Simulizi : Kosa
Sehemu Ya Pili (2)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"haya haraka sana fungeni hiyo diary nimewaambia" Ilisikika sauti ya mwanamke kutoka mlangoni ikiwapa amri Hassan na Hussein.
"mama! Umerudi?!"" Wote kwa pamoja waliacha kusoma diary kisha wakamkimbilia mama yao halafu wakamkumbatia huku wakisema, "shikamoo mama".
"marahaba wanangu, wazima nyinyi?" Mams aliitikia salamu halafu akawajulia hali.
"sisi wazima mama, za safari?" Hassan alimuuliza mama yake.
"salama tu, wanangu mnasahau hadi kula hebu twendeni kwanza mkale, saa mbili hii " Mama yao aliwaambia, Hassan na Hussein walishtuka kusikia kuwa muda wa kula umefika tayari. Usomaji wa shajara uliwafanya hata wasitambue kama umeenda kiasi hicho, wote kwa pamoja walitazamana kwa mshangao.
"hivi hiyo diary kawapa nani? Baba yenu?" Mama yao aliwauliza.
"Ndiyo mama" Hussein alijibu.
"haya fungeni mkale mje kuendelea kusoma wanangu wazuri" Mama yao aliwaambia kisha akatoka chumbani kwao.
Hassan na Hussein walimfuata mama yao kuelekea katika ukumbi wa chakula, walimkuta baba yao akiwa tayari yupo mezani akiwa anakula na chakula. Nao walijumuika naye katika chakula hicho wakiwa kimya kuonesha nidhamu ya kula baada ya kumuona mama yupo mezani, kitendo cha mama yao kuchukia maongezi wakati wa kula ndicho kilichopelekea ndicho kilichopelekea mapacha hawa wakae kimya. Hassan na Hussein walikuwa wakila kwa haraka tofauti na ilivyo kawaida yao, jambo hili liligunduliwa hata na mama yao. "hey! Hivi nyie mnakimbizwa?!" Mama yao aliuliza kwa jazba kutokana na kushindwa kuvumilia kuwaangalia wakila namna hiyo, Hassan na Hussein walishindwa kujibu swali hilo na wakabaki wameinamisha vichwa vyao. "si nawauliza nyie, mpo vitani hapa mpaka?! Naona diary ndiyo inawachanganya sio, sasa mkimaliza kula muilete!" Mama yao aliongea kwa ukali akiwa anawatazama usoni kila mmoja. "mke wangu wasemehe....na nyinyi hebu kuleni taratibu" Baba yao aliongea. "hapana Baba Ilham hii sio adabu ya kula yaani hata dini hairuhusu kula namna hii, inabidi niwanyang'anye hiyo diary ili washike akili zao" Mama yao aliongea. "usifanye hivyo mke wangu, nimewapa kwa lengo maalumu na nitakuambia hilo lengo....haya na nyinyi hebu kuweni na adabu ya kula" Baba yao aliongea kumtuliza mke wake kisha akawageukia Hassan na Hussein akawakaripia. Baada ya hapo mlo ulilika kwa taratibu hapo mezani hadi wanamaliza, hali hiyo kidogo ilimfurahisha Mama yao na akawa ameondoa hasira yake aliyokuwa nayo hapo awali. Baada ya kumaliza kula jambo walilokuwa wanaliwaza vichwani mwao ilikuwa ni kwenda kuendelea kusoma shajara, walinawa mikono yao baada ya kula waliondoka ukumbini hapo kuelekea chumbani. Wahka wa kusoma shajara hiyo ndiyo uliokuwa unawasumbua kwa muda huo walikuwa wanaona wanachelewa kwenda kuisoma shajara hiyo, walipofika chumbani kwao waliifungua shajara kwa pupa hadi walipoishia kisha wakaanza kuisoma. ****
"Maneno yake kwangu hayakusikika ingawa yalikuwa yanasikika na watu waliokuwa pembeni yangu, binti huyu alizidi kuongea akijua nipo naye kutokana na macho yangu kutonasuka katika uso wake kama yamenasa na gundi. Akitabasamu kwangu ilikuwa ni ugonjwa tosha hata mapigo ya moyo yakienda mbio muda wote, binti huyu aliongea sana na hatimaye akaniuliza swali ambalo sikulisikia kutokana na kuwa mbali kimawazo. Kitendo cha kutolijibu swali lake kilisababisha anigundue kama sipo naye, aliniuliza swali hilo tena na nikawa sikumjibu kutokana umbali ambao mawazo yangu yako. Binti huyu alipoona sikumjibu swali lake kwa zaidi ya mara mbili na macho yangu yakiwa yanamtazama bila kupepesa hata jicho moja, aliamua kunirudisha kwenye gari hilo kimawazo kwa kunifanyia kitu kilichonirudisha ndani ya gari kimawazo kwa kunipiga kibao cha mkono baada ya kushindwa kupepesa macho hata aliponisogezea vidole vyake karibu na macho yangu. Kibao hicho kilinishtua sana na nikawa kama mtu mwenye hofu asikiapo sauti ya kutisha, kushtuka kwangu kulisababisha huyu binti acheke na hata abiria wengine nao wacheke. Abiria waliokaa upande wa nyuma wote walikuwa wananitazama huku wakicheka, nami nikajikuta nikicheka sana baada ya kushtuka vibaya. "is jy okay(upo sawa)" Binti aliniuliza kwa lugha ya kiafrikaas baada ya kuacha kunicheka. " ek okay(nipo sawa)" Nilimjibu huku nikiwa najihisi nimefanya jambo la aibu kwa kuwa mbali kimawazo. "okay, My naam is Sarina en jou?(sawa, jina langu ni Sarina na wewe?) Aliniuliza swali baada ya kumjibu kama nipo sawa. "my naam is Abdul...Abdulhafidh" Nilijitambulisha baada ya binti huyu kuhitaji utambulisho wangu, hapo ndipo nilitambua kama anaitwa Sarina na jina lake liliendana na urembo wake alionao kabisa. Hakika alikuwa mzuri kama jina lake lilivyo zuri, nilijikuta nikivutiwa na jina lake sana. "befok naam, is jy moslem(jina zuri sana, hivi wewe ni muislamu)?"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alilisifia jina langu kisha akaniuliza. "ja ek moslem(ndiyo mimi ni muislamu) Nilimjibu swali lake, napenda nishukuru tu kwa kupata nafasi ya kuishi katika kijiji ambacho rafiki yangu Jonas alinikaribisha na akanipa hifadhi kama ndugu yake, vinginevyo ningekuwa nababaika sana katika kuongea lugha ya kiafrikaas. Kule ndipo shule yangu ya awali ya kuijua lugha hii na iliyonifanya nisibabaike katika kuongea mbele ya mtoto wa kike, mapigo ya moyo bado yalikuwa yapo juu sana kila muda hasa binti anapozidi kuongea na mimi. "good ek moslem te(vizuri mimi ni muislamu pia)" Sarina aliniambia kwa uchangamfu sana na kunifanya nisahau sehemu ya matatizo yangu yaliyonikuta kwa kipindi hicho, ninavyoongea hivi unaweza kusema labda nimechanganyikiwa kila nilipoliona tabasamu la Sarina au labda nimelogwa na muonekano wake wake. Hali niliyonayo mimi inaweza hata kumkuta mwanaume yoyote rijali na asiye na mtu kama mimi, napenda niseme Mungu kamjaalia kila kizuri na hata kasoro nilikuwa sizioni na nilimuona alikuwa ni mwanadamu aliyekamilika. Uzuri wake Sarina ulinifanya hata nikufuru kwa kumfananisha na malaika waliotukuka katika ufalme wa Muweza wa kila kitu, maongezi baina yetu yaliendelea yakilenga kufahamiana zaidi kwetu sote. Sarina nilikuja kumuelewa kama ni binti mzaliwa wa mataifa tofauti yaani chotara anayefanya kazi huko Widhoek ninapoelekea, baada ya masaa kadhaa gari ilifika Swakopmund ikaweka kituo cha muda mfupi kisha ikaendelea na safari baada ya muda wake wa kuwa hapo kituoni kuisha. Safari yetu iliendelea kwa amani huku maongezi kati yetu yakizidi kuchukua nafasi zaidi, Sarina mchangamfu, Sarina mrembo na Sarina huyuhuyu mwenye kuvutia ndiye aliyenipa furaha kwa mara ya kwanza tangu napatwa na matatizo.
Hadi tunaingia jiji la Widhoek baada ya masaa manne tangu tusafiri, nilianza kuhisi huzuni ikianza kuingia taratibu ndani ya moyo wangu hasa kila nikifikiria kuwa muda mfupi ujao tutatengana gari hiyo itakapofika mwisho wa safari. Tulipofika mwisho wa safari ilitubidi tuagane na kila mmoja ashike njia yake, hapo ndipo ukawa mwisho wa kuongea naye kwa siku hiyo. Moyoni nilijihisi kuumia na nikaona kuwa sitoweza kuonana naye tena ndani ya jiji hili kubwa la nchi hii, niliamua kujikaza kiume nikawa natoka ndani ya kituo cha mabasi cha jiji hilo. " Verskoon my(samahani)" nilisikia sauri ikitokea nyuma yangu iliyonifsnya nigeuke, nilimkuta kijana kashika kasha dogo lenye rangi nyeusu. "is jy Abdul?(wewe ni Abdul)?" Kijana huyo aliniuliza. "ja(ndiyo)" Nilimjibu huku nikiwa nina maswali mengi sana ambayo nilitaka majibu yake, yule kijana alinipatia lile kasha jeusi ambalo nilipolishika nilihisi lina kitu chenye uzito wa wastani ndani yake. Nililipokea lile kasha kisha nikataka kummuliza swali lakini nilijikuta nikijikuta nikisukumwa na kikumbo cha mtu kutoka nyuma yangu hadi nikataka kuanguka, nilipogeuka nilikutana na mtu aliyebeba mabegi mawili makubwa ya kuwekea nguo.
" Jammer!(samahani!)" Yule aliyenipiga kikumbo na mabegi yake aliniomba radhi kwa haraka, nilikubali kumsamehe kisha nikageuka nyuma nilipomuacha yule kijana aliyenipa kasha. Hakika nilikuwa nina maswali mengi sana ambayo yalihitajika kujibiwa na huyo kijana, maswali yangu yaliishia moyoni tu baada ya kutomuona yule kijana mahali nilipomuacha. Nikiwa nafikiria huyu kijana kaondoka muda gani eneo nililomuacha, lile kasha lilianza kutetemeka kisha mlio wa simu ukaanza kusikika ukitoka ndani ya kasha hilo. Nililifungua hilo kasha kwa haraka nikaiona simu ikiita kwa fujo pembeni yake kuna ufunguo wa wenye bango lenye namba 108, niliipokea ile bila hata kufikiria inatoka wapi kutokana na kuchanganywa na matukio yanayonitokea kama vile kujikuta nchini humo na jinsi kijana aliyenipa kasha alivyoondoka bila hata kumuona. "Abdul karibu Widhoek jiji kuu la Namibia, sasa ondoka hapo jirani na mlingoti wa taa za kituo cha basi na uelekee kwenye kituo cha taksi na hapo utakuta teksi nyingi katikati kukiwa kuna gari yenye rangi tofauti na teksi hizo. Panda hiyo gari na utulie kama maji mtungini hadi utakapofika mwisho wa safari yako" Sauti ninayoifahamu ilinipa maelezo ya kitu ambacho ninatakiwa kukifanya, maelezo haya kiukweli yalinishangaza sana kwani anayeongea sauti yake ilikuwa sio ngeni kwangu na alionekana kutambua nilipo. Sikuweza kutambua ananiona vipi lakini akili yangu ilinipa uhakika wa jambo hioo kuwa ninaonekana na mtu anayenichezea mchezo huu, ni kweli nilisimama jirani na nguzo ya taa kwenye kituo cha mabasi na hata aliniambia nitoke eneo hilo nilijikuta nashtuka. Niliirudisha ile simu kwenye kisha nikaenda hadi kwenye kituo cha teksi nilichoelekezwa na nikaikuta gari niliyotajiwa, niliingia ndani ya gari hiyo bila hata kujifikiria nikakuta pembeni yangu kuna suti nadhifu na viatu. Mbele kulikuwa na dereva akiwa yupo kwenye usukani na mkanda kafunga. "vua hayo matambara na uvae hiyo suti na viatu vyake" Dereva wa gari hiyo aliniambia kwa kiswahili fasaha bila hata kuniangalia, nilitii kila alichoniambia na nikavaa suti iliyonifanya nionekane kama nilivyokuwa jijini Dar es salaam nikiwa kwenye kazi zangu.
Dereva huyu alianza kuendesha kwa mwendo wa taratibu kisha akaongeza wa gari baada ya kuingia barabara kubwa, baada ya dakika kadhaa tulikuwa mbele ya hoteli ambayo nilikuwa nimechukua chumba nilipokuja kwa mara ya kwanza ndani ya nchi hii kibiashara na chumba hicho nilikuwa nakifanyia malipo ili nikipata safari ya kibiashara nikija tena nchi hii nifikie hapohapo. Hilton hotel ndiyo hoteli niliyochukua chumba na hadi namba ya chumba nikawa naikumbuka, nilishuka baada ya dereva kunitaka nifanye hivyo nikawa nimebaki nikiwa nashangaa huku lile kashaa likiwa mkononi mwangu. Nilijifikiria kwa muda mfupi kisha nikatoa ufunguo nilioukuta ndani ya lile kasha na nikaitazama namba iliyopo kwenye kibango cha ufunguo huo chenye umbo la kadi ya benki, namba 108 niliiangalia kwa mara ya pili na nikajikuta nikiikumbuka kuwa ni namba ya chumba changu katika hoteli iliyopo mbele yangu na funguo ni yangu. Sikujua ile funguo kaitoa kwani mara ya mwisho ilikuwa nyumbani kwangu katika kabati langu na mwanzo nilishindwa kuitambua kwa sababu ya papara ya kulifungua kasha nililopewa baada ya simu kuita. Kuchanganyikiwa kwa jambo linalonitokea nilianza kukuzoea na hata hapo niliona kawaida, niliondoka kuingia ndani ya hoteli hiyo huku nikipokea salamu za wafanyakazi kutokana na unadhifu wangu hasa nikiwa katija vazi la suti niliyoikuta ndani ya gari.
Nilipita mapokezi katika hoteli hiyo kisha nikaingia kwenye lifti iliyonipeleka hadi ghorofa ya tatu, lifti ilipofika ilijifungua mlango na nikatoka kuelekea chumbani kwangu. Niliingia ndani ya chumba changu kwa amani na nikajikuta natabasamu baada ya kuyafikia mazingira niliyoyakumbuka kwa muda mrefu, nilifunga mlango kisha nikajitupa kitandani ili kulilalia godoro laini kwa mara ya kwanza tangu nilipojikuta ndani ya nchi hii. Ulaini wa godoro nilianza kuusikia ukinipa burudani kwenye mgongo wangu ambao ulikuwa umelala kwenye kitanda kikukuu kwa muda wiki kadhaa, niliona raha ya aina yake kwa kulalia aina ya kitanda nilichokuwa nina hamu nacho kwa muda mrefu. Raha hiyo haikudumu kwa muda mrefu kwani ilikatishwa na mlio wa simu ikiita kwa fujo, hapo niliipokea simu kwa haraka. "naona unastarehe sana ukijisahau una kazi iliyokuleta huku, sasa basi jiandae ukaanze na mwanamke anayeitwa Jasmin muda huu na orodha nyingine ipo kwenye meza ya kioo iliyopo katikati ya masofa" Sauti ile ile iliyonipa amri mwanzo ndiyo iliyotoa maelezo kisha simu ikakatika hapohapo ikiniacha nikiwa sina furaha hasa nilipoifikiria kazi hii ninayoenda kuifanya kwani sikuwa tofauti na malaya anayefanya mapenzi kwa ajili ya pesa. Dola za kimarekani ndiyo zinanifanya niende nikafanye mapenzi na wanawake nisiowajua ili kuzipata katika kipindi hichi cha shida huku ugenini tena nikiwa nachungwa kama vile mfugo. Niliifuata karatasi iliyokuwa kwenye meza ndogo ya kioo nikaitwaa kisha nikaanza kuisoma vizuri, majina yaliyokuwa kwenye ile barua hayakuwa tofauti na haya yaliyokuwa humu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jasmin Peterson nyumba namba 14 mtaa wa R.Van der walt, ndiyo nililotakiwa kulianza katika orodha hiyo. Nilipomaliza kulisoma sikuwa na muda wa kupoteza kuanzia hapo na ilinibidi niondoke muda huohuo kuelekea nilipoelekezwa na karatasi ile, nilishuka hadi chini kwa kutumia lifti kisha nikatoka hotelini hapo nikaingia kwenye teksi moja niliyoikuta ipo pembeni ya hoteli hiyo. "R.Van der walt street house number 14(mtaa wa R.Van der wailt nyumba number 14)" nilimuambia dereva wa teksi niliyopanda ambaye hakuongea lolote zaidi ya kuitikia kwa kichwa kisha akaweka gia na kuachia breki, gari iliondoka hotelini kwa mwendo wa wastani kuelekea nilipomuelekeza. Baada ya dakika kumi gari ilikuwa imeshafika jirani na nyumba niliyoelekezwa, nilimlipa dereva ujira wake kisha nikasogea hadi mbele ya geti la nyumba namba kumi na nne ambayo ni ya kifahari sana. Pembeni ya geti kubwa la nyumba hiyo kulikuwa kuna geti dogo la kupitia watu ambalo ndiyo nililolisogelea nikiwa nina wasiwasi sana kutokana na ugeni wa kazi hii niliyopewa, mlango wa geti dogo ulifunguka baada ya mimi kufika karibu na mlinzi mwenye nguo zilizofanana na askari ndiyo alikuwa mbele yangu na begani ana bunduki nzito sana. "welcome sir(karibu mzee)" Mlinzi huyu alinikaribisha kwa uchangamfu na alionekana kuutambua ujio wangu, wasiwasi uliniingia ndani ya kichwa changu ingawa nilijikaza kisabuni nisijulikane nina hofu yoyote. Niliingia ndani ya uzio wa nyumba hiyo iliyoonekana ina ulinzi mkubwa sana kutokana na uwepo wa walinzi wengine wenye suti ndani ya jengo la nyumba hiyo, mmojawapo wa walinzi wenye suti aliniongoza hadi ndani ya nyumba hiyo ya kifahari kwenye sebule. "mam your guest(mama mgeni wako" Yule mlinzi niliyeingia naye alimuambia mwanamke mwenye kigauni kifupi cha kulalia niliyemkuta sebuleni hapo. "welcome handsome boy(karibu mvulana mzuri) Yule mwanamke ambaye kwa kukadiria angekuwa na miaka takribani arobaini na ushee alinikaribisha kisha akasimama kunifuata, alinikumbatia kisha akanibusu linaloitwa busu la kifaransa mlinzi wake akiwa pembeni.
Aliporidhika kunibusu alimuangalia mlinzi aliyekuwa kasimama pembeni yake halafu akamkaripia,"you bloody fucking what are you waiting for , get out!". "ok mam(sawa mama)" Mlinzi aliitikia kwa utiifu kisha akatoka nje akatuacha tukiwa wawili katika sebule hiyo na hakuwa na kufanya zaidi ya kutii amri aliyopewa na bosi iliyo na matusi mazito juu yake. Huyu mwanamke ambaye nilimtambua kama Jasmin alianza mambo yake papo hapo na mimi ikanibidi nitimize wajibu ulionileta hapo kwa mbinu zote ninazozijua, baada ya masaa matatu nilikuwa nimemaliza nusu ya kazi yangu iliyonileta ambayo niliifanya kwa msukumo tu. Kitendo cha kufanya mapenzi na mwanamke nisiyemjua kwangu niliona ni kazi ya kujidhalilisha ingawa tayari nimefanya na sasa ninahitajika nifanye kwa mara nyingine, mtaka cha uvunguni siku zote lazima ainame na huwezi ukachukua cha uvunguni ukiwa umesimama. Pia mtaka waridi sharti avumilie miiba, namaanisha ukitaka jambo lolote zuri kwa njia ya mkato lazima ukubaliane na hali ya kulipata hilo jambo. Binafsi nilikuwa nataka dola milioni moja ili niokoe kampuni yangu kwa muda wa siku kumi hivyo lazima nikubaliane na njia rahisi ya kuipata na masharti yake.
Baada ys kuimaliza nusu ya starehe kwa Jasmin Peterson na nusu ya kazi ya kulazimishwa na mtu nisiyemjua, tulienda katika bafu la kisasa lililopo ndani ya nyumba hiyo ya kifahari. Jambo lingine nisilolitaka ndiyo nilikuwa nalifanya nikiwa ndani ya himaya ya mwanamke huyu mwenye ulinzi kama kiongozi wa nchi, kuoga na mwanamke nisiyempenda wala kumjua ndiyo jambo nisilolitaka lakini ikanibidi nifanye hivyo kwani sikuwa na jinsi. Jasmin mwenyewe alionekana kulifurahia tendo la kuoga na mimi mithili ya mwanamke anayeoga mpenzi wake, majina kadhaa ya kimapenzi aliniita wakati akiusugua mgongo wangu kwa namna ya kuvutia ambayo kwangu sikuiona kama inavutia. Maneno yake ya kimahaba aliyokuwa akiniita humo bafuni humo yalikuwa ni wimbo unaokera ndani ya masikio yangu, ilinibidi tu nijilazimishe tu kutabasamu kila aliponiita jina la kimahaba lakini moyoni nilitamani hata nimpige vichwa vya pua kwa jinsi maneno yake yalivyokuwa yakinikera. Humo bafuni ndipo nilipobaini kwamba usichokipenda hutapenda chochote juu yake, yaani ukiwa humpendi mtu basi hata jambo lolote litakalofanywa na huyo usiompenda utaliona ni karaha hata kama likiwa la kupendeza kwa wengine. Jasmin kwa muonekane ni mwanamke wa kuvutia na mwenye umbo kama msichana ingawa kavuka umri wa kuitwa msichana sasa anaelekea kuitwa mtu mzima, ngozi laini umbo pamoja na sura ya kitoto aliyokuwa nayo bado ilikuwa haikuwa sababu tosha ya kunifanya nifirahie kufanya tendo ambalo wenzangu wa imani tofauti na dini yangu wanaita kuvunja amri ya sita. Maneno haya ninayoyaongea kwa kijana ambaye hana akili timamu anaweza kuniona sipo timamu huku akiiona kama ni bahati kufanikiwa kufaraguana na mwanamke mwenye pesa kama Jasmin, lakini kwangu haikuwa bahati hata kidogo na niliona ni sawa kuwa mtumwa wa ngono kwasababu ya pesa ambayo dola milioni moja ningempatia huyu mtu anayenifanya niwe mtumwa wa ngono kwa ajili ya pesa ambazo ningempatia papo hapo kama ningekuwa na kadi yangu ya benki. Nilikuwa mvumilivu wa kero za kutazama mwili mtupu wa Jasmin tukiwa bafuni akiwa anafanya kila kituko cha kutaka kunitamanisha mimi, tulipomaliza tulienda chumbani kwake na akanifanyia kila jambo analohitaji kufanyiwa mwanaume na mke wake. Chakula kililetwa baada ya sote wawili kuhisi njaa ikishambulia matumbo yetu, tulikula chakula kitamu na kizuri ambacho kwangu hakikuonekana kama kitamu kutokana na vituko vya Jasmin akinifanya kama mume wake. Ilikuwa ni karaha sana kwangu kutokana na kutopendezwa na mambo aliyokuwa ananifanyia hapo mezani, joho la uvumilivu ndiyo niliuvika mtima wangu ili kusitiri hasira isije ikaniletea matatizo ndani ya himaya ya huyu mwanamke mwenye kila jeuri ya pesa. Tulipomaliza kula vyombo vilikuja kutolewa na vijakazi wake wa kike wenye vazi maalum ambao ndiyo mwanzo walileta chakula kwa kitoroli maalum chenye kusukumwa mithili ya kitanda cha hospitali. Maisha ya kifalme ndiyo aliyokuwa anaishi Jasmin katika nyumba yake hiyo ya kifahari na alikuwa ana uwezo wa kumfanya mtu chochote ikiwa tu atamuudhi, muda huo pia ndiyo nilijua kuwa Jasmin si mwanamke mwenye roho ya kawaida yaani ni mwanamke mwenye roho ya chui au simba. Niliyajua haya baada ya kujikaza kisabuni nikamuuliza sababu ya wafanyakazi wake kuwa watiifu namna ile.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"lazima wawe watiifu kwani wakileta ujinga nakata vichwa vyao au kumwaga ubongo wao kwa risasi, hebu angalia pale ukutani" Jasmin aliongea kwa kiswahili fasaha kilichonishangaza sana yaani kama mtu aliyekaa Tanzania kwa muda mrefu huku akinionesha kidole ukutani halafu akabonyeza kitufe kilichopo kitandani mwake. Nilipoangalia ukutani niliona ukuta ukiwa umejigawa katika chumba chake na ndani yake kukiwa na silaha za aina mbalimbali za kivita, hapo ndipo karaha za Jasmin niliziona ni raha na nilimeza mate kwa kihoro hadi nikahisi kama yananikaba kutokana na uoga niliokuwa kila nikimtazama Jasmin aliyekuwa akiongea nilimuona kama akisimulia visa kale. Yaani hata kuuliza swali jingine niliogopa kwa kuhofia angeniona mpelelezi kisha aninyofoe kichwa.
"kila mfanyakazi wangu anatambua kama sipendi mzaha ndiyo maana yule hanithi pale sebuleni nilimpokaripia alitoka nje anajua ningenyofoa koromeo lake kama angeendelea kukaa" Jasmin alizidi kuongea na kunifanya nizidi kuwa kihoro ndani ya moyo wangu, alifunga ile sehemu aliyoifungua kisha akanisogelea halafu akaniambia "nahitaji tena kuondoa baridi iliyovamia ndani ya mwili wangu". Alipoongea maneno hayo akianza kunibusu busu la kifaransa lililochukua dakika kadhaa, mimi nilianza kazi yangu iliyonileta kwa mara ya pili tena safari hii nikija na nguvu mpya baada ya kuona nipo kwenye eneo la hatari sana na sikuhitajika nimkwaze mwanamke huyu. Nilipomaliza wajibu wangu tayari nilikuwa nimechoka na Jasmin naye alikuwa amechoka na usingizi ndiyo ulichukua nafasi yake ndani ya muda huo baada ya kufanya kazi hii nzito tena kwa nguvu za ziada. Ilikuwa ni usiku ambao sikuutambua ni saa ngapi tulipomaliza purukushani za kubadilishana tusichonacho kwa kila mmoja, asubuhi na mapema niliamka baada ya kushtushwa na mlio wa kukokiwa kwa bunduki na nilipofumbua macho nilikutana na bomba mbili za bunduki zikiwa zinanitazama. Nilifikicha vizuri kisha nikafungua macho tena na nikaona vile vile ninaangaliana uso kwa uso na bunduki ya bomba mbili yenye kitako kimoja tu na isiyo na sehemu ya kuning'iniza kibeba risasi maarufu kama magazine, Jasmin ndiye aliyekuwa ameishika bunduki hiyo akiwa na uso usio na mzaha hata kidogo akinitazama machoni. Nilijikuta nikishindwa hata kupepesa jicho kwa uoga na nilikuwa nimekodoa macho mbele huku nikihema kama kifaru mwenye hasira, uoga ulikuwa upo ndani ya nafsi yangu kwa muda huo lakini nilijikuta nikishindwa hata kutetemeka ndani ya eneo hilo kwa kuoneshewa bunduki yenye bomba mbili wakati sikuwahi hata kuoneshewa bastola usoni mwangu. Jasmin kwa kumtazama usoni hakuwa akitania hata kidogo yaani alionekana kumaanisha kile alichodhamiria, nilipoangalia kidole chake cha shahada kilikuwa kwenye kifyatulio kikiminywa taratibu.
'PUU!' Sauti ya mto nilioulalia ndiyo ulinifanya nihisi nimelengwa na risasi na nilipoangalia sehemu ya mto huo nilikuta imepasuliwa kitu ambacho si risasi ya moto, muda huo Jasmin alikuwa akicheka kwa nguvu kisha akaniangukia kifuani mwangu huku akiniambia, "nimependezwa na ujasiri wako, ingekuwa mwingine angezimia kwa kutishiwa bunduki yenye risasi za mpira". Wakati anaongea maneno hayo bado sikuwa na amani ingawa ni kweli nilitambua risasi iliyopiga mto ilikuwa ni ya mpira kutokana na kutokuwa na dalili ya risasi ya moto kupiga mto huo, risasi ambazo hutumiwa na polisi katika kutawanya watu wanaoandamana ndiyo niliyotishiwa hapa na huyu mwanamke anayeona ni sehemu ya utani wa kawaida.
"nimependa ujasiri ulionao na nimetokea kukupenda hivyo nitakulipa mara mbili ya kazi yako" Jasmin aliongea akiwa yupo kifuani mwangu akichezea sehemu ya bustani iliyopo katika kifua changu.
****
"Hussein hebu acha kusinzia unanipa tabu yaani unaniegemea kama umeegemea mto" Hassam aliongea huku akimsukuma Hussein aliyekuwa amemuegemea baada ya kuzidiwa na usingizi, Hussein alishtuka huku akipifa miayo inayoashiria kazidiwa na usingizi na alihitaji kulala na si vinginevyo.
"sasa hivi saa ngapi" Hussein aliuliza huku macho yake yakiwa yanarembua kama mlevi aliyezidiwa na kilevi.
" hebu ngoja niangalie....heh! kumbe saa sita kasoro hii" Hassan aliongea baada ya kuangalia saa ya kwenye simu yake ya mkononi.
" tulale tu maana bi mkubwa ukichekewa kuamka kwake ni kesi" Hussein aliongea huku akiifunga shajara kisha akanyanyuka akaenda kwenda kitanda kingine kilichopo jirani. Usingizi ndiyo ulichukua nafasi kwa kila mmoja kwa muda huo baada ya kugundua kuwa walikuwa wamepitiliza muda wa kulala.
Asubuhi na mapema wote waliamka kwa pamoja na wakaelekea uwanjani kwa ajili ya kufanya mszoezi ya viungo wakiwa pamoja na wenzao wa mtaa wanaoishi, saa mbili asubuhi walirejea nyumbani baada ya mazoezi kuisha. Walienda kusafisha miili yao kisha wakaelekea mezani kupata kifungua kunywa kilichokuwa tayari kimeandaliwa na msaidizi wa kazi nyumbani kwao, walipomaliza kupata kifungua kinywa walielekea moja kwa moja chumbani kwao kwa ajili ya kuisoma shajara kama kawaida yao.
"dah! Ujue kuna wanawake dunia hii wana roho za shetani, si ulimsoma Jasmin jana alivyokuwa anafanya" Hassan aliongea huku akiichukua shajara baada ya kuingia chumbani mwao.
"kama ni mimi haja zote hapohapo bunduki si mchezo wewe hata kama ya mpira isiyoua" Hussein aliongea huku akiketi kitandani kujiandaa kusoma shajara hiyo.
"aisee bunduki ni habari nyingine kabisa halafu mdingi si nilisikia aliwahi kucheza krav maga akiwa mdogo, kwanini asimkalishe huyo mwanamke" Hassan aliongea huku akicheka.
"wewe bunduki si ngumi useme utaijua kuipangua, hebu fungua tuendelee kusoma muda unaenda" Hussein aliongea na Hassan akafungua kitabu ili waendelee kusoma.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
****
Moyo wangu ulipata amani baada ya Jasmin kuonesha dhahiri hakuwa na nia ya kuniua, asubuhi hiyo tulioga kwa pamoja kama ilivyokuwa jana kisha nikavaa nguo zangu nilizoingia nazo hapo awali na Jasmin akavaa nguo yake mojawapo ya gharama iliyopo kwenye kabati la nguo humo chumbani. Jasmin akinipatia bahasha iliyotuna ambayo niliifungua kuihakikidha na nikakuta nimepewa malipo kama aliyoniahidi hapo awali na akanipatia funguo ya gari huku akiniambia, "kwa ajili yako kwa kunifikisha ninapopataka". Niliupokea huo ufunguo kisha nikampokea yeye aliyejileta kwa lengo la kupokea kumbatio kutoka kwangu, busu zito alinipatia kisha akanitoa hadi nje kwenye gari aina ya buggati yenye rangi nyekundu.
"nadhani ufunguo unao" Aliniambia huku akirmlegeza macho yake, niliutoa ule ufunguo alionipatia kisha nikaminya kitufe cha rimoti na gari nayo ikatoa mlio kuashiria mlango upo wazi. Niliingia ndani nikiwa siamini kama nimekabidhiwa gari yenye bei sana kama hiyo kwa kulala na mwanamke kwa usiku mmoja tu pamoja dola laki mbili, niliiwasha gari nayo ikatii amri kisha nikaitia gia halafu nikaiondoa taratibu huku Jasmin akinioneshea ishara ya busu. Nilipotoka ndani ya geti la nyumba hiyo nilifuata barabara ambayo nilipita jana wakati nakuja na teksi hadi hotelini kisha nikaiegesha kwenye maegesho ya hoteli nikaingia ndani hadi chumbani kwangu, nilijitupa kitandani kwangu nikiwa nayafikiria ya siku iliyopita ambayo yalikuwa yanapita kama mkanda wa sinema katika kichwa changu. Tukio la kuwekewa bunduki usoni mwangu pamoja na tukio la kuona zana za kivita ndiyo matukio yaliyokuwa yakipita ndani ya kichwa changu kuliko matukio yote ya siku iliyopita. Ukweli sikutarajia kama nitakutana na mwanamke mwenye roho ya paka kama Jasmin mwenye matani ya ajabu kama jambazi, nilipotoka salama kwenye himaya yake nilibaki nikimshukuru Mungu kwa mara nyingine kuliko ninavyopaswa kumshukuru nikiiona siku mpya nilipolala baada ya kuzini na nikaamka salama. Mawazo hayo yalianza kuniletea usingizi wa mapema ambao haukudumu baada ya simu niliyokabidhiawa kuanza kuita kwa fujo, niliipokea simu hiyo kisha nikatulia kimya kusikiliza maelezo ya huyu anayepiga.
"Abdulhafidh hongera kwa kumaliza wajibu wako umebakisha siku tisa kasoro na unatakiwa ukamilishe dola laki tisa zilizobakia. Sasa huna muda wa kupumzika inabidi uende mtaa wa Diaz nyumba namba 10 kwa mwanamke anayeitwa Daniella raia wa kihispania asiyejua kingereza kiswahili wala kiafrikaas, anajua kihispaniola tu sasa utajijua mwenyewe utaongea naye vipi ila tambua anakusubiri..Pia nilipokuambia ni wanawake wanaokaa mtaa ya wa watu wenye nszo sikumaanisha wanakaa mtaa mmoja nilimaanisha mitaa, una masaa 206 yakukamilisha kazi hii ambayo ni sawa ya siku nane na nusu. Kazi ianze kama unataka kunusuru kampuni yako" Sauti ileile inayonipa amri ndiyo ilisikika ikiniambia tena nikafanye mapenzi kama nagawa dawa kwa wagonjwa, sikuwa na jinsi zaidi ya kukubali kukubali kufanya kazi hiyo. Niliondoka chumbani kwangu kwa haraka hadi nilipoiacha gari niliyokabidhiwa na Jasmin kisha niliiwasha na nikaondoka kwa mwendo wa kasi hotelini hapo nikielekea mtaa wa Diaz kama nilivyoelekezwa na nilikuwa nikitumia ramani ndogo iliyopo ndani ya gari iliyounganishwa na GPS kuniongoza. GPS ambayo kirefu chake ni GLOBAL POSITIONING SYSTEM ni kifaa kinachoonesha mahali ambapo kifaa kingine kilichonganishwa nacho kilipo au kuonesha ramani ya sehemu kwa kutumia mwezi usio wa asili(artifiacial satelite) katika kutafuta mitaa, GPS iliyopo kwenye gari hii niliitumia kutafuta mtaa wa Diaz na pia kunielekeza kwa kufuata barabara ninayoiona kupitia ramani iliyopo kwenye kioo cha kifaa kilichopo ndani ya gari. Baada ya dakika kumi na tano nilifanikiwa kufika hadi kwenye geti la nyumba niliyoekekezwa, mlinzi wa gapo getini alipoliona gari langu hapo alikuja hadi usawa wa kioo cha dereva kisha akanitazama halafu akasema, "welcome sir (karibu mzee)". Alikuwa ni mlinzi mwenye mwili mnene na uliojengeka kimazoezi ambaye alionekana kuutambua ugeni wangu eneo hilo, geti lilifunguliwa nikaingiza gari ndani ya uzio wa nyumba hiyo. Nililifikisha kwenye maegesho kisha nikashuka baada ya kufunguliwa mlango na mlinzi kwa heshima, niliangaza kila sehemu ya nyumba hiyo niliposhuka tu na macho yangu yakatua kwa msichana wa takribani miaka ishirini na tisa au thelathini akiwa amesimama mbele ya walinzi wawili wenye miili mikubwa sana.
"eres bienvenido guapo(unakaribishwa mzuri) " Msichana huyo alikaribisha kwa lugha ya kihispaniola akiwa na tabasamu mwanana kisha akasogelea hadi nilipo halafu akanikumbatia.
"gracius querido(asante mpendwa)" Nilimjibu kutokana na kuifahamu lugha ya kihispaniola kupitia biashara zangu nilizokuwa nikifanya nchi mbalimbali duniani ikiwemo zinazotumia lugha hiyo.
" ¡Vámonos dentro(twende ndani)" Msichana ambaye ana kila sifa ya urembo aliniambia huku akiwa amejilaza kifuani kwangu mbele ya walinzi wake, tulielekea kwenye mlango wa nyumba ya kifahari unafanana na mlango wa kasri la kifalme ambao tayari ulikuwa umefunguliwa na walinzi waliopo mlangoni. Tuliingia ndani ya nyumba hiyo ambayo ni ya kifahari kuzidi hata ya Jasmin, ulinzi uliopo humo ndani ulikuwa mkubwa sana kuliko hata wa rais wa nchi hiyo. Vijana wenye mitutu ya bunduki walikuwa wametapakaa kila kona kuhakikisha usalama wa humo unakuwepo, Muda huo yule msichana alikuwa habanduki katika kifua changu na mkono wake kazungusha sehemu ya chini ya ubavu wangu wa kushoto. Walinzi wote waliinamisha vichwa vyao kila tulipopita kuonesha utiifu wao kwa huyu msichana ambaye alionekana ni bosi wao.
"sentir en casa(jisikie upo nyumbani)" Yule msichana aliniambia huku tukikaa kwenye kochi kwa kupakatana ambapo yeye alikuwa juu mimi chini.
"gracius(asante)" nilimjibu huku nikiwa nimekamata kiuno chake sawia akiwa juu ya mapaja yangu
"delante de Daniella nada imposible sentir en casa querido(mbele ya Daniella hakuna kinachoshindikana jisikia upo nyumbani mpendwa)" Daniella aliniambia kisha akawaambia walinzi wake,"salir(ondoka)".
Walinzi wote walitoka nje baada ya kuinamisha vichwa vyao kuonesha wameridhia amri waliyopewa, tulibaki peke yetu tukiwa huru kuliko ilivyokuwa awali mbele ya walinzi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nafasi ya kubaki wawili mimi pamoja na Daniella ndiyo ilikuwa wasaa mzuri uliompatia uhuru mwanamke huyu wa kihispaniola mwenye kila kigezo cha kuitwa mrembo na wanaume wote wa dunia hii, mwanamke huyu mwenye ngozi laini yenye weupe wa kizungu wenye kupendeza. Daniella huyu kwa mtazamo na hata kwa kukadiria bado alikuwa binti mdogo tu kama nilivyokadiria umri wake hapo awali, mrembo huyu ni mwenye urembo wa asili ukiwa umeongezwa na urembo wa kisasa. Yaani kuuelezea naweza nikamaliza sifa zote za kusifia na bado nikawa sijautendea haki urembo wake, Daniella pamoja na uzuri wake huo bado hakutaka kukaa na mwanaume wa maisha yake na alitaka awatumie kama nguo au jinsi anavyotaka kunitumia mimi. Tukiwa tumekaa hapo kwenye kochi vurugu ndogondogo za kitandani ndiyo zilianzia na Daniella alionesha kweli kuhitaji liwazo la mwili kuliko kitu kingine kwa muda huo, alifanya kila aina ya uchokozi katika mwili wangu kwa lengo la kuniweka kwenye ulimwengu usio wa kawaida ambao hutumika kuishi viumbe wawili wa jinsia tofauti. Alionekana alikuwa na uhuru wa kufanya chochote katika himaya yake ndiyo maana alikuwa huru sana kuliko kawaida, nilipotaka nikae vizuri ili tuendelee kutokana na kukaa ndivyo sivyo wakati anaanza vurugu zake niliambulia mkwara mzito akidai nisimakatishe starehe yake. Kwakweli ilinidi nijibu mapigo nikiwa nimekaa ndivyo hapo kwenye kochi na akiwa amenikalia juu huku akishambulia kifua changu baada ya kuvuta shati langu kwa nguvu hadi akakata vifungo vyake. Suruali yangu nayo ilikuwa imevutwa hadi ikawa imeharibiwa zipu na kishikizo cha juu, kiukweli nilikuwa sina cha kufanya nilibaki nikijibu mapigo huku nikiziangalia nguo zangu ambazo nimeingia nazo hapo ndani. Kila nilipozidi kumfanyia utundu binti huyu ndivyo alivyozidi kufanya vituko kama aliyepandwa na wazimu, nguo zake alizozivaa pia alizichana moja baada ya nyingine nikizidi kumfanyia utundi wangu. Nilipoanza kazi iliyonileta hadi namaliza tayari nilikuwa na alama za meno na kucha mgongo na begani kwangu, Daniella alifanya yote hayo baada ya kuzidiwa na raha ya ulimwengu mwingine wa wawili wawili. Baada ya kumaliza kazi hiyo yeye alibaki akihema mithili ya mkimbia mbio ndefu huku akinitazama kwa macho malegevu, hakutambua muda huo kama alikuwa kaniparua na kucha wala kuning'ata na meno.
"gracius guapo(asante mzuri)" Alitoa shukrani huku akijiinua kivivu kutokana na shughuli iliyoisha muda mfupi uliopita, aliniinua na mimi kwa kunivuta mkono kisha tukapanda ngazi za kuelekea ghorofani hadi sehemu yenye sebule ndogo pamoja na ukumbi mwembamba mrefu unaotenganisha vyumba vilivyopo jirani na sebule hiyo ndogo. Akiwa anatembea kwa mwendo wa madaha bila hata kuwa na nguo yoyote mwilini kutokana na kuchana nguo zake wakati tunaanza shughuli, aliingia moja kwa moja katika mlango mmojawapo uliopo jirani na ukumbi mwembamba unaotenganisha vyumba. Mimi nikiwa kama kondoo anayekwenda machinjioni bila kujijua niliamua kumfuata tu hadi anaingia kwenye chumba hicho, nilipoingia nikiwa nyuma yake niliona mandhari nzuri ya chumba cha kulala ikiwa na vitu vyote muhimu. Daniella aliniongoza kukipita chumba hicho na tikaingia kwenye mlango wa kioo ulipo pembeni ya chumba hicho ambao nilikuja kuutambua ni bafu la kisasa, huko tulioga kwa pamoja na baada ya kumaliza tukatoka hadi kwenye chumba tulichokipita huku uchokozi wa kimahaba ukiendelea kama kawaida na Daniella akiwa ameniachia uhuru kuliko ilivyokuwa awali. Shughuli iliyokuwa imeishia mapumziko hapo awali ilianza tena kwa kasi ya ajabu, nikiwa na nguvu baada ya kuumwagia mwili maji na hadi tunamaliza kila mtu alikuwa kachoka na usingizi ndiyo uliochukua nafasi yake kutokana uchovu niliokuwa nao. Sikutambua kinachoendelea hadi pale niliposhtuliwa na kitu chenye ncha kali kikiwa kimegusa shingo yangu, nilipofumbua macho nilikuta panga kali sana likiwa shingoni mwangu. Nilishtuka sana nilipoliona panga hilo tena likiwa limeshikwa na mwanaume mzungu mwenye mwili mkubwa sana alivaa suti nadhifu sana.
"so you slept with my fiancee, you have to die. Son of bitch(kwahiyo umetembea na mchumba wangu, unatakiwa ufe. Mtoto wa mbwa)" Mwanaume huyu aliongea akiwa hana hata chembe ya mzaha usoni mwake na nyuma yake Daniella alikuwepo akiwa tayari amevaa nguo na alikuwa ameshikiliwa na watu weusi wenye suti nyeusi akiwa anatetemeka.
"You son of bitch I'll cut your throat(wewe mtoto wa mbwa nitakata koromeo lako)" Yule mwanaume huku akinyanyua panga juu ili atimize azma yake, kiukweli nilikuwa sina la kufanya zaidi ya kufumba macho ili nisishuhudie damu zangu zikiruka.
" mi amor(mpenzi wangu)" Daniella alimuita huyu mwanaume huku akitokwa na machozi
"shut up bitch and close your dustbin otherwise I'll your throat(nyamaza mbwa jike na ufunge pipa lako la taka vinginevyo nitakata koo lako) Yule mwanaume aliongea akimuangalia Daniella huku mkono wake alioshika kisu ukiwa umeshikilia kisu kikiwa usawa wa koo langu. Hakutambua kama alikuwa amefanya kosa kubwa sana kumuangalia Daniella muda ule, akili zangu zikarudi kipindi cha nyuma nilipokuwa najifunza mchezo hatari wa kiyahudi uitwao Krav maga ambao hutumiwa sana na wanajeshi wa israel. Mbinu zote nilizofundishwa na rafiki wa babu yangu ambaye alikuwa mwanajeshi mstaafu wa Israel ndiyo zilinijia kichwani katika muda huo wa hatari mbele ya mwanaume huyu wa shoka. Sikutaka kusubiri ageuke wakati anamuamkaripia Daniella, hapohapo niljivuta pembeni kwa kasi kisha nikaudaka mkono alioshika panga nikaupinda kwa haraka hadi akaacha ukelele na panga likawa limemtoka mkononi. Nilimpiga pigo hafifu la nyuma kisogo akawa ametulia kama maji mtungini, wale wapambe waliomshikilia Daniella walipoona nimeshachafua usalama walikuja kwa kasi lakini waliambulia kipigo kizito kutoka kwangu hadi wakazirai. Nilipowamaliza wote nilitazama Daniella kwa macho makali ingawa aliishia kutabasamu tu huku akianza kupiga makofi nilipoanza kumtazama, milango ya kabati la nguo lililopo humo ndanj lilifunguliwa na mtu mweusi mwenye kimo kirefu alitoka ndani ya kabati akiwa ameshika kamera ndogo na mkoba mdogo.
"Hero You deserve to get our Madam's money for your work(Shujaa unastahili kupata pesa za bosi wetu kwa kazi yako)" aliongea yule mtu akinipatia mkoba alioushika, Niliupokea ule mkoba kisha nikaufungua na nikabaki nimekodoa macho kwa nilichokiona.
"you suppose to get 200000 us dollars but madam gave you 800000 us dollars for your work(ulitakiwa upate dola 200000 za kimarekani lakini Madam amekupa dola 800000 kwa kwa kazi yako) Aliongea yule mtu huku na kunifanya nijione nipo ndotoni kwa kuweza kukalimisha dola milioni moja kwa kulala na wanawake wawili tu badala ya kulala na wanawake kumi kama nilivyoambiwa. Nilizipokea zile pesa kisha nikapokea nguo mpya za kisasa zilizokuwa ndani ya kabati, muda wote huo Daniella alikuwa anatabasamu baada ya kushuhudia vurugu nililolianzisha pale kitandani kwa wale watu ambao hadi muda huo nilikuwa nimeshatambua kama walikuwa wametumwa waje wanifanyie jaribio hatari.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"everyman who fail this test he suppose to die and not to get money for his work. Congratulation for saving yourself, this is your staff(kila mwanaume anayeshindwa jaribio hili anatakiwa afe na si kupata pesa kwa kazi yake. Hongera kwa kuiokoa nafsi yako, hivi ni vitu vyako) Aliongea yule mwanaume huku akinipa pesa zangu , funguo ya gari pamoja na simu iliyokuwa. Nilivipokea vitu hivi ambavyo vilikuwa vipo kwenye nguo zangu nilizokuja nazo kisha nikapokea busu zito la Daniella aliyekuwa amesogea karibu yangu muda huo, nilitoka humo chumbani nikiwa nimeshika mkoba mkono mmoja na mkono mwingine ukiwa kiunoni kwa Daniella, yule mwanaume ambaye alinikabidhi mkoba akiwa yupo nyuma yetu akitufuata. Tulienda hadi nje kwenye maegesho kisha nikaingia kwenye gari niliyokuja nayo baada ya kuagana na Daniella, niliondoa gari kwa mwendo wa kasi nikifuata uelekeo wa hotelini nilipochukua chumba. Namshukuru mungu niifika hotelini kisha hadi katika maegesho ya hotelini hapo, niliegesha gari kisha nikashuka nikiwa na mkoba niliopewa na Daniella. Niliamua kutembea kuelekea ndani lakini nilisita baada ya kusikia sauti ikiita jina langu ikitokea nyuma yangu, nilipogeuka nilimkuta mwanamke aliyevaa shungi la rangi ya kijani na nikabu kwenye uso iliyomfanyia sura yake isionekane hata kidogo. Mwanamke huyu alinikimbilia kisha akanikumbatia akiniacha nimebaki njia panda kutokana na kutomtambua.
Mwanamke huyu alionesha kunitambua kabisa kutokana na jinsi alivyoanza kunichangamkia
"Hoe gaan dit(uhali gani)?" alinijulia hali kwa sauti yake nyororo yenye hadhi ya kumfanya kiziwi aweke umakini ingawa hawezi kusikia kabisa.
" Goed, dankie. wat gaan dit(sijambo, asante. wewe ni nani?)" Nilimwambia hali yangu ilivyo kama alivyoniuliza kisha nikamuuliza yeye ni nani kutokana na kutouona uso yake zaidi ya kuona macho yake yaliyopakwa wanja kwa namna ya kuvutia, nilipomuuliza hivyo alinyanyua nikabu yake akanipa wasaa wa mimi kuiona sura yake halisi iliyonifanya nishtuke sana kwani sikutegemea kumuona hapo na wala sikutarajia kumuona tena.
"Sarina is jy?!(Sarina ni wewe?)" Nilimuuliza kwa mshangao Sarina baada ya kutorajia kumuona hapo katika muda kama huu, nilijikuta nikimkumbatia bila hata kuelewa ujasiri wa kumkumbatia niliutoa wapi. Sarina naye alinipokea nilipomkumbatia na ikawa tumekumbatiana.
" waar was jy(ulikuwa wapi wewe)?" Nilimuuliza kwa mshangao kutokana na kutomuona kwa siku mbili tu ambazo kwangu niliziona ni miezi.
" Ek was in my huis op Thia stad, in die hotel bly jy ? (nilikuwa nyumbani kwangu katika mji huu, unaishi katika hoteli hii?)" Alinijibu huku uso wake ukiwa umepambwa na tabasamu kisha akaniuliza swali papo hapo.
"ja, kan jy my gas wees? (ndiyo, unaweza kuwa mgeni wangu?)" Nilimjibu kisha nikamuuliza swali lililomfanya ajifikirie huku akipeleka mboni za macho yake pembeni kwa namna inayomfanya azidi kupendeza, halafu akajibu, " seker nie, hoekom nie( hakika, kwanini iwe hapana)". Jibu lake lilinifanya nitabasamu na nikajikuta nimemshika mkono wake kumuongoza hadi ndani. Tulipanda lifti ambayo ilitupeleka hadi ghorofa ambayo ndiyo chumba changu kinapatikana, lifti iliposimama nilimuongoza hadi chumbani kwangu ambapo aliingia bila wasiwasi.
"vyfster kamer, mooi(chumba cha nyota tano, kizuri)" Aliongea alipokuwa anakishangaa chumba changu.
" Jy is welkom om my gas(unakaribishwa mgeni wangu)" Nilimwambia huku nikifanya utiifu wa kumkaribisha ajihisi kama malkia.
"dankie(asante)" Alinishukuru huku akikaa kwenye kochi mojawapo lililopo kwenye chumba hicho.
"Ek herhaal weer, welkom om my nie-permanente
behuising(narudia tena, karibu kwenye makazi yangu yasiyo ya kudumu)" Nilimkaribisha kwa mara ya pili Sarina huku nikimtazama usoni.
"Dankie, ek voel warm binne omdat ek hierdie rokke(asante, nahisi joto nikiwa nipo ndani hasa nikiwa nimevaa vazi hili)" Sarina aliongea huku akivua juba alilovaa na akabaki na nguo nyingine ndani zilimsitiri sehemu za mwili zake ikiacha wazi sehemu ambazo zingeweza kusitiriwa na juba hilo, alitoa kibanio alichokibana katika nywele zake ndefu kisha akaziachia nywele hizo kwa kutikisa kichwa chake. Niliuona uzuri wake ambao ningeamua kuuelezea hapa nisingeumaliza hata kwa karatasi kumi za maandishi ningekuwa sijautendea haki katika kuuelezea, nilibaki nimetoa macho kama kurunzi ya mlinzi wa makontena ya bandari nikimshangaa. Sarina aligundua kama namuangalia kwakuwa nilibaki nikiwa nimesimama bila hata kusogea na ikamlazimu anitazame usoni.
" jy wonder hoekom?(unashangaa nini)" Sarina aliniuliza baada ya kuniona nikiwa namuangalia kama mtu aliyepumbazika ghafla.
"Sarina jy is baie mooi, is die mooiste pêrel(Sarina wewe ni mrembo sana, ni mzuri zaidi ya lulu)" Nilijikuta nikimpa sifa nzuri kutokana na urembo aliokuwa nao Sarina hadi nikamuona ni zaidi ya lulu ipatikanayo baharini kwenye maji yenye kina kirefu, napenda niseme ukweli tu maana uongo dhambi. Nilitokea kumpenda Sarina tangu mara ya kwanza namuona na nilijiapiza laiti ningempata basi yeye ndiye angekuwa mwanamke wa maisha yangu, yaani isingekuwa janga la kuokoa kampuni yangu basi ningekuwa tayari nishatangaza azma yangu kwake ili niweze kumpata.
Nikiwa bado namtazama nilipompa sifa mrembo huyu ambaye aliishia kutabasamu huku kainamisha macho yake chini, simu iliyopo mfukoni mwangu ilianza kuita kwa fujo hadi Sarina akawa ananitazama baada ya kuusikia simu hiyoCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Abdul ontvang oproepe laat(Abdul simu inaita hebu pokea) Sarina aliniambia kwa maneno ya kiafrikaas ambayo sikuyaelewa kabisa kutokana na kutoijua sana lugha hiyo, niliitoa simu hiyo baada ya Sarina kunipa ishara ya kuipokea simu hiyo na mimi nikaipokea halafu nikaiweka sikioni mwangu kisha nikasema, "hallo".
"hongera kwa kupata mtoto anayekuchangamkia namna hiyo Abdul, sasa unatakiwa upeleke mzigo wangu nilipokuelekeza halafu ujiandae kwa kazi mpya ya kuifanya" sauti ya mtu anayenipa amri ya kufanya mambo nisiyoyapenda.
"hivi nimekukosea nini wewe mpaka unifanyie hivi, kama pesa uliyonitajia si ungeniachia nikakupatia kwenye akaunti yangu kuliko kunigeuza malaya wa kiume huku ugenini" Nilimlalamikia huyu mtu nisiyemjua ambaye ananipa kazi nisizozitaka.
"nataka uonje uchungu wa kutafuta pesa uliomkuta mwenzako kwa ajili yako" Sauti ile iliniambia.
"kwaajili yangu? kivipi?" Nilimuuliza baada ya kutojua wala kutoelewa kwanini ananiambia hivyo, muda huo nilikuwa nimeshasahau kama Sarina yupo ndani ya chumba changu tena alikuwa akinishangaa ninavyoongea kiswahili ingawa hakutambua wala kuelewa ninachoongea.
"sina muda wa kujibu maswali yako hayo, cha msingi ni kufuata kila ninachokuambia kama unahitaji mali uzikute kama zilivyo. Ukifanya ujanja wowote tu jua utakuwa umejiumiza mwenyewe na utajuta kwa ulichokifanya, peleka hizo pesa kwenye sanduku la posta la Walvis bay na si vinginevyo ndani ya siku kumi nizikute pesa zangu" Sauti ya mtu ambaye anayenipa amri iliongea ikinipa amri nyingine, baada ya kusikia suala la mimi kusababisha mtu apate uchungu wa kutafuta pesa nilibaki kutomuelewa na hata simu ilivyokatika nilikaa chini bila ya kupenda na matatizo yote niliyopitia tangu nilipojikuta nipo ndani ya nchi hii ndiyo yakanijia kichwani mwangu. Mikono niliweka kichwani kwangu kutokana na kuchanganyikiwa na matatizo haya yanayonipata, nilijiona nipo peke yangu na wala sikuwa nafikiria suala la uwepo wa Sarina eneo hilo. Hatua niliyofikia muda huu ilikuwa ni kuelekea kuwa kichaa kwa jinsi nilivyochanganyikiwa na matatizo yanayonikumba, mawazo yangu yote yalikuwa yamehama nje ya chumba hicho ndani ya muda huo.
" wat is die probleem?(nini tatizo?)" Sauti ya Sarina ilinirudisha ndani ya chumba hicho na nikakumbuka uwepo wake kwa muda huo, niliinamisha uso wangu chini hata baada ya kusikia swali lake . Sarina aliamua kunishika kidevu kisha akaniinua juu uso wangu na nikawa natazamana naye, hapo ndipo nikatambua kama Sarina ametoka kwenye kochi alipokuwa ameketi na sasa yupo mbele yangu.
" Vertel my wat is die probleem?(niambie nini tatizo)" Sarina aliniuliza huku akinishika shavuni kwa mikono yake milaini hadi nikajihisi nimesisimka mpaka kwenye nywele zangu, niliinamisha kichwa changu chini nikihofia kuonekana naongea alinacha kama nilivyoonekana na Jonas kwa mara ya kwanza nilipomueleza matatizo yaliyonikuta. Nikiwa nimeinamisha kichwa changu hivyo mkono laini wa Sarina ulichezea nywele zangu za singa ambazo sikuwa nikizitunza, mwili wote ulinisisimka kwa jinsi alivyokuwa anazichezea nywele zangu.
"Sarina is 'n lang storie te vertel, maar ek het besef ek
het ernstige probleme(Sarina ni hadithi ndefu nikikusimulia ila tambua nina matatizo makubwa)" Nilimuambia Sarina huku nikiangalia juu ya dari kinyonge sana kutokana na matatizo niliyonayo, macho yangu juu ya dari yalivutika ni kitu nilichokiona na nikabaki nikikihakikisha kwa umakini.
"Haa! Dit dwaas(Haa! Pumbavu huyu)" Nilisema kwa hasira huku nikisimama nikiangalia juu ya dari nikiwa nimekunja sura.
Maneno yangu yalimshtua hata Sarina na ikambidi aangalie juu nilipoangalia mimi ili aweze kuona kilichonifanya nipayuke kwa hasira, kamera ndogo sana ya CCTV (Closed Circuit Television) ilikuwa imefumgwa kwa ustadi mkubwa jirani ns taa ya kisasa ya kuning'inia iliyopo humo chumbani. Ufungwaji wa kamera kama hii katika chumba cha hoteli ni kinyume na utaratibu wa sheria za hoteli yoyote ili kuwapa uhuru wateja wao, siku zote kamera za hotelini huwa zinafungwa kwenye ukumbi mwembamba unaotenganisha vyumba vya hoteli na si vyumbani. Sasa hapo ndipo nikaona kuwa nafuatiliwa na mtu ananifanya mimi mtumwa wake kwani kunipa kazi yake haramu, pia nilikumbuka kwa mara ya kwanza nilipoingia humo ndani nilijitupa kitandani na nikapigiwa simu na huyu mtu akitaka nikafanye kazi na si kustarehe. Hapo ndipo nilipopata uhakika kuwa natazamwa na huyu nikiwa humo ndani, mawazo yangu hayo niliyawekea uhakika lakini niliuondoa uhakika huo na jambo la kuwa nafuatiliwa kila hatua yangu hata nje ya hoteli ndiyo lilinijia kutokana matukio kadhaa yaliyonikuta nikiwa nchini Namibia. Kwanza tukio la mimi kuletewa barua kule kijijini kwenye ghuba ya Walvis na tukio la kupigiwa simu pale kwenye kituo cha basi niliposhuka nikitakiwa nitoke kwenye nguzo ya taa, mawazo hayo yalipita kwenye kichwa changu kwa dakika moja tu na dakika iliyofuata nikaweka meza ndogo jirani na eneo ilipo kamera hiyo kisha nikapanda nikaivuta na nikaitoa hapo nikabaini uwepo wa waya mwembamba ambao ulionekana unaelekea kushoto kwangu ukiashiria muwekaji wa hii kamera hayupo mbali na eneo hili. Sarina muda wote alikuwa ananitazama tu bila hata kutambua kipi ninachokifanya, wasiwasi mwingi ulikuwa usoni mwake kwa kila kitendo ninachokifanya hakuelewa zaidi ya kuitazama kamera hiyo. Kamera hii ilionekana kuwekwa na mtu ambaye hayupo mbali na eneo hili na akili yangu ikaniambia niangalie chumba cha kushoto kwangu na si vinginevyo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" is wat(kuna nini)" Sarina aliuliza akiwa na sura ya wasiwasi sana kutokana na mambo niliyokuwa nayafanya muda huo.
" iemand geplaas sommige kameras hierin, en wag
vir my hier( kuna mtu kaweka kamera humu ndani, nisubiri hapa") Nilimwambia Sarina ambaye mwili wake ulikuwa hautulii, Sarina alikubali kwa kutikisa kichwa na mimi nikatoka nje kuelekea kwenye chumba kilichopo kushoto mwa chumba changu kwa haraka sana. Nilipofika kwenye chumba hicho mlango ulifunguliwa na akaonekana kijana mmoja mwenye asili ya kihindi akiwa na haraka sana na aliponiona mimi alionekana kushtuka sana, kitendo cha yeye kuonesha wasiwasi kilinipa asilimia mia kwamba kuna kitu anakijua kinachonihusu ingawa sikutambua ni kitu gani. Sikutaka hata kumpa nafasi ya kufikiria jambo jingins lolote baada ya hapo kwa kuhofia kuzidiwa ujanja naye, nilimpiga teke la tumbo lililomrudisha ndani ya chumba kisha na mimi nikaingia ndani kwa haraka bila hata kuangalia usalama. Huko nilikutana na vijana wawili wenye ngozi nyeusi wakiwa wamekaa kwenye vioo vya tarakilishi zaidi ya moja vikiwa vinaonesha mandhari ya chumba changu kwa kila upande ikionesha kwamba kamera ipo zaidi ya moja mule chumbani. Wale vijana waliokaa kwenye vioo vya tarakilishi waliponiona waliniwahi kwa mapigo mbalimbali ambayo hayanikia kabisa, nilipambana nao kwa nguvu zote hadi nikawanyamazisha kwa muda kisha nikamgeukia yule mhindi ambaye alikuwa kaanguka chini akitoa miguno ya maumivu kutokana na teke zito nililompiga tumboni. Niliukamata ukosi wa nguo yake aliyovaa kisha nikamuinua huku nikimtazama kwa hasira, hasira za mambo ninayofanyiwa zilianza kunipanda kichwani na nikajikuta nimemuachia ngumi mfululizo kisha nikamvuta hadi dirishani. Nilifungua dirisha kisha nikamtoa nje nikamuinamiaha kichwa chini akiwa anatazama eneo la maegesho.
"who sent you(nani kakutuma)?" Nilimuuliza nikiwa sijali makelele aliyoanza kupiga muda huo.
"I don't know him (simjui yeye) simjui kabisa nakuapia" Mhindi huyu aliongea kingereza huku akichanganya kiswahili kutokana na uoga na hapo ndipo nikabaini anajua kiswahili.
"utatumwaje na mtu usiyemjua?" Nilimuuliza huku nikitishia kumuachia ghorofani aanguke.
"napokea emails na simu za ketu lakini simjui zaidi ya kuitambua sauti yake" Mhindi huyu alijibu huku akionesha kwamba ni muoga wa kifo na si mtu mwenye roho, Nilimrudisha juu kisha nikampiga pigo moja la kisogoni akazirai. Nilitoka humo chumbani kwa haraka na nikarejea chumbani kwangu nilipomuacha Sarina, nilipoingia tu nilichukua mkoba wa pesa na vitu vya muhimu kisha nikamshika mkono Sarina nikaondoka naye nje bila hata kusema lolote. Tulishuka hadi mapokezi kisha tukaingia kwenye gari yangu na tukaondoka eneo hilo upesi sana, Sarina alibaki ametulia tu akiwa na wasiwasi mwingi sana. Niliondoa gari kwa kasi sana nikiwa sina uelekeo maalum wa kuelekea kwa dakika takribani kumi na tano hadi nikawa nimeuacha mji mbali kidogo na sasa nikawa nipo katika sehemu tulivu yenye miti mingi pamoja na nyumba chache.
"is jy reg(upo sawa)" Nilimuuliza Sarina huku nikiegesha gari pembeni ya barabara.
"ja , Wat gaan aan?(ndiyo kuna nini kinaendelea)" Sarina aliniuliza huku akiwa na wasiwasi mwingi sana hata akawa anaelekea kuniogopa kwa mambo ninayofanya, niliamua kumsimulia kila kitu kuhusu mimi nikiwa naficha baadhi ya mambo kama vile kutembea na wanawake wawili ambao ni matajiri pamoja na suala langu la kuchukua machangudoa nilikuwa jijini Dar es salaam. Maelezo yangu yalimfanya Sarina ashushe pumzu halafu akanipa pole kwa yaliyonisibu na akaniambia
" dit het gelyk asof niemand is verontreg en nou is
hy het teruggeslaan, is daar iemand wat jy
aanstoot?(inaonekana kuna mtu umemkosea na sasa analipa kisasi, je kuna mtu umemkosea?)". Swali la Sarina lilinifanya nijifikirie sana ili kukumbuka sehemu nilipomkosea mtu lakini mwisho wake sikukumbuka kama nilimkosea mtu kiasi cha huyo mtu kuamua kunifanyia hivi. Ukweli mwanadamu ana kawaida ya kusahau kila kitu na hata kama akifanya jambo baya huweza kusahau kabisa, ndivyo na mimi nikawa nimesahau kama niliwahi kumfanyia ubaya huyu mtu anayenipigia simu kila kitu.
" Nee, ek het nie aanstoot iemand te bereik hierdie
stadium voer(hapana, sijamkosea mtu mpaka afikie hatua ya kunifanyia hivi)" Nilimjibu Sarina huku nikionekana kuchanganyikiwa kabisa na hata gari lenyewe nisingeweza kuendesha.
" maw ek het nêrens om te gaan in hierdie stad (yaani hapa sina hata pa kwenda)" Niliongea kwa unyonge huku mikono nikiwa nimeweka kichwani nikiwa nimeuegemea usukani wa gari, Sarina alikuwa akifanya kazi ya kunifariji huku mikono yake ikiwa inatalii kichwani mwangu hasa kwenye nywele. Nilipoinua uso wangu juu nilimuomba Sarina aendeshe gari kama anaweza, alikubali na mimi nikamuachia usukani akawa ananiongoza kwa kutumia uelekeo nisioujua. Sarina alipita njia mbalimbali za mkato na mwishowe akawa ametokea sehemu nyingine ya mji wa Widhoek ambayo nilikuwa siijui, tulikatisha mitaa kadhaa na hatimaye tukaingia sehemu yenye nyumba nyingi zinazofanana zenye hadhi ya kutumiwa na watu wenye maisha ya kawaida zikiwa na namba kwa kila nyumba. Sarina aliingiza gari kwenye uzio wa nyumba mojawapo na hapo ukawa ndiyo mwisho wa safari yetu, alishuka kwenye gari na mimi nikashuka sambamba naye. Tuliingia ndani ya nyumba hiyo yenye muonekano wa kawaida wenye kuvutia, Sarina alinikaribisha katika nyumba hiyo huku akinifahamisha kuwa ndiyo nyumba yake katika mji huo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alinieleza kuwa ndiyo sehemu ambayo anaishi na ndiyo sehemu aliyokuwa anakaa siku zote katika mji huo, nilipata faraja angalau kidogo kwa kupata sehemu ya kujihifadhi kutokana na tukio langu la kuchafua usalama kule hotelini. Nilijua fika tukio langu la kumpiga teke yule mhindi pale mlangoni litakuwa limeonekana na kamera ya ulinzi iliyopo kwenye ukumbi mwembamba unaotenganisha vyumba pale hotelini, niltamani sana Sarina anikaribishe hapo kwake walau nikae kwa muda kabla hajaniambia nitakuwa niikiishi pale na hata aliponiambia nitakuwa nikiishi pale nilishukuru moyoni. Ukarimu alinionesha Sarina kwa kunipa hifadhi ulinifanya nimshukuru mungu kwasababu yeye ndiyo chanzo cha kukutana na mwanamke mkarimu na mwenye moyo wa kipekee mpaka anafikia kunipa hifadhi mtu kama mimi niliyejuana naye siku mbili zilizopita katika basi dogo litokalo Walvis kuja huku Widhoek, ingekuwa mwanamke mwingine asingejaribu kufanya hivyo hasa kwa mambo niliyokuwa nayafanya pale hotelini. Ukweli alinifanya nimuone ni mwanamke wa kipekee sana hapo nikamlinganisha na Huwaida kwa mara ya pili nikaona kuwa Huwaida halingani naye hata kama wote wangekuwa ni vito vya thamani basi Sarina sngekuwa yupo juu zaidi, nilianza kukumbuka jinsi nilivyomuona Huwaida kwa mara ya kwanza na jinsi nilivyohangaika naye ili kuupata moyo wake lakini nikaukosa.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment