Search This Blog

Thursday 29 December 2022

KUFA TU HAKUNA NAMNA (2) - 1

 

 Simulizi : Kufa Tu Hakuna Namna (2)

Sehemu Ya Kwanza (1)

 


IMEANDIKWA NA : ZUBERI MARUMA


********************************************************************************


Simulizi : Kufa Tu  Hakuna Namna (2)


Sehemu Ya Kwanza (1)




Tuliishia...




Akumjua Madam 'S' Mwanamama machachari katika kombi ya mapigano na mkuu wa usalama wa taifa,akubahatika kumuona kabla yeye aliwajua wale vijana watano ambao Katarina aliwamaliza msituni....




Vijana Wale walipo mkamata walimtesa wakimlazimisha aeleze ni nani anayemtuma, wakatesa ila Zena akufumbua mdomo wake mateso yalipozidi akapoteza fahamu,hapo ndipo madam 's' alipokuja kumtazama sura yake akiwa hana fahamu akatoa amri akauwawe porini msitu pande kesho yake,madam akatoka...




Ivyo Zena akumjua kabisa madam 'S' kufa kwa wale vijana saba akajihakikishia usalama wa sura yake,ndo maana hata alipopona akaamua kurejea makao makuu akijua yupo salama,pasina kujua madam 's' alikuwa ofisini tena kashika picha yake,akimtambulisha kama mtu hatari kwa usalama wa taifa,




"mkuu anamgeni!?"




Alimuuliza Katibu Muhtas Wa Kamishna aliyekuwa bize na laptop yake,kwa kuwa dada yule alikuwa bize akawa kajisahau kwamba punde madam 's' aliingia si akatingisha kichwa kumruhusu Zena Kuingia,ZENA akausogelea mlango na kuufungua kabla ajakutana na risasi za bega,ile anageuka atoke akalambwa za mgongoni




Zena akaenda chini,




Kamishna Haruni akabaki kaduwaa,macho kayatoa akikosa neno la kuongea,




Madam sasa akawa akimsogelea Zena Pistol yake mkononi moyoni akiwa ameadhimia kwenda kummalizia palepale,




Alipofika alimnyo oshea silaha kwenye kichwa kabla ajamtwanga na kumsambaratisha ubongo kamishna akapayuka...




"hapana,unaenda kinyume na haki na sheria,mahakama ina kazi gani?,hata magaidi pia wanahukumiwa mahakamani,madam ukimuhua huyo mi ntakuwa shahidi namba moja mahakaman kukushtaki"




Madam 's' akasitisha zoezi lake akamgeukia kamishna,akiwa kamkata jicho kali akamwambia...




"adui wa taifa hukumu yake ni hapa hapa aina aja ya mahakama kulinusuru taifa huyu binti ni mbaya zaidi ya ufikiriavyo huyu ndo 'ZK' atoaye siri za taifa lazma afe..."




"hapana,hapa upo ofisini kwangu,pia huyu ni mtumishi wangu kusanya ushahidi tutampandisha mahakamani jua hapa upo katika mamlaka yangu...




Palepale Kamishna Haruna akachukua simu na kumtwangia katibu muhtas wake,"namuhitaji inspekta Nurdin,na baadhi ya maaskari ofisin kwangu"




"sawa mkuu!"




Punde maafande hao wakaingia,wakampigia saluti mkuu wao wakijaribu kuzuhia mishangao katika nyuso zao,




"Nurdin,mpigeni Pingu koplo Zena mumuwaishe muhimbili wewe utahakikisha anatibiwa mpaka kupona akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi..."




"hapana atalindwa na kijana wangu"




Madam 'S' akarukia,insp Nurdin akasita kabla ajachangamshwa na amri 'two'




"fata amri ya mkuu wako kijana mtu huyo akifa utawajibika"




Palepale Insp Nurdin na wenzake wakachangamka kumtia pingu ZENA na kumtoa kumuwaisha hosptal,Madam 's' naye akaongoza kufata msafara




'hakikisha madam amdhuru huyo binti'




Wakiwa Kwenye gari insp Nurdin akasoma meseji kutoka kwa kamishna wake,akamjibu 'sawa mkuu'




*********




Kamishna Haruna Gozigozi hakiwa kabakia ofisini kwake mwenyewe baada ya vurumai lile sasa akawa akiwaza peke yake,




'je alichofanya ni sahihi?!,'




Akakumbuka Simu alopigiwa na Raisi Kuombewa Zena kufanya kazi pale...




"ni binti yangu huyo kafukuzwa jeshini si vibaya kumweka katika idara yako aanze na ukoplo,mlinde tafadhali mkuu"




"sawa muheshimiwa Rais,nitampokea,na ntamlinda pia!"




'NITAMLINDA PIA' Akakumbuka hiyo ahadi gozigozi alokwishaga kumuhaidi muheshimiwa Raisi,kwa Kipindi Kile hakutaka kujibebesha mzigo kuwaza ni ulinzi gani Rais alo maanisha Zena apewe?,lakin kwa siku hii aliutambua uo ulinzi,akajikuta akitabasamu kwa kufanikiwa kutimiza ahadi ya kumlinda aliyo muahidi muheshimiwa Asamoye,




Je ni kipi sasa kifatie?!




kumjulisha Rais,




Ndio,




kumjulisha Rais kila kitu kilichotokea mpaka z,ajue Rais atamjibu nini,palepale akampandia muheshiwa hewani




Akamsimulia kila kitu,toka madam 's' aje amuulizie Zena sifa chafu alizozitoa juu ya binti huyo ghafla Zena alipotokea madam akamtandika risasi naye kuingilia!




"vizuri sana,umefanya vizur mzee yule ni mtu wangu tutaongea vizuri wacha niongee na vijana wangu kwanza umesema kapelekwa muhimbili eeh"




"ndio muheshimiwa,ok kuna vijana wangu ntawapatuma waende pale kwa ajil ya ulinzi wakifika pale ntakushtua uwatoe hao wako"




"sawa muheshimiwa,"




"ni kwa usalama wa taifa kamishna iwe siri yako"




"sawa mkuu"




Palepale simu ikakata,




Kamishna akawa kashapata picha mchezo mzima ulivyo,kuna vita kali chini kwa chini...




Kwa upande wa Asamoye palepale akampigia mwanaye kumuhitaji arejee nyumbani (ikulu) haraka,




Daniel kufika,Rais akaingia garin wakaondoka...




Njiani Raisi alimsimulia kila kitu Mwanae Daniel,




Daniel akapaki gari eneo wanalofanyaga maongezi,




"Katarina pekee ndo mwenye jukumu la kumuokoa mwenzake,katarina akamlinde binti hosptal na kumtorosha pia"




"ok,mpigie basi simu aje,"




Katarina akiwa nyumbani anasaidiana na bibi kupika ghafla simu yake ikaita,kwenda kupokea ni Daniel




"njoo Uwanja wa ikulu huku nyuma kuna gari nyeusi, haraka sana nipo ndani yake,usije na gari chukua bodaboda wai haraka sana"




palepale Katarina akachomoka ndani ya dakika kumi zilizofatia alikuwa ndani ya gari ile pemben yake akiwepo Rais kwenye usukani akiwepo Daniel




Wakampa maelezo yote kila kitu kilivyotokea na kazi ilokuwa mbele yake...




Kk,akakubali Kwa moyo mweupe kwa mara nyingine tena kubeba dhima ya kwenda kumlinda na kumuokoa pia Zena palepale Dani akawasha gari kumpeleka muhimbili,




Walipofika nje ya hosptal ile wakamshusha,




Ukifika ndani huko utubeep hili hao wanaomlinda waondoke ubaki peke yako nahisi na huyo mmama sawa...




Wakati Katarina akishuka kwenye gari,gari nyingine aina ya tax ilopaki pembeni yao akashuka kijana mtanashat alivaa suti ilo mpendeza, akajongea kuelekea ndani ya hosptal ile Katarina akiwa mbele yeye nyuma,huyu si mwingine ni kidume DON G




Baada ya kufika hosptal mgonjwa akaingizwa wodini kutolewa risasi madam 'S' wakiwa nje ya wodi ile pamoja na kina insp Nurdin,akatumia muda huo kumwita DON alitaka huyu amwache akae pale badala yake,kwa kisingizio cha kumlinda,ila kazi yake nyingine ni kuakikisha ana muua...




kasheshe....




Kamishna Haruna Gozigozi, anafanikiwa kumzuhia Madam 'S' mmama machachari kumuua Zena,na Kufanikiwa kuwaagiza vijana wake kumuhaisha hospitalini,




Madam naye habaki nyuma akiwa ameapa kumwangamiza kwa namna yeyote ile binti yule,




Wakiwa hospitalin Madam anamuita kijana wake Don G,akimpa kazi ya kumlinda Zena,na kumwangamiza pia,huku Rais Asamoye akisaidiana na mwanae Daniel wakimtuma mwanadada machachari Katarina kumlinda na ikiwezekana kumtorosha Zena hosptalin pale je upande upi utashinda kati ya upande wa usalama wa taifa one unaosimamiwa na madam 'S' kumlinda Rais au Usalama Wa taifa two uliyoko chini ya muheshimiwa Rais Asamoye wenye madhumuni ya kuyaanika machafu yote ya waziri mkuu




twendelee!...




Katarina alifika pale mapokezi baada ya kuuliza uliza akaelekezwa moja kwa moja mpaka nje ya wodi ambapo aliwakuta kina inspekta Nurdin na madam 'S' nje ya wodi ile ya 'icu' akawasalimia wakati huo akimjulisha Daniel kwamba ameshafika,Daniel akamjulisha kamishna Haruna,ambaye alimpigia simu Nurdin na kuwaruhusu tu waondoke ulinzi ungebakia chini ya mwanadada yule,




Madam 'S' naye akamwacha Don G' moyon mwake akijua binti alokuja katarina ni polisi wa kawaida kutoka makao makuu mwenye mafunzo ya upolisi ccp




"G,hakikisha unakaa na huyu afande wa makao makuu kumlinda huyo mwalifu asitoroke,fanya kazi kama nilivyokwambia kila kitu ntakujulisha sawa?"




"Sawa mkuu"




Don alijibu akitabasamu, Madam akashindwa jizuhia kumkata jicho kali Katarina kisha akaelekea zake kwenye lift kushuka chini...




Nje ya Icu wakabaki watu wawili,watu hatari,Don G yeye akiwa na lengo la kuangamiza huku Komando Katarina 'kk' akiwa na nia ya kulinda,kwa dakika kadhaa hakuna alomsemesha mwenzake,kila mtu akiwa na mawazo yake kichwani,Don akitamani mlango ukifunguliwa daktari akija aje na habari mbaya,




kifo!...




Alitamani kusikia habari ya kifo tu katika masikio yake,bila shaka kwake hiyo ndo habari nzuri...




Punde mlango ukafunguliwa, daktari akatoka,wote wawili Kk na Don G wakainuka kumfata daktari




"Vipi daktari mgonjwa anaendeleaje?"




Katarina akahoji,




Daktari akatabasamu kidogo, tabasamu la matumaini...




"alipigwa risasi tano tatu mgongoni mbili kifuani tumefanikiwa kuzitoa zote na kwa sasa anaendelea vizuri punde atatolewa icu kupelekwa wodi ya kawaida"




Katarina akatabasamu,ila kwa upande wa Don alinuna, akufurahia ripoti ile




'Utakufa tu hakuna namna!'




Akawaza punde kweli kitanda kikatolewa icu,Zena akiwa juu yake pasina ufahamu...




Bado alikuwa akitumia mashine ya kupumulia hewa ya oxygen,dripu ya dawa na damu zikitiririka katika mwili wake,




Wakawafata madaktari wale nyuma mpaka katika wodi moja




"samahani daktari ningependa mumpe privet room chenye vitanda vitatu"




Katarina aliomba kabla Don ajadakia,kwa kuongezea...




"na kingine ningeomba nimpige pingu kwani huyu ni mshtakiwa"




"hapana kwa saivi hali yake bado si nzuri ni mapema sana kupigwa pingu akipata uhafueni zaidi mtampiga wacha tukashughulikie kwanza chumba"




Daktar akajibu huku akiondoka, Katarina akamkata jicho Don akamnong'oneza kwa sauti


ya taratibu




"nikijana handsome, mtanashati mwenye sura ya upole ila unaonekana una roho ya tofauti roho mbaya,chafu na pia waonekana katili..."




"binti,huyo binti ni adui wa taifa jua ilo ni hatari hata zaidi ya ufikiriavyo ingepaswa auwawe na si kumchunga chunga ni hatari kwa taifa tambua hilo binti"




Don naye akajibu kwa sauti ya taratibu,kama Katarina aliyo iongelea Katarina akujibu kitu,japo alijua pale pana kazi,tena kazi kubwa sana...




Ukimya ukatawala baina yao ukimya ulompa wasaha kila mmoja kuwaza lake kichwani




ZIDU,




Jina la mtu huyo likamjia katarina kichwani,ilikuwa vigumu kumfuta




Akalitafuta Jina lile katika simu yake na kumpigia simu ikaitaaa,mpaka ikakata, akapiga tena,hali ikawa ile ile,tena na tena,hali ikawa bado ni ile ile,




Katarina akakunja Sura,Don kwa pembeni alikuwa akimpimia,mabadiliko alokuwa akiyaonesha...




Katarina alijua aliye ondoka na furaha yake ni mtu mmoja tu!




Suzan,




Katarina akakumbuka jinsi alivyo mpenda binti yule,na kumchukulia kama mdogo wake,kazi akumwachia afanye mwenyewe alikuwa akimsaidia,pia akakumbuka kipindi mumewe alipobadilika akawa akitoka na Salome, yeye ndiyo alikuwa mstari wa mbele kumtia moyo,kumpa faraja na nguvu pia...




Leo hii naye anakuwa mwiba tena wenye ncha kali kuuchoma moyo wake!




je ntakuwa nafanya kosa nikimuua?!,nimemtahadharisha lakini ajataka kunisikia, bora na mwenzake Salome alinisikia akaukimbia mji,huyu sito mwacha




Sitomwacha nasema




*NITAMUUA,NITAMUUA TENA KWA MIKONO YANGU SINA JINSI SUZAN LAZIMA AFE'*




'Mamy unawaza nini?!'




Ghafla Katarina akashtushwa na sauti nzito ya Don,akajishtukia na kujichekesha macho yake yakatua katika kitanda alicholala Zena akajikuta akiwaza huku macho yake yakiwa yamenata usoni kwa binti huyo...




'pona mamaa,pona tutoke huku nikamfundishe adabu huyu Suzan'




**************




Madam 'S' akiwa ofisini kwake, kichwani alikuwa na mawazo sana akiwaza hasa ni nani aliyekuwa nyuma ya Zena,akakumbuka Richard Mombi kijana mmoja wapo aliyepona kati ya vijana wake watano na kukutwa ndani ya chumba kimoja kijijini kule,akakumbuka pia maelezo yake alieleza kwamba wakiwa msitu mabwepande walivamiwa na watu walovaa mavazi ya ninja wakawaua wenzake kwa risasi naye kumchukua kama mateka,




Madam 'S' alijua kwa nini Mombi Akuuwawa ni hili afikishe habari ile kwamba watu wale walihitaji uhuru,




Je ni uhuru gani sasa walouhitaji? na kuumaanisha?!




Je ni uhuru wa vyombo vya habari?,au uhuru wa kichama!


ITAENDELEA


  


Simulizi : Kufa Tu  Hakuna Namna (2)


Sehemu Ya Pili (2)






Je watu wale ni waasi wa serikali?,au wapo chama pinzani ccm!




Madam 'S' akupata jibu, akakumbuka mateso vijana wake kabla awajauwawa,walo mpa Zena lakin hakusema kitu wala walo mtuma,




Leo hii anakuja kugundua Zena tofauti na uwaandishi wa habari wa kujificha kwa mask kama 'ZK' pia ni afisa wa polisi tena wa cheo cha chini kabisa nyota moja koplo!




Madam 'S' akazidi kuwaza,jinsi kamishna makao makuu pale alipokuwa mkali pale alipohitaji kumwangamiza 'ZK' pale ofisini,




Jinsi alivyoaminika na kuwa mkali!,au kamishna anaujua huu mchongo?!




'lazima kamishna hatakuwa anajua chochote na kwa maana hiyo lazima ashughulike na, kamishna!,lazima atekwe,ateswe kamishna mpaka eleze 'Zk' anatumiwa na nani!




Madam 'S' akatabasamu na kushika simu yake,akampigia mtu kumuita ofisini kwake...




Dakika chache mtu yule aliwasili,akampa kazi ile,kumteka Kamishna Kumtesa vibaya hata kwa kumkata kiungo kimoja kimoja mpaka aeleze anachojua kuhusu 'ZK' mwisho auwawe...




mtu yule akatoka akihaidi kuifanya kazi kwa ukamilifu,naye hakuwa mtu wa kushindwa!...










Madam 'S' anamtilia shaka kamishna Haruni Gozigozi baada ya kumzuia kumuua Zena kwamba anamjua Zena waliyoko nyuma yake ana amua kumpigia simu mtu wake na kumpa kazi amteke kamishna na kumtesa mpaka aeleze Zena anatumwa na nani je nin kiliendelea twendelee na sehemu hii kujua kilichojiri...




Mtu yule aliingia ndani ya gari lake na kutoka eneo lile la ofisi ya waziri mkuu, akaelekea moja kwa moja mpaka nyumbani kwake,akawa akivuta muda kusudi akaitende kazi aloipewa...




Mtu huyu hakuwa mwingine zaidi ya Richard Mombi,ni Kijana aliyetokea kuaminiwa na madam 's' pasina kutambua kuwa kijana huyu pia anatumika na raisi ofisi ya waziri mkuu akiwa kapachikwa tu ,hakiwa nyumbani kwake sebuleni kakaa aliona bora amjulishe Daniel Juu ya kazi aliyopewa,




"mkuu madam kanipa kazi ya kumteka kamishna na kumtesa mpaka aeleze chochote anachojua kuhusu Zena"




"ahaaa,vizuri kamishna yupo upande wetu na kama unavyojua yeye ndo alimzuia yule malaya kumuua Zena lazima tucheze mpango,we jifanye unamteka tutamjulisha kila kitu ila tutapanga maaskari na lazima ukamatwe najua atakutoa tu"




"fact"




"we kwani umepangaje kumteka?"




"saiv nipo home mkuu navuta vuta muda jioni nielekee makao makuu nikamchukue kimyakimya"




"unatumia gari gani,"




"la makao makuu,madam kaniambia nitumie gari la ofisi,"




"vizuri,je unajua ni kwa nin kakwambia utumie gari la ofisi ya wazir mkuu"




"hapana"




"basi ni ivi,kila gari la serikali ofisi ya waziri mkuu na ya ikulu yote kategesha kamera,pamoja na vinasa sauti kwa siri sana,ivyo ukimteka kamishna ukamwingiza ndani ya gari ataona kila kitu kinachoendelea,hiyo kwa upande wetu ni vizuri kwa kuwa ataona wakati ukimwingiza kwenye gari ukiwa njiani ukikimbizwa mpaka utakapokamatwa yeye ataona kila kitu huu mchezo kwetu ni mdogo tu"




"ha ha ha Daniel We hatari!"




"kauanzisha mwenyewe wacha tumchezeshe"




Daniel akaendelea kumuabarisha Richard Mombi,




"ok,wacha niwasiliane na kamishna ni mpange kusudi naye awapange vijana wake?"




"ok mkuu!"




Daniel akakata simu,muda ule ule akamtwangia Kamishna...




*********************




MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI




OFISI YA KAMISHINA




4:20 PM




Ni kutokana na kazi za asubuhi mpaka mchana kutwa ndizo zilizomchosha Kamishna,




Kama kawaida meza yake aikukosa mafahili mengi yalomchosha akili yake na kumfanya asinzie pale kwenye kiti alichokalia,




ngriiii! ngriiii ngriiii




Ghafla akashtushwa na sauti ya simu haraka akapiga mwayo mkubwa kabla ya kuipokea...




"ndiyo Dani nambie!"




"madam kacharuka kajua kuna kitu unakijua kuhusu 'ZK' ivyo kamtuma mtu wake ambaye pia ni mtu wetu aje akuteke akutese umweleze kuhusu 'Zk' unamtambuaje,na anatumiwa na akinanani mwisho uwawe"




"heee" kamishna akashtuka,binafsi akudhani wala hata kufikiri kwamba mambo yangefika huko kutesana na kuuana,akufikiria katu!




Hapo ndipo alipoanza kuiona hatari mbele ya macho yake,kuingia mgogoro na usalama wa taifa aliijua hatari ilokuwa mbele yake,sasa maisha yake yalikuwa hatarini akajikuta akianza kutetemeka na kujikuta akijuta kwa kujiingiza kumtetea Zena,bora tu angemwacha madam 'S' afanye atakacho




"ivyo lengo la kukupigia simu ni kuendeleza gemu washtue vijana wako wakae 'stend bay' hapo nje ukiingizwa tu kwenye gari utapiga yowe moja kwa nje maaskar ulowapandikiza nje watakufatilia huyu alokuteka kumbuka ni mtu wetu ukiwa ndani ya gari yake kila kitu mtakachokuwa mnafanya madam 's' atakuwa anaona ivyo jamaa atajitahidi kadri ya uwezo wake wote kuwashinda maaskari ila mwisho atakamatwa wewe utaendelea kuwa huru ok...




Kamishna akajikuta akitabasamu, faraja ikaanza kujijenga upya katika moyo wake,

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog