Search This Blog

Friday, 30 December 2022

KIAPO CHA MFUNGWA (5) - 1

   

Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (5) 


Sehemu Ya Kwanza (1)


IMEANDIKWA NA : ZUBERI MARUMA

********************************************************************************

Simulizi : Kiapo Cha Mfungwa (5) 

Sehemu Ya Kwanza (1)





Alipokuja mama Mimi nikamweleza madaktari walivyosema na hela inayoitajika ya intrasound



Mama akasema jamani sasa elfu hamsini sisi tutaipata wapi?,mama aliongea kwa unyonge mpaka Mimi mwenyewe nikamuonea huruma,



Nikamwambia usijali mama Mimi na ka akiba kangu kadogo wacha nikakachukue,mama akatabasamu!, akanambia basi kama una ka akiba we nenda ukakachukue haraka mtoto afanyiwe matibabu nikwambia sawa mi nikarudi zangu nyumbani



Nikachukua ka akiba kangu nikampigia simu mwenzangu yeye jina lake aliitwa Said 'white' nikamwambia akanambia sawa amna shida nikasafisha vyombo,unajua mama alikuwa amepika ila vyombo akusafisha na yule mdogo wangu Rahma Kazi Yake Ilikuwa Ni Kuzurura tu,nilipo maliza kusafisha nyumba nikakoga nikatoka kurudi zangu hospital kufika nkampa mama zile pesa akaenda kulipia,mama akutaka kuniacha mwenyewe pale alitaka tukae nae mama yangu aliwapenda sana wanangu,sasa nkamwambia mama tukikaa wawili huku vipi biashara kule si afadhali mi nirudi tu,mama akasema sawa!,



"dada shaa vipi kuhusu kunyonya ikiwa ulimuacha mama na mtoto?"



"kaka zuberi,mwanangu aliacha kunyonya mdogo sana nilipokuwa nikimnyonyesha alikuwa akitapika,ndo alipokata kunyonya wakat huo akiwa na miez kumi mtoto kaacha kunyonya,basi siku hiyo mi ndo nikarudi zangu nyumbani asb yake naenda zangu hosptal tukapeana mazamu mimi na mama,maisha ya kaendelea hivyo ivyo wifi yangu kitambo tu alisharuhusiwa wakiniacha pale hosptalin hata kabla atujasafiri,ila hakuna alogeuza kichwa nyuma,si baba yake wala mashangaz zake,



Hosptal kila kukicha inatakiwa pesa mara leo akapimwe hiki kesho apimwe hichi,na kila apimwacho hana maradhi

mama akapeleka pesa akaambiwa intrasound inapgwa jumatano,



Kufika jumatano akapelekwa katika chumba cha intasound akapigwa sehemu zote akaonekana ni mzima kinacho msumbua madokta awajakikua ni kitu gani,



Ikabidi apimwe choo kikubwa nacho ni elfu thelathin nikatoa pesa,nikampatia mtoto akaenda kupimwa choo kikubwa hana tatizo lolote,



Mama akawaambia madaktari ina bidi mtupe ruksa tu tukamwangaikie na kwingine,madaktari wakaturuhusu tukarudi zetu nyumban



Ule Upande Wa Mpz Wangu Mpya side 'white' Mamake Akawa Akinipiga Vita Vikali Sana,alikuwa akimkataza mwanaye kuwa na mimi siku hiyo white akaja nyumbani kuja akanambia



"shaaa mama kanambia ntakapokuoa wewe hana radhi na mimi,"



Yani Kaka Zube Niliumia Sana,mwanangu huku anaumwa,nako Side 'white' ananiongezea machungu,ilhali alikuwa akinipenda sana huyo Saidi akiambiwa kitu na mamake anakuja kuniambia mama kanambia hivi,hiv na hivi mi nikamwambia isiwe tabu said basi mi na wewe tuachane akanambia hapana mi nakupenda sana Shaaa na nakuhaidi ntaishi na wewe watake wasitake,kwan wao ndo wanaoishi na wewe au mimi?



Nikamwambia hapana Said wangu usilazimishe mapenzi,ikiwa wazaz wako awataki tunaweza ishi mimi na wewe ndoa isiwe ya baraka,



Kwanza tutafungiana rizki wewe utanifungia mimi na mimi ntakufungia wewe yan ikiwa kuna mtu anataka kuja kuniposa akijua nipo na wewe atoniposa tena ndo ivyo namaanisha"



Akanambia hapana shaaa siwezi kukubali kukupoteza ilhal moyo wangu Unakupenda Kikubwa tumuombe allah wajallah atufanyie wepesi,kwan hakuna ashindwacho yeye beby wangu!"



Nikamjibu Sawa,akaondoka Zake,mama akaja akanambia sikia shaaa maneno nayoyapata mtahani ni mabaya sana mi nnachokuomba achana na huyu mwanaume hana nia mbaya kwako wazazi wake wanakuchukia vibaya sana,mama kunambia vile mimi nikamsikiliza mama yangu yule mwanaume mi sasa nkawa namkwepa na huku kwa dully anataka kuoa sasa harusi ishakuwa mbivu mi sikujal katika nafsi yangu alikuwa hayumo



Siku Hiyo Kaka Zube Natoka Zangu Nyumbani Nakumbuka Mapande Ya Mchana Mchana hivi naelekea zangu kwa shoga yangu dada mwaj, nikakutana na ndugu yake dully akanipiga kikumbo,nilimgeukia kumgeukia akanisonya sikumjibu kitu nikasonga zangu mbele,basi nikiwa nimekaa kitako pale dukani kwa dada Mwaj Kukaa Kitako Yule Mwana akaja Akaita mwaj nimekuja kukualika shughuli



Mwaj Akamjibu



"wee Mwana Wewe Si Umekuja Kualika tu saivi hapa?!"



Akajibu eti Kwa Kujishebedua "ndo Nilisahau" Mwaj akamshushua "au kwa kuwa umemuona Shaaa Kaja apa ndo waja kumuumiza roho,mwenzako ana hata habari hizo"



Akamjibu Mim Hata Sijaja Mrusha Roho Mtu Nimekuja Kukwambia tu,mi nikamjibu



"aya ndo kashasikia wenenda zako,yule wifi yangu akaruka eeh kwani nilikwambia wewee,nikamwambia eee kelele tena unisikilize kwa umakin wa hali ya juu,usinipande kichwani najua huko kwenu ujafunzwa kuongea na watu nitakuchakaza kampande kichwani huyo mama yako alokuzaa akakuleta humu duniani"



"mwanga mkubwa wewe,kwani nani asiyekujua kama wewe mwanga ulizuia ya mara ya kwanza zuia na hii mchaw mkubwa wewe...



Kaka Zube Sikujua Ni Sa Ngapi Nilinyanyuka Pale Nikamsogelea Ila Nachokumbuka Ni Mtu Alikuwa Chini Damu Zikimtoka Kichwani,watu Pale Dukan Wakaanza Piga Kelele Shaaa Umeua Shaaa Umeua Sikuwaza Mara Mbili Wakati Watu Wamemzunguka,....







Zidu na ISACK Baada Ya Kukamatwa Viongozi Wa Nchi Ya KINTE wanaweka kikao,na mwisho wanapendekeza atekwe mke wa raisi Goodluck Silvestar Bi Jacklin kisha atishiwe kuuwawa kupona kwake ni Zidu Na Isack Kuachiwa huru je unadhan ninin kiliendelea?!



TUSONGE!



Mambo Kwa Siri Sana Yakapangwa Na Kupangika, hotel ambayo angefikia bi Jack Ilitambulika,Gambi akachukua chumba jirani na chumba ambacho bi Jack angefikia...



Gari ambayo ingemtoa pale giraffe hotel mpaka kiwanja cha ndege cha siri ambapo angepandishwa katika ndege na kusafirishwa mpaka kinte!,



Jinsi Ilivyopangwa Ndivyo Ilivyokuwa, siku Mbili Kabla Ya Uhuru bi Jack aliwasili,akapelekwa mpaka katika hotel aloandaliwa!, na kwa bahati mbaya zaidi alikuwa na mlinzi mmoja tu tena wa kike



Kama Ilivyopangwa Mida Ya Saa Mbili,gambi Alienda Kugonga Kile Chumba alicholala bi Jack Mlinz Akijua Ni Muhudumu Kaja Kufanya Usafi Alipofungua mlango tu Gambi Akaurusha Mkono Wake Wa Kulia Shingoni Kwa Dada Yule Mkono Wake Wa Kushoto Alishika Silaha Alomnyooshea Malkia Yule Wa Ganyama!



"tulia Hapo Hapo Ukijitingisha tu! sitokuwa na msahada na wewe ni vyema ukatulia tu ivyo ivyo!"



Gambi Akakoroma,Jack Alikuwa Akitetemeka Mwili Mzima,bado Akujua Kilichokuwa Kikiendelea Ndipo 'kidume' kilipoiachia Shingo Ya Mlinzi Yule,akaporomoka chini,tayari hakuwa na uhai tena!



Jack akuamini kile kilichotokea



"yakupasa taratibu uamke!,ufate maelekezo"



Bi Jack huku akitingisha kichwa mwili wote ukimtetemeka,jasho likimtitirika aka amka na kufata maelekezo,akatolewa mpaka nje akaingizwa ndan ya gari,gambi Akaitoa Gari Kwa Kasi Mpaka Katika Kiwanja Kidogo Kile Akamkabidhisha Mwanamke Yule Kwa Watu ambae alishapewa maelekezo,ndege ikapaa!



Baada Ya Ndege Kupotelea hewani ,'roho ya paka' mwanaume Gambi akarejea mpaka ndani ya gari yake,akaiwasha na kuelekea mpaka ofisini kwake,akampa taharifa bosi wake,naye akampigia mh Rais Akampa Simu Aongee Moja Kwa Moja Na Gambi!,



"kazi nzuri mwanangu najivunia kuwa na kidume kama wewe!,"



Mh Moreti ii akaongea kwa furaha,



"Usijali baba ni wajibu wangu kuifanya kazi yako vizur,wacha niendelee na kaz huku!,tutaongea Mungu akipenda"



"Ok mwanangu!"



Gambi akiwa katabasamu akamkabidhi mkuu wake simu,yeye binafsi si kwamba hakuruhusiwa kuwa na simu hapana,kazi yake aikuruhusu awe na simu!,baada ya mkuu wake kumruhusu kwenda kuendelea na kazi ndo ndipo alipokumbuka kuelekea msituni katika kambi ya waasi kuwaokoa wanawake na watoto walotekwaga,kukumbuka kule akatabasamu,pasina woga wowote,mwanaume safari hii akachukua kifaru,akaongoza maaskari kadhaa wa serikali,wakaelekea katikati ya msitu pande palipo na kambi ya waasi!



AIKUJULIKANA KILICHOENDELEA KULE...



Huyu ndo LAURENT MORETI MERNELI GAMBI



Mtoto pekee wa mh Raisi Moreti Merneli Gambi au Moreti ii Raisi wa Kinte



***



Baada Ya Taifa La Kinte Kumteka,mke Wa Rais wa Ganyama Wakaa Kimya Kwanza Pasina Kutangaza Chochote!...



Rais Silvestar akujua kilichokuwa kikiendelea,yeye alijua mkewe asingekuwepo katika Muungano na kutokana na ubize siku mbili zile akuwasiliana na mkewe, hatimaye siku ya muungano ikawadia,akiwa ajui hili wala lile,ndani ya uwanja wa mashujaa,akijiandaa kutoa amri Zidu na Isack,bila Kumsahau Katarina Wanyongwe Ghafla Sms Ikaingia Katika Simu Yake,ikamlazimu asitishe kuhesabu kwanza akafungua ujumbe ule kilichofatia alitoa macho ya mshangao,akamnong'oneza kitu waziri wake!



Dunia Yote Watu Walikuwa Wakilitazama Lile tukio laivu likiendelea katika runinga zao!,kikao kikawekwa haraka katika meza kuu,wakaongea jambo,na mwisho msemaji akatangaza kusimamishwa kwa tukio lile,japo sababu aikuelezwa moja kwa moja zaidi ya kuelezwa kuwa kuna matatizo makubwa yametokea!



Dunia Ikabaki Katika Hali Ya Taharuki!,kutoelewa Kilichokuwa Kikiendelea,maskini Rais Silvestar Alishikwa Pabaya!



Palepale Sherehe Zile Za Muungano Zikavunjwa!...



"tafadhali Naomba msiniulie mke wangu kama ni Zidu na Isack ntawaachieni ili nimpate mke wangu akiwa hai!"



Wajumbe Wale Wa Kinte Walokutana Siku Chache Zilizopita Na Kupanga Mpango Ule,wakaachia Kicheko,walifurah Sana Kwa Ushahuri Wa Mzee Yule!



"mkeo Ni Mateka Wetu,ili tumuachie huru tunatoa masaa sita,mumpandishe Zidu ndani ya ndege waje huku!,wakitua tu nchini kwetu nasi ndo tutamwachia huru malkia wenu!"



Dah,sharti Lile Hakika Kwao Lilikuwa Ni Gumu,ila Wangefanyaje Sasa!,



"nina Wazo!," Wazir Wa Jeshi Amani Na Ulinz Wa Ganyama Kwa Kujiamin! Akatoa rai yake,viongoz Wote Wakawa Tayar Kumsikiliza,



"mchezo Uendelee,huyu Zidu Naona tumtumie kwa manufaa yetu,tumtumie kumwangamiza raisi wake Moreti ii"



"kivipi sasa?!" viongozi wakahoji,waziri akatabasamu kidogo kisha akaendelea...



"udhaifu wa Zidu tayari nishautambua ni Katarina,Zidu anampenda sana Katarina zaidi ya kitu chochote,nadhani mnakumbuka alipotumwa kuja huku lengo ni kukuua wewe mh rais ila mwisho alisahau kaz ilo mleta na kujikuta akiangaika kumfatilia katarina,na katarina ndo chanzo cha yeye sisi kumkamata,na wakati akiwa gerezan alikuwa akimtaja tu Katarina...



Ivyo tuutumie udhaifu huo kumfanya awe wetu!"



"tutautumiaje sasa?!"



"swadakta,tunarusha jiwe moja tunaua ndege wawili,cha kwanza tunamruhusu Zidu Na Huyo Isack Wake Kiurahisi tu,tunawapakia ndani ya ndege yao kama wenyewe walivyodai,pili,kabla atujampakia tunamuweka chini Zidu tunamwambia kama taifa lake lilivyoamua kumteka malkia wetu,tumemwacha huru yeye na mwenzake ila Katarina Ataendelea Na Hukumu Yake Katika Magereza Makubwa Wakumuokoa Ni Yeye,kivipi Sasa Kwa Kazi Moja tu,kumuua Moreti ii..."



Watu Wote Wakapiga Makofi, lilikuwa Ni Bonge La Wazo,wote Wakaliunga Mkono,kweli ZIDU akaletwa,mbele ya jopo lile,akaambiwa wazi kuwa kaachiwa huru,ila ili mpz wake naye apate kuwa huru ni lazima aende akamuue Rais Wake!,alompa Kazi,mambo Yakawa Yamegeuka!



Na Zidu Umwambii Kitu Kwa Katarina,ni Dhaifu,dhaifu Kupindukia



"nipo tayari kufanya ivyo ila msiniulie mpz wangu,tena hata gerezani asiwekwe ana mwanangu eti!"



Zidu aliongea kwa majonzi akaambiwa,ilo alitowezekana ili mpz wako awe huru na uweze kuish naye ukafanye kazi hiyo!



Mwanaume Haraka Sana Akakubali!,akapewa Nafasi Ya Kumuwaga kipenziwe!,



Siku Hiyo Katarina Akuamini Kumuona Mpenziwe,bado Alikuwa Akimlilia 'sai' akijua Huyu pekee ndo awezaye kumuokoa jehannam jail gereza lenye mateso makali...



"mpz wangu naondoka kuutafuta uhuru wako naenda kukukomboa, nakuacha kama mfungwa ila utakomboleka mamy"



Katarina Alilia.....



"mwanao Yupo Kwenye Hali Mbaya Muda Wowote Anaeza Akatoka Fanya Unitoe Huku babaa!"



Maaskar Wale Wa Kike waliokuwepo pale Wakacheka, Katarina hakuwa na msimamo ni dakika chache mbele yao alikuwa akimlilia 'sai' kwa kujua yeye pekee ndo mkomboz wake!



"najua mamaa,ntafanya juu chini kesho kukamilisha kaz niliyopewa mpz wangu uwe huru"



Viongoz Wale Wakazid Kufrah!



Zidu Na Isack Wakapakiwa Katika Ndege Ya Kinte,kinte Wakijua Ni Ushindi Pasina Kujua Moyo Wa Zidu Ulishageuka!...



Na kwa sasa ni aduh yao



*JE UNAHISI NIN KITATOKEA?! NDO KWANZO TUKO MWANZO*





ZIDU anaachiwa huru ila akiwa katika mtihani mpya,ili kumuokoa Katarina Mwanamke ampendaye ni lazima amwangamize Rais Wake Mernel Gambi,ila Kwa Kuwa anampenda Kata Anakubali,je Nin Kiliendelea?!



TUENDELEE...



Mawazo yalikishambulia kichwa chake kazi ile kwake ilikuwa ni nzito ili ondosha kabisa furaha yake,



Tofauti Na Mategemeo Ya Wengi Kuwa Angerudi Nyumbani Kwa Furaha Mambo Yalikuwa Kinyume,kazi Alopewa Kwake Ilikuwa Ngumu,ngumu Kuliko Ile Ya Kuja Ganyama Kumuuwa Rais Silvestar,ndani Ya Ndege,si Isack Wala Zidu Aliyeongelea Swala Lile,kila Mmoja Alikuwa Katika Mawazo Yake!



Ghafla 'automatic' akajikuta kaachia tabasamu,ni baada ya kukumbuka kitu,



'Martin Luda'....



Jina hili likaja katika kichwa chake,huyu ni mtaalamu wa kutengeneza ngozi bandia aliyoko katika idara ya jeshi la polisi,nchin Kinte,uweza Kutengeneza Sura Kopi Na Yako Akimvisha Mtu,mtu Akiwacheki Anaweza Shindwa Kuwatofautisha Mapacha Nyie,alishajua Cha Kufanya,amani Sasa Ikajijenga Katika Moyo Wake,



Punde tu wakafika kinte,Zidu akuamin uma alokutana nao,uwanja wa ndege ulifurika maelfu ya watu wakiwa na mabango 'shujaa umerudi' mengine yakaandikwa 'mtetezi wa kinte' machozi ya furaha yalimtoka zidu,kulikuwa na ulinzi wa kutosha,akaingia katika gari maalumu safari ya kuelekea ikulu,ikafatia njiani watu wengi walifurika,kwake yeye hii ilikuwa nikama 'sapraiz' japo moyo wake ulimuuma akutekeleza kazi,alopaswa aifanye,leo hii awaulie Rais Wao,hapana Martin Luda Atakuwa Kimbilio Langu'



Akaendelea Kuwaza,walifika Ikulu Wakakaribishwa Vizuri,Zidu Akapewa Pole, Isack naye alimmis Mery Wake Ivyo Siku Hiyo Iyo Akasafiri Kurudi Zake Tanzania



Zidu Akiwa na rais akapendekeza ombi lake,"naitaji kesho nirudi ganyama kutekeleza kazi niliyopewa! nikiwa na sura ya huyu mwanamke Jack,tusimpe uhuru!"



Wazo Lile hata Raisi mwenyewe alikubaliana nalo haraka sana Martin Akapewa kazi ya kuchonga sura ya Jack Ndani Ya Nusu Saa Ikawa Tayari akaivaa na safari ya kurejea Ganyama Ikafatia!



Jeshi Hatua Chache tu kutoka masanja road chini ya ardhi lilizidi kujifua ipasavyo!...



"beby naomba tuonane hotelin sansk,nimekumisi mume wangu,siitaji mapokezi yoyote wala msafara wowote!"



Rais Goodluck Wala akuushangaa sana Ujumbe Ule Alimjua Vyema Mke Wake,akupenda Misafara,pia Alikuwa Akipenda Starehe Kukutana Katika Mahoteli Makubwa Makubwa,ivyo Kwake Ilikuwa Sawa tu,akapakia ndani ya gari lake safar ya uwanja wa ndege ikawadia,kweli mkewe alishuka kwenye ndege akamkumbatia pasina kujua yule ni Zidu jitu katili,lenye roho mbaya,wakaelekea Sansk Hotel!



Hii Hotel Kubwa Ili Milikiwa Na Mh Rais Ilikuwa Ni Hotel Ya Kitalii,wakapanda Mpaka Ghorofa Ya Juu! Wakati Hayo Ya Kiendelea Jeshi La Kinte Likaivamia Ganyama Na Kuanza Kuipiga Wakianzia Pale Mpakani!...



Rais Alienda kuoga,wakati akiwa bafuni Zidu Akaivua Ile Ngozi Akavaa Nguo Za Kijeshi,Rais goodluck kutoka,mambo yalisha badilika,wakati akiwa katika butwaa akapokelewa na teke,teke lililo mzindua,Rais Goodluck Pamoja Na Ukatil Wake Wote Akujua Kupigana,ZIDU alimshika na kumsogeza dirishani,akamtupia nje,toka ghorofa ya saba,huo ndo ukawa mwisho wa raisi yule,raisi katili,mwenye uchu wa madaraka



Vita vilipigana kidogo tu,ila taharifa zilizo kuja kuwa rais kauwawa,hii kisheria duniani ni kwamba taifa lilishashindwa,Rais moreti ii akatangaza kuwa yeye ndo rais wa taifa la kinte ganyama ikawa chini ya Kinte,ZIDU na KATARINA wakawa pamoja wakafunga ndoa kubwa jijin Bamala! Wakaanza Kuishi Kama Mume Na Mke,Rais MERNEL akampa cheo cha uwaziri wa jeshi ulinzi na aman bwana gambi,ila kwa bahati mbaya mimba ya Katarina Iliharibika!



SIKU CHACHE BAADAYE



"HAIWEZEKANI,KWA NIN YEYE AKUBALIKE KULIKO MIMI NA ANAONEKANA KUTAKA KUINGIA KATIKA SIASA ASIJE KUJA KUNIPINDUA MWITIKIO WAKE KWA WANANCHI NI MKUBWA SANA MAPEMA LAZIMA NIMZUIE,KABLA AJALETA MADHARA,LAZIMA NIMWANGAMIZE KATIKA USO WA DUNIA HII UTANSAMEHE ZIDU!



Rais Mernel ii aliwaza,ni baada ya kuona zidu akikubalika na wananchi kuliko yeye,akaijenga chuki katika moyo wake na kuapa kumuua mapema tu Zidu Kabla Mambo Ayajaaribika!...



Ataweza?!





Moyo wa Rais Mernel Gambi ii aukuwa na amani kabisa jinsi jitu katili likomandoo Zidu Lilivyokubalika Na Wananchi Kwake Ilimtia Uchungu Na Kuanza Kuona dalili za jitu lile kuingia ikulu na ilo yeye kama yeye akulitaka



Kila Walipopita Zidu Wananchi Walimshangilia Zaidi Yake Wakimwita 'mkombozi' eti 'mtetezi wa kinte'



'lazima Zidu Afe'



Rais Mernel Gambi akajiapiza palepale akaanza kufikiria ni mbinu gani mahsusi angeitumia kukiondosha iko kiumbe duniani,



Ilikuwa Ni Lazima atumie 'majambarika' yenye uwezo hata zaidi ya Zidu Mwenyewe,ila Je Angewapata Wapi Watu hao?!



Hilo Ndo Swali Lililo Mkereketa ,ila ilikuwa ni lazima apate ufumbuzi mapema sana!



Ni akili,kubwa sana ilipaswa aitumie mbaya zaidi jeshi lake lote lilikuwa chini ya 'kc' au kwa jina lingine Zidu K' Kila Njia aloifikiria aikuzaa matunda alipata usingizi usiku sana na hata alipoamka kichwa kilimuuma kwa sababu ya mawazo mazito,mke wake aliligundua hilo kwamba baba gambi hakuwa sawa ,alipo uliza sababu Merneli ii akuwa tayari kuwa muwazi bado alihitaji kufikiria zaidi kipi afanye...



***



Kundi La Mafia lilikuwa ni kundi au mtandao mkubwa wa kiuhalifu nchini Marekani Ulio Milikiwa Na 'mr X' mmiliki halali wa kundi hilo akuwah kutambulika zaidi ya jina hilo la 'mr x',ila msaidizi wake alitambulika kwa jina la Henry Leyland Au Lion Man Kijana alofuzu mafunzo ya kikomandoo na mwanachama wa fbi aliye hasi,



Fbi Ni Shirika La Kijasusi Nchini Marekani,



Lion akiwa katika jumba lake la kifahari lenye ulinzi mkali,ukiwa ni usiku wa manane ghafla akashtuliwa na mvurumisho wa simu,akafumbua macho yake,pembeni yake alilala mrembo wa kinyarwanda,akamwangalia kisha taratibu akatoka nje ya chumba kile na kupokea simu!



"ndio mr x"



Ni Neno Moja tu alilotamka, akakata simu macho yake yakadondokea katika saa ya ukutani ilokwepo pale sebuleni kwake Ilikuwa Ni Saa Nane Kasoro Za Usiku,Henry akarudi chumbani kwake,



Akapanda Kitandani,ila Akulala No akamgeuza chali yule binti alokuwa akikoroma,akampandia juu akausweka mkono wake katika shingo ya binti yule,akaanza kumnyonga,mnyarwanda na urembo wake maskin akatapa tapa pale mwisho akakata roho!



Hii Ndo Ilikuwa tabia ya mwanaume huyu,kunyonga na kuulia mbali mwanamke astarehe naye kingono,baada ya hapo akambeba mpaka nje kabisa ya nyumba yake akamtupa ndani ya shimo refu,walinz wa getin wakamsaidia kufukia...



Baada Ya Hapo Akarejea Sebuleni Akafungua Kabati Na Kutoa Bia Akawa Akinywa taratibu,alishika simu yake na kutuma sms kwa watu tofaut tofauti watano usiku ule ule,muda ule ule!



Ndani Ya Dakika Kumi Na tano toka ametuma ile sms gari zikaanza kuingia...



Kwao Ni Kama Kulikuwa Kumekucha!



Mbele Yake Kulikuwa Na Vijana Watano alowatumia sms na muda huo huo waka acha usingizi wao wakaja pasina kuchelewa



'snake man' au Richard Bowl alikuwa ni komandoo aliyelihasi jeshi lake la cuba na kupelekea kutorokea nchini Marekani na kujiunga na kundi la mafia lililokuwa chini ya mr x!



Pembeni Yake alikwepo mzungu mwingine alotambulika kwa jina moja tu la 'tiger man' huyu alikuwa ni komandoo wa marekani aloliasi jeshi naye kujiunga na kundi ilo la mafia



Pia Alikwepo Rich Killer,naye Alikuwa Ni Hatari Alopitia Mafunzo Ya Kikomandoo,na Kujiunga Na Kundi Hili Haramu,mwingine Alikwepo Ni Double Killer Akitokea Cuba Aliyelisaliti Kundi Lake La Moseti na kujiunga na kundi hili hatarishi na lipigwalo vita nchini Marekani Pia Alikwepo Mchina Aloitwa Kingyao Naye Kama Wenzake Alikuwa Ni Msaliti Wa Shirika La Upelelezi Nchin China Aliyesakwa Kwa Udi Na Uvumbi



Tofauti Na Hawa Watu Wa 5 Hatari Pia Mr X Alikuwa Na Washirika Duniani,na Alikuwa Na Makomandoo Walo Hasi Nchi Zao Wengi Sana



"'Black Snake' Ajawasili?!"



Lion Man Akahoji!



"haaa Atakuwa Kakumbatiwa Huyo!"



Snake Man Akajibu,



"ok,sis atusubiri mtu,tutamtoa katika hili deal acha sis tuendelee..."



Henry Akaongea Akiwa Kakasirika,



"lakn Boy Mara Kibao tu huwa nakwambia deals za usiku na watoto wa kike uziache!,.."



Kabla awajaendelea,nje ikasikika gari ikiwasili,mlango ukafunguliwa,ukatangulia mguu uliovishwa viatu virefu,kisha akashuka mdada,hakika alikuwa ni mrembo,mrembo haswaaa alivaa kimini kilicho acha paja zote nje,paja zilizo nona na kuleta mvuto kwa mwanaume amtazamaye kwa mwendo wa madoido akapiga hatua kuingia ndani ya jumba lile,huyu ndo alitambulika kwa jina la black snake,binti hatari zaidi ya hatari yenyewe,akukosewa kuitwa nyoka mweusi,uzuri wake ulikuwa tofauti na roho yake,



Lilipokuja Swala La Kuuwa Black Snake Alikuwa Katili Zaidi Ya Wote Pale,ukiingia Katika Mtego Wake,kupona Ilikuwa Ni Shughuli!...



Kuingia tu ndani wote wakanyamaza,akaketi kwenye kiti kilichokwepo wazi,Henry leyland akaendelea!

"kilichofanya niwaite usiku huu ni kutokana na simu niloipata kutoka kwa bosi 'mr x'...



Ndivyo Walivyo Mtambua Hakuna Walo Mfahamu Kwa Sura Wala Jina Lake Halisi Hata Msaidiz Wake Mwenyewe Aliishia Kuwasiliana Naye tu!



akuwah kumjua bos wake

kwa jina wala kwa sura!,basi akaendelea...



mr x katoa kazi na inapaswa tuifanye haraka sana,ikiwa ni order kutoka kwa rais mernel ii wa Kinte,kazi Yenyewe Ningependa Kuitoa Kwa Mtu Mmoja Coz Atuwezi Kuifanya Wote Kazi Ndogo Hii,sijui Hii Kazi Nimpe Nani!,lengo La Kuwaita Hapa Ni Ili tushauriane kaz hii afanye nani!...



"afanye black snake,itapendeza zaidi!"



"yah afanye yeye"



Wote Wakampendekeza Binti Yule Hatari Sana!







Kushangiliwa Kwake,kukubalika kwake na wananchi kunatengeneza chuki kali dhidi ya mwanaume wa kazi,jitu katili,jitu la miraba 4 Zidu K,anapanga kumuondosha katika dunia hii akihisi mbeleni kuja kukalia kiti chake,anatoa kazi kwa kundi hatari sana la mafia,nao kundi la mafia wanamtuma mwanadada hatari 'black snake' je unadhan nin kiliendelea black snake atauweza moto wa Zidu?,twende Pamoja!...



Kikao Kikafungwa Kukiwa Na Makubaliano Ya 'Black Snake' Mwanamke Wa Shoka Kufanya Kazi Ile,akukuwa Na aja tena ya kuondoka tena usiku ule waliamua kulala palepale,



Asb Sana Ndipo Walipotawanyika Henry akimwandikia hundi kiasi kikubwa cha hela, Masaa Manne Badaye Black Snake alikuwa anashuka katika uwanja mkubwa wa Kinte Na Ndege Ya Shirika La Ndege Nchini Marekani!



Akatembea Mkononi Kabeba begi lake,akaenda upande wa ukaguzi akakaguliwa akatoka kuelekea nje ya uwanja ule!



Nje alisimama kidogo,akiwaza ni kipi ambacho angekifanya, akachukua tax



"wapi madam"



"maeneo ya ikulu"



Uzuri Mmoja Ikulu Aikuwa Mbali Na Uwanja Wa Ndege,dereva Akawasha Gari Na Kuliondoa ,black Garl aliijua lugha ya kiswahili vizuri na siyo yeye tu,wana mafia wote waliitambua lugha hiyo na ndio waliyoitumia katika mikutano yao!



Walifika Maeneo ya ikulu,'snake' akamlipa dereva yule ela yake,akashuka garini,



"nikusubiri madam"



"hapana unaweza ukaenda"



Dereva Yule Akuongea Kitu Akaliondosha gari Lake taratibu,akimwacha mwanadada yule akielekea mahali ikulu ilipo



Mbele yake alikwepo askari aliyevaa nguo za kijeshi,huyu ni mmoja wapo wa walinzi wa pale ikulu!



"unamiadi naye?!"



Askari yule aliuliza pasina kupepesa jicho wala kuonesha tabasamu,alikunja sura,



"sina miadi naye,ajui juu ya ujio wangu ila mimi ni mgeni wake kutoka marekani!"



"uwezi kumwona"



Askari Yule akamjibu kwa mkato na kwa dharau,kitendo kile kilimkasirisha mwanamke yule

alitaman palepale amtemee sumu yake,lakin akawah kujitahadharisha, kwa kufanya ivyo alijua angeiaribu kabisa kazi yake!...



Kwa jicho alilo mkata askari yule,askar yule alishtuka na kuweka silaha yake tayari,black snake akarudi nyuma kidogo,akaishika simu yake na kuanza kuibonyeza bonyeza,yule askari na askar wengine walikuwa wakimtazama tu,ghafla yule askari akapiga hatua kumsogelea,



"tafadhali nakuomba uondoke maeneo haya!"



Askari Yule Akatoa Amri Pasina Kujua Anaendelea Kumkera Kwa Kiasi Gani Mdada Yule Hatari!



'katika Kuua Ntaanza Na Wewe Sitokuacha hai wallah'



Black Snake Akawaza



"mi Ni Mgeni Wa Muhimu sana wa mheshimiwa Raisi plz niruhusu nionane naye"



Black Snake garl akaamua kubembeleza baada ya kuona sasa akitakiwa aondoke eneo lile,kumuona mh Rais aikuwa kazi nyepesi hata!



"nimekwambia uwez kumuona mh kama huna miadi naye tafadhali nakuomba toka nisije nikausambaratisha ubongo wako!"



yule jamaa sasa akaanza kupayuka



"ukiingia kwenye mikono yangu sitokuacha hai haki"



snake garl akashindwa vumilia yule askar alitoa macho,akabak kaduwaa pasina kuamin kile alichokisikia



"e..e..e.ti..unasema..nin?" yule askari akauliza kwa kigugumizi,pasina kuamin kile alichokisikia,kabla ajafanya kitu ghafla askari mwenzake akawafata pale



"kuna nini Sam mbona Kama Mwagombana?!"



"hapana Kaka atugombani,mimi ni mgeni wa mh Rais,nimekuja kwa kumsapraiz na mwambia huyu ananzuia kumwona na mwisho kumtisha isiwe kesi ngoja niwasiliane na mtu,awasiliane naye mtaniruhusu tu!



Palepale Black Garl Snake akashika simu yake akatafuta namba flan akazipiga

"bos,nimefika hapa ikulu wamekataa nionane na mh rais embu ongea na mh niruhusiwe kuonana nae!"

upande wa pili,Henry Leyland Akampigia Simu 'mr X' Mkuu Wao,



"kuna Mtu Wangu Nje Ya Ikulu Kakataliwa Kuingia Ongea Na Mh Rais Aruhusiwe!"



Upande Wa Pili Aukujibu Kitu Ukakata simu,



Mh Rais alikuwa katika chumba chake kidogo alichokitumia kama ofisi yake,



Kichwani bado alikuwa na mawazo sana juu ya Zidu Ghafla Simu Yake Ikaita,haraka Sana Akaipeleka Sikioni



"kuna Mtu Wangu Nje Askar Wako Wanamzuia Kuingia embu ruhusu akutane nawe!"



"s...sa..wa"



Mernel ii akajibu kwa wasiwasi, akashika simu yake akampigia mmoja wapo ya wale walinzi pale nje!,

akatoa amri huyo mtu hapo nje aruhusiwe kuingia!

'Snake garl' akampiga kikumbo yule askari alokuwa akimzuia na kumwachia na sunyo,akaongozwa mpaka ndani ya ikulu!...



katika ofisi ile ndogo ambapo dakika chache Rais alijikalia peke

yake,sasa walikwepo wawili



"kilicho nleta kwako mh,kwanza moja nipate ifadhi,nyumba nzur gari,pili unipe information mahali ninapoweza kumpata huyu Zidu,ratiba Ya Mikutano Yake sababu najua inajulikana pia nipajue mahali anapoishi...



Rais akamwelelekeza kila kitu alichoitaji!,



"nahtaji Sam Huyu Kijana Hapo Nje Anipeleke Katika Hiyo Nyumba Ninayoenda Kuishi"



"aina tabu binti yangu!"



Rais Akaitika Akista ajabu kwa jambo lile,ila moyon mwake alijua pengine yule binti kashampenda huyo sam lakin kumbe aikuwa ivyo!

'huyu mpuuzi niliapa kumuonesha ndo atakuwa kafara ya ufunguz wa mahali nnapoenda kuishi'

haya ndo yalikuwa mawazo ya mwanadada black snake man,alitaka kumuoneshea Sam kwamba si kila mtu Niwa Kumdaharau!...







Basi rahisi alimruhusu Sam, ampeleke Snake Garl Katika Moja Ya Nyumba Zake Kubwa,

Sam alimuonea aibu binti yule kwa majibu alompa,



"si unajua tena kazi!"



"wala usijal najua ilo toa wasiwas juu yangu nishasahau"



snake garl aliongea huku akitabasamu,kwa nje alijionyesha ni mchangamfu,ila moyoni kulikuwa na chuki kali dhidi ya mtu yule!,



akupenda jinsi alivyo mdharau!

wakafka katika ilo jumba ambalo snake garl ndo alitakiwa afikishwe!...



Sam akafungua geti akaingiza gari,nyumba ilikuwa ni nzuri kama vile kuliishi watu,katika uwa kulikuwa na bustan nzur yenye miti iloleta hewa nzur,bwawa la kuogelea,pemben ya bustan ile kulizungukwa na marumaru katika uwa mzima mpaka getini,

snake garl aliinjoy kukaa katika jumba lile,Sam akashuka akafungua nyumba ya ndani kufungua tu akakutana na zulia la sufi,snake alikuwa akimfata kwa nyuma,mbele yake kuliko na korido ilogawa sebule na vyumba,sebule ilikuwa ya kisasa na safi! yani pale kulikuwa na wafanyakazi maalumu walokuwa wakienda kwa ajili ya kufanya usafi tu,na ajira yao iliishia siku hiyo,na ndivyo rais alivyofanya hivyo kwa nyumba zake zote!...



"sasa nikuache mrembo,mi nirudi kazini!"



Sam akaaga ile anageuka aondoke,nyuma yake akasikia sauti akiitwa!,akageuka akuamin macho yake pale alipotazamana ana kwa ana na bastola!,



Unajua mwanzo alidhani pengine kile ni kimada cha raisi,kwa kuwa ile ndo ilikuwa tabia ya raisi kuwajengea watoto wazuri nyumba kama ile ivyo binti yule kupewa nyumba ilo alikumshangaza,yani pamoja na uaskari wake akujua yule binti ni hatari!,si mtu wa kawaida yule



'kumbuka nilikwahidi hili ya kuwa sitokuwacha mzima,na snake garls,abatilishaji kile akipangacho...



Ulifanya kosa kubwa sana kunidharau pasina kujua mimi ni mtu wa namna gani!,mimi nikwambie tu natoka katika koo za hylear nchini marekani sijui kama ushawah sikia koo hizi sisi unyonya damu na kula nyama pia na tukikaa katika nyumba mpya kama hizi ni lazima kuzifungua kwa kumwaga damu na nyumba hii namwaga damu yako narudia tena ulifanya kosa kubwa sana kunidharau pasina kujua Mimi ni mtu wa namna gani...



Natokea wapi ni nani kwa Rais na nina shida gani naye,



Snake garl aliongea bastola ikiwa mkononi akipiga hatua ndogo ndogo kusogea eneo alilosimama Sam alokuwa akimwangalia kwa mshangao pengine alikuwa akijiuliza mtoto mzuri kama huyu anawezaje kuwa muuaji?!,japo jeshini walifundishwa kutomdharau mtu ila kwa binti huyu alijihisi yupo ndotoni....



Snake garl alilitambua ilo,akataka amdhihirishie kwamba ayupo ivyo amfikiriavyo!



"Najua uamini hiki nikisemacho na ili uamini,sitotumia silaha kukuulia ntatumia mkono,bastola ile akaitupa kochini,sambamba na kujirusha,ila Sam ghafla akazinduka,akajikunja kidogo mwanadada akapita na kwenda chini,akageuzisha shingo nyuma kumtazama Sam Kwa dharau,akajinyanyua na kuaanza kumpigia makofi!



akakaa mkao wa mapigano, akamfata Sam Akamtandika teke mbili kifuani Sam akazipangua,ya tatu akawa kama vile nayo anaituma kifuani,ghafla wakati sam anaipanjua akabadilisha uelekeo na kuusweka usoni,Sam akaachia yowe,



Akasambaratika chini ile anataka kusimama Snaje Aliruka Kwa Mtindo Wa Ajaku Akamsokotea Mapajani Mtindo Wa Kinyoka Nyoka,Sam na uanaume wake akashindwa furukuta,akamng'ata shingon na kuanza kumnyonya damu sambamba na kumnyonga hakika alimuua kifo cha ajabu sana ambacho akiwezi andikika,



baada ya hapo akaenda stoo akatoka na mamifuko makubwa akamuingiza mule ndani akaufunga,akarudi store akachukua sururu na beleshi akazunguka nyuma ya nyumba ile,mwanamke yule akaanza kuchimba shimo mfumo wa kaburi aliporidhika akaubeba ule mwili na kwenda akaufukia!



'nishafungua kazi kwa mafanikio,anaye fuata sasa ni huyu Zidu,jiesabie Una Masaa Kadhaa tu ya kuendelea kuish kabla ujaingia kwenye mikono yangu Zidu'



akawaza huku akifunga geti lake,akaenda kuoga!,akajikalisha sebuleni kuwaza njia nzur ya kummaliza Zidu!



***



Kadri Siku Zilivyozidi Kwenda Ndivyo Zidu alivyozidi kupata sifa,watu wakaanza kumshahuri miaka ijayo agombee uraisi,jambo lile alilipinga kwa mikono miwili,yeye binafsi akupenda ile nafas hata uwaziri wenyewe aliupokea basi tu,kutomkatalia mh rais nafasi ile alompa,ndani ya chama cha uhuru pakatokea mgawanyiko,wengine wakipendekeza miaka mitatu ijayo apewe zidu wengine wakisema rais mernel ii amalizie ndipo Zidu awekwe!



kwa machaguo yote mawili kwake Mernel Yalikuwa Mabaya,alitaman baada ya hiyo miaka mitatu yeye aendelee na baada ya miaka mitano amweke mwanaye pekee Gambi,mjeda Aliyoko Nchini Kongo Akilinda amani



'utakufa tena vibaya tu!'



akazidi kumuwazia vibaya Zidu Wakati Huo Ghafla Breaking News Ikaoneshwa Kwenye taharifa habari kutoka shirika la habari bbc kwamba askar wa umoja wa mataifa Laurent Mernel Gambi Amefanikiwa Kuwaokoa Wamama Na Watoto Walotekwa Na Waasi Nchini Kongo!,kwa Sasa Kijana Yule Pekee Wa Rais Wa Kinte Mernel Gambi Akazidi Pata Sifa,baada Ya Habari Ile Simu Za Pongez Kwa Rais Zikaanza Kuingia Moja Wapo Ya Watu Walompongeza Ni Waziri Wake Wa Jeshi,ulinzi Na Aman Zidu Kite!



Rais Mernel Akacheka kwa dharau!...







Rais Mernel ii akacheka kwa dharau!,



"kuna mkutano wa 45 wa umoja wa mataifa mwaka huu unafanyika nchini mwangu mkoani gano tafadhali mh wazir mi sipo vizuri naomba ukaniwakilishe!"



"sawa mh Rais usijal kwa ilo,nitaenda"



Zidu akajibu,akakata simu, akamgeukia mgeni wake alomtembelea kamanda mkuu wa majeshi kamanda laizer nyoshi,



"nilikuwa nikiongea na mh rais kaniomba nikamuwakilishe gano katika mkutano mkuu wa kimataifa"



Zidu akampa taharifa rafiki yake yule,walopendana,katu akujua kule alikuwa kaandaliwa kifo!,baada ya kumaliza kuongea na Zidu Muheshimiwa Rais Ambaye Kwa Sasa alikuwa na namba za snake

garl akampa habari kwamba kesho kutwa hiyo ilikuwa jumatatu yan jumatano ilitegemewa Zidu angeenda katika mkutano mkoani gano ivyo ndo muda wa kwenda kukamilisha kazi alokwisha mpa,snake garl akamtoa wasiwas akimwambia aesabie tu kazi ile imeshaisha!,Mernel ii akatabasamu!



****



NCHINI MAREKANI



IKULU



Ikulu nchini Marekani Kulikuwa Na Kikao Kilichohusisha Viongozi Mbalimbali Wa Nchi,

Majemedari, makanali Wa Jeshi Na Viongozi Mbalimbali Wa Juu Kitu Kikubwa hasa walichokuwa wakikijadili ni juu ya kumkamata gaidi no 1 duniani Osama Bin Laden,eneo Alilokwepo Huko Nchini Pakistan Lllishatambulika Ni katika milima iliyokwepo karibu kabisa na kambi ya jeshi!...



makomandoo mahsusi walisha andaliwa,ila kikao kile kilikwepo kujadili ni mtu yupi hasa ambaye angeweza kumuua mtu yule alosemekana kwamba ni gaidi!



Orodha Ya Majina Ya Makomandoo Wa Kubwa Wa Kimarekani Ilikwepo Mezani Ila Bado Aikukidhi Ikapendekezwa Pia Majina Ya Wanajeshi Wa Nje Walowah Kufanya Maajabu Akiwemo Isack,



Zidu Na Hata Mtoto Wa Rais Mernel ii aliyekwepo nchini kongo kwa kazi ya umoja wa mataifa,

wakaanza kwa kumchambua Zidu,huyu Sifa Yake Ni Kuweza Kumwangamiza Waziri Alex,pia Akiwa Katika Sura Ya Bandia Akaweza Kumuua Rais Silvestar wa ganyama,

ITAENDELEA

Simulizi : Kiapo Cha Mfungwa (5) 

Sehemu Ya Pili (2)





Je huyu atafaa,abadilishwe sura,wazo ili wengi wakalipinga wakamjadili pia Isack,sifa Yake Kubwa Ni Wakati Akiwa Mafunzoni Aliweza Kumwangamiza Kamanda Wao Alokuwa Akijibadilisha Na Kuuwa Baadhi Ya Maaskari,ila mazoezi Ya Kikomando Isack Akuwa Nayo,pia Jina Lake Likawekwa Pembeni Jina La tatu lilikuwa ni la mtoto pekee wa mh Mernel ii k'g au komandoo gambi!,



Kutajwa tu kwa jina hilo watu wote wakapiga makofi,tabasamu likachanua katika nyuso zao,sifa yake kubwa aliwah kutumiwa na waasi wa iraq kumkamata rais wao Sadam Hussein Akiwa Peke Yake Katika Mapango Huko Nchin Iraq Pia Sifa Yake Nyingine ni hii ya majuzi tu akiwa nchini kongo akiwa na baadhi ya wanajeshi wa kongo walielekea mpaka ilipo kambi ya waasi kabla awajafika roho ya paka gambi alishuka na wakati kifaru kile kikishambulia yeye kwa miguu alifanikiwa kumteka askar mmoja akavaa nguo zake,



Kwa siri sana akawatorosha mateka walotekwa,waliposhtukiwa alipambana kiume,mpaka akafanikiwa sifa hizi mbili zikampa point ya kuchukuliwa kwenda kufanya opereshen hiyo ya kumuua osama bin laden!,kamanda wa mawasiliano akapewa kaz awasiliane na umoja wa mataifa aikuwa kaz ngumu sana kwa kuwa ofis za umoja wa mataifa zilikuwa palepale baada ya kikao akaenda kuonana na mkuu wa umoja ule akampa habari zile,mkuu akawasiliana na serikali ya kongo!



Kesho Yake asbuh Gambi alikuwa mbele ya jopo lile la viongoz wa kubwa wa kijesh wa kiongozwa na Rais wao Barack Obama,akapewa Juu Ya Kazi Ile Alopaswa Kwenda Kuifanya!



Gambi akuamin,moyo wake ulipasuka kwa furaha,raman ikawekwa mezani, akaisoma, mipango ikapangwa kwa siri sana ndege isonaswa na siteline na ndege zinazoendeshwa na rimoni tatu na za maroboti mbili zikatumwa,



Wakati ndege zile zenye maroboti zikiwasil hatua chache nyuma ndege isonaswa na sitelait ilishuka chini kidogo,mwanaume gambi akashuka kwa kutumia kamba wakati walinzi wa pango lile wakiangaika kushambulia zile ndege pasina kujua zinakontroliwa na rimoni gambi na wenzake wakazama ndani ya pango ambapo kulikuwa kumejengwa, pale pale gambi akafyatua risasi kadhaa kifuani mwa osama bin laden,wakati huo huo ndege zenye mabom ziliwashambulia walinzi wa ngome ile,



Osama kwa kuwa alikuwa ana sifa ya kupotea au kubadilika kuwa wengi wakamchukua na kumtupia ndani ya pipa la tindikali lililokwepo kulekule ndani ya pango!...



Huo ndo ukawa mwisho wa Osama Bin Laden,mazish Yake Wala Kifo Chake akikuonekana,kwa sababu ndani ya pango lile apakuwa na kamera za aina yeyote,na wanajesh wale awakukumbuka kuja na kamera!,ila tukio lile fbi walilishughudia kupitia sitelite zao wanazojua wenyewe jins walivyozitegesha,wakajidhihirisha kuwa K'g alifanikiwa kumuua Osama Bin Laden!



Gambi jina lake likazidi kupaa,akazidi kupata sifa,akalipwa mabilion ya ela,akarudi zake kongo akiwa na furaha,alikuwa sasa ni zaidi ya komandoo!



'nisingeogopa ningemtumia mwanangu kwa kazi hii lakin atanfikiriaje mimi?'



Mernel aliwaza baada ya kupokea taharifa za mwanae kufanikisha kumuua Osama Bin Laden!...



Huyo Alikuwa Ndo Gambi Roho Ya Paka!



*****



GANO



Mkutano Wa 45 wa umoja wa mataifa ulikuwa ukifanyikia gano,hotel mbalimbal karibia na ukumbi mkubwa wa giraffe zilifurika,



Snake Garl aliwasili gano mapema tu,akaelekea moja kwa moja katika hotel iloitwa Shamsi Hotel akupitia mapokezi akapanda ngazi mpaka ghorofa ya tano chumba no 3 akabonyeza 123 mlango ukajifungua akazama ndani akafunga mlango na kukaa kitandani!...



Zidu Naye Aliwasili Katika Hotel Ile Ile,akafikia Mapokezi

"naeza Pata Chumba"

Akamuuliza Muhudumu alomkuta pale mwenye asili ya kizungu,akumshangaa sana si hotel ya kitalii ile

"chumba baki moja tu ghorofani nikupatie"



"yah!"



mzungu akampa kitabu Zidu

akajaza jina lake,namba zake,siku atakazokaa,akaruhusiwa akakwea lift mpaka ghorofa ya tano,chumba namba tatu! akaingiza funguo!...



Kule Ndani Wakati Mwanadada Kajilaza head fone masikion ghafla akanong'onezwa huyo mtu anakuja,akainuka kwa ghafla silaha mkononi hatua ya kwanza ya pili nyuma ya mlango,kitasa kikatingishika ishara ya kufunguliwa mlango ukaanza kufunguka Zidu akazama ndani pasina kujua kuna mtu nyuma ya mlango,binti hatari sana!







Rais Mernel ii anamweka Zidu Katika mtego,anamtuma katika mkutano na katika hotel ambayo Zidu anafikia anategesha mtu,Zidu pasina kujua anafikia katika hotel mojawapo anakuta kimebakia chumba kimoja tu huko juu ghorofa ya tano,anaomba apewe icho icho pasina kujua mwanamke hatar kashajifika anafungua chumba kile na kuingia snake gar anajibanza nyuma ya mlango!...



Tusonge...



Snake garl kabla ajafyatua risasi,alihisi pigo butu mkononi,risasi ikapaa!...



Pigo butu ni lile pigo lisilo leta maumivu ila upigwa kwa nia flani,snake garl akujua ni sangap Zidu alimuona na sangapi alimfikia pale!



Zidu alikuwa ni mwepesi



Sasa wakawa wakiangaliana, hakuna alofumbua mdomo wake kuongea kitu japo Zidu Kichwan Kwake alikuwa na maswali mengi ya kujiuliza,



yule ninani?!,



katumwa na nan,au lengo lake ni lipi hasa?



na kwa nin atake kumuua?!



Lakin Ule Muda Ulikuwa Si Muda Wa Kumuuliza Maswali Yale,alijua asingepata majibu sahii,majibu upatikana baada ya muulizwaji kuwa hoi,ndo kwanza muulizwaji wake alikuwa kakaa mtindo wa mapigano,usoni kapendezeshwa na tabasamu lililo muongezea urembo!



Yule binti alikuwa ni mrembo hasa,mtu akikwambia ni binti hatar ni vigumu kukubali,ila Zidu alikuwa tofauti na Sam kudharau mtu kutokana na uzuri wake,wakati akiwa katika dimbwi la mawazo mwanamke yule akaruka teke,likiwa limebakia kidogo kumfikia Zidu akalipangua sambamba na kurusha ngumi shavuni kwa mwanadada yule,damu zikaanza kumtoka mdomoni,wakati akisikilizia maumivu yale Zidu akamsweka teke la tumboni,mwanadada chini!



Zidu akamfata pale alipo, akamkanyaga shingoni na kuanza kumsigina!



"nani kakutuma wewe uniue,au kwa nin unataka kuniua?"



Akamuuliza huku akiwa bado anamsigina ila yule dada akujibu kitu!,kila teso Zidu alilo mpa dada alikuwa kimya!



Kwa sasa Zidu akutaka kumuua ila aliamua kuiachia sheria, angeteswa Lazima Angeeleza Kila kitu,baada ya kuwasiliana na polisi,polisi waliwasili wakamvisha pingu yule mwanadada wakamtoa chini ya ulinzi mkali Zidu alipoenda mapokezi cha ajabu akumkuta yule mzungu alompa chumba na hata alipo uliza katika hotel ile apakuwa na mfanyakaz mzungu!,Zidu alichoka!



ile kesi akampa kijana brown aifatilie,ni kijana aliyemwamini yeye akaudhuria mkutano ule!



Brown Stanley, alipaki Gari Lake Maeneo Ilipo Magereza, akapiga hatua ndefu ndefu kuelekea ndani ya magereza yale,siku Ya Leo Ilikuwa Ni Siku Ya tatu anamuoji yule binti pasina mafanikio, akulitambua jina lake halisi,kwa nin alitaka kumuua mh waziri



dada alikuwa sugu,



jambazi sugu!



Kwa Uzoefu Wake tu,brown aling'amua yule si mtu wa kawaida,siku hii ya leo alikuja na mbinu mpya kumchoma sindano itakayo mfanya mtu yule aeleze ukweli kufika ndani ya magereza akashtuka baada ya kukuta mwili wa yule dada umelala sakafuni,kwa kuuona tu bila kuugusa aligundua tayari ni maiti yule!



maswali mengi yakakishambulia kichwa chake,amekufaje?,ila akutaka kujiuliza sana akijua madaktari pekee ndo walikuwa na majibu ya maswali yale,haraka sana akampigia simu mkubwa wake Zidu Kumwambia,zidu alishangazwa na jambo lile,akamwambia tu ripoti ya hosptalin ampatie!...



Brown,akaitikia,akawageukia walinzi wa zamu!



"kuna yeyote alokuja kumcheki?!"



"yah walikuja vijana wa nne wenye asili ya kizungu wakaongea naye,ila sisi tulikwepo,wakampa pole na chakula wakaondoka zao"



"chakula icho walikionja?"



"ndio mkuu walikionja!"



"kilikuwa chakula gani?!"



"wali maharage"



Badae Ripoti Ilipokuja Kutoka Hosptalin Ni Kwamba Yule Dada 'black Snake' alikufa kwa kula sumu!



Sasa kama chakula akikuwa na sumu,kivipi afe kwa sumu?,na walo mletea chakula hiko ni wazungu wakisema ni ndugu zao,mbona huyu ni mwafrika?



hali ya sintofahamu ikazuka katika fikra zake,mtu pekee wa kushauriana naye si mwingine zaidi ya Zidu!,ule Mwili Ukazidi Kuwa Chin Ya Askar Wa Upelelez Kwa Uchunguz,cha ajabu sasa hata wale wazungu walojiita ndugu zake awakuonekana tena!...



Baada Ya Uchunguzi Sana Ikiwemo Kuchukua Alama Za Vidole Kukagua Katika Wahalifu Sugu Hatimaye Ikagundulika Kuwa Yule Dada Ni Mwanachama Wa 'Mafia'



Mwili Wote Wa Zidu Ukasisimka,alilijua Kundi Lile Hatari Duniani,



Kwa Nin Sasa Atake Kumuua?!,kakosa Nini,au Kama Ni Order Imetolewa Na Nani!,ilipaswa Sasa Awe Makini,aliona Maisha Yake Sasa Ayapo Huru!



'nala *kiapo* Kwa Yeyote atakayeingia katika anga zangu sito muacha hai'



Zidu aliwaza sononeko moyoni mwake!



****



MAFIA NCHINI MAREKANI



Watu wale walikutana tena,mioyon mwao wote walikuwa na majonzi ni baada ya kupata taharifa ya kukamatwa kwa mwenzao snake garl



"sasa kazi hii ya kumwangamiza huyu mtu itafanywa na nyinyi wote wa nne,kesho mtasafiri kuelekea Kinte,cha Kwanza Muakikishe Mnamkabidhi Kidonge Cha Kifo Snake garl kwa siri sana ili akibanwa sana ajimalize!



kisha mumuwinde huyo shetan mwa kiafrika mumuue kikatili sana,mkumbuke nusu ya ela nishapokea na nusu ndo mshahara wenu,mkirudi huku mrudi kwa mawili mrudishwe maiti au mrudi na ushindi sawa?!" Henry Leyland aliongea kwa uchungu!



"ndio mkuu!"



Vijana Wale Wakaitika Wote Wakiwa Wamekasirika,hasira Zao Juu Ya Zidu azikumithilika,



Kesho Yake Saa tano za asbuh walikuwa wakishuka kwenye ndege yao,wakaelekea katika hotel walopangiwa!



Saa Saba Kasoro Walichukua Chakula Wali Maharage Hotelin Pale Na Kuelekea Mpaka Gerezani,wakahitaji Kuonana Na Snake Garl Yule Aloshika Sahani Ya Chakula Kwa Chin Alishika Kidonge Kile Cha Sumu,askar Wakawaambia Waonje Wakaonja Kijiko Kimoja Kimoja Wakati Wanampa Sahani Kwa Chin Kulikuwa Na Ile Sumu, wakakonyezana,snake Garl Akabandua Ile Sumu,akala Chakula,usiku Ndipo Alipomeza Kile Kidonge, akalala milele!, halmashauri ndo walouzika mwili wake baada ya uchunguzi kukamilika!...







Nyumba Ya Zidu Ilikuwa Ni Nyumba Moja Wapo Ya Nyumba Iliyoko Maeneo Ya Kisangire,



Kisangire Ni Eneo Walilokuwa Wakiishi Viongozi Wa Nchi Na Watu Matajiri



Zidu aliishi yeye mke wake Katarina Na Dada Wa Kazi,jion hii vijana wale watatu walikuwa katika bar ndogo moja ilokuwa jirani na nyumba ile wakipata bia kumsubiria Zidu Awasili,



Ndani Ya Jumba Lile aliketi kijana snake man katika kochi kubwa chini ilikwepo maiti ya msichana wa kazi katika meza ndogo ya kioo ilikwepo bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti yani 'perforated sylinder' nje ya nyumba ile katika uwa alikwepo Rich Killer aliyesababisha mauaji ya walinzi wa nyumba ile na kuwaifadhi katika chumba chao geti liliachwa wazi kimtego!...



Watatu Wale Walobakia Kwenye Ile Bar Ndo Walotoa taharifa kwa wale wa ndani,watu wote walikuwa na hearfoni katika masikio yao kwa ajili ya mawasikiano



Kwa Wale Wa Bar hakuna alotia shaka uwepo wao mahali pale kwani walionekana kama wateja wengine



Dakika Chache Badae Gari Likawasili,ndani alikwepo Zidu,aliliingiza gari lake katika nyumba yake akishangazwa na kuachwa wazi kwa mlango na kutowaona walinz pale getini akujal sana ilo alipanga apeleke gari lake parking akalipaki kisha ndo harudi kujua kulikoni!



Akafika akalipaki vizuri akashuka, sasa akawa anaelekea getini ghafla akashtukia pigo moja katika shingo yake 'cating' machale yakamcheza,kwa wepesi wa ajabu Zidu Akajigeuza Nyuma Kumuona Adui kwa teke kali,kwa bahati mbaya Rich alijipinda na wakati huo huo alirusha ngumi nzito ilo mpata sawia Zidu Katika Mdomo Wake Zidu akaserereka kidogo ila akakaa vizur akawa tayari kashajigeuza!



Macho Kwa Macho Na Adui!



Mzungu!...



Mafia Man!,



kengele Ya Hatari Ikagonga Kwenye Kichwa Chake Akajitahadharisha Kuwa Makini



Japo Pale alipopigwa ngumi mdomoni kulimuuma na kuvuja damu katu akuthubutu kuugusa mdomo eneo lenye maumivu akijua fika hiyo nafasi ingemmaliza ikabidi Zidu ajiongeze amchanganyie adui mapigano akatumia 'savate' huu mtindo alijifunza ufaransa akipiga ngumi na mateke ila siyo ya kupiga kick box,niya kutega na kudonoa!



Wakawa Sasa Wanaviziana,staili hii ikamsaidia kupunguza spidi ya Rich Killer Na Kwa ghafla alichutama akanyoosha mguu kwa lengo la kumpiga mtama Rich,kitendo Kile Kilisomwa Mapema Na Rich akaruka kidogo mguu ukapita muda ule ule akaukanyaga ule mguu kwa nguvu ukalia kaaa!



Zidu akaachia yowe dogo la maumivu,



"nishavunja Mfupa Mmoja"



Alibweka Rich Killer akimsindikiza Zidu Na teke kali,Zidu akaenda chini



Rich Palepale akabonyeza kifaa katika hearfone yake na kuongea maneno machache "njoo huku nje!"



Snake Man Pale Sebuleni alipokunja nne,ghafla mlio ukaingia kwenye simu yake!



Akautazama Na Kutabasamu,akachukua Bastola Yake Na Kuisweka Kibindoni Akauruka Ule Mwili Wa Mfanyakazi Akatoka Zake Nje!



***



Ni Kila Kwenye hatari tendo hilo umtokea,toka akiwa kazini akili yake aikumtulia,alihisi hatari katika kichwa chake kwa kuwa muda ulikuwa umeenda saa kumi na moja kasoro akajinyanyua akaingia ndani ya gari lake tayari kuelekea nyumbani!



Alipofika alikuta geti la nyumba yake lipo wazi Katarina Akashangazwa Na Ilo 'ni Nin Kinachoendelea Hapa?!" Akawaza,akapiga honi mara mbili akaona aingie tu

baada ya kuingiza gari akashuka na kufunga geti,akaenda chumba cha walinzi huku akiita ile anafungua chumba kile akakutana na miili ya walinzi wake,ikiwa na matundu ya risasi ile anageuka akakutana na kitu kizito,akaenda chini!

palepale giza likautawala uso wake akapoteza fahamu,pasina kujua hata alomshambulia ni nani!



ni pigo la haraka,la ghafla na alopigwa sehemu mbaya!



Vijana Wale 2 hatari walokuwa wamejibanza nyuma ya kijumba kile wakamnyanyua Katarina Wakamuingiza Nyuma Ya Gari Yake,mmoja akaingia ndani ya gari akawasha mpaka maeneo ya parking pale ambapo Zidu alizimishwa akasimamisha gar



"mlejen huyo humu!"



"atakaa sasa huko ndani"



"atakaa bwana!"



"no awekwe kwenye buti sote atutatoshea humu ndani"



"wengine si watakuja na gari ile"



Rich Akajibu Akioneshea Kidole Ile Gari Ya Zidu Alokuja Nayo!



Mabishano Yakafatia!



Mwisho Wakakubaliana Waondoke tu na gari moja ivyo mwili wa Zidu Waloufunga Kwa Pingu Wakauwekwa Kwenye Buti,katarina wakakaa naye kule ndani!



Gari Ikatolewa Kwa Mwendo Mkali Ndani Wakishangilia Kwa Kazi Nzuri Waloifanya Waliiacha Barabara Ya Lami Na Kuelekea Katika Msitu Mnene wa Lwana Msitu Ulosifika Kwa Kuwa Na Wanyama Wakali



Wakiafikia Kuchimba Shimo Na Kuwafukia Wote Kwa Pamoja Wakiwa Wazima Wazima Huku Wakiwachukua Kamera Kama Ushahidi!



Waliwasili Lwana Wakaitoa Miili Ile Ya Katarina Na Zidu!,ilopigwa Pingu Za Miguu Na Mikono!,tayari Ilikuwa Saa Moja Za Usiku Wakaanza Chimba Shimo Baada Ya Kumaliza Wakaidumbukiza,kabla Awajaifukia Rich Killer Akatoa Wazo



"tumpigie Simu Mheshimiwa Kumwambia Kuwa Ndo Tunamfukia Atoe Idhini"



Wakampigia Muheshimiwa Rais Ambaye Hata Ivyo Aliwaambia Asubir Awasili Mwenyewe Kuja Kushughudia!,



"autochelewa Muheshimiwa?!"



"hapana Nakuja na ndege yangu binafsi dakika tano tu!



Kwel Dakika tatu badae mlio wa ndege ukaskika ikatua,ikaja mpaka maeneo yale,Rais Mernel Akashuka!



Zidu akuamin eti kama Rais Wake Ndo Aliye Mfanyia Vile,akakumbuka Alivyojitoa Kwake Ganyama Leo Hii Anamlipa Kifo!,machozi Yakaanza Kumtoka!



"najua unajiuliza kwa nin nakuua,kukubalika kwako na wananchi ndo kunanifanya nikuue,nisipofanya hivi badae utakuja ninyang'anya kiti changu nami sipo tayari bado namiaka mitano ya kuitawala Kinte Na Baada Ya Hapo Mwanangu Gambi Ndo Kitaimiliki hii ardhi lakin si wewe!,leo nakuua na aitojulikana umekufaje na nani kausika kifo chako kitabaki siri,ha ha ha ha ulifurah ulivyoitwa mtetez wa Kinte!,eti Mkombozi Jikomboe Sasa,eti Kc Mara Zidu Leo Ndo Mwisho Wako!"



Rais Mernel ii aliongea kwa dharau Zidu Na Katarina Wakiwa Chini Pingu Za Miguuni Na Mikononi Zikishindwa Kuwafanya Wajitetee Wakajua Sasa Huu Ndo Mwisho Wao Wakafumba Macho Kusubiri Kifo Chao!



Tayari Rais Alishamuelekezea Zidu Bastola,usoni, Zidu Kafunga Macho Ivyo Akaanza Kuhesabu



Moja..Mbili...Tatu



Paaaaaaaa



Mlio Wa Risas Ukasikika!,damu Zikaruka,ubongo Ukatawanywa...



Ni Zidu Au Katarina Katawanywishwa




ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog