Search This Blog

Thursday, 29 December 2022

KUFA TU HAKUNA NAMNA (2) - 5

  

 Simulizi : Kufa Tu Hakuna Namna (2)

Sehemu Ya Tano (5)




Alitinga Jinsi lake moja la kiume tisheti nzur nyekundu koti zito lenye kofia chini akatupia raba,




Muda ule ulikuwa ni saa sita usiku akuangaika kupitia getini akihofu akitoka ingempasa aache geti wazi,akauparamia ukuta na kushukia nje...




Akaanza kutembea kwa haraka kuelekea alipokuwa amepanga Sara akiishi na mpz wake Sudi,




Kwa kupitia shotcut mida mingine akikimbia saa kumi kasoro alikuwa nje ya mlango wa chumba kile,alikuwa na khofu je angekuta kitu ndani?,kwani masiku mengi yalikuwa yamepita toka Sara auwawe,




Akaingiza ufunguo wake bandia na kufungua akazama ndani,akamulika mulika na simu yake akaipata swichi akaiwasha taa




Alishangaa Kukuta Chumba Kimetandikwa Vizuri tu!




'ina maana ndugu wa marehemu mpaka sasa wanajipa moyo ndugu yao yupo hai au!'




Zena aliwaza moyo ukimchoma kwa maumivu makali,ila hakuwa na jinsh kwa upande mwingine alishkuru kwani angekuta chumba cheupe asinge fanikiwa lililo mleta!




akaingiza mkono chini ya kitanda akatoa viatu akatazama viatu vya kike vivaavyo na sox akavipata




Ndani ya sox kweli si akaikuta kiifadhi kumbukumbu (memory card) haraka akakichukua na kukiingiza ndani ya simu yake,




Kuingiza kwenye simu yake alimshughudia mh waziri akiwa anafanya uchafu pamoja na msanii maharufu wa bongo movie miss g au Magreth




'mh! siri yenyewe ndo hii kesho mchana lazima niipost'




Aliwaza akiufunga mlango wa watu,kama alivyoukuta!




Na Kesho yake kama alivyosema akaipost katika akaunti yake ya utube! akiandika kichwa cha habari!




HUYU NDO RAIS WETU AJAYE!,




Video hii ndiyo iliyo onwa na


madam 's' na kummaliza nguvu hata za kuendesha gari!...




Habari hii ikashika 'head line' katika vichwa vya habari,ikawa sogo midomoni mwa watu "ZK" akarudiwa kutajwa na kuwa maharufu,video ile ikatazamwa na mabilioni ya watu!




IKAWA BONGE LA SKENDO KWA WAZIRI MKUU PAMOJA NA MSANII MAGRETH WA BONGO MOVIE...




Skendo ile ikasindikizwa na skendo nyingine iloibuliwa na mbunge wa jimbo la dodoma mjini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi mh bi Rukia Saidi Juu ya mkataba feki ulosainiwa na waziri mkuu huku akijua ni feki na kwendea kupoteza mabilioni ya fedha kupitia wizara ya fedha




Chokochoko za chini kwa chini uraiani zikaanza,waziri mkuu ajiuzulu,hatumtaki tuirudishe ccm yetu hawa atuwataki waziri mkuu fisadi atuwataki,uchaguzi urudiwe kirudishwe chama chetu!,tulikipenda hivyo hivyo hata kwa tabu zao tuliwapenda hivyo hivyo hawa tumewapa nafasi wameshindwa hatuwataki!'




Hali ilikuwa mbaya ilikuwa inaelekea anguko la kisiasa kwa chama tawala cha uwavyauta,mpaka sasa hata Rais Asamoye Mwenyewe akawa sasa akiogopa kwamba hata yeye anaweza akakosa kwa njia aitumiayo kumchafua mwenzie...




WAZIRI MKUU KIKANGONI KWA MARA NYINGINE AWAMU HII BADO ATAGOMA KUJIUZULU?! SKENDO MBILI KWA MPIGO CHANZO KIKIWA RAIS ASAMOYE!




MBONA PATAMU HAPO,




ZIDU ATUJAJUA ALIFIKIA WAPI KATIKA KUMUOKOA MPZ WAKE KATIKA OPERESHEN YAKE








Hali ya hewa inabadilika dalili za mvunjiko wa amani zinaonekana ni baada ya kuvuja kwa mikataba feki na kuliingizia taifa katika hasara ya mabilioni ya fedha wananchi wanaanza kupaza kelele wakilazimisha waziri ajihuzulu,




Je wazir Jj atakubali kujihuzulu?!




TUSONGE KUPATA MWENDELEZO!...




UWANJA WA NDEGE WA DIA




Ndege kubwa kutoka shirika la ndege la British Air way,baada ya kutua ardhini na kutembea ikaenda kusimama mahali pake,mlango ukafunguliwa na abiria mbalimbali wakaanza kushuka,




Walishuka abiria mchanganyiko wenye asili ya kizungu na pia wachache wao wakiwa wa africa




Katika Wachache wale wenye asili ya kiafrica,alishuka mzee mmoja aliye onekana yupo vizuri kiuchumi alikuwa na nywele chache kichwani kipara kikiwa kimetawala




"pole mr Leonard!"




Alipewa pole na kijana aliye onekana kama ndo alokuja kumpokea,mzee yule aliachia tabasamu na kuongeza hatua kumfata mtu yule,




Wakaongozana mpaka kwenye gari, yule jamaa akafungua mlango yule mzee akaingia




"nambie mr Roga Vipi familia yangu inaendeleaje?"




Mzee yule aliyetambulika kwa jina la Leonard akauliza huku akipiga mwayo, mwayo ulotokana na uchovu wa safari




"mzee familia ipo salama sijui wewe huko ulikotoka"




"namshukuru Mungu kama unavyo niona hatimaye nimestahafu sasa na nimerejea nyumbani miaka 54 siyo mchezo"




Mzee yule aliongea wote wakaishia kucheka




"Vipi wakati unakuja kunichukua mama alikuwa nyumbani?!"




"hapana hakuwa nyumbani ni kama nilivyokueleza mkuu siku ya tatu hii mama hayupo"




"na watoto wote umesema wapo bording?"




"ndiyo mzee wakifunga shule ndo huwa naenda kuwachukua!"




"ok,kama tulivyo ongea sihitaji ajue kama nimerudi ilo swala lake niachie nitadili nalo"




Mzee yule aliongea, akionekana wazi kuwa na chuki kali moyoni mwake...




Safari yao iliishia katika moja ya jumba la kifahari lenye ghorofa tatu ndilo alilokuwa akiishi mzee yule.




Baada ya kupumzika kidogo Mzee Leonard alitoka tena na dereva wake wakaenda mpaka supermaket aliponunua vitu vidogo vidogo vya kupika,




Mzee akujali pesa wala utajir alokuwa nao,mzee Leonard aliingia jikoni wakisaidiana na Loga kupika wakala pamoja,akaingia ndani kupumzika...




Mzee Leo alijaribu kuvuta usingizi ukagoma,mabadiliko ya mke wake bi Salma walofunga ndoa miaka kumi na tano nyuma yalimuumiza sana,yeye alikuwa kikazi nchini Marekani,ila kila baada ya wiki moja mkewe alikuwa akimtembelea na kukaa naye siku mbili,kwa kipindi chote alichoishi huko,Leo alikuwa akipata likizo alikuwa akirejea Tanzania Kuungana na familia mambo hayo yote yalikatika ghafla mwanzon tu mwa mwaka ulopita!




"mume wangu muunganiko wa vyama vya upinzani umeshinda kwa kishindo hivyo taifa linaingia katika utawala wa chama kingine,ivyo nitakuwa bize mume wangu sitaweza kuja huko tena kila baada ya wiki moja hali katika usalama wa taifa si nzuri nitakumisi sana mume wangu itabidi tusubiri hiyo miaka saba ulobakisha iishe ustahafu ila ukipata likizo we njoo"




Mr leo anakumbuka mambo ndo yalianzia hapo,wakawa awaongei tena usiku,kila akimpigia simu aipatikani akawa akisikia mara mkewe bi Salma kaja marekani kikazi amtafuti,




Naye akumuuliza,wakawa wanaongea ile basi tu,mara moja moja sana,mwisho akaomba astahafu




"mzee mama anasiku ya pili ajarudi nyumbani na hii ni kawaida yake umaliza wiki,wiki mbili kuto onekana nyumbani!"




"dah,kesho njoo earport narudi nyumbani usimjulishe kitu nimeshastahafu ni muda wa kurudi nyumbani na kuja kula matunda yangu ya kuitumikia marekani kwa kipindi kirefu"




Leonard aliongea kiutani ila kweli siku ilofatia alirejea!,na sasa alikuwa juu ya kitanda chake,alichozoea kulala akiwa na mke wake bi Salma leo hayupo na ajuhi ni wapi alipo,




Alichelewa sana kupata usingizi usiku huo...




Badae sana ndipo alipoupata!




MASAKI




Ndani ya usiku ule katika jumba lile la kifahari la siri ndani walikuwa wapenzi walopendana madam 's' na mh waziri Jemes John 'JJ'




"siku ya tatu sasa mama kijacho unamuacha analala mbali na joto lako mwanaume una roho mbaya wewe!"




Madam 'S' aliongea kwa kudeka akiwa kakilalia kifua cha mzee yule naye mkono wake ukawa ukilipapasa tumbo la mwanamama yule na kumpa hamasa za kihisia!




"anashndwa kunipa vile unipavyo wewe unajua wewe mwanamke u mtamu sana?!,yani unajua kunitoa katika mawazo yote na kunisaulisha machungu ya vyam...




"shiiii... we mwanaume tukiwa kwa bed mambo ya siasa weka pembeni,sitaki uongelee kabisa chukua ulimi wangu mpz,napenda sana jinsi unyonyavyo unajua penzi lako limenichanganya sana limenifanya mpaka nimemsahau hata mume wangu huko marekani..."




"basi mamy sipendi umwongelee huyo mtu..."




"basi kipenz..."




Madam akamkatiza, akimpa ulimi,mh Jj akaupokea ndimi zao zikawa zikinyonyana na kuwapa starehe ya ajabu"




Kilichoendelea kiliamisha kabisa akili zao,




Asbuh kama kawaida walitoka pamoja na kuelekea ofisini,asbuh ile palikuwa na kikao ofisini kwa waziri mkuu wakijadili ni jinsi gani wanaweza kuizima ile skendo ilokuwa ikiendelea mtahani!...




Kiukweli Waziri hakuwa tayari kujiuzulu,kipi sasa kifanyike?!


Swali hili ndilo ilipaswa walijadili watatu wale Madam S,don G,na waziri mkuu!




"mi nina wazo,hivi kwa nini tusiunge genge la kiuhalifu livamie maduka ya watu waibe..."




Don aliongea, wote wakamtumbulia macho dizaini kwamba hawakumuelewa!




"tuunge magenge ya kiuhalifu?!,kivipi sasa?!"




"hili kuua hii kashfa isisemwe semwe midomoni mwa watu yapaswa tuanzishe kitu kitakacho head line midomon mwa watu wawe wanakizungumzia hicho hili la kwako litasahulika!"




"ahaaa,hapo nimekupata sasa hii kashfa imeniharibia kwa kwel jana nimesoma gazeti moja limechambua fedha zilizopotea ha ha ha mchambuzi anasema hizo bilioni kadhaa za madafu eti unaweza kuzipanga elfu kumikumi toka morogoro mpaka dar na zikabaki.."




"achana na hiyo... madam akamkatisha kisha yeye akaendelea




"yule mtangazaji mpumbavu 'ZK' limerusha kwenye akaunti yake kwamba hizo bilion kadhaa unazo ziita za madafu unaweza kumpa kila mtanzani laki tatu mpaka wale walioko kwenye matumbo ya wazaz wao"




"teh teh teh..."




Wote wakaangua kicheko,




"mpz,lakin mapesa yote hayo wee unayapeleka wapi? waliingizia taifa hasara kubwa ivyo"




"hapana hiyo ela sijaila mwenyewe kuna watu nimegawana nao,nanyi pia mtakula kidogo hapo nyingine nakusanya kwa ajili ya kampeni mwaka kesho kutwa!




"kwa hiyo wenzako uliwagaiwaje uliwarushia kwenye akaunti zao?!"




"yah! no hapana zilikuwa nyingi mno , zilikuwa nyingi sana niliwarushia katika akaunt zao za benk za huko nje,za ndani na nyingine walizibeba kwenye magunia!"




"dah acha wee"




"tuachane na hizo habari vipi kuhusu kufunika hii skendo midomon mwa watu kila mara dili la wizara ya fedha,dili la wizara ya fedha!"




"hilo swala niachieni mimi nitalimaliza kwanzia kesho hii ishu ndogo sana,wa Tanzania waoga nitaunda kigenge cha uhalifu vitoto vidogo tu vitatumia mapanga vitaingia kariakoo vitafanya tukio baada ya tukio nyuma ndo maaskari watawasili,vitaleta jambia jambia kitaa kila mtu atazungumzia,kila mtu atazungumzia chui uraiani,chui uraiani vyombo vya habari vyote vitazungumzia,ishu hii hitadumu kwa miezi kadhaa kuifuta ishu yako kisha tutaizima kimya kimya"




"dah umenikumbusha mbali sana hii stori nilishawahi isikia kutoka kwa babu zangu kipindi cha miaka ya zamani awamu ya nne kama sikosei Ccm ikiwa madarakani wazir mkuu wao aliwah pataga skendo akasaini mkataba feki wakaitaga Richmond sijui escro kama si Epa Kukazuka vikundi kama hivi unavyosema kipindi icho vilizuka panya road,sijui mbwa mwitu Kumbe mambo haya yapo"




Waziri mkuu aliongea kwa kustahajabu!




"hakika yapo! ndo kama ivyo sasa dah awamu ya nne mbona zaman sana huyo babu yako alokusimulia bado yupo?"




"kashakufa kitambo sana,alinisimulia nikiwa mdogo naye alibahatika kuwa na miaka mia na kitu zaman sana!"




"na leo naona yanataka yajirudie kwako"




"kwa kuwa siasa ni ile ile,japo watu ubadilika na karne usogea lakin vilivyoko ndani ya siasa aviwezi badilika kwa kuwa ni asili yake,asili ya siasa ni mchezo mchafu,siasa ni uongo,siasa ni kucheza na akili za wanyonge na hii ndiyo siasa"




Waziri mkuu aliongea kwa kujiamini!...




Kikao Kiliendelea Wakipanga ili na lile,hatimaye wakafunga wakimwachia kazi ile Don G,kufuta kile kilichozagaa mtahani na midomoni mwa watu,magazetini,na hata maredioni bila kusahau katika ma televisheni...




**************




Zidu Katili alishuka kwenye gari lake haraka sana na kuelekea kwenye jumba moja bovu aliyoelekezwa,




Nyumba Ile Ilikuwa ni lipagara lililokuwa na vyumba vingi ndani ambavyo avikumaliziwa!




Akapita Chumba Kimoja Kimoja akukuta kitu akatokea kwenye mlango aloupita na kutokea kwenye ua ambao pia kulikuwa na vyumba,




Nyumba Ile ilitengenezwa kwa mfumo wa gesti ambayo kulikuwa na vyumba vya ndani na hata vya nje pia,




Kwa hiyo ule mlango alopita ulitokezea katika vyumba vya nje au vya uani,




Bastola Ilikuwa Mkononi kaielekeza kwa mbele,


akitembea kwa kunyata, wenzake Nobi,na J4 Wakimfata kwa nyuma...




Walikuwa na uhakika lazima watamkuta Katarina na mpz wake Suzan ndani,wakazidi kunyata wakipitia chumba kimoja baada ya kingine wakamaliza vya upande mmoja pasina kukuta mtu,


Waka amia vyumba vya upande wa pili navyo vilikuwa sita,




chakwanza 'emty'




cha pili 'emty'




cha tatu na cha nne pia 'emty'




Sasa vilibakia vyumba viwili cha tano na cha sita!...




ILIVYOKUWA




Baada ya Suzan Kuingia ndani ya gari Katarina akaliondoa kwa kasi moyoni mwake kulijaa hasira,chuki juu ya mwanamke yule alokaa pembeni yake,




Muda Wote Suzan alikuwa akilia kujutia kile alichokifanya,




"nakuomba usimdhuru mama yangu mimi ndo niliyekukosea na si mama yangu mimi"




"unaongea nini wewe malaya,mama yako ajakukosea alokupa kidonge na ushahuri wa kunisaliti ni nani kama si huyo mama yako,wote mnatakiwa *KUFA TU HAKUNA NAMNA*"




Katarina aliongea akizidi kukanyaga mafuta safari yake ikaishia mbele ya pagara moja akamshusha na kumwelekezea ndani chumba cha mwisho kabisa,chumba cha sita,




Alimkuta Mama yake akiwa tayari kafungwa miguu na mikono katembezewa kipigo yupo tu akigugumia hapo chini kwa maumivu makali!,




"wema wangu wote umeusahau msahada wangu wote niliowasaidia ikiwemo kuwajengea nyumba mama pia ulisahau ukamshahuri mwanao anipokonye mume ukijua mume wangu ni mdhaifu wa mtoto ukitumia udhaifu huo huo kuniacha mimi akijua ana mimba yako na kukuchukua wewe na kunichukia mimi kumbe wamuongopea na mna nia mbaya naye,nia yenu ni kumuua...




Ghafla Simu Ya Suzan Ikaita...




Katarina akaenda kumnyang'anya akaicheki 'my live' uhai wako huu




"ndiyo ni uhai wangu na atakuja kuniokoa utonifanya kitu Katarina!"




Suzan akaongea kwa ukali,na hasira,simu yake ikakata na kuita tena...




"atakuokoa subiri utaokolewa muda huu ni vyema ungesali umuombe mola wako msamaha aipokee roho yako"




"utoniua katarina na nakuapia wewe ndo utakufa,"




Kauli Ile Ikazidi Mkera na kumpandisha hasira Katarina,ile anataka amfate ghafla simu yake ikaita




Alikuwa ni Zidu akapokea,




"mh mume wangu leo umeamua kunipigia..."




"Katarina,najua umemteka mke wangu nisimkute hata na mchubuko..."




Ghafla simu ya Katarina Ikazima Chaji,akamgeukia Suzan




"kasema eti akija asikukute hata na mchubuko dah maskini ajui kama atakuta maiti tu hapa na naanza na huyu mama yako,




Akamsogelea mama Suzan aliyekuwa hoi,si ndo akaanza kumnyonga,




Mama anauma,Suzan akujua alizipata wapi nguvu alijinyanyua na kubeba bonge la tofali lililokuwa pembeni yake




kwa kuwa Katarina alikuwa bize kumnyonga mtu kuindoa roho yake,




Akuweza Kumwona Suzan alipojinyanyua ila alichokuja kushtukia ni kitu kikitua katikati ya utosi...




Katarina akaenda chini,na kupoteza fahamu, Suzan akaichukua ile simu ilozima chaji yenye ushahidi wa memory,akaokota tofali lingine akiadhimia kummaliza kabisa,




Akalishusha Kichwani, akachukua Ufunguo wa gari akambeba mama yake na kumtoa nje,akamuingiza kwenye gari la Katarina alokuja nalo,akaliondoa kwa kasi,kumuwaisha mama yake hosptalini!...






MWISHO WA SEASON 2, ENDELEA NA SEASON 3


0 comments:

Post a Comment

Blog