IMEANDIKWA NA : MAUNDU MWINGIZI
*********************************************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"…Yaani kweli Ramla umeamua kunitenda kiasi hiki?Pamoja na mapenzi yote niliyokupa lakini umeamua kunisaliti…Nimepoteza pesa zangu nyingi kukusomesha nikiamini wewe nd’o utakuwa mama wa wanangu lakini leo wema wangu umegeuka kuwa mkuki wa sumu uliokita moyoni mwangu! siamini Ramla, kwanini hasa umenitenda haya Ramla? aaaah." Niliendelea kulalama peke yangu huku nikilia kwa uchungu, shuka yote ikiwa imelowa jasho na machozi pale kitandani
"Kitendo ulichonifanyia Ramla kinaniuwa ndani kwa ndani, huu ni zaidi ya ukatili… yaani umesahau ahadi zetu zote tulizowekeana." Niliendelea kujisemea peke yangu mithili ya mwendawazimu, maneno yalikuwa yakinitoka utadhani ninayeongea naye yuko hapo
Taarifa hizi za uchungu kuwa yule mwandani wangu niliyempandisha daraja na kumfanya kuwa mchumba wangu kwa sasa ananisaliti kwa kutoka na na kigogo maarufu jijini Dar es Salaam niliambiwa na rafiki yangu kipenzi aitwaye Mwalimu Honde, sikuwa na sababu ya kuipinga habari hiyo kwakuwa nilimuamini sana mwalimu Honde ambaye mbali ya kuwa rafiki yangu, pia alipata kuwamwalimu wangu pale chuo kikuu cha Dar es Salaam na kwa sasa ni Muhadhiri katika chuo cha IFM ambacho anasoma mchumba wangu Ramla hivyo alichoniambia bila shaka ana uhakika nacho kwa asilimia zote kwa kuwa naye muda mwingi huwapo chuoni hapo hivyo kushuhudia na kusikia mambo kadha wa kadha yatukiayo
Kilichoniuma zaidi ni pale nilipotajiwa na jina la huyo kigogo ambaye Kwanza ni tajiri na mfanyabiashara maarufu anayemiliki miradi mingi. Magari na majumba anayomiliki yametapakaa kila kona ya jiji mithili ya utitiri, anamiliki Cassino kubwa na maarufu kuliko zote jijini Dar iitwayo Hookup Couner, mbali na miradi hiyo, pia anahusishwa na Biashara haramu ya dawa za kulevya, ujambazi wa magari na biashara ya nyara za serikali… huyu si mwingine ni Tajiri Pablo Mwaki.
"…Hata nikitaka kumfanyia ubaya sitaweza.." Hasira zangu nilijaribu kuzimaliza kwa kuendelea kubwabwajamaneno huku nikiangua kilio cha nguvu mle chumbani. Hatimaye nikanyamaza, nikajikaza,nikainuka pale kitandani na kwenda kuoga.. tofauti na siku zingine, siku hii nilitumia karibu saa nzima nikiwa bafuni na hatimaye nikatoka nikiwa sijajimwagia walau kopo moja la maji, macho yangali mekundu kwa kilio nilichoangusha punde tu.
Huko bafuni nilikuwa nimesimama tu kichwa kikiwa na zaidi ya Kilo miamoja za mawazo. Nikarudi mpaka chumbani na kupanda kitandani kulala vivyo hivyo, bila ya kuoga wala kula lakini usingizi ukawa ni bidhaa adimu kabisa chumbani mwangu,
Amaa kweli mapenzi yana nguvu!
Usiku kucha niliwaza na kuwazua nifanye jambo gani ili nimrejeshe mchumba wangu mikononi mwangu, sikuwa na la kufanya zaidi ya ujasiri wa kipuuzi uliochipuka moyoni mwangu kuwa nitapambana na Pablo Mwaki bila ya kuogopa utajiri wala ujambazi wake.
Hakika sikumjuwa vizuri Pablo!
*****
Karibu na Posta mpya jijini Dar es salaam, Jengo kubwa la kibiashara lililonakshiwa kwa kila aina ya mapambo ya kifalme yenye kila ishara ya ughali, yalikuwa yakilinadi jengo la MIKINDA BUSSINESS CENTER, Ndani ya Jengo hilo mashuhuri kwa karibu wafanyabiashara wote na hata wale wasiojishughulisha na biashara kuna kila aina ya Biashara zinaendelea humo;Supermarket, Slot machine, Bureau De Change, matawi ya benki kadhaa, na pia ndani ya jengo hilo kuna Cassinokubwa na mashuhuri kwa kuuza makahaba, mashoga, na wasagaji. kila utakachohitaji utakipata ndani ya jengo hilo.
Naam mjengo huo na vyote vilivyomo ni mali ya Tajiri Pablo Mwaki!
Pablo Mwaki ni mtu mzima, Mzee wa makamo japo ukimwona hauwezi kumdhania kama ana angekuwa ameshateketeza karibu miaka hamsini tangu awasili rasmi duniani. Yote hayo ni mazoezi, chakula bora, na pesa zake nd’o vimemnawirisha kiasi cha kumfanya aonekane angali kijana tu.. Si mnene wala si mwembamba, mweupe wa wastani anayependelea zaidi kunyoa kipara.
Mbali na mjengo huo, pia Pablo Mwaki anamiliki miradi mingine mingi ikiwemo kampuni ya Harish Mining inayojishughulisha na uchimbaji madini, Kampuni ya usafiri wa majini na Angani, pia ana hisa kwenye baadhi ya makampuni makubwamakubwa ndani na nje ya Nchi, Sifa zake hakuna asiyezijuwa jiijini. Si jambo la ajabu kusikia Miradi, magari, na majumba kadhaa ya kifakhari vikitajwa ama kuhusishwa naye.
Wapo waliodiriki hata kumsujudia Pablo kutokana na utajiri wake lakini pia wapo waliomchukia na kumlaani kutokana na kuwaharibia vijana wao kwa kuwatumia katika biashara zake haramu.
Kihistoria Pablo alishawahi kuhukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumteka na kumwua kijana mmoja mfanyabiashara wa madini aitwaye Samson Shirima na kumpora pesa nyingi, Lakini alitumikia kifungo hicho kwa takriban miaka mitano tu kablahajakata rufaa…baada ya hekaheka za msuguano wa kisheria mahakamani hatimaye akashinda kesi hiyo na kuachiwa huru. Punde baada ya kurejea uraiani akaanza kufanya biashara na kutokea kuwa Tajiri wa kutupwa, kitu kilichofanya wengi waamini kuwa alimwua kweli yale mfanyabiashara na kwamba ametumia pesa alizomdhulumu kutoa hongo mpaka kuachiliwa akiwa hanahatia, na albaki ya pesa hiyo kuanzishia biashara!
*****CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku iliyofuata niliwasili ofisini na kuomba ruhusa kwa bwana Jimmy ambaye mbali ya kuwa Bosi wangu katika kampuni ya Sajam Marine, pia ni Mume wa Mama’ke mdogo na Ramla…nilimweleza kuwa naumwa sana tumbo japo haikuwa kweli. Lengo langu likiwa ni kupata fursa ya kwenda kuonana na Mwalimu Honde tu.
Akaniruhusu!
Nilipotoka tu ofisini nikaenda moja kwa moja mpaka Chuo cha usimamizi wa fedha(I.F.M) nikapokelewa vizuri namwalimu Honde japo hatukuwa katika ule ucheshi na uchangamfu wetu. nilishindwa kabisa kujizuwia na kujikuta nikionesha waziwazi hali isiyo ya kawaida usoni mwangu! Mashaka, simanzi na huzuni vikidhiri.. Baada ya salamu mazungumzo yakendelea
"Nisikilize Naufal mimi nakushauri kama mtu wako wa karibu, kwakuwa namfahamu vizuri Pablo naamini akikujua tu utakuwa katika hali ya hatari..”
“Kwa hiyo wewe unataka nifanyeje?” Nikadakia kabla hajamalizaalichokusudia kunishauri
“…Ukubali matokeo na uachie ngazi mapema, Pablo humuwezi ndugu yangu.. Yule ni zaidi ya mnama atakupoteza…ana mtandao mpana shetani Yule, anatumiliwa mpaka na mawaziri kupitisha biashara zao haramu za dawa za kulevya na nyara za serikali kwa kivuli cha kampuni zake."
“Yaani Honde badala ya kunishauri tufanyeje ili tuwaachanishe we unataka niachane na Ramla? Are you serious?”
"Kaa ukijua Pablo kaishatangaza ndoa , na Ramla amelipokea kwa furaha suala hilo, sasa kama unataka kuiweka roho yako rehani, endelea…Lkini nakuhakikishia kuwa Pablo atakupoteza asubuhi na mapema…atakuzima kama kibatali."
"Hivi Honde una akili timamu kweli wewe? unajua mimi na Ramla tumetoka wapi? unataka nikubali kirahisirahisi kuibiwa na bwege huyo kisa ni tajiri?, Kwanza wataoana vipi wakati Ramla ni Muislam na huyo mjinga wake ni Mkristo?”
“Upo dunia gani kaka? Ramla ameshabadili dini na sasa ni Mkristo japo nasikia wanafanyasiri kwa sasa.” Maneno ya mwalimu Honde akazidi kunilipua moyo wangu
“Nilichogundua na wewe nawe ni msaliti tu, utakuwa umetumwa ili univunje moyo… maana Sio bure!" nikanyanyuka kwa hasira na kuanza kuondoka bila hata ya kuaga.
Nilimsikia Honde akijaribu kuniita ila hata sikujisumbua kugeuka nikaenda mpaka barabarani upande wa pili ulipo ukumbi wa Makumbusho ya taifa nikachukua Bodaboda na kutokomea zangu.
Nilipofika nyumbani nikajipumzisha kwenye kochi huku nikiwa na mawazo mapya kichwa,
“Hivi inakuwaje rafiki yangu wa karibu kama Honde anashabikia tukio hili? Tena bila hata ya aibu anasema nimuache Ramla!ina maana amekosa ushauri wa kunipa zaidi ya huo upuuzi wake? Sasa nimeanza kumshtukia, Haiwezekani! huyu itakuwa naye katumwa na huyu mjinga mwenzao ili anishawishi tu nimuache Ramla wangu au pengine hata yaweza kuwa ni yeye ndiye anayemtaka.” niliendelea kujifariji huku sasa lawama na hofu zangu zote zikiwa ni kwa Honde.
Nikainuka pale kwenye kochi nikaenda bafuni kuoga, nikiwa bafuni nilisikia simu yangu ikiita nilipokwenda kuiangalia alikuwa ni Honde akinipigia simu nikaiangalia simu ikiita bila kuipokea kisha nikarudi bafuni huku nikijisemea mwenyewe "Akkkh hivi huyu mjinga anafikiri miye hayawani kama yeye.."
Nikiwa bafuni naendelea kuoga simu yangu iliita tena ila wala sikujisumbua kwenda kuiangalia nikijuwa atakuwa ni huyohuyo Honde tu huyo.
Nilipomaliza kuoga nikaenda kuiangalia simu yangu, kumbe hakuwa Honde, alikuwa ni Ramla kipenzi cha moyo wangu, Asali iliyogeuka shubiri ya moyo wangu… haraka nikajifuta maji mwilini kisha nikachukua simu yangu na kumpigia..
“Hallow.” ilikuwa ni sauti nyororo ya mrembo Ramla, Sauti ya kinanda, sauti niliyoizowea kuisikia ikiniliwaza na kunibembeleza mara kwa mara
"Hi darling,” Nilijibu huku nikijifanya kama hakuna kilichotokea
“Mzima mume wangu?”
“Miye mzima wa afya, habari za chuo?”
“Nzuri tu, mbona kimya sana tangu jana?.. halafu na leo nimekuona umekuja chuo nikajua utanipigia simu tuonane lakini ukanichunia… sio vizuri hivyo.”
"Hapana sijakuchunia mpenzi wangu nilikuwa na haraka sana kuna Laptop yangu alikuwa nayo Mwalimu Honde nd’o nikawa nimeiijia… kulikuwa na kazi ya muhimu sana leo ofisini.”
"Okay Baby, kesho nitakuja kwangu nijipikie mwenyewe.. nimechoka na haya mambo ya hostel kila siku chips tumpaka zinachosha." Alitaka kuja kwangu kupika! Tuliendelea kuzungumza kwa madaha kila mmoja akimhadaa mwenziye, mimi nilimhadaa kwa kujifanya kama hakuna tatizo lolote nililolisikia, naye bila shaka akinihadaa mimi kwa kuniita majina mazuri ya baby, mume wangu, nk wakati alijua fika kuwa kwa sasa yeye ni mali ya Pablo Mwaki.
Baada ya kukata simu Nikajitupia kitandani nikiwa nimechoka mwili mpaka akili! mawazo ya kila aina yakizunguka kichwani mwangu. Nilikuwa nusu naamini nusu siamini kuwa Ramla amenisaliti, hapo hapo nahisi kuwa Honde ndyie anataka kutugombanisha, hapohapo natamani nimtafute huyo Pablo Mwaki nimfanyie kitu kibaya japo haikuwa rahisi, ni matamanio tu yasiyowezekana
Waswahili wanamsemo wao kwambaDua la Kuku halimpati mwewe.
Nikiwa pale kitandani nilisikia mlango ukigongwa, nikajinyanyua kwa uchovu mpaka mlangoni na kuufungua! nilipofungua tu akaingia msicha. mrembo, mcheshi na mchangamfujapo kwa leo sikuuona ule uchangamfu wake niliuozoea kuuona.. ni kama aliyekuwa ametatizwa na jambo fulani, huyu si mwingine ni Ntahondi ambaye ni rafiki wa karibu sana na Ramla na pia wanasoma wote chuoni, IFM
“Karibu Ntahondi.”
“Ahsante Shem.”
“Mpaka nimeogopa mbona usiku hivi? Kuna usalama kweli?”
Akaachia tabasamu, tabasamu la uchungu!
“Usiku gani wa kutisha huu? Nd’o kwanza saa moja maghrib… au hautaki wageni shem?”
“Hapana sio kama sitaki wageni ukizingaitia wewe si mgeni, hapa ni kwako sema tu kawaida yako, haya karibu uketi.”
“Okay!Ahsante.” Baada ya kumkaribisha nilirudi kwanza kuufunga mlango kisha nikaenda mpaka kwenye Friji ili nimuangalizie japo kinywaji lakini akaniwahiCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Shem wala usihangaike na kinywaji, miye si mkaaji kabisa, nataka tu tuongee haraka niondoke zangu.”
“Acha roho mbaya, hautaki hata kuniwekea Baraka ndani!”
“Usijali nitakunywa hata siku nyingine.”
Baada ya Ntahondi kukataa kinywaji nikarudi mpaka karibu ya kochi alilokuwa ameketi na miye nikakaa kwenye kiti cha uvivu kisha Ntahondi akaanzisha mazungumzo, nilijiweka sawa kitini kupokea habari ile iliyoonekana kuwa ni nzito sana kwa jinsi muwasilishaji alivyoonekana usoni.
“Kwanza kabisa naomba unisamehe kwa hili n’takalo kwambia kama nitakukwaza maana siye wanaadamu hatujakamilika… pili hata kama halitokufarahisha lengo langu mimi ni kunusuru maisha yako hivyo naomba nawe uninusuru kwa kuificha siri hii. hata kama hautoipenda.” Ntahondi alikuwa akiongea huku akiniangalia usoni bila hata ya kupepesa macho. Nikatikisa kichwa changu juu chini ikiwa ni ishara ya kumwelewa alichoniambia,
"Kwa kifupi maisha yako yapo hatarini… muda wowote unaweza kuitwa kwa jina moja tu la Maiti…” baada ya kuvuta pumzi akaendelea “…Na anayekuangamiza na ku kuuwa ni Mchumba wako.. Ramla.”
“Ramla? kivipi aniuwe? Mbona sikuelewiNtahondi” Nilishtushwa sana na taarifa hii japo nilianza kuhisi kuwa huenda sasa huu ukawa ni muendelezo wa ile habari niliyopewa na Honde
“Tulia na unisikilize kwa umakini… Ramla hivi sasa anakusaliti, amepata mwanaume mwingine anayetoka naye kimapenzi, mtu huyo anaitwa Pablo Mwaki, ni kigogo mmoja maarufu tu bila shaka unamjuwa.. na kwasasa wanataka kufunga ndoa.”
“Unauhakika Ntahondi?”
“Mpaka nimetoka huko nitokako na kuja hapa kukupa habari hii mimi sio mwehu.. mimi nasoma na Ramla na ni rafiki yangu wa karibu. lake langu langu lake…Kwa kifupi Pablo Ameshapewa taarifa zako kuwa wewe ndiye mchumba wake na Ramla hivyo yupo kwenye mchakato wa kukusaka, akukamate ikiwezekana hata kwa kukuteka ili wao wawe huru na mapenzi yao na ndoa yao bila ya bughudha." Ntahondi alihitimisha kauliyake kwa kusimama huku akimalizia “…Mimi naondoka, ila jitahidi kuwa makini na Ramla kwa usalama wako anaweza kutumiwa yeye ili kufanikisha mpango wao
“Aisee! mbona kama nachanganyikiwa Ntahondi? yaani Ramla anaweza kufikia hatua hiyo kweli?”
“Na kwa taarifa yako huyo Bosi wako Jimmy ni rafiki wa karibu sana wa Pablo… na hata kwenye hiyo kampuni yenu Mwaki ana hisa zake humo.. na pia ujuwe kuwa Mke wa Jimmy ambaye ni mama’ke mdogo na Ramla ndiye aliyemshawishi Ramla akuache wewe ili awe na Pablo hivyo inawezekana hata huyo Jimmy akawa anaujuwa mchezo mzima… hivyo naye kuwa naye makini sana.” Wakati huo tunaongea habari hizo tulikuwa tumeshanyanyuka Ntahondi akiwa mbele, naminikiwa nyuma yake mpaka mlangoni ambako tulisimama na baada ya maelezo hayo Ntahondi alifungua mlango na kuondoka zake na kuniacha nikiwa nimeduwaanisijuwe cha kufanya,
Niliufunga mlango nikarudi mpaka kitandani nikiwa natetemeka wa hofu, uoga na hasira za hali ya juu.
Nilizidi kuingiwa na hofu kubwa kufuatia tahadhari alizoniachia Ntahondi, chumba nilikiona kidogo utadhani nimo ndani ya yai, kila nilipojaribu kujikaza na kukiendea kitanda kuutafuta usingizi ilishindikana, niliendelea kujilaza tu pale kitandani huku nikiugulia.. hatimaye niliposhtuka ilikuwa ni saa kumi na mbili asubuhi,
Kilichonishtua ni mlio wa simu yangu!
Nikaamka na kuiangalia simu yangu ili nijuwe nani anayenipigia simu asubuhi yote ile,
Alikuwa ni Jarufu, kaka yangu aishiye huko mkoani Tabora pamoja na wazazi wetu
“Hallow.”
"Enhh za asubuhi!"
“Salama tu bro za huko?”
“Aah nzuri kiasi, pole kwanza na matatizo yako”
“Ahsante nashukuru, mbona umesema nzuri kiasi kuna nini?”
“Mama yuko hoi huku, Presha imepanda… hapa tuko Hospitalini Kitete.”
“Ama! imekuaje?”
“We si ulimpigia simu na kumueleza hayo mambo ya huko kwako.”
“Ndiyo nilimpigia lakini…..”
“Sasa kwanini ulimpigia na unamjuwa jinsi alivyo na hamaki!?”
“Lakini mimi sikumpigia kwa nia mbaya, ilikuwa ni kumfahamisha tu hali ilivyo huku..”
“Sasa mwenzio ulivyompigia tu akapandwa na jazba zake akajiandaa na hapo hapo akaenda huko Rufita kwa mama Ramla.”
“Jamani enhee ikawaje?”
“Nasikia alivyofika tu wakaanza kutukanana sana yeye na mama Ramla almanusura washikane, nasikia wasamaria wema nd’o wakawaamua… Sasa kilichomzidisha hasira zaidi Mama Nasikia huyo mama Ramla alikuwa akitoa maneno machafu sana kuhusu wewe! anasema tunamuonea wivu mwanaye kwa kuolewa na Tajiri pia anasema kama mwanamke hakutaki tena ya nini kumng’ang’ania kama mliyelishana yamini?”
Maneno ya Jarufu yalizidi kuniumiza, kila nikikumbuka jinsi huyu Mama alivyokuwa akiniheshimu na kunijali kipindi chote nilichokuwa nikimsomesha na kumuhudumia mwanaye, Kumbe ilikuwa ni geresha tu na sasa anamjali tena tajiri ambaye hamjui hata kwa sura tu.Nikiwa bado nimeshikilia simu yangu sikioni, kaka alizidi kunivuruga kichwa
"Baada ya mama kurudi nyumbani ghafla ndipo akaanza kuishiwa nguvu, mara akapoteza fahamu… nadhani itakuwa ni Presha, nd’o hapa tupo Hospitali." Baada ya kumaliza kuniambia maneno hayo alikata simu nikabaki nimeduwaa kama Chizi.
Hkika siku hiyo kwangu ilikuwa mbaya na iliyojaa hofu na simanzi, Hofu itokanayo na maelezo niliyopewa na Ntahondi kuhusu usalama wangu, na Simanzi iliyochagizwa na
hasira dhidi ya Ramla na mama yake Mzazi ambao wote wamekula fadhila
zangu za pesa na misaada kadhaa Lakini leo wananiona si chochote si
lolote na kuamua kushirikiana kunisaiti kinyama, Pia nilikuwa namuwazia mama yangu mzazi aliyeko Tabora akiwa hoi kitandani kwa ajili yangu.
Nikainuka na kujiandaa harakaharaka kwenda kazini, muda mfupi baadaye niliwasili ofisini na kuanza kutekeleza majukumu yangu kama kawaida japo nilishangazwa na hali niliyomkuta nayo
Bosi wangu Bwana Jimmy. Hakuwa katika hali ya furaha wala uchangamfu niliozowea kumuona nao siku zote, nilianza kuhisi kuwa hali haikuwa shwari kabisa kwa maana huyu bwana mkubwa inasemekana ndiye anayetumiwa na Pablo kumunganishia kwa Ramla hivyo inawezekana amegundua kuwa nimeshajua hila zake zote zinazoendelea.
Sikujali nikaendelea na shughuli zangu kama kawaida
Nikiwa naendelea kuchapa kazi kwenye Computer yangu pale ofini nilipokea
ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwa Ntahondi akinilaumu
‘Nilikuomba uwe na Subra pia uwe msiri lakini sasa u nikamjibu hamefanya nini?’
Nikamjibu harakaharaka
‘Kwani kuna nini tena Ntahondi?’
‘kwanini umemueleza mama yako mambo haya?, sasa Mama yako kaenda
nyumbani kwa Mama’ke Ramla wametukanana sana na sasa Imeshajulikana
kuwa wewe umegundua mpango wao ndipo ukampigia simu mama yako.. na sasa Mwaki anamtafuta anayevujisha siri zao sasa unataka niuawe?’CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sikuwa na cha kujitetea kwa kuwa tayari nilikuwa nimeshajua kuwa ni kweli Mama alienda kwa Mama Ramla na
walilumbana sana ila sasa hofu yangu ikawa kwa usalama wa Ntahondi endapo atagundulika kuwa ndiye anayenipa siri zao nyeti,
Nikiwa bado nawaza jambo hili nikaanza kupata picha ya kwanini Mr Jimmy hakunichangamkia wakati naingia ofisini, kitu ambacho si kawaida yake
Vita!
Nikaendelea na kazi katika hali hofu kwa takribani wiki tatu mfululizo bila ya kuwa na Mahusiano mazuri ya kimazungumzo na Bosi wangu, haikunipa tabu kwa kuwa nilikuwa nimeshamjua Vema kuwa ni miongoni mwa watu hatari katika maisha yangu kwa sasa,
Nikajiepusha naye!
Lakini pia katika kipindi hiki chote sikuwasiliana na Ramla kitu ambacho si kawaida yetu! hali hii ilizidi kunithbitishia kuwa sasa taa ya hatari ilikuwa imeshamulika, Ila nachoshukuru Mungu ni kuwa nimeendelea kupokea taarifa za kuimarika kwa hali ya Mama kule nyumbani, pia nami nimekuwa nikipokea massage za kunifariji na kuniliwaza kutoka kwa ndugu zangu kutokana na matatizo haya, Pia niliendelea kupata taarifa za kiusalama kutoka kwa Ntohondi japo kwa sasa haikuwa taarifa Nzito pengine hakuwa akipata taarifa kutokana umakini mpya kufuatia kuvuja kwa siri zao, au pengine alizipata ila hakuniambia kwakuwa haniamini sana katika utunzaji wa siri hizo..
Siku moja majira ya saa mbili kasoro(usiku) nilikuwa nimeenda nyumbani kwa Mwl Honde katika kujaribu kujipendekeza kwake baada ya kumcukia kwa ukweli aliokuwa akinipa kuhusu Ramla na kumwona kama mchonganisha tu na fatani wa huba letu, Tukiwa katikati ya mazungumzo Ghafla nilipokea ujumbe mfupi wa Maandishi kutoka kwa Ntahondi akinitaka tuonane haraka sana maeneo ya Leaders Club,
Ikanibidi sasa harakaharaka nisimame na kumuaga Honde ili nimuwahi Ntahond nikijuwa tu kuna taarifa za muhimu sana nikazipate, nikaondoka moja kwa moja mpaka huko katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni.. japo kulikuwa na foleni ndefu ila kwa umahiri wa dereva bodaboda niliekuwa naye ndani ya dk 20 tukawa tumewasili,
Nilipofika nikaenda mpaka sehemu ya Kiwanjani pembeni ya Bendi ya Muziki iliyokuwa ikitumbuiza nikachukua kiti na kuagiza kinywaji, kisha nikatoa simu yangu na kumpigia Ntahondi ili nimtaarifu kuwa nimeshafika,
"Nimeshakuona ulipo nakuja hapohapo ulipo,” Alijibu baada ya kupokea simu kisha akakata
Baada ya muda kidogo akaja mpaka pale nilipo kisha akaketi na kunisalimu, naye akaagiza kinywaji chake kisha akaniambia kuwa tungeenda upande wa pili kule wanapouza Nyama choma ili tuwe salama zaidi.. tukainuka na kwenda ule upande wa pili, Tukaanza mazungumzo baada ya kuketi huku mie nikiwa na mchecheto zaidi wa kutaka kujuwa kinachoendelea. Bila ajizi akaanza kufunguka
“Haya mambo vipi?”
“Poa tu za tangu jana?”
“Nzuri tu hivyohivyo, kwanza pole na Mchoko.”
“Ahsante wangu, lete maneno.”
“Sasa nimekuja kukuongezea mchoko mwingine.” Maneno haya yalipenya sawia katika masikio yangu nikawa namsikiliza kwa makini, kisha akaendelea
"Ni hivi Mwaki sasa yuko serious anataka kumvisha pete ya uchumba Ramla, na Tendo hilo wamepanga kulifanya hadharani tena itakuwa ni siku ya Graduation yetu, Wakati wa kutoa zawadi ndio Mwaki amepanga kumpa Ramla zawadi ya Gari ya kifahari na kisha baada ya hapo atamvisha Pete ya uchumba…” Akashusha tena pumzi kabla ya kuendelea kufunguka “…Na tayari sasa ameshaanza mchakato wa kukusaka ili usije ukaleta usumbufu siku hiyo, na kama atakutia mikononi pengine nd’o itakuwa mwisho wa maisha yako, hivyo kuwa makini ikiwezekana hata kazini kwa sasa usiende maana Bosi wako naye ni mwanamtandao… pia ikiwezekana hata pale kwako uhame haraka na ukipata muda ni bora ukatoe taarifa Polisi kwa usalama wako.” baada ya maelezo hayo mdada akasimama kisha akaniaga na kunisisitiza niwe makini sana,
Wakati tunaondoka akanikumbusha tena jambo linguine
“Pia inabidi ubadili namba yako ya simu maana hawa jamaa wana mtandao mkubwa wasije wakatufuatilia wakagundua mambo yetu… kuwa tunawasiliana.”
Tukaagana! Nikashika njia yangu huku Ntahondi naye akishika yake,
Sikutaka kulaza damu, nikaondoka mpaka kituo cha polisi cha Msimbazi ili kutoa taarifa ya kila kinachoendelea…
Nilikumbana na vikwazo vya hapa na pale kutoka kwa maaskari wapenda rushwa ambao wanaijuwa vyema nguvu ya Pablo Lakini Mwaki.. Baada ya vuta nikuvute hatimaye nilifanikiwa kufungua kesi kisha nikarudi mpaka kwangu
Nilipofika chumbani nikajilaza kidogo juu ya kochi ili nitafakari pa kwenda kulala tofauti na pale Nyumbani kama alivyonielekeza Ntahondi lakini hapo hapo usingizi ukanipitia..
*****
Upepo wa ubaridi ndio ulioniamsha, na hivi nilikuwa nimelala bila ya kujifunika shuka nd’o nilinyong’onyea kabisa.. Nikaamka na kwenda kuoga haraka kisha nikarudi ndani kuvaa ili niende tena kwa Mwalimu Stephen Honde nikamueleze hali ilipofikia, Pia nikiwa na lengo la kwenda kukata tiketi ya Bus nirudi kwanza nyumbani Tabora nikatulize akili ili nijipange kupambana na huyu fedhuli.
Nilipotoka kwangu nikatembea mpaka barabarani, ikanibidi nikachukue Teksi kiusalama maana sasa sikupaswa kuonekana kwakuwa tayari nilikuwa kwenye mtego wa Mwaki.. ni kweli Pablo ni mtu hatari sana lakini mbaya kuliko zote ni kwamba Pablo ni zaidi ya mtu mbaya
Hilo sikulifahamu!
Nikamchukua TaxDriver ambaye huwa ananibeba mara kwa mara na kumuelekeza anipeleke Stand ya Ubungo ili nikakate tiketi na kisha anipeleke IFM Kwa Mwl Honde
Tukiwa njiani dereva aliniomba tupitie Sheli tukaweke mafuta, nikakubali! ila cha ajabu huyu dereva alikuwa akiendesha huku akiwa bussy na simu yake akichart… kitu ambacho nilishindwa kuvumulia ikabidi nimlalamikie naye kwa upole akanitaka radhi, akaendelea kuendesha mpaka Sheli ya mafuta.
Baada ya kujaza mafuta akatoa pesa na kumlipa mhudumu, Kabla hatujaanza kuondoka wakatokea jamaa wawili, watanashati, wakamwambia dereva kuwa awapeleke Ubungo, dereva akawajibu kuwa tayari ana abiria mwingine japo naye anaenda hukohuko hivyowajaribu kuniomba kama nitaridhia kuwasaidia twende sote, aliponiomba nikaona acha tu nimsaidie kijana huyu aingize riziki,nikawakubalia wakaingia ndani ya gari vijana wale wakaketiseat za nyuma na tukaendelea na safari yetu
Tukiwa ndani ya gari ghafla kijana aliyekaa nyuma yangu akanishika begani, nilipogeuka tu nikasikia nimepigwa na kitu kizito kichwani… kabla sijakaa sawa huyu mwingine aliyekuwa nyuma ya dereva naye akanipiga ngumi nzito, CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ikawa ni kichapo juu kichapo mpaka nikawa nasikia kizunguzungu!
Mara, mmoja akaniwahi mikono kisha huyu mwingine akanifunga kitambaa cheusi usoni,
Kiza kikatanda usoni!
Wakati haya yakiendelea huyu Dereva alikuwa katulia kimya akiendelea kuendesha gari taratibu… hapo nd’o nikajua kuwa alikuwa anajuwa kila kitu ninachotendewa.. lakini sikuelewa ikawaje mpakanaye akashiriki katika kunitendea kitendo kile wakati yeye ndiye dereva wangu mkubwa wa kila siku!
Nikiwa nimefungwa kitambaa usoni nilimsikia Yule kijana aliyekuwa nyuma ya dereva akimuuliza dereva kuwa anaielewa vema njia waliyomuelekeza? Dereva naye akajibu kuwa anaijuwa vizuri… hapo sasa nikajuwa tayari nimeingia mikononi mwa PABLO MWAKI,
Gari ilikuwa ikitembea kwa kasi huku nikiwa sijui tunaelekea wapi, Nikawa katika majuto ya hali ya juu sana, Lengo langu la kwenda Tabora sasa limekufa na hata Mwl Honde nd’o simuoni tena, Nilijua sasa Kifo kipo mlangoni,
Gari ikiwa inaendelea kuchuka kasi ghafla meseji ikaingia kwenye simu yangu, sikujuwa ni nani kwakuwa nilikuwa nimezibwa sehemu ya usoni mwangu.. yule kijana aliyekuwa nyuma yangu akaingiza mkono kwenye mfuko wa suruali yangu na kuitoa simu yangum, Nikasikia akishangaa na kuniuliza
"We mbwa! huyu Ntahondi nd’o nani?" nikajua tu itakuwa ni Ntahondi ndiye amenitumia ujumbe ule, na kabla sijajibu chochote akaendelea kuongea "…Kumbe huyu ndiye anayetoa siri zetu eenh?, tutamshughulikia." Nilizidi kuchanganyikiwa na sikujuwa Ntahondi alikuwa ameniandikia ujumbe gani. Japo mimi tayari nimeshakamatwa ila niliamini kuwa wa kuniokoa ni Ntahondi tu kwakuwa alikuwa akijuwa kila kinachoendelea hivyo kama atawasiliana na watu wa kwetu akawapa maelekezo yote huenda wakamtia nguvuni huyo Pablo na hatimaye nikapatikana, lakini sasa naye kaishagunduliwa na kwakuwa hajajua kuwa ameshajulikana basi angekamatwa kama kuku.
Msafara uliendelea huku nikiwa nimefungwa kitambaa cheusi usoni, Majadiliano yaliyokuwa yakiendelea ndani ya teksi kati ya hawa maharamia na huyu dereva teksi yaliashiria kuwa dereva huyu alikuwa amelipwa kwa ajili yakufanikisha mpango wa kuniteka, nawalimfuata na kumshawishi baada ya kufuatilia na kugunduwa kuwa huwa ninamtumia sana katika safari zang.. iliniuma sana kwa jinsi nilivyomuamini kijana huyu leo kwa tamaa yake ya pesa tena pesa yenyewe itakuwa ni kidogo tu nd’o ameamua kushiriki kitendo cha kunitoa uhai wangu. Sikua na la kufanya kabisa!
Safari ikazidi kuchukua kasi! Ilituchukuwa takribani saa moja na nusu hivi tukiwa njiani tu, hakika ilikuwa ni safari ndefu!
Hatimaye tukafika eneo lililokusudiwa!
Teksi ilisimama kwa muda kama wa dakika mbili kisha nikasikia Geti likifunguliwa na kisha teksi ikaingia ndani baada ya gari kusimama walishuka vijana wale wawili na mmoja akafungua mlango wa mbele upande niliokuwa nimeketi mimi, akanivuta kama kiroba nikajikuta nimeshuka kama mzigo mpaka chini kisha akanifungua kitambaa usoni.
Nikaona mazingia mapya!
Nilijaribu kuangaza huku na kule lakini sikuelewa tuko wapi! ilikuwa ni ndani ya uzio kubwa iliyozunguka Jengo kubwa sana chakavu mfano wa maghala ya kuhifadhia Tumbaku. mle ndani kulikuwana vijana wengine watatu, wote warefu, waliojazia misuli yao vilivyo, wawili wametinga miwani myeusi, na mmoja akiwa hana miwani na kavaa Suti nyeusi.
Walinichukuwa na kuniingiza ndani kabisa ya jengo hilo..
Mazingira ya ndani ya Jengo hilo yalikuw ni ya kutisha sana maana kulikuwa na ukimya wa hali ya juu, pia hata hawa jamaa sura zao zilivyokaa kikatili ukiwaangalia tu utahisi harufu ya kifo. nilipo fikishwa mle ndani nikafungwa kamba mikono kisha wakanining'iniza juu mithili ya mbuzi anaesubiri kuchunwa ngozi kisha jamaa hawa wasio na huruma hata chembe walianza kunichapa mijeredi ya nguvu, nililia nakupiga kelele mpaka nikawa naishiwa nguvu lakini kelele zangu hazikuwazuia hawa jamaa kuendelea kuniadhibu. mwili wote ulikuwa umevimbavimba kwa alama za fimbo..
Baada ya Muda akaja kijana mmoja akiwa ameshika Msumari wa moto nadhani ndo ulikua umetoka jikoni kwajinsi ulivyowiva ukabadilika rangi nakuwa mwekundu,
Naam ulikuwa umewiva kisawasawa… akaja mpaka pale nilipokuwa nimetundikwa akaanza kufanya kama vile anachora maandishi kifuani kwangu, Mapajani, na mgongoni nilisikia maumivu makali sana, nililia kwa sauti mpaka nikajihisi sasa kupoteza fahamu..
Hakuna aliyenisikia!
Ndani ya dakika kama kumi na tano nilizofikishwa mle ndani nilikuwa nimeshaharibika mwili mzima kwa adhabu na mateso makali niliyokumbana nayo. Vidonda vilitapakaa wiliangu!
Wakati nikiendelea kupewa adhabu za kila aina ghafla akaja yule kijana aliekuwa amevaa suti, alikuwa kama amechanganyikiwa na jambo Fulani
"Jamani kuna hali ya hatari kidogo.."
wale viajana wote wakamgeukia na kumsikiliza, kisha akaendelea "…Wakati akina Zungu wanamteka huyu Dogo, nasikia walianza kumpiga mle ndani ya Teksi.. sasa kuna watu walishuhudia hilo tukio hivyo wamechukua namba ya Teksi na wameenda kutoa taarifa Polisi.."
Baada ya maelezo hayo kutoka kwa jamaa huyu ambaye alionekana kama ndiye msimamizi wa kitengo kile cha mateso akadakia kijana mwingine aliyekuwa akiniunguza kwa Msumali wa moto
"Hili sasa ni tatizo.. tena kubwa! lakini kwa kuwa huyu TaxDriver hajaondoka mie nadhani tumzuwie mpaka Soo likitulia huko town nd’o tumuache aende..." kabla hajamaliza kuongea yule mwenye suti akadakia
"Hapana! hatupaswi kumuachia, akibanwa huyu atasema tu… muingizeni ndani mummalize kimyakimya." Nilishtuka sana niliposikia kuwa kijana yule anatakiwa auawe, hapo ndipo nikajuwa kuwa sasa hata mimi sitapona tena. baada ya maelekezo yale vijana wa kazi wote wakatoka nje wakaniacha mie nikiwa pale juu naning’inia.
Ndani ya muda mfupi walirejea ndani wakiwa na kijana yule dereva teksi japo hawakuingia naye katika chumba nilichokuwepo miye, wakaenda naye mpaka chumba cha mbele
Punde nikaanza kusikia kelele kali za kilio kutoka kwa kijana yule, alilia kwa sauti ya hali ya juu, sauti ya uchungu na kukata tamaa kisha akatulia kimya, Kimyakabisa!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sikumsikia tena wala sikujua wamemfanya nini
Baada ya muda wakaja wale vijana waliokuwa wakinitesa mimi walipofika pale usawa wangu wakaikata kamba niliyokuwa nimefungwa nayo pale juu nikaanguka kama kiroba cha taka mpaka chini kisha wakanimwagia maji mengi halafu wakaondoka, kwa mbali nikahisi kama kurejewa na nguvu na uhai niliouhisi ukinipota. Nikalala hapohapo sakafuni kwa muda mrefu sana.
Jioni ikafika, kiza kikaingia na kunikuta nikiwa nimelala palepale chini nilipoanguka kama mzoga baada ya kukatiwa zile kamba nilizokuwa nimefungwa waliingia tena wale vijana na kuniinua kisha wakaniambia niwafuate. nilianza kuwafuata huku nikichechemea kwa taabu kutokana na maumivu niliyoyapata siku nzima, tukafika mpaka kwenye Chumba kilichoandikwa maandshi makubwa PEPO HURU. Sikuelewa maana ya neno hilo nikahisi ndani mule kuna raha japo kidogo ila hali ilikuwa tofauti baada ya kuingia na kukaribishwa na tukio la mwaka!
Nilikuta maiti ikiwa imelala juu ya dimbwi la damu, utumbo ukiwa umetoka nje. Niliogopa sana hali ile nikajikaza na kusogea eneo lile Kuangalia vizuri,
TOBAA!
Alikuwa ni yule kijana dereva Teksi.. wameamua kumwua ili asiende kutoa siri huko mjini. Sasa nd’o wamwue kinyama kiasi hiki? Ama hakika jamaa awa na mashetani wa kibinaadamu. hapo sasa nikazidi kupoteza Bima ya Matumaini kama nitatoka salama mle ndani.
Vijana wale wakaniamuru nimnyanyua maiti yule kisha nimpeleke nje halafu nirudi kusafisha damu na uchafu wake wa haja kubwa na ndogo vilivyomtoka wakati akikata roho. Nilishindwa, kila nilipoiangalia maiti ya mtutuliyekuwa naye muda mfupi uliopita. Nilimuonea huruma sana kijana huyu kwa kifo cha kinyama kama kile japo niliamini Mungu ameamua kunilipia kwa ushenzi alionifanyia mimi wa kunikamatisha kwa maharamia hawa kwa Tamaa ya pesa kitu,
Nikiwa bado nashangaa nikashtuliwa kwa teke kali nililopigwa mbavuni na kuniangusha mpaka sakafuni, nikajizoazoa na kusimama wima huku nikitengeneza sura ya huruma kwa mabazazi hawa wenye roho mbaya na ngumu kupindukia, Nikasogea mpaka alipolala kijana huyu ili nimnyanyue, Cha ajabu wakati nikiwa nimeinama naanza kuibeba maiti ile nikashangazwa na mwanga ambao niligunduwa kuwa ulikuwa ni wa kamera,
Kwanini wanipige picha?
Wanataka kunitendea nini kingine?
Sikuelewa!
Niliogopa kuhoji kuhusu picha hizo nilizokuwa nikipigwa nikijuwa nitapewa kiminyo kingine kikali kuliko kile cha awali, nikaibeba maiti ile mpaka nje kabisa ambako nilimkuta mtu mwingine akichimba shimo bila shaka ni la kufukia dereva teksi.. nikaicha maiti kisha nikarudi ndani nikiwa chini ya ulinzi kusafisha lile eneo alilouliwa.. baada ya hapo nilirudishwa ndani kuendelea na Adhabu,
Niliteswa kinyama, nilipigwa wa kila aina ya silaha.. Malungu yaliyotumika kunipigia magotini na mikononi yalivunjikavunjika na kuniacha nikiwa kama niliyepooza viungo vyangu
Ikapita wiki moja nikiendelea kupata mateso makali sana ikiwemo kupigwa na shoti za Umeme, Hali ilikuwa ngumu sana kwangu, kila siku nilikuwa nikapata adhabu kali na za kila aina huku nikipewa chakula kidogo sana na maji. Mwiliwangu ulisawajika na kuwa mfanowa mzoga wa mbwa tu ila niliendelea kujipa moyo tu huku nikiamini kuwa endapo Ntahondi atatoa taarifa kwa Mwalimu Honde basi ukombozi utanifikia.
Siku moja nikiwa nimefunguliwa kamba niko nimekaa kwenye sakafu napata chakula nakumbuka ilikuwa ni ugali na dagaa za chukuchuku Ghafla nilisikia mlango ukifunguliwa kisha akaangizwa Msichana mmoja akiwa kalainika sana bila shaka ni kwa kichapo alichopewa na mafedhuli hawa, Msichana alikuwa taaban, ngozi yake ikiwa nyeusi kama aliyepakwa masizi, Sikumjua kwa haraka ila nilipotuliza macho hana kumuangalia vizuri nikamtamba.. sikuyaamini achoangu, alikuwa ni Ntahondi, Shemeji yangu kwa Ramla, ilikuwa ni vigumu kumtambua kwa urembo wake mpya aliokuwa nao.damu, jasho na hayo masizi viligandiana mwilini mwake na kutengeneza rangi Fulani aajabu sana.. inaonekana alipigwa nakuteswa kinyama.
Nilijisikia majonzi mpaka hamu ya kula iliniisha!
Nilipomsogelea niligundua kuwa alikuwa amepoteza fahamu, Roho iliniuma sana nikiamini kuwa ni mimi ndiye nimemponza mpaka kufikishwa pale, nikiwa nimesimama nisijue cha kufanya likaniijia wazo… nikaenda pembeni mwa chumba kile nyuma ya Mashine ya umeme waliyokuwa wakiitumia kunitesea nikachukua Dumu la maji nikaja nalo mpaka pale alipolala nikammwagia maji mengi kichwani na mwilini, baada ya muda mfupi alizinduka
Akainuka kwa taabu na kuketi, aliponiangalia na kunitambuwa alianza kulia kwa uchungu sana, nilijaribu kumbembeleza lakini hakunyamaza mpaka baadaye kabisa ndipo alitulia… nikamwacha kwanza atuliendipo baadaye akaanza kunisimulia yaliyomkuta japo alikuwa akiongea kwa taabu sana kutokana na maumivu anayoyapataCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"…Siku uliyopotea ghafla tulijitahidi sana kukutafuta bila ya Mafanikio, kesho yake kaka yako wa Tabora alikuja Dar tukaendelea kukutafuta kila kona bila ya Mafanikio, tulipata ushirikiano warafiki zako wengi ila cha ajabuRamla aligoma kushiriki kabisa kukutafuta, yeye alikuwa busy na Mipango yao ya Kuvishana pete na hatimaye Ndoa. Mwaki ameamua kugharamia Sherehe yote ya wahitimu, Hakuna mwanachuo yeyote kulipa gharama za Sherehe.." alikaa kimya kwa muda, akakohoa sana kisha akaendelea kutiririsha stori iliyoniachia majeraha makali kuliko hata yale ya msumari wa moto..
Majeraha ya moyo!
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment