Search This Blog

Thursday, 29 December 2022

KUFA TU HAKUNA NAMNA (2) - 4

  

 Simulizi : Kufa Tu Hakuna Namna (2)

Sehemu Ya Nne (4)



Mama yule hakuwa amemuona akasimama na kutoa simu katika pochi yake,Nikama Mungu tu aliamua kumfunulia Katarina kujua yale asiejua...




Mama Suzan akapokea ile simu baada ya kugundua ni mwanae anampigia na kwa kuwa alikuwa na matatizo ya kusikia ni mpaka aweke kitoa sauti nje ( loud speaker) ndipo asikie alokuwa akiongea naye....




"Alooh mwanangu Suzan"




Katarina kusikia limetajwa jina la Suzan pale pale akasimama kusudi asikilize wanachoongea simu yake ikiwa mkononi




Upande wa pili wa Suzan ukajibu




"mama kale kamwanamke leo si kamekuja katika hili jumba letu jipya,akadhani ataingia kiurahisi kilichotokea akuamini,alikimbia mwenyewe kanipigia simu nimemsaga akuongea kitu,mume wake nimemuweka hapa ni muda wa kula vyao"




Katarina alishtuka kusikia maneno Yale akapata wazo amchukue video mama yule kusudi amwoneshe Zidu akaanza kumchukua video kwenye simu yake alokuwa kaishika




"tena umshike vizuri,mpe mafundo yote nilokufunda!"




Mama akaongea pasina kujua anachukuliwa video




"mama mimi si nilikuwa najua tatizo lake ni mtoto nimemwongopea na zile dawa unipazo zinazidi kufumua tumbo utasema kweli na mimba ya miezi mitatu lakin havina madhara kweli mama?!"




"Madhara yatoke wapi? Mwanangu vingekuwa na madhara ningekupa?!,we endelea kuvitumia huku ukiongeza na juhudi ya kumtafutia mimba ya kwel tukishapata tunavyohitaji ntakupa mbinu ya kumuua mali zake zote zibaki cheni yetu!"




"sawa mama"




Katarina alishtuka kumbe Suzan hakuwa na mimba na alikuwa na lengo la kumuua mume Wangu!?




Kabla ajamuua Mimi naenda kumuua mshenzi huyu wema wote niliyemtendea leo anataka kuniulia mume itakupasa *KUFA TU HAKUNA NAMNA*




Katarina akawaza huku akimsogelea mama Suzan




Mama Suzy akakata simu kugeuka nyuma si ndo aonane macho kwa macho na Katarina,kabla ajaongea kitu Katarina akamkamata na kumgusa shingoni,akamkata fahamu,hakuwa na muda wa kupoteza akambeba mpaka katika gari yake akamwingiza nyuma ya boneti akalifunga akaingia ndani ya gari na kuliondoa kwa mwendo wa kasi tayari alishapata pa kuanzia...




*JE NINI KITAENDELEA KATARINA KAMTEKA MAMA YAKE SUZAN NA KAGUNDUA NA KUREKODI SIRI KUBWA MAMA SUZAN ALOKUWA AKIONGEA NA MWANAYE KIPI KITAENDELEA?*










Madam 'S' anamchoma sindano ya kuongea ukweli Jane kwa mawazo kwamba binti huyo pengine anatumika na watu wasiyo na malengo mazuri na muheshimiwa waziri ambaye ameapa kumlinda kwa hali yeyote ile na skendo zote je nini kitaendelea?,




twende pamoja twendelee kuburudika...




Baada ya dakika takribani tano kukata hatimaye madam 'S' akamfunga tena yule binti mkononi na kuutafuta mshipa akavuta kiasi cha dawa na kumchoma Janath,




Baada ya kumchoma sasa alikaa pembeni yake akijua muda wowote binti atazinduka apate kumjibu maswali yake,




Punde Kweli Jane akafumbua macho yake,madam akatabasamu,akamwinamia na kuanza kumuuliza




'Unaitwa nani?!"




"naitwa Janeth"




Dada aliyelala kwenye kitanda akajibu kiuchovu,madam S akatabasamu!




"unafanya kazi wapi?!"




Madam akamuuliza swali lingine akiwa ndiyo anaelea kwenye 'point'




"ofisi Ya Kamishna mkuu makao makuu ya jeshi la polisi"




Madam 'S' akazidi kutabasamu palepale akampachika swali jingine




"makao makuu pale unafanya kazi gani?!"




"ni katibu muhtasi wa kamishna"




"kwa saivi kamishna yupo wapi?!"




"ameuwawa?!"




"ni nani aliyemuua na kwa sababu gani?"




"madam 's' ndiye aliyemuua sababu mi siijui"




Janeth aliongea kile alichokijua bila kujielewa anaongea nini,na anaongea na nani madam akakunja mdomo,hasira zikaanza tena kumpanda!




"una uhakika madam ndiyo anayehusika?!"




Janeth akatingisha kichwa kuhafiki,




"nipe ushahidi wa kuweza kuamini maneno yako niamini kwamba madam 'S' anahusika"




"mtu wa kwanza kuingia ofisini siku hiyo kuonana na kamishna ni madam...




Madam akashtuka kwa kauli ile,ukumbuke kwa muda huu madam aliya amini maneno ya Jane kwa kuwa alikuwa ndani ya hali nyingine,hali ya kujieleza ukweli bila mwenyewe kujielewa baada ya kudungwa ile sindano ambayo madam aliichukua kwa lengo la kumdunga nayo kamishna lakini kwa bahati mbaya akamkuta tayari ni maiti,akaendelea kumsikiliza Jane




...na kabla ajaingia mi niliongea na kamishna kwa simu nikamuuliza madam anataka kuongea na wewe akaniruhusu nikamruhusu madam kuingia kabla ajatoka na kuniambia nani kamuua kamishna!"




Madam 'S' akakuna kichwa, akamgeukia Don G ambaye muda wote alikuwa kimya akifatilia yale maongezi,




Akarudisha shingo yake kwa Jane na kumuuliza tena akionekana kuanza kuitilia shaka ile dawa!




"una uhakika uliongea na kamishna mwenyewe kabla ujamruhusu madam Kuingia akakuruhusu madam aingie?"




"ndiyo niliongea naye"




Jane hakakubali huku akitingisha kichwa,




Madam akasogelea kile kichupa akakisoma




"daktari alinambia nguvu ya dawa ndani ya mwili wa mwanadamu inakaa ndani ya dakika arobaini na tano ndipo inaisha,ila mbona hii dakika tano tu nahis huyu binti anazidi kuniongopea"




"lazima tuchunguze kupata uhakika lazima tupate rekodi ya mwisho kutoka kwenye simu ya kamishna kuhakiki je ni kweli kamishna aliongea na huyu binti kweli au huyu binti alikuongopea na kuongea na simu hewa pale ulipokuwa umesimama mbele yake yote yapaswa tujue!...




Kingine mkuu usikute ni kweli huyu binti aliongea na kamishna na kumruhusu uingie kamishna baada ya kugundua unakuja akajitwanga risasi,kujiua..."




"Hapana nakataa kwa hilo yapaswa ujue baada ya kugundua kamishna kauwawa nilichunguza eneo lile lote sikukuta bastola wala bunduki,huyu kauwawa"




Wote walijikuta wakichoka vichwa vyao,




"ngoja niende makao makuu ya simu ttcl nikachunguze kuhusu simu na sauti hapa ndo tutajua pa kuanzia we kaa na huyu malaya hapa punde tu narudi"




Madam 'S' akamwambia Don G aliyeishia kutabasamu, alijijua yeye ni mlemavu wa watoto wa kike,sasa kuachiwa tena binti mrembo akiwa katika hali ya ufahamu wa kutojifahamu kitendo hiko kilimfuraisha sana, akaulamba mdomo wake kwa tamaa, madam tu alipotoka akafunga mlango na kukiparamia kitanda,




Jane akiwa ajielewi akajikuta akimpokea na kumpa ushirikiano,wakazama penzini!...




*****




Gari ilizidi kukata mbuga,yule binti kule nyuma alitamani hata kuitoa sauti yake kuomba asamehewe lakin kitambaa alichofungwa mdomoni akikumuwezesha kufanya ivyo,




Wakati Suzan akiwa bado kakasirika ghafla mlio wa meseji ukaingia kwenye simu yake akaifungua ile meseji kuisoma...




"ingia whatsupp mdogo wangu nina zawadi yako nzuuuriii"




Suzan akashtuka,akatoa 'ear phone' zake na kuzivalisha kwenye simu kuzuia sauti kutoka nje akawasha data meseji zika anza kuingia...




Akaikuta Video alokwisha kutumiwa na Katarina,chini yake iliandikwa ukishatazama video hii nipigie...




Akai 'danload' Ile video na kisha kuitazama,hakuamini kile akionacho palepale akamwambia dereva asubiri,yani asimamishe gari,akashuka kuongea na simu akiwa acha watu kwenye gari wakishangaa mshtuko aloupata Suzan




Kule nje nyuma ya gari Suzan akampigia Katarina huku hofu yake ikionekana waziwazi




"nilikuwa na mawazo nimtumie mume wetu hii video aone upumbavu na malengo ya mke mwenzangu, ila nikaona si vyema nikafanya ivyo bila kukujulisha hata tupange kipi tufanye pengine unaweza nishawishi kitu nikafikiria msamaha,pili mama yako ni naye wa kumuokoa ni wewe kivipi sasa?!,naitaji uje peke yako mbezi ya huku kimara ukifika stendi hapo unijulishe mi ntakuja kuonana na wewe hapo,narudia tena uje peke yako ukiena kinyume na hili nikwambialo wallah hii video namtumia mchumba ako Zidu,uone kitu atakachokufanya na pili mama yako mzazi utamkuta katupwa cocobeach au mbezi beach kama siyo msitu pande nikutakie kila la kheri"




Katarina akakata simu,Suzan akuongea chochote alikuwa ndani ya butwaa,ghafla si ndo azinduke,




"mshusheni huyo dada mnipeleke mbezi ya kimara"




Suzan huku akiwa kama kachanganyikiwa akatoa amri...




Palepale yule binti akafunguliwa kamba, kitamba kile cha mdomoni akashushwa gari ikageuzwa kuelekea huko mbezi...








Madam 's' anagundua ni kweli Jane katibu muhtasi wa kamishna aliongea na kamishna sekunde chache kabla ya yeye kuingia kule ofisini na kumkuta ni maiti,kivipi sasa,hali hiyo inampa maswali mengi kichwani kwake anayoshindwa kuyapatia majibu twendelee nayo tuzidi kuburudika na kuelimika pia!...




'itawezekanaje lakini?, kamishna alikufaje kufaje au muuaji akupitia mlangoni?!'




Madam alizidi kuwaza huku akizidi kusonga kuelekea palipo na maegesho ya magari



ITAENDELEA


Simulizi : Kufa Tu  Hakuna Namna (2)


Sehemu Ya Tano (5)




'inawezekana!,itanipasa nikaichunguze tena ile ofisi ya kamishna kwa mara nyingine na kwa umakini zaidi pengine yule binti ajui kitu maskini'




Akazidi Kuwaza akiingia kwenye gari yake,na kuirudisha nyuma




'zk!,...huyu si mwingine zaidi ya huyu mwanaharamu anazidi kukichanganya kichwa changu sitomwacha hai nasema'




Madam akazidi kuwaza, akikanyaga mafuta na kubadilisha gia,alijikuta akiwa na mawazo rundo,




'lengo hasa la Zk ni nini na binti huyu anatumiwa na nani?!'




Wazo lile la awali likajirudi kwenye kichwa chake,wazo lililokuwa likikiumiza icho kichwa na kumkosesha raha wakati akiwa bado yupo katika mkanganyiko ule wa mawazo ghafla simu yake itaita haraka sana akaipokea baada ya kutazama katika kioo na kuona jina la alompigia...




"nambie Don G!"




"ingia utube katika akaunti ya yule zk"




"kapost!?"




"tumekwisha madam we ingia uone"




Palepale madam akakata simu na kuingia katika akaunti hiyo...




Alichokutana nacho alijikuta akiiachia simu mpaka chini na wakati akiwa katika harakati za kuiokota akajikuta kwa kutetemeka akiikanyaga,




Alichokiona Kilitisha,ikabidi Apaki gari kwa pembeni presha itulie maana moyo ulikuwa ukimwenda mbio,ninini alicho ona!...




TWENDE HAPA




SURA YA SABA




MBEZI




Ni katika jumba moja la kitajiri maeneo ya mbezi ni lile jumba alilopewa Katarina na muheshimiwa Raisi,ndani wakiwa wanaishi watu wa nne,bibi na babu kama walezi wa nyumba,mwanadada Zena pamoja na Zena kama mmiliki wa nyumba hiyo,




Siku kadhaa zikiwa zimepita toka wafanye shambulio la kumuua kamishna siku hii ya leo




Ndani ya usiku ule usingizi ulimpaa Zena akiwa ndani ya chumba chake kajilaza alijikuta akitafakari baadhi ya mambo katika fikra zake,ghafla akakumbuka jambo,




Haraka sana akaamka na kwenda kuichukua ile line yake ya siri na kuipachika kwenye simu yake!




akasachi upande wa meseji!, akabaki kaduwaa akiishangaa meseji moja




'ushahidi wa waziri upo nyumbani kwangu chumba nilichokuwa nimepangisha ndani ya viatu vyangu ndani ya sox rasa"




"Rasa?!"




Zena akawaza akitafakari ilo neno la mwisho,ile meseji anakumbuka kuna siku Raisi alimtumia meseji ndipo akaweka ile line ile meseji ikaingia ila aliipuuzia baada ya kumuuliza Rais,Rais hakakana kwamba ajamtumia meseji kama ile,kwa kipindi kile aliamua kuipotezea akijua pengine ni meseji ya mtego,akuiweka kichwani sana kipindi kile...




Leo hii akiwa pale kitandani si ndo akaikumbuka na kuitia line kwenye simu na kuisoma,akaitafakari sasa kwa makini!




'Rasa?!...' akarudia tena lile neno la mwisho ambalo alikuleta maana katika sentensi yote ile 'Sara!' Akajikuta akitamka baada ya kulisoma kinyume!




'huyu pekee ndo anaweza kuijua hii namba,kwa kuwa naye ni mwandishi yupo pia katika group la waandishi




Akakumbuka Ile siku akichukua video tukio lile akiteswa akilazimishwa atoe kihifadhi kumbukumbu ghafla akauwawa tena mbele ya macho yake kabla yeye kupigwa na kitu kizito nyuma yake kamera na hata simu yake ikachukuliwa!




*SARA?!*




Suzan akaita kwa sauti ya taratibu akista ajabu kuchelewa kugundua lile...




"nimekutoa gerezani nimekusaidia hili nawe unisaidie,utafanya kazi chini yangu ila ripoti utonipa mimi,hapana...




naitaji uwe mwandishi wa habari ila ficha sura yako isitambulike ovu lolote utakaloliona katika serikali yangu nilione katika televisheni?...




...na maana yangu na ipo siku utajua nini namaanisha...




...najua ni kazi ngumu ninayokupa ila ifanye kwa weledi utafanikiwa...


na utaona matunda yake




Maneno yale aliyo kwisha wahi kuambiwa na Rais wake,yakajirudiakatika mawazo yake,na palepale akajinyanyua kwa kuwa kwa saivi yule mwandishi mvaa....alikuwa akisakwa akuangaika kuvaa vile


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog