Simulizi : Kiapo (Agano La Damu)
Sehemu Ya Nne (4)
Sasa Walikuwa Wakielekea Katikati Ya Mji!,kwa Mwendo Wa Kasi Wakitegemea Nusu Saa Kuingia Jijini!
Moyon Mwa Isack Kulijaa Aman Alitaman Kukutana Tu Na Madam Wake Amsimulie Kilichomkuta!
Sasa Alijua Kwa Madam Ataish kwa amani hakuwa na shaka na madam wake yule kwani upendo alisha anza kumuonesha kabla akajikuta akitabasamu mwenyewe ndani ya gari!
taratibu wakaanza kuingia mjini ambapo walipokelewa na shamrashamra mtahani picha ya mr alex ikiwa ukutani juu pakiwa na maandishi MPENI KURA ANAFAA KUONGOZA JIMBO LETU
"Dah huyu mr alex atapita anaroho nzur sana"
zinja aliongea akiitazama lile karatasi lililobandikwa
"tena si ndo yupo kwenye chama tawala lazima apite"
muda wote Isack Alikuwa Kasinzia Ghafla Akazinduka Na Kutupa Macho Nje Si Akaliona Lile Karatasi
"MUNGU wangu baba anagombea ubunge nimekwisha mimi!.."
Akajikuta Mwenyewe Tu Kazungumza Kwa Sauti
"umekwisha?!,baba Nani?!"
Wote Wakauliza Kwa Pamoja
"huyo Mr Alex Ndo Yule Nlowaambia"
"whaaat?!!!..."
Wote Walishtuka Pasina Kuamin Kile Walichokisikia!,
kasheshe!
No 22
Kitu Chenye Ncha Kali Kikachoma Katikati Ya Moyo Wake Baada Ya Kuona Picha Ile,simanzi Ikamvaa Kumbukumbu Zikatiririka Katika Fikra Zake,akakumbuka Mateso Mtu Yule Alokuwa Akimpa Jinsi Hata Alivyochana Chana Hata Daftar Lake
"yule Si Mtu Mzuri Afai Kuwa Mbunge Afai Kuongoza Hata Jimbo Letu"
Akaongea Kwa Sauti Ya Upole Yamkini Ni Kama Alikuwa Akizungumza Mwenyewe Ila Sauti Yake Ilipenya Mpaka Kwa Wawili Wale Walokuwa Pembeni Yake Dereva Zinja Na Alwatan
"kwel Uyasemayo! Kama Ndo Huyu Mmmh Mbona Makubwa"
Alwatan Akatamka
"but Ya Ngoswe Tumuachie Ngoswe Nje Anajifanya Mzuri Anatoa Misaada Anaonesha Kujali watu kumbe ni bonge la nyoka,chui alovaa ngozi ya kondoo usiwaze dogo soma kwa bidii mbona yataisha tu!"
ZINJA alimtia moyo Safari Ikaendelea Isach Aliwaonesha Njia Mpaka Nyumbani Kwa Madam Jane!
Walifika Kwa Bahati Nzur Walikuta Mlango Wazi Wakaugonga Baada Ya Dakika Chache Zikasikika Nyayo Za Mtu Na Kitasa Kikifunguliwa,awakuwa Na Shaka Kwamba Afunguaye Ndo Madamu Jane Mwenyewe,
***
Ilikuwa Ni Jumamosi Tulivu Kama Wikiendi Zingine Ni Siku Ambayo Mwanadada Huyu Alipenda Kuitumia Kufanya Usafi Katika Nyumba Yake Ile,pamoja Na Kufua
Ila Siku Hii Ilikuwa Tofauti Na Jumamos Nyingine Akuwa Na Raha,Na Akujua Kwa Nin Anakuwa Katika Hali Ile
Isack!...
Jina Hilo Alikumtoka Kichwani,wiki Nzima Iloisha Mtoto Yule Akuonekana Shule Na Akujua Sababu Ya Kutoweka Kwake!,alishanusa Harufu Ya Mateso Ya Mtoto Yule Kivipi Eti Roho Itulie?!
Alikumbuka Kuwa Jibu Alilopewa Na Brayton Alhamis Baada Ya Kumtuma Aende Kwa Wazaz Wake Kuuliza Kwa Nin Mtoto Haji Shule Aliambiwa Kachukuliwa Na Ba Mdogo Wake!
Kama Ni Kwel Kwa Nin Huyo Ba Mdogo Wake Asije Mchukulia Uamisho?! Au Kampeleka Privet?!
Majibu Ya Maswal Yale Yakamfanya Madam Wikiend Ile Imwangukie Vibaya
Alijua Au Alihis Lazima Tu Mtoto Yule Atakuwa Kwenye Matatizo,alijishangaa Moyo Wake Kuteseka Kwa Ajil Ya Mtoto Yule,wakati Akiwa Katika Dimbwi La Mawazo Ghafla Akasikia Kugongwa Kwa Mlango,akijua Pengine Ni Mashoga Zake Akaacha Kufua Na Kufata Geti Akashika Kolea Na Taratibu Akaanza Kufungua Geti Lile!
Ahmad Alichokiona Akuamin Alhisi Pengine Macho Yake Yanamdanganya
Isack Na Vijana Wawili Zinja Na Alwatan Walikuwa Mbele Yake
Isack Hakuweza Kuvumilia Kumkumbatia Madam Wake Yule!,machozi Ya Furaha Yaliyochanganyika Na Ya Uchungu Yalimchuruzika
"wanataka Kuniua Madam!"
Kwa Sauti Ya Upole Isack Akazungumza,sauti Ilopaa Mpaka Katika Ngoma Ya Sikio La Madam Yule
Madam Akahis Amesikia Vibaya,akamwachia Kwanza Isack Akamwangalia Kwa Macho Ya Mshangao Pasina Kuamin Kile Alichokisikia...
"una..Sema..Wanataka Kukufanyaje?"
Madam Akahoji
"Wanataka Kuniua Madam!"
Isack Akarudia Huku Akilia
"kukuua?!,kinanani Ao?"
"mi Siwajui Madam Sijui Nimewakosea Nini Mimi!..."
"basi Mwanangu Usilie Karibuni Ndani Tuzungumze"
Madam Ikabidi Awakaribishe Ndani Sebulen,ambapo Aliwa Andalia Chai Ya Maziwa Na Mikate!
Baada Ya Kumaliza Kunywa Ndipo Walipokaa Chini Kuzungumza Yalomtokea Mtoto Yule Yatima
"ehe Isack Nielezee Sasa Kilichokupata Mdogo Wangu Wiki Nzima Ujaja Shule!"
Ikabid Isack Aanze Kusimulia Kile Kilichotokea,toka Alipotembelewa Na Yule Alojitambulisha Kama Ba Mdogo Kumbe Muuaji! Madam Alisikitika Sana Kumbe Mawazo Yake Yalikuwa Sahihi
"huyo Mtu Unaweza Kumtambua Tukamshtaki?! Na Hiyo Nyumba Unikumbuka"
Madam Jane Akauliza Ila Alwatan Akadakia
"aina aja Tuachane Naye Tu Kwenda Kumshtak Ni Kuzua Mengine Ila Nnachohis Familia Ya Mheshimiwa Inahusika"
"kweli!,"
Wote Wakaitika!,
"sasa Tufanyaje?!"
"cha Kufanya Mtoto Asome Mi Ntaishi Nae Akikuwa Atajua Cha Kufanya Ntamsomesha Ntamvisha...
Wote Walifrah!
Zinja Na Mwenzake Wakaaga Wakiwa Na Uhakika Wamemuacha Sehemu Salama!
Madam Jane Alijitahid Kuwa Muongeaji Kwa Kumfuraisha Isack Kusudi Asipate Muda Wa Kuwa Na Mawazo
Akamnunulia Daftar Mpya Na Sare Mpya Za Shule Jumatatu Wiki Ilofatia Isack Akarejea Shule!
Shule Ile Ile
Alokuwa Akisoma!
***
SURA YA SABA
SHERATON MOTEL
Ni moja wapo ya hotel kubwa ilokwepo katikati ya jiji lile,katika ghorofa ya tatu chumba namba tano ndani ya chumba kile ilisikika minong'ono ya kimahaba!
watu walosema penzi la wizi ni tamu awakukosea na sasa wapenzi wale ambao ni bi neema na mwalimu gibson lilishaota mizizi
azikupita siku mbili bila kukutana na kuirizisha mioyo yao..
Na Pindi Ukiingia Katika Usaliti Lazima Kuwe Na Mabadiliko,ndiyo,hata Kwa Bi Ney Mabadiliko Yalikwepo
Mabadiliko Ambayo Yeye Mwenyewe Akuyajua,akujua Kama Kabadilika!
Mumewe Mr Alex Ambaye Kwa Kipindi Icho Alikuwa Bize Na Kampeni Ya Kugombea Ubunge Baada Ya Chama Chake Kumpitisha Si Kwamba Akuyaona Mabadiliko Ya Mkewe La Hasha!
Ila Yeye Alijaliwa Subira!,alisubiri Kipind Kile Cha Mpito Kipite Ndo Aanze Kufatilia Maswala Ya Mkewe Japo Alijua Mkewe Anamsaliti
Bi Ney Wala Akujal,aliufurahia Ubize Wa Mumewe Na Kuutumia Kubanjuka Na Mwalimu Yule Na Leo Hii Walikuwa Ndani Ya HOteli Ile Ya Kifahari Wakila Raha,
"mpenzi! nkuulize kitu!"
mwalimu gibson akauliza huku akiwa kalaliwa kifuani na mlimwende yule wakiwa kama walivyozaliwa
"niulize tu beby!"
Bi Ney Akatamka Kwa Sauti Aloitolea Puani,sauti Ya Mahaba,sauti Iwezayo Hata Kumtoa Nyoka Pangon Atazame Ni Nani Aitoaye Sauti Ile
"ulisema Isack Kachukuliwa Na Bamdogo Wake? Saiv Yupo Wapi?"
Bi Ney Akashtuka Kwa Swali Lile Ni Kama Akulitegemea Na Pia Akupendezwa Nalo Eti Kakakunja Sura Kuonesha Chuki Zake Waziwazi Kisha Akafungua Domo Lake
"sipendi My,unaniudhi Sasa Kwani Lazima Umzungumzie Huyo Mtoto?! Mfyuuu"
"siyo Ivyo Love!"
"ila?!"
Bi Ney Akauliza..
Akijinyanyua Mapajani Kwa Shababy Yule
"nimekuuliza Hivyo Mpenzi Kwa Kuwa Leo Isack Kaja Shuleni Tena Kapendeza Kin..
"unasema?!"
Bi Ney Akauliza Pasina Kuamini Kile Alichokisikia Mshtuko Alouonesha Hata Mwalimu Gibson Mwenyewe Ulimshangaza!
"ndio!,leo Jumatatu Isack Kaja Shule Tena Kaletwa Na Yule Madam Jane Na Wakati Wa Kuondoka Kampandisha Kwenye Gari Yake Haoooo Wakaondoka Ndo Maana Nkakuuliza Au Yule Madam Ana Undugu Na Yule Mtoto?!"
Mwalimu Gibson Akazidi Kusisitiza Ila Katu Bi Ney Akuamini Kile Alichoambiwa
"una Uhakika Ni Yeye?! Hapana Si Kweli Bhana Utakuwa Umemfananisha"
Bi Ney Alikataa Katakata,mwalimu Gibson Akaachia Kicheko,kicheko Cha Dharau!
"ina Maana Mi Simjui Huyo Isack Au Tena Kaja Na Daftar Zote Mpya...
"subiri Kwanza! Embu Ngojea...
Bi Ney Akamstopisha Na Kuvuta Pochi Yake Ilokwepo Pembeni Ya Kitanda! Akatafuta Namba Ya Mumewe Na Kuipiga Simu Ikaita Na Mara Ikapokelewa
"mume Wangu Una Uhakika Yule Mtoto Alikufa?!"
Bi Ney Aliuliza Pasina Kumjali Yule Mwalimu Alokuwa Pembeni Yake Akiyapapasa Mapaja Yake Taratibu,mwalimu Gibson Alishtuka!
"mtoto?!,mtoto Yupi?!"
Upande Wa Pili Ukauliza
"si Isack,mbona Naskia Yupo Hai?!"
"unasema?! Eti Isack Yupo Hai?"
Mzee Alex Naye Akauliza Pasina Kuamini!
"ndiyo Mume Wangu Kuna Mtu Kanambia Isack Yupo Hai Tena Leo Kaonekana Shulen"
"nakuja Sasa Hivi Hapo Nyumbani"
Mzee Alex Aliongea Na Kukata Simu,bi Ney Naye Bila Kupoteza Muda Akajinyanyua Haraka Haraka Na Kuanza Kuvaa Nguo Zake,bado Mwalimu Gibson Alibaki Katika Hali Ya Sintofahamu
"embu Nieleze Kuna Nin Kinachoendelea Dhidi Ya Huyo Mtoto?"
"kwa Saiv Siwez Kukueleza Kitu Ngoja Niende Nyumbani Nkaonane Na Mume Wangu Ntakutafuta Na Kukueleza Kila Kitu Wacha Niwai Akifika Nyumbani Asinikose"
Bi Ney Alimalizia Na Kuchukua Begi Lake Huyo Akatoka Akimwacha Mwalimu Yule Katika Mshangao
*dah Mambo Yanaanza Kuwa Mabaya Kwa Isack Nin Kitaendelea?!,mzee Alex Atachukua Uamuzi Gani Baada Ya Kugundua Isack Yupo Hai,*
Maisha Yake Yamejaa Mitihani Ambayo Hata Ajui Atavukaje!
Roho Yake Inawindwa Kama Almas Pasina Kosa Lolote,je Nin Hatma Ya Maisha Yake Twende Pamoja Katika Riwaya Hii Utajifunza Mengi!...
NA HII NI SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
Baada Ya Mpenzi Wake Yule Kuondoka Naye Mwalimu Gibson akiwa Sasa Na Rundo La Maswali Naye Akajiinua Kitandani Pale Na Kuamua Kuondoka Akipanga Kesho Yake Shuleni Ampeleleze Isack Na Madamu Jane Kujua Swala Lile Kiundani
Mbio Alizotoka Nazo Sheraton Motel Zilizaa Matunda Kwani Alifika Kabla Ya Mumewe Na Kujikalisha Sofani Kumsubiri Mume Wake!
Dakika Kumi Toka Aingie Na Kujitupa sofani nje ilisikika muungurumo wa gari akuwa na shaka ni mume wake!
ndiyo! akukosea,mzee Alex Alishuka Kwenye Gari Yake Hata Kufunga Mlango Alisahau Alikuwa Na Haraka Kushinda Upesi!
"mama Mery...Mama Mery....Mama..."
Alianza Kumuita Mkewe Mbali Huku Akikimbia Kuufata Mlango,bi Ney Aliishia Kutabasamu Kwani Alimuona Mumewe Kupitia Dirishani Alipofungua Mlango Tu Bi Ney Akaweka Pazia La Pale Dirishani Vizur Macho Yake Akayaamishia Mlangon,mlango Ukafunguliwa,mzee Alex Akaingia...
Pasina Hata Salamu Akaanza Kuuliza
"embu Nambie Vizur Mke Wangu Umesema Isack Yule Mtoto Yupo Hai?!..."
Mzee Alex Akaoji pasina kuamini
"ndiyo mume wangu,mimi mwenyewe nimeshangaa kama wewe nlpopata izo habari"
"si kwel! Zidu Awezi N'danganya Kwanza Ni Nani Kakupa Hizo Habari!"
Bi Ney Akashtuka Kwa Swali Lile Akutegemea Kama Angeulizwa!,akajikuta Akibabaika Kulijibu!,je Angemtaja Mwalimu Gibson Ambaye Ni Awara Ake?!
aikumwingia akilini,akajikuta akibabaika,ila ghafla akapata wazo!
wazo yakinifu!,ambalo alilitendea haki!,akili yake ikafanya kazi zaidi ya kompyuta
"sikia nikwambia baba Mery kuna Yule Mwalimu Alojiweka Karibu Na Mim Kwa Maendeleo Ya Isack Si Unamkumbuka?!"
"yah! Yule Wa Hisabu Siyo!"
"yah!,wiki Ilopita Jumatano Alinipigia Simu Kuniulizia Isack Yupo Wapi Mbona Aji Shuleni!?,basi Mimi Nkamwambia Alichukuliwa Na Ba Mdogo Wake,ila Jana Alinpigia Na Kunambia Isack Karejea Shulen Na Daftar Mpya Kuna Matatizo Gani Baina Yetu Na Mtoto Yule?! Nlishtuka Mume Wang,tena Aliletwa Na Yule Mwalim Wa Kike Na Jioni aliondoka naye!.
"una uhakika na usemacho?"
"niamini mume wangu Isack Yupo Hai"
Mzee Alex Akusema Kitu Akaishika Simu Yake Na Kutafuta Namba Aloisevu Zidu Akaipiga Na Kuiweka Sikioni!
"ni Kaz Ya Kwanza Kukupa Na Ukafeli Kijana!"
Mzee Alex Akakoroma,zidu Akapigwa Na Butwaa
'kafeli?,zidu Katili Katili Kaharibu Kazi!,alikuwa Ni Mtu Aliyejiamini Kwa Kile Akifanyacho Akuelewa Kile Yule Mzee Alichomweleza!
"una Maanisha Nini Mzee?!"
Kwa Sauti Kavu Nzito,sauti Isotetereka Zidu Akahoji! Naye Mzee Alex Akamwambia
"kesho Katalii Shule Ya Msingi Gulioni Akikisha Kila Sura Ya Mtoto Unaiona Utajua Nin Namaanisha,mzee Alex Akaongea Kwa Jeuri,sambamba Na Kukata Simu!
'mmmh Eti Nikatalii Shule Ya Msingi Gulion Nihakikishe Macho Yangu Yanatazama Uso Wa Kila Mwanafunz Kuna Mtu Mwenye Uwezo Huo Kwel?!,mbona Makubwa!,ila mzee yule ana maana gan?!,ni kazi mpya anataka kunipa au!,au nimeharibu kazi! hapana Zidu Aharibugi Kazi'
Zidu Alijiwazia Akiwa Kakaa Katika Sofa Lake Katika Jumba Lake Lile La Kazi,jumba Apendalo Kukaa Kwa Kupumzika,na Kupanga Mipango Yake!
MASAA MACHACHE BADAE:
Muda Usimami,muda Unasogea,masaa Yakasonga,hatimaye Mida Ya Saa Kumi Kasoro Zidu K Alikuwa Ndani Ya Shule Ile Kama Vile Kuna Mtu Anamsubiri Bado Wanafunzi Walikuwa Awajaruhusiwa,ila Wengi Wao Walikuwa Wakizagaa Wengine Wakifanya Usafi,
Ghafla Mlio Wa Simu Yake Ukaskika,ulikuwa Ni Mlio Wa Meseji Akaitazama Simu Yake!.
"kuna Corola Nyekundu Umeiona Ifatilie Corola Hiyo!"
Zidu Akatabasamu,alijua Ni Kazi Mpya Na Katu Akujua Corola Ile Ilikuwa Ni Ya Madamu Jane!,ghafla Mlio Wa Kengele Ukasikika Wanafunzi Wakakusanyika Na Baada Ya Kama Robo Saa Wakaruhusiwa!
Bado Macho Yake Yaliendelea Kuifatilia Corola Ile,ghafla Akapatwa Na Mshtuto Baada Ya Kumuona Mtoto Mmoja Alosimama Pembeni Ya Corola Ile!
Ni Kama Alimsubiria Mwenye Gari Aje!
Kwa Mara Ya Kwanza Zidu Alipatwa Na Mshtuko Usioweza Hata Kuandikika,akuya Amin Hata Macho Yale Alihisi Ayakuona Vizuri!,akafungua Kadroo Kalichokuwepo Katika Gari Yake Akatoa Miwan Ya Macho Na Kuipachika Machoni
Pamoja Na Kuvaa Mawani Bado Taswira Aloiona Ni Ile Ile!,
"ni Yeye Au Wanafanana?!"
Akajiuliza Akizidi Kumkazia Macho Huku Kumbukumbu Zake Zikirudi Nyuma
Akakumbuka Wakati Simba Walipokuwa Wakimshambulia Kule Porin Alipowatupa leo abaki hai!
hapana alikataa katakata!.
Badae madam jane Alitoka Ofisini Akaingia Ndani Ya Gari Ile!,Isack naye akazunguka upande wa pili madam akamfungulia mlango akaingia! akawasha gari na kuliondoa pasina kujua kuna Alokuwa Akiwafatilia!
Zidu Bado Alikuwa Katika Bumbuwazi!,ghafla Gari Ile Ikaanza Kuondoka Naye Bila Kujiuliza Akajikuta Akiwasha Yake Na Kuifata Kwa Nyuma Huku Akijiuliza Kaponaje?! Au Watoto Wale Wapo Mapacha!...
Wakati Akiendelea Kuwafatilia Ghafla Simu Yake Ikaingia Ujumbe Mfupi!
"ukuwaigi Kuniharibia Kazi Ila Nahisi Kwa Mara Ya Kwanza Umeona Utumbo Ulofanya Utarudisha Ela yangu au utafanya kazi?!
zidu akutaka kujibu meseji ile alitaka kuijibu kwa vitendo!
akaachia tabasamu la jeuri!
"kama haka katoto kalipona mara ya kwanza kwenye mdomo wa mamba katika kisima changu!,kakaja kakapona kwenye mdomo wa simba hatopona katika mdomo wa bastola hii atopona kamwe! ngoja nkuoneshe...
akaongeza mwendo gari yake,silaha ikiwa mkonon akielekea upande alokaa Isack Na Kwa Bahati Mbaya Zaidi Kioo Kilikuwa Wazi!,mwanaume Akawasha Taa Ya Kuomba Kupishwa (over Take) Madam Jane Pasina Shaka Akamruhusu Kijana Akakanyaga Mafuta Alipofika Usawa Wa Dirisha La Upande Ule Alioko Isack Akainyanyua Silaha na kumpima!
paaaa paaa paaaaa paaaaaaaa
milio kadhaa ya risasi ikasikika!....
Bado Maisha Ya Kijana Isack yapo hatarin!,akitoka shulen akiwa ndani ya gari la madam Jane wanashambuliwa na risasi na kijana wa kazi Zidu Katili Je Isack Hatapona?! Twende Pamoja
*NA HII NI SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE*
Ni Kama Vile Mungu Alikuwa Upande Wake Kwani kabla risasi azijarushwa kuna kitu kikamsukuma ainame kidogo chini ile anataka kuinuka milio ile ikasikika,akajikuta amelala vilevile!
hata kwa upande wa madam Jane Alijikuta Akiinama Huku Mwili Ukimtetemeka!
Zidu Baada Ya Kupiga Risasi Za Kutosha kwa kuwa ilikuwa ni barabara kubwa akutaka kupoteza muda hapo akakanyaga mafuta na kuliondoa gari kwa kasi akijua Kwa Risasi Zile Alizopiga Azitamuacha Mtu Salama!
Watu Walilizingira Gari La Madam Jane ila walishangaa kukuta wote waliyoko ndani ni wazima ila ni kioo tu cha upande wa kushoto kiliharibika!
Watu Hawakuacha Kumpa Pole Madam Jane Kwa Kuwa Mpaka Muda Huo Trafk awakuja,ilamlazimu Jane aelekee Kituoni alipotoa Maelezo!
Akumtilia Shaka Mtu Yuyote!
Askar Wakamtoa Hofu Kwamba Wangefatilia Na Kumbaini Huyo Muhalifu
Madam Jane Na Isack Wakatoka Kituoni Pale Kila Mmoja Akiwaza Yake Kichwan
"madam Nahis Muuaji Alikuwa Na Malengo Ya Kuniua Mimi! Sijui Nimemkosea Nini Mimi Target Yake Yote Ni Kunimaliza Mimi"
Isack Aliongea Kwa Uchungu, machozi Yakimtiririka!,madam Jane Akapata Kazi Ya Kuanza Kumbembeleza Japo Moyon Mwake Akupingana Na Maneno Ya Kijana Yule Ila Alijaribu Kumtia Moyo Akimtengeneza Kisaikolojia!
"usiwaze Hivyo Mdogo Wangu Kama Mungu Ajapenda Ufe Utokufa Utaishi Milele Hii Ni Mitihan Tu Hakuna Marefu Yasiyo Na Ncha!"
Kila Mda Madam Alijitahidi Kumpa Moyo Mtoto Yule!,mwisho Isack akawa Sawa!
***
Kijana Wa Kazi Zidu Alipaki Gari Lake Eneo La Siri Alolijua Yeye,muda Huo Huo Akapanda Bodaboda Akihitaji Kurudi Eneo La Tukio Akajue Matokeo Juu Ya Kazi Ile Aloifanya!
Alipofika eneo La tukio alishtuka
Baada Ya Kutoikuta Ile Gari Aloishambulia Kwa Risasi Dakika Kadhaa Nyuma,
"nishushe Hapa"
Dereva Bodaboda pasina kusema kitu akamshusha Zidu Akamlipa Bodaboda Akaondoka Zake.
Zidu Akasogea Kwenye lile eneo kulpokuwa na mkusanyiko wa watu kusudi adake mawili matatu!
"duh kwel wale wanamuu..wanamungu bwana zile risasi zote azikuwapata yesu na maria washukuru thana bwashee"
kijana mmoja aliongea kwa lafudhi ya kichaga maneno yake yakaenda moja kwa moja mpaka katika masikio ya zidu k,kwa mara nyingine tena akang'amua kuwa kamkosa mtoto yule!
kapoteza risasi zake bure!,
Moyo wake ukapandwa na ghadhabu....
Akajikuta Akizidi Kumchukia Mtoto Yule Ambaye Kwa Kiasi Flan Toka Aanze Kazi Ile Ya Uhalifu Kazi Ile Alokuwa Akiidharau Hapo Mwanzo Alijikuta Ikianza Kumsumbua!
"mburanata Washee Usinambie! Niliskia Paaa Nikajua Bom Kumbe Nirisasi Kwa Hiyo Ijadhuru Kabisa?"
"alaaa,si Ndo Nakwambia Sasa! Kunawatu Wameaga Kwao Hati! Hasara Walopata Wale Ni Kuvunjika Kwa Kioo Tu! Bas! Ila Kwa Nin Washambuliwe Bwasheee?!"
"nahis Yule Dada Alikuwa Na Hela Ivyo Yule Jambazi Lengo Ni Kumuibia Zile Hee,zile Ela Bwana!"
"hapana Washee Nakataa Kabisa,ingekuwa Ndo Ivyo Lazima Yule Jambazi Angeshuka Baada Ya Kupiga Zile Risasi Ila akushuka! baada ya kupiga risas kadhaa akachomoka kwa kasi tarimo kuna watu wana roho mbaya ati!"
"alafu naskia ni yule madam mgeni wa shule ya msingi gulion"
"ndo yeye bwashee!..."
Zidu Alishavutiwa Na Maongezi Ya Vijana Wale Wawili Wakichaga Akawa Makini Kuendelea Kuwasikiliza Akijua Lazima Pale Angeng'amua Kitu Na Pakupata Pa Kuanzia Na Kwel Punde Si Punde Alipata Pa Kuanzia!...
"kwa Hiyo Sasa Baada Ya Tukio Lile Bwashee Walielekea Wapi..."
"tulimshauri Aelekee Polisi Kwanza Ndo Kaelekea Kituo Cha Kati!...
Zidu Akutaka Kuendelea Kupoteza Muda Pale,pale Na Kituo hiko Cha Polisi hapakuwa Mbali Akaruka upande wa pili na kudandia bodaboda!
"Elekea kituo cha kati"
Dereva bodaboda yule akatii sheria akawasha pikipiki yake na kuihingiza barabarani!.
Dakika tatu walikuwa nje ya kituo kile!,mwanaume Wa Kazi alifrahi baada Ya Kuiona gari Ile alioishambulia Masaa Kadhaa hapo Nyuma Alijua Bado Amsakae Yumo Humo Ndani
Wala Akuangaika kushuka,alikaa Kama Dakika Kumi Tu Macho Yake Yakiwa Langoni Mwa Kituo Kile Na Ghafla Alimshughudia Madam Jane Na Mtoto Isack Wakitoka Ndani Ya Kituo Kile,wakaingia Ndani Ya Gari Yao Ile Na Kuondoka!.
Zidu Akiwa Pembeni Kabisa Ya Kituo Kile akamwamrisha dereva aifate Ile Gari.
Dereva boda boda alishtuka ila Zidu Akamtoa Wasiwasi Akimwambia Yule Ni Ndugu Yake Na Hapo Anamlinda Kisiri Baada Ya Kumjulisha Kuwa Kapigwa Risasi Na Watu Wasojulikana!, dereva Yule akaamin Na Kuondoa Wasiwas Akaanza Kufatilia Kama Alivyoambiwa,pasina Kujua Kabeba Bonge La Jambazi!
Baada Ya Mwendo Kidogo hatimaye Walifika Katika Nyumba Ile Ya Madam,baada Ya Madam Kuingiza Gari Yake Ndani Ya Geti Pasina Kujua Anafatiliwa,zidu Akashuka Akamlipa Dereva Boda Boda Yule Ela Yake Boda Boda Akaondoka Zake Baada Ya Kupotea Machoni Mwake Mwanaume Akapiga Hatua Kulifata Geti Bastola Yake Ikiwa Kibindoni!
'Safari hii utopona isack'
Akajiwazia akizidi kulisogelea geti lile kichwani mwake akiwa ana nia moja tu!
Kumuua isack,au wote wawili yeye na mwalimu wake!.
Alipofika akagonga kengele ilokuwa pale getini ilopeleka taharifa mpaka ndani!.
Kwa wakati huo isack alikuwa chumban kwake akibadilisha nguo na madam Jane alikuwa ndo anajiandaa kuingia bafuni kuoga.
"isack..."
akaita kwa saut isack akatoka
"kamfungulie mgen getin nasikia mlio wa kengele mi naenda kuoga mara moja"
"sawa madam"
Isack Akaitikia Akaufungua Mlango Ule Wa Sebulen Akatokea Uwani,akapiga Hatua Zake Ndefu Kulifata Geti Kubwa,pasina Kujua anaenda kumfungulia adui yake,aisakaye roho yake,na mwenye hasira,chuki na yeye mwanaume wa kazi zidu kite!
kosa!!!...
Je huu ndo mwisho wa Isack sijui na jamaa alivyo na hasira nae ha ha ha
Mwanaume Wa Kazi Zidu Kayanza Kite almaharufu Kama Zidu K Au Zidu Katili,anang'amua Bado ana Kazi nzito Ya Kumwangamiza Mtoto alomdharau Na leo yupo nje Ya Geti Baada Ya Kugonga Kengele Madam Anamwambia Isack Akafungua Mlango Pasina Kujua Ni Hatar Inayo Mnyemelea Mtoto Yule Naye Anachepuka Kuelekea Getini! Je Atanusurika Kwa Izrael Wa Kibinadamu Huyo Aliyeyapania Maisha Yake? Twende Pamoja
*NA HII NI SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO*
TUSONGE WAUNGWANA.......
*SURA YA NANE*
Madamu Jane mapema tu toka Mtoto Yule Aje Pale Nyumbani Na Kumwelezea Jinsi Alivyotekwa Na Mtu Alojifanya Baba Mdogo Wake Na Hatimaye Kutaka Kumuua Tena Kwa Kumtupia porini machale yalimcheza,akajua ile vita isingeishia pale! lakini kwa nini watake kumuua mtoto yule swali lile alikupata jibu ndani ya ubongo wake!
Alijua vita ile peke yake asingeiweza! lazima apate msaada wa polisi,tena hata kukaa na mtoto asiye wake kisheria alijua ni kosa,ivyo kwa siri sana akaelekea kituoni,ambapo kwa bahati nzur kituo alimkuta inspekta Nurdin Wengi Wa Wapenz Wa Riwaya Zangu Si Wageni Wa Inspekta Huyu,ni Inspekta Aijuaye Kazi Yake Vizuri,madam Jane Akamsimulia Kila Kitu Hata Insp Nurdin Aling'amua Muhusika Mkuu Atakuwa Ni Huyo Mzee Alex Ivyo Lazima Wamtafutie Ushahidi!...
Madam jane akaaga kuelekea nyumban pasina kujua zidu anamfatilia kwa nyuma,
konstebo kisogo alishaona dalili za dili pale na akutaka impite,japo alikuwa ni askar alofanya kazi muda mrefu pasina kupandishwa cheo chuki na serikali ikamvaa akawa msaliti ndani ya jeshi akifichua siri za jeshi nje!.
Hili Nako Akutaka Impite Kwa Muda Ule Ambapo Mzee Alex Alikuwa Mgombea Wa Ubunge Alokubalika Katika Jimbo Lile Na Namba Zake Zilizagaa Mtahan Konstebo Kisogo Akampandia Hewani Mheshimiwa Yule Akiwa Eneo La Kujificha Mzee Alex Akapokea!
"mi ni Askar Wa Jeshi La Polis Nina Habari Nyeti Mkonon Mwangu Twawez Onana!"
Mzee Alex Akashtuka,macho Akayatoa Pima Kwa Muda Ule Alikuwa Katika Kikao Cha Chama Ivyo Baada Ya Simu Kuita Alisogea Tu Pembeni Kuipokea
"hapana Aisee nipo Katika Kikao Muhimu Cha Chama Sitoweza Kutoka Hapa Nidokezee Tu Kak Kama Inawezekana"
ITAENDELEA
Simulizi : Kiapo (Agano La Damu)
Sehemu Ya Tano (5)
"Ok Muheshmiwa Kuna Ela Ya Chai?!"
"yah Ofcorze"
konstebo kiso akatabasamu kidogo na kuanza kumwaga siri zote!
"juzi juma mosi kuna dada alikuja na mtoto mmoja mdogo hapa ambapo yule mtoto alikuwa ametekwa na kwa maelezo yak kuna kila dalili kwamba unahusika mzee..."
"kivipi tena mi niwe na husika afande!?"
"hatuna ushahidi wa kukukamata ndo unaotafutwa na
mbaya zaid leo dada yule kashambuliwa na risas na mtu asiyefahamika naomba kama unahusika kuwa makini kila hatua upigayo nyongeza mzee wangu nyumbani kwa yule bint kumetegeshwa kamera kila kona kuwa makin na vijana wako kwaher mzee wang kwa habari hii sijui utantoa sh ngapi"
muda wote mzee alex alikuwa kimya kila alichoambiwa kilikuwa kwel na kwa muda ule akutakiwa kubisha alipaswa amtumie afande yule kujua kila kitakachokuwa kikiendelea kituoni
"nashkur kijana angu ntumie no yakuingiziwa pesa benk nikufanyie mchakato kila litakaloendelea usiache kunjulisha kijana angu"
konstebo yule mnoko aka achia tabasamu akamtumia namba za akaunti yake ,kichwa cha mzee yule kilizidi changanyikiwa!
habari ile imefka kituon na inafatiliwa na inspekta,alimjua vizur inspekta yule kazi zake na ufanyaji kaz wake aliutambua vizur toka katika riwaya ya mzimu ulorejea alipokuwa na mzimu jb wakifanya kazi pamoja,katika riwaya ya upendo pia alionesha makucha yake kivipi asimtambue sasa?!
kivipi asiwe na mawazo?!
muda ule ule akamkumbuka kijana ake zidu k,alijua kwa vyovyote yeye ndiye aliyeshambulia gari lile na kwa vyovyote kwa muda ule lazima atakuwa anawafatilia,kwa haraka akaishika simu yake na kumpandia hewani zidu k.
*****
Zidu k' akiwa pale getini ghafla simu yake ikaita,alipoangalia alikuwa ni bosi wake,akasita kuipokea alitaka kuongea na mzee baada ya kukamilisha kazi,
akairudisha mfukoni,ila muda ule ule ikaita tena,akaipokea kwa ghadhabu na hasira tele!
"mzee ndo npo hapa getini kwao nilikuwa nawafatilia bado nawawinda ndani ya dakika tano kazi itakuwa imeisha!...
"unasema? huko hapo nyumbani kwa madamu toka haraka hapo wala usifanye tukio lolote!...
ikawa zamu ya zidu kushtuka!,kivipi astopishwe tena!
"haaa! kwa nin tena bosi?!"
"nimesema toka hapo si sehemu salama kuna ulinz madhubut"
'ulinzi?!!'..
akageuza shingo yake kuangalia kila upande,akuona chochote cha kumwogopesha au ulinzi wowote
kivipi sasa bosi wake amtishe
"ulinz upi mzee?!"
"nimesema toka hapo usifanye tukio lolote hapo utaamishia jeshi zima hapo we potea hapo haraka!"
duh zidu akatingisha kichwa kwa masikitiko,taratibu akageuka kuondoka eneo lile,pasina kujua isack ndo alikuwa akifungua sasa mlango,akashangaa kutokuta mtu,akafunga geti na kurudi zake ndani
"madam hata amna mtu!"
"amna mtu!? embu subiri"
madam jane akiwa na uso ulojaa tabasamu akaelekea katika laptop yake ilounganishwa na camera za nje na kuonesha mandhar ya nje
akaanza kurudisha nyuma matukio yalotokea nje ya nyumba yake dakika chache nyuma akasimamisha alipomuona mtu kasimama nje ya geti lile akaanza kufatilia kile kilichotokea!
alishughudia zidu akipokea simu na kuongea kwa ghadhabu
"mzee ndo nipo hapa getini kwao nilikuwa nawafatilia bado nawawinda ndani ya dakika tano kazi itakuwa imeisha!"
madam jane akashtuka!,kusikia maneno yale,akaendelea kufatilia kilichoendelea akishangazwa na jins mtu yule alivyoshtuka,akujua ameambiwa nini na yule alompigia simu ila alisikia akitaja jina ulinzi na kutoka taratibu bila shaka aligundua pale kuna ulinz wa kamera ila je kagunduaje? na ni nan huyo bos wake aliyekuwa akiongea naye?! ila pale palikuwa ni pazur kwa kuanzia!
"Isack embu njoo"
akapaza sauti kumwita mtoto yule isack akatii!
"embu nambie huyu mtu unamjua?!"
akamuuliza akiikuza ile picha ya zidu akiwa kasimama pale getini isack alishtuka kuiona
"ndo huyu, huyu huyu alojifanya ba mdogo akaja kunichukua akanitesa na kutaka kuniua umemjuaje madam"
madam akujib kitu aliishia tu kucheka,
"kazi imeisha sasa utaish kwa amani wacha nikaonane na insp nurdin nimjulishe juu ya hili aanze kusakwa huyu mtu ili mradi imepatikana picha yake huu ni ushahidi tosha!...
No 26
Madam Jane ana amua kumsaidia Isack Kwa Kuishi Naye Baada ya kugundua maisha ya mtoto yule yapo hatarini!
anaenda kuchukua kibali cha kuishi na mtoto yule polis ambapo inampasa asimulie maisha ya mtoto yule kwa insp wa jeshi la polis nurdin wanapanga mtego wa kumnasa yule atakaye kumuua yule mtoto na mtego unamnasa mwanaume wa kazi zidu k! je nin kitaendelea?! twende pamoja
*NA HII NI SEHEMU YA 26*
Pasina Kupoteza Muda Madam Jane Akashika Simu Yake Na Kumpigia Insp Nurdin Ambaye Kwa Muda Huo Alikuwa Ofisin,simu Ikaita Ikapokelewa...
"insp Na taharifa nzur yule alojifanya ba mdogo wake isack kamera zime mnasa kumbe alikuwa akitufatilia tulipoingia ndan naye ndo akagonga ila kuna mtu bosi wake alimpigia simu akamwambia hapa pana ulinz ivyo aondoke..."
insp Nurdin Akashtuka!,bosi Wake Ndo Nani Au Ndo Mheshimiwa Na Kama Ndo Yeye Kajuaje Pale Pana Ulinzi!
"save Hayo Matukio Katika Flash Njoo Nayo Hapa Kituon Sura Yake Si Inaonekana Vizuri?!"
"kabisa"
"huyo Atakamatwa Atateswa Lazima Ataeleza Tu Ni Nani Kamtuma Awe Ni Alex Au Nan Ataeleza Tu"
Insp Nurdin Akaongea Kwa Hasira Kitendo Cha Kulitaja Jina Alex Likamzindua Afande Kiso,akaongeza Umakini Kufatilia Kila Kitakachoendelea
Baada Ya Dakika Chache madam jane akawasili kituoni pale na flash yake,wakaipachika katika laptop ilokwepo katika ofisi ile ndogo!
"huu ni ushahidi tosha na kwa sasa mimi na kiso twaingia kazini kumsaka huyu mtu"
Baada Ya Kuitazama Ile Flash Nurdin Aliongea Kwa Furaha Akihisi Moyon Mwake Mambo Yanaenda Kuisha!,insp Nurdin Alikosea Sana Kuwaza Ivyo...
Madam Jane Baada Ya Maongez Akaaga Akimuachia Insp Nurdin Flash Ile Kama Ushahidi,insp Nurdin Akaifungia Ndani Ya Droo Lake!
Kwa Upande Wa Konstebo Kisogo Alienda Eneo Lake La Siri Akampigia Simu Mzee Alex,simu Ikaita Baada Ya Sekunde Chache Ikapokelewa...
*******
Zidu Katili Kichwa Chake Kilijaa Mtiririko Wa Maswali Asiyoyapatia Majibu!
Ila Aliamin Baada Ya Dakika Chache Angepata Majibu Ya Maswal Yale,kwa Muda Ule Moyo Wake Ulitaman Tu Kuua!
Zidu Hakuwa Mtu Wa Kushindwa!,aliendelea Kukanyaga Mafuta Kuwah Ofisini Kwa Bosi Wake Ajue Kwa Nin Alimzuhia Kukaua Kale Katoto Na Kudai Pale Pana Ulinzi Mbona Sasa Yeye Binafsi Aku Uona Huo Ulinzi Hata Dalili Zake?!
Akajikuta Akiachia Tabasamu!,
Dakika Tano Mbele Alifika Ofisini Kwa Bosi Wake Yule Akapak Gari Lake Na Kushuka,akapiga Hatua Kuelekea Ilipo Ofis ya bosi wake yule ambapo ilikuwa ni lazima apitie kwanza mapokezi
alimkumbuka msichana wa pale mapokezi mara ya mwisho alipotaka kumpiga risas kwa kumpotezea muda wake!,
"leo akinizingua tu sitomwacha sipendag dharau mimi'
mwanaume yule alofanya vizuri katika riwaya ya morose chuki akawaza akipanda ngazi kuelekea juu ilipo ofisi ya mr alex
aligonga mara moja mlango akusubiri kuitikiwa mwanaume akazama ndani,macho yake yakatua kwa binti yule yule!
macho yao yakagongana,macho ya zidu yakiwa makali huku ya yule binti yakiwa yamejaa khof,wasiwasi na woga tele!
"naitaji kuonana na mr alex"
zidu aliongea kibabe na wala akusubiri aruhusiwe akaufata mlango na kuufungua!..
mwanaume akazama ndani!...
"bos kwa nini umeniambia nisitishe kumuua yule mtoto na hali yakuwa unajua ela yake nshakula?!"
"najua ilo kijana ila kwa sasa inabidi tupotezee kwanza swala hili mpaka uchaguzi upite"
Zidu K Akashtuka!
Uchaguz Upite?!,uchaguz Na Kazi Yake Wapi Na Wapi?!,ni Kama Wazo Lile Mzee Alex Alilisoma Kwenye Mawazo Yake Akalijibu!
"najua Unashangaa Wai Nakwambia Kwa Sasa Tuachane Na Jambo Hilo Taharifa Kwamba Mtoto Yule Anasakwa Auwawe Zishafika Makao Makuu Ya Jeshi La Polis Na Anayehisiwa Ni Mimi Na Faili La Kesi Hii Kapewa Insp Nurdin Alifatilie!"
"eti Nini?!"
Zidu Alishtuka Kwa habari ile,insp nurdin hata yeye pia alimjua na mara kibao tu walishaparangana kwenye matukio mbalimbali huko uraian alijua ufanyaji kazi wake,ila je aliyezifikisha habari hizi polis ni nani uyo?!...
"ni yule madam,sikia ulipo mtupa porin yule mtoto alipopona alimsimulia kila kitu madam ,ikabidi madam akatoe ripot polis ambapo yule polis alijua lazima tutamfatilia akampa madam yule kamera akategeshe nyumb yake ivyo si ajabu sura yako...
kabla ajamalizia ghafla simu yake ikaita alipoangalia mpigaji alikuwa ni 'afande riporter' ndivyo alivyo msevu afande kisogo katika simu yak alijua kupigiwa kwake simu ni
habari ile ile akajikuta ameweka loud speaker
"mheshimiwa nadhan unakumbuk nlikwambia uwe makini wewe na watu wako!,nadhan pia unakumbuka pia nilikwambia kila pembe ya nyumba ya yule madam kuna camera za dstv na tayar zishanasa sura ya kijana ako mmoja akiwa nje ya geti ghafla akapokea simu na kusema ndo ameenda kukamilisha kazi umpe dk 5 na ghafla kama ulimkanya akaondoka,kwa sasa mtu huyo anasakwa kuwa makin mheshimiwa"
"nashkur kwa taharifa yako ntaiwezesha akaunti yako ya benki"
"ntashkur mzee"
kiso akaitikia na kukata simu!, mzee Alex Akamgeukia Zidu
"nadhan Umesikia Kwa Masikio Yako!,hatari Iliyopo mbele yetu,kwa sasa ingia mafichon mpaka kipindi hiki kipite nikiwa mbunge ntakuwa na nguvu zaidi
pili kwa sasa chama cha upinzani kikipata fununu ya haya nimekosa kura ivyo kwa sasa miezi hii mitatu tumuache mtoto huyo adunde"
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment