Simulizi : Kiapo (Agano La Damu)
Sehemu Ya Kwanza (1)
MEANDIKWA NA : ZUBERI MARUMA
********************************************************************************
Simulizi : Kiapo (Agano La Damu)
Sehemu Ya Kwanza (1)
UTANGULIZI
Kwanza nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema na kuniwezesha kuandaa tena riwaya hii ambayo bila shaka itakufunza mengi na kukuburudisha pia!
Shukran zangu za pili nizilete kwenu wasomaji wangu kwa sapoti yenu...
TUANZE SASA.....
Ilikuwa ni familia moja wapo ya kimasikini katika familia nyingi zilizopo katika kijiji kile,kula yao ilikuwa ya tabu malazi yao na hata makazi yao pia.
Waliishi katika nyumba ya udongo tena ilomea upande mmoja na kutishia kuanguka wakati wowote dua yao kubwa ni kumuomba Mungu mvua kubwa isinyeshe kwa maana uwezekano wa kupona kwao ulikuwa mdogo pindi kama mvua ingenyesha
Pembeni ya nyumba hiyo ya Mzee John kulikuwa na nyumba moja ya kifahari wenyeji wa nyumba hiyo ni wazi awakutambua shida ni kitu gani hii ilikuwa ni nyumba ya Mzee Alex alokuwa diwani wa kijiji kile
Mzee jeuri mwenye dharau na tamaa ya kiwango cha juu alijilimbikizia Mali za serikali na wala akujali maisha waloishi wananchi wake,alijaliwa watoto wawili wa kike ambaye mmoja aliitwa Mery huyu alikuwa kidato cha Tatu katika shule ya kimataifa na wa pili aliitwa Agnes huyu alikuwa darasa la saba palepale kijijini yeye alikataa kukaa mbali na wazazi wake na kwa kuwa alikuwa kifunga mimba wao wazazi wao waliridhika kuishi naye
Agnes alikuwa ni binti mwenye dharau sana na dharau zake alizionesha wazi hata kwa majirani zake!,kutokana na ufukara ulowazunguka ilimlazimu Isack kipindi cha likizo awe anaenda katika jumba lile na kufanya kazi kujipatia ada na ela ya matumizi!
Huko alikutana na Agnes alokuwa mdogo kwake alomsakama si kwamba wazazi wa Aggy awakuona la hasha hao waliona ni sawa
Moyo wa uvumilivu aloumbwa nao Isack ulimjenga kujiamini na kuona ni sawa tu na ni jambo la kawaida kwa fukara kudharauliwa maisha ya kasonga!,na likizo ile ikaisha Isack akarudi shuleni!
Siku hiyo moyo wake ulikuwa mgumu furaha ilienda kando huzuni ilitawala katika fikra zake akujua kwa nini,hisia za machozi zilimlenga lenga usoni hata alichofundishwaakikuingia,alikuwa jambo la kawaida kwa Isack alijua lazima kuna kitu!
Jioni alitembea haraka haraka kuwahi nyumbani moyoni akiwa na uchungu usiomithilika!
Kwa mbali kabla ajafika nyumbani alishtushwa na umati alouona nyumbani kwao
"Kuna nini?!"
Akawaza akiongeza mwendo na mwisho akaamua kukimbia kabisa
"Moto! Moto! Jamani motooooooo moto!"
Kadri alipokaribia kufika alisikia kelele za moto mwili ukamsisimka,mapigo ya moyo wake yakaongeza kasi ya upigaji
Akuamin kile alichokuwa akikiona katika macho yake alihis ni ndoto na muda wowote angezinduka,ila aikuwa hivyo ni kweli nyumba alokuwa akiishi ilikuwa ikiteketea kwa moto akazid kukaza mwendo huku akishindwa kujizuhia kuachia ukunga alipofika watu wakamzuhia
Wazazi wake walikuwa ndani ya nyumba ile wakipiga kelele wasaidie ni nani angekuwa na moyo wa kujitosa kusaidia?!
Wengi walibaki kujikusanya makundi makundi wakishangaa huku wengine wachache wao wakiangaika na ndoo za maji kujaribu kuuzima moto ule ambao ndo ilikuwa kama wakiuchochea
Bado sauti ya wazazi wake Isack wakiomba msaada zilisikika,na kuzidi kumtia uchungu kijana yule ambaye alikuwa bado akiwategemea wazazi wake ila majirani walizidi kumshika kumzuhia
Ila ghafla kimya kikatawala mule ndani!,hiyo ilikuwa ni tafsir mpya kwa majirani walikuwa wakijaribu kuuzima moto ule!....
Isack alilia mpaka sauti ikamkauka na ghafla Giza likamtawala mwili ukamlegea na kuporomoka chini!...
Hali ya sintofahamu ikazidi kuzagaa maeneo yale
*****
Kichwa kilikuwa kizito macho yaliona kiza akang'amua kwamba ameyafumba akajaribu kuyafumbua yakagoma
Ghafla masikio yakazibuka na kupokelewa na kelele za vilio bado hali ya sintofahamu iliendelea kumzonga
Taratibu akajaribu tena kuyafumbua macho yake safari hii akawa akifanikiwa na mwisho yakafumbuka kabisa!
Alikuwa chini,akiwa amezingirwa na umati wa watu wachache wakimpepea
"Kazinduka jamani tumpeni hewa sogeeni"
Mzee mmoja aliongea kwa furaha!,ni kipi kilichotokea bado akutambua hasa akataka kunyanyuka lau akae kitako akashindwa akabaki amelala vilevile!
Bado mayowe majina ya wazazi wake yakitajwa ilisikika! Ila akukumbuka kilichotokea ikabidi atulize mawazo afikirie kwa kina!
Kwa mbali akaanza kukumbuka toka alipotoka shule na kushughudia nyumba yao ikiteketea huku sauti za wazazi wake wakiomba msaada zikisikika
Nguvu zikamjia wasiwasi ukamvaa akajikakamua na kujinyanyua akakaa kitako ila alipotupa macho yake mbele alichokiona kilimrudisha chini Isack akatulia tuli!....
Watu wote wakabaki wamepigwa na butwaa!...
Kijana Isack anatoka katika familia ya kimasikini,matatizo yanakuwa sehemu ya maisha yake ila ajali ilo anaelekeza nguvu zake katika masomo akijua ipo siku elimu anayoipigania itamtoa pale alipo!
Ila siku hiyo akiwa darasani ghafla anajikuta akikosa raha si hali ya kawaida anajua lazima kuna tatzo nyumbani anakaa darasani pasina furaha yoyote mpaka muda wa kuruhusiwa anaelekea nyumbani akiwa na mashaka tele!
Kila anapopiga hatua kukaribia nyumban mashaka Yale yanaongezeka na anapoingia katika mtaa wao anasta ajabu kwa mbali kuona watu wameizingira nyumba yao 'kuna nini?!' Anajiuliza ila kwa mbali anasikia sauti za motoooo moto motoooo anaamua kukimbia kabisa
Anapofika pale ahamini baada ya kuikuta nyumba yao ikiteketea tena kwa mbali akisikia sauti ya wazazi wake wakiomba msaada anapotaka kujaribu kuingia katikati ya moto ule kwenda kuwasaidia anazuiwa,watu wanaendelea kujaribu kuuzima moto pasina mafanikio
Wazazi wa Isack kule ndani wanakata tamaa ya kuokolewa na hewa inazidi kupungua wanasogeleana na kukumbatiana tayari kukipokea kifo kwani hapakuwa na namna yoyote ya kujiokoa
Isack anashindwa kuvumilia kuendelea kuona matukio Yale na ghafla anadondoka na kupoteza fahamu dakika kadhaa mbele anazinduka ila anachokiona mbele yake kinamwondosha tena fahamu kwa Mara nyingine je ni nini Isack alichokiona?!....
Na vipi wazazi wa Isack watapona katika moto ule?!....
Twende sasa
Wananchi kwa shida sana walifanikiwa kuuzima moto ule ulounguza nusu ya nyumba ile!,walipoingia ndani walistaajabu kuikuta miili ile ikiwa imekumbatiana imebadilika rangi na kuwa meusi hakika ilikuwa imeharibika vibaya!....
Kwa jinsi ilivyoungua ilikuwa ni vigumu kutambua mama ni nani na baba ni nani,wakasaidiana na kuitoa nje wakaibandua!
Kilio kikatapakaa kwa majirani wale,bado majirani wengine waliendelea kumpepea Isack na kujaribu kumpa huduma ya kwanza wengi walionekana wakimwonea huruma kijana yule ambaye kiumri alikuwa bado mdogo kwa mbali macho yakaonekana yakicheza ni Kama alikuwa akijaribu kuyafumbua wakazidisha juhudi na ghafla Isack akazinduka!....
Akuelewa alikuwa wapi!,na nini kilichotokea akajaribu kuvuta kumbukumbu Ahmad kumbukumbu zote zikarejea nguvu zikamjia akajinyanyua na kukaa kitako
Ila macho yake yakatua katika miili ilokuwa mbele yake miili ilotoa harufu ya kuungua harufu ya nyama ya kuchoma!,japo akuweza kuitambua kwa macho mwili ulimlegea Giza likamtawala muda ule ule akapoteza fahamu tena!
Ndo kwanza miili ile ilikuwa imetolewa ndani ikafunikwa vizuri!,
Mwenyekiti akaitisha kikao haraka eneo lile lile wajadili kipi kifanyike kwa kuwa familia ile aikuwa na ndugu tatizo lile ilikuwa lazima walibebe wao!
****
SURA YA PILI:
Mzee John na mke wake alotambulika kwa jina la Aneth walikuwa katika moja ya shamba lao wakipalilia mazao yao
Kwa mbali ilionekana gari ya kifahari ikisimama pembeni ya shamba lao wote wakagandisha macho yao kulitazama gari lile milango ya nyuma ya gari lile ikafunguliwa na wakashuka vijana wawili wote walivaa suti nyeusi na miwani myeusi zilizowapendezawakaelekea milango ya mbele wa kulia upande wa dereva akaufungua na dereva akatoka wakushoto naye akaufungua mlango wake Mzee mmoja wa makamo akatoka wavaa suti wale wakamfata nyuma Mzee yule ni wazi walikuwa ni walinzi wake wakimuacha dereva nje ya gari lile
Wakulima wale walimtambua fika Mzee yule ambaye sura yake ilitawala ukwasi na aikuonesha shida yoyote, alikuwa ni jirani yao na pia hasimu wao Mkubwa walomtambua kwa jina la Mzee Alex
Walikuwa ni maadui wa muda mrefu Mzee yule akazidi kukatisha shamba kuelekea eneo Mzee John na mkewe walipokuwa wakifanya kazi ila kabla ajawafikia Mzee John akatupa jembe na kumfata huku akifoka....
"Unafata nini hapa we mwanahizaya mtoto haramu usiye na hisaya..."
Mzee John akaongea kwa ukali,ila Mzee yule tajiri akakenua meno yake yalopangilika vyema katika mdomo wake akaachia cheko!
Cheko la dharau,cheko la kiburi!,
"Mzee John nadhani umesahau Mimi ni mtu wa namna gani pesa ya kile kiwanja nilichojenga jumba langu sitokulipa na lengo la kuja hapa nakupa wiki moja tu uwe umehama pale kile ni kijumba gani kinaharibu hata 'shape' ya nyumba yangu?!"
Mzee Alex aliongea kwa dharau maneno Yale yakamkera Mzee John akanyanyua jembe lake juu ila kabla ajalishusha mlinzi mmoja akajifyetua na kuachia pigo la mbavuni pigo lililompeleka chini Mzee John yeye na Jembe lake
Bi Aneth akamkimbilia mume wake akimwangalia kama ameumia Mzee Alex akujali ilo
"Mkumbuke ni wiki moja tu yani siku saba muwe kwa hiyari yenu tu mmeondoka katika kijumba kile lasi ivyo kitakachowakutaamtakuwa na muda wa kulaumiana"
Baada ya maneno Yale wakageuka na kuondoka maneno Yale ayakuwaingia kabisa Aneth na mumewe ni kama awakuyasikia
"Umeumia mume wangu?!"
Aneth alimuuliza mumewe akijaribu kumuamsha pale chini
"Wala hata sijaumia ila nisamehe Mke wangu wewe ulinshauri nisiuze kile kiwanja sikusikia ona sasa kulipwa atujalipwa ni masimango tu ila ngoja ntamuonesha"
Mzee John aliongea akijitahidi kusimama!
Wakafunga kazi muda ule ule! Na kuelekea zao nyumban kila mmoja akiwa na hasira zake katu swala lile la kuama ni kama awakulisikia hata kuliongelea awakuliongelea
Madhara yake ndo haya ya kuunguziwa nyumba nao wakiwa ndani!
****
Shamba lao halikuwa mbali na iliponyumba yao walipofika nyumbani walistaajabu kuliona lile gari la kifahari nje ya nyumba yao
Ni kama Mzee Alex alitambua kuwa wenyeji wangekuja mda ule!
"Lakini huyu Mzee anantafuta nini Mimi lakini?!"
Mzee John alimuuliza mkewe ambaye akuwa najibu zaid ya kumfata mumewe nyuma
"Naomba nikukumbushe ni wiki moja tu yani siku saba muwe mmeondoka katika hiyo nyumba ikiwa mtakaid kitakachowakuta?! Tusije kulaumiana!....
Mtu na mkewe wakatazamana kwa mshangao!!!!!!
Sasa maneno Yale ndo yaliingia katika masikio yao
Eti wahame?!......
Shamba lao alikuwa mbali na iliponyumba yao walipofika nyumbani walistaajabu kuliona lile gari la kifahari nje ya nyumba yao
Ni kama Mzee Alex alitambua kuwa wenyeji wangekuja mda ule!
"Lakini huyu Mzee anantafuta nini Mimi lakini?!"
Mzee John alimuuliza mkewe ambaye akuwa najibu zaid ya kumfata mumewe nyuma
"Naomba nikukumbushe ni wiki moja tu yani siku saba muwe mmeondoka katika hiyo nyumba ikiwa mtakaid kitakachowakuta?! Tusije kulaumiana!....
Mtu na mkewe wakatazamana kwa mshangao!!!!!!
Sasa maneno Yale ndo yaliingia katika masikio yao
Eti wahame?!.
Waame katika nyumba walojenga kwa mikono yao,wakabaki wakimtazama Mzee yule ambaye akupepesa macho naye aliwatazama tena kwa macho makali
" unasema nini wewe eti tuame tukuachie hii nyumba yetu?!"
Mzee John akauliza kwa ukali pasina kuamini kile Alichokisikia kutoka mdomoni kwa Mzee Alex
"Haa haaaa haaaaaa haaaaaa wenye nyumba wakiambiwa watoke 'washee' na wewe utatoka?!,hiyo nayo nyumba nadhani ushanielewa nilichokwambia mi naenda ila kwa usalama wako fata nilichokwambia ni siku saba tu!"
Mzee Alex akazidi kuongea kwa kiburi huku akimpa ishara dereva aiondoe gari , kuelekea katika jumba lake Mzee John akasonya akageuka kuelekea katika kajumba kake!
Moyoni hakuwa na wasiwasi kabisa na katu akujua kama mwenzake alikuwa akimaanisha!
Ndiyo! Mzee Alex alikuwa akimaanisha kile akisemacho!
Siku zikasonga chokochoko zikapungua ila kichwani mwa Mzee Alex Alisha adhimia kumwangamiza Mzee John na mkewe kusudi eneo lile lote libaki chini yake
Alijihisi vibaya kupakana na kajumba kama kale japo eneo lile aliuziwa na Mzee John na hata ivyo hakumlipa ela zote ilo yeye akujali!
Siku alizompa hatimaye zikaisha na kesho yake ndo alipanga iwe siku ya mwisho kwa viumbe vile viwili
Mbele yake kulikuwa na vijana kadhaa!,ni vijana alowapa pesa kidogo kusudi kesho yake waiteketeze kwa kuichoma nyumba ya Mzee John nawo wakiwa ndani!
Vijana wale wakakubali na kweli kesho yake alasiri wakiwa na vigeleni vya petrol wakiakikisha Mzee John na mkewe wapo ndani wakafunga mlango kwa nje na kuimiminia nyumba yote petrol kisha wakaichoma na moto ulipozid wakatoweka kabla awajarejea kama wananchi wakawaida kushughudia kazi walofanya
Wakasaidiana na wananchi kuzima moto ule ila wao vigeleni walobeba vilijaa petrol kwa uangaliaj wa kawaida ni lazima ungejua ni maji!
Huo ndo ukawa mwisho wa Mzee John na mkewe wakimwacha mtoto mmoja Isack
***
Kikao kiliwekwa palepale nyumbani mwenyekiti wa kijiji kile na wananchi walisikitika sana kwa tukio lile!
Mzee Alex (diwani) alisimamia mazishi Yale na baada ya mazishi akaomba apewe mtoto yule aishi naye kama mtoto wake!
Hakukuwa na wakupinga
Kwa Mara ya kwanza Isack akaamia nyumbani kwa Mzee Alex katu akujua kama Mzee yule ndo muhusika wa mauaji wa wazazi wake!
Eneo lote lile likawa Mali yake!
Kichwani kwake akiwa na malengo ya kumuua mtoto yule ili mashamba na lile eneo lote libaki chini yake na kusiwepo na kizuhizi chochote juu yake
***
Siku Tatu za mwanzo Isack aliishi maisha mazuri ila taratibu mambo yalianza kubadilika!
Akaanza kudharauliwa waziwazi
Manyanyaso yakaanza akageuzwa mfanyakazi katika nyumba ile nguo afue yeye, kudeki yeye, bustani yeye na chakula alipewa kidogo tena makombo
Moyo ulimuuma kijana yule ila je angefanyaje!?,bado nguvu zake alizielekeza katika elimu na muda mchache ule aloupata aliutumia kujisomea kwani alijua elimu pekee ndiyo ambayo ingemkomboa katika mateso Yale
Siku hiyo alichelewa kutoka shuleni kutokana na masomo ya jioni alipofika nyumbani tu alipokelewa na kipigo
Bi Neema ambaye ndo alikuwa Mke wa Mzee Alex alimpiga pasina huruma tena kwa kutumia mwiko
Baada ya kuridhika akampa nguo saa kumi na mbili ile afue tena kwa kutumia mkono japo mashine za kufulia zilikwepo
Alipomaliza kufua na kuzianika akaambiwa adeki uwa ule ,hakika ulikuwa ni ua Mkubwa alipomaliza akaelekea ndani ya nyumba akianzia sebuleni na chumba kimoja baada ya kingine
Huku nyuma Agnesi akazishusha nguo zote zilizofuliwa na kutoka nazo nje ya geti palipokuwa na tope akazibwaga na kuzikanyaga kanyaga akazichafua na kuzirudisha uani
Baada ya kumalizia zote akacheka na kukimbilia chumbani kwake
"Ngoja sasa tuone utakachopata Leo"
Agnes akajisemea akijitupa kitandani,bintihuyu ambaye alikuwa rika moja na Isack tena wakiwa wote darasa la saba ila shule tofauti Isack akiwa shule ya kata huku Agnes akiwa shule za kimataifa tena alipelekwa na gari na kurudishwa na gari
Bi Neema aliyatoa macho kama kabanwa na mlango pasina kuamini kile alichokiona
"Isackiiiiiiiiiiiiiii...."
Akaita kwa ukali sauti ilopenya mpaka katika masikio ya kijana yule aloacha kudeki huku akitetemeka akakimbia kuelekea nje alipotwa
Alipiga breki naye akayatoa macho pasina kuamini kile alichokiona
Bi Neema alimkamata na kuanza kumpiga huku akimshushia Matusi ya nguoni
Agnes aliwatazama kupitia dirishani moyoni mwake alfrah kwa adhabu ile mwenzake alopewa alimchukia sana Isack tena bila sababu yoyote
Isack ikabidi arudie zile nguo tena huku akilia mwili wote ulimuuma
Mpaka inatimia saa sita usiku ndo alipomaliza kazi zote akashika daftar lake na kuketi sebuleni tayari kuanza kusoma.
Chumbani kwake taa ilichomolewa kusudi asisome na hata kitanda kilitolewa alilala chini ni maisha yalomlazimu ayazoee!
"Hivi wewe sheitwani mtoto haramu mzimu wa baba yako au huyo mzimu Malaya wa mama yako unansaidiaga kulipa luku ikiisha ndo utumie umeme mpaka sasa?!"
Isack alishtushwa na sauti Kali alipotupa macho mbele yake alisimama Mzee Alex akiwa na taulo na singlend mkononi akiwa kashika mkanda!
Akimwangalia kwa hasira
Wasiwasi ukamvaa Isack,meno yakaanza kugongana machozi yakaanza kumchuruzika!
Ni muda mchache tu mama mwenye nyumba alimpiga na sasa baba naye,Isack alihisi MUNGU amemtenga
Akanyanyuka kwenye kiti na kuanza kurudi nyuma taratibu ila akufika mbali kitu kizito kikatua katika kichwa chake Maskini Isack akaachia yowe kabla kitu kile akijatua tena kichwani awamu hii kikitoka na nyama!....
*kah binadamu tuna roho gani lakini?!*
Kijana Isack John mtoto pekee anayetoka katika familia ya kifukara anapoteza wazazi wake wanayeungulia ndani ya nyumba
Diwani wa kata ile ambaye pia ni jirani yake na msababishi wa vifo vile Mzee Alex anabeba jukumu la kumlea mtoto yule
Hata ivyo yeye na familia yake wanamtesa mtoto huyo pasina huruma je nini kitaendelea katika maisha ya kijana huyo?!
Twende pamoja!...
Damu zilianza kuchuruzika kichwani ila Mzee yule akujali jambo lile pasina huruma akaanza kumchapa tena kwa kutumia bakoli la chuma lililokwepo katika mkanda ule
"Shhhhhhhhh nyamaza sitaki nisikie sauti yako usiku huu au nikuongeze!..."
Mzee yule pasina uso wa huruma alifoka ikamlazimu Isack anyamaze kusudi asiendelee kuchapwa
"Unajifanya unauchungu wa kusoma basi si ungepata yote katika mitihani yako"
Mzee yule akazidi kuongea safari hii akisogelea daftari lile pale mezani na kulishika,bado Isack alilia taratibu kwa kigugumizi
Mzee Alilikagua kidogo na ghafla akaanza kulichana chana
"Nione sasa utasoma nini! Shhhhhh nimesema nyamaza kwanza nenda kalale....
Isack kwa unyonge akaelekea chumbani kwake kulala, hata alipofika chumbani aliendelea kulia kwa maumivu makali alokumbana nayo damu bado zilimchuruzika
Mpaka inafika saa kumi za usiku bado akupata hata lepe La usingizi kwa maumivu makali ya vidonda alivyokuwa navyo!,saa kumi na moja kasoro usingizi ulimnyemelea na hatimaye akaupata ila alilala dakika kumi tu na saa kumi na moja na dakika tatu bi Neema aliamka alishangaa kumkuta Isack bado ajaamka
Alipoelekea chumbani kwake alimkuta kajiinamia kichwa kwenye magoti mama yule akasonya na kutoka aliporejea alikuwa na beseni lililojaa maji tena ya baridi pasina huruma pasina kujua kuwa yule ni kama mtoto wake akainyanyua ile ndoo na kumwagia maji yote bila kujua kwa kitendo kile ni lazima yule kijana angepata homa
Maskini Isack alishtuka ...
" hivi wewe kikaragosi umekuja hapa kulala au kufanya kazi?!,nilikwambia muda wa kuamka ni sa ngapi?"
"Saa kumi na moja kamili" Isack alijibu huku akitetemeka kwa baridi
"Ehe na saivi ni sangapi?!"
Mama yule mwenye roho mbaya alizidi kumuuliza akiwasha taa yake ya sola na kummulikia saa ilokuwa ukutani
Saa alowekewa makusidi kusudi ajue muda wa kuamka saa ilomshtua kwa alamu pindi ikifika mida hiyo ya saa kumi na moja kamili
"Nisamehe mama"
"Ishia hapo hapo Mimi si mama yako wala uwezi kuwa na mama Kama Mimi kama unataka kuita mama kamfukue mama yako kule makaburini ndo umwite mama aya bila kupoteza muda anza kazi Mara moja na utoenda shule mpaka ukamilishe kazi zote"
Wala Isack hakuwa mbishi akaanza kazi akifua makapeti ya chini tena ya Sufi magumu na mazito alipomaliza alideki akaosha vyombo mpaka Saa mbili ndipo alipomaliza
Alikuwa na maumivu makali ya kichwa ila ugonjwa wake ule kilio chake kile angemuwasilishia nani
Naaaam waenga waliponena kuwa "yatima adeki" awakukosea
Isack akajizoazoa tayar kwa kuelekea shuleni akiwa amechelewa alikimbia na alipofika aliwekwa kwenye kundi la wachelewaji ambapo alichapwa na kuruhusiwa kuingia darasani
Mwalimu wa hisabati akaingia huyu alitambulika kwa ukali na aliingia na rundo la fimbo aina ya mwanzi wanafunzi wote wakaanza kutetemeka alipoingia tu akaanza kuwachapa fimbo Tatu Tatu kila mwanafunzi kwa sababu ya kelele
"Oooooh raita students Jana niliacha omwek ( home work) Kama unajua ujafanya pita mbele na kila mmoja aweke daftar juu niweze pitia na kusahihisha"
Wanafunzi wote wa darasa lile wakashika mabegi yao na kuanza kutoa madaftar hapakuwa na ambaye akufanya kazi ile ivyo hata Isack aliona aibu kutoka mwenyewe akakausha pale pale katika siti yake meno yakigongana kwa hofu ya woga
"Ok!,ooooh raita wote aithink ( I think) mmefanya kazi niliyoiacha his gud kusanya daftar ziletwe mbele yangu"
Viongozi wa darasa 'Montar' na ' montress' wakafanya kazi yao wakazikusanya na kuziwasilisha kwa mwalimu daftar zile mwalimu hitlar kama walivyomuita wao akazihesabu na alipoitimisha akawahesabu wanafunzi na kukunja sura!
"Ni nani ambaye ajakusanya daftari yake hapa"...
Akauliza kwa ukali akiwaoneshea fimbo wanafunzi kimya
Maskini mtoto Isack kumbukumbu zake zikarudi Jana yake wakati baba yake mlezi Mzee Alex akiichana chana daftar yake
Machozi yakaanza kumlenga lenga Leo hii angemueleza nini " Hitler" alovimba kwa hasira hapo mbele ya darasa?!
Mbona kitimtimu?!....
Nyumbani matatizo!,shuleni matatizo hivi kweli Mungu yupo na kama yupo kamuumba yeye kuja kuteseka analalia fimbo anaamkia fimbo na Mungu kweli anaangalia?!,
Kwa nini kawachukua wazazi wake tena katika mateso ya moto Isack akajikuta akizama katika Lindi la mawazo na kutosikia chochote 'hitler' alichokuwa akiongea
Hitlar yeye alikuwa akiita mwanafunzi mmoja mmoja na kumwamuru apite mbele ambapo aliweka daftari lake pembeni na kuendelea na mwingine hatimaye akawamaliza wote macho yake makali akamtumbulia yule alobaki!
Naaam ni Isack!
Ticha akaachia kicheko!
"Oooh raita student Ujachapwa unalia....
Akamsogelea fimbo akainyanyua juu ikatua begani kwa mtoto yule alokuwa mbali kimawazo
" lipo wapi daftari lako?!"
Ticha Hitler akamuuliza kwa ukali
Isack alishtuka akaanza kumumunya maneno akiwa ajui aongee neno gani!
"Haya pita mbele adhabu utapata Mara tatu ya kunisumbua,kutofanya kazi na kutokuja na daftari kashike masikio mbele ingiza mikono katikati ya miguu ndo ushike masikio"
'Hivi matatizo aliumbiwa binadamu?!,na binadamu mwenyewe ndo mimi pekee?!'
Isack akupata jibu akaenda kushika masikio kipindi kizima cha mwalimu yule Mara kadhaa akimchapa fimbo za mgongoni pindi alipolegalega
Alipomaliza kipindi akamwambia ile ni adhabu ya usumbufu akamwomba alale chini ampe adhabu ya kutoandika kazi yake akamchapa fimbo tano za 'matako' mbele ya wanafunzi wote,fimbo zilizoingia barabara
Kisha akamwambia aongoze ofisini akampe adhabu ya mwisho,adhabu ya kupoteza daftari
Isack akaongoza huku akiendelea kutetemeka
Ofisini sasa kama kawaida ya walimu vijembe mchafu yeye eti mtoto wa diwani mchelewaji yeye hakika walimchambua mwisho akaambiwa akamwite mzazi
Isack alishtuka!,akamlete mzazi?! Si ndo atakuja kuuwawa hapo shuleni akuruhusiwa kurudi darasani mpaka mzazi wake aje!
Je amlete baba au mama?!,kwake wote wabaya
'Wazazi wangu wangekwepo ningewaleta maskin sasa ntamleta nani wai mi ( why me) matatizo kwangu tu?!"
maskin Isack akawaza akaona bora aelekee makaburini kwa wazazi wake alipofika alianza kulia kwa uchungu akiwalilia wazazi wake
"Kwa nini mmeondoka wazazi wangu na kuniacha katika mateso makubwa namna hii!,dunia yote imenielemea kula kwangu tabu masomo yangu ya tabu kupigwa kwangu ni sehemu ya maisha yangu mngekuwa wazazi wangu nisingeteseka hivi Mimi Leo hii naambiwa nikawaite wazazi ningekupeleka mama ungentetea Mimi nisichapwe kwa mapenzi mazito uliyokuwa nayo juu Yang ningekupeleka baba ungentetea mwanao sasa ntampeleka nani Mimi wale wataniua wazazi wangu kwa nini mmeenda.....
Isack dongo lilimkaba kooni akashindwa kujizuhia akaachia kilio aliwalilia wazazi wake
Kwa mbali alihis Giza kizunguzungu kikali kikamshika na ghafla akaporomoka chini tena akidondokea kaburi lililopembeni ya makabur ya wazazi wake lililotengenezwa vizuri akatulia tuli!
Macho akiyatoa Pima.....
Machozi yalimchuruzika,akujijua ni kwa muda gani alilala pale?!,na ile hali ya kuzimiazimia kila Mara ilimtisha! Ikamuongezea msongo wa mawazo katika fikra zake akiihofia hali yake
Akajinyanyua pale chini na kuyaangalia makaburi ya wazazi wake kwa uchungu moyoni mwake akijua fika ndani yake ndipo walipo wazazi ambao ndio lililokuwa kimbilia lake
Alitamani naye hata angekufa apumzike akaungane nao ila ilo alikuwezekana kwa wakati ule,
Akageuka na kuanza kuondoka taratibu akigeuka nyuma kila Mara yamkin akitegemea labda wazazi wake wangefufuka akawaona na kuwafikishia kilio chake ila hapakuwa na mabadiliko ya aina yoyote!
Akazidi kusonga kutoka eneo lile la makaburi aliamua kurudi nyumbani na kitakachotokea na kitokee!,akuwa na pa kukimbilia ilikuwa ni lazima arudi akamweleze ukwel mama atakachomfanya na amfanye tu!
Tayari Isack alishajikatia tamaa
Kama ni kuchapwa alijua hata angefanya nini kwa wanavyomchukia ni lazima angechapwa kwani shuleni asingepokelewa pasina kwenda na mzazi hivyo ilikuwa ni lazima kusema ukweli litakalotokea litokee kusudi apate amani ya moyo
Bi Ney alishtuka kumuona Isack akirejea nyumbani mapema kutoka shuleni kwa namna yoyote ile kwa mtazamo wake alijua lazima Kijana yule kuna kosa hatakuwa amefanya
"Haya kuna nini tena huko shuleni mbona umewahi kutoka"
Bi Neema aliuliza kwa nyodo ilo changanyikana na mshangao wa waziwazi
"Nimerudishwa nimlete mzazi!"
"Eti?!,unasema umerudishwa eti umpeleke mzazi haya ni kosa gani ulilolifanya huko hata uambiwe umpeleke mzazi"
Bi Neema aliuliza kwa hasira akinyanyuka katika kochi alilokuwa amekaa akitazama tv na kumsogelea Isack ambaye akuonesha kufanya juhudi zozote za kukwepa ujio wa Dada yule
"Paaaaaaaaaaaaaaaa" kibao kikali kikatua katika shavu la mtoto yule mpaka kuacha alama za mkono pindi alipoutoa ladha ya mate kwa kibao kile yakabadilika na kuwa matamtam nyota nyota zikazagaa mbele ya macho yake na sikio la upande ule kilipotua kibao likaziba kwa muda zzzzzzzzzzzzz!!!!!!
"Sinakuuliza wewe?!"
Aliisikia sauti hiyo kwa mbali tena kupitia katika sikio la upande ambao akupigwa!
Machozi yakaanza kumchuruzika
"Mpumbavu Mkubwa wewe unalia ujapigwa unatuletea uchuro katika nyumba yetu....
Akamdaka na kumvutia kwake akaanza kumfinya
....haya nieleze ulichofanya shule"
"Nisamehe mama!,..."
"Sema umefanya nini huko shuleni?!"
Bi Neema aliendelea kumuuliza huku akiendelea kumfinya kwa ukucha wake mrefu alokuwa akiufuga na kutoka na nyama pale alipofinya
"Sema! Sema! Nakwambia sema umefanya nini huko shuleni lasi ivyo Leo ntakuua"
"Ni.ni..nisamehe mamma sijaandika....wala....kukusanya.... kazi na daff...tari nimepoteza"
Hapo ikawa kama Isack kakiamsha kichaa cha mama yake mlezi yule mwenye roho mbaya alimshika mkono akamvuta akamzungusha alimpmuachia Isack alienda chini akapigiza kichwa Ney akamsogelea na kumvua mkanda alokuwa ameuvaa akaugeuza upande wa bakoli na kuanza kumchapa nao
"Umesikia ela tunayokununulia madaftari tunapewa na mizimu ya wazazi wako siyo mtoto mpumbavu wewe na Leo utantambua"
Pa pa pa pa pa pa pa
"Nisa..mehe ma..ma...sito..rudi.a"
Bi Ney aliendelea kumchapa pasina huruma mtoto yule utadhani ajazaa au aujui uchungu wa Mwana!
Mtoto wa mwenzako ni wako mpende kama umpendavyo mtoto wako ndivyo Mungu atakavyokupenda
Unavyomnyanyasa mtoto wa mwenzako kisa ujamzaa jua hata Mungu anakuchukia je unapata faida gani kwa kumtesa ama kumchukia?!....
Bi Ney ni kama akusikia kilio cha mtoto yule akazidi kumuadhibu mtoto wa mwenzako ni wako kauli hii aikuwa na maana kwa Dada yule ambaye ilikuwa ni kama ajazaa au akuujua uchungu wa Mwana
Je mwanamke ni mtu mwenye huruma sana?!
Kwa mama huyu ungepingana na kauli hii wanawake wa dizaini hii wapo si kwamba awapo tujirekebisheni dunia inazunguka miaka inaenda mambo yanabadilika yule unayemdharau kuna Leo na kesho ujui anaweza kukusaidia wakati gani
Ujui badae atakuja kuwa nani katika taifa hili hata kama ni mbumbumbu Kila mtu na riziki zake
Baada ya kumchapa na kuridhika akajiandaa kumpeleka shuleni huko nako akiwa amepania kumuadhibu ipasavyo
Bi Neema alimchukia Isack kupitiliza
Huzuni ilitawala moyoni mwake,meno mdomoni yaligongana kwa kutetemeka uoga,kichwa kilimuuma kwa kulia kila Mara na mawazo ya muda mrefu angeishi maisha Yale mpaka lini?!
Mateso Yale hitimisho lake ni lini?!
Kila siku kwake tu!?
Walifika shuleni Isack akamuongoza mzazi wake mpaka ofisi ya walimu ambapo baada ya kumuona maneno yalianza
Wakieleza jinsi mtoto yule anavyochelew kuja shuleni tena anakuja mchafu afanyi kazi
"Nimemshindwa huyu mtoto walimu nanyi nisaidieni kila Mara huwa namuamsha mapema saa kumi na mbili anaamka ila akishavaa nguo za shule uwa anarudi kulala....
Bi Neema akaanza kuongopa kitendo kilichomfanya Isack aanze kulia
Hakuna uchungu mbaya kama wa kusingiziwa kitu ambacho ujafanya moyo ulimuuma,yule yule mama ndie ambaye alimpa kazi asb na kupelekea achelewe shuleni Leo hii anageuza mambo?!...
Isack akaonekana mtukutu
" mama huyu tuachie sisi awezi tushinda na Leo fimbo tutakazo mpa ni lazima tumuachie kilema cha maisha"
Mwalimu Hitlar aliongea akigawa fimbo mbili mbili kwa walimu wale ofisini pale walikuwa walimu kumi na moja!
"Naomba na Mimi mwalimu nimuanzie"
Mama yake akasema Hitlar akampa fimbo mwanamke yule mwenye roho mbaya.......
Mateso,unyanyasaji kuchapwa bila sababu imekuwa sasa ni kawaida katika maisha ya mtoto Isack baada ya baba yake mlezi kumkuta sebuleni anasoma anamuamshia noma na kumchania daftari lake!
Hii inaamsha noma nyingine shuleni matokeo yake mwalimu wa hisabat ajulikanaye kwa jina la ticha Hitlar kumuamshia noma nyingine na mwisho anamuamuru akalete mzazi!
Isack anaenda kumwambia mama yake bi Neema ambaye naye anamuadhibu vibaya sana nasasa wapo ofisini Hitlar kagawa fimbo kwa kila mwalimu tayari kwa kumuadhibu kijana yule!
Je nini kiliendelea?!
Twende sasa....
NA HII NI SEHEMU YA SITA
Baada ya Neema kuridhika mwalimu Hitlar akashika fimbo yake
"Oooh rightar mi uwa naadhibugi hii nyama ya serikali nadhani wajua sasa kamatia vidole ukinyanyuka tu nafuta"
Ticha Hitlar aliongea huku akiwa katabasamu,Isack akashika vidole mwalimu akanyanyua fimbo juu ikatua makalion mwa mtoto yule akanyanyua tena ya pili ya tatu ya nne Isack katulia yatano yasita mtoto akanyanyuka huku akilia
"Umefuta ilibaki moja sasa naanza tena hii fimbo ni kwa ajili ya kufuta ujinga wako ulokuwa nao hapo kichwani....
Hitlar aliongea huku alimpiga piga na ile fimbo kichwani
Isack akawa akiweka mkono vidole kuzuia kwa hiyo mwanzi ule ukawa ukitandika vidole vyake
....haya kamata chini haraka nimesema"
Na ghafla akarauka akimchapa fimbo ya mgongoni , Isack huku akilia akaenda chini
Hitlar akaanza mwanzo vilipotimia saba pale alipochapwa pakiwaka moto akasogea kwa mwalimu mwingine
"Lete mkono"
Mwalimu yule ambaye alikuwa wa kike alimuamrisha akamchapa fimbo saba katika mkono wa kushoto akaenda kwa mwalimu mwingine hivyo hivyo awakumruhusu abadilishe mkono
Wakati wote huo kuna mwalimu alotambulika kwa jina la madamu Jane alokuwa akifundisha somo la kiswahili kwa madarasa mengi pale shuleni muda wote alikuwa kashika tama akimuonea huruma mtoto yule!
Madam yule ambao wanafunzi walimvisha jina la 'sista' kutokana na upole wake na hata fimbo zake pia zilikuwa haziumi kutokana na kuchapa taratibu
Muda wote toka Isack akiadhibiwa na Hitlar Jane alikuwa akimuombea msamaha ila walimu awakumsikiliza sasa alikuwa akilengwa lengwa na machozi walipofika walimu nane na kubakia watatu uvumilivu ulimshinda akabeba kitabu chake na kutoka hakuna alomsemesha hata walimu walimjua kwa huruma na upole alokuwa nao
Safari ya mwalimu yule iliishia darasa la nne 'b' darasa alilosoma Isack kwa muda huo ndo alikuwa na kipindi katika darasa lile
"Leo ntasahihisha kazi ya Jana kimya kitawale viongozi wa darasa nikusanyieni madaftar nileteeni hapa mbele"
Aliongea akikaa katika dawati lililokuwa mbele kabisa mwa darasa lile kushoto kidogo mwa ubao,utaratibu wa kukusanya daftar ukafanyika dakika chache baadaye daftar za wanafunzi wa darasa lile zikawa mbele yake akaanza kusahihisha
Ila mawazo ayakuwa pale kila alipojitahidi kuyafuta ilishindikana
'Lazima mtoto huyu atakuwa na matatizo makubwa sana'
Madamu Jane akawaza akikumbuka jinsi mama wa mtoto yule Bi Ney alipokuwa akimchapa pasina huruma na hata walimu walipokuwa wakimchapa yeye alionekana kufurahia
'Mmmmmmh!!!!'
Ghafla mguno wa mshangao ukamponyoka
'Itakuwa yule si mtoto wake wa damu uwezi furahia wala uwezi mfanyia mtoto wako vile'
Mwalimu yule Mrembo akazidi kuwaza huku akiendelea kusahihisha daftar zile ghafla akapata wazo akaliangalia darasa ambapo wanafunzi walikuwa wakinong'ona walipo ona mwalimu wao ana watazama wakanyamaza kimya
"Brayton"
"Present madam"
Mwanafunzi yule aliyeitwa akajinyanyua na kuelekea mahali alipokaa mwalimu
"We si ndo rafiki yake na Isack John"
"Hapana mwalimu!"
Brayton alikataa akihofia kuadhibiwa au kusemwa kwani kwa sasa jina la Isack lilishachafuka darasani mule hata marafiki zake walishaanza kumtenga
"Kwani ukai nae dawati moja"
Madam Jane akauliza kwa hasira akichukia kudanganywa
"Ndio madam nakaa naye dawati moja"
"Aya embu nletee begi lake lenye daftar zake zote"
Brayton akarudi katika dawati lake na kuchukua begi kuukuu la Isack akaelekea nalo kwa mwalimu akamkabidhi
"Najua Isack ni rafiki yako sana usinifiche kitu nieleze ukweli wa kila ntakachokuuliza sawa"
Madam Jane akaongea huku macho yake yakikagua daftari alizochomoa katika begi aliloletewa
Kwanza alistaajabu kwa unadhifu wa daftar zile alijua pengine ni daftar ya kiswahili tu ndiyo ilojaladiwa ila alikuta daftari zote zikiwa zimejaladiwa
Madam Jane akajikuta akitabasamu!
Swala la kusahihisha alishaacha kwa wakati ule!
'Nilijua ni kiswahili tu ndo anachofaulu mbona masomo yote yupo vizuri embu angalia kwanza hata ati yake'
Madam Jane alijiwazia akiendelea kuyapitia na kuzidi kushangaa
'Na hisi huyu mtoto atakuwa vibaya tu katika hisabu'
Mwalimu yule akazidi kuwaza
"Brayton embu nambie kwanini rafiki yako Isack anakuwa hivi?!,ni kila siku afanyagi hisabu au?!"
Akamuuliza mwanafunzi yule akiingiza madaftar Yale katika begi lile
Brayton akatingisha kichwa kukataa "anafanyaga mwalimu"
"Huwa si mvivu kabisa wa kuandika"
"Ndio mwalimu!"
"Nyumbani kwao anakaa na nani?!"
"Na wazazi wake lakini wanamtesa!"
Brayton akaanza kuropoka Yale Isack anayomwelezaga kwani yule alikuwa ndo rafiki yake Mkubwa
"Wanamtesa?!,kivipi wamtese mtoto wao?!"
"Mmh mwalimu! Si wazazi wao wakumzaa wazazi wake walishafariki"
"Ahaaaaaaaaa"
Mwanga ukaanza kujionesha machoni mwa madamu yule ambaye alikuwa na chembechembe za ugeni bado katika shule ile
"Ok! Nenda kakae ntajua cha kufanya"
"Plz mwalim msaidie Isack anateseka sana"
Brayton akaongea kwa kubembeleza
"Usijal we nenda kakae"
Brayton akachukua lile begi la Isack na kuelekea nalo kwenye dawati lake
'Lazima nimsaidie mtoto huyu'
Madam Jane akajiwazia akiendelea kusahihisha daftar zile
*****
Baada ya walimu wote kumi kumaliza kumchapa mwalimu alosimamia nidhamu katika shule ile mwalimu Hitlar akaangalia saa yake
Baada ya kuiangalia kwa sek kadhaa akaufungua mdomo wake
"Sasa ni saa sita kasoro robo hizo dakika kumi na tano zilizobakia utaenda hapo nje kushika masikio mpaka kengele igongwe ya chakula nadhani kwa adhabu hizi utorudia tena asbuh utawah kazi utafanya mama we nenda utamnunulia daftar la 'mets' kesho aje nalo"
"Nashkur mwalimu ntampa daftar na asipokuja nalo mumuadhibu kama Leo mlivyomuadhibu"
Dada yule mwenye roho mbaya akaongea akidhamiria kutompa ela ya daftar ahadhibiwe hivyo hivyo siku inayofatia.
"Usijal mama hapa amefika"
Hitlar akaongea wakatoka nje Isack akashika masikio Neema na Hitlar wakawa wakiongea kwa pembeni
"Mwalimu bora hata unsaidie toto jizi livivu si wakumuonea huruma huyu...
Wakati Neema akiendelea kum'mwagia sifa mbaya kwa mwalimu nyoka katika shule ile darasa la nne lililotazamana na ofisin alitoka mwalimu Jane kwanza alishtuka kumuona mtoto yule akiwa kashika masikio
Hakika mwalimu Jane alishikwa na hasira
Akawakata jicho baya mwalimu na mzazi waliokuwa wakiteta ambapo wote walishtuka kwa uangaliwaji ule walioangaliwa
Kisha akamfata Isack pale chini
" amka hapo nenda darasani!"
Akamwambia Isack akaamka na kuelekea zake darasani
"Unafanya nini mwalimu?!"
Hitlar akauliza kwa ukali akimfata mwalimu Jane akihis kudharaulika tena mbele ya mzazi
"Mna roho ya kishetani ama kwa kuwa amna watoto ndo mmnyanyase mtoto wa mwenzenu hivi?!"
Madam Jane akaongea kwa hisia akionekana kuchukia
Mwenye Asili ya ukorofi ni mkorofi tu ni kwel Hitlar hakuwa na mtoto japo alioa miaka mitano ilopita tusi lile likamkaa kooni.
Akashindwa kujizuhia akawa tayari kumvaa madamu yule na kumfundisha adabu
Mateso kwa mtoto Isack bado yanaendelea kuyatafuna maisha yake!
Lakini akiwa katikati ya tanuri la mateso mwokozi anatokea na kuhaidi kumsaidia kwa hali na Mali!
Ni madam Jane!!!!....
Mwanadada Mrembo mpole mwalimu pekee anayetokea kumjali mtoto yule
Je nini kitaendelea katika maisha ya mtoto huyu?!....
Songa nayo ujifunze
NA HII NI SEHEMU YA SABA....
Mdomo ulifumuka,sehemu ya shavu pakachubuliwa kwa kisu kile bado Isack aliendelea kulia kwa maumivu...
Mzee John akuishia hapo akaendelea kumfinya kwa kisu kile katika mapaja ,akamuunguza na mkono kwa kisu kile cha moto pasina kuwa hata na chembe ya huruma
Maneno kibao yakimtoka mdomoni akimgombeza na kuendelea kumpiga Ney aliendelea kufrah akichochea mtoto yule aendelee kupigwa,Agnes aliruka ruka huku akifurahia kaka yake wakufikia pekee kwa kile alichokuwa akifanyiwa
Mzee John alimuumiza vibaya sana,ila pasipo kujali maumivu Yale nguo zikatolewa eti afue!,ashike maji ya baridi na asugue nguo zile!
Akauangalia mkono wake kwa uchungu,akaupeleka mkono wake katika lengelenge ila aliutoa haraka baada ya kupata maumivu makali alikuwa kama kautonesha
Kuugusa tu kapata maumivu Yale je angewezaje kufua hizo nguo!?
Akabaki kajisimamia mchirizi wa machozi ukichirizika ishara ya maumivu makali yaloushambulia moyo wake
"Ndani ya dakika tano ziwe zimetakata na uzianike akuna alokufa nilishakwambia kalilie makaburini kwa wazazi wako akaa a!"
Bi Neema akaongea kwa ukali,Isack akuwa na budi kufanya alichoambiwa kukwepa kupigwa tena akasogea mpaka katika rundo la nguo zile ambazo zilikwepo jinsi kadhaa za Mzee Isack taulo na nguo zake za ndani
Vivyo hivyo nguo za Neema mpaka za ndani ambazo alipaswa afue mwenyewe na za mtoto wake Agnes walimpa yatima yule wa darasa la nne awafulie makusudi tu kumkomoa
Pasina kumuonea huruma!
Sasa angefanya nini?!,akachukua sabuni ya unga na kuimiminia katika beseni kubwa akaingiza mkono wake ule wenye lengelenge na kuanza kuchanganya sabuni kwenye maji Yale!
Bado tatizo lilibaki katika kusugua!
Angesuguaje?!,alibaki akiwaza
Baada ya sabuni kuchanganyika akachukua nguo laini na kuzitumbukiza akaanza kuzisugua taratibu akiparangana na maumivu makali
Haya yalikuwa maisha yake ilopaswa ayazoee,maisha ya mateso
Siku ile ikapita!
Na hatimaye kesho yake saa kumi na moja akashtuliwa na alamu ya saa yake Isack akajiamsha mkono ulivimba na ulimuuma ila angemlalamikia nani?!
Akashika ndoo yake ya maji na kuanza kudeki , kuosha vyombo,akabandika chai ya maziwa na kuandaa staftahi mezani akaingia zake ndani kuvaa
Siku hiyo alifanya kazi haraka haraka mpaka saa saa moja kasorobo alikuwa katika 'uniform' zake za shule akatoka chumbani kwake na kuelekea sebuleni ambapo aliketi mama Agnes,Mzee John na mwanao Agnes wakinywa chai na mikate 'blue band' na planetbatter zikiwa pembeni mayai pia ayakukosekana
Na vyote mtoto Isack ndiyo aliyeviandaa
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment