Search This Blog

Thursday 29 December 2022

KUFA TU HAKUNA NAMNA (2) - 2

  

 Simulizi : Kufa Tu Hakuna Namna (2)

Sehemu Ya Pili (2)





...nadhani umenielewa nahisi bado dakika kumi jamaa atawasili,nikate simu uwapange vijana wako ok"




"sawa kijana wangu!"




"hakikisha unatumia vijana unawowa amini ambao itapaswa wawe upande wetu kwani lazima uwaweke wazi ishu nzima jinsi ilivyo,narudia tena ni lazima uwe una waamini na wawe wasiri sawa kamishna?"




"ok,mkuu"




Daniel akakata simu,muda ule ule kamishna akampigia simu katibu muhtasi wake,




"niitie insp Nurdin Na Afande marwa Na Koplo Nobi ofisini kwangu"




"ok mkuu"




Punde Vijana hao watatu wakaingia,ni watu ambao Kamishna Haruna aliwa amini ukimtoa koplo Zena ambaye kwa sasa alikuwa hosptalini,




"nimewaita nyinyi kwa kuwa ni watu ninao waamini,ni watu wangu wa karibu ni watu mlotayari kupigania nchi yenu sina muda mwingi sana wa kuwapa maelezo mkanielewa ila ntawaeleza kwa kirefu baada ya kazi hii,narudia tena sina muda mwingi sana wa kujibu maswali yenu ila ninachotaka kuwaambia dakika tano zijazo nitaja kutekwa hapa ofisini ninyi mnachotakiwa kufanya ni kuniokoa mimi,"




Vijana wale watatu wakashtuka,maswali yakavishambulia vichwa vyao ila wakajizuia kuuliza wakiikumbuka amri waloipewa awali,wakazidi msikiliza mkuu wao...




...mtaenda nje parking pale mi ntatolewa na mtu na kuingizwa ndani ya gari ntapiga kelele gari itatolewa kwa kasi nanyi mtaifukuzia kwa nyuma,mnaweza kuishambulia kwa risasi,pia mnaweza mpiga dereva risasi ila chunga msimpige kichwani piga panapotibika narudia chunga msimdhuru dereva kwa kuwa nae ni mtu wetu"




'mtu wetu?, kivipi!,mtekaji naye ni mtu wetu'




Maswali yakarindima kwenye vichwa vyao,ila awakuuliza kitu...




"mnaweza mkaenda nadakika tano tu hapa kawaini kukaa kwenye gari,nyongeza hakikisheni gari full tank,kingine muwe na risasi za kutosha msimshirikishe mwingine katika jambo hili ok!"




"ndiyo mkuu"




Vijana wale watatu ambao ni Inspekta Nurdini,koplo Nobi afande marwa huyu akuwa na cheo chochope polisi,




Wakatoka!...




*******************************




Richard Mombi alinyanyuka kwenye kochi alilokaa akatoka mpaka nje akaingia ndani ya gari ilokuwa ikimilikiwa na usalama wa taifa ofisi ya waziri mkuu tawala na tamisemi,




Upande Wa Pili Ofisi Wa Madam "s" ghafla alarm ikaskika katika faili moja lililopo katika kompyuta yake,pakawa panawaka kitaa chekundu,




Madam 'S' akatabasamu!




akaelekeza kimshale pale katika lile faili akalifungua,na kuliongeza ukubwa (zoom) likatawala katika kioo kizima,




ilikuwa ni kama mchezo wa gemu ule wa gari,




Katika Kioo Kile alionekana Richard Mombi akiwa ndani ya ile gari na alipoliwasha tu ndipo 'alarm' iliposikika katika kompyuta yake...




akawa sasa akifatilia,kama anaangalia 'movie' alijua dereva akujua kama anafatiliwa,gari ilienda mpaka makao makuu ya jeshi la polisi akashughudia Mombi akishuka!




sasa akawa akiona ndani ya gari,kama baada ya dakika tano hivi alishughudia mtu akiingizwa kwenye gari mlango ukafungwa Mombi akakimbia upande wa pili wakati akizunguka upande wa pili alimsikia kamishna akipiga yowe,akamshughudia Mombi akiingia upande wa dereva


"unapiga kelele siyo kwani ndivyo tulivyoelewana"




Akaisikia sauti ya Mombi,palepale akamtandika ngumi nzito mdomoni na kuliondoa gari kwa kasi!




madam 'S' aliona kila kitu




JE NINI KITAENDELEA?! HUU NDO MCHEZO WA SERIKALI BWANA RAIA TUISHI TU ILA VILIVYOKO NDANI YA SERIKALI ISHIENI KUVISOMA HUMU KWENYE RIWAYA




KAZI YA URAIS, UWAZIRI, UBUNGE SI NYEPESI KAMA TUDHANIAVYO...










Madam 'S' anahisi kwa vyovyote vile lazima Kamishna Haruna Gozigozi atakuwa akijua kitu kuhusu 'Zena' ana amua kumtuma kijana wake Richard Mombi kumteka kamishna yule pasina kujua mchezo anawochezewa, Richard anamteka,ila nyuma anakimbizwa na maaskari je nin kitaendelea




Tusonge!...




Madam 'S' alishughudia kila kitu jinsi Mombi alivyokuwa akikimbizwa na gari ile ya polisi mpaka ikamfikia na kuanza kuishambulia kwa risasi




'shit,this is it?!'




Madam 'S' akalaani kimoyo moyo akijilaumu moyoni mwake,tayari alishajua kampoteza kijana wake mwingine,




Kijana aliyemtegemea na kumwamini alizidi kufatilia lile tukio na mbaya zaidi kwa kuwa walipitia lami trafki nao wakaunga msafara kumkimbiza,wakiwapigia simu na wenzao hatimaye Richard akatiwa nguvuni akishushiwa kipigo kikali,




kumteka kamishna wa jeshi la polisi?!




Akaenda Kutupwa Lupango kusubiri Kukamilika Kwa Upelelezi Kwanza,




Kichwa cha madam 's' Kilizidi Kumuuma Kwa Mawazo,kwa vyovyote vile kulikuwa kuna mawili ilikuwa lazima amtoe Mombi gerezani ikishindikana basi amuue,




Alijua akiendelea kuwa chini ya mikono ya maaskari na kuteswa angeweza kutoboa siri zake!,pia swala la kumteka kamishna na kumuhoji amweleze siri zote lilikuwa katika fikra zake,




kivipi sasa angefanikiwa?!




ilipaswa kazi ile sasa aifanye yeye mwenyewe!




'ishu ni kumjua muhasisi wa mpango wote huyu ndo wa kudeal naye na watu wawili niki deal nao vizuri ntajua kila kitu,kamishna na huyu Zena,wafe au wanambie ukweli wanatumika na nani,mtu au kikundi gani na lipi hasa lengo lao,yah nimepata wazo...




Angel,




Angel atanifumbulia kila kitu ngoja nikamwone,madam akavaa kikoti chake na kutoka ndani ya ofisi yake ile...




*******************************




MUHIMBILI HOSPITAL




CHUMBA MAALUMU




SAA SABA USIKU




Usiku ulikuwa umetawala, kimya kikiwa kimeshika hatamu katika chumba kile ambacho ndani kilikuwa na watu wa tatu,




Zena akiwa kalala katikati mkononi akiwa na pingu kwa sasa ile hewa ya oxygen hakuwa nayo wala dripu japo hali yake aikutengemaa kuruhusiwa kutoka pale...




kitanda cha pembeni yake upande wa kulia alilala katarina na upande wa kushoto alilala Don G,




Don G kwa muda ule hakuwa hata na lepe la usingizi ni kama alikuwa akiwaza kitu,ghafla akajiamsha na kukaa kitako, macho yake yalikuwa bize yakimtazama Katarina upande wa pili kule aliyekuwa akikoroma akaridhika kwamba si wa kuamka muda huo akajiamsha na kunyata mpaka kitanda cha Zena




Palepale mkono wake wenye nguvu akaupeleka shingoni kwa Zena na kuanza kumnyonga kwa nguvu ila ghafla alihisi pigo zito likitua juu kidogo ya kiuno au chini kidogo ya kwapa,wakati anageuka kutaka kumwangalia ni nani alo mshambulia huku akiiachia shingo ya Zena kiza kikali kikatanda usoni mwake na ghafla akaporomoka chini,




Palepale Katarina aliyekuwa nyuma yake akamburuta mpaka katika kile kitanda chake akamnyanyua na kumlalisha kitandani pale akamfunika vizuri akamsogelea Zena na kumfungulia ile pingu mkononi kisha akaanza kumuamsha




Zena akafumbua macho!




"tuondoke" Katarina akamnongoneza palepale Zena akajiamsha cha ajabu alikuwa ni mzima kabisa akiwa na zile zile nguo za hosptali wakaufata mlango na kutoka...




Walikuwa tayari kwa kutoroka!




SIKU TANO NYUMA




OFISI YA DAKTARI MKUU




MUHIMBILI




Daktari Ebeneizar mwakashoro daktari mkuu wa hosptali ya muhimbili akiwa katulia ofisini kwake mara ghafla ikapigwa hodi mara moja,kabla hata ajaitika mlango ukafunguliwa akaingia mtu!




Alikuwa ni mnene kiumbo,ila si bonge akiwa kavaa nguo za kawaida,usoni alivaa kepu iloficha uso wake,pia alivaa shati la drafti drafti lenye mikono mirefu alilichomekea alivaa suruali nyeusi mkanda wa kawaida tu na chini alivaa viatu vyeusi ambavyo vilipakiwa rangi japo aikukukolea...




Mtu yule alikuwa na kitambi lakini akikuonekana sana pengine ni kutokana na unene alokuwa nao




"karibu mzee wangu!"




Daktar Ebeneizar akamkaribisha kwa ukarimu kama kawaida yake alikuwa ni daktari mkarimu, alojawa na huruma na hata mpole pia,akamwoneshea kwa ishara sehemu ya kukaa mtu yule akakaa pale pale akaitoa ile kofia ilokwepo kichwani kwake na kupelekea sura yake ionekane vizuri!




daktari akashtuka baada ya kumuona mtu yule ila akujali akaeleza kile kilicho mpeleka,




"mimi nadhani unanijua ni Rais Asamoye nimeamua kufanya ziara ya kushtukiza ofisini kwako nimefrah kukukuta na nimependa pia ulivyonipokea,nimekuja na shida moja nadhani kwa kuwa ipo ndani ya uwezo wako utansaidia,"




"sawa muheshimiwa shida gani?!"




"ni kwa ajili ya usalama wa taifa letu,kwanza iwe siri mimi kukutembelea hapa ndo maana nikaja kihasara hasara nisitambulike,na tutakacho ongea pia ni siri na ikiwa kitavuja nje sitokuwa na budi kukwangamiza kama adhabu narudia tena ni kwa sababu ya usalama wa taifa,hapa tupo wawili mimi na wewe sina mlinzi labda ni malaika na hatuna ushahidi wa macho kuwaona,kuna mgonjwa wangu mwanamke ni askari polisi anaitwa Zena Kaletwa jana,yupo chini ya ulinzi wa polisi wawili walovaa nguo za kiraia mwanamke mmoja na mwanaume mmoja sijui una habari yake?"




"hapana mkuu"




"basi chunguza kuhusu mtu huyo simamia matibabu yake,ila usijionyeshe kwa wale maaskari wasijue kama unafatilia matibabu yake hapa namaanisha kuwa karibu na daktari wake,pili hata akipona asiruhusiwe mpaka atakapotoroka au kuondoka mwenyewe asipewe ruhusa mtu huyo sawa?"




"sawa muheshimiwa raisi"




"naenda zingatia hili"




Muheshimiwa Rais akaondoka na kurejea kwenye gari la Daniel,Dani alimtuma mzee wake kwa kuwa yeye angeenda asingethaminika kama baba yake mh Rais Asamoye,




Akamjulisha kila kitu Katarina kwa njia ya 'sms'




Kwel Daktari akafanya kama alivyoagizwa akamtafuta daktari alosimamia matibabu ya Zena akampa maelezo, daktari akaelewa,siku mbili mbele Zena alishapona kabisa ila bado alijifanya mgonjwa daktari akazidi walalisha,




Don G maskin akawa ajui kinachoendelea,mpaka siku hiyo usiku alipoamka ili amuue,ila kumbe Katarina hakuwa amelala




Aliposhughudia akimnyonga mwanamke alijirusha toka kitandani kwake alipolala na kumtandika teke maeneo nyeti,teke alilojua litamuondosha fahamu mtu huyo,na kweli akafanikiwa akamuamsha Zena baada ya kumfungua pingu wakatoka nje na kuingia kwenye lift wakashuka mpaka chini,sasa wakawa wakielekea getini huku wakiwaza watapitaji na kuna walinzi hapo getini!,tena geti huwa linafungwa,usiku ule,tena usiku wa manane wangepitaje?!...




Hii Ikawa Ni Shida nyingine kwao.....






Katarina anafanikiwa kumzimisha Don G na kumtorosha Zena Ila Ishu inakuwa ni getini palipo na walinzi,je watapitaje?!..




twende pamoja mtunzi akujuze,




Katarina na mwenzake Zena walizidi kujongea eneo la getini walinzi walikwepo kwenye kajumba chao wamelala,




Walizidi kunyata na kulifikia geti,taratibu akafungua kageti kadogo,wakatoka na kukavuta kukarudishia kama kalivyokuwa,sasa wakaanza kuchepuka ilikuwa ni lazima wafike Mbezi eneo walilokuwa wakiishi usiku ule ule,ila kwa kuwa wote walishapitia jeshi awakujali kwa kutembea,ndo kwanza wakakaza mwendo...



ITAENDELEA


imulizi : Kufa Tu  Hakuna Namna (2)


Sehemu Ya Tatu (3)




**************




Asubuhi baada ya Don G kushtuka alishangaa kujikuta mwenyewe ndani ya wodi ile,palepale pasina kupoteza hata chembe ya nukta ya muda akashika simu yake na kumtwangia Madam kumjulisha hali ilivyokuwa,




Madam 'S' alikasirika, palepale ndipo alipopata picha kuwa yule 'Katarina' ambaye hapo awali walimchukulia kama askar wa kawaida walijidanganya sana,'kuna siri kubwa sana nyuma ya pazia na hiki kikundi ni kipana na kina watu hatari! na wa siri sana kamishna anahusika na ofisi yake




Akajiapiza lazima atajua kila kitu,




Apende asipende ,atake asitake...




Akashika simu na kumpigia mtu wake




"upo wapi saivi?!"




Akamuuliza Don




"nipo ndani ya gari naja hapo ofisini"




"fanya haraka kabla mambo hayajazidi kuwa mabaya"




Robo saa ilofatia ndani ya ofisi ya Madam 'S' kulikuwa na kikao cha watu wawili,




Madam 'S' na kibaraka wake Don 'G'




"tuna vita kubwa sana,mbaya tena ya hatari,na hatari yake inatokana kwamba tunapambana na watu tusiowajua wanajishughulisha na nin na kipi hasa lengo lao, ila mpaka sasa tuna nyenzo mbili makini za kuelewa kila kitu,nyenzo moja imetoweka tumebakia na nyenzo moja tu ambayo yapaswa tu 'deal' nayo kutwambia ukweli,tukishajua mpango huu una shikiliwa na kitu fulani basi ndo tuanze ku deal nacho,na kwa kawaida kama ilivyokuwa kwa Sara,mpaka tukamuua , Zena mpaka akaokolewa na hata kamishna pia najua hawezi fumbua mdomo wake aseme kweli,ivyo kwa mara nyingine itapaswa tumteke na kazi hii ya kumteka ntaifanya mimi mwenyewe wewe utanisubiria katika jumba letu la kutesea tayari nishaonana na dokta Angal kanipatia dawa,hii nikimchoma kwa kutumia sindano atasema kila kitu anachojua!'




Madam 'S' aliongea pasina kupepesa macho akimwonesha Don kichupa flani,alichokitoa kwenye begi lake na bomba la sindano!




Katu awakujua wala kuhisi,kuwa katika maeneo ya ikulu,uwanja uliopo eneo lile la ikulu ndani ya Gari Ya Daniel kulikuwa na watu wa tatu wakisikiliza kila kitu madam alichokuwa akiongea na kijana wake,yeye akijua ni siri,katu akujua vijana watatu walikuwa wakisikiliza kila kitu ndani ya gari ile,kupitia simu ya Daniel,mtoto wa Raid Asamoye




Na wakati huo muheshiwa Raisi ndani ya ikulu alikuwa akiongea kwa furaha tu na waziri mkuu wake,wakijadili jinsi ya kuliongoza taifa,na changamoto wanazokumbana nazo, Rais Asamoye akiwa ameificha chuki yake juu ya Jj Kwa muda wote,




"mh Rais kwa sasa umebakisha miaka miwili kumaliza miaka yako mitano na kunipisha hapa ikulu ila kuna changamoto ambazo nadhani uzijui zipo chini ya usalama wa taifa wakipeleleza na lengo lao ni kunichafua mimi na chama chetu kusudi uchaguzi ujao tukose ushindi,na hawa mi najua si wengine ni chama cha mapinduzi 'ccm' ndiyo wapo nyuma ya mpango wote huu wenyewe ndiyo wamempachika yule mwandishi anayetoa siri zangu " ZK" ,na kwa saivi chama kipo kwenye hatari kubwa sana tusipokuwa makini tutamegeka"




"yote uyaongeayo ni kweli ila yote yanatokana na tabia yako ya umalaya,kwa nini usitulie...




"Asamoye" Waziri akaita...




"nisikilize muheshimiwa waziri bado sijamaliza,wakati skendo ya kwanza ilipotokea ukausishwa na uhuzaji silaha tena ukitumia vijana wa usalama wa taifa nilikuomba ujiuzulu kujisafisha, ulinisikia?,si ulinitukana ukisema hapa mimi umenipachika na sina kauli kwako sasa ndugu waziri unaenda kuikosa hii nafasi!,kwel tena nakwambia,usipokuwa makini,hii miaka miwili yapaswa ujijenge utulie ufanye maendeleo kurudisha amani katika taifa lako,biashara za skendo skendo achana nazo kwa sasa,we unadhani hao usalama wa taifa unao watumia ki itikadi ni wote awana chama?i,ujawah kusikia kuhusu makomandoo wa vyama!,si tunao hata kwenye vyama vyetu tunawapeleka jeshi wanasimamiwa na chama wakifanya vizuri tunawapeleka nje kwendelea kusoma wakirudi wanafanyia kazi serikali wakiwa hawana vyama lakin wangapi tulikuwa tukiwatumia wakitupa siri za chama tawala kipindi kile?!,umewasahau kina Richard Mombi,huyu si usalama wa taifa toka kipindi chama cha mapinduzi kikiwa madarakani lakini alikuwa chini yetu,kipi kitafanya nisiingie ikulu?!"




"kaka nani kakudanganya jeshi linachama?"




"sijasema ivyo mimi ila nilichosema kwa saiv sisi ndo tupo madarakani,sisi ndo serikali, sisi tunaweza toa amri jeshi likafata kivipi tukose nchi kikubwa kwa sasa tulinde muungano wa vyama vyetu!"




"vizuri sana!" Asamoye ikabidi tu akubali huku akimcheka mwenziye alijua mbaya wake anatoka chama cha upinzani, ndiye anayemchafua kumbe mbaya wake ni yule alokuwa mbele yake!




SIASA!!!...




****




NDANI YA GARI




Baada ya watu wale wa tatu ambao ni Daniel mtoto wa Rais Asamoye,Komandoo Katarina na Koplo Zena kusikiliza ile sauti ilokuwa ikitoka kwenye simu ya Daniel,mwanajeshi na pia mtahalamu wa 'IT' akawaangalia wenzake...




"kama mlivyosikia, maisha ya kamishna bado yapo hatarini,bado anawindwa na saivi mwanamke,mama hatari anaingia mwenyewe mchezoni nani ataweza kumkabili?!"




Akawapachika maswali dada wale wawili,




Zena akakumbuka wakati aliporudi ofisini akamkuta yule mwanamama ndani,aliukumbuka uwepesi wake na hata shabaha alokuwa nayo,




"mimi Ninawazo...




Katarina akaongea,wote wakageuka kumtazama naye akaendelea




...ikiwa tutamuua madam tuta amsha vita ambayo itakuwa ni ngumu sisi kuizima,madam 's' kupitia usalama wa taifa ana vijana hatari zaidi ya elfu moja wote watahitaji kuingia kazini kujua chanzo cha kifo cha mkuu wao,Dani tutapona kweli?"




"hapana atutapona kwa kweli"




Zena akajibu akitingisha kichwa




"na tena ndo kwanza tutamweka Raisi matatizoni kuna uwezekano pia wa kuliweka taifa katika matatizo?,kipi kifanyike sasa?!




Kamishna ni mtu wetu ila kwa manufaa ya taifa,kwa ulinzi wa taifa letu tumfanye kama chambo kumnasa 'madam' ikiwezekana tumuingize kwenye kashfa hata atoke kwenye icho kiti,"




"kivipi?!"




Dani akahoji,Katarina akaachia tabasamu dogo akaendelea kuongea kwa sauti ndogo zaidi kama ananong'ona ila wote walimsikia




"kumzuia madam 'S' kumkamata kamishna tumeshaona ni ngumu,basi yatupasa sisi tumuwah kamishna kabla ajaingia mikononi mwa yule mama sisi tumuue"




Wote Zena na Dani wakatoa macho




"kumuua?! hakuna njia nyingine zaidi ya kuua?" Dani Akauliza huku sasa akionekana wazi akiogopa




"hapana!,hapana,hapana Dani hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo kamishna anapaswa *KUFA TU HAKUNA NAMNA*




"kufa tu hakuna namna?!" dani akauliza tena akiwa ametoa macho




"yapaswa *KUFA TU HAKUNA NAMNA*"




YALIYOKO NDANI YA SERIKALI TUYA ACHE TU TURIDHIKE NA UHURU NA AMANI TULONAYO!,KUNA MAKUBWA HUMO NDANI








Vijana watatu, vijana makini wanapitisha maamuzi ili kuendelea kuficha siri zao wanakubaliana kumuua kamishna,kabla ajatiwa mkononi na madam 'S' mwanamama katili mwenye uwezo wa mapigano,




Zena anafanikiwa kumuua sekunde chache kabla madam ajaingia na kesi ile inamdondokea madam S,




je nin kiliendelea?




Twende pamoja kuendelea kuburudika...




Kilikuwa ni chumba kidogo kilichotumika kwa ajili ya mahojiano,ndani ya chumba kile walikwepo watu wawili inspekta Nurdin aliyesimama pembeni ya meza ambayo juu ilibeba faili naye Nurdin Mkononi alikuwa kashika biki...




"ok,jane ilikuwaje mpaka kugundua mzee kauwawa na madam kukukaba?"






Inspekta Nurdin alimuuliza ndipo Jane alipoanza kujieleza




"asbuh ya leo kama kawaida niliwahi kazini nikafungua ofisi na kufanya usafi nikianza ofisini kwa mkuu,baada ya kumaliza nikakaa ofisini kwangu punde mkuu alifika akanisalimia na kuelekea ofisini kwake haukupita muda mrefu ndipo madam alipowasili akaitaji kuonana na mkuu nikampigia mkuu na kumwambia madam anahitaji kumuona akanruhusu...



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog