Simulizi : Code X 5 N.g.s.s. (Next Generation Super Soldiers)
Sehemu Ya Tano (5)
***********************************
“Mimi ni kamanda wa kikosi cha TW, adui yupo mita ishirini mbele. Ruhusa ya kuanza mashambulizi” aliongea Talbot. “Ruhusa umepata, over” HQ ilijibu, “Rodger” Talbot aliitika. “Kikosi ngao kitaanza mbele, kitafuatiwa mizinga mizito na ya masafa mafupi na mwisho itakuwa mepesi ya masafa marefu. Jipangeni katika mfumo wa pembe tatu” alitoa amri yake ya kwanza kwa kikosi chake. “Umesomeka mkuu” waliitika kwa pamoja. Sio kama walikuwa sehemu moja wote, laa! Walikuwa maeneo tofauti. Kitika sehemu kulikuwa na gari sita, za mbele mbili zilikuwa na ngao kubwa sana ya chuma. Nyuma yake kila upande zilifata gari mbili za mizinga mizito na katikati zilikuwepo mbili za mizinga mepesi.
“Pembe tatu zimekamilika” waliongea madereva kwa pamoja, “tunaanza mashambulizi ndani ya sekunde tatu, mbili na moja” ilitoka amri kwa msaidizi kamanda Emelda. Mashambulizi yalianza kasi ya ajabu, zile gari zenye ngao zilizilinda gari zinazofanya fanya mashambulizi. Gari za mashambulizi mzito ya masafa mafupi zilishambulia gari za usoni wakati zile za makombora mepesi zilishambulia gari za mbali na usoni. Kila kombora lilivyotuwa ulisikika mtetemeko wa ardhi.
Kambini kwa waasi.
“Mpango unakwenda kama nlivyoupanga” aliongea Matvei akiwa na kikombe cha kahawa mkononi, “unaendaje wakati mashine zetu zinazidi kuangamia” aliuliza Michael ambae alionekana kuchoshwa mchezo anaocheza Matvei. “Kijana tulia, tuachie magwiji wa vita tukupe ushindi” aliongea Alfred Jackson na kumkata jicho kali sana Michael. Isiwe tabu akaamuwa kujamaza na kuwaachia wafanya watakavyojisikia, yeye alitaka ushindi tu. "Matvei mzinga mkubwa upo tayari” alifika Jason CJ na kutoa taarifa, “acha tuwaonyeshe kuwa kutangulia sio kufika” alijibu Matvei na kumuangalia Andrew Cross nae akatikisa kuondoka.
Alifika katika lifti na kupanda kisha akabonyeza kitufe cha kwenda juu mpaka ilipofika ghorofa ya mwisho kabisa juu. Akashuka na kupanda ngazi mbili kisha akawa yupo juu kabisa nje, mbele yake kulikuwa mashine kubwa yenye bomba ndefu sana mithili ya bunduki ya udunguaji aina ya macmillan TAC50. Pembeni kulikuwa na kiti kilichoungana na kompyuta, alikaa kwenye kiti hicho na kuanza kucheza na kompyuta akijaribu kupiga hesabu fulani mpaka alipojridhisha. “Tuone bila sehemu ya kupata amri na maelekezo mtapigana vipi. Kwa lugha nyingine tunawapofuwa macho” aliongea kubonyeza kitufe cha “OK” kwenye kompyuta hiio.
Mtamba ukaanza kujiseti wenyewe mpaka ulipofika ulipotakiwa kukaa, kisha kwa pembeni ukaanza kutembe mkanda mkubwa ulobeba mabomu mengi mithili ya mkanda wa risasi za SMG. “Machine bomb launcher (MBL)” ndilo jina mtambo huwo mkubwa. Kwa kasi ya ajabu mtambo huwo ulianza kufyetuwa mabomu yenye ukubwa futi tano na nusu. Yalisafiri angani kwa kasi sana kuelekea upande ambao kambi kuu BHGP ilikuwepo. Mabomu yaliofyetuliwa yalikuwa mengi mno na yalifatana kama watoto wa bata.
“HQ, mnanisoma. Kuna mvu ya makombora inakuja huko, Over” aliongea Alfred aliekuwa akipambana na lile dege kubwa la kivita. “Over, tunakusoma. Endelea na kazi yako kwa sasa, amri hazijabadilika na kwa vikosi vingine pia” alijibu kamanda Mark. “Rodger” vikosi vyote viliitika kwasababu kila kilichoongewa kilisikika na kila mtu. Mfumo wa ulinzi wa kambi kuu ya BHGP ulijitahidi kuyatunguwa makombora hayo lakini ilikuwa ni vigumu kuyamaliza kutokana na wingi wake. Mengine yalianza kutuwa na kusambaratisha baadhi ya mitambo ya usalama. Na Baada ya muda ilishindwa kabisa na kuruhusu makombora hayo yafike kambi kuu. Sekunde kumi baadae ulisikika mlio mkubwa sana na redio zote zikaingia chenga. “HQ mnanisoma”, kimya. Hakukuwa na jibu lolote.
“Vikosi vyote, tumepoteza mawasiliano na makao, makuu na hatujui nini kimewakuta. Lakini amri ni amri hivyo kila kikosi kitaendelea na amri yake ya mwisho kutoka makao makuu” iliongea sauti ambayo haikusikika kwa muda mrefu sana tokea vita ianze. “Rodger Supreme General” vikosi vyote vikaitika kwa wakati mmoja, ari ya vita ilirudi tena mioyoni mwa wapiganaji wa kikosi BHGP. “Naona mawimbi kwa mawimbi ya wanajeshi yakiingia mitaani” aliongea kamanda Jesca, “wadunguaji, anzeni kazi” alimalizia kwa amri. “Hakikisheni hampotezi risasi, kila risasi ni uhai mmoja” ilisikika sauti ya Ghulamna kuwafanya wote kutabasamu.
Kikosi cha waenda kwa miguu (GW) chini ya kamanda Kelvin Bull (Ghost) na msaidizi kamanda Sweety, kilikuwa kimejficha kwenye majengo na madaraja kwa ajili ya mashambulizi ya kushtukiza. Kikosi cha waasi kilianza kupuputishwa na wadunguaji wengie waliokuwa wamjeficha maeneo kadha wa kadha. “Mbali sana kwenye kiza nimelela, utakuja mlio ambao hutausikia” aliongea Charlie na kucheka, msemo huwo wa wadunguaji ndio uliowapa kiburi cha kuzidi kufanya mahambulizi.
“Nini hiki lakini?” aligaka Matvei kwa hasira, “hawa wapumbavu hawana utu hata kidogo, makao makuu yao yamesambaratishwa lakini wameamshwa kutoka usingizini badala ya kulala” alifoka kwa hasira. “Andrew chukuwa kikosi chako na uwawinde wadunguaji wao” aliongea Alfred Jackson, “rodger” aliitika Andrew na kuondoka na kikosi chake. Kwa umakini wa hali ya juu wakatoka kambini ni kuingia kwenye majumba makubwa kwa ajili ya kufanya kazi. Walinza kutafuta sehemu zilipotoka risasi za wadunguaji pinzani kwa kuangalia upande ambae wenzao walirushwa na risasi.
“Nimewaona, kaskazini thalathini na tano na ishirini na mbili” aliongea mmoja wao, “uweni yeyote atakaengia kwenye darubini zenu” ilitoka amri kwa Cross (Andrew). Risasi ya kwanza iliosafiri kutoka kwa wadunguaji hao iliingia begani kwa msaidizi kamanda Shey na kuusambaratisha mkono wake wa kulia. Ajabu hakupiga hata ukwenzi, alilala chini na kuuma meno kwa nguvu. “Msaidizi kamanda” aliongea mwanajeshi mmoja na kuinuka, akatupwa huko na risasi ilizama kichwani. “Wanajeshi endeleeni na mashambulizi” ilitoka amri kwa msaidizi kamanda aliekuwa akiugulia. “Japo walitaka kumsaidia, lakini amri ni amri na kila mtu akarudisha akili yake vitani.
“LRS unatusoma, kuna wadunguaji wa waasi wameanza mashambulizi” aliongea Jesca, “kamanda msaidizi yuko chini ila hatuwezi kumsaidia kwasasa kwasababu tumewekwa chini ya jicho” aliendelea kuongea. “MRS, rodger. Unasomeka na endeleeni na mashambulizi kama kawaida. Hao wengine tuachieni sisi” aliongea Charlie na kutabasamu tabasamu lililokuwa na harufu ya damu. “Muko tayari kunywa damu za vichwa” aliongea akiashiria kikosi chake. “Ndio chakula chetu” walijibu kwa pamojana sauti zao zilikuwa za barridi. Kufanya kazi na Charlie kuliwabadilisha wengi na kuwapa muonekano wa kinyama zaidi kuliko kibinadamu. Wote walionekana kama Charlie mwenyewe tu, “atakaepasuwa vichwa vingi nitamlipa dola mia mbili kila kichwa” Ghulam aliongezea.
Kauli ikamfanya kila mdunguaji atoke ute na kufikiria kuvunja angalau vichwa mia hivi ili apate dola laki mbili. Wale wawindaji wakageuka wawindwaji, sekunde chache tu baada ya kutoka amri. Walianguka ishirini upande wa Cross, “inavyoonekana wana vikosi viwili vya wadunguaji kwasababu tulokuwa tunawashambulia mwanzo wanaendelea na mashambulizi yao japokuwa tumewaangusha zaidi ya saba” alitoa taarifa mmoja wao. Ghafla pembeni yake alianguka mwanajeshi na hata hajafikria afanye nini kichwa chake kikapasuka.
“Kama una muda wa kuongea kaongee na mungu huko unapoelekea” aliongea Ghulam akiramba midomo yake, kwa mbali ute mwemba sana ulionekana kushuka kutoka mdomoi kwake. Sio yeye tu, Charlie aliekuwa akiichezesha bunduki yake huku na kule na kuikoholesha mara kwa mara. Tabasamu halikuondoka kichwani mwake, “waone hawa jamaa wanavyosikia raha kama mwanaume anaefika kileleni” aliongea mwanajeshi mmoja huku na yeye akitabasamu. Kikosi hicho kwakweli hakikuwa na watu wa kawaida hata kidogo, kilikuwa na wanyama katika ngozi ya binadamu.
Yule aligeuka upande aliokuwa Kelvin, “Supreme general unafanya nini hapa” Kelvin alijikuta akiuliza. “Supreme general ndio nani” aliuliza mtu huyo. “Si wewe Supreme general Alex” alijibu akisimama, ni kweli mtu huyo alionekana kufanana na Alex. “Hapana mimi sio supreme general labda umenifananisha” aliongea mtu huyo na kumpa mkono. “Jina langu ni Alexander Senior” alijitambulisha, badala ya kujibu Kelvin akabaki amekodoa macho tu. Wakati akiendelea kushangaa, ghafla mlango ukafunguliwa. “Tulieni hivyo hivyo, wekeni mikono juu” iliskika sauti na moja kwa moja Kelvin aliitambuwa sauti hiyo. Hakuwa mwengine isipokuwa Jeff na nyuma yake alifuata Alex na Adrian.
“Sisi siyo maadui” aliongea Alexander Sr bila kugeuka, “Kelvin uko sawa” aliuliza Jeff huku akimsogelea. “Niko sawa Chief” Kelvin alijibu akisimama. “Nyie ni kina nani na kwanini mko hapa” sauti nzito kutoka kwa Alex Jr ikasikika na kumfanya Alexander Sr kugeuka. Macho yake yalikutana na ya Alex Jr na wote wawili waksashangaa. “Ni kivipi wewe mzee uko hai, si ushakufa wewe” aliongea Alex Jr, “unamaanisha nini” Alexander Sr aliuliza. “Supreme General huyo unae ongea nae anaitwa Alexander Sr, ndivyo alivyojitambulisha na ndie alienisaidia kabla ya kufika nyie” aliongea Kelvin. Alex akamuangalia vizrui kisha akainuwa mkono wake juu, “vikosi vyote tulieni” akaongea. “Rodger” alijibiwa na vikosi viwili vya wadunguaji vikashusha bunduki zao.
“Nilijuwa tu hamtakuwa pekeenu, ni wabaridi kama ulivyokuwa. Hujabadlika hata kidogo little Vampire” aliongea Alexander Sr na yeye akainuwa mkono juu. “Stand down” aliongea na vikosi vyake vilivyokuwa vimejifika vikaweka silaha chini. “Umelijuaje jina hilo” aliuliza Alex Jr, “Akham! Sikujitambulisha vizuri. Jina langu ni Alexander CJ the first (wa kwanza) au Alex Sr. Nawewe ni Alexender CJ the second (wa pili) au Alex Jr au nikuite kwa jina lako la kuzaliwa, Ethan” aliongea Alex Sr. Alex Jr hakuwa na la kuongea maana hakuhitaji ushahidi mwingine kama huyo alikuwa kaka yake. Kwasababu jina lake la kuzaliwa walilifahamu wanafamilia tu, baba, mama na kaka yake basi. Wengine walimtambuwa kama Junior tu kabla hajachukuwa jina la Alexander.
“Tutaongea zaidi kambini” aliongea Alex Jr na kumpa ishara Jeff waondoke, pia akampa ishara Alex Sr amfuate na bila kipingamizi alikuwabili. Walishuka ghorofa hiyo na kutoka nje kwa umakini wa hali ya juu. Wakiwa wanafuatana taratibu kikosi cha Alex Sr kikaanza kuujitokeza na kuungana nao katika msafara huwo. Baada ya mwendo wa kikakamavu wa dakika kumi, hatimae wakawasili CPc (check point C). “Samahanini kwa kuwaweka gizani” ilisikika sauti ya kike kweye vifa vya mawasiliano, wote waliitambuwa kama sauti hiyo ilikuwa ni ya Brain. “Hii ni HQ mnanisoma” ilifuata sauti ya Mark. “Rodger HQ tunakusoma, alijibu Adrian”.
“Tunahitaji vikosi vyote virudi kambini, kuna mabadiliko ya mipango yamefanyika” aliongea, “lakini kambi imeripuliwa” aliuliza mwanajeshi mmoja. “Soldier, uti wa mgongo hauwezi kuwa lele mama. Kama kambi inaripuliwa mwanzo maana yake vita tumeshindwa. Kambi iko vizuri kabisa na hakuna hata bomu moja lililoingia”. Wote wakashusha pumzi na safari ya kurudi kambini ikaanza, ilikuwa ni njia ya chini ya ardhi kutoka CPc. Nusu saa baadae walikuwa kambini, mwanzo wengi walidhani ni maneno tu ya kuwatia nguvu lakini macho yaliwatoka kukuta kambi iko safi kabisa bila hitilafu yeyote ile.
Talbot alifika pamoja na wanajeshi wengine na kuwachukuwa majeruhi, wakawapeleka katika hospitali iliokuwepo kambini hapo. Sekunde cha alifika Martina akiongozana na Brain pamoja na Mark. Alex Sr alikuwa akimuangalia sana mpaka Martina akaanza kujishuku. “Tumewahi kuonana” alivunja ukimya, “hapana lakini nimewahi kuonana na mtu ambae amefanana na wewe” alijibu Alex Sr na kutabasamu. “Unamaanisha umekutana na pacha wangu?”, “kama ni hivyo, ndio nimekutana nae na niamini kama wewe ungekuwa mwanaume ningekusambaratisha kichwa sasa hivi” aliongea na kuonesha chuki ya wazi kabisa kwa Martin.
Kutajwa kwa jina hilo kukawashtuwa wengi waliokuwa wanamjuwa, ila kabla mshtuko wao haujaondoka “ni macho yangu ama nyie wawili mumefanana” aliongea Brain. Na hapo sasa hata wengine wakatikisa vichwa kuashiria kuungana nae. “Oh nimesahau kabisa kumtambulisho, makomredi huyu ni Alex Sr na ni kaka angu” aliongea Alex Jrna kuwafanya wote wacheke. “Jamani hatuna muda wa kucheka” aliongea Mark na vicheko vikakata. “Vizuri, sasa iko hivi. Tumefanya kama tumeathirika na bomu ili kusudi kumpa mwanya adui yetu acheze karata yake ya muhimu. Japokuwa tumepoteza baadhi ya wenzetu wengi lakini tumefanikiwa kujuwa uwezo wake wa kivita. Mbinu yetu ya kwanza haitafanya kazi kama tulivyokusudia. Na kuendana nae na sisi tutapigana vita nzima kama alivyotaka, na..”.
“Nasikitika kuwambia kuwa hiyo mbinu haitafanya kazi” alikatikazwa Alex Sr, “unamaanisha nini” alihoji Mark. “Kwanza mnapaswa mtabue kuwa mnapambana na mtu mwenye akili sana duniani, mukitaka kushindana nae kwa akili kamwe hamtafanikiwa”. “Umenivutia hapo” aliongea Mark na kukaa vizuri akiwa na kusudi la kumtaka aendelee. “Munaepambana nae anajiita Michael, lakini jina lake halisi ni Martin. Yap! Usitoe macho Martina, ni huyo huyo unaemfikiria. Pacha wako” alitulia kidogo kumuagalia mwamamam huyo ambae tayari umri umeanza kumtupa mkono.
“Haiwezekani, Martin nilimuuwa mwenyewe kwa mikono yangu” alibisha Martina akihisi miguu yake kukosa nguvu na kutaka kuanguka. Mark aliekuwa pembeni yake akamuwahi na kumueka kitako. “inavyoonekana kuna kitu unakijuwa sisi hatukifahamu” aliuliza Jeff na kumuangalia. “Ndio ni vingi tu na hivyo ndio ufunguo wa kushinda vita hii” alijibu. “Tueleze” ilikuwa sauti ya Alex Jr.
**************************************
Alianza kueleza “Martin ama Michael kama munavyomtambuwa nyinyi. Yeye binafsi anaichukulia ndie binadamu mwenye akili zaidi duniani kuliko yeyote. Na ni kweli ulimuuwa kwa mkono wako Martina lakini ulichelewa kidogo. Martin alipatwa na tamaa ya kuitawala dunia milele, na ili kufanikisha hilo alihitaji aishi miaka mingi sana kama sio bila kufa. Hapo ndipo alipoanza safari ya kuchunguza namna ya kuweza kuhifadhi uwezo wake akili pamoja na mawazo yake yote. Baada ya miaka kupita alifanikiwa kutengeza kifaa ambacho kina uwezo wa kusakinisha (download) fikra na uwezo wake wa akili. Kifaa hicho ni kompyuta ambar huwa anakaa nayo mwenyewe muda wote”.
“Siku mbili kabla ya kukutana na kifo chake, alisanikisha fikra na uwezo wake wa akili kwenye mashine hiyo na kumkabidhi mwanadada mmoja alieitwa Alice. Ni kweli ulimuuwa lakini aliendelea kuishi kompyuta hiyo akitafuna namna ya kuweza kutumia mwili wa mtu mwingine kama wake. Alifanikiwa na haijalishi ni mara ngapi atawauwa, ikiwa hiyo kompyuta yake ipo basi atarudi tena na tena. Njia pekee ya kumuuwa ni kuiharibu hiyo kompyuta na kila kinachohusika nayo.” Maelezo hayo yalizidi kuifanya vita hiyo izidi kuwa ngumu.
Kupambana na mtu mwenye akili zaidi duniani, mtu ambae hata akifa atarudi tena katika sura nyingine ilikuwa ni kero tosha. “Ukiachia hilo, ana silaha zake kubwa tano bado hajazionesha na mniamini kama hamtokuwa makini mtatapuputishwa kama nzige. Hapa naomba munisikilize kwa umakini, Matvei kipindi cha uhai wake. Alifanikiwa kutengeza mashine ambayo ilimuwezesha kutengeza nakala kivuli z watu halisi (clones). Watu hawa huwa natabia kama mtu halisi na kuwa na kumbukumbu zote mpaka siku ambayo mtu zilichukuliwa seli zake. Kwa kufanya hivyo alifanikiwa kutengeza nakala vivuli za watu wengi sana lakini hao si tatizo. Tatizo ni hao watano niliwataja kama silaha, walikuwa watu mashuhuri sana katika medani za kivita. Nyinyi munapofikiria hatuwa moja wao wamefikiria tatu. Na mpaka sasa wanawajuwa idadi na bila shka mbinu mnazotumia kwasababu baadhi ya hizo mbinu waliziandika wao”.
“Watu hao ni Chief Supreme General Commando Alfred Jackson, code name Death, first class indvestigator General Jason CJ, Battle analyzer and strategist Supreme commando Matvei (mwanamipango), Mtu asie na jina Mr Nobody huyo ni nakala yangu na Supreme Commando Andrew Cross, original Beast Sniper. Hao nilowataja wote munawajuwa na sio kuwajuwa kimajina tu bali uwezo wao halisi katika kupambana. Mpaka hapa uwezo wa kushinda vita hii ni asilimia iso zidi arobaini ikiwa hamataniingiza mimi. Mimi kipande pekee ambachp Martin hana taarifa kama nipo hai, na hawa unao waona na kikosi cha CODE X cha pasifiki. Sisi ndio watu pekee ambao ambao Martin hajatutilia maanani kwa sababu hajui hasa kama tupo.”.
“Watu hao ni Chief Supreme General Commando Alfred Jackson, code name Death, first class indvestigator General Jason CJ, Battle analyzer and strategist Supreme commando Matvei (mwanamipango), Mtu asie na jina Mr Nobody huyo ni nakala yangu na Supreme Commando Andrew Cross, original Beast Sniper. Hao nilowataja wote munawajuwa na sio kuwajuwa kimajina tu bali uwezo wao halisi katika kupambana. Mpaka hapa uwezo wa kushinda vita hii ni asilimia iso zidi arobaini ikiwa hamataniingiza mimi. Mimi kipande pekee ambachp Martin hana taarifa kama nipo hai, na hawa unao waona na kikosi cha CODE X cha pasifiki. Sisi ndio watu pekee ambao ambao Martin hajatutilia maanani kwa sababu hajui hasa kama tupo.”.
"Unamaanisha nini kusema wewe ndie kipande pekew ambacho Martin hakitambui" aliuliza Brain ambae kipindi chote alikuwa kimya. "Martin anadhani ameniuwa", " ina maana uliwahi kukutana na Martin uso kwa uso kabisa". "Ndio! Baada ya kutenganishwa na Junior, jeneral David alinikabidhi kwa Matvei ambako nilifutwa kumbukumbu zangu. Shukrani zangu ni kwa kemikali inayozunhuka mwilini mwangu. Kumbukumbu zikawa zinanirudia kama ndoto usingizini. Nahisi waligunduwa hilo wakaamuwa kuniangamiza. Nakumbuka siku ile nilishtuka baada kusikia hatuwa chumbani kwangu".
**********************
"Niko hapa kuongea tu Alexander Sr" Alingea mtu aliekaa kwenye kiti, "wewe ni nani" nilimuuliza. "Siku chache nyuma nimekutana na jenerali David. Niliongea nae mawili matatu na kuniambia Alex Jr ana kaka. Nimekutafuta sana na hatimae nimekupata" aliongea. " Jitambulishe ndio uendelee kuongea" nilifoka. "Oh! Samahani, jina langu ni Allen James na ni rafiki na mdogo wako", "nitakuamini vipi?". "Huhitaji kuniamini, lakini unahitaji kuamini hiyo briefcase pembeni. Hilo no bomu na litalipuka ndani ya sekunde sitini. Alex Jr yupo hai lakini kwa sasa huwezi mpata kwasababu yupo katika kazi muhimu sana" aliongea hivyo akasimama na kuondoka.
"Sikutaka kuwaza sana, nilitoa bastola yangu ndogo na kujipiga risasi mbili kwenye maungio ya bega na kuvunja kabisa ungio hilo. Nikaukata na kuuacha kisha nikatoroka kabla bomu halijalipuka. Nilielekea Afrika na kufanya Congo kuwa makazi yangu ya muda nikisubiria siku ambayo nitakuja kumlipa Martin na Matvei kitu walichonifanyia. Ila nikasikia kuwa wote pamoja na kikosi chao wameuwawa. Ukweli iliniuma sana na kutamani nimuue alieniibia kitoweo changu. Hata hivyo nilipiga moyo konde maana niliufahamu mpango wa Martin. Kufuatia hilo nikaanza kukusanya taarifa na kugunduwa Martin amekufa lakini alofanikiwa alichokusudia. Nilianza kuzunguka kukusanya makomredi wenzangu kwa ajili ya kulipa kisasi." .
Alex Sr alimaliza kuelezea na kumuangalia Alex Jr, "Allen James, ahsante" alijisemea Alex Jr. "Najuwa kuna mambo mengi mnataka kuongea, lakini ningeomba muyaweke baada ya vita hii. Kama mutakuwa hai basi mtaongea na kama itakuwa vinginevyo basi mtakwenda kuongea mbinguni" aliongea Mark. "Hatuna la kuongea sisi" walijibu kwa pamoja, "sawa". Walianza kupanga jinsi ya kuimaliza vita hiyo kwa muda mfupi tena bila kupoteza makomredi. Wakati wakiendelea kupanga na kupanguwa, Brain alikuwa kimya. Alionekana kuzama katika dimbwi zito la mawazo.
" Janeth" alishtuka baada ya kuitwa, "mbona unaroka damu puani" aliuliza aliemuita. Hapo ndipo akashtuka kama kila mtu alikuwa akimuangalia. Akatoa leso yake mfukono na kujifika kisha akasafisha koo na kuomba kusikilizqa. "Nahisi nimepata mbinu lakini kwa mara ya kwanza sina uhakika na ninachotaka kuwaambia" aliongea na kuwatazama. "Hiyo ndio mbinu tunayoitaka, ikiwa kichwa kama wewe huna uhakika na mbinu yako basi hata Martin atakuwa hajafikiria hivyo" aluongea Mark na kuwashangaza wote. "Kwa ninavyohisi ni wazi Martin alijuwa akitubana hivi na sisi tutataka kupiga vita nzima bila bikosi (all out war)" walikubaliana nae.
"Sisi tutapigana kama alivyotaka lakini na kwa mfumo tunaotaka sisi. Kama Ethiopia walivyoshinda vita na muitaliano. Ilikuwa vita ya kawaida lakini kutoka na miundo mbinu ya nchi ile kuwa ni ya milima. Faida ilikuwa kwa wenyeji, sisi hatuna milima lakini tuna majengo na kingine sisi hatuendeshwi kiakili bali tunajiendesha wenyewe. Hiyo ndio faida yetu kubwa. Tutachanganya aina mbili za vita, vita ya kawaida kwa mfumo wa kiethiopia na vita vya nyani nikiwa na maana vitabya kuvizia. Tutakuwa na vikosi vinne kwa jumla, kikosi kimoja kitakaa kwenye majengo marefu. Kikosi hiki kitahusisha wadunguaji wa masafa ya aina zote. Kikosi cha pili ni chambo, hiki kitafanya kazi ya kidanganya wapinzani. Kikosi hiki kitambana pale tu inapohitajika. Kikosi cha tatu ni cha vita ya nyani, watakuwa wamejificha nankushambulia kila atakaepita katika kumi na nane zao".
" Kikosi cha nne ni kikosi cha makondo tu, kikosi hiki kitakuwa na kazi ngumu sana ya kuvamia ngome kuu ya waasi. Ikumbukwe kuwa kifa na kupona katika aina hii ya kupambana ni asilimia hamsini kwa hamsini na si vingenevyo. Na katika mpango huu kikosi cha anga hakihusiki. Kitaendelea na kazi yake kilichopewa awali, kulindq anga na kushambulia ndege zozote ambazo hazitambuliki. Kuanzia sasa tutapiga vita ya hasira (aggressive war). Aidha uwa ama uwawa hakuna namna nyingine. Tukifanya hivyo inawezekana tukawatoa majenerali wao nje na kazi yetu itakuwa rahisi ikifikia hapo." alimaliza kuongea.
"Unaonekana kama mpango mzuri, lakini Martin ataishtukia tu" aliongea Alex Sr. " Hata akishtuka tutaendelea na mpangu huu huu. Sisi tunahisi Martin anatuzidi hatuwa kwa kila tumachofikiria lakini ukweli ni kwamba sisi tunafanya kile anachotaka yeye. Kama atashtuka akabadiliaha mfumo wake qa upambanaji, atajipa uhakika kuwa na sisi tutabadilisha mbinu. Ila tusipobadilisha mbinu tutamfanya ajiulize mwenyewe. Ikifikia hapo atakuwa hana imani na maamuzi yake, hiyo ni hatuwa ya kwanza ya kumshinda anaedhani ana akili sana" alijibi Janeth. Wakati alionekana mtu tofauti kabisa na majibu yake yalikuwa na ukali sana ndanj yake. "Una uhakika kuwa akishtuka na tukawa hatujabadilisha mfumo wetu tutashinda".
" Sina uhakika, ila niamini kwasababu nimepambana na watu aina hiyo huko nlipotoka. Na kukujuza tu, kwa sasa mimi ndio mtu ninaeshikilia rikodi ya mtu mwenye akili zaidi duniani IQ mia mbili na ishirini. Imepanda tokea nlovyojiunga na kikosi hiki". Kila mtu alibaki akiwa ameduwa asijue cha kuongea, kila mtu hapo alijiona kilaza. "Senior huwezi kupishana nae, hapo tayari ashapiga hesabu zake na kashajuwa asilimia halisi ya kushinda au kushindwa vita hii ila hayuko tayari kusema. Hapo alipo yupo katika ubora wake na akili yake inafanya kazi mara tatu kuliko yeyote kati yetu" alifafanuwa Alex Jr.
"Natumai kila mtu amesikia mpango mpya, vikosi vyote visivyokuwa vya wadunguaji na anga vitaungana. Vikosi vywa wadunguaji tangulieni kwenye majengo marefu yanayozunguka mji. Kikosi cha anga fanyeni kazi yenu, na Alfred una ruhusa ya kutumia CRONOS" aliongea Mark. Kusema hivyo kulipeleka tabasamu kubwa sana usoni kwa Alfred. "Cronos muda wa kuamka umefika" alijisemea na kutabasamu zaidi. "Marubani wote nifuateni" alitoa amri na kuondoka. "Kila kiongozi atatoa amri kwa vile anavyohisi sahihi" aliongea Mark kwa nguvu. "Wadunguaji wote nifuateni" aliongea Charlie na kuondoka pia.
"Kelvin chukuwa kikosi cha vita ya nyani" aliongea Jeff. Kelvin akatikisa kichwa na kutoa amri kikosi hicho kimfuate. Martina na kikosi chako, nahitajj uendelee kuangalia uwanja vita pamoja na kufanya mashambulizi ya kimtamdao. Natumai unaelewa nilichomaanisha" aliendelea kuongea Jeff. Martina akakitika na kuondoka na kikosi chake. "Senior waambie kikosi chako wajigawe katika vikosi hivyo, kila mtu aingie kwenye kikosi anachohisi kinamfaa" aliongea Alex Jr. "Washakusikia" alijibu. "Wewe utaungana na sisi, kikosi cha mwisho cha makomando. Utakuwa na mimi, Jeff na Adrian". " Sawa".
*******************
Kikosi cha anga.
Ndani ya ndege kubwa sana yenye mashine tisa, ndege hiyo ilionekana kama mji mdogo kwa mbali. "Nisikilizeni kwa makini, ndege hii hairushwi na rubani mmoja kitokana na ukubwa wake. Inarushwa na marubani tisa ila nahitaji marubani wawili wawili katika kila sehemu moja ya kuongozea. Pale pal wakajitokeza marubank kadhaa, waliobaki wakapangiwa majukumu mengine. Wapo walioenda kwenye chumba cha silaha, wengine walikuwa tayari kwa lolote lile. Juu ya ndege hiyo kubwa kulikuwa na ndege nyingine ndogo ndogo nyingi. Kila rubani aliingia kwenye ndege moja na kukaa tayari kwa amri yeyote ila itakayotoka kwa kiongozi wao huyo.
Taratibu mashine kubwa za ndege hiyo zilianza kutoa kelele. Mtikisiko mkubwa wa dege hilo ukasababisha mpaka ardhi kutetemeka, taratibu mlango mkubwa sana ukaanza kufunguka na kusababisha maji ya ziwa tara kuanza kupunguwa. "Marubani wote jiandaeni kumpeleka CRONOS angani. Hakikisheni anakwenda vizuri maana ndio mara yake ya kwanza kuonja upepo wa anga" aliongea Alfred kutoka kwenye chumba chake cha kuongozea. "Cronos atainuka ndani sekunde 9, 8, 7, 6, 5, 4, 3, 2, moja" sauti kali ikasikika huku ndege hiyo kubwa kuwahi kutokea duniani ikianza kuinuka.
Kikosi cha wadunguaji.
"Mumesikia kilichosemwa, ni uwa au uwawa. Sisi ni sehemu muhimu sana ya kukamilisha mpango huu. Hakikisha bunduki yako imefungwa na kiwambo cha kuzuia sauti. Darubini yako isipinguwe chini ya uvutaji wa mara nane. Na kama unahisi bunduki inakuzidi wakati wamkufyatua beba miguu ya kuwekea. Beba magazine zisizopunguwa ishirini pamoja na kioo maalumnza kuongezea kwenyw darubini ikiwa utahisi kiza kinakusumbuwa. Mwisho kabisa kila roho utakayochukuwa ihesabu. Atakaechukuwa nyingi atapata zawadi" alitoa maelezo Ghulam na kuwafanga wote wafurahi. Baada ya maelezo hayo walijigawa na kuingia majengoni kwa ajili ya kutemgeza viota vyao (sniper's nest).
Kikosi cha vita ya kuvizia (vita ya nyani).
Kikosi hiki kilihigawa katika vikosi viwili na ndio kikosi kikubwa kuliko vyote. Kina wanajeshi zaidi ya mia saba. Kikosi kimoja kilikuwa chambo na kingine kilikuwa kimejificha kwa ajili ya mashambulizi ya kushtukiza. Kikosi kilichokuwa chambo kazi yake ilikuwa ni kujitokeza mbele ya kikosi cha waasi na kutoweka kuwaacha wakiwasaka. Hapo kikosi cha mashmbulizi ya kushtukiza kilijitokeza na kufanya kazi yake. Chini ya uongozi wa Kelvin, amri zilikuwa ni kumwaga damu tu.
Kikosi cha makomando.
Alex Sr, Alex Jr, Jeff pamoja na Adrian, walibeba kila walichohitaji kwa ajili ya uvamizi wa kambi ya waasi ambayo kwa wakati huwo waloshagunduwa ilipokuwepo. "Tunahitaji kukabidhiana majukumu" aliongea Adrian, "mimi nitachukuwa mafasi ya mdunguaji" aliongea Jeff. "Mimi nitakuwa natangulia kuangalia hali kisha nitawapa ishara" aliongea Alex Sr. "Mimi nitachapa yeyote atakaepita mbele yangu" aliongea Alex Jr. Adrian alinyamaza kidogo maana kwa watu alikjwana macho ya kikatili tu. Kila mtu alikuwa anawaza kuuwa tu. "Mimi nitakuwa nitakuwa nafanya mawasiliano kati yetu, hivyo tutaweza kuwa pamoja katika kazi yote" aliongea.
Kikosi cha makomando.
Alex Sr, Alex Jr, Jeff pamoja na Adrian, walibeba kila walichohitaji kwa ajili ya uvamizi wa kambi ya waasi ambayo kwa wakati huwo waloshagunduwa ilipokuwepo. "Tunahitaji kukabidhiana majukumu" aliongea Adrian, "mimi nitachukuwa mafasi ya mdunguaji" aliongea Jeff. "Mimi nitakuwa natangulia kuangalia hali kisha nitawapa ishara" aliongea Alex Sr. "Mimi nitachapa yeyote atakaepita mbele yangu" aliongea Alex Jr. Adrian alinyamaza kidogo maana kwa watu alikjwana macho ya kikatili tu. Kila mtu alikuwa anawaza kuuwa tu. "Mimi nitakuwa nitakuwa nafanya mawasiliano kati yetu, hivyo tutaweza kuwa pamoja katika kazi yote" aliongea.
Kambini kwa Michael.
"Muda si mrefu wataingia kwenye mtego utakao wamaliza" aliongea Michael na kutabasamu. Wakati Matvei anapanga mikakati bila kujuwa kuwa alichokuwa anakisema chote ni kutoka kwa Michael, aliendelea pasi na kushtuka kwasababu mwili na akili yake havikuwa na uwezo wa kugundua hilo. "Endelea kutoa maelekezo ninayokupa tu" alijisemea tena Michael. Tabasamu zito likiwa limeupamba uso wake. "Michael unadhani wataingia kwenye mtego wako kweli au" lilokuwa swali kutoka kwa Alice. " Kwasasa hawana ujanja baada ya kuona kila mbinu inafeli, wataamuwa kupigana vita nzima bila amri moja. Kila kikosi kitaongozwa na kiongozi wake. Hiyo ni sheria ya gawa na ongoza na ndio nitakayoitumia kuwaangamiza" alijibu kwa kujiamini sana. Alice nae akatabasamu japo alihisi kuna kitu kimepunguwa lakini hakukigundua, "nitajuwa mbeleni huko" alijisemea.
Vikosi vya Michael vilizagaa mitaani kuwasaka maadui zao, katika saka saka hiyo mmoja wao akafanikiwa kumuona mwanajeshi mmoja wa kikosi cha waliinda amani. Akawageukia wenzake na kuwapa taarifa na pia kuituma makao makuu yao. Baada ya hapo wakaanza kuelekea upande ambao alimuona. Kikundi hicho kilikuwa na wanajeshi zaidi ya thalathini, ghafla mmoja wao akaanguka chini. Kichwani alikuwa na tundu la risasa, "mdunguaji" alipiga kelele mmoja na kuzama ndani ya jengo lililokuwa karibu. Wengine wakafuata, hilo ndio kosa lao kubwa pasi na kufahamu walijikuta wakiingia mikononi mwa waviziaji na wote wakateketea kama matone ya mvua yalogusa ardhi na kusambaratika. "Usafi umepita tayari" aliongea Kelvin kupitia kifaa cha mawasliano, "rodger tunaendelea na hatua ya pili" upande wa pili ulijibu.
"Tunawaona upande wa kusini magharibi" iliingia taarifa kwa Kelvin, "fanyeni kazi" alijibu, "rodger". Hayo yalikuwa ni mashambulizi ya mnyororo, yalipangwa na vikosi viwili. Wadunguaji na kikosi cha kuvizia, wadunguaji waliangusha mmoja kati ya maadui na kuwatia tafrani. Waliposambaratika na kuingia majengoni kwa ajili ya kujificha. Huko walikutana na waviaziaji na kuuwawa. Kikosi cha Michael kilianza kupuputisha kama kama mauwa ya muembe kwenye pepo kali sana. " Hichi nini" lilikuwa swali kichwa mwa Michael, "nini kinatokea naombeni jibu" alifoka sasa. "Vikosi vyetu vinapuputika katika hali ambayo hatuifahamu" alijibu Jason CJ. "Hata mimi naona hilo, nataka mniambie ni kivipi. Nipeni jibu na si kunambia hali ambayo hamuifahamu sitawaelewa" aliongea kwa hasira.
"Michael punguza hasira" aliongea Alice aliekua pembeni yake. "Nyamaza mpumbavu mkubwa, mtu mwenye uwezo mdogo wa akili kama wewe huwezi nishauri jambo" alimkoromea. "Lakin Michael", "mtoeni huyujinga humu ndani" alikatizwa na amri ya Michael. Waliingia wanajeshi na kumuomba atoke chimbani humo. Alive hakuwa mbishi japo alielanza kuelewa nini kinaendelea, "wamekupiga bao katika mchezo wako" ilikuwa ni kauli yake ya mwisho kabla ya kutoka. Michael alimuangalia kwa jicho kali sana la hasira.
**************************
Wakati sintofahamu ikiendelea kambini kwa Michael, makomando watano walikuwa wakijongea taratibu. "Jeff tupe taarifa" aliongea Alex Jr (Killer), "hakuna adui yeyote ndani ya mita mia tano" alijibu. "Senior fanya kazi yako" aliongea tena, alikuwa kama kiongozi. Alex Sr akachomoka kwa kasi na kutangulia mbele, alifika sehemu na kujibanza. Akachunguza kwa umakini na alipojiridhisha kila kitu kipo sawa. Akapeleka kidole sikioni na kubonyeza, "kila kitu kipo sawa" aliongea. "Rodger" walijibu kwa pamoja. Jeff akarudisha bunduki yake mgongoni na kushuka sehemu aliokuwa kajificha. Alex Jr na Adrian wakaelekea sehemu aliokuwa Alex Sr. Jeff akasogea mita mia mbili na kuingia kwenye jengo jingine na kupanda mpaka juu. Akachomoa bunduki yake na kulala chini, Alex Jr na Adrian wakafika alipo Alex Sr na kuungana.
"Kuna watu wawili mita kama kumi hivi kutoka mlipo" alionhea Jeff, "umesomeka" Alex Jr alijibu. Taratibu akaanza kusogea walipo, kwa kasi ya ajabu alichomoka na kuwavaa akiwa na kisu mkononi. Aliuchezesha mkono wake mara mbili tu, walianguka chini shingoni wakitokwa damu. Aliiburuza miili yao na kuiweka sehemu ngumu kuonekana kisha akarudi na kuungana na wenzake. "Clear" alisema, jua tayari lilishaanza kuzama hivyo kufantmya kuwe na mwanga hafifu sana.
Wakati makomando hao wakitengezea njia yao kuelekea kambini kambini kwa Michael. Minguromo yenye nguvu ilianza kusikika na ndege kadhaa zilipita. Lakini kabla hazijafanha mashambulizi ziliangamizwa na makombora makali sana yaliotoka kwenye ndege kubwa "cronos". "Anga ni yangu kama hufanani na mimi huna haki ya kuitumia" aliongea Alfred na kutabasamu. Ndege nyinginw kadhaa zilionekana zikielekea ilipo cronos huku zikafanya mashambulizi ya kasi sana. Lakini hakuna hata moja lililofanikiwa kuigusa ndege hiyo ya kisasa zaidi. Sio kwamba ilikuwa ikikwepeshwa, laa! Ndege hiyo ilizungukwa na utando mkubwa wa sumaku usio onekana (electro magenetic field). Utando huwo uliizunguka ndege hiyo kwa umbali wa mita tano, na ulizuia kitu chochote chenye asili ya chuma kupita. Huko angani kulikuwa na kazi ya pash pash, ndege za upande wa waasi zilijikuta zikiwa katika wakati mgumu sana kutokana na mashambulizi yao kutozaa matunda yeyote yale.
Hali hiyo iliifanya kambi ya Michael kuzidi kuwa na tafrani, "pelekeni ndege kubwa zote" alitoa amri Michael. Ndege tatu kubwa zinazokaribia ukubwa wa cronos ziliondoka kambini hapo na kupotelea angani. Alfred alipoona wamecheza karata dume akafurahi sana, "hii vita tuipeleke usawa wa bahari" aliongea kupitia kifaa cha mawasiliano. "Rodger" marubani wengine wakaitika na kuanza kuigeza ndege hiyo kubwa. Nyuma kabisa ya ndege hiyo kulikuwa na maandishi makubwa yalisomeka "God of the sky" (Mungu wa anga). Taratibu ilianza kuchanganya huku ikitoa mlio mkali sana. Nguvu ya mashine zake kubwa, ilisababisha mpaka baadhi ya vioo vya majengo kupasuka. Kutokana na ukubwa na uzito wake, cronos ilikuwa na hasara moja tu nayo ni kuchelewa kuchanganya. Lakini ilipochanganya ilikuwa inakimbia kweli kweli.
**********************
Turudi kwa makomando wanne sasa, "kuanzia hapa ni vita ya moja kwa moja" aliongea Adrian wakiwa wamekusanyika wote wanne. "Walitaka vita na sisi tutawapa na watalipa kwa kila walilolitenda. Ubaya ni hapa hapa duniani kwa mungu tutakwenda kufungiana mahesabu tu" aliongezea Jeff akivaa gloves zake nyeusi zenye ncha za chuma kwenye konzi. "Bila shaka tukitoka hapa watajuwa kuwa tumewavamia. Watajibu mashmbulizi kwa nguvu zao zote kuhakikisha hatufiki kwa wakubwa zao" Alex Sr aliongezea. "Ndio itakavyokuwa hivyo, haitakuwa raha ikiwa sisi tu tutashambulia kwa uwezo wetu halafu watupige makofi tu" sauti nzito yenye mikwaruzo kutoka Alec Jr ilisikika akivua gwanda yake ya juu na kuvaa koti ya kuzuia risasi. "Inabyoonekana vampire ana njaa" aliongea Alex Sr na kutabasamu. "Baada ya vita hii tukanywe kidogo kushehrekea ushindi" aliongezea Jeff akifunga kitambaa kilichobeba cheo chake mkono wa kulia "Death" Kilisomeka hivyo.
Adrian hakuwa nyuma alitoa yake ya silver yenye kichwa cha bweha ni kuiniglng'niza shingoni ilikuwa na maandishi yaliosomeka "silver fox". Alex Sr alivua nguo wake ya juu na kuacha mkanda uliojaa visu ukiwa unaonekana. Kifuani alikuwa na maandishi yaliosemeka "I got no name, Mr Nobody". Maandalizi yalikamilika na muda kuuwasha moto ulioandika hiatoria mpya duniani uliwadia. Makomando hao walichomoka sehemu waliokuwa wamejificha na kuwavaa walinzi waliokuwa wakilinda mlango wa kuimgilia kambini kwa Micheal kichwa kichwa. Iliwachukuwa sekunde chache tu kuwaangamiza na kuzama ndani ya jengo kubwa na maarufu sana katika mji huwo. Kwa msaada wa bingwa wa mtandao na akili ya Janeth walikuwa wakifahamu kabisa Michael na majenerali wake wako wapi.
" Viongozi wetu weshavamia kambi ya waasi, ni jukumu lwtu kuhakikisha hakuna anaelekea kambini huko. Vita yetu imebadilika kutoka kujilinda mpaka kufanya maangamizi. Ninapoongelea maangamizi namaanisha uwa kila anaehusika na uwasi" aliongea Mark na kusababisha tabasamu za uchu kwa kila mwanajeshi. "Rodger, all the best kwa viongozi wetu" wanajeshi karibia wote walijibu kwa pamoja. Hilo lilizidisha makali ya moto yaliokuwa katika vifuwa vya makomando ambao kwa wakati huwo wameweka maisha yao rehani kwa kuingia pangoni kwa nyoka.
Kambini kwa Michael hali ilikuwa tete, "rudisheni vikosi vyote kambini" aliongea Michael kwa hasira. "Haiwezekani nji zote zimefungwa na kikosi cha walinda amani" alijibu Jason Cj. "Kwani hapa kambini tuna wanajeshi wangapi waliosalia", "kwa haraka haraka ukituacha sisi hawazidi mia mbili" alijobu Matvei. "Nilikosea wapi?" alijiuliza Michael akishika kichwa, "wamekupiga bao katika mchezo wako" aliyakumbuka maneno ya Alice wakati anatoka. "Alimaanisha hivi au" kwa mara ya kwanza Michael anajikuta akikosa jibu. Ama kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Wakati wao wakiendelea kubishana, makando wanne walizidi kusogea na kila walipopita waliacha miili uso uhai. "Jamani hawa sio watu" alifika mtu mmoja akihema na kuongea, "unamaanisha nini?" aliuliza Mr Nobody. "Wako ghorofa kutoka hii, wanajeshi wote wameuwawa wamebakia wachache tu na.." hakumaliza kuongea ncha ya kisu ikatokea shingoni kwa mbele.
"Well! Martin habari yako" aliongea Alex Sr, "inakuwaje uko hai" alibwata Martin (Michael). "Ndio hivi niko hai, unakumbuka niliwahi kukwambia kuwa na akili nyingi sio chanzo cha maarifa". "Ah! Hata hivyo mnadhani mtashinda, watano kwa wanne" aliongea Michael kwa dharau. "Nani alikwambia wako wanne" ilisikika sauti nyingine. "Vipi umekamilisha kazi yako" aliuliza Alex Jr. "Ndio mkuu, Alice na kompyuta ya Martin. Wako mikononi kwa Martina" alijibu Jason CJ jr aliongea. Martin alizidi kuchanganyikiwa. "Sasa ni watano kwa watano" aliongea Alex Sr. "Michael ondoka hawa tuachie sisi" aliongea Matvei.
"Well! Martin habari yako" aliongea Alex Sr, "inakuwaje uko hai" alibwata Martin (Michael). "Ndio hivi niko hai, unakumbuka niliwahi kukwambia kuwa na akili nyingi sio chanzo cha maarifa". "Ah! Hata hivyo mnadhani mtashinda, watano kwa wanne" aliongea Michael kwa dharau. "Nani alikwambia wako wanne" ilisikika sauti nyingine. "Vipi umekamilisha kazi yako" aliuliza Alex Jr. "Ndio mkuu, Alice na kompyuta ya Martin. Wako mikononi kwa Martina" alijibu Jason CJ jr aliongea. Martin alizidi kuchanganyikiwa. "Sasa ni watano kwa watano" aliongea Alex Sr. "Michael ondoka hawa tuachie sisi" aliongea Matvei.
Martin akatikisa kichwa na kuondoka, "yule ni mpumnavu, hawezi kwenda mbali" aliongea Alex Sr. "Mnadhani mnaweza kitushinda" aliuliza Alfred Jackson. "Kwa asilimia mia moja bila hata kutoka jasho" alijibu Jeff. Alfred Jackson akamsogelea Jeff na kumuangalia kwa umakini sana, akamuangalia mkononi na kuona kile kitambaa kilichoandikwa Death. "Naona unapenda vyeo vikubwa" aliongea na kuvua gwanda yake ya juu. Mkono wake wa kulia alikuwa na mchoro wa fuvu kubwa, chini lilikuwa na maandishi yaliosomeka "Death". " Mimi ndio mwenyewe, halisi" aliongea kwa majigambo.
"Kwanini tuongee, tuoneshane kwa mikono yetu nani halisi na nani ni nakala kivuli" alijibu Jeff na kukunja ngumi na kumuekea kidevuni. Alfred Jackson akatikisa kichwa kuashiria kukubali mpambano huwo. "Ila hii sehemu ndogo sana, kuna pengine popote tunaweza tukatimiza lengo" aliongea Jeff. "Nifuate" Alfred Jackson aliongea na kuongoza njia. "Cross hakikisha Martin anatoka salama" aliongea Matvei na Cross akaondoka hapo. "Jason Jr hakikisha Martin haondoki, usimuue lakini" aliongea Alex Jr. Jason akatikisa kichwa na kutaka kuondoko. Mr nobody akataka kumzuia lakini akajikuta akirudi nyuma kwa kasi baada ya kukoswa koswa na kisu cha uso. "Huyo dogo sio kazi yako, wewe ni kitoweo changu" aliongea Alex Sr. Mr Nobody hakuongea kitu zaidi ya kutabasamu.
"Mi nahisi nitakwenda na Matvei" aliongea Alex Jr, Adrian akatabasamu maana kupambana na mkubwa wake aliekuwa akisifika kipindi cha uhai wake ndio kitu pekee alichokuwa akitamani japo hakuipata hiyo nafasi. "Unajuwa first class investigator, mpaka leo inasemekana hakuna aliefikia uwezo wako" aliongea. "Na haitatokea" Jason Cj Sr alijibu. "Nimeapa nitaivunja rikodi yako na leo ndio nitatimiza lengo langu. Nikikushinda hapa, nitakushuha pale kwenye ubao" aliongea Adrian akiwa na tabasamu zito usoni kwake. Hali ya hewa ndani ya chumba hicho ilikuwa nzito, laiti kama angekuwepo mtu mwenye moyo dhaifu basi amgezima kabisa. Wakati wakiendelea kutazamana, ghafla Matvei akachomoka na kupita mlango jirani na alipokuwepo.
Alex Jr hakutaka kufikiria ni kwasababu gani amekimbia, mzee lakini mwepesi akaruka meza iliokuwa mbele yake na kumuingia. "Kumbuka Matvei ni mwanamipango" aliongea Alex Sr kwa nguvu, "hata mimi mwanamipango" alijibu na kuzama mlango uleule aliopita Matvei. "Sidhani kama huyo mwenzenu atarudi tena" aliongea Jason CJ Sr. "Niamini, laiti kama angetaka apambane na nyie wote peke yake basi nyie ndio msimgerudi" alijibu Adrian. Macho ya Jason Sr yakaonesha mshtuko fulani hivi, kauli ile ilitoka kwa ujasiri wanhali ya juu. "Ah! Tusubiri tuone" alijibu, "hutakuwepo kuona matokeo, na hata mkikutana kuzimu sidhani kama utamtambuwa Matvei. Ninachotaka kukwambia ni kwamba, Matvei hana hata asilimia sifuri nukta moja ya kushinda, ameangukia kwenye mikono mibaya sana" alizidi kugongelea msumari.
****************
Hali ya hewa ya baridi iligubika usiku huwo, juu kabisa ya ghorofa Jeff na Alfred Jackson walikuwa wakipambana. Ngumi kali sana ilituwa tumboni kwa Jeff na kumfanga ajikunje kama mgonjwa wa tumbo. "Hichi ndicho wanachokipata wenye jeuri" aliongea Alfred Jackson. "Kwa hiyo unataka kuniambia huu ndio uwezo wako wote" alijibu kwa swali.
"Unahamu ya kufa si ndio"
"Ndio lakini si leo na si kwa mkono wako" alijibu Jeff.
"Basi urakufa leo na kwa mkono wangu"
"Jaribu ila nakuhakikishia utakufa wewe, nimekuacha sana ufanye utakavyo kwasababu nilitaka kupima uwezo wa mtu ambae nilikuwa namkubali watu wote duniani. Lakini wewe mjinga unamdhalilisha mtu huyo kwa uwezo mbovu kiasi hicho. Natumai unafahamu kama wewe ni nakala kivuli cha mtu mwenyewe. Na kutokana na sheria za kifizikia na kibaolojia uwezo wako ni nusu tu ya uwezo halisi wa mwenyewe halisi".
" Unaongea sana, thibitisha maneno yako kwa vitendo" alifoka Alfred Jackson. Jeff akatabasamu na kwa kasi akamsogelea na kurusha ngumi mbili zilizosafiri kwa kasi ya umeme. Alfred Jackson aliiona ya kwanza na kufanikiwa kuikwepa lakini kwa ya pili alichelewa. Ngumi hiyo nzito ya mkono wa kuahoto kutoka kwa Jeff ikagonga taya ya chini ya mdomo na kumfanya aweweseke. Kabla hajakaa sawa alichea teke kali sana la kifua lililomrusha mita kadhaa kutoka eneo alilokuwa. "Vipi, mbona umekuwa mwepesi" aliuliza Jeff, machoni alionekana akiumia sana kumpiga mtu aliemleta duniani hata kama alikuwa nakala kivuli. Alfred Jackson alijizoa na kusimama, mpaka hapo alishafahamu kuwa mtu aliekuwa anapambana nae alikuwa akicheza tu mwanzo. "Kama mbwai na iwe mbwai tu" alijisemea na kumfata.
Alirusha ngumi mfululizo lakini Jeff aliziona na kuzikwepa zote, hakumpa hata nafasi akamtandika kichwa cha nguvu na kumrudisha nyuma. Alfred Jackson aliona maruerue kabla ya kukaa sawa, akapeleka mkono wake nyuma na kutoa kisu. "Amgalia hicho kisu kisije kikakidhuru mwenyewe" aliongea Jeff na kukaa vizuri. Alfred Jackson akasogea kwa kasi na kuanza kurusha kisu, kwa mtu wa pembeni amgezani alikuwa akikirusha hovyo tu. Lakini ukweli alikuwa fundi kwenye kutumia silaha hiyo ya vita ya karibu. Jeff alikuwa akikwepa kwa umakini wa wa hali ya juu maana alifahamu kisu hicho huenda kikawa na sumu. Alfred Jackson aliteleza kidogo wakati wa kushambulia na hilo ndio likawa kosa. Jeff alitumia nafasi hiyo kumshika mkono na kwa mfumo wa judo akamkwatua na kumbamiza chini huku akiwa kaielekeza ncha ya kisu shingoni.
"Huu ndio mwisho, waliokufa waache wapumzike kwa amani" yalikuwa maneno ya mwisho kutoka kinywani mwa Jeff kabla ya kukizamisha kisu hicho kooni kwa babaake mzazi. Machozi yalikuwa yakimtiririka japo alofahamu hilo ndio lilikuwa jambo sahihi kufanya. "Kama si ombi la Martina, Martin ningekupa kifo kibaya sana" alijisemea na kulala pembeni ya mwili wa nakala livuli ya baba ake mzazi.
****************
Kelelel za visu kugongani zilisikika mara kwa mara, mpambano kati ya Mr Nobody na Alex Sr ulikuwa umepamba moto. Kila upande haukutaka kunyanyua mikoso pasi na kuumizana sana. "Nimekwambia huwezi kushinda ukiwa na mkono mmoja" aliongea Mr Nobody akiwa kajibanza sehemu. "Kama unaweza nishinde na mikonk yako miwili lakini sidhani" alijibu Alex Sr akihema. Damu nyingi ilikuwa ikimtoka, "nikiendeleza huu mpambano kwa mida mrefu itakula kwangu" alijisemea akijweka sawa. "Na huyu nikimuacha itakuwa hasara kwa wengine" alizidi kujisemea. Akapeleka mkono wake nyuma na kugusa pochi iliozuia na makanda wa suruali. Akatabasamu kidogo kisha akashusha pumzi "samahani Junior, huyu ndio hatari kuliko wote" Akachomoka sehemu aliojificha na kumfara Mr Nobody kichwa kichwa. Visu kadhaa vilizama mwilini mwake lakini hakusimama mpaka alipomfikia. Akapeleka mkono nyuma na kufungua ile pochi, akatoa kisu kikubwa sana na kukizamisha shimgoni kwa Mr Nobody. "Huna haki ya kuishi katika ulimwengu huu, umefang mengi sana mabaya" aliongea na kuanguka chini taratibu macho yake yalianza kupoteza nuru na hatimae yakafunga kabisa. Moyo nao ukaanza kupunguza kasi ya kuzima damu na mwishowe ukasimama kabisa.
Adrian alishuhudia yote hayo, "nenda kwa amani komredi. Tumejuana muda mfupi tu lakini ni kama tumejuana tokea zamani. Utaendelea kuishi katika mioyo yetu mpaka siku tutakapoungana baada ya maisha" alijisemea akitabasamu. Mpambano kati yake Jason CJ Sr ulikuwa wa moto, walitupiana makonde kisawasawa. Lakini baada ya kifo cha Mr Nobody kasi ya mashambulizi kutoka kwa Jason CJ Sr ikaanza kupunguwa. Adrian alilishtukia hilo na kuamua kurudi nyuma kwanza ili athibitishe. Na ndipo alipogunduwa kama Jason CJ Sr alikuwa akitokwa na machozi. "Umeshinda" yalikuwa maneno toka kwa Jason CJ Sr, Adrian alibaki ameshangaa tu. "Kivipi ilibidi aulize tu", "unajua kila nlipokuwa nikimuangalia Mr Nobody nilikuwa nafarijika sana, sikujuwa kwanini. Kuona mwili wake ukiwa hauna uhai, nimehisi maumivu makali sana moyoni. Unajuwa ni kiasi ameumia mwanangu kujiuwa mwenyewe" aliongea.
"Unamaanisha nini", "nakumbuka kila kitu, Alexander, Ethan au Alexander Junior. Kumbukumbu zangu zimerudi na nafahamu kabisa kama mimi ni nakala kivuli" aliijibu. Taratibu akaaogea ulipo mwili wa Alex Sr, "umefanya kazi nzuri sana kijana wangu, pumzika sasa" aliongea na kunyanyua bastola ndogo iliokuwa pembeni "kijana mwambie Ethan astaafu jeshi, mwabie hayo ndio maneno ya mwisho ya kakaake". Aliongea na kujitandika risasi ya kichwa. Mwili wake ukaanguka pembeni ya mwili wa Alex Sr na huwo ndio ukawa mwisho wake. "Heshima mpaka mwisho, ama kweli siwezi kukufikia" aliongea Adrian. Ghafla mlango ulifunguliwa, akaingia Alex Jr akiwa anamburuza Matvei. "Mpumbavu huyu alikuwa akiruka ruka kama nyani tu" aliongea na kumueka juu ya meza. Mpaka wakati hakuwa ameona chochote, "kwa mipango ile kiasi uwe mpuuzi, hukuwa na hadhi hata ya kupewa cheo supreme commando" aliongea na kupeleka mkono kiunoni. Alafungua pochi na kutoa bastola ndogo kisha akaiingiza mdomoni kwa Matvei na bila huruma akafyatua risasi.
Adrian hakuongea chochote kwanza, Alex alipogeuka tu macho yake yakagongana na mwili wa kakaake. Akatabasamu kidogo, "umenikimbia tena" huku machozi yakimtoka aliongea. Akasogea na kumnyanyua. "Ila sasa nahisi utakuwa na amani huko ulipo, pumzika na tuonane tena baada ya maisha" aliongea na kuikata cheni iliokuwa inaning'inia shingoni kwa kakaake. Sekunde chache baadae aliingia Jeff akiwa na mwili wa babaake. Alipouona mwili wa Alex Sr. Aliusha mwili wa babaake na kuinama kwa muda kidogo, "utaishi katika mioyo yetu milele".
*************************
Martin afanikiwa kutoka nje ya jengo hilo, uso kwa uso na dadaake. "Huyo ndio Martin" aliongea Alice aliekuwa na pingu mikononi. Wakati Martina amepigwa na bumbuwazi, ghafla ukasikika mlio wa bunduki, kishindo kikasikika nyuma ya Martin. Andrew Cross alianguka kichwani akiwa na tobo la risasi iliopogwa kutoka mbali sana. Jason CJ Jr alifika na kutabasamu, "kazi nzuri Charlie" aluongea kupitia kifaa cha mawasiliano. "Katika ulimwengu huu Beast ni mimi tu" Alijibu.
"Martina, unataka kuniuwa tena" aliuliza Martin, "sikuuwi nakupeleka tu sehemu unayostahiki kuwepo". Akatoa bastola na kumuoneshea, Martin akatabasamu na kuongea "fanya haraka unimalize". "Unadhani sijui kama nikukuuwa kabla ya kuiharibu kompyuta yako nitakuwa nimefanya kazi bure" aliuliza Martina. Martin akashtuka kidogo, "ndio, muda mfupi nlokuwa nayo nimeweza kuivamia na kujuwa kila kitu". Martina akaibwaga chini ilw kompyuta na kuimiminia risasi za kutosha mpaka ikawaka moto. "Umeniacha bila chaguo" aliongea Martin na kutoa rimoti mfukoni. Martina akabadilisha magazine haraka haraka na kumchapa risasi kadhaa za.kifua lakini alikuwa kachelewa. Tayari alishabonyeza rimoti.
Alfred akiwa anaimaliza ndege ya mwisho, lilipita bomu kwa kasi sana mbele yake. Kompyuta ya ndege hiyo ikaonesha wapi linakwenda kutuwa bomu hilo. Bila kufikiri mara mbili, akabonyeza kitufe na sehemu aliokuwepo yeye ikajitenga na ndege kubwa na kuanza kulikimbiza bomu hilo. "Kuna bomu linakuja huko" aliongea kupitia kifaa cha mawasiliano. "Tunajuwa lakini hatiwezi kulikwepa, hilo bomu lina nguvu ya kuangamiza mji mzima" alijibu Brain. Alfred akashusha pumzi na kuongea, "ilikuwa ni heshima kubwa sana kufanya kazi bega kwa bega na nyie, hapa ndio mwisho wa safari yangu. Bila kafara hatuwezi kuimaliza vita hii kama tulivyopanga". Akakata mawasiliano, na kuongeza kasi ya ndege yake.
Alifanikiwa kulizunguka bomu hilo na kukutana nalo uso kwa uso, "Alfred" Brain aliita. Lakini akashikwa bega na Talbot, "mwache aende bila kujuta". Mlipuko mkubwa sana ukasikika na usiku ukawa kama mchana. Wote waliinamisha vichwa chini, "nenda kwa amani komredi" walisema kwa pamoja.
*******************
Wiki mbili baadae, makaburi ya wazalendo.
"Hapo wamelala wanawake na wanaume, vijana kwa waschana. Wote hawakupata nafasi ya kutimiza malengo yao hasa yaliokuwa mioyoni mwao. Na yote ni kwasababu ya kuhakikisha amani na usalama wa watu ambao waliwaamini. Kwa raia wakawaoda hawa huenda wakawa wanajesho tu walioanguka vitani lakini kwetu walikuwa familia. Familia ambayo ilikuwa bora kuliko familia iliounganishwa na damu. Tumepoteza marafiki, waume, wake na ndugu zetu katika medani za kivita. Wameyatoa kafara maisha yao ili kulinda amani yetu. Nasi twawaambia daima tutaenzi zawadi hii na hatutamuelewa yeyote atakaefanya kinyume. Nendeni kwa amani, safari yetu ni moja ipo siku tutakutana tena" Alimaliza kuongea Jeff.
Baada ya shughuli hiyo watu walianza kutawanyika, mbele ya makaburi mawili walisimama kikosi kizima cha Jeff na Alex Jr. "Alfred G. Jones, mfalme wa anga" kaburi moja lilisomeka hivyo, "Alexander J. CJ Sr, a man with no name" jingine lilisomeka hivyo. Hakuna alieongea kitu, walikaa kimya na baada dakika tano walianza kutawanyika. Waliondoka wote isipokuwa Janeth, "kama ningejuwa ungeniacha mapema hivi nisigefunguwa moyo wangu kukupenda. Ila umejitoa muhanga ili mwanao aishi vizuri" aliongea akiligusa tumbo lake dogo na kuondoka.
MWISHO.
"Yeyote anaetamani vita, ni kwasababu tu havijamkuta" Gold Prime General Alex Killer.
"Vita visikie kwa jirani yako tu, vikigonga hodi nyumbani kwako, utaikimbia nyumba" Chief General Supreme Commando Jeff Death.
"Matokeo ya aina yeyote ile vitani, iwe kushinda au kushindwa. Huacha kidonda kisichopona" First Ivestigator Silver Fox Adrian Shadow.
"Hakuna mshindi katika vita" Alexander Senior, a man with no name.
RIWAYA HII NI KWA AJILI YA WALE WOTE WANAOWEKA MAISHA YAO REHANI KWA AJILI YA USALAMA NA AMANI NA DUNIANI.
0 comments:
Post a Comment