Search This Blog

Thursday, 29 December 2022

KUFA TU HAKUNA NAMNA - 3

   

Simulizi : Kufa Tu Hakuna Namna 

Sehemu Ya Tatu (3)





"marhaba pole umefanyaje?"




"nimeanguka nikavunjika mkono,"




"pole mwaya eeh unaitwa nani?"




"naitwa Salama"




"una Miaka mingapi salama?"




"kumi na nne"




"upo darasa la ngapi"




"la saba"




"ok,wakati huyu mgonjwa anafika ulibahatika kumuona?"




alimnyooshea kidole Katarina,Salama akatingisha kichwa kukubali kuwa alimuona




"uliona hata mara moja wakisalimiana na yule...


Akamnyooshea Kidole Katarina




Salama akatingisha kichwa kukataa,leo asb eti yule alitaka kuondoka huyu akamzuia kwa kumwita mke mwenzake unaenda wapi wakat ujaruhusiwa?"




"ndiyo alisema"




Wakati huo huyu alikuwa kabeba nini wakati anataka kuondoka?!




"alibeba mfuko wake,"




"kwa hiyo awakuwah kuongea kama wanajuana kabla ya hapo na baada ya huyo dada kurudi waliongea chochote kingine?"




"kuna kitu alimnong'oneza ila sikukisikia!"




Zena akamtazama Nurdin,kulikuwa na kitu,




"asante mtoto mzuri na pole!"




"aya dada"




Zena sasa akarudi kitanda cha Salome




"kuna kitu huyu mtoto kasema ulinong'onezwa ni kitu gani?!,




JE SALOME ATAJIBU NINI ZENA ATAWEZA KUMGUNDUA KATARINA NDIO ALOMSHAMBULIA SALOME KWA RISASI"








Koplo Zena anaingia katika idara ya jeshi la polisi huku pembeni akiwa na kazi nyingine,




Akiwa kama mwandishi avaaye mask nyeusi kuficha uso wake,akifichua Maovu ya waziri mkuu agizo linatoka usalama wa taifa 'Zk' auwawe je nin kitaendelea tusonge katika sehemu hii ya kumi na sita,




Salome alibaki kaganda kichwani akijiuliza amjibu vipi afande yule aloonekana ni mzoefu idara ya polisi hasa katika kitengo kile cha upelelezi...




Hata Insp Nurdin alishangazwa na ulizwaji maswali wa koplo yule,ni kama alikuwa mzoefu kumbe hata hakuwa na muda mrefu jeshini...




"alinambia nisijali nitapona"




Salome alijibu kwa unyonge,akapiga hatua mpaka alipo Katarina akamtwanga swali lile lile




"ulimnong'oneza nini huyu mwenzako"




Kwa kuwa Katarina alisikia jibu alilojibu Salome naye akajibu vilevile




"exactyly,but kuna kitu mnakificha nitakijua tu na najua kwa namna moja au nyingine Katarina unahusika kumshambulia huyu na hata huyu anajua ila si umempa onyo nakuhakikishia nitautafuta ushahidi na nitakufunga wewe"




Kwa Kujiamini Koplo Zena akaongea kwa ujasiri tena kwa chuki ya hali ya juu,




"kwa hiyo unataka kunitisha siyo?"




Katarina naye akajibu kibabe,tatizo lake Kata alikuwa na jazba,na hasira za karibu na vile alipitia jeshi alitokea kudharau khaki, pasina kujua hata yule khaki ni geresha tu mazoez yake ni ya gwanda za mabaka tena mazoezini akiwa mbabe...




"si kwamba nakutisha nakwambia real ni ushahidi tu nautafuta"




"achana naye afande siye twende zetu" Nurdin akaingilia kati,




"hapana afande kwa nini tusimtie pingu huyu akawa mshtakiwa namba moja mi nishamtilia shaka eti"




"unitie pingu kisa wanshukia ujanijua vizur binti tafuta ushahidi nikamate acha maswala ya kise.."




Kabla ajamaliza kauli akanyamaza ghafla baada ya kumuona Koplo yule akipeleka mkono wake kiunoni,Katarina alijua binti yule alitaka kuchomoa nini,akutaka kuendelea kuzubaa pale kitandani akajiinua wakati Zena anaunyoosha mkono wake akakumbana na teke la mkononi silaha ikaruka pale pale akaukunja mkono wake na kumtandika ngumi ya usoni ilo mfanya akapepesuka na kudondokea kitanda cha mgonjwa...




Nurdin Palepale akachomoa bastola yake na kumuelekezea Katarina,hapo ndipo katarina alipotulia,Zena akaenda iokota bastola yake akamnyooshea Katarina,inspekta Nurdin akamfunga pingu ,huku bado Zena akimwelekezea bastola wakatoka nae,wakiongozana na Zidu pia...




Salome huku nyuma alitetemeka,siku ile ile akaomba ruhusa alipopatiwa akarejea kwao akiwa na malengo ya kumchukua mdogo wake warudi zao kijijini wakalime,




wakati wakiwa katika gari ya polisi Nurdin na Zena kila mtu alizama katika mawazo mazito...




Zena alikuwa akiwaza wepesi wa Katarina,jinsi alivyo mtandika teke la mkono sambamba na ngumi ya usoni,yani kwa mapigo yale mawili alitambua mtu yule si 'leval' zake,si mtu wa kawaida yule...




Ni nani sasa?,isije ikawa ni mwana JWTZ wakaitafuta vita,unajua mpaka muda ule awakuwatambua zidu na Katarina Kama ndo wale makomandoo wa kinte ambayo kwa sasa nchi ile iliitwa Ganyakite baada ya Ganyama kuungana na Kinte Kama ilivyokuwa awali,kabla awajatengana...




Kwa saivi walibadilika sana




Walinenepa sana,




Kwa upande wa Insp Nurdin yeye alikuwa akiwaza wepesi wa Katarina na pia alishangazwa na ulizwaji maswali wa koplo Zena ulimtia shaka hasa kwa kuwa ndo kwanza alikuwa Na muda mfupi toka aingie idara ya jeshi la polisi,




Kwa upande wa Zidu alikuwa akishangazwa pia na koplo yule hasa kwa umahiri wake wa kuhoji,




Ajilikuta akimpenda na kupanga kuanza kumfatilia pindi tu vuguvugu lile litakapoisha,




'Na hata ikiwezekana nimuingize katika idara yangu'.




Zidu akajikuta akiwaza huku upande wa Katarina yeye alimuwaza Salome,furaha yake tu ni kumuua achilia mbali akifungwa ila moyo wake uwe katika uhuru,




Katarina alikuwa akichukia amechukia na akiamua kitu awezi kukibatilisha,




Alikuwa kashapanga Salome kumuua ilikuwa lazima amuue,si alishamkanya akajifanya mjanja sasa ilikuwa lazima naye amuonyeshe ujanja wake...




Wakafika makao makuu ya idara ya polisi,wakashuka wakimshusha na Katarina Wakamsweka Kwanza Rumande...




Wakaelekea na Zidu Ofisini,Insp Nurdin bado alimpa kibali Zena cha kumuhoji Katarina...




"mke Wako anajua juu ya mahusiano yako na huyo mfanyakazi wako?,"




"sijui kama anajua ila kwa akili yangu nadhani hajui"




"wala hajawahi kukutilia shaka yoyote?"




"hajawahi afande"




"ok,nyumbani kwako unaishi na nani mwingine tofauti na mkeo?"




"mfanyakazi!"




"mkuu unalolote la kumuuliza bro hapa"




Nurdin akatingisha kichwa kukataa




"ok,unaweza ukaenda!"




Wakati alipotoka Zena akutaka kubaki nyuma alijua kwa vyovyote lazima Zidu angeelekea kwake,ivyo kumruhusu alipanga amfatilie akamuhoji mawili matatu huyo mfanyakazi,akutaka kuomba idhini kwa Zidu kwan angeweza kumtumia meseji akamwambia tunakuja na askari ivyo usieleze chochote,ivyo yeye alichotaka ni kuwa shtukizia...




"afande nami naomba ruksa nitoke kuna shughuli naenda shughulikia mara moja"




"vipi na huyo mtu wako huko ndani?"




Nurdin aliuliza akimaanisha Katarina,




"huyo Mwache nitakuja ku deal naye mwenyewe mbona ataeleza kila kitu?"




Zena aliongea huku akitoka, na kumwacha Nurdin Katika tabasamu mwanana,akifrah kushirikiana na mwanadada yule...










Koplo Zena analivalia njuga swala la Salome kupigwa risasi,anakusanya ushahidi wakutosha akipania kulipandisha kalabrasha la kesi ile juu mahakaman je nin kitaendelea?!




Katarina atafungwa?! ,




twendelee pamoja kuburudika zaidi...




Baada ya Zena kuondoka Salome akamuhoji mdogo wake alichoulizwa na yule afande mdogo wake akumficha akamueleza kila kitu...




"unasema alikuonesha picha ya shemeji yako na ukamwambia alilala siku tatu hapa?"




"ndiyo dada"




"Mungu wangu Paul mdogo wangu nimekwisha"




"kwa nin tena dada?"




Ikabidi sasa Salome amwadisie kila kitu mdogo wake...




"na lazima turudi zetu kijijini"


Na mwisho akaitimisha kwa kumtaka mdogo wake warudi kijijini,




"dada siyoni sababu ya kurudi kijijini kukimbia mji na kurudi kijijini ni sawa na kwenda kuanza maisha mapya na miradi yote ulonayo,tayari yule yupo mikononi mwa polisi iyachie polisi ifanye kazi yake"




"tatizo ataniua sasa!"




"atakuuwaje na yupo mikononi mwa serikali?!,kikubwa pambana ukatoe ushahidi kwamba ndo alokushambulia afungwe usiwe muoga dada!"




"hapana Paul,wacha nikapumzike kidogo kijijini huu msala upite simamia maduka yangu vizuri mtu yeyote akija kuniuliza mwambie ujui nilipoenda sawa?!"




"sawa dada,"




Salome akaandaa nguo zake chache kwenye begi siku ilofatia alikuwa ndani ya gari kuelekea kijijini Kwa Minajili ya kumkwepa Katarina,




**** ** **** ** *****




Mwanamke mikono yake ilifungwa juu akawa akining'inia pembeni yake alisimama mwanaume,ni yule mwenye roho mbaya mwili wake wote uliloa jasho,alikuwa kifua wazi na suruali yake ya kijeshi mkononi alijizungushia mkanda aloutumia kumuadhibia yule binti kusudi aeleze kile alichokuwa akimuuliza,




Binti alikuwa na kibri aliona ni afadhali kufa kuliko kuzungumza, alishapitia dhoruba za mateso mengi ikiwa kubakwa na mtu yule kuchanwachanwa na viwembe huku akimwagia spriti katika vidonda vyake,kukalishwa katika kiti na kupigwa shoti lakin katu binti akufungua mdomo wake kuzungumza mahali ilipo memory,wala kusema 'ZK' ni nani kitendo iko kikazidi kulikasirisha jitu lile lenye roho mbaya asiye hata na chembe ya huruma alotambulika kwa jina la Red Deval kuzidi kumuadhibu kwa kumchapa kwa mkanda ulokuwepo katika mkono wake kulikuwa na uwezekano mkubwa wa Sara kupoteza maisha Red wala ilo yeye akujali akazidi muadhibu kama amwadhibiaye gaidi au muasi wa nchi yake...




Aliacha kufanya kitendo kile pale tu binti alipopoteza fahamu alimfungua na mwili wake kuuacha hapo sakafuni...




Red akatoka akiwa kakasirika sana...




Ulikuwa ni usiku wa manane ,mlango ule ukafunguliwa akaingia mtu mmoja alojifunga kininja kuificha sura yake,




Alienda mpaka eneo alilolala binti yule alokuwa na hali mbaya,




"nakupa dakika mbili chukua simu hii wasiliana na mtu yeyote mtumie msg aje akusaidie maisha yako yapo hatarini ikiwa hapatatokea msaada haraka"




Sara akamtazama sana mtu yule pasina kumjua ni nani na lipi lengo lake hasa!,huku mikono yake ikimtetemeka akachukua ile simu na kumtumia mtu meseji!




"nenda chumbani kwangu ndan ya kiatu changu ndan ya sox zangu chin ya mvungu kuna memory kadi yenye ushahidi wa waziri"




Akatuma ile meseji,palepale na kuifuta akamkabidhi yule mtu simu yake mtu yule akatoka,ila meseji ile katu aikupokelewa Na Sara akujua kama aikupokelewa,aliituma kwa 'Zk' namba ilotumiwa whatsupp katika kundi la waandishi,namba ile 'ZK' aliitumia mara moja moja pale alipohitaji kuwasiliana na watu wake...




Ikiwa Rais atamtumia meseji 'red' katika lain yake ya kawaida basi ndo angeweka laini ile kuwasiliana naye na kuitoa,au pengine alitaka kutoa ripoti katika vyombo vya habari basi angetumia laini ile...




Wakati hayo yakiendelea Zena mwenyewe alikuwa mahakamani kupeleka ushahidi wa Katarina na siku ya kesi ikapangwa...




Siku Zikasonga,hatimaye Katarina Kwa mara ya kwanza akapandishwa kizimbani,




Mahakamani watu walijaa, akasomewa shtaka




Mahakama ile haikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi ile ivyo akupaswa kujibu chochote kesi yake ikapandishwa katika mahakama ya ngazi za juu...




Siku zote Katarina alizokuwa rumande Zidu hakuwah mtembelea moyo ulimuuma sana,hata siku ya kwanza kusikilizwa kesi yake pia Zidu mumewe akutokea...




Zidu yeye baada ya kugundua kuwa Salome kakimbia kusiko julikana ndo kwanza akazidi kumchukia mkewe,kwa mawazo kwamba kama si yeye yule mwanamke ampendaye asingemkimbia, alijaribu kumpeleleza sana Paul mdogo wake Salome bila mafanikio...




Akajilazimisha tu kumsahau, nyumbani walibaki wawili yeye na mfanyakaz wake Suzan,kula walikula pamoja,Suzan akawa akimfulia ukaribu ule ukazidi jenga hisia baina yao...




Siku ya siku Zidu si akamtongoza binti yule,




"lakin baba mimi namwogopa mama"




"kwani utamwambia?,kwanza yule atafungwa kwa kesi ile awezi achwa huru mi ntakuongezea mshahara na akifungwa tu si twasherekea nakuoa mi nataka mtoto Suzy chochote utakacho mi ntakupa"




Zidu aliongea huku mikono yake ikichezea mapaja ya binti yule,tayari Suzan hisia zilisha anza kumpanda akampokea Zidu wakajikuta kwa mara ya kwanza wakiingia penzini...




Kwa mara nyingine tena Zidu akajikuta akimsaliti mkewe alokuwa katika wakati mgumu rumande,wote wakitaman afungwe kusudi tu wawe huru na penzi lao...




Siku ya kusikilizwa kesi kwa mara nyingine ikawadia, mshtakiwa akiwa na pingu zake akapandishwa kizimbani,uso ulikuwa umemvimba kwa kulia,aliangaza macho yake kwa watu wote walokuwa wamemtembelea,kwa mara ya kwanza akatabasamu baada ya kuwaona watu wawili ni Mery na mume wake Isack ambaye kwa mara ya mwisho alikuwa na hali mbaya,kuja katika kesi yake jambo hilo lilimfuraisha sana...




Mwendesha Mashtaka akamsomea shtaka kwamba mnamo tarehe fulani ulimshambulia Salome kwa uwivu wa kimapenzi unakubali unakataa,Katarina akakana kama kawaida yake akapandishwa shahidi ambaye hakuwa mwingine ila ni koplo Zena...




Zena alieleza kila kitu toka mara ya kwanza Zidu Kumleta Kituoni Salome akamkatia pf3 akidai ni mpenz wake,akaanza kufatilia kesi ile hosptalin alipokutana naye ushahidi wa sauti wa yule bibi na hata yule mtoto ushahidi wa mfanyakazi Suzan na hata paul,akaitimisha kwa kuomba mshtakiwa apewe adhabu kali...




"kuna chochote upande wa wakili wa mshtakiwa"




Kijana Brayson alokuwa wakili kutoka serikalini alokaa upande wa Katarina akamtwanga swali afande Zena...




"afande"




"naaam" Zena akaitika




"tofauti na izo audio kama ushahidi je yupo shahidi yoyote kati ya hao wenye hizo sauti ambaye anaweza kudhibitisha hayo uyasemayo?,hima mume wake huyo Zidu,huyo bibi,huyo mtoto,au hata huyo aloshambuliwa Salome au huyo mfanyakaz wao yupo yeyote wa kudhibitisha ilo?!"




Kwa Swali Lile Katarina akatabasamu,Zena akajibu...




"sikuona haja ya kufanya ivyo hali ya kuwa sauti zao ninaz...




"sauti kitu gan afande,mfano mimi naweza chukua simu yangu nikarekodi wewe umenshambulia kwa risasi nikaongea saut ya kike mfano...




Wakili yule alikuwa na uwezo wa kuongea sauti ya kike




"afande ni kwel huyu kanshambulia risasi...




Watu wote pale mahakaman wakatabasamu wakili akamgeukia Zena aka 'pley' ile audio...




"je hii sauti inayo ongea huku ni ya kike au ya kiume?"




"ni ya kike" Zena akajibu...




"ila alorekodi niwa kike au wa kiume?"




"wewe si ndo umerekodi kwa sauti ya kike"




"vizuri,basi hata hizo sauti katika kajisimu chako zinaweza zikawa zimerekodiwa na mtu mmoja kwa saut tofauti tofaut kuna watu wengi tu wana uwezo huo"




"mfano nani? na kwa nin nifanye ivyo kwa manufaa gani?"




"mfano nani?,mfano mimi si nimeongea hapa sauti ya kike,mfano pia joti yule mwigizaji anauwezo wa kuongea kama babu,binti na hata mtoto kwa hiyo nimwombe muheshimiwa hakimu autupilie mbali huu ushahidi wa sauti na atuletee watu hai na si sauti..."




HAKIMU: Shahidi no moja afande Zena Je unaweza kutuletea baadhi ya watu walio miliki hizo sauti hapa mahakaman moja wakakiri ni sauti zao,na pili wakasimama kama mashahidi?"




"ndiyo,naweza nikawaleta baadhi ila awa wagonjwa sitoweza huyu bibi na huyu mtoto ila ntamleta huyo mshambuliwaji Salome aje akiri ni kweli alishambuliwa,pia nitamleta huyo mume wake akiri kumleta kituoni huyo Salome baada ya kushambuliwa na pia nitamleta mfanyakaz wao Suzan akiri ugomvi mshtakiwa na mumewe walokuwa nao na pia nitamleta mdogo wake na mshambuliwaji naye aikubali sauti yake na kukiri alichosema ni kweli"




"basi mshtakiwa atarudishwa rumande na kesi hii tunaihairisha mpaka Jumatatu ijayo ya tar 15 mwez huu shahidi aweze leta hao mashahidi alowataja hapa"




"kooooortiii"




Kesi Ile Ikafungwa Na Katarina akarejeshwa katika karandinga tayari kwa kupelekwa rumande kusubiri hiyo wiki ijayo...




Alitaman hata awapungie mikono Isack na mkewe ila akuweza mikono ilipigwa pingu,waandishi mbalimbali walimpiga picha,machozi tu yalikuwa yakimchuruzika,




Koplo Zena anaendelea kushughulikia kesi ya Katarina akipanga kumfunga,kwa bahati mbaya ushahidi wa sauti alokuwa akiutegemea unakataliwa mahakaman na kuahidi kuwapeleka baadhi ya watu wenye sauti zile kusudi wadhibitishe kwa mdomo kile akisemacho tuendelee na seh ya 18 ya riwaya hii ya kusisimua...




Koplo Zena baada ya kutoka pale alienda moja kwa moja ofisini akamweleza kila kitu Nurdin,




"dah Pole sana kwa hiyo utafanyaje?!"




Ins Nurdin akamuuliza...




"yapaswa nionane na Zidu,Salome,yule mdogo wake Salome na hata yule mfanyakaz wao"




"ha ha ha ha usinifuraishe Zena unataka kunambia Zidu anaweza kuwa shahidi wa kumfunga mkewe? really"




Zena akatabasamu,




"lah!,sina maana hiyo"




"bali?"




"yeye akiri tu kwamba ni kweli walishambuliwa pili kwel walikuja kituoni kukata pf3 na mwisho akiri Salome ni mfanyakaz wake na Katarina ni mkewe,hivyo tu"




"ahaaa hapo nimekuelewa!"




"vizur kwa kunielewa,watakao mfunga ni yule mfanyakazi wao kwa kukiri Kutolala nyumbani kwa Zidu ndani ya siku tatu siku ya nne ambayo ndo siku Salome aliposhambuliwa Zidu alirudi nyumbani na kuanza kumpiga mkewe,mpaka kumuunguza na uji! basi hapo ntakuwa nshamaliza kazi"




"dah nakuvulia kofia asee we ni hatari ulishakuwa wakili kabla ujaingia idara ya polisi nini!




Zena akuongea kitu zaidi ya kuishia kucheka...




"sasa mkuu wacha nikaonane kwanza na Zidu"




"kazi njema afande...




***** ** ***** **




SURA YA NNE




GEREZA LA SEGEREA




Safari hii Katarina baada ya kutolewa pale kituoni alipokaa siku nne kabla ya kupandishwa mahakama ya mwanzo,baada ya siku mbili akapandishwa mahakama ya wilaya ambapo kesi yake ilisomwa na kuahirishwa baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha , akapandishwa katika karandinga la wafungwa safari yao ikaishia segerea...




Lilikuwa Ni gereza kubwa baada ya kuingia walipewa namba na manguo mekundu,




Wakaandikishwa majina na kutupwa lockup...




"hoya Mery huyo ni mchumba wangu mtu asimguse asee"


Mmama mmoja aliongea kijeuri huku akimfata mfungwa msichana mrembo alokuwa na miaka 18 au 19 muda wote binti yule alikuwa akilia toka wakiwa karandingani...




Alipoingizwa tu ndani ya lock up ile mdada mmoja alotambulika kwa jina la Mery alimkimbilia na kuanza kumbembeleza,kabla sauti ya kibabe iliposkika ikimtahadharisha Mery kukaa mbali na binti yule eti ni mchumba ake!




Kwa mara ya kwanza Katarina akatabasamu,




"Sweet huyu utansamee Getrude nilikuachia lakin huyu aki ya mama tutauana"




"unajifanya mjeuri siyo..." yule mwanamke alokomaa alotambulika kwa jina la sweet akanyanyuka na kumsogelea Mery,watu wote walikuwa wakiwatazama...




"Mery nimekwambia mwachie kiuno huyo mwanamke ni wangu"




"simwachii"




"ebwana eeh nyinyi washamba nini mmepata wageni wawil mwamgombania mmoja, mmoja si amchukue huyo mchumba au yeye kashatumika kotekote nin"




Binti Mwingine alokuwa kajikalia pembeni akaropoka akimnyooshea Kidole Katarina!




Bila shaka akumjua vizuri Katarina,




Katarina hakuwa mwenzake, akamkata jicho na kupiga hatua na kumsogelea




"unasemaje eti we malaya?!"




Akamuuliza,alipo Mfikia akazishika kola ya 'ovarol' lile alilovaa akamnyanyua na kumtandika ngumi ya mdomo,binti chini,palepale wakanyanyuka wanawake wengine watano na kukunja duara wakimweka Katarina Kati,wakawa sasa wakisogea lengo wamshike wengine wamshambulie,ile wamemfikia ndo wanataka wamkamate binti alijirusha na kuwatandika mateke kila mmoja akasambaratika upande wake,


Hakuna alosubutu kumsogelea...




"haya na nyie niwaone mnagombana mtanijua mimi nani Sweet rudi pale"




Yule binti alo mfata mwenzake,akimgombania mrembo akarudi eneo alilokuwa amekaa awali




"unajifanya mjanja hapa siyo ukonga ngoja madam mama anakuja utaona sasa!"




Dada yule alopigwa baada ya kutoa maneno machafu,akawa akiongea huku damu puani na mdomoni zikimtoka,aliamini moyoni mwake Katarina ni mfungwa aloamishwa gereza,maana si kwa ubabe ule,




Katarina wala akumjibu kitu akatafuta eneo akaketi,




"njoo hapa binti"


Akamwita yule binti mdogo aloanza kugombaniwa




"unaitwa nani binti?!"




"naitwa Scolastica"




"unamiaka Mingapi Scola"




"kumi na nane"




"daah pole sana Scola kitu gani kilichokufanya mpaka ukawa hapa?"




Badala ya kujibu Scola akaanza kulia,




"pole sana kama nimekutonesha kidonda usilie mama we nielezee"




Ndipo Scola alipoanza kumsimulia...




Ni mtoto pekee katika familia ya mzee Damas,ajabahatika Kuwa na kaka na hata dada wala wadogo zake,maisha wanayoishi ni maisha ninayeweza kusema ni ya kimasikini,mama yangu uuza pombe ndipo upata ela ya kunisomesha,baba afanyi kazi yeyote zaidi ya kunywa pombe,asbuh mchana jioni yeye ni kalewa,usiku umpiga mama ni kwa muda mrefu sana amekuwa akifanya ivyo nami nikiingilia uwa ananipiga...




Sasa juzi usiku alidhamiria kumuua mama alimpiga sana akambania kwenye ukuta na kumnyonga mi nikajua angemuulia pale mama ,nikachukua mwiko mkubwa wa kusongea ugali wa pombe ndo ulikuwa hapo kitandani na kumpiga nao kichwan,baba alianguka palepale na kufa na hata alipo muachia mama naye kumbe alishakuwa amemuua, ikabidi nianze kupiga kelele watu wakajaa nikaeleza ndipo nilipopelekwa ofisi ya kijiji,asbuh jana ndipo nilipo pandishwa mahakaman nikasomewa shtaka na kuletwa huku nikiwa sijui ntasomewa lini hukumu,ntahukumiwa nin...




Katarina alimuonea huruma sana yule binti,alikuwa ni mrembo,tena mrembo hasa ila alijua urembo ule usingedumu...




"je na wewe dada yangu nikipi kilichokufikisha hapa?"




Katarina naye ikabidi aanze msimulia,dada pia alisikitika,akampa pole...




Kengele ya chakula ikagongwa wote wakaelekea kupata chakula,




Hakuna alo msogelea tena Katarina wala yule binti alojitambulisha kwa jina la Happy Wakala vizuri na kurudi zao katika lock up zao wakufungiwa...




Mida ikasonga,saa kumi kumi lango likafunguliwa




"Katarina?"




"Naam afande"




"Kuna ndugu yako anataka kukuona"




Katarina alfrah akajua pengine ni Zidu kaja kumwangalia mke wake,ila kufika alikuwa ni Isack na mkewe Mery,wakampa Chakula,na pole nyingi




'Isack shemeji yangu nakuomba mfate Zidu mwambie hata aje aniangalie mie mkewe naumia sana nakuomba shem.."




"Usijal shemeji yangu ntajitahidi kwa ilo na nahakikisha nakuekea mawakili unashinda hii kesi"




"Usiangaike shem kupoteza gharama zako huyu huyu wa serikali yupo vizuri naimani nitatoka tu"




"hey muda wa maongez umeisha..."




Muda ule ule askar akamrejesha Katarina Selo...




Mpaka muda ule Katarina alikuwa ajamjua nyapara wa selo yao ile japo alidodosewa anaitwa madam mama au big mama,yule alo mpiga ndo alikuwa mpenzi wake,




Katarina alitaman sana huyo big mama aje...




Hatimaye Saa kumi na moja na nusu ikawadia,yule binti akafungulia kulia,punde lango likafunguliwa na wafungwa wengine walo onekana tu wametoka kwenye kazi wakaingizwa,




Yule Binti alokuwa akilia alinyanyuka na kumkimbilia mwanamke mmoja mnene yeye nguo alivaa tofauti na wenzake yeye alivaa ovaroli la njano alipomfikia akamkumbatia huku akilia...




Katarina akatambua huyo sasa ndio big mama




"unalia nin mpz wangu nani kakukwaza"




Tofauti na mategemeo ya wafungwa wote yule binti akamnyo oshea kidole Happy Big mama akacheka tena sana tu...




"usilie mpz huyu adhabu yake ni usiku"


Big mama akaongea kwa sauti yake nene kilichoendelea hapo si cha kuandikika...




Katarina akuingilia kwa kuwa wote wawili walifurahia kitendo walichokuwa wakikifanya na mbaya zaid big mama alikuwa na uume wa bandia alouchomoa mfukoni mwa suruali yake,alikuwa akitembea nao...




"Usijal Scola huyu binti kaogopa kunitaja kajua nitamwaribu haribu huyo mpz wake,sasa hakuna atakayekugusa hiyo usiku mimi si nipo"




Katarina alimtoa khofu baada ya kuona Scola akitetemeka...




"alafu naona na wagen wawili,mimi ndo nyapara wa selo hii wafungwa wote mpo chin yangu jitambulishen tafadhali"




"mimi naitwa Katarina"




Kata akajitambulisha "ehe nawe mrembo ulo mliza mpz wangu unaitwa nani?"




"mimi?!" Scola akauliza huku akitetemeka




"ndiyo wewe kwani naongea na nani?" Big mama akajibu kishari,




"Scola!"




"vizur usiku utaipata shuruba yangu unaona hii,utajuta kukiliza kipenzi changu"




Big Mama akazidi kumtisha huku akimuoneshea kiungo chake kile cha bandia...








Nyapara madam mama akasema




"Alafu naona na wagen wawili,mimi ndo nyapara wa selo hii wafungwa wote mpo chin yangu jitambulishen tafadhali"




"mimi naitwa Katarina"




Kata akajitambulisha "ehe nawe mrembo ulo mliza mpz wangu unaitwa nani?"




"mimi?!" Scola akauliza huku akitetemeka




"ndiyo wewe kwani naongea na nani?" Big mama akajibu kishari,




"Scola!"




"vizur usiku utaipata shuruba yangu unaona hii,utajuta kukiliza kipenzi changu"




Big Mama akazidi kumtisha huku akimuoneshea kiungo chake kile cha bandia...




"Usijali mamy hili mradi mi nipo hakuna kitakachokupata"




Baada ya Katarina Kumtia Moyo kidogo Scola Wasiwasi ukampungua,




Big mama aliendelea kukaa na Happy akimbembeleza,




Yalikuwa ni maajabu ndani ya gereza lile la kike wanawake kwa wanawake walikuwa wakisagana,pasina hata tone la haya usoni masaa yakasonga hatimaye mida ya chakula ikatimia wakafunguliwa lockup wakaenda maeneo ya jikon,




Kila mtu akapewa sahani yake wakajipanga mstari na kuanza kupewa chakula,




Katarina alikaa nyuma ya Scola bado alionekana ni binti mdogo hivyo alijua ilipaswa akae nae karibu kumlinda na walojiona wababe wa gereza, walichukua chakula na kwenda eneo lao wakakaa na kuanza kula,




Pembeni yao madam mama alikaa na wenzake walomsimulia ubabe wa Katarina,jinsi alivyowapiga kule ndani big mama alicheka sana akajinyanyua na kuwasogelea lengo lake ampokonye chakula Katarina,




Alitaka Kumpima Uwezo Wake,




Akujua yule ni mtu mwingine ayupo kama amfikiriavyo,




"yani wageni mje leo na mle embu lete iko chakula,"




Big mama akamnyang'anya ile sahani Katarina,akawa akikila,Katarina akujibu kitu akabaki tu akimwangalia, wafungwa wakawa wakishangilia,alipo maliza akamnyang'anya na Scola Ile sahani yake...




"mrudishie huyo sahani yake"


ITAENDELEA


     


Simulizi : Kufa Tu  Hakuna Namna 


Sehemu Ya Nne (4)






Katarina aliongea kwa ukali akionekana kukasirika,




"eti,unasema?"




Big mama akauliza huku akimkabidhi sahani ile rafiki yake,




"Nimesema mrudishie huyo sahani yake!"




Katarina akapaza sauti,akijinyanyua...




Big mama akaachia cheko la dharau




"ha ha ha ha nadhan ujanijua mimi ni nani,na kwa bahati mbaya mi ndo nyapara wako,ngoja sasa nikufunde adabu siku ingine ukome kunipazia sauti mpumbavu we.."




Palepale akataka amnase kibao,lilikuwa kosa,Kata akamkamata mkono na kumvutia kwake,ile big mama anakuja akamuhepa big akaenda chini Kata akamuwah yule dada na kumnyang'anya chakula akamrudishia Scola...




Big Mama akajizoa zoa na kujiamsha sasa alikuwa kavimba kwa hasira miaka zaidi ya ishirini akuwahi kutokea wa kumpiga pale gerezani,




Katarina ndo wa kwanza naye akukubali ile kamfikia Big akamrushia teke Katarina akalipangua kwa mkono Big aliposhusha mguu akarusha ngumi kadhaa ambazo zote Kata alizihepa binafsi akutaka kurudisha mapigo alikuwa na maana yake...




Wakati Kata akiendelea kukwepa mapigo ya Big kelele za watu walokuwa wakishangilia ziliwafikia maaskari wa magereza yale,palepale wadada wa nne wakiwa na silaha walifika wote wakaanza kumshambulia Katarina,




"kumpiga Nyapara ni sawa na kutupiga sisi sasa leo utaona cha mtema kuni,"




Walimpiga Mpaka Kata akawa nyang'anyang'a si kwamba hakuweza kupambana nao au kurudisha mapigo yale




la asha




Uwezo ule alikuwa nao,ila akutaka na alijua kwa nini alifanya vile...




Baada ya kumpiga Kata na kuwa nyang'anyang'a walimbeba wawili mmoja akishika miguu mwingine mikono,




Wakaenda Nae upande wa pili na kumtupia ndani ya selo ambapo kilikuwa ni chumba cha mateso ndani kilitawala giza tu,na alikuwa peke yake...




Baada Ya Kutupwa Lango Likafungwa,kata alihisi harufu kali kama ya kufa kitu akuweza kuona ni nini kutokana na giza lililotawala...




Ghafla akahisi maumivu makali mwilini na akitembelewa na vitu,mfano wa siafu...




Kutokana Na Kipigo alichokipata uwezo hata wa kuinuka hakuwa nao,akabaki akivumilia yale maumivu makali,huku akilia...




Baada ya maaskari wale wa magereza kuondoka na Katarina,




Nyapara alikichukua chakula cha Scols na kukila,Scola alibaki tu akilia,kama mkombozi wake kachukuliwa je ni nan ambaye angemuokoa?,aliona sasa hatari ndo inaenda kumkuta...




Baada ya chakula waka hesabiwa wafungwa na washtakiwa wakarudi katika lockup zao...




"huwa Kila anayejaribu Kushindana Na Nyapara mwisho wake ua ndo ule..."




Madam mama aliongea kwa majivuni,




"Scola usisahau usiku utaichezea hii"




Big akamkumbusha binti yule mdogo huku akimuonesha kile kiungo chake cha bandia,




Scola alibaki kujiinamia akilia,alielewa Big alikuwa na maana gani alipanga bora kufa lakini si kuchezewa mwili wake na mwanamke mwenzake,hakuwa tayari kwa ilo...




***** ** ****




Giza lilikuwa limetawala, ndani ya chumba kile kidogo ndani kulisikika mguno wa maumivu,




Mtu alikuwa katundikwa mikono juu ya paa akining'inia akiwa uchi kama alivyozaliwa...




mwili wake wote ulitapakaa majeraha,ya kupigwa alikuwa akigugumia kwa maumivu makali alokuwa akiyapata




"kama ukihitaji kuwa huru tukuachie tupe hiyo memory au twambie ilipo tukaichukue wenyewe lasi ivyo utafia hapa nakwambia,"




Mtu yule alotundikwa Sara,alikumbuka maneno aloambiwa na yule alokuwa kila mara akimuhadhibu...




Sara hakuwa tayari,ilikuwa lazima aivujishe tu video ile,




Imesababisha kampoteza mpz wake Sudi,mwanaume alo mpenda,hakuwa na shaka waziri ndo alohusika kama si yeye,kapata mateso makali pia kwa ajili ya video ile,swali lililokuwa likimuumiza katika kichwa chake ni je,meseji yake ilimfikia 'ZK' hakuwa na uhakika wa jambo hilo,na je yule mtu ni nani,alovaa kininja na alikuwa na maana gani kuhitaji kumsaidia?!...




Wakati akiendelea kuwaza kuhusu mtu huyo huku akiendelea kuning'inia juu ya paa alipofungwa mikono alihisi mlango kufunguliwa,akaingia tena yule mtu...




"SARA nataman sana kukuokoa ila sijui nitakuokoaje nilikupa simu uwasiliane na mtu unaye ona ataweza kukusaidia juzi mpaka sasa sioni dalili na hata ukisema mahali ilipo hiyo memori utobaki mzima tutakuua tu kesho tuna kaa kikao cha mwisho ivyo jua upo hatarin SARA muda wowote kwanzia kesho unaweza kufa..."




Mtu yule aliongea kwa huzuni,na kuzidi kumshangaza Sara,




"la..la.lakini..wewe ni nani?"




Sara akajikakamua na kumuuliza...




"upaswi kufikiria kunijua mimi ni nani! lah!,fikiria ni kwa vipi utaokoka hapa au uyapendi maisha yako? kesho nikija ntakuja kwako kwa mara ya mwisho moyo wangu wantuma sana nikusahidie"




Mtu yule alojifunga kininja aliongea na kutoka,Sara akashusha pumzi ya kukata tamaa




*** *** ***




Kitara Cha Polisi Kilisimama nje ya nyumba alokuwa akiishi Salome,akashuka Mwanadada machachari na kuisogelea nyumba ile,akagonga mara moja,ikasikika sauti ingia mlango upo wazi...




Koplo Zena akafungua mlango na kuingia




"nimemkuta Salome?!"




Akamuuliza yule kijana ambaye alimjua kama mdogo wake Salome,Paul,




"Dada ayupo alisafiri!"


Paul akajibu kwa unyonge...




"kasafiri?!,eh,tangu lini kaenda wapi?!,na anarudi lini?"




"tangu wiki ilopita,ajanambia siku atakayorudi!"




"Mungu wangu,na nampigia hapatikani,au unazo namba zake nyingine?!"




"hapana mi sina,"




Koplo Zena alichanganyikiwa Salome ndo alikuwa kichwa wa ile kesi,sasa kama katoweka,dah kwa kweli Zena alichoka,ikabidi ambembeleze Paul siku ya jumatatu akawe shahidi,paul akamtoa khofu kuwa atakwepo...




Zena alishkuru akaaga akatoka,sasa alikuwa akielekea nyumbani kwa Zidu kuonana na yule mfanyakazi Suzan alijua mida ile Zidu atakuwa kazini!,




Ila alifika na tofauti na mategemeo yake akawakuta wote,akakaribishwa sebuleni,Zidu alifurah sana kumuona Zena,




"nilijua sitakukuta ntakukuta kazini!"




"nafungaga kazi saa saba wakati wa lanch kazi ikijitokeza napigiwa simu nadandia gari naenda"




Zidu akajibu akimshushia tabasamu mwanana , tabasamu ambalo mara nyingi lilikuwa sumu kwa watoto wa kike,aka amua kulitumia pia kwa binti yule,na kweli likamtega,japo alifanikiwa kulimeza lisitambulike kwa Zidu...




"una taharifa zozote za Salome mpz wako?!"




Zena alihoji tena mbele ya Suzan,pasina Kujua Suzy alikuwa ajuh juu ya Salome,na Kwa Kipindi Iko Suzy ndo alikuwa mpz wake Zidu,




"aliondoka bila hata kuniaga,sijui kaenda wapi na hata simu yake pia haipatikani!"




Zidu aliongea kwa unyonge,Zena alipo mwangalia usoni aligundua kile Zidu aongeacho ni cha kweli...




Wote walitambua kuwa Salome Itakuwa alimkimbia


na kuzidi kumpandisha hanjamu za kimahaba!,




Ushahidi huo ulitosha kumfunga kabisa Katarina,




...20...




Baada ya kumkumbatia kwa muda hatimaye wakaachiana, Zena akaangalia pembeni kwa aibu uso wake ukiwa umebadilika kidogo,




"wacha mimi niende jumatatu mahakaman msije niangusha kwanza Zidu nipe kabisa namba zako"




Zidu akamtajia namba akaziandika na kumpigia namba zake zikaja katika simu ya Zidu,akazisevu




"sasa wacha mimi niende tutawasiliana!"




Zidu naye akaamka kwa lengo la kumtoa,huku nyuma Suzan alikunja mdomo, ukaribu wa yule afande na Zidu aukumpendeza...




Suzy alitawaliwa na chembechembe za uwivu,akalikimbilia dirisha na kufungua pazia akawa akichungulia nje,Zidu alikuwa akimsindikiza Zena mpaka eneo alilopaki kipira chake,Zena akaingia kwenye kipira,Zidu ndo akarejea ndani,Suzan akarudi haraka kwenye siti yake!...




Zidu alipoingia akaenda kuketi pembeni yake...




"vizuri sana mpz wangu, lazima tutoe ushahidi Katarina afungwe hili mimi na wewe tuendelee kuishi kwa uhuru!"




"lakini mama akuwah kunambia kuwa anataka kumuua Salome,mama atanielewaje mimi?!"




"yule si mama yako,ni muda wa kulipigania penzi lako yule tukitoa ushahidi anafungwa maisha mimi naishi na wewe ndo unakuwa mke wangu usiwe mjinga Suzzy watu wengi wanaitaman hii nafasi"




"basi mpenzi nimekuelewa, usijali ntafanya chochote kulilinda penzi langu"




Zidu akatabasamu,




"mambo sindo hayo sasa"




Akaamka Na Kumbusu shavuni akambeba wakaelekea chumbani...




*** *** ***




SURA YA TANO




Kimya kilitawala, nikatika chumba kimoja ambayo ilikuwa ndo ofisi ya madam 's' mkuu wa kitengo cha usalama wa taifa




Mbele yake walikwepo vijana watano,vijana hatari na walioaminiwa na mkuu wa idara ile serikalini madam 's'




Baada ya kimya kile kifupi ambacho kilitokana na madam 's' kuwa bize na laptop ilokuwa mbele yake...




Akamimina maji katika glasi yalokuwepo kwenye chupa kubwa akanywa kidogo kusafisha koo,akawa angalia vijana wake wote...




"red deval,pizo,chronic Killer,veko,m'd...




Akawataja majina mmoja mmoja wote walimtazama pasina kusema kitu,madam 's' akaendelea...




...Jana niliitwa na waziri mkuu baada tu ya kuingia ofisini,kalaani kitendo cha mimi kutuma vijana wangu wakamdhuru Sudi,na kaagiza jambo moja lifanyike kati ya mambo mawili,moja ni bora tu tumwachie huyo mtangazaji Sara,kama hatutaki kumuua, pili huyo 'ZK' asakwe auwawe nimemuhaidi ndani ya siku tatu kutimiza haya,nimeitisha kikao hiki kujua mlipofikia Red je huyo binti kakueleza chochote kuhusu ilipo memoricard na juu ya huyo ZK?"




Macho ya wote sasa yakamgeukia 'Red deval' kijana katili asiye hata na chembe ya huruma apendaye kuua




"mkuu,nimemtesa sana yule mtu,nimemchanja chanja na kiwembe nikimpaka sipriti nimemfunga juu ndani ya siku tatu akining'inia ila kaona bora kufa lakin si kuongea yule binti si wakawaida mkuu ana uwezo mkubwa sana wa kuficha siri,"




"Veko katika uchunguzi wako tulokutuma ukaichunguze familia ya Sara umegundua nini?"




"anatoka katika familia ya kawaida,wazaz wake wanaishi gongo la mboto kasoma Reginald Mengi Sekondan Iliyoko Gongolamboto akafeli akaenda chuo cha uandishi cha Tumaini journalism akachukua setificate na baadaye diploma,baada ya hapo alishafanya kazi vituo mbalimbali ikiwemo TBC1,ITV,CHANEL TEN,na mwisho ndo hapo alipo Tumahini Tv,ripoti yeyote kwamba alipitia jeshi,hakuna...




Mahusiano yake na Sudi niya muda mrefu na walikuwa wakiishi pamoja,pia tumesachi kila kona katika chumba chake bila mafanikio...ndo hayo tu mkuu"




Madam 's' akaguna ni kama akurizishwa na ripoti zile ila alipaswa akubali,kwani vijana wake wale aliwa amini sana,hakutaka kujenga kuwatilia shaka...




"na vipi kuhusu huyu mwandishi ZK?"




"Hapo sijagundua kitu mkuu ila huyu ZK,siyo ZIDU KATILI kweli?"




"ZIDU KATILI?!"




Wote wakatamka kwa pamoja kumbukumbu yao ikirudi kwa Komandoo hatari Wa Ganyakite ambaye kwa sasa alikuwa akiishi Tanzania akiwa na kampuni yake ya upelelezi,

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog