Simulizi : Siku Ya Graduation
Sehemu Ya Pili (2)
"…Kilichotushangaza zaidi baada kama ya siku tatu mbele uliokotwa Mwili dereva teksi akiwa ametumbuliwa tumbo, katobolewa macho nk walipojaribu kuupekua vizuri mwili wake wakakuta picha mbili zikikuonesha wewe nd’o uko naye akiwa maiti.. kila mtu akaamini kuwa ni wewe ndiye umemwua.. na Mpaka sasa vyombo vyote vya habari vimesha riport kuwa wewe ndiye mwuaji na unasakwa kwa udina uvumba" Maneno ya Ntahondi yalizidi kunifanya niwe kama kichaa, nilizidi kuchanganyikiwa, yaani sasa mimi n’do natafutwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ambayo sikushiriki, huku nateswa na kule nasakwa.. hivyo hataka nitaokoka huku, nikifika huko mjini nitaangukia mikononi mwa mapolisi ambao baadhi yao ni wafuasi wa Pablo.. nilishindwa kujizuia nilianza kulia nikijua sasa vyovyote iwavyo Mwisho wangu umefika.. ikawa sasa ni zamu ya Ntahondi kunibembeleza mimi.
Ntahondi aliendelea kunipa habari kuwa kule mjini Mama yangu amekuwa akipoteza fahamu kila mara kufuata ia taarifa z kutoweka kwangu na taarifa za habari zinazoendelea kukazia kuwa natafutwa kwa tuhuma za mauwaji ya dereva teksi, Pia akaniambia mpango uliopo chini ya Pablo ni kwamba tunatakiwa kuuawa siku hiyohiyo ya Graduation ili Ramla na hawara yake Mwaki waweze kuishi kwa Amani.. Pia Ntahondi alinieleza kuwa anayenishughulika zaidi kule mjini ni Jarufu, pamoja na Mwalimu Honde. nilifarijika kidogo kusikia kuwa swahiba wangu Mwalimu Honde ananishughulika, nilipata matumaini kwa kuwa najua fika Mwalimu Honde ni mdogo wake na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Munanowaanzania hivyo niliamini kuwa inaweza ikawa ahueni kama ataamua kulifikisha suala hili kwa Mhe Waziri.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikiwa naendelea kububujikwa na machozi kutokana na maneno yaliyouchuma na kuuunguza moyo wangu kutoka kwa Ntahondi, naye aliendelea kunipa Story za kila kinachoendelea kule mjini na mpaka yeye kukamatwa na kufikishwa kule Msituni.
"…Nilipopata taarifa kuwa unatakiwa kukamatwa siku hiyo nikawahi kukutumia ujumbe mfupi kwenye simu yako ili uzidi kujihami kumbe tayari ulikuwa umeshakamatwa, sikupata majibu yoyote kutoka kwako, nikakupigia simu yako ikawa inaita tu bila kupokelewa.. nikawa nimechanganyikiwa, nikaamini kuwa utakuwa umeshatekwa lakini akili nyingine ikaniambia kuwa utakuwa salama sehemu tu.. siku mbili baadaye nikapokea meseji kutoka kwako kuwa tuonane Maeneo ya Coco Beach, kumbe walioijibu meseji ile walikuwa ni hawa Majambazi wa Mwaki na hatimaye nikaenda huko Coco, wakatokea nagari ndogo wakanitia nguvuni, wakanipiga sana na kunitesa kinyama, nimeumizwa sana, mbaya zaidi nimedhalilishwa kwa kuvuliwa nguo zote kisha nikaanza kuchapwa bakora mwilini mpaka nikapoteza fahamu, nazinduka nd’o najikuta humu." Alimaliza kuongea Ntahondi kisha akanitaka na mimi nimuelezee hali ikoje kwangu na mle ndani kwa ujumla, na vipi tungejikomboa kutoka katika makucha ya Ibilisi huyu.
Nami nilimueleza mateso niliyopewa mle mndani, ila ikabidi baadhi ya mateso nimfiche nikihofia kumzidisha hofu na kumkatisha tamaa ya kuishi, lakini Mwisho kabisa nikamwambia sisi ni vijana makini Lazima tupiganie Maisha yetu na tuhakikishe tunatoka ndani ya ngome ile ya mauti, wakati nikiongea kwa uchungu maneno haya ya kijasiri ambayo naimani bila shaka kichwani mwa Ntahondi ilikuwa ni Ndoto ya mchana au ni sawa na kujifunika Tishu kwenye mvua ya Elninino
*****
TABORA,2009
Ilikuwa ni mwaka mmoja tangu nipate kazi kwenye kampuni ya Sajam Marine inayojishughulisha na masuala ya usafirishaji mizigo majini, nikiwa Mhasibu.. nikachukuwa likizo fupi kwa ajili ya kwenda kumsalimu Mama yangu mzazi Bi Shammy aishiye mkoani Tabora, niliifurahia sana safari hii kwakuwa ilikuwa ni muda mrefu sana sijaenda nyumbani hivyo nilitaraji kuonana na Mama yangu kipenzi, ndugu zangu, na marafiki zangu ambao tulikuwa tukikaa wote kijiweni tukibadilishani stori kadha wa kadha..
Nikaifanya safari!
Niliwasili Tabora majira ya saa kumi na mbili jioni, nilipokelewa na wadogo zangu waliokuja Stand ya Mabasi kunipokea kisha tukaondoka mpaka nyumbani ambako nilipokelewa kwa shangwe na Mama na ndugu wengine waliokuwa pale nyumbani, ilikuwa ni siku ya furaha sana kwangu, kama kawaida ya wageni mambo kama Jogoo na mpunga huhusika kwa asilia miamoja wakati wa mduara wa chakula cha usiku na kila aina ya vinywaji maalum kwa ajili ya takrima kwa mgeni.. hakika siku nzima ilikuwa ni ya furaha! Tuliongea na kukumbushana mambo mengi ya amani mpaka mshale wa aa uliponadi kuwa imetimu saa sita kasoro za usiku niliondoka na kwenda chumbani kwa mdogo wangu wa kiume na kujiandaa kwa ajili ya kulala..
Asubuhi ya siku iliyofuata niliamka mapema, na baada ya kuoga na kupata kifungua kinywa nikajipumzisha kidogo pale ukumbini na kisha nikamuaga Mama kuwa ninaenda kijiweni kuwasalimia jamaa zangu kisha kuna Mzigo nilipewa na Mke wa Jimmy, Bosi wangu ili niupeleke mtaa wa Rufita kwa Bi Ayman Gamba ambaye ni dada wa huyo mke wa Bosi wangu.. baada ya hapo nikaanza kujongea kijiweni ambako pia nilipokelewa kwa furaha sana na s zangu swahiba zangu wa kitambo niliowaacha wakati naenda masomoni Dar es Salaam. tukiwa katikati ya Soga ndipo alikatiza binti mmoja aliyeunawirisha moyo wangu.. Hakika ni msichana wa kiwango cha urembo, mirindimo mithili ya Mjaluo, Mrefu mwenye mwendo wa madaha mithili ya Twiga, sio Mweupe wala si mweusi, Hips kama ameficha panya, yaani kama we ni Rijali lazima ungegeuka mara mbili kumtazama. Hakuwa mwingine ni Ramla.
Baada ya kuwaulizia jamaa zangu kuhusu binti huyu waliniambia kuwa anakaa mtaa wa Rufita, kuhusu shughuli zake niliambiwa kuwa anafanya kazi za msimu katika ofisi za Tumbaku(ATTT)
Nilitamani kujua mengi zaidi yamuhusuyo binti huyu maana tayari mabishano ndani ya moyo wangu yalianza.. sikuambulia kitu zaidi ya kuchekwa tu kile kilichoonekana kama tama tu iliyonikumba.. Jamaala walibadili mada na tukaendelea na Soga zetu
Baada ya muda mrefu wa maongezi na michapo niliwaaga jamaa zangu ili niende sasa nikamtafute huyo Bi Ayman wa mitaa ya Rufita maana nilikuwa simjui wala sipajui hapo nyumbani kwake anapokaa,
Nikachukua bodaboda kisha kutokea hapo kijiweni mpaka mtaa wa Rufita katika maeneo niliyoelekezwa, tukasimaa kisha nikateremka kwenye bodaboda na kwenda kumwuliza kijana mmoja aliyekuwa upande wa pili wa barabara ile ya Rufita
Lakini kabla sijavuka barabara akatokea msichana mmoja ndani ya nyumba niliyokuwa nimesimama, akamwaga maji nje bila shaka alikuwa akifanya usafi kama si wa vyombo basi wa nguo, nilipogeuka na kumwangalia nikahisikufahamiana naye.. nikamkazia macho, naye akanikazia yake, Punde kumbukumbu zikanijia, alikuwa ni yule binti mrembo aliyepita kule kijiweni..
Kabla sijasema chochote akaniwahi yeye kwa kunisalimia kwa furaha kama anayenifahamu pia
"Mambo."
"Poa, mzima wewe?”
"Mie mzima, mara tu umefika huku?" Akanitupia swali lililonishtua kiasi.. nikahisi labda pengine amenifananisha, nikiwa bado najaribu kuzisoma hisia zake ili nimjibu kitu sahihi akaniwahi kwa swali jingine
"Au nimekufananisha? Kwani wewe si nilikupita na jamaa zako mmekaa kule Minazi mikinda?"
Hakika hakunifananisha kamwe!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Duh una kumbukumbu sana wewe, yeah ni mimi.. kumbe unakuu huku?” Nilimtupia swali la uchokozi
“Ndiyo, na humu nd’o kwetu.”
“Okay thanks! sasa miye naomba kukuuliza tu, napaulizia kwa Bi mkubwa mmoja aitwaye Bi Ayman Gamba, unaweza kupafahamu?"
“Bi nani?” Aliuliza kwa wahka huku akitengeneza abasamu la mshangao usoni mwake
“Bi Ayman.. kwani vipi?” akacheka kidogo kama anayenicheka mimi, kisha akanijibu kwa Pozi
“…Na unayeongea naye hapa ni binti yake aitwaye Ramla… karibu ndani." Tukaangaliana na kisha kwa pamoja tukaangua vicheko vya haja. nikamwomba yule dereva wa bodaboda anisubiri kidogo
Tukaangia ndani!
Tulipofika ndani tulipokelewa na Bi mkubwa mmoja mnene mweupe! Baada ya kusalimiana naye Ramla alinitambulisha kuwa Yule ndiye Bi Ayman Gamba mwenyewe. Alinipokea kwa ucheshi wa kuridhisha tu, ilikuwa ni kawaida kwa waswahili wa mkoa huu kukirimu wageni.. Nikapewa kiti na kujipumzisha huku nikimweleza kilichonipeleka
"Naitwa Naufal natokea Dar japo asili yangu ni hapahapa Tabora… nimepewa mzigo huu kutoka kwa mke wa Bosi wangu, kaniambia nimkabidhi dada yake aitwaye Bi Ayman" Niliongea kwa utulivu huku nikiukabidhi huo mzigo, ilikuwa ni kifurushi kikubwa kiasi kilichofungwa ndani ya bahasha kubwa ya kaki, sikuweza kujuwa ni kitu gani!
Aliupokea mzigo na kunishukuru sana.. nilitamani niendelee kuketi ili nimwone Ramla akipitapita lakini apakuwa na cha kuniweka pale.. Nikainuka, nikaaga na kuondoka.
Wakati naondoka Ramla akaniwahi "Umeshamaliza shida zako hata hauniagi eenh? Ningekwacha ukapotea."
"Nilijuwa uko nje… haya nakusubiri unisindikize." Binti yule mcheshi akanifuata kama anaye nisindikiza vile!
Nyota ya Jaha!
Tukaanza kutoka nje taratibu huku tunapiga stori mbili tatu japo hazikuwa za msingi.. ilikuwa nikutafuta kujuwana tu, baada ya utani wa hapa na pale tukaagana,
“Kwahiyo tutaonana lini tena?” Nilichombeza
“Siku yoyote tu,” Alijibu
“Hata leo?”
“Leo tumeshaonana nasidhani kama ulipanga kuonana na mimi.”
“Sidhani kama itakuwa vibaya kama huu utakuwa mwanzo wa kujuana kwetu.. kama hautojali nja’alie namba yako ya simu.” Akacheka Ramla.
Cheko ya furaha au ya kunisanifu? Sikujuwa haraka zaidi ya kugundua kuwa kumbe mrembo Yule anamiliki mwanya katikati ya meno yake meupe
Akaniangalia tena safari hii akionekana aliyeingiwa na aibu usoni, hakuna nilichokiona zaidi ya ulegevu wa macho yake laini mithili ya samaki aliyekula kungu! Akaipokonya simu yangu aina ya Sumsung kisha akaandika namba yake huku akinitupia jicho la chinichini, alipomaliza kuiandika akajibeepkwenye simu yake ili naye abakie na namba yangu..
Tukaagana huku tukiachaniana zawadi ya matabasamu ya nguvu!
Ishara nzuri!
Niliporejea nyumbani furaha iliongezeka maradufu, akili ikawa ni kwa Ramla tu, nilitamani nirejee kule mtaani kwao ili nijaribu kumvizia nimwone tu japo kidogo, hakika aliukonga moyo wangu. Baada ya chakula kitamu kilichoandaliwa na mama yangu, siku hiyo sikutaka hata kutoka ndani, haraka nikaenda kuoga na kurejea chumbani kwangu kwa ajili ya kulala.
Nikiwa kitandani, nikaanzisha uchokozi wa kumtumia meseji, haikujibiwa! nikatuma tena, nayo haikujibiwa! Nikampigia simu haikupokelewa.Nguvu zikaniisha! Nikajiuliza kama nimemtumia meseji mbaya kiasi cha kumchukiza, lakini nilipozidurusi meseji zangu nilizomtumia zilikuwa za kawaida tu, Sasa nini tatizo? Kabla sijajipatia jibu mwito wa meseji ukaita, kuangalia alikuwa ni Ramla amenijibu huku akinitaka radhi kwa kutokujibu meseji na kutokupokea simu yangu huku akijitetea kuwa alikuwa nje wakati simu ikiwa ndani.. Tukaanza kuwasiliana kwa meseji tamutamu huku tukitaniana, tukisifiana, na kupambiana kwa lugha ya kifundi.. Hakika sikulala siku hiyo! Kwa kifupi Ramla alikuwa ni binti mrembo aliyeumbika kike, apendezeye machoni pa kila rijali hivyo kukosa kwangu usingizi kwa ajili yake si ajabu kabisa. Hatimaye tukalala baada ya kuamua kuwa tusitishe mawasiliano kwa usiku huo!
Tuliendelea kuwasiliana kwa takribani siku tatu mfulilizo huku sasa dhamira yangu ikiwa wazikabisa kuwa nataka kummiliki mrembo Yule, kutamka sasa ikawa kisanga! Japo dalili za Ramla kwangu zilikuwa wazi kabisa kuwa atanipokea.. mwishowe kijana wa Kinyamwezi nikajitosa kutamka maneno matamu ya kuomba hifadhi ya nafsi yangu katika bustani ang'avu la moyo wake, haikuwa kazi rahisi sana kama nilivyotaraji!
Mbwembwemaringo na mapozi nilivyokutana navyo kwake havikunifanya nikate tama, nikaendelea kila siku kumgasi kwa lugha ya kubembeleza hatimaye akinielewa na kunikaribisha sio tu sebuleni bali mpaka chini ya uvungu wa moyo wake…
Sidhani kama kuna maneno yakayotosha kuelezea furaha niliyokuwa nayo baada ya kupokelewa moyoni mwa Ramla..Tukafungua ukurasa mpya, ukurasa wa Mapenzi.
Ikawa ni mapenzi motomoto, mapenzi shatashata, mahaba niuwe, mahaba nigaragaze.. mapenzi mpaka kizunguzungu!, Kila siku nilikuwa nikibuni na kuongeza vionjo vya kila namna ili tu huba lisichuje… tulijaribu kujibana lakini ule msemo kuwa mapenzi kikohozi, kuyaficha hauwezi yakadhihiri! Habari za Naufal na Ramla zikaanza kunong’onwa katika baadhi ya viringe vya wadaku, Hatukujali!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndani ya wiki kama mbili tu za mapenzi yetu motomoto muda wangu wa kurudi Dar ulifika, nilitamani siku zigande niendelee kula raha lakini haikuwezekana.. nikawa sina budi kuondoka..
Nakumbuka tuliagana siku hiyo kwa furaha iliyojawa na majonzi, Ramla alikuwa akilia akilalama kuwa huenda nitamsahau nikifika mjini..nilimbembeleza na kumwahidi kuwa sitamtupa kamwe, pamoja na ahadi nyinginezo pia kimwahidi kuwa nikifika Dar baada ya wiki mwezi mmoja ningemtumia nauli aje ili nimfanyie mpango wa Shule maana alikuwa amenieleza mambo mengi kuhusu familia yao kuwa wanaishi maisha ya tabu na dhiki tangu baba yake mzazi alipoikimbia familia yeye akiwa mdogo sana… Alinieleza kuwa aliishia kidato cha nne hivyo alitamani sana kuendelea na masomo lakini hali ya kiuchumi haikuwa nzuri kwao.. Na kwamba Mama yake hataki Ramla aende Dar kwa huyo mama’ake mdogo ambaye ndiye mke wa Bosi wangu Mr Jimmy..
Kisa? Mam’mdogo alibadilishwa dini na Jimmy na kuolewa hivyo Bi Ayman anahofia kuwa kama akiienda kukaa kule naye ataweza kushawishiwa kubadilishwa dini kwa ajili ya kuolewa. Akakubali ofa yangu.. Tukaagana name nikaondoka mkoani Tabora!
Kila siku nilikuwa nikiwasiliana na Ramla huku ahadi zetu zikiendelea kukaribia kuwa kweli, mbali ya meseji tamu za kumliwaza pia nilikuwa nikimtumia pesa za kumkimu. mwezi mmoja baadaye nikamtumia pesa za nauli kwa ajili ya kuja.. nikamwongezea na pesa za kumwachia Mama yake pale nyumbani ili asipate taabu siku za mwanzoni baada ya yeye kuondoka.
Siku kama tatu hivi mbele akawasili Dar, nilimpokea na kumlaki kwa kila anachpaswa kufanyiwa mwanaadamu mwenye jinsia ya kike.. ilikuwa ni kazi kubwa kwangu kumtowa tongotongo za macho kwa kumtembeza kila kona ya Jiji hili la maraha ili naye auone na kuutambuwa mji, aliburudika na kufurahia kila uchwao!Maisha yakawa ni raha mustarehe! baadae nilimtafutia chuo pale IFM kama nilivyomuahidi, nikamtafutia na Hostel akawa anaishi palepale chuoni.
Mahitaji yake yote ya muhimu niliyajua mimi, kuanzia malazi, mavazi, chakula, ada, matibabu nk. ikabidi sasa mama yake ajuwe kila kitu kuwa kwa sasa mimi ndiye niko na mwanaye na ndiye ninaye msomesha na kumhudimia kwa kila kitu.. Niliendelea vizuri na kazi huku Ramla akiendelea vizuri na masomo, mapenzi yetu yalinawirika ipaswavyo na hatimaye tukaanza kufanya mazungumzo ya uchumba, kwa tulivyopendana hakukuwa na pingamizi baina yetu. Nikapeleka kwao Barua ya Uchumba ili akimaliza chuo tu nimuoe, Wazazi wangu wakaniwakilisha na kuzifanya familia zetu kutambuana zaidi..
Nikawa sasa namuhudumia mpaka na mama mkwe pindi apatwapo na matatizo maana ulevi wa penzi umeshanikolea. nashukuru Mungu Mama mkwe aliniheshimu na kunithamini sana.. japo Ramla alikuwa anenda kwa mama yake mdogo kumtembelea lakini ilikuwa ni mara mojamoja sana kutokana na tahadhari alizosomewa na mama yake mzazi.
Hivyo ndivyo nilivyokutana na Ramla. Kumbukumbu hizo nzuri zimegeuka hisia za uchungu moyoni mwangu!
*****
Wakati nikiwa katikati ya mazungumzo na Ntahondi mle ndani ya chumba cha mateso ghafla mlango ukafunguliwa kwa kasi kisha akiingi Mtu mmoja mnene… bila Shaka alikuwa nd’o PabIo Mwaki kwa jinsi alivyo, mimi sikua nikimjua kwa sura zaidi ya kumjua kwa sifa zake tu
Baada ya mlango ule kufunguliwa kwa kasi aliingia kijana mmoja Mnene mweupe. hakuwa mrefu san, niliendelea kumtathimini jamaa Yule huku nikiamini kuwa ndiye Pablo Mwaki.. Tajiri aliyeamuwa kuvunja penzi langu kwa Ramla kwa kutumia Ukwasi awake… na hatimaye kuniteka na kuidhinisha niteswe sana kabla ya kuuawa. Baada ya Njemba ile kusogea mpaka pale chini tulipokuwa tumekaa tukijaribu kuwaza na kuwazua njia ya kujiokoa, Aliuliza kwa sauti kali ya kukaripia huku akiniangalia usoni
"We ndiye Naufal?"
"Ndiyo," Nilijibu kwa unyonge
"Ni nani Mwingine zaidi anayejua kuwa ulikuwa na matatizo na Pablo?"
"Hakuna anayejua mkuu."
“Una uhakika?”
“Ndiyo.” baada ya hapo akaja upande wangu wa kushoto Kisha akamuangalia Ntahondi usoni, akamsemesha kwa kejeli na dharau
"Ntahondi.. Mrembo wa IFM" Kisha akauliza "..Ni nani mwingine uliyempa story za Pablo?"
"Hakuna ajuaye." Baada ya maswali hayo jamaa akatoka nje akituacha tukiwa tumepigwa na butwaa huku tukiangaliana,
Nilijua fika kuwa walichotaka kufahamu ni nani mwingine anapaswa kutekwa kabla hajavujisha taarifa zozote zinazoendelea kati yangu na Pablo Ili watakapotuwa watuuwe pamoja.. mambo yao yaendelee kubaki Siri.
Muda mfupi tena waliingia vijana wengine wawili wakiwa na kamba miwao, sura zao zilionesha kila dalili ya utumiaji mkubwa wa mihadarati kwa jinsi zilivyotisha, mmoja mbali ya kuwana ngeo kubwa kwenye ukingo wa jicho lake la kushoto pia alionekana kama aliyevimba usoni, mwenziye alikuwa amenuna tu na kuzidi kuifanya sura yake kuwa kama buti chakavu la mgambo.. Wakaniinua, wakanifunga kamba mikononi na kunining'iniza juu kama mbuzi anaesubiri kuchunwa, muda wote huo Ntahondi alikuwa akiushuhudia mkanda mzima.. alijaribu kutengeneza sura ya huruma lakini haikufua dafu kwa jamaa hawa waionesha japo chembe ya huruma.. Wakamsogelea Ntahondi, naye wakampeleka mpaka pembezoni mwa kitanda cha Simenti ambacho huwa nalalia mimi usiku, pembezoni mwa kitanda hicho kuna kiti maalum ambacho hutumika kutolea mateso kwa Umeme, wakamfunga kisawasawa halafu wakatoka nje. Ntahondi alikuwa akilia kwa kuomboleza na kuhitajia msaada mpaka nami nikajikuta nikitiririsha chozi
Tulikaa katika hali ile ya Sintofahamu huku kila mmoja akiwaza yake juu ya nini tulikuwa tunakuja kufanyiwa… sikutaka kuamini kama nd’o umewadia, nilijipa moyo kuwa hatutauawa muda ulekwakua nilishadokezwa na Ntahondi kuwa tungeuawa siku ya Graduation iliyoandaliwa kufanyika miezi miwili baadaye.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikuwaikiwa naomba dua na sala za kila namna ili Mungu mkuu atutendee muujiza, nilitamani nimalize maombi ya dunia nzima kwa sekunde kadhaa, ilifikia hatua mpaka sasa nikawa nachanganya maombi…Nilijikuta nasoma mpaka dua ya kuchinjia kuku!
Usiombee Matatizo yakufike kooni!
Ghafla akaingia tena yule Bonge aliyekuja kutuhoji maswali pale awali, safari hii akiwa amevalia kikazi zaidi. Bukta ya Jinzi, fulana mchinjo, na raba nyeusi za kichina.viganya vya mikono yake vikiwa ndani ya Gloves huku akiwa ameshika waya maalum kwa ajili ya kutolea adhabu, sindano ndefu sikujua ni ya nini, mawe ya kupimia uzito kwenye mizani, na vifaa vingine vingi ambavyo sikuelewa ni vya nini?, Nilipomtpia jicho Ntahondi maskini alikuwa akilia kwa Uchungu sana.
Njemba ile ikaja usawa wangu na kuniuliza "Umekataa kutaja mtu anayejua kuhusu suala hili huko nje?"
"Siwezi kukudanganya kaka, hakuna anayejua," Nilijibu huku nikitetemeka mwili mzima. Akanitazama kwa sekunde kadhaa kabla hajahamia kwa Ntahondi, naye akamuuliza swali kama aliloniuliza mimi… kilichonishangaza ni ule ujasiri wa Ntahondi pale alipojibu kwa ghadhabu, bil ya uwoga. pengine alikwishakata tamaa ya kuishi
"Tumechoka na mateso yenu.. usiniulize tena maswali yako ya kifedhuli, ni bora mkatua tu" majibu yale yalimkera sana yule njemba mwenye kipara king’aacho kama kama kioo.. akamrukia Ntahondi na kumshushia mvua ya ngumi na mateke mfululizo kama anapigana na mwanaume, nilijisikia uchungu mpaka nikashindwa kustahmili nikajikuta nami napiga kelele, Ntahondi alikuwa akilia kwa sauti ya Uchungu na maumivu, nilishindwa kuendelea kuangalia tukio lile, nikafumba machompaka niliposikia ukimya ndipo nikafumbua na kumwona Ntahondi akiwa ametapakaa damu mwili mzima!
Nkaiona ile Njemba ikihamia kwangu, kila dua iliniruka kichwani.. alipofika hakuuliza, ilikuwa ni adhabu juu ya adhabu, nilichapwa sana na waya mpaka nikatengeneza matuta mwilini mwangu kwa jinsi nilivyo vimbavimba,
Jamaa akachukuwa ile sindano aliyokuja nayo, akanisogelea mpaka karibu yangu, akanishika viganja vya mikono yangu, akaninyoosha vidole kisha akaanza kunichoma na ile sindano kwenye ncha za vodole vyangu na kuizamisha nusu nzima, nililia kama mbuzi, nilikuwa nikiusikia uchungu mpaka kwenye ubongo, aliendelea kufanya hivyo kidole kimoja baada ya kingine.. niliusikia mkojo ukinitoka bila kipingamizi
Kijana huyu aliendelea kunipiga bila ya kunipa mapumziko huku akinisisitiza nitaje mtu anayejua mkasa huu, nililia huku nikijitetea kuwa hakuna anayejua, baada ya kipigo cha muda mrefu kilichoniacha na maumivu makali na majeraha akaniacha na kurejea kwa Ntahondi akaanza kumpa sasa mateso mengine kwa Shoti ya Umeme,
Kelele za Ntahondi almanusra zipasuwe ngoma za masiko yangu, Hakuna aliyemsikia huko nje! nikaanza kupoteza matumaini kama angeweza kustahmili ukali wa mateso yale.. nikajuwa tu angemtaja Mwalimu Honde ambaye bila Shaka ndiye mtu aliyebaki huko uraiyani akijaribu kutupigania.
Akarejea kwangu na kuichomoa ile sindano aliyokuwa ameizamisha katika kidole changu cha kati, nilipiga kelele kali za uchungu.. kisha akaniuliza, “Utaseamaama hautosema?”
“Hakuna ajuwaye kaka, unatutesa bure tu.”
Hakunijibu kitu, akaiweka sawa ile sindano kasha akanisogelea mpaka usoni, akaupeleka mkono wake mpaka jichoni mwangu, akalitanua vizuri jicho langu licha ya jitihada zangu zakulifumba
“Sasa nakutoboa jicho hapahapa, si hautaki kusema eenh?” kwa jinsi alivyonifunga kamba vizuri sikuwa na kipingamizi chochote cha kulinusuru jicho langu.. ikawa kama bahati tu, akaitwa nje, akaniacha na kutoka huku akifuka jasho mwili mzima, Hakurejea!
Dakika kumi baadaye wakaja wale vijana waliotufunga kamba mwanzo, wakatufungua tukiwa hoi bin a’aban, wakatuacha. tulikaa kama saa mbili hivi ndipo wakatuletea chakula kidogo sana na maji. Ugali wa dona na dagaa wenye kila dalili za kuharibika. ikabidi miye nijifanye nimeshiba ili Ntahondi ale peke yake maana chakula kilikuwa kidogo kiasi kwamba kisingemtosha hata mtoto mdogo.. Ntahondi akagoma kula peke yake, tukala hivyohivyo wote wawili. Baada ya hapo tukalala mpaka asubuhi huku ubaridi wa sakafu ukitonesha majeraha mwilini!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mateso yaliendelea kila siku jioni huku tukiambiwa kuwa wangeacha kututesa kama tutawataja japo watu wawili wanaojua habari ile. Tuliteswa tukateseka lakini hatukumtaja mtu!
Siku moja baada ya kukatika kwa takribani wiki moja alikuja yule Baunsa aliyetutesa kila siku na kumchukua Ntahondi.. akaondoka naye, sikujua alikompeleka! Nilibaki na hofu kubwa nikijua kuwa pengine huko ataadhibiwa sana mpaka atatoa taarifa za watu wanaojua sakata hili, na wangeweza hata kumwua hukohuko kama angeendelea na msimamo wa kutotaja, Nikajipa moyo kuwa angerejea tu kwakuwa siku yetu maalum ya kuuawa haijawadia, ikapita saa ya kwanza.. ya pili.. ya tatu..
Ilipofika saa moja na nusu jioni kama bahati vile Ntahondi alirudishwa ikiwa ni takribani saa tatu zimepita tangu waondoke naye.
"Vipi uko salama kweli? nilijua wameenda kukuuwa," nilimuuliza Ntahondi kwa wahka
"Niko salama wangu, miye mwenyewe nilijua sitakukuta tena Thanks God tuko salama." Nikaendelea kumuhoji kilichojiri huko, naye bila ya kusita akaanza kutiririka
"Mwenzangu ni makubwa! now we have to do something, kwa kifupi huyu jamaa kajana mapya… ananitaka kimapenzi na ameniahidi kuwa endapo nitamkubali hatokuwa anatutesa tena na tutapewa chakula kizuri kila siku mimi na wewe.. amesema atajitahidi kutufanyia mpango wa kutoroka humu kabla ya siku ya Graduation ambayo nd’o imepangwa kuwa Pablo Atakuja kutuuwa." Nilijikuta nimeshusha Pumzi nzito nikiwa sina cha kushauri maana kutoroshwa nataka, lakini sitaki binti huyu audhalilishe mwili wake kwa kumpa Rushwa ya penzi mtu asiyemjuwa vema, pengine ni muathirika wa magonjwa mbali mbali ikiwemo Ukimwi, pia inawezekana ni tamaa zake tu za ngono ndizo zinazo mwongo.. na akipata akitakacho tu shurba inaendelea kama kawaida. Lakini sasa hata akikata ataweza hata kubakwa tu!
Mtihani!
Nikiwa bado sijajuwa cha kushauri Ntahondi akendelea kufunguka
"ameniambia kuwa Leo anaenda mjini kuonana na Pablo hivyo ataacha maagizo kwa vijana wake kuwa watupe chakula kizuri na maji katika kipindi chote atakachokuwa hayupo.. atakaa huko mjini kwa muda wa siku tano kisha atarudi hivyo akirudi tu atataka ngono.. kaniambia siku hiyo atakayorudi akifika tu atawaondoa vijana wake wote wataenda huko mbele nasikia kuna mji mdogo, atabaki peke yake hapa akilind.. lngo lake ni kupata nafasi na uhuru wa kufanya mapenzi na mimi.”
Nilichanganyikiwa, mjadala ukawa mkubwa sana tukitafuta suluhu ya jambo hilo, sasa tukiwa katikati ya majadiliano ya nini cha kufanya mlango ukafunguliwa, akaingia mmoja kati ya wale vijana ambao huwa wanatufunga kamba kabla ya kuanza kuteswa. Safari hii aliingia akiwa na Ndoo mbili za maji, akaziweka chini kisha akatoka nje na kurudi na Mfuko mweusi una nguo, viatu, shuka nasbuni ndani yake… akatuamuru tukakaoge, akatuelekeza sehemu ya kuogea. Tukagawana nguo na kwenda kuoga, Sikuamini kinachotokea maana karibu mwezi sasa sijaoga zaidi ya kumwagiwa maji ili nizinduke baada ya kuzimia kutokana na kuzidiwa na kichapo kikali nachopewa mara kwa mara halikadhalika Ntahondi.
Ung’avu wa ngozi zetu ulionekana kwa mbaali baada ya kupata maji, japo nilikuwa na vidonda vilivyotokana na moto niliokuwa nikinguzwa na ule msumari, na Sindano iliyonitoboa ncha za vidole vyangu, baada ya kuoga tukavaa nguo tulizopewa,
Ntahondi alikuwa na upele mwingi usoni na mikononi uliotokana na M’bu waliokuwa wakituuma siku zote tulipokuwa tukilala kwenye simenti hata ya Shuka wala chandarua.
Tukiwa temeketi mle katika chumba cha kifo, akaingia yule kijana, akatuchukuwa na kutupeleka kwenye chumba kingine ambacho walau kilikuwa na dalili ya uhai.. Kilikuwa ni kikubwa kiasi kikiwa na vitanda vidogo viwili vilivyotandikwa vizuri huku vyandarua vikining’ia kwa juu, kabati moja la mbao, na meza moja iliyokuwa na chakula juu,
"Chakula chenu hicho hapo, mkimaliza kula mnaweza kulala, kila mtu kwenye kitanda chake." kisha akatoka zake. Nilibaki nikimtazama Ntahondi kwa macho ya mshangao, naye akinishangaa mimi. walau sasa tulifarijika kiasi kutokana na huduma mpya tulizopewa, sikuwa na furaha sana kwakuwa niliamini kuwa siku tano zijazo itampasa Ntahondi awajibike kuzilipa huduma hizi na sikutaka kabisa kitendo hicho cha kidhalilikifanyike, sikujuwa nitakizuia vipi!
Baada ya Chakula tulipumzika na kisha tukaendelea na majadiliano yetu. Nilitoa ushauri kwa Ntohondi wa nini cha kufanya, kwa asilimia nyingia aliafikiana name
"Huu nd’o muda wetu wa kutoroka… muda wa kuokoa maisha yetu..muda wa kuzipigania nafsi zetu! cha msingi ni kuwa majasiri tu kwa kila hatua. kwakuwa hiyo siku ambayo jamaa anataka ulale naye atakuwa peke yake humu akiwa kama Mlinzi itatupasa tuitumie fursa hiyo kumzidi akili.. tumtie nguvuni sisi na hatimaye tuondoka humu ndani."
"Tutaondokaje? Na tutamwaghaje? Au tutamuwekea sumu?"
"Humu ndani hatuwezi kupata sumu kirahisi hivyo."
"Kwahiyo tutafanyaje?"
"Itabidi kwanza tujuwe Bunduki yake huwa anaiweka wapi ili ukiwa naye kitandani miye n’taingia ghafla na kuichukua.. huwa najua kutumia Bunduki ipasavyo hivyo nikiitia mikononi tu sitamkawiza, nitausambaza Ubongo wake na safari yetu itaanza hapohapo kabla hao wenzie hawajaja, cha msingi ukishaingia naye tu Chumbani hakikisha hammfungi mlango."
"Naufal hiyo ni hatari sana, tunaziweka roho zetu rehani.. una uhakika kuwa unajua kutumia Bunduki kweli?"
"Ondoa shaka, miye zamani nilikuwa naenda Porini kuwinda na kaka yangu, huko nijifundisha kutumia Bunduki za aina nyingi." Ntahondi aliinuka kwa furaha akanisogelea na kunikumbatia kwa wazo zuri nililitoa!
Tukaanza kujiandaa tu na utekelezaji wa mpango kazi!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*******
Siku zilizidi kuyoyoma kuelekea kwenye Graduation, siku ya furaha kwa Ramla, siku ambayo mbali ya kuhitimu masomo yake pia alikuwa akijiandaa kuvishwa pete ya uchumba na Pablo na kupokea zawadi ghaliku ya majonzi na simanzi kwangu na kwa Ntahondi, naam ni siku ya majonzi maana hakuna atakayefurahia kwa ridhaa yake siku yake ya kufa..
Hasira zilinichemka kichwani kila nilipombuka jinsi nilivyokutana na Ramla kwa mara ya kwanza, nikamtoa Tabora na kumleta Jijini Dar Es Salaam… nikikumbuka gharama kubwa nilizokuwa nikizitumia kwa ajili ya kumlipia ada, malazi na Chakula bila ya kusahau jinsi nilivyokuwa nikituma vijisenti vyangu kwa mama yake Mzazi huko Tabora, Leo amenisaliti kisa kapata Mwanaume Tajiri na Maarufu kuliko mimi.. Mama yake nilietegemea angekuwa ndiye kimbilio langu naye kaingiwa na tamaa ya pesa kiasi cha kushabikia usaliti wa mwanaye huku akibariki aolewe tu!
Tangu aondoke yule Baunsa mweupe anayemtaka kimapenzi Ntahondi tuliendelea kuishi chini ya ulinzi mkali wa vijana wake wa kazi japokuwa hali ya mateso kwa sasa haikuwepo tena bila shaka ni kutokana na maelekezo aliyowaachia, Tulikula na kunywa, chakula kizuri tofauti na kile cha awali, Maji ya kunywa na kuoga yalikuwa safi na salama,
Tuliendelea kulala Chumba kimoja mimi na Ntahondi kwa kipindi chote hicho na Tuliitumia ipasavyo nafasi hii kila siku kujipanga kisawasawa juu ya kuutekeleza mpango wetu wa kutoroka, Kila mara tulijikumbusha mipango hiyo ili kuwekana imara kifikra, tulihisi hiyo ndiyo njia pekee ya kutuokoa.
Ilikuwa ni kitu kigeni kwa mtoto wa kiume kulala chumba kimoja na mtoto wa kike.. tenaaliyeumbika kisawasawa halafu asipate hisia na mihemko ya kimapenzi, lakini kwetu iliwezekana, hakuna aliyejishughulisha kuwaza mapenzi, ukizingatia ndiyo yaliyotufikisha pale! kila mmoja alikuwa busy akiumiza kichwa namna ya kujiokoa ukizingatia siku za Jamaa kurudi zilikuwa zimekaribia.
Siku tano zilitimu tangu Njemba ile iende mjini kuonana na Pablo, sasa tukawa tayari tukijuwa siku hiyo ilikuwa nd’o siku tuliyokuwa tukiisubiri. Ntahondi alijitahidi kujiweka katika hali ya Urembo ili kuzidi kumchanganya jamaa atakaporejea japokuwa hakua katika kiwango kile cha IFMKutokana na hali ya mazingira tuliyokumbana nayo
Tuliendelea kumsubiri yule Baunsa bila mafanikio ya kumwona, usiku ukaingia , matumaini yakakatika, Tukaingia kulala tukiwa na kiu ya kuutekeleza mpango wetu.
Tulilala mpaka asubuhi tuliposhtushwa na sauti za watu waliokuwa wakiongea na kucheka kwa sauti nje ya Mjengo ule uliojaa kila hali ya kutisha na kuogofya, Nilijaribu kutulia na kuelekeza masikio yangu huko nje kujua kinachowafurahisha ndipo nilipoing’amua sauti ya Yule Baunsa, alikuwa amerejea na bila shaka alikuwa akipokelewa na vijana wake baada ya kuwasili, nikainuka taratibu na kwenda mpaka katika kitanda cha Ntahondi, nikamuamsha na kumpa taarifa za ujio wa Jamaa ili awe tayari kukabiliana naye, kisha nikarudi kitandani kwangu na kujifunika shuka halafu nikatulia kama vile niko katika usingizi mzito.
Hazikupita hata dakika tano nikasikia mlango wa Chumbani kwetu ukifunguliwa, hatukuwa tukiufunga! niliendelea kujifanya nimelala, kisha nikamsikia Yule Baunsa akimwamsha Ntahondi
"Enhee hujambo binti?”
“Sijambo.”
“Unalala mpaka saa hizi?”
"..Nilikuwa nimeshaamka ila usingizi ukanipitia tena."
"Vipi hakuna mtu yeyete aliyekusumbueni tangu nilipoondoka?"
"Hakuna aliyetusumbua, nashukuru." Ntahondi kwa sauti laini ya mahaba alikuwa akijibu, niliisikia sauti yake ikipenya kwenye shuka zangu mpaka kuyavamia masikio yangu
"Usiogope, sema kama mlipata tabu yoyote, hawa ni vijana walio chini yangu hawapaswi kukiuka maagizo yoyote nayotoa mimi." Jamaa aliendelea kujizolea sifa lukuki kutoka kwa Ntanhondi, wakati huo miye nikiwa bado nimejifunika shuka yangu halafu nimetulia tuli.
Baada ya mazungumzo hayo mafupi jamaa akaanza kutoka mle chumbani huku akimwambia Ntahondi amfwate, akainuka wakaanza kutoka nje, nikamsikia jamaa
"Huyu Bwege naye kalala tu kama yuko kwa baba yake humu." Baunsa aliuliza kwa dhihaka, ailkuwa akimaanisha mimi, nilitulia kama siwasikii vile mpaka walipotoka,
Sikujua wamekwenda wapi!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nami nikamka ili niwe tayari kwa lolote, nilikaa kama dakika Ishirini bila kupata hata dalili ya kinachoendelea huko nje.. kwa mbali nikasikia sauti za nyayo zikicharaza sakafu na kuja usawa wa mle chumbani kwetu, nikajiegesha ukutani nikijifanya kama nd’o nimetoka kuamka. Mlango ukafunguliwa na akaingia Ntahondi, mkoni ameshika sahani yenye Mkate uliopakwa Blueband na jam na mkono mwingine amebeba kikombe kikubwa cha chai ya maziwa. akanisogelea huku akiwa na tabasamu, akanikabidhi kifungua kinywa hicho nikakipokea
"Imekuaje huko?" Nilimdodosa
"Jamaa kanipeleka hadi chumbani kwake anakolala, akaniletea chai, mayai, na mkate.. wakati nakunywa akaanza kuniuliza kama nimeafiki suala lake, na miye kwa mapozi nikamkubalia, hakika kuna wanaume wanatamaa ya Ngono kuliko maelezo, Eti ndani ya Dakika tano tu nimeishaitwa majina yote mazuri mara baby, sweat, dearMweeh! tumekubaliana kua Leo jioni wale vijana wake wataondoka na kwenda mitaa ya mbele huko kuna center ya kijiji. atabaki yeye tu kama mlinzi kwahiyo nitaenda kulala naye Chumbani kwake." baada ya maelezo hayo tukaanza sasa kuboresha mipango yetu upya na kwa uhakika. Kilichozidi kunifariji ni maneno ya kijasiri na kishujaa ambayo ki ukweli sikutegea kuyasikia yakitoka kinywani mwa mtoto wa kike tena mdogo kama huyu,
"Huu ni mpambano wa kuokoa roho zetu ikibidi hata kwa kutoa roho ya yeyote atakayekuwa mbele yetu hivyo inabidi tuwe makini, tuna asilimia tisini na tisa ya kufanikiwa kutoroka mpaka sasa ila pia tuna asilimia moja tu ya kushindwa kutekeleza mpango huu hivyo tusiiruhusu asilimia hii ikazizidi asilimia zote za ushindi." Ntahondi alikuwa akiongea kwa maneno makali huku akionesha kujiamini, Akaendelea "…Nilipoingia chumbani kwake nimemuona akiwa na bunduki mbili, moja kubwa akiwa kaining'iniza juu ya kiti aina ya office chair kilichopo karibu na kitanda, nyingine ni Ndogo Bastola ameining'iniza usawa wa kiunoni kwenye suruali yake.. hivyo nikiwa naye chumbani we tayaritayari, kwakua huyu Shetani anaonesha ni mtu wa tamaa ya mapenzi mie nitamlaghai mpaka nihakikishe amelainika kama mgonjwa wa degedege, ukisikia tu nakohoa kwa sauti kubwa ujue picha iko tayari hapohapo usichelewe uje fasta mlango sitaufunga nitauegesha tu hivyo ukifika we unaingia moja kwa moja,ukachelewa utakuta nimeliwa." nilikuwa nikimsikiliza kwa makini mdada huyu akiwa hana hata chembe ya woga usoni mwake, nikamuuliza
"Sasa vipi kwa bahati mbaya nikishaingia halafu hizo bunduki nisizione?"
"Mimi kwakuwa nitakuwa humohumo chumbani nitakuwa namwangalia anavyoweka kila kitu hivyo kama asipoweka maeneo hayo nilipoziona mwanzo nitaona ameweka wapi.. nitakupa Ishara ya haraka mahali zilipo halafu wewe utaenda moja kwa moja kuchukua. ukishaichukua usichelewe. We mfyatue tu."
Tulipanga kila kitu mpaka mwisho tukawa tumekaa tu tunasisitizana na kufanya marejeo.
Hatimaye muda ukafika, ilikuwa majira ya saa moja magharibi. hali ilikuwa tulivu kabisa na giza lilikuwa limeanza kutinga kwa kasi bila shaka ni kutokana mazingira ya mle msituni, tukiwa chumbani kupitia katika madirisha yaliyofunikwa na pazia jepesi tuliwaona wale vijana wawili wakitokome.. tukajiweka sawa na tayari kukabiliana na Ibilisi huyu aliyebakia,
Tuliendelea kukaa mle ndani kwa muda mrefu tu mpaka ilipotimu majira ya kama saa tatu kasoro usiku tukasikia mlango wa chumbani kwetu ukifunguliwa, akaaingi kijana mmoja akiwa na Bunduki yake mkononi
"Bosi anakuita chumbani kwake." Nilishangaa kuona kumbe bado kuna mtu mwingine humu ndani
"Okay naja," alijibu Ntahondi kisha kijana yule akatoka, ile hali ilimshtua hata Ntahondi, naye aliamini kua hakukuwa na mtu mwingine yeyote ndani ya mjengo ule lakini sasa dalili sio nzuri kumbe kuna huyu kijana alieyonekana ni Mlinzi pia, Ntahondi akasimama huku akiwa na mfadhaiko usoni, nikampa moyo
"Nenda, fanya kama tulivyokubaliana, kuhusu huyu kijana ondoa Shaka tutajua namna ya kumkabili ila mipango yote ni kama tulivyopanga." Ntahondi alitikisa kichwa kuashiria ameafiki Kisha akatoka na kwenda chumbani kwa Baunsa.
Kadri muda ulivyozidi kwenda niliendelea kupata nguvu ya kupambana, japo kibinaadamu mapigo ya moyo hayakuacha kucheza sarakasi, jasho jembamba liliendelea kunitiririka mwilini, kilichozidi kunitia hofu ni hali ile ya ukimya, sikusikia Sauti ya Ntahondi akikohoa kama tulivyokubaliana na sasa imeshakua takribani saa moja tangu aende kule chumbani alikoitwa, nilipojaribu kuchungulia nje usawa wa getini japo ilikuwa ni mbali na chumba hiki nilimuona yule kijana mlinzi aliyekuja kumwita Ntahondi, akiwa ameketi kama vile aliyepitiwa na usingizi,
Kumbe ni mlinzi wa getini!
Nikataka kutoka na kwenda huko chumbani aliko Ntahondi lakini kengere ya hatari ikalia kichwani mwangu nikakumbuka jinsi Ntahondi alivyonisisitiza kuwa nisiende mpaka nikimsikia anakohoa kwa nguvu. Nikashusha pumzi na kurudi mpaka kitandani,nikajitupia. Dakika tano, kumi, kumi na tano… Kimya!
Baada ya kama nusu saa tena nikiwa nimejilaza pale kitandani nikamsikia sasa waziwazi Ntahondi akikohoa kwa sauti kubwa kama vile aliyepaliwa na machicha ya nazi. Nikasimama haraka, nikaenda mpaka dirishani tena na kumchungulia yule mlinzi kule getini akiwa ameketi vilevile. nikaufungua mlango wa chumba taratibu kisha nikatoka haraka.. Kisu kikiwa mkononi, kisu hiki nilikikuta pale kwenye korido juu ya pipa kubwa la maji,
nikaenda mpaka kwenye chumba cha nne kutoka kile chetu, hapo ndipo walipokuwemo Ntahondi na Huyu haramia, nilipoufikia mlango nikaangaza huku na kule, nikajaribu kuusukum.. Laahaula!
Mlango ulifungwa kwa ndani, Sasa nifanyeje? nikazidi kupata hofu nisijue la kufanya, Nikiwa bado sijajua nifanye nini, kupitia mlangoni hapo nikamsikia Ntahondi akimwambia yule jamaa ampeleke msalani, nikashusha pumzi!Nikaondoka haraka, nikarudi mpaka chumbani kwetu.. nikatulia huku kwa tahadhari nikichungulia kwa jicho moja kupitia kwenye pazia nyepesi aliyokuwa mlangoni.
Haikuchukuwa dakika mbili nikwaona wakitoka chumbani wakielekea upande wa pili wa korido ile ndefu ambako ndiko kuna vyoo,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baunsa akiwa amevaa bukta huku akiwa kidali wazi, na Ramla akiwa amejifunga khanga. walipokatiza tu kuingia maliwatoni mimi sasa nikawa nimejawa na mshawasha wa nguvu nikipiganisha ubongo wangu unipe mwongozo wa nini cha kufanya.. ghafla kama niliyesukumwa nikatoka chumbani na kwenda mpaka koridoni, nikasimama kisha nikaenda mpaka pale mlangoni walipotoka nikaingia mle chumbani wao wakiwa hawajarejea.
Kilikuwa ni chumba cha kawaida tu, kilicho na mwanga hafifu wa taa za kichina, nilijaribu kuyasoma mazingira harakaharaka huku nikipepesa macho huku na kule nikitafuta silaha,
Hamadi!
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment