Simulizi : Kiapo (Agano La Damu) (2)
Sehemu Ya Pili (2)
wale wauzaj awakushangaa kwa kuwa kulikuwa na wateja wengi,zidu kichwani akiwa na kofia aina ya bushor
na miwani katika macho yake akaingia rasmi mtahani!
alijua pa kuanzia!
****
"Where are you taking us "
(unatupeleka wapi?!)
Mery Alimuuliza Mtu Yule Ambaye Hata Ivyo Akumjibu Kitu Wakatoka Mpaka Nje Ya Gati Palipokwepo Na Gari
Akawaingiza Siti Ya Nyuma Naye Akaket Mbele Kwenye Usukani Akaiondoa Gari Kwa Kasi!
"You have rescued us now where are you taking us?"
(umetuokoa Sasa Unatupeleka Wapi?)
Mery Bado Alizidi Kulia Ila Mtu Yule Ni Kama Alikuwa Bubu!
Walipita Vijiji Kwa Vijiji Ndan Ya Masaa Manne Kijiji Kabisa Cha Ndani Huko Katika Nyumba Moja Nzur
Ndipo Yalipokuwa Makaz Ya Mtu Yule Ambaye Aliishi yeye pamoja na mkewe!
nikijiji ambacho naweza nikasema nichamwisho kwa maendeleo nchini Tanzania!,
nyumba Kwanza Zilikuwa Mbalimbali Maduka Ayakwepo Wengi Walikuwa Wakulima Vitu Vingine Wakinunua Katika
Minada Kama Mafuta Sabuni!
Kijo Baada Ya Kutoroka magereza Ndo Alienda Kujenga Huko,hata Familia Yake Aikujua Akaoa Huko huko
Baada Ya kuishi takribani Miez Mitatu Pale Kijijin Hamu Ya Kulipiza Kisasi Kwa Zidu Ikamjia!,kwa Kuwa
Zidu Akujua Juu Ya Uwepo Wake Akarudi Mjini Akachukua hotel Iliyopo Karibu Na Nyumba Ya Zidu Akawa
Akikaa Juu Ya Ghorofa Katika hotel Ile Macho Yake Yakifatilia Mienendo Ya Zidu
Mara Kadhaa Zidu Alipokuwa Akitoka!,aliruka Ukuta Na Kuingia Ndani Ya Jumba Lile Na Kusachi Kila Chumba
Kwakuwa Alikuwa Ni Mtaalamu Wa Kompyuta Akitoka Alifomat Picha Zote Zilizo Onesha Sura Yake Na Kutoka!
Raman Yote Ya Nyumba Ile Kijo Ikakaa Katika Kichwa Chake!
Akagundua Vitu Vingi Sana Na Sasa Alipanga Kumchomea Kama Yeye Alivyomchomea!...
Mkumbuke Zidu Nyumba Ile Aliitumia Tu Kiuhalifu Na Si Nyumba Alokuwa Akiishi!
Zidu Aliishi Yeye Na Mke Wake Mery Sehemu Ingine Kabisa Japo Hata Uko Kwa Mke Wake Alionekana Kwa Nadra
Kutokana Na Kusakwa Kwa Vitendo Vyake Vya Ualifu!
Siku Hiyo Kijo Akiwa ndo kwaza katua ukutani ndan ya nyumba ile ghafla akaskia kama honi nje ya nyumba
ile!
kwa wepesi wa ajabu akajibanza chini ya maua macho yake yakiangalia getini,mawazo yake yalikuwa sahihi
alishughudia gari ya Zidu Ikija!,kwa Kasi!
'duh Ningewai Kidogo Huyu Mwamba Leo Angenikuta Ila Leo Simwachi Hai Lazima Nimuue Huyu Hata Nikisema
Nimuunguzie Polis Atatoka Huyu!'
Kijo Aliwaza Tofauti Na Mategemeo Yake Akitegemea Labda Zidu Angeingia Ndani Alimshughudia Akirudi Nje
Akajua Anaenda Funga Geti!
Akazidi Kutulia Palepale Ghafla Akasikia Tena Muungurumo Wa Gari Na Kulishughudia Gari Ingine Ikija Hii
Ilikuwa Niya mr Alex, alishughudia Mzee Akishuka Katika Gari Ile Macho Yake Akazidi Kuyakaza Akumjua
Mzee Yule Ni Nani Ila Aliziona Furaha Katika Nyuso Zao!
'kuna Ishu Gani Inaendelea Hapa?'
Akawaza Alishughudia Mlango Wa Nyuma Wa Gari Ya Zidu Ukifunguliwa Na Zidu Akamtoa Mtoto,
kijo Pale Bustanin Alipojificha Akayatoa Macho Ya Mshangao!
Wakaingia Na Yule Mtoto Ndani!
'lazima Nijue Kinachoendelea Lazima Nikuaribie Mipango Yako Yote Zidu Najua Ilo Ni Dili La Ela'
Wazo Hilo Likapita Katika Kichwa Chake!
Ghafla Akatoka Pale Na Kuufata Mlango Akazama Ndani Kwa Kunyata mambo yalikuwa sebuleni!
akajibanza kwenye kingo kona
inayounganisha varanda ya vyumbani na sebule akaanza kula chabo!
alishughudia mtoto yule akiwekwa kwenye kiti cha shoti! na kuzinduliwa! mapigo ya moyo kijo yakaanza
kumwenda kasi
pale kwa yeye sasa apakuwa salama!
akakumbuka matukio yale yote angeweza kuyaona hata akiwa chumbani kwake aliposeti compyuta zile kule
ndani kurusha kila kitu katika compyuta yake program hiyo aliitengeneza siku kadhaa nyuma wakat
alipokuwa akiendelea kumchunguza zidu!
akatabasamu!
kwa haraka kijo akarejea katika ile hoteli chumbani alipofikia akawasha kompyuta yake!
ikasachi na mara ikaonesha kila kilichokuwa kikiendelea! mpaka Mery Alipoingia Wakamchanganya Na Isack
Kila Kitu Kijo Alikishughudia!
"huu Sasa Ni Muda Wa Kwenda Kufanya Yangu Ntawaokoa Hawa Watoto Na Mchezo Utaanzia Hapo Acha Waendelee
Kusherekea!"
Akawaza Akajivalisha 'ninja' Yake Akabeba Na Bom Alijua Kazi Yake,akaenda Kuichukua Gari Yake Alipoipak
Mda Mrefu Tu Maegesho Katika Hotel Ile Akaipak Nje Ya Geti Ya Nyumba Ya Zidu Si Zilipakana Akaingia
Mpaka Ndani Bomu Lile Akategesha Masaa Alojua Yeye Katika Gari La Zidu Naye Akaelekea Katika Kile
Chumba Mery Na Isack Walimoifadhiwa Akawabeba Nakutoka Nao Mpaka Nje Akawaingiza Kwenye Gari Lake
Akalitoa Kwa Spidi,
HIVI NDIVYO ILIVYOKUA
****
Bado hali ya Isack Ilikuwa Mbaya Mke Wake Kijo Mwanyandachilao Aliyekuwa Kidogo Akiifahamu Mitishamba
Alikuwa Akijitahidi Kumtibu!
Hali Ya Mery Kidogo Ilikuwa Nzuri!
"Can you explain to me what happened"
(unaweza Kunieleza Kilichotokea?)
Kwa Mara Ya Kwanza Kijo Akazungumza Kwa Kingreza,Mery akaachia tabasamu la mbali yamkini la faraja
kwani akutegemea kama kijo aliijua lugha hiyo
"Dad wants to kill us"
(baba anataka kutuua)
Kijo Akushangaa Sana Mery Kusema Yule Baba Yake Anataka Kuwaua Kwani Lile Alilijua Toka Kule Kwenye
Kompyuta Yake
''Why your dad wants to kill this boy"
(kwanin Baba Yako Anataka Kumuua Huyu)
Akauliza Swali Lingine Akimnyooshea kidole isack ambaye mpaka muda ule hakuwa na fahamu!
"Honestly I have no idea about that"
(kwel kwa ilo sijui)
"Ok don't worry you are in a safe place and everything will be alright Okey?"
(ok usijal hapa ni sehemu salama kila kitu kitakuwa sawa ok?)
Kabla Mery Ajajibu Ghafla Meseji Ikaingia Kwenye Simu Yake Kwa Njia Ya Whatsupp Akaifungua Na
Kuidanloadd Ile Video
Kijo Akuamini Alichokiona Ilikuwa Ni Katikati Ya Pori Baba Yake, mama Yake Na Mdogo Wake Wa Pekee
Walifungwa Kwenye Mti
Miili Yao Iliharibika Kwa Kuchapwa Na Bado Zidu Aliendelea Kuwachapa! Ghafla Akaigeukia Camera!
Akaachia Tabasamu!,
"mchezo Bado Unaendelea Nakupa Dakika Tano Nakutumia Video Nyingine Nimemchinja Mdogo Wako Then Ntakupa
dakika kumi na tano nyingine ntamchinja baba yako but kama ujafka ndan ya dk kumi na tano nyingine
nammalizia mamako ku solve yote haya ndani ya dakika tano lete hiyo miili yangu na wewe ukiwepo ila
ndani ya dakika arobain thalathin na tano huna familia swaiba tuanze kuesabu tik tik tik tik...."
"noooo Zidu Usifanye Ivyo"
Kijo Akaachia Ukunga Ghafla Simu Yake Ikaita Ilikuwa Ni Video Call Akapokea
"dakika Nne Imebakia Dakika Moja Utashughudia Nikimchinja Dada Yako...
"k..ak..a Nj.o..o..Ns.ai.die"
kwa mbali iliskika sauti ya mdogo wake ikilia kwa uchungu
Kijo boy Anaingia Vitani Pasina Kujua Anapambana Na Mtu Wa Namna Gani!,lengo ni kulipiza kisasi kwa
yale Zidu Katili Alomtendea Pasina Kujua Anauchezea Moto ambao anashindwa kuuzima!
anawaokoa watoto walotekwa na Zidu Mery Na Agnes ila Zidu Anajibu Mapigo Kwa Kuiteka Familia Nzima Na
Kuisweka Porini!
Ujanja Ujanjani...
Twende Pamoja Kujua Nini Kiliendelea!...
SEHEMU YA THALATHINI NA NANE
Moyo wake ulimuuma sana kijo,aliipenda familia yake japo ni muda mrefu akuiona,mwili wote ulimtetemeka
kwa wasiwasi alimjua vizuri Zidu,akupangua Lile Alilopanga Wakati Akiangaika Kumpigia Ghafla Meseji
Ikaingia Kwenye Simu yake mbio akaenda kuifungua
Ilikuwa ni video huku mikono ikitetemeka haraka haraka akaanza idanload macho yake ayakuamin zidu
alimkata kwel kichwa mdogo wake pekee wa kike!
"nilikupa dakika tano uwe umeileta hiyo miili katika msitu pande kumuokoa dada yako umeshindwa sasa
jaribu kumuokoa baba yako una dakika kumi na tano tik tak tik tak kila la kher"
"nooooh Zidu"
Kijo Alipiga Ukunga Akipiga Magoti Chini,machozi Yalimchuruzika Kama Bomba La Maji Wazo Lililokuwa
Kichwani Kwake Tu Nikuwaokoa Wazaz Wake!
Akili Yake Sasa Ilienda Kuchanganyikiwa,pasina Ridhaa Yake,pasina Kujua Kwamba Anatakiwa Awapeleke Wale
Watoto ndo apewe wazaz wake
Akajikuta ameingia ndan ya gari yake na kuiondoa kwa kasi msitu pande ulikuwa mbali sana tena sana na
pale alipokwepo!
Alikanyaga mafuta kwa mwendo ambao si wakawaida na hatari kwa maisha yake,ajali ikiwa nje nje!
muda ule Wote Mery Alibaki Akimshangaa Kijo Pasina Kujua Kwa Nin Kachanganyikiwa Vile!,
kwa Muda Ule Mke Wa Kijo Alikuwa Kaenda Msituni Kutafuta Dawa Pale Walibakia Wawili,tayari Alamu Ya
Kengele Ilishagonga Katika Kichwa Chake!
Ilikuwa Ni Lazima Aondoke Eneo Lile,ila Je Vipi Kuhusu Isack Na Vile Hakuwa Na Fahamu!
Akajaribu Kumbeba Pia Alishindwa Isack Alikuwa Mzito
Mery Akakosa Raha,au aondoke Amuache?,wazo Hilo Akalipinga Baada Ya Kukumbuka Jinsi Ampendavyo Mtoto
Yule!
" I swor to protect him and if he die we will die together but I can't leave him alone"
(niliapa Kumlinda Na Kama Kufa Basi Ntakufa Naye Ila Siwezi Kumuacha)
Mery Akawaza Akiwa Kajishkia Tama Ghafla Akapata Wazo,akatabasamu Akanyanyuka Pale Na Kuzunguka Nyuma
Ya Nyumba Aliporejea Alikuwa Na Wilbaro Lile La Miti Na Tairi Moja Mbele Akamnyanyua Isack Akampakia
Kwenye Wilbaro Lile!
Huyooo Akaanza Kuondoka Kutoka Eneo Lile...
*****
Nchi Ya Tanzania Ilizizima Furaha Ilitawala Kwa Mara Ya Kwanza Mtu Mwenye Hali Ya Chini Kiuchumi,ambaye
Akwepo Na Usomi Wowote Elimu Yake Ikiwa Ni darasa la nne la mkoloni,
aliyeishi kwa kutegemea kilimo mr max maliwale alikuwa kashinda tena kwa kishindo kuwa Rais wa jamhuri
ya muungano Tanzania!
Baba Aliyeishi Maisha Ya Shida Na Familia Yake Yenye Mtoto Mmoja Aliyeitwa Brayson!
Mzee Max Wakat Matokeo Yakitangazwa Bado Akuamini Akakumbuka Maish Yake Alokuwa Akiishi!
Leo Yeye Na Familia Yake Wanaenda Ikulu
Mtu Alokosa Hata Ela Ya Kumnunulia Mtoto Wake Begi,begi Aliokota Barabaran Baada Ya Yule Mmiliki
Kukimbia Isack Kipindi Icho!
Leo Angempeleka Mtoto Wake Akasome Nje Ya Nchi,mtoto Wake Bray Ndo Yule Alokuwa Rafik Yake Kipenz Na
Pekee Kwa Isack! Alotumika na mwalimu gibson kuweka simu katika begi la isack,isack akaonekana mwizi na
hatimaye kufukuzwa shule katika vipande vya huko nyuma vya riwaya hii!
Jambo lililokuwa mbele yake ni kupanga baraza lake la mawaziri!
Wakati hayo yote yakiendelea kwa upande wa mzee Alex Yeye Alipita Kwenye Ubunge Furaha Yake Iliingia
Doa Baada Ya Mtoto Wake Ampendaye Mery Kupotea Kwenye Mazingira Ya Kutatanisha!
Mtoto Wake Yule Alijua Siri Zake Nyingi Wazo Lake Ni Kumuua Tu,alimpiga Mke Wake Kwa Kuhisi Kuwa Yeye
Ndiyo Alovujisha Siri um Zile Kwa Wanaye Katu Akujua Kuwa Ni Tabia Yake Ile Ya Kuropoka Pasina Kujal
Watoto!..
kila dakika aliwasiliana na Zidu Kujua Amefika Wapi?!
"itakugharimu Zidu I Swear To God Sitokuacha Hai Ikiwa Wale Watoto Atutowaua Na Wakafika Mikononi Mwa
Polisi"
"usijal Mzee Kuwa Na Aman Najua Nifanyacho Yule Shetani Atanletea Watoto Mwenyewe Tulia Mheshimiwa"
Mzee Alex Akakata Simu Alibugia Kinywaji Ghafla Sms Ikaingia Kwenye Simu Yake!
"kutokana Na Ufanyaji Kazi Wako Mzur Katika Kata Yetu Enzi Ukiwa Diwan Wetu Nimependa Uwe Katika Baraza
Langu La Mawaziri Kama Wazir Wa Ulinzi Ndugu Alex"
Alex Alipekecha Macho Pasina Kuamini Kile Akionacho Kwanza Kupokea Meseji Kutoka Kwa Rais Pili
Kuteuliwa Kuwa waziri dah! yey mwenyew ubunge ilikuwa ndoto leo hii waziri?
akajikuta akicheka mwenyewe hata mkewe alokuwa akilia kwa kipigo alijikuta wakiungana katika furaha
ile!
sasa alikuwa mke wa waziri,toka mke wa diwani!,hata mtoto wao agnes nay alifrah pia baba yake kupata
cheo kile!,huzuni ikageuka furaha!,ila wakati hakiwa katikati ya furaha ile ghafla akakunja sura ni
baada ya kukumbuka kitu.
"furaha yangu itakamilika vile vitoto vitakapokufa embu ngojea"
akaongea kwa sauti akimpandia hewani Zidu
"umefikia Wapi wewe?"
"kwa Sasa Nipo Katikati Ya Msitu Pande Nimeiteka Familia Nzima Ya Kijo Nimempa Nusu Saa Awe Amewaleta
Watoto Hapa Kwa Sasa Anakuja Yupo Kwenye Gari"
"vizuri Sana Akifika Ua Wote Untumie picha kuna zawadi yako nzur tu na kwa sasa naenda kuwa waziri tena
wa ulinz ntakuwacha huru uish vizur na familia yako bila kujificha ficha tena naweza kukurudisha
jeshini sawa?"
maneno yale yakaongeza morari ya zidu ili azidi kumuogopesha eti akamchinja mdogo wake kijo nakumtumia
picha pasina kujua kwa kufanya vile kamchanganya mwanaume yule hata kusahau kuichukua miili ile na
kukimbia kwenye gari kwa lengo la kuwahi kuisaidia familia yake!
kosa
maskin kijo akujielewa mwendo aloenda nao tena katikati ya msitu kwenye miti mingi kumbukumbu za dada
yake akichinjwa zikazidi changanya kichwa chake!
paaaaaaaaaaaa
alijikuta akikosa mwelekeo akaenda kuupamia mti,kijo alifia palepale...
dakika kumi na tano zilipopita zidu katili akamchinja baba yake kijo akichukua katika kamera
akamrushia!
baada ya kurusha akasubiri kama dakika tano za kudanload kisha akampigia lengo amuulize kafika wapi!
maskin,akujua kwa muda huo kijo alikuwa maiti,simu ikaitaaaa pasina kupokelewa!
akapiga tena!
vivyo hivyo,akapiga tena na tena!
jibu lile lile!,je ni kiburi?! yah inawezekana alimjua kijo kwa kiburi sasa afanyaje?!
akabaki akipiga,piga na kupiga!
jioni sana akammalizia mama yake kijo na kutoweka eneo lile!
akiacha miili ile palepale!
Wote Wawili Vichwa Viliwawaka Moto!,kitendo Cha Zidu Kumwambia Ameshindwa Kilimchanganya
"kwa Nini Apokei Simu?"
Wakati Wakiwa Katika Tafakuru La Swali lile katika ofis ndogo ya mh Alex ghafla masikio yao yakavutika
kuya imiza macho yatazame mbele palipokuwa na tv
vipindi vilikatishwa na kipindi hasa kilichokuwa hewani ni habari zilizotufikia hivi punde(breaking
news)
yalitajwa matukio mawili ya kutisha!,tukio la kwanza ni kukutwa kwa miili mitatu katikati ya msitu
pande ikiwa imefungwa kwenye miti na yote ikiwa imekatwa vichwa vikiwa chini! yalikuwa mauaji ya
kutisha
"ha ha ha ha ha ha kwel we katili aisee"
mzee alex mwenyewe alikubali zidu katili!
"lakin ndo ivyo aijazaa matunda!"
Zidu Akajibu Akiwa Kanuna Ila Walishtushwa Na Habari Ya Pili Kuwa Huko Kijiji Cha Madongo Kuinama
Imekutwa Gari Katika Pori La Gonja Likiwa Limegonga Mti!
Wote Wakashtuka Zidu Akapayuka!
"kijoo!" Akiwa Kautumbulia Macho Mwili Ule Uloharibika Vibaya Hasa Usoni!
"ina Maana Akuwabeba Wale Watoto Au?!"
Zidu Akauliza Swali Ambalo Mh Alex Akuweza Kulijibu
"na Ndo Maana Alikuwa Apokei Simu Sasa Itakuwa Hatar Kwangu Ikiwa Polis Wataikagua Ile Simu Wakakuta No
Zangu Na Picha Nikiwachinja Vile Viumbe
nilimtumia"
zidu aliongea kwa wasiwas!
"tayari wewe ni wanted tu toka kitambo hata wakijua awakupat cha kufanya zima simu pasua line hiyo weka
laini ingine"
"yap nice kwanza hii line niya kazi tu"
Zidu Akajibu Akiitoa Ile Line!
"na Hapo Hapo Jeshi La Polis Limewapata Watoto Wawili Katikati Ya Msitu Huo Wa Madongo Kuinama Wakiwa
Katika Hali Mbaya Pasina Fahamu,mmoja Alitambulika Ni Mtoto Wa Mbunge Mh Alex Kyao Ila Mwingine Akuweza
Kutambulika Miili Yao Ipo Hosptalin Kwa Uchunguzi Zaidi Mwandish Wetu Jm Moudy Anatuabarisha Zaid"
Habari Ile Ya Nne Iliwashtua Wote Wakaganda Kama Sanamu Wakiitumbulia Tv ile macho!
"ziduuu ataropoka yule shetan wangu nenda kaue kabla ajazinduka kataropoka kale haraka sana toka hapa
nenda madongo kuinama hosp"
"sawa mheshimiwa"
zidu akanyanyuka na kutoka ofisin pale akaingia ndani ya gari lake kuelekea madongo kuinama akiwa na
silaha za kutosha
Ni noumaaaa kama mjuavyo mery ni mropokaji je ataropoka? au zidu atamuwah?
Vyombo Vya Habari Vinatangaza Kutokea Kwa Matukio Matatu Tofauti,ikiwa Ni Breaking News Matukio Yote
Matatu Yanaonekana Kuwashtua Watu Wawili Zidu Katili Na Mheshimiwa Alex Kwakuwa Wao Ni Wahusika Wakuu
Mheshiwa Alex Anamtuma Zidu Aende Ndan Ya Kijiji Hiko Cha Madongo Kuinama Katika Hospital Walolazwa
Mtoto Wake Na Kijana Isack Aakikishe Anawateketeza Kabla Awajapata Fahamu
Je Zidu Atafanikiwa?!
Songa Nayo
NA HII NI SEHEMU YA THALATHINI NA TISA!
Baada Ya Zidu Kuondoka,mzee Alex Akutaka Kupoteza Muda Akajinyanyua Tayari Kuelekea Nyumbani
Kichwa Chake Kilikuwa Katika Mawazo Mazito!,
Upande Mwingine Inspekta Nurdin Akiwa Ndan Ya Ofisi Yake Kichwa Kilikuwa Kimejaa Mawazo Akujua Ni Wapi
Angempata Yule Mtoto!
Akiwa Katikati Ya Mawazo Yale Ghafla Simu Yake Ikaita Japo Ilikuwa Ni Namba Geni Ila Nurdin Hakuwa Mtu
Wa Kudharau Simu Apigiwayo Akaipokea Haraka Akasimama Huku Akiwa Kama Kachanganyikiwa
"kiso,jafary,na Kito Nifateni!"
Akaongea Kwa Kujiamin Askar Wale Wakamfata Nyuma, wakaingia Ndan Ya Gar Ya Polisi Wakatoweka Eneo Lile!
Mwendo Alotoka Nao Nurdin Uliwashangaza Maaskar Wale Ambao Awakujuwa Ni Wap Walipokuwa Wakipelekwa!
Masaa Kadhaa Walifika Katika Kijiji Kile Cha Madongo Kuinama Mbele Yao Kulikuwa na miili miwili!
"raia mwema kanpigia simu kuna watu wamechinjwa embu tujigawanye kukagua msitu huu...
wakati inspekta Nurdin Akiendelea Kutoa Maelezo Ghafla Gar Ingine Ilifika Pale Wakashuka Vijana Wawili
Mmoja Akiwa Kashika Kamera Na Mwingine Kashika Maiki Hawa Walikuwa Ni Waandishi Wa Habari
"kama Mlivyo Ona Na Hili Ntukio La Tatu Lililotokea Katika Msitu Huu Tofaut Na Matukio Yale Mawili
Likiwemo La Ajali Na Lile La Kukatwa Vichwa Kwa Watu Wawil...
Insp Nurdin Akashtuka Akawapa Ishara Vijana Wake Wale Wawil Kutulia Kwanza Akapita Upande Wa Nyuma Ya
Kamera Akamvuta Yule Kamera Man Kando
"hayo Matukio Mawili yametokea wapi?"
kamera man yule akashtuka,iweje polis aliyepaswa kujua swala lile hata kabla yake aje amuulize yeye
akampuuza akamjibu!
wakawapakia wale watoto ndani ya gari yao,wakaenda walipoelekezwa kwenye mwil wa kijo nao wakaubeba na
ile miili miwil ya wazaz wak kijo nayo wakaipanga nyuma ya gar yao ya polis safar ya kuelekea hosptalin
ikafatia!
huku nyuma ndipo waandish wa habar walipotangaza habari zile zilizowafikia mpaka kina Mr Alex Na
Zidu,ndipo Mheshimiwa Yule Akamtuma Kijana Wake Akamalize Kazi Pasina Kujuja Inspekta Nurdin Yupo
Karibu Sana Na Wale Watoto Kuwalinda!
*****
Inspekta Nurdin Akutakaka Kubanduka Kitandani Alipolala Mtoto Isack! Hamu Ya Kuendelea Kufatilia
Matukio Yale Ilimuandama!
Kwanza Kukutwa Kwa Mwili Wa Mtoto Wa Mheshimiwa Waziri Alex Kulimshangaza!,kukamfanya Atamani Mery
Apate Fahamu Kusudi Apate Kujua Ni Kipi Kilichotokea!,
Wakati Akiendelea Kuwepo Pale Ghafla Mama Yake Mery Bi Ney Aliwasili,alimkimbilia Mtoto Wake Na Kuanza
Kumlilia!
Baadaye Akaonana Na Daktari!
"naitaji Nimchukue Mwanangu Akatibiwe Nje Ya Nchi!"
"mtoto Wako Yupo Chini Ya Ulinzi Kwa Mahojiano Na Maaskar Hivyo Wewe Kumchukua Ipo Nje Ya Uwezo Wetu
Kaongee Na Yule Askar Pale Akikubal Basi Sawa
Bi Ney Akashtuka!
'eti Kumchukua Mwanaye Eti Hadi Polisi Aruhusu?'
Ilo Aliona Kwake Ni Jambo Lisilowezekana Akampigia Mumewe Simu!
"baba Mery Mwanetu Ana Hali Mbaya!"
"atajua Mwenyewe Mi Nlimtuma Anifatilie?,nakuomba Rudi Nyumbani Haraka Sana"
Bi Ney Akashtuka Akuamin Maneno Kama Yale Yanatoka Mdomoni Kwa Mume Wake Baba Wa Mtoto Wake Yule,
"mume Wangu Kumbuka Huyu Ni Mtoto Wet Tena Madaktar Wamekataa Nimchukue Kumpeleka Kwenye Tiba Nzur..."
"eti Nin?!...Umchukue?,kwan Hapo Apati Tiba Au Unataka Kuchezea Ela Tu Nisikie Umemtoa Huyo Mtoto Hapo
Mfyuuu"
Mzee Alex Alimalizia Na Kukata Simu Hakika Alichukizwa
na maneno ya mke wake!,yey alitaka mtoto afie palepale katu akujua kama insp nurdin alikuwa karibu sana
na watoto wale!
"sasa kuna hizi dawa hapa amna ni vyema ungeenda kumchukulia!"
daktar alimweleza insp Nurdin Akimkabidhi Kikaratasi Alichokiandika Dawa Zile
Nurdin Akakipokea!,alitaman Pale Angemuacha Mtu Ila Je Angemuacha Nani? Hapo Akamkumbuka Madam Jane
Tokea Tukio Lile Limetokea Akuwasiliana Naye Hata Kumjulisha,akakumbuka Hata Simu Yake Pia Akuiwasha!
Akaingiza Mkono Mfukoni Akaitoa Simu Yake Akaiwasha Na Kumtafuta Madam Jane Akampigia
"simu Unayopiga Kwa Sasa Aipatikan Jaribu Tena Badae"
Akairudisha mfukoni!
akajinyanyua kwenye kitanda kitanda kile cha Mery Alichokikalia Tayari Kutoka Kuelekea Mjin Kutafuta
Hizo Dawa!
Ghafla Kuna Kitu Kikamtuma Ageuke Nyuma Kumtazama Mery!
Alishtuka!
Mery Alikuwa Kafumbua Macho Yake Machozi Yakimtoka
Inspekta Nurdin Akamfata Kwa Spidi Na Kuanza Kumwita!
"isack!,isack!,isack"
Mery Akuitika Zaidi Ya Kutaja Ilo Jina Huku Machozi Yakimchuruzika
"isack?!,isack Kafanyaje?!"
Inspekta Nurdin Akauliza Kwa Kimuyemuye Ila Mery Ni Kama Akumuelewa Jamaa Yule Anaongea Nin Yeye
Akazidi Ita Tu Isack! Isack!
Nurdin Akazidi Changanyikiwa!
Wakati Hayo Yakiendelea Mwanaume Wa kazi,izrael wa kibinadamu ndo kwanza alikuwa akishuka kwenye gari
yake nje ya hospital ile!
mwanaume akaanza kulifata jengo la hospital kiunon akiwa na pistol yenye kiwambo cha kuzuia sauti na
kisu kidogo
akaachia tabasamu!
"nakuja isack,nakuja mery,naja kuondoka na roho zenu"
akawaza kulifikia lile jengo,akaelekea kulipo na ngazi za kupandia juu zilipo hodi za watoto! japo
hosptal ile ilikuwa kijijin ila ilikuwa ni hosptal kubwa na nzur yenye ghorofa tatu ikiwa tumejengewa
toka enz za ukolon wa waingreza
basi baada ya Nurdin Kutoelewana Na Mery Akaenda Kumshtua Daktar!
"Huyu binti kashapata fahamu ila
Nimemchoma sindano ya usingizi akizinduka atakuwa poa,we nenda kalete hizo dawa"
Nurdin Baada Ya Maelezo Yake Akatabasamu Akaondoka Na Kuzifata Ngaz Za Kushuka Chini
Wakati Akishuka Mwanaume Wa Kazi Zidu Ndo Alikuwa Akipanda!,lau Kama Angegeuka Tu Kulia Kwake Angepata
Kumuona
Huyu Akashuka,yule Akapanda!
Nurdin Akalifata Gari Lake Na Kuliwasha Tayari Kuelekea Mjini
Mwanaume Wa Kazi Zidu K Akaelekea Mpaka Mapokez Alipomkuta Binti Mrembo!
"samahan Eeh Dada Kuna Wagonjwa Wawil Wameletwa Wamekutwa Porin?!..."
"ahaaa Unawasemea Yule Mery Mtoto Wa Waziri Na Yule Kijana..."
"yah Isack Mwanangu Yule!"
"ooh Pole Sana"
"huyo Kashazinduka yupo wodi namba nne"
"asahte!"
Zidu Izrael Wa Kibinadamu Akashkur Akiachia Tabasamu Akaelekea Zilipo Wodi Hizo!
Akafungua Mlango Na Kuzama Ndani Mkono Wake Wa Kulia Ukiwa Tayar Nyuma Ya Surual Yake Tayar Kuivuta
Paipu!...
Mwanaume Zidu Katili Hatua Kijijini Madongo Kuinama Ndani Ya Hosptal Ambapo Ndani Kuna Watoto aliyepewa
kazi ya kuwaua!,baada ya kuulizia mapokez akaelekezwa chumba alicholazwa mwanaume akaelekea huko!
akafungua mlango na kuzama ndani mkono wa kulia ukiwa nyuma alipoweka pisto yake je nin kiliendelea?!
twende pamoja katika kujua nin kilichotokea!
NA HII NI SEHEMU YA AROBAINI!
Kabla Inspekta Nurdin Ajalifikia Geti La Kutokea Hosptal Ile Akakumbuka Amesahau Simu Yake Mule Wodini
Wakati Alipomtafuta Madam Jane!
Haraka Sana Akageuza Gari Kurejea,akashuka Huku Akipiga Hatua Ndefu Kuelekea Zilipo Ngazi Za Kuelekea
wodi waliyelazwa wale watoto!...
Zidu Katili Baada Ya Kuzama Ndani Macho Yake Yakapokelewa Na Vitanda Vingi Na Wagonjwa Wengi!,tabasamu
Likayeyuka Katika Mdomo Wake,mawazo Yake Alijua Ni 'privet Wodi' Sasa Pale Angeuwaje?!
Akabaki Kanata Pale Mlangoni Ubongo Wake Ukifikiria chakufanya hapo hapo macho yake yakijaribu kupitia
mgonjwa mmoja mmoja yakiwatafuta watoto wale
ghafla akawaona tayari alishajua cha kufanya taratibu akapiga hatua kuwafata,kwa sasa alishapitisha
maamuzi asiogope mtu aue atoweke pale,tena kabla ajawafikia wazo lingine likapita achomoe silaha
awamiminie risasi atoweke,akapeleka mkono nyuma ile akaishika silaha yake ile anaichomoa akakutana na
ukinzani alihisi kama mtu amemshika mkono kwa nyuma akageuka kuangalia ni nani alomshika!
kosa,
alipokea ngumi nzito akapepesuke ila kabla ajadondoka akafanikiwa kujiweka sawa!
sasa walikuwa wamegeukiana wakiangaliana kwa hasira!
Ni Inspekta Nurdin Na Zidu Katili,
Inspekta Nurdin Akamsogelea Zidu Na Kurusha Teke,zidu Akalipangua Muda Huo Huo Akirusha Ngumi Ambayo
Insp Yule Akuweza Kuiona Ila Alijikuta Tu Maumivu Makali Yakiambaa Katika Uso Wake!
Mwanaume Akaufata Mlango Na Kuufungua Akatoka!
Insp Nurdin Akukubali Akaufata Mlango Na Kuufungua silaha ikiwa mkononi nje patupu!,kitendo icho
kilimshangaza,akutaka kufatilia sana akarudi zake wodin kule akionekana wazi kuchanganyikiwa!
Zidu Baada Ya Kuingia Ndani Ya Gari Yake Bado Hasira Zilimuendesha,uwezo Wa Kumuua Inspekta Nurdin
Alikuwa Nao Ila Akutaka Kufanya Ivyo Akiofia Kutafuta Bifu Na Idara Ya Polisi
Yeye Alishapitia Jeshi,mkono Wa Serikali Kiusalama Aliutambua!,
mbinu Ile Ilishindikana,ila Akutaka Kuondoka Katika Kijiji Kile Bila Kuua!
Bila kufanikisha kazi Yake
Kwa Kuwa Nurdin Akuitambua Gari Yake Akutaka Kuondoka Eneo Lile La Hosptal Alibaki Ndani Ya Gari Yake
Akifikiria Ni Kipi Angefanya!
Wazo Lililomjia inspekta Nurdin Ni Kuwahamisha Wale Watoto Chumba Ili Awaweke Katika Ulinzi Mzuri!
Akaenda Kuongea Na Daktari Akalipia VIP Chumba Kimoja Wakalala Isack Na Mery!
Sasa Akiwa Na Uhakika Kwa Muda Ule Mtu Yule Asingerejea Na Hata Kama Angekuja Asingejua Kalazwa Chumba
Kipi Akatoka Na Kuingia Ndani Ya Gari Yake!
Pasina Kujua Zidu Alimuona, kitendo Tu Cha Inspekta Nurdin Kuondoka Yeye Akashuka Kwenye Gari Tayar
Kurudi Kwenye Wodi Ile kumaliza shughuli yake
alipofungua mlango tu watu wote walishtuka kumuona kwani walimkumbuka lakin macho yake yalipodondokea
kwenye vile vitanda vilikuwa vitupu!
akupata shida kung'amua kuwa watu wake walisha amishwa pasina kuongea na mtu akageuka kuelekea chumba
cha daktari!
pasina kujali kuwa kuna mtu alikuwa akiudumiwa akaingia!
"we fata zamu ina maana uoni kama kuna mtu!?"
daktar yule ya wodi za watoto aliongea kwa ukali akijua pengine yule ni mgonjwa ila hilo zidu akujal
"we mama na mtoto wako token nje mara moja nadharura!..."
"hapana haiwezekani fata zamu...
Kabla ajaendelea,alitazamana na kitu ambacho kwenye maisha yake akupata kukiona laivu zaidi ya kwenye
tv,si kwake tu hata daktar mwenyewe alishtuka!
Kwa unyonge yule mama akajiinua kutoka nje,
"na usiseme chochote kinachoendelea humu ndani! kwanza usitoke utaniaribia kaz kaa hapo pemben!,"
Zidu Akaielekeza Bastola Kwa Daktar!
"naomba Nieleze Chumba Kipi Walichoamishiwa Wale Watoto Lasi Ivyo Natawanya Ubongo"
"hapana Baba Wapo VIP huko chini Chumba Namba 4"
"natoka Nawafungia Kwa Nje Ole Wako Un Danganye Sitosita Kukuangamiza Nipe Koti Lako Ilo Na Icho
Kipimo"
Daktar Akavivua Zidu Akavaa,alipendeza Alikuwa Kama Daktari,akatoka Na Kufunga Mlango
"daktar Mbona Unawafungia Hawo waliyomo humo Ndani!?"
Mgonjwa Mmoja Aliyekuwa Hapo Nje Akisubiria Zamu Yake Aliuliza Kwa Mshangao akisahau kwamba huyo ni
yule kijana aliyewapita dakika chache pale akawaacha wakinung'unika
"wamepumzika!,kwa Sasa Nyie Nenden Matibab Mpaka Kesho"
Wagonjwa Wale Kwa Mshangao wakatawanyika!
Zidu akazifata Ngazi Na Kushuka Ghorofa Ya Kwanza wodi aliye elekezwa akafika
akafungua mlango na kuzama ndani!
aliachia tabasamu baada ya kuwakuta ndani ya wodi ile wapo wawili tu
tena walikuwa wamelala!
akamsogelea Mery Lengo Kumuamsha Alitaka Kuwaua Wakiwa Macho Akakishika Kichwa Chake Na Kukigongesha
Kwa Nguvu Kwenye Kitanda Kile Cha Chuma!
Mery Akafumbua Macho Damu Zikaanza Kumtoka Kisogoni,akamgonga Tena Kwa Nguvu Awamu Hii Gonga Ile
Akidhamiria Kuua!
Mery Akatulia!
Zidu Akaachia Tabasamu Akamfata Isack Pale Alipolala Akakishika Kisu Chake Akamfikia Akakizamisha
Tumboni
"ha ha ha ha ha"
akaachia kicheko wala akuangaika kuking'oa kile kisu tumboni kwa isack akavua lile koti na kujifutia
damu
akaliacha palepale,akatoa simu yake na kuwapiga picha kisha akamtumia bosi wake mwanaume akatoka akijua
kamaliza kazi!
akaingia ndani ya gari yake na kutoka maeneo yale!
****
Inspekta Nurdin Alishuka Kwenye Gari Yake Akaelekea Chumba Cha Daktar Alishtuka Kukikuta Kimefungwa
Akujal Sana!
Akaelekea Wodini,akafungua Mlango!,alishtuka Sana Pasina Kuamini Kile Akionacho Akabaki Pale Mlangoni
Kaganda Pasina Kujua Nikipi Angefanya!
Mwili Ukabaki Umemsisimuka
Maisha Bado Ni Mabaya Kwa Mtoto Isack!,kila Nuru Ya Ukombozi Inapommulikia Inazimwa Na Kubaki Katika
Kiza Cha Mateso! Je Nin Hatma Ya Maisha Yake? Tusonge Mbele Kujua Nin Kilichotokea Pale!
SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA!
Kwa mara ya kwanza ujasiri ulimtoka,machozi yalimtiririka pasina mwenyewe kujielewa akabaki vile vile
kaganda pasina kujua kwa muda ule angefanya nini!
Ni kama kwa muda ule alikuwa ametokwa na ufahamu ila ghafla alizinduka na kumkimbilia Isack Akaanza
Kumuamsha Ila Isack Akufumbua Macho Yake Insp Yule Akapeleka Masikio Yake Kusikiliza Mapigo Ya Moyo
Ghafla Alinyanyuka Tena Akiwa Anakimbia akaufata mlango na kuufungua akatoka huku akikimbia kwa bahati
nzur nje kule alikuta kuna madaktar wawil walokuwa wakijadili jambo!,
wote wakamfata mpaka pale wodini!
"dokta kimario yupo wapi?"
daktar mmoja aliuliza wakati wakielekea wodi ya mahututi!
madaktar kadhaa wakakutana wakati wengine wakiendelea na huduma wengine walikaa kikao kujadili swala
lile!
"yeye ndo mwangalizi wa hawa watoto itakuwa yupo wapi sasa ofisin kwake mmemwangalia?"
daktar mkuu aliuliza!
"ndiyo dokta ofisi yake imefungwa na akipigiwa simu apokei"
Daktar mwingine alijibu,hali ya sintofahamu ikazuka baina yao!
wakati hayo yote yakiendea
Upande wa pili nyumbani kwa mheshimiwa Alex Ilikuwa Ni Furaha Kwa Muheshimiwa Tayari Alisha Apishwa
Kuwa Waziri!
Picha Alizo Oneshwa Na Zidu Kisu Kikiwa Mwilin Mwa Isack Zilimfuraisha Sana!
"awamu Hii Akipona Bas Tena Yule Atakuwa Si Binadamu!"
"ha ha ha ha bosi ataponea wapi kwa mfano!"
wote waliongea kwa furaha!
"namchukia sana yule mtoto kwanza kasababisha nimempoteza mtoto wangu"
Moyo Wa Mzee Yule Wala Ukuhumia Kumpoteza Mwanaye Kipenzi,uchungu Ulikuwa Kwa Mama!
Muda Ule Wakati Wakipongezana Pale Mama Mzazi Wa Mery Bi Ney Alikuwa Akijiandaa Yeye Na Mwanae Kuelekea
Hospitalini Kuuchukua Mwili wa mwanae!, roho ilimuuma alilia ila hakuwa na lakufanya tayari mume wake
alikuwa na nguvu!
"nenda kaulete ule mwili wa kitoto chako tukazike wa kale katoto kengine kaache palepale manispaa
wakazike!"
Mzee Yule Aliongea Kwa Furaha Akimimina Kinywaji Katika Glasi Yake Wala Mkewe Akumjibu!
Akatoka Zake Na Kuingia Ndani Ya Gari Lake Tayari Kuelekea Katika Kijiji Cha Madongo Kuinama
*****
Dokta Kimario Akiwa Kule Ndani Alisikia Simu Yake Ikiita Kivipi Angepokea Wakati Alishafungwa Mikono Na
Miguu yake katika kiti alichokalia!
akamwangalia yule mama alofungwa pembeni yake yeye alibaki kulia ghafla akapata wazo!
"toto! toto..."
akamwita mtoto wa yule mama mdogo mwenye umri kama wa miaka mitano hivi aliyekuwa akimlilia mama yake
yule mtoto akamcheki huku mdomo ukitetemeka kwa hasira ni wazi alihisi mama yake kamtenga kakataa
kumbeba,katu akujua kama mamaye yupo kwenye matatizo
"njooo lete ile toto!"
daktar yule akamwambia akimnyooshea simu yake mtoto akatingisha mabega kukataa! ni kama alima anisha
hataki urafiki na yule daktari!
daktar akampa ishara mama yake mama yake akamwagiza katoto kakacheka kakaanza kutembea kakaifata ile
simu pale mezani kakaichukua na kumpelekea mama yake!,mama yake akampa ishara abonyeze mtoto yule
akatii na ghafla wakawa wamempigia daktar!
Wakati Madaktar Wale Wakijadili Cha Kufanya Katika Kikao Chao Kile Kisicho Rasmi Ghafla Simu Ya Daktar
Mmoja Wapo Ikaita!
"samahani Dokta Ndo Huyu Anapiga"
Daktar Yule Alitamka Akipokea Simu Ile!
"njoo Mtusaidie Tumefungwa Huku Ofisini"
Wote Walishtuka Wakiongozana Na Inspekta Nurdin Wakaelekea Ilipo Ofisi Ya Daktar Yule
Ikawalazimu Wavunje Mlango
Kwa Kuwa Zidu Aliondoka Na Ufunguo!
Wakawatoa Daktar Na Yule Mama Na Mtoto Wao Daktar Akaeleza Kilichotokea!
Waandishi Awakuwa Nyuma Kuripoti Kila Kinachotokea!
Muda Ule Ule Mama Yake Mery Aliwasili si yeye tu,maaskar waliongezeka,na hata madam jane pia alienda!
hosptal ile ilifurika watu,japo insp nurdin alimtambua mzee alex ndo muhusika wa kila kitu alimficha na
mtu yule aliyepambana naye akueleza wazi kuwa ni zidu aliamua kufanya siri akiwa na maana yake!
"mama mtoto wako ni mzima ila amepata adhari kichwani kapoteza kumbukumbu"
Bi Ney Akashtuka,furaha Ikamvaa Akaishika Simu Yake Na Kumpigia Mumewe
"mume Wangu Mtoto Wetu Anaendelea Vizuri Japo Kapoteza Kumbukumbu Baba Mery!"
"ok Nakuja Hapo Saivi!"
Mzee Alex Alijibu Moyon Mwake Akiwa Ajafurahia Kabisa Habari Ile!
"kale Katoto Kangu Akajafa Ila Kamepoteza kumbukumbu nilazima tukakaone!"
mzee alex akamwambia Zidu Ambaye Kwa Wakati Ule Alishampa Uhuru Kwa Cheo Chake Cha Uwaziri Na
Kumrudisha Jeshini! Kwa Malipo Ya Kufanikiwa Kumuua Isack!
Si Kwa bi ney pekee aliyekuwa na furaha hata kwa inspekta Nurdin Na Madam Jane Nao Kwa Upande Wao
Walikuwa Na Furaha!
Kile Kisu Baada Ya Kuchomwa Kwa Kitendo Cha Zidu Kukiacha Na Kutokukichomoa Kulisababisha Kutopitisha
Hewa Na Damu Kutovuja Nyingi Ivyo Operesheni Ilifanikiwa Kwa Asilimia Mia!
Furaha
Zikatawala Pande Zote!
Nje Ya Hospital Ile Msafara Wa Magari Uliwasili Pakiwa Na Maaskari Wengine Wakutosha,
Mheshimiwa Alex Akiwa Na Mlinz Wake Zidu Katili Akiwa Ndani Ya Suti Akashuka!
Safari Ya Kuelekea Wodini Kumcheki Mwanaye Ikafatia!
Usoni Alionekana Na Majonzi Ila Moyoni Kulikuwa Tofauti!
Aliwashkuru Madaktari Wale Kwa Jitihada Zao!
"dah Ongereni Ila Huyo Aloletwa Naye Kwa Bahati Mbaya Ndo Kafariki?!"
Mzee Alex Akauliza Akitegemea Jibu La Ndio!
Daktar Akacheka!
"ha ha ha ha hapana dokta kwa bahati nzuri kisu akikuleta madhara sana ndani ya tumbo kwa sasa
anaendelea vizuri!"
"unasema?!"
mzee alex akabadilika palepale ofisini mbele ya daktari mkuu,dokta akashtuka!
akamkata jicho kali Zidu!
Akamgeukia Tena Daktari!
"naitaji yule mtoto afe!,ikiwa unayapenda maisha yako"
mzee alex aliongea kwa sauti ya taratibu,ila ilofika kwenye masikio ya daktari mkuu yule!
"ila huo si utaratibu wa kazi yangu mkuu?!"
"staki kujua ilo kamchome sindano ya sumu sasa afe atuto ondoka hapa mpaka utekeleze ilo tofauti na
ivyo tutaondoka we u maiti nadhani umenielewa!"
Hakika Daktar Yule Alihisi Yu Ndotoni Taratibu Akaenda Katika Kabati Lake Ofisini Mwake Mule,akatoka Na
Bomba La Sindano Na Kichupa Cha Sumu Huku Mikono Ikimtetemeka!
"Zidu ongozana naye akikisha anatimiza hili sawa?!"
Zidu Akanyanyuka! Na Kupiga Saluti!
"sawa Mkuu"
Zidu akaitika wakatoka pamoja dokta akiwa mbele,Zidu nyuma!
wakamuacha mheshimiwa mwenyewe mule ofisini!
*dah hatari bado inamuandama isack ataipona sindano ya sumu kwel?!*
Maisha yake yamezingirwa na mitihani ambayo ni uwezo wake Mungu Tu Kumwezesha Kufaulu Mitihani Ili,kila
Mara Ananusurika Kufa Ila Je Ninin Hatma Ya Yote Haya! Twende Pamoja Kujua Nin Kiliendelea Juu Ya Mtoto
Isack!
SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI
Daktar akiongozana na Zidu K Waliwasili Katika Wodi Ile Wakafungua Mlango Na Kuingia Ndani
Wote Walishtushwa Na Kile Walichokiona Isack Akuwepo Zaidi Ya Mery Na Mama Yake Pekee
"huyu Mtoto Ameenda Wapi?"
"wazazi Wake Washamchukua"
Bi Ney Aliongea Akimkazia Macho Zidu!
"sasa Tufanyeje?" Daktari Yule Akaongea Kwa Unyonge
"nifate"
Wakarudi Zao Ofisini Wakamweleza Kila kitu mheshimiwa!,Alex akacheka sana!
"goods naona huyu mtoto sasa amekuwa chakor nami baianj si kitu!"
Taratibu akanyanyuka pale na kumsogelea zidu akamnong'oneza Kitu!
Zidu Akamfata Daktar!
"naomba Hiyo Sindano Uloshika Na iko Kichupa"
Dokta Yule Huku Akitetemeka Akamkabidhi Kichupa Kile,Zidu akavuta dawa na pasina huruma akamdunga nayo
daktar yule!
ITAENDELEA
.
Simulizi : Kiapo (Agano La Damu) (2)
Sehemu Ya Tatu (3)
dokta akupata hata muda wa kujitingisha!
"huyu kafa kwa kuwa alishajua lengo letu! twenzetu hawa watu ntawajua cha kuwafanya"
"saiv nimerudi jeshini mkuu Nurdin Naweza Mwangamiza Pasina Tabu Yoyote!"
Wakati Wakiwa Kwenye Gari Zidu Aliongea Kwa Kujiamini
"aina haja huyu ntampa uamisho then tutamfungulia madam jane mashtaka ya kuishi na mtoto wako yule
madam lazima aishie jela nasi tubaki na isack tumuue kilaini tu!."
"fact!..umefikiria nin mkuu"
"unajua yule mtoto saivi jeshi la polis wanamfatilia sana wakiongozwa na huyo Nurdin So Tukisema Tumuue
Tu Kienyej Enyeji tutazalisha upelelezi usio na kichwa wala miguu kwa sasa tumuamishe kwanza tumpeleke
kijiji cha mbali kichosifika kwa uhalifu umuangamizie huko hata idara ya usalama ijue ni majangili wa
huko wamefanya yao!"
Na Ndivyo Ilivyokuwa,inspekta Nurdin Akaamishwa Kwenda Eneo Lingine Ila Tofauti Na Matarajio Yao Nurdin
Alielewa Ile Ni Mbinu Yakumuweka Mbali Na Mtoto Isack,
Moyo Wake Ulimtuma Akaishi Na Mtoto Yule! Hata Kule Aendapo!
Katu akujua lengo la kupelekwa kule ni ili auwawe yeye alijiamini na maisha yake akijua hakukuwa na wa
kumwangamiza!
alijidanganya
"Nurdin Mpz Kwa Kuwa Amri Imetoka Ndani Ya Masaa 24 Uwe Umeripoti Kazini Wenenda Niache Na Isack
Tuangaikie Uamisho Tutakuja Ishi Na Wewe!"
"hapana Siwezi Kuondoka Nikamuacha Isack Nyuma Najua Hizi ni njama tu za mh waziri kitendo tu cha
kusafir wanamuua bora niwe naye awe katika ulinzi
zaidi"
"no my wacha niangaikie uamisho saivi mpaka kesho jion kila kitu kitakuwa tayari kesho kutwa asbuh
tunakuja mpz wangu akuna baya litakalompata mtoto"
Madam Jane Akajitahidi Kumbembeleza Inspekta baada ya majibishano Sana Hatimaye inspekta Akakubali
Kumuacha Isack kwa shingo upande
Kosa!
Kwa Upande Wa Mtoto Wake Mery Akuona Haja Ya Kumua tena kwa kuwa alishapoteza kumbukumbu alikuwa nikama
mtoto aliyezaliwa kila kitu kilichotokea kwenye maisha yake alikisahau
alikuwa ni Mery Mpya,baba yake alimtafutia mwalimu wa kuanza kumfundisha lugha (kisw) kuandika na
kusoma!
******
Madamu Jane Alibaki Akiishangaa Ile Karatasi Kwamba Anaitajika Mahakamani Mapigo Ya Moyo Wake Yalianza
Kumwenda Mbio!,siku Ilofatia ambapo ndo alipanga aanze kufatilia maswala ya uamisho ilimlazimu aende
Mahakaman Ambapo Alisomewa Shtaka Lake La Madai Kwa Kuiba Mtoto Na Kuishi Naye Bila Idhini Ya Baba
Mdogo Wa Mtoto Mr Zidu Kite!
Kwa Ilivyosemekana Mtoto Isack Alikuwa Akiishi Na Jiran Yake Mzee Alex Baada Ya Nyumba Ya Wazazi wake
kuungua moto!,kipindi icho bamdogo wake akiwa nje ya nchi,taharifa iliendelea kueleza kwamba bamdogo
wake aliporejea alimchukua toka kwa hao jiran zao na kwenda kuishi naye kabla mwalim wake yule wa shule
ajamchukua na kuishi naye!
Baada Ya Madam Jane Kusomewa Shtaka Lake Lile Wakapandishwa Mashahidi,shahidi Wa Kwanza Kupanda Alikuwa
Ni Jirani Bi Ney,akakiri Ni Kweli Aliwah Ishi Na Mtoto Yule Kabla Ya Ba Mdogo Wake Kuja Kumchukua!
Wakili Wa Zidu Akamuoji Isack Je Alishawah Kuishi Kwa Yule Mama Baada Ya Nyumba Ya Wazaz Wao Kuungua?
Isack Akajibu Ndiyo Aliwai Ishi Naye,bi Ney Akarudi Kukaaa!
Baada Ya Bi Ney Kushuka Akapanda Shahidi Wa Pili!
Moyo Wa Madam Jane Ulipasuka!,akuwa Mwingine Zaidi Ya Yule Alokuwa Mpz Wake wa zamani Mwalimu Gibson
Mwalimu Yule Alieleza Kumtambua Bi Ney Kama Mzazi Wa Isack Na Mara Kibao Alishaenda Shuleni Kumuadhibu
Pindi Akikosea Japo Madam Jane Alikuwa Akimtetea Mtoto Huyo Kumbe Alikuwa Na Lake Jambo!
Baada Ya Mwalimu Gibson Kutoa Maelezo Yake Sasa Ukawa Wasaa Wa Madam Jane Kujitetea Au Kutoa Maelezo
Yake!
Akaapishwa!,baada Ya Kula Kiapo Ndipo Alipoanza Kujieleza Pasina Uwoga Aliona Ukwel Ndio Ungemuweka
Huru!...
"mimi Nikiwa Kama Mwalimu Wa Taaluma Katika Shule Ya Msingi
gulioni nilishangazwa na kushuka kwa maendeleo ya mtoto huyu,kama mwalimu ndipo nilipoanza kuyafatilia
maisha yake nakumbuka kwa mara ya kwanza siku hiyo mwalimu gibson alikuja na mtoto huyu ofisin akatupa
fimbo walimu wote kumi tumchape mi sikuweza ndipo nilipoendelea kufatilia maisha yake nikagundua mtoto
huyu ananyanyaswa sana na walez wake ambaye ni mh wazir alex na mke wake bi ney!,
kuna kipindi mtoto huyu wik nzma sikumuona shule alipokuja alikuja na vijana wawili walinz wa msitu
pande wakasema wamemwokoa baada ya baba yak mdogo kumtupa kwa lengo la kumuua!
Nilienda kutoa maelezo polisi nashkur polisi walinipa idhini ni ishi na huyu mtoto ndo naishi naye
mpaka sasa!"
"ahsante madam jane kwa maelezo yako maref je kwa nin jesh la polisi alikumtia nguvuni huyo ba mdogo
wake?"
"alikuwa anatafutwa mpaka sasa"
"ha ha ha ha mh hakimu nadhani mdaiwa anaiongopea mahakama sidhani mtu anayetafutwa na jeshi la polisi
anaweza kujileta mahakamani"
watu wote pale mahakaman wakatabasamu madam jane akaona haya wakili wa Zidu Akaendelea
"unaweza Kuleta Mashahidi Akiwemo Huyo Inspekta Alokuruhusu Uishi Na Mtoto Ambao Si Mali Yako Pamoja Na
Hawo Walinzi Wa Porini Walomuokoa Huyo Mtoto?"
"ndiyo Muheshimiwa"
"Basi Natangaza kuahirisha kesi hii mpaka tareh 5 ya mwez huu ambayo ni wiki ijayo! mshtakiwa ulete
mashahidi"
Kesi Ile Ikafungwa,ulikuwa Ni Mwanzo Mbaya Kwa Madam Jane,toka Insp Nurdin Aondoke Akurejea Simu Yake
Aikupatikana!
Siyo Ivyo Tu Hata Jinsi Ya Kuwapata Wale Walinzi Wa Msitu Pande Ilikuwa Ngumu Akajipa Moyo Kesho Yake
Akasafiri Kuelekea Msitu Pande Nyumbani Akimwacha Isack Peke Yake
SIKU HIYO HIYO ASB
Ndege ya jeshi ilitua katikati ya msitu pande,ndani ya ndege ile alishuka mtu mmoja tu aliyekuwa ndani
ya gwanda za polisi kifuani akiwa na silaha akaelekea alipopajua yeye
Nusu saa mtu yule alirejea akaingia ndani ya ile ndege rubani akaiondoa tayari alishamaliza kazi ya
pili kati ya tatu alizokuwa nazo
Na sasa ilibakia moja tu
Isack!!!
ROBO SAA BAADA YA MTU YULE KUONDOKA!!!
Madam Jane Aliwasili Na Gari Lake Langoni Mwa Msitu Ule Alishangazwa Na Watu Wengi Akashuka Na Kuelekea
Pale Penye Watu
Alishtuka Kuwaona Wale Alowategemea kama mashahidi
Walinzi wa Msitu ule Wote Wakiwa Wamelala Chini Pasina Uhai Wakiwa Wametapakaa Damu!
Mwili Ulimsisimuka
'ni Nin Kilichotokea?!'
Akupata Jibu La Moja Kwa Moja Taratibu Akarejea Kwenye Gari Lake Na Kuondoka! Kichwani Alikuwa Na
Mawazo Mengi Sana
Tegemeo Lake Lilibaki Kwa Inspekta Nurdin Angempataje?!...
KIJIJI CHA NDASYO
Kilikuwa Ni Kijiji kinachokuwa,
inspekta Nurdin Alishuka Kwenye Gari Basi Alokuja Nalo Akaelekea Katika Kituo Alichoelekezwa
Wakati Akiwa Njiani Akakumbuka Ampigie Simu Mpz Wake Madam Jane Na Kumwambia Amefika Salama!
Alipoitoa Simu Alishtuka Kukuta Hata Mnara Ausomi,line Yake Kule Aikuwa Na Kazi Akarudisha Simu Mfukoni
Akaendelea Kukaza Mwendo Kukifata Kilipo Kituo!
Kulikuwa Ni Milimani Na Kulikuwa Na Hatua Ila Baada Ya Mwendo Mrefu Hatimaye Akakikuta Kituo Akaingia
Kituo Kilikuwa Na Chumba Kimoja Tu Na Askar Alikwepo Mmoja Aloweka Miguu Yake Juu Ya Meza Akisoma
Gazeti
Baada Ya Kuhisi Mtu Amekuja Akalitoa Usoni Lile Gazeti inspekta nurdin akamuona vizur mtu yule
aliyekwepo ndani ya gwanda za jeshi!
naaam si mwingine ni Zidu Katili,kubwa La Maadui!
Likaachia Cheko La Kiburi!
"mwanzo Nilikhofia Kukuua Kwa Kuwa Sikuwa Katika Idara Ya Polisi Ila Leo Sitokuacha Mzima Japo
Mheshimiwa Aliona Kukupa Uhamisho Inatosha Ila Kwangu Kifo Kitakupendeza Zaidi"
Mwanaume Akavua Mkanda kiunoni mkanda wa jeshi,Nurdin kuona ivyo akageuka ili akimbie hatua mbili tu za
zidu Nur Akawa Mikonon Mwake
"tafadhali Usiniue Mkuu Nipo Chini Ya Miguu Yako Sitomfatilia Tena Yule Mtoto"
ins Nurdin Akaomba Machoz Yakimtiririka,alijua Gwaride La Mjeda Naye Mafunzo Yake Ya Ccp,bado alitaman
kuishi!
"nisamehe mkuu usinifanye kitu wallah sitomfatilia tena huyu mtoto naomba usinidhuru"
hakuna asiye ogopa kifo ndugu msomaji! Cheko Likamtoka Zidu Huruma Ikamwingia Akamwachia Insp Yule
"usionekane Jijini Mwaka Huu,usifatilie Juu Ya Mtoto Yule Nimekusamehe!"
"asante Sana Baba,nimekuelewa Ndugu Yangu Sitokuja Mjin Na Ntafata Kila Nlichosema"
"maisha Mema"
Zidu Akaaga!...
'madam Jane,isack Utansamehe Nikicheza Ntapoteza Maisha Yangu Wacha Ntulie Zangu mie!'
Insp Nurdin Akawaza,ndan Ya Kituo kizima alikuwa yeye peke yake
"Wacha niende kule porin nkaue wale walinzi then wakat madam anakuja huku porini mim nikamalizane na
kale katoto chake'
jitu Zidu Likawaza Likiingia Ndan Ya Ndege ya kijeshi iloenda kumshushia Msitu Pande! Mwanaume akafanya
yake kisha
Akapaa Tena!
Sasa Alikuwa Mbele Ya Mtoto Isack! Katika Nyumba Ya Madam Jane!
Akiwa Kamshikia Bastola Mtoto Yule
"usiniue Baba..."
Isack Alilia,ila Kilio Chake Wala Uso Wake Ule Wa Majonzi Ukumuuzunisha Jitu Zidu Alidhamiria
"umentesa Sana Isack Mara Ngapi Umepona Kifo Changu Awamu Hii Sikuachi Nakuapia Moja Mbili Tat...
Zidu Akawa Akiesabu Huku Kidole Chake Kikiwa Kimeshakamata Kifyatulio
ISACK kwa mara nyingine tena anaingia mikononi mwa mwanaume wa kazi zidu k lengo likiwa moja tu
kummaliza!
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment