Simulizi : Behind The Curtain: September 11
Sehemu Ya Nne (4)
Kitivo cha Town Planning (Flight 11)
Baada ya waongozaji ndege ardhini kugundua kuwa flight 11 imedhibitiwa na watakaji, moja kwa moja saa 08:37 AM wakawasiliana na Northeast Air Defense Sector (NEADS) jijini New York.
NEADS wakawasiliana na kituo cha kijeshi la Anga, Otis Air Force Base kilichopo Mashpee, Massachusetts, kuomba ndege ya kivita ya F-15 kuifutilia Flight 11 na ikiwezekana kuidungua.
Baada ya mawasiliano hayo kufanyika, ndege ya kijeshi F-15 ilikuwa tayari huku ikisubiri ruhusa ya kupaa na kuanza kuifuatilia Flight 11.
Saa 08:43 AM flight 11 ilikata kona ya mwisho kuingia New York eneo la Lower Manhattan.
Saa 08:46 AM ruhusu ilitolewa kwa ndege ya kijeshi F-15 kuruka kuifuatilia flight 11 (iliruka saa 08:53 AM).
Wakati ambao F-15 inapewa ruhusa ya kuruka saa 08:46 AM, tayari Mohamed Atta alikuwa amefikisha flight 11 kwenye target..
Kwahiyo muda huo wa saa 08:46 AM, flight 11 ikiwa na abiria 81 na wahudumu 5 na ikiwa kwenye mwendo wa kilomita 748 kwa saa, na kwenye tank la mafuta ikiwa na Lita 38,000 ya mafuta… flight 11 ilibamizwa na Mohamed Atta kwenye North Tower ya World Trade Center katikati ya ghorofa ya 93 na 99.
Iliua abiria wote ndani ya ndege na mamia wengine waliomo kwenye jengo.
Miongoji mwa abiriia walikufa alikuwemo Mtengenezaji wa kipindi cha televisheni cha Frasier, Bw. David Angell na mkewe Lynn Angell. Pia alikuwemo muigizaji Berry Berenson na Mtunzi wa 'Family Guy', Bw. Seth MacFarkine.
Kitivo cha Town Planning II (flight 175)
Nilieleza namna ambavyo Al-Shehhi na wenzake wa Kitivo hiki waliiteka na kuidhibiti hii ndege.
Saa 9:01AM flight ikaanza kwenda kwa kasi kushuka kwenye eneo la Lower Manhattan.
Saa 09:03 sekunde ya 2, flighg 175 kwa muelekeo ilikuwa inaonekana kana kwamba itajibamiza kwenye jengo la 'Empire State' lakini ilikata kona kali ghafla na kwenda kujibamiza kwenye South Tower ya World Trade Center kwa kasi ya kilomita 950 kwa saa ikilipua Lita 38,000 pia zilizokuwamo kwenye tank na kuua abiria wote 56 na wahudumu 9 waliokuwamo kwenye ndege na mamia wengine waliokuwemo kwenye jengo.
9112.jpg
Flight 175 ikiendeshwa na Marwan al-Shehhi ikikaribia kujibamiza South Tower ya WTC huku pembeni North Tower ikiendelea kuteketea baada ya kulipuliwa na flight 11 iliyoendeshwa na Mohamed Atta.
Kitivo cha Fine Arts (flight 77)
(Nilieleza pia namna ilivyotekwa na Hani Njour na Kitivo chake)
Baada ya kukaribia kabisa ofisi za Pentagon, Hani inakadiriwa kuwa alikatisha kona ndege kwa nyuzi 330 kuelekea upande wa magharibi mwa Pentagon na kusafiri mita 670 kutoka juu angani kushuka chini.
Saa 09:37 AM Hani Njour aliibamiza ndege upande wa magharibi mwa Pentagon (west wing) gjorofa ya kwanza, kwa kasi ya kilomita 853 kwa saa.
Kitivo cha Law (flight 93)
(Nilieleza pia namna walivyoidhibiti)
Baada ya Ziad Jarrah na wenzake kufanikiwa kuingia kwenye chumba cha marubani inasemekana kuwa waliwajeruhi marubani na kuanza kuiondoa ndege kwenye njia yake.
Baada ya hapo; Ziad Jarrah akatoa tangazo kwa abiria, akawaambia;
"..ladies and gentlemen. Here the Captain. Please sit down. Keep quite…"
(sikiliza audio ya sauti ya Jarrah hapo chini)
Saa 09:35AM sekunde ya 09 Ziad Jarrah akinua ndege juu mpaka kufikia umbali wa mita 12,400.
Hii iliwafanya waongozaji wa ndege kuondoa ndege nyingine zote kutoka kwenye njia hiyo.
Saa 09:39 AM Ziad Jarrah akatoa tangazo lingine kwa abiria, akiwaambia;
"..here is the Captain. I would like to tell you all to remain seated. We have a bomb, and we are going back to the airport, and we have our demands. SK please remain quite.."
(Sikiliza audio ya sauti ya Jarrah hapo chini)
Kutokana na kitivo hiki kuwa pungufu ya mtu mmoja tofauti na mkakati wao walioupanga awali (kumbuka al-qahatani aliyerudishwa airport), hivyo iliwabidi wawarudishe abiria nyuma ya ndege na kufunga milango kuingia 'business class' na chumba cha rubani.
Kutokana na abiria kuachwa peke yao nyuma ya ndege hii iliwafanya kuwa huru kufanya mawasiliano wa watu ardhini.
Jumla ya simu 35 zilipigwa kutoka kwenye ndege kwenda chini ardhini.
Moja wapo ya simu hizo za majonzi makubwa ilipigwa saa 09:47AM sekunde ya 57 ambayo ilipigwa na muhudumu wa ndege aliyeitwa CeeCee Lyles ambayo alimpigia mumewe ambayo hakuwa karibu ma simu na ikambidi aache ujumbe wa sauti (voicemail).
(Sikiliza audio chini)
Saa 09:57 AM abiria aliyeitwa Tom Burnett aliwaongoza abiria wenzake kufanya 'Mapinduzi' ili kuiweka ndege kwenye udhibiti wao.
Hivyo wakaanza kutimia nguvu kwa pamoja kubomoa mlango wa business Class na hatimaye kuanza kubomoa mlango wa chumba cha marubani.
Saa 09:59 sekunde ya 52 Ziad Jarrah aligundua juu ya nia ya 'mapinduzi' hayo yanayotaka kufanywa na abiria, kwahiyo akaanza kuendesha ndege kama anaibiribgisha (roll) ilikuwafanya abiria wakose 'balance' ya kusimama na kuwajeruhi.
Saa 10:00AM sekunde ya 03 Ziad Jarrah akaituliza ndege.
Baada ya kuituliza licha ya abiria wengi kuwa wamejeruhiwa lakini wakaanza tena harakati za kuingia kwenye chumba cha marubani.
Baada kidogo zinasikika sauti za Jarrah na wenzake wakishauriana kuidondosha ndege kabla ya kuifikia target (whitehouse) ili kuepuka ndege kudhibitiwa na abiria na kutua chini salama.
Saa 10:01AM sekunde 00 Ziad Jarrah ma wenzake wanasikika wakipiga "Takbir.!"
Saa 10:03 AM sekunde 01 Ziad Jarrah akiendesha ndege kwa kasi ya kilomita 906 kwa saa aliendesha ndege kwa nyuzi 40 kuelekea chini na kuidondosha kwenye eneo la Shanksville, Pennsylvania na kuua abiria wote 37 na wahudumu 7 waliokuwemo ndani ya ndege.
9113.jpg
West wing ya Pentagon ikiwa imeteketea na kuharibika vibaya baada ya kulipuliwa na flight 77 iliyoendeshwa na Hani Hanjour.
9114.jpg
Zimamoto, wahudumu wa dharura na raia wakifanya uokoaji baada ya maghorofa ya WTC kudondoka baada ya kuwaka moto kwa takribani dakika 102.
'Blank' Reaction
Katika moja ya vitu ambavyo bado vinabishaniwa sana kwenye nyanja ya usalama na saikolojia ni 'reaction' ya Rais George W. Bush Mara baada ya kueleza hili tukio nililolieleza..
Siku hii ya 9/11 Rais Bush alikuwa ametembelea kwenye Shule ya Awali ya Ema E. Booker Elementary School iliyopo Sarasota Florida.
Katika moja ya shughuli ambazo alizifanya shuleni hapo ilikuawa ni kuwasomea wanafunzi kitabu cha "The Pet Goat" (kitabu hiki pia kilitajwa na Bin Laden kwenye video yake iliyosambaa sana kwa wanachama wa al-qaida mwaka 2004 (nitaeleza hii "coincidence" huko mbeleni)).
Aliwasomea watoto kitabu kwa dakika 13 kabla ya kuja kunong'onezwa jambo na Katibu Mkuu kiongozi wa Ikulu Bwana Andy Card.
Jambo ambalo Andy Card alimnongoneza Rais Bush ilikuwa ni taarifa kuwa kuna shambulio kubwa la ugaidi limefanyika kwenye ardhi ya Marekani..
Ajabu ni kwamba Bush hakuonyesha reaction yoyote (tazama Picha tena)
Hakukasirika, hakustuka, hakucheka wala kuchukia.. Reaction yake ilikuwa ni "blank".
Na ajabu zaidi akaendelea kuwasomea watoto kitabu kwa dakika saba zaidi (jumla dakika 20).
Baada ya hapo Maafisa wa Secret Service wakamuondoa na kufanya darasa moja kama ofisi ya dharura ili Bush aweze kupewa briefing kutoka vyombo vya usalama
9115.jpg
Rais George W. Bush akiwasomea wanafunzi kitabu siku ya 9/11 katika shule ya Emma E. Booker.
9116.jpg
Katibu kiongozi Andy Cardy akimnong'oneza Rais kuhusu shambulio linaloendelea.. (tazama facial expresion.. iko neutral.. 'blank')
Katika sehemu ya hizi Tisa za mfululizo wa makala hizi kuhusu 9/11 nimemaliza kueleza namna ambavyo tukio la 9/11 lilipangwa na kutekelezwa… niliahidi kuendeleza sehemu zitakazo fuata kwa kuangalia upande wa pili wa suala hili kwa kuyaangazia masuala yenye utata.
Sasa basi,
Yako maneno mengi na nadharia nyingi sana zinazo jaribu kueleza utata wa suala hili.
Kwa mfano, hiko nadharia isiyo na ushahidi wowote (lakini ajabu inaaminiwa na wengi) kwamba Bin Laden na Al-Qaida "wamesingiziwa" kuhusika na tukio lile. Labda hii inapewa nguvu zaidi kutokana na misimamo ya kiimani na kiitikadi, lakini binafsi sio mfuasi wa hili nadharia ya "kusingiziwa" Osama kuhusika na shambulio.
Lakini hii haiondoa uhalisia kwamba kuna mambo mengi mazito yenye kutia shaka kuhusu kufanikiwa kwa shambulio la 9/11.
Kuelewa kwa ufasaha utata huu, inapasa kufukunyua kwa kina taarifa za siri kutoka IC (Intelligence Community) za Idara mbali mbali nchini Marekani.
Katika mjadala wangu nitaangazia masuala haya yenye utata kwa katika milengo ya nadharia za dizaini mbili kuonyesha nini kilikuwa kinaendelea kwenye IC.
Misingi ya nadharia hizi ni zifuatazo;
1. LIHOP (Let It Happen On Purpose)
Nitaeleza dalili zinazoonyesha kuwa kulikuwa na watu waandamizi kwenye Serikali ya Marekani waliokuwa na ufahamu juu ya kinachoendelea lakini kwa makusudi wakapuuzia au kudhoofisha utendaji wa vyombo vya usalama kukabiliana na hatari.
2. MIHOP (Make It Happen On Purpose)
Nitaeleza dalili za baadhi ya watu waandamizi ambao zinaonyesha kuwa walipanga au kushiriki au kuwasaidia magaidi kufanikisha tukio lile.
SEHEMU YA 10
ABLE DANGER PROGRAM
Mwaka 1999 kupitia Idara ya Defense Intelligence Agency Marekani ilianzisha progfamu maalumi ya Ujasusi iliyoitwa Able Danger Program.
Lengo kuu la programu hii ilikuwa ni kung'amua mienendo ya magaidi kimataifa na kushauri vyombo vya Usalama vya Marekani juu ya hatua stahiki za kuchukua kabla hatari haijawa kubwa zaidi.
Programu hii ilikuwa inaendeshwa kidigitali zaidi.
Walikuwa wanatumia mbinu za "data mining" ili kufanya shughuli hii ya utambuzi.
(Data mining ni namna ambavyo unaweza kuchukua kiwango kikubwa cha taarifa za kielektroniki (data set) na kuzibadilisha katika mfumo ambao unakuwa rahisi na wenye kueleweka kwa ajili ya matumizi maalumu. Ili kufanikisha hili zinatumia mbinu kama artificial Intelligence, machine learning, statistics na database systems.
Kwa lugha nyingine tunaweza kusema kwamba 'data mining' ni hatua ya awali ya uchambuzi katika masuala ya "Knowledge Discovery in Database)
Kwahiyo, katika programu hii ya Able Danger, walikuwa wanatumia mbinu hiyo ta 'data mining' kuhusianisha taarifa zinazipatikana katika mifumo huru ya kompyuta (open source information) na kuzihusianisha na taarifa za siri za kijasusi (classified information) ili kuweza kufuatilia mienendo ya watu wanaotiliwa shaka kimataifa, na hatimaye wawezo kutafsiri dhamira/mipango waliyo nayo ili hatimaye waweze kuvuruga mipangk hiyo, au kuwakamata au kuwa'nuetralize' kabla hawajaleta madhara.
Nimeanza kwa kueleza hili (Able Danger Program na walichokuwa wanakifanya) kwa makusudi ili kuweka msingi wa hoja ninayotaka kuijadili.
Mwaka 2005, Mwezi June tarehe 27 mwakilishi wa Pennsylvania katika Bunge la Congress, Bw. Curt Weldon alitoa hotuba ambayo ilikuwa ni mwanzo wa watu kuanza kuhoji juu ya tukio la 9/11.
Nanukuu kipande kifupi cha Hotuba yake:
"..Mhe. Spika, nimesimama kwa sababu kuna taarifa za uhakika nimezipata katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, taarifa zinazoogofya sana. Nimefahamu kuwa, kwa uhakika, moja ya vyombo vyetu vya usalama, kwa hakika, walikuwa wameng'amua mienendo ya Atta na kijiwe chake cha New York (New York Cell), yaani walimng'amua Atta na wenzake watatu na kuwatilia shaka………… lilipotolewa pendekezo kuwa FBI wawakamate, wanasheria wa Serikali wa kipindi hicho wakaeleza vyombo vya ulinzi kuwa Mohamed Atta yuko Marekani kwa Green Card na inaweza kuleta utata kwenye jamii…. Kwahiyo wakatumia vigezo vya kisheria kuizuia FBi kufanya chochote.."
Turudi nyuma miaka minne kabla… 2001.
PRESIDENT'S DAILY BRIEF
Rais wa Marekani, kila siku kabla hajaanza shughuli zake za kiofisi huwa anapatiwa nyaraka ya siri (top secret document) kutoka kwa Mkurugenzi wa Taifa wa Intelijensia (Director of National Intelligence).
Mkurugenzi huyu wa Intelijensia, huwa ana-summarise ripoti kutoka CIA, NSA, FBI na Defense Intelligence Agency na kuziweka kwenye nyaraka hii na kuiwasilisha kwa rais kila siku saa 07:45 AM, kabla Rais hajaanza shughuli yoyote.
Lengo la nyaraka hii ni kumpa update Rais kuhusu hali ya usalama wa Taifa, matishio yanayoikabili nchi na mienendo ya maadui wa Marekani.
Siku ya Tarehe 6, mwezi August 2001 (siku 36 kabla ya 9/11) nyaraka hii iliwasilishwa kwa Rais George W. Bush ikiwa na kichwa cha habari "BIN LADEN DETERMINED TO STRIKE IN US"
b956e3495ab5f21548cd49b4393a76d2.jpg
PDB iliyopelekwa kwa Rais Bush tarehe 6 August 2001.
Nyaraka hii inaeleza kinaga ubaga kuhusu tishio hilo na ikifanya reference mashambulizi ya ubalozi jijini Dar es Salaam na Nairobi.
Pia inaeleza kuhusu taarifa juu ya tishio la shambulio linalopangwa kufanya ndani ya Marekani na pia licha ya CIA pia hata Idara ya Ujasusi ya Misri inathibitisha juu ya Tishio hilo ndani ya Marekani (Neno "Egyptian Intelligence" limefutwa).
Swali la kujiuliza, je kwanini taarifa hii ifike mezani kwa Rais Bush na ishindwe kufanyiwa kazi kuepusha tukio la 9/11.
Ili kufahamu hili, tufukunyue tena kuanzia miaka kadhaa iliyopita kabla ya 2001.
Genesis..
Ili kuelewa kwa ufasaha zaidi utata wa tukio la 9/11 inapasa kuanza kuangalia suala hili kuanzia miaka mingi iliyopita, kwenye mzizi wake kabisa.
Mwaka 1984 katika ofisi ndogo ya CIA nchini Misri, kuna kijana alifika ofisini hapo ili kufanya mazungumzo na Maafisa wa CIA ili 'kumrecruit'.
Kinana huyu alikuwa anaitwa Ali Abdul Soud Mohammed.
Baada ya mazungumzo ya kina licha ya CIA kudai kuwa hawakuwa wanamuamini 100% lakini alipewa fursa ya kufanya kazi na CIA kama "junior officer".
Katika kipindi hiki ambapo Ali Mohammed alikuwa anajiunga na CIA alikuwa anatokea kwenye jeshi la Misri ambako alikuwa ni Meja katika kitengo cha Intelijensi ya kijeshi (Egyptian Army Intelligence Officer).
Baada ya kuingia CIA, Ali Mohammed alipangiwa kituo cha kufanya kazi nchini Ujerumani, jijini Hamburg.
Akiwa huko alipangiwa kuzi ya 'ku-infilitrate' kikundi cha Hezbollah ambao walikuwa na 'tawi' hapo Hamburg katika msikiti mmoja maarufu.
Kwa mujibu wa CIA wanadai kuwa, badala ya Ali Mohammed kuwachunguza waumini wanaohudhuria Ibada msikitini hapo, yeye akafanye kinyume akaenda kuongea na Imamu na watu wa Hezbollah na kujitambulisha kwao kuwa yeye ni mtu wa CIA na wamempandikiza ili awachunguze.
CAI wanadai kwamba, Ali Mohammed akashawishiwa na kugeuzwa ili aanze kuichunguza CIA na kupeleka taarifa kwa watu hao msikitini.
Sasa hapa ndipo ambapo kunaanza utata na dalili ya kwamba CIA wanasema uongo na kuna jambo zito wanalificha.!!
Katika mazingira ya kawaida lazima CIA wangeacha kushirikiana na Ali Mohammed au kumpoteza kabisa ili asiendelee kutoa siri za CIA kwa Hezbollah.
Lakini badala yake likatokea jambo la ajabu zaidi.. Tarehe 6, mwezi September 1985 Ali Mohammed aliwasili nchini Marekani.
Miezi michache baadae akumuoa mwanamama kutoka Santa Clara anayeitwa Linda Lopez na akafanikiwa kupata Uraia wa Marekani.!!
Yaani, msaliti wa CIA… kwanza anaachwa aemdelee kuishi, pili anaingia Marekani na si hivyo tu mwishowe anapeqa Uraia.!! Hili linawezekanaje?? Alipataje ruhusa ya kuingia Marekani???
Tukifukunyua nyaraka za kumbukumbu za Uhamiaji, tunakuta kwamba Ali Mohammed aliingia Marekani kwa ufadatibu maalumu wa "Visa-Waiver Program".
Chini ya utaratibu huu, mtu anapewa ruhusa maalumu ya kuingia nchini Marekani pasipo kufuata taratibu za kawaida za uhamiaji ikiwemo kuomba viza na kadhalika.
Sasa swali, ni watu wa aina gani wanapewa huu 'upendeleo' au Idara gani inasimamia hii program ni suala ambalo haliko wazi. Programu hii kwa kiwango kikubwa bado haijawekwa wazi namna ambavyo inafanya kazi na nani anayeisimamia au Idara ipi.
Lakini tukitafakari na kutafuta ushahidi zaidi, utagundua kwamba CIA pengine ndio Idara pekee (ukimuondoa Rais) yenye uwezo wa kusimamia programu ya dizaini hii.
Ukipitia Sheria ya Kuanzishwa kwa C.I.A ya mwaka 1949 kipengele 403h (Central Intelligence Agency Act 1949, (codified) 50 U.S.C 403h) inasema hivi;
Nanukuu;
"..the admission of a particular alien into the United States for a permanent residence is in the interest of national security or essential to the furtherance of the national mission, such alien and his immediate family shall be admitted to the Unites States for permanent residence without regard to their inadmissibility under immigration or any other laws and regulations.."
Tafsiri isiyo rasmi;
"..kama ruhusa ya raia wa Taifa lingine kupata makazi ya kudumu ndani ya Marekani kunaleta faida katika usalama wa Taifa au kuchochea kufikiwa kwa malengo ya taifa, basi mtu huyo na familia yake watapewa ruhusa ya ya kuingia Marekani na kupata makazi ya kudumu hata kama ikidhihirika kuwa wasingeweza kupata ruhusa hiyo kwa mujibu wa taratibu za uhamiaji na sheria nyingine.."
Mwisho wa kunukuu.
Hivyo basi, japokuwa kuna usiri kuhusu usimamizi wa "Visa-Waiver Program" lakini CIA ndiyo Idara pekee yenye uwezo wa kisheria kuisimamia, ndio kusema kwa maneno mengine kwamba Ali Mohammed aliingia Marekani kwa ruhusa ya CIA.
Mwenendo huu wa kushangaza haukuishia hapo tu, mwaka 1986 Ali Mohammed aliomba nafasi ya kujiunga na jeshi na kukubaliwa.
Akapangiwa Fort Bragg ambapo kuna "Special Oparations Command" (hapa ndipo ambapo 'Special Forces' wanakuwa trained).
Baada ya kuhitimu kama mwanajeshi mwenye weledi wa juu (US Special Force) wakubwa wake wakamuomba akasomee shahada ya Uzamivu kuhusu Tamaduni za Mashariki ya kati na Uislamu.
Baada ya kuhitimu PhD yake, Ali Mohammed akaingiza katika programu maalumu ya kufundisha wanajeshi wa Marekani kupanua ufahamu wao juu ya Tamaduni za Mashariki ya kati na Uislamu.
(Tazama hapo chini nimeweka video adhimu iliyopatikana hivi karibuni ikimuonyesha Ali Mohammed akitoa dar'sa kwa viongozi wa ngazi za juu kwenye jeshi kuhusu mahusiano kati ya Uislamu na siasa/dola… moja kati ya sentesi muhimu anazozisema ni kwamba "..in order for Islam to survive it needs political domination.. That's why there is a need to establish an Islamic State")
Mwaka 1993, kulitokea shambulio la kwanza katika majengo ya World Trade Center. (Shambulio hili halikuwa kubwa au madhara kama lile la 9/11).
Baadae watuhumiwa wa tukio hilo Mohammed Abouhadima, Mohamed Salameh na Siddig Siddig Ali walikamatwa.
Uchunguzi zaidi ulipofanyika ukabaini kuwa watu hawa wote kwa nyakati tofauti tofauti walikuwa na mawasiliano na Ali Mohammed na kulikuwa na kila dalili kuwa yeye ndiye aliyewafundisha kutengeneza mabomu.
Kesi ikafunguliwa dhidi ya watuhumiwa hao wote watatu lakini jambo la ajabu ni kwamba Ali Mohammed alipelekwa mahakamani kama Shahidi wa serikali na sio mtuhumiwa.
Mwishoni mwa kesi wenzake wote watatu walitiwa hatiani lakini yeye aliachiliwa huru.
Miaka kadhaa baadae, 1998 kulitokea mashambulizi kwenye ubalozi wa Marekani nchini Kenya na Tanzania.
Baada ya uchunguzi, ikabainika kuwa Ali Mohammed aliwahi kusafiri mpaka Yemen na Somalia katika harakati za kuratibu matukio hayo.
Lakini pia alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na nyaraka kadhaa ambazo zinamlengo wa mafungamano na Al-Qaida.
Kwahiyo February, 2001 akaunganishwa kwenye kesi na watuhumiwa wengine katika kesi ya kuhusika kwenye mashambulio hayo ya balozi nchini Kenya na Tanzania.
Kesi ikaunguruma kuanzia mwezi huo February mpaka mwezi July ambapo Ali Mohammed ambapo alikiri kuhusika na tukio hilo.
Hivyo ilikuwa wazi kwamba Ali Mohammed atahukumiwa kifungo cha maisha jela bila uwezekano wa kupata Parole. Lakini ajabu ni kwamba hukumu haikusomwa na kesi ikahairishwa.
Mwezi octoba 2001, takribani mwezi mzima baada ya tukio la 9/11 kesi ya Ali Mohammed ikaendelea tena kwa ajili ha kusomwa hukumu. Lakini kumbu kumbu za mahakama zinaonyesha kuwa Ali Mohammed na Serikali ya Marekani waka-struck a deal maalumu ya na hivyo hukumu ikaharishwa kwa muda usiojulikana mpaka leo hii.
Ali Mohammed mwenyewe hajulikani amewekwa wapi na serikali ya Marekani, maana hakuna records zake kwenye gereza lolote la Marekani.
Hili suala la kuiweka hukumu 'pending' mpaka leo hii inaonekana kama ni mbinu ya kufanya nyaraka za mahakama kuhusu kesi hiyo kuendelea kuwa 'sealed' ili kulinda usiri wa 'deal' ya Ali Mohammed na Serikali.
Mara kadhaa kwa miaka yote hii 16 mwanasheria wake amekataa kuongelea chochote kuhusu "deal" ya mteja wake na serikali kwa sababu moja kuu, "hukumu bado haijatolewa" hivyo hawezi kuvunja sheria kwa kuingilia Uhuru wa mahakama.
Mkewe pia amekataa kuongelea chochote kuhusu deal hiyo, kwasababu hiyo hiyo kwamba wanasubiri hukumu, lakini wote wanathibitisha kuwa yuko hai japokuwa hawajui amewekwa wapi na serikali. (Ali Mohammed alizaliwa June 3, 1952 kwahiyo mpaka sasa atakuwa na miaka 65).
Sasa basi,
Swali: kwanini nimemuongelea Ali Mohammed kwa mapana hivi??
Turudi tena nyuma kidogo,
Mwaka 1988 Ali Mohammed akiwa mwanajeshi (Special Forces) kituo cha J.F. Kennedy aliomba ruhusa ya kusafiri kwenda nchini Afghanistan.
Akiwa huko alishiriki katika vita ya Mujahedeen dhidi ya vikosi vya Urusi akipigana upande wa vikundi vya Mujahedeen.
(Nilieleza mwanzaoni wa Makala hizi namna Serikali ya Marekani kupitia CIA walivyokuwa wanafadhili na kuunga mkono vikundi vya Mujahedeen).
Akiwa huko, Ali Mohammed alishiriki pia kutoa mafunzo kwa vijana wapya waliokuwa wanajiunga na Mujahedeen.
Mojawapo ya vijana ambao aliwapatia mafunzo hayo alikuwa ni Osama bin Laden, na Ayman al-Zawahiri (kiongozi wa sasa wa Al-Qaida).
Ndio kusema kwamba, Ali Mohammed ndiye 'kungwi' wa kwanza kumfunda Bin Laden katika masuala ya kijeshi. (First trainer)
Baadae mwaka huo huo 1988 akarejea Marekani.
Mwaka 1989 Ali Mohammed akaomba tena ruhusa ya kwenda tena Afghanistan (kumbuka ni kipindi hiki hiki ambapo Osama, al-Zawahiri na Azzam walikuwa wanaanzisha Al-Qaida).
Akiwa huko taarifa zabujasusi zenye uhakika zinaonyesha kuwa alishiriki kuwapatia mafunzo "first batch" ya wapiganaji wa Al-Qaida.
Pia alitumia ujuzi wake na weledi wa 'Special Forces' kuandaa "msahafu" wa Al-Qaida (Al-Qaida Playbook). Ambapo ulihusu masuala mbali mbali adhimu ya kijeshi kama vile Covert Operations, Kutengeneza mabomu, kuunda vijiwe (cells), ushushushu na kadhalika.
Ali Mohammed aliendelea kuwa na mawasiliano ya karibu na Osama kwa miaka mingi iliyofuata (nitaeleza huko mbeleni).
Sasa, kwanini mtu ambaye japokuwa CIA wanaficha na kumficha lakini imethibitika pasina shaka yoyote kuwa ni "asset" ya CIA awe na mafungamano kiasi hiki na Bin Laden?? Je Bin Laden alikuwa ni mshirika pia wa CIA/Marekani??
SEHEMU YA 11
Katika sehemu ya 10, nilimalizia makala ile kwa swali hili?
Sasa, kwanini mtu ambaye japokuwa CIA wanaficha na kumficha lakini imethibitika pasina shaka yoyote kuwa ni "asset" ya CIA awe na mafungamano kiasi hiki na Bin Laden?? Je Bin Laden alikuwa ni mahirika pia wa CIA/Marekani??
Wacha nieleze tena japo kwa uchache ambapo kwa makusudi kabisa kuna dalili zinaonyesha kuwa watu wa ngazi za juu kabisa labda waliacha kwa makusudi kabisa Osama ajiimarishe na mtandao wake wa Al-Qaida kushamiri.
MAY, 1998
CIA kwa miezi kadhaa walikuwa wamekusanya Intelijensia ya kutosha kuhusu eneo fulani nje kidogo ya mji wa Kandahar nchini Afghanistan.
Katika eneo hili kulikuwa na nyumba za matofali ya matope zipatazo themanini ambazo ziko ndani ya ukuta wenye urefu wa futi kumi.
Kwa kutumia Intelijensia kutoka kwa asset baadhi ya raia wa Afghanistan walikuwa wanaishi karibu na eneo hilo, CIA walifanikiwa kuitambua nyumba mojawapo kati ya hizo themanini kuwa ilikuwa ni nyumba ya moja ya wake wa Osama bin Laden, na Osama huwa anaenda kulala hapo mara kadhaa.
CIA wakafanikiwa 'kumap' eneo lote hilo na kutengeneza 'compound' kama hiyo nchini Marekani kwa ajili ya mazoezi.
Mwaka 1997 wanafanya mazoezi ya kina Kwa mara mbili.
Mwaka 1998 wanafanya tena mazoezi kuhusu oparesheni waliyokuwa wanataika kuifanya.
Mwaka huo huo 1998 wakaijulisha Ikulu ya Marekani kuhusu mpango huo waliokuwa nao. Rais Bill Clinton akakataa CIA kuhusika moja kwa moja kutekeleza oparesheni hiyo ili isije kuleta mdororo wa kidiplomasia ikitokea Afghanistan na nchi za kiarabu wakigundua.
Hivyo CIA ikabidi wabadili mkakati wao, safari hii wakaja na mpango wa kutumia vikundi viwili vya kikabila ndani ya Afghanistan kufanikisha oparesheni hiyo.
Mpango wao ilikuwa kwamba, siku ambayo Osama ataenda kulala hapo kwa mkewe basi kikundi kimoja kitamkamata kisha watampeleka mpaka jangwani na kumkabidhi kwa kikundi cha pili ambacho watakaa naye kwa mwezi mzima (ili kuondoa hisia za uhusika wa Marekani) kisha watamkabidhi kwa CIA ambao watamsafirisha mpaka kwenye jela zao za siri Ulaya au nchi rafiki ya Kiarabu.
Mwezi March 1998, wanafanya mazoezi ya tatu kuhusu hiyo Oparesheni wakihusisha pia wawakilishi wa vikundi hivyo vya kikabila kutoka Afghanistan.
Tarehe 20 mpaka 24 May yakafanyika mazoezi ya mwisho yaliyohusisha Maafisa wa CIA, FBI na wawakilishi kutoka Afghanistan.
Tarehe 27 May, Mkurugenzi wa CIA aliandika MNO (Memorandum Of Notification) kwenda Ikulu kwa Rais Bill Clinton kuomba 'Approval' ya oparesheni hiyo ambayo walipanga ifanyike June 23 na Osama asafirishwe kutoka Afghanistan mwezi mmoja baadae yaanj July 23.
Pia MON iliomba wawakilishi wa CIA wafanye kikao Tarehe 29 na washauri wa Rais kuhusu masuala ya Usalama.
Jambo la kushangaza ni kwamba, kikao hicho hakikufanyika (washauri wa Rais hawakutokea kwenye kikao), ile MON haikujibiwa na hawakupewa 'Approval' ya Oparesheni hiyo.
Bw. Tenet ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa CIA kipindi hicho, anaeleza kuwa yalikuwa ni moja ya maamuzi ya kushangaza zaidi ya Rais Bill Clinton ambayo mpaka leo hii hajui alitumia utashi gani kuyafanya.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment