"Sawa
kabisa, lazima tujuwe tunapambana na South Afrika na haikosi shirika lao la
ujasusi 'BOSS', linasaidiwa na mashirika mengine ya ujasusi ya nchi za kibeberu.
Hivyo tutakuwa na kazi ngumu maana watu hawa nimewahi kupambana nao ni watu
hatari kabisa".
"Tumwombe Mungu atasaidia".
"Na wewe
ukijisaidia", nilijibu.
Wote tukacheka na kutoka ndani ya gari. Ilikuwa saa
kumi na moja. Hivyo kabla hatujavuka barabara nilionelea nifike ofisini kidogo
halafu niende nyumbani.
"Sherriff mimi nafika nyumbani kidogo, nitakuona saa
kumi na mbili kamili".
"Sawa nitakusubiri hapa duka la kahawa".
oke basi
saa kumi na mbili".
Niliingia ndani ya gari na kuondoka. Nilipofika ofisini
nilimkuta Eddy na vijana wengine. Linda alikuwa ameshaondoka.
"Eddy kuna
mtu mmoja anaitwa George Kiki, alikuwa akifanyakazi kwenye ofisi ya Kamati ya
ukombozi kama tarishi?, hapa aliingia kama mkimbizi baada ya kutoroka Afrika
Kusini. Alifika ofisi za chama cha SANP, ambao walimpeleka kwenye Kamati ya
Ukombozi waweze kumsaidia angalau kazi yoyote. Inawezekana hana kisomo cha
kutosha. Nataka ukague habari hii kwa kutumia njia zetu za kawaida. Unaweza
kuwajulisha makomredi wetu kule Soweto, nadhani watakuwa na maelezo kamili.
Habari hizi nazitaka haraka. Kila kitu, aliingiaje hapa alikwendaje kwenye ofisi
za SANP alikuwa anaishi namna gani, nani walikuwa rafiki zake nk. wewe
unajua".
Eddy aliyekuwa anachuku maelezo haya alijibu.
"Atashughulikiwa bosi, usiwe na wasiwasi".
"Chifu
yuko?".
"Kaondoka".
"Haya
asante, usitoke mpaka nitakapokujulisha tena".
"Mimi
nipo".
Ndio sababu nilimpenda mtoto huyu. Nidhamu yake kwangu
ilizidi ya mdogo wangu ambaye tumetoka ndani ya tumbo la Mama Willy. Niliingia
ndani ya gari nikaelekea zangu Upanga.
Niliposimamisha gari mbele ya mlango, moja kwa moja
macho yangu macho yangu yakaangukia kwenye kitu kilichokuwa kwenye ubao wa juu
ya mlango mkubwa wa kutokea nje. Nilitoka nje ya gari haraka haraka nikiwa
tayari kwa mapambano.
Nilikuta ni kisu chenye mpini mwekundu kama kile
tulichokikuta kwenye kifua cha maiti Kiki; ncha yake ilitumiwa kama kipini cha
kubandika kipande cha karatasi pale mlangoni.
Niliking'oa nikachukua karatasi na kusoma
yaliyobandikwa hapo yalisema.
Willy
Gamba, kama unathamini maisha yako achana na hao watu wa gazeti la Afrika. na
kama ni rafiki zako waambie waondoke hapa mjini tunawapa mpaka saa kumi na mbili
jioni wawe uwanja wa ndege. Vinginevyo yaliyompata Kamara Frank yatawapata na
nyinyi. Hili ni onyo kali na si mchezo. Shughulika na mambo yako usishughulike
na mambo ya watu wengine. Wapo wenyewe wanaohusika waachie. Nasema tena saa kumi
na mbili jioni leo wawe uwanja wa ndege na wewe baada ya kuwafikishia habari
hizi tusikuone unashughulika zaidi ya kazi yako ya kawaida ya AIA
Subiani.
Kwanza nilicheka maana niliona kazi sasa inaanza. Hii
inaonyesha upelelezi wetu ulikuwa umewashitua kuliko wa Polisi. Nilijua yule
kichaa alifanya kazi yake vizuri sana, maana ni yeye tu aliyetufahamisha kwa
majahiri wenzake. Hiki kisu chenye mpini mwekundu ilimaanisha damu. Nami niljua
damu imeanza kunuka.
Nilifungua mlango nikaingia ndani, nikakoga haraka
haraka kisha nikabadilisha nguo nilifungua sanduku langu la silaha na kuchukua
bastola zingine mbili kwa madhumuni ya kuwapa Sharriff na Verokika kwani
hakukuwa na mchezo tena, maana upatapo onyo toka kwa watu kama hawa huwa
hawatanii. Kisha niliinua simu na kupiga kituo cha Polisi cha Salendar
Bridge.
"Hallo kituo cha Polisi hapa".
"Sikiliza,
nenda Kinondoni Hananasifu, Estate kwenye nyumba ndogo ndogo za shirika la
Nyumba nambari IIC utakuta kuna maiti ambayo ina zaidi ya masaa ishirini na
nne", kabla hajatamka neno nilikata simu. Niliangalia saa yangu muda ulikuwa
umekimbia na ilikuwa saa kumi na mbili kamili. Niliingia ndani ya gari
nikakimbilia New Afrika.
Nilipoingia duka la kahawa sikumwona Sherriff nikapata
wasiwasi. Nikaenda mapokezi kuuliza wakaniambia aliacha habari kuwa amekwenda
dukani mara moja nimsubiri. Nilirudi nikasimama nje pale magari yanapoleta watu
New Afrika yanapozungukia. Niliangaza huku na huku na mara nikamwona Sharriff
anakuja akiwa anavuka tawi la Benki ya nyumba. ghafla alipokuwa anataka kuvuka
barabara ilitokea gari sijui wapi ikapiga breki, wakatoka watu wawili haraka
kama umeme, wakamvuta Sharriff ndani ya kiti cha nyuma cha gari, na gari hilo
likaondoka tena kama umeme. Kitendo hiki hakikuchukua hata nukta tano.
Watu wote
waliduwaa wasijue cha kufanya, lakini mimi Willy nilijua la kufanya. Nilikimbia
kwenye gari Eddy alilokuwa amekodi na kuliacha New Afrika. Kwa vile alikuwa
ameliegesha vizuri niliingia na kuondoka kama umeme. Nilikuwa nimeona lile gari
linakata kulia kutoka barabara ya Azikiwe kuingia Azania Front. Nilipoingia
Azania Front niliona gari lao linafika kwenye ofisi za NASACO
nikacheka.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
TWATOANA JASHO
Niliongeza
gari moto ili wasije kunipotea. walikata kulia wakaingia mtaa wa Railway,
nilipoingia mimi mtaa huu wao walikuwa wamefika kwenye mzunguko wa 'Clock Tower'
na kuingia mtaa wa Nkurumah.
Kwenye
mtaa huu wa Nkurumah niliwakaribia kabisa, nikiwa nimeacha gari mbili tu kati
yangu na wao. Niliona mmoja katika gari lao akitoa kichwa nje na kuangalia
nyuma, nadhani wanadhani nitawafuata na gari langu ambalo wanalijua sana. Lakini
hawajui Willy ni mtu wa namna gani. Wakati huo nilikuwa naendesha gari aina ya
Fiat 132 GLS, na si Colt Gallant Sports kama ambavyo walikuwa
wanafikiria.
Walikwenda moja kwa moja na kushika barabara ya Pugu.
Walipofika kwenye njia panda ya barabara ya chang'ombe na Pugu, walikata kushoto
na kuingia barabara ya Chang'ombe. Saa hizi magari hayakuwa mengi hivyo kila
gari lilikwenda kasi. Nilikuwa na bahati kuwa magari yale mawili yaliyokuwa kati
yangu na wao nayo yalikata na kuingia barabara hiyo hiyo kuzidi
kunificha.
Walipofika kwenye sehemu ambayo barabara ya Mbozi
inagongana na Chang'ombe walikata kulia na kufuata barabara hiyo. hizi gari
mbili mbele yangu zilionyesha kuwa zilikuwa zinaendelea na barabara ya
Chang'ombe. Nilipunguza mwendo ili wasije wajanitambua. Mara nilisikia wanapiga
honi ya namna ya pekee kabla ya kufika kwenye jengo la Kampuni ya rangi ya
Sadolins.
Ghafla lango la uwa la bohari moja lilifunguliwa na
bila hata kupunguza mwendo, gari hii ilikata kushoto na kuingia ndani na hapo
lango likafungwa. Mimi nilipitiliza kama kwamba sina habari na watu hawa.
Ilikuwa inakaribia saa moja za jioni, hivyo giza lilikuwa limeanza kuingia.
Nilisimamisha gari langu kama mita mia mbili hivi, nikaanza kurudi haraka kwa
miguu.
Bohari hili ambalo lilikuwa limezungukwa na ukuta wa
matofali ya saruji, lilikuwa limeandikwa 'Mamlaka ya Pamba'. Mimi nilishangaa
sana kwani sikujua hii ni maana gani. Ukuta wa uwa huu ulikuwa na urefu usiozidi
futi kumi na mbili, hivyo kwangu ukuta kama huu kuupanda ni kazi ndogo.
Nilikwenda kwenye upande wa lango kubwa, nikazunguka pembe ya kushoto ya uwa
huu. Ukuta huu ulikuwa unapakana na ukuta wa bohari nyingine la namna hiyo hiyo
kwa upande huu wa kushoto.
Nilikwenda
kama hatua tatu hivi kwenye nafasi hii ya kati ya mabohari haya, nikavua viatu,
nikarudi nyuma kidogo halafu nikaurukia huu ukuta na kuukwea huku mikono yangu
ikikamata juu yake. nilivuta mwili wangu wote kimya kimya kama paka
nikachungulia ndani ya uwa.
Pale
karibu na mlango nilimwona mtu amevaa koti refu la khaki rangi nyekundu
lililokuwa linavuka magoti yake kidogo huku ameshikilia bunduki ya aina ya 'SMG'
na akiangalia mlangoni. Bila kufanya hata chembe ya kelele nilivuta mwili wangu
wote na kutambaa kama nyoka juuya ukuta huu uliokuwa na upana wa futi moja.
Nilitambaa mpaka nikawa karibu kabisa na mtu huyu kwa juu yake bila yeye
kufahamu. Nilijirusha chini na kufanya kishindo kidogo nae akageuka. Mimi
nilikuwa tayari nikamkata karate ya shingo kabla hajajua nini kinamjia.
Akazilai. Nikamshikilia na kumlaza chini taratibu. Muda kitambo
aloikufa.
Nilimvua lile koti lake nikalivaa mimi, halafu
nikamnyanyua tena nikamlalisha chini na kumwegemeza kwenye ukuta. Nilichukua
bunduki yake ambayo ilikuwa imejazwa risasi, nikafurahi sana kishika silaha
namna ile. Mimi nikiwa na silaha namna ile hata likija jeshi la watu mia
hawaniwezi. Nilijidhatiti tayari kwa mapambano zaidi nikanyata kwenda nyuma ya
jengo la bohari ambako niliamini kuna mlango mwingine. Nilipofika kwenye pembe
ya ukuta wa kushoto nilichungulia. Niliona kuna mlango wa mbele wa mlango
alisimama mlinzi mwingine akiwa amevaa sawasawa na yule wa kwanza; koti refu
jekundu.
Alikuwa nae ameshika bunduki ina ya 'SMG', niliona
anafungua mlango anasema kwa sauti kali "Fanhyeni haraka bwana, kama hataki
kueleza si niambieni mimi akaonane na babu zake huko ahera". Alirudisha mlango
akaangaza huku na huku. Kutokana na maelezo yake ni kwamba Sherriff alikuwa
anaswalishwa na majahiri na bila shaka alikuwa akipata kipigo kikubwa.
Nilitumbukiza mkono ndani ya mifuko ya koti nililovaa
nikakuta mna sigara na hamna kiberiti. Wazo likanijua nikamfanyia yule mlinzi
'sss' aligeuka akaniona akidhani ni mwenzake, nilimuonyesha sigara na kuwa
nataka moto. Bila kusita akaja akatoa kiberiti na kwa ajili ya giza sasa
hakuweza kunitambua sababu ya lile koti. Aliponyoosha mkono kunipa kiberiti.
Kama radi nilimrukia na kumpiga karate ya mikono miwili shingoni. Sikuwa na haja
ya kumwangalia maana nilijua kwa kipigo hicho hawezi kuishi. Nilimvutia upande
huu wa kushoto na kumwegemeza kwenye gari lao. Nilichukua bunduki yake iliyokuwa
na ukanda mrefu nikaingika begani na kuiweka mgongoni.
Sasa njia
ilikuwa wazi kwenda mpaka mlangoni, kwa kutokana na ujuzi wangu wa kuiga sauti
ya yule mlinzi wa nje kwa maneno yake aliyosema mimi nilisema. 'Vipi hajasema
lolote?," nikiwa nimefungua mlango kidogo na kuchungulia ndani. Bohari lilikuwa
limejaa robo tu ya marobota ya pamba. Sherriff alikuwa ameshikwa na watu wawili
na mmoja alikuwa amebeba bao akimtandika tumboni kwa nguvu sana.
"Sema nyie
si waandishi wa magazeti ila ni wapelelezi, ndio".
"Yote ya
kweli nimeshaeleza ".
Kabla hajaanza kumpigab tena nilisema. "Mmoja wenu aje
hapa, mimi mnanijua hivyo hatachukua dakika kabla hajasema uweli
wake".
Shomvi alikuja akikimbia, nikamfungulia mlango na
kurudisha mara moja. Alipoangalia ba kutambua mimi si Luis akataka kupiga kelele
lakini nilimwahi karate ya katikati ya kichwa akafa bila kelele. Watu wa mle
ndani waliokuwa wamemshikilia Sherriff walikuwa hawana bastola mikononi ila
zilionekana kwenye mapaja. Nilifungua mlango ghafla SMG mkononi nikamwahi mmoja
wao kabla hata hawajaelewa nini kinatokea.
"Ukijaribu
chochote umekufa", nilisema kwa sauti ya kutetemesha.
Sherriff
alishangaa kuniona akaruka ile maiti akasimama upande mwingine. Niliona ile SMG
ya pili nikampa, akatabasamu. Jinsi alivyoijaribu mkononi nilikua huyu mtu
anajua kuitumia.
"Chukua hizo silaha zake", Sherriff alimkagua akatoa
bastola mbili zenye sailensa na visu viwili vyenye mpini mwekundu.
"Ah, ni
wakati wako sasa kujibu maswali yetu, nyinyi ni nani", nilimwuliza.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mimi sijui, mimi niliajiriwa tu leo hii asubuhi na
Kimkondo, huyu uliyemwua hapo chini, kuwa kuna kazi ya kumkamata mtu mwenye
habari ambazo wakubwa wake wanataka. Pesa tulizolipwa zilikuwa nyingi, shilingi
elfu kumi kwa kila mtu kwa kazi ya masaa machache tu nami nikakubali, kusema
ukweli sijui lolote".
"Yeye Kimkondo anafanya kazi gani?".
"Yeye ni
jambazi tu anayepewa kazi ya ujambazi hapa na pale".
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment