Search This Blog

Thursday, 29 December 2022

KUFA TU HAKUNA NAMNA - 1

  

Simulizi : Kufa Tu Hakuna Namna 

Sehemu Ya Kwanza (1)

    


IMEANDIKWA NA : ZUBERI MARUMA


********************************************************************************


Simulizi : Kufa Tu  Hakuna Namna 


Sehemu Ya Kwanza (1)






Wengi walimtambua Kwa Jina la 'ZK' mwandishi wa kujitegemea ambaye wengi awakuijua sura yake wala uhakika wa jinsia yake kwa ajili ya usalama wake,




Alipenda kuvaa maski nyeusi usoni,koti jeusi mkononi alitupia 'gloves' nyeusi pia alivaa 'jeans' nyeusi na chini kabisa alivaa viatu vilivyobebwa na soli nzito,pia vikiwa ni vyeusi,...




'ZK' alijipatia umaharufu kwa kuvujisha siri mbalimbali za serikali,na hata za watu binafsi,mara kibao aliruka vizingiti vya kifo,pia sehemu alipokuwa akiishi ilikuwa ni kificho mpaka siku hiyo alipokuja kugundulika na kuacha mshangao ndani na nje ya nchi wengi wakishindwa kuamini kama ndo yeye...




SURA YA KWANZA




Siku hiyo 'ZK' alitoka katika miangaiko yake akiwa juu ya pikipiki yake,




Alikuwa akielekea nyumbani, wakati akiwa njiani katikati ya usiku ule ghafla gari moja ikampita kwa spidi,




Akashawishika kuitazama namba ilosajiliwa katika gari ile alishtuka baada ya kuona ni namba za serikali,




Kwa mantiki hiyo gari Ile Ilikuwa ni ya serikali,




Hali ya udadisi ikamtawala mtu yule,




Kama mwandishi Na Pia Kama Mpelelezi Kwa Kazi Ilokuwa Siri yake aloifanya kupitia kivuli cha uandishi akatamani kujua juu ya gari ile ya serikali kumpita tena kwa spidi usiku mzito kama ule?!...,




'Inaenda Wapi,ndani yuko nan?!...'




Maswali kibao yakajijenga katika kichwa chake




Akakata shahuri liwalo na liwe wacha aifate pengine imeibiwa,kwa siri sana akaanza kuifatilia!...




Kadri alivyokuwa akiifatilia gari ile ndivyo alivyozidi kupatwa na wasiwasi,siyo wasiwasi wa uwoga!, la ashaaa!




hapana!...




Ila wasiwasi kwamba wale si watu wazuri,ilo akujali ndo kwanza damu ikazidi mchemka , akazidisha umakini, kiunoni alikuwa na bastola yake yenye risasi za kutosha,pia aliuamini uwezo wake wa kupambana,ivyo akutaka kuiruhusu hofu imtawale akazidi kusonga kuwafatilia...




Katu akujua kwamba nyuma alikuwa akifatiliwa na watu hatari...




Akili zake alizishurutisha kufatilia mbele tu katu akujua nyuma pia kulikuwa na gari ilokuwa ikimfatilia na walokuwa kwenye gari hiyo ya nyuma walikuwa wakiwasiliana na wa mbele,naye alikuwa kawekwa kati...




Ndani ya gari ile ya serikali kulikuwa na watu watano, nyuma alikwepo msichana mmoja ambaye alikuwa kafungwa mikono yake na miguu kwa pingu uso wake wote ulikuwa umevimba kuonesha alipata mateso makali pia nguo zake zililoa damu,alikuwa akilia ila walokuwa ndani ya gari ile awakuonesha kujali kilio chake ndo kwanza walikuwa wakicheka huku wale vijana wawili walomuweka kati wakimchezea mwili wake kijinsia...




"oyaaaaa Veko Leo ana kwa ana na 'ZK' piga ua leo ndege wawili tunaua kwa jiwe moja"




Dereva alotambulika kwa jina la Pizzo aliongea akionesha wazi kufurahia kumuona "ZK" mbele yao...




Wao Kama wao Walimjua yule 'ZK' ni Mwandishi tu,na toka muda mrefu amri ilishatoka makao makuu ofisi ya waziri mkuu chini ya kitengo maalumu cha usalama wa taifa kuuwawa kwa mwandishi yule...




Hii ni kutokana na yeye kuvujisha siri nyingi za serikali,ivyo akawa akiichafua serikali,katu ofisi ya waziri mkuu aikujua kuwa yule kapandikizwa na Raisi makusudi ili akivujisha vile Raisi anapata faida fulani kivipi sasa?!.....




MTU HUYU NA RAISI WALIKUWA NA SIRI NZITO!




Mtu yule 'ZK' akiwa juu ya pikipiki yake alikumbuka siku wakiwa 'privet' na mh Rais,maneno rais alomwambia...




"kijana wangu naamin ufanyaji kazi wako, nimekutoa na kukusaidia hili nawe pia unisaidie,utafanya kazi chini yangu ila ripoti utonipa mimi,hapana...




Naitaji uwe mwandishi wa habari ila ficha sura yako isitambulike ovu lolote utakaloliona katika serikali yangu nilione katika televisheni!..




....na maana yangu na ipo siku utajua nini na maanisha...




...najua ni kazi ngumu nayokupa ila fanya kwa weledi utafanikiwa"




Mtu yule juu ya pikipiki yake alizidi kukumbuka,na kujikuta akizidi kukanyaga mafuta kuifatilia gari ile kujua hasa lipi lengo lao...




Gari ile ikazidi kuchanja mbuga kuingia maeneo ya porini, 'ZK' akazidi kuifatilia




Mbele kidogo gari ile ilisimama naye 'ZK' akasimamisha pikipiki yake milango ikafunguliwa vijana wawili wakashuka kutoka milango ya mbele wakafungua mlango wa nyuma kijana mmoja akashuka akamvuta mtu na kumtupa chini




Yule dada akaachia yowe,haraka 'zk' akashuka kwenye pikipiki yake aloipaki nyuma kidogo akijua ajashtukiwa akaanza kuwafata kwa kunyata silaha ikiwa mkononi,kwa kujificha akawa akisogea eneo lile,alijua giza lilimsaidia,




Wale watu wa tatu walokuwa na gari wakiwafata kwa nyuma nao walishuka kila mmoja akiwa na silaha yake wakawa wakisogea eneo alilopo 'ZK' kwa uangalifu kukwepa kumshtua...




"utatupa hiyo memory au utupi?"




Zk alisikia mtu mmoja akiuliza kwa ukali kabla dada yule ajajibu mtu yule akaunyanyua mguu wake na kuushusha kichwani kwa mwanamke yule ambaye aliachia yowe




ZK alimtambua yule mwanamke kama mwandishi wa habari sasa akawa akijiuliza ni memory gan wanayoitaka ambayo mtu yule anayo?!




Pili kwa pale alipaswa afanyaje,je aokoe au apige picha na siku inayofuata atoe habari zile kama Rais alivyo mwagiza?!




Palepale akatabasamu baada ya kukumbuka kuwa wale watu wanataka kitu kwa yule dada ivyo wasingemuua mpaka yule dada aseme ilipo hiyo memory kumleta kule ni kumtishia tu ivyo ilipaswa afanyaje?!




Afanye Kaz yake ya kuchukua tukio lile mpaka mwisho




Alijua mwisho baada ya kumtesa na kupoteza fahamu wangemrejesha na kesho kuendelea kumtesa mpaka aeleze ilipo hiyo memory card ivyo tukio la kuripoti lingemfanya mwandishi yule kuwa huru hapo 'ZK' akatabasamu kwa mara ya kwanza akamuelewa Rais Wake alikikuwa na maana gani kumpa kazi ile




Akavua Kibegi Chake Na Kutoa Kamera akaanza chukua tukio lile pasina kujua watu walokuwa nyuma yake walishughudia kila kitu alichokuwa akifanya...




"usemi siyo 'P' maliza"




'ZK' akuamini macho yake pale aliposhughudia risasi zikikishambulia kifua cha yule dada,mwili ulimlegea akajikuta akishindwa kuishika ile kamera na kuiachia ila ghafla kitu kizito kikatua kisogoni mwake,giza likatawala,akaenda chini!


Akapoteza fahamu!




Ilikuwa ni kazi nzuri ilofanywa na wale watu walokuwa nyuma yake bila yeye kujua mmoja alimpiga na kitako cha bunduki kisogoni baada ya yeye kupigwa na butwaa baada ya kushughudia binti yule akiuwawa mbele yake bila yeye kutarajia










TURUDI SIKU CHACHE NYUMA




Gari kali la kifahari lilipiga honi nje ya geti mlinzi akafungua geti na gari lile kuzama ndani ya nyumba ile kubwa na ya kifahari,ilokuwa katika mitaa wanaoishi matajiri maeneo ya Mbezibichi,




Gari Ile Ikaelekea Mpaka maeneo ya kupaki,ikapakiwa katika eneo lake kisha dereva alokuwa akiliendesha lile gari akashuka!




Mbele yake alitazamana na nyumba yake yenye ghorofa tatu,jumba la kifahari,mtu yule maridadi akapiga hatua kuifata nyumba yake ile...




Pembeni ya mlango kulikuwa na kakengele akakabonyeza ambapo mlango ulifunguliwa na msichana aloonekana wazi ni msichana wa kazi,jamaa yule akaingia ndani chumbani alimkuta mkewe ambapo baada ya mwanadada yule kumuona mumewe akainuka tayari kwenda kumpokea ila mumewe alimzuia!...




Na hata pole yake pia hakuitikia,




Jamaa yule aliukunja mdomo wake kwa hasira,alikuwa na chuki Kali sana dhidi ya mkewe




"Zidu mume wangu nimekukosea nini mimi mpaka kunihukumu hivi tambua wewe ndo furaha yang..."




"ishia hapo hapo,niwe nafuraha hali ya kuwa sijapata wa kuniita baba,Katarina naitaji mtoto miaka mitatu sasa twaishi kwa amani hapa Tanzania lakini unashindwa beba mimba mi nifurahi?,"




"usiseme ivyo mume wangu kupata mtoto ni majaliwa,ni hosptal ngapi tumeenda kupima mume wangu sote tumeonekana safi huna budi kuvumilia babaa"




Katarina aliongea kwa huzuni,ni miaka mitatu sasa toka wachukue uraia wa Tanzania kutokea Ganyakite baada ya kashikashi ya mfungwa Gambi Sasa Zidu alikuwa na mafanikio makubwa sana katika kampuni yake binafsi ya upelelezi ...




Ila Kilio Chake Kwa Mke Wake ni mtoto,ukumbuke katika kiapo Katarina alishapata mimba mara mbili na kuishia kuharibika,mara ya kwanza ni wakati alipokuwa akimsaka walikutana 'club' wakafanya ngono zembe kwa bahati mbaya mimba ile ilikuja kuharibika,ujauzito mwingine ukaja kuharibikia hospitalin wakati alipopigiwa simu na Mery Mke Wake Isack Na Kumpa taharifa ya kifo cha Zidu,Katarina kwa mshtuko alidondokea tumbo na kwa bahati mbaya mimba iliharibika,toka kipindi iko mpaka sasa Katarina akubahatika kushika mimba tena kitendo hiki kikampa mawazo Zidu akajikuta akianza kumchukia mke wake,akijua pengine labda ana matatizo wakaenda hosptalini kupima ila wote walionekana wapo vizuri!




'Tatizo nini sasa huyu mwanamke asibebe mimba?!,'




Zidu K akulipatia jibu swali hili,mwisho akahisi au labda mke wake anamchezea mchezo wa kuonga na pengine alishatolewaga kizazi!




Akajikuta akipata ushahuri kutoka kwa marafiki ajaribu na nje anaweza akabahatika...




Zidu k akaona aanze na katibu muhtasi wake...








****




SURA YA PILI




MAKAO MAKUU YA MUUNGANIKO WA VYAMA VYA UPINZANI TANZANIA (UWAVYAUTA)




Ni ndani ya jengo la makao makuu ya Umoja wa vyama vyote vya upinzani 'Uwavyauta',mbele Kulikuwa na wajumbe wakuu wa vyama mbalimbali walikuwa wamemsimamisha mgombea wao Christopher Asamoye kuwa mgombea uraisi,




Mwanzo alokuwa amepangwa kugombea ni mwenyekiti wa chama cha UKOMBOZI WETU TANZANIA (UWT) mh Jemes John ila ndoto zake zilikufa baada ya siku tatu kabla ya kwenda kuchukua fomu kupata skendo ilotolewa na mgombea wa chama tawala CCM ivyo ili kunusuru chama ikabidi 'Uwavyauta' wamuweke Christopher Asamoye wa chama cha 'Demokrasia ya kweli' Kama Mgombea wao agenda ikiwa ni atawale hiyo tu miaka mitano kisha mitano ijayo ilipaswa amwachie Jemes John,pia agenda ilisema ikiwa watashinda basi ilimpasa Asamoye Kumteua Jemes kama waziri mkuu wake...




Asamoye alikubaliana na agenda zote bila ubishi,kikao kikafungwa,kampeni zikaanza...




Kwa Mara ya kwanza zaidi ya miaka 50 ya chama cha mapinduzi kutawala,baada ya vyama takribani kumi kuungana na kumuunga mkono mheshimiwa Asamoye wanachama wa vyama vyote vya upinzan wakampigia kura Asamoye,siku Ya Matokeo Mh Asamoye akashinda tena kwa kishindo,




Historia Mpya Ikaandikwa nchini Tanzania.




Asamoye akaingia ikulu,kama alivyoambiwa akamteua Jemes John waziri mkuu na kuchagua baraza lake la mawaziri, ila Mh Rais Asamoye alimjua vizuri waziri mkuu wake,alikuwa ni fisadi,hata katika uongozi wake ndani ya miezi minne tu tayari alishasaini mikataba hewa iloingizia taifa hasara,pia Rais aligundua John alikuwa akijishughulisha na biashara ya uuzaji silaha nje ya nchi na pia usambazaji madawa ya kulevya vyote hivyo vilimuumiza sana Mh Asamoye Ila Kwa Kuwa Katika Kiti Kile alipachikwa ilibidi awe mpole japo aliumia ndani kwa ndani!...




'sitokubali huyu mtu muhula wangu wa pili nimwachie hiki kiti atatuuza ntapambana naye'




Mh Rais aliwaza pasina kujua angepambanaje naye kuilinda nafas yake miaka mitano ijayo!




kwake bado ilikuwa kizunguzungu




***




KAMBI YA JESHI




Ni katika mafunzo ya mwisho mwisho jeshini, bado viongozi wa juu wa jeshi walishangazwa na uhodari wa mwanadada Zena,huyu alikuwa ni binti jasiri,jeuri,kila zoezi yeye akushindwa kulifanya hata yale ambayo ayakuruhusiwa kwa watoto wa kike,Zena yeye alifanya,kitendo hiko kikamfanya apendwe na msimamiz wao wa mazoezi alotambulika kwa jina la Komando Lutu pandikizi la jitu jeusi lililoenda hewani!...




Lutu akajikuta akimtamani mwanamke yule alokwisha kwiva,juhudi za kumtongoza azikuzaa matunda zikiwa zimebaki siku tatu kumaliza mafunzo Lutu akatega mtego


kusudi aje ambake,ila siku hiyo ulipotegwa mtego,asbuh yake ulikutwa mwili wa Jemedar yule ukiwa umevunjwa vunjwa mifupa,




Uchunguzi ulipofanyika ikagundua Zena anahusika hatimaye akasekwa katika gereza la kijeshi!...




Ilikuwa ni hatari...




***




Wiki Sasa Zidu alikuwa akiwah ofisini kuliko kawaida,yote ni kumuumiza mke wake...




"ukimaliza shughuli nakuomba na mazungumzo na wewe Salome"




Zidu kwa sauti ya upole aliongea akimwambia katibu muhtas wake macho yake yakiwa katika 'laptop' yake!




Salome alitokea kumuogopa sana bosi wake Zidu yote ni kutokana na u siriazi wake,




"sawa bosi"




Salome aliitika akachangamsha mkono kudeki kule ofisini, akafuta futa maeneo husika,




Akaenda na ofisini kwake mapokezi,akafuta futa,alipo maliza akampigia simu bosi wake...




"nikuletee nin bosi"




"nletee kahawa,nawe uje kama ni chai au maziwa na kikao na wewe"




"sawa bosi"




Salome aliitikia kichwani akijiuliza ni kipi hasa bosi anacho mwitia,hakika alimwogopa sana Zidu,




Wazo Kuwa anaenda kutongozwa alikuwa kabisa kichwani mwake...








Kilikuwa ni kikao cha watu kadhaa ndani ya jumba la kifahari lililo milikiwa na tajiri mwenye asili ya kizungu alotambulika kwa jina la sir Stewart Greyson




Kikao kile kilihusu kuzuhiwa kwa makontena kadhaa ya silaha yalokuwa yakienda nje na jeshi la wananchi,Grey alivimba kwa hasira baada ya kupokea habari ile,ndipo alipoanzisha kikao kile na watu wake maalumu!




Akashika simu yake na kutafuta namba ya muheshimiwa waziri akaipiga Ile namba muda ule ule ikaita ikapokelewa akatoa malalamiko yake kwa kuwa ule mzigo ulikuwa na sheya ya waziri mkuu waziri akaahidi kulifanyia kazi swala lile...




Mheshimiwa Rais Asamoye alikuwa na mawazo sana ni kitu kipi afanye kusudi kumuunguzia waziri wake na kumpa kashfa kusudi miaka mitano ijayo aendelee kubakia katika nafasi yake?!




Alijiuliza pasina kupata majibu ila ghafla akapata wazo,akaachia tabasamu akashika simu yake na kumtwangia waziri wa ulinzi mh Paul Kazimoto,akampa maelekezo kuwa anahisi bandarin hapako salama,ivyo abadilishe walinzi wanaokagua mizigo maeneo yale,Kazimoto akamtoa khofu muheshimiwa baada ya kukata simu naye akampigia mkuu wa majeshi Samwel Nyaki na kumpa maelekezo Nyaki naye akampiguu mkuu aliyeko katika kitengo kile na kumpa taharifa zile...




Mkuu Wa Kitengo Cha baharini na ulinzi bandarini kamanda Ambros Raymond baada ya kupata taharifa kutoka kwa mkuu wa majesh ofisin kwake alikuwa na vijana kadhaa wa 'JWT' kazi ilokuwa mikononi mwao ni ukaguzi bandarin meli zinazoingia na zitokazo,Isack akiwa mmoja wapo...




Baada ya kupewa kazi ile walitoka mpaka bandarin na kwa bahati mbaya ile wamefika tu wakakutana na meli kubwa ilokuwa ikijiandaa kuondoka,vijana wakaanza kazi wakati huo Isack alikuwa ofisini wakimaliza makabidhiano na waliyokuwepo hapo awali,




Baada Ya Makabidhiano Ile anatoka akashtuka kukuta kuna meli kubwa ilosindikizwa na ulinzi wa kijeshi,




"mmekagua hiyo meli ina nini?"




Akawauliza baadhi ya vijana wake ambao walimshangaa , watakaguaje meli yenye wanajeshi!,




Isack alilijua ilo ila wasiwasi wake ni meli ile,kama ingekuwa ni vifaa vya jeshini lazima vingebebwa na meli za kijeshi ila ile si meli ya kijeshi ikamtia shaka,




"naombeni mkague hiyo meli,kwanzia risiti zake zote za kodi huko tra na kila kitu"




Kwenda Pale Wakaambiwa Ile Ni Meli Ya Mkubwa Stewart Greyson,Isack akashtuka , mkubwa ndo asilipe tena anauza silaha nje,akauzuia ule mzigo...




Hapo ndipo taharifa ilipomfikia Sir Stewart na kumpigia simu waziri Jemes aloahidi kushughulikia swala lile,




Isack akamjulisha mkuu wake Ambros ambaye naye akamjulisha mkuu wake Nyaki,ila Kabla Nyaki ajamjulisha waziri mkuu,wazir mkuu akampigia na kumwambia ule ni mzigo wake uachiwe,Nyaki naye akamjulisha Ambros ambaye Ambros akamtafuta Isack hewani kwa bahati mbaya akupatikana akajaribu katika radio call yake pia aikupatikana,Ambrosi akahisi kuchanganyikiwa




BANDARINI




Wanajeshi wawili walikuwa wakipeana makavu mmoja ambaye alikuwa pamoja na ile meli kama kiongozi alitambulika kwa jina la Veko huyu alikuwa usalama wa taifa,alikuwa akitupiana maneno na mwanajeshi mwenzake Isack Kisa tu kamzuia kuondoka hata baada ya kuwambia mzigo ule niwa muheshimiwa




"utakufa maskini wewe na usipoangalia hilo vazi unaloringia utalikosa umeletwa leo unajifanya mjuvi wa mambo siyo umetoka Monduli Juzi nin?" Veko aliongea kwa jeuri Isack akacheka kwa dharau...




"niwe nimetoka juzi au hata leo iyo ayihusu amtoenda popote na hili nikuakikishie simuogopi huyo mheshimiwa wako hii ishu mi naitangaza"




Palepale Kwa Kujua angeweza pigiwa na wakubwa wake kumwambia aachie meli ile akazima simu na kutoa laini na kupachika nyingine akawambia na wenzake wazime redio call zao palepale akampigia mwanadada Sarafina huyu ni mwandishi wa televishen ya 'Tumain Tv' dakika mbili alikuwa pale tena 'live' akiripoti tukio lile,la kukamatwa kwa meli ilokuwa ikisafirisha silaha inayosadikika ilimilikiwa na tajiri Stewart Pamoja Na Kigogo mmoja wa serikalini, si Veko pekee aloshtuka,hata bilionea Stewart Akuamin,haraka Sana akamtwangia waziri mkuu ambaye naye alikuwa katika mshangao,




"nilimpigia mkuu wa majeshi akahaidi kuwazuia vijana sijui nin kilichotokea bosi,nipe muda nimpigie mkuu kujua"




"unajua serikali yako nayidayi shilingi ngapi,unajua nimekusayidia kwa mangapi bado mwaniingiza hasara!"




Stewart alizidi kuongea kwa hasira huku mishipa ya kichwa ikiwa imemtoka




"nisamehe mimi mkuu"




Waziri Mkuu alizidi kuomba, ila kwa upande wa Raisi Kwake Ilikuwa Ni furaha alianza vizuri,na kigogo aliyetajwa yeye alimjua ni waziri wake mkuu,akapanga kukusanya vielezo na kumvujishia siri mh Sospitar Bingo huyu alikuwa ni Rafiki yake japo kisiasa walionekana ni ma aduhi,huyu alikuwa ni mbunge wa Singida Mjini Kwa tiketi ya CCM,alikuwa na sifa ya kuongea na kuvujisha siri mbalimbali za chama tawala cha 'UWAVYAUTA' wengi wa viongozi wa Uwavyauta awakujua siri zao zavujishwa na nani walijua ni mmoja wapo ndani ya chama ila hapakuwa na alomtilia shaka raisi,




Raisi akaonana na Bingo Na Kumpa data zote,ambazo mh Bingo angeenda kuzitema cheche kesho yake bungeni na kumchafua waziri mkuu Jemes,ivyo kuchafuka kwa Jemes Ingekuwa faida kote upande wa chama cha upinzani na pia upande wa Raisi Asamoye




***




Ambros Raymond alikasirika, ni baada ya kumkosa hewani Isack na kuvuja kwa ishu ile jinsi alivyogombezwa na mkuu wake S Nyaki aliona wazi Isack alifanya kusudi kwa nin azime simu na atangaze katika televisheni pasina ruhusa yake?!...




Ni wazi alimdhalilisha,kwa kosa lile alipanga kumwangamiza iwe fundisho akashika simu yake,na kumtafuta mtu alomjua yeye huyu ndiyo ambaye alipanga kumwangamiza iwe fundisho kwa vijana wengine...




...4...




Isack yeye binafsi alikuwa aishi kambini kwakuwa alikuwa aki ishi na familia yake,jioni ile alikuwa akirejea nyumbani katu akulitilia shaka gari lilokuwa likija nyuma yake yeye akaendelea na safari,ghafla gari lile lilipomfikia mtu mmoja aliachia risasi kadhaa kifuani Isack akaenda chini gari ile ikatoweka maeneo yale kwa mwendo mkali!...




Watu Sasa Wakawa wamemzingira Isack Wakimshangaa,kwa bahati nzur msamaria mwema akajitoa kumsaidia Isack akampakia ndani ya gari tayari kumkimbiza hospitalini...




Alikuwa Kwenye hali mbaya na uwezekano wa kupona kwake ulikuwa mdogo...




Kufikishwa hosptalin kwa kuwa vitambulisho vyake vilimtambulisha ni mwana usalama haraka sana akaingizwa chumba cha mahututi na operesheni kuanza mara moja...




***




Ilikuwa Ni hotel ya kifahari,hotel wakahao matajiri au watu wasio na hela za mawazo,kimjini mjini tunazihita hoteli za nyota tatu...




Katika Meza moja aliketi Zidu akiwa na katibu muhtas wake alotambulika kwa jina la Salome, Zidu alishafanikiwa kumuingiza katika 'target' yake Salome na tayari walishachukua chumba Zidu alikuwa akisubiri tu wamalize kula,katu hata moyo ukumuhuma kumsaliti mke wake ndo kwanza alijihisi furaha,kwa Upande wa Katarina siku hiyo nyumbani alijikuta akikosa raha,japo akujua sababu ni nini inayo mkosesha raha,alitaman kulia ila akusubutu akupenda kulia pasina sababu ila akajua ni pengine nikwakuwa mume wake Zidu sasa alibadilika,




Zidu hakuwa Zidu yule alomjua, pengine hiki ndiko kinacho mnyima raha,wakati akiwa katika mawazo yale ghafla simu yake ikaita kuangalia mpigaji aliisevu Emilliana huyu alikuwa ni rafiki yake kipenzi walojuana saluni,




"nambie Emilly"




"shoga mumeo Kaja hapa hotelini kwetu na mwanamke na sahivi wamechukua chumba"




"unasema una uhakika?"




"pengine uniamin njoo mwenyewe udhibitishe"




Katarina akaikata simu yake alikuwa ni kama mtu alochanganyikiwa hasira zilimpanda,




'Sitokubali hakika, Zidu Wa kunsaliti mimi?!'




Aliwaza huku akielekea nje ya nyumba yake,alipoufikia mlango akaufungua ila kabla ajatoa mguu akapata wazo,akarudi nyuma hatua moja na kuufunga ule mlango akarudi zake sebuleni na kuketi!




'kwa saivi yule mwanaume kapoteza upendo na mimi kimantiki hata nikienda mfumania sitokuwa nimejenga ndo kwanza ntazidi kujiaribia,sasa nifanyeje?,yah itapaswa ni dili na huyo mwanamke ni mwambie aachane na mume wangu ntampa onyo ila akiendelea sitokuwa na budi zaidi ya kumuua...'




Ghafla akakatishwa mawazo yake na mlio wa simu kuangaliya mpigaji ni yule rafiki yake haraka sana akapokea.




Kwa hiyo Kata unakuja au?"




"hapana emmy sitoweza kuja ila naomba wakiondoka tu nishtue naitaji kuja kukagua kamera nimtambue huyo mwanamke"




"mh,sawa"




Binti yule akaitikia kwa unyonge,akista ajabishwa na maamuzi ya Katarina,ilikuwa mwanamke akiambiwa mume wake anakusaliti haraka angewasili na kuwaletea fujo ila huyu anawaacha,Emmy akajua bila shaka Katarina alikuwa akimuogopa mumewe,na ndivyo ilivyokuwa




Mida ya saa kumi na moja jioni ndipo Zidu Na Mwenzake Walipokabidhi Ufunguo,baada Ya Kuondoka Ndipo Emmy alipompigia shoga yake na kumwambia wameondoka, haraka sana Katarina akaingia garini,na kuliondoa kuelekea katika hotel ile,kiu yake kubwa ni kumjua huyo mwanamke alokuwa akitembea na mume wake,katu akudhan wala kuhisi ni Salome 'secretary' Wa mume wake kwani alimjua vizuri binti yule...




***




SURA YA TATU




Ilikuwa ni mida ya saa tano za usiku wakati mwanadada Sara Mwandishi Wa habari akirejea nyumbani kwake,ghafla mlio wa meseji ukaingia katika simu yake akaufungua na kuusoma




"kuna dili la habari ikiwa tu utanitumia laki mbili nikupe mchongo"




Sara aliitambua namba ile ni ya msanii mmoja wa bongo movie mwenye mvuto wa kipekee,alotambulika kwa jina la Magreth,msanii huyo mara nyingi alivujisha siri zikiwemo picha,meseji au hata kuwashtua waandishi pindi akiwa na mtu maharufu na kuingiza kiasi cha fedha,




Leo hii katika usiku huu alikuwa ndani ya gari la waziri mkuu wakielekea ndani ya hotel kubwa,




Baada Ya Sara Kuipata habari ile haraka sana akamtumia ela msanii huyo akaanza kumpa maelekezo walipokuwa wakielekea , mwisho walifika katika hotel moja kubwa ya Sleapway Wakachukua Chumba Makusudi Sara akijifanya kuzidiwa na joto wakati ndani ya chumba kile kulikuwa na ac,akasogeza kidogo pazia la dirishani kusudi sara aweze chukua video vizuri,




Ilo Sara akafanikiwa, akachukua video tukio lile aliporidhika akarudi kwenye gari lake na kutoweka eneo lile,waziri Mkuu akujua kuwa alisha chukuliwa video na kama zingevuja basi zingemuweka pabaya...




Sara ndani ya gari alikuwa na furaha sana tukio lile lingemwingizia fedha na kumfanya azidi kupendwa na bosi wake,alfrah sana juu ya ilo...




Alipofika Kwake Kwa furaha alokuwa nayo mpz wake si ndo akamuulizi,ikabidi Sara amweleze Sudi Bapa alishika mdomo kwa mshangao,




"hili dili la ela my love,dah ongera sana tutachuma ela mpaka basi"




Sudi Aliongea Kwa Furaha




"yah Ni Kweli Na Litanipa hata tuzo ya mwandishi bora,mwandishi ninayejiamini kuanika uchafu wa waziri mkuu si mchezo"




Sudi akakunja mdomo,




"Hapana hii habari usiiripoti itayaweka maisha yako hatarini tuiuze"




"Tuiuze?! kivipi"


Sara akaoji kuonesha wazi kuanza kukasirika,




"kazi hii itafanywa nami Sudy we tafuta namba za waziri mkuu tutamtumia video moja then tutampigia na kumwambia ili video hii tusi ivujishe atoe milion kadhaa then kila wakat nitakuwa nikifanya hivi mpaka tutajirike"




Sara akatabasamu wazo la mpz wake lilikuwa zuri na lenye mafanikio walikuwa na uhakika waziri asingechomoa,kutoaribu sifa yake,




"basi kesho nikienda ofisini nitacheki namba zake"




"sawa hiyo memory kadi yapaswa uitunze zaidi ya kitu chochote,kwanza nitumie hizo video nami niwe nazo, Sara akafanya ivyo akatoa memory kwenye kamera akaiweka kwenye simu akazituma zile video na picha kadhaa kwenye simu ya Sudy Bapa,akafanya hivyo hivyo pia katika simu yake nyingine baada ya kukamilisha akarudisha memory ile ndani ya camera,wakalala wote wakiota ndoto za utajiri




Kesho yake Sara alipofika tu kazini kitu cha kwanza nikutafuta namba za waziri mkuu na kumtumia mpz wake,haraka sana Sudy akazisevu kwa bahati nzur zilikuwa na whatsupp akarusha picha kadhaa na video zake,kisha chini akamwandikia naitaji milioni mia nne kutovujisha picha hizi kwa waandishi wa habari azikupita hata dakika mbili mheshimiwa akampigia...




...5...




Mwandishi Wa habari Sara anafanikiwa kupata habari ya muheshimiwa waziri mkuu Jemes John ambayo bila shaka ingekuwa ni kashfa kwake kama ingetangazwa,




Sara anamfikishia mpz wake taharifa ile ambapo Sudi Bapa anaona ni bonge la dili ambalo anamshawishi mpenzi wake asiitangaze bali wamuuzie mh waziri Sara ana afikiana na wazo hilo anapofika kazini anamtumia namba za Waziri Sudi naye anamtumia waziri mkuu picha na video chini akiandika anaitaji milion mia nne kutotangaza habari zile,punde muheshimiwa anampigia simu...




Songa...




Waziri mkuu Jemes alionekana wazi kuchanganyikiwa mpaka akawa akiongea kwa kigugumizi...




"u..u..u.po..wapi kijana?!"




"upo tayari kutoa izo hela?!"




"hata sasa hivi,ila u..sitangaze hizo habari"




"ok nahitaji uje maeneo ya mikoroshini huku nitakupa sighn tuonane wapi uje peke yako tena na tax kama raia wa kawaida ukija tofauti na ivyo kesho tutaanika kila kitu mbele ya vyombo vya habari"




"s.s..sa.wa..nimekuelewa mkuu sitoenda ki...nyume na usemavyo"




"nakutakia kila la kheri muheshimiwa"




Waziri Mkuu alihema moyo ukaanza kumwenda mbio ghafla katika taharifa ya habari ambapo bunge lilikuwa likiendelea mwanzo mawazo yalisha ama katika televishen yake ila aliyarudisha baada ya kusikia jina lake likitajwa na mheshimiwa mbunge wa Singida Kwamba anausika Katika uuzaji wa silaha nje Ya nchi akishirikiana na tajiri mwingreza Sir Stewart Greyson,kama Kawaida Yake Bingo alieleza ushahidi anao ni katika mikataba ilosainishwa kwa siri akaipeleka kwa spika,Waziri alizidi changanyikiwa mara dufu ghafla akapigiwa simu na mh Rais akapokea




"unafanya nin waziri?,jua ndo kwanza tumeikamata nchi na huu ndo mwaka wangu wa kwanza nikiwa nimebakisha miaka minne nikuachie nafasi unaandamwa na skendo kiasi hiki huna budi kujiuzulu au nikutengue kusudi kujisafisha na kujitengenezea njia ya kuingia ikulu hapo mbeleni...




Mh Rais Asamoye alijaribu kumshahuri wazir mkuu wake,ambapo muda wote alikuwa kimya akimsikiliza




"Asamoye Kwanza futa wazo hili la mimi kujihuzulu japo katiba inasema una uwezo wa kutengua cheo ulichonipa ila kumbuka cheo hiki si wewe ulonipa ila ni muunganiko wa vyama vya upinzani na ukumbuke mimi ndo mwenyekiti wa Uwavyauta Na Chama Changu Cha 'UWT' ndicho chenye wanachama wengi hapa nchini baada ya Chama Cha Mapinduzi,kikifuatiwa Na hiko chako cha Demokrasia ya kweli ivyo mimi kama mwenyekiti kumbuka ndiyo niliyopendekeza wewe uchukue fomu baada ya yule mjinga wa upande wa pili kunipa skendo ivyo tambua upo chini yangu uwezi jiamulia tu kunitengua,malizia miaka yako unipishe ikulu"




Baada maneno yale 'JJ' akakata simu, aliongea kwa hasira sana kwani alichanganywa na vitu viwili kwanza kuvuja kwa picha zake na msanii wa sinema za kibongo Magreth Pili swala hili la kuhusika katika skendo ya kukamatwa kwa silaha...




Alijua Ni Lazima angetakiwa ajieleze ila kabla ajafanya au kutakiwa kufanya ivyo ilipaswa azuie skendo ya picha alizotumiwa kwa kumlipa huyu mtu!...




Kwa kuwa skendo hiyo ingevuja ndo ingemuaribia kabisa!




Rais Kwa Upande Wake alikuwa katika furaha ya ajabu,hata baada ya kuongeleshwa vibaya na 'Jj' Wala akujali,'nikipata nafasi ya kugombea miaka mitano mingine kama katiba ya nchi isemavyo ntammalizia mbali huyu kifaru,sijui anajiaminia nini'




Rais aliwaza akimalizia kunywa chai,siku hii akutaka kutoka nyumbani alikuwa akimngojea mwanaye alotoka katika mafunzo huko Monduli,alikuwa na miezi kadhaa nyumban kabla ajarejea kambin,Rais Asamoye alimpenda sana mwanaye wa pekee aloitwa Daniel...




Daniel Asamoye!...




***




Katika Chumba Kimoja Ndani Ya Ofisi Ya Waziri Mkuu aliketi mmama wa makamo alojitanda ushungi na kuvaa baibui lake mama huyu alitambulika kwa jina la Salma au madam 's'




Huyu alikuwa ndiyo mkuu wa usalama wa taifa japo pia makao yake makuu ofisi yake ilikuwa katika jengo la ikulu ila kote pawili alikuwa na uwezo wa kukaa na kufanya kazi zake vizuri,wiki takribani mbili sasa aliamua kuweka makaz pale katika ofisi ya waziri mkuu baada ya kuhisi wazir hayupo katika hali yake ya kawaida,




Na hata siku hiyo aliweza yanasa maongezi kati ya Sudi na wazir asubuh hiyo katika laptop yake aloiunganisha na kamera zilizopo kila maeneo katika jumba lile,na pia aliunganisha moja kwa moja na ikulu,ivyo kila kilichoendelea ikulu alikiona na kila kilichoendelea pale alikiona,haraka sana akamtumia meseji kijana wake ambaye alikuwa nje ya jengo lile;!




"Veko waziri ayupo sawa, nahis kuna picha kama si video alizopigwa ivyo anaitajika alipe kias cha milion mia nne kusudi picha hizo zisisambazwe atatoka hapo pasina ulinzi na mbele atachukua tax mfatilieni kwa umakini muakikishe mwamdhibiti huyo mtu na kumpokonya vizibiti alivyonavyo ikiwezekana mumwangamizie mbali mtanitaharifu kila hatua mpigayo"




"sawa madam nimekuelewa"




Kijana yule aliongea akakata simu akawapa maelekezo na wenzake,ndani ya gari walikuwa vijana wa nne mbele wawili nyuma wawili,punde waziri akatoka na begi maalumu zile za kubebea ela kimuonekano alibadilika alivaa shati refu Na suruali ya kitambaa na chini alivaa viatu vyeusi vilivyochoka kidogo




Kichwani alivaa kofia aina ya kapelo walinzi nje wala awakumtambua walijua ni mtu tu alokuja na shida zake akanyoosha njia kuelekea ilipo barabara!




Japo walinzi wa kawaida awakumtambua ila si kwa walinzi wa usalama wa taifa ambao tayari walishakuwa Na habari zake kutoka kwa mkuu wao madam 'S'




Ivyo wakaanza mfatilia kwa siri,John alipofika barabarani akachukua tax Na kumpa maelekezo waelekee 'Tmk' maghorofani maeneo ya Mikoroshini!




Dereva tax pia akumjua akatia gari mafuta pasina kujua Pizo na wenzake walikuwa wakiwafatilia...




Kichwani kwa waziri kulitawala mawazo,hasa kwa skendo zilizokuwa zikimwandama...




****




Katarina aliwasili katika hoteli ile na kuelekea moja kwa moja mpaka kwa Emmy,ambapo Emmy alimuonesha picha kadhaa alizompiga Zidu na Salome,pia alimuonesha na video,




Katarina aliumia sana moyo wake leo hii Zidu mume wake anamsaliti tena na mfanyakaz wake kisa ajazaa?!




Kasahau walipotoka,kasahau kashikash walizo zipata pamoja leo kirahisi tu anamsaliti,mchomo mkali ukauchoma moyo wake akamuaga shoga yake yule na kumwachia pesa kidogo ya shukran akaingia ndan ya gari yake,mwili wote ulimlegea alipofika aliuegemea mstelingi alilia kwa uchungu hakika kitendo kile kilimuumiza sana,




Taratibu akaliondoa gari mpaka nyumbani kutokana na foleni akajikuta muda mwingi akiutumia barabarani kufika akashuka na kuingia ndani ilikuwa tayar ni saa mbili kasoro




Kumbe mwenzake Zidu saa kumi na moja ile baada ya kutoka pale hotelin wala akurejea kazin kwa kuwa Salame alimchosha akaamua kurejea zake nyumbani kupumzika alishangaa kutomkuta mkewe ndipo akamuuliza mfanyakazi wao Suzy ambaye alimwambia mama aliondoka mida ya saa kumi na moja akumuaga na wala akujua alienda wapi




'kumbe huyu mshenzi mimi nikitoka naye anatoka leo arobain yake wallah namuua'




Zidu akawaza akaelekea zake chumbani ambapo aliingia bafuni kuoga akarejea sebulen akaket akichek tv,




Wala akutaka kumshtua kwenye simu alitaka kumuona angekuja sangapi!...




Ndo mpaka mida hiyo ya saa mbili Katarina aliwasili alishtuka kumuona Zidu,




Kidume Kikatabasamu,'naona umelika huko nje mpaka macho yamebadilika rangi malaya mkubwa wewe kumbe mimi nikitoka nawe unatoka haya sema umetoka wapi?"




Zidu aliongea kwa ukali,Katarina angejibu nin?,akajikuta akianza kulia...




"naona unahamu ya kulia ujapigwa unalia subiri nikuoneshe"




Zidu akaliendea kabati na kutoka na mkanda wa jeshi




"sasa ngoja nikupige ili ulie vizuri!"




ZIDU akaongea akinyanyua mkono tayar kumtandika mkewe,na mkanda ule ungetua mwilini mwa Katarina Basi ungeondoka na nyama na Zidu alipania kumtandika nao usoni kumuaribu hiyo umbo uzur kusudi wanaompenda na kumdanganya huko nje wasimpende tena...




...6...




Katarina anapewa taharifa na shoga yake Emiliana kwamba Zidu Mumewe yupo katika hoteli afanyayo kazi na mwanamke mwingine,Kata moyo unamuuma ila anafuta wazo la kwenda kumfumania kwani amjuavyo Zidu kumfumania akutamjenga bali ndo atazidi kubomoa anachopanga ni baada ya wao kumaliza Kata aende akachunguze ni mwanamke gani huyo anayemzuzua mume wake?!




Kweli anaenda na kugundua ni Salome Katibu Muhtasi Wa Mume Wake Moyo wazidi kumuuma mara dufu,ila anaamua kurejea nyumbani ambapo kwa bahati mbaya kutokana na foleni kubwa Katarina anafika nyumban usiku ambapo anamkuta Zidu akimsubiria,




Zidu anachukua mkanda tayari kwa kumuadhibu,je unahis nin kitaendelea?, tusonge katika sehemu hii ya sita ya riwaya hii ya kusisimua...




Zidu ile anaushusha mkanda tena akiulenga usoni Katarina sasa akiwa kapandwa na jazba akauepa kwa kuinama alipoinuka akapiga hatua moja nyuma akaukunja mguu wake na kuufyetua kwa kasi teke kali likamwendea Zidu,ambalo Kwa Kuwa akutegemea pigo lile likampeleka akajigonga ukutani na kuporomoka chini,




Zidu akajiamsha, huku akinung'unika "yani unamakosa alafu unanipiga?!"



ITAENDELEA


     


Simulizi : Kufa Tu  Hakuna Namna 


Sehemu Ya Pili (2)




Zidu akazidi kunung'unika huku akijiandaa kurusha ngumi ambayo Katarina aliikinga kwa mkono wake akauachana miguu yake kimapande kisha mguu wa kulia akaukunja na kuupiga kwa nguvu sehemu za siri kwa kutumia goti,Zidu akaachia yowe...




akishika sehemu zake za siri,




Wakati Wote Wanandoa Wale Wakipigana binti wa kazi Suzan alikuwa akihaha pasina kujua afanyaje...




Ghafla akapata wazo ni mtu mmoja tu ndiyo ambaye angeweza kuamua ugomvi ule naye si mwingine Zaidi Ya Isack,haraka akatafuta namba za Mery mke wa Isack na kumpigia...




"eti?,Isack kapigwa risasi? mpo hapo muhimbili...sawa nawambia




Zidu Na Katarina bado walikuwa wameshikana wakiparangana,ila wote walishtuka kusikia Isack kapigwa risasi,Zidu akaacha kupigana na mkewe akapiga hatua ya kwanza hatua ya pili alikuwa pembeni ya Suzan,




"unasema Isack Kafanyaje Shem?"




"kapigwa Risasi Na ana hali mbaya shem yupo icu..."




"sawa nakuja saiv"




Pasina kujali ni usiku Zidu akalifata gari lake huku Katarina akimfata nyuma,akafungua mlango upande wa dereva na Katarina akakaa kiti cha pili na kuliondoa gari kwa kasi,uaduh wao ilipaswa wa usahau kwa kipindi hiko,




walikaa kimya kwa muda kabla Zidu ajaanzisha maongez




"ndo maana mi nikakataa we kuendelea na jeshi ndo mambo kama haya"




"usilaumu mume wangu hii ni ajali kazini"




"itanipasa kuingia kwenye kazi mpya kumtambua ni nan alomshambulia Isack Na Kwa malengo gani,"




Katarina akujibu kitu waliwasili hosptalin,moja Kwa Moja Wakaelekea Mpaka Wodi Alolazwa Isack,pembeni Yake alikwepo Mery akiwa kajishikia zake tamaa




Isack alilala kitandani pasina ufahamu akipumulia mashine ya oxygeni dripu ya damu maji na dawa zikiingia mwilini mwake taratibu




"ni kitu gan kilicho mpata Isack Shem"




Zidu alimuoji Mery huku machozi yakimlenga lengo,Isack si kwamba tu alikuwa kama rafiki lahasha kwa saivi alimchukulia kama ndugu,ikabidi Mery aanze msimulia toka alipopigiwa simu na mtu alojitambulisha kama raia mwema alomsaidia Zidu baada ya kupigwa risasi na watu wasojulikana akabeba dhima ya kumsaidia na kumleta hapa hospitalini..."




"raia mwema huyo yuko wapi?"




"kwa saiv kaelekea kwake ila kesho kasema atakuja kumwangalia mgonjwa"




"Itapaswa kesho mapema tu nionane naye"




Zidu aliongea kwa uso ulotawaliwa huzuni baada ya kumwangalia mgonjwa wakaaga wakiahidi kurejea mapema siku inayofuata


Zidu akipanga ndo siku ambayo angeianza rasmi upelelezi wake




*************




Pamoja na kuwa mh Rais alionekana wazi kufurahia kumwona mwanaye Dani,ila Dani aligundua baba yake hakuwa sawa kimawazo,




"mama nahisi baba ayupo sawa anatatizo gani,ni mtu mwenye mawazo"




"Nitajulia wapi mwanangu na hizo siasa zake,kaa naye chini umuulize labda atakueleza,"




Dani baada ya kutomwelewa baba yake hapo ndipo alipo muhoji mama yake,baada ya mama yake kushindwa kumweleza siku ilofatia Dani akamkabili mwenyewe baba yake na kumuuliza kinacho msumbua...




Rais akuona haja ya kumficha mwanaye akamweleza wazi juu ya John na hata tabia yake,Dani alimsikitikia sana baba yake na mwisho alimuunga mkono!




"ni kweli huyo mtu apaswi kuongoza nchi"




Rais akatabasamu "wanshauri tufanyaje mwanangu?"




Dani kwa dakika kadhaa alikaa kimya yamkin alikuwa katika mawazo mazito na ghafla akaachia tabasamu!...




"shida yako baba ni mwandishi utakayekuwa unamvujishia siri za J' Kisha yeye anazitoa katika vyombo vya habari,"




"ZENA atafaa baba"




"Zena?,zena ndo nani"




Ikabidi Sasa Dani amwelezee baba yake kuhusu huyo Zena,uhodari wake mpaka kufikia kufungwa baada ya kusemekana kuwa yeye ndo aliyemuua kamanda wao"




Rais akaguna baada ya kuiskia historia ya huyo binti,"sasa huyu atafaaje katika kazi yetu kwanza si mwandishi wa habari pili tayar huyo ni mwalifu au wewe una maana gani kumtaja?!"




JE DANI ATAMJIBU NIN BABAKE NI VIPI ZENA ATATUMIKA NA RAIS ATAKUBALI USHAHURI WA MWANAE


HII BADO NI MWANZO








Rais Asamoye bado akumuelewa mwanae Daniel anamaana gani,ikabidi Daniely kumwelewesha baba yake...




"yule binti 'Zena' yupo vizuri katika mapigano kwa kuwa ayupo katika jeshi ila ana mafunzo yote ya kijeshi yapaswa umpe msamaha umtumie wewe!"




Raisi Asamoye nikama akumwelewa mwanaye kipi anacho maanisha,hakuwa na papara akaendelea kumsikiliza...




"yapaswa umtoe pili umtafutie kazi katika chombo chochote cha habari awe anaripoti kile unachotaka wewe,akiwa katika sura ya kificho na pili ili kuwapumbaza watu zaidi tutamwingiza katika idara ya polisi ivyo atafanya kazi yako kwa mwamvuli wa upolisi,mwandishi wa kawaida kukufanyia kazi yako ni ngumu sana baba unadhani usalama wa taifa utamwacha?"




"yah ni kweli mwanangu ulicho ongea,ntafanya ivyo we acha nitoe msamaha kwa wafungwa kadhaa Zena akiwa mmoja hapo nusura ya kuendelea kuwa raisi naiona mwanangu"




Dani alicheka tu akajiinua na kupanda juu ya meza palipokuwa na taa kuna kidude akakigusa pale katika ile taa na kushuka zake...




Kwa muda wote Rais alokaa pale ikulu na familia yake awakudhani wala kuhisi kuwa ile taa hapo sebulen kwao ilikuwa ni kamera,ila kuingia kwa Dani alipoiona tu aliitambua kwani jeshini walifundishwa aina mbalimbali za kamera ivyo kabla ajaanza mazungumzo na baba yake akaizima na walipo maliza ndipo alipoiwasha na kumwacha mzee wake katika mshangao wa hali ya juu!...




Wakati Mh Rais akiwa katika mshangao ghafla simu ikaita kwenda kupokea akaambiwa kuna vijana kutoka ofisi ya madam 's' wanaitaji kumuona,




Rais Asamoye akawa kashajua ni ugeni kutoka usalama wa taifa, akawaruhusu ambapo waliingia vijana wawili wakapiga saluti




"kuna kamera za ulinzi zimekata mawasiliano ofisini kwa madam tunaitaji kuangalia mkuu"




"ha ha ha mwanangu ndo alozima kamera nilikuwa namaongezi naye nyeti ila kashawasha"




Kijana Mmoja akapanda juu na kuitazama ile taa kwel ilikuwa 'on' akashuka wakaaga




Kweli Madam 's' akiwa ofisini kwake alishangaa ghafla mawasiliano na ikulu yakakata,wasiwasi ukamvaa ndipo alipotuma vijana wawili waende wakakague hizo kamera,ila badae mawasiliano yalirudi kama kawaida...




*** ** ***




Upande wa waziri mkuu akiwa ndani ya tex alifata maelekezo alokuwa akiambiwa na Sudi,pasina Kujua nyuma alikuwa akifatiliwa na vijana wa madam s hatimaye walifika mikoroshini eneo fulani akaambiwa ashuke,atembee kwa miguu mtaa wa kwanza wapili mpaka katika jumba moja bovu kama pagara akaambiwa aziweke huko atoke,




Waziri mkuu akafanya ivyo,akaweka na kutoka,simu bado ilikuwa masikioni




"ok,muheshimiwa sasa unaweza kwenda sitoripoti popote"




Waziri akaondoka wasiwasi ukiwa umemuisha,huku nyuma Sudi ambapo alikuwa mbali kidogo na eneo lile japo aliona wakati waziri akiingia na bruefcase zake mbili baada ya kushughudia akiondoka na kupotelea mtaa unaofatia taratibu akasogea pagara lile na kuingia ile anainama kuokota zile sanduku




Ghafla akahisi kama watu wameingia akaziokota na kugeuka,alishtuka baada ya kutazamana na bastola,tayari Pizo na mwenzake Veko walikuwa mbele yake,




Kwa kuwa walivaa nguo za kiraia Sudi akajua pengine ni majambazi waloushtukia mchongo wake




"masela eeh msinidhuru kama ni majala aina doro nyie chukueni niachen life langu"




Sudi aliongea kwa wasiwasi huku akitetemeka,




"uoni aibu unaihibia serikali?,upo chini ya ulinzi,taratibu bila kuleta ujuaji wa aina yeyote kama marafiki utaongoza kufata kila tutakachokwambia haya beba bruefcase zako"




Sudi akatii majamaa wale wakarudisha silaha zao kibindoni wakatoka mpaka mahali walipopaki gari yao wakatoweka maeneo yale,




WAZIRI AKUJUA KILICHOENDELEA ILIKUWA NI SIRI YA USALAMA WA TAIFA




Wakiwa ndani ya gari Pizo aliwasiliana na madam 's' na kumpa taharifa juu ya kufanikiwa kumkamata huyo anayesemekana ana picha za mh waziri,




"mmemkuta na hizo picha!?"




"hapana mkuu!"




"basi akikisheni anawakabidhisheni hizo picha kisha mumwangamize astahili kuishi huyo"




"ok madam!"




Baada ya kukata simu Veko akamgeukia Pizo alokuwa akiendesha gari,




"ehe lete maneno"

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog