Search This Blog

Thursday, 29 December 2022

CODE X 5 N.G.S.S. (NEXT GENERATION SUPER SOLDIERS) - 2

   

Simulizi : Code X 5 N.g.s.s. (Next Generation Super Soldiers)

Sehemu Ya Pili (2)


“Scarlet, ni muda mrefu sana hatujaonana” alivunja ukimya Alex, “ndio ni siku nyingi sana” alijibu Scarlet. “Adrian naona umri unakutupa mkono” alimgeukia Adrian na kuongea, “jiangalie na wewe pia” Adrian alijibu na wote wawili wakacheka na kupeana mikono. “Christina au nikuite Darling” aliongea Scarlet, “Christina, Darling nimeliacha muda mrefu sana. Nimestaafu, nimeamuwa kulea watoto wangu tu” alijibu. “Ni jambo jema, maana nimezaa mmoja tu na hata hivyo sijakaa nyumbani hata kumlea” aliongea Scarlet.


“Kuna mengi sananataka tuongee, lakini kwanza tumalize hii sherehe halafu tutaongea vizuri” aliongea Alex, sherehe ikaendelea mpaka mwisho. Watu wakaanza kutawanyika, na baada kama ya saa nzima hivi watu wakawa wameondoka ukumbini. “Adrian na Scarlet, kuna mazungumzi kidogo” aliongea Alex, wakaondoka ukumbini hapo na kuelekea katika hoteli nyingine. Wakachukuwa ukumbi mwengine mdogo ambao ulikuwa maalum kwa vikao vya siri sana.


“Scarlet, Adrian tunfaruhi sana kuwaona. Tulitaka sana kuwatafuta lakini jambo gumu kama kuwasaka wachunguzi wa siri wa kimataifa (SPY)” aliongea Alex. “Ah! Hata sisi tumejaribu sana kuyatafuta mawasiliano yenu lakini pia imeshindikana hasa ukizingati muda tunakuwa nje ya nchi kikazi” alijibu Adrian na kutabasamu. “Lakini ni jambo jema kwamba tumekutana kupitia vijana wetu” aliingilia Jeff, “kweli kabisa” aliongea Scarlet.


“Sasa kuna jambo tunataka tuongee, ni jambo kubwa sana na kwa kiasi kikubwa linatuhusisha sisi wote kama tulivyokuwa mwanzo” aliongea Alex na kuendelea “natumai hivi karibuni mumesikia mambo mengi sana yakiendelea. Ni kweli hayo mambo yapo na ndio lengo letu la kuwaita. Tunahitaji nguvu yote katika ubora wake, tunahitaji watu zaidi ili kupambana katika hii vita. Vita ambayo itakuwa ya mwisho kupiganwa katika wakati huu”. “Lini mnategemea kuibumburuwa” alihoji Adrian, “tumeshaianzisha na kuwajeruhi sana waasi, labda ndani ya miezi miwili na wao watarudi ulingoni kuja kulipa kisasi” aliongea Jeff.


“Sawa, sisi ni ndugu katika medani za kivita. Na ndugu wanapohitajika hujitokeza na kufanya kile ndugu wanachotakiwa kufanya. Ndani ya wiki moja nitahamisha vikosi vyangu vyote na kuvileta kambini kwenu, alitutafuta na atatupata. Kachezee sharubu za panya na sio simba kwa sababu atakuuma” aliongea Adrian na kutoa bastola kiunoni na kuiweka mezani. Wengine nao wakafanya hivyo kama ishara ya kuungana tena kwa mara ya pili. Gold Prime General Alex, Supreme General Commando Jeff na Silver Fox General Adrian, majina hayo yalisomeka kwenye bastola tatu zilikuwepo mezani hapo.


“Black Hawk Ghost Pirates (BHGP) ndio jina la kikosi chetu kipya, na operesheni hii itaitwa DESASTER (JANGA). Alex atakuwa Supreme General, Mimi jenerali wa kwanza na Adrian ni jenerali wa pili” aliongea Jeff. Akaendelea “kuanzia sasa kutakuwa hakuna kikosi Ghost, Pirates wala Black Hawks mpaka pale kazi hii itakapokamilika. Hii huenda ikawa vita yetu ya mwishona tutakufa acha tufe tumetabasamu” alimalizia na kutoka magazine kwenye bastola yake. Alex na Adrian nao wakafanya hivyo na kisha wakabadilishana risasi. “Tutapigana mpaka mtu wa mwisho” waliongea kwa pamoja.


“Mhh! Sijawahi kuona watu pasuwa kichwa kama hawa” alijisemea CJ ambae alikuwa ameketi kimya wakati wote huwo. “Hii huenda ikaandikwa kwenye historia ya ulimwengu, Mungu awasaidie wanaodhani watachezea amani ya dunia na wakaondoka salama” aliendelea kujisemea kichwani. “Ndani ya wiki moja nitakutumieni ujumbe utakaowaelekeza kambi mpya” aliongea Jeff na kuwaangalia wote wawili. Wakatisa vichwa kuashiria kukubaliana nae. Kikao kilivunjwa na wote wakatawanyika na kila mtu kuelekea kwake kwa ajili ya kupitisha usiku huwo ambao tayari ulishakuwa mkubwa.

********************************************************************

Sehemu isiojulikana.

“Unajisikiaje mpenzi wangu” aliongea Michael akimuangalia Alice alienza kufumbuwa macho baada ya usingizi wa siku tatu. “Najihisi mweny nguvu sana” alijibu Alice na kujivuta kisha akakaaa kitako kitandani. Michael akasimama na kuchukuwa kioo kilichokuwepo chini, akamasogezea karibu na usoni. Alice alitabasamu baada ya kujiona mschana mbichi kabisa. Huwezi amini kama Alice huyo huyo siku tatu zilizopita Alikuwa mtu mzima wa miaka hamsini na tatu. Wakati huwo alionekana kama binti wa miaka ishirini na kidogo.


“Si ulinambia unanipa mwili mwingine” alihoji, “nilitaka kufanya hivyo ila nikaona haina haja kwasababu nimefanikiwa kutengeneza kemikali ambayo inazipa seli nguvu ya ujana. Si unajuwa kadiri umri unavyokwenda ndivyo miili yetu inavyozalisha seli chache sana ambazo zinatufanya tuzeeke. Kasi ya kufa kwa seli ni kubwa kuliko kasi ya kuzaliwa. Sasa mimi nimetengeza kemikali inayofanya kinyume na hivyo, kemikali hii inapunguza kasi ya kufa kwa seli na kuongeza kasi ya kuzaliwa kwa asilimia tisini na tano hivyo kutufanya tuwe vijana kumuonekano na nguvu lakini umri mkubwa” alifafanuwa Michael.


Alice alibaki ameshangaa maana hakutegemea Michael awe na akili kiasi hicho, kwasababu tokea alivyomjuwa alikuwa akiishi na mwili wa bandia ambao ulikuwa umebeba uwezo wake halisi wa akili japo ulionekana kutokuwa mkubwa kivile kutokana na mwili huwo kukosa mambo ya msingi ambayo binaadamu anayahitaji. “Vaa tuanze kazi, hakuna muda wa kupoteza na kazi ni kubwa sana” aliongea na kumrushi nguo. Alice alizidaka na kuvaa kisha akasimama na kujiangalia umbile lake lililomkumbusha kipinid akiwa mschana mdogo tu.


Michael akiwa anaongoza, walitoka chumbani humo. “Tunaelekea wapi huku maana hakuna njia” aliuliza Alice. “Wewe nifuate tu, kuna kitu nataka nikakuoneshe” aliongea na kuongoza. Walifika mwisho kabisa wa koridoo hiyo ambako kulikuwa na ukuta. Michael akapapasa katika ukuta na kubonyeza sehemu, ukuta ulifungua na kutoka kimashine fulani kama kompyuta. “Enter password” yalisomeka maneno hayo kwenye kioo cha mashine hiyo. Akavuta kicharazio (keyboard) na kuanza kuandika password. Alice alipigwa na butwa baada kuona jinsi password hiyo ilivyokuwa ndefu na yenye kuchanganya.


“Welcome Michael” ilisikika sauti kutoka kwenye mashine hiyo na sehemu ya chini ikaanza kufngunguka na kuonekana ngazi iliokwenda chini na kupotea huko kutokana na kiza kikubwa sana. “Nifuate” aliongea na kunza kushuka ngazi hizo. Walitembea kwa dakika kumi na tano mpaka walipofika chini kabisa. Kulikuwa na mlango mwiningine, Michael akabonyeza sehemu na huwo mlango ukafunguka. Akapiga kofi mbili na taa zikaanza kuwaka, Alice hakuamini macho yake kama kulikuwa kuna kitu kama hicho chini ya eneo ambalo amekuwa akifanya kazi kwa zaidi ya miaka thalathini sasa.


Mbele yake kulikuwa na majokofu mengi sana, na ndani walionekana watu wakiwa wameganda kutoka na baridi kali iliokuwemo ndani ya majokof hayo. Yalikuwa ni mengi kiasi cha kushindwa kuyaona mwisho wake. “Yako mangapi haya” aliuliza, “elfu tatu mia tano na hamsini”. “Lakini sikuja haoa kukuonesha haya” aliendelea na kuanza kutembea mpaka kwenye mlango mwingine. Akaingiza Password na mlango huwo ukafunguka. Ndani humo kulikuwa na majokofu mengine matano na yalionekana kuwa ni makubwa sana. “Hawa ni kina nani” aliuliza kwa shauku ya kutaka kuwajuwa, “hawa ndio majenerali watakaongoza kikosi changu. Kutana na Alfred Jackson, Matvei, Jason CJ, Alex mkubwa na Andrew Cross.” Alijibu na kucheka kwa nguvu tena kicheko hicho kilijaa ubaya, ghadhabu na chuki.

INTERMISSION



Mbele yake kulikuwa na majokofu mengi sana, na ndani walionekana watu wakiwa wameganda kutoka na baridi kali iliokuwemo ndani ya majokof hayo. Yalikuwa ni mengi kiasi cha kushindwa kuyaona mwisho wake. “Yako mangapi haya” aliuliza, “elfu tatu mia tano na hamsini”. “Lakini sikuja haoa kukuonesha haya” aliendelea na kuanza kutembea mpaka kwenye mlango mwingine. Akaingiza Password na mlango huwo ukafunguka. Ndani humo kulikuwa na majokofu mengine matano na yalionekana kuwa ni makubwa sana. “Hawa ni kina nani” aliuliza kwa shauku ya kutaka kuwajuwa, “hawa ndio majenerali watakaongoza kikosi changu. Kutana na Alfred Jackson, Matvei, Jason CJ, Alex mkubwa na Andrew Cross.” Alijibu na kucheka kwa nguvu tena kicheko hicho kilijaa ubaya, ghadhabu na chuki.


“Hawa watu wote si walishakufa kitambo, wewe umewapataje?” aliuliza Alice, “hawa sio wenyewe halisi bali ni vivuli vyao (clones) lakini wanafanana kwa asilimia tisini na tano wenyewe” alijibu Michael na kuzidi kumchanganya Alice. “Najuwa hujafahamu nilichoongea, ngoja nikueleze kwa kituo mpaka hivi leo” aliongea na kuendelea “baada ya kuungana na Matvei nikiwa mdogo kabisa na kuonesha uwezo wa akili usio wa kawaida ndipo akaamuwa kunionesha jambo ambalo hakuwahi kumuonesha mtu”.


Karibu miaka arobaini iliopita.

“Michael, umewahi kuwaza kuishi milele” aliongea Matvei na kumuangalia Michael, “Hapana sijawahi kufikiria” alijibu Michael. “Mimi nimefikiria ikiwa nitakufa kabla sijatimiza lengo langu itakuwaje, na hapo ndipo nikafikiria njia ambayo itaniwezesha kuishi milele”, “utawezaje kufanya hivyo” Michael alionekana kuvutiwa na jambo hilo. “Kwa kutengeza kivuli changu”, “kivuli?”.

“Ndio Michael”

“Bado sijakuelewa vizuri”

“Iko hivi, kwa kuchukuwa seli katika mwili wangu ambazo bado hazijajitanabahisha kwa kazi fulani nikiwa na maana kuwa zinaweza kujitengeza kuwa seli yoyote ile katika mwili pale zitakapohitajika kufanya hivyo. Kwa kuziweka katika mazingira ambayo yataruhusu seli hizo kuishi, nitaziprogramme zitengeze viongo mbali mbali vya mwili na mwishoe kuukamilisha mwili mzima”.


“Sasa seli hizo zitawezaje kukutengeza wewe mwenyewe zikiwa nje ya mwili wako?” aliuliza Michael. “kila seli katika mwili inabeba kumbukumbu halisi ya mtu na kila kitu chake na hii ndio inayompa kila binaadamu muonekano wake. Jambo hili litachukuwa muda lakini tayari nimeshaanza kazi, na ikitokea siku nikauwawa au nikafa. Kazi hii utaendelea nayo wewe mpaka itakapokamilika, tatizo kubwa linakuja kwenye kuipa uhai miili ya bandia itakayozaliwa kwa njia hii. Hilo mpaka sasa ndilo linaloniumiza kichwa. Ila nina imani kuwa ipo siku wewe utapata jibu, twende ukaone” aliongea na kuongoza njia.


Walitembea mpaka chumba fulani na kuingia, ndani kulikuwa na mashine nyingi sana zilizokuwa zikifanya kazi zenyewe. Matvei alienda mpaka kwenye friji kubwa na kutoa vichupa vitano, kila kichupa kilikuwa na jina nje. “Hizi ni seli za watu wenye uwezo mkubwa sana, ambao nimeshindwa kuwashawishi waungane na mimi katika harakati zangu za kufanya mapinduzi katika dunia hii. Kwa vile nilishindwa kuwashawashi na pia sikuweza kuwaacha wawe hai kwasababu wangeniharibia malengo yangu” alinymza kidogo.


“Ila sikutegemea kama angetokea mtu mwengine kama Alfred Jackson, ambae alikuwa kikwazo kikubwa kwangu. Ghost, kwasababu nisizozifahamu huyu mtu ana nyendo kama za Alfred Jackson na kwasasa ndio kikwazo kikubwa sana kati ya mimi na ndoto yangu na sina uhakika kama huyu nitaweza kumuondoa” alionesha wasi wasi wa hali ya juu. “Hivyo Michael lolote litakalotokea ni juu yako kusimamia kazi yangu na kumalizia kazi nilioanzisha.

*********************************************

“Hivyo ndivyo Matvei aliyokuwa” aliongea Michael na kumuangali Alice kisha akaendelea, “tokea siku aliokufa nimekuwa nikisimamia kile alichonambia mpaka leo na haya ndio matunda yake. Lilibaki ni kuwapa uhai tu ili watimize lengo nilillowatengenezea.”. Alice alibaki kimya asijue aongee nini maana macho ya Michael yalimpa majibu yote aliokuwa akiyahitaji baada ya hadithi aliomsimulia. “Sawa nimekuelewa, je? Umepata njia ya kuwapa uhai maana bila hivyo hao ni midoli tu”, “ndio maana nikatengeneza kemikali ya NEN, kemikali hii itatumika kama damu katika miili yao. Mimi sihitaji hisia zao bali nahitaji uwezo wao na ndio itakayowapa uhai japo kwa mud mfupi.

“Kivipi” aliuliza Alice, “kuna vitu maalum katika kemikali hiyo, ambavyo vinatumika kuuma mwili uwezo wa kibinadamu. Vikiisha tu mwili utaanguka na kurudi kuwa kama awali”. “Sasa si utaongeza tu kemikali”, “haitawezekana, kwasababu kemikali hiyo inaharibu kila kitu katika mwili ni kama moto tu” alijibu. “Oh! Sasa inatumika kwa muda gani”, “miezi mitatu tu ndio mwisho, hivyo hii vita haitakiwi kuzidi muda huo tutakuwa katika hasara” alijibu Michael.


Ziwa Tara, kusini mwa nchi ya RDC.

Ziwa ambalo linalotambulikana kuwa ni kubwa kuliko yote katika nchi hiyo, kwa muonekano lilionekana la kawaida lakini sivyo. Mita mia tatu chini kwenye sakafu ya ziwa hilo kulikuwa na mawe makubwa sana, miongoni mwa mawe hayo kulikuwa na jiwe lililoonekana kuwa na maandishi kadha na yalisomeka “BHGP HQ” makao makuu ya kikosi kipya kilichoundwa siku chache nyuma cha BHGP. Chini ya sakafu ya ziwa hilo ndio jambo kubwa na la maajabu. “Mkuu” alifika mtu mmoja na kuita, “tayari tumeshaitanuwa sehemu hii kuwa sawa na ziwa lenyewe”. “Vizuri, sasa endeleeni na sehemu ya pili ya kutandika vyuma vya kuzuia sakafu ya mto kupasuka” aliongea kiongozi huyo na kutabasamu. “Ndani ya miezi mitatu kambi itakuwa imekamilika.


Sector Zero Ghost layer.

Katika simu ya Jeff unaingia, “fika nyumbani kwangu” Mr Aby. Aliurdhisha simu mfukoni na kuondoka mpaka sehemu ya gari. Aliingia kwenye gari na safari ya kuelekea nyumbani kwa raisi mstaafu, Mr Aby au Abykin Dos Santos Juniour. Kichwani mwake alikuwa akiwaza juu ya wito huwo wa kushtukiza, aliwaza mambo mengi lakini akaona haina haja kuwaza sana maana atajuwa alichoitiwa akishafika huko. Aliingia barabara kuu na moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Mr Aby. Alipofika, alishuka na kumkabidhi funguo mtu aliekuwepo yeye akaelekez ndani.


“Jeff amefika” aliingia mtu mmoja chumbani kwa Mr Aby na kutoa taarifa, “mwambie apite” alijibu. Baada ya sekunde kadhaa Jeff aliingia chumbani na kutoa salamu. Mr Aby alikigeuza kiti chake na kumuangalia Jeff. “Kitambo sana hatujaonana” aliongea, “ndio, mambo yalikuwa yakipandana juu kwa juu. Nisamehe kwa hilo”. “Usijali kijana, sijakuita hapa kuja kukuuliza kwanini hujaja, laa. Kuna jambo muhimu sana ambalo nimeligunduwa baada ya kupitia baadhi karatasi za uchunguzi zilizoachwa Chief Supreme Commando Alfred Jackson. Na ndilo jambo ninalotaka tuongee” aliongea Mr Aby.


Jeff akavuta kiti na kukaa maana alifahamu mpaka ameitwa, jambo analotaka kuambiwa si dogo. Mr Aby akafunguwa droo kwenye kweny meza yake na kutoa bahasha, akampatia Jeff. Aliipokea bahasha hiyo na kuifunguwa, ndani kulikuwa na nakala nne zenye maandishi na mbili zenye mchoro. Alizipitia zote kwa umakini na kadri alivyokuwa akiendelea kuzisoma ndivyo mapigo ya moyo wake yalivyokuwa yakiongezeka kasi. Kijasho chembamba kilianza kumchuruzika japokuwa ndani ya chumba hicho kulikuwa na kiyoyozi.


“Hilo ndilo jambo lilikuchukulia baba ako Jeff” aliongea Mr Aby Jr na kumuangalia Jeff akihema kwa hasira na kuendelea “baba ako alitaka aimalize vita ambayo munakwenda kuianza nyie kabla hata haijaanza lakini Matvei alimuwahi. Kutoka na taarifa hizo, si rahisi wanajeshi wa kawaida kupambana na jeshi la Matvei ambalo bila shakwa kwa sasa linakwenda kukamilika, aliliita NEXT GENERATION SUPER SOLDIERS. Nadhani unafahamu namaanisha nini mpaka sasa, kupigana na kiumbe kisicho kawaida na wewe unahitaji jeshi lisilo la kawaida”.


“Nafahamu sana ila swali ninalojiuliza, hilo jeshi lisilo la kawaida sijui nitalitoa wapi. Maana kwa taarifa zilizokuwemo kwenye karatasi hii ni wazi bila kuwa na kikosi cheny uwezo mkubwa hatuwezi kushinda hata kwa kuufikiria tu”. “Hilo nakuachia wewe, we unataka mimi nifanye nini” aliongea Mr Aby, “naomba unisaidie kufikisha taarifa za vita hii kwa mheshimiwa raisi, ikiwezekana watu waodolewe katika mji mkuu. Kutokana na maelezo ya Chief Suppreme Commando, huenda vita ikapoga katika mji mkuu” aliongea Jeff. 




“Nafahamu sana ila swali ninalojiuliza, hilo jeshi lisilo la kawaida sijui nitalitoa wapi. Maana kwa taarifa zilizokuwemo kwenye karatasi hii ni wazi bila kuwa na kikosi cheny uwezo mkubwa hatuwezi kushinda hata kwa kuufikiria tu”. “Hilo nakuachia wewe, we unataka mimi nifanye nini” aliongea Mr Aby, “naomba unisaidie kufikisha taarifa za vita hii kwa mheshimiwa raisi, ikiwezekana watu waodolewe katika mji mkuu. Kutokana na maelezo ya Chief Suppreme Commando, huenda vita ikapoga katika mji mkuu” aliongea Jeff.

********************************************

Miezi mitatu sasa imekata na hakuna jambo lolote lililotokea, BHGP HQ ilikuwa ndio inaelekea kukamilka. “Jeff ndani ya siku mbili kambi hii itakuwa imekamilika” aliongea mkufunzi mku aliekuwa akisimamia. “Vizuri ngoja niwatumie ujumbe wengine ili waanza kusogea nchini” aliongea Jeff na kuondoka. Kwa kutumia njia za chini, alipanda gari yake mpaka sehem fulani. Ukuta mkubwa wa eneo ukafunguka, alitokea ndani ya nyumba sehemu ya kuwekea gari.


Ukuta ukajifunga, Jeff akabonyeza kitufe kwenye gari yake na geti kubwa likafunguka. Alitoka kwenye nyumba hiyo na kuelekea nyumbani kwa raisi mstaafu, Mr Aby Jr. “Jeff, karibu. Maandalizi yanaendeleaje” alimkaribisha na kuongea. “Kila kitu kinakwenda kama tulivyopanga” alijibu na kukaa kwenye kiti, akaendelea “vipi huko serekalini?”. “Ah! Nimewafikishia taarifa lakini wengi akiwemo raisi wanaonekana kuwa wazito katika jambi hilo”, “nilijuw tu hilo litatokea kwasababu ya kuwa na amani kwa muda mrefu sana. Kiasi inakuwa vigumu kuwashawishi kuwa ipo siku kutatokea machafuko”.


“Il usija…”, “achana nao, nitamalizana nao mimi” alikatishwa na Jeff. “Wewe umeshajiandaa”, “ndio”. “Utaenda nchi gani” aliuliza Jeff. “Nimefikiria sana, nimeona niende Afrika. Kuna nchi moja nimeisoma mtandaoni na inaonekana ina vitu vya asili vingi sana na mambo ya kitalii” aliongea Mr Aby Jr. “Nchi gani hiyo, Afrika Kusini au?” aliuliza Jeff. “Kwani unaposikia Afrika, unafikiria kuna Afrika Kusini tu, laa zipo nyingine nyingi tu zenye mandhari mazuri na kuyavutia kuliko Afrika Kusini.”


“Najuwa lakini sidhani kama utakuwa salama katika hizo nchi” aliongea Jeff na kuonesha wasiwasi wa hali ya juu. “Nitakuwa salama, hakuna atakae juwa nimeenda wapi kwa hiyo usijali. Nitaenda Tanzania kufanya utalii kidogo” aliongea Mr Aby Jr na kutaja nchi anayokusudia kuenda ili kuepuka vurumai ambalo litatokea wakati wowote ule. “Kama ni hivyo basi sawa, ikibidi uondoke mapema”, “safari yangu ni mwisho wa wiki hii, nchi hii nitaiyacha mikononi mwako, kama itaanguka anguka nayo” aliongea Mr Aby Jr na kupiga saluti. Jeff akasimama na kufunga mguu kwa ukakamavu kisha akarudisha saluti hiyo na kuongea “hii nchi ilipiganiwa na babu na baba zetu ili iwe huru, na mimi nitapambana na sitaanguka mpaka nihakikishe waasi nimewafuta kwenye uso wa dunia, hiyo ni ahadi.”.


Ahadi hiyo iliwekwa kati ya makomando wawili, Mr Aby Jr alitabasamu na kumuangalia Jeff usoni. “mtoto wa nyoka ni nyoka tu” akajisemea moyoni. Baada ya kikao hicho Jeff aliondoka nyumbani kwa Mr Aby Jr na kuelekea Sector Zero Ghost layer.


Sector Zero Ghost layer

“Martina watumie ujumbe kina Alex na Adrian, tutakutana jumamosi ya wiki hii” aliongea Jeff na kuka kwenye kiti chake. Akachukuwa simu yake na kuwatumia ujumbe makomredi wake wote, Charlie, Talbot, Alfred, Janeth na Anitha waliwasili dakika moja baadae baada ya kupokea ujumbe huwo. “Kuna mambo nataka tuongee lakini hatuwezi kuongea pekeetu. Ni lazima Alex na Adrian wawepo” aliongea Jeff. “Ila jambo nililowaitia hapa si hilo, kuna uwezekana mkubwa hii vita tunayoisubiri ikapigwa katika ardhi ya nyumbani. Njia pekee ya kushinda ni kupana na kila kitu chetu” aliendelea na kuwaangalia machoni. Macho hayo yatosha kuwambia kuwa “tunalifahamu hilo”.


“Kuanzia kesho tutaanza kuhama kuelekea kambi mpya, ili kuepusha taharuki tutapita njia maalum iliotengezwa chini ya ardhi. Njia hii itatupeleka moja kwa moja mpaka katika kambi mpya” aliongea Jeff. “Gari, ndege na silaha tu ndio vitu tutakavyoondoka navyo, vingine vyote vitabakia”, “bila hizi mashine itakuwa vigumu sana maana unafahamu kuwa hizi ni za kisasa zaidi” aliongea Martina. “Hizo sio za kisasa, zimeshapitwa na wakati. Huko kuna zawadi nono nimewaandalia” aliongea Talbot na kumtoa wasiwasi mwanamama huyo. Kikao kiliendelea kwa muda, mambo mengi yalizungumzwa, kilifikia mwishoni na kila mtu akatawanyika na maandili ya safari yakaanza.


Usiku wa siku hiyo jesho zima linalopatikana katika kambi hiyo lilipewa taarifa na maandalizi yakaanza. Siku iliyofuata kikosi hicho kikaanza kuhama, na kwasababu walikuwa wakisafiri chini ya ardhi tena kukatiza katikati ya mji. Safari ilikuwa ni ya mwendo mdogo, iliwachukuwa takriban saa thalathini na saba mpaka kuwasili katika kambo mpya ambayo nayo ilikuwa tayari imekamilika. Jeff alitoa rimoti mfukoni na ukuta mkubwa uliokuwa mbele yao ukafunguka.


Kila alieingia alijikuta akipatwa na mshangao jinis kambi hiyo ilivyokuwa kubwa, wengi walidhani Sector Zero Ghost layer ndio ilikuwa kambi kubwa kuwahi kutokea, mbele ya kambi hiyo ilionekana kama chumba tu katika ghorofa kubwa sana. “karibuni katika makuu makao makuu ya kikosi cha muungano” aliongea Jeff, “hata katika ndoto zangu sikuwahi kuotaka kama kuna siku nitakutana na kambi kubwa kama hii” aliongea Alfred.


“Hatuna muda kushangaa, tupumzikeni kidogo kisha tutaanza ziara katika kambi hii musije mukapotea” aliongea Jeff na kuwafanya wote wacheke. Saa chache baadae katika kambi hiyo shughuli za hapa na pale zilianza kupamba moto. Jambo kikosi Ghost kilikuwa na wanajeshi mia nne na thalathini lakini kambini hapo nisawa na familia moja ndogo sana. Hata haikuonekana kama wanajeshi hao ni wengi.


The Pirates

“Tumepokea ujumbe kutoka kwa mshirika wetu, kuanzia kesho tutaanza safari ya kuelekea nchini RDC. Tutakwenda kule kwa ndege za kawaida, tutakuwa kama raia wengine tu” aliongea Alex mbele ya kikosi chake kilichosheheni watu wa kazi. “Vipi kuhusu silaha” aliuliza Prime General CJ, “tutakwenda kama raia wa kawaida, sasa raia wa kawaida anabeba silaha” alijibu Alex na kutabasamu, “kila kitu mtakuta huko” alimalizia. Alimaliza kuongea na maandalizi ya safari yakaanza, Alex aliekea ofisini kwake na kukaa.


Dakika chache baadae alifika CJ, “mzee, kunashida yeyote. Unaonekana umepauka sana” aliongea CJ na kukaa kwenye kiti. “Hapana sina shida yeyote ile, ni uchovu tu. Si unajuwa kipidndi hiki nimekuwa nikifanya mazoezi makaili ili kuuanda mwili kukabiliana na changamoto za kivita” alijibu. “Sawa, lakini jiangalie afya yako, katika kikosi hiki cha muungano wewe ni mtu muhimu sana. Kosa dogo katika maamuzi yako, litautikisa muungano” alimalizia CJ akasimama na kuondoka. Kwa kumuangalia tu alifahamu kuwa babaake hakuwa na vizuri kiafya.


Black Hawks, Visiwa vya Indiana Marekani.

Taarifa kusogea kambini zilitangazwa kwa kikosi kizima na kila mtu akaanza kujiandaa na safari, “Scarlet mke wangu, katika hii vita nakuomba usiingie” aliendelea kubembeleza Adrian wakiwa chumbani. “Unadhani siwezi kupambana au” Scarlet hakuonekana kuwa ni mwenye kuelewa anachokiongea mwanaume huyo. “Hapana sio kama huwezi lakini katika hali yako ya sasa hutaweza kupambana katika ubora wako” aliongea Adrian akilipapasa tumbo la mwanamama huyo lililoanza kuwa kubwa. “Lakini natamani sana niwepo katika uwanja wa vita” alinung’unika.


“Nakuahidi nitarudi nikiwa mzima kabisa, nataka kumuona mwanangu wa mwisho. Pia baada ya vita hii nitaachia mikoba ya kijeshi na kufanya shughuli nyingine. Umefikia wakati sasa wa kuwaachia kizazi cha sasa kuhakikisha usalama wa nchi hii” aliongea Adrian na kumbusu Scarlet katika paji la uso. “Kabla sijaondoka nitakupeleka Mississipi kwa mama ako, nitakuja kukuchukuwa baada ya kushinda hii vita maana bila ushindi hakutakuwa na sehemu ya kumlea mwenetu anaetarajiwa.”.




“Nakuahidi nitarudi nikiwa mzima kabisa, nataka kumuona mwanangu wa mwisho. Pia baada ya vita hii nitaachia mikoba ya kijeshi na kufanya shughuli nyingine. Umefikia wakati sasa wa kuwaachia kizazi cha sasa kuhakikisha usalama wa nchi hii” aliongea Adrian na kumbusu Scarlet katika paji la uso. “Kabla sijaondoka nitakupeleka Mississipi kwa mama ako, nitakuja kukuchukuwa baada ya kushinda hii vita maana bila ushindi hakutakuwa na sehemu ya kumlea mwenetu anaetarajiwa.”.

***************************************************

BHGP HQ

Katika chumba kikubwa kiasi, kwenye meza ya wa duara walikuwa wameketi watu sita. Supreme General Alex, jenerali kwa kwanza Jeff akiwa na maluteni jenerali wawili; Lut Jenerali Charlie na Luteni Jenerali Alfred. Jenarali wa pili Adrian akiwa na maluteni jenerali wawili nao ni Luteni Jenerali CJ na Luteni Jenerali Mack. “Kutokana na taarifa nilizozipata hivi karibuni ni kwamba, tunaekwenda kupambana nae ana jeshi kubwa lisilo la kawaida” aliongea Jeff. “Sijapata taarifa kamili lakini nina uhakika mara tutapambana na jeshi ambalo wanajeshi wake wameongezwa uwezo zaidi ‘genetically enhanced humans’ au jina lao jingine ni NEXT GENERATION SUPER SOLDIERS” alimalizia.


“Ni kama wale walioongezwa uwezo kwa kemikali ya CODE X?” aliuliza Alex. “Ndio, lakini hawa nahisi itakuwa zaidi, kutokana na taarifa ilioachwa na Chief Supreme General Commando Alfred Jackson. Hao wanajeshi wanajuwa kitu kimoja tu, nacho ni kuuwa tu” alijibu Jeff. “Kwa maana nyingine tunahitaji kuwauwa na wao au” aliingilia Charlie na kuramba midoo kama mtu alieona chakula. “Hilo ndio lengo lakini tukitilia maanani kuwa hao wanajeshi kwa namna moja ama nyingine watakuwa na uwezo wa kuvumilia risasi zetu na kuendeleza mapambano tutakuwa katika wakati mgumu sana” aliongea Adrian.


“Kuna njia moja tu ya kupambana nao” aliongea Alex, wote wakamgeukia na kumuangalia. “Kupambana na wanyama, tunahitaji kutengeza wanyama wa kwetu” sentensi fupi yenye uzito na kusababisha hewa ya baridi kutembea katika miili ya wengine. “Una maanisha nini Supreme General” aliuliza Jeff kwa mshangao. “Sio kama sisi hatuna namna ya kuwaongeza uwezo wanajeshi wetu, tutaitumi kemikali cindrex ootliviaso deca endroline X (CODE X) kwa mara ya mwisho. Hii ni vita ambayo tutahitaji kutumia kila aina ya silaha tuliokuwa nayo kuishinda” alifafanuwa Alex na macho yake yalikuwa makavu na yalibeba taswira ya simba aliejeruhiwa.


“Huoni kama tutakuwa tunatengeza hatari nyingine” aliuliza jenerali Adrian, “hakuna hatari yeyote” alijibu. “Fafanuwa tafadhali” aliongea Lut jenerali CJ, “iko hivi, tokea siku niliojuwa kuwa tutaingia vitani na kikosi cha waasi. Nilielewa fika kuwa hatutakuwa tukipambana na kikosi cha kawaida. Hivyo nikaamuwa kufanya uchunguzi juu ya kemikali ya CODE X kwa kuifanya ifanye kazi kwa muda maalum tu na sio milele kama ilivyo kwangu, kwa Jeff au CJ” alifafanuwa. CJ kusikia hivyo akashtuka, maana yeye hakuwahi kutumia kemikali hiyo, lakini alipomuangalia babaake akapewa ishara atulie.


“Hapo sasa nimekuelewa” aliongea Adrian, hakuna alietaka kujuwa zaidi. Kila mtu aliekuwepo hapo alishaelewa nini kifanyika ili waibuke kidedea baada ya vita hiyo. “Sasa tuingie mada ya pili” aliongea jenerali wa kwanza, Jeff. “Muundo wa vikosi vyetu, huu ni muhimu sana na inatakiwa kutafakari katika kila njia ili kutoweka mapengo”, “hilo ni la msingi sana, mimi nashauri tutumie mbinu kuilinda na kushambulia kwa wakati mmoja” aliongea luteni jenerali Mack ambae alikuwa kimya katika kipindi chote hicho.


“Fafanuwa Luteni” aliongea Supreme General, “jeshi letu litatakiwa kuwa na vikosi vidogo vidogo kama saba au nane. Gari, zinazojiendesha kama zitakuwepo itakuwa vizuri zaidi. Gari hizi zitawekwa silaha nzito zenye uwezo wa kukiharibu kifaru, na zitafanya kazi kama washambuliaji wa mstari wa kwanza na pia walinzi. Gari hizi zitakuwa na ngao kubwa mbele, faida yake ni kuwa, ikiwa maadui zetu watakuwa na silaha nzito za maangamizi. Hizi gari ndio zitakuwa alama zetu, na zitakabiliana na hizo silaha” akanyamaza kidogo.


“Kikosi cha pili kitakuwa kikosi cha anga, hichi kitakuwa na kazi mbili mbili. Ya kwanza kitakuwa macho yetu kwa sababu sio kila sehemu tutakuwa na uwezo wa kuona, pili kitashambulia silaha nzito na kuziharibu ili kusafisha njia kwa kikosi cha tatu cha waenda kwa miguu. Kikosi cha tatu kitakuwa cha mashambulizi ya juu ya ardhi, kitahusisha wanajeshi waliobobea kwenye ulingo wa mapambano ya ana kwa ana. Hawa watabeba silaha nyepesi ili zisiwachoshe, na kazi yao itakuwa ni kukabiliana na yeyote atakaekuja mbele yao. Kwanini iwe, ni kwasababu tukitumia sana mashambulizi kwa ndege tutuharibu mji mzima na hatuwezi kufanya hivyo kwasababu hatutokuwa tofauti na wao”.


“Kikosi cha nne kitakuwa cha wenda kwa miguu lakini chini ya ardhi, tunafahamu maeneo ambayo yanatumika sana kufanya mashambulizi ya kushitukiza ni kupitia maeneo ambayo watu hawatikuwa wakiyalinda. Kikosi hiki kitamuondoa yeyote asie kati yetu watakaemkuta akitangatanga katika njia za chini ya ardhi hasa za kupitia njia za maji taka. Kikosi cha tano kitahusisha wadunguaji wa masafa ya kati, hawa kazi yao itakuwa ni kukilinda kikosi cha waenda kwa miguu. Kwa maana nyingine, kikosi hichi kitafanya kazi kama jicho la tatu likiangalia maeneo ambayo yatakuwa vigumu kuonekana na kikosi cha waendao kwa miguu”.


“Kikosi cha sita kitahusisha wadunguaji wa masafa marefu, hawa watakuwa na kazi mbili. Moja itakuwa ni kuwalinda wadunguaji wa masafa marefu kwasababu watakuwa wameshughulika na kukilinda kikosi cha waenda kwa miguu. Na ya pili itakuwa ni kuwasaka wadunguaji wengine, ili kuepusha usumbufu katika vikosi vitakavyokuwa mbele. Wote hapa tunafahamu kuwa wadunguaji ni wasumbufu sana na wao ndio sehemu ya kuharibu mipango ya watu. Kikosi cha saba kitakuwa kinahusisha matabibu na wanajeshi ambao watakuwa wakipeleka silaha kwa wale ambao watakuwa wakipambana na kuwachukuwa majeruhi kwa ajili ya kupata huduma ya kwanza”


“Kikosi cha sabab kitakuwa ni kikosi maalum kitakachohusihsa wanajeshi ambao lengo lao kubwa litakuwa ni kuwaondoa majenerali wa kikosi cha maadui. Ninaposemea ni muhimi nina maanda ya kuwa, kinahitaji watu wenye uwezo wa hali ya juu katika mapambano ya aina zote. Kwasababu sitegemei kama mejenerali wao watakuwa na uwezo sawa na nyumbu wengine. Hivyo kuwapeleka wanajeshi wetu kupambana nao ni sawa na kuwapeleka kwenye makaburi yao na hatuko tayari kuona nguvu ikitoweka”.


“Kikosi cha mwisho, cha nane. Kitahusisha wote watakaobakia kambini. Hawa watakuwa macho ya vikosi vyote ambavyo vitakuwa vinapambana. Kikosi hiki ndio kitakuwa akili ya jeshi hili, kwa kufanya maamuzi ya aina zote wakati wa kupambana. Na ndio kitakuwa moyo utakaokuwa unasukuma damu ya ujasiri kwenye mioyo ya wanajeshi ambao watakuwa karibu na kunyanyua mikono. Kuna wakati kitahitajika kifanye maamuzi magumu yatakayowatoa machozi lakini itabidi kifanye maamuzi hayo macho yakiwa makavu kabisa. Kumuonea huruma mwanajeshi ambae anajuwa muda wowte wakiwa huenda akafa, ni kuudhalilisha msimamo na ujasiri wake. Kikosi hiki ndio kitovu cha jeshi letu, ikitokea kukavurugika huku, Mungu atusaidie.” Alimaliza kuongea na kuwaangalia.


Wote walionesha kusikiliza kwa makini huku kila mmoja akipiga mahesabu yake kichwani. Walionekana kutafakari kwa kina mpango wa Mack. Ni kweli ukiuangalia kwa juu juu utasema ni mpango dhaifu katika medani za kivita. “Katika mpango huu, mshambulizi hayatasimama. Tutakuwa tunashambulia na kujilinda kwa wakati mmoja. Unaonekana kuwa mpango mzuri hasa katika mandhari ya mjini” Jeff alikuwa akimumunya maneno kwa sauti ndogo. “Lakini pia ni mpango ukienda vibaya tunaweza kuoteza karibu nusu ya nguvu yetu ya jeshi. Hiyo ni kama kubeti tu, hamsini kwa hamsini. Itabidi huyu Mack nimuweka na Brain. Hizi akili mbili zikikaa pamoja, ushindi ni lazima” aliendelea kumumunya maneno kwa sauti ndogo. 



Wote walionesha kusikiliza kwa makini huku kila mmoja akipiga mahesabu yake kichwani. Walionekana kutafakari kwa kina mpango wa Mack. Ni kweli ukiuangalia kwa juu juu utasema ni mpango dhaifu katika medani za kivita. “Katika mpango huu, mshambulizi hayatasimama. Tutakuwa tunashambulia na kujilinda kwa wakati mmoja. Unaonekana kuwa mpango mzuri hasa katika mandhari ya mjini” Jeff alikuwa akimumunya maneno kwa sauti ndogo. “Lakini pia ni mpango ukienda vibaya tunaweza kuoteza karibu nusu ya nguvu yetu ya jeshi. Hiyo ni kama kubeti tu, hamsini kwa hamsini. Itabidi huyu Mack nimuweka na Brain. Hizi akili mbili zikikaa pamoja, ushindi ni lazima” aliendelea kumumunya maneno kwa sauti ndogo.


“Mbinu yako ni nzuri, ili kuing’arisha zaidi. Nitakuomba ukamuelezee Janeth (Brain). Mkifanya kazi pamoja nina uhakika itakuwa mbinu bora kuwahi kutokea” aliongea Jeff baada ya mmumunyo wa muda mrefu. “Ikiwa nitapata ruhusa kutupa Supreme general nitafanya hivyo” aliongea Mack, “ruhusa umepata, lengo letu kubwa ni kushinda hii vita kwa njia yeyote ile” aliongea Alex. Siku hiyo alionekana mtu tofauti, siku zote alikuwa ni Alex ila muda huwo alikuwa amekivaa cheo chake vilivyo. Hakuwa yule Alex aliezoeleka bali ni yule wa kwenye THE DIRTY GAME. Mtu aliekuwa na sura ya kazi iliojaa tafsiri za kikatili.


Adrian na Jeff walimuangalia kisha wakatabasamu na kwa pamoja wakasema “He is back, Alex the Killer” kwa sauti za chini. Waliondelea kujadili mambo mengi, hatimae kikao kikafikia tamati na kughairishwa. Walitoka ofisini na mara moja ikatoka amri kikosi kizima kikusanyike kwa ajili ya maelekezo. Honi ikaanza kulia na hatuwa za watu kuelekea eneo la mkusanyiko zikaanza kusikika. Wanajeshi waliovalia kombat za aina tofauti walikusanyika eneo moja na kujipanga katika mistari iliyonyooka.


Supreme general akiwa mbele, kulia kwake akiwa kasimama jenerali wa kwanza Jeff. Kushoto kwake akiwa kasimama jenerali wa pili, Adrian. Nyuma ya majenerali hao walikuwepo maluteni jenerali; Jason CJ Jr, Charlie, Mack na Alfred. Watu hao walikuwa wamevaa sura za mamba, hata kama wangecheka wamgeonekana wanakenua midomo tu bila dalili zozote za hisia. “Hii vita walipigana baba zetu, na sasa ni juu yetu kuhakikisha kile walichokipigania kinaendelea kuwepo, nacho ni uhuru” alianza kuongea Sup. General Alex.


“Najuwa kati yenu kuna watu wenye vyeo vikubwa, na wanaumia kuweka katika daraja moja na walioko chini yao. Kama wewe ni miongoni mwa watu hao, unaweza ukatoka kwenye kikosi hichi mapema sana” alipofika akanyamaza kidogo na kuwaangalia wanajeshi waliokuwa wamejipanga mbele yake. “Kimya” hakuna hata mwanajeshi mmoj alieinuwa mguu. Si mwanamke wala mwanaume, wote walitulia kama masanafu. Wakiwa wamesimama kikakamavu, vifua mbele na macho mita mia moja mbele. “Itakuwa vita ngumu kuliko zote ulizowahi kukutana nazo, kifo kitakungenisha na rafiki, mke au mume na makomredi wenzako. Hatuwezi kuahidi nani na nani atarudi na nani ataanguka katika uwanja wa vita”.


“Hata nikianguka mimi, jenerali yeyote au luteni jenerali yeyote. Usibabaike, bakia kwenye mfumo uendelee kupambana. Yatawekwa matanga baada ya vita na kama utataka kulia, utalia huko mpaka machozi yakauke hutaulizwa na wala hutanyamazishwa” alimalizia na kumgeukia Jeff kisha akatikisa kichwa. Jeff akapita mbele na kuwaangalia wanajeshi walioko mbele yake, “Baada ya mkusanyiko huu, wote tutavuwa gwanda zetu, hakutakuwa na vikosi vitatu tofauti bali kutakuwa na kikosi kimoja chenye sare ya aina moja mpaka vita hii itakapokwisha” aliongea Jeff.


“Na kuanzia sasa matumizi ya simu, baruwa pepe au mfumo wowote wa kimawasiliano wa kidigitali umezuiwa. Toa simu yako weka chini na uikanyage kwa mguu wako mwenyewe” alipomaliza tu kila mwanajeshi akatoa simu na kuiweka chini. Vikasikika vishindo kadhaa na sauti ya vitu kuvunjika, hakuna aliewaza mara mbili. Kila mmoja alifahamu kuwa amri ni kanuni na kanuni lazima izingatiwe na kufuatwa bila kushurutishwa. Jeff alirudi nyuma na kumwangalia Sup General Alex, Alex akatikisa kichwa na kumuangali jenerali wa pili, Adrian na kumfanyia ishara.


Adrian akapita mbele na kutabasamu kidogo, “kama una ujumbe unataka uufikie familia au ndugu zako, andika kwenye karatasi na uuwasilishe katika kitengo cha mawasiliano. Hiyo ni fursa kwa siku ya leo tu, kuanzia kesho, mazoezi maalum ya pamoja yataanza hivyo hutopata nafasi ya kuandika ujumbe huwo tena” alimaliza na kurudi alipokuwa mwanzo. Mkusanyiko huwo ukaruhusiwa na kila mwanajeshi akakimbilia chumba anacholala kwa ajili ya kuandika ujumbe kama ilivyotolewa fursa. Ama kwa hakika wingu zito lilikuwa likija na tayari kikosi hicho kilishaanza kutafuta miamvuli kwa ajili ya kujiknga mvua itakayotokana na wingu hilo ambayo haijulikani itaisha lini.

**********************************************

Raia waliokuwa wakiishi katika mji mkuu nchini RDC walianza kuhamishwa na kupelewa katika makambi maalum ya muda mfupi ili kupisha vita itakayorindima ndani ya miezi michache ijayo. Na kwasababu mji huwo ndio ulikuwa mkubwa kabisa na wenye watu wengi zaidi kuliko miji mingine nchini humo. Barabara na mitaa zilifurika magari na watu waliokuwa wanahama. Waziri wa usalama na amani Dr Paul Hance alikuwa akilisimamia zoezi hilo akiambatana na vikosi vya kulinda usalama vya nchi hiyo. “Mheshimiwa, mpaka asilimia hamsini ya watu wote wameshatoka nje ya mji” alifika mtu mmoja na kuongea.


“Ongezeni kasi, maaan hatujui huyo mwehu anaetaka kushambulia atashambuli muda gani” aliongea waziri. Wakati akiendelea kutoa maelezo, simu yake ya mezani ikaanza kuita. Alinyanyua mkonga na kuupeleka sikioni, “habari yako Mr Paul” ilisikika sauti nzito ikiongea upande wa pili. “Wewe nani na unataka nini, kama huna jambo la msingi la kuongea usinipotezee muda nina majukumu natakiwa kuyatekeleza” alifoka waziri. “Usijali, sitawashambulia raia wa kawaida kwa sasa. Hivyo wahamisheni taratibu kabisa musije mukawaumiza raia nitakaokuja kuwaongoza baada ya kuwaondoa mnaowategemea sana” aliongea mtu huyo na kukata simu.


Michael alirudisha simu yake mfukoni na kucheka sana, “kweli wananiogopa sana” aliongea. Alice alikuwa pembeni yake akipata kifunguwa kinywa. “Unataka uongoze kwa mfumo gani” alitupa swali, Michael akageuka na nyuma kabla ya kujibu swali hilo na kumpa mgongo Alice. “Katika utawala wangu kila kitu kitakuwa huru, hakutokuwa na mahakama walawafungwa. Kila mtu atakuwa huru kufanya kile anachotaka. Dunia itarudi katika zama ambazo mwenye nguvu alikuwa anapata kila kitu na dhaifu wanabakia kuongozwa tu. Hivyo kila mtu atakuwa na haki sawa ya kufanya kile anachohisi kitamridhisha” alijibu Michael na kushusha pumzi.


“Huoni kama hiyo itasababisha umwagikaji damu uliopitiliza?”, “hahaha! Mimi nitakuwa Mungu katika hii dunia, ukitaka ulinzi wangu nitakupa silaha ili upigane na anaekudhalilisha. Nitakuwa mtu tajiri kuliko yeyote aliewahikutokea tokea kipinidi Solomon. Nikifikiria tu majanga na harufu ya damu, vilio vya watu na milio ya bunduki; harufu ya baruti za risasi na vitu kuunguwa, mwili unasisimka. Hatimae binadamu atakuwa yule aliekuwa kabla ya haya matehama na usasa” Michael alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa. “Hii nlokuwa nayo ni ndoto ya mwendawazimu, na naipenda sana” alimalizakuongea na bila kujitambuwa ute ulikuwa ukimtoka mdomoni kwa uchu wakuona dunia ikiingia kwenye majanga.


Alice hakuwa na la kuongea, alifahamu vya kutosha kuwa alichoambiwa hakikuwa utani hata kidogo. Michael alikusudia kuiwasha dunia moto ambao kama utawaka ungechukuwa karne ama milenia nzima kuuzima. Kitu ambacho hakukifahamu ni jambo gani lililomsukuma Michael mpaka kufikia uwamuzi huwo. Ni wazi kabisa kuwa, alifikwa na jambo lililomuuma na kuuchana chana moyo wake angali yu hai. Na kila alipotaka kuuliza sababu ya matendo yake, Michael alilikwepa swali hilo kwa kuazisha mada nyingine tofauti na swali aliloulizwa.


Walimaliza kupata kifunguwa kinywa, wakatoka na kuelekea yalipo yale majokofu. “Kila kitu kitakwisha kabla ya ulimwengu kugunduwa ni kimewakuta” aliongea Michael na kutabasamu na kuangalia ukutani ambako kulikuwa na kitu kama saa kubwa sana. Juu kabisa ilikuwa na maandishi yaliosomeka “Majanga yatawakumba ndani ya miezi kumi na moja ijayo”.

Imesalia miezi kumi ba moja mpaka siku ya vita.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog