Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (4)
Sehemu Ya Tatu (3)
'usiku wa leo lazima nikamtembelee'
akajikuta akiwaza,pasina kujua muda ule angepaswa kuwaza atafanyaje kazi ya kumwangamiza raisi,akajikuta akiutumia kuwaza mwanamke,pasina kujua ni kosa lile...
Baada ya hali ya kutoelewana kutokea kati ya nchi mbili Kinte na Ganyama Rais Wa Kinte anaamua kumtumia mtu rais wa Ganyama Zidu Katili (Komandoo Chaka) lengo akamwangamize,na huo ndo ungekuwa mwisho wa vurugu hizo,
Habari Za Kutumwa Kwa Kijana Huyo Zinamfikia Rais Godluck Silvestar naye anajipanga kwa kumtumia mwanadada machachari alotua tu kutoka mafunzoni Komandoo Katarina(kk),je kk atafanikiwa kumkamata 'kc' na 'kc' atafanikiwa kumwangamiza Rais Yule ambaye kwa sasa anaulinz mkali?!...
TUSONGE
Mapenzi ujenga furaha katika moyo,pia mapenz usafisha moyo,Japo kuwa moyo wa Sai ulijaa gubu hasira chuki vilitoweka,safari yao iliishia katika club ile,wakaenda moja kwa moja mpaka mapokezi,ambapo ambapo baada ya kujitambulisha wakamuuliza muhudumu juu ya pikipiki ile!,
muhudumu yule akawaambia pikipiki ile bado ipo na aikuchukuliwa,Sai na 'kk' waka angaliana kwa mshangao,wote awakutegemea kupokea jibu lile!...
Wala hata awakuangaika kuichukua,wakaweka kama mtego,wakamweka kijana alotambulika kwa jina la brown pale lengo siku Zidu akija kuchukua pikipiki yake,brown ajulishwe naye ajulishwe makao makuu Zidu atiwe nguvuni!...
Masaa yakakatika,muda ukaenda,hatimaye jioni ikawadia,zidu akaanza kujiandaa tayari kwa kuelekea Bamala,alivaa,alipaka Nywele,kope Zake Mvi,akavaa Koti Kuu Kuu,akashika Fimbo,alikuwa Ni Kama Babu Wa Miaka 60 Au 70 Katu Usingeweza Kudhani Huyu Ndo Yule Sharobaro Juzi Yake Usiku alowafundisha adabu bodabada!...
Wana Mzuva,waliwapenda Na Kuwaheshimu Wazee Wazee Walitibiwa Bure,walisafiri Bure,walikuwa Na heshima yao ya pekee katika kijiji kile,ivyo kwa udhaifu ule ulimwezesha 'kc' vizuri tu kusafiri,hatimaye kwa mara nyingine akaingia bamala!
Alikuta mvua ikinyesha tena mvua kubwa ilo akujali tena ndo alifrah akaelekea palipo makazi ya Komandoo Katarina,moyo Wake Ulimwenda Mbio,alitaman Sana amwone katarina moyo wake ndipo ungetulia...
Wakati huo akiwa anakaribia karibia katika jumba lile,
Ndani Ya Nyumba Ile,mezani Waliketi Watu Wawili Wakilishana Chakula,hawa Si Wengine bali ni wapenzi walotokea kupendana!...
"mh love mbona umepika chakula kingi?!"
Sai akauliza ni baada ya kushiba!
"ni bora kibaki tushibe kuliko kisitoshe mpz!"
Kk akajibu akiachia na tabasamu la uchokozi,macho yake yalimlegea,mwili wote ulimsisimuka,na macho yalikuwa mazito!...
"lakini sasa ukikimwaga si unakufuru?,wengine wanatafuta wanavikosa mamy!"
Kabla Kata ajajibu ghafla kukasikika kengele ikimaanisha kuna mgeni nje ,kata akasitisha kujibu akanyanyuka na kuingia chumbani akatoka na mwamvuli na kuelekea nje!,maswali mengi yalikichakaza kichwa chake ni nani huyo agongaye,na mvua ile,kwani mvua ilikuwa ni kubwa ambayo akutegemea kuna mtu angeweza kutembea nayo!
akafungua geti,alishtuka ni baada ya kumkuta mzee akiwa kaloa,haraka sana akiwa na uso wa huruma akamkaribisha ndani!,mzee yule alikuwa akiomba msaada!,alisema toka jana usiku hakuwa ametia kitu mdomoni,kk akamtoa wasiwasi,akamkaribisha mpaka sebuleni,yule mzee kwanza alishtuka kumuona kijana yule!
"beby umeona maajabu ya Mungu Ulisema tusipike chakula kingi na huyu mzee angekula nini?!"
Maneno Yale Kwanza Yalimchoma Zidu,mapigo Ya Moyo Yakaanza Kumwenda Mbio Kumbe Yule Mtu Ni Mpz Wa Katarina?!...
Akajiwazia Akiulaumu Moyo Wake Kwa Kimbelembele Cha Kupenda!
"sasa Mzee Kabadilishe Hizo Nguo Katika Kile Chumba Pale Uje Ule Kisha tuongee"
kk akaongea,zidu akajinyanyua kuelekea ndani ya kile chumba kwa ajili ya kubadilisha!,huku nyuma Sai akamuuliza mpz wake...
"unamchukua mzee ambaye umjui utataka akae hapa!"
"kama hana pakukaa itabidi akae tu hapa mpz,kwa maana mbili moja lile lizidu wakati tukiwa hatupo linaweza likaja na kufanya chochote nasi tusijue,ila huyu mzee pindi ugeni usiowakawaida ukija kwa kuwa yeye atakuwa mwangalizi wa nyumba ataweza kutujulisha,na pia tutamuweka kama chambo,ikiwa tutarudi na kukuta kauwawa tutajua humu ndani kumechunguzwa ivyo ni vyema pakawa na mtu"
"kama umeamua ivyo sawa!"
Sai akakubali kwa shingo upande,ghafla mzee yule akatoka ndan akiwa kabadilisha 'kk' akamchotea chakula,Zidu akaendelea kula...
alipomaliza kula,akashukuru sasa ndo wakamuuliza...
"ehe mzee unatokea wapi na ipi shida yako hasa?"
"mimi kwa jina naitwa mzee lyatuu,natokea kijiji cha mbaliii huko mzuva land!"
"mzuva land?!"
Kwa pamoja katarina na Saimon Wakaulizana,walikijua Kijijikile,kijiji kilichotawala iman potofu,kijiji kilichojiongoza chenyewe kwa kutumia mila zao!...
"nilituhumiwa mchawi katika kijiji kile siku niliposikia wamepanga kunichomea ndani ndipo nilipotoroka na kuja huku sijui familia yangu ipo katika hali gani!...
Ghafla Machozi Yakaanza Kumchuruzika,"pole Sana babu utakaa hapa kesho pakipambazuka sisi tutaenda kijijini kuchunguza habari hizi je ni kweli?,na tutakuletea habari za familia yako!"
Katarina aliongea kwa kujiamini,yeye kama afisa polis asingeweza kukaa na mtu pasina kujua kama akiongeacho ni kweli au si kweli,alitakiwa Awe Na Uhakika Na Yule akaaye naye
Zidu aliona sasa ndo anaenda kuaibika!...
Mapenz yanamsukuma Zidu katili kwenda kuishi na adui yake kwa muonekano wa uzee,
Kutokana na ufichaji nyaraka mbalimbal za kazi hapo nyumbani 'kk' wanampokea pasina kujua ndo adui wakimuweka kama mtego wa ulinzi songa nayo kujua kilichoendelea!
Baada Ya 'kk' Kuongea Maneno Yale akamuonesha chumba ajipumzishe!,
kule chumbani Zidu usingizi ulimpaa alikuwa akifikiria kuhusu mwanamke yule!,moyo wake ulisononeka baada ya kugundua yupo katika mahusiano,
Akukubali Kushindwa,alijiona Mbabe 'huyu dem ni mali yangu na lazima nimmiliki mimi hata ikibidi kuua ntaua'
Zidu Kuitwa Katili Jina hili alikukosewa,ni kweli alikuwa na roho ya kikatili,kuua kisa mapenzi yeye kwake ni sawa tu,
Aliuthamin Moyo Wake Zaidi,usiku Ule Ukapita...
Kesho Yake Ikawadia Kila Mmoja Kwa Wakati Wake aka amka,'kk' akaandaa chai,wakakaa mezani wakanywa
"umesema unaitwa nan tena"
"mzee lyeyatuu!"
"unaweza kunielekeza kijiji chako mpaka mahali unapoishi?"
Zidu Kimoyoni Akacheka,alijua Ilo Ivyo toka jana alivyotoa maelezo alijiandaa!
nikwel,siku ile aloondoka jioni mzuva land toka juzi jirani na kagest kale palikuwa na nyumba moja ya mzee mmoja alotambulika kwa jina la lyeyatuu walikuwa wakituhumiwa kwa uchawi,mchana wa siku hiyo ambayo jioni ndo aliondoka anakumbuka wakati akiwa ndan ya chumba chake ndani ya gesti ile ghafla alisikia kelele nje,kama ukunga huku kelele za watu wengi sindo ikabidi atoke,akashughudie kunani
Macho Yake Yalikumbana Na Wananchi Wenye Hasira Kali Wakiwa Na Mapanga Marungu Chini Alikwepo mbibi na wanaye na wajukuu zake kadhaa,walikuwa wakipigwa wakilazimishwa wataje mahali alipokimbilia baba mwenye nyumba mzee lyeyatuu
"nyie niwachawi na leo lazima tuwakomeshe huyo mumeo si katoroka labda asirudi hapa kijijini..."
Wananchi Walizidi Kuongea Kwa Hasira,na Mwisho Mwenye Kiti akaruhusu familia ile isambaratishwe,kile kilikuwa ndo kijiji cha mzuva land,wananchi walijichukulia sheria mkononi na serikali aikuingilia wala awakukifatilia kijiji kile!...
Nikama Awakujua Juu Ya Uwepo Wa iko Kijiji,Zidu akuingilia kitu,aliangalia jinsi familia ile ilivyopigwa na kuuwawa kwa familia yote mwenyekiti akatoa amri miili ile irudishwe ndani na nyumba ile ichomwe moto na ndivyo walivyofanya mwisho wakati Zidu anaondoka ndo aliacha wakizika vichwa na mabaki!...
'naenda kwa mtindo huu wa uzee nikijifanya na shida niishi tu na yule mwanamke niwe karibu naye mpelelez yoyote lazima ajue asili ya nlopotokea...
LIJITU zidu lilivyofikiria hvyo likaachia tabasamu...
'ntajitambulisha mzee lyeyatuu kwa kuwa najua yule mzee awez rudi pale na familia ile si imeangamizwa,yes fantastic plan,akienda kule atakuta maelezo yangu ni ya kweli'
likazidi waza,likiwa ndani ya gari,mpelelezi mahiri utengeneza majibu ya maswali ambayo alijua angeulizwa ikiwa angepokelewa!...
Na ndivyo ilivyokuwa kwa jitu hili,alikutakaga kupoteza point hata moja katika mipango yake eti...
Hivyo Kama tulivyo ona lilifika salama Bamala,mvua Ikiwa Inanyesha,lenyewe eti ndo likawa likifurahia hali ile,litahurumiwa zaidi,likaenda bisha hodi likakaribishwa!...
likatoa maelezo,kama lilivyopangilia na kupewa chumba...
asb baada ya kunywa chai pale 'kk' na 'sai' wakamwambia ndo wanaelekea kijijini kuchunguza yale waloambiwa isiwe ikawa wanafuga lijambazi,kk akampa na simu
"babu hii namba yangu chochote kikitokea usisite kunambia!"
"sawa mjukuu wangu!,uwape chochote familia yangu umwambie bibi yako na wadogo zako nipo salama huku watoe wasiwasi nawapenda sana,waambie hivi pakitulia ntarudi"
"sawa babu"
wakatoka!
'blood shit ntakupata tu Katarina,sai Lazima Ufe'
Zidu Likajiwazia Likisahau Kabisa kazi ya kumwangamiza raisi alopewa,na kilichompeleka kule!
mawasiliano na Kinte aliyakata,kwa sasa kipaumbile chake ni kumpata tu KATARINA...
KINTE
IKULU
Kikao cha dharura kiliwekwa,ni baada ya siku kadhaa kupita huku Zidu akiwa hapatikani hewani,
"au atakuwa amekamatwa?"
Rais Mernel ii alioji
"sidhani mh rais kwa maana angekamatwa basi lazima wangetangazia!"
"vp Isack bado yupo chini yetu?!" mh rais akahoji
"yah! anamkataba wa miaka mitatu yule kule kijiji nakaya jeshi dogo lilipoweka kambi chini ya ardhi!"
Ndo kule palipo na kanyumba cha makuti kwa juu ila chini ya ardhi kumejengeka!
"ok,jemedar wa majesh siyupo kule wasiliana naye apewe kazi aende kinte
akachunguze,kama ZIDU yu hai au wamemwangamiza kimyakimya"
"sawa mkuu!"
Wakati ayo yakiendelea kwa upande wa GANYAMA,raisi naye alikuwa na kikao chake! na baadhi ya mawaziri wake na viongozi wakubwa wa jeshini...
Rais Silvestar akaanza kuzungumza
"siku kadhaa nyuma tulipata habari kuwa KINTE wamemtuma mtu aje kwa dhumuni la kuniua,wazir hapa akampachika demu wake...
Viongoz wote wakacheka unajua Rais yule japo ni katili ila alikuwa mcheshi na mwingi wa utani,baada ya watu kumalizikia kucheka akaendelea...
...akanambia ndani ya masaa 24 zidu atapatikana,24 hiyo mpaka sasa nadhani ayajaisha...
juzi Maskin Mtoto Wa Watu Nikakoswakoswa Na Risasi Demu Kanipiga Mtama Chali!...
Watu wakaangua kicheko,akaendelea,duh sasa nikashangaaa eti demu badala akamsake mtu anakuja kulilia kukaa mgongoni mwangu na kunipiga mitama,sijui nilimpa kazi ya kunipiga mitama au kumkamata muhalifu,bas baada ya hapo nikampa masaa 24 nikijua pengine atampa kazi mtu mwingine matokeo yake kakaacha kalekale ka demu kake...
na mbaya zaidi juzi,juz nasikia kamelala na huyo Zidu Pasina Kujua,asb Zidu Kamzid Nguvu Kamkimbia Kapiga Bodaboda Wetu...
Watu Wote Wakaacha Mdomo Wazi,hakuna aloijua habari ile hata waziri gozigoz mwenyewe!
Je Ni Nani Aliyeivujisha Kwa Raisi?!...
Hili hakuna Alojua,ni Siri Ya Rais Pekee
"sasa Basi Kwanzia Sasa Namtengud Bwana Gozgoz Kutokuwa Waziri Wa Aina Yeyote Atabaki Mbunge Tu!...
Na Nafasi Yake Itachukuliwa Na Bwana Philip Ghali Kipikicho Huyu Ndo Atakuwa Waziri Wa Jeshi Ulinzi Na usalama Na Kijana atakayepewa kazi ya kumtia mkononi Zidu Si Mwingine Ni KOMANDOO SAIMONI KIEREHERE (SAI)
Watu wote wakapiga makofi lakin ghafla simu ya mh gozigozi ikaita akapokea akaweka loud spiker ni RICHARD BULL,huyu ni shushushu wa ganyama nchini Kinte
"mh hali ya sintofahamu inaendelea huku mawasiliano na zidu na huku yamekata,siku mbili tatu hizi mawazo yao uenda amekufa ila wanamtuma kijana ISACK kuja huko kuchunguza kama zidu yu hai au vipi! ndo hayo mkuu
nb' anaingia kupitia shotcut rod masanja place nguvu zaid ziwekwe hapo!...
simu ile ikakatwa
viongozi wote wakatazamana!...
Waziri Mpya Alochaguliwa Palepale Akakabidhiwa Kazi Isack Akituwa tu auwawe na mwili tu urejeshwe kinte!
maskin wakat huo Isack Ndo Alikuwa Akiikaribia Masanja Akijua Ndo Njia Nzuri Kumbee Kimbembe!...
Mambo Yanazidi Kunoga ZIDU APANGA KUMWANGAMIZA 'SAI' KWA WIVU WA KIMAPENZI,HUKU HUYO HUYO SAI AKIPENDEKEZWA KUISHIKA KAZI YA KUMSAKA ZIDU JE ATAIPOKEAJE,NA NI NANI ALOVUJISHA SIRI YA KK KULALA NA ZIDU ASB KUZIDIWA NGUVU KWA RAIS?,KK ATACHUKULIAJE KITENDO CHA KUSIMAMISHWA KUFATILIA KESI YA KUMKAMATA ZIDU NA KUPEWA MPZ WAKO UTATA UTATANI:
Baada Ya Masaa Kadhaa hatimaye wakaingia mzuva land,wakafata ramani waloelekezewa na mzee lyatuu mpaka katika eneo lile,kwanza walishtuka baada ya kukuta pagara tu!
ikabidi waulize!,kwa baadhi ya wapita njia wakaelezwa hali halisi kuwa familia ile ilikuwa ikituhumiwa kwa uchawi,ivyo mzee lyatuu mwenyewe akujulikana alipoelekea ila watoto na wajukuu walichomwa moto!
"maskini sijui yule mzee ataipokeaje taharifa hii!,si tunaweza kumpoteza"
'kk' alimnong'oneza Saimon,wote walishangazwa na maajabu ya kijiji kile,kijiji kilichosaulika na kutupwa na serikali,kijiji ambacho wananchi walijichukulia sheria mkononi,baada ya kupata ushahidi wakiamini kwamba yule mzee ni mtu salama wakaianza safari ya kurejea kwao Ganyama!
"huyu Zidu ni mtu atumiaye akili sana ila naamin ipo siku atapatikana tu,alinihaidi atarudi na atarejea mwenyewe kwenye mikono yangu!"
Katarina Kwa Sauti Ya Upole Yenye Kusisitiza Aliongea,
Sai alicheka kimoyoni, alishamdharau sana Katarina,akakumbuka pindi alipomchongea kwa Raisi,alitaman sana yeye apate nafasi ile,akuona shida hata kumpoteza katarina aliyekwisha kueleza hisia zake kwake!,ghafla simu yake ikaita,kuangalia ni namba maalumu,waliitajika ikulu!,akamsisitizia Katarina kuongeza mwendo,robo saa baadaye walikuwa mbele ya Rais Na baraza lote la viongozi wakubwa!
Agenda Ikapitishwa,Saimon akakabidhiwa kazi ile rasmi ya kumsaka Zidu,Katarina akawa chini yake,ilikuwa ni amri ya kijeshi aikupaswa kupingwa japo moyoni mwa Katarina kulijaa simanzi ila hapakuwa na budi!...
"na kitu kingine inapaswa uelekee masanja rod taharifa tuloipata ni kwamba nchi ya Kinte Imepoteza Mawasiliano Na Zidu Na Kwa Fikra Zao Uhisi Pengine Zidu tumemwangamiza kimya kimya japo sis bado tunaendelea msaka kilichopo kawekeni kizuio katika hiyo njia huyo chalii akiwasili mumkamateni mumuue kikatili mmchukue na kamera vyote vitumwe Kinte tuzidi kuwaumiza!
"mkuu nina rai!"
"ambatanisha!"
"kwanza nimshukuru Mungu Pili Wewe Rais Wangu Kwa Nafasi Adhwimu Ulonipa Ikiwemo Ya Kumtia Nguvuni Zidu Katili Nasema ahsante sana,naomba nikuhaidi mimi na mwenzangu Katarina tutaifanya kazi hii kwa ari,moyo,kasi na weledi wa hali ya juu tukilitumia jeshi la polisi!...
mh raisi,sikwamba nakupinga ni oja yangu tu kwa nini huyu kijana Isack tusimkamate na asiuwawe ila tumtumie huyuhuyu kumpata huyo Zidu,kivipi sasa?,tutamfatilia kila hatua atakayotumia kwa kuwa nahisi ana vitu kama siyo mawasiliano ya huyu Zidu,ambayo binafsi sisi hatuna,ivyo tukimtumia huyu itakuwa nyenzo rahisi ya kumpata Zidu!,then akipatikana ndipo tutawaua"
Makofi Yakatawala,kwa Mara Ya Kwanza Rais akatabasamu!,akafungua mdomo wake...
"niseme tu wewe ni zaidi ya jabali,kwa sasa na amani na ntakuwa natembea huru sasa,hapo awali nilikuwa na khofu mashaka,ila unaijua kazi,fanya vile unavyo ona inafaa...
Katarina nyumba ulokabidhiwa utamkabidhi mwenzako nawe utarudi kambini..."
"hapana mkuu mwache akae pale ni karibu na nnapoishi kambin mbali aisee mi ntaishi kwangu naye mwache aishi hapo"
Sai akajidai kuombelezea,moyoni alijua anaishi naye,basi Rais hakuwa na shida,wakapewa ruhusa,
"wacha mimi niende masanja road wewe kwa sasa nenda nyumbani ukamwambie ukwel yule mzee atakuwa na wasiwas sana!"
"maskin ataipokeaje habari hii!..."
"ni kweli ataumia,atalia atauzunika ila ni bora umwambie ukwel muda huu ajue kwa maana hata ukimficha ipo siku ataujua ukwel hataumia vilevile bora umwambie ukwel sasa wacha nikawah kabla huyo jamaa ajapita..."
"sawa ntakuja!"
***
Muda huo jitu Zidu Lilikuwa sebuleni limekaa,akiwa na 'tooth spick' mdomoni akichokonolea nyama,
'mapenz nikitendawili ambacho ni gumu kutegulika...
Likajiwazia
'sijawah Kufurahia Mapenzi,mwanamke wangu wa kwanza yuko gerezani sasa Rose,nilimpenda Kule Kijijini toka ndani ya moyo wangu,ila alipenda pesa,akaamua kutoka na rafiki yangu Erick,erick Sargion,nikaja Nikampenda Mery mwanamke aloshindikana kijijini mpaka kuitwa makushindikana kutokana na mateso alopewa na mume wake Erick Nikaamua kuwa naye,nikampenda nikazama kwake,ila thaman yangu ikakosa thaman kwake akatoka kimapenz na adui yangu mh alex huko Tanzania,mwisho Akaja Kufa Kisa Gari...
Nikaapa Kutopenda tena ila adui yangu mwingine Katarina Najikuta Nikimpenda!,hivi Na Mkosi gani mimi?,kuna mapenzi kwenye uhadui...
kazee kale kakajikuta kakiwaza huku usoni machozi yakiwa yamemlengalenga
ghafla akasikia simu yake ikiita,kuangalia ni Katarina,akapokea
"njoo Fungua Geti!"
Simu Ikakatwa,ila Zidu Alibaki kaganda,mapigo ya moyo wake yalikuwa yakimwenda mbio,sauti ile iliingia moja kwa moja mpaka katika ubongo wake,taribu akaenda na kuufungua mlango Katarina Akaingia
Wakawa Wameketi Sebuleni!
"babu Kweli tumefika kijijini,ila itabidi uvumilie kwa ntakachokwambia!"
"ni..ni..nini mjukuu wangu!"
Kabla Katarina Ajaendelea Kichefuchefu Kikali Kikamshika Akanyanyuka Haraka Haraka Kwenda Kutapika!
'nina Mimba Nini!'
Akajiwazia,akirejea! "nambie mjukuu wangu familia yangu inaendeleaje huko?!"
"pole sana babu kweli tumefika kijijin na uliyetueleza yote ni ukweli,baada ya wewe kuondoka wananchi waliikamata familia yako yote wajukuu bibi wakawapiga mpaka kuwaua!...
Palepale ghafla mzee akaenda chini!,katarina akajitahidi kumuamsha kimya!
aliposikiliza mapigo ya moyo yalidunda!,ni wazi mzee lyayatuu alikuwa kapoteza fahamu!...
Katarina Akachukua Kanga Na Kuanza Kumpepea akimkazia macho usoni
"mh!" ghafla Katarina akaachia mguno akipeleka mkono wake katika sharubu kwa nia ya kuzivuta,alihisi kitu juu ya mzee yule...
MAKUBWA!
Ile kabla mkono wake ujashika Sharubu Zile za mzee yule ghafla akajinyanyua kwa haraka na kueleke mpaka katika sinki la maji,akawa kama anataka kutapika lakin akutapika!...
Alihisi kichefuchefu kikali kikimtawala,akaelekea jikoni nakuchukua ndimu akailamba pengine ni ili kukata kichefu chefu kile,alihis moyon kukereka na aikuwa hali ya kawaida hiyo kwake!,aikumpa tabu kujihisi yu mjamzito,akajikuta akikosa raha!...
Japo Ile Siku alo 'date' na Zidu Kesho Yake akiwa bado katika siku zake za hatari akakutana pia na Saimon lakin moyo wake ulimsukuma kuamini kuwa kama kweli ana mimba nilazima itakuwa ya Zidu
Akajikuta akikunja sura,
'hii mimba ntam'bambikizia Sai najua siyo yake lakini mwanangu siwezi kumkosesha baba,na siwezi kumpa mwanaharamu yule kuwa ni mwanaye!...
Akawaza akiendelea kunyonya ile ndimu,ghafla akamkumbuka yule mzee na Sharubu Zake,akachepuka Kutoka Kule Jikoni Kuelekea Sebuleni akamchunguze zaidi,ndimu yake ikiwa mkononi!...
MASANJA ROAD
Sai aliwasili katika barabara ile,akutaka kuweka kizuizi chochote,akaweka kambi katika duka moja dogo tu lililokuwa likiuza bia,akachukua safari yake moja akawa akiinywa taratibu huku macho yake yakiwa barabarani mpakani kwa Kinte,akitegemea Muda Wowote angemwona Isack akiwasili!
Na Kweli baada ya kama dakika tano hivi kupita alimuona Isack,alimtambua Fika Kutokana Na Kuelezwa Jinsi alivyo,pamoja na kwamba alivaa element iloficha uso wake,akuwa na shaka kuwa ndiye,kwa haraka akajinyanyua na kuingia ndani ya gari lake akaliwasha tayari kuifatilia pikipiki ile!...
Isack Kwa Kupitia Saidmirrow alishagundua anafatiliwa,wala akujali aliendelea na safari yake akitaka kujua mwisho wa yule kijana ni upi alishndwa kuelewa ni nani aliyevujisha ujio wake!,safari yake iliishia katika lorge moja akapaki pikipiki yake akashuka,akaenda mpaka mapokezi akachukua chumba baada ya kukabidhiwa chumba akaweka begi lake ndani kisha akatoka mpaka nje kabisa mpaka maeneo ya parking,akaangaza macho yake kuangalia yale magari ni kama alikuwa akitafuta kitu na ghafla macho yake yakanata katika gari moja ambalo alilitambua ndo lile lililokuwa likimfatilia...
Akuwa nashaka alikuwa akifatiliwa,akajionya kuwa makini,akapiga hatua kuelekea mahala pa kulia,akaagiza chakula alichopenda yeye akala akajinyanyua kuelekea chumbani kwake tayari kwa kupumzika!
Akakifikia Chumba Chake,kwanza alishtuka kukikuta wazi wakati mara ya mwisho alikifunga ndipo akaelekea nje,ila akujali kabla
ajashika Kitasa Na Kufungua akapeleka mkono wake kibindoni,alipoutoa ulikuwa na silaha,mkono wa kushoto akautumia kufungulia mlango huku mkono wa kulia ukiwa umeshika ile silaha,ghafla akazama ndani!
patupu!
Ila nguo zote zilikuwa zimetolewa begini na kuzagaa kitandani,ni kama kule ndani kulisachiwa!
Akutaka Kuumiza Kichwa Kujiuliza Ni Nani Alosachi,alijua Ni Yule alokuwa akimfatilia apakuwa na mwingine!,akarudishia nguo zake vizuri kwenye begi,akalirudisha mahali pake alipokuwa ameweka awali!...
Akajitupa Kitandani,ila ghafla alijihisi mkojo akapiga hatua kuufata mlango wa chooni,choo kilikuwa mulemule ndani,akakishika kitasa na kukikunja kabla ajaufungua mlango akahisi pigo lililo mrusha mita kadhaa nyuma,ila akajitahidi kuinuka!...
Mbele Yake alikuwa kijana mwenye mwili mdogo lakini ulojengeka kimazoezi,alikuwa akimwangalia kwa tabasamu baya,bila shaka huyu ndo alokuwa akimfatilia toka mpakani kule,na ndo alochunguza begi langu,alikuwa anatafuta nin?,ni nani,na kama ni askari kwa nin asmkamate?,kumbe alikuwa kajificha chooni,akajiwazia akikaa sawa kwa mapigano...
Jamaa akiwa kakunja ngumi akamjia kwa kasi akarusha ngumi ya kwanza,Isack akawah kutanguliza mkono wake kuipangua ngumi ile,yapili hiv
yo,hivyo yatatu,ya nne,nayo akaipangua naye akajiandaa kwa kuukunja mkono wake,akaipanchu ile sambamba naye kurusha yake kuelekea usoni kwa mtu yule,ambaye ghafla aliinama chini ngumi ile ikapiga hewa,muda ule ule akapiga hatua moja kubwa nyuma,na kwa wepesi akaukunja mguu wake na kuufyetua teke kali likampata Isack akaserereka chini,akutaka kubaki palepale chini ishara ya kukubali kushindwa japo teke lile lilimuumiza vibaya akajitahidi kujinyanyua ila akakumbana na ngumi nzito ya mdomoni,na mkato wa ghafla akaserereka chini tena,damu zikaanza mtoka mdomoni!
"we ulipaswa tukuue turejeshe kichwa chako Kinte kwa huyo alokutuma ila sitofanya ivyo,icho kilichokuleta kitaraisisha kazi yetu ya kumpata huyo mtu wako,ivyo tutakufatilia kila hatua uipigayo...
Yule mtu aliamua tu kumwambia wazi Isack hali halisi,alimwambia kwa mawili,kwanza moja alijua Isack asingeweza rudi Kinte bila ripoti maalumu,juu ya Zidu kama yu hai au amekufa,na pili ili Isack akamilishe kazi yake ni lazima kwa njia yoyote ile awasiliane kama si kuonana na Zidu,ivyo hata kumwambia ukwel ule isingebadilisha msimamo wa jamaa yule
Kwa hiyo ni kama alimuweka chalii yule mtegoni,na Isack alikiri ilo,akajiwazia
'kama asiponiua yapaswa nimuuwe mimi kauli ile ikampa nguvu akajinyanyua kwa ghafla na kujirusha akiachia teke ambalo hata ivyo jamaa alipanchu teke lile likapiga hewa,jamaa yeye akarusha teke lake Lililompata Isack Vyema mguuni Kikasikika Kikilia Kaaa,mwenyewe akaachia yowe na kwenda chini!,maumivu makali yakauvaa mguu ni kama ulivunjwa!...
"sikupenda kukufanya mlemavu ila umetaka!"
Isack aliisikia sauti ile kwa mbali!...
Ghafla akapoteza fahamu!...
SAI akabaki kutabasamu,akishangaa kitendo cha kumvunja mtu mguu tu kimempotezesha mtu fahamu,tena mwanajeshi alishangazwa kwa jambo hilo
MASAA KADHAA BADAYE
Wakwanza kuamka mezani pale alikuwa ni mzee Lyatuu,akidai ameshiba akaelekea zake chumbani kwake!,
Wakati akiwa chumbani huko sebuleni akasikia Sai akimweleza Katarina Juu Ya Kufanikiwa Kumteka Isack Na Kumpeleka hospitalini kwa lengo la kupasuliwa na kuvalishwa kifaa ambacho kingeweza kuonesha mahali ambapo yupo,hivyo ingekuwa ni rahisi kwake kufatiliwa pasina kujua kama anafatiliwa kwani mashine tu ndo zingetumika,siku hiyo ilikuwa jumatatu ilitegemewa huyo daktari kuingia nchini Jumatano,
Maneno yale kidogo yalimshtua Zidu!,wasiwasi Ukamvaa,moyo Ukaanza Kumsuta Kwa Kukumbuka kuwa ameaacha kilicho mleta na kuanza kufatilia wanawake,kwa mara ya kwanza akakumbuka kuwa aliacha udhaifu umvae,amesaliti pia *kiapo* alichokula mbele ya Rais,waziri Wake Wa Jeshi,ulinz Na Usalama Na Mbele Ya kijana Isack ambaye kama si kukataa kwake kuja naye pengine angekuja naye tatizo hilo lisingemkumba!
afanyaje sasa?!,jibu lilikuwa rahisi tu ilikuwa lazima aende Sheraton hospital akamsaidie Isack Kwa Kumtorosha kabla ajavalisha iko kifaa cha mionzi ambacho kingemuonesha kila mahali ambapo yupo!,kisha Waifanye Kazi Kwa Pamoja Na aachane na suala la mapenzi,eti likatingisha kichwa kuafiki swala lile!...
Ukwel Umweka Mtu huru, katarina Ni Kweli alimpenda sana Saimon,japo mwanzo alipanga kumwongopea kwamba ana mimba yake ila sasa aliamua kumweleza ukweli,akiwa na maana mbili!
Maana ya kwanza aliijua yeye mwenyewe,si mimi wala si wewe ila maana ya pili ni ili aone upendo wa Sai Kwake,kwa jambo lile angechukua maamuzi gani!
Baada Ya Mwanaume Zidu Kukubaliana Na akili yake kwa sasa kuachana kabisa na maswala ya mapenzi na kuianza rasmi kazi ilompeleka akijilaani kwa kufanya ngono zembe ilo mzamisha na kujikuta akipenda,tena akipenda haswaaa mpaka kufikia kuweka kazi pembeni!
"Sai mume wangu!...
Mchomo Mkali Wa Wivu Ukauchoma Moyo Wake,ni Baada Ya Kumsikia 'Kk' Mwanamke Ampendaye,akiliita Jina La Mwanaume Mwingine Kwa Mapenzi Mazito,akupenda Jambo Lile,ila akajizuia si alishapanga kuachana na mapenzi!
...Sory Kama ntakukwaza nimeamua tu nikwambie ukweli kusudi unipe ushahuri...
Maneno Yale Ya 'kk' Yakazidi Kuingia Kwenye Masikio Yake akatamani kuendelea kusikia,akatega sikio lake vizuri
"ehe nambie" Saimon akaafiki 'kk' akaendelea
.....nina mimba mpz wangu!..."
"waoooh!" ilisikika sauti ya furaha kwa Sai,
"ila Nahisi Hii Mimba niya Zidu sababu ile siku nlokutana naye ilikuwa ni ya hatari zaidi mmh na kitu alichonifanyia ilikuwa lazima iingie"
Paaaaaa,Sauti Ya kibao ikasikika!
"unasemaje wewe mpumbavu!,unajua sasa unaongea na nani,hiyo mimba lazima ukatoe siwezi lea mtoto haramu ambaye si damu yangu kama utaki utatoka hapa wewe mwanamke malaya sana wewe!...
"sasa hubby hayo yote yanatoka wapi?!,nimekwambia tu,ila mimi mwenyewe si kwamba nilitaka nikae na hii mimba naenda kutoa!"
Zidu Kule Ndani Moyo Wake Ulimwenda Mbio,furaha Iliutawala Moyo Wake,kwa Mara Ya Kwanza toka miaka mingi akamkumbuka mwanaye gidiony alokufa kwa kuuwawa yeye na mke wake Mery akajikuta akikumbuka mbali sana...
"mume wangu nina mimba..."
Siku hiyo wakiwa wanakula chakula cha usiku Mery
alimwambia mumewe Zidu anajihisi yu mjamzito,Zidu alfrahi akamkumbatia mke wake,akampiga mabusu!...
"yooh naitwa baba,yeeeh naitwa baba"
Alikumbuka Alinyanyuka Na Kucheza,akamnyanyua Mke Wake Mpaka Chumbani
"acha Beby Nikatoe Vyombo Mezani!"
"hapana Mpz Wangu,lala Umpumzishe Mwanangu,mimi Nitatoa Vyombo,mimi Ntadeki,mimi Ntakufulia,kukupikia Na Hata Kukuogesha Pia"
"mmmh beby!,waoooh furaha iliyoje mume wangu..."
Akajikuta Machozi Yenyewe Yakichurizika,alimpenda Sana Mery,na Aliishi Naye Kwa Upendo Na Amani Mpaka Waziri Wa Ulinzi Mh Alex alipo mwita ofisini kwake siku moja na kumpa kazi,kazi
ambayo iliharibu maisha yake na mwisho kukiteketeza kizazi chake!...
Leo hii tena mwanamke alozalisha bustani ya upendo moyoni mwake,anabeba mimba!,mwisho anataka aitoe,amtoe mwanaye wa pili! katika kizazi chake,hapana haiwezekani,
'Nala *KIAPO* sitokubali hili litokee nitailinda damu yangu kwa gharama yeyote ile,ilikuwa niondoke hapa sitaondoka,haiwezekani umtoe mwanangu!,napenda mtoto leo hii kirahisi tu umtoe nala nanyi sahani moja na NAAPA kabla sijamwangamiza raisi ikiwa mtatoa icho kiumbe hapo tumboni basi nitaanza na nyinyi'
Mwanaume Uso Wake Ukiwa Umejikunja Kwa Hasira alijiwazia!
"kesho ntakupeleka kwa daktari wangu akakutoe hiyo mimba kwa usalama zaidi!"
"sawa mume wangu"
'kwa ilo alitowezekana asee' ZIDU naye kule ndani akawaza akitabasamu,tabasamu lake lile baya lisilopendeza hata chembe!
Tabasamu lililojaa kiburi jeuri na dharau ya hali ya juu!,
Usiku Ule ulikuwa ushaharibika kwake,hata usingizi aukumea katika mawazo yake,angelala vipi hali ya kuwa kwa sasa alishajipachikia kazi ambazo azikuwa katika mlolongo wake,alibaki kuwaza hili na lile mpaka badae sana ndipo alipopata usingizi,ila ule wa mang'amung'amu!,
Kulipopambazuka,yeye alichelewa kuamka kama kawaida,alipoamka akanawa akajijumlisha na wenzake kupata chai,moyoni mwake hakuwa na furaha kabisa,wale wote pale mbele yake aliwachukulia kama maadui zake wakubwa wenye nia ya kumdhulumu uzao wake,kukosa kwake raha kukatafsiriwa
Ni Kwa Sababu aliipoteza familia yake,ila ukweli aliujua moyoni mwake,aliamini hata kama yeye alikuwa adui lakini mwanawe akuwa na hatia kwa nin Kata atake kumtoa,kwa siri sana akawa akiwakata jicho la chuki!...
"sasa Itabidi tutoke hapa tuelekee hospitali na kwa uzuri zaidi huyu huyu dokta ndo atafanya kazi zote mbili ya kwako na ya Isack"
Sai aliongea akijua yule mzee akuelewa kitu,ila Zidu Moyoni tu alibaki kuwacheka!
"kwani kazi hiyo itafanyikia katika nyumba maalumu au!"
"hapana!,ni hatari na nirahisi pia kumshtua Isack Pindi Atakapozinduka yapaswa tuifanyie katika hospital ya kawaida tu tena hosptal ya mkoa,kusudi akizinduka aendelee na kazi yake kama kawaida"
"ok!"
Wote Waliongea Pasina Kujua Yule Mzee alokuwa kimya,akijifanya macho yake yawe bize na tv,lakini masikio yake yalikuwa bize kuwasikiliza kile walichokuwa wakiongea!
"kwa hiyo anaingia saa ngapi!" kata aliuliza
"ameingia saa moja,asb kazi ya kwanza ni ya kwako ivyo yapaswa tuwayi"
"basi sawa,mi hapa hata nshashiba ngoja nkajiandae"
Ile ananyanyuka akashtuliwa na sauti ya babu...
"mjukuu wangu nami ulinihaidi leo utanpa ela nkanunue nguo!"
Kata akacheka "babu na wewe ila usijali ntakupa"
Akaingia Ndani Kama Umjuavyo Mwanamke Utumia Muda mwingi kujipamba,baada ya kuridhika akatoka,tayari Sai alishatangulia nje,akampa mkono wake,lengo Mzee lyatuu apokee zile ela!,
kugutanisha mikono yao,hisia flani zikaivamia miili yao!,bila ridhaa ya akili yake 'automatic' tu akajikuta mzee akibaki kaushika ule mkono akiusugua sugua!
"babu na wewe uzeeki tu niachie bhana ukikutwa na Baba Mwenye Nyumba" Kata Akaongea Kwa Sauti Ya Kudeka Akiwa Kamrembulia Mzee Jicho!
"mwili tu ndo wazeeka ila huku,pako full mjukuu wangu,ng'ombe azeeki maini!,"
Mzee akaongea akiuachia ule mkono wa binti yule,wote wakaachia kicheko,mzee lyatuu kama kata alivyo mtambua akashukuru,"asnte mjukuu wangu Mungu akuzidishie,akupe watoto wawili wawili tena mapacha" akamalizia huku akimkonyeza,
ITAENDELEA
Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (4)
Sehemu Ya Nne (4)
Kata akaitikia 'amin' huku akipeleka macho pembeni aibu,akaondoka zake!
Unajua Mapenzi Ni hisia,'automatic' hisia zao zilisha semeshana na mapenzi ni upofu,katarina Pindi alipogutanisha mikono yake na ya mzee yule,mwili wote ulimsisimuka,akajikuta akimkata jicho mzee lyatuu ambaye aliishia kukonyezwa,kilichomshangaza sasa 'Kata' Ni Uimara Wa Ile Mikono tofauti na mikono ya kizee,mikono ya kizee aikuwa imara vile,akakumbuka na zile sharubu pindi alipokuwa amezimia ni kama zilinatishwa!
hisia fulani zikaanza kumtembelea (machale) akapanga kuanza kumchunguza vizuri mzee yule!...
Wakiwa Ndani Ya gari kuelekea hosptalin waliendelea na stori zao za kawaida,'kata' akumgusia mwenzake juu ya kuanza kumtilia mashaka,aliamua kufanya siri yake kwanza!,na hata kama ni yeye,alipanga kumkamata,kumfikisha pasina msaada wa askari yeyote ili amwoneshe Rais Silvestar juu ya uwezo wake na kumtoa kule katika kesi ile amekosea tena,amekosea sana!...
Baada Ya Kk Na Mwenzake Kuondoka,mzee Lyatuu Naye akutaka kupoteza muda,kk alimkabidhi laki na arobaini na tano akatoka,mgongoni akiwa na begi lake,akaelekea nje,alipochukua boda boda,ilompeleka mpaka katika duka kubwa la shriivedge,duka lililosifika kwa kuwa na nguo nzuri!,akashuka juu ya bodaboda ile!
"babu nikusubiri?!" mwendesha bodaboda yule alotoka naye nyumbani akaoji!
"hapana ntakupigia simu!"
Mzee akajibu huku akizidi kutembea,bodaboda yule akashtuka,mzee yule hata namba zake akuwa nazo angempigia simu kivipi!...
akajua ni uzee,pengine Kuna Namba Ya Bodaboda alishaichukuaga pale kituoni ila akajisahau!
Akaamua Kumsubiria Palepale!
Mzee Lyatuu baada ya kuingia kule ndani,alichagua suruali moja tu,akaomba akaoneshwe chumba cha kubadilishia,akaoneshwa,huko sasa ndo palikuwa sehemu salama ya kubadilisha nguo,tofauti na pale nyumbani kulikozagaa mikamera ya kila dizaini,akatoa sharubu zile,akavaa tishart yake vizur na jeans chini raba kali kichwani boshori!,na mawani zile nguo za kizee akazi ingiza katika begi,akatoka nyuma ya duka lile palipokuwa na makaz ya watu akaulizia choo,kuingia akakuta choo ndo iko iko bafu na kuna sabuni,akatoa bushori na kunawa kichwa vizuri,kutoa yale marangi ya mvi!...
Sasa alikuwa mtu mwingine kabisa!
'Sheraton hosptal' akawaza akijua sasa ndo safari ya kuelekea huko!...
kwa kuwa ile nyumba aloombea chooni yani ndo ilikuwa ikimiliki ile frem ya duka nikiwa na maana duka lipo mbele,pakubadilishia nguo katikati pakiwa na milango miwili,wa kuelekea dukani,na kuelekea uwani,yani katika nyumba kubwa,hivyo kwa wateja iliwapasa wakitoka chooni,lazima warudie njia ya dukani kukwepa kutolipa!
Na Ndivyo Zidu alivyofanya, aliporejea dukani kwa kuwa yeye alishalipa mwanzo,akuangaika tena kumfata muuzaji,ila muuzaji alishtuka kumuona akamwita!,ZIDU kugeuka muuzaji alishtuka,kwa kuwa ndani kule akukuwa na wateja,kilichofatia kwa muuzaji yule Mungu Pekee Ndo Anajua!
"oya Broo!" Alimwita Zidu Akageuka,
Muuzaji Akatoa Macho Pima
"z..z...z"
Zidu akumpa muda wa kumalizia kutajwa jina lake,akakisambaratishia mbali kifua chake!
Mwanaume Akachukua Koti Moja La Kofia Akavaa,akaficha Sura Yake Akatoka!
Nje Alishtuka Kumuona Yule Boda Boda Akimsubiri!...
Boda Boda Naye alishtuka,kumuona yule mtu,kilicho mshtua zaidi ni lile begi!,begi kama la mzee alomleta!
"mzee lyatuu"
akaita kwa nguvu,ila zidu akugeuka,akafanya kosa kubwa sana la kumfata
kosa!
TUSONGE......
Pengine Akujua yule ni mtu wa namna gani!,ni hatari kiasi gani!,
Matokeo yake akazidi kuongeza mwendo wa pikipiki yake kumfatilia,mtu yule wala akuongeza mwendo ndani ya akili yake alishajua cha kumfanyia,tayari alishamwona hatari katika maisha yake!,hasa kwa mipango yake! alipomfikia kabla ajamsemesha kitu kwa haraka mtu yule akaruka nyuma juu ya pikipiki yake na kumnong'oneza!
"mwanangu nimeiba mamilioni humu ndani,embu nisave nitoe hapa ntakutoa fungu la maana"
Zidu akaongea kwa kusihi,dereva yule wala akufikiria mara mbili!,alichofanya ni kuongeza mwendo wa pikipiki yake!,
"tuelekee wapi bro?"
"katika pagara bovu bovu,au nyumba ambayo aijamalizwa,tugawane huu mpunga! mbal na polis na macho ya watu!
"yah nimekumbuka,kuna hifadhi ya maliasili hapo chini itakuwa sehemu nzuri zaidi!"
"si mbali na hapa?!"
"wala hata! si mbali ni hapo tu,kuna kama kapori"
'yaaaas! kifate kifo chako shetan wewe utakoma kuwafatilia wanaume!' Zidu Likawaza Kisha Likatasua Domo Lako
"inaonekana Patakuwa Pazuri Zaidi Ongeza Mwendo Ninja Kabla Wajomba awajatufatilia"
Bodaboda Yule akujibu kitu akazidi ongeza mwendo maskin,pasina kujua anakiwah kifo chake,tayari ubongoni alishafikiria vitu vya kununua!
'kama akinipa milion kadhaa kwanza namfungulia Secy Saluni aache kunisumbua,namalizia nyumba yangu na mwisho kwa furaha yani namnunulia mwandish Maruma Kompyuta Ya Maana Kama Sapraiz aache kuandikia andikia visimu' akajikuta akitabasamu mwenyewe,na kuzidi kuongeza mwendo!
Dakika Tano Waliingia Katika ako kapori,kusimamisha tu Zidu Akashuka,ile Naye Kashuka ghafla alipokelewa na teke liitwalo,judko!,
hili ni teke lirushwalo kidevuni,yani juu kidogo ya shingo na ukipigwa ni lazima upeleke kichwa juu!...
Niteke ambalo lina maumivu makali,na watu wengi utumia teke hili kwa nadra!
Zidu baada ya kurusha teke lile akushusha mguu chini aliupiindisha nyuma,kama anaufanyisha zoezi alipounyoosha ni moja kwa moja kifuani jamaa akadondokea boda boda yake,akiachia yowe!...
"niliapa kila atakayeingia kwenye njia yangu awe aduhi yangu au rafiki yangu sitomuacha hai,kwa bahati mbaya nawe pasina kujua umejiingiza katika domo la mamba unategemea atakuacha hai mpumbavu wewe?"
Zidu alimwambia huku akimtazama usoni jamaa yule ambapo alikutana na mkunjo wa sura ya maumivu,ni kama akusikia kile ambacho Zidu alikuwa akimwambia!...
Zidu akaruka hatua moja hatua ya pili alikuwa pale ambapo bodaboda kaangukia juu ya pikipiki yake akiugulia maumivu!
Akaunyanyanyua mguu wake juu kidogo tu,boda boda akaweka mikono yake mbele ya uso wake,sasa sijui ni kujaribu kuomba msamaha,au ni kuuzuhia ule mguu wa zidu!
Zidu Kuona Ivyo akakapiga ako kamguu teke kisha ule mguu wake ulobeba kiatu aina ya raba akaudondoshea shingoni mwa bodaboda yule,akawa anausigina bila huruma,
Ninaposema Zidu Katili Ni Katili Kikweli Kweli,jicho alilitoa tayar alishageuka 'izrael wa kibinadamu' akazidi sigina akitumia nguvu zake,mtu yule akaanza tupa tupa miguu na mikono akiushika mguu ule wa Zidu kujaribu kuzuia,macho kayatoa akiung'ata ulimi kupigania roho yake!
Jamaa Lile Likaendelea Kusigina mpaka alipoakikisha katulia ndipo alipotoa guu lake!...
Jamaa alikufa kifo kibaya sana hata kumwangalia usoni alitisha,aliyatoa macho kwa mshangao ulimi kaung'atia!,Zidu akaokota kakipande cha mti,akatoboa toboa macho yake!,kusudi sura yake isibaki katika macho yake!
Akaifata Pikipiki akapanda na kuiwasha,akapotea maeneo yale!...
Robo Saa badaye alikuwa nje ya hospital ile ya 'sheraton hosptal',akashuka kwenye pikipiki kichwani kwake akiwa na mawazo je atamkuta Katarina bado ajafanyiwa 'abortion' kunyofolewa kiumbe chake kile?!...
haraka sana akachepuka kuingia ndani ya jengo la hosptal ile!...
Alienda moja kwa moja mpaka mapokezi,
"samahani dada,kuna dokta mmoja danny masley kutoka nje ya nchi amenambia ameingia jana nchin unawez kunkutanisha nae?"
Dada Yule Akamwangalia Mwenzake!
"Monny dokta masley kashaingia wodini?!"
Dada Yule akamuuliza msichana mmoja alotambulika kwa jina la monica,aloingia mule ndani muda ule ule
"yah! kama dakika tatu hivi kaingia privet room"
"ok kaka inakupasa umsubiri!"
"ok dada!,ok,samahani ofisi yake iko wapi? au icho chumba kipo wapi nikamsubir nje na shida naye kubwa sana nisaidie!..."
Wadada Wale Wakaangaliana!,kwa Mshangao
"nakuomba Dada Yangu Ukaniitie C hukua hata hii ile"
Akatoa Pochi Yake Na Kuwaesabia 50000 akawapa!,dada wale wakabaki kushangaa kwa bahati nzur apakuwa na mtu mwingine katika dirisha lile la mapokezi!
"Monica mpeleke bas pengine anashida kubwa!"
Yule Dada Mmoja aliongea kwa kusihi akizitazama zile ela tayar alishajihesabia ana sh 25000
"lakini Elly Si Unajua Ni Kinyume Na Kazi"
Monica aliongea kwa majonzi,
"kweli dada yangu nashida nae kubwa sana,we nsaidie ntakulinda"
Zidu akazidi kusihi,penye udhia penyeza rupia,akatoa hamsini nyingine akawatupia mezani,safari hii awakuongea chochote kila mtu akachukua 50 yake! akaisweka anapopajua yeye!
"nifate"
Monie akamwambia Zidu!,ZIdu akamfata!
'mtu asipite huku' kulikuwa na kibao kilichotaadharisha mshale wake ukielekezea chini!,ikiwa na maana huko ni chini ya ardhi,wakazikwea ngazi wakawa wanashuka,kwa kasi sana!...
"tuwah dada huyo ni mke wangu anataka chomoa mimba yangu ivyo nataka nimuwah kabla ajatoa!"
Zidu aliongea kwa lengo la kumsisitizia kusudi wawahi!,akisahau mwongo yapaswa awe na kumbukumbu!,ghafla yule dada akasimama sura kaikunja!
"mbona unasema unashida na Dani?,mara Huyu Ni Mkeo?,toka Lini Katarina Akawa Mke Wa Mtu,mpumbavu Sana Wewe Chukua Pesa Zako Na Usinizoe,usijekunikosesha kibarua changu!,akamtupia ile 50 usoni,akageuka sasa akawa anarudi juu,akimwacha Zidu Limeganda Kama Sanamu La Michelin!....
TUSONGE......
Mbona unasema unashida na Dani?,mara Huyu Ni Mkeo?,toka Lini Katarina Akawa Mke Wa Mtu,mpumbavu Sana Wewe Chukua Pesa Zako Na Usinizoe,usijekunikosesha kibarua changu!,akamtupia ile 50 usoni,akageuka sasa akawa anarudi juu,akimwacha Zidu Limeganda Kama Sanamu La Michelin!....
Ghafla akili ya Zidu ikarudi,akainama kwa haraka na kuokota zile ela akazisweka mfukoni,
"Sasa utanipeleka hiyo wodi aliyoko dokta au niusambaratishe ubongo wako"
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment