Simulizi : Code X 5 N.g.s.s. (Next Generation Super Soldiers)
Sehemu Ya Nne (4)
Ulipofunguka na kupitisha mwanga tu, Alex aligeuka na kama risasi alimpita aliefunguwa huwo huku akizamisha kisu kitovuni na kumraruwa tumbo. “Tieni loko milango yote, na mumtafute” aliongea mtu mmoja aliekuwepo ndani ya chumba kile alichokuwemo Alex lakini alijibanza sehemu na kutulia tuli kama paka aliemwagiwa maji ya baridi. Milango yote ikafungwa kwa loki, vikosi vya askari waliokuwa wanansimamia eneo hilo vilisambazwa na kuanza kumsaka. Alex baada ya kutoka kwenye chumba hicho, akili yake ikamwambia aende moja kwa moja mpaka katika kile chumba walichokuwa wanalala. Huko walikuwepo watoto wengine na aliwachukia sana kwasababu walikuwa wakimcheka kila alipokosea.
Alipofika akakuta mlango una loki, akarudi nyuma na kuvuta pumzi nyingi kisha akakaza misuli ambayo ilendelea kuumuka. Akaupika kikumbo kimoja na kuanguka nao ndani, watoto wote walishtuka na kujikusanya sehemu moja. “Chekeni sasa, si nimeanguka na mlango” aliongea kwa sauti nzito na mdomoi alikuwa akitokwa ute. Bilakuchelewa aliwavaa na kuwachana chanak kwa kisu alichokuwa nacho mpaka akawamaliza wote. “Zaidi zaidi, hii haitoshi nahitaji kuona damu ikimwagika” aliongea akitoka ndani ya chumba hicho na kuanza kusaka roho nyingine.
“Tunaomba ruhusa ya kumuuwa huyu mtoto” aliongea mtu kupitia kifaa maalum cha mawasiliano, “negative, anahitajika akiwa hai” alikataliwa. “Anakuja hu..” hakumaliza alichotaka kuongea zikasikika chenga, alikuwa chini akitokwa damu kooni baada ya kisu kupita eneo hilo. Aliendelea kuwatia kasheshe mpaka aliponza kuchoka na hapo ndipo wakafanikiwa kumkamata. “Hili ni dudu katika umbiele la binadamu” aliongea mwanajeshi mmoja akimuangalia Alex ambae alikuwa amelegea na kuonekana akiwa kama mtu mwenye usingizi mzito.
“Nipe taarifa” aliongea mtu kupitia kifaa cha mawasiliano, “ni hatari mkuu, tumetengeza silaha ya maangamizi. Idadi ya watu aliuwa leo inafika thamanini ukichanganya na wale watoto wenzake” alijibiwa. “Mchomeni sindano ya usingizi na muanze taratibu za kumuhamishia kambi kubwa ya pasifiki” alitoa amri na kuzima kifaa chake cha mawasiliano.
*********************************************
Jenerali David baada ya kufyetuwa risasi iliosafiri na kuzama kifuani kwa Alex mkubwa, aliitumia ile nafasi ambayo Alex alitikiswa na kumfanya aone kama kamuuwa yeye. Jambo halisi ni kwamba bastola aliokuwa nayo Alex Alex haikuwa hata na risasi moja. “Sikutegemea kama angekuwa hivi” alijisemea na kutabasamu, baada ya kufyetuwa risasi aliirudisha bastola yake kiunoni na kusoma hali ya hewa. Kitendo cha kumsikia Alex Jr akicheka akatambuwa kabisa kuwa mtoto huyo alirukwa na akili hivyo akajisogeza pembeni kujiingiza kwenye kipembe kabla hakujaharibika na hiyo ndio ilikuwa pona yake.
Alisogea mpaka alipoanguka Alex mkubwa na kumuekelea vidole viwili shingoni, akatabasamu “ulidhani nitapoteza nguvu kazi kama wewe” alijisemea akitabasamu. Akambeba na kutoka nae katika chumba hicho, akatoka nae hadi nje ya kambi ambako helikopta ilikuwa ikimsubiri. Walifika watu na machela ya kubebea wagonjwa, Alex mkubwa akalazwa juu ya machela na kupatiwa huduma ya kwanza kisha akapakizwa kwenye helikopta. Taratibu ikaanza kupaa na hatimae ikapotolea angani.
Safari hiyo ilifikia kikomo mjini Rio nchini Brazil kwenye kambi ndogo ya kikosi hicho, hapo Alex mkubwa alishushwa nakupelekwa ndani kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi. Jenerali David alitoa simu na kubonyeza nambari kadhaa kisha akapiga, “David, ni muda mrefu sana hatujawasiliana” iliongea sauti ya upande wa pili. “Kwa kweli, Matvei” jenerali David aliitika, “na mpaka umenitafuta kuna jambo kubwa unataka kunambia” aliongea matvei na kucheka kidogo. “Ndio, si unakumbuka mara ya mwisho nilikwambia kuna projekti fulani nafanya”, “ndio, ulinambia sijui inaitwa Project CODE X au kitu kama hicho” aliongea akionekana kukusanya kumbukumbu zake vizuri.
“Ndio hiyo hiyo, nilihangaika sana kutafuta njia ambayo ingenipa majibu ya hara ila sasa nimefanikiwa na hivi tunavyoogea. Kuna vijana wawili ikiwa tutawapa mafunzi vizuri wanaweza kuiwasha dunia moto usiozimika kwa maji ya kawaida”.
“Wawili hawatoshi, tunahitaji angalau kikosi cha watu kama elfu kumi hivi. Yaani hapo ndio ikiwa tumekosa kabisa watu”.
“Ah! Hao ni wa kuanzia tu, na muda si mrefu tutakuwa jeshi la kutosha kufanya mapinduzi. Tutaongoza kwa misingi yetu.”
“Vizuri sana, kama itawezekana umlete huku huyo kijana apate mafunzo na wengine kisha atarudi mikononi mwako mafunzo yatakapokamilika”.
“Ni wazo zuri, ngoja akiwa tayari tutawasiliana. Vipi huko maandalizi yanaendaje?”
“Huku kila kitu kinakwenda sawa isipokuwa kuna kunguni anajaribu kunichunguza ila dawa yake ipo jikoni.”.
“Ah! Kama ipo jikoni usisubiri mpaka ikachemka sana, itapoteza uhalisia”
Walimaliza maongezi yao, jenerali David akakata simu na kuelekea chumba alicholazwa Alex Sr. “Anaendeleaje?” aliuliza baada ya kuingia ndani humo, “anaendelea muda si mrefu fahamu zitamrejea, vipi tumuache hivi hivi au?” aliuliza tabibu aliekuwa anamshughulikia. “Kama munataka kufa muacheni hivyo hivyo. Akifumbuwa macho tu mumeumia” alionya jenerali David. Yule tabibu kusikia hivyo tu akawafanyia ishara wenzake wamafungue kwa mikanda maalum iliokuwa pembeni ya kitanda hicho. Hiyo ndio ilikuwa pona pona yao, ile wanamaliza tu mkanda wa mwisho. Alex Sr alifumbuwa na kuanza kufurukuta. Japo umri wake ulikuwa mdogo lakini mishipa mikuwa ya shingi ilionekana vizuri kabisa na hiyo ilikuwa ni ishara tosha kuwa mtoto huyo alikuwa na hasira.
Baada ya purukushani za dakika kadhaa walifanikiwa kumchoma sindano ya usingizi, “tungechelewa tu ingekula kwetu” aliongea mmoja kati ya wasaidizi waliokuwemo chumbani humo. “Apewe maji tu yenye virutubisho kwa njia ya dripu na kila atakapoamka mdungeni sindani nyingine ya usingizi” alitoa maelezo jenerali David na kutoka ndani ya chumba hicho. Moja kwa moja ofisini kwake, alipokaa kwenye meza alinyanyua simu nyingine na kupiga. “Mumefikia wapi?” aliuliza ilipopokewa, “tunakaribia kambi ya kubwa ya bahari ya Pasifiki” upande wa pili ulijibu.
“Vizuri, mutakapomfikisha huyo mkabidhini kwa Meja Akira atajuwa cha kufanya” alitoa maelekezo mengine na kukata simu. “Ndege wawili kwa jiwe moja” alitabasamu, alitoka ofisini kwake na kuelekea chumbani kwake ambako alioga na kujipumzisha kwa ajili kuendelea na mpango unaofata. Jenerali David kada mkubwa wa kikosi cha waasi kilichojulikana kama “THE REVOLUTIONARIES”. Wakati huwo alikuwa akihudumu kikosi maalum nchini marekani lakini alikuwa ni bweha ndani ya ngozi ya kondoo. Kwa nje alionekana mwenye uzalendo na nchi na alifnya kazi yake kama kawaida. Ila ndani ya sura ya uzalendo kulikuwa na siri kubwa ya uasi na moja kati ya malengo yake ilikuwa ni kutumia jeshi la nchi hiyo kuunda kikosi ambacho kingemtii bila kuuliza.
Kiza kiliingia, alitoka chumbani kwake na kuenda katika chumba kingine. Aliingiza neno la siri na mlango ukafunguka. Aliingia ndani ya chumba hicho ambacho hakikuwa chumba bali ni koridoo ndefu sana, mwisho wa koridoo hiyo kulikuwa na mlango mwengine. Aliufungua na kuingia, “nilikwambia nikitaka langu huwa nalipata kwa njia yeyote ile” aliongea akikaa kwenye kiti. Mbele yake kulikuwa na mtu mwengine, “mi najuwa ukitaka lako unalipata lakini ipo siku ulolipigania kwa nguvu zote litakutokea puani” alijibu mtu huyo. “Hahaha! Hebu jiangalie kwanza, nchi yako mweyewe haijafatilia kifo chako. Mke wako nimemuua na watoto wako nimewafanya kuwa mashine za kuulia. Jason CJ, nilikwambia ungana na mimi ukaona natania. Yeyote atakaekataa kuniunga mkono atapotea kama utakavopotea wewe leo” aliongea jenerali David.
“David kuna jambo wewe hulitambui kuhusu binaadamu na jambo lenyewe ni upendo. Upendo ni silaha kubwa ya binadamu na niamini, ni bora Alex mkubwa unaweza kumdhibiti. Ila siku Alex mdogo akikuponyoka basi maisha yako hapa duniani yatakuwa yanakaribia ukingoni. Kwanini nasema hivyo, Alex mdogo amezaliwa na tatizo fulani hivi la kisaikolojia, Blood Lust Syndrome au Vampire Syndrome. Tatizo hili humfanya apoteze akili pale anapoon damu, tofauti na ilivyozoeleka kuwa kuna watu wanaogopa damu (Blood phobia). Kwa Alex mdogo ni tofauti, yeye anapenda damu na akiiona ndiyo anahisi yuko hai. Alex mkubwa ndie mtu ambae alikuwa akimuweka chini ya udhibiti muda wote na kwasasa umewatengenisha bila kufahamu kuwa hilo ndio kosa lako kubwa katika maisha yako yote ulilowahi kufanya, kwanini iwe hivyo?” alinyamza na kutabasamu kidogo
“David kuna jambo wewe hulitambui kuhusu binaadamu na jambo lenyewe ni upendo. Upendo ni silaha kubwa ya binadamu na niamini, ni bora Alex mkubwa unaweza kumdhibiti. Ila siku Alex mdogo akikuponyoka basi maisha yako hapa duniani yatakuwa yanakaribia ukingoni. Kwanini nasema hivyo, Alex mdogo amezaliwa na tatizo fulani hivi la kisaikolojia, Blood Lust Syndrome au Vampire Syndrome. Tatizo hili humfanya apoteze akili pale anapoon damu, tofauti na ilivyozoeleka kuwa kuna watu wanaogopa damu (Blood phobia). Kwa Alex mdogo ni tofauti, yeye anapenda damu na akiiona ndiyo anahisi yuko hai. Alex mkubwa ndie mtu ambae alikuwa akimuweka chini ya udhibiti muda wote na kwasasa umewatengenisha bila kufahamu kuwa hilo ndio kosa lako kubwa katika maisha yako yote ulilowahi kufanya, kwanini iwe hivyo?” alinyamza na kutabasamu kidogo.
“Kuna neno lolo alililoongea Alex mkubwa kabla hujawatenganisha” aliuliza Jason CJ, “alisema maneno fulani ya kitoto hivi” alijibu jenerali David. “unaweza kuniambia”, “alisema, Alex fanya kama walivyosema, ipo siku utakuwa muuaji mkubwa sana na utawarudia kuja kulipa kifo changu” aliyarudia maneno ya Alex mkubwa. “David, umekwisha” alionge Jason CJ na kutabasamu kisha akatoa pumzi ndefu sana, “nimekw…” kabla hajamaliza kuuliza swali lake alimshudia akianguka na kutulia tuli. Aliijaribu kumtikisa lakini hakuwa na majibu yeyote, akamuwekea kidole shingoni ili kusikilizia mapigo ya moyo na hapo ndipo akagunduwa kuwa tayari mtu huyo alishaachana na ulimwenguni wa binaadamu.
Aliinuka na kutoka nje ya chumba hicho huku akikosa majibu ya mwisho ya jambo alilotaka kuuliza, jambo hilo hilo lilimchukiza sana. Alipotoka mlango wa mwisho alitoa simu yake na kuingiza nabari kadhaa akafaya kama anazipiga. Ghafla kile chumba ambacho ulikuwepo mwili wa hayati jenerali Jason CJ kikaanza kujaa gesi na baada ya sekunde chache kikawaka moto. Japo walikuwa mahasimu wakubwa lakini jenerali David hakuacha kumpa heshima ya mwisho jenerali mwenzi kwa kumpigia saluti. Ila moyo ulimuuma sana kugunduwa kuwa kuna siri kubwa kati ya Alex wawili ambayo yeye hakufahamu.
***************************************************
Miezi mitatu baadae.
Ndege ya kifahari ya binafsi ilikanyaga uwanja wa ndege maalum nchini RDC, wakashuka watu watano waliojazia kisawa sawa pamoja na mtoto na mtu mzima mmoja. Hawakuwa isipokuwa jenerali David na Alex mkubwa, “uwe na heshima, ndio maana sijakufunga pingu wala sijakuleta ukiwa hujitambui” aliongea jenerali David. Alex mkubwa akatikisa kichwa kuashiria kukubaliana nae, walitoka nje wa uwanja huwo na kukuta msafara mkubwa ukiwasubiri. “Karibuni RDC, alifikia mtu mmoja na kuwakaribisha, “ahsante” alijibu jenerali David. Yule jamaa akawafanyia ishara ya mkono wamfuate mpaka kwenye gari iliokuwa pale kwa ajili yao, wakaingia na safari ya kuelekeo mafichoni ikaanza.
Saa mbili baadae waliwasili katika kambi kubwa ya kijeshi, kwa nje ilionekana kama ni kambi ya jeshi la serekali lakini ilikuwa ni kambi ya waasi waliokuwa wakijiandaa kufanya mapiduzi. Matvei alikuwa nje akiwasubiri, waliposhuka alionesha tabasamu. “Karibu David” aliongea, “ahsante, yametukuka mapinduzi”. “Yametukuka mapinduzi” Matvei nae alijibu na kwa pamoja wakakunja ngumi na kuigandamiza vifuani mwao. “Huwo ndio mzigo wenyewe” aliuliza Matvei akimuangalia Alex mkubwa, “ndio huwo” alijibu jenerali David.
“Ana macho makali sana ya chui na muonekana wa baridi mithili ya nyoke, huyu mtoto hafai kuwa mwanajeshi bali ni muuaji kama izraeli” aliongea Matvei na kutabasamu. “Hata mimi nililitambuwa hilo”, “kabla ya yote tumpeleke kile chumba cha sobibo kwanza ili akatawadhwena kutoka akiwa mpya na msafi” aliongea Matvei na kuinuwa mkono, walifika watu kadhaa na mitutu kisha safari ya kuelekea chumba cha sobibo ikaaza. Wakiwa njiani, Matvei na jenerali David walizungumza mambo mengi sana hasa kuhusiana na mpango wao wa kupinduwa serekali zote za dunia.
Mwendo wa dakika kumi waliwasili nje chumba, juu kilikuwa na maandishi makubwa yaliondikwa SOBIBO. Wale watu waliokuwa wakisindikiza msafara walimshika Alex Sr kwa nguvu na kuingia nae ndani ya chumba hicho. Kisha wakamuweka kwenye kiti cha chuma na kumfunga kwa mikanda maalum, walipohakikisha kila kitu kipo sawa wakatoka na kupiga saluti kwa Matvei. Aliipokea na kuwaruhusu waondoke, kisha yeye na jenerali David wakaingia ndani ya chumba hicho kwa ajili ya kuanza kazi ya kumtawaza kijana Alex Sr.
“Hatuwa ya kwanza tunamvunja kisaikolojia kwa mateso makali sana, yaani tutamsukuma mpaka atamani kufa kifo cha aina yeyote ile. Halafu tunamsafisha kichwa kumfuta kumbukumbu kwa kutumia mawimbi makali sana ya umeme” aliongea Matvei. Jenerali David hakuongea kitu, alivuta kiti na kukaa ajionee kama Alex Sr atafanikiwa kutoka akiwa ndani ya chumba hicho. Watoto wengi safari yao iliishia ndani humo na kuelekea upande wa pili wa maisha.
Bila kuchelewa mateso makali sana yalianza, mara kadhaa Alex Sr alizimia kutokana na maumivu aliokuwa akiyapata. Alipozinduka mateso yaliendele tena kwa kasi mpya kabisa, “huyu mtoto ni balaa kwa kweli. Masaa matatu bado hajavurugika” aliongea Matvei na kutabasamu, “lakini mimi ndio ninaowapenda hawa” alimalizia na kuendelea kumsulubu kijana mdogo kabisa. Baada ya takriban saa sita hivi, Alex Sr akawa tayari amevunjika kisaikolojia na kuomba kuuwawa huku akisema hawezi tena kuvumilia mateso. “Niuwe tu” hilo ndio neno pekee lililokuwa likitoka kinywani mwake.
“Hata kwa kukuta kiungo kimoja kimoja” aliuliza Matvei, “ndio” Alex Sr alijibu. Matvei akatabasamu baada a kuona matunda ya kazi yake. Akasogea kwenye meza iliokaribu na kuchukuwa kofia fulani hivi ya chuma. Alirudi nayo alipokuwa Alex Sr na kumvalisha kisha akaiwasha, pembeni ya kofia ulionekana mchoro kama wa betri ambayo ilikuwa ikijichaji. Dakika kumi, ule mchoro ulikuwa umejaa. Matvei akabonyeza kitufe fulani kwenye rimoti ndogo aliokuwa nayo mkononi. Mawimbi makali sana ya umeme yaliachiwa kutoka kwenye kofia hilo na kusafiri kwa kasi ya hali katika ubongo wa Alex Sr, hali iliomfanya mtoto huyo kutetemeka huku ute mzito mweupe ukimtoka mdomoni na mboni za macho kutoweka.
Matvei akabonyeza tena kitufe kwenye kirimoti chake na lile kofia likaacha kutoa mawaimbi ya umeme, akamvua na kulirudisha mezani. Wakati Alex Sr alikuwa kapoteza fahamu na Matvei hakutaka kufanya haraka ya kumuamsha. Akamuacha mpaka alipozinduka mwenyewe, aliangaza huku na kule kwa macho yake mazito yaliopitisha mwanga hafifu sana. “Unaitwa nani” alisikia swali, “jina langu ni… ni..” hakulikumbuka. “Wewe ni mwanaume au manamke” swali jingine lilifuata, “mimi ni..” nalo pia akashindwa kujibu. Maswali yaliendelea lakini hakuwa na jibu hata la swali mmoja, si hilo tu mpaka baadhi ya maneno aliyasahau. Alikuwa kama mtoto aliekuwa akijifunza kuongea.
Matvei baada ya kuona kila kitu kimekamilika, akasogea mlangoni na kugonga. Mlango ukafunguliwa na watu wawili wakaingia. Walikwenda alipo Alex Sr na kumfunguwa kisha wakamnyanyu na kumtoa chumbani humo. Akapelekwa bafuni ambako aliogeshwa kwa maji ya baridi sana kisha akavalishwa nguo nyingine na kuungana na watoto wenzake waliokuwa katika kambi hiyo. Hawakukaa sana, wakafika Matvei na jenerali David. “Watoto hamjambo”, “hatujambo, yametukuka mapinduzi” wote kwa pamoja isipokuwa Alex Sr peke yake walijibu. “Leo tumepata mgeni na atakuwa na sisi kwa muda mrefu sana. Mpeni kitabu achague jina lake maana bado hana jina” aliongea Matvei.
Akafika mtoto mmoja akiwa na kitabu kikubwa kiasi na kumkabidhi, lakini Alex Sr hakukipokea. Yule mtoto akataka kumlazimisha akichukue lakini akagoma, basi akakiweka pembeni. “Ni lazima uchague jina na sio hiyari yako” aliongea mtoto huyo ambae kiumri alionekana mkubwa kuliko wenzake huku akimkwida Alex Sr. Hilo ndio kosa alilofanya, mwili wa Alex ulifanya kazi wenyewe bila amri kutoka kwenye ubongo kwasababu haikuwepo. Alimshika mkono kwa nguvu na kuutoa kwenye shati yake, kisha akamtandika kichwa na kumrudisha nyuma. “Usithubutu kunigusa” alifoka, yule alirudi tena akiwa kavimba kwa hasira. Kwa kutumia muhimili wa kati wa mwili wake (kiuno), Alex alizunguka kwa kasi ya ajabu na kuvurumisha mateke manne mfululuzo yaliongea maeno tofau tofauti ya mwili. Yule mtoto mwengine alianguka na kupotoza fahamu.
Askari waliokua wakisimamia walimvamia kwa nguvu na kumlaza chini, Matvei akatabasamu na kuondoka eneo hilo. Alijuwa kabisa amepata mashine ya kuulia, wakati anapambana na mwenzake, Matvei alikuwa makini sana kuangalia mashambulizi yake lakini akagunduwa kuwa kila shambulizi lililotoka lilikuwa na harufu ya kuuwa tu
Askari waliokua wakisimamia walimvamia kwa nguvu na kumlaza chini, Matvei akatabasamu na kuondoka eneo hilo. Alijuwa kabisa amepata mashine ya kuulia, wakati anapambana na mwenzake, Matvei alikuwa makini sana kuangalia mashambulizi yake lakini akagunduwa kuwa kila shambulizi lililotoka lilikuwa na harufu ya kuuwa tu.
*********************************************************
Miaka kumi na nane baadae
Mr Nobody (Alex Sr) akiwa ndani ya bar moja hivi, mjini Gwangzhou nchini china. Alikuwa akipanda mvinyo baridi uliosindikizwa miziki mbali mbali ya kimataifa na ya kichina. Jina lake hilo la Mr Nobody amelipata baada ya kukataa kuchaguwa jina moja kati ya majina yaliokuwemo kwenye kitabu cha majina alichopewa wakati anajiunga na kambi ya Matvei. Hivyo Matvei mwenyewe akaamuwa kumuita Nobody akiwa na maana mtu huyo hayupo hasa. Baada ya miaka mingi ya mafunzo hatimae alianza kupewa kazi ndogo ndogo, kazi hizo zikalipaisha jina lake mpaka watu wakubwa waliojiiita madon wakamjuwa.
Siku hiyo alikuwa katika kazi maalum nchini China, akitambulika kama mtu asie jina, Mr Nobody alikuwepo mjini Gwangzhou kwa ajili ya kufanya kununuwa chemikali maalum kutoka kwa mwanasayansi mmoja wa kimarekani. “Kumbuka watu unaokwenda kufanya nao biashara ni mafia, na watu hawa hawachelewi kukugeuka” aliakumbuka maneno ya Matvei. Akamalizia mvinyo wake kwenye gilasi na kuondoka kaunta. Kisha akaelekea gorofani ambako ndipo watu aliokwenda kukutana nao walipandisha.
Kwa mwendo wa taratibu alipandisha ngazi mpaka juu, alifika katika chumba walichokubaliana na kukutana na walinzi nje. “Hurusiwi kuingia na silaha ndani” aliongea mlinzi mmoja, alitabasamu na kuingiza mkono nyuma ya koti lake. Wale walinzi kuona wakataka kutoa bastola lakini wakasita pale walipoona akitoa bastola mbili na kuwakabidhi. Kisha akajipapasa pande zote mbili za kiuno, kulia na kushoto na kutoa bastola nyingine mbili. Baada ya hapo akavua koti lake la juu, hapo ndipo waliposhangaa. Maana koti hilo kwa ndani lilijaa magazine za risasi, aliwakabidhi kisha akatabasamu na kuinama. Akashusha soksi na kuchomoa kisu kidogo na kuwakabidhi.
“Hizo ndio silaha zote nlokuwa nazo” aliongea hukua akiendelea kutabasamu, wale walinzi walijikuta wakimeza mate kwa pamoja. Kisha mmoja wao akafunguwa mlango na kumruhusu aingi, “karibu sana” aliongea mzee mmoja aliekula chumvi kiasi. “Nimekaribia” alijibu Mr Nobody na kukaa kwenye kiti, “natumai umepewa maelezo na jinsi tunavyofanya kazi” kiliongea kile kibabu cha kimarekani. “Ndio nimepewa na pia nimeambiwa nyie ni wakorofi sana na hamuchelewi kuwageuka wateja wenu” alijibu Mr Nobody na kumuangalia. Kibabu kikalazimisha tabasamu japo maneno yale yalimkera kiasi, “tunageuka tunapoona kuna haja ya kufanya hivyo” kilijibu.
“Nionesheni mzigo, sina muda mwingi hapa” aliongea, kile kikainuwa mkono akafika mtu akiwa na briefcase na kumkabidhi. Kile kibabu kikabonyeza sehemu, ukatoka mwanga kidogo, akasogeza jicho ule mwanga ulikuwa mwekundu lakini baada kile kibabu kuweka jicho, ukabadilika na kuwa kijani kisha ile briefcase ikafunguka. Ukatoka moshi kiasi ambao ulikuwa ni wa baridi, “mzigo huu hapo” aliongea na kumgeuzia Mr Nobody. Alipojiridhisha akatoa simu yake na kupiga, “nimeuona, unaweza kutuma pesa sasa” aliongea punde tu ilipopokewa upande wa pili. Kisha akakata na kuiweka mezani, “baada ya sekunde kumi angalia simu yako” aliongea na kuegemea kiti chake.
Sekunde kumi zilipotimia, simu ya kile kibabu ikatoa mtikisiko fulani. Aliifunguwa na kuangalia “hamisho la fedh limekamilika, umepokea jumla ya dola za kimareka milioni mia moja kutoka kwa Mr Nobody” ulisomeka ujumbe huwo kwenye kioo. Kikatabasamu na kusimama, Mr Nobody nae akasimama wakapeana mikono. Mr Nobody akatoka nje na kuchukuwa dhana zake kisha akaanza kushusha ngazi kuutafuta mlango wa kutokea. Wakati anatoka ghafla akahisi hai ya hewa ya pale chini imebadilika, hata hivyo hakujali akaendelea kupiga hatuwa kuelekea mlango mkubwa wa kutokea nje.
“Oya! Simama” alipoukaribia mlango akapigiwa kelele, akasimama bila kugeuka na kushusha pumzi ndefu. “Acha hilo briefacase hapo mlangoni ndio utoke” sauti ile iliendelea, “hapana siwezi kufanya hivyo labda kama nine briefcase jingine, lakini kama ni hili nililoshika hapa. Kwa kweli siwezi kufanya hivyo” aliongea. “Mwana mdogo una jeuri si ndio” ile sauti iliongea kwa ukaribu zaidi na huyo mtu akamshika begani. Mr Nobody aligeuka kwa kasi mkononi akiwa na bastola ambayo moja kwa moja aliizamisha mdomoni kwa mtu huyo na bila kusita akafyetuwa risasi na kumchawanya kinywa.
Kelele zikazuka ndani ya bar hiyo na papo hapo vurugu likaanza, kabla hawajaanza mashambulizi wakashangaa kuona Mr Nobody akiwa katoweka eneo hilo pasi a kutambulika ameelekea wapi. “Pumbavu sana nyinyi, mumempoteza munajuwa ile kemikali ina faida kubwa nda ndio fomula iliobakia” kiliongea kile kibabu. “Hata sisi hatujui ni kimetokea, kila kilifanyika haraka haraka” aliongea mtu mmoja kati ya wale waliopewa kazi ya kulirudisha lile briefcase. Wakati wakiendelea kubishana ghafla simu ya kile kibabu ikaanza kuita, namba haikuwa na jina. Aliwapa ishara wanyamaze ili aipoke, “hello” aliongea.
“Nimekuachia zawadi ndogo sana hapo mezani, nilitegemea kama ungesimama kweye makubaliano lakini ukaamuwa kuonesha umafya wako” uliongea upande wa pili. Kile kibabu kikaangaza meza na kukuta kidude kidogo sana mithili ya kifungo cha shati, “wasalimie” upande wa pili ulimaliza na kukata simu. “Shit! Tumekw” kabla hajamaliza mlipuko mkubwa sana ukatokea na kulisambaratisha jengo zima, raia wa kawaida wengi pamoja kikosi cha kibabu kizima wakakutwa na mlipuko huwo na kupoteza maisha. Mr Nobody akiwa mita mia kutoka eneo la tukio akarudisha simu yake mfukoni na kutokomea pasipojulikana.
Siku iliofuata mapema sana Mr Nobody aliwasili nchini RDC na kuukabidhi mzigo kwa Matvei, “Kazi nzuri sana” aliongea na kutabasamu. Alivuta brifcase jingine na kumkabidhi, “kuna ameomba kufanyiwa kazi na kwenye hilo briefcase kuna malipo na maelezo ya kazi hiyo. Ameomba iwe imekamilika ndani y a masaa sabini na mbili” aliongea Matvei. “Hakuna shika nitaifaya kesho” aliongea na kuondoka, moja kwa moja akaelekea nyumbani kwake. Aliliweka lile briefcase kwenye meza kuelekea chooni kwa ajili ya kufanya usafi wa mwili.
Akiwa bafuni alifunguwa bomba la mvua na kuacha maji yaulowanishe mwili wake, aliegemea ukuta na kugubikwa na msongo wa mawazo. Matukio yote aliowahi kuyafanya yalirudi kichwani mwake kama treni ilikosa brek. Jambo hilo lilisababisha kichwa kumuuma na kujikuta akikaa chini bila kupenda, naaam ndiyo hivyo. Kuoga kwa Mr Nobody ndio wakati mgumu sana kwake, kwasababu anakuwa amerelax. Katika matukio yote kuna tukio moja humjia ambalo ana uhakika hajawahi wa kulifanya. Katika tukio hilo anakuwa na bishana mtoto mdogo huku mtoto huyo akililia viatu vyake. Baada hutokea mzee mmoja kumuita “Alex Jr, viatu vya kakaako havikutoshi” halafu wote hucheka na kuonekana kuwa na furaha sana.
Alimaliza kuoga na kutoka bafuni humo, akaelekea chumbani kwake na kuvaa nguo jingine kisha akajilaza kitandani kwa ajili ya kupumzika. “Alex Sr kimbia, uko hatarini” alisika sauti, aligeuka upande ilipotokea na kukuta watu watatu. Watu wazima wawili na mtoto mmoja, “kaka kimbia eneo hili si zuri” aliongea mtoto yule na kumfat na kutaka kushika mkono. Ghafla Mr Nobody akakurupuka kutoka usingizini na kusikia mlio fulani hivi. Akageuka upande ulipokuwa unatokea na kukuta lile briefcase alilopewa linawak taa nyekundu. “Kaboom” Matveo akiwa ofisini kwake na kirimoti kidogo alisema neno hilo na kukibonyeza. Mlipuko mkali sana ukatokea nyumbani kwa Mr Nobody sekunde chache baada ya kushuhudia kile kitaa. Na huwo ndio ukawa mwisho wa Mr Nobody, mwili wake hakukutwa eneo la mlipuko kutokana na mlipuko kugeuza kila kitu majivu. Ila katika majivu yalokusanywa na kikosi cha Matvei walikuta vinasaba vinavyohusiana na Mr Nobody au Alex Sr.
Alimaliza kuoga na kutoka bafuni humo, akaelekea chumbani kwake na kuvaa nguo jingine kisha akajilaza kitandani kwa ajili ya kupumzika. “Alex Sr kimbia, uko hatarini” alisika sauti, aligeuka upande ilipotokea na kukuta watu watatu. Watu wazima wawili na mtoto mmoja, “kaka kimbia eneo hili si zuri” aliongea mtoto yule na kumfat na kutaka kushika mkono. Ghafla Mr Nobody akakurupuka kutoka usingizini na kusikia mlio fulani hivi. Akageuka upande ulipokuwa unatokea na kukuta lile briefcase alilopewa linawak taa nyekundu.
“Kaboom” Matveo akiwa ofisini kwake na kirimoti kidogo alisema neno hilo na kukibonyeza. Mlipuko mkali sana ukatokea nyumbani kwa Mr Nobody sekunde chache baada ya kushuhudia kile kitaa. Na huwo ndio ukawa mwisho wa Mr Nobody, mwili wake hakukutwa eneo la mlipuko kutokana na mlipuko kugeuza kila kitu majivu. Ila katika majivu yalokusanywa na kikosi cha Matvei walikuta vinasaba vinavyohusiana na Mr Nobody au Alex Sr.
******************************
TURUDY KATIKA WAKATI ULIOKUWEPO.
“Ni hivi tutakuwa na jumla ya vikosi nane viyakavyofanya kazi chini makomanda tofauti, kikosi cha kwanza kitahusisha mashine zitakazokuwa zinaendeshwa kwa kutumia kompyuta. Hasa hasa kikosi hiki kitahusisha gari zilizowekwa silaha nzito za maangamizi, kitakuwa chini kamanda Talbot akisaidiana na msaidizi kamanda Emelda. Kikosi cha pili kitakuwa ni cha angani, hiki kitahusika na kuharibu silaha nzito na kufanya kazi kama jicho letu katika maeno ambayo yatakuwa nivigumu ya kuyaona. Kikosi hiki kitakuwa chini ya mfalme wa anga kamanda Alfred akisaidia na msaidizi kamanda Loveness. Kikosi cha tatu kitakuwa cha waenda kwa miguu juu ya ardhi, hichi kitafuata kwa mita chache myuma ya kikosi cha kwanza. Kitahusisha wataalamu wa kutumia silaha za aiana zote pamoja wataalamu wa vita vya ana kwa ana. Kitaongozwa na kamanda Kelvin Bull akisadiana na msaidizi kamanda Sweety”.
“Kikosi cha nne kitakuwa cha waenda kwa miguu wa chini ya ardhi, nahichi pia kitahusisha wataalamu wa silaha za moto na vita vya ana kwa ana. Hichi kitaongozwa kamanda Aneth Spin akisaidiana na msaidizi kamanda Eugine. Kikosi cha tani kitakuwa ni wadunguaji wa masafa ya kati (M.R.S), hichi kitaongozwa na Kamanda Jesca She Beast akisaidiana na msaidizi kamanda Shey, kazi yao itakuwa ni kuhakikisha usalamawa kikosi namba tatu. Kikosi cha tano kitakuwa ni cha wadunguaji wa masafa marefu (L.R.S), kitaongozwa na kamanda Charlie Beast akisaidia na msaidizi kamanda Ghulam na kazi yao itakuwa ni kuwawinda wadunguaji wa maadui zetui. Kikosi cha saba ni Special Force, hichi hakitakuwa kamanda kwasababu wote ni makamanda. Kitwahusisha Gold Prime General Killer Alex Jr, Chief General Supreme Commando Death (awali akitambulika kama Ghost) Jeff Alfred na Silver Fox General Shadow Adrian. Hawa watashughulika na visiki vitakavyothibitisha ni vigumu kupitika. Kwa maneno mengine watapambana na majenerali wa maadui zetu”.
“Kikosi cha nane kitakuwa HQ (Headquater) kikosi hiki kitakuwa chini yangu mimi, Kamanda Mark nikisaidiana na msaidizi Janeth Brain. Sisi tumepewa amri na Supreme general kuangalia vita nzima nakubadilisha majukumu pale panapohitajika. Tutatoa amri kwa vikosi vyote isipokuwa kikosi cha nane tu, hichi kitafanya kazi kwa vile kinavyoona inafaa kufanywa. Kikosi changu kitakuwa na vikosi vingine vidogo vidogo ndani yake, kutakuwa na kikosi cha mtandao (Cyber army) kitakachoongozwa na Martina. Kikosi cha matabibu kitachoongozwa na Anitha, kutakuwa na kikosi cha wakimbiaji (runners) kitakuwa kikosi kinachoingia katika uwanja wa vita na kutoka kwa kazi tofauti hasa kwa kuleta silaha”
Alimaliza kuongea Luteni jenerali Mark na kuwaangalia wanajeshi wote waliokuwa mbele yake, akageuka na kupiga saluti kwa wakubwa zake. Akarudi sehemu yake na kusimama, Supreme jenerali Alex Jr akapita mbele, “mimi sitaongea kitu hapa, kuhusiana na mipango ya kivita yote tumewaachia HQ. Cha msingi ni kutambuwa kwamba si kila atakaekwenda vitani atarudi salama. Kuna ambao tutawapoteza na kuna ambao watapoteza viuongo vya lakini tunapaswa kukumbuta bila kuwepo kwa kafara hakutakuwa na ushindi. Kama utaweza kupigana pigana hadi mwisho wa uhai wako, ukikatika mkono tumia mkono mwengine, ukikatika mguu tambaa. Hatujui tutarajie nini kwenye vita hii dhidi ya nguvu tusioitambuwa uwezo wake” aliongea na wanajeshi wote wakafunga mguu na kupiga saluti. Sura zao zilitosha kusema kuwa hawakuja hapo kurudi nyumbani, walikuwepo hapo kuhakikisha waliowaacha nyumbani wanaishi kwa amani.
******************************
“Kila kitu kinakwenda kama nilivyopanga” aliongea Michael akichezea nywele za Alice, walikuwa kitandani ndege hao wawili. “Ushindi ni wetu lakini tusiwadharau wale watatu. Na naamini unajuwa namaanisha kina nani” aliongea Alice akijivuta na kulala kifuani kwa Michael. “Nimetilia maanani kila kitu, sitaki yatokee makosa yeyote yale wakati wa vita. Hawataona kitakachowakumba bali kitaacha matundu kwenye mioyo yao” alijibu Michael. “Sawa mi nakuamini, hujawahi kufanya makosa kwenye hesabu zako” aliongea Alice na kumbusu Michael mdomoni kisha akashuka kitandani.
“Kila kitu kipo sawa” aliongea Matvei, “tuna vikosi vitano tu, kikosi cha kwanza kitahusisha silaha nzito. Hapa nakusudia vifaru, ndege na gari za kivita. Kikosi cha pili kitahusisha wanajeshi wa kawaida, watakuwa mstari wa mbele. Kikosi cha tatu kitahusisha NGSS (next generation super soldiers), kitafuata nyuma ya kikosi cha watu wa kawaida, kikosi cha nne kitahusisha wadunguaji na cha tano ni special force” akaeleza mpango wake. “Hapo sijaona mpango wa vita” akaongea Jason CJ Sr, “mpango wa kivita utakwenda na kubadilika kutokana na aina ya mashambulizi tutakayopokea kutoka kwa adui zetu” alijibu.
Majenerali hatari watano walikuwa mezani wakipitia muhtasar mzima wa vita ambayo waliipa asilimia mia moja za ushindi. Alfred Jackson, Jason Cj, Alex Sr, Matvei na Andrew Cross, wakongwe hawa wa kivita hawana historia ya kushindwa hasa katika ulingo wa kivita. Waliamini katika ushindi wa kishindo kikubwa sana (total Victory). Enzi za uhai wao hawakuonja neno kushindwa mpaka vifo vilipowakuta na wote walikuwa wakiwa na amaini kabisa. Lakini sasa vivuli vyao vimerudi kuja kupambana na wale ambao kipindi chau uhai wao walikuwa wakiwalinda.
Michael alitoka chumbani kwake akiwa kashajiandaa, alikuwa amevalia gwanda maalum nyeusi zilizokuwa zimejaa vyeo vya kujitunuku. Wakati huwo alijihisi kama Mungu, alipoingia tu ukumbini wanajeshi wote waliacha kazi wanayofanya na kuinuwa ngumi zao juu kisha wakaziegemeza upande wa kushoto na kwa pamoja wakasema “yametukuka mapinduzi”. Michael akatabasamu na kupokea salamu hiyo kama kiongozi wa waasi.
“Ule wakati ambao tulikuwa tunausubiri kwa kipindi kirefu sasa umefika, ile ahadi niliowapa sasa iko mbele ya mikono yenu. Ni juu yenu kuishika au kuiacha iende, kabla hujaingia vitani kumbuka walikufanya nini ulipokuwa ukipigania haki yako. Kwasababu walipewa mamlka hayo walidhani wako sahihi. Mi nasema walikosea kuwafanyia vile, kwasababu si kila anaeshika silaha ni gaidi bali wengine watetea haki zao kwa njia mbadala maana njia ya amani ilishindikana. Wauweni mpaka roho zenuziridhike, watendeeni kama waliokutendeeni. Baada ya vita hii, hakutakuwa na sheria wala dini. Kila mtu atafanya kile kitu ambacho roho yake inapenda. Waacheni walimwengu wale matunda walioyapanda kwenye vifua vyetu kwasababu kila mtu ana haki hiyo” alimaliza kuongea na kutabasamu baada ya kuona mikunjo ikitokea kwenye nyuso za watu wake, wanawake kwa wanaume.
********************************
Congo, DRC.
“Inaonekana Michael au nikuite kwa jina lako halisi” aliongea mtu mmoja na kutabasamu, Aliinuka kutoka kitandani alipokuwa amelala na kushika bega la upande wake wa kulia ambalo halikuwa na mkono. “Ulidhani katika dunia hii mwenye akili ni peke yako, hahah! Umeumia tokea ule wakati ulioamuwa kucheza na nyoka ukiamini umemdhibiti” aliendelea kuongea na kuvua shati lake. Mgongoni alikuwa na alama kubwa ya X, juu karibu na bega kulikuwa kumeandikwa maandishi madogo yaliosomeka “Project”, PROJECT X. Alivaa shati nyingine na kofia, kisha akainuwa kitanda na kufunuwa sehemu fulani kwenye sakafu. Akatoa brief case kubwa kiasi na kuliweka mezani kisha akalifunguwa, “muda umefika sasa wa kurudi kazini” alijisemea akiangalia silaha zake zilizopangwa vyema kwenye briefcase hilo. Akalifunga na kulinyanyua kisha akatoka katika nyumba hiyo na kuelekea lilipo gari aina ya Jeep. “Asante Congo kwa kunilea ila nasikitika inabidi niondoke sasa” aliongea na kuwasha gari, akaweka gia na taratibu akaliondoa
Congo, DRC.
“Inaonekana Michael au nikuite kwa jina lako halisi” aliongea mtu mmoja na kutabasamu, Aliinuka kutoka kitandani alipokuwa amelala na kushika bega la upande wake wa kulia ambalo halikuwa na mkono. “Ulidhani katika dunia hii mwenye akili ni peke yako, hahah! Umeumia tokea ule wakati ulioamuwa kucheza na nyoka ukiamini umemdhibiti” aliendelea kuongea na kuvua shati lake. Mgongoni alikuwa na alama kubwa ya X, juu karibu na bega kulikuwa kumeandikwa maandishi madogo yaliosomeka “Project”, PROJECT X. Alivaa shati nyingine na kofia, kisha akainuwa kitanda na kufunuwa sehemu fulani kwenye sakafu. Akatoa brief case kubwa kiasi na kuliweka mezani kisha akalifunguwa, “muda umefika sasa wa kurudi kazini” alijisemea akiangalia silaha zake zilizopangwa vyema kwenye briefcase hilo. Akalifunga na kulinyanyua kisha akatoka katika nyumba hiyo na kuelekea lilipo gari aina ya Jeep. “Asante Congo kwa kunilea ila nasikitika inabidi niondoke sasa” aliongea na kuwasha gari, akaweka gia na taratibu akaliondoa.
RDC
Mji mzima ulikuwa kimya, watu wote walishaondolewa na kupelekwa katika makazi ya muda mfupi kuachia uwanja kwa vita iliotegemea kurundima ndani ya wakati. Kutokana na watu kukaa mbali na makazi yao, uvumilivu ulianza kuwashinda na kuanza kufanya fujo za kutaka kurudi majumbani mwao. Wengi walidai kuwa hakuna vita wala nini, ilikuwa ni mpango wa serekali tu kuwahamisha bila ridhaa yao. “Mimi nimechoka kukaa huku kama mkimbizi, wakati nina nyumba nzuri tu ya kuishi” aliongea mzee mmoja akioekana kukerwa na jambo hilo. “Mume wangu, usiwe na hasira. Kama hakutakuwa vita tutapewa taarifa na wote tutarudi majumbani” alijibu mkewe huku akimbembeleza mtoto wao mdogo wa miezi kadhaa aliezaliwa katika makazi hayo ya muda mfupi.
Hakuwa peke yake mwenye wazo hilo, watu wengi walikuwa wakiongea na kuonesha kukerwa na kitendo cha wao kuondolea majumbani mwao kwa zaidi ya miezi kumi sasa. “Jamani tunawaomba mtulie, kwa ajili ya usalama wenu” iliskika sauti kutok kwenye kipaza sauti. “Hatutaki, tunataka kurudi makwetu” alijbu mtu na ghafla zikazuka kelele. Kuna vijana wanne walikimbilia kwenye gari yao na kuanza kuelekea ndani ya mji. Walikuwa wakifurahia kuwatoroka katika wakati ambao wanatuliza zogo, walifika mpaka njia kuu ya kuingilia ndani ya mji ambako kulikuwa na bango kubwa lililoandikwa “WAR ZONE” (eneo la vita).
“Pelekeni ujinga wenu huko” aliongea dereva wa gari hiyo na kukanyaga mafuta, “tunathibitisha kuwepo kwa gari moja linaloenda katikati ya mji” aliongea mtu mmoja aliekuwa juu kabisa kwenye jengo refu la eneo hilo. “Rudia maelezo yako” aliongea kamanda Mark kutoka HQ, “narudia, nathibitisha kuwepo kwa gari inayoelekea ndani ya mji, ni gari ya raia wa kawaida” alirudi mtu. “Rodger, check point A izuieni hiyo gari lakini kuweni makini” alitoa amri kamanda Mark. “Rodger HQ” kiongozi wa check point A akaitika na kuwapa ishara wenzake. Wakaingia barabarani mkononi wakiwa na tocho waliokuwa wakiiwasha na kuizima kuelekea upande ambao ilikuwa inatokea hiyo gari. Wale vijana walipoona tochi wakacheka, “oya kama vipi wagonge tu” aliongea mmoja wao. “Mwanangu wanajeshi wale” alijibu dereva, “wakiwa wanajeshi je, gonga tu” aliogea yule mwanzake kwa ukali.
“Inavyoonekana hawana nia ya kusimama, pasua tairi” aliongea kiongozi wao, na mdunguaji aliekuwepo eneo hilo akajipanga kutekeleza amri. Lakini kabla hajafanya ulisikika mlio wa kitu kama ndege na kitendo cha kupepesa macho tu ile hari ikalipuka. “Wote kaeni tayari, HQ unanisoma”, “nakusoma, tumesikia mlipuko huko”. “Positive, gari imeripuliwa na chanzo kisichojulikana”, “kuna yeyote aliekoka”. “Negative, hakuna aliepona”, “rodger, check point A kusanyikeni sehemu salamana musubiria amri nyingine, over and out”.
Kelele y mlipuko huwo ulifika mpaka kule kwenye kambi ya makazi ya muda mfupi, “watu wote mnatakiwa murudi katika maneo yenu” sauti kutoka kwenye kipaza sauti. “Jamani watoto wangu wako wapi” aliongea mama mmoja akizunguka huku na kule. “Samahani mama tunakuomba rudi ndani kwa ajili ya usalama wako” alifika mwanajeshi mmoja na kuongea. “Siendi popote mpaka niwapate watoto wangu” aligoma kabisa. “Tumepokea taarif kuwa kuna gari ya raia wa kawaida imengia katika uwanja wa vita na bahati mbaya imekutwa na mashambulizi. Miili ya vijana wanne imekutwa eneo la tukia, na kutokana na masalia tumefanikiwa kumtambuwa mmoja, Jonathan Frank” sauti ilisikika tena kwenye kipaza sauti. Yule mama kusikia hivyo alianguka na kupoteza fahamu.
**********************************************
“Vikosi vyote nipeni taarifa” aliongea kamanda msaidizi wa HQ, Brain. “Mimi ni kamanda wa kikosi cha technowar (TW), kila kipo sawa kwangu” aliongea Talbot, “Kamanda wa kikosi cha anga, Sky War (SW). Naona kikosi cha watu kutokea kusini mashariki” alitoa taarifa Alfred. “Rodger endelea kuwafatilia” aliongea Brain. “Kamanda Kelvin wa kikosi cha juu ya ardhi (GW), kila kitu kipo sawa”, “Kamanda Aneth Spin, kikosi cha chini ya ardhi, kila kitu kipo sawa”. “Msaidizi kamanda Shey wa kikosi cha wadunguaji wa masafa ya kati (Mid range snipers (MRS)) kil kitu safi”, “msaidizi kamanda Ghulam wa kikosi cha wadunguaji wa masafa ya mbali (Long range Snipers (LRS)), na sisi pia tunaona kikosi kikija kutokae kusini mashariki”. “Rodegr endelea kukifatilia” kila kikosi kiliwasilisha taarifa yake kwa wakati na kukaa tayari kwa kupambana na yeyote atakae kuja mbele yao.
Wakati kila mmoja akiwa anajizatiti, ghafla yakapita makombora kadhaa na yalikuwa yalikuwa yakielekea makao makuu ya BHGP. “HQ, makombora kadhaa yamepita kuelekea huko” aliongea Alfred akiwa tayari kusibiria amri ya kuyazuia. “Hata huku tayari tumejuwa, ila hayo ni mashambulizi matupu. Wanafanya hivyo kutaka kutusambaratisha kiurahisi” aliongea kamanda Mark. “Kila kikosi kibaki neo lake” akatoa amri. Jambo halikugahamika kwa maadui ni kwamba ndani ya kilometa moja mpaka makao makuu ni eneo la makombora ya usalama. Kitendo cha makombora hayo ukuingia ndani ya uzio wa kilometa hiyo, yalianza kushambuliwa na kumalizwa kabla hayatuwa.
Wakati Mark akiendelea kugawa majukumu, Brain alikuwa akichezea kompyuta. Alipiga hesabu zake na kugundua sehemu yaliotoka makombora hayo. “Arobaini na mbili, kusini tatu” aliongea, “command, mabomu kumi kuelekea arobaini mbili kusini tatu” Kamanda Mark akarudia na kuweka mkazo. “Rodegr, arobaini na mbili kusini tatu, mabomu kumi yataachiwa ndani ya sekunde tatu, mbili na moja” aliitikia Martina na kubonyeza kitufe kilichoandikwa “Launch”. Makombora kadhaa yakaibuka kutoka majini na kusafiri kwa kasi zaidi.
Upande wa Michael.
“Incoming” alipiga kelele mwanajeshi mmoja, lakini alikuwa kachelewa. Makombora hayo yalituwa kwenye jengo moja kubwa kiasi a kulisambaratisha. “Inavyoonekana tumewadharau sana. Sikutegemea kama wangejibu papo kwa papo” aliongea Matvei akikuna kichwa. “Lakini lengo letu limetimia” aliingilia Jason. “Ndio sasa tunajuwa makao makuu ya kambi yao yako wapi” aliitika Matvei na kutabasamu. “Kikosi cha kwanza na cha pili kiingie kazini” alitoa amri na vifaru, ndege pamoja na ndege za kivita zikaanza kuondoka kambini. “Vita imeanza rasmi” aliongea Michael aliekuwa amekaa kwenye kiti chake.
Uwanja wa vita.
“Mimi ni kamanda Alfred wa kikosi cha SW, naomba ruhusa ya kuanza mashambulizi. Naziona ndege kadhaa mbele”, “Rodger, SW ruhusa mnayo” HQ ilijibu. “Tutafanya hii katika mfumo wangu” aliongea Alfred, “SW 1 na SW 2 mtaongoza mashamulizi, SW 3 na SW4 mtamaliza ndege yeyote ile itakayoonekana inajikongoja baada ya mashambulizi ya SW1 na SW2” alitoa amri, “Rodger” vikosi vyote vilivypewa kazi vikaitika na kuondoka kwa kasi. “Let the game begin” alijisemea na kujinyoosha, SW1 na SW2 walizivaa ndege za waasi kichwa kichwa na kuanza kujibizana kwa risasi. Marubani wa ndege hizo za pande zote mbili walionekana kujuwa nini wanafanya.
SW3 na SW4 hawakuwa nyuma, kila ndege ya waasi ilokuwa ikianguka waliimaliza kambla haijafika chini. “Kamanda, naona ndege kubwa sana inakuja kwa kasi. Ruhusa ya kufanya mashambulizi” aliongea rubani mmoja, “negative pilot, rudini kwenye formation” Alfred alikataa na kutoa amri vikosi vyake virudi. “Rodger kamanda” aliitika na kugeuza wakarudi, “taarifa, nimepoteza ndege sita. Mpaka sasa sijui kama marubani wa ndege hizo wako hai au laa, HQ rodger” alitoa taarifa. “Rodger, tutatuma watu kuelekea maeneo zilzoanguka ndege hizo kuthibitisha, HQ over and out” HQ walijibu. “Inavyoonekana wanataka vita ya nani ana vyuma vyenye kuzuia risasi” aliongea Alfred na kutabasamu. Ndege kubwa iliokuwa juu zaidi ya ndege nyingine ilianza kushuka huku ikiongeza kasi, pembeni iliandikwa “I rule the skies” (naongoza anga). Ndege hiyo kubwa yenye injini sita ilikuwa ikiongozwa na Alfred mwenyewe, “ndege zote zitakaa nyuma yangu, hakikisha hugusu na kombora hata moja la hiyo ndege. Ni hatari, over” aliongea.
SW3 na SW4 hawakuwa nyuma, kila ndege ya waasi ilokuwa ikianguka waliimaliza kambla haijafika chini. “Kamanda, naona ndege kubwa sana inakuja kwa kasi. Ruhusa ya kufanya mashambulizi” aliongea rubani mmoja, “negative pilot, rudini kwenye formation” Alfred alikataa na kutoa amri vikosi vyake virudi. “Rodger kamanda” aliitika na kugeuza wakarudi, “taarifa, nimepoteza ndege sita. Mpaka sasa sijui kama marubani wa ndege hizo wako hai au laa, HQ rodger” alitoa taarifa. “Rodger, tutatuma watu kuelekea maeneo zilzoanguka ndege hizo kuthibitisha, HQ over and out” HQ walijibu. “Inavyoonekana wanataka vita ya nani ana vyuma vyenye kuzuia risasi” aliongea Alfred na kutabasamu. Ndege kubwa iliokuwa juu zaidi ya ndege nyingine ilianza kushuka huku ikiongeza kasi, pembeni iliandikwa “I rule the skies” (naongoza anga). Ndege hiyo kubwa yenye injini sita ilikuwa ikiongozwa na Alfred mwenyewe, “ndege zote zitakaa nyuma yangu, hakikisha huguswi na kombora hata moja la hiyo ndege. Ni hatari, over” aliongea.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment