Search This Blog

Friday, 30 December 2022

KIAPO (AGANO LA DAMU) (2) - 4

 


Simulizi : Kiapo (Agano La Damu) (2) 

Sehemu Ya Nne (4)




"bosi Namuua Kukudhibitishia Ni Mkeo"



"potelea Pote Ua" Mh Zidu Akaongea Kwa Hasira Kwani Alikuwa Na Uhakika Yule Si Mkewe Na Atakayeuwawa Ni 

Mwingine



Alijidanganya



Ili Kumdhibitishia Mh Yule Ni Mkewe Zidu Akaamua Amuue Palepale Hotelin







Maisha Ya Mtoto Isack Yanapitia Katika Vikwazo Vinavyohatarisha Hata Maisha Yake!



Ikijulikana Kwamba Ameuwawa Anachukuliwa Na Mtu Asojulikana Mwenye Asili Ya Kizungu Na Kupelekwa Katika 

Nyumba Moja Ya Kifahari!,mtu Yule Anatoka Na Kuondoka Zake!



Je Ni Wapi Kule Alipopelekwa Na Mtu Yule Ni Nani?! Twende Pamoja Kupata Majibu Ya Maswal Haya!



NA HII NI SEHEMU YA AROBAINI NA NANE



NDANI YA JUMBA LILE



Ndan Ya Jumba Lile Katika Chumba Kimoja kilichokuwa na mandhari ya hospitalin kwa ndani,katika kitanda 

alilala mtoto isack!



Pembeni Ya Kitanda Kile Alikwepo Daktar Ambaye Alikwepo Kumshangaa Yule Mtoto!



Ni Baada ya kugundua kuwa yupo hai wakati alishazoea kuletewa watoto wafu ila akutaka kufatilia sana 

jambo lile kwani hiyo aikuwa kazi yake kazi yake ni kumpasua mtoto yule kumweka madawa na kumshona!



akaamua kumpiga kaputi,baada ya kumpiga kaputi akampasua na kupanga pakiti kadhaa za madawa ya kulevya 

akamshona!



baada ya kazi ile kukamilika akampigia simu yule mzungu ambaye aliwasili akiongozana na toyota yenye 

bodi na wamama kadhaa wakiwa wamekaa kwenye gari ile! ilopangwa kimsiba

wakashusha jeneza na vijana kadhaa wakaingia nalo ndani wakamuingiza isack ndani ya jeneza lile!,puani 

akaekewa pamba,wakamuingiza ndani ya gari na gari kutoka,ilionekana ni kama msafara wa msiba!



wakaelekea mpaka ear pot ambapo mait ile aikukaguliwa ikapandishwa kwenye ndege ikiwa ndani ya jeneza 

lake tayari kusafirishwa! kwenye ndege walipanda wamama kadhaa wa kizungu ndege ikapaa! na kuiacha 

ardhi ya tanzania!



***



Wakati Isack Akiwa Ndani Ya Ndege Upande Wa Pili Zidu K' Aliendelea Kufatilia Nyendo Za Bi Ney Na 

Mwalimu Gibson!

Sasa Walilewa Na Kwenda Kuchukua Chumba!



Wakati Wakiwa Chumbani Ilimbidi Mwalimu Gibson Aingie Bafuni Kuoga!



Ni Wakati Huo Wakiwa Bafuni Ghafla Mlango Ukagongwa!



Bi Ney Akijua Pengine Ni Muhudumu Akajinyanyua akiwa na kaupande cha khanga aliumbika kwa kwel hasa 

huko nyuma akausogelea mlango kuufungua!



ile kaufungua tu,hata kabla ajamuona wa nje Zidu Akaingia Na Kumkamata Mdomo Kwa Mkono Mmoja,mkono 

Mwingine Akamchoma Nao Kisu Alipoakikisha Amekata Roho Akamuachia Kwa Kumshusha Taratibu Kukwepa 

Kishindo,baada Ya Hapo Akaufunga Mlango Kwa Ndani Akalirukia Dirisha Na Kutoka Haraka Sana Akaenda 

Kuufunga Kwa Nje



Muda Ule Ule Akapiga Simu Polisi Kama Raia Mwema!...



Mwalimu Gibson Alitoka Bafuni Ghafla Alipigwa Na Butwaa Kwa Kile Alichokiona! Kwa Sekunde Kadhaa 

Akabaki Kaganda Kama Sanamu Akiushangaa Mwili ule kama ndo anauona kwa mara ya kwanza,ghafla akazinduka 

na kuukimbilia pasina kujielewa akakigusa kile kisu kwa mshtuko pasina kujua ana acha alama zake za 

vidole,akawa akiita kwa nguvu mpz mpz mpz!,machozi yakimtoka!



ghafla akasikia hodi nje!,hapo ndipo aliposhtuka!



hapo ndipo alipoiona hatari ilokuwa mbele yake,ambayo hapo awali akuiona!



kwa vyovyote vile alijua bi ney atakuwa kajiua lakin kwa nini afanye hivyo?

kwanini amuweke katika hatari kubwa kiasi icho?



kwanini?!



"nimekwisha mimi!" akajikuta akijilaumu akisahau majuto ni mjukuu na majuto ujaa baada ya tatizo!



ghafla mlango ukavunjwa na maaskari wakiwa na mitutu sambamba na waandishi wa habari waloanza kwa 

kupiga picha chapchap wakaingia!



mwalimu Gibson Akawekwa Chini Ya Ulinzi!



Kaua Mke Wa Waziri?!



Ilikuwa Kesi Ngumu Ambapo Kwake Kuishinda Ilikuwa Ni Vigumu!,



Akatolewa Chini Ya Ulinzi Mkali Mpaka Ndani Ya Karandinga La Polisi,mwili Wa Bi Ney Nawo Ukatolewa 

Ukaingizwa Kwenye Ambulance Kwenda Kufanyiwa Uchunguzi



Katika Wingi Wa Watu Wale,Zidu pia alikwepo! kama si yeye msababishi watukio lile,awamu hii meseji 

alomtumia bosi wake ni angalia tv mida hii!



makubwa...



***



Waziri Alex Alimuamini Sana Mke Wake,akutaka Kumuamini Zidu Kwa Swala lile,wakati bado akiwa ofisini 

ghafla mlio wa msg ukaingia katika simu yake! washa tv!



akastaajabu,ila akubisha akashika rimonti baada ya kubonyeza swichi ukutani akaiwasha tv! kile 

alichokutana nacho akuamini! sura ya mke wake ilikuwa chini kisu kifuani! ikisemekana kauwawa hotelini!



ghafla simu zika anza kuingia za kumpa pole moja wapo ikiwa ya mheshimiwa max rais wa nchi!,akapokea...



"pole sana kwa msiba mheshimiwa!"



"ina maana ni kweli mama mery amekufa?"



badala ya kujibu naye akamuuliza,rais akajua huyu mtu ayupo sawa akakata ile simu!



mh alex akazima simu kabisa kukwepa usumbufu! kumbukumbu zake



zikarudi nyuma kidogo! masaa kadhaa nyuma Zidu Alipompigia Na Jinsi Alivyomjibu Mpaka Kumruhusu Kuua Na 

Kwel Kaua!...



'ina Maana Kwel Mke Wake Alikuwa Msaliti?'



Anakumbuka Kabisa Zidu Alimpigia Kwa Mara Ya Kwanza Akamkatia,akampigia Tena...



"nilikwambia Nikikukatia Simu Zidu Nipo Kwenye Kikao"



"najua Muheshimiwa Ila Dharura Ni Kwamba Nikwambie Saiv Utoe Maamuz Ntekeleze Muda Huu"



Akakumbuka Zidu Alimwambia Awashe Data Na Kwel Akawasha!



Palepale Muheshimiwa Akaiwasha Simu Yake Kwa Mara Nyingine Na Kwenda Upande Wa Galary Akaanza Kucheki 

Picha Alizotumiwa,ambazo Mara Ya Kwanza Alizipuuzia! Akakumbuka Hata alipompigia simu mkewe akamwambia 

ampe aongee na mwanaye akaongea naye!



huko hotelini je kaenda sangapi?!,akuamini akampandia hewani,simu ikaita pasina kupokelewa,ghafla kiti 

kikawa cha moto pakawa apakaliki tena! akasimama na kutoka mule ofisini akaingia ndani ya gari lake 

akaliwasha!



akaingia barabarani,akujua anaelekea wapi,je aelekee hospitalin au nyumbani bado hakuwa na jibu 

sahihi,bado akuamini mawazo yak ilikuwa lazima aende nyumbani aka akikishe je Alipomuomba Aongee Na 

Mery Naye Akampa Ni Mery Yupi?



hali ya sintofahamu ikazidi kuushambulia moyo wake!



Mery Na Mdogo Wake Agnes Baada Ya Mama Yao



kutoka awakuwa na kingine cha kufanya zaidi ya kuwasha tv na kuanza kuangalia,ile ndo ilikuwa starehe 

yao pekee ilobakia!



wakati wakiendelea kuangalia ghafla simu ya Mery Ikaita!



"mom Anapiga"



Mery Akaongea Akiipokea Ile Simu!

Mama Yake Akampa Maelekezo Naye Akafanya Ivyo Ivyo Mpaka Wakamaliza!



"lakini Siyo Vizur Ivyo Dada Mnavyofanya Hivi Unajua Mama Ni Wapi Yupo?"



Agnes Alimuuliza Dada Yake Baada Ya Mery Kumsimulia Kila Kitu



"kwa Hiyo Mimi Ningefanyaje Egi! Ni Kweli Tabia Ya Mama Mimi Mwenyewe Siridhiki Nayo Kila Mara Anatoka 

Atujui Ni Wapi Anapoelekea...



Ghafla Akanyamaza,wote Wakaduwaa Macho Yao Yakanata kwenye screen katika tv waliyokuwa wakiitazama

"mamaaa!"

wote wakaita kwa pamoja!



vilio vikatawala!



hata muungurumo wa gari la baba yao awakulisikia,ila mheshimiwa alex naye alishtuka kusikia vilio ndani 

ya nyumba yake!

hapo ndipo alipoamini mke wake ni maiti!

hapo ndipo alipoya amini maneno ya Zidu! Akafungua Mlango Na Kuingia Ndani! Watoto Wote Wawili 

Wakamkimbilia Na Kumkumbatia! Huku Wakilia



Kwa Mara Ya Kwanza Familia Ya Mr Alex Ikaingia Katika Majonzi,uzuni Simanzi Ikatawala Baina Yao!



UWANJA WA NDEGE MAREKANI



Ndege Ile Ilombeba Isack Ilitua Katika Uwanja Wa Ndege Mdogo Nchini Marekani

Mlango wa ndege ukafunguliwa na jeneza lililombeba isack likashushwa,likapakiwa katika gari lilokwisha 

andaliwa,wamama na wakaka wale walovaa nguo nyeusi wakasaidiana kupakia lile jeneza kwenye gari,gari 

ile ikaondoka kutoka nje ya uwanja ule wenyewe wakiimba mapambio ya msiba!



Isack mule ndani ya jeneza bado akuwa na ufahamu wa chochote kilichokuwa kikiendelea!



dokta alimpiga nusu kaputi iliyomlevya moja kwa moja!



pembeni kabisa ya mji kwenye uwanja mkubwa wa makaburi,kaburi moja lilikuwa likimaliziwa kuchimbwa hili 

ndilo angezikiwa Isack baada ya kutolewa mzigo uliokuwa katika tumbo lake!







Wakati Akiwa Katika Hatua Za Mwisho Kudondoshewa Kisiman Na Kuyeyuka,mh Alex Anapigiwa Simu,badae 

Kidogo Anakuja Kuchukuliwa Na Mzungu Mmoja Anasafirishwa Mpaka Nje Ya Nchi Akiwa Kaekewa Madawa Ya 

Kulevya Ndani Ya Tumbo Lake!

Tayar Kaburi Lake Limesha Andaliwa Je Nin Kitaendelea?!

Songa Nayo Sasa Ujifunze:



Bilionea Macdonald Mwenye Asili Ya Mmarekan Mweusi Alikaa Kwenye Kochi,mawazo Yake Yalikuwa Mbali,mbali 

Sana!



Mkewe Bi Sarah Alikaa Pembeni Yake Naye Akuwa Na Furaha,ni Kama Kuna Majadiliano Yasiyokuwa Na Mwafaka 

Yalipita Baina Yao!



Walikuwa Ni Miongoni Mwa Matajiri Wakubwa Nchini Marekani!



Ghafla Akanyanyuka kwa hasira!



"nataka mtoto!"



akaongea neno moja na kutoka zake!



Daktar Horace Alishtuka Baada Ya Kugundua Yule Mtoto Yu Hai! Ni Katika Hatua Za Mwisho Za Kuushona 

Mwili Ule!...

Akashika Simu Yake Na Kumpigia Bos Wake!



"ule Mwili U Hai Bosi"



"ua"



Bosi Wake Akampa Jibu Moja Na Kukata Simu!



Pamoja Na Kwamba Dk Horace Alikuwa Akifanya Kazi Ile Ila Alikuwa Na Uwoga Na Mungu,kuua Kwake Lilikuwa 

Ni Swala Lingine!



Akabaki Akimwangalia Isack Aliyekuwa Akipumulia Hewa Ya Oksyjen Aliyemwekea Baada Ya Kugundua Yu Hai!



"sijui Hata Ntakusaidiaje Mtoto?"



Akajikuta Akiwaza Ila Kabla Ajapata Maumivu Ghafla



simu yake ikaita tena,mpigaji alikuwa ni yule yule bosi wake!...



Niwafanya Biashara Wawili Wakubwa Marafiki Wakubwa Walopendana,



"ndo Ivyo Rafiki Yangu Hili Ndo Tatizo Lililopo Mbele Yangu"

Macd Aliongea Kwa Simanzi Alimsimulia Kila Kitu Rafiki Yake Yule Horace Juu Ya Adha Ya Mtoto!



"nenda Kachukue Katika Vituo Vya Kulelea Watoto Mnaweza Kupata Hata Katoto Kachanga Mkakalea Nyinyi Au 

Kama Jau Kaongee Na Manesi Wawaibie Mtoto!..



Ghafla Simu Yake Ikaita!



"sory Embu Subiri,ehe Nambie Dokta,yupo Hai,ua"



Mac Akatoa Macho!



"kuua Tena Ninin Swaiba?"



"haaa Si Unajua Tena Kazi Yangu Nikatoto Kalicholeta Mzigo Kumbe kapo hai,"



Mac Akatoa Macho,



Maumivu Anayoyapata Katika Kutafuta Mtoto Aman Imeshatoweka Katika Nyumba Yake Kisa Mtoto Leo Rafiki 

Yake Anasema Ua Tu!



"huyo Mtoto Anakama Umri Gani!"



"sijui Hiyo Habar Tuachane Nayo Ndo Kama Nilivyokueleza Nenda Hosptal Ongea Na Nes Toa Ela...



"hapana Namuitaji Huyo Tafadhali Zuia Asiuawe"



Horace Akashtuka!,akayatoa Macho Ya Mshangao Kumshangaa Rafiki Yake Yule



"eti Unasema Unamtaka Nani?!"



Akauliza Pasina Kuamini,



"namtaka Huyo Mtoto Aliyeleta Mzigo Huyo Ndo Atakuwa Mwanangu!"



"kivip Sasa Mac Mbona Sasa Unataka Kunletea Shida Kwanz Dokta Atakuwa Kashakaua"



"naomba mpigie simu saivi nijue moja! yupo hai au amekufa"



"ila mac katoto kale kubaki hai ni hatari kwangu! istoshe nikakubwa na kana akili kanatambua wazaz wake 

maswal yake tutayajibuje?"



"aijalishi! mi sindo nakulinda,nakupigia kifua kutogundulika bas fanya kama nlivyokwambia haiwezekan 

wengine tutafute watoto kwa shida nyie muue kizimbe"



"bas swaiba si yameisha"



Horace Akamalizia Akishika Simu Yake Akampigia Yule Daktar Wake Huku Moyon Akiombea Awe Tayari 

Ameshakaua!



"ehe Nambie Dokta Yule Mtoto Umeshamuua?"



"ndi..Hapa..Hapana,bado Nlikuwa Namalizia Kazi"



"bas Uskaue Akikisha Yupo Salama Tunakuja Hapo saivi"



"sawa bosi"



wakakata simu!



"bado yupo hai mh"



"ok tunaweza kwenda kumuona"



kiongoz yule wa ngaz za juu katika jesh la polis nchin marekani sir macdonald alimalizia, wakajinyanyua 

na kuingia ndani ya gari safar ya kuelekea kule katika jumba aliloifadhiwa isack ikafatia,



BAADA YA SIKU MBILI:



Mwili wa madam jane ulifukiwa simanz majonz aibu vikitawala



baada ya mazishi ndipo macho ya watanzania yakageukia kwa mwalimu Gibson!



Kesi Ya Kusababisha Mauaji Ikaanza Kurindima,kwa Kuwa Vidole Vyake Ndivyo Vilivyo Onekana Kwenye Kisu 

Akapewa Hukumu Ya Kifo!



Kunyongwa Mpaka Kufa



Familia Yake Baba Mama



wadogo zake bado walimtegemea ila tamaa ilo mponza fisi nayo ikamponza na yeye



waswahili awakukosea pale waliposema mwisho wa ubaya ni aibu ni kwel malipo ni hapa hapa duniani

ule ndo ulikuwa mwisho wa mwalimu gibson na mwenzake bi ney!



Mzee Alex Aliamua Kuwapeleka Watoto Wake Nje Ya Nchi Kwa Ajili Ya Masomo!



SURA YA KUMI NA NNE



ST LUCY COLLAGE



Hiki kilikuwa ni chuo kikubwa sana nchini marekani,chuo cha vipaji ambacho walisoma watoto mbalimbali 

viongoz wa nchi!



katika kiti maeneo ya restraunt walikaa watu watatu hawa ni kutoka taifa moja TANZANIA!



Alikwepo Mery,Agnes,watoto wa wazir wa ulinz nchini Tanzania,pia alikwepo mtoto alojulikana kwa jina la 

Brayson huyu ni mtoto wa rais max anayeitawala nchi ya Tanzania



watoto wale wa viongoz walikutana katika nchi moja wakitoka katika taifa moja

wakatokea kuwa marafiki wakubwa wote watatu wakisomea siasa!



Bray Huyu Ndo Yule Rafiki Yake Isack Alotumiwa Na Mwalimu Gibson Kuweka Simu Katika Begi La Isack!



Mery Akumkumbuka Tena Isack,na Mdogo Wake Agnes Alifumbwa Mdomo Kutomueleza Chochote Dada Yake Juu Ya 

Isack!

Naye Kwa Kuwa Alijua Isack Kwa Sasa Ni Maiti Akumweleza Kitu Dada Yake



Gari Yao Ikapiga Breki Nje Ya Jumba Lile La Kifahari Ambalo Ndani Kulikuwa na chumba kilichogeuka kuwa 

wodi!

watu wale wawil,marafik waloshibana wakashuka kwenye gari na kuingia ndani ya jumba lile!



wakaelekea katika chumba alicholazwa isack!



"wa..na..taka kuni.ua. wa..na..taka kun.i.ua"



ilikuwa ni kama yupo ndotoni!



"nani hao wanaotaka kukuua?"



sar donald akauliza kwa mshangao



"wa.nat.aka..,ku.ni.u,a"



"nani hao?" horace naye akaoji



"mh alex!"



wote wakashangaa,ila muda huo huo daktar akatokea kwan alikuwa chumba kingine!



"kashazinduka ila bado kumbukumbu azijatulia ni lazima achomwe sindano za mapumziko"



wakampisha daktar akamchoma sindano mtoto yule akalala tena!



kwa muda ule kila mmoja alikuwa na mawazo yake



sir donald alikuwa akimshangaa yule mtoto alimpenda aliapa kuishi naye na huyo ndo mwanaye!



ila ni kama isack alikuwa na nyota ya mikosi,kwa upande wa sir horace yeye alimuona yule mtoto kama 

balaa mropokaji,



kitendo cha kumtaja mr alex mbele yake akikuwa kitendo kizuri yule mh alex ni mfuas wake,kumtafutia 

watoto kuwasafirisha kwa kaz yake! yule kujua kuwa alitaka kuuwawa na mheshimiwa yule kwake likawa kosa



roho mbaya ikamvaaa



'lazima haka katoto kafe'



akawaza akitoa simu yake mfukoni akaingia upande wa internet katika email akatuma meseji mbona 

umenletea mtoto mzima,badala ya maiti? sasa kanaharibu mambo huku



Muda Huo Mheshimiwa Alex Alikuwa Bungeni,baada Ya Kusoma Meseji Ile Akatoka Na Kuelekea Chooni 

Akampigia Yule Mzungu Sir Horace



"unasema Nani Yupo Hai?"



"kale Katoto Ulichokaleta"



"nini?!..."



Kizunguzungu Kikali Kikamshika Mheshimiwa Yule Giza Likatawala Machoni Pake Na Ghafla Akaenda Chini!...



*dah Mh Alex Aambiwa Isack Bado Yupo Hai Apoteza Fahamu Huku Alomwambia Akieka Nadhiri Ya Kukaua Katoto 

Hako,nin Kitatokea?!*









Jinamiz La Mauaji Bado Linamuandama Mtoto Isack!

kila hatua anayoipiga kwake inakuwa ni ya hatari anakata tamaa ya kuish ila Mungu Bado Anamlinda! je 

Nin Hatma Ya Mateso Yake Yote Yale!



TWENDE PAMOJA MTUNZI AKUENDELEZEE



NA HII NI SEHEMU YA HAMSINI



Walinzi Ndio Walogundua Kuwepo Kwa Mwili Wa Mh Alex Ndan Ya Choo,haraka Sana Mlango Ukavunjwa Mzee Alex 

Akatolewa Akuwa Na Ufahamu Akaanza Kufanyiwa Huduma Ya Kwanza



Akiwa Ndani Ya Chumba Kimojawapo Cha Tiba Kilichomilikiwa Na Bunge Lile Atimaye Alipata Fahamu,kichwa 

Kilikuwa Kinamuuma,akajaribu Kuvuta Kumbukumbu Kilichotokea!



"isack Yupo Hai" Akanong'ona

mwenyewe ni kama akuamini kile alichokisikia



"unaendeleaje mheshimiwa?"



mmoja hapo wa daktari wa bunge lile alimuhoji alex! ambaye alisema anajiskia vizuri tu



"ni shock mshtuko tu ulipata mheshimiwa"



daktar yule akazidi kumtanabaisha, mh alex awamu hii akuongea kitu akajinyanyua Na Kuufata Mlango 

Akatoka Zake!



Alishindwa Kuelewa Yule Mtoto Ana Kitu Gani? Mara Ngapi Ameshindwa Kumuua,mbona Lakini Alikufa 

Imekuwaje?!



Robo Saa Baadaye Alikuwa Ndani Ya Jumba Lile La Zidu,



Si Kwa Yeye Pekee Hata Zidu Akuamini Kile Alichokisikia!

Isack Yupo Hai?,alijikuta Yey Mwenyew Tu Hata Hamu Ya Kuendelea Kumuandama Kwa ajili ya kumuua 

ikiyeyuka!



"kesho yapaswa usafiri kuelekea nchini marekani huko utapokelewa na mtu wangu ambaye atakuonesha mahali 

anapopatikana huyo mtoto! dah! anatutesa kwa kwel"



Zidu Japo Kazi Ile Sasa Ilishamchosha Akuwa Na Jinsi Zaidi Ya Kukubaliana Na Bosi Wake!



Wakatoka Kwenda Kushughulikia Usafiri Wa Hiyo Kesho!



Kesho Yake Asubuh Na Mapema Kama Walivyopanga Zidu Alikuwa Ndani Ya Ndege Akielekea Nchini Marekani Kwa 

Kazi Ile Maalumu!



MAREKANI



Hali ya isack sasa ilishatengemaa sir Mac donald akamchukua na kumpeleka kwake!

mke wake bi Sara Alimpokea Kwa Mikono Miwili! Alionesha Kumpenda Mtoto Yule!



"huyu ndo mrithi wa mali zangu"



Macdonald Aliongea Kwa Furaha!



"yapaswa Sasa Umkatie Urahia"

Bi Sara Akamkumbusha Mwenziye!,

"hiyo Shughuli Ntainza Kesho Huyu Sasa Ni Mwanetu Isack Mimi Ndo Baba Yako Na Huyu Ndo Mama Yako"



Isack Alifrah Sana,ghafla Machoz Yakaanza Mchuruzika!



Wote Wakashtuka,baba Yake Na Mama Yake!



"unalia Nini Isack?" Bi Sara Akamuoji Kwa Mshangao Ikabidi Isack Aanze Kuwasimulia Kuwa Mapenz Kama 

Yale Aliyapata Kipindi Wazazi Wake Wakiwa Hai,japo Walikuwa Maisha Duni,kula Yao Ilikuwa Tabu Ila 

Upendo Kama Ule Aliupata



Ila Aukudumu Akawapoteza Wazaz Wake,kuwapoteza Wazaz Wake Kukawa ndio ufunguo wa mateso toka katika 

familia ya mh alex alokuwa jirani yao,akaja chukuliwa na ba mdogo wake ambaye alitaka kumuua,



mpaka muda ule kwa akili zake za kitoto alijua Zidu Ni Ba Mdogo Wake Lakin Sasa Kwa Nini Atake Kumuua?!



Ilo Hata Sir Donald Na Mkewe Awakuwa Na Jibu La Kumdhihirishia,akaendelea Kuwaelezea Kuwa



Ndipo Alipo Okolewa Na Mwalimu Wake Toka Porin,mwalimu Wake Ambaye Kwa Sasa Akuwa Hai,isack Akazidi 

Kulia,alikumbuka Alivyoishi Na Madam Yule Pamoja Na Ins Nurdin Ambaye Mpaka Sasa Ajui Yuko Wap Bila 

Shaka Naye Wamemuua!



Isack Alilia,akalia,mwisho Akaomba Aondoke



"sitaki Kuwasababishia matatizo kila ninayeishi naye lazima afe,sitaki nyinyi mfe nimezaliwa kuteseka 

niacheni nteseke Mungu Atanlinda"



"hapana Isack Useseme Ivyo!,muuaji Ni Mtanzania Na Huku Ni Marekani Awez Jua Kama Hupo Huku Nami Baba 

Yako Pia Ni Polis!"



"mbona Mjomba Nurdin Naye Ni Polis Lakin Amekufa"



"basi Kama Una Khofu Na Maisha Yetu Jumatatu Tutakupeleka Bording"



Isack Hapo Akatabasamu!



"kama Ivyo Basi Sawa!"



"we Unapendelea Kipaji Gani?!"



"sheria Nije Niwe Hakimu Niwahukumu Wanaotaka Kuniua,napia Napenda Niwe Polis Japo Naogopa Kufa Kama 

Mjomba Nurdin"



Wote Wakacheka!



Katu Awakujua Kuwa Zidu Mzee Wa Kaz Muda Ule ndo alikuwa kashatua kwenye ardhi ya Marekani...



Sir Horace Ndiye Aliyempokea...

Akampeleka Mpaka Hotelin Na Kumpa Maelekezo Mahali Anapopatikana Isack!



"ila Anaishi Na Mwanausalama Yapaswa Uwe Makini!"



Zidu Alishtuka Kidogo Ila Kimapigano,kutumia Silaha Alijiamini!



Siku Hiyo Hiyo Mida Ya Jioni Aliichunguza Ile Nyumba,kesho Yake Yani Juma Mosi Usiku Ndipo Siku 

Alopanga Avamie!



Jumamosi Asb Mac Na Isack Wakatoka,ambapo Alipelekwa Shopping Kununuliwa Nguo Za Nyumban,za Shule,vifaa 

Vya Shule...



Hatimaye Wakarudi Nyumbani,isack Akujua Chuo Atakacho Kupelekwa Ndicho Kile Asomacho Mahasimu 

Wake,akiwemo Mery,Agnes,na rafiki yake kipenzi Brayson



Jioni Wakiwa Sebuleni Wanakula,ghafla Taa Zikazima



Kiza Kikatawala!



Mnyama Zidu Alikuwa Ndani Akiwa Na Bastola Yenye Bomba Mbili



Alivaa Nguo Nyeusi,yeye Ndiye Aliyezima Umeme



Alikuwa Tayari Kwa Kazi,na Kabla Ajazima Umeme Aliwachungulia Pale Walipoketi Na Kuwawekea Target! 

Ndipo Alipozima Taa



lengo aue wote,bila kupoteza muda risas zikacheua na kuzalisha mayowe kule apigapo kimya kikatawala!



akaachia tabasamu!





maisha ya mtoto Isack Bado Yanatembelewa Na Umande Wa Umauti!



Akiwa Kapata Mtu Anayemjal Nchin Marekan,siku Ya Pili Tu Wanavamiwa Na Zidu,umeme Unakatika Zidu 

Analenga Mahali Alipo Kwa Risas Mfululizo Mayowe Yanasikika!



Je Unahisi Ni Nin Kilichoendelea?!



Twende Pamoja Mwandishi Akujuze!...



Zidu Alijua Kashawamaliza Akauelekeza Mkono Kuliko Na Swichi Akaiwasha! Macho Yakidondokea Pale Mezani!



Alishtuka! Akukuwa Na Mtu Alodhurika Wote Walilala Chini! Ile Anataka Aunyooshe Mkono Wake Wenye Silaha 

Kuwaelekezea Bi Sara Na Isack Pale Chini Ghafla Alishtukia Kitu Kikitua Shingoni Mwili Wote Ukamlegea 

Akaenda



chini silaha ikimponyoka akapoteza fahamu,pasina kumuona hata yule alompiga!...



Nywele Zilimsisimka, kopezilimcheza, meno Yaligongana Hii Kwake Ilikuwa Ni Kama Machale!



Machale Ni Hisia Azipatazo Mtu Kuonesha Hatari Iliyoko Mbele Yake!,wapelelez Au Makachero Wengi Sana Ua 

Awapendi Kudharau Machale



Ndivyo Hivyo Hata Kwa Mac Donald Afisa Upelelez Na Anayetoka Katika Shirika La Ujasusi Marekani Fbi 

Alijua Lazima Kuna Kitu Kitatokea!



Kitendo Cha Umeme Tu Kukatika Akaachia Yowe,ambalo Lilikuwa Ni Kama Taharifa Ya Hatari Kwa Mke Wake 

Naye Akajibu Akienda Chini Sambamba Na Kumsukuma Chini Isack



Sekunde Ile Ile mirindimo ya risasi ikaskika,Donald Akatambaa Kuelekea Kuliko Swichi Akawa Nyuma Ya 

Zidu Ile Zidu Kaiwasha Taa Tu Akamuachia Pigo Maalumu Shingoni!



Pigo Lililomzimisha,akamsogelea Na Kumwangalia Vizuri,akaishika Simu Yake Kupiga Idara Ya Polisi,dakika 

Chache Polisi Na Waandishi Wakawasali Na Kumbeba!



Isack Alilia Akujua Kwanin Mtu Yule Aliisakama Roho Yake!,baba Yake Yule Alimtoa Wasiwasi Akimwambia 

Kwa Sasa Awe Na Amani Tu Zidu Atotoka Kamwe Rumande! Atafia Huko...



Habari Za Kukamatwa Kwa Zidu Zilimshtua Sana Mzee Alex,akampigia Simu Rafiki Yake Kipenz Walokuwa Nay 

Pamoja Katika Biashara Ile



"kwa sasa mtu yule anashikiliwa na maaskar wa upelelez kumtoa ni ngumu wala tusijaribu na huyo mtoto we 

achana naye usishindane naye tena yupo kwenye mikono ya mtu hatari mkuu wa upelelez! fata maisha yako 

hii kitu ukija kugundulika unahusika unaishia gerezan mkuu"



Sir Horace Akamtia Joto Tumbo,mwili Wa Mzee Yule Ukazidi Loa Jasho,kwel Alitaman Sana Kumuokoa Zidu Ila 

Angemuokoaje Pale?!

Kikubwa Aliomba Mungu Zidu Asimtaje!



Zidu Alikuja Shtuka,moyo Ulimwenda Mbio,akagundua Kwamba Kashtuliwa,alikuwa Kafungwa Kwenye Kiti Na 

Chuma,kiti Chenyewe Cha Chuma,mikanda Ya Chuma!

Mbele Yake Alikwepo Mtu Wa Miraba Minne



alikuwa kifua wazi mwili wake ulijengeka kimazoezi!



usoni alikuwa na tabasamu baya,alivaa suruali ya jeshi la polisi la marekani!



"kwa jina naitwa p,m,k Macdonald Kirefu Cha P.m.K Ni Polis mwenye Mamlaka Ya Kuua kwa kifupi npo 

shirika la fbi ni mkuu pale,ningependa tujuane best unaitwa nan umetoka wap na imekuaje ukawa hapa?"



Zidu Alishangaa Mzungu Yule Akiongea Kiswahili Kizuri Tu,tena Tabasamu Liliupendezesha Uso Wake Katu 

Akujua Kama Huyu Ndo Aloenda Kuvamia Jumba Lake Hiyo Jana! Kwa Kiburi Zidu Akabaki Kimya!



"napendaga Mabubu Kama Wewe Mbona Utasema Tu?"



Akaiendea Switch Na Kuibonyeza Zidu Pale Akaanza pigwa shoti akaachia kilio,ila bado akufumbua mdomo 

wake!



kazi ikawa ile ile kupigwa shoti mpaka akapoteza fahamu! mac akatemana naye akatoka kiti chote kikiwa 

kimetapakaa damu!



kaushi nayo aliyoivaa ilichafukia damu zilizomtoka kwa wingi puani



badae akafumbua macho tena,mwili wote ulimwiva,mbele yake alikwepo daktari aloshika sindano na kachupa 

cha dawa!



"dokta mchome! si ataki kusema ukweli"



sindano ile ikiwa utachomwa tu bila kujielewa nilazima utasema ukweli bila kujijua na mwisho inakuua! 

ndivyo ilivyoundwa Zidu Akatoa Macho Ya Mshangao Na Woga Akil Ikafanya Kaz Zaid Ya Kompyuta!



"msinichome ntasema kweli!"



"daktar acha haya sema"



Mac Aliongea Huku Akiandaa Tape Recorder Yake Zidu Aka Amua Kujivalisha Mzigo Akijua Lazima Mh Alex 

Angekuja Mtoa



"kwa Jina Naitwa Zidu Ni Afis Wa Polisi Nchin Tanzania Nikiwa Kama Mlinzi Wa Wazir Wa Ulinz Mh Alex"



Wote Wakashtuka,japo Mac Alitambua Yule Ni Polis Lakin Katu Akujua Kama Ni Mwenye Cheo Kikubwa Namna 

Ile!



"umekuja Hapa Marekani Kufata Nini"



"kuna Mtoto Nimekuja Kumuua?"



"kwa Nini Umuue Huyo Mtoto!.."



Ghafla Machozi Yakaanza Kumtoka Zidu,ilikuwa Nilazima Atumie Mbinu Za Hali Ya Juu Kwa Kile Akiongeacho 

Kiaminiwe Ivyo Akaanza Kuongea Kwa Hisia

sana,..,



"miaka mingi nyuma nilikuwa nikiish nchin kinte na kule ndipo niliposomea jeshi ila siku mbili kabla ya 

mahafali tulimbaka kamanda mim na rafik yangu John (akadanganya Badala Ya Kijo Akamweka Baba Yake Isack 

John) ivyo mahafali Tulifukuzwa Jeshini Tukakimbilia Nchini Tanzania Huko Tulikuwa Majambaz Wakubwa Ila 

Mwenzangu John Akaja Ntapel Na Kuniunguzia Kwa Maaskar Nkafungwa Mimi Akazitaifisha Mali Zangu Zote Na 

Kuzifanya Zake Niliapa Siku Nikitoka Ntakiangamiza Kizaz Chake Chote!



Kwel Miaka Ikasonga Siku Moja Nikiwa Selo Niliitwa Nikachukuliwa Na Kupelekwa Mpaka Wizara Ya Ulinz 

Kuna Opereshen Nikaipewa ya kufa kupona na nikifanikiwa ningeungwa na jeshi na kusamehewa"



"ni opereshen gan hiyo?"



"yah alshababy waliteka ikulu ivyo ilipaswa nikawasambaratishe na kumuokoa rais nilifanikiwa ile 

operesheni!"



Ghafla Macdonald Akaachia Tabasamu!,aliwah Lisikia Lile Tukio Katu Akujua Kama Aliyewasambaratisha 

Wanamgambo Wale Ni Yule Alokuwa Mbele Yake!



"ongera Sana Kijana,"



Zidu Naye Akatabasamu!



"basi Baada Ya Kufanikiwa Nikasajiliwa Kama Mwanajeshi Wa Tz Kitu Cha Kwanza Nilichofanya Kwa Kuwa 

Nilisha Weka Kiapo kwa Agano La Damu Kuisambaratisha Ile Familia Ya Mr John Nikawachoma Moto Mim Ndiye 

Niliyewachoma,ila kwa bahati mbaya kakabakia haka katoto nakakosa kosa kukaua ila lazima kiapo na agano 

la damu nililoapa litimie lazima nikauwe hako katoto"



"nimekuelewa bwana mdogo,mim ndiye mzaz wa isack kwa sasa,nitahakikisha unafia gerezani kulinda kiapo 

chako kisitimie! ushahidi wote huu hapa! utokuwa huru wewe"



Baada Ya Maneno Yake Mac Akatoka Zake Pasina Kujua Yote Aloelezewa Kaongopewa Akuna Cha Kiapo( Agano La 

Damu) Alijua Mwenye Chuki Na Mtoto Yule Ni Zidu Pekee Pasina Kujua Mtu Yule Kamlinda Muhusika Mkuu Wa 

Mateso Ya Mtoto Yule Mheshimiwa Alex Na Zidu Alijua Mheshimiwa Yule Lazima Angemtoa Tu Na Harakati zake 

za kumtoa duniani isack zingeendelea palepale,

katu akujua mzee alex alishajaribu akashindwa na kuamua kuachana na habari zile!



kesi mahakaman ikasomwa hukumu ikatolewa



ZIDU AKAFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA KATIKA GEREZA LA GUANTANAMO



Gereza lenye mateso ya kila namna akiwa upande wa wanajeshi,kila leo ilikuwa afadhali ya jana! akataman 

kufa,mazingira ya kujiua ayakwepo!



saa,siku,wiki,miez,mwaka,miaka ikakata akisubiria atolewe akuonekana Alex Wala Familia Yake



Mwisho Wa Ubaya Aibu!



Mwisho Akaamini Yale Ndo Maisha Yake! Akakubali Ayaishi Akijuta Kumtumikia Kafiri! Majuto Ni Mjukuu!...



HUU NDO UKAWA MWISHO WA ZIDU KWA UBAYA:



SURA YA KUMI NA TANO



Gari la kifahari lilisimama katika chuo cha st Lucy akashuka Mac,mke Wake Bi Sara Na Mtoto Wao Isack



Wakawa Wakielekea Zilipo Ofisi Za Chuo Kile!



"isackiiii"



Ghafla Wote Watatu Wakashtuliwa Na Sauti Za Watu Wawili Nyuma Yao!



Ile Kugeuka Isack Akuamin Macho Yake Ni Rafik Yake Brayson Na Agnes Ndiyo Walomwita!



Ila Macho Ya Isack Yalikuwa Kwa Mery! Naye Akajikuta Akiita Sambamba Na Kumkimbilia



Mery!!!...



Akamkumbatia



Wote Wanne Wakabaki Wameshangaa

Sir Donald,bi Sara,agnes Na Bray!...



No 52



Hatimaye Izrael Wa Kibinadamu Zidu Aliyekuwa Akiisaka Roho Ya Isack Aishia Gerezani!

Mh Alex Anaacha Kumfatilia Mtoto Isack Baada Ya Kuona Harakati Zake Zile Zingemfikisha Pabaya!

Katika Chuo Cha Lucy Collage Watoto Wanne Walopotezana Kwa Muda Mrefu Wamekutana



Ni Brayson Mtoto Wa Rais Max,mtoto Aliyewah Kuwa Rafiki Mkubwa Wa Isack Ila Akashawishiwa Na Mwalimu 

Gibson Kumwekea Vitu Vya Wiz Katika Begi Lake Kwakosa Ilo Isack Akafukuzwa Shule!



Pia Yupo Agnes Mtoto Alowah Mdharau Kipindi Akiishi Kwa Baba Yake Mzee Alex Na Wa Mwisho Ni Mery Bint 

Pekee Aloamua Kuyapigania Maisha Yake Kumsaidia Katikap Ya Pori



ila wakaja tenganishwa wakiwa pamoja hospitalini na leo kwa mara nyingine isack anamwona mery anajikuta 

furaha zikimkamata,akashindwa kuzizuhia kwenda kukimbia kumkumbatia...



wote wakabaki wamepigwa na butwaa twende pamoja kujua nini kilichoendelea!



NA HII NI SEHEMU YA 52



Katu akujua kuwa yule si Mery Wake,mery Wake Alikufa Pale Zidu Mwenye Roho Ya Kikatili Aliposhika 

Kichwa Cha Binti Yule Hospitalini Na Kukigongesha Kwa Nguvu Kwenye Kitanda

Mery Akapoteza Fahamu,alipozinduka Alikuwa Mery Mpya,mery Asiejua A Wala E,ba Wala Be



Mery Alopoteza Kumbukumbu Na Kuanza Upya,mery Asiyemtambua Wala Kumkumbuka Mery Akamtoa Kifuani Mwake 

Na Kumsukuma!



"heeee we kaka vipi unanikumbatia kumbatia hapa unanijua?!"



watu wote walokuwepo maeneo yale wakaangua kicheko,



Isack Aibu Ikamvaa!,alipowa Angalia Kina Bray Walibaki Wakimcheka Tu!



"Isack umewafananisha bwana achana nao twende zetu ofisini"



Baada Ya Kuona Isack Anazidi Kuumbuka Mac Akamwambia Isack Kwa Unyonge Akiacha Nyuma Vicheko Akasonga 

Kumfata Mzaz Wake Yule!



"tumemkomesha Sisi Tumemuita Anamshobokea Mwingine Teh Teh Teh"



Bray Alicheka Kwa Dharau Akimnong'oneza Janeth!



"kwani Yule Ni Nani Mbona Mimi Simjui?"



Mery Aliongea Kwa Wasiwasi Akionekana Wazi Kumshangaa Isack



"sisi Wenyewe Atumjui Dada Atakuwa Kakufananisha Tu"



Agnes Akiongea Wote Wakacheka,



Kitendo Cha Kuchekwa Kilimtia Aibu Isack Mbele Ya Wanafunz Wengi,kuaibika Kwa Isack Kukamfanya Agnes na 

mwenzak bray wauchune vilevile kuwa awamjui laiti kama wangesema wanamjua aibu ile ingewala mpaka wao!



"dah wanafanana isee binadamu wawili wawili yule siyo kwanza yule maskini,awez soma shule kama hii baba 

yake ni John Na Siyo Mzungu!...Ila Kama Ndo Ivyo Kamjuaje Mery?!



Wawili Wale Bray Na Agnes Waliendelea Kujadili Pasina Kumshirikisha Mery



Mwisho Wakapanga Waulizie Habari Za Mtoto Yule Kwa Wazaz Wao Tanzania! Ila Kwa Muda Huo Walikubaliana 

Kumtenga Na Kutoshirikiana Naye Mpaka Aibu Ile Ipite!



Kwa Upande Wa Isack Baada Ya Kuandikishwa Jina Akaoneshwa Litakalokuwa Darasa Lake,..



Akaoneshwa Bweni Lake,mwisho Akaagana Na Baba Yake Akiwa Kamwachia Ela Ya Kutosha!



Kwa Kuwa Shuleni Pale Apakuruhusiwa Simu Baba Yake Alimuhaidi Kuja Kumtembelea Mwisho Wa Mwezi Kule 

Awakuruhusiwa Kutoka Mpaka Likizo!



Ivyo Wazazi Walimuachia Ela Ya Kutosha!



Alex Akaelekea Zake Darasani



Ile Kuingia Tu Wanafunzi Wote Wakaangua Kicheko! Mpaka Mwalimu Mwenyewe Akashangaa!



"haya Mnacheka Nini?"



Mwalimu Aliuliza Macho Yake



yakimkagua Isack pengine angeona kile kilichowachekesha wanafunzi ila akuona!



wanafunzi wakaacha kucheka kwa uoga!



"Brayson ukikaa hapo na Mery ni makelele haya toka hapo kakae na agnes yupo peke yake pale haya we 

mtoto kakae pale kwa Mery"



watoto wakaangua kicheko tena!,Isack akabaki kaganda!



"akaah mwalimu mi staki kukaa naye!"

Mery Akaja Juu Kitendo Kilichofanya Wanafunzi Waendelee Kucheka



'Mery kawaje,nimemkosea nini mimi?,mbona ananchukia,alafu Agnes na Bray mbona kama wanantenga!,kwanza 

wamenikana kunijua ninin kina choendelea Mungu wangu namkosi gani mimi!"

mawazo yale yakapita katika kichwa cha Isack,ghafla Akashtuliwa Na Sauti Ya Mwalimu



"kwa Nin Utaki Kukaa Naye Kwanza Tangu Lini Ukaleta Ubishani Na Mwalimu Haya We Mtoto Kakae Pale"



Isack Akachepuka Mpaka Katika Dawati Alilokaa Mery Akajikalisha!



"mambo Mery?"



Akampa Salamu



"mfyuuu" Badala Ya Kuitika Mery Akamsonya Na Kuangalia Zake Pembeni,Isack wala akujal akaangalia mbele 

alipo mwalimu wake



"ok,mgeni jitambulishe niwap unatoka jina lako nk"



"kwa jina naitwa Isack!"



Brayson na Agnes wakaangaliana kwa mshangao!



NIKUELEWESHE KIDOGO HAPA NDUGU MSOMAJI



Ni kuwa mpaka muda ule Agnes Na Mwenzake Brayson Awakuwa Na Uhakika Kuwa Yule Ni Isack yule 

chokoraa,akili nyingine iliwatuma ndiye kutokana na sura kufanana naye kumtambua Mery ila akil nyingine 

iliwatuma siye kutokana na maisha alokuwa akiishi Tanzania,



ndo maana wakawa wanataka kuakikisha kwa wazazi wao kwamba ndiye siye?!



sasa Isack Alipoambiwa Ajitambulishe Wakawa Makini Kusikiliza Utambulisho Wake Isack Kutaja Jina Lake 

Isack Kukawapa Mshangao Na Kujua Ndiyo Nin?!

Ila Walijikuta Mioyoni Mwao Tu Wakitaman Awe Siye!



"ok! Isack Nan Na Unatokea Wapi Na Lipi Hasa Lengo Lako La Kutaka Kusomea Sheria Ikiwewo Uakimu?!"



"kwa Jina Naitwa Isack Macdonald..."



"mhuuu!" Janeth Na Bray Kwa



pamoja walijikuta wakifurahia jibu lile japo awakuliamini moja kwa moja!



"dah dunia ina mambo watu wafanana hadi majina?!"



Bray akaongea kwa kibur



"si ndo hapo"



Agnes naye akajibu



"huyu jamaa nisipokuwa nae makini atanchukulia mchumba angu aisee"



"loooh wewe Mery Mchumba Ako?!"



Agnes Akauliza Kwa Mshangao



"sasa Kwani Wewe Ujui?!"



"Wewe Bray Una Nin Lakin Uchok Kupiga Kelele Kakae Pale Kwa Alice,haya Chris Njoo Kaa Hapa Na Agnes"



Mwalimu Baada Ya Kuwaona Wanazidi Kunong'ona Akawatenganisha Tena!

Masomo Yakaendelea Kama Kawaida!



***



BWENINI



Zikiwa Zimebakia Dakika Kumi Vipindi Viishe,Bray alokuwa kiongoz pale chuoni tena kiongoz mkuu akatoka 

kwenda kufungua ma bweni,

baada ya kukamilisha akafungua bweni lao,akaingia



akaliangalia begi la Isack kwa kejeli akapiga hatua kulifata akafungua na kutoa nguo zote akaanza 

kuzichana chana na wembe,fedha zote akabeba



'karibu chuoni isack'



akanong'ona akirudisha zile nguo kwenye begi tena bila kuzikunja akafunga begi akapanda zake juu ya 

kitanda!



taratibu wanafunz wakaanza kuingia bwenini!



isack akaliendea begi lake maskini,akalifungua,akayatoa macho ya mshangao

ghafla akawa akizitoa zile nguo huku akizishangaa azikufaa kuzivaa tena alizichana upande

wa makalion,mashati nyuma ya mgongo!



isack akaanza lia

ela zangu,nguo zangu



watoto ndani ya bwalo lile wakazidi tu kumcheka!



"we mtoto wa mama unalialia nini,acha kulia kishoga yapaswa udeki bweni ivyooo wiki nzima hii dekio 

utoe nguo yako moja,kingine,kila mtu atoe nguo zake chafu huyu mgeni afue!"

Bray akaongea kwa kiburi,



Isack Akamgeukia Akiwa Na Hasira! Macho Yamemuwiva Mekunduuu!



"inatosha Bray! Hivi Wewe Ndo Yule Bray Rafiki Yangu Kipenzi Uliyekuwa Ukinipa Moyo Kule Gulioni?"



Bray Akashtuka,akaruka Toka Juu Kabisa Double Deka Kitanda Cha Sita Mpaka Chini



"Isack ni wewe?!"



akauliza pasina kuamini,



"ndo mimi Bray Niliskia Baba Yako Kawa Raisi"



Isack Ikawa Sasa Kama Kamkumbusha Bray Kuwa ile Siyo Leval Yake Tena Akacheka Kwa Majivuni



"ha ha ha ha kwa sasa baba yangu ndo rais na ndo maana nipo katika chuo kama ichi tunachosoma watoto wa 

matajiri sasa wewe maskini umefata nini hapa na umepata mfadhili gani alokuleta? nijuze best"



Bray akazidi kuongea kwa majivuni,Isack akawa kimya Bray Akamsogezea Kichwa Isack Akawa Anamnong'oneza 

Watoto Wengine Awakusikia Nin Isack Alichoambiwa



"mambo Ya Tz,tuya Ache Tz Huku Ni U,S,A Na Mim Si Yule Bray Rafik Yako Kwa Sasa Mimi Ni Bray Mwingine 

Cha Mwisho Achana na Mery,utaishi vizuri apa chuo si umeona hata akujui yule ni mchumba angu mimi! 

nadhan umenielewa ok! mwisho...



apo ndipo alipopaza sauti watu wote wakasikia



..,mimi ndiyo head boy wa chuo hiki ivyo nisemacho ni sheria akipingwi,vaa ovar rol hil mpaka 

utakapopata nguo miez nane ni ming et sijui utapat wap ela ya kula,chukua nguo hapo kafue"



"sabuni sasa!"



"khaaa kafulie na sabuni yako asee"



Isack Akuwa Na Jinsi Akavaa Ovar Rol Lake Nguo Zake Azikufaa Kuvaliwa Tena!

Akatoka Tayar Kwenda Kufua!



*dah Isack Ataishije Katk Chuo Icho Pasina Ela,pasina Mavazi? Nin Hatma Ya Maisha Yake?*







Maisha Ya Isack Bado Yanaandamwa Na Mikosi,

Anawasili Chuoni Huko Anakutana Na Watu Alokuwa Akiwafahamu Hususan Rafiki Yake Kipenz Bray Tofaut Na 

Mategemeo Yake Wanamgeuka,na Kujifanya Awamjui Mbaya Zaidi Bray Anamwibia Pesa Zake Zote Za Matumizi Na 

Mbaya mbovu Zaidi Anamchania Chania Nguo Zake Zote Na Kiwembe Amri Anaitoa kama head boy Afue Nguo 

Chafu za wanabweni wote Inamlazimu Isack Kutimiza Jambo Lile Akiwa Tena Anatumia Sabuni Yake!

Je Nin Kiliendelea?!



NA HII NI SEHEMU YA HAMSINI NA TATU



Isack akatoa mche wa sabuni katika begi lake akakata kipande cha kutosha,akachukua ndoo kubwa na kuweka 

nguo za watoto wale akatoka nazo nje tayari kuzifua!



akili sasa ilianza kukomaa miaka 18 si haba...



Kozi ya pale chuoni ilikuwa ni ya miaka mitatu hivyo angetoka pale akiwa na miaka ishirini na ikiwa 

angefaulu vizur ingempasa aendelee mbele!



mawazo yake akayaweka katika masomo!



'elimu pekea ndiyo ilikuwa mkomboz wake'



aliendelea kufua zile nguo mpaka mkono ukawa ukimuuma ila hatimaye alimaliza akaanika akaelekea 

chumbani alipowakuta wanadom wenzake wakiwa wanakula biskut,na vikopo vya juisi pamoja na matunda 

takataka wakawa wakizitupa chini,walipomuona tu Wakaanza Kumcheka



Isack Akaenda Kwenye Kitanda Chake Akakaa,akimezea Mate



laiti kama angekuwa na ela zake naye angeenda nunua ila si alishaibiwa!



"ndo shida ya kusoma na maskini asiye na hela siye tunakula yeye anatushangaa mambo gani haya khaaa"



Bray Akaongea Kwa Kiburi Watoto Wote Waka angua kicheko,ghafla Kengele Ya Mlango Wao Ikagongwa,mlango 

Ukafunguliwa Akaingia Kijana Wa Kizungu Na Kibaiskel Cha Kusukuma Juu Kikiwa Na Vibakuli Kadhaa Vya 

chakula



Chuo Kile Wakat Wa Chakula Wahudumu Walikuwa Na Taratibu Za Kuwapelekea Vyakula Wanafunzi Vyumbani 

Mwao!



Yule Muhudumu Akavipanga Vyakula Vile Pale Mezani Na Kutoka Zake!



Tumbo Lilimnguruma Isack Ikiwa ni Dalili Ya Njaa,kwa Kuwa Yeye Ali Kuwa na njaa alichukua bakuli moja 

tayari kwa kula ila kina Bray Wakamnyang'anya Na Kumwambia Shulen Kwao Awapo Vile,kabla Ya Kula Ni 

Lazima Waombe Kwa Pamoja Lakin Yeye Kaenda Kinyume! Kwa Kosa Lile Isack Akupaswa Kula kama adhabu



Bray Akamnyang'anya Kile Chakula Na Kukigawa Katika Kila Sahani!


ITAENDELEA

Simulizi : Kiapo (Agano La Damu) (2) 

Sehemu Ya Tano (5)



Baada Ya Kukamilisha Akamtupia Sahani Apo Chini



"nadhan Siku Nyingine Utajirekebisha Sisi Tuombeni Tuleni"



Watoto Wote Wakafumba Macho Na Kuanza Kukiombeba Chakula



Wakati Wakiwa Katika Maombi Ghafla Wazo Likamjia Isack Achukue Bakuli Moja Na Kuanza Kula Mpaka Sala 

iishe Lazma Angekuw Amemaliza,haraka Akaokota Sahan Na Kuanza Kula Akikata Matonge Makubwa makubwa!



Mpaka Bray Anaitimisha alishapiga Nusu ya bakuli ile



watu wote walitumbua macho kumshangaa Isack



Ndo Kwanza Pasina Kujal Mtoto Akawa Akikata Matonge na kuyatupia mdomon



Bray Akawah Kumnyang'anya Kile Chakula Na Kukimwaga Chini,

"adhabu Yako Utadek Hapa Chini Nyie Chukuen Vyakula Endeleen Kula Mi Ntaendelea Kula Hiki 

Nlichokichukua Restraunt!



Bray Aliongea Watoto Wale Wakachukua Vile Vyakula Na Kuendelea Kula



Baada ya vijana wale kumaliza kula,wakamtaka Isack Achukue Ndoo Iliyomo Mule Bwenin Akachote 

Maji,ilikuw Ni Ndoo Kubwa Ya Lita 20 Isack Akuweza Kupinga Mtoto Wa Watu Akaenda Chota Maji Akaambiwa 

Aoshe Vile Vyombo Wakati Aikuwa Kaz Ya Mwanafunz Yeyote pale chuoni zaidi ya wahudumu ila wenyewe 

walimpa kazi ile Isack kumkomoa



"wiki Hii Yote Isack Utaosha Vyombo Na Kudeki Wiki Ingine Zamu Inaenda Kwa Mtu Mwingine Sawa?"



Isack Akujibu Kitu Akasuuza Suuza Vyombo Vile Akamaliza,akapitisha Dekio Mule Ndani Alipoitimisha Sasa 

Ilikuwa Ni Muda Wa Kwenda Michezoni!



Wakaongozana Mpaka Uwanjani!

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog