Simulizi : Vipepeo Weusi : Mkakati Namba 0034
Sehemu Ya Tano (5)
Akanieleza kuwa nyumba hiyo ilikuwa imekodiwa kwa miaka mingi na benki kuu kutoka kwa mwanachama mmoja wapo wa The Board. Baada ya Benki kuu kuacha kutumia nyumba hiyo kuhifadhi sarafu The Board wakaendelea kuitumia Nyumba hiyo kwa shughuli zao nyingine.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kaburu akanieleza kuwa katika kumbukumbu za jiji nyumba hiyo imeorodheshwa kama “ghala” lakini kiuhalisia nyumba hiyo iko tupu. Haina watu wanaoishi wala hakuna kinachohifadhiwa.
Kaburu akanieleza kuwa mara chache The Board huwa wanafanya vikao vyao humo.
Kaburu alinieleza kuwa hisia zake kwamba The Board wananweza kutumia nyumba hiyo kama sehemu ya dharura kuhifadhi files zinatokana na kwamba nyumba hiyo ndiyo sehemu salama zaidi kwa dharura ili kuweka kuitumia kwa madhumuni hayo.
Kaburu akanieleza kuhusu milango ya chuma na “Vault” ya kienyeji iliyotengenezwa na Jeshi La Kujenga Taifa (JKT) iliyotengenezwa miaka hiyo ya sabini kipindi ambacho Benki Kuu ndio ilikuwa inaanza kutumia nyumba hiyo kuhifadhi sarafu.
Kutokana ma sababu hizo, Kaburu alikuwa na uhakika kabisa kuwa hapo ndipo files zitaenda kuhifadhiwa kwa dharura.
Taarifa hii ilikuwa ni taarifa adhimu sana, lakini rohoni mwangu nilikuwa sidhani kama The Board, wanaweza kwenda hapa Upanga moja kwa moja kuhifadhi files.
Kutokana na mpango wangu wa kuwatumia Usalama Wa Taifa kama chambo kwenda CRBB tawi la Lumumba, nilikuwa naamini kwamba Mallya na The Board wataamini kuwa Idara ya Usalama wa Taifa ndio ambayo inahusika pekee kwenye mpango huu.
Kwahiyo niliamini kwamba, kama The Board wataamini kuwa Idara ya Usalama Wa Taifa wamegundua zilipo file zao, lazima watahisi kuwa labda wamefahamu hata historia kiduchu ya The Board na nyumba hiyo ya Upanga waliyokuwa wanahifadhi files zamani.
Kwahiyo hapa ndipo nikawaza kwamba napaswa kutumia kwa ufasaha ile nadharia yangu ya “long con”!
Nikawaza kwamba, kama nikifanikiwa kuwaaminisha The Board kuwa Idara ya Usalama wa Taifa wanafahamu file zilipo, na hatimaye wakahisi kuwa pia Idara ya Usalama wabafahamu kuhusu nyumba ya Upanga, watabakiwa na chaguo pekee la kwenda nyumbani kwa Mallya ili wakajipange kutokea hapo kujua wapeleke wapi file.
Lakini kama nitafanikiwa kuwapandikiza vijana ambao wataenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Mallya kama Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, habari hii ikiwafikia Mallya na The Board kuwa kuna upekuzi unafanyika nyumbani kwake na Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, moja kwa moja wataamini kuwa ‘kumbe’ Usalama wa Taifa hawafahamu kuhusu nyumba ya Upanga, kwa sababu ya simple logic tu.. Kama wangejua kuhusu nyumba ya Upanga na inavyotumiwa na The Board basi wangepeleka Maafisa huko pia kufanya upekuzi.
Ndipo hapa nikahisi kuwa The Board wataona nyumba ya Upanga kama sehemu salama ya kuhifadhi faili hizo kwa muda pasipo kujua kuwa nawaingiza kwenye mtego niliouandaa mahususi. kabisa.
Ndipo hapa ulikuja umuhimu wa kuwasiliana na Chifu, yule Mzee wa Kipemba wa Mbagala Kizuiani. Kwa kuwa Chifu alikuwa ni ‘mchora ramani’ mzuri wa matukio ndipo hapa nilihitaji anisaidie.
Chifu alikuwa anatakiwa kuandaa vijana wake maeneo ya Upanga na kufanya ambush, pindi ambapo Mallya na na wenzake wakifika kwenye nyumba ya Upanga.
Niliwataka watumie utaalamu wao na uzoefu wao, wasubiri Mallya na wenzake wakiingia ndani ya hiyo nyumba ndio wafanye ambush. Nilitaka tukio hilo lifanyike bila majirani kujua kinachoendelea.
Kwa kuwa sikuwa na fedha ya kutosha, maana tulikuwa tumebakiwa kama na milioni nne tu na tulikuwa hatuwezi kutoa fedha kwenye akaunti zetu kuhofia kujulikana sehemu tulipo, hivyo ilinibidi kutumia ushawishi wa hali ya juu kumfanya Chifu akubali kunisaidia mpango huu.
Ahadi yangu kwake ilikuwa kwamba kama angenisaidia kufanikisha hili nilikuwa tayari kumkabidhi na kummilikisha kampuni ya ulinzi ulinzi binafsi, yaani ‘Perolsonal Security’ au ‘bodyguards’ kwa lugha nyingine.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hapa nilikuwa nalenga wale vijana walionisaidia kufanikisha kuwaingiza The Board kwenye mtego.
Kwahiyo nikamuahidi kuwa kutokana na siri nzito nilizonazo ambazo zitahitajika na Idara ya Usalama Wa Taifa, nitatumia ushawishi na akili yangu yote kuhakikisha kuwa anapewa deal ya thamani kubwa kuhusu masuala ya ulinzi kupitia kampuni hiyo.
Japokuwa tulikuwa tumefahamiana kwa muda mchache na Chifu labda ilikuwa ngumu kwake kuniamini kwa asilimia zote, lakini nilijua pasina shaka kuwa alikuwa anaamini uwezo wangu wa akili na ushawishi kutokana na mambo machache aliyonisguhudia nikiyafanya kwa siku hizi chache zilizopita.
Chifu akakubali kunisaidia kipengele hicho cha ambush.
Ndipo hapa siku ya leo mimi na vijana wangu tulikuwa tumemaliza kufanikish a kuwaingiza The Board katika mtego, kilichokuwa kimebakia ni Chifu na vijana wake kutimiza wajibu wao.
Tulikubaliana kuwa nikamsubiri nyumbani kwake, ndiyo sehemu pekee salama anayoiamini ili kunikabidhi ‘mzigo wangu’ endapo wakifanikiwa.
******************
Kama majira ya saa moja kasoro, mimi na Cheupe tulikuwa tumefika nje ya geti la nyumba ya Chifu Mbagala Kizuiani.
Baada ya kushuka kwenye taxi, tuligonga mara moja tu na tukafunguliwa geti bila kuulizwa chochote na yule binti tuliyemkuta siku ile ya kwanza.
Tofauti na siku ya kwanza leo hii walikuwa mabinti wawili, wakatukaribisha moja kwa moja mpaka sebuleni na kutuletea vinywaji juisi bila kutuuliza chochote kile.
Nikaelewa kuwa leo alikuwa ameachiwa maagizo kuhusu ujio wetu ndio maana ahoji maswali yoyote.
Tukaka pale sebuleni karibia dakika ishirini pasipo kuongea chochote kile.
Cheupe akainuka na kuja kukaa karibu yangu.
“Calm down honey! Its going to be OK!” Akaniuliza huku ananipapasa mgongoni.
“This has to work!” Nikainuka kwa kupaniki na kuanza kutembea tembea pale sebuleni.
Kila baada ya dakika nilitupa jicho kwenye saa ukutani, huku naendelea kutembea tembea.
Damu ilikuwa inanichemka na presha imenipanda kweli kweli.
Nikaanza kufikiria itakuwaje kama hili suala halitafanikiwa?? Nitafanya nini?? Maana akili yangu yote nimeiwekeza kwenye mpango huu.. Kama hili halitafanikiwa hakika ni hakika naelekea kuingia kwenye mtafaruku mkubwa na Idara ya Usalama wa Taifa.
Kwanza nimewazunguka kuhusu suala hili, na si hivyo tu lazima watakuja kugundua kitengo feki cha Idaya ya Usalama wa Taifa nilichokianzisha.. Ukijumlisha yote haya hawawezi kuniacha salama! Lazima wanimalize..
Na hilo likitokea vipi kuhusu Mzee wetu wanaye mshikilia? Nini kitamkuta??
Nini pia kitamkuta Cheupe wangu?? Nini kitatokea kwa mwanangu tumboni??
Presha ilizidi kunipanda…
Wakati nikiwa kwenye hili lindi la mawazo, ghafla tukasikia honi inapigwa nje.
Yule binti mmoja akatoka nje haraka kwenda kufungua geti.
Nikasikia kwa makisio kama magari mawili yameingia.
“Kaniandalie kisanduku cha first aid jikoni..!!” Wote pale sebuleni tulisikia sauti ya Chifu akimuamuru mkewe huko nje.
Mara ghafla mkewe akarudi anakimbia kuelekea jikoni.
Muda huo huo wakaingia vijana wawili wamembeba mwenzao watatu mabegani na upande mmoja wa ubavu ameloa damu tapa tapa, huku akionekana dhahiri amepoteza fahamu.
Presha ikanipanda zaidi. Kijasho kikaanza kunitoka.
Mara akaingia Chifu ameongozana na vijana wengine wawili.
Wale vijana wawili walikuwa wamebebab mabegi mawiliakubwa ya mgongoni. Kwa muonekano wa jinsi yalivyokuwa yametuna ilikuwa dhahiri kwamba walikuwa wameficha bunduki.
Chifu mwenyewe hakubeba chochote.
Akili ikakumbuka haraka haraka jinsi yule kijana wangu Echo wa Team C alivyonielezea hayo alichobeba Mallya wakati anatoka Golden Jubilee Tower.. “mikoba miwili myeusi ya kiofisi”.
Jambo la ajabu Chifu na vijana wake hawakuwa na mikoba yoyote myeusi ya kiofisi zaidi ya mabegi ya mgongoni yenye bunduki.
Nikamuangalia tena yule kijana wa Chifu aliyebebwa mabegani akipelekwa jikoni huku damu ikivuja na kuancha mstari kutoka sebuleni kuelekea jikoni
Nikajihisi nakaribia kuzimia, nililoa jasho mwili mzima, presha ikiwa juu kweli kweli.
” Chifu nini kimetokea??” Nikauliza huku natetemeka jasho likinitoka.
“Nifuate ofisini kwangu” Chifu akanijibu bila kuniangalia akielekea kwenye kile Chumba anachokiita ofisi.
Nikahisi Dunia yangu yote inapasuka vipande vipande. Miguu yote ikafa ganzi nisiweze hata kupiga hatua.. Moyo ilikuwa unaenda kasi kweli kweli.
Nikavuta pumzi ndefu ndani na kuzishusha. Nikajikaza kiume kuelekea kule ofisini kwa Chifu.
Nilikuwa natembea taratibu kana kwamba nanyatia kitu fulani. Kuna upende fulani wa moyo wangu ulikuwa hautamani nifike kule kwenye chumba cha ofisi ya Chifu, nilitamani niaifahamu kilichotokea, sikutamani kusikia ananiambia “tumezikosa files”.
Nikapiga hatua za taratibu mpaka kwenye kile chumba anachokiita ofisi na kuingia.
Chifu mweneze alikuwa ameketi chini kwenye zuria la manyoya kama kawaida. Mbele yake kulikuwa na kifungu cha majani kama mchicha ambayo nilipoangalia vizuri ninagundua kuwa ilikuwa ni mirungi. Kwa kiasi fulani nilimuona kuwa alikuwa na wasiwasi japokuwa alikuwa anajifahidi aonekane yuko kawaida.
” Nini kimetokea Chifu?” Nikauliza nikiwa bado nimesimama mara baada ya kuingia.
“Kaa chini kijana!” Akanijibu bila kuniangalia.
Sikutaka kuwa mbishi, nikaa chini na kusubiri jibu lake.
“Wale watu ni kina nani hasa maana siku ile umekuja hapa na Eric mlinieleza juu juu tu.!” Akanijibu huku anaongea mdomoni amejaza fundo la mirungi shavu moja limetuna kama vile anaumwa jino.
“Chifu hayo sio maswali ya kuulizana sasa hivi.. Kama ulikuwa na maswali kama haya ungeniuliza toka juzi! Tafadhali nieleze ni nini kimetokea??” Nikamjibu huku nahema juu juu.
“Sijawahi kuona nyumba binafsi ina vault ndani, vault ambayo hata matawi ya kawaida ya benki hawana.. Na hizo files unazozitaka wanazilinda kuliko hata uhai wao.!” Akaongea bila kuniangalia, huku anachambua vijiti vya mirungi kwa mdomo utadahi mbuzi anatafuna mchicha.
“So what happened??” Nikamuuliza kana kwamba sikusikia alichokuwa anaongea.
“Aisee! Ilibakia kidogo tuwamiminie risasi kwa kujihami.. Ubaya tu nina Sheria moja katika kazi zangu.. Ni marufuku kuua mtu” akaongea huku anaendelea kuchambua mirungi kwa mdomo.
“Na files zimekuwaje?” Nikauliza safari hii kwa hasira.
“Tumezipata!” Akanijibu na kuniangalia usoni.
Nikahisi kama moyo umesimama ghafla. Badala ya kuruka kwa furaha, jasho likaanza kunitoka na presha kupanda tena. Sikutegemea hili jibu.!
“Whaaaat??” Nikauliza kwa mshangao nikihema.
“Ndio kijana.. Tumezipata file zako.!!”
“Ziko wapi?” Nikauliza kwa papara.
“Taratibu kijana.. Utafahamu! Nimekuita huku ofisini ili tuongee kwanza kabla ya kukukabidhi.”
“Mambo gani?” Nikaanza kupandwa na hasira kwa mbali. Nikahisi kama huyu Mzee anataka kunizunguka.
“Una uhakika kuhusu ulichoniahidi.. Maana nadhani jinsi hili suala lako lilivyonigharimu.. Kijana wangu mmoja amepigwa risasi, nategemea atapona lakini itanigharimu fedha nyingi sana kumtibia na itachukua miezi mingi kabla hajarudi tena kazini.. Ndio maana nakuuliza una uhakika kuhusu ulichoniahidi?” Chifu akaniuliza huku amenikazia macho.
“Chifu nisikilize, nimekwambia nitakukabidhi kampuni ya ulinzi pamoja na tenda za kuanzia kazi moja kwa moja na namaanisha hilo.. Liko ndani ya uwezo wangu.!” Nikaongea kwa kujiamini ili kumpa Chifu uhakika wa ninachokisema.
“OK! Nataka iwe milioni 120.!”
“Milioni 150 zimefanyaje?”
“Huo mkataba wa kwanza wa tenda nitakaopewa, nataka thamani yake isipungue milioni 150”
“Its done! Nitahakikisha hilo linafanyika..” Nikamjibu tena kwa kujiamini.
“OK! Inabidi uondoke usiku huu na mzigo wako..” Akaongea huku anaanza kuinuka.
“Alafu sijaona kama mna huo mzigo kwa kadiri ninavyoufahamu ‘mzigo’?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kijana huwezi kufanya tukio na kwenda kulala chumba kimoja na ulichokiiba.. Ikitokea umekamtwa unakuwa umerahisisha kabisa kupatikana ushahidi… Kwahiyo tumeuhifadhi mahala Salama.. Ukishanieleza wapi unaelekea basi tutaangalia tuupitie vipi mzigo nikiwa nakusindikiza..”
“Nashukuru sana chief, asante sana kwa msaada wako… nakuahidi sito kuangusha kwa hili nililokuahidi!”
“Na jitahidi usiniangushe kijana.. Maana mimi sio serikali, nitakutafuta na tutamalizana kwa mtindo kama huu huu niliokusaidia.!”
Nikamuelewa. Hiyo “mtindo kama huu huu niliokusaidia” alikuwa anamaniisha risasi na umafia ulitumika kupata files.
Hii ilikuwa ni mara ya kwanza chief kunipiga mkwara tangu nimefahamiana naye, na nilijua fika kuwa alikuwa anamaanisha alichokisema.
“Kijana usidhani nawafukuza… mngeqwza kulala hapa muondoke kesho lakink kutokana na uzito wa hili suala sitaki wahusika wote tuwe sehemu moja ikitokea siri imevuja.. Kwahiyo hii ni tahadhari kwa usalama wetu sote… pamoja na hilo wale watu kule upanga kuna wawili tumewapiga risasi mguuni na mmoja ubavuni.. Sitaki waendelee kuvuja damu vile wasijekupoteza maisha yakazuka mengine.. Kwahiyo muda si mrefu tuna itaratibu wetu wa kuwataarifu polisi wafike pale” akaongea huku anabofya bofya simu na kuiweka sikioni.
“Usijali Chief! Naelewa vizuri tu!”
“Juma, lete gari nyumbani!” Akaongea na simu yake, kisha akakata.
“Kwa hiyo niwapeleke wapi?”
“Aaahh tupeleke tu magomeni.. Magomeni mapipa!” Nikawaza haraka haraka na kumjibu.
Tukatoka kule ofisini na kurejea sebuleni.
“Vipi huyo hali yake?” Chief akamuuliza moja ya mabinti wale wawili ambaye alikuwa anapita pita kila mara pale sebuleni.
“Imetengamaa kiasi!” Yule binti akajibu huku akielekea kule jikoni aliko kijana wa Chief aliyepigwa risasi.
Nikaenda mpaka alipo Cheupe na kuanzia kumsaidia kubeba mabegi yetu ya nguo na kumuashiria kwamba “safari imeiva”.
” how is it?” Cheupe akaninongoneza.
“So far, so good” nikamjibu kwa sauti ya chini.
Tukatoka ndani pale wote wa Tatu mpaka nje kwenye geti. Hapo tukakuta kuna taxi imepaki, nikahisi huyu ndio Juma aliyepigiwa simu na chief kwamba alete gari.
“Kakabidhi hesabu kwa mama ndani mimi nina safari kidogo” Chief akamueleza Juma huku tukiwa tunapanda kwenye ile Taxi.
Chief akakaa kwenye usukani na mimi na Cheupe tukakaa siti ya nyuma. Safari ikaanza.
Tulipotokea tu barabara kubwa ya kizuiani, chief akatoa tena simu akabofya bofya kisha akaweka sikioni.
“Kilwa road, Mtoni kwa Azizi Ally! Niko na taxi yangu” akaongea na simu kwa kifupi tu kisha akakata simu.
Akaendesha gari huku wote tukiwa kimya bila kuongeleshana chochote mpaka tulipofika mtoni kwa azizi ally. Akapaki gari pembeni karibu na kona ya barabara inayochepuka kwenda Chang’ombe.
Tukasubiri hapo kama dakika tano hivi, mara ikaja gari ‘Rav 4’ nyeusi ikapaki karibu yetu.
Akashuka jamaa mwenye mwili uliojengeka hivi amevalia tisheti nyeupe na jinzi bluu.
Mikononi alikuwa amebeba “mikoba miwili myeusi ya kiofisi”.! Roho yangu ikapasuka, paaaaaaaaaa.!!
Akaja mpaka kwenye dirisha la upande aliokaa chief, Chief akashusha kioo.
Hawakusemeshana chochote, yule jamaa akamkabidhi Chief mabegi kisha akarudi kwenye gari yake na kuondoka kwa mwendo wa kasi.
Chief akafunga kioo kisha akageuka na kunikabidhi “mzigo” wangu. Nikapokea huku mikono inatetemeka. Kwa kiasi fulani nilishindwa hata kushangilia maana nilijihisi kama vile naota. Finally, files ziko mikononi mwangu.!! Nilihisi hii ni ndoto hakika, labda nisubiri mpaka nikipata wasaa wa kuzipekua na kuhakiki ndio zenyewe ndipo nitang’amua huu ni uhalisia na si ndoto..!!
Cheupe akanikumbatia kwa nguvu na kunibusu shavuni, “You did it!”
Nikashindwa hata kujibu, nikabaki nakodolea macho tu ile mikoba niliyopewa.
Chief akawasha gari na tukaifuata tena kilwa road, kisha akaanza kuifuata Mandela Road.
“Mbona unapita huku, nimekueleza tunaenda magomeni mapipa!” Nikamueleza huku nimekumbatia “mzigo” wangu utadhani katoto kachanga.
“Tumepita hiyo njia wakati tunatoka upanga.. Sitaki kupita tena.. So tutapita ubungo, then tutarudi mpaka magomeni”
“Ooh OK!” Nikamjibu huku natazama ile mikoba yenye files.
“Unafahamu kilichomo kwenye hii mikoba? Umeangalia” nikamuuliza Chief.
“Hapana, sifahamu na sijaangalia.!” Chief akanijibu huku amekaza macho kwenye barabara.
“Hujapata hamu hata ya kuangalia ukizingatia jinsi tulivyosumbuka namna hii ili kuipata?” Nikamuuliza tena.
“Ray, kazi yangu ilikuwa kufanya ambush na kuchukua hiyo mikoba.. Kuhusu kilichomo ndani sihitaji kufahamu.. Hivyo ndivyo ninavyofanya kazi yangu.. Natimiza wajibu wangu tu! Mengine namuachia client mwenyewe..”
“OK! I like that, very professional.. Lakini mimi ningekuwa wewe ningechungulia walau mijue nilichomo ndani.!”
“Hahah! Ukizingatia kwamba watu tulioenda kuzipokonya walikuwa tayari kufa lakini sio kutuacha tuchukue hiyo mikoba.. Hiyo ina maana kuwa kuna siri nzito sana humo..”
“Kwahiyo hutaki kujua siri nzito?”
“Ray, kwa umri wangu huu na shughuli ninazozifanya nimejifunza mambo mengi sana.. Moja wapo ni ‘mind your own business’.. Kutojiingiza kwenye mambo ambayo hayanihusu.. Na kuhusu kujua siri nzito, nimejifunza kwamba sio kila siri ina faida ukiijua.. Kuna siri nyingine ukishazijua zinakuondolea kabisa amani yako kwenye maisha.. Kwahiyo ni bora kutokujua muda mwingine”
Chifu akaongea huku macho ameyakaza barabarani. Maneno yake haya yalinichoma mno. Yalifanana kabisa na kile alichonihusia Kaburu kuwa nisiangalie hizi file nikipata, nisitake kujua kilichopo ndani.
Sikumjibu Chifu kitu chochote, nikakaa kimya tu.
Tulipofika Ubungo kwenye mataa tukapinda kulia kuifuata Morogoro Road na kama dakika 15 baadae tulikuwa tumefika Magomeni Mapipa.
Tukashusha mabegi yetu, Cheupe akiwa amebeba mabegi ga nguo na mimi nimeshikilia ile mikoba miwili myeusi.
Baada ya hapo, tukaagana na Chief na akaondoka na kutiacha hapo.
Ilikuwa tayari inakaribia mishale ya saa Tatu usiku hivi.
“Why tumekuja mapipa?” Cheupe akauliza mara tu baada ya Chifu kuondoka.
“Tunaelekea Ubungo Ila sikutaka afahamu tunakoenda.. Nadhani hata yeye amejua hilo.!”
Nikamjibu Cheupe huku naita taxi.
Baada ya taxi kuja tukapanda na akatupeleka moja kwa moja Ubungo. Tuliposhuka hapo ikabidi niongee na wale ‘wapiga debe’ wa magari ya mkoani kuwa tuna haraka tinaenda Iringa atuelekeza kama tunaweza kupata usafiri wa gari ‘private’ linaloelekea huko muda huu.
“Kuna jamaa ana Harrier anenda Mbeya, anataka abiria watano tu twendeni huku.”
Tukaongozana naye mpaka karibu na Ubungo Maji.
Hapo tukakutana na hiyo gari na huyo muhusika. Alikuwa bado hajapata ‘abiria’ hata mmoja kwahiyo mimi na Cheupe ndio tulikuwa abiria qa kwanza. Nikaingiza mkono mfukoni na kutoa elfu tano nikampa yule mpiga debe aliyetuleta ili aondoke tuongee na huyu jamaa.
“Mwana, sisi tunataka utuache Kibaha Maili moja tu hapo..” Nikamueleza baada ya yule mpiga debe kuondoka.
“Aaaaahh sasa maili moja si mpande Kosta au Noah, kuna gari kibao mnapata..” Jamaa akanijibu huku amekereka haswa.
“Tuna haraka sana ndio maana”
“Dah mi nataka abiria wa Iringa au Mbeya, angalau hata ungekuwa unaenda Morogoro ningekupakia”
“Skia mwana, nakulipa elfu hamsini… unatuacha Maili moja hapo unaendelea na safari zako naamini huwezi kukosa kichwa Chalinze au Morogoro”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Uko serious??” Jamaa akaniuliza kwa mshangao.
Sikutaka maneno mengi, nikazama mfukoni na kutoa noti tano za elfu kumi kumi na kumkabidhi.
Tukapanda kwenye gari na kuondoka.
Uzuri ilikuwa ni Usiku kwa hiyo hakukuwa na foleni kubwa, mpaka kufikia saa Tatu na nusu tulikuw a tumefika Kibaha, Maili Moja.
Tukashuka kwenye gari na jamaa akendelea na safari yake ya Iringa.
Baada ya kushuka, tukavuka barabara mpaka upande wa pili na kuelekea Njuweni Hotel ambapo tukachukua chumba namba 1023 ili tupumzike kwa usiku wa Leo na kupanga mkakati wa hatua inayofuata kumaliza suala hili.
“Opppppppppsss…!!” Cheupe alijirusha kitandani baada ya kuingia chumbani.
“Pole mama, I can imagine kiasi gani umechoka.. It has been a long day..” Nikampa pole huku naweka mezani ile mikoba myeusi.
“Aiseee…” Cheupe akajibu huku anainuka kutoka kitandani na kuja karibu na meza niliposimama.
“Hongera sana kichwa.. You did it.!!” Akanipongeza na kunibush midomoni.
“No.. We didi.. Nisingefanikiwa hili bila wewe.. Thank you honey..” Nikamjibu huku namrudishia mabusu mdomoni.
“Sasa inabidi tujadili ‘kifuatacho ITV’ nikitoka tu chooni” akaongea huku anaelekea bafuni.
“Sawa mama!” Nikamjibu nikimuangalia akiingia bafuni na kufunga mlango.
Nikakaa kwenye kitandani na kuanzia kuvua viatu. Macho yangu yalikuwa yameganda kwenye ile mikoba myeusi yenye files za The Board. Kila nilivyojitahidi nisifikirie, nijifanye kama vile hazipo pale, lakini akili ilikuwa inakataa. Niliendelea tu kuikodolea macho.
Nikaanza kukumbuka maneno ya Chief, kwamba kuna baadhi ya siri ukizijua unaweza kujikuta unakosa amani maisha yako yote.
Kisha maneno ya Kaburu yakaanza kupita kichwani, kwamba nisifungue na kuangalia hizo files. Si lazima kujua kila siri. Kina siri ukizijua unaweza kujuta na kutamani usingeli zijua. Kwamba muda mwingine, ‘ignorance is a blessing’.
Namna ambavyo Kaburu alinambia maneno yale ilikuwa kana kwamba kuna kitu Fulani hivi anakijua na kwa utashi wake alikuwa hatamani mimi nikifahamu kwa faida yangu.
Kadiri nilivyofikiria hivi ndivyo ambavyo moyo wangu ulizidi kutamani kujua kilichomo, japokuwa roho yangu ilikuwa inaniambia nisifungue hizo files lakini moyo ulikataa, ulitamani kujua kuna nini.
“Honeeeyy.. Mi naoga kabisa.!” Cheupe aliota kutoka bafuni.
“Okey honey!” Nikamjibu kwa kifupi.
Nikasimama na kuanza kusogolea tafatibu meza zenye ile mikoba kama vile nanyata.
Nilipofika mezani nikaushika mikoba mmoja na kuanza kuufungua. Mikono ilikuwa inatetemeka.
Ndani yake kulikuwa na mafaili makubwa manne. Kwa haraka haraka kila file ilikuwa na karatasi kwa makadirio zisizopungua mia moja.
File zile kwa juu ziliandikwa. TBS I, TBS II, TBS III na TBS IV.
Nikatafsiri hii ‘TBS’ kama ‘The Board Strategy’ hivyo nikaelewa kwamba mafaili haya ndio yalikuwa yanamikakati ya The Board, kuanzia mkamati wa kwanza mpaka huu wa sasa wa 34.
Nikaweka mkoba huu pembeni. Nitapitia hiyo mikakati mmoja mmoja baadae.
Nikafungua mkoba wa pili. Huu nao ulikuwa na mafile makubwa maane yenye karatasi nyingi kila file kama mkoba ule wa kwanza. Tofauti ni kwamba file hizi ziliandikwa tofauti.
File ya kwanza ilianzikwa; Brothers
Baada ya kupitia haraka haraka karatasi zake nikaelewa kuwa file hii ilikuwa na majina ya wanachama wa The Board tangu kuanzishwa kwake mpaka sasa.
File ya pile iliandikwa; Friends
Nayo nilipopitia haraka haraka nikaelewa kuwa ilikuwa na majina ya vibaraka wa The Board serikalini na sekta binafsi na maelezo yao kuhusu maisha yao, familia zao, historia zao na kadhalika.
File ya tatu iliandikwa; Books
Nayo baada ya kuipitia haraka haraka nikaelewa kuwa ilikuwa na orodha za akaunti za siri za The Board, nyumba za siri, magari, kampuni na mali nyingine wanazozimiliki kwa usiri mkubwa.
File ya nne ilikuwa tofauti na nyingine zote. Kwanza ilikuwa juu imeandikwa Chairmen Memos.
Nikaelewa kuwa file hii ilikuwa imebeba moja ya siri kubwa zaidi ndani ya The Board.. Chairman!
Ndani yake ilikuwa na vi-file vingine vidogo vitatu.
Ki-file cha kwanza kiliandikwa SIR. NIXON MURPHY (1951 – 1968). Kilikuwa na kama karatasi ishirini hivi au thelathini.
Ki-file cha pili kiliandikwa CHANDE R. CHANDE (1968 – 1984). Hiki kilikuwa na kama karatasi hamsini hivi.
Nikapigwa na butwaa na bumbuwazi. Chande Ramadhani Chande, Waziri Mkuu kipindi cha awamu ya kwanza ya uongozi kumbe alikuwa ni mwanachama wa The Board. Na sio mwanachama tu bali pia alikuwa Chairman. Aisee..
Nikafungua ki-file cha tatu.
Ki-file hili kilikuwa tofauti kabisa na file zote. Kwanza kilikuwa na karatasi nyingi zaidi, kama karatasi mia hamsini au mia mbili hivi.
Nilipoangalia juu kilivyoandikwaanzoni nikahisi nimesoma vibaya. Baada ya kusoma tena mara ya pili nikahisi labda macho yangu yana tongo tongo hayaoni vizuri. Nikayafikicha kwa nguvu na kusoma tena.
Sikukosea, wala sikuwa naota, nilichokiona ndicho kilikuwa sahihi. Nilisikia kama moyo unataka kupasua kifua na kutoka kwa jinsi ulivyodunda kwa nguvu.
Nikahisi pumzi zimekata. Mwili mzima ilikuwa ganzi sikuweza hata kutikisika. Ndani ya sekunde kumi tu shati lilikuwa limelowa jasho kama nakimbia marathoni.
Nisikia kichwa kinakuwa chepesi, nilisikia kama nataka kufa. Nilijihisi kama ufahamu unapotea.
Ile file ndogo ya tatu ilikuwa imeandikwa.
CHARLES B. KAJUNA (PRESENT)
“Ray… Ray! Ray.. Raaayyyyy!! Rayyyy.!!
Sijui ni kwa muda gani Cheupe alikuwa amesimama pale chumbani na kuanza kuniita baada ya kutoka bafuni. Inawezekana hata ni dakika kumi nzima, lakini sikusikia mpaka sasa hivi. Akili haikuwepo kabisa, na hata mimi mwenyewe nilihisi sikuwepo.
“Ray.. What’s wrong!” Cheupe akaniuliza huku amekodoa macho kwa woga kuniona katika hali ile.
Nikageuka kama roboti kumuangalia nikiwa bado kamkama sijitambui, na neno pekee nililoweza kulitamka ni,
“Cheupe… we are in big trouble.!”
1992: DAR ES SALAAM
Charles akiwa ameongozana na vijana watatu wanausalama wa The Board pamoja na kijana mwingine wanne ambaye alikuwa kamasaidizi wake, walikuwa Upanga kwenye jumba la siri mali ya The Board.
Jumba hili ndilo ambalo kwa miaka kadhaa lilikuwa linatumika kuhifadhi sarafu za benki kuu ingawa kwa sasa karibia miaka mitano limekuwa tupu baada ya Benki kuu kuacha utaratibu wa kuhifadhi hapa sarafu.
Leo hii kulikuwa na shughuli maalumu ya siri inaendelea hapa.. The Board walikuwa wamemleta hapa kwenye jumba hili kijana wa kitanzania Yusuf Someti kwa ajili ya kuunda bomu!
Yusuf alikuwa amwishi Pakistani kwa takribani miaka kumi. Licha ya kwamba alikuwa huko Pakistani kwasababu ya masomo lakini haijulikani haswa ni namna gani akiwa huko alikiwa amejifunza vitu vya hatari ikiwemo kuunda mabomu.
“Vipi maendeleo..” Charles akamuuliza Yusuf mara baada ya kuingia kwenye chumba kikubwa cha gereji iliyomo ndani ya jumba hili ambayo ina mlango wa geti la kuvuta kutoka juu karudi chini.
“Mpaka jioni nitakuwa nimekamilisha kama mtakuwa mmenipatia vifaa nimalizie kusuka ‘detonator’!” Yusuf akajibu huku akiwa anendelea na shgughuli yake.
“Na bado umeshikilia msimamo wako kuwa hutaki kushiriki kwenye tukio?” Charles akamuuliza huku anasogelea gari ambalo Yusuf alikuwa analifanyia kazi.
“Nimeshakueleza boss, nikimaliza kuunda mnachokitaka unanilipa hela yangu na wala sitaki kushiriki mnakokwenda kulipua na wala sihitaji kufahamu.” Yusuf akamjibu kwa lafudhi yake ya kitanga huku anaendelea kupakia viroba vya mbolea kwenye gari.
Walichokuwa wamekifanya, walikuwa wamechukua gari aina ya “hiace” kama tunavyoziita, kisha wakatoa siti zote na kuacha siti mbili za mbele pekee. Kisha ndipo ndani ya gari hii Yusuf alikuwa anafanya “installation” ya bomu.
“Kwa hiyo likishakamilika linafanya kazi, yaani namaanisha.. Linalipukaje??” Charles akauliza huku anazunguka zunguka kutazama gari kila upande.
“Bado haujanieleza kama ni Shambulio la kujitoa muhanga au Shambulio la kumdhuru mnayemlenga tu?”
“No no no! Hakuna mambo ya kujitoa muhanga hapa.. Sio mujahedeen sisi.. Tunataka kumpeleka kuzimu tunayemlenga tu.!”
“Na tukio litafanyika wapi?” Yusuf akauliza huku ameacha kuunga unga nyaya pale kwenye gari na kumuangalia Charles.
“Mbona una maswali mengi sana Yusuf.. Nadhani umesema hutaki kujua zaidi.?” Charles akamjibu huku anatabasamu kwa kumuinjoi.
“Sihitaji kujua zaidi lakini nimekuuliza hivyo ili nijue natengeneza waya wa urefu wa kiasi gani kitoka gari litakapokaa mpaka mlipuaji atakapo kuwepo.!”
“Usijali kuhusu hilo Yusuf.. Tengeneza ways wenye urefu ambao utakiwa Salama kwa mlipuaji asifikiwe madhara ya mlipuko.!”
“Sawa boss.!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“So, how does this work?” Charles akauliza huku anasogelea pale karibu na gari inayoundiwa bomu.
“Don’t worry, nitatengeneza switch mlipuaji kazi yake itakuwa ni kubonyeza switch tu!”
“That’s good! Lakini umesema wewe hutakuwepo kwenye tukio so nataka unipe details kamaili ili nijue kila kitu.. Huwezi kujua labda kitu Fulani kitasumbua.. Si unaona jinsi makorokoro yalivyo Mengi?” Charles akaongea huku anagusa gusa vifaa pale kwenye gari.
“Please please! Naomba usiguse chochote, tafadhali sana.!” Yusuf akahamaki.
“Ooohh samahani.. So how does this work?” Charles akauliza tena.
“Tatizo sidhani kama utanielewa!” Yusuf akamjibu bila kumuangalia akiendelea kuunga unga nyaya.
“Try me!” Charles akamjibu huku akiwa makini kumsikiliza.
“OK.!” Yusuf akaanza kumjibu na kumuelezea.
“OK… kama nilivyokusisitiza kuwa nahitaji mniletee TNT ili nikamilishe kutengeneza tunaita ‘detonator’.. Sasa mlipuko wenyewe unaanza kwa kulipuka ‘detonator’ ambayo nitaitengeneza kwa TNT na malighafi nyingine.. ikishalipuka inatengeneza kitu tunaita ‘detonation wave’… sasa nishati ambayo iko kwenye detonation wave kiwango kikubwa cha Ammonium Nitrate kilichopo kwenye mbolea ku-vaporise.. Nadhani unanielewa nikisema ku-vaporise??”
“Yes, nakuelewa..!!”
“OK.. Baada ya ku-vaporise.. Maana yake kwamba mbolea ile ambayo ni solid ghafla ndani ya robo sekunde inageuka kuwa gesi kwasababu Ammonium nitrate inagawanyina katika molecule za Ammonium na molecule za Nitrate ambazo nazo zinavunjika vunjika na kuacha ghafla kiwango kikubwa cha Oxygen.. Hii oxygen inachochea zaidi uwezo na nguvu ya detonation wave na kufanya mafuta ya kwenye gari na fuel tutakayoweka pembeni ya detonator kuungua kwa kasi zaidi… na kadiri fuel itakavyoungua inasababisha oxygen zaidi kutolewa kutoka kwenye break down ya Ammonium na nitrate na hivyo detonation wave inapata kasi zaidi na nguvu zaidi.. Tuko pamoja??”
“Yes nakusikiliza..!”
“Kumbuka hiyo process yote niliyokieleza inatokea ndani ya muda mfupi sana usiofika hata robo sekunde.. Kwahiyo nguvu ya nishati na joto linalotengenezwa na detonation wave inakuwa ya ghafla na inasafiri kwa ghafla kwa kasi kubwa ipatayo karibu speed ya kilomota tano kwa sekunde.. Na kasi hii ya detonation wave pamoja na nishati na joto inayosafiri nayo ndio ule mlipuko.. Na ndio inayodhuru, kuua na kuleta madhara mengine.. Kwahiyo that’s it..!!”
Yusuf akamaliza kuelezea na kugeuka tena kuendelea kuunga unga nyaya kwenye gari.
“Wow! That’s genius.. I like that..!” Charles akasifia huku anapiga makofi nankugeuka kumuangalia msaidizi wake yule aliyekuja naye. “Yusuf.. Mpaka jioni malighafi za kitengeneza detonator zitakuwa zimekufikia.. Tafadhali hakikisha kuwa mpaka kesho asubuhi nikija uwe umemaliza kwasababu tayari kwa upande wetu tuko nyuma ya ratiba.!” Charles akaongea huku anafunga vizuri vifungo vya koti la suti kuashiria anataka kuondoka.
“Ukifika kesho utakuta kila kitu kiko tayari.. Usisahau mzigo wangu!”
“Usijali Yusuf.. Pesa yako iko tayari.. Kesho utakabidhiwa..!” Charles akaongea huku anageuka na kuanza kuondoka na walinzi wake ma yule msaidizi wake.
Moja kwa moja wakapanda katika magari, ambapo Charles na yule msaidizi wakapanda gari moja huku yule msaidizi akiensesha na wale walinzi watatu wakapanda gari nyingine.
“Chairman! Una hakika kuhusu hili?” Yule msaidizi akauliza.
“Shirima, nisikie.. Kama tusipo muondoa Rais basi atatumaliza sisi sote..!” Charles akamjibu kwa kujiamini.
“Nafahami hilo chairman, lakini je haudhani labda tutumie njia nyingine.. Maana nahisi Rais akiuwawa kwa dizaini hii moto utakaowaka kwenye vyombo vya Usalama utatugjarimu mno..” Yule msaidizi, shirima akaeleza.
“Shirima tumejitahidi kuwa diplomatic lakini wenzetu wamekuwa wahuni.. Waziri mkuu Chande amewekwa kizuizini miaka karibia minne na baadae amefariki kwa utatanishi mkubwa na mimi na wewe tunafahamu pasina shaka kuwa ile ni assassination.. Chifu Sekioni vivyo hivyo.. Ni vizuri nilijiuzuru Ugavana kwa hiari yangu la sivyo mpaka sasa yawezekana wangekuwa wameshaniondoa.. Kwahiyo ni vyema tumuwahi kabla hajatuwahi.. Licha ya hayo yote pia uwepo wake serikalini unakwamisha kuanza kwa mkakati namba 0032.. We need to do this fast.!”
“Sawa Chairman!” Shirima akamjibu kwa utii.
“Ni lini ulisema unatakiwa uondoke kwa ajili ya masomo yako ya PhD? Ulisema itakuwa Princeton, right??” Charles akauliza.
“Ndio Chairman, ni Princeton University! Na mwezi ujao natakiwa niondoke!” Shirima akajibu tena kwa unyenyekevu.
“Itakuwa vizuri sana ukiwa nje ya nchi.. Nitaitisha kikao cha dharura kesho.. Baada ya hili tukio nataka tu-‘lay low’ kwa miaka miwili.. Nataka kila mtu ‘apotee’.. Tutasitisha shughuli za The Board kwa miaka miwili.. Kisha 1994 tutarejea tena ili tuanze michakato ya kumuaandaa mtu wa kumuingiza Ikulu Mwaka 1995 ambaye atatusaidia kufanikisha mkaka 0034.!”
Charles akaongea tayari wakiwa wameikamata barabara ya Old Bagamoyo kuelekea Mbezi Beach.
****************
Majira kama ya saa tatu usiku, Charles na mkewe Sophia walikuwa kwenye meza ya chakula wakijadili mustakabali wa familia yao.
“Baba Dorothy huwezi kunisafirisha mpaka Bukoba na watoto wadogo hivi.. Kuwa na huruma tafadhali.!” Sophia aliongea kwa sauti ya unyonge karibu atoe machozi.
“Mama Doro, nimekwambia Rweyemamu unaweza kumuacha kwa dada yangu Mwembe Chai.. Kwa nini utakaka tubishane kila siku?” Charles akaijibu huku akijitahidi kuzuia hasira zake.
“Charles siwezi mumuacha mtoto wa miaka miatu ma mtu mwingine.. Watoto wadogo namna hii.. Samahani Charles siwezi kufanya hivyo.!” Sophia akalalama.
“Sophia.. Huyo Dorothy sio mtoto mdogo, ana miaka 17.. angekuwa kijijini angekuwa ameshaolewa.. Lakini Rweyemamu nakuomba umiache Mwembe Chai kwa dada.. Ninakwambia hivi kwa nia njema kabisa.. Kuna sababu za kiusalama ambazo siwezi kuzijadili na wewe, na ndio maana nakwambia kuwa nahitaji umuache Rweyemamu kwa Dada Mwembe Chai.. Nahitaji abaki hapa Dar as Salaam ambapo mimi nipo.. Wewe na Dorothy nendeni Bukoba.. Nisamehe kwa hili Sophia.. Ila tunafanya hivi kwa muda tu.!”
Charles akajitahidi kuongea kwa sauti ya kubembeleza. Licha ya kubadilika sana na ukaribu na mkewe kupungua tangu ajiunga na The Board Takribani miaka 16 iliyopita lakini bado kwenye sakafu ya moyo wake alikuwa ana upendo na mkewe Sophia.
“Sababu gani za kiusalama mme wangu.. Kwa nini umekuwa hivi baba Dorothy kwanini??” Sophia akaanza kulia. “Charles hujui kiasi gani natesema karibu Mwaka wa kumi na tano huu baada ya kuanza kuishi maisha yako ya usiri.. Naumia sana Charles.. Naishi ili siku ziende na sasa hivi naishi tu kwasababu ya watoto wangu.. Lakini nateseka sana Charles.. Nini kimekutokea mime wangu.. Nini kimekubadilisha hivi??” Sophia akalia kwa kwikwi na kujiinamia kwenye meza.
Charles, akashindwa aseme nini akabakia kimya tu.
“Kuna mambo yako nje ya uwezo wangu!” Hatimaye Charles akaweza kutamka neno.
Sophia akaendelea kulia kwa takribani dakika kumi nzima bila kusema chochote.
“Sawa mume wangu, nitafanya hivyo.. Nitaondoka na Dorothy.! Rweyemamu nitamuacha kwa shangazi yake Mwembe Chai.!” Sophia akaongea baada ya kwa muda mrefu.
“Thank you Sophy!” Charles akashukuru huku moyoni akiwa karibu aanze kulia kama mkewe.
SIKU TATU BAADAE
Charles, Shirima na walinzi watatu pamoja na kijana mwingine walikuwa tena kwenye lile jumba Upanga, lakini leo walikuwa kwenye chumba kimoja wapo ambacho kimezibwa madirisha yote.
Charles na Shirima walikuwa wameketi kwenye viti. Mlinzi mmoja alikuwa amesimama mule mule ndani kwenye chumba huku walinzi wengine wawili wakiwa nje ya nyumba.
Yule mtu mwingine wa mne alikuwa naye ameketi kwenye kiti na mbele hake kulikuwa na meza yenye vifaa kadhaa vya elektroniki na mawasiliano.
“Point A, Point A.. Manisikia.!” Radio call moja pale mezani ikaita na kusikika sauti.
Yule jamaa akaichukua na kuanza kuongea nayo.
“Tunakusikia Point A” yule jamaa akaongea.
“Mwali anaondoka, narudia mwali anaondoka” sauti kwenye radio call ikaongea.
“Nimekusikia Point A, yukoje?” Yule jamaa akauliza.
“Yuko ‘light’, ana wapambe wanne, yeye katikati na washangiliani wawili kichwani na mkiani.” Ile sauti ikaongea tena.
“Nimekusikia Point A” yule jamaa akajibu na kuwema radioa call chini.
Walichokuwa wanakiongea ni kwamba, mtu wao waliyemuweka karibu na Ikulu waliyemuita Point A, alikuwa anawapa taarifa kuwa “mwali”, yaani msafara wa Rais ulikuwa unatoka Ikulu. Na yuko na ‘light’ yaani ulinzi mdogo, ikimaanisha kuwa Rais kuna sehemu anaelekea ndani ya jiji hili hili la Dar as salaam.. Kwahiyo yuko na ” wapambe” wanne, yaani magari manne ya wanausalama na “washangiliaji” wawili.. Yaani gari mbili za polisi, moja mbele ya msafara nyingine nyuma ya msafara.
Yule jamaa akaongea radio call nyingine.
“Point B, upo?” Akauliza kwenye radio call.
“Nipo!” Sauti ikaitikia kwenye Radio call.
“Standby, mwali yuko kwenye mwendo” yule jamaa akamaliza kuongea na kuweka chini.
Alikuwa anaongea na jamaa yao mwingine waliyemuweka kwenye bara bara inayoelekea surrender bridge.
Akachukua radio call nyingine pale mezani.
“Point C, unanisikia?” Akauliza.
“Nakusikia.!” Sauti ikaitikia kutoka kwenye radio call.
“Standby, mwali yuko kwenye mwendo.!”
Akampa taarifa mtu wao mwingine aliyeko surrender bridge ambapo walikuwa wamepaki ile hiace yenye milipuko pembeni ya barabara kama magari mengine yaliyowekwa pembeni na askari wa usalama wa barabarani kupisha msafara wa Rais.
Akaweka radio call juu ya meza na kumgeukia Charles.
“Chairman, ndani ya dakika kumi tunaenda kubadilisha historia ya Tanzania.!” Yule jamaa akaongea kwa shauku akimuangalia Charles na Shirima.
” Let’s do this.. Let’s show them who we are.!” Charles akaongea pia kwa shauku iliyochanganyika na hasira.
“Wamenipita hapa nilipo, wana dakika tano kabla ya kufika surrender bigde” Radio call iliongea, yule wanaye muita ‘Point B’ alitoa taarifa.
Yule jamaa aliyeko na kina Charles na Shirima ambaye alikuwa anashughulikia mawasiliano akinua radio call nyingine mezani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Point C, standby! Una dakika tatu kabla mwali hajafika”
“Sawa mkuu! Naomba ruhusa ya mwisho!” Point C akajibu.
Yule jamaa wa mawasiliano akageuka kumuangalia Charles. Charles hakusema chochote akamuonyesha tu ishara ya dole gumba, ‘OK’!
“Point C, umepata ruhusa ya mwisho, ni OK! Narudia ni OK!”
“OK” Point C akaitikia.
Safari hii hakuweka radio call chini akaendelea kuishilia mkononi ili waendelee kupatiwa maelezo kuhusu tukio linavyoendelea.
“Point C hapa” sauti ya ikaongea tena kwenye radio call.
“Ndio Point C tunakusikia”
“Naona mwali anakaribia kabisa kwenye harusi” akawaeleza kuhusu msafara kukaribia surrender bridge.
Jamaa wa mawasiliano na akina Charles hawakusema chochote. Wakasubiria maelezo zaidi.
“Wamekaribia kama mita 50”
Akina Charles wakaenelea kusikiliza.
“Mita kama 30”
Wakaenselea kusikiliza.
“Mita 10….ah nini sijui kinaendelea.. ah sijui nini!!” Point C akaanza kuhamaki.
“Point C, tupe taarifa nini kinatokea hapo?” Jamaa wa mawasiliano akauliza kwa kuhamaki.
“Sijajua nini kinatokea, lakini naona mwali amesimama mita kumi kutoka kwenye harusi.!” Point C akawaeleza.
“Wanafanya nini?” Jamaa wa mawasiliano akauliza akiwa amepaniki haswa.
Charles naye alikuwa amepaniki haswa, mpaka ikabidi asimame, na kujishika mdomo. Alikuwa amenza kuhisi kuna mambo hayako sawa, mpango una dalili ya kwenda Kombo.
“Mwali amesimama tu hakuna aliyeshuka… ah nahisi kama mwali anataka kurudi nyuma.. Naomba ruhusa, mwali bado hajaingia kwenye harusi, naomba ruhusa” Point C akawaeleza kinachoendelea huku akiomba apewe maelekezo afanye nini.
“Asiruhusu msafara urudi nyuma mwambie amalize.!!” Charles akaongea kwa hasira na kupaniki akimuelekeza yule jamaa wa mawasiliano ampe agizo Point C ya kulipua gari walilolitega.
“Point C, maliza kazi! Narudia Point C,Aliza kazi” Jamaa wa mawasiliano akamuelekeza Point C.
“Nimesikia mkuu, lakini nasisitiza mwali yuko mita 10 nje ya harusi” Point C akawapa angalizo.
“Point C maagizo yako ni kumakiza! Narudia maliza!” Jamaa wa mawasiliano akampa agizo kwa jazba.
Ghafla….
“BAAAAAAAAAANNNNNGGGGG”
Mlio mkali wa mlipuko ukasikika.
Charles na wenzake wakakaa kimya kwa takribani dakika nzima bila kusema chochote wala kutikisika.
“Point C” Jamaa wa mawasiliano akajaribu kuwasiliana na Point C.
“Point C, naomba taarifa ya harusi!” Jamaa wa mawasiliano akarudia tena.
Kila alipokuwa anajaribu kuwasiliana na Point C, hakupata jibu lolote ingawa radio Call ya Point C ulikuwa iko ‘hewani’.
Kitu pekee walichokuwa wanakisikia ni milio ya risasi na watu wakikimbia na kupiga kelele kwa taharuki.
Kelele za vilio na taharuki zilikuwa zinasikika kila kona.
“Point C, upo na sisi?” Jamaa wa mawasiliano akajaribu tena kuwasiliana na Point C bila majibu. Sauti pekee waliyokuwa wanaisikia ilikuwa ni vilio, taharuki na milio ya risasi.
Jamaa wa mawasiliano akageuka kuwaangalia Charles na Shirima.
“Point C, hayuko hewani.. Sijui nini kimetokea.!” Jamaa wa mawasiliano akaongea kwa sauti ya huzuni.
“Kuna mtu ametonya!” Charles akaongea huku anatembea kutoka upande mmoja wa chumba na kurudi upande mwingine.
“Unasemaje Chairman?” Shirima akauliza.
“Kuna mtu amewatonya kuhusu gari la milipuko tulilolitega surrender bridge haiwezekani wageuze msafara ghafla baada ya kufika kwenye mtego..” Charles akaongea huku bado anatembea tembea ndani ya chumba kutoka upande mmoja kwenda mwingine.
“Lakini hatuwezi kujua labda tumefanikiwa, nadhani wote tumesikia sauti ya mlipuko.!!” Shirima akajaribu kumtuliza Charles.
“Of course mlipuko umetokea lakini je, umeleta madhara tuliyolenga??”
“Chairman hilo inabidi tusubiri labda tumuagize Point B akimbie eneo la tukio kisha atupe mrejesho kama tumefanikiwa ama la?”
“Shirimaaa!! Kama tumefanikiwa kwanini hatumsikik Point C, na hiyo milio ya risasi inatoka wapi?” Charles akaongea kwa jazba huku bado anatembea tembea.
“Kuna mtu amewatonya..” Charles akaongea huku akaendelea kutembea tembea ndani ya chumba. “Na swali la kujiuliza, kama wanafahamu kuhusu Bomu tulilotega, je wanafahamu vingapi vingine??”
Sentesi hii iliwachoma wote moyoni wakabaki wanaangaliana kwa hofu na mshangao. Ni kweli kabisa, kama kuna mtu aliwatonya serikali kuhusu Bomu, je amewaambia vingapi vingine??
****************
January, 2017.
Bado nilikuwa nimeganda kama sanamu nikimkodolea macho Cheupe.
Cheupe alitembea mpaka pale niliposimama na kuchukua file kutoka mkononi mwangu.
“What is Ray?” Akaniuliza huku anaanza kupekua pekua zile file.
“Angalia hiyo file ya mwisho!” Nikamuelekeza huku naenda kukaa kwenye kitanda na kujiinamia mikono kichwani.
Nikamsikia Cheupe anafunha funua karatasi. Kisha kikafuata kimya cha kama dakika tatu hivi.
“My gorrrsssshhh!” Nikamsikia Cheupe amehamaki.
Nilishindwa hata nimuambie kitu gani au nimfariji au niseme nini!
“Ray.!” Cheupe akaniita, lakini nilishindwa hata kutamka neno moja.
“Ray.. Sijaelewa ina maana kwamba…. What.. Sijaelewa.. Oooh My gorsh!” Cheupe akashikwa na kigugumizi asijue aseme kitu gani.
“Hujaelewa nini mama?” Hatimaye nikajikuta nimepata nguvu ya kuongea. “Nimefungua huu mkoba wa kwamba nimekuta files ambazo nina amini zinaeleza kuhusu mpango yao.. Mipango yote kuanzia wa kwanza mpaka wa sasa hivi.. Sijaisoma bado.. Nikahamia hilo begi la pili ndio nimekuta hizo file za kwanza zina majina ya wanachama, kuna majina ya vibaraka wao, kuna file za akaunti zao na Mali zao.. Ndio kisha nikafika kwenye file hiyo ya nne… Daaaammnn najuta hata kwanini nimeangalia.!!”
Nikajiinamia tena chini nilishindwa kumalizia sentesi yangu.
“Kwahiyo ina maana kwamba.. No no no no! This can’t be!” Cheupe naye akahamaki na kuja kukaa pale kwenye kitanda na kujiinamia.
“Yes hny! This can’t be.. But ndio hizo file zinasema hivyo.. The Board imewahi kuwa na Chairman watatu.. Wa kwanza somebody Murphy, alafu akafuata Waziri Mkuu Chande.. Damn it, waziri mkuu?? Waziri mkuu Chance?? Fuuuucckk..” Nikajikuta napatwa na hasira na mshangao kwa pamoja.
“And then, file zinasema Charles B. Kajuna ndio mwenyekiti wa sasa.. Baba yangu mzazi?? How can this be?? How.. This is impossible!!” Nikajikuta naongea kwa jazba na kusimama.
“Ray, I thought you dad is dead??” Cheupe akaongea kwa huzuni na mshangao pamoja na woga.
“Yes! He is dead.. Yeye pamoja na mama yangu mzazi na Dada yangu Dorothy.. Wote wamekufa kwenye ajali ya MV. Bukoba.. How can my dead father be Chairman of The Board.!?” Nikang’aka kwa hasira na kupiga ngumi ukutani.
“Baby calm down! Let’s think about this.. Ukipaniki ndio hakuna tutakachofanya mume wangu.. Calm down let’s think please.!!” Cheupe akaongea kwa sauti yake ya huruma ambayo mara zote ina miujiza ya kushusha hasira zangu.
“OK.. OK.. OK hny.. OK let’s think.. Let’s think.!!” Nikaongea huku nahema juu juu nikiwa nakaa kwenye kitanda.
“Thank you hny.. Thank you” Cheupe akaongea huku ananipapasa mgongoni kunishusha mori ya hasira.
“Now let’s start from the beginning.. Mara yako ya mwisho lini kumuona baba yako” Cheupe akaniuliza huku anafungua fungua mafaili.
Nikajikuta natikisa kichqa na kutoa tabasamu la uchungu lililonifanya machozi yaanze kujaa machoni.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sijawahi kumuona!” Nikamjibu huku nafuta machozi ambayo tayari yalianza kutiririka mashavuni.
Cheupe alishindwa kusema chochote. Akageuka tu na kunitolea macho ya mshangao.
“Yes hasnat! I have never seen my father!” Nikaongea tena nikishindwa kabisa kuzia machozi yangu.
*******************
Usiku wa Jana sikujua hata ni muda gani nilipitiwa na usingizi. Ninachokumbuka ni kwamba nilikuwa nimeishiwa nguvu ya kufikiri au kusema chochote.. Cheupe alinikumbatia na tukajilaza kitandani nikilala juu ya kifua chake. Sikuweza kuwaza chochote kile na hatimaye sikujua ni muda gani usingizi ukanipitia.
Muda huu yapata saa tano mchana ndio nilikuwa naamka.
Cheupe alikuwa amevaa gauni jepesi yuko anatenga vizuri sahani za chakula mezani mule mule ndani ya chumba cha hoteli.
“Karibu tena duniani.!” Cheupe akanisalimia huku anatabasamu, “sijawahi kukuona umelala kiasi hiki mume!”
“Ooops! Hivi saa ngapi hii?” Nikamuuliza nikiwa najiinua kitandani huku nafikicha macho.
“Inakaribia saa sita kasoro hii..” Cheupe akanijibu.
“Ooops yani kichwa nakisikia kama bado kinauma.. Ile habari ya jana.……”
Kabla sijamaliza kuongea Cheupe akanikatiza.
“Aaaaannnhha.! No no, acha kwanza hizo habari.. Nenda bafuni oga uje kule kwanza.. Hujala tangu jana mchana.!” Cheupe akaongea huku anakuja kunishika mkono na kunivuta kwa mahaba niinuke.
Hakika Cheupe ni baraka kubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye maisha yangu, kila ambavyo nikijaribu kuwaza ni namna gani naweza kuishi bila uwepo wake, nashindwa kupata jibu.
Nikainuka moja kwa moja mpaka bafuni.
Nilipoingia kwa takribani dakika kumi nzima nilishindwa kuoga. Nilifungulia maji kwa takribani dakika kumi nzima lakini maji yalikuwa yanatiririka tu mwilini lakini sikuweza kupaka sabuni wala kufanya chochote.
Kichwani mwangu nilikuwa najitahidi nisiwaze kile ambacho nilikiona jana kwenye files za The Board. Lakini kadiri ambavyo nilikuwa najitahidi nisiwaze ndivyo ambavyo akili yangu nilikuwa ikifirikia kuhusu file hizo.
Nikaanza kukumbuka stori zote ambazo shangazi ekuwa akinipa kuhusu familia yangu, kuhusu wanafamilia yangu wote watatu walivyofariki kwenye ajali ya MV Bukoba.
Nikakumbuka maelezo yote ambayo shangazi alinipa kwamba miili ya wanafamilia yangu yote haikupatikana.
Ndipo hapa nikaanza kujiuliza kama ni kweli baba yangu yuko hai, je vipi kuhusu mama yangu? Vipi kuhusu dada yangu? Je, nao kuna uwezekano wako hai?
Mawazo kadha wa kadha yakapita kichwani mwangu! Je, Shangazi alikuwa anafahamu hii siri? Au naye amewekwa gizani kama mimi miaka yote hii?
“Raaayyyy.!!” Cheupe akiniita huku anachungulia mlangoni.
“Yes honey.!” Nikamuitikia huku nachukua sabuni haraka haraka na kujifanya naoga.
“Mbona unaoga masaa yote hayo? Are you OK?” Cheupe akauliza.
“Oohh! Si unajua jinsi mwili ulivyochoka, naacha maji yatiririke mwilini kuondoa uchovu.!” Nikamjibu hiku najisugua na sabuni.
“Au unadeka unataka nije kukuogesha hahahah!” Cheupe akongea kwa uchokozi.
“Hahaha! Ukiingia humu haitakuwa kuoga tena.. Yatakuwa mengine walahi!”
“Oga haraka baba.. Nakusubiri tule”
Cheupe akafunga tena mlango wa bafuni na kuondoka.
Nikajitahidi kutuliza akili na kuoga haraka haraka na ndani ya kama dakika tano nikamaliza na kutoka bafuni.
Nilivyotoka tu bafuni macho yangu moja kwa moja yakaganda kwenye mabegi yenye files ambayo Cheupe alikuwa ameyaweka kitandani ili kuacha nafasi mezani tuweze kula.
Nikajikita nimesimama kwa muda mrefu nayaangalia huku najifuta na taulo.
“Chakila kinapoa baba!” Cheupe akanishika mkono na kunivuta mezani.
Ilinibidi nijilazimishe kula ili kumfurahisha Cheupe lakini ukweli ni kwamba chakula kilikuwa hakipigi kooni.
Akili yangu yote ma mawazo yangu yalikuwa yanawaza zile files kitandani.
“So, what are thinking?” Cheupe akaongea huku yuko bize na sahani anaweka chakula.
“Naam!” Nikaitikia kwa kuuliza.
“Kuhusu files tunafanyaje?” Akaniuliza safari hii akiniangalia usoni.
Nikazuta pumzi ndefu na kushusha.
“Ndio nilichokuwa naumiza kichwa usiku mzima.. Nini cha kufanya!” Nikamjibu huku naanza kula.
“And umeamua nini?”
“Leo nataka nipeleke hizo files kama tulivyopanga… Lakini nitapeleka huo mkoba mmoja tu.. Huo mwingine utabaki!”
“Kwanini unaubakisha..?” Cheupe akaniuliza kwa mshangao.
“Nahitaji kujua ukweli kuhusu Charles B. Kajuna.. Huo ndio mkoba utakao baki, ila huo mkoba mwingine wenye nyaraka za mikakati sitaki hata kujua details za hizo Nyaraka.. Nitawapelekea Leo..!”
“I understand honey.. Pole!” Cheupe akanipooza huku ananifariji kwa kunipapasa mgongoni.
Tukaendelea kula na stori za hapa na pale. Tukajitahidi kwa kila namna kuepuka kuongelea The Board au files pale juu ya kitanda.
Tukaongea, tukalala kidogo, tukaamka tena.. Tupiga tena stori.. Hatimaye ikafika mida ya saa kumi na mbili jioni. Nikaanza kujiandaa ili kuondoka kuelekea eneo la tukio kupeleka files.
“So unadhani watu wa usalama wataelewa?” Cheupe akauliza.
“Kuelewa nini mama?” Nikamuuliza.
“Ile ‘code’ uliyowaachia pale.. papers968@gmail.com.!” Cheuepe akanikumbusha.
“Ooohh!! I hope wataelewa.. Maisha yao yote yamejaa mafumbo.. So they better understand it” nikamjibu huku nanyanyua ule mkoba mmoja ambao una nyaraka za Mikakati ya The Bold.
“All the best honey.. Nakusubiri hapa usikawie kuridi baba..”
Nikamkumbatia na kumuaga Cheupe kisha nikashuka chini ya ghorofa la hoteli na moja kwa moja nikavuka bara bara mpaka kituo cha magari cha Maili moja.
Hapo kituoni nikapanda hiace ya kutoka Tumbi ambayo inaelekea Ubungu.
Nikiwa ndani ya Taxi nikachukua Simu na Kubofya namba ya simu.
“Niaje Dickson.!” Nikasalimia mara baada ta simu kupokelewa.
“Poa poa! Niaje brother kimya sana.!” Dickson akaongea upande wa pili wa simu.
“Mihangaiko tu kaka! Niko njiani nakuja town.. Tunaweza onana?”
“Niko katikati ya mji, but muda si mrefu narudi home.!!”
“OK! Basi nitakuja straight Nyumbani kwako.. Kama baada ya lisaa limoja nitakuwa nimewasili.!”
“Poa poa kichwa utanikuta!”
“Poa kaka”
Nikakata simu.
Nilikuwa naongea na simu na rafiki yangu wa muda mrefu Dickson, ambaye tumefahamiaka toka kipindi niko sekondari A-level Tambaza High School.
Dickson alikuwa anafanya kazi Bandari na Mwenyezi Mungu alikuwa amemjalia kipato kizuri cha kuweza ‘kutamba’ mjini.
Makazi yake ya kuishi, yaani Nyumbani kwako alikuwa anaishi kwenye Jengo la Canal Residency maeneo ya Upanga West ambako alikuwa na apartment.
Kama dakika arobaini baadae nilikuwa tayari nimefika Ubungo, na mara baada ya kushuka tu kwenye hiace nikachukua Taxi kuelekea Upanga.
Takribani kama saa moja na nusu jioni nilikuwa nimewasili kwenye apartment za Canal Residency, Upanga West.
Apartment ya Dickson ilikuwa ghorofa ya tisa, kwa hiyo nikapanda lifti mpaka huko juu. Baada ya hapo moja kwa moja nikaelekea mpaka apartment namba 0096 na kugonga mlango.
“Aaaaaaahh kichwaaaaaaaaaa.!” Dickson akanikaribisha kwa uchangamfu kama kawaida yake.
“Niaje ‘mtoto wa mjuni’?” Nikamtania jina tunalomuita tangu tukiwa sekondari Tambaza. ‘Mtoto mujuni’! Mujuni alikuwa ni mwalimu wetu wa fizikia ambaye alikuwa na urafiki naye mkubwa.
“Hahahaha! Karibu sana kichwa.. Pita ndani.!” Dickson akanikaribisha ndani bado akiwa na uchangamfu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kuketi na salamu za hapa na pale, hatimaye nikataka nianze maongezi naye yaliyo nileta hapo na kabla ya kuanza maongezi Dickson akataka anikarimu kwa kinywaji ili tuongee huku tunashusha kilaji.
“Nikuletee nini Kichwa? Bapa, heinkein au bado unakunywa fanta passion , hahahaha” Dickson akaongea kwa utani huku anaelekea kuchukua vinywaji.
“Hahahaha! Dah, nipe juice Bob kama ipo kama hakuna nipe maji tu au yeah nipe fanta passion!” Nikamjibu pia kwa utani.
Baada ya kama dakika Dickson akarejea na na vinywaji, mimi akinipa juice na yeye akiwa na glass yenye kinywaji ambacho sikukijua mara moja lakini chenye muonekano kama maji ya kunywa.
“Dickson.!” Nikaanza maongezi baada ya Dickson kuketi na kuanza kunywa vinywaji vyetu.
“Ndio Ray!” Dickson akaniitikia.
“Kwanza nisamehe kwa kukushitukiza namna hii.. Najua hatujaonana miezi mingi sana.!” Nikaendelea.
“Usijali Kichwa.. Wewe ni ndugu yangu!”
“OK! Nimekuja nina suala moja muhimu sana nataka unisaidie.. Kuna mtu muhimu nataka nionane naye na nimemuelekeza aje hapa ili tuonane.!”
“OK.. Mtu wa namna gani kichwa nifafanulie!”
“Ni mtu wa serikali.. Nilikuwa nahitaji nikae nae sehemu Salama kuna mzigo nataka kumkabidhi.!” Nikaongea huku nikiangalia ule mkoba mweusi niliouweka juu ya meza. Dickson naye akageuka kuungalia.
“Dah! Kichwa bhana mambo yako.. Ndio maana washkaji wanasemaga wewe mtu wa system aisee!! Ni kweli nini wewe Usalama wa Taifa?” Dickson akaniuliza kwa shauku ya kama mtoto wa sekondari kuhusu hayo masuala ya Usalama wa Taifa.
“Hahahaha! Hapana Dick, mimi sio Usalama.. Labda tu niseme hao Usalama ni watu ambao nina ukaribu nao kwa ajili ya maslahi mapana zaidi kwao na kwangu.!”
“OK! So ulikuwa unataka nisaidie nini?”
“Kwanza nilikuwa nataka uniruhusu nikutane na mgeni wangu hapa kwenye apartment yako.. Na pili nilikuwa naomba faragha na mgeni wangu.. Unipe dakika kadhaa niongee naye.. Unaweza ukabaki ukawepo hapo ila tahadhari ni kwamba unaweza ukasikia mambo ya siri ambayo labda hata wewe mwenyewe usingelipenda kuyasikia.. Na pia nisingependa huyo mgeni ajue kuwa umeyasikia coz anaweza kuanza kukufuata fuata.!”
“Kichwa, wewe ni ndugu yangu! You do your thing mimi nitawapa privacy mnayohitaji sidhani kama kuna umuhimu wa mimi kusikia au kujua chochote.. Aah unategemea aje saa ngapi hapa?”
“Sasa hivi naona hapo na saa mbili kasoro kumi.. Kama atafuata jinsi nilivyomuelekeza nategemea awepo hapa saa mbili kamili.!”
“OK! Basi wacha mimi nikuache hapa ukiwa unamsubiri mimi naenda hapo mtaa wa pili MUHAS kuna mtoto mzuri nikamsalimie hahahaha!”
“Hahahaha hujaacha tu mabalaa yako.. Thank you man.. I appriate it.!”
“Usijali Kichwa.. Ila next time usinisuprise namna hii na mishe zako za kininja maana umenitisha karibia nijikojolee hahahaha.!”
“Jitahidi kuubana huo mkojo ukamkojolee mtoto mzuri wa MUHAS hahahaha”
Tukacheka, tukafurahi kisha Dickson akaondoka na kuniacha peke yangu pale kwenye apartment yake.
Nilibaki nimekaaa chini pale kwenye sofa kama roboti nikikodolea macho saa kwenye simu.
Ilikuwa tayari imetimia saa mbili kamili lakini bado hakuuwa na dalili ya mgeni yeyote.
Nikaanza kujiuliza labda ile ‘code’ niliyoiacha jana ofisini Makumbusho ilikuwa ngumu wameshindwa kuing’amua. Au labda nilikuwa nimekosea kuiandika. Au labda wameghairi kuja wanadhani nimewamisslead kama nilivyowamisslead kuhusu CRBB Lumumba.
Nikainuka kutoka kwenye Sofa na kuanza kutembea tembea pale sebuleni.
Ghafla nikasikia mlango unagongwa. Nikafupa jicho kwenye simu ilikuwa ni saa mbili na dakika tano.
Nikaenda kufungua mlango.
Nilipofungua tu, nikakutana uso kwa uso na baba bite. Kama kawaida akatabasamu.
“Kijana code haiandikwi namna ile.!” Baba bite akaongea huku anaingia ndani ya apartment kitemi bila ya salamu akiwa ameongozana na wanausalama wengine wawili.
“Uzuri ni kwamba umeelewa.!” Nikamjibu huku nafunga mlango.
“Of course nimeelewa.. papers968@gmail.com.. Hahahaha what a stupid code” akaongea huku anaketi kwenye sofa na wale wenzake wawili wakienselea kusimama.
“Stupid??” Nikajifanya kushangaa.
Baba bite akaweka koti lake la suti vizuri kisha akaanza tena kuongea.
“papers.. So nikaelewa unaongelea something kuhusu vitabu.. Hujui tu nikahangaika kwa masaa mangapi baada ya hapo.. The ndio nikaanza kuipa maana herufi moja moja.. P-present, A-at, PER-peers na S-store.. So ni ” present at peers store.. Hilo duka la vitabu hapo chini ya Jengo hili la Canal Residency.. Then nikaanza kuhangaika na namba ulizoandika.. 968, then baadae sana ndio nikaelewa kwamba 9-unamaanisha ghorofa ya Tisa.. Temhen ukiisoma 9 na 6 kwa pamoja unamaanisha apartment namba 0096 na hiyo 8 unamaanisha Eight O’clock.!! Code ya kipumbavu kabisa.. Ingekuwa mtu mwenye akili nyepesi ingenichukua mwaka mzima kuielewa..”
Baba bite akaongea kwa kukereka lakini pia kwa ufahari kuonyesha akili yake kwa kuelewa code niliyoandika.
“Well.! Najua wewe ni genius, so nilijua utaelewa.!” Nikamuinjoi.
“What the fuck are you doing Ray!” Baba bite akaongea kwa hasira. Sikuwahi kusikia anatukana kabla, hii ilimaanisha alikuwa amekasirika haswa.
“calm down.!” Nikajaribu kumpooza Baba Bite nikienda kukaa kwenye Sofa lililopo mkabala na pale alipokaa yeye.
“Usinambie ni calm down! Hivi unajua ujinga ulioifanya? Mabwana wakubwa huko wamechachamaa kwa jinsi ulivyotupotosha na kutupa taarifa za uongo..!” Baba bite akaendelea kuongea kwa jazba.
“I can explain it.!” Nikaendelea kujaribu kujitetea.
“Huna cha kunieleza.. Tena nilikuwa natakiwa kama nitakukuta hapa nikukamate ni kukupeleka mahali husika.. Kwanza umetupotosha na kama hiyo haitoshi umetengeneza maafisa feki wa Usalama kukusaidia kwenye upuuzi wako.. Unajua tukikushtaki utakaa jela miaka mingapi?” Aliendelea kufoka kwa jazba bila kunipa nafasi ya kuongea.
“Nilifanya hayo kwa nia njema tu!”
“Nia njema gani? Kuidanganya Idara ya Usalama wa Taifa?”
“Unajua kuwa sina maana hiyo!”
“Hivi Ray unafahamu kuwa uvumilivu wetu umeisha juu yako?? Maana sasa umegeuka kuwa liability badala ya asset.. Hebu nipe sababu kwanini nisikukamate sasa hivi na kwenda kukubinya mpaka utuambie tunachokitaka?”
“Well, mnaweza kufanya hivyo mnavyotaka lakini kama mtafanya hivyo nataka kuwahakikishia kuwa hamtakuja kuzipata files za The Board tena.. Kwanza mimi mwenyewe haijalishi mnibinye kiasi gani siwezi kuwaeleza ukweli.. Ni bora mniue tu.. Na Leo mpaka kufikia saa tano usiku nisipo rudi mahali Cheupe alipo, nimemuagiza azichome moto files zote.! Kwa hiyo hata usijaribu kufikiria kuniteka kama mlivyo Fanya siku ya kwanza.!”
Nikampa mkwara kwa kujiamini.
“Narudia tena, what the fuck are doing?” Baba Bite akauliza tena kwa hasira.
“Well yote yale nilitoyafanya kama vile kitengeneza wanausalama feki na mengineyonaweza msikubaliane nayo lakini niliyafanya kwa nia njema tu ili nifanikishe kuzipata file”
“Ulikuwa ma uwezo wa kutueleza zilipo na tungeweza kwenda kuzichukua, lakini badala yake umetupa taarifa za uongo na wote tumeonekana wajinga kwa mabwana wakubwa kwa kukuamini!” Akaendelea kuongea kwa sauti ya hasira.
“I’m sorry kama haukubaliani na mbinu zangu, lakini habari njema ni kwamba nimezipata files” nikaongea huku natabasamu.
Nikaona Baba Bite amepigwa na mshangao ghafla na uso wake ukajaa shauku.
“Ziko wapi hizo files?” Akauliza kwa shauku kubwa.
Nikatabasamu.
“Hizo hapo mbele yako” nikaongea nikitabasamu na kumuonyesha kwa kidole ule mkoba mweusi juu ya meza.
Baba Bite hakunijibu chochote, haraka haraka lakini kwa makini sana akaanza kuufungua ule mkoba.
Baada ya kuufungua akaanza kuzitoa zile file nne moja moja na kuzikagua kwa haraka.
Kisha akazirudisha file zote kwenye mkoba.
Kwa jinsi alivyokuwa na shauku nilimuona mpaka jasho linaanza kumtoka kwa mbali.
Akachukua ule mkoba na kumkabidhi moja ya wale wenzake wengine wawili aliokuja nao ingawa wao muda wote walikuwa kimya tu.
“Hizi ni file zote zimekamilika?” Akaniuliza huku anasimama.
“Hapana sio zote!” Nikamjibu bila kumuangalia na mimi nikiwa nasimama.
“Whaaaaat??!” Baba Bite akahamaki.
“Nimesema sio file zote!” Nikamjibu tena.
“Ray nahisi sasa unatufanyia maigizo.. File nyingine ziko wapi?”
“Look! Nimewaletea hizo file nusu ili niwaonyeshe dhamira yangu ya dhati kwamba nina nia ya kuwakabidhi file zote.. Hizo nusu zilizobaki kuna jambo nahitaji kulifanya kisha nawakabidhi..” Nikaongea kwa kujihami huku najiamini kabisa.
“Ray hivi unafamu kwamba hii ni ishu yenye maslahi ya kitaifa.. hili sio suala la mimi na wewe! Hii ni ishu inayotishia usalama wa Taifa. Unanielewa?” Baba bite akaanza tena kuongea kwa jazba.
“Naelewa hilo toka siku ya kwanza.. na ndio maana nimekwambia nimeleta nusu ya files ili kuonyesha dhamira yangu ya kutaka kukabidhi hizo files zote.. Kama nilivyosema hizo nusu zina taarifa ambazo nahitaji nizifanyie kazi!”
“Taarifa gani?”
“Ni suala binafsi sana.. Ni ishu inayonigusa maisha yangu binafsi moja kwa moja! Siwezi kuendelea mbele maisha pasipo kuweka hilo sawa.. Ni suala binafsi sana.. Naamini utanielewa, na I deserve this.. Miezi kadhaa yote hii nimepambana kufa na kupona.. Nimehatarisha maisha yangu nawisho wa siku file nimezipata na nimewakabidhi nusu kuonyesha kuwa sina nia ya kubaki nazo.. Nadhani nastahili kuaminiwa na nastahili kiachwa nishughulikie suala langu.. Siku nikikukabidhi files zilizobakia utaelewa.. Its something very personal.!”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikaongea kwa hisia kubwa japokjwa sikutoa machozi, lakini maneno yangu nahisi yalimgusa Baba bite na alionaantiki ya ninachoongea.
Hakusema chochote karibia dakika nzima, alikuwa ananitazama tu. Nahisi alikuwa ananisoma hisia zangu na pia alikuwa anajaribu kupambanua kile nilichomueleza.
“Unahitahi muda gani kabla ya kuwasilisha files zilizobaki?” Akaniuliza baada ya kimya kirefu akiwa amenikazia macho.
“Nahitaji angalau wiki…….”
“Nakupa siku tatu tu!”
Alinikatiza sentesi yangu kabla sijamaliza kuongea.
“Siku tatu?? No no no, siwezi kufanikisha kwa siku tatu!” Nikahamaki.
“OK eidha tuongozane sasa hivi ukanipe hizo files au nikuachie siku tatu.. Chaguo lako!”
Nikajiinamia kama sekunde thelathini hivi nikitafakari.
“OK! OK OK.. Thank you.. Baada ya siku tatu mnazipata file zenu!” Sikuwa na jinsi ilibidi tu nikubaliane nao.
Baada ya kuwajibu hilo, hawakujisumbua kuniaga wala nini, wakaondoka kutoka kwenye apartment wakiwa na ule mkoba mmoja mweusi wenye files.
Walipotoka nikaangalia saa kwenye simu. Ilikiwa inakaribia saa mbili na nusu.
Nikatoa simu na kumpigia Dickson.
“Hey! Ushamalizana na watu wako?” Dickson akaniuliza mara tu alipopokea simu.
“Yeah, nimeshamalizana nao na wameondoka.. Nadhani ungerudi sasa maana nataka niondoke” nikamjibu.
“Kichwa, mtoto mzuri hapa hataki niondoke.. So wewe nichie tu funguo hapo chini ya mlango!”
“OK poa! Basi nishtulie dereva Taxi unayemfahamu aje kunichukua hapa niondoke.!”
“Poa poa! Dakika sifuri tu!”
Nikakata simu na kuanza kusubiri Taxi ije.
Kama dakika kumi baadae Taxi ikafika. Moja kwa moja nikamwambie anipeleke Ubungo.
Ubungo tulifika kama majira ya saa tatu kamili usiku.
Siku ya leo ilikuwa kama Bahati, japo muda ulikuwa umeenda lakini nilifanikiwa kupata Hiace inayoelekea tumbi. Nikapanda na tukasubiri kama dakika kumi na tano ili hiace ijae na baada ya hapo tukaondoka.
Muda wote nilipokuwa ndani ya gari nilikuwa najitahidi kuumizwa kichwa ni namna gani nitaweza kutengia hiki kitendawili cha Charles B. Kajuna ndani ya siku tatu pekee.
Nikaanza kupanga kichwani kwamba nikifika Hotelini inanipasa nisilale leo. Itanibidi nitumie usiku mzima kusoma file zote zile za Chairmen wa The Board tangu kuanzishwa kwake na niweke mkazo zaidi kwenye file iliyoandikwa Charles B. Kajuna (Present).
Saa nne kamili tulikuwa tumefika Kibaha maili moja na nikashuka hapo.
Nikavuka bara bara mpaka upande wa pili na kwenda Hotelini Njuweni tulipofikia mimi na Cheupe.
Nilipofika nikapandisha juu ghorofani mpaka kwenye chumba chetu. Nikafungua tu mlango ambao haukuwa umefungwa na funguo.
Nikaanza kujisemea kimoyo moyo nikiwa naingia chimbani kwamba inabidi nikae na kumpa tena somo Cheupe tena kwa kumfokea kuhusu kufunga mlango na funguo. Nilimkataza kabisa asiache mlango wazi.
Nikaingia ndani Chumbani nikakuta juu ya kitanda Nguo zetu ambazo zilikuwa kwenye mabegi zimemwagwa juu ya kitanda kana kwamba mtu alikuwa anatafuta kitu kwenye mabegi.
Nikaangaza macho pale Chumbani lakini sikumuona Cheupe. Nikajua lazima atakuwa bafuni.
“Hasnat, hasnat hasnat.!” Nikagonga mlango wa bafuni bila majibu.
Nikafungua mlango na kuchungulia. Ndani ya bafu hakukuwa na mtu.
Nikaanza kusikia presha inanipanda.
Kutokana na uzito wa suala linalotukabili Cheupe hawezi kutoka hata kwenda mapokezi tu kwa kuogopa kutambuliwa sura zetu. Ma usiku huu wa saa nne ndio kabisa hawezi kwenda kokote.
Jasho likaanza kunitoka na kulowanisha tisheti niliyovaa.
Nikashuka chini mapokezi haraka haraka.
“Samahani dada.. Aah umemuona mkewangu ambaye niliingia naye hapa jana usiku?” Nikamuuliza dada wa mapokezi.
“Nyinyi mko chumba namba….”
“Namba 1023!”
“Hapana kaka, sijuona mkeo kutoka tangu muingie jana!” Akanijibu huku ananidadisi usoni, “kuna tatizo kaka?”
“Hapana! Kila kitu kiko sawa..!” Nikamjibu haraka haraka na kupanda ngazi haraka haraka kurejea tena Chumbani.
Nilipofika chumbani sikujua hata nifanye nini. Nikabaki nakodoa tu macho kwenye lundo la nguo zilizomwagwa pale juu ya kitanda.
Kisha nikaanza kuangaza macho kila kona mle chumbani ili walau nipate hata kuhisi ni wapi Cheupe ameelekea.
Nikiwa napepesa macho nikaona kama kuna karatasi juu ya meza.
Nikaisogelea haraka haraka nione ni karatasi ya namna gani na imeandikwa nini?
Nilipofika mezani na kuisoma ile karatasi nilihisi kama moyo wangu unapasuka vipande vipande. Kwa hofu kuu iliyotua ghafla ndani yangu.
Hofu yangu haikuwa kwa sababu tu ya Cheupe kupotea ghafla, au kuikuta hii karatasi hapa juu ya meza.
Hofu yangu ilitokana na kilichoandikwa kwenye hii karatasi.
THOU SHALT NOT TOUCH THY ANOINTED
Naunua huu ujumbe kama ambavyo naijua sura yangu. Na si hii sentensi pekee ninayoijua bali pia najua hii handwriting.. Najua huu mwandiko kama ninavyojua mwandiko wangu mimi mwenyewe.! Naunua huu mwandiko kama ninavyojua kiganja cha mkono wangu…
Huu ulikuwa ni mwandiko qa Isaack.!!
Kichwani mwangu nilikuwa naumiza akili kuelewa nini hasa kilikuwa kinaendelea.
Kwanza nilikuwa nimechanganyikiwa, ni namna gani Issack amejua mahali tulipo.? Na alikuwa na nia gani kuondoka na Hasnat?
Kuna vitu huwa vinatokea unatamani labda uwe unaota, unatamani muda wowote uamke na kukutana na uhalisia mwingine?? Issack??
Nikahisi kichwa kinauma kwa jinsi ambavyo ubongo ulikuwa unajitahidi kuchakata akili kupata jawabu lakink ulikuwa unaambulia patupu??
Isacck??
Nikaangalia tena kile kikaratasi mkononi mwangu,
“THOU SHALT NOT TOUCH MY ANOINTED “
Akili yangu ikakumbuka mbali sana, ikakumbuka kipindi tuko sekondari Kibaha, mimi na Isaack.. Wote tukisoma mchepuo wa Sayansi lakini pia wote wawili tukaongezea somo la Biblia (divinity/bible Knowledge).
Shuleni hatukuwa na mwalimu wa Divinity lakini shule ilikuwa inaruhusu mwanafunzi kufanyia mtihani somo hilo kama ungependa kwa hiari yako.
Kwahiyo tulikuwepo wanafunzi kadhaa ambao tuliamua kujaza kukubali kulifanyia mtihani somo hilo. Japokuwa somo la Divinity halikuwa na combination au umuhimu wowote wa kitaaluma, lakini karibia wote tuliokuwa tunalisoma ili tuweze ” kuongeza points” katika madaraja ya ufaulu. Yaani japokuwa somo hili halikuwa na ‘combination’ lakini lilikuwa linahesabiwa kwenye kupanga daraja la ufaulu.
Somo hili lilitusaidia sana matokeo yetu yalipotoka, kwani mfano mimi nilikuwa nasoma jumla masomo tisa ya kawaida na nikiongeza somo la Biblia jumla nilikuwa na masomo kumi niliyofanyia mtihani.
Katika masomo tisa ya kawaida, kwenye matokeo ya mwisho ya kidato cha nne, masomo sita nilipata alama A, na masomo matatu yaliyobakia nilipata alama B.
Somo la Biblia nilipata daraja A na hivyo kunifanya jumla niwe nimepata alama A kwenye masomo saba na hivyo matokeo yangu kusomeka kuwa nimepata daraja la kwanza nukta saba, au kama wenyewe tulivyokuwa tunaita, “one ya saba”!
Issack naye alipata daraja la kwanza nukta nane, au kama tulivyoita, ” one ya nane”! Na yeye pia akisaidiwa na somo la Biblia.
Sasa kipindi bado hata hatujafanya mitihani ya mwisho, kwa kuwa hatukuwa na mwalimu wa Biblia, hii ilitufanya tutenge siku kadhaa katika wiki tuwe ‘tunadiscuss’ Biblia na kuisoma.
Baada ya kuwa wote ‘tumeiva’ kwenye Biblia, kuna kipindi katika ‘group discussion’ na wanafunzi wenzetu tuliokuwa tunasoma somo la Biblia ulitokea ubishani mkubwa sana ambao mpaka leo hii wote tumekuwa watu wazima lakini bado tunakumbuka.
Ubishani huu ulihusu tafsiri sahihi ya maneno fulani yanayofanana kwa kiasi fulani ambayo yapo kwenye kitabu cha Zaburi na kitabu cha Wafalme I (Wafalme Wa Kwanza).
Maneno haya yalikuwa yameandikwa “usimguse mpakwa mafuta wangu”.
Baadhi yetu wakiongozwa na Issack walikuwa wanadai kwamba mstari huo unakataza watu ‘kuwa-critisize’ watumishi wa Mungu. Kwamba mtumishi wa Mungu akikngea hiyo ni ‘sauti ya Mungu’
Upande wa pili wakiongozwa na mimi tulikuwa na msimamo kwamba mstari huo katika zama zile za kale ulikuwa unakataza Wana wa Israel kuwadhuru/kuwaua Manabii wa Mungu. Kwahiyo tulikuwa na hoja kwamba mstari huo hauna ‘relevance’ katika zama hizi kwa sababu tuna sharia zinazokataza kuua mtu yeyote na si manabii pekee.
Ubishani wetu ulichukua wiki kadhaa kila tulipokutana kwa ajili ya ‘group discussion’ na mjadala ukawa mkubwa mpaka ikafika kipindi ilibidi tuanze kutafsiri mstari huo katika kwenye Biblia ya Kingereza ya King James Version toleo la zamani kabisa ambapo ndipo imeandikwa “Thou Shalt not touch thy anointed”..
Kuna wengine wakadai kuwa mstari huo unadhihirisha ‘lugha’ ambayo Mungu alikuwa anaitumia kuongea na watu wa ‘mataifa’ na lugha aliyokuwa anatumia kuongea na wana wa Israel, Kwahiyo wenye msimamo huo wakabadili ‘gia angani’ wakadai kuwa mstari huo unawakataza watu wasio wana wa Israel wasithubutu kuwadhuru au kujenga uadui na Israel.
Kiuhalisia ubishani wetu hakuwa na faida yoyote katika kutusaidia kwenye somo la Biblia lakini ubishani uliendelea kwa wiki nyingine kadhaa kutokana na kila upande kujifanya ‘wajuaji’ zaidi na kila mtu alikuwa hakubali kishindwa.
Ndipo hapo ambapo jumamosi moja tukafunga safari mpaka kijiji fulani hivi ambacho kipo karibu na Shule ya Kibaha.
Kijiji hiki kinaitwa Mwanalugali. Hapa kulikuwa na kanisa la EAGT (Evangelical Assemblies of God, Tanzania).
Kabisani hapo tukaomba kuonana mchungaji na baada ya kusubiri sana, hatimaye tukapelekwa ofisini kwa mchungaji. Hii ndio ikawa mwanzo wetu wa kutengeneza urafiki na Mchungaji Enock Shoo.
Shida yetu ya kuonana naye ilikuwa ni kumuomba yeye kama mwana theolojia atusaidie tafsiri ya mstari huo wa “usimguse mpakwa mafuta wangu”.
Mwanzoni alitushangaa sana, maana hili suala tulilokuwa tunalifanya ulikuwa ni ‘utoto’ wa hali ya juu. Lakini nahisi kwa kiasi fulani alifurahi kutuona tunabishana kuhusu tafsiri ya mstari wa Biblia badala ga ubishi wa 50 cent na Ja Rule nani mkali?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa hiyo akatupa muda wake na akaanza kutusikiliza kwanza sisi hoja zetu.
Niliona ni namna gani tulikuwa tunamkuna bara bara na hoja zetu.
Mwishoni hakuongea sana, akatupa jibu la ‘kisiasa’ tu kwamba ” kile Roho wa Mungu anachowashuhudia rohoni mwenu basi hicho ndicho sahihi.!”
Binafsi sikupendezwa na jibu hili la kiroho, kwa sababu sisi tulikuwa tunaisoma Biblia kama somo lingine, hatukuwa tunaishi maisha ya kiroho wala kuyatamani.
Mchungaji Shoo akaona jinsi ambavyo nilikuwa sijaridhishwa na jibu lake, na ili kutupooza akatualika kuwa kama tunapata muda kila Jumamosi twende ofisini kwake kwa ajili ya majadiliano ya Biblia.
Kwa kuwa hatukuwa na mwalimu wa Biblia shuleni, hivyo tukaona hii ni fursa kumtumia huyu mwana theolojia kuobgeza ufahamu wetu kuhusu Biblia.
Na huu ndio ukawa mwanzo wa sisi kwa muhula mzima wa mwisho tukiwa kidato cha nne, kila jumamosi tulikuwa lazima twende kijijini Mwanalugali kanisa la EAGT kuonana na Mchungaji Shoo.
Nikakiangalia tena kile kikaratasi mkononi mwangu. “Thou shalt not touch thy anointed”.
Ni nini Issack amekifanya?? Kitu gani anajaribu kuniambia??
Nikaangalia saa ukutani. Ilikuwa yapata saa nne na nusu usiku.
Nikaangalie tena kile kikaratasi. Nikajiuliza kwanini aniandikie huu mstari??
Ghafla taa ikawaka kichwani mwangu.
Hisia zangu zikanieleza kuwa Issack anajaribu kunielekeza eneo. Eidha shuleni Kibaha au Mwanalugali, EAGT.
Nikafungua mlango haraka haraka na kushuka mpaka chini mapokezi.
Nikamkuta tena yule dada. Safari hii alikuwa ananiangalia kwa macho ya udadisi sana mpaka nikaanza kupata wasiwasi.
” kaka kuna tatizo gani kwani?” Akaniuliza kwa udadisi mkubwa.
“Hapana kila kitu kiko sawa! Kwanini unauliza?”
“Hapana sikuelewi tu! Mara unamuulizia mkeo, Mara nakuona kama hauko sawa.. Kama kuna tatizo niambie!”
“Hakuna tatizo Dada, mkewangu atakuwa alitoka labda alipopita hapa ulikuwa umetoka… ah hivi tunadaiwa shilingi ngapi?”
“Laki moja.!”
“Hii hapa laki mbili.. Nalipia siku mbili tulizokaa na siku mbili zijazo.. Kuna sehemu naenda kidogo.. Kama sitorudi usiku huu chumba chetu msikuze kesho kwa mteja mwingine na mkifanya usafi chumbani kwetu tafadhali zile nguo kitandani msizivuruge, sawa?”
“Sawa kaka!” Akaniitikia huku bado ananiangalia kwa udadisi.
Sikutaka kuongea naye tena chochote kile. Nikatoka nje na kuelekea barabarani.
Hisia zangu zilikuwa zinaniambia kuwa, Issack alikuwa anataka nifike Kibaha Sekondari au kijiji cha Mwanalugali. Na hisia ziliambia kuwa ni Mwanalugali ambapo alikuwa anataka niende.
Sasa kutoka hapa Maili moja kwenda Mwanalugali kuna njia mbili. Unaweza kwenda mpaka mbele kidogo kwenye Yard ya Scania ya zamani na kufuata mchepuko wa bara bara kuelekea Hospitali ya Tumbi na baadae Kibaha Sekondari na baadae nafuata barabara ya kwenda Mwanalugali.
Uzuri wa kupita huku ni kwamba nifaua ndege wawili kwa jiwe moja. Yaani naweza kupita Kibaha Sekondari ambapo nilihisi nako kwamba Issack anataka niende ni nisipoona dalili ya Cheupe na Issack basi nanyoosha kwenda Mwanalugali.
Lakini hii ilikuwa na changamoto zake.
Changamoto yake ya kwanza ni kwamba huu usiku kwa mida hii siwezi kupata usafiri wa kwenda huko. Na nikitembea kwa miguu inaweza kunichukua lisaa lizima mpaka kufika. Na nikifika changamoto nyingine ni kwamba naenda wapi hapo shuleni? Mabwenini, madarasani, ofisini au barabaran?
Nikaona chaguo hili sio sahihi..
Chaguo la pili ilikuwa ni kwenda Mwanalugali moja kwa moja. Na uzuri wa Chaguo hili ni kwamba kulikuwa na sehemu mahususi nitakayoenda kuwaangalia nikifika. Kanisani EAGT. Na pia uzuri ni kwamba naweza kupita njia ya mkato kutoka hapa Maili moja mpaka Mwanalugali na haitanichukua zaidi ya nusu kufika.
Nikaamua nifanyie kazi hisia hii. Niende Mwanalugali.
Kwahiyo niafuata barabara iliyopo ng’ambo ya Kituo cha mabasi cha Maili moja ambapo zamani kulikuwa na mnada/soko.
Zamani barabara hii ilikuwa ya vumbi ila kwasasa imewekea lami nadhifu kabisa.
Kulikuwa na giza kweli kweli usiku wa leo, angani hakukuwa na nyota wala mwezi hivyo nilikuwa natembea huku roho inanidunda haswa kwa sababu inaweza kunikita hatari yoyote ile. Kama nikikutwa na Polisi natembea peke yangu usiku huu mitaa ya ufichoni kiasi hiki, hawawezi kushindwa kunitilia shaka na kunikamata. Na nikikutana na ‘wajanja wa usiku’ wafanisaula mpaka bukta.
Nikapita kwenye shamba la miti ambalo tangu nasoma Kibaha lilikuwepo, kama dakika kumi baadae nikatokea mtaa fulani hivi ambao sikuwahi kuujua jina tangu kipindi nasoma.. Mtaa huu walikuwa wanaishi watu wengi wenye kipato cha kati, kwahiyo karibu kila nyumba ilikuwa na mbwa.
Kila nilipopita kwenye kila nyumba nikasikia mbwa wanabweka na mara kadhaa wenye nyumba wakiwasha taa nahisi kuniangalia mimi nilivyokuwa napita.
Kama baada ya dakika ishirini nikatokea kwenye ‘nyumba za kota’ za wafanyakazi wa Shirika la Elimu Kibaha.
Hapo nikafuata kushoto kwenye barabara ya vumbi inayoelekea Mwanalugali.
Dakika kumi baadae nikawa nimeingia kwenye kijiji cha Mwanalugali.
Ilikuwa yapata miaka kumi au kumi na moja sijawahi kukanyaga hapa Mwanalugali tangu nimalize Shule Kibaha Sekondari. Kulikuwa na mabadiliko kiasi. Nyumba nzuri zilikuwa zimeongezeka na mambo mengine machache.
Nikanyoosha barabara mpaka kuelekea maeneo ya pembezoni mwa kijiji ambako ndiko kulikuwa na kanisa la EAGT.
Dakika tano baadae nilikuwa nimefika kwenye kanisa. Kanisa lilikuwa limebadilika mno.
Zamani kipindi mimi na Issack tunakuja hapa, kanisa lilikuwa dogo tu la kawaida kama kawaida ya makanisa ya Kilokole. Lakini kanisa hili lililokuwa mbele yangu lilikuwa kanisa kubwa na la kisasa. Pembeni yake kulikuwa na jengo dogo ambalo niliamini kuwa ilikuwa ni ofisi ya mchungaji.
Pia nje ya jengo hilo kulikuwa na magari mawili aina ya V8 yamepaki.
Japo kuwa tayari hii ilikuwa ni saa tano usiku lakini taa ndani ya jengo hili la ofisi zilikuwa zinawaka. Nikaelewa kuwa ‘niko mahali sahihi.’
Nikasogea mpaka mlangoni mwa hii ofisi na kugonga.
Kama baada ya sekunde thelathini mlango ukafunguliwa. Nikaingia ndani.
Ofisi ilikuwa kubwa sana. Kama vile vyumba viwili vya kuishi uviunganishe.
Ndani ya ofisi kulikuwa na takribani watu kumi na mmoja.
Kwanza kulikuwa na Mchungaji Shoo mwenyewe aliyekaa kwenye kiti cha ofisi mbele ya meza yake.
Mchungaji alikuwa amebadilika sana, lakini alibadilika kwa uzuri, alikuwa amenawiri kana kwamba alionekana sasa alikuwa na maisha bora zaidi.
Mchungaji Shoo alikuwa evalia suti yenye kola ya kichungaji shingoni.
Pembeni kulikuwa na kochi la watu wawili ambao walikuwa wameketi Issack na Cheupe.
Mbele yao kulikuwa na kochi la watu watatu ambalo waliketi watu wawili waliovaa suti.
Pia pembeni ya mchungaji kulikuwa na mtu mmoja ambaye alikuwa amening’iniza bunduki began.
Pia kulikuwa na wengine wawili wamesimama mlangoni nao mmoja alikuwa amening’niza bunduki.
“Kaa hapo!” Yule jamaa aliyenifungulia mlango akiniamuru nikae pale kwenye kochi la watu wawili walilokaa Cheupe na Issack.
Nikajipenyeza na kukaa pale pale.
Nikawaangalia wale wajamaa kwa haraka haraka. Hawa walikuwa ni watu wa usalama wa Taifa.
Nilikuwa nimeshakuwa na uzoefu wa namna ya kuwatambua haiba zao.
Nikaanza kuhisi kama nataka kuchanganyikiwa. Nimetoka kuonana na maafisa usalama masaa machache yaliyopita. Hawa walikuwa wanataka nini tena?
Nikageuka kumuangalia Issack, nikajiuliza amefikaje huku wakati alikuwa anatakiwa kubaki Morogoro?
Imekuwaje wako hapa na Cheupe? Kwa mazingira niliyowaona nao ilionyesha kuwa wamekuja hapa kinyume na hiari yao, kama vile wametekwa na maafisa usalama.!
Nikamuangalia Mchungaji Shoo, hakuwa na ‘expression’ yoyote ile usoni. Hakuwa ameshtuka, hakuwa anajiamini, hakuwa anaogopa, hakuwa anafurahi wala kununa.
Alikuwa anaangalia tu kinachoendelea kama vile anaangalia kwenye runinga hayupo hapa.
Nikaanza kujiuliza tena, nini kinaendelea hapa? Na kwanini kifanyike hapa kanisani kwa mchungaji shoo??
Sikuwa na jinsi, nikasubiri nisikie hicho nitakachoambiwa.
Itaendelea…
Note: Tumebakiza Episode moja tu ya mwisho ili tuweze kumaliza msimu wa kwanza wa simulizi hii ya “Vipepeo Weusi”! tafadhali usikose kuungana nami siku ya jumamosi jioni ambapo nitahitimisha simulizi hii kwa msimu huu wa kwanza.
Yule jamaa afisa usalama ambaye nilihisi kuwa ndiye alikuwa kiongozi wao, akatoa simu akaanza kubofya bofya kisha nikahisi kama kuna ujumbe wa maandishi alikuwa anausoma, kisha akarudisha simu kwenye mfuko wa suruali.
“Files ziko wapi?” Yule jamaa akaniuliza huku ananiangalia.
Nikachukua kama sekunde thelathini nzima kujaribu kuchekecha jibu la hili swali analoniuliza.
Ana maana gani file ziko wapi? Anamaanisha files kwenye mikoba yote myeusi au file za kwenye mkoba ule niliompelekea baba bite?
Nikamsikia Cheupe ananibinya mgongoni kunipa ishara. Nikamuelewa kuwa naulizwa kuhusu file zote.
“Nimewakabidhi watu wa Usalama wa Taifa!” Nikajibu pasipo kuzunguka zunguka
“Umewapa file kwenye mikoba yote?” Akaniuliza tena.
“Ndiyo!” Mikamjibu kwa kifupi.
“Umemkabidhi afisa gani?” Akaniuliza
“Nimempa Justin!” Nikamjibu nikimaanisha Baba Bite.
Yule jamaa akatoa tena simu na kuanza kubofya kisha akaweka sikioni.
“Hallo Mkuu… ndio…. ndio.. ah ametupa jibu kama la wenzake Mkuu.. ndio…..ndio.. Amemkabidhi Justin…. ndio…. Sawa Mkuu.!!
Katoa simu na kunipa niongee nayo. Nikaanza kusikia mapiga ya moyo yanaongezeka.
” hallo.!” Nikaongea kwa woga.
“Hujambo Rweyemamu?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Moyo ukanipasuka. Nikasikia sauti ya mtu anayeonekana kuwa ni Mzee sana. Kichwani nikahisi hii sauti nimewahi kuisikia, lakini sikujua haswa nimeisikia wapi.
“Sijambo! Shikamoo..”
Ikapita takribani dakika nzima upande wa pili wa simu sikusikia akiongea chochote kile.
“Hallo.!” Nikaongea kujua kama bado kuna mtu upande wa pili au simu imekatika.
“Unapajua Simba Hill?” Hatimaye akaongea tena.
“Dodoma?” Nikauliza.
“Yeah.! Napafahamu..”
“Kesho saa nane mchana nataka ufike pale?”
“Kufanya nini?”
“Ili mtoto Hasnat, Isaack na mtoto wako tumboni waendelee kuishi.. Kesho saa nane mchana nataka ifike pale peke yako… mrudishie simu aliuekupa.!”
Huko kikongwe akaongea kwa vitisho kisha akaniamuru nirudishe simu.
Nikarudisha simu huku mikono inatetemeka.
“Hallo Mkuu.. ndio…ndio…. ndio Mkuu.. Sawa… Sawa Mkuu.!” Yule jamaa akaongea na simu baada ya kumrudishia.
“Wewe na wewe.. Ondokeni.!” Akawanyooshea kidole Issack na Cheupe.
“No no.. Siwezi kuondoka bila Ray.!” Cheupe ‘akawadindia’.
Yule jamaa hakusema chochote akageuka na kuniangalia.
“Hasnat.. Pleas naomba muende its going to be fine!” Nikamuondoa wasi wasi Cheupe. Nikaongea huku nimemkazia macho nikimuhakikishia kuwa nahitaji yeye na Isaack waende.
Cheupe akanikumbatia kwa nguvu kisha akanibusu kwa hisia Kali kwenye paji la uso. Kisha wakainuka, yeye na Issack na kuondoka kutoka mle ndani.
Baada ya kama dakika tano hivi baada ya Issack na Cheupe kuondoka, yule jamaa akaanza kuongea.
“Tukupeleke wapi?” Akaniuliza.
“Dodoma mjini?” Nikamjibu kwa kifupi.
Baada ya hapo wote tukatoka mle ndani ofisini tukimuacha mchungaji Shoo peke yake.
Tukatoka ma kupanda kwenye magari. Gari nililopanda mimi tulikuwa watatu tu. Yaani mimi, yule jamaa aliyekuwa ananihoji muda wote na jamaa mwingine aliyevaa suti. Wale maafisa usalama wengine wote wakapanda ile gari nyingine.
Magari yakaondoka kuelekea Maili moja. Tilipofika maili moja, lile gari walilopanda wana usalama wengi, likapinda kuelekea Dar es salaam, na gari nililopanda mimi na wale maafisa wawili, likapinda kushoto kuelekea Morogoro.
Kwahiyo tukaanza safari ya kuitafuta Morogoro na hatimaye tuelekee Dodoma. Ilikuwa tahari karibia imefika saa saba usiku.
Kichwani nilikuwa nawaza mambo mengi sana. Kwanza nikang’amua hawa maafisa usalama walikuwa ni vibaraka wa The Board.
Pia nikatambua kuwa kwa namna moja au nyingine walifanikiwa kung’amua mimi na Cheupe hoteli ya Njuweni tuliyofikia.
Vivyo hivyo pia walifanikiwa kumteka Issack kutoka Morogoro na kuja naye mpaka Kibaha.
Lakini bado nilijiuliza maswali, kama hawajui kuwa mikoba mmoja sijaupeleka na wao hawajauona, je mkoba huo uko wapi?
Nikakumbuka namna ambavyo Cheupe alinibinya mgongoni nilipoulizwa swali hilo, nikahisi kwamba kitakuwa na ujanja fulani hivi ameufanya.
Swali lingine nililokuwa najiuliza ni kwanini waliamua twende kukutana pale kanisani kwa Mchungaji Shoo?
Je, mchungaji Shoo n Afisa Usalama? Au pia ni Kibaraka wa The Board?
Lakini pia nikawaza au walihitaji sehemu ya karibu ya kuonana pindi nitakapo rudi, na walipombana Issack akatoa pendekezo la kanisani kwachungaji shoo?
Mwili ulikuwa unaniuma kwa uchovu, na kichwa kilikuwa kinaniuma kwa kuwaza. Nikaona haya masuala niache kuumiza kichwani, nikabili kilichopo mbele yangu. Kukutana na huyo mzee kikongwe niliyeongea naye kwenye simu.
Kila nilipokumbuka sauti yake, nilikuwa napata hisia kwamba kama nimewahi kuisikia hiyo sauti, lakini sikukumbuka ni wapi neisikia.
Kwa mbali rohoni mwangu nilikuwa nahisi ni nani nilikuwa naenda kuonana naye. Na kila nilipofikiria hilo roho yangu iliwaka moto, moyo ulipasuka. Nikatamani kulia lakini hakuna machozi yaliyotoka.
Majira ya kama saa kumi na mbili asubuhi tuliwasili Dodoma. Nikawaambia wanipeleke mtaa wa Airport, pale kwenye logde ninayoipenda, Samali Lodge.
Wakaniacha hapo, kisha wakaondoka.
Nilipoingia Chumbani nikajitupa kindani bila hata kuvua viatu.
Sikutaka kuwaza chochote, wala kufikiria chochote. Nilitamani kulala tu japo kwa muda mchache nipumzishe akili na mwili uliokuwa unauma kwa uchovu.
Nikafumba macho taratibu, usingizi ukanipitia.
***************
Nilikuja kushtuka muda wa mchana jua limeshakuwa kali tayari. Nikaangalia saa na ilionyesha saa saba na dakika tano.
“Damn it.!” Nikaongea huku navua nguo haraka haraka walau niweze kuoga. Nilikuwa tayari nyuma ta muda. Saa nane kamili natakiwa kuwa Simba hill.
Nikaoga haraka haraka na baada ya kama dakika kumi hivi tayari nilikuwa mapokezi nawaomba waniitie taxi.
Dakika kumi baadae taxi ikawasili. Nikapanda na kumuelekeza kuwa anipeleke mtaa wa ‘Area D’ na mikamueleza kuwa aendeshe haraka kwani niko nyuma ya miadi yangu inayonipeleka huko.
Dakika kumi tu baadae tulikuwa tumefika mtaa wa Area D. Nikamlipa hela yake na kushuka kuanza kutembea kwa mguu kuelekea Simba Hill.
Ukiwa unaingia mji wa Dodoma mfano kitokea Morogoro.. Mwanzoni kabisa ukiwa ndio unawasili Dodoma mjini, mkono wako wa kushoto kwa mbali hivi utaona kijimlima chenye mawe makubwa sana juu yake. Hapo ndio Simba Hill nilipoelekezwa niende.
Nikatembea kwaguu takribani kwa dakika kumi na tano mpaka nikafika chini ya kilima.
Nikasimama kidogo, ili nipumzike na kujishauri kama nipande juu ya mlima au nisubiri hapo chini.
Nikiwa najishauri, kwa mbali nikaanza kuonana kuna gari linakuja kwa kasi muelekea huu niliosimama.
Mandhari ya mlima huu yalikuwa katika mtindo ambao, kwanza mlimia ulijitenga mbali sana na makazi ya watu, pia upande wa uwanda wa mbele wa mlima ulikuwa mkame sana, kwa kiasi Fulani kama jangwa hivi, ingawa upande wa pili, yaani upande wa nyuma una uwanda mpana sana unaoelekea kwenda mbali sana na upeo wa macho na kulikuwa na vijimisitu fulani hivi.
Gari hii aina ya ‘Rav 4’ ya kijivu ikaja kusimama mpaka pale nilipo. Hakuna mtu ambaye alishuka kwenye gari, nikaona kioo tu kinashushwa na mmoja wa watu walioko ndani ya gari akanipa simu fulani hivi ya ajabu.
Baada ya kuipokea tu ile simu, gari ikageuzwa na kuondoka kwa mwendo kasi kurudi ilikotokea.
Nikaanza kuiangalia ile simu na kuigeuza geuza. Ilikuwa inafanana kwa kiasi fulani na ‘radio call’ lakini yenyewe ilikuwa kubwa zaidi.
Na pia ilikuwa na kioo kikubwa pia.
Baada ya kuigeuza geuza na kuichunguza nikagundua kuwa ilikuwa ni ‘Satellite Phone’. Aina ya simu ambayo inafanya mawasiliano kwa kutumia mawimbi ya Satellite pasipo kutegemea hii mitandao ya kutoa huduma za mawasiliano. Simu hizi huwa zinauwezo wa kuwasiliana zenyewe kwa zenyewe. Hazipokei wala kupiga simu kwenda simu ya kawaida.
Nikabakaendelea kuingalia tu jinsi ilivyo. Hii ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuishika ‘Satellite Phone’.
Ghafla nikaanza kuona kitaa cha kijani kilichopo pembeni ya simu kinawaka kwa mtindo wa ku-blink. Inawaka ma kuzima. Pale juu kwenye Screen nako kulitokea maandishi “SSC-3?.
Nikahisi kwamba kuna mtu anajaribu kunipigia.
Kulikuwa na vitufe kama saba hivi kwenye simu, nikabofya kitufe ambacho kilikuwa na rangi ya kijani. Miaweka simu sikioni.
” hallo” nikaongea.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Zunguka nyuma ya mlima, kisha tembea kilometa mbili kwenda ndani ya msitu mpaka ukute cabin nje kuna gari imepaki.!”
Nikaisikia sauti ya yule mzee kikongwe niliyeongea naye jana ikiniongelesha kunipa maelekezo kisha simu ikakatwa.
“Hallo.. Hallo..halloo.!” Nikaongea bila kuisikia jibu. Simu ilikuwa imekatwa tayari.
Sikutaka kupoteza muda.
Nikazunguka nyuma ya mlima na kuanza kutembea kuelekea ndani ya msitu.
Niaktembea kwa takribani dakika ishirini nzima mpaka nikakutana hicho kijumba nilichoelekezwa.
Nje kulikuwa kumepaki gari fulani hivi ya muundo wa ‘pickup’ nyeusi. Lakini nilipoiangalia kwa makini ilikuwa ni gari ya kisasa aina ya Ford, F-150.
Kijumba chenyewe kilikuwa ni kidogo kama cha vyumba viwili tu na kilikuwa kimejengwa kwa mbao tupu kuanzia juu mpaka chini. Vijumba vya namna hii nimezoea kuviona kwenye runinga kwenye nchi za magharibi na wenyewe wazungu huviita “cabin”.
Nikasogea mpaka mlangoni na kuanza kugonga.
” hodi.. hodiiii.. hodi.!”
“Ingia.!”
Nikasikia sauti inayofanana kabisa na ile niliyoisikia kwenye simu ikiniruhusi niingie.
Nikaufungua mlango taratibu sana kwa tahadhari kubwa. Nikaufungua mpaka mwisho na kuingia ndani.
Kijumba hiki licha ya kujengwa kwa mbao juu mpaka chini, lakini pia mpaka sakafu yake ilikuwa ya mbao.
Ndani hakukuwa na kitu chochote zaidi ya viti viwili vya mbao.
Kilichonishtua zaidi haikuwa mandhari ya hii nyumba, wala sakafu yake.
Kilichonishitua kilikuwa ni mtu aliyeketi kwenye kiti. Ilikuwa ni kama kwamba najiangalia mimi mwenyewe. Kana kwamba mbele yangu nilikuwa namtazama Rweyemamu akiwa amezeeka.
Sikutaka kuamini kile nilichokuwa nakiona japokuwa nilikihisi tangu nakuja.
Sikutaka kuamini kile ubongo wangu ulichokuwa unafikiri.
“Ujambo Rweyemamu?” Yule mzee akanisalimia.
“Baba???” Nikauliza kwa mshangao mkubwa.
“Keti kwenye kiti mwanangu.!” Akaongea huku akinionyesha kiti cha mbao kilichokuwa karibu na pale mlangoni niliposimama.
Nikahisi kama mwili wote umekufa ganzi.
Nikaketi kwenye kiti. Kati kati yetu ilibakia nafasi ya kama hatua kumi hivi.
Alikuwa amevalia suti nadhifu nyeusi, na kwenye ukosi wa koti la suti alikuwa ameweka ile pini ya The Board, pini ya dhambarau yenye picha ya kichwa cha simba cha dhahabu.
Mkononi alikuwa ameshikilia bastola na sakafuni kulikuwa na bahasha ya kaki.
“Hujambo Rweyemamu?” Akarudia tena kunisalimia.
“Wewe ndio Chairman?” Nikamuuliza bado nikiwa kwenye mshangao mkubwa.
“I used to be, lakini kwakuwa umeshaharibu kila kitu sidhani kama ni sahihi ukiniuta Chairman” akaongea na kutabasamu kwa hasira.
“Nimeishi maisha yangu yote nikiamini kuwa umekufa!” Nikaongea kwa hasira.
“Kuna mambo huwezi kuyaelewa Rweyemamu, nilifanya hivyo kwa usalama wangu ma usalama wa Umoja ninao uongoza.!” Akanijibu kwa upole.
“Kwahiyo mama na dada nao wako hai au wamefariki?”
“Wako wazima wa afya kabisa, wanaishi Uganda Central region, wilaya ya Kyankanzi… lakini nao kama wewe wanajua nimefariki siku nyingi tu.!”
Sijawahi kujisikia uchungu kiasi ambacho nilikuwa najisikia muda huu. Nilitamani niinuke na kumrarua vipande vipande huyu kikongwe aliyekuwa mbele yangu.
Nikasikia machozi yanaanza kunitoka.
“You are a monster! Unawezaje kuwafanyia hivi familia yako?”
“Kuna sacrifices ni lazima zifamyike kwa maslahi mapana ya nchi.. Hicho ndicho nilichokifanya!”
“Maslahi mapana ya nchi au uroho wenue wa Mali?” Nikafoka.
“Huwezi kuelewa sasa Rweyemamu, lakini The Board ndio inayofanya hii nchi iendelee kusonga mbele.. Ipo siku utaelewa hilo.!”
“Ndio uitese familia yako maisha yao yote?? Hivi unajua ni kiasi gani nimeteseka kwa kuishi maisha yangu yote bila kuwahi hata kumgusa mama yangu mzazi au dada au baba??”
“Its a sacrifice! Ni kama wewe tu unavyofanya.. Mimi na wewe hatuna tofauti Rweyemamu!”
“Whaaaaaatt??” Machozi yalikuwa yananitoka na nimepandwa na hasira mpaka natetemeka.
“Think about it.. Umeacha chuo nankuanzisha taasisi ili kusaidia vijana wenzako kujiajiri.. That is a sacrifice.. Tena sacrifice kubwa.. Ni kama sacrifice niliyoifanya kuiacha familia yangu kwa ajili ya nchi yangu.!”
Haya majibu Yale yalizidi kunipandisha hasira zaidi. Machozi yalitiririka na nilikuwa natetemeka kwa hasira.
“What do you want from me?” Nikamuuliza kwa hasira. Nilihisi haya maongezi kadiri yanavyoendelea yanaelekea kubaya. Na sikutaka kabisa kuendelea kumuona au kuongea naye.
“Rweyemamu, wewe ndiye uliyeharibu kila kitu na wewe ndiye unatakiwa ku-fix hili sula.. Hii nchi haiwezi kwenda mbele bila uwepo wa The Board… so you need to fix this”
“What do you want?” Nikamuuliza tena, nilikuwa nataka aende moja kwa moja kwenye hoja yake sio kuzunguka mbuyu.
“Unaona hiyo bahasha?”
Nikaangalia ile bahasha pale chini sakafuni. Sikumjibu chochote. Nikageuka tena na kumwangalia.
Akaendelea kuongea.
“Tuliwahi kufikiria scenario kama hii.. Ikitokea The Board imekuwa compromised na tukajulikana wanachama wote na mikakati yetu.. Nini kifanyike?? Sasa kwakuwa timeshakuwa compromised na naamini ndani ya masaa 24 yajayo serikali itaanza kuwakamata wanachama wote wa The Board.! Kwa maneno mengine huu ndio mwisho wa The Board..!! Sasa kuna ‘safe deposit box’ iko kwenye benki moja nchini Switzerland kwenye mji wa Zurich.. Kwenye hiyo deposit box kuna maelekezo ya nini cha kufanya in case ikitokea situation kama hii tuliyo nayo sasa.. Kwahiyo kwa kuwa wewe ndio umesababisha hii, I want you to fix this..!”
Mzee akaongea kwa kujiamini.
“You are crazy old man.. Nimepambana kufa na kupona ili kuibomoa The Board, now you want me help you get back?? You are crazy.. This is crazy!” Nikafoka na kusimama kwa hasira.
“Rweyemamu narudia tena na tena, nchi hii haiwezi kwenda mbele bila ya The Board.. Ipo siku utanielewa.. Ninachotaka ufanye, chujua hii bahasha.. Ndani yake ina maelekezo ya jina la hiyo bank, mtaa ilipo, namba ya deposit box pamoja na maelekeza ni namna gani utapata access ya kuifungia na kuchukua kilichomo ndani.. Kwahiyo kama nilivyo kwambia naamini ndani ya masaa 24 wanachama wote wa The Board watakamatwa na serikali… sasa nakutaka wewe, siku yoyote ambayo utakuwa tayari, kama ni kesho au mwezi ujao, au mwakani.. Siku yoyote ile.. Nataka uende Zurich.! I want you to fix this.!”
Mzee akajitahidi tena kunishawishi.
“That will never happen!” Nikamjibu kwa kifupi na kwa hasira kubwa.
Mzee akabaki amenikazia macho tu. Sikujua ni nini alichokuwa anafikiria, lakini kwa takribani dakika mbili nzima tulikuwa tunatazamani pasipo yeyote kati yetu kusema chochote.
Baada ya kama dakika mbili akaacha kunitazama machoni na kuanza kuongea bila kunitazama usoni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Najivunia kwamba nimefanya ninachokiamini kwa maisha yangu hapa duniani! I have fought a good fight! I have kept the faith.. Nimepigana vita njema maisha yangu yote hapa duniani, naamini nimetimiza kusudi la mimi kuletwa ulimwenguni.. I have finished the race.. Nadhani napaswa kupumzika sasa.!”
Nkkamuona anainua mkono wa kushoto alioshikilia bastola.
Akainua bastola mpaka usoni kwake.
Akaingiza bastola mdomoni.
“BAAAAAAAAANNNNNNGGGGG”
Niliruka kama nimepigwa na shoti ya umeme. Nilitetemeka kwa woga ambao sijawahi kuusikia tangu nizaliwe.
Damu ilikuwa imetapakaa ukuta wote upande ule ambaozee alikuwa amekaa. Ubongo ulikuwa umejibandika ukutani kama matope.
Ndani ya sekunde chache pale chini sakafuni kulikuwa kumejitengeneza dimbwi la damu.
Mwili wazee ulikuwa umelala pale chini bila uhai.
Nilibaki nahema kwa nguvu kwa woga ulionipata ghafla.
Bila kufikiria sana, nikamsachi mzee mifukonk na kuchukua funguo ya gari.
Sijui ni shetani gani au malaika gani alikuwa amenipanda kichwani mwangu, nikajikuta nimeichukua na ile bahasha mzee aliyoisema kuhusu Zurich, Switzerland.!
Nikatoka nje huku nakimbia, nikapanda kwenye gari na kuiondoa kwa kasi ya ajabu.
***************
Kama saa nne na nusu usiku nilikuwa nimefika Upanga mtaa wa Mindu Nyumbani kwa kina Issack.
Nilifanikiwa kuwakuta wote, Issack na Cheupe.
Jambo la kwanza kuwauliza ilikuwa ni wapi ulipo ule mkoba mwingine mweusi. Cheupe akanijibu kuwa wako nao pale pale nyumbani.
Akanieleza kuhusu namna ambavyo aliuficha kabla ya kutekwa na wale wanausalama vibaraka wa The Board.
Akanieleza namna ambavyo aliwaona kutoka juu ghorofani wanausalama wakiwasili na kuanza kuchunguza pale hotelini.
Akanieleza namna ambavyo alichukua begi moja la nguo na kuweka ule mkoba ndani yake, kisha kwenda kumkabidhi dada wa mapokezi na kumsisitiza kuwa hata mimi nikienda nisipewe na asinieleze chochote kile kwa kuwa tuna ugomvi mkubwa ulitokea usiku ndio maana nimeondoka mchana ule.
Kwahiyo akakabidhi begi mapokezi kama mzigo mwingine unavyokabidhiwa kwa taratibu za hoteli.
Akanieleza kuhusu baada ya kutekwa na wanausalama akawaeleza kuwa nimeondoka na mikoba yote kwenda kumkabidhi Justin (baba bite).
Baada ya wao kunipa taarifa hiyo na mimi nikawaeleza kila kilicbotokea Dodoma mpaka mzee alipojipiga risasi.
Lakini jambo la ajabu ambalo hata mimi mwenyewe nilijishangaa, ni kwamba sikuwaambia kuhusu lile suala la Zurich, Switzerland.. Na wala sikuwaambia kuhusu kuchukua ile bahasha mzee aliyodai ina maelezo kuhusu namna ya kuifikia na kupata access ya ‘deposit box’!
Nilijihisi kuwa suala hili liwe siri yangu.
“So nini kifuatacho ITV??” Cheupe akaniuliza baada ya wote kumaliza kupeana mrejesho.
“Nahitaji kwenda kukabidhi huo mkoba uliobakia.. Kesho asubuhi na mapema inabidi nifanye hivyo.!”
*******************
MIEZI MITATU BAADAE; Nashera Hotel, Morogoro
Hii ni moja ya siku yangu muhimu zaidi tangu nizaliwe.
Hii ni siku ya kukumbukwa zaidi katika historia yangu, ni siku ambayo niliandika tena ukurasa mpya wa dhahabu katila maisha.
Leo hii tulikuwa hapa Nashera tunazindua mradi wa mpya wa*SOTE HUB* kwa ajili ya vijana. Mgeni rasmi katika uzinduzi huu, ambaye sasa alikuwa ni rafiki yangu mkubwa, Raia wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa amenisaidia kupata mkataba mnono kati ya taasisi yangu ya SOTE HUB na shirika la NSSF.
NSSF walikuwa wanawekeza kiasi cha shilingi bilioni kumi katika mradi wetu mpya wa kuibua makampuni mapya yanayomilikiwa na vijana.
Muda huu Rais alikuwa anahutubia. Kila baada ya sentesi kadhaa alikuwa ananisifia juu ya ‘uzalendo’ wangu uliotukuka.
Alinimwagia sifa kede kede mpaka nikajihisi niko ‘on top of the world’!
Nikageuka kutazama upande wa wageni waalikwa. Nikamuangalia Cheupe wangu. Moyo wangu ukaburudika.
Nikamuangalia Godi, nikapata faraja.
Nikageuka kuwaangalia Chifu, yule mzee wa mbagala akiwa na vijana wake wale tuliompatia. Moyo wangu ukajawa na furaha.
Kampuni yao ya ulinzi itakuwa ni moja ya wanufaika wa uwekezaji huu.
Kipindi kile tumewaita vijana ili kutengeneza kitengo feki cha Usalama wa Taifa tulikuwa tunajita Unimax Marketing, lakini wao baada ya kuifanya kampuni ya ulinzi walijiita UNIMAX SECURITY (Uniquely Maximized Security).
Niliwaangalia watu wote waliohudhuria, mbunge, Meya, Mkurugenzi wa NSSF na watu wengine mashuhuri nikasema hakika Mungu yu mwema.
Leo hii Ray amekaa meza moja na watu hawa, na Rais wa Tanzania.
Mungu yu mwema hakika.
Wakati mimi nafurahia baraka hizi kubwa, huko mahakamani wanasiasa nguli, wafanyabiashara wakubwa na watu wengine mashuhuri, wote walikuwa wanachama wa The Board na vibaraka wao walikuwa wanakabiliwa na kesi za Uhaini na Uhujumu uchumi.
Moyo wangu ukazidi kuburudika.
Cheupe & Kichwa
Tayari ulikuwa umepita mwezi mmoja tangu SOTE HUB tuzindue mradi wetu kwa kushirikiana ma NSSF.
Baada ya kila kitu kukaa sawa, nilikuwa nimeomba likizo ya wiki tatu ili niweze kurelax walau kidogo maana sikuwahi kupumzika tangu niko kwenye masahibu na mpaka sasa niko nchi ya ahadi.
Ujauzito wa Cheupe ulikuwa unakaribia miezi mitano, kwahiyo kwa mbali kitumbo kilikuwa kimeanza kutokeza.
Likizo hii ya wiki tatu tulikuwa timepanga tufanye ‘vacation’ sehemu nzuri ya kupendeza.
“au twende Uganda ili uapte nafasi ya kuonana na mama pamoja na wifi yangu Dorothy..?” cheupe akapendekeza..
“no no! sitaki kudeal na hayo mambo sasa… tukirejea na kutulia ndio tutaenda Uganda kuwatafuat!” nikamjibu.
Baada ya hapo Cheupe akapendekeza Zanzibar, nikakataa.
Akapendekeza Mombasa, nikakataa.
Akapendekeza Afrika Kusini, nikakataa.
Akapendekeza Mayotte, nikakataa.
“Heeeee… sasa unataka wapi baba?”
“Twende sehemu ambayo tunaweza hapa kuja kuwasimulia wajukuu.!” Nikamjibu.
“OK! So where should we go baby?” Akaniuliza huku ananiangalia kimahaba.
“Zurich, Switzerland.!! “
Cheupe akanibusu na kuruka ruka kwa furaha.
Nikatabasamu. Sikuwa na uhakika kwanini nataka kwenda Zurich… lakini nilijua nafsini mwangu. Haikuwa kwasababu ya ‘vacation’ pekee.
Chochote kitakachotokea, Mungu ndiye anajua… lakini moyoni mwangu naami kwamba, nimefanya jukumu langu kwa nchi yangu.
I have fought a good fight,
I have finished the race.!!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MWISHO.
THE BOLD.
Daah?! Binafsi hii simulizi imenivutia sana aisee...#VIPEPEO WEUSI 👍💪🔥
ReplyDeleteYaan akili ya Ray nimeikubali kinouma...ningeipa hii simulizi nyota 5 aisee...🌟⭐️⭐️⭐️⭐️...ni kali mno...big up brother ...nimeikubali sana hii simulizi✨👌