Simulizi : Mikono Ya Jasusi
Sehemu Ya Tano (5)
"Tafadhali niharakishie kwani ninahitaji hili lifanyike kwa haraka sana...!"
"nataka jua didi pitia huo mwili?" Aliuliza yule mzee wa kihindi.
"Nini kimepelekea kupoteza kwake maisha." Alijibu Alan kisha akamshuhudia Daktari yule akinyanyuka na ule mfuko wa nailoni baada ya kuzikusanya zile noti nne za shilingi elfu kumi kisha akaufungua mlango uliopo nyuma ya kile kiti ambao hata Alan mwenyewe hakuwa amegundua hilo. Alan alibaki akiitazama ile ofisi huku mawazo mengi yakipishana kichwani mwake. Alimfikiria sana Zaituni na kifo chake kilimuumiza mno, alikuwa na hasira sana na mtu aliyesababisha kifo hicho na aliapa kuhakikisha anampata na analipa. Alifikiri sababu ya Zaituni kuuawa na nani ambaye angeweza kumhusisha moja kwa moja na kifo kile. Fikra zake zikampeleka hadi kwenye simulizi ya Zaituni ambayo ilikuwa ikihusiana na yule jamaa ambaye alilazwa kama mgonjwa. Ni siku hiyo hiyo alimueleza kuwa jamaa yule alikuwa akitoka usiku wa saa saba na kuelekea kwenye lile jengo. Moja kwa moja akajenga mashaka na bosi wa Zaituni yaani mganga mkuu huwenda kwa asilimia kubwa huyo mtu anahusika, kwani kuna uwezekano wakati Zaituni akiwa anatoka pale mlangoni kwa mujibu wa maelezo yake kuna uwezekano mkubwa alikuwa akionekana na mganga mkuu.
Alifikiri sababu ya Zaituni kuuawa na nani ambaye angeweza kumhusisha moja kwa moja na kifo kile. Fikra zake zikampeleka hadi kwenye simulizi ya Zaituni ambayo ilikuwa ikihusiana na yule jamaa ambaye alilazwa kama mgonjwa. Ni siku hiyo hiyo alimueleza kuwa jamaa yule alikuwa akitoka usiku wa saa saba na kuelekea kwenye lile jengo. Moja kwa moja akajenga mashaka na bosi wa Zaituni yaani mganga mkuu huwenda kwa asilimia kubwa huyo mtu anahusika, kwani kuna uwezekano wakati Zaituni akiwa anatoka pale mlangoni kwa mujibu wa maelezo yake kuna uwezekano mkubwa alikuwa akionekana na mganga mkuu.
SONGA NAYO....
Sasa alama yake kubwa ilikuwa kwa Dokta Richard Bango. Hata hivyo ilikuwa ni lazima amuone yule mzee kwanza na mzee huyo ndiye angemfunulia mengi au hata kujua Dokta anaishi wapi hapa mjini, akapanga ifikapo usiku wa saa nne ni lazima awe mgeni wa huyo mzee anayefahamika kwa jina la mzalendo hata hivyo kabla ya hapo alidhamiria kwanza aelekee kwa Maisara mahali anapopatumia kusubiria wateja wake ili nako ajihakikishie kazi ya mwanadada yule.
Mawazo yake yalikatishwa na mlango ule ambao yule Daktari wa kihindi aliingia ambaye kupitia kibao kilichopo mezani aliweza kulifahamu jina lake. Aliitwa Dokta Salman Bhataan.
"Natumia buda refu sana nachelewesha veve...!" Alizungumza Dokta Salman kwa kiswahili chake cha kigeni huku akijichukulia nafasi kitini mwake. Mkononi alikuwa amekamata kipande kidogo sana cha karatasi ambacho kilibeba maelezo machache ya kiuchunguzi.
"Si muda mrefu sana ambao umetumika Dokta." Alijibu Alan akijiweka sawa kitini ili kupokea majibu ya uchunguzi wake.
"Nafanyika bema chuguza chuguza hii veve, naona uyu butu likuwa gomvi na butu hatari sana na buuaji kuba...!" Alianza kueleza Dokta Salman hata hivyo Alan akamkatisha kwa swali.
"Kwanini unazungumza hivyo Dokta...?"
"Nazugubu...eeh! Naona kifo chake vile nauliwa yeye." Lugha ya kiswahili ilionekana kumpiga chenga sana Dokta Salman hata hivyo alijitahidi kuongea.
"Nakufa na dangerous poison, naonekana buuaji natubia zindano au vyovyote. Naona aina hii ya poison vile nakuwa hatari sana. Poison hiyo naitwa VX Nerve Agent...!" Maelezo ya Dokta Salman yalipofikia hapo moja kwa moja yakamjulisha Alan jinsi hatari ilivyo, hata Dokta huyo alipokuwa akizidi kutoa maelezo hakuwa radhi tena. Hakutaka kumsikiliza Dokta huyo tena alichokifanya ni kuchukua ile karasi na kutoka nayo kisha akaiweka mfukoni mara tu alipoikaribia gari yake. Saa yake ya mkononi ilikuwa ikimwambia kuwa yalisalia masaa mawili tu kufikia muda wa saa moja kamili usiku. Alikiri kuwa alipoteza muda mrefu sana nyumbani kwa Zaituni hasa baada ya kujihakikishia kuwa binti yule alipoteza maisha. Akili yake ilivurugika sana. Sasa alikuwa na uhakika kuwa alikuwa na kazi nzito ambayo ilihitaji umakini mkubwa kwani wauaji hawakuwa wakifanya kazi yao kimzahamzaha hata kidogo. Aliendesha gari yake kwa pupa sana kwani kwa wakati huo hata njaa nayo ilikuwa ikimsumbua sana. Hadi muda huo hakukuwa na mtu mwengine aliyekuwa akimfuatilia kwani tokea tukio lile la kutokea kwa wale watu waliokuwa wakimfuatilia na kufikia hatua ya kupambana nao, hakukuwa na ufuatiliaji tena na hali hii ilimpa sana wasiwasi. Muda huu kwake ulikuwa ndiyo autakao kuanza harakati zake za kiuchunguzi, aliendesha gari yake hadi Chumbageni. Akazunguka akaja mpaka barabara ya majimaji akatafuta maegesho mazuri pembeni ya barabara hiyo akaegesha gari yake. Aliteremka toka garini mara baada ya kuona barabara hiyo ikiwa imepooza sana haikuwa hata na mtu aliyekuwa akiranda eneo hilo. Aliifunga gari yake vizuri kisha akazirusha hatua zake harakaharaka hadi alipofika upande wa pili wa barabara ile akiwa kama anataka kuchukua uelekeo wa duka la Kobelo. Hapa akaona pikipiki ikiwa inatoka Chumbageni kuelekea barabara za namba kupitia njia hiyo. Akaipungia mkono, dereva wa pikipiki ile akasimama na kuigeuza kisha akasogea karibu na Alan.
"Wapi bosi...?" Akauliza dereva wa pikipiki.
"Mtendele Hotel; Chuda." Akasema hitaji lake Alan.
"Utanipa buku jero tu kaka?"
"Nitakupa buku twende...!"
"Poa panda twende zetu." Alisema yule dereva wa pikipiki akaiondosha pikipiki yake akichukua njia ambayo ilikuwa kumfikisha stesheni ya reli, wakaipita barabara ya kwanza, pili, tatu na nne. Dereva wa pikipiki hiyo alipofika barabara ya nane, akaingia kulia na kuifuata barabara iliyokuwa ikielekea Chuda. Baada ya mwendo mfupi dereva yule akapunguza mwendo na kutaka kuegesha pembezoni ya baraba mbele yake kukiwa na Hoteli hiyo ya Mtendele.
"Samahani nifikishe Kwaminchi?" Alan akazungumza na jamaa akaongeza mwendo.
"Utaniongeza nauli bosi?" Akasema dereva wa pikipiki.
"Toa shaka." Alan akajibu. Punde wakawa mzunguuko wa barabara wa Kwaminchi, dereva akafanya kama anaifuata Mombasa road baada ya kupata maelezo ya mteja wake, walipolipita duka kubwa la wakala wa huduma za kipesa akasemama pembeni ya barabara. Alan akalipa shilingi elfu mbili na kumuacha dereva huyo akiondoka eneo hilo, alipohakikisha ameshafika mbali, akatembea pembezoni mwa maduka akaja kutokea kwenye kile kituo cha teksi akabana mahali na kuyasoma mazingira ya eneo hilo. Aliutafuna muda wa dakika tatu nzina hadi pale alipojihakikishia usalama hata hivyo eneo lile lilibakiwa na teksi tatu tu na mingoni mwa teksi hizo, gari ya Maisara haikuwepo. Akapiga hatua Alan huku akijiaminisha labda Maisara atakuwa amepata mteja. Aliifikia teksi moja na kufunguliwa mlango kisha akajiweka ndani yeke upande wa nyuma. Kijana mmoja akaingia upande wake na kujituliza.
"Unaelekea wapi kaka?" Akauliza yule kijana.
"Chumbageni utakwenda kuniacha barabara ya majimaji."
"Ok, hakuna shaka bosi, utanipa shilingi elfu tano." Alisema kijana huyo huku akiiondosha gari yake maegeshoni. Walipoingia barabarani, Alan akajiweka sawa kitini na kumtazama dereva yule kupitia kioo cha dereva pale mbele akamuona jinsi kijana yule alivyokuwa akijishughulisha na usukani wa gari yake.
"Gari naona ziko chache sana maskani kwenu?" Akauliza Alan huku akimtazama yule kijana.
"Yaa, ni kweli lakini si kama hazipo, zipo ila nyingi zimetoka."
"Anhaa, ila wewe ni mgeni machoni mwangu sina hakika kama uko pale kwa muda mrefu?" Yule kijana akacheka kidogo kisha akauliza badala ya kijibu.
"Mimi mbona ile ndiyo maskani yangu kaka, labda kama hukuwahi kunikuta."
"Itakuwa ni hivyo kweli...!"
"Kwani huwa unafika pale mara kwa mara?" Akawahi kuuliza yule kijana. Alan akatazama nje na kuona giza likiwa limeshamiri pia akatazama nyuma nako kulikuwa shwari.
"Yaa," akajibu na kuendelea. "Mimi ni mteja mzuri sana wa pale na huwa nilikuwa nikitumia gari ya msichana mmoja hivi machachari." Yule kijana akamtazama Alan kupitia kioo cha juu ya paa la gari yake kisha akatazama mbele. Akacheka sana. Alipokoma kucheka akasema.
"Unajua hizi kazi kaka zinataka sana moyo, yule alikuwa akiona labda wanaume tunafaidi sana hivyo akaona ajaribisshe. Kwanza sijui ile gari ilikuwa ni ya basha wake, sijui ya ukoo au ilikuwepo tu nyumbani kwao haina kazi...!"
"Kwanini? Kwani alikuwa hapati wateja?" Akakatisha Alan. Gari ile ikawa imefika misitu na kupita, ilikuwa ikiendeshwa taratibu sana.
"Si kama alikuwa hapati wateja, wateja alikuwa akiwapata vizuri tu ila hakuonekana kuwa na dhati ya kweli na hii kazi. Huwezi amini amedumu kwa muda wa wiki mbili tu ndani ya hii kazi hivi ninavyoongea na wewe ni siku ya tatu sasa hahaonekana maskani." Kauli hii ya huyu kijana ikamfanya Alan ajenge hoja nzito sana kichwani mwake kuhusiana na Maisara. Siku ya tatu sasa haonekani maskani? Yalikuwa maajabu makubwa sana na alijiuliza vya kutosha mno na jibu hakupata. Inawezekana ni baada ya kunitambua mimi mara tu nilipoongia hapa jijini ndipo akaacha hii kazi ya dereva teksi hata kama ni hivyo, iweje akubali kufanya na mimi mapenzi ikiwa alishanitilia mashaka au alishanitambua kuwa sikuwa mwema? Alijiuliza Alan. Yote hayo aliyafanya baada ya kutoka kwenye tafakuri nzito sana. Au ilikuwa ni njama yake pia ya kutaka kunijua zaidi kuwa mimi ni mtu wa aina gani? Alizidi kuwaza na alipokuwa katika harakati za kuwaza, akatazama nje, akaona akiwa anaingia barabara ya majimaji akaonelea aulize kabla dereva hajasimama.
"Kwahiyo mwanangu unataka kuniambia demu amembwela."
"Aaah! Amembwela kaka, hata hivyo hizo wiki mbili zenyewe alikuwa akisuasua hakomai kama wana alivyotukuta. Haonekanani kabisa mjini hapa bila shaka amepata doni aliyevutiwa na umbo lile si umemuona mwenyewe mtoto alivyoumbika, sasa doni akivutika si anamfungia ndani tu."
"Dah! Kweli kaka...unaposema haonekani unakosea lakini kwani yupo anayepajua nyumbani kwake au mahali anapoishi?" Akauliza Alan huku akimshuhudia dereva huyo akiliegesha gari lake pembeni ya hiyo barabara ya majimaji.
"Wapi? Muda huo wa kujua hadi anapoishi nani anao kwanza alikuwa si muwazi. Si unajua mademu ya macho juujuu kaka ni ngumu sana kueleza anapokaa anadhani kufanya hivyo ni dhambi kubwa sana. Tumekutana maskani hasa siku alipokuja kuomba kufanya kazi maskani ile basi hakuna ambaye alikuwa na muda naye...vipi kaka ulivutika nini pale maana si mchezo hata mimi ninayeongea nakiri kuwa yule mtoto alikuwa balaa...!" Alisema yule kijana na Alan akaishia kucheka tu huku akitoa waleti yake na kuchomoa noti ya shilingi elfu kumi na kumkabidhi huyo kijana.
"Wapi? Muda huo wa kujua hadi anapoishi nani anao kwanza alikuwa si muwazi. Si unajua mademu ya macho juujuu kaka ni ngumu sana kueleza anapokaa anadhani kufanya hivyo ni dhambi kubwa sana. Tumekutana maskani hasa siku alipokuja kuomba kufanya kazi maskani ile basi hakuna ambaye alikuwa na muda naye...vipi kaka ulivutika nini pale maana si mchezo hata mimi ninayeongea nakiri kuwa yule mtoto alikuwa balaa...!" Alisema yule kijana na Alan akaishia kucheka tu huku akitoa waleti yake na kuchomoa noti ya shilingi elfu kumi na kumkabidhi huyo kijana.
SONGA NAYO....
"Vipi nizuie yote nini...!"
"Aah! Wapi kaka, hali ngumu sana bwana hata hivyo tunasafiri kigumu tu tufanyeje." Akajibu Alan. Wakacheka na kuagana baada ya yule kijana kurudisha kiasi kilichobakia na kuondoka. Alan alipohakikisha kijana yule ameondoka naye ndipo akanyoosha na hiyo barabara hadi mbele kidogo ambapo aliliacha gari lake. Akalikagua akiwa mbali na alipohakikisha hakukuwa na mtu ndipo akalifuata na kuingia ndani yake. Sasa alikuwa na uhakika kuwa Maisara hakuwa mtu mzuri kwake na pengine akaanza kumjengea mashaka makubwa na prngine ndiye anayemuandama mjini hapo. Akaondoka na kuranda mji akijitafutia mgahawa mzuri kwa ajili ya kupata chakula.
__________
Wakati Alan akiwa anazidi kutafuta mahali pa kuweza kujipatia chakula, upande mwingine wa shilingi hali ilikuwa iko katika utulivu wa kipekee sana. Hapa palikuwa ni pale pale ambapo watu wale walipenda kukutania hata hivyo hakukuwa na watu wengi kama ilivyozoeleka. Watu walikuwa wawili tu pekee. Alikuwapo yule bwana mwenye kupenda kuchonga ndevu zake kwa mtindo wa 'O' bwana nadhifu; Mohammed Saloom akiwa na mzee Zayd Aboushariff. Walikuwa hapa wakisubiri taarifa mbili muhimu ya kwanza ikiwa ni ya kuhusiana na vijana watatu waliotumwa kumfuatilia mtu ambaye waliambiwa kuwa anaweza kuwa si salama kwenye mipango yao. Na ya pili ikiwa ni ya Dokta Richard Bango ikiwa inamhusu muuguzi Zaituni ambaye alikuwa ameonekana akimfuatili yule mgonjwa aliyekuwa amelazwa kule Hospitali. Walikuwa wakipiga soga za kawaida huku wakinywa mvinyo ghali sana taratibu mno. Muda wa dakika thelathini ulishakatika tangu kuwa kikaoni hapo na wote wawili walikuwa wamesitisha zoezi lile na kunywa mvinyo kwa kuogopa kulewa. Wakawa wanaendelea kusubiri kwa maongezi ya hapa na pale. Muda mfupi mbele, mlango ukagongwa mara mbili kisha mgongaji akatulia. Akagonga tena mara moja na kuufungua mlango. Alikuwa ni yule jamaa njorinjori; Mathew Bangile. Akatwaa nafasi akaketi. Akawatazama mabwana wale usoni kwa kitambo kidogo huku Mohammed akimmiminia Mathew ule mvinyo.
"Hakika lile kontena si salama na lina bidhaa sumu sana ndani yake hata hivyo tuliweza kuliangamiza kwa haraka mno...!" Akasema Mathew, kusema kwake kule kukasababisha Mohammed kusitisha lile zoezi la kumimina ule mvinyo na kumtazama moja kwa moja usoni. Mathew akaendelea.
"...Ua tulilokuwa tumelipandikiza sehemu moja hapa mjini kama ambavyo niliweza kuwasiliana na ninyi ni kwamba liliweza kugundua nyuki ambaye hasa alikuwa akitegemewa kunasa hata hivyo si nyuki wa kutengeneza asali ya kawaida kama ambavyo tulidhania. Nyuki yule anatengeneza asali yenye sumu tena walaji wa asali hiyo tukiwa ni sisi wenyewe...!"
"Unamaanisha nini Mathew ukisema hivyo?" Akauliza kwa kudakia Zayd.
"Maria akiwa hospitalini Bombo akiwa kama mfuatiliaji wa kila kinachoendelea pale, akaweza kugundua kontena hili ambalo tulidhani...!"
"Hebu fafanua sasa maana naona hatari ilivyo acha mafumbo...!" Alifoka Zayd.
"Maria alimgundua muuguzi mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye lile jengo la Cliff na mwanzoni kwa maelezo yake alidhani yule muuguzi si mbaya hata hivyo baada ya kutokea lile tukio la mgonjwa kuuawa ndipo hisia zake zikampa majibu kuwa yule hakuwa muuguzi mzuri. Taarifa zile akafikishiwa mwenzetu Dokta Richard kuhusiana na tabia ya muuguzi wake Dokta akasema kuwa hilo halina shaka na atalifanyia kazi mapema sana. Hivyo mchana wa leo hii amefanikiwa kumuondoa duniani yule muuguzi kwa kumvamia nyumbani kwake na alifika wakati mvua ikiwa inanyesha. Ni rahisi sana maana wati akiwa anaingia alimkuta huyo binti akiwa anaelekea bafuni kuoga, nadhani mnaona jinsi ilivyo rahisi tena bila kelele." Akaweka hitimisho mwishoni mwa kauli yake akawatazama tena wale mabwana.
"Hiyo si mbaya enhee! Taarifa ya Maisara?" Akauliza Mohammed Saloom. Yule jamaa njorinjori akajiweka sawa na kusema;
"Nyuki yupo na ameshaanza kutengeneza asali kwa kuyatumia maua tuliyoyapandikiza...!"
"Aaah! Hizi ni dharau...hizi ni dharau Mohammed yaani ameshaanza kula uroda na watu wetu na hakuna tulichokifanya hadi sasa...!" Alifoka kwa sauti ya juu kabisa Zayd huku akiuegemeza mgongo wake kitini kwa nguvu sana hata hivyo yule njorinjori akamuwahi.
"Hapana si hivyo mkuu, Maisara amefanikiwa kumtambua yule jamaa na haikutosha kumtambua kwa kumhisi tu bali akaamua kumtumia watu wamuangamize kabisa kwa kuwa kawaida ya Maisara hatoi penzi lake bure na pia kupitia watu hao aliowatuma alitaka kujihakikishia kama kweli mtu huyo ni nyuki husika ama la! Amefanikiwa lakini bahati mbaya ni kwamba watu waliotumwa hakuna aliyerudi na taarifa muhimu hata mmoja...!"
"Unamaanisha nini?" Akauliza Mohammed Saloom.
"Wale jamaa waliotumwa hakuna hata mmoja aliyerudi nikiwa na maana kuwa wale jamaa wameuawa." Kimya kikagonga kila kona ya chumba kile na kuwatazama mabwana hao walivyokuwa wakitazamana wenyewe kwa wenyewe kama mapaka shume. Kama isingelikuwa Mathew Bangile kuuvunja ukimya ule, hakika hakungekuwa na wa kuzungumza.
"Jamaa hajulikani alipo hadi sasa huwezi amini." Akasema.
"Hii ndiyo tabia ya wapelelezi wa Tanzania Mathew, ni waoga sana hata hivyo woga wao unamadhara makubwa sana maana hujui wataibukia wapi, lini na saa ngapi, mimi nawajua sana hawa." Akasema Zayd Aboushariff kisha akaendelea baada ya kujipa utulivu wa muda mfupi.
"...kuweni makini sana Mathew na huyu mtu ambaye tayari madhara yake mmeweza kuyaona...au hamjawaona kabisa watu mliowatuma?"
"Hapana, watu wale tuliwafuatilia kule walikokuwa wakimfuatilia yule jamaa hadi tulipofika eneo la viwandani ambako ndiko mapigano makali yalikoibuliwa. Wawili walichabangwa risasi lakini mmoja alichezea kichapo kikali kabla ya kuuawa kikatili sana."
"Umeona sasa? Hakikisha unamwambia Maisara awe makini na huyu mtu na amfuatilie kwa uangalifu mkubwa najua hajamuwekea alama yoyote ya ufuatiliji bali ameshajua anamfuatilia mtu wa namna gani kupitia wale watu aliowatuma kama alama yake, tunataka akishajua alipo kisha atoe taarifa kwako popote pale atakapomuona, najua atakuwa na hasira naye sana kwa kuwa amegundua kuwa ni adui ikiwa tayari ameshakula uroda wake. Asizitumie hasira zake kwa pupa awe makini zaidi. Ningependa sana nimuite hapa ili nimuulize kwanini hakumuua hapo hapo alipomhisi vibaya hata hivyo inatosha wewe kumpelekea hizi taarifa. Akasema Zayd kisha akaendelea.
"...ni hatari sana na sijui ni nani huyo mpuuzi anayevivuruga vichwa vyetu mapema namna hii. Wacha niwasiliane na Bango ninyi endeleeni kufanya kazi yenu na mtafika hapa kama kutakuwa na kazi nyingine ya ziada."
"Sawa mkuu." Akajibu Mathew na kusimama kisha akaondoka kwa mwendo wa kawaida akaufikia mlango na kujitoa kabisa nje.
"Haloo Dokta!" Aliita Zayd Aboushariff mara baada ya Mathew kutoka mule ndani. Simu ya upande wa pili ikapokelewa na mzungumzaji akaitika salamu.
"Safisha Bango, safisha...mpeleke huyo mzee KB na ikiwezekana umuue maana hana faida kwetu zaidi ya hasara na nilikuambia mapema mimi kuwa huyo mzee usipende kufanya kazi akiwa yupo ukasema hana madhara. Mimi najua tu huwenda kuna jambo analijua ila anajifanya ni mlevi asiyejielewa...!" Akaongea kwa kirefu Zayd na kusikiliza upande wa pili wa simu. Upande wa pili wa simu ukaafiki suala lile na mazungumzo yale yakafika tamati. Zayd akaweka simu kwenye kikalio chake na kumtazama Mohammed Saloom usoni.
"Inabidi kesho usafiri hadi Nairobi ukawape hawa jamaa hii taarifa kuanzia mwanzo hadi mwisho ikiwezekana wawe macho au hata wafanye jambo jingine la kuwashtua watu wao hatari wajiandae maana tayari mambo yanaelekea kubaya. Hii ndiyo Tanzania Saloom. Nchi hii mimi naijua nimeishi humu takribani miaka ishirini na tano, naijua nyama yake ya nje na utumbo wake. Ina wapelelezi na majajusi wabaya sana ambao wapewapo kazi huwa hawafanyi makosa hata kidogo na wengi wa majasusi wa nchi hii ni kama wafu wafanyao kazi kama mizimu unashtukia tu wamekuibukia chumbani ukiwa unavaa chupi, unadhani kuna kupambana hapo kama siyo kupakatwa kama mtoto wa kike na kuulizwa unataka huduma gani na ukilegea unalawitiwa kweli! Alaa...! Tusitoleane macho tu hapa tukasubiri hizi mimba zisizotarajiwa zitufikie? Ni muda wa wanaume wenzao kuingia kazini sasa na kuwaonesha ubabe."
"Nitafanya hivyo inabidi nitoe taarifa ya kuandaliwa nafasi ndegeni ili jimbi la kwanza litakapoinadi afajiri basi niwe angani." Alijibu Mohammed kisha kikao kile kikafika tamati na kila mmoja akaondoka wakiiacha nyumba ikiwa pweke.
___________
Ilikuwa yapata saa tatu na dakika ishirini na tatu, muda huu Alan alikuwa maeneo ya barabara ya kumi na tisa akiwa kwenye mwendo wa taratibu sana. Hakuwa akitumia gari kwa majira hayo na ni baada ya kutoka kulituliza tumbo angalau, mikono yake ilikuwa mfukoni huku akiwa haachi kuangalia nyuma kila wakati kutazama kama kulikuwa na mtu aliyekuwa akimfuata. Alipofika kwenye kituo cha mafuta ambacho kilikuwa kikitazamana na kituo cha mabasi madogo mjini, akataka kuvuka barabara kama atakaye kuingia ndani ya kituo kile lengo lake likiwa ni kupanda na hii barabara ya kumi na mbili. Akiwa hajafanya amuzi hilo, upande wa mkono wake wa kushoto sehemu ambayo kulikuwa na saluni ya kike na dula la vifaa vya shule, akamuona mtu mmoja akiwa anachepuka kutokea nyuma ya ile saluni akitokea kwenye uchochoro mmoja wa jengo moja na jingine. Mtu huyu alimtilia shaka hata hivyo hakuonesha kama aliogopa, akatupa hatua zake kuivuka barabara hii ya upande aliopo ili kuendelea na safari yake.
Alipofika kwenye kituo cha mafuta ambacho kilikuwa kikitazamana na kituo cha mabasi madogo mjini, akataka kuvuka barabara kama atakaye kuingia ndani ya kituo kile lengo lake likiwa ni kupanda na hii barabara ya kumi na mbili. Akiwa hajafanya amuzi hilo, upande wa mkono wake wa kushoto sehemu ambayo kulikuwa na saluni ya kike na dula la vifaa vya shule, akamuona mtu mmoja akiwa anachepuka kutokea nyuma ya ile saluni akitokea kwenye uchochoro mmoja wa jengo moja na jingine.
SONGA NAYO....
Mtu huyu alimtilia shaka hata hivyo hakuonesha kama aliogopa, akatupa hatua zake kuivuka barabara hii ya upande aliopo ili kuendelea na safari yake. Akageuka tena kwa kasi Alan kabla hajaivuka baraba ya taifa hata hivyo hakutaka kumuonesha adui kama alimshtukia. Hapa akajikuta anakumbwa na hofu kubwa kwani hakuwa yule mtu pekee bali kuliongezeka mwengine mmoja na huyu alikuwa ni mwanamke. Muda huu bado pitapita ya watu ilikuwa kubwa lakini isingemfanya Alan aamini kuwa alikuwa salama. Akavuka barabara ya taifa kwa haraka na kuingiaya upande wa pili pia akiliwahi gari lililokuwa likitaka kupita. Alikuwa yuko kwenye barabara hii ya kumi na mbili akiwa anatembea kwa mwendo wa kasi kidogo. Alipogeuka nyuma tena aliwaona wale watu wakiwa wanamfuata huku wakimuangalia. Walivaa majaketi meusi huku kila mmoja akiwa ameutia mkono wake mmoja kwenye mfuko wa jaketi. Hawa watu si salama sitakiwi...sitakiwi kabisa kujiaminishia usalama. Aliwashangaa sana watu hawa kwani hakuwaona tangu alipokuwa akitokea barabara ya kumi na tisa ambako kulikuwa na mgawahawa wa kawaida ambao yeye aliutumia kujipatia chakula. Kwanini watu wale waibuke ghafula tena sehemu asiyoitarajia na si kule alikotokea. Akawaza Alan huku akiongeza maradufu kasi ya mwendo wake. Alikuwa anauvuka msikiti uliopo karibu kabisa na kituo cha mabasi zamani na sasa ni kituo cha daladala ili kuingia kwenye soko la Ngamiani. Upande huu ulikuwa umepoa sana hakukuwa na mishemishe za watu kama ilivyo kwa hili eneo la kituo cha mabasi madogo. Hapa akawaona wale watu wakiwa wamemkaribia kwa kiasi kikubwa na sasa walikamatia bastola zao mikononi. Alan akaanza kukimbia na kuivuka ile barabara akawa anapita kandokando ya soko la Ngamiani, hawa watu huku nyuma nao wakawa wameongeza kasi. Alan alikimbia hadi alipofika mwisho wa soko la ngamiani hata hivyo hakuivuka barabara ya Jamaa akakunja upande wa kushoto. Alitaka kuwapoteza hapahapa sokoni kwani maeneo haya ya hili soko ndipo aliweza kuiacha gari yake akiwa anataka kwenda kupata chakula. Hii ndiyo ilikuwa tabia yake, hupenda kuliacha gari umbali mrefu ili kusiwe na mtu wa kumtilia shaka. Alipofika mwisho wa upande wa kaskazini mwa soko lile akawa na lengo la kunyoosha na ile barabara ili atokee nyuma ya Hoteli ya Maua Inn hata hivyo wazo hilo akapingana nalo kwa kuwa kuanzia pale alipo hadi kufikia kwenye jengo jingine kulikuwa wazi sana na taa zilikuwa zikiangaza eneo kubwa. Alikuwa kwenye hatari kubwa sana na hakuona njia ambayo ingeweza kumuweka mbali na hatari ile, alijibana ndani kidogo ya lile soko alibana pumzi zake huku akiwa macho kutazama kila upande ili kuona wale watu watatokea upande gani. Akatazama kule alikotokea akaona kukiwa kumepoa sana hata hivyo hakujiaminisha usalama, alipoangalia upande wa mbele nako kulikuwa kimya. Akageuka tena upande wa nyuma kwa haraka sana ndipo akawaona wale jamaa wakiwa wanasogea taratibu silaha zao zikiwa mikononi. Damu zilimuenda mbio sana hofu ikiwa juu, pale alipo hapakuwa na nafasi kubwa ya kuweza kumficha na asiweze kuonekana. Wale jamaa walikuwa makini sana kwani walikuwa wakipekua kila mahali na kila hatua waliyokuwa wakipiga walihakikisha wanatazama kwa umakini wa hali ya juu. Hawa ni akina nani? Akawaza Alan. Akafikiria namna ya kuweza kuwakabili na kupambana nao, haikuwa shida sana kuwashambulia kwa risasi hata hivyo hakuona kama ule ulikuwa ni wakati muafaka zaidi alitaka kujua kwanini wanamfuatilia na wametumwa na nani. Akatazama upande linakozamia jua pembeni kidogo ya kituo cha kujazia mafuta cha mahali hapo. Akaliona gari lake likiwa palepale. Akageuza shingo kwa upande ule ambako wale jamaa walikuwako, bado walikuwa mbali. Akatabasamu na kuona hakuna namna zaidi ya kuwaacha kwenye mataa. Alinyata akirudi nyuma nyuma hadi alipofika umbali fulani ndipo alipoanza kukimbia na kuliwahi gari lake akaingia mara baada ya kulichunguza akaliwasha na kuteremka na barabara ya kumi na moja. Haukuwa utaratibu wa kiuendeshaji lakini hakuwa na namna nyingine zaidi ya kufanya vile na kwa kuwa kulikuwa hakuna gari inayopandisha, ikawa rahisi kwa yeye kuweza kuondoka pasipo kuwa na shaka lolote.
Alan alinyanyua mkono wake uliobeba saa akajikuta ametumia muda mrefu sana kinyume na matarajio yake hata hivyo hakujilaumu sana kwa kuwa alilipoteza kabisa lengo la wale jamaa. Japo alijiuliza kuhusiana na wale watu kuwa ni akina nani na kwanini wamekuwa wakimfuatilia kwa kiasi kile. Hakuwa na jibu la haraka hadi pale alipokumbuka kauli ya wale watu wa kwanza ambao aliwaangamiza kule kwenye lile eneo la viwandani. 'Tumetumwa tukuangamize' haya ndiyo maneno ya wale watu. Hapa akajua fika kuwa yuko kwenye hatari isiyoweza kuelezeka na hata hao pia watakuwa wametumwa kama walivyotumwa wale ingawa hakumjua mtu aliyewatuma ni nani. Alifanikiwa kuwakimbia maadui zake na huku nyuma, wale jamaa walitafuta hadi wakakubali kuwa waliachwa kwenye mataa. Sasa akaliendesha gari lake kwa kasi sana barabarani akiwa kwenye barabara ya Bombo Hospitali.
Alan alikuja kuegesha gari yake nje ya uzio wa Hospitali ya Bombo, alikuwa ni kama aliyekuwa akielekea Raskazone. Kulikuwa kumepoa sana maeneo haya na hakukuwa hata na gari moja iliyokuwa ikikatiza hili eneo, mawimbi makubwa ya bahari yaliyokuwa yakipiga ufukweni ndiyo yaliyokuwa yakisikika kwa wakati huo mbali na hayo mawimbi, kilichokuwa kikisikika kingine ni wadudu wa usiku na si zaidi ya hivyo. Hakutoka kwa haraka ndani ya gari yake Alan, bado alikuwa akitazama usalama wa eneo lile kama unaridhisha. Alipojihakikishia hilo ndipo aliteremka na kuufunga vizuri mlango wa gari yake kisha akaliacha lile gari taratibu na kuingia kichakani akiambaa pembezoni mwa uzio ule wa Hospitali. Giza lilikuwa zito na kulitisha sana. Alan hakuwa akitumia kurunzi ya aina yoyote kwa kuhofia kuweza kuonekana kwa wepesi na watu waliyoko ndani ya uzio ule hivyo alikuwa akitumia hisia kali sana hasa wakati akiwa anakanyaga chini. Alitembea huku ile hali ya woga ikiwa imeanza kumnyemelea tena kwani mahala alipokuwa akipita kulikuwa ni kwenye vichaka na miti iliyofungamana kwa kiasi kikubwa sana. Chini ya miti ile kuliweka giza nene hata hivyo hakurudi nyuma. Akili yake ilikuwa ikimfikiria mtu ambaye alikuwa akimfuatilia muda ule na aliapa kama angefanikiwa kumkuta basi ilikuwa ni lazima aeleze ukweli kuhusiana na uvamizi ambao ulifanyika nyumbani kwa Zaituni na kusababisha mauaji ya binti mdogo asiye na hatia yoyote. Alikuwa akipita karibu kabisa na jengo la kuhifadhia maiti hapa akaongeza kasi mara baada ya kupata nafasi nzuri ya kutembea kwani hapakuwa pamefungamana sana. Alifika nyuma ya lile jengo la Cliff akalipita hadi alipokuwa nyuma ya lile gofu ambalo hasa ndilo alilokuwa akilikusudia. Akachungulia kwa upande wa ndani hakukuwa na kelele wala watu wa aina yoyote. Hakukuwa na magari mengi nje ya ofisi ambayo kwa maelezo ya marehemu Zaituni alisema kuwa ofisi ile ndiyo iliyokuwa ikitumiwa na mganga mkuu. Kulikuwa na gari moja tu ambayo ilikuwa imeegeshwa eneo hilo la kuegeshea magari. Akiwa anajiandaa kuurukia ule ukuta kwa lengo la kuingia ndani, akasikia mchakacho wa kama mtu apigaye hatua nyuma yake. Nywele zikamsimama na damu kumsisimka mwilini mwake. Woga ukamuingia na kuuhisi mwili wake ukipatwa na baridi kali mno. Akatega sikio kwa umakini mkubwa ili kuweza kuzisikia hizo hatua. Hatua zilikuwa hazipigwi tena. Akazipuuzia na kuamua amuzi lake na kuuparamia ule ukuta hata hivyo hakufikia maamuzi hayo kwani ule mchakacho ulirejea kwa mara nyingine na kumsababisha Alan kujipapasa kiunoni kwa haraka sana na kuikamata vema bastola yake huku hofu ikimvaa kwa kiasi kikubwa sana. Alipogeuka nyuma hakuona tena kitu zaidi ya giza nene lililokuwa limetanda. Akatumbukiza mkono mfukoni na kutoa kurunzi yake ndogo ya kijasusi ambayo ilikuwa na mwanga mwembamba na mkali sana. Akamulika. Hakukuwa na kitu cha kuogopesha kulikuwa kweupe kabisa. Akatabasamu kwa kujilazimisha kwani aliona wazi kuwa pale woga tu ndiyo uliokuwa umemtawala kiasi cha kufikia hatua ya kujitisha mwenyewe. Aliirudisha kurunzi ile mahala pake na kuudandia ule ukuta akauparamia na kudondokea upande wa ndani. Alikimbilia ndani ya lile gofu kwa upande wa nyuma huku akiwa ameinamia kiunoni mithili ya namba saba. Alipofika upande wa ndani wa lile gofu aliamua kuitoa kurunzi yake na kumulika kila mahali alikokuwa akipita mule ndani. Kimya kilikuwa kikuu sana hadi kulifanya jemgo lile kutisha. Aliingia mlango mmoja baada ya mwingine akiwa makini na kile alichokuwa akikifanya. Jengo lile lilionesha kuwa kubwa sana, lilibeba vyumba vingi hata hivyo juu halikuwa na paa lolote lilikuwa wazi kabisa. Wingu zito lilikuwa limetanda angani huku mara chache mwanga mkali wa radi ukimulika, aliamini muda wowote mvua kubwa ingenyesha mara baada ya ile iliyopiga mchana kukata kwa takribani madaa matatu nyuma. Hali hii ilimfanya kusitisha kutumia kurunzi ile tena na badala yake akawa anatumia ule mwanga ambao kila baada ya sekunde kumi na tano umekuwa ukiwaka. Alipita kwenye kila chumba huku bastola yake ikiwa mkononi, akakatiza korido hii na ile hadi akaja akatokea upande wa mbele wa lile jengo hata hivyo hakusubiri ule mwanga wa radi umkute akiwa sehemu ya wazi. Alan alinyata kwa kasi kidogo hadi akaweza kujibana kwenye ukuta wa jengo lile ambalo lilikuwa likitumika. Hadi hapo alipofikia hakuwa ameona kitu chochote mule kwenye lile gofu ambacho kingemdhihirishia kuwa kulikuwa na makutano ya watu ya mara kwa mara, alidhamiria kuingia ndani ya lile jengo linatukika kama ofisi sasa. Ndani ya chumba kimoja taa ilikuwa inawaka hasa upande ambao yeye yupo, upande wa mbele wa hilo jengo taa zilikuwa zikiangaza kwa kiwango kikubwa sana kiasi kwamba ingekuwa ni vigumu sana kupita pasipo kuonekana. Gari ile aliyoiona haikuwa umbali mrefu kutoka mahali alipo hivyo ingekuwa ni rahisi zaidi kulitumia hilo gari kujifichia kuliko kutumia njia nyingine. Akanyata na ukuta huku akijificha kwenye maua machache ya eneo lile hadi alipotokea pale kwenye gari. Akatazama ndani ya ile gari kwa shida kidogo kutokana na kutokuwepo kwa taa iliyokuwa ikiwaka ndani ya lile gari hata hivyo aliweza kuona. Kulikuwa hakuna kitu cha aina yoyote ndani ya gari hiyo aina ya Vitiz, akatazama kwenye lile jengo akiwa ameigamia kwenye lile gari hapa akaona vyumba vitatu vikiwa vinawaka taa. Akatafakati namna ya kuweza kuingia na kufanya upekuzi kwenye ofisi moja na nyingine. Aliyakumbuka maneno ya marehemu Zaituni kuwa ofisi ya mwisho ambayo ilikuwa ikipakana na lile gofu ndiyo iliyokuwa ikitumiwa na Mzalendo hata hivyo ofisi ya mganga mkuu ilikuwa karibu zaidi na ya Mzalendo kiasi cha kwamba kila kitu alichokuwa akikifanya Mganga mkuu ilikuwa ni rahisi kuonwa na Mzalendo. Hakuwa na shaka kuwa asingemkosa mzee huyo kwani sababu ya kuitwa Mzalendo ni kutokana na ufanyaji kazi wake wa muda mrefu. Alinyata kulikakabili lile jengo mara baada ya mwanga mkali wa radi kuwaka huku nguruko nyepesi ya usiku ikifuatia. Baada ya mwanga huo kilichokuwa kikibaki angani ni giza zito la wingu lililotanda. Akausukuma mlango Alan mara baada ya kuukaribia, mlango haukuwa umefungwa. Akazama ndani taratibu huku silaha yake akiwa ameifutika mafichoni, alikutana na ofisi moja ambayo ilikuwa na vifaa vya uchapaji, utoaji wa nakala na kadhalika. Akajua hii ilikuwa ni ofisi ya katibu muhtasi. Hakupata shida kuichunguza sana, akaipita na kuelekea mlango uliopo upande wa kulia ambao ndiwo uliokuwa ukimpeleka kwenye chumba cha Mzalendo nako kulikuwa kutupu. Akachanganyikiwa huku akijiuliza kichwani mwake nini kimetokea hadi mzee huyo asiwepo hapo na ikiwa aliambiwa kuwa ni lazima awepo hasa kwa majira hayo ambayo yalikuwa yakikimbilia saa nne na nusu. Ofisi hii ilikuwa ni ya kawaida sana na haikuwa na vitu vingi. Kulikuwa na meza ya mraba moja na viti viwili kimoja cha kiofisi na kingine kikiwa cha mteja. Juu ya meza kulikuwa na karatasi nyingi na mafaili matatu, Alan akafunua faili moja baada ya jingine na kuona hakukuwa na ziada yoyote zaidi ya maelezo tu ya kidaktari. Akaachana nayo na kuitazama ile ofisi vizuri. Ikuwa na rafu moja ya kuhifadhia vitabu vya kitabibu na mafaili mbalimbali pembeni ya rafu ile kulikuwa na kalenda hata hivyo upande mwingine wa ukuta kukiwa na picha ya Rais wa Tanzania akiwa kwenye tabasamu safi kabisa. Kila alipojaribu kuitathmini ofisi ile aliona namna ambavyo kwa siku hiyo nzima huwenda haikuwa imekaliwa na mtu kwani hakukuwa na utumikaji wowote. Akahamishia uchunguzi wake kwenye droo mbalimbali akianzia kwenye ile rafu hadi kwenye meza, nako hakuna alichoambua zaidi ya kutoa makaratasi na kalamu nyingi zisizo na idadi. Alichoka Alan, alichoka akili kwa kiwango cha juu sana na alijiona ni mtu wa kupoteza wakati kwani hakupenda kabisa kumkosa Mzalendo ambaye kwa namna moja ama nyingine angekuwa anapajua hata nyumbani kwa mganga mkuu. Akiwa pale kwenye kiti cha kiofisi akitafakari namna ya kufanya, akasikia hatua za viatu zikiwa zinaingia ndani ya lile jengo kutokea nje. Akasikiliza kwa umakini kabisa akapata kujua hatua hizo hazikuwa za mtu mmoja. Kadiri alivyokuwa akisikia ndivyo alivyojipa uhakika kuwa watu hao walikuwa wakiingia kwenye ofisi hiyo aliyopo yeye. Haraka na kwa kasi ya umeme ya bila kelele alijitoa pale kitini na kwenda kujificha nyuma ya ile rafu ya vitabu na mafaili akatulia kimya huku akichungulia kwa uchache ili kuona watu hao ni akina nani. Alikuwa ni mwanamke na mwanaume na wote wakiwa wamevaa sare za kiuguzi. Manukato yenye rihi kali yalizisurubu pua za Alan na akajua fika mwenye kupata manukato hayo alikuwa ni yule wa kike. Walipofika kwenye ile meza walionekana wakifungua droo hii na ile na kutoa makaratasi na kuyaangalia kama waliokuwa wakitafuta jambo fulani. Yule wa kike akasogea hadi kwenye ile rafu na kuangalia kitabu hiki na kile mara faili hili na lile, hapa Alan ndipo alipojihakikishia kuwa yule msichana ndiye aliyejipulizia manukato yale kwani aliweza kukutana na ile harufu kwa ularibu zaidi. Alan akaongeza kujificha kwake mara dufu huku akiendelea kuchungulia kwa uchache. Akatoka na faili moja yule mwanamke ambalo lilikuwa upande wa chini.
"Ofisi hii huwenda isipate mtumizi kwa muda kidogo." Yule wa kike akasema. Alan akamtazama vizuri akamuona kwa usahihi na kuvuta picha ni wapi alipata kumuona huyo mwanamke. Ilikuwa si vigumu sana kuweza kukumbuka kwani haikuwa ni siku nyingi na alipata kumuona usiku huo huo na ni wale waliokuwa wakimkimbiza kule mjini.
Walipofika kwenye ile meza walionekana wakifungua droo hii na ile na kutoa makaratasi na kuyaangalia kama waliokuwa wakitafuta jambo fulani. Yule wa kike akasogea hadi kwenye ile rafu na kuangalia kitabu hiki na kile mara faili hili na lile, hapa Alan ndipo alipojihakikishia kuwa yule msichana ndiye aliyejipulizia manukato yale kwani aliweza kukutana na ile harufu kwa ularibu zaidi. Alan akaongeza kujificha kwake mara dufu huku akiendelea kuchungulia kwa uchache. Akatoka na faili moja yule mwanamke ambalo lilikuwa upande wa chini.
"Ofisi hii huwenda isipate mtumizi kwa muda kidogo." Yule wa kike akasema. Alan akamtazama vizuri akamuona kwa usahihi na kuvuta picha ni wapi alipata kumuona huyo mwanamke. Ilikuwa si vigumu sana kuweza kukumbuka kwani haikuwa ni siku nyingi na alipata kumuona usiku huo huo na ni wale waliokuwa wakimkimbiza kule mjini. Hapa akapata uhakika kuwa huwenda hawa watu walikuwa na ushirikiano mkubwa sana na mganga mkuu.
"Hivi Mzalendo alikuwa na madhara kiasi gani hadi wampeleke Kibaranga shimoni?" Yule mwanaume akauliza baada ya kauli ya yule mwanamke. Kimya kidogo kikapita kutokana na yule mwanamke kuwa alikuwa akisoma lile faili.
"Mzee yule alikuwa makini sana na kuna muda alimuuliza bosi nini sababu iliyokuwa ikimpeleka ndani ya hili gofu usiku wa saa saba, saa nane."
"Alaah...! Na bosi alikuwa akimjibu nini?"
"Alikuwa akimjibu kimasikhara hata hivyo akiwa na umakini mkubwa moyoni mwake kupitia mswali yale. Alikuwa akimwambia apunguze pombe ambazo alikuwa akizinywa hadi usiku na pombe zenyewe zikiwa ni kali sana za kienyeji."
"Kweli alikuwa akimjibu kiutani sana hata hivyo kama asingemuondoa hapa na kumpeleka huko huwenda angekuwa na madhara makubwa sana kwetu. Wacha akataabike kwa muda huko kwenye magofu ya mamlaka ya mkonge." Akasema yule mwanaume. Yule mwanamke alipotaka kuongeza kitu, akasita mara baada ya simu yake kuita.
"Eenh! Bosi," akaitikia simuni baada ya kuipokea. Akaweka tuo kusikiliza upande wa pili kisha akaendelea.
"...hakuna kitu tumejaribu kuangalia sehemu zote ulizozitilia shaka hakuna...!" Akasikiliza tena halafu akasema;
"...sawa hakuna shaka, tunaondoka muda huu kwani bado tuna hamu kubwa usiku huu wa kuhakikisha tunafanikisha kimoja wapo...!" Alipozungumza hivyo, akaishusha simu kutokea sikioni na kulibeba lile faili na kulirudisha mahali alipolitoa na kurudi pale mezani.
"Nadhani ni ofisini kwake na ametoa maagizo ya kutokupoteza muda kabisa hili eneo." Akasema yule wa kike kumwambia yule mwanaume. Yule mwanaume akatoka na yule mwanamke akakusanya baadhi ya karatasi na kutoka hata hivyo kuna kipande cha karatasi kutoka katikati ya zile karatasi alikidondosha chini. Alan akakiona na kukitamani, alipohakikisha watu wale wametoka na kupotelea kwenye ofisi nyingine, akatoka pale mafichoni na kukiokota kile kikaratasi. Kilikuwa kimechorwa Ua kama ilivyo kwa kile ambacho alikiona kwenye jengo la Cliff wakati akifanya upekuzi wake. Lilikuwa ni lile lile la Bee Balm. Inamaana hawa mabinti wapo wangapi kwenye hiki kikosi na kwanini wanatumia utambulisho mmoja? Akawaza Alan akiwa amekikamatia kile kipande cha karatasi mikononi mwake. Hakika hawa watu ni hatari sana sasa nimegundua kitu kuwa haya ndiyo maua ambayo yamepandizwa mitaani ili waweze kumnasa nyuki wanayemzungumzia hasa kwenye maongezi yao. Alizidi kuwaza Alan. Akiwa hapo anawaza akasikia tena hatua za miguu zikitokea chumba kimoja. Akakimbilia mlangoni pale na kutega sikio, akawasikia wakipita na kupotelea nje. Alikimbia dirishani na kutazama upande wa nje akawaona wakitoka kwa mwendo wa miguu wakikatiza kwenye jengo la Cliff na kuifuta njia anbayo ilikuwa ikiwapeleka katikati ya majengo yale ya Hospitali. Alan hakupoteza muda hata kidogo alitoka mule ndani na kuingia kwenye ofisi ambayo wale watu walitoka. Ilikuwa ni ofisi kubwa iliyosheheni vitu vingi sana na ilikuwa ni ya kipekee mno. Akatazama kwenye kiti kile cha kuzunguuka akapekuwa droo na sehemu mbalimbali hata hivyo hakuna alichoambulia. Akatoka akiwa ameliacha lile Ua la Bee Balm mezani kwa mganga mkuu na kutoka huku akitembea kwa haraka akiufuata uelekeo walioelekea wale watu hakutaka kujificha tena na kurudi na njia ile aliyojia na badala yake alikuwa akijichanganya na wafanyakazi wa Hospitali ile. Alinyoosha moja kwa Moja Alan hadi alipokuja kutokea mahali wanapopumzikia wagonjwa na wauguzi wao hasa nyakati za mchana ama usiku kama huo pia walikuwapo wale ambao walikuwa wakilala hapo kwa ajili ya wagonjwa wao. Alikuta watu wengi wakiwa wamejilaza wake kwa waume. Akapita na kuifuata njia iliyokuwa ikielekea kwenye jengo la kuhifadhia maiti. Hakutaka kuonekana na mlinzi wa huko hivyo alichokifanya ni kutazama mlinzi alipo na yeye kupita upande mwingine na kufika kwenye uzio wa ukuta wa Hospitali, akaambaa na huo ukuta hadi alipofika mahali ambapo ndipo alipenda kupatumia kurukia. Akaruka na kunguakia nje. Akatoka hapo kichakani na kulikaribia gari lake. Akalikagua kwa mbali kabla hata hajalikaribia kabisa. Kimya kilikuwa kikuu na usalama ulikuwepo hivyo akalisogelea na kuingia ndani yake akaliwasha na kuondoka. Alikuwa akirudi na barabara hii hii ya Hospitali hadi alipofika kwenye mataa ya darajani ndipo akaingia upande wa kulia huku kichwani mwake akiwafikiria wale watu waliokuwa wakimfukuza katikati ya mji hadi kufikishana nao kwenye soko la Ngamiani ambapo aliwaacha kwenye mataa. Baada ya kumbukumbu ile kupita akaibua nyingine nayo ilikuwa ikiwahusisha hao hao tena wakiwa wamevaa mavazi ya kiuguzi walipomkuta kule kwenye ofisi ya mzee wanayemuita Mzalendo huku wakionekana kutokuwa na shaka yoyote. Akaamini kabisa kuwa mtandao wa maadui zake haukuwa mdogo.
_____________
Alan alikuja kuegesha gari yake kwenye maegesho ya Hoteli ya Maua Inn kama ilivyo ada yake. Akaweka pozi kidogo akiyasoma mandhari ya hapo hadi pale alipojihakikishia usalama ndipo alitoka garini na kuingia ndani. Hadi hapo alikuwa na uhakika mkubwa kuwa anatambulika kwa adui yake na hata hapo hotelini hapakuwa salama kwa upande wake kwani kama Maisara anamfahamu ni wazi lazima atakuwa anamfuatilia sana. Alikuwa matumatu na alijiwekea umakini mkubwa. Hakuwa na shaka kwani maegeshoni pale kulikuwapo na gari tatu na zote zilikuwa zikimilikiwa na Hoteli ile na ya kwake iliyoongeza idadi ndiyo ilikuwa gari binafsi. Ilikuwa imetimu saa tano na dakika tano hiyo ikiwa na maana alitumia muda wa saa moja kuanzia kuingia ndani ya jengo la Hospitali hadi kutoka kwake. Alipita mapokezi ambako aliwakuta warembo wawili wakizungumza yao akawasabahi na kuwauliza kama kulikuwa na mgeni wake ama ujumbe wake wowote ulioachwa hapo. Hakuambiwa kama vyote hivyo vilikuwepo hivyo akawaacha na kuelekea chumbani kwake. Aliufungua mlngo wa chumba chake na kuingia ndani, kitu cha kwanza kukihisi ni ugeni uliokivamia chumba chake maana kulikuwa tofauti mno na kulikuwa kukinukia harufu ya manukato ya kike. Hili lilimshtua sana ingawa alilitarajia, hakuwa ameacha maagizo yoyote kwa wahudumu wa Hoteli ile ya kufanyiwa usafi kwa chumba chake hivyo moja kwa moja akapata picha kuwa chumba chake kilipekuliwa na mpekuwaji hakuwa na lengo zuri. Mpekuwaji alikuwa fundi na anayeijua kazi yake vema hata hivyo mwenye chake hadanganywi kwani Alan aliweza kuling'amua hilo kutokana na kuona baadhi ya vitu vikiwa haviko sawa. Shuka la kitanda chake lilikuwa limekunjamana kwa namna fulani ikiwa yeye alitandika kitanda vema na kukiacha kikiwa safi na shuka lake kunyooka sana. Hii ilikuwa ni alama ya kwanza ya kumuonesha kuwa ndani kwake kumepekuliwa. Kitu kingine ni aina ya manukato ambayo yalitumiwa na wavamiaji au mvamiaji. Hakuwahi kuyafikiria kuyatumia. Yalikuwa ni manukato makali na ghali sana, akawaza Alan namna ya kuweza kujua nani hasa aliyeingia. Alipata majibu tofauti na moja likiwa ni huwenda mtumiaji wa manukato hayo yupo ndani bado au alitoka muda si mrefu. Akapata mashaka makubwa mara baada ya kuona mlango wa kabati la mule ndani ukiwa uko wazi. Aliitoa bastola yake mafichoni na kuikamata barabara mkononi mwake kisha akaanza kutafuta kwa umakini mkubwa akianzia uvunguni mwa kitanda chake huku akijaribu kuvuta fikira zake ni wapi manukato ya namna ile alipata kuyanusa. Alipokuwa akijaribu kufikiri huku akiendelea na utafutaji wake wa hapa na pale, akawakumbuka wale watu wawili ambao alikutana nao kule Hospitali ya mkoa ndani ya ofisi ya Mzalendo. Yule mwanamke alikuwa akinukia uturi wa aina hiyo na aliweza kuunusa mara tu baada ya wale watu kuingia mule ndani na alijihakikishia zaidi hilo mara baada ya yule mwanamke kusogea kwenye ile rafu ya vitabu na mafaili ya kitabibu. Harufu ile ya uturi ilikuwa yenyewe. Akajihakikishia kuwa ndani ya chumba chake eidha upo ugeni wa wale watu au wametoka hivyo punde. Alan alilisogelea kabati na kuufungua mlango wake, kabati lilikuwa tupu kama alivyoliacha, akazunguuka nyuma ya lile kabati ambako kulikuwa na mkoba wake. Mkoba akaukuta upo vile vile hii ilikuwa na maana kuwa watu hao hawakuweza kujua kama ameuficha huko. Chumba kilikuwa kitupu kisicho na mtu kabisa. Wametoka hivi punde hawa wapumbavu. Akawaza Alan huku akiirudisha bastola yake mafichoni. Akiamini kuwa hakukuwa na kiumbe mtu mule ndani. Akiwa anataka kulekea dirishani na kutazama nje yaliko maegesho ya magari ili kuona kama kulikuwa na gari yoyote iliyokuwa inatoka, hapo ndipo alipoyakutanisha macho yake na kipande kidogo cha karatasi. Kilikuwa ni kipande cha aina ile ile kama ambacho yuko nacho ambacho alikiokota kule kwenye ofisi ya Mzalendo. Akakiokota kujiridhisha, hakika kweli kilikuwa kimechorwa Ua aina ile ile ya Bee Balm.
"Alama yao..!" Akajisemea huku akikiambatanisha na kile kingine kisha akalikabiri dirisha na kuchungulia kwenye maegesho ya magari. Hakukuwa na gari iliyokuwa ikitoka, gari zilikuwa nne kama ambavyo aliziacha.
"Wamejuaje kama naishi kwenye Hoteli hii...?" Akajiuliza hata hivyo hakujipatia jibu tofauti na fikra zake zilizokuwa hasa zikimfikiria Maisara kuwa ndiye afanyaye hayo kwani hakukuwa na mwingine na hasa kilichompelekea yeye kuhisi hivyo ni lile Ua la Bee Balm. Ghafula Alan alijirusha kwa sarakasi moja matata ya ubavu ubavu mara baada ya mlango wake kufunguliwa kwa kasi na kishindo kikuu, akatua kitandani kama Chura. Risasi mbili zilizotoka kwenye bastola iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti zilikita ukutani pale dirishani ambako alikuwa amesimama.
Hii ilikuwa na maana gani...?
Hii ilikuwa na maana kuwa lile Ua ulikuwa ni mtego pekee aliotegewa na maadui zake, endapo angefika kwenye Ua lile na kulishangaa ndipo jamaa hao walipanga kuitumia nafasi hiyo kuweza kumuangamiza. Walifanya vile makusudi kwa kuwa Ua lile walilolichora kwenye karatasi wamekuwa wakilidondosha kila mahali na waliamini fika adui yao alikuwa akikutana nalo hivyo hapo napo walitaka uwe kama mtego wa kumuangamiza adui yao. Haikuwa hivyo. Hisia zake zilikuwa macho muda wote hivyo kile kitendo cha kuguswa kwa mlango wake kabla ya kufunguliwa kwa kasi na kishindo kikuu, alishang'amu. Alan alipogeuka kuutazama mlango, macho yake yalikutana na kijana aliyekuwa hatanii kwani alimuandamisha kwa risasi pale kitandani huku yeye akijitahidi kumnyima shabaha kijana huyo kwa kuruka hapa na pale huku akitafuta namna ya kuweza kumdhibiti adui yake. Alan alikuwa kwenye wakati mgumu sana kwani yule jamaa hakuwa na mzaha hata kidogo. Alan alirukia upande ambao kulikuwa na mito akakutana na mto mmoja na kumrushia yule jamaa huku na yeye akiruka kuufuata. Jamaa yule alikuwa akiuchabanga ule mno risasi kwa namna ya kuchanganyikiwa hadi pale alipo shtukizwa na teke zito la uso ambalo lilipigwa kiufundi na Alan. Alibweka yule jamaa kwa yowe kali na kuiachia silaha yake ikidondokea mahali asipopajua. Alijipigiza ukutani kisha akajiweka sawa kuweza kumkabili adui yake ambaye hadi hapo alishamuonesha uwezo mkubwa alionao. Hata hivyo hakufanikiwa kufanya lolote kwani Alan alishafika hilo eneo na kumpelekea jamaa huyo makonde mazito kadhaa ambayo yalimchosha adui yake mapema sana na kumdondosha chini.
"Nani aliyekutuma muje kunivamia chumbani kwangu na mko wangapi?" Aliuliza Alan akiwa karibu kabisa na kijana huyo tena akiwa amechutama.
Alan alikuwa kwenye wakati mgumu sana kwani yule jamaa hakuwa na mzaha hata kidogo. Alan alirukia upande ambao kulikuwa na mito akakutana na mto mmoja na kumrushia yule jamaa huku na yeye akiruka kuufuata. Jamaa yule alikuwa akiuchabanga ule mno risasi kwa namna ya kuchanganyikiwa hadi pale alipo shtukizwa na teke zito la uso ambalo lilipigwa kiufundi na Alan. Alibweka yule jamaa kwa yowe kali na kuiachia silaha yake ikidondokea mahali asipopajua. Alijipigiza ukutani kisha akajiweka sawa kuweza kumkabili adui yake ambaye hadi hapo alishamuonesha uwezo mkubwa alionao. Hata hivyo hakufanikiwa kufanya lolote kwani Alan alishafika hilo eneo na kumpelekea jamaa huyo makonde mazito kadhaa ambayo yalimchosha adui yake mapema sana na kumdondosha chini.
"Nani aliyekutuma muje kunivamia chumbani kwangu na mko wangapi?" Aliuliza Alan akiwa karibu kabisa na kijana huyo tena akiwa amechutama.
"Niko mwenyewe...!" Yule jamaa alijibu swali moja huku akijifanya kutolisikia swali lililotangulia, alikuwa akitweta si kawaida. Alan akarudia.
"Nani aliyekutuma?" Jibu hili halikujibiwa na yule jamaa na badala yake alikuwa akitabasamu. Mara yule jamaa akarusha ngumi kali sana ya kushtukiza ambayo ilikuwa ikielekea kumpiga Alan kifuani hata hivyo Alan akaizuia kwa mkono wake. Haikuwa dawa jamaa ni kama aliyepandwa na wazimu, alijizungusha pale chini na makalio na kumchapa Alan mtama mmoja matata sana kisha akamzawadia na teke la kusukuma ambalo lilimsukuma Alan nyuma na kumpigiza kwenye kitanda. Naumivu makali yalimtambaa Alan mgongoni baada ya uti wake wa mgongo kupigizwa kwenye mguu wa kitanda. Alijikunja akipambana na maumivu hayo kama mtu aliyepigwa pigo la kwenye korodani. Jamaa yule alikuja kama Sokwe anayeshambulia alitembea kwa miguu na mikono mithili ya ng'ombe kisha akarusha ngumi tatu; mbili za kifua na moja ya uso ambazo zote zilimuingia Alan barabara kabisa. Alipatwa na maumivu ya aina yake. Jamaa hakutaka kumpa Alan nafasi kwani alirusha pigo jingine zaidi hata hivyo Alan hakutaka na hilo limkute, alijigeuza kama mtoto anayejifunza kusimama vile aamkapo kutokea chini. Pigo lile lililokuwa na dhamira ya kuliharibu taya la Alan likapiga juu ya mgongo Alan akagumia hata hivyo naye akabweka kama mbwa mara baada ya teke la aina yake kupiga mbavuni lakini Alan naye akijigonga usoni vibaya sana kwenye mbao ya kitanda kwa vile alivyokuwa akinyanyuka kisha akajiweka tenge.
"Ulitaka anitume nani wewe mpuuzi...?" Aliwaka yule jamaa.
"Hamuwezi kujiongoza wenyewe ninyi hata kidogo, ni lazima mpokee oda kutoka kwa mabwana zenu wanaomikaza ndiyo mulete makalio yenu machafu hivyo najua tu umetumwa na ndiyo maana nataka kumjua huyo mumeo aliyekutuma." Alan alimdhihaki yule jamaa kwa maneno makali jamaa alighadhibika kwa kutusiwa matusi yale. Aliuma meno kama mbwa aliye udhiwa akaja mbele kwa kasi sana akarusha makonde kadhaa hata hivyo alikutana na mtu aliyeamua kufanya kweli kwani mkono mmoja wa kuume wa yule jamaa ulikamatwa vizuri na kuvunjiliwa mbali.
"AAAAAAGHH...!" Jamaa alipiga yowe baya sana baada ya mkono wake kuvunjwa hapo hapo akanyamazishwa na ngumi safi iliyopigwa kwenye shavu la kushoto jamaa akalegeza mdomo hata hivyo hakupewa nafasi nyingine kwani kichwa matata kilichotua kwenye mwamba wake wa pua kilitosha kumfanya jamaa aone nyota nyingi zikikatiza machoni mwake. Akaanguka kwa kishindo.
"Ni nani aliyekutuma...?" Akauliza Alan akiwa amechutama tena.
"Si...sijui...sijatumwa mimi...!" Aliongea kwa kitetemeshi jamaa huyo huku akihema juujuu.
"Kwanini umeamua kunivamia na kufanya upekuzi kwenye chumba changu?" Akazidi kuhoji Alan. Jamaa yule akatulia kimya pasipo kujibu chochote ni kifua chake tu ndicho kilichokuwa kikipanda na kushuka kwa kuhema kwa hofu huku udenda mzito uliochanganyikana na damu ukimtoka hovyo kinywani mwake kutoakana na pigo lile la shavuni.
"Umekuja kufanya nini kwenye chumba changu nakuuliza na kwanini univamie?" Alifoka Alan hata hivyo jamaa badala ya kujibu alikuwa akitabasamu. Alan alikuwa makini sana kwa kijana huyo kwani tabisa za hao watu za kujiua wenyewe alisha zing'amua hivyo alikuwa makini kwa hila yoyote ile ambayo jamaa huyo angeamua kuifanya. Ngumi nzito nyingine ikatua kwenye mwamba wa pua wa yule jamaa na kusababisha damu nyingi kuongezeka kumtoka. Aliguna Mh! Huku akiikamata pua yake iliyokuwa ikimuuma.
"Sema...!" Akakazia Alan, jamaa akasema;
"Tumekuja kukuchunguza wewe ni nani na kwanini ni hatari hivyo...!"
"Mmejuaje kuwa mimi ni hatari?"
"Kumbuka kuwa ulitumiwa watu wakufuatilie na kwa bahati mbaya ukawaangamiza wote hivyo kuanzia pale ukaanza kuwekwa kwenye alama mbaya sana na tukatumwa tukufute popote pale na tukujue wewe ni nani na kwanini ni hatari kwenye mipango yetu!"
"Unamjua aliyewatuma wale watu kunifuatilia?"
"Ndiyo,"
"Ni nani?"
"Bee Balm no. O2." Jina Bee Balm namba 2 likamfanya apige kimya Alan na kilichomfanya apige kimya ni kusikia kuwa hawa watu walikuwa na namba. Nani alikuwa Bee Balm namba 2 hili ndilo lilikuwa swali lake kubwa ambalo aliamini angelipatia majibu kutoka kwa huyo jamaa.
"Hawa Bee Balm wanahusika na nini hasa na wako wangapi?" Akazidi kuuliza Alan, jamaa akakohoa huku akitapika damu. Alijishika kifua kwa maumivu makali kisha akaendelea kujibu.
"...Bee Balm ni maua pendwa kwa viumbe wapendao ladha ya utamu kama nyuki, popo, mbung'o, ndege wa aina mbalimbali na kadhalika. Ni maua yaliyopandwa baadhi ya sehemu za jiji hili kwa lengo la kumnasa nyuki yeyote mwenye nia ya kutengeneza asali lakini asali isiyo na faida kwa watumiaji bali hasara. Hivyo endapo nyuki huyo akijitokeza basi huchunguzwa ni nini dhamira yake na kama dhamira yake ni mbaya hapa mjini basi hutegewe mitego ya kuuawa. Bee Balm wako wane tu."
"Hao wane wote wako hapa mjini?"
"Hapana, hapa mjini wako watatu na kuna sehemu inasemekana kuwa ndiko mipango kabambe inakoundwa, yuko mmoja na huyo ndiye Bee Balm no. 01 ambaye yuko hapa mjini kwa lengo maalumu na si kama hawa wengine."
"Lengo gani?"
"Ni siri sana hilo na halijawa wazi... AAAAGHR...! Sisi wa chini ni vigumu sana kujua siri zote, vingi tunafichwa kuepuka siri kuvuja...!" Alisema huyo jamaa huku akilalamika kwa maumivu makali ya kifua. Alan alimtazama kwa umakini na kugundua kweli alikuwa hajui hilo alilomuuliza hata hivyo akaendelea kuuliza.
"Wanatambulika vipi kama huyu ni no. 01 au 02 na kuendelea?"
"Chini...khoho, khoho, khoho Aaah...! Chini ya uwa ukitazama vizuri utaona namba." Alijibu yule jamaa hata hivyo alikuwa akipitia maumivu makali sana ya kifua na mbavu.
"Majina yao ndiyo haya au kuna mengine?" Akauliza Alan.
"Kila mmoja ana jina lake hii Bee Balm ni majina waliyopewa kama warembo wenye mvuto kwa lengo la kumtia nguvuni adui mwanaume mwenye tamaa ya kupenda ngono kwa warembo kama hao. Lengo ni kukutia nguvuni wewe. Umeponea chupuchupu sana kupona kwa Maisara ambaye alikupa mwili wake kwani Maisara huwa hatoi mwili wake bila mafanikio ya kazi. Hakika wewe ni hatari na unatakiwa kujivunia kwa hilo kama angekufahamu mapema hakika usingeponyoka kwenye mikono yake...!" Alisema huyo jamaa hata hivyo Alan akamkatisha.
"Tena kama ukipata nafasi ya kuwa hai, mfikishie salamu zangu kuwa sijawahi kukutana na kahaba mtamu na anayejua kujituma kitandani kama yeye...! Tuachane na hizi salamu, mwenzako yuko wapi na ni vema sasa ukaniambia aliyewatuma, sitakuuwa?" Akazidi kuuliza Alan huku akiendelea kukusanya muda kwani kwa kichapo kile alikuwa na imani thabiti kabisa kuwa jamaa yule asingetoka akiwa hai hata kama asingemuongeze kipigo kingine.
"Mwenzangu hayupo hapa karibu, hii kazi ilikuwa ni yangu mara baada ya mimi na yeye kukufuatilia na kufanikiwa kutupotea pale kwenye soko la Ngamiani...!"
"Na kwanini mlifika hadi kwenye ofisi ya Mzalendo?" Akakatisha Alan, yule jamaa alishtuka na kuyatoa macho yake nje.
"Ulituona...?" Akauliza kwa hamaki.
"Ndiyo na ningedhamiria kuwaua ni wazi pale asingetoka mtu hata hivyo nilitaka kupata mawili matatu kutoka kwenu ndiyo maana niliwaacha mkiwa hai hadi muda huu na utaendelea kuwa hai kama utakuwa wazi kwangu zaidi." Alan alijibu huku akizidi kumhadaa jama kwa uhai na ilhali alipo si wa kuwa hai tena. Jamaa alicheka, alicheka hadi akakohoa kupitiliza hadi Alan akahisi jamaa huyo angepoteza nguvu na kufa pasipo kujua machache ya mwisho hivyo akamtuliza kwa kumpigapiga mgongoni. Jamaa akatapika damu nyingi sana hadi akaanza kulegea na kupoteza nguvu.
"Tuli...tulitumwa tusa...tusafishe ili...!" Akashindwa kumalizia, akanata kwa muda.
"Kwanini mlitumwa msafishe na mlitumwa msafishe nini?" Akauliza Alan huku akiomba jamaa asije kupoteza maisha kabla hajamwambia chochote cha mwisho. Jamaa alimuangalia Alan kwa muda kisha akasema;
"Mzalendo alikuwa ni mtu makini sana na hapo awali baada ya kuanza kujengewa madhaka kuwa kuna mambo huwenda akawa anayajua, alipata kuhojiwa maswali ya mtego tu na bosi akajibu pasipokufikiria hili likamjulisha bosi kuwa Mzalendo alikuwa hatari hivyo...hivyo akaagiza atolewe pale na kwenda kufichwa shimoni KB...!"
"KB...? KB ni wapi?" Aliuliza Alan kujihakikishia kama huyo jamaa alikuwa akimjibu kwa dhati kabisa kwani hilo neno 'KB' alishalipatia maana akiwa kule kwenye ofisi ya Mzalendo na wao ndiwo waliokuwa wakijadili kuhusiana na mzee huyo kupelekwa huko shimoni.
"Mzalendo alikuwa ni mtu makini sana na hapo awali baada ya kuanza kujengewa madhaka kuwa kuna mambo huwenda akawa anayajua, alipata kuhojiwa maswali ya mtego tu na bosi akajibu pasipokufikiria hili likamjulisha bosi kuwa Mzalendo alikuwa hatari hivyo...hivyo akaagiza atolewe pale na kwenda kufichwa shimoni KB...!"
"KB...? KB ni wapi?" Aliuliza Alan kujihakikishia kama huyo jamaa alikuwa akimjibu kwa dhati kabisa kwani hilo neno 'KB' alishalipatia maana akiwa kule kwenye ofisi ya Mzalendo na wao ndiwo waliokuwa wakijadili kuhusiana na mzee huyo kupelekwa huko shimoni.
"Kibaranga huko kwenye mashamba ya mkonge, kulipokuwa na kiwanda cha kuchakata mkonge kuna jengo moja lipo kule ambalo ndilo alilohifadhiwa Mzalendo na anaweza akauawa tu maana hana faida kwetu." Alan akamtazama huyo jamaa na kumuona sasa alikuwa akijibu huku akiwa hajui anajibu nini. Alikuwa muwazi sana na hata hivyo hakukuwa na uwongo wowote kwenye majibu yake kwa namna alivyomtazama. Kwani hata hivyo neno KB alipata kuliona kwenye simu ya yule jamaa aliyepambana naye wa mwisho kule eneo la viwandani na ulitumwa kama ujumbe kwenye simu yake ukimtaka wampeleke yeye huko shimoni endapo wakimdhibiti hata hivyo hawakufanikiwa kwani wote aliwaangamiza kwa mikono yake. Huyo jamaa sasa alikuwa akipoteza nguvu kabisa na muda wowote angeaga dunia.
"Bosi wako ni nani...?" Akauliza Alan.
"Unasema...?" Akauliza yule jamaa kwa sauti ya chini kabisa ya kuitega vizuri ili kumuelewa anaongea nini maana ilikuwa ikitoka kwa mkoromo. Alan akarudia;
"Bosi wako ni nani...?"
"Mganga mkuu...mkuu wa Bombo Hospi...!" Akajibu kwa shida.
"Jina lake nani...?" Akauliza Alan akiwa ameinama karibu kabisa na sikio la huyo jamaa.
"Dokta Rich...Richard Bangooo...!" Alijibu jamaa huku akipoteza kabisa sauti ikidhihirisha kuwa hakuwa na muda zaidi, Alan akalihifadhi hili jina vizuri kwenye memori yake kichwani kisha akakumbuka kuuliza swali muhimu sana.
"Anaishi wapi...?"
"Sahare kigorofani...nyu...jengo namba 09 ghorofa ya 03...?"
"Anaishi na nani kwenye ghorofa hiyo ya 03...?"
"Mwenyewe...!"
"Unajua watu anaoshirikiana nao...?" Alan aliuliza kwa haraka sana ili kuendana na hali ya huyo jamaa hata hivyo swali hilo la mwisho kabla ya kulijibu akagoa damu na kutapika damu nyingi sana ambazo kama Alan asingejitahidi kuzikwepa zote zingemuishia usoni.
"Sijui...!" Alijibu kwa sauti ya chini sana, Alan aliweza kuisikia mara baada ya kumuona akijiandaa kuzungumza hivyo kuegesha sikio lake kinywani mwa jamaa huyo. Akamtazama usoni na kuona ni kama amedangwanywa. Akausogeza mdomo wake sikioni na kumnong'oneza kwa sauti nzito yenye kupenya ndani kabisa ya ngoma ya sikio.
"Unawajua watu wanaoshirikiana na bosi wako?" Akamtazama tena usoni kuona kama jamaa atajibu hata hivyo alikata tamaa baada ya jamaa kuangusha shingo kwenye beba lake la kushoto. Alikuwa ameshaaga dunia tayari. Alan akasimama na kumtazama kisha akasema;
"Asante kwa msaada wako na ushirikiano uliounesha kwangu. Nenda salama uendako." Akaelekea nyuma ya kabati na kuchukua kilicho chake akavaa begi lake mgongoni na kuifuata bastola ya yule jamaa ilipoangukia akaiokota kwa kitambaa maalumu alichokitoa mfukoni na kuiweka karibu ya ule mwili usio na uhai. Akaupekua ule mwili na hakuna chochote alichoambulia zaidi ya pakiti moja ya kondom kiberiti cha gesi sambamba na sigara moja Embassy ikiwa kwenye mfuko wa shati. Hakika watu wanajijali sana. Alawaza Alan mara baada ya kumkuta jamaa akiwa na pakiti moja ya Kondom. Akaacha kila kitu kama kilivyo na kutoka mule ndani. Alipita mapokezi akakuta hakuna mtu hata mmoja hivyo ilikuwa ni nafasi nzuri kwake kuweza kupita bila kujengewa mashaka. Alipiga hatua za taratibu akiyakaribia maegesho ya magari huku akitazama huku na huko kuona kama kungekuwa na gari yeyote maegeshoni hapo, ili kujihakikishia kama hapo awali hakuweza kuiona wakati anaingia kwenye Hoteli hiyo au aweze kumtambua mtu yeyote wa kuweza kumtilia mashaka. Hakukuwa na mtu yeyote wala chombo chochote cha usafiri hivyo aliingia kwenye gari yake na kujifungia kisha akatoa simu yake mfukoni na kutoa taarifa polisi kisha akaiondoa gari yake hapo maegeshoni akirudi na barabara ya nane.
Alan alikunja kushoto mara baada ya kuingia barabara ya Taifa. Akatazama majira kwenye saa yake ya mkononi hakika muda ulikuwa unakimbia kwa kasi sana na muda huo likuwa ikikimbilia saa sita kamili usiku. Akapiga mahesabu na kufikiria muda ambao aliutumia akiwa ndani ya chumba chake kwenye Hoteli hiyo ya Maua Inn. Alianza kuijengea mashaka makubwa sana kazi yake ambayo hapo ilipofikia ilikuwa bado hata nusu yake. Kitu pekee kilichokuwa kikimpa amani moyoni ni kwamba kwa namna fulani alikuwa tayari ameshaijua safari yake ya kukipeleleza kifo cha Luteni Jenerali Leous Mipango na alishaanza kuuona mwanga wa kufika kwenye kilele cha kuijua sababu ya kifo hicho japo mwanzoni alihisi ni jambo la kawaida na lisingeweza kumuumiza kichwa ila kwa yale ambayo anakutana nayo ndani yake, hakika haikuwa kazi ya kuidharau kwani inahitaji umakini wa hali ya juu na uvumilivu mkubwa. Bado alikuwa katika mawazo mazito sana ambayo yalimfanya awe anandesha gari kwa kasi huku akiwa na ghadhabu za wazi kabisa kwa watu ambao wanamfanya hadi majira hayo akiwa hajalala huku wao wakiwa kwenye usingizi mzito pengine.
Hakika alikuwa na ghadhabu za wazi kabisa. Alishaiacha barabara ya Taifa na sasa alikuwa akiikimbiza gari yake akiwa juu ya barabara ya Jamhuri akiivuta Makorora kwa kasi kubwa. Dakika mbili pekee zilitosha kumtoa hapo alipo hadi sahare kigorofani aliegesha gari yake chini ya mwembe pembeni ya uwanja wa shule ya Sekondari. Akateremka na kuufunga mlango wake madhubuti na kutoka. Alitembea kwa mwendo wa haraka hadi alipofika kwenye mtiririko wa majengo yale marefu ya ghorofa akaanza kuhesabia kuanzia ghorofa namba nne hadi alipofika tisa. Alilitazama lile jengo la ghorofa kwa upande wa nyuma na kuona kuwa vyumba vyote kuanzia jengo la chini, ghorofa ya pili, ghorofa ya nne na ghorofa ya tano ambayo ndiyo ghorofa ya mwisho, vikiwa vimemezwa na giza zito. Ghorofa ya tatu kulikuwa kuna chumba ambacho ndicho pekee kilichokuwa kikiwaka taa na kwenye ghorofa hiyo ndiyo maelezo ya yule jamaa aliyepambana na Alan yalisema kuwa ghorofa hiyo ndiyo anayokaa Dokta Richard Bango. Hapa Alan aliweza kujihakikishia uwepo wa mtu huyo ndani yake. Alilizunguuka hilo jengo kwa upande wa mbele na kuyazunguusha macho yake kila kona ya jengo lile. Kulikuwa na mwanga mkali ambao ulikuwa ukiangaza kutoka kwenye taa zilizopandwa kulizunguuka jengo hilo. Alianza kupanda ngazi taratibu akikatiza ghorofa ya kwanza, akapanda ngazi tena kuifikia ghorofa ya pili kisha akaingia ghorofa ya tatu. Taa zilikuwa zikiwaka kwa mwanga mkali mno zikimulika kwenye kila baraza ya ghorofa moja na nyingine. Alipofika kwenye baraza hiyo ya ghorofa husika kwanza alichokifanya Alan, alianza kukagua namna ya kuweza kujiokoa pindi kukitokea rabsha zozote. Hii baraza ilikuwa imekingamwa na ukuta mfupi ambao ulikuwa ukiishia kiunoni na kutokea hapo hadi usawa wa kichwani kulizibwa kwa drili maalumu ambazo isingekuwa rahidi hata kwa mtoto kuweza kuchungulia upande wa nje. Alan aliitazama milango miwili ya jengo hili akaona mlango mmoja ukiwa umefungwa kwa kufuli na huu mmoja ukiwa haujafungwa na milango yote ilikuwa ni ya makomeo ya kawaida. Akiwa hapo akijishauri namna ya kufanya. Akiwa bado anaendelea kujishauri namna ya kufanya, mara alisikia hatua za mtu zilizokuwa zikija upande wa kule juu. Akaangaza macho yake kila mahali akaona hakuna namna zaidi ya kujificha ili asiweze kuonekana na watu hao ambao walikuwa wakipanda huko ghorofani huku wakipiga domo. Alikimbia kwa hatua za kimya kimya hadi mwisho wa ile baraza ambako aliziparamia zile drili na kutokea upande wa nje kisha akasogea hadi ukutani na kujizuia kwa kujishikiza kwa mkono mmoja ukutani na mkono mwingine ukiwa umekamatia vyuma vya ile drili huku vidole vya miguu yake vikiwa vimekanyaga kwa uchache kwenye ule ukuta mfupi wa baraza. Lilikuwa ni zoezi gumu sana kuweza kujizuia hapo hata hivyo hakuwa na namna nyingine zaidi ya hiyo, vinginevyo labda akubali kuonwa na watu hao
"Yaani huwezi amini shoo ya leo ilikuwa poa sana mpenzi, nimeinjoi kuliko siku zote ambazo niliwahi kutoka na kwenda kutazama shoo kama hii ya msanii huyu." Ilikuwa ni sauti ya kike ikisikika ikisifia juu ya kile walichotoka kustarehea.
"Huyu jamaa akipanda jukwaani huwa hafanyi makosa anahakikisha anaiteka hadhira yote na hiki ndicho kinachomfanya anakuwa juu kuliko wasanii wote hapa nchini." Alijibu mwanaume. Walikuwa tayari wanazikwea ngazi za mwisho za kutokea ghorofa hiyo aliyopo Alan.
"Kweli kabisa mpenzi ila nimechoka sana leo yaani nikishatoka kuoga ni kujitupa tu kitandani." Ilisema sauti ya kike.
"Hunishindi mimi love." Sauti ya kiume ikaongezea na sasa wakawa wameshafika kwenye ile baraza na kukunja kona kisha wakaendelea kupanda ngazi za ghorofa za juu. Walikuwa wameshikana viuno huku mwanamke akiwa amevaa sketi fupi iliyokomea juu kidogo ya magoti hivyo kupelekea kuonesha uvungu wote wa nyuma ya magoti na mapaja yake kwa uchache. Alikuwa na umbo zuri kiasi ambalo aliliongezewa na kuvaa viatu vyenye visigino virefu huku jamaa yake akiwa amevaa suruali ya jeans ambayo haikuwa ikijulikana ni nyeusi au buluu kutokana na mwanga wa taa. Walishatokomea juu ya zile ngazi tayari. Alan alirudi taratibu na kutua pale barazani sasa akiwa hana mzaha tena. Aliukabili ule mlango ambao ulikuwa haujafungwa kwa nje ambao kwa tathmini yake ya harakaharaka kwa upande wa nyuma aliweza kuona taa ikiwa inawaka kwenye moja ya dirisha. Alijaribu kuusukuma ule mlango hata hivyo haukufunguka na kwa namna kitasa chake kilivyo ilikuwa ni vigumu sana kuweza kuufungua kwani haukuwa ule wa kunyonga kitasa. Huu ulikuwa umefungwa kwa ndani kwa komeo mfano wa hili la nje hivyo kupelekea kukata tamaa. Aliachana na ule mlango na kujifikiria vile atakavyoweza kuingia ndani. Alipokuwa akiwaza huku akiangaza macho yake aliweza kuvutwa na dirisha moja la pale barazani ambalo lilikuwa likitokea ndani ya sebule kwa muundo wa jengo hilo lilivyo. Alalisogelea dirisha lile na kuanza kulikagua. Alan alilivua begi lake haraka na kulifungua kisha akatoa bisibisi akalifunga begi lake na kulirudisha mgongoni. Alifanya vile kwa kuwa dirisha hili halikuwa la nondo wala vioo vya aluminiam bali lilikuwa limetengenezwa kwa ruva ngumu zilizotengenezwa kwa mawe madogo madogo na mchanga wenye kokoto ndogondogo uliochanganywa na saruji nyingi kiasi kuifanya kuwa imara. Ruva hizi zilikuwa zimefungwa kwa skrubu maalumu ambazo kofia yake ilikuwa ina kifereji kidogo cha kufungulia kwa bisibisi mfano wa 'key way.'
Alan alianza kuzifungua haraka haraka zile ruva na kuzipanga pale dirishani hadi alipopata upenyo wa kuweza kupita ndipo alipita na kuingia ndani kisha akavichukuwa vile vipande alivyovifungua na kuviweka chini kwa ndani kwa utaratibu mkubwa akarudishia pazia na kutoa kurunzi yake ndogo mfano wa kalamu na kuiwasha. Eneo la sebuleni lilikuwa limezimwa taa hivyo giza lilikuwa limeshamiri vibaya mmno. Sebule ilikuwa ya kawaida sana iliyo na makochi ya kisasa, meza ya kioo katikati, kabati dogo la vyombo na jokofu kwa ajili ya kugandishia vyakula. Alipotazama pembeni kwenyw kona moja ya ukuta kwa chini, aliona kitu kilichomvutia nacho ni buti kubwa lililofanana na buti la kijeshi. Alilisogelea lile buti na kunyanyua moja akaligeuza na kutazama kwenye soli yake. Ilikuwa na soli ngumu sana hata hivyo kilichomvuta zaidi hakikuwa ugumu wa soli ya buti hiyo bali ni kashata za buti hilo.
Sebule ilikuwa ya kawaida sana iliyo na makochi ya kisasa, meza ya kioo katikati, kabati dogo la vyombo na jokofu kwa ajili ya kugandishia vyakula. Alipotazama pembeni kwenyw kona moja ya ukuta kwa chini, aliona kitu kilichomvutia nacho ni buti kubwa lililofanana na buti la kijeshi. Alilisogelea lile buti na kunyanyua moja akaligeuza na kutazama kwenye soli yake. Ilikuwa na soli ngumu sana hata hivyo kilichomvuta zaidi hakikuwa ugumu wa soli ya buti hiyo bali ni kashata za buti hilo. Zilikuwa ni zile ambazo aliziona kwenye nyumba ya marehemu Zaituni. Hapa akajiaminisha kwa asilimia mia moja kuwa mmiliki wa buti hizo ndiye aliyehusika na kifo cha muuguzi Zaituni. Alan aliiacha hiyo sebule na kuelekea upande wa jikoni huko hakukumvutia sana akatoka na kuingia kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa wazi akakikagua kile chumba. Hakikuwa na vitu vingi zaidi ya kitanda pekee. Akaachana nacho na kuifuata korido nyingine ndogo ambayo ilimfikisha kwenye chumba ambacho ndicho pekee kilichokuwa kikiwaka taa. Bado taa ilikuwa ikiendelea kuwaka huku muziki ukisikika kwa sauti ya chini sana. Alan aliikamatia bastola yake mkononi na kuchungulia kwa ndani kupitia tundu dogo la funguo. Aliweza kuona kitanda kwa uchache sana kwani kitanda kilikuwa upande wa kushoto. Akatega vizuri sikio mara akaweza kusikia sauti ya mwanamke aliyekuwa akilalama ni kama chumbani humo kulikuwa na watu wakiwa wanafanya ngono. Alijaribu kuusukuma mlango taratibu Alan na kufanikiwa kuufungua kwani haukuwa umefungwa kwa ndani. Alichungulia kidogo kupitia uwazi mmdogo wa mlango na kufanikiwa kumuona mtu akiwa amelala kiubavu bila nguo hata moja huku mikono yake ikiwa inasugua zakari yake huku filamu ya ngono ikiwa inaendelea kwenye tarakilishi yake aliyoiweka kwa upande wa mbele wa kichwa chake.
Alan akakumbuka maneno ya yule jamaa aliyepambana naye kwenye Hoteli ya Maua Inn kuwa Daktari huyo hakuwa na mke wala watoto. Hapa Alan akajipatia majibu kuwa Daktari huyo ameathiriwa kwa kiasi kikubwa sana kwa tendo hilo la kujichua (Punyeto). Aliufungua taratibu ule mlango hadi alipofanikiwa kuingia ndani kabisa ya kile chumba. Dokta Richard alikurupuka na kutaka kukimbilia shuka ili ajifunge kujisitiri hata hivyo hakufanikiwa kwani Alan aliruka na pigo moja baya la teke ambalo lilimrudisha Dokta pale kitandani akiwa mtupu kama alivyokutwa.
"Dokta Richard Bango, hujui kama umepewa karama ya utabibu na Mungu kisha taifa hili likakupa mamlaka makubwa sana ya kuhakikisha huduma kwa wagonjwa inatolewa kikamilifu? Hujui kama wauguzi na madaktari wote wanataka muongozo kutoka kwako ili waitende kazi yao vema? Hujui pia kama hukutakiwa kuwazuia wauguzi wasiifanye kazi yao kikamilifu? Hata hivyo wewe umepewa mamlaka na uwezo mkubwa na Mungu amekupa zawadi hiyo ya pekee ili kuhakikisha afya za wagonjwa zinaimarika, vipi kuhusu hili? Mbona unakwenda kinyume. Unauwa waguzi wako, unawateka wataalamu na kwenda kuwaficha unapojua wewe tena kikatili zaidi kwanini?" Aliongea Alan akimtupia lawama Daktari huyo kwa maswali lukuki.
"Unaongea nini wewe mbona kama umechanganyikiwa, unajua hapa ni wapi na uko na mtu gani mbele yako?" Aliuliza Daktari kwa kujifanya hajui kitu huku akijikalisha vizuri pale kitandani na kujifunika shuka kuificha zakari yake.
Ni kama hayawani.
"Unadhani naongea na nani kama si wewe...naongea na wewe ambaye akili yako ilivyo na taaluma uliyonayo ni vitu viwili tofauti. Wewe ni mwanaume wa aina gani ambaye unaona kujichua ndiyo dili. Nimezoea kuwaona madaktari kama ninyi mkitoa nasaha kwa wagonjwa waliothiriwa na tabia hizo za kujichua lakini nashangaa kukuona wewe ukiwa unafanya huu ujinga."
"Ngoja kwanza kijana unaonekana umekuja kunitusi si ndiyo, wewe umekuja kimakosa sana na unakoelekea ni kubaya zaidi...ni vema ungekuja na kujitambulisha kisha kujieleza kuwa wewe ni nani na hapa kwangu umefuata nini...!"
"Haitakusaidia hata nikiamua kujieleza, wewe sitisha huo mchezo kwa kuwa nimekuja kukuuliza maswali yangu machache tu na ya msingi sana."
"Uliza...uliza nikujibu." Alisema Dokta Bango huku akiitupa mikono yake kuonesha msisitizo.
"Kwanini unawatuma wale vijana wanifuatilie?" Alianza kuuliza swali la mtego Alan kwani alijua fika kuwa Bango hakuhusika na kuwatuma wale vijana na walitumwa na Bee Balm no. 2, sasa alitaka kuona kama kutakuwa na tashwishi yoyote usoni mwa daktari huyo.
"Vijna...sijamtuma mtu mimi akufuatilie, wewe unadhani naweza kupoteza muda wangu na kumtuma mtu akufuatilie wewe na ilhali sikujui?" Alijibu akiwa anajiamini Bango.
"Hukumtuma mtu...? Sawa, leo ulinitumia watu wanifuatilie na wakanisumbua sana hapa mjini bahati nzuri niliwaacha kwenye mataa hata hivyo bado hawa watu wakaendelea kunifuatilia. Hivi unadhani mimi ni mjinga nikuulize kitu nisichokijua na kwanini hujiulizi hapa kwako nimepajuaje? Nilikuwa nikikutafuta sana kwa udi na uvumba nikakutembelea kazini kwako sikukuta nilipokuwa ofisini kwa Mzalendo, nikawaona vijana wako wawili walewale ambao uliwatuma kwangu na kunikosa. Uliwapigia simu na kuwaambia wasafishe unadhani sijui pia...!" Aliongea Alan. Dokta Bango alishtuka kwa maelezo hayo hadi akajiuliza kichwani mwake kuwa huyu kijana ni mtu wa aina gani.
"Wewe ni nani...?" Haikutosha kujiuliza kwenyewe hivyo akaamua kumuuliza.
"Ni yule unayenitafuta na sijui unanitafuta kwa lengo lipi labda?" Akajibu kwa mtindo wa swali Alan.
"Mimi sikuwa nimekutafuta wewe na sikutafuti kabisa." Alijibu Dokta Bango akiwa na tashwishi fulani usoni mwake ambayo ilishaanza kujengeka.
"Utaniambia hujui kama uliwatuma vijana wako kwenye chumba changu cha Hoteli pale Maua Inn, wakachangua kila mahali na wasipate kitu hata hivyo yule wa kiume hakuwa na bahati maana aliingia kwenye boksi la hatari nikamtuliza na ndiye aliyenipa maelekezo haya nadhani kesho ukipata nafasi unaweza kwenda kumkuta kwenye chumba cha kuhifadhia maiti...?"
"Umemuua Stalone...?" Alijibu kwa hamaki Dokta Richard Bango hapo ndipo Alan alipojihakikishia kuwa hata huyo alikuwa akijua kila kitu.
"Stalone ni nani kwani na wewe hukumtuma mtu kwangu na...!" Hakumalizia alichotaka kukisema Alan kwani Dokta Richard Bango alishajifyatua pale kitandani na kuruka hewani kwa mateke kadhaa hata hivyo yalikuwa butu kwani Alan alikuwa makini sana na alishamuona wakati akiwa anajiandaa kufanya hivyo. Mateke yale aliyafuta na kumfanya Dokta Richard kutua chini na kujiweka sawa huku akijifunga kwa shuka lake kiunoni. Alimfuata Alan tena kwa kasi kubwa na kumchanganyia mapigo tofauti tofauto ikiwemo karate, judo na Konfuu, Alan akawa na kazi ya kuhakikisha hakuna hata pigo moja ambalo lingeweza kuingia mwilini mwake. Mzee huyo alionekana kuwa hodari sana ila Alan naye hakuwa lelemama hata kidogo. Alijigeuza kama mwewe anayekwepa pigo la mwenye mfugo aliotaka kuushambulia kisha akamsukuma yule Dokta kwa teke la kifua. Dokta alijipindua na kusimama kitandani kisha akajirusha tena na kumfuata Alan. Wakakutana tena na kupelekeana mapigo ya haja, safari hii Dokta Bango alikuwa ngangari kwani kwa muda mfupi tu alifanikiwa kumpa Alan pigo moja baya sana ambalo lilimtupa kwenye kabati la nguo lililopo ukutani. Mzee huyo hakusubiri Alan ajipange kwani alishauona uwezo wa kijana huyo haukuwa mdogo hivyo alimfuata hapohapo alipoangukia na kumshindilia ngumi kadhaa. Alan akajidhatiti na kufanikiwa kuzuia yale mapigo na kumsukuma na teke jingine ambalo lilimbeba hewani na kumrudisha pale kitandani ambako alikwenda kuiangukia ile tarakilishi ambayo alikuwa akiitumia kuangalia mkanda wa ngono, aliivunja vibaya sana ile tarakilishi. Akapata ghadhabu maradufu na kutaka kunyanyuka hata hivyo hakuwa amefanikiwa kwani Alan alishamfikia na kumchapa mateke mawili moja likimpiga kwenye mbavu na jingine likimpata kwenye shavu. Alipinduka vibaya Dokta hata hivyo alipoangukia palikuwa ni sehemu yake ya kuhifadhia silaha. Akanyanyuka na bastola. Alan alijifyatua kwa kasi ya umeme na kuupiga teke mkono huo uliobeba silaha. Bastola ile iliruka na kupenya kwenye dirisha ikaangukia nje. Dirisha la hapo chumbani halikuwa kama la kule sebuleni. Hili halikuwa la luva bali lilikuwa la vioo na kwa wakati huo kioo kilikuwa kimefunguliwa kabisa na pazia kuvutwa pembeni ili kuruhusu hewa kuingia. Kitendo kile cha bastola kuanguka nje kikamfanya Dokta Bango ashangae, likawa kosa. Alipigwa ngumi mbili za mbavu na kupepesukia dirishani, Alan akamkamata mkono na kumrudisha ndani kwa kumvuta akaangukia pale kitandani tena akiimalizia ile tarakilishi yake kwa kuivunja kabisa aliponyanyuka, alinyanyuka na kisu ambacho kilikuwa chini ya mto pia, kwa kasi kubwa akapeleka lile pigo la kisu. Alan akakwepa kwa mara ya kwanza, pili lakini mara ya tatu ikamshinda kisu kile kikakita kwenye nyama za bega lake. Alan alipiga kelele kwa maumivu makali aliyokumbana nayo, Dokta Bango alikichomoa kile kisu ili kukichoma tena sehemu nyingine ya mwili wa adui yake. Haikuwa hivyo, Alan alijivuta na kumzawadia mzee huyo kichwa kizito kilichotua kwenye mwamba wa pua. Mzee. huyo akayumba huku akiendelea kuking'ang'ania kisu chake, Alan akaongeza ngumi moja ya mbavu na nyingine ya chini ya kifua. Dokta Bango akatapika damu huku akihisi nyota zikikatiza machoni mwake na hali ya kutapika ikimjia mara dufu. Alipiga mwereka mbaya sana chini huku kile kisu kikimtoka mikononi. Mkono wake wa kulia ukavunjika vibaya sana baada ya kuuangukia. Akapiga kelele mbaya mno kutokana na maumivu ya kuvunjika kwa mkono wake. Alan alimsogelea pale na kumuuliza maswali mawili matatu huku kile kisu akikitupia uvunguni kwa guu lake.
"Ni akina nani unaoshirikiana nao kwenye mpango huu wa kuendeleza mauaji ya watu muhimu kwenye jeshi letu la ulinzi wa nchi hapa mjini?" Aliuliza Alan. Hata hivyo Dokta Bango hakujisumbua kujibu ni kama swali lile hakulijua. Alan akarudia kwa mara nyingine bado hakukuwa na majibu. Akauchukua ule mkono ulio vunjika na kuanza kuunyonga.
"AAAAAAGHH! Unaniumiza mwanahizaya wewe...!" Alilalama akiwa na hofu kubwa sana moyoni mwake.
"Nijibu swali langu nililokuuliza la sivyo nitaendelea na hili zoezi." Akasisitiza Alan.
"Unajisumbua kijana hutafanikiwa kupata kitu chochote na badala yake ni kwamba utakufa...!"
"Hilo sio swali nililokuuliza swali langu liko wazi." Akasema Alan huku akiushika tena ule mkono na kutaka kuunyonga.
"AAAAAAGHH! Unaniumiza mwanahizaya wewe...!" Alilalama akiwa na hofu kubwa sana moyoni mwake.
"Nijibu swali langu nililokuuliza la sivyo nitaendelea na hili zoezi." Akasisitiza Alan.
"Unajisumbua kijana hutafanikiwa kupata kitu chochote na badala yake ni kwamba utakufa...!"
"Hilo sio swali nililokuuliza swali langu liko wazi." Akasema Alan huku akiushika tena ule mkono na kutaka kuunyonga.
"Ni wengi sana ninashirikiana nao...!" Akajibu akiwa na hofu ya wazi wazi Alan akahisi huwenda mambo yaliyopo ni makubwa sana na watu hao walikula kiapo kikali cha kutunza siri maana hata usemaji wao haukuwa wa kawaida. Alikuwa na woga mwingi mno.
"Ni akina nani hao...?" Akauliza Alan akiwa makini sana kwa mtu huyu maana alishaona mengi kichwani mwake kutokana na hofu aliyonayo.
"Huwezi kuwajua kwa kuwa hata mimi mwenyewe siwajui...Aaahg!" Alijibu Dokta Richard Bango huku akilalama kwa maumivu ayahisiyo. Alan akamtazama usoni na kufanikiwa kugundua kuwa jibu lile halikuwa la ukweli na kuna jambo alikuwa akilificha na ni kwa faida ya hao wenzake. Hakuona haja ya kuendelea kumuuliza swali hili akaona ni bora abadilishe. Akatia mkono mfukoni mwake na kutoa vipande vitatu vya karatasi. Kimoja ni kile kilichokuwa kimeanguka kwenye droo ya kabati dogo pembeni ya kitanda cha kulazia wagonjwa kwenye wodi namba 04; ndani ya jengo la Cliff alipopambana kwa mara ya kwanza na yule jamaa mgonjwa wa kutengeneza. Ya pili ikiwa ni ile aliyoidondosha yule msichana kule kwenye ofisi ya Mzalendo na ya tatu aliiokota kwenye dirisha la chumba chake kwenye Hoteli aliyofikia ya Maua Inn.
"Najua haya unajua maana yake na yote yalikuwa yakiachwa mahali kwa maana fulani, mimi sitaki hiyo maana ila nataka uniambie hawa ni akina nani?" Akauliza Alan huku akimuangushia vile vikaratasi. Dokta Bango alivitazama kwa muda kisha akageuza shingo na kumtazama kijana yule.
"Hao ni watu wawili tofauti, mmoja anafahamika kwa jina la Maria huyo ni huyo mwenye Ua namba 03 na huyo mwenye Ua namba 04 anafahamika kwa jina la Dokii. Wote hao ni Ua aina ya Bee Balm, wapo hapa mjini kwa lengo moja tu kuhakikisha wanamtia mikononi nyuki msumbufu ambaye sasa ni wewe." Akaeleza Dokta Bango.
"Unadhani ni kwanini mmeamua au wameamua kunitega kwa namna hii?"
"Unajua siri kubwa ya majasusi wengi ni umalaya au anasa. Majasusi wengi wa kiume hawana wanawake wa kudumu nao hivyo hujikita kwenye ngono na kila msichana mrembo anaye kutana naye. Hii pia ipo sana kwa majasusi wa Tanzania. Hivyo wakuu wakapanga ili kuwazidi ujanja ni kuwaandalia wanawake warembo sana ambao ni hatari ili kuweza kukunasa mapema ila umekuwa mjanja sana hadi nashangaa na mbaya zaidi umelala na Bee Balm namba mbili hii imekuwa kama dharau na binti huyo anahasira sana na wewe kwa kuweza kumdharaulisha kwa mabosi zake. Ametukanwa sana kwa kitendo cha kukuvulia chupi na asikutie mikononi." Alijibu Dokta Bango. Alan akatafakari majibu yale kisha akatabasamu moyoni mwake na kuona jinsi ambavyo kazi ile ilivyo kubwa na bado alikuwa na kazi kubwa na ya ziada. Alimtazama yule Daktari kwa namna alivyokuwa akipitia maumivu makali hata hivyo bado alikuwa na maswali mengi na muhimu ya kutaka kumhoji miongoni mwa maswali hayo moja lilikuwa ni akina nani ambao anashirikiana nao na kwanini anajawa na hofu nyingi kila aulizwapo swali hilo. Alan alimsogelea tena na kuushika ule mkono mzee yule akaanza kuhema kwa nguvu sana akiwa na hofu.
"Niambie watu unaoshirikiana nao hata mmoja tu inatosha?" Akauliza. Yule mzee akakumbwa na tashwishi kubwa sana machoni. Alan akaanza kuukunja ule mkono, Dokta akaanza kulia kama mtoto mdogo huku akisema kuwa kijana huyo atakufa bila kufika popote kwani watu hao ni hatari sana. Alan akamuachie ule mkono baada ya kumuona hayuko tayari kujibu.
"Mzalendo anaishi vipi huko aliko?" Akakumbuka kuuliza swali la muhimu mara baada ya kukumbuka maneno ya muuguzi Zaituni ambaye aliuawa na mtu huyo hasa baada ya kukuta buti ambalo daktari huyo alilivaa siku ya kutekeleza mauaji. Hasa ilikuwa ni baada ya Zaituni kumwambia Alan kuwa akimpata Mzalendo na kumuuliza chochote kuhusiana na mganga mkuu anaweza kujua baadhi ya mambo na kumueleza kwa undani.
"Kesho atakuwa marehemu maana tumemtumia mtu usiku huu kwa ajili ya kwenda kumpumzisha."
"Kwanini unauwa hii hazina muhimu hapa nchini wewe kuna nini unapata kwenye hili?" Akauliza Alan. Dokta Richard Bango alicheka sana, alicheka mno kisha akasema;
"Pesa...napata pesa nyingi sana kupitia hii kazi na pia tunatunza siri. Hatupendi siri zetu zitoke nje na hiki ndicho tunachokifanya endapo tukigundua mtu yeyote kuwa ni mwiba kwenye harakati zetu hizi za kupigania haki basi mtu huyo hana nafasi ya kuishi...!"
"Kupigania haki?" Akawahi kuuliza Alan.
"Ndiyo, kupigania haki. Mpango huu upo kwa ajili ya kuhakikisha viongozi watatu wa ngazi za juu wanapoteza maisha hii idadi bado haijatimia na huwezi kujua ni viongozi gani na kwanini idadi haijatimia. Hii ni siri na itabaki kuwa siri na ndiyo maana nikakuambia huwezi kufika popote utakufa tu...utakufa kijana, jamaa hawa wakiamua kukufungia kazi kwani ndani ya mpango huu kuna mikono imara ya jasusi hatari." Jibu hili likamfungua akili Alan sasa akawa sahihi juu ya wazo lake kwa mkuu wake wa kazi kuwa mpango huu bila shaka unasukwa na jasusi na hata mauaji yake yanaongozwa na jasusi kwani haiwezekani mtu wa kawaida akawa na uwezo wa kupambana na wanajeshi mahili na kuwaangamiza kwa vifo vibaya namna ile. Hatari ilikuwa kubwa sana na hakika alitakiwa kuwa makini kabla hata hajaingia mikononi mwa jasusi huyo au watu hao hatari asiyojua wanapambania haki ipi.
Kifo cha Luteni Jenerali ambacho ndicho kilichomfikisha hapa jijini na kuanza kukipeleleza, akaona jinsi kinavyokwenda kumfunulia hatari kubwa sana ndani yake. Hata hivyo yeye pia alikuwa ni jasusi tena wa daraja la juu kabisa aliyepokea mafunzo yake ya kijasusi kutoka kwenye mashirika makubwa matatu ya kijasusi hapa duniani. Shirika la kwanza ambalo linatoa mafunzo ya kijasusi likiwa ni la huko nchini marekani akiwa bado hajafuzu mafunzo hayo akaingizwa kwa siri sana kwenye shirika jingine la kijasusi la huko Iziraeli hapo pia hakudumu sana akamalizia mafunzo yake hadi kufanikiwa kufuzu kabisa mafunzo ya kijasusi huko nchini Cuba ambako lipo shirika moja la siri sana duniani na ogopwa linalotoa mafunzo ya kijasusi kwa nchi marafiki. Na kwa kuwa Tanzania inao uhusiano mzuri na taufa hilo hivyo ikawa rahisi kwa nchi yake kumpeleka huko ambako alifanikiwa kuwa kijana hatari na hodari sana anaetazamaiwa kuwa jasusi tishio duniani. Hivyo hakuwa na wasiwasi Alan kwa kuwa mbinu zote za kijasusi alikuwa akiziju na mapigano ya aina yote alikuwa akiyajua na kuyatumia vizuri na hiyo ndiyo sababu hata ikapelekea kuhisi kuwepo kwa jasusi hatari ndani ya vifo vya wajumbe wale hata kifo ambacho ndicho anachokipeleleza cha Luteni Jenerali Leous Mipango kilichotokea jijini hapo.
"Ni nani unaoshirikiana nao sasa?" Alan aliamua kuuliza huku akiwa ameweka utani kando na alibadilika kabisa.
"Sijui bwana nimekuambia mbona...!" Alijibu Daktari huyo hata hivyo hakuwa amefika mwisho wa kauli yake. Alilikunja guu lake la kulia na kulifyatua kiasi akamsukumia Alan nyuma na kumfanya kijana huyo kuangukia mgongo. Lilikuwa ni shambulio la ghafula sana hivyo Alan hakuwa amelitarajia. Kitendo kile kilimfanya achanganyikiwe kwa kiasi kikubwa. Dokta Richard Bango alijinyanyua na kukimbilia kitandani akanyanyua godoro na kutoka na bastola akasimama wima akimlenga Alan hata hivyo hakufanikiwa kuachia risasi. Alan alijikunyua kwa haraka pale chini na kuichomoa bastola yake kiunoni mara tu baada ya kuijua janja ya mzee yule. Risasi aliyoiachia Alan ikalichapa tumbo la Dokta Richard huku ikiacha tundu dogo kwa mbele na nyuma ikiuchangua uti wa mgongo wa mzee huyo kutokana na ukaribu uliopo na nguvu ya risasi ile. Dokta Richard Bango akabakia akiachama kinywa chake huku akisukumwa nyuma na kupita dirishani. Miguu yake ikawa imenasia kwa ndani lakini kiwiliwili chote kikiwa nje. Alan alimuwahi ili kumkamata miguu hata hivyo alichelewa, Dokta Richard akachomoka na kushuka chini ya jengo lile akiwa na bastola yake mkononi huku akiwa amejifunga shuka tu kiunoni. Alan alipanda pale kitandani na kuchungulia chini, alijikuta akifumba macho mwenyewe kutokana na picha ya kutisha aliyoiona ikitokea chini ya jengo lile baada ya Dokta bango kutua chini kwa kishindo. Hata hivyo hakudumu sana pale dirishani, alirudi ndani na kuipekuwa ile nyumba kuanzia pale chumbani hadi sebuleni kisha akahamia kwenye upande ule wa mlango uliokuwa umefungwa kote huko hakuna kitu alichoambulia. Akiwa anataka kutoka na kuzima taa akiwa kwenye upande ule wa mlango uliokuwa umefungwa kwa kufuli, akavutiwa na simu ndogo iliyokuwa chini ya meza, akahisi labda huwenda simu hiyo ilianguka na mwenye simu hakuwa ameiona. Akaiokota na kuiangalia kama ilikuwa nzima ama lah! Simu ilikuwa nzima na ilikuwa haijazimwa, akaipekuwa kwenye sehemu ya majina. Akakuta hakuna jina lolote, akahamia kwenye namba zilizopigwa nako hakukuwa na kitu alipoiangalia kama ilikuwa na laini, akagundua kuwa laini ilikuwepo lakini haikuonekana kama ilikuwa ikitumika. Huwenda ndiyo maana muhusika akaitelekeza huku kwa kuwa haikuwa na madhara. Akawaza Alan huku akihamia upande wa jumbe zilizotumwa na alizotuma mmiliki wa simu hiyo. Kwa upande wa jumbe alizotuma mmiliki wa simu hiyo yaani sent box, hakukuwa na kitu lakini kwenye jumbe alizotumiwa yaani inbox, akakuta ujumbe mmoja tu mfupi wa maneno. Akaufungua na kuusoma. 'Nitakuwa Soni siku ya Alhamisi saa tatu usiku hivyo ni vema tukaonana hapo Dokta maana sitakuwa na muda kwani ni kwa ajili ya matekelezo ya kusafisha kontena jingine lenye bidhaa zenye sumu.'
"Shiit!" Alan aling'aka huku akiifumbata ile simu kwenye mkono wake wa kulia. Alishikwa na ghadhabu sana kuhusiana na harakati hizi za watu hawa. Wanataka kutekeleza mpango wa kuteketeza kontena jingine lenye bidhaa sumu? Inamaana walishateketeza moja au zaidi ya moja lakini sasa ni kontena lipi hilo? Na kwanini wakutanie Soni na si mahala pengine. Soni kuna bandari? Alijiuliza Alan na hakupata jibu hata kidogo kichwa chake kikabaki kikiwa na bumbuwazi kubwa sana. Alijiona akizongwa na mambo mengi sana, hata moja hajafika nalo mwisho anakuta jingine jipya likiibuka na hakukuwa na mtu mwingine wa kulitatua isipokuwa yeye.
Alichanganyikiwa.
Aliitazama ile simu kisha akautazama ule ujumbe kujua ulitumwa lini. Akagundua ulitumwa siku ya juma nne saa 16:30 alasiri. Inamaana kuwa ni siku ya usiku huo wa kuamkia siku inayofuata ambayo ni juma tano. Akatazama jina au namba ya mtu aliyepiga akakuta hakuna namba. Inamaana hii ilikuwa ni 'private number' namba inayofichwa kwa makusudi maalumu. Alighadhibika Alan na kuipiga chini ile simu na kuifanya ichanguke vibaya sana. Akakimbilia dirishani upande wa nyuma akachungulia na kuuona mwili wa Dokta ukiwa uko palepale ukimwaga damu hovyo. Akatoka mule ndani na kuufunga mlango kama ada kisha akaufunga na ule mwengine kwa komeo na kushuka ngazi kurudi chini. Alipotazama saa yake ilikuwa ni saa saba usiku, alijipongeza sana kwa kujua kuutumia muda vema.
Akatazama jina au namba ya mtu aliyepiga akakuta hakuna namba. Inamaana hii ilikuwa ni 'private number' namba inayofichwa kwa makusudi maalumu. Alighadhibika Alan na kuipiga chini ile simu na kuifanya ichanguke vibaya sana. Akakimbilia dirishani upande wa nyuma akachungulia na kuuona mwili wa Dokta ukiwa uko palepale ukimwaga damu hovyo. Akatoka mule ndani na kuufunga mlango kama ada kisha akaufunga na ule mwengine kwa komeo na kushuka ngazi kurudi chini. Alipotazama saa yake ilikuwa ni saa saba usiku, alijipongeza sana kwa kujua kuutumia muda vema. Akaenda kule nyuma ulipoangukia ule mwili wa Dokta Bango ambao ulikuwa hauna uhai tangu unatoka kule juu. Akazichukua zile bastola mbili moja ikiwa ni ile iliyotangulia na nyingine ikiwa ni ile aliyoshuka nayo muhusika akiwa ameing'ang'ania mkononi. Alilifungua lile shuka na kuufunika ule mwili huku zile bastola akiziweka juu ya ule mwili ndani ya shuka kitaalamu kabisa ili zisionwe kirahisi huku akihakikisha haachi alama hata moja ya uhusika wake. Alan aliondoka hapo akiwa mzito sana wa mawazo kichwani mwake. Kichwa kilikuwa kikimuuma sana. Mambo aliyoweza kuelezwa ni mazito hata hivyo alijiona yupo kwenye sintofahamu kubwa kutokana na kutokuyajua yote kwa undani. Alipokuwa ndani ya gari yake akiyasoma mazingira ya eneo hilo, wazo la kuwa Mzalendo alikuwa akiuawa siku inayofuata huko Kibaranga likamjia. Akafikiri umbali wa kutoka hapo hadi huko Kibaranga ulikuwa ni zaidi ya kilometa 10 akafikiria na njia pia na ubovu wa barabara. Akaona anaweza kufika kabla hata ya saa kumi alfajiri kama atapitia njia ya Amboni kisha Pande hadi Mjasani ambako huko angeeiacha njia ya kwenda kijiji cha Kwangena hadi Bamba na kukamata njia itakayomfikisha huko Kibaranga. Hakutakiwa kusubiri kukuche kwani endapo angesubiri asingefanikiwa kumkuta huyo mtu anayefahamika kwa jina la Mzalendo wangekwisha kumuua na safari yake isingekuwa na maana yoyote.
_____________
Ulikuwa ni mwendo mrefu mno na wa kuchosha, muda huo Alan alikuwa akiiacha barabara ya lami iliyokuwa ikielekea Maramba, Horohoro na kuingia kushoto akiifuata barabara iliyokuwa ikielekea Digo; Pande hadi Mjasani. Huko alikuwa akipambana na changarawe na mawe madogo madogo barabarani. Giza lilikuwa kubwa na njia yenyewe ikipambwa na vichaka vidogovodogo, baadhi kukiwa na nyasi nyingi ndefu, mapori machache na nyasi fupifupi wakati mwingine. Kimya kilikuwa kikuu sana na cha kutisha, kuna wakati alikuwa akijiwazia mambo ya ajabu hadi kupelekea kujitisha mwenyewe na kumfanya ajikute akiichukia kazi yake hiyo ya kijasusi. Japo alikuwa akiifanya kazi hiyo ndani ya taifa lake hata hivyo haikuwa ndogo na ilitishia maisha yake kwa kiwango kikubwa sana. Alianza kuipita miti mikubwa ya miembe huko Pande au Digo kwa umaarufu wake. Barabara ilipambwa na miti mikubwa ya miembe Viringe pembezoni mwa barabara kiasi kupelekea uwepo wa giza la kutisha na utulivu mkubwa. Alan alipoona ukimya ulikuwa umemzonga sana. Aliwasha redio yake iliyopo garini na kuchomeka flashi diski iliyopo kwenye dashibodi ya gari yake kisha akauruhusu muziki laini wa kinyumbani ukawa unamburudisha. Alichomoa pakiti ya sigara kutoka kwenye mkebe mmoja wa kwenye dashibodi na kuchomoa sigara tatu akazitupia juu ya dashibodi na kuvuta kiberiti cha gesi na kujiwashia sigara yake na kuanza kuivuta. Muziki na sigara vikawa maliwaza wake. Mwendo wa gari ukaongezeka hadi alipofika Mjasani Darajani.
Hapo mvua kubwa ikawa inanyesha kwa fujo sana kiasi cha kushangaa iweje kote huko hakukuwa na mvua na aje aikute mahali hapo. Hata hivyo hakuwa na namna kwani hiyo ilikuwa ni kazi ya Mungu pia hicho kilikuwa ni kipindi cha vuli hivyo kunyesha kwa mvua za mara kwa mara halikuwa ni jambo lenye kushangaza sana. Alan aliliacha daraja kwa upande wa kulia na kuingia barabara ya upande wa kushoto ambayo ilikuwa mbovu yenye mawe na mifereji mibaya iliyokatiza barabarani, ni baadhi ya sehemu tu ndizo ambazo zilikuwa zikipitika kwa wepesi lakini sehemu nyingine zikihitaji umakini mkubwa katika uendeshaji. Hakuwa na shaka na gari yake. Toyota Harrier hiyo ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kazi yake hiyo ya kijasusi na ndiyo maana ikawa ni mingoni mwa gari alizowekewa na kitengo chake cha kijasusi nchini ikiwa ni pamoja na gari nyingine ya kazi aina ya Pegeout 404 ambayo ilihifadhiwa kwenye maegesho ya magari ya Mkonge Hoteli. Alan aliendelea kuvuta sigara yake taratibu na hiyo ikiwa ni sigara ya mwisho miongoni mwa zile tatu alizokuwa ameziandaa. Gari ilikuwa imechafuka kwa tope vibaya mno kiasi kwamba hata rangi yake ilikuwa ni ngumu kutambulika sawasawa, hata hivyo aliweza kuimudu barabara hiyo vema ingawa alikuwa na uchovu uliokithiri. Gari ilikuwa ikiingia kijiji cha Kibaranga taratibu huku ikipokewa na ukimya mzito. Mvua kubwa bado ilikuwa ikiendelea kunyesha na alipotazama majira ilikuwa bado ni saa kumi alasiri. Huu ndiyo muda ambao alijitabiria. Alikwenda na gari yake na kwenda kuitelekeza kwenye jengo moja lililokuwa ni miongoni mwa kambi za wafanya kazi wa mashamba ya mkonge kipindi hicho cha Mwalimu. Aliyasoma kwanza mandhari ya hapo kwa umakini mkubwa. Yalikuwa ni mandhari tulivu yasiyo na hata dalili ya kuwa na watu. Akazitazama nyumba kadhaa za kambi ambazo kwa kipindi hiki nyumba hizo zimekabidhiwa wananchi wa kawaida mara baada ya mamlaka ya mkonge kushindwa kuyaendeleza mashamba hayo ambayo yalikuwa ni ma-ekari na ma-ekari. Mashamba hayo yalikuwa yameanzia Mpakani mwa Maramba; Kauzeni, baadhi ya sehemu za Muhinduro, nyuma ya kijiji cha Bamba, Kichangani, Jirihini, Bantu, Lanzoni ambako nako pia kulikuwa na kiwanda cha kuchakata Mkonge na kujengwa kwa kambi nyingi za wafanyakazi, mpakani mwa kijiji cha Mavengero, Darajani ambako kulikuwa na jumba kubwa la Sido almaarufu Kwamayowa. Pia mashamba hayo yaligusa mpakani mwa kijiji cha Mwarimba, Kwangena na Mjasani ambako nako kulikuwa na kiwanda kikubwa kabisa cha kuchakata mkonge na uandaaji malighafi safi ya zao hilo. Kote huko kwa sasa kumekuwa ni mashamba ya wanachi baada ya serikali kutoa tamko la wananchi kupewa maeneo kwa ajili ya kilimo na tamko hilo lilitolewa na Rais wa awamu ya tano Muheshimiwa John Jesph Pombe Magufuli kupitia kauli yake ya HAPA KAZI TU ingawa kwa sasa zipo tetesi kuwa mashamba hayo yameanza kuwa mtihani mkubwa baada ya wanaojiita wenye mamlaka kuwapora wananchi mashamba hayo na kuanza kupandwa tena mkonge upya. Kama ni kweli hili lipo basi serikali haijawatendea haki wananchi wake ambao walimwaga jasho jingi katika kuyaandaa mashamba hayo leo hii yachukuliwe kiholela tu pasipo kiwafuta machozi.
Jicho lile ambalo serikali iliyatazama mashamba hayo na kuona mashirika yenye mamlaka hiyo ikishindwa kufanya kazi kwa nguvu na kupelekea kuuwa baadhi ya viwanda kama kile cha Mjasani, Lanzoni, Kauzeni na Kibaranga huku ikibakisha viwanda vichache ambavyo navyo vinasuasua kama kile cha Muheza Estet na Ulowa na vingine vichache ambavyo hivi ndivyo vinavyochakata mkonge huku kukiwa na uhaba wa viwanda vya kutengeneza kamba zenye ubora ule unaotambulika hapa nchini. Ni viwanda vichache tu na vidogo vilivyosalia na vyenyewe vikiwa haviwezi kukidhi mahitaji ya bidhaa hiyo kikamilifu kutokana na uchakavu wa mashine zake na ukongwe wa mitambo ya viwanda hivyo.
Alan aliweza kujihakikishia ubovu wa majengo hayo ambayo zamani yalitumika kama kambi za wafanya kazi hata hivyo hilo halikumhusu, mara baada ya kujihakikishia usalama na kuliweka eneo lote lile kwenye ubongo wake. Alan alichukua koti refu la kijasusi la kujikinga na mvua lililokuwapo upande wa nyuma wa gari yake. Akalivaa na kufungua mlango na kuteremka. Alikuwa amevaa kiatu kikubwa cheusi cha kijeshi miguuni na glovu za kazi huku bastola yake ya kazi akiishindilia vema kiunoni mwake baada ya kuhakikisha kuwa ilikuwa na risasi za kutosha. Alipiga hatua za taratibu akikatisha kwenye jengo hili na lile huku akiwafikiria waliolala ndani ambao hawakuwa wakijua chochote kilichokuwa kikiendelea upande wa nje. Alitamani sana kuwa kama wao na kuwaza pengine nyakati kama hizo angekuwa amelala fofofo hata hivyo aliipenda mno kazi yake ya kijasusi na kila awapo kazini alijiona ni mtu muhimu sana hapa nchini na mwenye kutegemewa hivyo kujikuta akifanya kazi kwa ari kubwa na umakini mkubwa. Alizimaliza zile nyumba ambazo zilikuwa ni za makazi ya watu wa kawaida kisha akakipita kichaka kimoja kilichokuwa kimefungamana hadi alipokuja kutokea kwenye uwanja mdogo ambao ulijaa magofu mengi ya majengo yaliyovunjika. Akaweka umakini zaidi huku akiingia kwenye gofu moja na kutokea kwenye gofu jingine. Akafika mahali akawa anatazamana na jengo refu ambalo kwa juu lilikuwa limeezuliwa paa lake mwanzoni huku rangi ya kuta zake zikiwa zimepapatuka baadhi ya maeneo na kulifanya jengo hilo kuwa na picha ya kutisha sana. Taa zilikuwa zikiwaka kwenye jengo hilo tu na sauti ya kitu mfano wa Jenereta likiwa linaunguruma ikisikika kwa umbali fulani. Kila kitu kwenye kijiji hiki kilikuwa kimeharibika, hata umeme kulikuwa hakuna na ilishangaza sana kijiji kama hiki ambacho kilikuwa na umaarufu mkubwa kukosa hata umeme wa msaada. Njia zake zilikuwa mbaya sawa hata hivyo zilikuwa zikipitika sasa ni maajabu makubwa kuona kijiji hiki kimekufa na kila kitu huku wananchi wanaokipenda kijiji chao wakiishi gizani kama wakimbizi wa kivita.
Hii ilishangaza sana.
Nyumba zote zilikuwa gizani huku wachache wanaojiweza ndiyo pekee ambao walitumia umeme wa nguvu za jua.
Alan alilisogelea hili jengo kwa namna ya pekee sana, alikimbia akiwa ameinama kiunoni kwenda juu mfano wa namba saba huku akizikwepa taa zilizokuwa zimepandwa kwenye jengo hili. Alifika kwenye ukuta akabana na kutazama mandhari ya eneo hili, kimya kilikuwa kikubwa sana. Akaambaa na huu ukuta taratibu hadi akatokea upande mwingine ambao ulikuwa ukiwaka taa kali mno. Hapa akachungulia kwa kificho na kuwaona walinzi wawili wakiwa wanapishana kwa kutembea hapa na pale silaha zao zikiwa mikononi tayari kwa kufanya lolote. Akafikiri namna ya kuweza kuwamaliza hawa walinzi kisha kuzama kwenye hili jengo kubwa. Akasubiri kwa kitambo kingi akiwategea walinzi wale waweze kusogea alipo yeye hata hivyo alijikuta akipoteza muda huku walinzi wale wakiwa hawana dalili ya kumkaribia. Akatoa bastola yake iliyofungwa kiwambo maalumu cha kuzuia sauti na kuwasubiri wakae gizani. Punde wakawa gizani kweli. Aliwashambulia kwa kasi kubwa kwa kuwalenga vichwani ili wasiweze kupiga hata kelele. Wale walinzi wakadondoka kimyakimya, Alan alikuwa tayari ameshalisoma eneo lile vizuri hivyo hakuona mlinzi mwingine. Haraka sana akatoka pale na kuzama ndani ya lile jengo kubwa ambalo halikuwa na mlango. Jengo hili lilikuwa kubwa sana na lililowazi kwa ndani mithili ya godauni, ndani kulikuwa wazi kabisa. Jengo hili kwa uzoefu wake aliamini kuwa lilikuwa likitumiwa kwa shughuli za uzalishaji wa malighafi ya mkonge. Hivyo lilikuwa likitumika kama sehemu ya kuendeshea mitambo mabalimbali. Sasa kulikuwa hakuna mtambo wala mashine ya aina yoyote lilikuwa wazi kabisa. Inawezekana mashine hizo ziling'olewa na mamlaka husika baada ya kushindwa kuendesha kiwanda ama watu wachache ndiyo wamefanya kazi hiyo kwa maslahi yao binafsi huku wananchi wakimalizia makombo kwa kung'oa vipande vya vyuma, reli zilizokuwa zikitumiwa na viberenge vilivyokuwa na kazi ya kubeba na kusambaza mkonge wakienda kuviuza kama vyuma chakavu. Sasa lilibakia kama behewa la garimoshi lisilo na kiti hata kimoja, hakika lilitisha. Akiwa anakaribia mwisho wa lile jengo Alan, akasikia sauti ikipiga 'ta, ta, ta, ta! Kila baada ya muda fulani. Ilikuwa ni sauti ya saa ya mshale. Akatazama kwa umakini upande ule wa mbele kisha akageuka nyuma kwa kasi sana, kote kulikuwa kimya. Mbele hakukuwa na njia na nyuma kulikuwa kutupu. Akadhani ni akili yake labda ilikuwa imezongwa na mawazo mengi, akatuliza akili na kusikiliza kwa umakini zaidi. Ile sauti ilikuwa ikiendelea kulia. Akasogea hadi mwisho kisha akalisogelea dirisha la ubavuni mwa ukuta wa jengo lile, akachungulia nje kwa tahadhari kubwa. Akaona kwa nje kulikuwa na jengo jingine dogo ambalo mlango wake ulikuwa umefungwa kwa kufuli imara. Alipochungulia vizuri, chini ya lile dirisha kulikuwa na mlinzi aliyekuwa amestarehe kwenye kiti, alipomchunguza akapata kuona alikuwa amevaa saa kubwa ya mshale mkononi na alipoweka utulivu huku macho yake yakiwa kwenye ile saa, aliweza kujihakikishia kuwa hiyo ndiyo iliyokuwa ikipiga kelele kwani sauti na mjongeo wa mshale wa sekunde wa saa yake vilishabihiana. Alijisifu kwa kuwa na masikio yenye usikivu mkubwa hasa awapo katika utulivu wa kazi ilikuwa ni kazi ngumu sana kuweza kusikia sauti ya mjongeo wa mshale wa sekunde uwapo mahali pa kutia hofu kama hapo. Hakika alijipa kongole. Kwanini walinzi wote hawa? Akawaza Alan kisha akajiuliza tena kama kuna kitu gani ambacho kilikuwa kikilindwa kiasi kile. Alipoona hakuwa na jibu. Akatoa kamba yake ya manila mfukoni na kuishika ncha na ncha akawa anaishusha taratibu chini. Ukuta ulikuwa mrefu sana kwa nje hivyo isingelikuwa rahisi kumshughulikia yule jamaa kwa aina nyingine ya kifo zaidi ya ile ya kumnyonga kwa kamba. Akaishusha ile kamba Alan hadi usawa wa shingo ya yule mlinzi, akailegeza ili asiweze kumshtua wakati akiwa anaizungusha shingoni mwake, bado jamaa yule alikuwa ametopea usingizini. Alipofanikiwa akaizungusha kwa kasi kubwa kwenye shingo, yule mlinzi akashtuka na kuikamata ile kamba hata hivyo alichelewa. Alan alishika madhubuti na kubembea kwa upande huu wa ndani kiasi kwamba mlinzi yule alishindwa kuing'ang'ania ile kamba akaiachia ikalikaba koo lake barabara. Alifurukuta kwa kitambo kidogo bila kelele hatimaye akatulia na kulegea. Akalegeza ile kamba na kumkalisha tena kama awali huku akiirudisha kamba yake na kuikunja kama mwanzo akairudisha mahala pake. Alilitazama lile eneo. Lilikuwa kimya bado. Akaona hakuna njia nyingine zaidi ya ile ya pale dirishani ili kuweza kulikabiri lile jengo dogo la upande huo hivyo aliparamia dirisha na kushuka taratibu hadi alipodondokea upande wa nje. Huku akakutana na balaa, balaa lisilosemekana.
NINI TENA KIMEMKUTA ALAN.
MWISHO WA SEASON 1... ENDELEA KUFUATILIA SEASON 2
0 comments:
Post a Comment