Search This Blog

Thursday, 29 December 2022

C.O.D.EX 4 (A MISSING SOLDIER) - 2

 

  Simulizi : C.o.d.ex 4 (A Missing Soldier)

Sehemu Ya Pili (2)



“Hamna shida, kwa leo nitaishia nje. Siku zingine nitakuja kula hadi ugali.” Alijibu Iris


“Haya baba. Kwa kheri eeh.” Timasi aliongea hayo na kuanza kuondoka lakini Idris alimuita tena na kumpa kadi yeke ya biashara ambayo inamawasiliano yake yote.


“Kwa lolote, usisite kuniambia.” Aliongea hayo wakati anampa kadi hiyo Timasi ammbaye aliipokea na kuanza kuelekea ndani kwake.


*****


“Lim, sasa ni nini kumfanyia vile Idris?” Timasi alimuuliza dada yake Limasi ambaye alikwishazowea kumuita Lim au dada. Maongezi hayo yalianza baada ya Idris kuondoka na Timasi kuingia ndani.


“Sina haja ya mapenzi. Majanaume mashenzi kama nini, Tim.” Aliongea Limasi huku anafungua kabati na kuanza kuweka mikoba yake aliyotoka nayo safari.


“Sasa kwani kakutongoza?” Akauliza Timasi.


“Sasa hadi uambiwe nakupenda au kupelekwa bichi na kununuliwa midoli ndio ujuwe hapa unatongozwa? Embu acha kuwa kama kipofu asiyesikia.” Alibwabwaja Limasi.


“Lakini mbona umepaniki ghafla sana?” Akaulizwa tena.


“Sitaki maswala ya mapenzi masikioni mwangu.”


“Ila unataka midomoni mwako. Uwe unawaungia watu eeh. Umekuwa kuwadi wewe?”


“Tim.” Akafoka huku anamuoneshea kidole dada yake. “Nakuomba sana tu! Mimi siyo kuwadi.” Ni wazi alikuwa na hasira Limasi.


“Basi ungetulia garini, sio kubwabwaja kama ndege wa asubuhi.” Timasi akaendelea kumpa somo lakini dada yake safari hii hakuwa akichangia lolote. “Halafu mbona ni HB tu! Kwa nini usimfikirie?” Akamaliza kwa maneno hayo huku anatoka nje na Limasi akageuka na kumuangalia kwa macho makali dada yake. Akaufuata mlango na kuufunga kwa kuubamiza huku msonyo mrefu ukifuatia.


“Kama Handosome, si umchukue wewe.” Akamaliza kwa maneno hayo na kuendelea kufanya mengine.


****


Muda wa saa nne usiku, ndani ya ukumbi mmoja wa starehe Jijini Arusha, Limasi na Timasi ambaye aliamua kwenda na dada yake katika ukumbi huo, walikuwa kwenye furaha kubwa ya kucheza muziki. Limasi licha ya usomi wake, lakini alikuwa ni mtu wa kupenda sana mambo ya starehe. Alimaliza tofauti zake na dada yake, kisha akamuomba usiku huo waweze kwenda katika ukumbi huo ambao ulikuwa maarufu sana pale Jijini Arusha kwa kutoa burudani.


Timasi akiwa kakaa kwenye kaunta anakunywa sprite ya kopo, alikuwa anamuangalia dada yake jinsi anavyocheza peke yake katikati ya ukumbi ule. Timasi akaamua kutoa pochi yake yenye simu na kuchukua kadi ya biashara aliyopewa na Iris, kisha akamtumia ujumbe ambapo wapo na dada yake. Iris akajibu kuwa anafika hapo muda si mrefu.


Limasi akiwa anakinyonga kiuno chake kwa ustadi mkubwa, akawafanya vijana na wazee wakware waanze kumtolea mate kwa tamaa eidha ya kucheza naye, au kufanya naye ngono. Limasi aliendelea kuyarudi mayenu huku akijipapasa kimahaba na kufanya watu wazidi kumtamani.


“Naweza cheza na wewe?” Sauti mwanana ilisikika masikioni mwa Limasi. Akamuangalia aliyemwambia hayo, uso wake ukatua kwa Iris aliyekuwa kavaa mavazi ya ukijana na kifua chake kipana kuonekana vema, lakini hilo halikumshawishi Limasi.


“Hapana. Huwa napenda hivi. Waweza kwenda kucheza na dada pale kaunta.” Akajibiwa hivyo Iris na Limasi, akasogea mbali naye akimuacha Iris aende kwa Timasi na kukaa kisha kuagiza kinywaji kimoja cha kileo.


“Achana naye huyo. Namjua sana katika wanaume. Si mrahisi kihivyo. Huwa hapatani na wanaume.” Akamtetea dada yake, Timasi.


“Hamna shida Timasi. Nimemuelewa.” Akajibu kilijari.


Baada ya kauli hizo za kufarijiana, walianza kuongea haya na yale kuhusu biashara na maisha mengine kwa ujumla huku wakiwa wamesahau kabisa kuhusu Limasi na mtindo wake wa kucheza kimahaba.


Wakiwa wamezama kimaongezi, mara kelele zinasikika ukumbini. Vijana wanakuwa kama wamepagawa ndani ya ukumbi. Walipotazama, walishuhudia Limasi akiwa kazunukwa na vijana wapatao kumi na wote walionekana wapo katika kulewa. Limasi alikuwa katika hali ya uoga na wale vijana ambao wengine walikuwa vifua wazi, walionekana wanataka kufanya naye jambo.


“Kaa hapahapa Timasi.” Akaongea Iris na kusimama tayari kwa kwenda pale alipo mrembo Limasi.






“Hamna shida Timasi. Nimemuelewa.” Akajibu kilijari.


Baada ya kauli hizo za kufarijiana, walianza kuongea haya na yale kuhusu biashara na maisha mengine kwa ujumla huku wakiwa wamesahau kabisa kuhusu Limasi na mtindo wake wa kucheza kimahaba.


Wakiwa wamezama kimaongezi, mara kelele zinasikika ukumbini. Vijana wanakuwa kama wamepagawa ndani ya ukumbi. Walipotazama, walishuhudia Limasi akiwa kazunukwa na vijana wapatao kumi na wote walionekana wapo katika kulewa. Limasi alikuwa katika hali ya uoga na wale vijana ambao wengine walikuwa vifua wazi, walionekana wanataka kufanya naye jambo.


“Kaa hapahapa Timasi.” Akaongea Iris na kusimama tayari kwa kwenda pale alipo mrembo Limasi.


ENDELEA.


“Hapana Iris, hao ni wakorofi wa Arusha. Usiende, watakuumiza bila sababu.” Alibwata kwa woga Timasi huku anajaribu kumvuta Iris asiende kwenye lile tukio.


“Kwa hiyo tuache dada yako anafanyiwe upuuzi?” Akauliza swali hilo ambalo lilimfanya Timasi amuachie mkono wake yule mwanaume aende kufanya alichokusudia.


Iris akaenda hadi katikati ya ukumbi ule ambapo Limasi alikuwa kazungukwa na vijana wa Kiarusha wengine wakiwa wamekamata chupa za vilevi vyao.



“Kila kitu kipo sawa vijana?” Iris akaongea kiuungwana ambapo wale vijana wa kiume waligeuka na kumuangalia aliyeongea hayo.


“Hayakuhusu braza. Kaa mbali na hii kitu.” Kijana mmoja mwembamba na mdogo kiumbo, akiwa kavalia kata mikono kama la wacheza kikapu, alibwatuka kwa lafudhi ya Kiarusha.


“Mnataka shilingi ngapi ili mumuache dada yangu.” Iris aliongea tena safari hii akiingiza mkono wake kwenye suruali yake ya kitambaa na kutoa kiasi kadhaa cha fedha na kuanza kuhesabu.


“Tunataka zote hizo, pamoja na huyu kuku tumbambie mpaka turidhike.” Kijana mwingine aliongea huku akipora kiasi kile cha fedha na kukifutika mbele ya sehemu zake za siri.


“Okay. Kwa upendo tu, chukueni hizo fedha na kumuacha huyo dada aendelee kucheza muziki peke yake.” Akashauri Iris.


“Unasemaje wewe bwege?” Kijana mwingine aliyekuwa kifua wazi na kakamata chupa kubwa ya mvinyo, alijitunisha huku anamfata Iris ambaye alitabasamu bila kupenda. “Hivi wewe unazijua charii za ara ama huzijui wewe.” Aliendelea yule kijana mwenye chupa ya mvinyo huku anazidi kutuna kila anapopiga hatua. Alivutia kwa kumuangalia na mwili wake mdogo lakini anajaribu kuutunisha.


“Dogo, bora ukalale kama umelewa na kuchoka.” Maneno yakamtoka Iris na bila kuuliza, yule kijana wa Arusha aliruka kwa haraka na kutaka kumpiga chupa ya kichwani Iris, lakini mwanaume yule alisogea pembeni kidogo tu, na kijana wa watu akapitiliza. Iris hakufanya makosa, akamsukuma kwa mguu kijana yule na kumfanya aende mbele kichwa kichwa na kwa kasi ya ajabu.


“Limasi. Toka hapo njoo huku kama hutaki kuchezewa na hawa madogo.” Iris aliongea lakini pale Limasi alipotaka kutoka katikati ya kundi la wahuni wa Arusha, akajikuta hapati njia ya kutokea na wakati huo, ukumbi mzima ulikuwa kimya na milango yote ikafungwa ili asitoke wala kuingia mtu. “Yoyote atakayejaribu kukugusa, namtengua mkono. Nadhani kila kijana kaelewa nachomaanisha.” Maneno hayo yakampa ujasiri Limasi na kuamua kuanza kutoka katikati ya kundi lile. Alipomfikia kijana mmoja, kijana yule akajaa mbele yake na kumzinga ili aispite. Iris akaenda hadi pale kijana alipozinga na kumshika bega kijana yule. “Muache apite.” Akaongea kwa utaratibu Iris.


“Huyu ni wetu braza. Huwa hatuogopi kitu sisi.” Aliongea kijana yule na kumshika mkono Limasi, lakini alichokutana nacho, nadhani hadi leo anakihadithia kwa wajukuu.


Iris alimtoa mkono wa yule kijana kwenye mwili wa Limasi, na kisha akaunyanyua juu kama refa wa ubondia akitangaza mshindi. Baada ya hapo, akamtwanga ngumi kali ya kwapa yule kijana. Alilia kwa sauti ya juu lakini haikumfanya Iris ashindwe kurudisha mkono wa kijana kwa kasi na kuuzungusha nyuma ya mgongo wake na kuubana vema.


“Nilikwambiaje dogo?” Akaulizwa kijana wa Arusha.


“Niache. Nasema niachee. Kaka ananiumiza huku.” Kijana yule alipiga ukelele mzito na sijui kaka yake alikuwa nani, lakini mara alitokea jamaa mmoja mrefu na mwenye mwili kiasi na kuruka teke la juu lililomkuta Iris kifuani na kumfannya amuachie yule dogo na kurudi nyuma kidogo.


Idris akakaa sawa na kumtazama yule kaka mtu ambaye alikuwa kavaa kapero na mdomoni mwake akiwa anatafuna bazuka.


“Kaeni mbali madogo. Muone nachomfanya huyu bwege.” Aliongea yule aliyeitwa kaka na wale vijana walisogea pembeni huku wakinong’onezana maneno ya kumsifu kaka mtu kuwa anapiga ngumi kama Donnie Yen.


Macho ya Iris yakawa makini zaidi kwa Donnie Yen wa Arusha ambaye naye bila uoga, alifyatuka kama risasi na kuruka teke la juu ambalo Iris alilikwepa lakini kijana yule ni kama alijua kuwa litakwepeka teke lake, akawa karusha ngumi ya haraka ambayo ilimkuta Iris kwenye shavu la kulia. Donnie Yen akatua chini kwa sarakasi ndogo lakini haikuwa kama alivyofikiria, Iris alikuwa amekwishafika nyuma yake na akamnyanyua jamaa yule kwa roba kali. Jamaa akawa ananing’inia juu kwa roba ya mkono mmoja. Lakini katika hali ya kushangaza, yule dogo mwenye chupa ya mvinyo alitokea kwa nyuma yake na kumtwanga Iris chupa ile ya mvinyo hadi ikapasuka.


Iris akamuacha Donnie Yen na kumtazama aliyemtwanga na chupa. Akamuona dogo yule na kipande cha chupa ambacho alitaka kukitumia kama silaha. Iris akamuwahi na kumshika mkono wenye chupa kisha akauminya hadi dogo akaiachia chupa ile, kisha akampa kofi zito lililomfanya apige kelele kama kafiwa.


Kelele hiyo ikawafanya wale vijana wengine wasogee na kuanza kufanya vurugu lakini Iris aliweza kuwamudu kwa kuwakamata na kuwatengua mikono yao. Ilikuwa ni kimuhe muhe ndani ya ukumbi ule wa starehe. Aliyejaribu kumpiga ngwara, Iris alimkanyaga hukohuko chini na kusababisha maumivu makali katika miili yao.


Dakika tano zilitosha kwa Iris kuwafanya wale vijana wawe wamekamata mikono yao kwa maumivu makali sana. Akamuendea yule kijana aliyechukua pesa zake na kuzitoa kule alipoziweka.


“Nilikwambia, chukua na ondoka, ukajifanya unajua. Sasa umekosa vyote.” Akamaliza kwa kumtisha kama anampiga ngumi ya uso, kijana yule akaziba uso na Iris hakupiga usoni bali kwenye mkono alioutengua. Kilio kikamzidi kijana aliyechukua hela.


Akamfata Donnie Yen ambaye alikuwa kakamata shingo yake na anagugumia kwa maumivu makali ya roba mbaya ya kijeshi.


“Wafundishe vijana wako tabia njema badala ya huu upuuzi.” Akamaliza kwa kumpiga kofi zito Donie Yen. Akasimama na kuanza kuondoka eneo lile akiacha ukumbi mzima unampigia makofi.


“Kapiga wababe wa Arusha leo.” Sauti za baadhi ya watu zilisikika lakini Iris hakuzifatilia na badala yake akaenda hadi kwa Limasi.


“Upo salama Limasi?” Akamuuliza, na mwanadada yule badala ya kujibu, alimkumbatia Iris.


“Nipo salama Iris.” Akajibu kwa sauti ya chini na wakati huo, Timasi alisogea hadi eneo la tukio na kuwataka waondoke haraka kabla ukumbi hujajaa wahuni wengine.


Safari ya watatu wale iligotea nyumbani kwa Idris ambapo Timasi na Limasi walianza kuongea haya na yale hasa kuhusu vurugu ambazo zilitokea kwenye ukumbi. Maongezi yalikuwa ya huruma na saa nyingine ya kufurahisha hasa kwa sababu hakuna aliyedhurika sana.


“Idris, niliona yule dogo alikupiga kwa chupa, vipi kakupa jeraha?” Akauliza Timasi huku anaenda pale alipokuwepo Idris na kutaka kumtazama kama alipatwa na jeraha lolote lakini Idris alikataa sana kuonesha sehemu ambapo alipigwa kwa chupa kwa sababu palishajirudisha katika hali yake muda mrefu sana.


“Hapana Timasi, nipo salama tu! Kuwa na amani.” Idris aliongea hayo kwa haraka huku anaelekea lilipo jokofu la vinywaji na kutoa kinywaji chake. “Mtatumia vinywaji gani jamani?” Akauliza Idris.


“Hatuna hata hamu ya vinywaji, tunaomba kwanza twende nyumbani tu! Siku nyingine tutakuja kukutembelea.” Akajibu Timasi.




“Basi hamna shida. Na ni tayari usiku sana. Ngoja niwapeleke.”


“Sawa Idris.” Majibu hayo yakawafanya vijana wale watoke ndani ya jengo mwanana na la kifahari la Idris na kwenda kwenye gari ambalo liliwapeleka nyumbani wanapoishi Timasi na Limasi.


“Usiku mwema Idris.” Akaaga Timasi huku anashuka ndani ya gari la Idris huku akimuacha dada yake akiwa bado kakaa ndani, sehemu ya mbele ya gari lile.


“Nawe pia Timasi.” Akajibu Idris na Timasi akawaacha wawili ndani ya gari.


“Idris…” Akaita kwa kusua kidogo Limasi lakini aliendelea na kilichombakiza ndani ya gari la Idris. “Kwanza naomba unisa….” Kabla hajasema maneno hayo, Idris alimuwahi na kumuwekea mkono wake mdomoni akikamkataza asiseme neno alilokusudia.


Limasi akamuangalia Idris kwa macho ya aibu na wakati huo taratibu Idris alitoa mkono wake na kisha kwa pamoja wakabaki wanaangaliana kwa macho fulani ambayo yalielezea ni nini kinachotaka kutokea.


Taratibu Iris alianza kusogeza kichwa chake kwenye kichwa cha Limasi. Limasi bado alikuwa hajafanya maamuzi sahihi ya kwamba naye asogee au abaki palepale. Mawazo hayo ndiyo yaliyomfaya ajikute kaganda hapohapo hadi kichwa cha Iris kikamfikia na kujikuta analambwa midomo yake na ulimi wa Iris. Hapo ndipo alishtuka na kutoka kwenye mawazo yake ya nini afanye na kisha akatanua midomo yake mitamu hata kwa kuiangalia, na kuruhusu ulimi wa Iris uzame ndani zaidi ya midomo yake. Wakajikuta wameingia kwenye dunia nyingine tofauti sana. Dunia ambayo iliwasisimua kuanzia nywele hadi kucha, visogo hadi visigino.


Ndimi zao ziliendelea kubadilishana nafasi kwenye vinywa vyao na wakati huo Iris alikuwa akijaribu kupapasa pia mapaja ya moto ya mwanadada Limasi. Limasi pia hakuwa nyuma, alikuwa akiingiza vidole vyake kwenye masikio ya Iris na kufanya tendo lile liende kwa utamu wa kipekee. Hadi dakika tatu zinatimia, ndipo waliamua kuachana kugandana midomo yao na kubaki wakiangaliana.


“We’ ni mtamu sana.” Ikabidi Iris ndiye atoe ukimya uliotawala kwa sekunde kadhaa na maneno hayo yalimfanya Limasi aone aibu na kutazama pembeni.


“Id, naomba niende kwanza nyumbani maana hapa naweza kuondoka na wewe nisipoangalia.” Akaongea Limasi akiwa bado na aibu.


“Kwani mimi kuondoka na wewe ni tatizo, Lim?” Naye Idris alifupisha jina la Limasi kama Limasi naye alivyofupisha lake kwa kumuita Id.


“Hapana. Ila kwa leo naweza kugombana na Dada kwa kuondoka wakati tulishafika hadi nyumbani.” Maneno hayo hayakuwa sahihi kwenye kichwa cha Idris, lakini mwanaume yule alielewa kuwa kwa mila za Kitanzania, hamna msichana ambaye huweza kukubali kirahisi siku hiyohiyo akalale na mwanaume, labda iwe biashara yake. Ila unaweza kulala naye au kushinda naye ndani, baada ya siku moja.


“Sawa Lim.” Akakubali Idris. “Kwa hiyo nikufuate lini uje ukae kwangu siku nzima.” Akatupa kete nyingine muhimu.


“Nitakupa taarifa kwenye simu, siwezi kukujibu hapa.” Limasi akaivunja ile kete iliyotupwa na Idris kwa jibu hilo.


“Sawa. Nasubiri mlio wako wa simu.” Idris akakubali huku anampatia kadi yake ya biashara Limasi ambaye aliipokea na kabla hajatoka garini, Idris alimvuta tena na kumuingizia tena ulimi wake kinywani. Wakabadilishana tena ndimi zao na ndipo Limasi aliposhuka garini na kwenda ndani ya nyumba anayoishi.






“Sawa Lim.” Akakubali Idris. “Kwa hiyo nikufuate lini uje ukae kwangu siku nzima.” Akatupa kete nyingine muhimu.


“Nitakupa taarifa kwenye simu, siwezi kukujibu hapa.” Limasi akaivunja ile kete iliyotupwa na Idris kwa jibu hilo.


“Sawa. Nasubiri mlio wako wa simu.” Idris akakubali huku anampatia kadi yake ya biashara Limasi ambaye aliipokea na kabla hajatoka garini, Idris alimvuta tena na kumuingizia tena ulimi wake kinywani. Wakabadilishana tena ndimi zao na ndipo Limasi aliposhuka garini na kwenda ndani ya nyuba anayoishi.


ENDELEA.


Akiwa na dada yake, Limasi alikuwa haamini kama aliweza kuingia mkenge kirahisi namna ile na kujikuta anachukua busu laini na nyevu la Idris.


“Yaani Tim mimi hata sijui nilikuwaje. Akili yote ilinihama.” Akawa anamuhadithia dada yake huku yupo kitandani kakamata mto wake na Timasi alikuwa akimtazama huku tabasamu hafifu likiupamba uso wake. “Nilikuwa napata msisimko wa ajabu ambao hadi sasa kama siiuelewi vile. Sijui kanipa nini yule mwanaume.” Maneno hayo yakamfanya Timasi naye akae kwenye kitanda cha Limasi na kuzishika nywele za dada yake kwa kuzilaza kwa nyuma.




“Lim. Hayo ndio mapenzi. Ndivyo yalivyo. Uhamisha akili na hupoteza kabisa kujiamini. Na saa nyingine, hata ngvu za mwili. Damu yote hujaa msisimko, unaopoteza nguvu kilaini. Kwa hiyo, usijali sana, ndivyo yalivyo na nafurahi kwa wewe kuingia huko tena. Naimani Idris ni mtu sahihi kwako.” Limasi alimuangalia dada yake kwa macho ya huruma, au tuseme macho ya kudeka.


“Dada naogopa kuumia mimi. Tayari waliniumiza hawa watu, na huyu akiniumiza mimi nitaishi kweli?” Safari hii aliongea huku akitamani kutoa machozi.


“Idris, ndilo chaguo sahihi. Wale wengine kumbuka niliwahi kukuonya. Ila huyu, nakuhakikishia, upo sehemu sahihi na utafurahia mapenzi.” Akajibiwa Limasi.


“Kaniomba niende kwake. Sijui niende lini.”Akachomekea na suala la kwenda kwa Idris.


“Sema anakuja keshokutwa. Ndio anatoka huko Afrika Kusini. Akija na ukasalimiana naye, unaweza kwenda hata mwezi mzima.” Timasi akamuelezea kuhusu kuja kwa mume wake ambaye yupo Afrika Kusini. Na maneno hayo yakampa faraja Limasi kwani alianza kujihisi hali ya kumpenda Idris kwa siku hiyohiyo moja. Hapo ndipo ule usemi wa mapenzi ni kama magugu maji, unapanda asubuhi, saa sita unakuta yametapakaa kiwanja kizima. Unatimia.


“Mwezi nzima. Sasa si bora nihamie.” Akaongea huku anacheka Limasi ambaye kwa muda mfupi tu! Ule ukanjanja wake ulipotea na alikuwa msichana mwenye hekima.


“Kuwa huru Lim. Wala usiogope, Namuamini sana Idris, yaani namuamini kuliko wale wengine. Jitahidi kumtunza awe wako pekee.” Akaongeza maneno mengine ambayo yalikuwa kama msumali wa mwisho kwenye kugongelea hisia za mapenzi kwenye moyo wa Limasi.


Hadithi ikawa hiyohiyo usiku huo hadi wakapitiwa na usingizi wakiwa hapohapo kwenye kitanda cha Limasi.


*****


HUKO Marekani, hali ilizidi kuwawia ugumu baada ya kutompata Idris Iris ambaye alikuwa Tanzania. Walipeleleza kila mahali lakini hawakupata jibu la alipokuwepo Idris. Waliweza kuchukua kamera za barabarani pamoja na za uwanja wa ndege ambao Iris alikwenda, lakini hamna walichoshuhudia. Waliangalia hadi pass za wasafiri wa wiki nzima ndani ya Marekani, lakini hawakumuona Idris wala jina ambalo walihisi ndilo analotumia.


“Mmefikia wapi Ally?” Alifoka kwenye simu Uzo baada ya mkuu wa CIA kupokea simu yake.


“Hamna kitu Uzo. Naomba unipe muda wa kuendelea kumtazama. Na pia kama unavideo za Dokta Ice, naomba uzilete hapa ili tuchunguze mambo kadhaa.” Akaongea Ally.


“Video zipo hadi za siku yake ya kufa. Hilo halina tatizo. Baada ya nusu saa, zitakuja hapo kwa ndege maalumu.” Maneno hayo yalienda sambamba na Uzo kukata simu na kumfanya Ally atoke ofisini kwake na kwenda kusimama kwenye kioo kikubwa ambacho kiliungwa kwenye kompyuta na kuonesha nchi nzima ya Marekani. Wafanyakazi wengi walikuwa wanaendelea kucharaza kompyuta zao, yote ni katika utendaji wao wa kazi.


Wakati hayo yanaendelea kujiri ndani ya Jiji la New York huko Marekani, ndani ya Jiji la Arusha, Tanzania, Idris alikuwa anapapasa kiuno hadhimu cha mwanadada Limasi ambaye alikuwa bado kalala na kajifunika shuka jeupe lililotandikwa kwenye kitanda cha Idris. Usiku mmoja uliopita, ni kelele na lugha za mapenzi ndizo zilizuka kwenye nyumba kubwa ya Idris. Idris aliendelea kuchezea kiuno cha Limasi ambacho kilikuwa kimefunikwa kwa shuka.


“Bwana niache nilalee.” Sauti ya puani ilimtoka Limasi baada ya kuona kashikashi za Idris zinazidi kwenye kiuno chake.


“Kwani nimekukataza jamani.” Naye Idris akajibu.


“Sasa ndio nini hivyo?” Akaendelea kuuliza kwa sauti yake ya puani.


“Basi tu, napenda hivi.” Akajibu tena Idris.


“Je nikifanya hivi.” Limasi akakatika kwa minato na kuzidi kumfanya Idris ahisi yupo dunia nyingine ya kisasa kuliko ile ya sasa hivi ambayo maisha magumu kuliko chuma.


“Ndio maana napapasa hapo kwa sababu jana mambo yaliyokuwa yanatokea, sikuyaelewa kabisa ni kwa sababu gani. Ni hichi ndio kilikuwa kinahusika?” Akafunguka yake Idris.


“Unaonaje kwani?” Safari hii Limasi alinyanyuka kabisa na kufunua shuka walilokuwa wamejifunika. Miili yao ambayo ilikuwa inangozi pekee, ikaonekana na macho yao kwa pamoja walikuwa wanaona jinsi ngozi zao zilivyobarikiwa.


“We’ ni mzuri Lim.” Maneno hayo yakamfanya Limasi asogee kwa Idris na kumlaza kifudifudi, kisha akampandia kwa juu kama farasi na kusogeza kinywa chake hadi kwenye kinywa cha Idris. Tendo la kuchukuliana mate, likapamba moto.


“Id, nimekuheshimu hadi hapa nipo katika kifua chako. Sipo hivi, ila unastahili zawadi hii. Lakini sijui mimi nastahili zawadi gani toka kwako.” Akaongea baada ya kunyonyana ndimi kwa dakika kadhaa huku bado akiwa kamdandia kama farasi.


“Huna unachostahili zaidi ya hicho kidoleni.” Maneno yalimtoka Idris na kumfanya Limasi atazame kwenye kidole chake. Hapo alikutana na pete ndogo lakini imenakwishiwa na jiwe la almasi inayopendeza sana.


“Id?” Akauliza huku katanua midomo yake. “Hii umeweka saa ngapi.” Bado alikuwa haamini. “Na kwa nini……” Akashindwa kumaliza kauli yake baada ya Idris kumvuta kwake na kuanza kunywa kinywaji cha mapenzi. Na mwisho wa yote, walijikuta wakilia kilio cha utamu, utamu ambao uliwafanya waahidiane mambo kibao ambayo sidhani kama wangekuwa hawapo katika dunia hiyo, wangepeana kizembe hivyo.


****


Baada ya mwezi mmoja. Si CIA, FBI wala C.O.D.EX waliokuwa wanataarifa za mwanajeshi aliyepotea (A missing Soldier). Wote walishindwa kutambua ni wapi alipokuwepo Idris Iris. Walichoka na kushindwa kabisa kuendelea kumtafuta mwanaume yule ambaye kwa wakati huo, alikuwa amefanya harusi kubwa sana na kumuoa rasmi Limasi.


Harusi ilikuwa kubwa sana Jijini Arusha. Kila ambaye aliweza kuhudhuria, alikubali harusi ile licha ya upande wa Idris kuwakilishwa na watu wachache sana akiwepo dereva wake pamoja na marafiki wa dereva huyo ambao walisimama kama ndugu wa Idris.


Kwa upande wa Limasi, alikuwa ni mwenye furaha kila mara. Familia za wazazi wake, zilifika katika harusi ile. Na ndugu wa mume wa Timasi nao walifika kunogesha harusi ile iliyokuwa babu kubwa jijini.


“Kwanza napenda kumshukuru MUNGU kwa kunipa pumzi leo, hadi nimesimama hapa kwenu. Bila yeye, mimi si kitu,” Sauti ya Limasi ilipaa baada ya kupewa wasaha wa kuongea. “Pili nimshukuru dada yangu Timasi, yeye ndiye kila kitu kwangu hasa baada ya wazazi wetu kuondoka duniani. Yeye na mumewe, wamekuwa bega kwa bega hadi nikafika hapa leo. Mume wangu Idris, umekuja kuwa wa muhimu sana kwangu. Nakuahidi nitakuheshimu na kukutunza daima. Hilo ndilo kubwa. Wazazi wangu popote walipo, juweni kuwa nawapenda sana na nimewakumbuka sana.” Kimya kikatawala wakati wa maneno hayo machache. “Pia ndugu wa baba na mama na wageni wote mliofika, sina cha kuwapa zaidi ya upendo wangu kwenu. Nawapenda sana jamani.” Watu wote ndani ya ukumbi wakanyanyuka na kupiga makofi kwa maneno hayo machache aliyoyaongea Limasi.




Upande wa mwanaume, pia Idris aliongea na kuhadithia historia ya uongo kuhusu wazazi wake. Wapo walioguswa na wapo waliosikitika sana na kuamua kumpa pole. Hivyo ndivyo harusi ya Idris na Limasi ilivyochukua nafasi katika Jiji la Arusha na wakati huo, mashirika ya kipelelezi na kijasusi, yakiwa yanamtafuta kwa udi na uvumba.


****


“Uzo, umeona hii video?” Ally Ahmed Ally, Mkuu wa CIA, alikuwa anacheza video ambayo ilikuwa inaonesha jinsi Uzo alivyokuwa anamlazimisha Dokta Ice ataje mambo aliyoyafanya. Video hiyo ndio ilionesha kifo cha Dokta Ice pia.


Walikuwa wamekutana kwa mara nyingine ili kupata muelekeo sahihi wa kumsaka Idris na siku hiyo, Ally alikuwa ana ahueni juu ya majibu ya kile wanachokitafuta.


“Hiyo video, mimi nilikuwepo, halafu unaniuliza kama nimeiona tena? We’ vipi bwana?” Alibwata Uzo.


“Yawezekana ukaigiza filamu lakini ukuwahi kuiangalia, ndio maana nimekuuliza.” Akaongea Ally.


“Nenda kwenye mada husika Ally.” Waziri wa Ulinzi ambaye alikuwepo wakati anatoa majukumu ya kumsaka Idris, aliongea na kumfanya Ally asimame na kwenda pale kwenye video.


“Sikilezeni hapa kwa makini alichokiongea Dokta Ice.” Akacheza video ile baada ya kuongea maneno hayo.


“Unajidanganya. Mimi ndiye alpha na omega kwenye kutengeneza hiyo kemikali na kuifanya iwe bora zaidi. Nilioshirikiana nao, wote mliwaua. Bado mimi ni jiwe la pembeni.” Maneno hayo ya kwanza yakasikika toka kwenye video, Wote waliokuwepo kwenye mkutano wakawa kimya zaidi.


“Una uhakika Ice?” Swali la Uzo pia likasika


“Unauliza maembe Tanzania mwezi wa kumi mbili?” Jibu hilo likamfanya Bastian, Mkuu wa FBI kurudisha mgongo wake kwenye kiti.


“Inaonekana unapajua sana Tanzania. Hamna kitu wale, tukiamua kuiangamiza ni dakika tano tu.” Ally hakutaka kuendelea kucheza video ile hadi mwisho bali kuirudisha tena nyuma hadi kwenye maneno aliyoona ni picha ya kuanzia kwenye upelelezi wake.


“Unauliza maembe Tanzania mwezi wa kumi mbili?” Akacheza sehemu hiyo kama mara saba kwa kuirudisha rudisha nyuma. Waliokuwepo kwenye kikao wote wakawa wameelewa anachomaanisha Ally.


“Unataka kusema Soldier yupo Tanzania?” Akauliza Uzo na wakati huohuo, Ally alirudi kwenye kiti chake na kukaa kabla hajajibu.


“Hapana. Nachotaka kukwambia, hivi sasa kaoa pia, huko Tanzania. Na hamna mpango wa yeye kurudi huku.” Akajibu Ally.


“Kwa hiyo unaushauri nini Ally?” Akauliza Waziri wa Ulinzi.


“Tanzania ni marafiki zetu sana. Na hawana uwezo wowote wa kutupiga wala kutengeneza silaha kama ile. Kwa nini tusimuache tu?”


“Yule ni zao letu bwana.” Akawaka Uzo. “Tukimuacha halafu akitoka kwenda nchi nyingine je?” Akazidi kupayuka.


“Kwa hiyo tufanyaje Uzo?” Akauliza Bastian, mkuu wa FBI.


“Tukachukue kilicho chetu.” Akajibu kifupi.


“Kwa sasa anauraia wa Tanzania. Anajulikana ni Mtanzania aliyeishi Marekani. Ni ngumu kumrudisha.” Akatiririka Ally.


“Wapelelezi wa kule wanasemaje kuhusu huyu mwanajeshi wetu?” Akauliza Waziri wa Ulinzi.


“Niliongea na Shirika la Siri la Kipelelezi la kule, wakaniambia wao hawawezi kumkamata mtu wa aina ile kabla ya kupata ruhusa toka kwa Rais wao. Tuliwatumia na video za jinsi mwanajeshi yule anavyofanya kazi. Wakasema watamuangalia asifanye ujinga wowote na yaonekana anatabia njema tu.” Akajibu Ally.


“Hamna tabia njema, yule arudishwe tu huku.” Akabwabwaja tena Uzo.


“Walipoongea na Rais, wakaambiwa kuwa jamaa anatakiwa arudishwe Marekani, kweli. Lakini hawataki waajeshi wetu waende kule kumkamata, wakasema watamkamata wenyewe.” Akaongeza Ally.


“Wataweza. Kuna mtu anaweza kumkamata yule Tanzania?” Akauliza Bastian kwa mshangao.


“Ndio. Rais wao alisema anamtu wake anamuamini sana katika hilo.” Akajibu Ally.


“Mh! Ni nani huyo?” Waziri wa Ulinzi akakaa kitako kusikia mtu ambaye hadi Rais wa nchi anamuamini.


“Wanamuita ‘The Undercover Agent’ au Agent Zero.” Akajibu Ally na kuendelea. “Wanasema huyo ndiye tegemeo la nchi ya Tanzania…” Hakumaliza, Waziri wa Ulinzi akamsitisha maelezo yake.


“Basi, namjua huyo. Hamna kitakachoshindikana.” Waziri akaongea.






“Wataweza. Kuna mtu anaweza kumkamata yule Tanzania?” Akauliza Bastian kwa mshangao.


“Ndio. Rais wao alisema anamtu wake anamuamini sana katika hilo.” Akajibu Ally.


“Mh! Ni nani huyo?” Waziri wa Ulinzi akakaa kitako kusikia mtu ambaye hadi Rais wa nchi anamuamini.


“Wanamuita ‘The Undercover Agent’ au Agent Zero.” Akajibu Ally na kuendelea. “Wanasema huyo ndiye tegemeo la nchi ya Tanzania…” Hakumaliza, Waziri wa Ulinzi akamsitisha maelezo yake.


“Basi, namjua huyo. Hamna kitakachoshindikana.” Waziri akaongea.


ENDELEA.


IKULU, TANZANIA.


Kijana mwenye mwili mdogo lakini uliyokaa kimazoezi, alikuwepo ndani ya chumba cha mazoezi kwenye Ikulu tukufu ya Tanzania. Alinyanyua vyuma vidogo na vikubwa kwa nyakati tofauti na aliweza kwenda kwenye mashine ya kutafutia pumzi ambayo alikuwa anakimbia juu yake. Jasho lililowanisha fulana yake ya mikono mirefu na rangi ya kijivu lakini hakuonekana kukoma kufanya mazoezi hayo licha ya kuchoka kwake hata kwa kumuangalia.


Alipomaliza mazoezi hayo ya pumzi pamoja na kunyanyua vyuma, alienda kwenye ‘punching bag’ na kuanza kulipiga ngumi pamoja na mateke makali ambayo yalikuwa yanaenda kwa mitindo mbalimbali anayoijua yeye ni wapi alijifunzia.


“Agent.” Ndilo jina ambalo mwanadada wa Ikulu alimuita. Naye bwana yule mfanya mazoezi aliacha kulitwanga lile dubwasha na kumfuata yule kimwana.


“Ndio mrembo.” Akanguruma huku anamtazama yule mwanadada ambaye si haba pia ukimuita mrembo.


“Rais anataka kukutana na wewe.” Akampa ujumbe wake huku bado kasimama mbele ya Agent.


“Wewe hutaki kukutana na mimi?” Agent akamuuliza huku tabasamu lake la kichokozi likipamba uso wake. Yule mwanadada akatazama eneo moja la pembeni na lililojuu ya paa ya Ikulu ile. Naye Agent akatabasamu bila kuangalia eneo lile ambalo lilikuwa nyuma yake. “Huwa sifanyi mazoezi yangu huku kamera zinanitazama. Hiyo kamera nimeshaizima zamani sana. Hapo waliokuwa wananitazama, wanaona napiga ‘push up’ bila kuchoka. Kwa hiyo ondoa shaka mrembo.” Akaongeza Agent safari hii akishika kidevu cha yule mwanadada.


“Bwana wewe, siyo hivyo, mi nimeolewa.” Dada yule aliongea kwa sauti ya chini na ya kuogopa kidogo.


“Sawa, kwani kuolewa kunakataza mimi nisikushike kidevu au kuku…” Agent aliongea hayo huku anasogeza midomo yake na kugusanisha na midomo ya mwanadada yule ambaye naye bila aibu, alianza kutanua midomo yake mwanana kama pipi.


“Agent.” Sauti kali ilisikika kabla hawajafanya kitendo kile cha aibu kwa Mwafrika. Agent akaangalia alipoitwa na wakati huo mwanadada mrembo alipatwa na mshtuko na kuondoka haraka eneo lile. “Wanawake utawaacha lini wewe?” Akauliza tena bwana aliyemuita. Agent akawa anakuna nywele zake za kisogoni bila kujibu lolote.


“Nasikia umeniita mkuu.” Akajitutumua kujibu asichoambiwa.


“Ndiyo. Na nimemtuma huyu mwanadada aje akuite lakini naona ulianza kutumbua mali zisizo zako. Acha ujinga huo Agent, ni wake za watu hawa na wanajiheshimu. Uwe unajiheshimu hata mara moja moja. Siyo kwa kuwa wadhaifu kwa mwili kama wako, basi ndio uwatese kwa tabia zako.” Rais wa Tanzania alionesha wazi kukasirishwa na tabia za Agent.


“Bahati mbaya mkuu.” Alijitetea Agent.


“Nyamaza.” Lakini alikatishwa na sauti kali ya Rais na kumfanya Agent yule anywee kama mchicha ndani ya sufuria lenye maji ya moto. “Twende huku.” Akaongeza Rais akimtaka waongozane hadi ofisini kwake.


“Sijaoga bado.” Akaongea Agent huku anaangalia kilipo chumba cha kujisafi.


“Kwa hiyo ulikuwa unataka uogeshwe na huyu mwanamke?” Akamjibu Rais na Agent hakuwa na jinsi zaidi ya kwenda pale mlangoni aliposimama Rais wake. Akamuona yule mwanadada aliyetaka kumbusu busu nyevu akiwa ndani ya aibu nzito. Akashusha pumzi ya nguvu. “Ni sekretali wangu. Muheshimu kama dada yako au mama yako mdogo, kama unataka, kachukue wapishi huko nje. Huyu sitaki hata umguse.” Akaongeza Rais huku anamtazama Agent.


“Kwa nini sasa Mkuu.” Agent aliongea huku akiwa anataka kucheka kwa sababu ya mkwara wa Rais wake ambao ulionekana kama unambania kuwa na yule mwanadada.


“Kaolewa na mtoto wa kaka yangu. Na hii kazi kaombewa na kaka yangu. Na pia, akiwa na mahusiano na jitu kama wewe, atatoa baadhi ya siri ambazo hupaswi kuzitambua. Umenielewa?” Akajibu Rais na kumfanya Agent anywee hasa kwa ule uhusiano wa Rais na yule mwanadada.


“Samahani dada eeh.” Agent alimuomba msamaha bila kuficha.


“Hilo ndilo la msingi. Sasa nisikie tena hata umemuita lodge zenu za shilingi elfu kumi na tano.” Akaongea tena Rais huku anaingia kwenye ofisi yake.


Agent wakati naye anaingia ofisini, akamtazama tena yule mwanadada, wakakutanisha macho yao na Agent akamkonyeza na kumfanya mwanadada yule atabasamu na kuendelea kucharaza kiparaza cha kompyuta yake.


*****


“Nimekuita hapa kwa jambo moja Agent.” Rais alianza kuongea mbele ya kijana aliyemuita ofisini kwake na wakati huo, ofisi nzima ilikuwa imefungwa na baadhi ya mitambo ya kutotoa sauti nje ilifunguliwa ili kile kinachoongelewa kiwe siri ya wawili tu.


“Ndio mkuu wangu.” Akakaa kitako tayari kwa kumsikiliza mkuu wa Nchi yake.


“Kuna mwanajeshi mpotevu, wao wanamuita ‘a missing soldier’. Lakini wamempatia Tanzania na anaonekana anakula raha zake huko Arusha.” Akaanza maelezo hayo na Agent alionekana akiwa makini kumsikiliza.


“Ni mwanajeshi wa wapi na kwa nini usitume wanajeshi wakamkamata?” Akauliza Agent kabla ya kumuacha Rais kuendelea.



“Ni Mmarekani, na kuhusu swali la pili, ndio nilikuwa nakuja huko.” Akajibu kifupi Rais na kuendelea. “Kwanza kabisa, ni mwanajeshi ambaye aliwahi kufa. Na baada ya kufa, ndipo Dokta mmoja ambaye naye ni marehemu, aliweza kumfufua kwa kumuingizia kemikali za C.O.D.EX.” Akakatishwa maelezo yake na Agent.


“Hizo kemikali si ndizo zile zilifungiwa miaka kumi iliyopita kwa sababu ya kuwaathiri sana Alex na Alex Junior ambao walikuwa wanajeshi tishio sana duniani.” Akaongea Agent.


“Wewe hayo umeyajuaje wakati yalikuwa ni ya siri kubwa?” Akauliza Rais.


“Kuna vitabu, kaviandika Tariq Haji na kaviita C.O.D.EX, vipo vitatu. Vinaelezea kinagha ubagha yote hayo. Ni kama riwaya, lakini nilipofuatilia, haya mambo ni kweli yalitokea.” Akajibu Agent.


“Okay. Ni kweli ulichoongea. Lakini CIA na FBI pamoja na serikali nzima ya Marekani, walifungua tena ile maabara na safari hii walikuwa wanachukua watu waliokwisha kufa hasa wanajeshi wa Kimarekani ambao walifia vitani au wananchi wenye IQ kubwa ili wawasaidie katika kutengeneza silaha.”


“Kwa hiyo huyo mwanajeshi yupo vipi?” Rais akavuta bahasha fulani na kutupa mezani ambapo Agent aliifungua na kuanza kuangalia baadhi ya picha ambazo zilionesha wanajeshi wa C.O.D.EX wakiwa katika mazoezi yao. Walikuwa wanatisha sana kwa wanachokifanya lakini walionekana kutojali wala kuhisi maumivu.


Baada ya picha hizo, Rais pia akampa kijana anayemuamini simu matata sana na kumchezeshea video ambayo ilionesha wale wanajeshi wakiungua na baadae kurudi katika hali yao ya kawaida. Na picha kadhaa za video zile, zilionesha ukatili na silaha zao hatari wanazotumia. Mwili ukamsisimka Agent.


“Hapa kuna kazi kubwa Mkuu.” Akaongea Agent huku anarudisha vile vitu alivyopewa.


“Ndio maana wanajeshi wetu hawawezi. Anahitajika mtu mjanja na mwenye uelewa wa kuwazuia hata kwa sayansi zake. Naye ni wewe.” Rais akatoa jukumu zito.


“Nahitaji kusoma kwanza na sehemu ambapo nitatengeneza baadhi ya silaha zangu.” Akaongea Agent na Rais akamuelekeza kwenye maabara fulani iliyopo ndani ya Ikulu yake. Kisha akamtolea mafaili baadhi ambayo alitumiwa na CIA kwa ajili ya kumtambulisha mtu wanayetakiwa kukamata. Baada ya hapo, akaanza kumuelekeza mambo mengine mengi ambayo alipewa na CIA. Hadi nusu saa inakatika, Agent alikuwa kashiba maneno mengi ambayo yangemuongoza kwenye msako wake.


****


Ndani ya maabara ambayo ilikuwa ndani ya Ikulu, Agent alikuwa kavaa mawani kubwa myeusi na alikuwa anachanganya vitu kadhaa kwenye chungu cha chuma na ambacho kilikuwa kimepata joto kali na kuwa chekundu sana. Kila alipotupia baadhi ya vitu alivyovijua yeye, moto mkali ulifumuaka na kuzidisha joto ndani ya maabara ile ya Kisayansi.


Baada ya kuridhika, alimwagia mchanganyiko ule kwenye sahani moja kubwa na ya bati. Pini ndo go ndogo nyingi sana zikaonekana ndani ya sahani, naye Agent akatabasamu baada ya kufanikisha zoezi lake la kwanza lakini hakuishia hapo, alizimwagia kemikali fulani ambazo zilifanya pini zile zisimame kwenye sahani na kuchongoka zaidi.


Akabofya kiparaza cha kompyuta yake ambayo alikuwa anatembea nayo, na ile sahani ikaanza kuzunguka taratibu kisha kuhama na kwenda sehemu moja ambayo kulikuwa na kijumba kidogo alichokibuni Agent kwa ajili ya shughuli zake za Kisayansi. Kijumba hicho yeye mwenyewe alikiita UHAI. Akimaanisha ni kijumba kinachoweza kuvipa uhai vitu ambavyo havina uhai.


****


Asubuhi iliyofuata, Agent alionana na Rais na kumuelezea kazi yake ilivyokwenda na alimwambia yupo tayari kwa kazi ambayo kamtuma.


“Sawa kijana wangu. Nakuamini.” Rais aliongea kwa tabasamu na kisha akampa simu yake ambayo safari hii, alimtaka aende kuitazamia chumbani kwake kwa sababu yeye hakai tena ofisi sababu ziara ya siku hiyo ya kwenda Tabora kufungua miradi ya treni za angani. “Humo utaona ni wapi mtuhumiwa wako unatakiwa kumpata. Fanya yako leo hii, apatikane. Nishawaambia kuwa kazi ni leo.” Akaongea Rais baada ya kumkabidhi ile simu.


“Sawa Mkuu.” Agent alikubali na kusimama tayari kwa kuondoka ofisini.


“Agent Zero.” Kijana wa Rais akageuka na kumtazama Rais wake. “Kuna zawadi pia kwa ajili yako ukifanikisha hilo, Dola Milioni Moja inakusubiri na yawezekana ikapanda hadi hamsini.” Akampa taarifa mwanana kijana wake na kumfanya Agent atabasamu na kupiga saluti ya kikakamavu. “Nikutakie kheri katika kazi yako.” Akamaliza na Agent Zero kama alivyomuita, akatoka nje ya ofisi.


****


Furaha kubwa ilikuwa imemtawala Idris ambaye kila wakati alijiona mwenye bahati kukutana na Limasi ambaye kama mapenzi alimpa yote mwanaume yule aliyeficha siri nyingi juu yake. Idris akiwa anarudi nyumbani na zawadi kadhaa alizomnunulia mke wake, alisimama njia panda moja ambayo ilikuwa ina mataa ya usalama barabarani. Ilikuwa yapata saa tatu na robo usiku wakati mataa hayo ya usalama yaliposimamisha gari lake.


Aliamua kutumia muda ule mdogo kupekua zawadi kadhaa alizokuwa amemnunulia mpenzi wake. Wakati anafanya hayo akiwa ndani ya gari lake lingine la gharama, kuna gari moja kubwa aina ya scania lilikuwa linatokea upande wa kushoto kwa kasi ya ajabu na ghafla lilikumba gari la Idris na kulipasua katikati kisha ile sehemu inapokaa injini, ililipuka na kusababisha taflani eneo zima la barabara.






Furaha kubwa ilikuwa imemtawala Idris ambaye kila wakati alijiona mwenye bahati kukutana na Limasi ambaye kama mapenzi, alimpa yote, mwanaume yule aliyeficha siri nyingi juu yake. Idris akiwa anarudi nyumbani na zawadi kadhaa alizomnunulia mke wake, alisimama njia panda moja ambayo ilikuwa ina mataa ya usalama barabarani. Ilikuwa yapata saa tatu na robo usiku wakati mataa hayo ya usalama yaliposimamisha gari lake.



Aliamua kutumia muda ule mdogo kupekua zawadi kadhaa alizokuwa amemnunulia mpenzi wake. Wakati anafanya hayo akiwa ndani ya gari lake lingine la gharama, kuna gari moja kubwa aina ya scania lilikuwa linatokea upande wa kushoto kwa kasi ya ajabu na ghafla lilikumba gari la Idris na kulipasua katikati kisha ile sehemu inapokaa injini, ililipuka na kusababisha taflani eneo zima la barabara.


ENDELEA.


Scania liligonga gari la Idris, lilienda kusimama hatua zipatazo ishirini tokea pale ambapo mlipuko umetokea. Kisha ikasikika sauti ya injini kupumua na mlango wa dereva kufunguka. Akashuka yuleyule kijana aliyetumwa na Rais wa Tanzania, wenyewe wanamuita Agent Zero ambaye usiku ule alikuwa kavaa suruali ya jeshi la Tanzania na kwa juu kavaa koti la leiza nyeusi, lililomkamata vema na ndani yake kavalia fulana iliyokuwa imeandikwa Hadithi App.


Upande wa Idris ambapo baada ya gari lake kugongwa vibaya, yeye alibakia kwenye kipande cha injini ambacho kililipuka na baada ya sekunde kama arobaini, mwanaume yule alionekana akitokea kwenye moto ule mkubwa na ngozi yake ilianza kujitengeneza taratibu na baadae kukaa vema huku akitokea kavaa nguo zake zilezile alizokuwa kavaa mwanzo.


“Karibu Tanzania mwanajeshi.” Agent Zero ndiye aliongea baada ya kumuona Idris kamaliza kujiunga mwili wake. Mikono yake aliiweka kwa nyuma na kila mara alikuwa akiitingisha kwa mbwembwe.


Idris akiwa na hasira baada ya vamizi lile la kushtukiza alichomoka ghafla pale alipo na kuanza kumkimbilia Agent na kitendo bila kusita, kutokea kwenye mkono wa koti lake, vile visindano alivyovitengeza Agent, vilishuka hadi kwenye kiganja chake cha mkono na kujaa kisha Agent alivinyanga vyote kwa pamoja na kuvirusha kumuendea Idris.


Vilikuwa vinatoa mlio wa fulani kama wa nzi wa chooni, na pia mlio wa vyuma vidogo kugongana ulisikika ndani yake. Vilipofika karibu na Idris, Agent ambaye alikuwa amesimama palepale aliposhukia na gari lake, alifunua mkono wa koti lake na saa moja matata sana ilionekana. Akaibonyeza kitufe kimoja kilichopo pembeni na sindano zile ndogondogo zilijitenga na kisha vimamvamia Idris shingoni na kuzunguka shingo ile na kumfanya akabwe.


Idris alipiga goti chini na kuanza kuhangaika kuvinasua vile visindano ambavyo vilianza kumchoma shingo yake na kusababisha damu kuanza kutoka kidogo kidogo.


“Hapa sio Marekani Mwanajeshi. Hapa ni Tanzania. Nchi yenye amani na yenye wingi wa wataalamu.” Agent aliongea huku taratibu akianza kusogea eneo ambalo alikuwa kapiga goti moja, Idris.


“Unataka nini?” Idris aliuliza akiwa wazi analazimisha kutafuta pumzi.


“Rahisi tu! Waliokutengeneza wanakutaka urudi nyumbani, Tanzania si kwako.” Akajibu Agent na jibu hilo likamfanya Idris amuangalie aliemwambia hayo.


“Unafanya kosa kubwa kijana. Watakuua na wewe tu.”


“Hapana Mwanajeshi, mimi kwanza nimeahidiwa donge nono nikikukamata. Na hapa navyokwambia, wapo njiani kuja kukuchukua. Kwa hiyo chaguzi ni lako.”


“Nooo.” Idris aling’aka kwa sauti na kushika zile pini zilizojiunga shingoni kwake na kuzivuta kwa nguvu nyingi sana. Nazo zikaachia shingo yake na Idris akazitupa kwenda kumuelea Agent ambaye hakuamini kama silaha yake itaweza kuzuiliwa kirahisi namna ile.


Idris alichomoka kwa teke matata sana ambalo lilimkuta Agent kifuani na kumrusha mbali kana kwamba kapigwa na shoti ya umeme.


Akiwa haamini kama kapigwa au kakagongwa na gari moshi. Agent alianza kugaa gaa chini kwa maumivu na bila kutegemea, Idris alikuwa karibu yake na alimnyanyua kwa mkono wake mmoja na kumbamiza kwenye kioo cha scania na kukifanya kioo kile kitengeneze nyufa.


Taratibu Agent alishuka chini huku damu zikimtoka mdomoni lakini hiyo haikuwa sababu ya kuachwa kutembezewa kipondo na Idris ambaye hasira zilimjaa kupita maelezo.


Agent alipokea ngumi kali toka kwa Idris iliyomfanya aingie hadi chini ya uvungu wa scania alilolitumia kuharibu gari la gharama la Idris.


Idris alipomchungulia Agent, aliweza kumuona akitambaa kwa haraka akijaribu kutaka kukimbilia upande mwingine wa lile Scania. Idris kwa nguvu zake nyingi, alisogea ubavuni mwa scania lile na kuanza kulisukuma kwa lengo la kulipindua na hali hiyo ilizidi kumtisha Agent ambaye alimua kutulia bila kutambaa hadi aliposikia kishindo cha gari lake kupinduliwa. Akajigeuza na kulala kifudifudi na hapo alimuona Idris akinyanyua ngumi yake na kutaka kumgonga nayo usoni ila Agent alibiringitia pembeni na ngumi ile ilikita kwenye rami na kuitoboa kabisa. Hapo ndipo Agent aligundua kamchokoza nguruwe pori kwa kumuibia vitoto vyake. Ikabidi naye aanze kujibu mapigo ya Idris ambaye alikuwa anataka kumkanyaga kwa viatu vyake.


Agent akabiringita tena kidogo na kiatu kile kikamkosa kwa mbali sana na kwa haraka, alirudi pale alipotoka wa kubiringita na kukamata mguu wa Idris na kuubana vema kama anataka kuuvunja. Idris akashindwa kustahimili, akakosa balansi na kujikuta akikubali kudondoka aridhini na uso kwa uso alikutana na ngumi matata ya pua kutoka kwa Agent Zero. Akahisi pua kuvunjika lakini hakuhisi maumivu na alipomtazama Agent, alishuhudia kiatu chake kikimfuata na kutua palepale kwenye pua. Akagugumia kwa maumivu machache aliyoyapata.


Agent akajibetua kiustadi na kusimama kisha kwa haraka, alikimbia kumfuata Idris ambaye alikuwa kalala kifudifudi. Sarakasi ya mtupu, ilimtoka Agent lakini aliweza kutulia miguu ambayo ilikanyaga juu ya kifua cha Idris ambaye alikohoa vibaya kwa pigo lile toka kwa Mtanzania mwenye mapenzi na nchi yake. Agent kwa ukakasi wa raha, alijibetua tena sarakasi ya mbele na kutua kwenye rami, na kisha kwa utamu wa raha zake, akajibetua sarakasi ya kurudi nyuma na kwa mara nyingine alitua juu ya kifua cha Idris lakini safari hii, magoti yake yakiwa yamekita juu kifua hicho. Idris akazidi kukohoa na kujitutumua kwa kumsukuma Agent pembeni ambaye naye hakuwa haba katika kujitetea.


Akabiringita kwa chini na kwa ustadi wa aina yake, akajibetua kwa sarakasi na hapo akatulia huku mkono wake mmoja upo chini na miguu yake miwili imechukua balansi. Ukimuoa waweza sema labda mwanariadha ambaye anataka kuanza mbio zake. Idris naye alisimama na kutazama kiumbe anachopambana nacho.




Kwanza kina kasi ya ajabu, pili kina mapigo ya kushtukiza, na tatu kina roho ngumu licha ya kuwa binadamu halisi. Kwa nini asikiulize kile kiumbe.


“Wewe ni nani?” Idris akajikuta anaropoka swali.


“The Undercover Agent.” Akajibu Agent Zero.


“Huna jina mbwa wewe?” Akabwata tena kwa sauti ya hasira.


“Niite Agent Zero. Agent wa kujitegemea, sinaga haja ya kushirikiana na mtu.” Akajibiwa tena kwa sauti ya utulivu. Lakini jibu lile likampa hasira zaidi Idris na kujikuta akianza kumfuata kwa kasi pale Agent alipoweka pozi la kiuana riadha.


Alipofika, alirusha teke lake kama anayebutua mpira lakini Agent aliliona na kupiga sarakasi ndogo ya kusogea upande mmoja na kisha kwa kasi ya ajabu, alinyanyuka kwa mateke matatu ya haraka ambapo moja lilimpata kwenye mguu, lingine likapanda hadi kiunoni na la mwisho likampandia kisogoni. Idris akajikuta anapepesuka kama mlevi anayeelekea kutumbukia shimoni na wakati huo Agent alitua chini na kusimama wima akiwa nyuma ya Idris, kisha kwa kasi alikwenda kumrukia kwa nyuma na kumkaba huku miguu yake ikibana tumbo la Idris.


Idris akaanza kuhaha kuchomoa kabali nzito aliyokuwa anaipitia kwa muda ule. Alihangaika bila kufanikiwa na kujikuta akipiga goti moja chini kwani tayari pumzi zilianza kumuisha. Kila alipotaka kuondoka kabali ile, alijikuta akizidi kukabwa.


Mara uso wake ukaanza kuona picha za ajabu ajabu. Mara alimuona mtoto akiwa anapelewa keki ya siku ya kuzaliwa. Na mara akamuona mwanamke akiwa anambusu kwenye paji lake la uso huku anamtakia heri ya kuzaliwa. Picha zilikuwa zinakuja kwa kuchanganyika sana na hakuweza kutambua zile picha zinatokea kwa sababu gani. Na wakati picha hizo ambazo zilikuwa kama video zinazidi kutokea, ndipo alipoweza kushuhudia mwanamke aliyembusu kwenye paji la uso akikatwa vibaya shingo yake. Na picha hiyo aliweza kuiona moja kwa moja kwenye kichwa chake. Na hapo ndipo akashuhudia mtu mwenye suti akiingia chumbani ambapo mwanamke yule alikatwa shingo yake kwa panga kali. Uso wa tabasamu ukawa umepambwa kwenye paji la mwenye suti.


Mara picha hiyo ikaanza kufutika na kumrudisha hadi eneo la tukio ambapo bado Agent alikuwa kang’ang’ania shingo yake. Idris akafungua macho yake na kusimama kwa nguvu na kusababisha uoga mkubwa kwa Agent Zero ambaye hakutegemea kuona yule bwana anasimama kirahisi namna ile. Idris akaaanza kuzunguka kwa kasi ya feni na kumfanya Agent ajihisi kizunguzungu na kujikuta akimuachia mwenyewe mwanajeshi yule ambaye alikuwa kama mbwa mwitu aliyejeruhiwa. Picha za kile alichokiona zikamrudia na kujikuta akiikumbuka sura la yule mwenye tabasamu.


“Uzo.” Akaongea kwa sauti ya chini huku akiwa kasimama na kuacha kuzunguka. Agent yeye alikuwa anagaa gaa chini huku akihisi kutapika lakini aliposikia Idris anataja jina la mtu aisyemjua, akili ikarudi na kumtazama yule mwanajeshi. Wakakutanisha macho, na Idris ndiye alikuwa wa kwanza kutaka kumfuata Agent pale alipolala lakini wakati anaelekea pale, mara alisikia milio ya nzi wa chooni na kwa haraka akaweka mikono yake shingoni na zilezile pini zikambana mikono yake kwenye shingo.


Agent akajibetua haraka kwenda nyuma na kutuma pini zingine ambazo zilienda kunasa kwenye mguu wa kushoto na zingine mguu wa kulia. Haikujulikana idadi ya pini alizozibeba lakini alikuwa anazitoa kwa wingi sana. Zile za miguuni, zikajiunga kwa pamoja na kufanya miguu ile iiunganike na kugandana kama sumaku. Idris kila akijipapatua, hamna kilichokubali kumuachia na viliendelea kujikaza eneo husika kila alipotaka kuvitoa.


“Hivi vinini wewe mbwa?” Akauliza kwa tusi lakini Agent hakujibu chochote zaidi ya kutuma tena pini zingine zilizoenda kuziba mdomo wake.


“Wewe si Mtanzania. Acha maneno mengi hapa.” Akaongea Agent na kurusha pini zingine ambazo zikaenda kumfunga kiuno chake na zingine kikaenda kunasa kwenye scania lililokuwa limepinduka. Pini zile zilizoenda garini, zikawasiliana na pini za kiunoni na kutengeneza kitu kama kamba. Napo kwa pamoja vikaanza kumvutia Idris kwenye lile scania. Idris akawa haamini kama kirahisi vile kashindwa hasa baada ya kubanwa kwenye gari na kunatia hapo.


‘Subiri wenzako waje wakuchukue.” Agent akaongea huku anafuta damu iliyokuwa inamtoka upande mmoja wa mdomo wake.








“Hivi vinini wewe mbwa?” Akauliza kwa tusi lakini Agent hakujibu chochote zaidi ya kutuma tena pini zingine zilizoenda kuziba mdomo wake.


“Wewe si Mtanzania. Acha maneno mengi hapa.” Akaongea Agent na kurusha pini zingine ambazo zikaenda kumfunga kiuno chake na zingine zikaenda kunasa kwenye scania lililokuwa limepinduka. Pini zile zilizoenda garini, zikawasiliana na pini za kiunoni na kutengeneza kitu kama kamba, napo kwa pamoja zikaanza kumvutia Idris kwenye lile scania. Idris akawa haamini kama kirahisi vile kashindwa hasa baada ya kubanwa kwenye gari na kunatia hapo.


“Subiri wenzako waje wakuchukue.” Agent akaongea huku anafuta damu iliyokuwa inamtoka upande mmoja wa mdomo wake.


ENDELEA.


Dakika kumi mbele, gari moja mfano wa daladala lakini yenyewe inavioo vyeusi na imekaa kipelelezi zaidi, iliingia eneo la tukio na milango ilifunguka. Akashuka Uzo akiwa na wanajeshi wawili wamekamata bunduki kubwa. Mmoja wa wanajeshi hao alikuwa ni Merice, mtoto wa Dokta Ice na Simeria.


Idris akaanza kupapatuka pale alipo kwa kutaka afunguliwe lakini hamna aliyemuelewa maana yake, kwa sababu ya kuzibwa mdomo.


“Ohoo! Ni wewe kumbe. Best?” Akaongea Uzo baada ya kwenda mbele ya Idris. “Au huku unatumia jina gani eti.” Akauliza tena kwa nyodo nyingi na hakutaka jibu na badala yake alienda hadi kwa Agent ambaye alikuwa amekaa juu ya jiwe moja lililopo pembeni ya barabara ile huku anachimbachimba chini.


Uzo akamtazama Agent na kisha macho yake yakarudi kwa Idris. “Yaani mtu akisema umelifunga domo lile jitu, hawezi kuamini kabisa. Hauendani na mambo yako kabisa.” Akaongea Uzo huku ametabasamu lakini Agent hakuwa na la kuongea. “ Unaitwa nani wewe?” Ikabidi ajibaraguze kwa kuuliza.


“The Undercover Agent.” Akajibiwa kifupi.


“Agent Zero.” Akaongeza Uzo. “Unayeaminika na Rais wako wa nchi. Kazi nzuri umefanya, nimekubali sana na nimeshawishika kukubali kwa nini Rais wako anakuamini.” Akatoa pongezi ambazo zilikuwa kama kelele masikioni mwa Agent.


“Nimemaliza kazi yenu. Nakumbuka nina dola kadhaa kwenu. Nazihitaji mapema sana.” Agent aliongea huku anatoa rimoti ndogo na kumpa Uzo. “Hapa ukitaka kumfungua. Mfano nataka kufungua mdomo wake, nabofya hapa.” Akabonyeza na zile pini zikaanza kumtoka mdomoni Idris. Akaelekeza pote ambapo wanataka kumfungua. Na Uzo alionekana kuelewa vema.


“Okay Agent Zero, The Undercover Agent, ahsante kwa msaada wako. Na hii ni zawadi yako.” Uzo akatoa bastola na kumuwekea kichwani Agent.


“Nilikwambia dogo, watakuua na wewe tu.” Maneno yalimtoka Idris kwa sababu tayari alikuwa kafunguliwa mdomo. Maneno hayo yakamfanya Uzo ageuke haraka na kumpiga Idris risasi ya mguu lakini likawa kosa kubwa sana kumuachia Agent kwani aliruka kwa pembeni na kwa kasi yake ya ajabu, akarusha pini zake.


Uzo alipogeeuka amuangalie Agent, alisikia sauti za nzi na vichuma vikigongana na hapohapo bastola yake ikavamiwa na pini za Agent. Akaitupa bastola ile chini na alishuhudia ikiliwa na zile pini huku pini hizohizo zikiongezeka na kuwa nyingi sana.


“Umevunja uaminifu mzee. Kosa kubwa sana umefanya.” Akaongea Agent huku yupo pembeni akimtazama kwa macho ya ghadhabu Uzo.


“Utakufa tu hapahapa, mbwa we.” Uzo akabwata na kisha akawaamuru wanajeshi wake wawili wamvamie Agent nao bila kusita walianza kumwagia risasi Agent ambaye alikuwa akizikwepa kwa sarakasi za haraka na waliposhtuka, risasi zao zilikuwa zimekwisha na ni sauti za nzi ndizo zilisikika kwenye masikio yao. Bunduki zao zikawa mali ya pini za Agent.


Agent akasimama wima na kuwatazama wale watu.


“Tatizo hamnijui, na wala siwajui. Ila hapa mmeingia sehemu mbaya.” Agent aliongea. “Tena mbaya sana.” Akasisitizia kauli yake. “Mmeona hii?” Akafunua mkono wake na kuonesha saa aliyoivaa. Saa hiyo ndio ilikuwa inakontroo zile pini. “Hiyo rimoti si kitu kama una hii. Hii inaweza kufanya yote unayoyafanya kwenye hiyo rimoti. Kwa mfano,” Agent akabofya saa yake na mara Idris akaanza kufunguka kimoja baada ya kingine huku pini zile zikimkimbilia Agent na kuingia kwenye mifuko ya nguo zake.


Wale wanajeshi waliokuja na Uzo, kuona hivyo, wakaanza kumkimbilia Idris lakini walikwishachelewa kwani tayari jamaa alikuwa huru. Ngumi za hatari zikamtoka Idris kwenda kwa wale wanajeshi ambao walipaishwa angani na kudondokea migongo.


“Mmenisaliti mimi, na mmemsaliti Rais wangu. Sivyo tulivyokubaliana. Mkamateni wenyewe, huyo hapo.” Idris alikuwa kama mbogo kwani alikamata kichwa cha mwanajeshi mmoja wa kiume na kuvunja shingo yake na wakati huo Merice naye alinyanyuka na kukaa vema tayari kwa kukabiliana na Idris aliyeonekana hana huruma mbele ya wale wanajeshi wenzake. Uzo akawa hana la kusema na macho yamemtoka kwa wahka pamoja na uoga.


Idris akamsogelea Merice na kumrushia ngumi lakini mwanadada yule aliikataa kwa kumzunguka Idris na kutokea nyuma yake ambapo alimtwanga ngumi nzito ya kisogo.


“Ouuch.” Agent alipiga kelele kwa ngumi ile ya kisogo lakini aliweza kumshudia Idris naye akirusha teke la kinyume nyume na kumtwanga Merice tumboni na kwa pamoja wakawa wanaachiana mmoja akienda mbele na mwingine akirudi kinyumenyume. Ilikuwa ni picha ya kusisimua.


Walipotulia, wakawa wanaangalia kwa macho ya uchu.


“Merice kamata huyo.” Uzo alibwata.


“Kumbe wewe ni Merice? Mwana wa Dokta Ice na Simeria.” Akaongea Idris na kutikisa kichwa chake. Picha zikaanza kumrudia tena kichwani mwake kwa haraka. “Inasemekana ulikufa na mama yako, kumbe upo?” Maneno hayo yakamfanya Idris ashushe mikono yake aliyoiweka kimpambano. Merice akawa katika mshangao. “ Uzo ni mtu mbaya sana, kaua familia yangu yote na baba yako ndio alinileta huku ili anifiche. Baba yako alitulea mimi na wewe kama wanawe. Tafadhali Merice, achana na hii kazi.” Idris akaendelea,


“Muue huyo.” Uzo akabwata tena lakini alipotaka kuongea akafumbwa na mdomo wake na pini za Agent. Akabaki kama bubu anayeomba chakula kingine.


“Acha watu waongee.” Agent aliongea kwa mbwembwe na kukaa juu ya jiwe lake alilokutwa kakaa mwanzoni.


“Dokta Ice alikufa siku mbili mbele ulipotoroshwa. Alijinyonga mwenyewe.” Merice alijikuta akiongea hayo na kumfanya Idris alie sana baada ya kugundua kuwa mtu aliyemlea alikufa kwa sababu yake.


Akamuendea Uzo na kumuinua kwa nguvu zake zote kisha akamrusha na kujibamiza kwenye bodi la scania alilokuja nalo Agent. Na wakati huohuo, ving’ora vya polisi vilianza kusikika kwa mbali vikija eneo lile.


“Ondokeni haraka. Polisi wameruhusiwa kuja hapa, msije mkaleta madhara kwa polisi wetu, nitawaua wote.” Agent aliwaambia Merice na Idris na macho ya Idris yalimuangalia kwa uchu Uzo lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kwenda kwenye daladala ya kipelelezi aliyokuja nayo Uzo, na kisha kuondoka eneo lile akiwa na Merice ndani yake.


Polisi walifika na kumkuta Uzo akijizoa zoa na wakati huo yule mwanajeshi aliyevunjwa shingo alijirekebisha katika hali yake na kusimama tena. Uzo akapata ahueni baada ya kuona ulinzi wake umerudi.


Baada ya polisi kufika, gari nyingine nyeusi ilifika eneo lile na Rais alishuka na moja kwa moja alimuendea Uzo.


“Umemsaliti mwanajeshi wangu. Umetaka kumuua, unataka nini sasa?” Rais alimfokea Uzo na Uzo akatabasamu kisha kwa mbwembwe nyingi akajitapa.


“Mbwa wako hawezi kazi, ilipaswa afe kama wewe.” Akaongea hayo na kujaribu kutaka kumkwida Rais lakini ghafla alisikia sauti za nzi na mara mikono yake ikafungwa kwa pini za Agent.


“Unadhani hii ni nchi yako na unaweza kufanya lolote utakalo?” Sauti ya Agent akiwa palepale kwenye jiwe lake ilisikika na kisha akaviruhusu vile vipini vimuachie.


“Washenzi nyie, hamjui sisi ni wa Marekani eeh’” Maneno hayo yakaenda sambamba na kumuamuru yule mwanajeshi aliyebaki kumteka haraka Rais ambaye alikuwa kasimama mbele yake bila uoga wowote.


Lakini kabla mwanajeshi yule hajasogea hata hatua moja, alijikuta akipokea risasi ya kichwa na risasi ilipofika ndani ya kichwa, ikapasuka na kufanya kichwa cha mwanajeshi yule kivurugike kama tikiti maji lililopigwa ngumi na roboti.


“Hujui kuwa hapa haupo Marekani?” Rais akamuuliza. “Vizuri sana Lisa.” Akampa sifa mtu aliyemtwanga risasi yule mwanajeshi. Anaitwa Lisa, mwanamke mjanja kwenye shirika la siri la kipelelezi la Tanzania.


“Ahsante Mr. President. Msalimie Agent Zero. Nimemaliza kazi yangu.” Sauti ilisikika kwenye simu ya upepo aliyokamata Rais wa nchi.


“Sawa binti yangu.” Akaitikia Rais na kumgeukia Uzo ambaye alikuwa haamini kama mwanajeshi wake kafa kizembe tena kwa silaha za Kitanzania. “Sikiliza nikwambie kijana.” Safari hii aliongea huku yeye ndiye anamfuata Uzo. “Umemsaliti mtu wangu kijinga sana. Tulikubaliana tufike hapa kwa pamoja, lakini wewe ukajidai mjuaji na kufika kabla yetu ili umuue kijana wetu. Unajua tumegharimu kiasi gani kumtengeneza huyu Agent? Unajua wakati tunamtengeneza ni wangapi walifeli na wangapi walifaulu? Unajua watu kama hawa wapo wangapi duniani? Wewe unataka kumuu kirahisi tu!” Uzo alikuwa kimya na mpole kama asomewaye mashitaka. “Sikuhitaji nchini kwangu, ondoka haraka sana. Huyo mwanajeshi unayemtaka, ni Mtanzania.” Rais akamaliza na kugeuka tayari kwa kuondoka.


“Ameondoka na mwanajeshi mmoja niliyekuja naye.” Uzo akaongea na kumfanya Rais ageuke na kumtazama.


“Kwa hiyo.” Akamuuliza.


“Nataka kuondoka na mwanajeshi wangu.” Akatoa wazo Uzo.


“Ruhusa. Kamchukue. Ukitaka beba wote lakini sitaki uwadhuru wananchi wangu wala miundo mbinu yangu na kitu chochote kile cha hapa nchini.” Akaongea Rais.


“Hamna shida. Nitaingiza wanajeshi kadhaa leo hii kwa huu msako.” Uzo akakubaliana na Rais.


“Ukiharibu chochote, nchi yako italipa. Nitawasiliana na Rais wako kuhusu hili.” Uzo akakubali na Rais akaanza kuelekea lilipo gari lake huku nyuma pia, Agent Zero alinyanyuka na kuelekea kwenye lilelile gari.


Uzo akabaki kuwatazama na kiburi chote kikamuisha hasa wanaume wale walivyokuwa wanaondoka na magari waliokuja nayo.


“Kumbe ndio Tanzania hii. Duh! Nimeingia kichwa kichwa hapa.” Akajiwazia.


*****


Idris aliegesha gari lake eneo moja lenye miti mingi na kumwambia Merice ashuke ili waelekee nyumbani kwake. Mwanajeshi yule wa kike, alikubaliana na hilo na moja kwa moja wakaanza kuelekea nyumbani kwa Idris ambapo palikuwa na umbali wa Kilometa zipatazo kumi na tano toka pale walipolitelekeza gari la kipelelezi.


Uzuri walikuwa ni wanajeshi imara ambao hawawezi kuchoka kizembe. Hilo liliwasaidia kufika nyumbani kwa Idris baada ya dakika kumi toka pale walipoliacha gari lao.




“Wao kipenzi. Ulikuwa wanipa mashaka sana kwa kimya chako, nini kimekukuta?” Limasi aliongea huku akiwa kamkumbatia Idris ambaye naye alikuwa kamkumbatia.

“Ni historia ndefu, lakini leo utajua kila kitu.” Idris alijibu na kumuita Merice ambaye yeye hakusogea eneo lile hadi pale alipoamuriwa. “Huyu anaitwa Merice. Ni mwenzangu wa kitambo sana. Tutakuhadithia mengi sana leo hii kabla ya kuondoka hapa.” Akaongeza Idris baada ya utambulisho.

“Unaondoka unaenda wapi Honey? Halafu nina habari nzuri kwako.” Limasi aliongea kwa kudeka bila kujali hisia alizokuwa nazo Idris wakati huo.

“Tuingine ndani kwanza.” Idris akapendekeza na wote wakaingia ndani.

ENDELEA.

Habari kubwa iliyozungumzwa humo ndani, ilikuwa ni tukio lililomkuta Idris. Alieleza kitu kama kilivyo. Hakusita kumwambia hali yake iliyosababisha yeye kupona ndani ya ajali ile kubwa na ya kupagawisha yeyote yule.

“Idris. Mbona mimi sikuelewi unachoniambia?” Swali likamtoka Limasi kwa sababu hakuamini lolote lile. Alimuona mume wake yupo sawa na salama kabisa. Hadithi anayompa ilikuwa kama inajambo ndani yake. “Au ndio njia ya kuniacha ili uwe na huyu mzungu wako?” Hatimaye mwanamke wa Kitanzania, alitabainisha hisia zake.

“Hapana Limasi. Embu ngoja nije ili unielewe nachomaanisha.” Idris alisimama na kwenda moja ya chumba kilichiomo mle ndani.

“We are soldiers. Dangerous soldiers. You have to believe your husband. (Sisi ni wanajeshi. Wanajeshi hatari. Unatakiwa kumuamini mumeo)” Aliongea Merice lakini Limasi aliona mapicha picha tu. Akakaa kimya akimsubiri Idris arudi. Na baada ya dakika moja, Idris alirudi akiwa kakamata kisu kirefu na kikali.

Alichofanya baada ya kufika na kisu chake, alivua shati lake na kuanza kujichana kutoka upande wa kushoto wa kifua chake hadi chini ya tumbo upande wa kulia. Pia akajichana upande wa kulia juu, hadi chini upande wa kushoto. Akawa kama kajichora X kwenye mwili wake. Damu zilikuwa zinamchuruzika na Limasi alikuwa anapiga kelele baada ya kuangalia picha ile. Alikuwa amejiziba usoni ili asiendelee kuangalia ile picha ambayo Idris alikuwa anaifanya mbele yake.

“Tazama Lim.” Idris alimwambia Limasi ambaye alitoa mwanya mdogo katikati ya vidole vyake na kuangalia jeraha la Idris. Aliona damu zinaanza kurudi ndani ya kidonda alichojichana na mara ngozi yake ikajifunga vema.

“How this happen? (Inawezaje kutokea hii?)”Akauliza kwa mshangao Limasi huku akiwa ametoa mikono yake usoni.

“Hili ndilo nilikuwa najaribu kukueleza Lim. Tafadhali nielewe sasa. Tupo hatarini, mimi na wewe na huyu dada yangu.” Akaongeza Idris kujibu swali la Limasi.

“Ndio maana siku zile club hukudhurika.” Akaendelea kujiuliza na kujijibu mwenyewe, Limasi.

“Lim. Embu tuachane na hayo, huu si muda wake. Tupo hatarini mke wangu, muda wowote tunavamiwa hapa.” Idris akawa anajaribu kumleta kwenye mada husika Limasi.

“Wakina nani waje kutuvamia?” Limasi akauliza kwa mshangao.

“Kuna wanajeshi zaidi ya mia moja kama sisi. Ni hatari na hawana huruma hata kidogo. Wakiingia humu, hamna atakayesalimika.” Idris akamuwelewesha kwa kifupi.

“Kwa hiyo unataka tufanyaje sasa?” Akauliza Limasi akiwa na kitete.

“Nataka nikuchukue, nikupeleke kwa dada yako sasa hivi halafu tuache sisi tupambane nao.” Idris akajibu.

“Hapana, nitapambana nikiwa na wewe. Ndiyo ahadi niliyoapa.” Akaonesha uanamke wake.

“Hawa hupaswi kupambana nao. Tafadhali Lim. Nielewe, tupo katika hatari kubwa.” Idris akazidi kumuelewesha mke wake ambaye alikuwa anaogopa lakini bado anataka kuwepo.

“Soldier. Go and discuss this on your bedroom. (Mwanajeshi. Nenda na mkajadili hili chumbani kwenu)” Merice ambaye alikuwa hana sura ya kutabasamu, muda wote alikuwa kanuna, alitoa wazo kwa sauti ya kikatili.

Idris akamchukua Limasi na kwenda naye chumbani. Ambacho kiliendelea huko ni kujaribu kumsihi Limasi akubali kuondoka pale haraka sana.

Saa sita usiku. Limasi alikuwa kaelewa alichoelezwa na Idris alitoa mkoba mmoja aliokuwa amehifadhi baadhi ya nyaraka zake za siri zikiwemo nyaraka alizopewa na Dokta Ice, akamkabidhi Limasi.

“Nenda kasome haya. Vyote vilivyomo humo nakukabidhi wewe. Ni muhimu sana. Usije ukavipoteza, sawa mama?” Hakutaka mwanamke yule ajibu, akamvuta na kumchapa busu zito la mahaba. Pia akampa na kompyuta yenye maelezo mengi kuhusu yeye. “Hii pia itakusaidia pale ambapo hujaelewa. Acha sisi tupambane kuwazuia hawa wajinga,” Idris alimaliza na kumpa kompyuta. Akaanza kumvuta Limasi ili warudi sebuleni na kisha kuondoka naye.

“Id.” Limasi akagoma kwenda na kumvuta Idris. Idris akawa anamuangalia kwa lengo la kumsikiliza sababu ya yeye kumvuta. “Nina mimba yako.” Limasi akaongea na Idris akatabasamu na kumkumbatia kwa nguvu Limasi.

“Ahsante kwa hilo mke wangu. Ila hatuna muda. Twende nikupeleke kwa dada yako.” Akaongea Idris na kisha kwenda hadi sebuleni ambapo walimkuta Merice amesimama dirishani huku taa zote zimezimwa.

“Tumechelewa mwanajeshi.” Merice aliongea kwa lugha ya Kiingereza. “Tayari wapo mtaani na wanaingia nyumba hadi nyumba.” Akaongeza na kumfanya Idris aende hadi pale dirishani na kushuhudia wananchi wakitolewa nje na kutishiwa mitutu ya bunduki na wanajeshi wa C.O.D.EX ambao walikuwa wametapakaa kila kona ya mtaa.

“Tunafanyaje sasa?” Akauliza Idris huku akimuhofia zaidi Limasi.

“Huna silaha zozote?” Akauliza Merice kwa lugha ileile ya Kiingereza.

“Twende huku.” Akamchukua Merice na Limasi na kwenda nao hadi katika stoo yake na kisha akasukuma pembeni mashine moja ya kukatia majani, akafunua sehemu moja iliyokuuwa sakafuni. Hapo kulikuwa na uwazi wa pembe nne, na akashauri waingie humo kwani ni handaki. Wote wakaingia na kisha wakafunga kwa kifuniko walichofungulia.

Ndani ya handaki hilo lililopo ndani ya nyumba kubwa na a kifahari, kuliwashwa taa na hapo macho ya Merice na Limasi yakashuhudia mali mbalimbali anazomiliki Idris. Magari ya kifahari pamoja na silaha mbalimbali za kivita, vilionekana ndani ya handaki lile. Kwa kifupi lilikamilika.

“Hapa tunaweza kupambana.” Merice aliongea lakini bila tabasamu kuonesha kuwa kakubali yale anayoyaona.

Idris akaenda hadi chumba kimojawapo na kuwasha runinga za mle ndani ambazo zilionesha nyumba yake nzima kuanzia nje hadi ndani. Pia aliweza kuuona mtaa mzima.

“Wapo karibu kufika hapa. Sitaki kuwalipua kwa sababu ni kazi bure tu. Na hapo unapoona hamna silaha za kuwasimamisha hawa wajinga. Hivyo dawa ni kuwachelewesha kwa mapigo yetu.” Idris aliongea na baada ya hapo. Akaenda kwenye sehemu zilipo silaha na kuanza kuzipanda ndani ya mabegi yaliyopo humo.

Bunduki, mabomu pamoja na visu, vilipangwa humo kwenye mabegi. Naye Merice alikuwa anajichagulia silaha zake na kuzipanga kwenye begi lake. Limasi akawa mtu wa kuangalia tu akiwa haamini anatazama filamu ya Rambo au anaona kitu mubashara bila chenga.

Baada ya kupanga silaha zao za kutosha, wakavaa mavazi mengine ya kijeshi na kisha kwenye mavazi hayo, wakaweka silaha zingine za moto. Kwa kifupi walikuwa wamedhamiria kupambana na jeshi la Uzo ambalo lilishuka usiku huo kwa ajili ya kuwasaka wao.

“Lim. Hawa ndio sisi. Tafadhali, usiwe na wasiwasi, upo salama na utafika salama popote pale.” Aliongea Idris.

“Na kitu ambacho kitakuwa kibaya kwake hata hapo baadae, ni sisi kwenda naye kwa dada yake. Huko kuna polisi na kama hawa majamaa watajaribu kutufuata, hiyo inamaanisha kuwa, tunawaingiza wote matatani.” Merice aliongea mawazo yake.

“Tunafanyaje sasa?” Akauliza Idris.

“Twende sehemu nyingine ili kuwapoteza hawa wajinga. Huko ndipo tutajua la kufanya. Bado na uchungu sana na baba yangu. Licha ya kutokuwa na kumbukumbu, lakini moyo wangu uliniuma sana kwa kile nilichokiona. Damu ilinisisimka kuliko kawaida. Kuna sauti iliniita kabla Dokta hajafa. Na mama yangu ndiye aliyemuua, anatakiwa alipe haya kabla sijafa.” Merice aliongea kwa kisirani na Idris alimfuata pale alipo.

“Nitakuwa nawe katika hili kwa sababu ya Dokta Ice.” Aliungana na Merice nao kwa pamoja wakaunga mikono kuonesha umoja usiokuwa na jina.

“Nina nyumba ipo Moshi. Nadhani Limasi tutamuacha huko, halafu sisi tutapambana na hawa wenzetu kwa njia ya vita.” Akaongeza Idris na kwenda hadi sehemu yenye uzio mkubwa uliopambwa kwa magari ya kifahari. Akachagua jeep moja nyeusi na yenye tairi kubwa. “Nadhani hili litatufaa kwa vita. Ni imara na haliingizi risasi. Twende kuwaonesha kazi wajinga hawa.” Wote wakakwea garini huku Idris akishika usukani na Merice akikaa upande wake wa kushoto na Limasi akikaa nyuma na kufunga mkanda vema tayari kwa kupelekwa Moshi.

Mwanaume akawasha gari na kubonyeza kiruninga kidogo kilichopo kwenye gari lile. Kikaonesha ramani ya wanapokwenda na pia kikaonesha watu waliopo nje. Akaanza kuliendesha gari lake kwa tararibu na alipofika umbali fulani, aliongeza kasi na kubonyeza rimoti moja hivi, mbele yake kukafunguka mlango fulani ambao ulishuka chini na kutengeneza mpandisho ambao Idris aliupanda kwa kasi. Katika hali ya kustaajabisha, alitokea mbele ya geti la nyumba yake. Akawasha taa ‘full’ na kuweza kushuhudia baadhi ya wanajeshi wakiwa mbele yake na mitutu yao kuisimamisha.

Idris bila uoga, akagonga wanajeshi waliokuwa barabarani na kusababisha taharuki kubwa kwa wananchi ambao walikuwa nje wakishangaa ule msako ambao hauna jina. Wanajeshi waliyosalia kwenye ajali ile, walianza kulishambulia gari la Idris lakini hamna walichoambulia kwani lilikuwa haliingizi risasi.

“Twendeni tuwakimbize hawa wajinga. Wanatutoroka.” Uzo alibwata akiwa na nguo za kjeshi la Marekani na wanajeshi wake hata wale waliopamiwa na gari la Idris, walianza kukimbia magari yao na kuyapanda tayari kwa kumfukuzia Idris, ikiwa imetimu saa saba kasoro usiku.

****

Taarifa za wanajeshi wa C.O.D.EX kuvamia makazi ya watu huko Arusha, zikafika hadi kituo kikubwa cha Polisi cha Arusha. Mkuu wa kituo akaamuru haraka polisi wake waende eneo la tukio kwa ajili ya kufanya mahojiano na wananchi waliokumbwa na msala huo.

Polisi walifika nyakati ambazo tayari wale wanajeshi wamekwishaondoka hivyo mahojiano yalikuwa ni kuhusu kile walichofanyiwa na walichokiona. Polisi macho yakawatoka baada ya kuambiwa kuwa kuna wanajeshi ambao hata wakigongwa na magari hawafi. Taarifa hizo za mahojiano, zikafikishwa kwa mkuu na mkuu akawasiliana na Jeshi la Polisi La Tanzania, nalo likapeleka taarifa hizo kwa Amiri Jeshi mkuu ambaye alishangazwa sana tabia aliyofanya Uzo.

“Huyu mbwa nilimkataza huu ujinga. Hanijui eeh, ngoja kwanza.” Akatwaa simu yake ikiwa ni usiku wa mnene. “Wewe unafanya nini eti.” Rais akabwata kwa hasira.

“Nawataka watu wangu.” Akajibu Uzo kwenye simu.

“Nilikwambiaje kuhusu usalama wa watu wangu?”

“Nchi yangu itakulipa.”

“Pumbavu wewe, unaweza kulipa maisha ya watu?”

“Hilo halinihusu. Fanya unaloweza.” Uzo akata simu na kumfanya Rais aitazame ile simu kwa dakika kadhaa akiwa haamini kama kuna watu wanakiburi vile.

“Mshenzi ananikatia simu huyu?’ Akajiuliza akiwa na hasira. “Yaani anaifanya hii nchi kama yake, si ndio eeh. Halafu hajui kuwa anacheza na maisha ya watanzania. Na huyo mwanajeshi kamuoa Mtanzania. Kama wanaye humo wanapotoroka? Si atakufa mwananchi wangu?” Rais akawa anawaza huku anaongea mwenyewe. “Ngoja nimuoneshe.” Akawasha tena simu yake na kuingia sehemu ya majina yaliyomo humo, akabonyeza kitufe cha kupigia. “Haloo Agent. Naona anakiburi yule mtu. Nenda kasaidie kumkomboa Mtanzania mmoja.” Rais akaongea kisha akasikiliza upande wa pili. “Nakutumia sasa hivi muelekeo wao.” Akamaliza maongezi na kukata simu. “Sitakagi ujinga mimi.” Akaongea huku anaelekea chumbani kwake.

****




“Hilo halinihusu. Fanya unaloweza.” Uzo akakata simu na kumfanya Rais aitazame ile simu kwa dakika kadhaa akiwa haamini kama kuna watu wanakiburi vile.

“Mshenzi ananikatia simu huyu?’ Akajiuliza akiwa na hasira. “Yaani anaifanya hii nchi kama yake, si ndio eeh. Halafu hajui kuwa anacheza na maisha ya watanzania. Na huyo mwanajeshi kamuoa Mtanzania. Kama wanaye humo wanapotoroka? Si atakufa mwananchi wangu?” Rais akawa anawaza huku anaongea mwenyewe. “Ngoja nimuoneshe.” Akawasha tena simu yake na kuingia sehemu ya majina yaliyomo humo, akabonyeza kitufe cha kupigia. “Haloo Agent. Naona anakiburi yule mtu. Nenda kasaidie kumkomboa Mtanzania mmoja.” Rais akaongea kisha akasikiliza upande wa pili. “Nautumia sasa hivi muelekeo wao.” Akamaliza maongezi na kukata simu. “Sitakagi ujinga mimi.” Akaongea huku anaelekea chumbai kwake.

****

ENDELEA.

Barabara ndefu na ya rami, ilikuwa inakiona cha moto kwa kuandamwa na magari yapatayo kumi ambayo tisa yalikuwa yanalikimbiza gari la Idris, na lingine moja ni Idris mwenyewe. Hali ilichafuka. Mapambano ya kurushiana risasi ndio yalichukua nafasi na yaliendelea kupamba moto muda huo wa saa tisa hadi saa kumi na moja ambapo tayari jua lilionekana likichomoza.

Merice akiwa anatokeza mara kwa mara dirishani kujibu mashambulizi, alionekana kuzidiwa kwa sababu ya wale wanajeshi kutupa vitu vyao mara kwa mara na kwa mbinu za kijeshi.

“Soldier, hapa ni pagumu sana. Wanaweza kutukamata hawa.” Merice aliongea baada ya gari lao kuwekwa katikati kwa kubanwa kushoto na kulia, huku nyuma pia Uzo akiwa anafanya vema kumzuia.

“Hapana. Hawana jipya hawa. Hizi mbinu ni za kizamani sana.” Idris alimpa moyo Merice. “Shika usukani mara moja.” Akamuamuaru Merice na kitendo bila kuchelewa, Merice akakamata usukani na Idris naye akawa anataka kubadilishana nafasi na mwanamke yule wa shoka.

Wakafanikiwa. Dereva akawa Merice na wakati huo Limasi alikuwa anatetemeka kama mwizi aliyeshtukiwa.

Idris akafunga mkanda vema na maajabu ya gari lile, mikanda ipo minne. Mmoja ukafunga kawaida, yaani toka begani hadi upande mwingine wa kiunoni. Mkanda mwingine ukafunga miguu, mwingine kiuno na mwingine kifua. Baada ya kuhakikisha kajifunga vema, akabofya kitufe kimoja kilichopo pembeni ya kiti chake. Ghafka kiti chake kikajipetua kwa kuzunguka. Kule alipokaa Idris kukaenda chini, na chini kukawa juu.

“Idris.” Limasi akapiga kelele kubwa baada ya kushuhudia hali ile lakini hamna alichojibiwa toka kwa Idris ambaye alipotea pale alipokuwepo, na Merice pia hakuongea lolote.

Huko chini, Idris alikuwa anaishuhudia rami lakini hakuigusa kwa sababu ile mikanda aliyojifunga ilimzuia vema na hivyo kuonekana kama aliyelala au mtu anayepaa huku miguu yake kainyoosha na mikono yake kaitanua.

Idris akatazama kushoto na kulia. Akaziona vema tairi za maadui wake. Kwa uangalifu mkubwa aliweza kutoa mabomu ya kisasa kwenye sehemu alizohifadhi. Kisha mabomu hayo akayapachika mbele ya bunduki maalumu kwa ajili ya kufyatulia mabomu hayo ambayo yalionekana kama kifuniko kidogo cha kopo la mafuta ya kupaka. Lakini mabomu hayo, yalikuwa meusi na yalinakishiwa na utepe wa siliva kwa pembeni.

Baada ya kuyapachika mabomu mawili kwenye bunduki ya kufyatulia (Launcher Gun), Idris alianza kulenga tairi la adui wake wa kwanza, alipofanikisha shabaha yake, akafyatua bunduki yake, nalo bomu lile dogo likaenda kunasa kwenye sehemu ambazo wanafunga boliti. Alipofyatua bomu la pili, lilienda kunasa chini ya tanki la mafuta.

Akapachika tena mabomu mengine mawili na kuligeukia gari la upande mwingine. Akafanya tendo lilelile na baada ya kufanikiwa, akabonyeza kitufe kilekile, nacho kikamgeuza haraka na kumleta ndani ya gari na kumkuta mke wake analia.

“Idris, unataka kufanya nini?” Aliongea huku anafuta kamasi, mwanadada Limasi ambaye ghafla tabasamu lilikuja huku bado machozi yanamtoka.

“Nimerudi mamaa, ona kitakachowatokea mbwa hawa.” Idris alijibu huku anamfuta Limasi machozi yake. Limasi akashika mkono wa Idris na kuubusu kwa nguvu. Hakika mapenzi yalikuwa yamemkamata mtoto wa kike.

“Umefanya nini huko chini?” Merice akauliza.

“Nimewategea, ‘magnetic power bombs’” Idris alimjibu Merice kuwa yale mabomu aliyoyatega yanaitwa Mabomu ya Nguvu za Sumaku na ndio maana alipoyatuma, yalikimbilia kunasa kwenye sehemu zenye asili ya chuma.

“Vema.” Merice akajibu na kutazama yale magari yalivyokuwa yanazidi kumbana ili apunguze mwendo. Na kuna nyakati, wanajeshi wa C.O.D.EX walikuwa wakipiga risasi nyingi sana kioo cha gari lao lakini hawakufanikiwa walau kumuona mtu wa ndani kwa sababu ya vioo vile kuwa vyeusi vyote.

“Muda wao wa ngebe umekwisha. Nadhani walio nje, wataona filamu nzuri ya vita kuliko sisi.” Idris aliongea huku akitoa kitu kama peni ya kubonyeza, na kisha akabonyeza sehemu ya juu ya peni ile. Bomo la kwanza kupandwa ndilo lilianza kulipuka, likapasua vibaya tairi la mbele na kusababisha gari lile lipoteze muelekeo. Bomu la pili ambalo lilipandwa kwenye tanki la mafuta, nalo likaitika. Hapo gari lilinyanyuliwa juu na kuzunguka kama mjiti uliyorushwa angani kwa nguvu nyingi sana.

“Hoolly! Shit.” Uzo alifoka ndani ya gari baada ya kuona gari la wanajeshi wake likiranda angani na kisha kutulia pua. Baada ya hapo, ukasikika mlipuko mkubwa toka kwenye gari lile.

Sekunde kadhaa mbele, gari la upande mwingine, nalo lilikumbwa na dhahama ileile. Ambayo imelikumba gari la kwanza. Merice akacheka kwa furaha kwa mara ya kwanza na kumsifu Idris kuwa ni mwanaume wa shoka huku akimsihi Limasi amlinde sana yule mwanaume.

Uzo kuona lile tukio, aliamua kupunguza mwendo wa gari lake na kumfanya Merice alichanganye la kwake na kumuacha umbali mkubwa sana.

“Wajinga hawa, wanatufanya sivyo. Sasa dawa yao ni kufa tu.” Uzo akaongea na wenzake kwenye magari mengine na kisha kwa mtindo wa kipekee, magari matatu yakampita Uzo na kukaa mbele yake, kisha yote matatu yikajitanua yikiwa mwendo sawa lakini mbele kidogo, lile la katikati likaongeza mwendo kiasi na kuwa mbele zaidi. Ikatengenzwa pembe tatu toka kwenye yale magari. Gari la Uzo nalo likasogea mbele kidogo, likiwa usawa wa lile la katikati. Napo kukatengenezwa alama ya pembe nne na wakati huo magari matatu ya nyuma nayo yakajitengeneza kama yale ya mbele lakini ile iliyokuwa katikati, yenyewe ikawa nyuma zaidi. Hivyo gari la Uzo likaonekana lipo katikati na yale mengine yakawa kama yanamlinda.

“Shenzi hawa. Wanatumia ‘Knife style’ kuchinjia kitu kimoja.” Idris aliongea baada ya kuona ule mtindo wa magari alioufanya Uzo ambao ulionekana kama karata ya kisu, na wakati huo tayari ilikwishatimu saa kumi na mbili asubuhi. Jua lilikuwa linaangaza kwa asilimia kubwa.

Uzo na mtindo wake wa karata ya kisu, kwa pamoja wakaongeza kasi ya magari yao ambayo nayo si haba, yalikuwa ni mitindo mipya ya magari ya kijeshi ambayo yaliongezwa vitu vingi sana vya kijeshi. Mwendo wa magari ya Uzo, ulikuwa mkubwa kulikoni ule wa gari la Idris hivyo hawakuchukua muda sana, tayari walikuwa wanalipumulia kwa nyuma Jeep la Idris.

Lile gari la mbele, kwa ustadi mkubwa wa dereva wake, likafunga breki ya mkono (Hand Brake) na kujigeuza, yaani nyuma kukatamazama mbele, na mbele kukatazama walipokuwa wakina Uzo. Na likawa linaenda vivyo hivyo kinyume nyume na wakati huo Mwanajeshi wa C.O.D.EX alifungua mlango wa nyuma na kutoka na silaha ambayo kwa kitaalamu wanaiita RPG.

Kwa huku Watanzania tumezoea kuita silaha ile Kombora. Mwanajeshi kwa haraka, akafyatua kombora lile ambalo mara nyingi hutumia kutungulia ndege au magari magumu ya kivita kama vifaru. Gari la Idris lilinyanyuliwa kwa nyuma kulipuliwa lakini uimara wake, likarudi tena chini huku humo ndani si Limasi wala Merice ambao hawakutoa sauti kali za mshtuko.

“Idris, tukilemaa tunamalizwa sasa.” Merice aliona hali inapotaka kuelekea na Idris akamuangalia mke wake kwa imani, akaona kuwa mwanamke yule atapotea kizembe kwa sababu yake.

“Hapana. Mimi ni mwanajeshi. Hamna atakayekufa.” Idris akawatoa hofu wanawake wale ambao walikwishaanza kukata tamaa.

“Nakupa nafasi wanajeshi. Punguzeni mwendo wa gari lenu, ama la, tunatuma RPG lingine.” Sauti ya Uzo ilisikika toka kwenye spika za gari la Idris lakini hamna hata mmoja aliyejibu.

Kwa haraka Idris akapachika mabomu yake ya sumaku kwenye ile bunduki na kisha akajibetua na huko chini aliweza kuliona gari ambalo lilijigeuza lakini safari hii, likiwa tayari linatembea katika hali ya kawaida. Akatupa mabomu mawili na yote yakaenda kunasa sehemu ya mbele ya gari au boneti kwa lugha inayoeleweka.

Dereva wa gari aliyaona mabomu yale na kwa haraka akabonyeza kitufe fulani kilichokuwa karibu na redio ya gari. Boneti ile ikawa ya plastiki na kufanya mabomu yale yatereze na kudondoka.

“Huwezi fanikiwa hilo soldier. Mabomu yake hayajanasa safari hii.” Sauti ilisikika baada ya Idris kurudi ndani na aliponyeza ile peni, yale mabomu hayakulipuka kwa sababu yalikuwa hayajanasa kwenye chuma chochote.

“Hali ni tete Merice, bomu linalofuata nadhani linatuzungusha hewani.” Idris kwa mara ya kwanza 

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog