Search This Blog

Saturday, 24 December 2022

ULIMWENGU MZIMA KIGANJANI MWA CIA - 2

   http://pseudepigraphas.blogspot.com/2020/06/ulimwengu-mzima-kiganjani-mwa-cia.html

Simulizi :  Ulimwengu Mzima Kiganjani Mwa CIA

Sehemu Ya Pili (2)



Hatua hii ilifatia baada ya tishio la kusambaa kwa ukomunist ulimwenguni kuwa mkubwa, CIA ilipanua shughuli zake kukabiliana na mambo ya kiuchumi, kisiasa na mambo ya kijeshi katika kulinda masilahi ya Marekani, na wakati mwingine kutumia njia za hatari ili kulinda maslahi hayo ya Marekani, Mkurugenzi wa CIA kwa wakati huo, Allen Dulles, alikuwa na wajibu wa kusimamia operesheni hizo duniani kote, hivyo jioni ya tarehe 7 mwezi 8 1960 Allen Dulles alituma ujumbe wa maneno kwenda kwenye kamati maalumu ya usalama wa taifa nchini Marekani, ujumbe huo uliokuwa na code namba SO444.PO1117 ulipokelewa na mwana mama Heren McKay aliyekuwa ofisni siku hiyo, Kwenye jengo la CIA Langley kulikuwa na kikao kilefu kilichomalizika saa 5:52 usiku kikao hicho kiliwajumlisha Rolando Cubela,Desmond Fitzgerald, Robert Kennedy, Bw. L.M. Lemnitzer, na Allen Dulles mwenyewe.


Azimio la kikao hicho ilikuwa ni kumshawishi Raisi Dwight D. Eisenhower kuhusu mpango wote ulio wasilishwa mezani na Rolando Cubela wa namna ya kuivamia Cuba, azimio hilo ulikuwa na mapendekezo matatu, Mosi ni kumshawishi Raisi Eisenhower kuidhinisha uvamizi huu bila kulishirikisha bunge, maana kama wangelishirikisha bunge wabunge wasingekubali kwasababu mda mfupi nchi ya Marekani ilikuwa inajiandaa kuingia kwenye uchaguzi mkuu, hivyo wanasiasa wengi wasingekubali kujitia doa wakati wakijianda kugombea nafasi mbalimbali, lakini hapo hapo chama cha Republican kisenge unga mkono mpango huo, hivyo waliona mpango huo ungependeza kama Raisi Eisenhower mwenyewe autekeleze kwa siri.


Pili, walipendekeza kuwa mpango huo utekelezwe na CIA wenyewe bila kushirikisha Kitengo kingine, hii ili kuwa na maana moja kubwa kuwa kwakuwa Marekani ilikuwa kwenye vita baridi na Urusi hivyo kuruhusi vyombo vingine kuhusika ingehesabika kuwa ni vita, hivyo Urusi ingeingilia kati na kuufanya mpango kuwa mgumu, swali la kujiuliza hapa ni kwanini Marekani iliiogopa Urusi kuingia kwenye vita hivyo? Lakini swali lingine zaidi la kujiuliza je ni kuwa Marekani haikuwa na uhakika na mpango huo? Yote haya nitayaeleza huko mbele.


Pendekezo la Tatu, ilikuwa ni wakati wanaivamia Cuba, lazima tukio la uvamizi lifanywe na wa Cuba wenyewe ili ulimwengu usione kuwa uvamizi huo taifa la Marekani halihusiki kwa namna yoyote ile.


Hivyo mapendekezo hayo yote matatu yaliwasilishwa na Rolando Cubela ambae alipewa kazi hiyo na Allen Dulles, kikao hicho kiliidhinisha mapendekezo hayo ambayo yalitakiwa kufika mezani kwa Raisi Eisenhower ikulu ya White house, wakati hayo yakiendelea ule ujumbe wa maneno wenye code namba SO444.PO1117 uliopokelewa na mwana mama Heren McKay aliyekuwa ofisni siku hiyo, Bi,Heren McKay ndie aliyekuwa msaidizi binafsi wa Raisi Eisenhower kwenye ikulu ya White house, mara moja akampelekea ujumbe huo raisi ofisini kwake, alimkuta Raisi Dwight D. Eisenhower akiwa na kikao na maafisa kadhaa wa ikulu, baada ya muda Raisi Dwight D. Eisenhower akakutana na Heren McKay, ambae alimkabizi ujumbe rais, ujumbe huo ulikuwa ukiomba Raisi Eisenhower kuandaa kikao maalumu na Allen Dulles, kwakuwa kikao hicho kilitakiwa kuwa na siri kubwa, utaratibu huu ulikuwa umezoeleka kati ya Allen Dulles na rais Eisenhower pale walipokuwa wanataka kuzungumzia mambo mazito yaliyoitaji siri kubwa za bila kuhusisha vyombo vingine.


Tarehe 20 mwezi wa 8, 1960...


Kwenye ofisi ya raisi wa Marekani oval office, White house Raisi Eisenhower alikutana na Allen Dulles, kujadili mapendekezo ya uvamizi wa Cuba, baada ya mazungumzo ya muda mrefu Raisi alikubali mapendekezo hayo lakini akapinga kufanyika operation hiyo bila kuishirikisha kamati maalumu ya usalama wa taifa hilo kwani Raisi Eisenhower alimtahadharisha Dulles kuwa mpango huo ungeitaji fedha katika kufanikisha mkakati huo, japo Allen Dulles alijaribu kumuonesha Raisi Eisenhower madhara ya iwapo mpango huo utahusisha vyombo vingi kungekuwepo na hatari ya mpango huo kugomewa.


Raisi Eisenhower alimuhakikishia Dulles kuwa mambo yangekwenda vizuri, tarehe 25 mwezi wa 8 1960 Raisi Eisenhower aliomba kikao na maafisa kadhaa wa Kamati Maalumu ya Viongozi wa Juu Kijeshi nchini Marekani yani Joint Chiefs of Staff Committee, ili kuweza kuwashawishi kumuunga mkono katika mpango wake wa kuivamia Cuba, Raisi Eisenhower aliwaeleza namna gani serikali ya Castro wanavyozidi kuwa tishio na kuhatarisha masrahi ya Marekani ukanda nzima wa America ya kusini, Rais Dwight D. Eisenhower aliwaomba maafisa hao kupokea mapendekezo ya shirika la CIA ya kuanza matayarisho ya kuivamiaCuba na kuupindua utawala wa Castro.


Baada ya kamati hiyo kulidhia mpango huo bado walisisitiza kuwa Raisi lazima mpango huo aupeleke mbele ya baraza la mawaziri ili uidhinishwe na kupewa baraka na serikali, hatua hiyo ilikuwa muhimu kwasababu mpango huo ulionekana kuhusisha hatua nyingi mpaka kukamilika kwake, hivyo lazima mpango huo ungeitaji fedha katika kufanikisha mkakati huo.


Rais Eisenhower alilidhia hilo na kukutana na mawaziri wake tarehe 2 mwezi wa 9 mwaka 1960, ambapo baraza la mawaziri kwa pamoja waliidhinisha mpango huo kwa azimio namba 7186 na kuiruhusi CIA kuendelea na operation hiyo, japo walitaka mpango huo kuwa na tahadhari sana, ili kuiepusha Marekani na kelele za kimataifa.


Hivyo...


Raisi Eisenhower akaikabidhi CIA faili la mapendekezo ya kuanza maandalizi ya maauji ya Castro na uvamizi wa Cuba, hatimae asubuhi ya Tarehe 13 mwezi wa 9 mwaka 1960, Kamati Maalumu ya Viongozi wa Juu Kijeshi nchini Marekani (Joint Chiefs of Staff Committee) chini ya Bw. L.M. Lemnitzer, iliidhinisha Operesheni iliyopewa jina la "Northwoods", kwa lengo la kutafuta sababu ya kuivamia kijeshi nchi ya Cuba, Chini ya operesheni hiyo, kamati ilipendekeza mfululizo mashambulizi yenye taswira ya kigaidi ndani ya miji ya Miami, Washington, D.C na kwingineko, meli za mizigo na abiria za nchi ya Marekani zingelipuliwa au kuzamishwa, ndege kutekwa, mauaji ya raia kutekelezwa makusudi, utoaji wa orodha 'feki' za wahanga wa mashambulizi ili kuufanya umma wa Wamarekani kuingia taharuki na kuipigia kelele za hasira serikali kulipiza kisasi kwa kuivamia Cuba. Kwa mujibu wa mpango huo, kila shambulizi lilipangwa kuhusishwa na nchi ya Cuba, lakini mipango yote hii ilitakiwa kusimamiwa na CIA.


CIA nao wakaandaa njia ambazo watazitumia kumuua Castro, njia hizo ziliandaliwa kwa ustadi wa hali ya juu na ubunifu wa hali ya juu, kwa mfano, vidonge vya sumu, mlipuko wa meli ya mafuta baharini, pia CIA ilitayarisha mpango maalumu wa mazumgumzo ya amani ya siri na Castro lakini lengo likiwa ni kumuua Castro kwa kumtumia mwanamapinduzi wa Cuba ambae alikuwa shushushu wa Marekani akiwa ni wakala wa CIA, wakala huyu alitwa Rolando Cubela, ambae alipangwa kumuua Castro kupitia shamburizi kwenye mkutano huo, alafu mauaji hayo yatafsirike kutekelezwa na Mcuba hivyo Marekani ijivue lawama za kuhusika, mpango huo ulipangwa na ofisa wa CIA aliyeitwa Desmond Fitzgerald, ambaye angejifanya yeye ni mwakilishi maalumu wa Robert Kennedy.


Mipango yote hiyo ikaonekana kushindwa hivyo ikafikiliwa mpango mkakati mwingine utakao leta matokeo chanya katika kufanikisha mkakati wao, ndio wakaja na mpango mpya wa kuivamia Cuba kijeshi, mpango huu ndio uliokuja kujulika kama "Uvamizi wa Bay of Pigs".


Bay of Pigs ilivyoratibiwa...


Uvamizi wa Bay of Pigs ulikuwa ni uvamizi wa taifa la Marekani kuivamia Cuba kupitia Ghuba ya nguruwe, ghuba hii ipo nchini Cuba kaskazini Magharibi mwa visiwa vya Cuba, uvamizi huu ni moja ya uvamizi mkubwa kufanywa na Marekani ambao ulishindwa kwa aibu kubwa, kwani uvamizi huu ulishindwa pamoja na kufadhiliwa na Marekani kwa fedha nyingi karibu dola billion 1.3 dhidi ya kuivamia Cuba mwaka 1961.


Uvamizi huu kwa Kiingereza unajulikana kama "The Bay of Pigs invasion" na kwa Kihispania unajulikana kama "invasión de bahía de Cochinos" wakati mwingine pia uvamizi huu huitwa "invasión de playa Girón" au "batalla de Girón", yaani mapigano ya Playa Girón.


Kama nilivyokwisha sema hako mwanzo kuwa hili lilikuwa ni jaribio la mapigano yaliyoshindwa ambapo serikali ya Marekani iliwafadhili Wacuba waliokuwa wakiishi uhamishoni kujaribu kuipindua serikali ya Cuba iliyoongozwa na Fidel Castro, uvamizi huu ulianzia kuvamia sehemu ya Kaskazini ya Cuba, Shirika la Ujasusi la Marekani CIA katika kufanikisha uvamizi huu lilifadhili kundi la waasi la Brigade 2506, ntalieleza kundi hili baadae kidogo, hivyo kundi hili ndilo lilofanya shuguri ya kuvamia Cuba tarehe 17 Aprili mwaka 1961 Katika mapigano ambayo yalichukua siku tatu.


Kundi la Brigade 2506...


Kundi hili la Brigade 2506 lilikuwa ni kundi la wapingaji wa Mapinduzi ya Cuba na serikali ya Fidel Castro ambao wengi wao walisafiri kwenda uhamishoni Marekani baada ya Castro kuwa ameitwaa Cuba baada ya kuiangusha serikali ya Dikteta Fulgencio Batista mwaka 1959, mapigano hayo pia yaliwahusisha baadhi ya wataalaamu wa kijeshi wa jeshi la Marekani.


Kundi hili likiwa wamepawa mafunzo na kufadhiliwa na CIA, kundi hili la Brigade 2506 lilikuwa ni tawi la kijeshi la chama cha Democratic Revolutionary Front (DRF) ambao walidhamiria kuipindua serikali ya Fidel Castro ambayo ilionekana inaegemea kwa kasi kwenye siasa za mrengo wa Ukomunisti, mipango yote ya kuvamia na kuipundua serekali ya Castro iliratibiwa huko nchini Guatemala na Nicaragua, majeshi ya uvamizi yaliandaliwa chini ya usimamizi wa Marekani, ambapo yakiwa huko walipokea malipo ya fedha kwa kila askali, walihaidiwa fedha zaidi na nafasi za uongozi ikiwa watayatwaa Madaraka.


Turudi nyuma kidogo ili kulifahamu kundi la "Democratic Revolutionary Front (DRF)"....


Ni kwamba mwaka 1952 nchini Cuba yalifanyika mapimduzi yaliyoongozwa na Generali Fulgencio Batista, mshirika mkubwa wa Marekani, dhidi ya Rais Carlos Prio aliyekuwa madarakani, mapinduzi hayo yalimlazimisha Rais Prio kuondoka Cuba na kwenda kuishi uhamishoni jijini Miami nchini Marekani, raisi Prio alipo fika huko uhamishoni Rais Prio, akamua kuanzisha kundi la uasi ili kuishambulia serikali ya Batista na kurejea tena Madaraka, kundi hilo likaitwa Democratic Revolutionary Front (DRF), kundi hili ndio baadae wa Marekani wakalitumia kuangusha utawal wa Castro, ikumbukwe kwamba Marekani ilimfadhili Batista kumgoa Prio pia Marekani hiyo hiyo ikaitumia kundi hilo la Prio kumgoa Castro.


January 3 mwaka 1961...


Kule Washington DC mpango wa 'kumnyoosha' Castro ulianza, Mpango huo, ulihusisha utoaji mafunzo maalumu ya kijeshi kwa vijana karibu 1400 kwa siri ndani ya kambi zilizojengwa jimboni Florida katika jiji la Miami, kusini-Mashariki mwa Marekani na nchini Guatemala, Amerika ya kati, Mafunzo hayo yaliandaliwa, kufadhiliwa na kuratibiwa kwa asilimia 100% na serikali ya Marekani kupitia Wizara yake ya Masuala ya Nje halikadhalika Shirika lake la Ujasusi (C.I.A), Wengi wa vijana walioshiriki, walikuwa ni Wa Cuba walioishi uhamishoni, waliompinga Castro na utawala wake.


Mtu aliyepewa kazi ya kusimamia mipango yote ya kuongoza uvamizi wa Bay of Pigs alikuwa ni Richard M. Bissell Jr, Naibu Mkurugenzi wa Mipango wa CIA yaani Deputy Director for Plans (DDP), jasusi huyu ndie aliyefanya kazi ya kutarisha maafisa wengine wengi tu ili kuweza kumsaidia kufanikisha mipango ya jaribio hilo, wengi wao wakiwa wale walioshiriki katika mapinduzi yaliyofanyika miaka sita nyuma yani mwaka1954 huko Guatemala, hawa ni pamoja na David Philips, Gerry Droller na E. Howard Hunt.


Bissell alimkabidhi Droller jukumu la kuwa kiongozi wa kuwakusanya Wacuba wanaompinga Castro miongoni mwa jamii ya Wacuba-Wamarekani wanaoishi uhamishoni na alimuomba Hunt kuunda kitu kama serikali iliyo uhamishoni ambayo CIA itakuwa inaidhibiti, Hunt alisafiri kwenda Havana, mji mkuu wa Cuba, huko alikutana na kuzungumza na Wacuba kutoka katika makundi mbalimbali.

Hunt aliporudi Marekani aliwataarifu Wacuba waioshio Marekani ambao alio kuwa anawakusanya kuwa wanatakiwa wahamishie harakati zao kutoka jijini Florida nchini Marekani na kwenda Mexico City nchini Mexico, kwa sababu idara ya Taifa ya Marekani kwa maana ya State Department ya Marekani imekataa kuwaruhusu CIA kupatia mafunzo yao ndani ya ardhi ya Marekani, kitendo hiki kulikuwa na maana kuu Tatu, Mosi Viongozi wengi waliona kuwa kitendo cha kuwaruhusu wakimbizi kufanya mafunzo ndani ya aridhi ya Marekani ingekiuka sheria za kimataifa ambazo ni kitendo cha uhalamia hivyo ingeichafua Marekani kwenye taswira za kimataifa.


Pili, kwakuwa Marekani ilikuwa kwenye uchaguzi mwezi November 1960, jambo lingeweza kuharibu uchabuzi na kufanya taharuki kwenye majimbo ya kusini ambapo chama cha Republican kilitegemea kupata kura huko.


Tatu, Kwakuwa taifa la Marekani lilikuwa kwenye vita baridi na Urusi, kitendo hicho kingetafsirika na Urusi kuwa uvamizi huo unafanywa na Marekani na sio wa Cuba wenyewe ambao wanaupinga utawala wa kikominist wa Castro, jambo hili serikali ya Marekani ilitaka ulimwengu uamini kuwa wao hawahusiki na chochote ambacho kingeendele huko Cuba.


Ingawa askali hao hawakuwa na furaha kusikia habari hizo, lakini waliipokea amri hiyo, hivyo vituo vya mafunzo vikaamia Mexico city, hatimae baadae wakaamia Nicaragua, Panama na Guatamala kwa mafunzo ya kuingia kuivamia Cuba.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog