Search This Blog

Thursday 29 December 2022

MPANGO WA NJE NI PIGO BUTU LA KIFO - 5

   

Simulizi : Mpango Wa Nje   Ni Pigo Butu La Kifo

Sehemu Ya Tano (5)



Haswaa!


Akili yangu ilitenda vema nilimuona yule kijana akitokea kule juu na kwa kuwa gari yangu sikuwa nimeizima haraka sana niliisogeza kwenye nyumba moja tulivu na kuegesha hapo nilijua hakuna mtu ambaye angeweza kuitilia shaka labda mwenye nyumba hiyo. Nilipoteza muda kidogo huku nikijiuliza nini hasa kilichopelekea yule kijana kupanda juu ya lile jengo na kutazama upande ambao kulikuwa na nyumba nzuri ya kifahari yenye uzio mfupi. Hapa nikajua ipo namna na kwa kuwa huyu kijana hakuwa mbaya kwangu, niliamua kufanya kitu nacho ni kulivamia lile jengo kisha kujiweka ndani yake hata hivyo nilitaka kulipuuza hilo wazo kwani sikuwa najua lengo kuu hasa na pia sikujua mtu huyo alikuwa akitaka kumuua nani kwa bunduki ya kudungulia. Je, kama nikiingia ndani ya hilo jengo najua mtu aliyeko ndani anahatari kiasi gani? Haya yote yalikuwa ni maswali niliyokuwa nikijiuliza. Nikiwa naendelea kujishauri namna ya kufanya, nikaukumbuka usiku uliopita. Nikaikumbuka ile simu iliyokuwa ikiingiza ujumbe mfupi wa maneno na ilhali wakati naingia mule ndani simu ile ilikuwa imezimwa. Pia nikaenda mbali zaidi na kulifikiria lile pikipiki ambalo leo ndiyo nimegundua muhusika wa pikipiki lile alikuwa ni huyo kijana mwenye rasta. Hapa lile wazo la kuivamia hiyo nyumba likajiunda tena. Ndiyo, kwani nilikuwa na imani kubwa kabisa kuwa mtu liyekuwa akiingia jana mule ndani ya nyumba ya hayati Welason na mimi kumuacha kwenye mataa, alikuwa ni huyo.




Hapa amefuata nini? Nilijiuliza bado hata hivyo nilikuwa tayari nimelipisha wazo la kuingia ndani mzimamzima liwalo na liwe lakini nikiwa makini na mtu huyo hapo juu. Nilipiga hatua ndefu huku nikiwa na imani kuu kabisa kuwa ule ujumbe ulioingia kwenye simu ya marehemu Welason huwenda ulimtaka aje hapa afanye jambo, sasa kwa kuwa ujumbe huo umemkuta huyo kijana, akaamua kuja kuona nini kitafanyika mahala hapo, nilikuwa bado nikiwaza huku nikiwa nayasoma mazingira ya hiyo nyumba ambayo ilikuwa na uzio wa ukuta mfupi huku upande wa magharibi mwa nyumba hiyo kukiwa na mtaro mkubwa ambao ulikuwa mkavu bilashaka ulitumika kupitisha maji ya mvua yanayotokea mitaani. Ulikuwa ukirudi mahali ambako niliegesha gari langu na kwa upande wa huko mbele ukiendelea kutokomea nisikokujua hata hivyo upande wa pili wa ule mtaro kulikuwa na nyumba nyingine ya kifahari ambayo ilikuwa na ukuta mrefu ambao ulikingwa na nyaya za umeme. Nilipojiridhisha kwa uchunguzi wangu wa haraka huku jicho langu makini likimtazama yule kijana kule juu ambaye alikuwa akianza kuifunga bunduki yake ya kudungulia. Niliruka ule ukuta na kuzunguuka upande wa magharibi mwa nyumba ile kisha nikajibana mahali nikimuacha mlinzi wa nyumba hiyo akiwa analanda huku na huko sikutaka kumbughudhi maana sikuwa na shida naye shida yangu ni kutaka kujua mtu yule pale juu alikuwa na shida gani. Nilijua fika mlinzi huyo hakuwa ameniona. Nilipomuona mlinzi amenipa mgongo akitoka nje ya uzio niliwahi mlangoni, hadi nafika mlangoni mlinzi alishapotelea upande mwingine wa nyumba ile. Nikausukuma mlango kwa bahati nzuri ulikuwa haujafungwa nikajihakikishia uwepo wa mtu ndani. Nilipoingia ndani sikuwa nikimuona tena yule kijana pale juu ya ghorofa japo nilikuwa na uhakika kuwa kwa kutumia bunduki yake ya kudungulia yeye aliniona. Kwa akili na ujuzi wangu wa kijasusi nilijua pia alikuwa akipambambana na hisia zake kuwa anishuti au aniache. Sijui kama fikra zangu ziliendana na zake nilijibana kwenye sofa katikati na kutulia kimya nikivuta subira.




Nikiwa hapo nikiendelea kutulia, nilianza kukifungua kitabu changu cha mawazo mengi yaliyopita nyuma huku nikijishangaa nilivyokuwa nikifanya kazi ambayo sikuwa na uhakika kama itanipeleka kwenye hitaji langu la kuwarudisha madaktari nyumbani. Mtu asikudanganye, hii kazi ilikuwa ngumu mno na sikujua namna ya kumfikia mtu anayefahamika kwa jina la Musa. Akili yangu ilikuwa kama imeganda kwa namna ambavyo ilikuwa ikiwaza mambo ambayo kwa akili ya kawaida ilikuwa ikionesha waziwazi kuwa haiwezekani. Nilimkumbuka Luteni mstaafu Abdallah Khalid Mapande kwa kauli zake za kunitahadharisha kuhusiana na kazi hii ambayo kiongozi wangu alivalishwa njuga naye akaamua kunivalisha mimi ikiwa anajua kabisa kuwa ngoma ambayo naingia kuicheza haikujulikana ni ya kabila gani. Unaweza kujikuta unacheza ngoma ya kabila ambalo njuga ni matusi, watakuuwa. Bado niliendelea kuwaza maneno ya AKM nikiwa hapo kwenye sofa nimejituliza tuli. Kwa muda wa kama dakika saba mbele za usubirifu wangu ambao haukunikatisha tamaa bado, niliona mlango ukiguswa kutokea nje na mgusaji hakuwa akitania bali alidhamiria kuingia ndani, sikutaka kujipa imani kwamba alikuwa ni mlinzi wa nyumba ile ah, ah! Nilijipa utulivu mahali hapo hadi mtu huyo alipoingia. Kwa mara ya kwanza nilidhani alikuwa ni Spider Man kwa namna alivyovaa, alijificha sura yake huku akiwa amebandika kisafirisha sauti kwenye vazi lake kifuni. Nilijua huyu alikuwa hapa kwa nia mbaya na huwenda huu ndiyo ujumbe ambao ulimleta yule kijana ambaye nilimfahamu kama mpelelezi. Kwa utashi wangu katika medani za kivita nilikuwa na uhakika kuwa huyu alikuwa akiwasiliana na mdunguaji hata hivyo sikuwa najua alikuwa ni mdunguaji yupi. Nilikaa pale nikitazama hadi mtu huyo aliponipa mgongo na kuuona mwendo wake hapa ndipo nilipogundua kuwa huyu mtu alikuwa ni yule ambaye mara mbili nilimkosa nyakati za usiku. Mwili ukanisisimka, damu zikanichemka mwilini kwa ghadhabu.










Nilijua huyu alikuwa hapa kwa nia mbaya na huwenda huu ndiyo ujumbe ambao ulimleta yule kijana ambaye nilimfahamu kama mpelelezi. Kwa utashi wangu katika medani za kivita nilikuwa na uhakika kuwa huyu alikuwa akiwasiliana na mdunguaji hata hivyo sikuwa najua alikuwa ni mdunguaji yupi. Nilikaa pale nikitazama hadi mtu huyo aliponipa mgongo na kuuona mwendo wake hapa ndipo nilipogundua kuwa huyu mtu alikuwa ni yule ambaye mara mbili nilimkosa nyakati za usiku. Mwili ukanisisimka, damu zikanichemka mwilini kwa ghadhabu.




Hapa sitakiwi kumuacha aende. Niliwaza kisha nikasimama wima nikiwa na lengo la kummaliza palepale, nikatoa nastola yangu na kuikamata mkononi hata hivyo tayari huyo mtu alishaniacha kwa hatua nyingi sana. Wakati nikiwa natafakari namna ya kutoka pale na kumfuata ama kumshuti, akili yangu ilizidi kunionya juu ya maamuzi yangu kwani niliamini kufanya maamuzi ya haraka ni kumruhusu mdunguaji wake kunimaliza.




Hapana, ni lazima afe na ni lazima nifanye namna ya kummaliza. Niliwaza zaidi.


Nikiwa namtazama huku nikijiandaa kumuwahi asikunje ile kona kuifuata korido nyingine maana sikutaka ninyooshe mkono wenye silaha hovyo kwa kutokuijua kasi ya mdunguaji, yule mtu akaonesha ishara ya kuruhusu chochote kutoka kwa mdunguaji wake kunihusu mimi, niling'amua, nilijua alikuwa anamaana gani. Nikarusha hatua moja mbele kisha nikarudi kwa hatua hiyo hiyo nyuma kwa kasi isiyotarajika. Risasi ikavunja kioo kwa sentimeta chache kutoka nilipo nikajitupa pale chini kwenye uwazi wa sofa huku niking'ata meno kwa hasira na nisijue nampata vipi yule mtu wa kujificha sura. Nilijisogeza kwenye ukuta kisha nikachungulia nje ambako niliona kwa usahihi kupitia kioo cha dirisha na ukuta ule wa uzio kunipa msaada wa kuona mbali kwa ufupi wake.




"Mungu wangu!" Nilihamaki huku moyo wangu ukipata kichaa na kubadili mapigo yake kwa kuacha mapigo ya kawaida na kwenda kwa kasi. Nje ya ule uzio kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa wamekamata silaha madhubuti wakinisubiria kwa hamu.




Ni akina nani hawa? Askari? Ah! Ah! Hakuna askari wa namna hii hata kama ni mgeni kwenye nchi hii? Niliwaza kwa kujiuliza maswali mengi huku nikijionya zaidi. Nikiwa hapo nikasikia kishindo cha kitu kizito kilichodondoka upande ule alikoelekea yule mtu wa kujificha kwa mavazi yake, sikutaka anikute, nilivuta pumzi kisha nikahesabia moja hadi nilipokomea tatu, nikapiga mahesabu yangu kuhusiana na ugumu wa kioo hicho kisha nikachukua kasi na kujirusha kwa haraka sana na kutokea upande wa nje nikabingilia mithili ya mwanasarakasi huku risasi kadhaa ambazo nilikuwa na hakika kabisa zilikuwa za mdunguaji zikichimba karibu kabisa na nilipo mimi kwa kunikosa. Nilitumbukia mtaroni na kuanza kukimbia kwa kuufuata mtaro ule ulikotoka, nilikimbia kwa kuinamna kama ndama kwa kasi kubwa hadi nilipofika mbele ndipo niliponyanyua uso wangu kutazama upande ambao niliacha gari yangu.


Lahaula!


Kulikuwa kumejaa watu hatari wenye silaha. Nikabonyea tena kama Nguchiro shimoni au Nyegere anayenyatia nyoka aina ya Kobra na kuanza mbio hadi nilipofika mbele ambako niliona nyasi nyingi ndefu nikajirusha juu ya nyasi zile kisha nikabingilia kama gogo hadi nilipofika kwenye nyasi ndefu zaidi huku upande huo kukiwa na uzio wa Seng'enge. Nilipofika hapo nikatazama huku na kule nikasikia sauti zikihimizana kuwa wanifuate nilipo kwani wapo wachache ambao waliniona nikikimbilia huko nikajua nikizubaa nakufa hapo kikondoo tena kipumbavu kabisa. Hilo sikutaka litokee, nilitazama ndani ya huo uzio wa seng'enge nikaona ungeweza kunificha kwa mbio zangu kwa kuwa kulikuwa na majani mengi bilashaka kilikuwa ni kiwanja cha mtu mnene kwa pesa au kampuni maana kilikuwa kwenye uangalizi imara. Nilidandia seng'enge na kutumbukia upande wa pili kisha nikaanza kutimua mbio zaidi. Hawa jamaa walikuwa makini sana nao wakajitumbukiza huku wengine wakijaribu kukimbilia kule ambako waliamini nitatokea. Nilizidisha kasi ili wasiweze kuniwahi, sikutaka kabisa kuingia mikononi mwao pamoja na kuongeza kasi ya ukimbiaji hata hivyo sikusahau kuwa kulikuwa na risasi zenye uchu nyuma yangu hivyo nikawa nakimbia kwa mtindo wa zig zag au mwendo wa Mbayuwayu. Nilifanikiwa kwani wakati nafika ukingoni wao bado walikuwa nyuma na kwa kuwa nilikuwa kwenye kasi niliweza kuruka sarakasi moja maridadi kama kishada na kuangukia upande wa pili ambako kulikuwa na majengo mengi yenye hadhi tofauti. Sikujua naelekea wapi pia sikujua kwanini hawa wajinga waliamua kunifukuza kwa namna hii. Akili yangu ilikuwa ikifanya kazi ya kuwafikiria huku nikijituma mwili kuweza kuwa mbali na maadui hawa. Nilijuta wakati mwingine na kujiuliza kwanini nimeingia sehemu nisiyoiju hatari yake hata hivyo hii ilikuwa ni miongoni mwa kazi yangu hivyo sikupaswa kuiogopa hatari yoyote zaidi ni kupambana nayo ili kushinda. Nilitokea barabarani na kuifuata barabara hiyo pana ambayo sikujua inaelekea wapi japo nilijua kuwa ilikuwa ikitokea jijini.


Mtumeee!


Huku nilikoamua kuifuata barabara nilijipalia makaa ya moto mwenyewe, gari mbili zile nyeusi zilikuwa nyuma yangu kwa kasi kubwa sana, nikaongeza mwendo kuweza kuziacha mbali zaidi hata hivyo kasi yangu haikuwa ikiendana na gari hizo huku watu waliomo garini wakiwa wameanza kuchungulia madirishani na silaha wengine kutokea gari nyingine wakiwa makini nyuma ya bodi na silaha pia. Mirindimo ya risasi nyuma yangu ikaanza akili ikafunguka sasa na kuamini kilichokuwa kikiwindwa ni roho yangu tu na si kitu kingine. Kwa mbali nilianza kusikia sauti ya chopa ikiwa inakuja nilipo.


Kifo.




"Wamepanga kunipoteza kabisa hawa wajinga." Nilijisemea huku nikiongeza kasi maradu na kwa wakati huo huo nikiwachanganya walengaji na kuzipoteza maboya risasi zao. Kuendelea kuifuata barabara hiyo ndefu na pana nisiyojua inaelekea wapi kwa wakati huo, ilikuwa ni kukiandaa kifo changu mwenyewe hata hivyo sikuwa na namna nyingine kwani hapo nilikuwa nje ya mji tayari na hakukuwa na makazi mengi ya watu. Nilizidi kukimbia kwa mtindo wa Mbayuwayu ili kuzipotosha shabaha zao. Nikiwa nazidi kuongeza kasi ile kali zaidi ili zile gari zisinifikie zaidi na kuwafanya wa kwenye Chopa wakifike eneo hilo wasinikute, mbele yangu kukatokea gari nyingine moja ifananayo na hizi mbili nyuma yangu.


Aisee!


Niliogopa sasa, moyo ulikuwa ukipiga kwa kasi kubwa huku jasho likinikatika kupita maelezo. Sikuwa na namna nyingine zaidi ya kujirusha upande wa kuume kwangu wa barabara ambako kulikuwa na korongo dogo. Nilifanya hivyo kwa maana kubwa kwani baada ya korongo hilo kulikuwa na mwendo mfupi wa kasi kulikabiri pori kubwa lililosongamana. Nilibingilia hadi mwisho wa korongo lile huku nikijipigiza kwenye mawe chipukizi. Sikuyajali maumivu yangu bali nilikimbia kwa kasi ya mbio fupi za marathon kisha nikageuka nyuma kutazama maadui zangu walipo. Mungu alinisaidi kwa kuniamuru nitazame nyuma kwani niliona mtu mmoja akiwa ananipima shabaha kwa bunduki kubwa huku Chopa ikiwa usawa wangu watu wawili wakiwa wamejitokeza huku na huku wakiwa na silaha, nikaruka kama nyani kichani na nilipotua na magoti nikatambaa kwa kitambo kidogo mithili ya nyoka anayewahi windo lake lisimkimbie nikasimama tena mbio kali zikaendelea. Zile risasi zilinikosa na kuchapa majani.




"Hawa wajinga wataniuwa nisipokuwa makini!" Nilijisemea mwenyewe nikiwa ndani ya pori lile sasa nikiwa na kazi ya kupambana na maadui wa chini, mdunguaji na waliyoko kwenye Chopa hii ilikuwa ni zaidi ya hatari kwangu.




"Asitokeee! Afie humuhumu!" Nilisikia sauti ikitoa amri sasa nikajua inayofuata ni vita ya msituni. Akili yangu ikanikumbusha haya mambo ya msituni nilipokuwa Austria kwenye msitu wenye nyoka wakali nikiwa kwenye mazoezi makali ya kijeshi ikiwa ni awamu yangu ya lala salama.




Wataisoma. Niliwaza.


Nilikuwa nikiendelea kukimbia huku nikiwa nimechoka sana, sasa nilikuwa napandisha kijimuinuko fulani kwa lengo la kuweza kuwatazama maadui zangu walipo huku Chopa ikiwa inazunguka juu ikiachia mvua ya risasi ambazo kwa bahati nzuri kwangu zilikuwa zikinikosa na kufyeka matawi ya miti. Nikiwa nazidi kuparamia ule muinuko huku nikiweka tahadhari, risasi moja ikapita pembeni ya shingo haraka sana nikajiweka nyuma ya mti, nyingine ikachimba ule mti mkubwa kwa nyuma yangu.




Mdunguaji. Niliwaza.




"Mungu wangu nafanya nini hapa?" Nilijiuliza nikiamini huyu mjinga aliyekamata 'Sniper refle' hakuwa mwenye uwezo mdogo. Nilijua fika kuchelewa kwangu hapo ni kuwafanya wengine wanikaribie au kuifanya Chopa ije mbele yangu na kunishambulia na vilevile kwa kuwa nilizijua tabia za wadunguaji hapa ni lazima anizunguukie ili kunipatia shabaha maana huwa wadunguaji hawapendi kupoteza risasi zao bure na kila moja inapotoka huwa inatoka kwa malengo maalumu. Nilitazama mbele yangu kwa umbali fulani nikaona mti mwingine mkubwa zaidi kwa haraka nikajitupa chini na kuanza kutambaa kama nyoka aina ya Bafe, taratiibu sana bila kutikisa majani wala kuacha sauti ya mchakacho. Bahati ilikuwa upande wangu kwani pale nilipokuwa nimesimama zilipita risasi kama mvua na sauti ya bunduki kali zikisikika sehemu mbalimbali na kutokea juu ya anga ambalo lilizingirwa na miti mikubwa.




Wamenikaribia sasa hakuna budi kupambana. Niliwaza nikiwa natambaa chini huku zile risasi zikipita hewani juu kidogo ya mimi nilipo na zile zitokazo kwenye Chopa zikichakaza matawi ya miti zikinikosa kwa sentimita chache mbele yangu na kunifanya nitulie kwanza kimya kisha baada ya utulivu niendelee mbele. Niliukaribia ule mti na kusimama nyuma yake huku nikiitoa mafichoni bastola yangu aina ya Browning Buck mark. Nikaishika mathubuti kisha nikafumba macho nikivuta hisia mahali maadui walipo nilikuwa na lengo la kutopoteza risasi hata moja kwani sikuwa na silaha nyingine kama hiyo zaidi ya visu viwili nilivyovihifadhi mafichoni. Nilijitoa mtini kwa kasi, risasi ya mdunguaji ikanikosa tena huku na mimi nikiachia za kwangu tatu. Nilisikia kelele za maumivu zilizotoka kwa awamu tatu nikajua nimetenda vema.




"Anatushambulia tuweni makini." Nilisikia sauti kali mahali ambapo hapakuwa mbali na mimi nikaamua kuwachezea mchezo ambao wao walikuwa hawaujui nao ni kuwazunguka na kukaa nyuma yao huku nikimpa kazi mdunguaji wao ya kutokujua anidungue kwa namna gani. Nilikimbia kwa kasi huku nikicheza na akili ya mdunguaji pekee ambaye nilikuwa na uhakika kabisa kuwa asingeweza kunishuti kutokana na kukimbia kwangu kwa kuifuata miti na kuizunguka. Mara nilisikia mlipuko mkubwa huku ile Chopa ikihangaika na kupoteza muelekeo, niliona hilo kupitia uwazi mmoja uliyopo kati ya mti na mti, nilikuwa kwenye kasi bado nikijiuliza ni nani ambaye alifanya kazi hiyo ya kuidungua ile Chopa ya maadui ambayo kwangu ndiyo iliyokuwa tishio. Nilipokuwa nikizidi kukimbia nikamkumbuka yule kijana ambaye awali kule mjini kulipoanzia hili sekeseke alikuwa juu ya nyumba nisijue anafuatilia nini. Nilikumbuka pia alikuwa na bunduki ya kudungulia, hapo nikapata nguvu na kujiamini huwenda sikuwa mwenyewe eneo hilo. Risasi kadhaa zilikuwa zikinikosa hata hivyo sikujali na sikupunguza mwendo. Nilikimbia hadi nilipopata utulivu sasa nikiwa nyuma ya maadui wengi. Nilianza kuwafuata na kuwamiminia risasi hovyo, walichanganyikiwa najua kwa kudunguliwa Chopa yao pia hawakudhani kama wangekutana na upinzani ambao nawapa, nilidhani hivyo, walichanganyikiwa kuliko kawaida na nilijua kuzitumia risasi zangu vema, nikiwa bado nashambulia huku nikisikilizia kama kulikuwa na mdunguaji, kimya kilikuwa kikuu kwa upande wao na niliweza kusikia utulivu huo kwa kuwa bastola yangu haikuwa ikitoa sauti.










Nilianza kuwafuata na kuwamiminia risasi hovyo, walichanganyikiwa najua kwa kudunguliwa Chopa yao pia hawakudhani kama wangekutana na upinzani ambao nawapa, nilidhani hivyo, walichanganyikiwa kuliko kawaida na nilijua kuzitumia risasi zangu vema, nikiwa bado nashambulia huku nikisikilizia kama kulikuwa na mdunguaji, kimya kilikuwa kikuu kwa upande wao na niliweza kusikia utulivu huo kwa kuwa bastola yangu haikuwa ikitoa sauti. Nilishambulia hadi risasi zilipokoma hata hivyo nilisikia sauti za risasi zikirindima tena na hizi zilikuwa zikiwadondosha maadui, nilitabasamu na nilijua fika atakuwa ni yule kijana amekuja kunisaidi. Hamu ya kutaka kuonana naye ikawa juu zaidi kuliko kawaida. Nilitaka kumuuliza kuhusiana na kwanini watu hawa wanauwa na nini zaidi hasa kinachoendelea hapa nchini vilevile yeye ni nani hadi anisaidie. Nikiwa hapo nikasikia sauti ikivuma.




"Acheni kushambulia hamjui kama mnauwa wanaomtafuta adui!" Sauti kali ilikuwa ikikalipia.




Waache kushambulia? Hawajui kama.....! Nilijiuliza mawazoni nikajua bado nilikuwa kwenye hatari hata hivyo pamoja na kujificha kwenye miti bado sikuona madhara ya mdunguaji aliyekuwa akinishambulia hapo awali. Nilipatwa na wasiwasi sana.




Kwanini hashambulii tena? Nilizidi kuwaza na kuwazua. Mbele yangu kulikuwa na mwendo mfupi kabla sijavuka mfereji mkubwa uliyokuwa ukipitisha maji. Akili yangu ikanituma nivuke huo mfereji na kuendelea mbele zaidi kwani sikutaka kurudi tena nyuma kwa kuhofia usalama wangu niliogopa sana, niliogopa kuingia kwenye matatizo wakati nikiwa sijafika popote. Nikiwa napiga hatua kuufuata ule mteremko nikasikia vishindo vya mtu aliyekuwa akikimbia kwa kasi nyuma yangu na alikuwa karibu yangu kabisa. Nilipogeuka kutazama, nilikuwa nimekwisha chelewa. Nilimuona mtu akiwa amevaa maski usoni akija kama Komba arukiaye tawi la mwembe au Chui aliyekuwa akimrukia Mbawala, akanivamia na kwa kuwa sikuwa nimejidhatiti, akanidondosha na kuanza kuvingirishana naye, alikuwa na nguvu sana na ni kama alikuwa akifahamu uwezo wangu maana alikuwa akijitahidi sana kunizuia mikono huku miguu yake ikiibana miguu yangu. Alikuwa na lengo la kuniweka chini na yeye awe juu. Sikukubali hata kama alinibana, niliminyana naye hadi hatua ambayo nilimuona akiachia mkono wangu mmoja na kunitandika ngumi ya uso hata hivyo nilitingisha kichwa changu na ngumi yake kupiga mchanga kisha kunizuia tena kwa haraka mikono yangu. Nikaona ananichezeshea shere huyu bwege mtozeni. Nilijivuta na kumchapa kichwa cha mdomo nilimsiki akiguna kama nyani aliyeona kundu la mwenzake lilivyo jekundu ilhali na yeye lake hivyohivyo ingawa halijui. Akalegeza mikono. Nikampiga ngumi mbili za mbavu kisha kwa kutumia miguu yangu niliyoikunja na kuikunjua, nikamsukumia nyuma akabingilika nikamuwahi hata hivyo aliwahi kusimama nikasimama pia. Alirusha mateke kadhaa ambayo yalinipa wakati mgumu kuyazuia japo nilijitahidi, nikamrukia na kumtandika ngumi ya uso nilipoona anataka kunizidi. Mara risasi ikamchana bega lake la kushoto nikajua ni yule mdunguaji amepata uhai na sasa badala ya kunilenga mimi akanikosa na kumjeruhi mwenzake. Nikachachawa huku nikiamini kifo changu kitakuwa ni hapohapo msituni wakati bado nilikuwa na kazi nzito.




"Ni mimi!" Nilimsikia akisema huyu mtu aliyevaa maski usoni baada ya kujeruhiwa na ile risasi hata hivyo nilimuona akitoa macho na kuanza kutimua mbio na kutokomea huku akitoa ishara fulani kama kuwaita wenzake. Sikujua ni kwanini hili limetokea pia sikutaka kujiaminisha. Nilitimua mbio maana ile ishara ya yule mtu ilikuwa ikiamrisha kitu ambacho kwangu kingekuwa ni hatari. Niliuvuka ule mfereji kwa kasi na kukimbia sana, mwili wangu ulikuwa na majeraha mengi hata hivyo sikusimama. Nilikuja kutokea kwenye mbuga kubwa nako nilizidi kukimbia hadi akili yangu ilipoanza kufanya kazi upya. Kwa mbali niliona shamba kubwa likiwa limepandwa mimea mingi ya muda mfupi na ile ya kudumu. Nilipotazama vizuri niligundua kuwa lile lilikuwa ni shamba la AKM nikatabasamu hata hivyo zilihitajika mbio nyingi na hekaheka za kupita vichaka vya miiba na kadhalika. Niliona mabwawa makubwa ambayo yalijaa ndege walao samaki kama Koho, Kongoti, Kobwe, Kukuziwa, Kwarara, Flamingo, Shakwe, Kulastara na Korongo wakiwa wanarukaruka kwenye mabwawa hayo mengi wakijitafutia kitowe. Niliwaona wakiruka na kutanua mbawa zao nyeupe huku wengine wakionesha ujuzi wao wa kuzama majini na kuibuka na Kambare wakubwa. Nilistaajabu uwezo wa Mungu na kwa muda niliyasahau maumivu nikiyapa macho chakula. Japo nilikuwa nikiwaza kuhusiana na wale watu huku nikikanyaga nyasi za eneo hilo kichovu zaidi hata hivyo nilimuomba Mungu nifike kwa Luteni mstaafu Abdallah Khalid Mapande salama salmini. Nikawa natembea huku mara chache nikitabasamu kwa sauti nzuri za ndege wajaao vichakani kama Kurumbiza na kadhalika. Nikiwa nazidi kutembea huku kichwa changu kikiwa na mawazo mia kidogo, nilisikia sauti ya mfoko wa hatari huku nyasi zikiwa zinatikisika. Nilihofu hata hivyo akili yangu ilienda mbali na kuukumbuka msitu wa mazoezi makali ya kijeshi ya hatua yangu ya lala salama ya mafunzo ya jeshi nchini Austria ambao ulikuwa na historia ya kuficha nyoka hatari sana na wenye sumu ambao wengi wakiwa na hasira hasa wakiona kitu kisicho cha kawaida kwao, hufoka namna hiyo.




"Huyu atakuwa ni nyoka na kwa mfoko huo bila shaka atakuwa ni nyoka aina ya Mamba mweusi (Black Mamba). Hata Kobra!" Nilijisemea huku nikiongeza umakini nilikuwa na hakika asingeweza kunidhuru kwa haraka kwa kuwa nilivaa mavazi ambayo kupitisha meno yake ilikuwa ngumu hata hivyo sikujipa imani ya ushindi. Nilitazama kwa kina zaidi. Asalaale! Alikuwa ni nyoka mkubwa mwenye jeuri na uwezo mkubwa wa kurusha mate yenye sumu. Alikuwa akisogea taratibu kama mwanamwali amdenguliyae mumewe kumsogelea. Kichwa chake kilikuwa wima kama kirungu cha Morani atafutaye Ng'ombe, ndimi zake mbili nyeusi nje. Hakika alikuwa ni nyoka asiyehitaji umchokoze ndipo akudhuru. Alikuwa ni Mafasa nyoka mkubwa mwenye macho mekundu huku katikati kukiwa na kiini chenye umbo la Diamond au karata ya kisu. Nyoka aina hii mara nyingi huwa na sumu kali mno na hapa nilitakiwa kuwa makini na macho yangu kwani alikuwa na uwezo mkubwa wa kurusha mate yenye sumu kwa umbali mzuri. Hakuacha kunisogelea nikaona kama nikiendelea kumtazama angeweza kuniwahi kwa mate yake yenye sumu. Nilikichomoa kisu changu pekee ambacho kilikuwa ndiyo silaha baada ya bastola yangu kuishiwa na risasi. Nilikirusha kile kisu ambacho kilikwenda kuikata shingo yake na kumuacha akigaagaa chini nami nikiwa nimeyakwepa mate yake ambayo aliyarusha kwa shabaha ya kuingia machoni, nilikiokota kisu changu nikakifuta na kukirudisha kwenye ala yake. Sasa sikuzembea maana niliamini huwenda eneo hilo kukawa na nyoka wengine wakali zaidi. Nilitimua mbio kali sikujali tena uchovu nilio nao.




_____________




Marietha na Mabule walikuwa wakikimbia hovyo huku wakimfuata Sembuyagi Mpauko mahali alipokuwa akielekea, wakati hilo lilipokuwa likiendelea, walikuwa wameshauvuka ule mtaro ambao hupitisha maji wakati wa mvua sasa walifanikiwa kumuona mtu ambaye ndiye waliyekuwa wakimkimbiza. Alikuwa ni mwanamke ambaye alionekana kuwa shupavu sana na jinsi alivyokuwa akikwepa risasi na kukimbia ilidhihirisha wazi kuwa hakuwa daraja dogo. Hii ilimjengea wasiwasi Mabule lakini pia Marietha. Kwanini wamkimbize mtu ambaye hakuwa akikimbizwa na askari bali watu ambao hawakuonekana kama ni wanausalama wala nini, hii ilikuwa ni nini maana yake. Walijiuliza sana hata hivyo Sembuyagi hakuacha kuwaamuru wakimbize na wakati mwingine kuwaamuru wapige risasi wapatapo nafasi ya kufanya hivyo. Ilikuwa ngumu sana kwa wao kufanya hivyo kwani taaluma yao kama wanausalama hawakuwa wakiendeshwa kufanya kitu bila wao kuwa na hakika kama ni cha msingi ama lah! Waliheshimu maamuzi hayo kutoka kwa mkuu wao tu na si mtu aliyepewa uongozi namna kama hiyo. Hapa Mabule akaanza kumtilia mashaka Sembuyagi. Hakuwa akijua kama hili hakulijua tangu hapo awali, hakuliona ama la! Akawa anafuata mkumbo ili kujiridhisha kama ni kweli huyo mwanamke ni adui yao ama naye anafuatilia wanachofuatilia wao na zaidi wakitaka kumjua kiundani. Kitu walichojiapiza yeye na Marietha kila mmoja kwa wakati wake ni kuwa wasingeweza kuruhusu risasi kushambulia pasipo kuwa na yakini na wamshambuliyae. Walikuwa wakimuandamisha sehemu mbalimbali kama barabarani hata alipokuja kuingia kichakani. Hawakuthubutu kupiga risasi wala hawakuthubutu kuzilazimisha nafsi zao ziamini kama kweli huyo binti alikuwa ni mbaya kwao.




Msitu ulikuwa mkubwa, Chopa ilikuwa ikizunguka kila walipo huku risasi zikimuandama yule binti, hali ilikuwa tete mno na ilitishia usalama wake. Kuna kitu kipya kingine Marietha alikiongeza kupitia kazi aliyopewa na mkuu wake. Hii ilijionesha kwa Sembuyagi, kwenye shati lake juu kidogo karibu na kola kulikuwa na kisafirisha sauti kidogo sana mfano wa kishikizo cha shati. Hakutaka kumgutusha na pia hakutaka kumwambia Mabule. Hili lilimuumiza kichwa mwenyewe, imani yake kwa wenzake hao ambao waliteuliwa kuifanya kazi pamoja ilimtoka. Inawezekana si yeye tu aliyekuwa akidhani visivyo labda kulikuwa na mwingine alikuwa akiwaza au akiamini ndani yao yupo mtu asiyeeleweka.




Ni kweli?...aaah! Hapana. Hata kama ni kweli hakuwa na imani ya moja kwa moja hii ikawa sababu ya neng'eneka na nafsi yake pekee.




"Marietha!" Aliita Mabule walipokuwa wamepewa amri walale chini wakimtega adui waliyeambiwa sharti wamuuwe. Mara wakasikia mlipuko kuashiria kuwa ile Chopa ilikuwa imedunguliwa pengine na kulipuka. Hii ikawaweka kimya hata ile sauti ya Mabule ya kuita ikawa imemezwa na ule mlipuko.




Hii chopa itakuwa umelipuliwa na nani....? Likawa swali lenye kupita kwenye vichwa vyao wenyewe....!




"Sema Mabule?" Akaitika Marietha kwa sauti ya chini huku akiitoa mikono yake masikioni baada ya ule mlipuko uliyoyazibua masikio yake maana mlipuko haukuwa mbali na hapo.




"Huyu mwanamke ndiye aliyefanya haya?" Akauliza Mabule.




Mwanamke ndiye aliyefanya haya? Akawaza Marietha bila kurudisha jibu alijualo la kwamba ndivyo adhaniavyo ama la...! Hata hivyo wito ulimuita mlipuko ukiwa bado? Sasa ni kweli alimuita kwa lengo hilo....au? Marietha akamtazama Mabule kwa macho makali kisha akasema.




"Hili limekuja baada ya wito wako Mabule, mlipuko ulikukuta ukiwa umekwishakuniita tayari, sema kilichofanya uniite?" Mabule akameza mate huku akishuhudia mapigano ya risasi yaliyokuwa yakiendelea kati ya huyo binti na watu wasiowajua kama ni askari au wanausalama maana walikuwa katika shuruti ya upande wao. Sehemu aliyolala na Marietha ilikuwa ni vigumu sana kwa wao kuweza kuonekana.


Walikuwa upande gani...? Wa maadui...?


Hakika nafsi yake ilikuwa ikiwaza mengi sana. Walijificha chini ya shina la mti mkubwa ambao ulijaa mizizi mikubwa huku moja kati ya mzizi ukiwa ndiyo mkingamo wake, Marietha alikuwa amezuiwa na muinuko hata hivyo ulimuwezesha kuona kilichokuwa kikiendelea mbele.








Hakika nafsi yake ilikuwa ikiwaza mengi sana. Walijificha chini ya shina la mti mkubwa ambao ulijaa mizizi mikubwa huku moja kati ya mzizi ukiwa ndiyo mkingamo wake, Marietha alikuwa amezuiwa na muinuko hata hivyo ulimuwezesha kuona kilichokuwa kikiendelea mbele.




Wanafanya nini...? Akawaza Mabule akiwa anafikiria hoja ya Marietha ya kuwa kipi kilifanya amuite. Wazo hili likawa limeelemea kwa shuruti za kiongozi wao wa msafara.




Kwanini awashurutishe kitu ambacho wao hawakukijua kiundani...? Akaliacha na kumgeukia Marietha huku akihakikisha atakachokisema hakisikiwi na Sembuyagi Mpauko ambaye alikuwa katikati ya kichaka huku mara chache akiruhusu risasi zienda upande ule wa majibizano makali ya risasi.




Anamshambulia nani...? Adui? Ni audui yupi sasa kati ya hao wanaowajua wao....ebo!




"Ume....umeona kitu kwenye shati la Sembuyagi?" Akauliza Mabule kijana makini toka kwenye kikosi maalumu cha kipelelezi ndani ya usalama wa taifa nchini Tanzania. Marietha akageuka haraka kumtazama Mabule, akajua fika kuwa Mabule alikuwa yupo kwa ajili ya kazi kweli na si mamluki ndani ya kazi kama hisia zake zilivyoanza kujiunda kwa kiongozi wao Sembuyagi. Alikuwa akimuhisi vibaya kwa kuwa alitoka na Sembuyagi taifa moja lakini kwa swali hilo akawa na nguvu na imani ya pamoja, akamuuliza kwa kumtega.




"Unahisi nini Mabule kwa ulichokiona....?"




"Tunapelekwa kama Punda wa dobi mbele ya Simba mwenye njaa ya ushindi tusiyoyajua mashindano yake Marietha, tutauwa watu muhimu halafu tuwaache wabaya...!"




"Nimekupa....!" Marietha alidakia kwa kumkatisha Mabule hata hivyo yeye mwenyewe hakufika mwisho akakatishwa na hali ya utulivu wa ghafula uliotokea punde baada ya majibizano ya kama dakika tano ya risasi kurindima. Ulikuwa ni utulivu mkubwa kama kwamba hakukuwa na makabiliano ya hatari hapo kabla, alipotazama mbele ambako kulikuwa kukiendelea majibizano hayo, alimshudia yule dada akihamanika huku akiitupa bastola yake pembeni. Alikuwa ameelewa kitu na alipomtazama kiongozi wake akagundua naye silaha yake ilikuwa imekwisha risasi hata hivyo alikuwa akiangalia kule ambako yule mwanamke yupo na kulikuwa na kitu akikitoa mfukoni mwake kwa siri kubwa.


Bastola ya yule dada iliisha risasi. Akawaza Marietha.




"Shambulia sasaa....! Shambulia huyo mwanamke afie humu hatakiwi kukimbia..!" Sembuyagi Mpauko alikuwa akibwatuka kwa sauti kubwa sana. Alikuwa akitoa amri ya watu kushambulia kwa kuwa yeye hakuwa na silaha.




Akh!... Tushambulie? Tumshambulie huyu mwanamke tena....? Hapana. Mawazo ya Marietha yalikuwa yakipingana na kauli ya kiongozi wake kwa asilimia kubwa sana. Bado walikuwa kwenye sintofahamu ya hali ya juu kuhusu mahusiano baina ya watu wale wasiyoeleweka kama ni askari na Sembuyagi au Sembuyagi na yule binti.


Mirindimo ya bunduki ikaanza upya, Mabule na Marietha wakaweka umakini mbele kutazama, hadi hapo bado hawakujua wafanye nini, walimuona yule mwanamke akikimbia kulikabili bonde moja lililoko upande wa magharibi.


Wakashangaa!


Mara wakaanza kuwaona watu wale ambao kwa upande wao walikuwa kama wakiwapa msaada kwa kupambana na yule binti japo hawakuthubutu kutupa risasi hata moja. Yule mwanamke alikuwa akikoswakoswa na risasi za wale watu kwa sentimita chache huku risasi hizo zikimegua magome ya miti na kuangusha miti midogo. Alikuwa akijikinga kwenye miti mikubwa kukabiliana na mashambulizi hayo ambayo yalimuelekea kwa kiwango kikubwa. Hakuwa na bastola wala bunduki yoyote kuweza kujibu majibizano yale hata hivyo walianza kuwaona wale watu wanaomshambulia yule dada wakidondoka mmoja mmoja tena kwa kiwango cha hali ya juu. Wakahamanika wasijue ni nani aliyekuwa akiwashambulia wakaanza kubadili mashambulizi kwa kutupa risasi hovyo hata hivyo hawakufua dafu.


Walikwisha.




Nani aliyekuwa akiwashambulia kiasi kile tena kimya kimya bila kusikika kwa sauti ya bunduki..?




"Kuna mdunguaji eneo hili?" Aliuliza Mabule hata hivyo Marietha hakujibu, hiyo ni mara baada ya kumuona Sembuyagi akitupa bastola yake chini ambayo nayo iliisha risasi na kumkilimbilia yule mwanamke. Kitu cha kushangaza zaidi ni kwamba Sembuyagi alivaa maski kuziba sura yake.




Kwanini? Aliwaza. Yule mwanamke alikuwa tayari akiukaribia mfereji mkubwa uliokuwa ukipitisha maji. Swmbuyagi akamrukia yule mwanamke na kumsukumia nyuma na kumbabatiza kwenye miti wakakamatana kama wanamieleka wakabingilishana huku na huko. Kila kitu kilikuwa kikionwa nao. Iliwachanganya sana hali hiyo akina Mabule na hawakujua kama lipi lilikuwa ni amuzi sahihi kati ya wao kuamini yule mwanamke hakuwa adui au Sembuyagi hakuwa upande wa maadui.......




__________




Kwa upande huu mwingine nao Frank akiwa na silaha ya kudungulia akiwa palepale juu ya lile jengo ambalo alikuwa akishuhudia kilichokuwa kikiendelea, walipata kuwaona watu wengi wakimkurupusha yule mwanamke na kuanza kumuandama kwa silaha. Aliweza kuona namna yule mwanamke alivyokuwa akikimbia kwa shida akijitahidi kukwepa magari yaliyokuwa yakimuandamisha huku wakati mwingine akikabiliana na waliokuwa wakimkimbiza kwa miguu. Frank akiwa pale juu aliiona Chopa kubwa ikiamka kutokea nyuma ya lile jengo refu la ghorofa ambalo alililona hapo awali likitua na kuchukua uelekeo ambao yule mwanamke alikimbilia.




"Blood fools....wapuuzi sana hawa wanataka kufanya nini...? Ooh! Gosh...!" Aliongea kwa ghadhabu kubwa akiwa pale juu sasa akauhisi mwili wake ukichemka kwa hasira na ari ya kufanya kazi ya ziada kuhakikisha anamsaidia yule mwanamke kutoka kwa watu wale wasioeleweka.


Hakusubiri tena.


Alitoka kwa kasi pale akishukia kule juu na kuja kutokea nje ya lile jengo akalikabili pikipiki lake na kulitoa kwa kasi hadi akawa anashuhudia yote yaliyokuwa yakiendelea akiwa umbali fulani. Hadi yule mwanamke anaingia msituni. Hakuwa na muda wa kupoteza, mwili wake ulijaa wasiwasi mkubwa sana na hakujua nini kingeweza kutokea huko porini. Moyo wake ulijaa ghadhabu za kuzidi mno. Juu lile Chopa lilizidi kuogopesha kwa kukatiza mara kwa mara huku watu waliokaa upande huu na huu kwenye ile Chopa wakimimina mvua ya risasi kila walipohisi huyo mwanamke yupo. Alishalitelekeza lile pikipiki lake na sasa alikuwa ndani ya msitu uliojaa makabiliano ya kutishia amani kwa kiwango kikubwa. Begi lake refu mfano wa mfuko wa kubebea gitaa lililokuwa limeibeba Pro Series 2000 HTR, 338 Lapua magnum, lilikuwa likining'inia mgongoni na mkononi akiwa amekamata bastola aliyoifunga kiwambo cha kuzuia sauti. Frank Matiale kazi yake kubwa ilikuwa ni kuwamaliza maadui kimyakimya bila kelele. Alikuwa na uwezo mkubwa sana na mapigano ya msituni na alishinda mashindano mbalimbali ya namna hiyo hata alipokuwa mafunzoni wakati akipata mafunzo makali ya kijeshi kubwa na alilokuwa akilimudu zaidi ni shabaha. Ukiachilia mbali mapambano ya ana kwa ana pia alikiwa na uwezo mkubwa wa kulenga shabaha na hiki kilikuwa ni kipawa alichokuwa akikiringia sana.




Alikimbia kwa kasi kubwa kutokea nyuma ya mti mkubwa aliokuwa amejibana kuipisha ile Chopa ipite akauruka mzizi mkubwa wa jiti moja kubwa na kujitupa chini akibingilia kuelekea korongoni ambako ndiko mapambano yalipokuwa yamepamba moto. Muda mwingine alikuwa akikoswa na mvua ya risasi iliyokuwa ikisababishwa na watu wale ambao walining'inia pembeni mwa ile Choma mithili ya popo. Alibingilia vilevile akijipigiza kwenye miti na mawe hadi alipokuja kutulia chini ya mti mkubwa akatazama huku na huko kutazama usalama alipoona kuko sawa akaanza kupigia mahesabu ile Chopa ambayo kwa kiasi kikubwa alimini kuwa hata yeye ameonekana. Alijiweka sawa na bastola yake maana Chopa ile ilikuwa haipiti umbali mrefu. Aliwatazama wale watu waliyokuwa wakining'inia huku na kule akavuta pumzi ndani ya mapafu yake na kuziachia kisha akaruhusu risasi mbili maridhawa ambazo zilitenda kazi aliyozituma. Watu wawili wa upande mmoja walikuwa wakipiga mayowe huku wakikosa muhimili kwenye Chopa ile. Wakaachia na kupigizwa kwenye matawi ya miti hadi chini kwenye mawe. Walikuwa ni marehemu tayari kwani walionekana wakivuja damu vichwani. Frank Matiale Bambi hakusubiri eneo hilo tena alijua ni lazima Chopa ile irudi kwani ilikuwa ikimshambulia yeye pia baada ya rubani au waliyomo kwenye Chopa hiyo kumuhisi vibaya. Alikimbia kwa umbali wa kama mita ishirini kutoka pale wakati Chopa ile ikiwa imeelekea upande wa mashariki mwa msitu ule.




"Kuna....kuna adui mwengine.....ameuwa watu wawili tayari na yupo katikati ya msitu.....narudia tena...yupo katikati ya msitu..!" Aliongea Rubani aliyekuwa akiiongoza Chopa ile na alikuwa akiwasiliana na Amsuni Bhehe kwani ndiye aliyekuwa akiongoza kikosi kile kijeshi kwa kuwa alizijua vema medani za kijeshi.




"Wengine wachukue nafasi......wengine wachukue nafasi hakutakiwi kuokoka mtu wauweni, nawasiliana na mdunguaji ahakikishe anamshughulikia na huyo mpuuzi...!" Sauti kutoka upande mwingine ilisikika hii ilimaanisha kuwa kulikuwa na mtu mwingine mbali na pale alikuwa akifuatilia mawasiliano yao. Rubani akafanya hivyo.


Warudi..? Eeh! Kazi ipo.




Chopa ililazwa upande wa kulia tena ililazwa ikiwa kwenye kasi kubwa, upande ule waliposhambuliwa wale watu wawili wakatokeza wengine wakiwa na silaha tayari kupeleka mashambulizi makubwa. Frank alikuwa akiitazama ile Chopa kwa kutumia darubini iliyopo kwenye bunduki yake ya kudungulia kwani tayari alishaiweka mikononi baada ya kuamini kuwa ni lazima imrudie.


Ilikuwa ikirudia upande ule aliyotoka.


Alikuwa nyuma ya mti mkubwa akiwa amepiga goti moja chini akiwa bado anaitazama ile Chopa ikizunguka huku watu waliyokuwa wamening'inia huku na huku wakimwaga risasi kupita maelezo eneo ambalo alikuwapo mwanzo. Akamuweka mmoja kwenye shabaha yake hata hivyo hakuwa akimpata sawasawa kutokana na Chopa kutokutulia....fucking buu...! Akatukana Frank.








Alikuwa nyuma ya mti mkubwa akiwa amepiga goti moja chini akiwa bado anaitazama ile Chopa ikizunguka huku watu waliyokuwa wamening'inia huku na huku wakimwaga risasi kupita maelezo eneo ambalo alikuwapo mwanzo. Akamuweka mmoja kwenye shabaha yake hata hivyo hakuwa akimpata sawasawa kutokana na Chopa kutokutulia....fucking buu...! Akatukana Frank.




Akalala kwa kujitupa chini sasa akiwa na lengo la kuishambulia ile Chopa. Kitendo cha kujilaza chini kwa ghafula ile ndiyo ilikuwa salama yake. Risasi ilimkosa kichwani na kuumeguwa mti kwa nguvu.




"Fucking blood fools..!" Alitukana akabingilia kama gogo na kujibana kwenye mti mwingine sasa akijua kuwa yule mdunguaji aliyemkosa yule mwanamke nyumbani kwa waziri wa nishati na madini aliyemaliza muda wake alikuwa hapo na alikuwa akimtamani. Ile chopa ilikuwa ikija alipo huku wale watu wakimwaga risasi kwa sifa lakini pia mdunguaji alikuwa akimsubiri ajitikise amalizane naye. Alikuwa kwenye wakati mgumu sana Frank. Alijibana madhubuti chini ya mti kisha akanyanyua bunduki yake kule ambako Chopa ilikuwa ikija. Uzuri ni kwamba watu wale walikuwa wakimimina risasi kwa silaha za AK 47 kwa kuelekea chini na si mbele. Akafikiri endapo atasubiri ifike alipo, ilikuwa ni vigumu kuzikwepa risasi zinazotokea juu kama mvua.


Angekufa.




Frank Matiale Bambi hakutaka kufa kikondoo, hakutaka kufa kwa risasi za vipofu waliyoko chopani wala hakutaka kudunguliwa na mdunguaji aliyemkosa punde. Alikuwa na kazi nyingi za kufanya na hajafika popote. Aliiweka kwenye shabaha yake ile Chopa kisha akaachia risasi mbili zenye akili na alipiga mahali ambapo alikuwa na uhakika kabisa kuwa ile Chopa isingehimili. Aliishuhudia ikifuka moshi huku watu wakihamanika. Bado hakuwa mjinga wa kujua kuwa mdunguaji alikuwa hapo. Akatazama juu akaiona ile Chopa ikielekea alipo huku ikiwa imeshika moto. Akajitupa mbele usawa wa ule mti akahisi kitu kama kisu kikimchana mgongoni, hakuzubaa akajiingiza kwe shimo dogo na kutambaa kwa tumbo akajiweka nyuma ya jabali kubwa. Risasi nyingine ikamkosa lakini kilichomjuza kuwa ni risasi ni mpasuko wa lile jabali, haraka sana akauficha uso wake chini ili kuzuia madhara yatakayojitokeza kisha akaelekeza mtutu wa bunduki yake upande ilikotokea ile risasi.


Alichelewa....!




Mlipuko mkubwa ukasikika baada ya ile Chopa kujipigiza chini nyuma ya ule mti ambao alikuwa amejificha. Hakusubiri kukaa hapo tena lakini pia hakutaka kumkimbia mdunguaji isipokuwa kumkabili zaidi. Akawa anakimbia kwa kuizunguuka ile Chopa kwa umbali ambo joto la ule moto lilikuwa halimfikii. Akajitupa mahali na kuweka jicho lake haraka kwenye darubini ya bunduki yake.




Shiit....! Huwezi kunikimbia mpuuzi wewe. Aliwaza akiwa haoni kitu chochote cha hatari mbele ya jicho lake. Akazidi kuizungusha bunduki yake kwa utaratibu. Akatikisika baada ya kumuona kiumbe mtu akiwa ameinamia kutokea kiunoni, akaachia risasi yake.




'AAAAGH...!' Sauti ya maumivu ikasikika akataka kupeleka nyingine hata hivyo kiumbe kile kilichokuwa kumekamatia bunduki ndefu kilishajiweka nyuma ya mti. Alimjeruhi begani. Akatabasamu Frank kwa kutokuitupa bure risasi yake japo halikuwa dhumuni lake. Dhumuni lake hasa lilikuwa ni kuuwa.




Bado aliendelea kutazama nyuma ya ule mti kwa umakini wa hali ya juu sana akiwa palepale.




Lazima afe na kifo chake ndicho kitakachomaliza usumbufu huu mkubwa. Aliwaza Frank hata hivyo alimuona mtu yule akiwa anatambaa kama nyoka aina ya Moma...taratiibu kwa shida kubwa akiufuata mti huu na ule.




'SHAMBULIAAAA......!' Sauti hii kali ya amri ikamtoa kwenye lengo Frank maana ilikuwa ikitoke nyuma yake na iilikuwa ni umbali wa kama Mita ishirini na tano. Msitu ukiwa umetanda hadi giza.




Nani...? Nani anayetakiwa kushambuliwa..? Hapana, ata..., atakuwa ni yule mwanamke..? Akawaza akijiuliza maswali hayo. Akarudisha jicho kwenye darubini yake. Yule kiumbe hakuonekana tena. Hakukuwa na shaka na hakuona kama yule mdunguaji ataleta tena madhara. Frank Matiale akanyanyuka kwa kasi na kukimbia akiwa amejikunja kuanzia kiunoni. Haukuwa uwongo kwani Amsuni Bhehe ile risasi ilikuwa imempa madhara makubwa begani na kumpa maumivu makali yaliyompelekea kupoteza imani ya kupambana tena sasa alikuwa akiikimbia medani ya kivita na kuwa mbali kabisa na mdunguaji ambaye alikuwa ni hatari na mwenye shabaha kali zaidi. Alifanikiwa kwenda mbali zaidi hadi alipozikuta gari akajipakiza na kusikilizia maumivu huku akijifunga jeraha lake madhuti lisitoe damu lakini akipokea na kutoa mawasiliano kwa Black Scorpion kwani yeye ndiye pekee mwenye kisafirisha na kinasa sauti aliyebakia na wote waliuawa.




Frank Matiale yeye alikimbia kwa kasi kubwa na kwa muda mfupi akajiweka nyuma ya jabali na kutumia bunduki yake kuliangalia eneo lile la msitu kwa umakini mkubwa hadi alipowaona maadui ambao hawakuwa wengi sana. Akatabasamu.




"Mmekwisha...!" Akasema kisha akaanza kuwahesabia mmoja baada ya mwingine kwa risasi. Zilipokwisha aliangusha magazini chini na kuchomoa nyingine kwenye begi lake refu la mgongoni akachomeka na kuanza kuwashambulia kimya kimya tena.


Hili ndilo lilikuwa likiwachanganya akina Mabule na wasijue jinsi hali ilivyo. Maadui wale walichanganyikiwa na kuhamanika huku wakigeuza mashambulizi yasiyo na macho. Dakika moja pekee ilitosha kuliacha eneo lile likiwa kimya tena kimya kikuu.


Walimalizwa wote..!




Frank baada ya kuona amemaliza kazi ile kwa muda mfupi akili yake ikahamia kwa yule mwanamke hapo akaanza kumtafuta. Hakuwa mbali na hapo hata hivyo alikuwa kwenye mapambano makali na mtu aliyekuwa amevaa maski usoni. Hili likamchanganya. Kwanini mtu yule avae maski..? Kuna kitu gani kilichojificha pale...? Huwenda labda kuna uhusiano wowote baina ya huyo aliyevaa maski na huyo mwanamke ama...?


Yalikuwa ni maswali ambayo hayakuwa na majibu mazuri hata kidogo na lilimuweka kwenye wakati mgumu mno. Yule mtu aliyevaa maski alikuwa na nguvu sana hata hivyo yule mwanamke pamoja na kuchoka sana hakuthubutu kuonesha udhaifu. Yule mtu mwenye Maski alikuwa akichomoa ngumi na kumsogelea yule mwanamke kwa umakini mkubwa. Hii ilikuwa ni hatari lakini alishindwa kushambulia Frank kutokana na jinsi walivyokuwa wamesimama aliogopa huwenda angemjeruhi yule mwanamke na halikuwa lengo.


kasubiri.


Kusubiri kule kukamuonesha hatari ya wazi. Akatafuta upenyo na kupeleka risasi ambayo kwa uchache ilimkosa yule mtu mwenye maski na kumpapuza begani akamuona akihangaika na kuwasiliana na mtu hata hivyo akatoa macho asielewe nini kimetoke. Akaogopa na kuhisi hatari zaidi. Akatumia mbinu ya mwisho ya kijeshi.


Akatimua mbio huku akitoa ishara zisizoeleweka.




Frank Matiale Bambi akawa makini kutazama lile eneo ndipo akaona watu wengine wawili mwanamke na mwanaume wakikimbia kuungana na yule aliyemkosa kwa risasi yake huku kwa wakati huo yule mwenye mask akiitoa maski yake kichwani na kuitupa. Akajua nini ilikuwa maana ya ile ishara.




"Wapuuzi nyinyi...! Siwaachi muende...!" Akasema huku akimuweka yule mwanamke kwenye shabaha yake hata hivyo hakukuwa na risasi iliyotoka. Akatukana na kupiga ngumi chini ya ardhi eneo alilopo.


Risasi hazikuwepo kwenye bunduki yake.




Akakasirika kwa kiwango cha juu sana kuwaacha watu wale aliodhani ni maadui waende. Hakuwa na namna akalipuuzia hilo na kuirudisha akili yake kwa yule mwanamke ambaye hasa ndiye aliyekuwa akimsaidi.




Hakuwepo.




Amekwenda wapi...? Haonekani...? Ebo! Akawaza. Mwisho wa yote ilibidi atabasamu maana alikubaliana na moyo wake kuwa alikuwa na mtu hatari nchini kwake.


Akaondoka taratibu huku akiwa ameukamata mtutu wake wa bunguki sawasawa.




_________




Amsuni Bhehe alifika mbele ya Malfrey Kobra kinyonge sana na kusimama kimya bila kuongea chochote huku bega lake likiwa limetapakaa damu iliyoanza kugandamana na nguo yake. Alikuwa akikodoa macho kama kwamba anasoma mandiishi madogo mwilini mwa bwana huyo. Malfrey Kobra akanyanyua macho kumuangalia Amsuni ambaye bila kuuliza alidhihirisha hakuwa sawa kiafya na kiakili. Mwili wake ulitapakaa damu iliyokuwa ikivuja kutokea kwenye jeraha baya lililopo kwenye bega lake ambalo lilisababishwa na risasi ya mdunguaji kisha akamuuliza kulikoni kama kwamba lile jeraha hakuliona.




"Tumepoteza kila kitu bosi....hakuna tulichovuna...! Ni hasara, hasara kupindukia." Aliongea Amsuni Bhehe akiwa anapambana na maumivu makali yaliyokuwa yakimtafuna haswa. Macho ya Malfrey Kobra yaliwaka kama kurunzi ya kichina kisha akayafinya kwa uchungu na kuyafanya kuwa madogo. Alikuwa akiumia sana juu ya maneno hayo ya kukatisha tamaa.




Wamepoteza...? Inamaana hakuna...? Hakuna walichoambua zaidi ya hasara waliyonipa haa! Sikubali....! Sikubali.




MZIMU ANAWEZA KUAMKA KWENYE MACHELA KWELI?








"Tumepoteza kila kitu bosi....hakuna tulichovuna...! Ni hasara, hasara kupindukia." Aliongea Amsuni Bhehe akiwa anapambana na maumivu makali yaliyokuwa yakimtafuna haswa. Macho ya Malfrey Kobra yaliwaka kama kurunzi ya kichina kisha akayafinya kwa uchungu na kuyafanya kuwa madogo. Alikuwa akiumia sana juu ya maneno hayo ya kukatisha tamaa.


Wamepoteza...? Inamaana hakuna...? Hakuna walichoambua zaidi ya hasara waliyonipa haa! Sikubali....! Sikubali. Aliwaza Malfrey akiwa anayazungusha macho yake huku na huko kama yanayomuwasha, akayanyanyua tena na kumtazama Amsuni, akamuona jinsi alivyokuwa amesimama kiume japo alikuwa akipitia maumivu makali sana. Kabla hajazungumza chochote, mlango ukafunguliwa kwa kishindo kidogo baada ya kubishwa hodi kwa utaratibu maalumu. Akaingia Black Scorpion akiwa anatweta.


"Black Scorpion...!" Alihamaki Malfrey Kobra.


"Bosi...!" Aliitika Black Scorpion huku akiwa makini zaidi.


"Kwanini siwaelewi na kwanini uko hapa hujui kama ni hatari wewe kuwa hapa muda huu?"


"Najua hata hivyo hakuna sababu ya kutokuwa hapa kwa kuwa hali ni mbaya. Hayupo mmoja kama tulivyokuwa tukidhani na inavyoonekana walijipanga kuweza kupambana nasi. Yule binti alikuwa kama chambo kwetu. Amsuni Bhehe alipogundulika na mdunguaji wa upande wa mahasimu wetu kisha kujeruhiwa, kila kitu kiliharibikia hapo. Tulizidiwa, japo nilikuwa nikipambana na adui ana kwa ana hata hivyo hakukuwa na majibu kwa kuwa mdunguaji alikuwa makini zaidi. Helkopta yetu ikaharibiwa vibaya yaani ilikuwa shaghalabaghali mbaya zaidi vijana wetu wote hakuna aliyetoka hata mmoja akiwa hai." Hii ilikuwa ni taarifa mbaya sana kwa Malfrey Kobra. Mwili wake ulimuwia mwepesi akiihisi akili yake kutaka kumkimbia, macho yakianza kuona ukungu mara giza mbele. Alijitahidi ili hali mbaya isimkute mahali hapo ili aweze kusikia kila kitu kilichokuwa kikielezwa hapo ambacho kilitokea kwenye mapambano hayo. Aliogopa sana, alijiona anakwenda kufa kama kaka yake. Tena anakufa akiwa ameshindwa kukamilisha kile alichomuahidi kaka yake kuwa ni lazima atakitimiza.




Ha...hapana? Si sasa mbona...mnani....! Akili yake ilikuwa ikitaka kuzungumza jambo akidhani litafika mbali hata hivyo lilikuwa likiishia ndani ya kifua chake na kurudi tena lilikotolewa. Shingo ikawa nzito na kuanza kushindwa kukibeba kichwa, kwa namna alivyokuwa akipambana na ile hali iliyomzidi nguvu, hakuwa akijua kama alikuwa akitikisika pale kwenye machela mithili ya mashine ya kukobolea mahindi ya kuendeshwa kwa dizeli. Akajiona akiingia kwenye wakati mgumu wa kupambana na giza nene huku neno moja lenye kumpa matumaini likizunguka akilini mwake.


Mpango wa nje......! Alipoteza fahamu.


"Bosi...bosi uko salama...?" Alipayuka Tally Man akiwa ametoka nyuma ya ile machela ambayo ilikunjwa kama kiti kisha kueleke ubavuni mwa Malfrey.


Kwanini hivi ghafla namna hii...? Kwanini..? Hali ilizidi kumchanga Tally Man na hakukuwa na namna nyingine isipokuwa kumuwahisha nyumbani kwake Samiado ambako angekwenda kupatiwa matibabu na daktari wake, dokta Lumoso Papi Mmbai aliyekuwa akiishi kama mtumwa huru.


"Amsuni fanya hima uweze kujitibu hilo jeraha haraka sana na kuanzia sasa uhakikishe huyo mwanamke anajulikana alipo, hii itakuwa kwako na kwa Black Scorpion kwani hadi sasa imeshakuwa hali mbaya kwa kiongozi." Alitoa agizo Tally Man kisha akabonyeza kitufe fulani chini ya kichwa cha Malfrey na ile machela ikashuka ikawa kama kitanda. Akamsukuma kwa uangalifu kumrudisha ndegeni na safari ya kurudi kwake kwa ajili ya kupata matibabu ikaanza.




Ni mwanajeshi...ni mwanajeshi yeye hawezi kushindwa...! Akili bado ilikuwa ikimzunguka Tally Man kama kitu gani sijui, huo ulikuwa ni ule muda ambao hakutaka utokee kabisa ila sasa alijiona yuko ndani ya kitu asichokiomba na asichokipenda.


Huku nyuma Black Scorpion alimuona Amsuni alivyokuwa akipata shida na alivyokuwa akivuja damu kilichokuwa kikifanyika ni uhatari uliokuwa ukipuuziwa, hakuwa na namna zaidi ya kuchukua maamuzi ya kulitazama jeraha na kuikata nyama ya bega iliyokuwa ikining'ini begani kutokana na madhara ya ile risasi ya mdunguaji iliyopigwa kutokea mbali iliyoichana na kuikata nyama ya bega vibaya sana. Pona pona yake ni kwamba risasi ile haikutana na mfupa wa bega. Baada ya kwisha kuikata vizuri ile nyama inayoning'inia begani bila huruma, alifanya namna ya kulidhibiti lile jeraha lisiendelee kuvuja damu kabla ya kutumia huduma nyingine za dharula.


"Najua kuwa hatutakiwi kukurupuka lakini pia tunatakiwa tupange kitu cha mwisho cha kumaliza kazi kabisa ambacho kitakumbukwa na taifa hili dogo milele.




_________




"ILIKUWA NI VITA FUPI ILIYOTAKA KUONDOKA NA MAISHA YANGU. Sikuwa na namna zaidi ya kupambana hadi tone la mwisho la pumzi yangu nashukuru nilishinda na japo ushindi wangu una wingi wa maswali ila ninachojua ni kwamba nimeshinda." Ilinibidi kumuelezea kila kitu Abdallah Mapande kile kilichonitokea msituni. Mzee huyo alinitazama kwa muda kwa jinsi nilivyokuwa sitamaniki kwa majeraha madogo madogo ya kukatwa na mawe sambamba na kukwaruzwa na miti yenye miiba. Aliingia ndani kwake na alipokuja kutoka mkononi alikamata kiboksi kidogo ambacho alikiweka chini karibu nami. Akachukua dawa ambayo ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kusafishia majeraha, alisafisha majera yote yaliyokuwa yakionekana kisha akanitazama usoni.


"Yalikuwa ni mapambano makubwa....!" Alizungumza kwa kauli yenye kuendelea, sikumjibu nilimtazama wakati akiwa ananipaka dawa yenye maumivu makali sana.


"....dawa hii ni maalumu kwa majeraha ya dharula ambayo humaliza kabisa maumivu na kukausha jeraha kwa muda mfupi." Alisema. Sikumjibu nilimtazama tu. Alizungusha mkono wake kutokea juu ya bega langu la kushoto kisha akawa kama anayenipapasa taratibu kushuka nyuma ya mgongo wangu. Nilimkazia macho ya wasiwasi maana alikuwa akifanya vile huku akinitazama kifua changu na usoni mara chache. Nilikuja kuhisi maumivu makali sana aliponishika pembeni kidogo ya uti wa mgongo. Nilimuona akishusha pumzi nyingi huku akiutoa mkono wake.


"Ume...umejuaje kama nimeumia mgongoni..?" Nilimuuliza kwa mchanganyiko wa aibu na maumivu kwani akili yangu ilishaanza kumdhania vibaya.


"Macho yako bado yalikuwa na zaidi ya maumivu na hili jeraha la mgongoni ni kubwa zaidi kuliko yote." Alinijibu kisha kasimama na kunizunguka.


"Vua hii nguo ili nilione jeraha!" Aliniambia.


Ni..nivue...ha..haap...! Niliwaza nikipingana na kauli yake moyoni mwangu.


"Tena bado linavuja damu, ni hatari hii!" Alisisitiza. Sikuwa na namna, nilifungua vishikizo kadhaa vya shati langu gumu la rangi ya khaki na kulishusha kwa kiasi fulani. Pamoja na ugumu wa shati hili lakini liliweza kudhurika kwa kashikashi nyingi za ule msitu uliotaka kuondoka na roho yangu. Nilizisikia pumzi za Abdallah Mapande zikitoka kwa pupa, nikaogopa sana hata hivyo hakudumu katika kupoteza muda alianza kunitibu lile jeraha ambalo ndilo lililonipa maumivu makali zaidi. Punde akawa amemaliza.


"Inabidi upumzike hapa kwa muda kidogo kabla hujaianza safari yako ya mwisho kama ulivyosema." Aliniambia huku akinyanyuka na kile kiboksi kidogo kilichosheheni dawa.


"Sitakiwi kupumzika mzee wangu kazi bado kubwa na sijafika popote."


"Tulichokifanya ni kutibu majeraha, umefanya busara sana kurudi hapa maana hali ni mbaya mbaya sana huko mitaani..!"


"Sijakuelewa maana yako AKM..?" Nilimuuliza nikiwa nimeweka umakini mkubwa zaidi. Aligeuka na kunitazama mara naada ya kuwa amenipa mgongo.


"Taifa hili ni kama lina laana...!" Akaiacha tena kauli yake ikining'inia hewani hata hivyo hakukawia kuiwahi. "....raia wanakufa hovyo...wanakufa na wanakufa kwa magonjwa ambayo mengine tiba yake ni ndogo kabisa...!"


"Sasa kwanini wanakufa..?" Nilimuwahi. Akanitazama kabla ya kumeza funda kubwa la mate na kunitazama akisema kwa masikitiko ya kukata tamaa.


"Ndani ya taifa hili hakuna hata bohari moja yenye dawa, bohari zote tegemezi zimevamiwa na kuchomwa hivyo kusababisha hasara kubwa kwa taifa..!"


"Hapana, inawezekanaje hii?" Nilimuuliza zaidi.


"Limekuwa ni jambo lililoanza kama masikhara tu taarifa zikitangaza kuwa taifa linaweza kukabiliwa na uhaba wa dawa kwa masiku kadhaa yajayo mbele, halikuwa ni jambo lililowahi kutokea hapa nchini hivyo hata namna lilivyokuwa likizungumzwa lilizingumzwa kama ngano tu lakini vyombo vya habari vyote hapa nchini vimeonesha habari hiyo hivyo si jambo la kuulizana tena. Lakini sasa hali ni mbaya hakuna....hakuna kitu." Alieleza Abdallah Khalid Mapande.


Hakuna dawa...? Kwanini na inawezekanaje hii...? Ni mkanganyiko na ni jambo lisiloweza kuelezeka.


"Kwasasa hapa mjini usipohudhuria mazishi ya jirani yako wala mtu hakushutumu vibaya maana anaamini kama hukufiwa na mkeo siku ya mazishi ya jirani huyo, huwenda ni mama yako mzazi au ni kiziwanda chako cha pekee. Watu wanazika kuliko kipindi chochote kile kilichowahi kupita nadhani unajua kuwa kuna watu wengine kila dakika ya maisha yao wanategemea dawa. Sasa jenga picha baada ya gundua dawa hakuna." Aliongea AKM akiwa anaelekea ndani kwake akiniacha mimi nikiwa na mawazo mengi pale nilipokuwa nimesimama. Hakuchelewa kutoka lakini akiwa bado hajanikaribia, simu yake ikaita. Akaitoa mfukoni na kuitazama huku akiitoa sigara yake kinywani ambayo aliipachika punde baada ya kuiwasha akitokea ndani. Alijipa utulivu kidogo na kuipoke. Hakuongea chochote na haikuwa ni kwa muda mrefu akaishusha huku akiirudisha sigara yake kinywani na kuendelea kuivuta akiwa mtulivu kuliko kawaida.




"Nataka kujua ulipoishia Catherine hata hivyo pia nataka kujua wapi ama ni hatua gani uliyobakiza, inakubidi unisubiri hadi nitakaporejea....!"


"Unakwenda wapi?" Nilimuuliza nikiwa na wahaka mkubwa. Sura yake haikuwa na amani ilijaa wasiwasi mwingi baada ya ile simu.


"Mkuu wa nchi amenitaka wito." Alisema.


"Unahisi labda kuna tatizo?" Nilimuuliza.


"Kama siyo hili huwenda kuna jipya na limemchanganya zaidi kama nilivyokuambia muheshimiwa Rais akipata jambo lolote liwe baya ama zuri ni lazima atanishirikisha mimi. Ameongea kwa masikitiko sana sasa wacha nikamsikilize huwenda kuna jipya na likakufumbua hata wewe kujua cha kufanya katika safari yako." Alisema kisha akaelekea kwenye maegesho ya magari ambako alichagua gari moja na kuondoka kwa kasi kubwa.




Muda wote nilikuwa na mawazo mengi sana ambayo yalikizonga kichwa changu kwa kiasi kikubwa. Nilikuwa nimejilaza angalau kuipa akili yangu utulivu na kutafakari mengi ambayo bado sikuwa nimeyakaribia. Niliwaza yaliyopita lakini pia niliwaza yanayonikabili na kuwazuwa yajayo. Nilimezwa na wakati mgumu sana. Nikiwa bado nimejilaza juu ya kitanda angalau niweze kuuvuta usingizi wa kama dakika thelathini, nikajikuta nalikumbuka tukio ambalo sikuwa nimelielewa kwanini limenitokea. Nilijiingiza nijue nini kilichopo cha ajabu ni kwamba nikajikuta nimebeba matatizo makubwa yaliyopo ambayo sikuwa nimeyategemea. Kuna kitu nilikuwa nikikiwaza kwa mapana zaidi nacho ni kuhusiana na yule kijana ambaye aliamua kubeba jukumu la kunisaidi kwenye matatizo yale.


Ni nani...? Yule ni mwanausalama huwenda naye yuko kwenye huu mchezo akifanya yake. Anafanya nini...Sina yakini kama tuko kwenye sakata moja. Mimi ninatafuta kilichonileta iweje yeye..? Niliwaza sana na hapa nikahisi huwenda taarifa zangu zimemfikia na kama zimemfikia zitakuwa zimemfikia kwa namna gani? Iliniumiza kichwa tana sana maana bado kulikuwa na mengi yaliyokuwa yakinipanda kichwani, nikimaliza hili linakuja hili, likiondoka lile linaanza hili. Ilikuwa tafarani dhafarani. Kila kitu nilikikumbuka hata yule niliyepambana naye akiwa amevaa maski usoni.








Mimi ninatafuta kilichonileta iweje yeye..? Niliwaza sana na hapa nikahisi huwenda taarifa zangu zimemfikia na kama zimemfikia zitakuwa zimemfikia kwa namna gani? Iliniumiza kichwa tana sana maana bado kulikuwa na mengi yaliyokuwa yakinipanda kichwani, nikimaliza hili linakuja hili, likiondoka lile linaanza hili. Ilikuwa tafarani dhafarani. Kila kitu nilikikumbuka hata yule niliyepambana naye akiwa amevaa maski usoni.




SONGA NAYO SASA...




"Lazima nimjue ila sijui nitamkaribia vipi anaonekana ni kijana makini sana!" Nilijisemea mwenyewe katika namna ya kujipa ushauri baada ya kutoka kumuwaza yule kijana mwenye rasta zaidi. Nikaachana na huyo kijana anayependa kuwa kwenye njia nipitazo kisha nikamkumbuka Jamali. Yaa, hapa nilimkumbuka Jamali Maigwa yule kijana ambaye nilikutana naye kwenye gari wakati natokea mjini nikija hapa nilipo. Sijui kwanini alinijia kwenye kumbukumbu zangu kwa haraka namna hii hata hivyo nilijikuta nikiwa na ari kubwa ya kutaka kuonana naye. Niliikumbuka simu yangu ambayo muda wote ilikuwa hewani na sikuwa nawaza kuizima kwani nilitegemea kupokea simu muhimu wakati wowote. Simu hii ndiyo niliyokuwa nikiitumia kuwasiliana na AKM na watu wengine kama akina Jamali Maigwa ambao ni mbali na kiongozi wangu wa kazi ambaye nilikuwa nikiwasiliana naye kwa mawasiliano ya siri zaidi. Sikutaka kuizima kabisa. Nilipoitazama nikagundua kuwa ilikuwa na chaji hafifu na wakati wowote ingeweza kuzima. Ni sahihi kuwa hivyo maana sikumbuki ni lini niliichaji. Ilinibidi ninyanyuke kitandani na kuiweka chaji kisha nikajiweka kwenye kiti sebuleni hapohapo, akili yangu iligoma kurudi tena ndani kulala maana sikuwa nikilala zaidi ya kuwaza na kuwazua. Nikiwa hapo simu ile iliita. Nikaitazama, namba sikuwa nimewahi kuihifadhi. Nikaiwahi na kuipokea kisha nikategea kuzungumza. Nikasikia sauti ya kiume.


"Hallo....!" Nilijibu kisha nikasikiliza tena.


"Ohoo! Jamali jamani kwanini sasa umeamua kukaa kimya kwa muda mrefu hivyo nikajua labda umeipoteza kabisa namba yangu...!" Nilizungumza baada ya kujitambulisha kwake. Nikasikiliza tena.


"Mimi bado niko hapa Muavengero sijaondoka japo sina muda mrefu nitaweza kuondoka.....!" Nilimwambia nikaendelea kusikiliza. Nilizisikia pumzi zake zikitoka kwa fujo nikajua ni matumaini aliyoyapata baada ya kumwambia bado nipo Muavengero.


"Hapana, kwa kuwa nimeipata namba yako sasa nitakutafuta muda wowote kwa ajili ya mazungumzo zaidi, unajua nilikukumbuka sana huwezi amini ila nikakosa namana ya kuwasiliana na wewe. Napenda uchangamfu wako na vile ulivyomkarimu...niahidi muda nzuri wa kukupigia maana huwa sipendi kukupigia ukiwa na mkeo...?" Nilimwambia kwa kumtega mwishoni. Hapa wanaume wengi hufeli na kuwakana wapenzi wao kwa ajili ya ingizo jipya sokoni.


Wataridhikaje wakati wamejaa uroho wa kutaka kumtafuna kila mrembo apitaye mbele yao.


Nikaisikia pumzi zikimshuka nikajua fika nimempeleka mahali fulani apatakapo.


"Asante kama naweza kukupigia muda wowote." Nilimjibu kisha yakafuatia mazungumzo ya hapa na pale kisha nikakata simu. Nikifarijika kwa kiasi fulani kwa kuipata namba ya huyo kijana sikujua sababu ya kufarijika kwangu hata hivyo nilikuwa nikiihitaji sana. Kijana huyu kwenye akili yangu nilimuona akiwa amejaa kwa kiasi kikubwa sana na sikujua kwanini. Sikutaka niendelee na kumuwazia yeye tena. Nikaachana na mawazo hayo nikatoka hapo sebuleni na kuelekea jikoni kwa ajili ya kujiandalia chochote kitu.




Nilikuja kumaliza kuandaa chakula baada ya saa moja mbele. Nikiwa natenga chakula mezani, nikasikia muungurumo wa gari ikija huko nje kisha baada ya kitambo kifupi ikisimama nje mahali ambapo Abdallah Khalid Mapande huwa anaegesha gari zake. Nikasogea lilipodirisha na kuchungulia. Alikuwa ni yeye. Aliingia na kunikuta nikiwa nimemaliza kuandaa chakuna pale mezani nikamkaribisha kabla ya kuulizana habari. Kwanza kabla ya kufanya chochote alifuata rimoti mahali ilipo kisha akawasha runinga kubwa ya bapa ipatayo inchi 52 iliyopo ukutani kisha akakaribia mezani tukaanza kula huku kimya kikiwa kimetawala kwa muda macho yetu yakishuhudia habari ya kifo cha aliyekuwa waziri wa nishati na madini. Ilikuwa ni habari niliyokuwa nikiitarajia wakati wowote ule kwani akili yangu kila wakati ilikuwa ikifanya kazi ya kujiuliza sababu kuu hasa ya tukio lile lililotoke kwenye nyumba ya muheshimiwa huyo ilikuwa ni nini.


"Nilijua...nilijua haikuwa bure..!" Nilisema. AKM akanitazama kwa mashaka usoni. Akaniuliza nilichokuwa nikikijua ama kukitarajia ni nini hasa.


"....hiki ndicho kilichonifanya niandamwe kutokea hapo kwenye hiyo nyumba ya muheshimiwa hadi msituni...!" Nilichukua jukumu la kumueleza kwa ufasaha sasa namna ilivyokuwa kuanzia tangu wakati nafika eneo lile na nia hasa iliyonifikisha eneo lile ilikuwa nini, nikamueleza namna nilivyokuwa nikiandamwa kama gaidi hadi nilipofika kwenye ile vita ya msituni.


"Hao ndio waliomuua waziri na sijui kitu kwenye kifo hicho...kwanini sasa waliamua kumuua?" Niliuliza baada ya kueleza kwa kina zaidi.


"Napata picha...!"


"Picha..?"


".....ndiyo, huu mpango haukusukwa leo...huu mpango unaumri mrefu hadi sasa. Nafurahi sana kuwa na mtu makini kama wewe Catherine...!"


"Kwa namna gani unaafiki hivyo?"


"....hii ni vita ya kisasi...!"


"Kisasi? Kwa namna gani?" Niliuliza kwa mshangao mkubwa sana. Luteni mstaafu alinitazama kwa macho yake makali ya kuogofya nikatulizana nilijua alimaanisha nini.


"....katika madaraka yake marehemu Abdallah Juma Kimbo, alikuwa makini sana na hakupenda masikhara kazini. Hii ilikuwa ni timu ya kazi ya Rais Mabandu ambayo ilikuwa ikitenda kazi hasa. Waziri huyu aliwahi kuzifungia kampuni mama za bwana mmoja aliyekuwa akiitwa Maleley Kobra. Kampuni hizi hazikufungwa kwa visa wala uonevu la hasha! Zilifungwa kwa kuwa zilikuwa zikikiuka taratibu na kanuni za nchi. Nadhani unajua madhara yapatikanayo kwenye makapuni ya uchimbaji na uchenjuaji madini. Kama hakuna mazingatio ya usafi na ujalifu wa afya za watu eneo hilo huwa ni hatari sana zaidi ya bomu la nyukilia. Kwenye kampuni hizo afya ya wafanya kazi haikujaliwa hata kidogo na hazikuwa zikizingatia suala la usafi hata kidogo, waziri Kimbo akazifunga hizi kampuni mara baada ya kutoa onyo la kwanza na la pili kali zaidi, baada ya kuona hakuna matekelezo zaidi ya upuuzwaji na dharau za kukithiri kwa matajiri hao waliodhani taifa wameliweka mikononi, akatoa amri kali ya kuzifunga kampuni hizo akishirikiana na waziri wa afya ambaye ni marehemu.


Kizaa zaa kilianzia hapo.




Kesi ziliunguruma mahakamani katika harakati za kudai haki zao lakini wapi. Baada ya miaka mitatu kesi ile ikazorota na hakukusikika kitu chochote kabisa. Ila miaka minne baadae ndipo kulipoanza kuibuka mauaji...mauaji hayo yalianzia kwa viongozi wa polisi na kusambaa zaidi hadi kumkuta waziri wa afya ambaye alichabangwa risasi za kutosha. Hiki kifo cha muheshimiwa waziri Kimbo ndicho kilichonifumbua sasa." Alinieleza AKM, nilielewa kwa kina na kupata kitu kwenye maelezo haya na kulikuwa kuna jambo ningependa kulijua kabla ya kuweza kuunganisha matukio ya mambo hayo. Nilimtazama Abdallah Khalid Mapande jinsi alivyokuwa akijishughulisha na kula. Nilijifuta midomo kwa mikono yangu na kutulia.


"Kama hii vita itakuwa ni ya kisasi je, inawezekana anayeendeleza kisasi akawa ni huyo Maleley Kobra?" Nilimtazama usoni kwa umakini mkubwa nikimuuliza swali hilo. Alinitazama naye kabla hajaamua kunijibu.


"Huyu mtu ilisemekana alifariki kwa ugonjwa, haikujulikana ni ugonjwa gani?"


Alikufa kwa ugonjwa na inaaminika kuwa ndiye aliyefanya mauji ambayo Luteni mstaafu anahisi huwenda yakawa ni mauaji ya visasi. Maiti anaendelea kuuwa au nini maana yake...? Inawezekana vipi hii...? Niliwaza lakini sikuishia kuwaza tu


"Kama ni kisasi kilikuwa kikifanywa na huyo Maleley Kobra sivyo..? Kifo kilikuja nyuma ya matukio hayo?" Nilimuuliza ingawa kwa hakika kabisa maiti hawezi kuuwa labda kama waliosabisha hayo ni washirika wenzake.


"Baada ya vifo vya waliokuwa viongozi wawili wa kipolisi na watu wengine kadhaa kwa wakati mwingine, tetesi ya kifo cha huyo bwana haikuwepo. Ukapita ukimya mkubwa. Miaka mingi ikakatika, baada ya ukimya huo, hapo ndipo ulipoibuka uvumi kuwa huyu bwana alipoteza maisha inamaana alipoteza maisha ndani ya huu ukimya." Alijibu AKM akiwa katika utulivu mkubwa. Nilimtazama tena. Kuna kitu nilikuwa nikikiona na ndicho hasa kilichokuwa kikinipa matumaini.


"Baada ya tetesi za kifo cha huyo Maleley Kobra hakukuibuka tena jambo ambalo lilihusiana na huyo mtu kama muendelezo wa kesi ile?" Niliuliza. Nilimuona AKM akiinamia sahani ya chakula kama anayetafuta chuya kwenye mchele nikajua ameingia kwenye tafakuri pengine. Alipoinuka akanitazama kwa macho makini mno.


"Sasa nimepata uhakika wa mawazo yangu kabisa...!"


"Kivipi?"


"...kivipi...? Catherine..! Mr. Dao ameniletea ufumbuzi wa tatizo langu hapa nchini lakini pia unaelekea kwenye hitimisho la kilichokuleta hapa nchini...!"


"Kwa namna gani useme hivyo Luteni..? Nilimuuliza nikiwa katika mshangao ambao ndani yake furaha pia ilikuwepo maana huwenda kuna jambo limefumbuka kichwani mwake.


".....ile kesi ya kuhusiana na kampuni iliibuliwa tena baada ya miaka kama kumi na tano ama sita hivi hii ilikuwa ni baada ya Maleley kufariki dunia... Hii ni nini maana yake Catherine....?" Luteni aliniuliza.


"Wapo washirika wa Maleley Kobra kama si ndugu zake...!"


"Haswaaa...!" Alidakia Luteni mstaafu Abdallah Khalid Mapande au AKM. Furaha ilikuwa kwake. Sikutaka kuendelea na hilo tena kwani sasa niliamini hili lipo na litanifikisha mahali.




Maleley Kobra aliumwa kwa tetesi kabla ya tetesi za kifo kumkuta pia. Inaleta picha....na kuna uwezekano mkubwa sana tetesi hizo zikahusiana na hili linaloendelea sasa. Kama Maleley Kobra alikufa huyu ni nani na kwanini anafuata nyendo za Maleley..? Inawezekana baada ya kushindwa kwa kesi naye akaamua kufanya mauaji haya ambayo ni tishio hapa nchini...? Liliniumiza kichwa hata hivyo nikaliweka pembeni na kumtazama AKM usoni huku kimya kile kikimezwa na mawazo yangu.


"Nini kimejiri huko?" Niliuvunja ukimya nikamuuliza AKM nikitaka kujua atokako kumetokea nini kilichopelekea kuitwa kwake. AKM akanitazama kwa utulivu mkubwa sana. Sura yake ilionesha kitu fulani kilichojificha.


Nilitaka kukijua.


"Catherine...!" Aliniita na kuweka kijiko kwenye sahani, akasema.


"Kuna kitu kimeingia hapa nchini na kinaweza kusababisha balaa kubwa...!"


Balaa kubwa!


"....haya yanayoendelea leo ni mambo yaliyokwishakupita muda mrefu sana na yanauhusiano pengine na haya tuliyotoka kuyazungumza, hayakuwa wazi na yalimchanganya sana muheshimiwa Rais. Kuna taarifa zimemfikia muheshimiwa na taarifa hizo zinamtaka afanye maamuzi ya haraka sana la sivyo balaa hili la ukosefu wa dawa kwenye mahospitali na vituo vya afya litakuwa kubwa na litamgarimu."


Inawezekana kweli...? Ni watu wa namna gani hawa wenye sauti na mamlaka ya namna hiyo? Niliwaza nikiwa nimeanza kujenga picha ya kila kilichokuwa kikiendelea.


Kweli balaa...balaa kubwa.


"Luteni inawezekaje hii?" Niliuliza nikiwa nimechanganyikiwa.


"Inawezekana Catherine....inawezekana tena inawezekana kwa kiasi kikubwa mno usione kila kitu ni kidogo. Nchi hizi za kiafrika zina utajiri mkubwa sana na utajiri huu ndiwo hasa unaotufanya sisi tuishi kwa mashaka na vilevile tuishi kwa amani. Amani tuishio sisi ni ile ya kukubaliana na matakwa ya wenye uwezo wa kuzichuma mali hizi na kuzipeleka ughaibuni. Endapo wakiweza kuchukua wanachotaka na kutuachia thamani kidogo isiyotutosheleza kiasi kwamba tutafikia hatua ya kuomba misaada kwao, hapa ndipo tuionapo hiyo amani...amani ya kutuacha tukiishia kufa masikini Afrika na kuchelewa kuyafikia maendeleo ambayo kila siku wao huyanadi kwa kutudanganya kama watoto wadogo watudanganyao na misaada mikopo yao midogo mithili pipi na kuzidi kunadi kuwa ni lazima tufikie maendeleo tuyatakayo....


maendeleo...?


Maendeleo yapi sasa....


Maendeleo haya...haya ya kutusaidia kwa kutukopesha huku wakijilipa kwa kuchimba madini wakituachia utajiri wa mahandaki ya kutisha yanaoogopesha vizazi vyetu wakiamini tumekaribiwa na bonde la ufa kisha kutuachi asilimia ndogo ambayo haitoshelezi kiasi tunaangukia kwenye kuwapigia goti tena... au ni haya ya kuwasomba wanyama pori wetu vile watavyo... ama haya ya kubeba samaki wenye minofu mikubwa huku wakituachia mapanki? Hakuna maendele ya namna hiyo ni wazandiki waongo.




Sisi maisha yetu Afrika ni maisha ya kuku tu, tunaishi ili tuwafaidishe wafugaji. Ukibisha unayakaribisha mashaka. Mashaka ya kuchinjwa kama kuku, mashaka ya kufungiwa bandani kama kuku ukipewa chakula duni. Mashaka hayo ndiyo yaliyomkuta muheshimiwa Rais wa nchi yetu hapa na mfano wa mashaka hayo hayo ni kama yale yaliyowahi kumkuta mpigania uhuru wa Afrika ya kusini Nelson Mandela. Na mashaka haya kwetu huja pale viongozi wazalendo na wenye uchungu na taifa lao wanaposhika madaraka. Viongozi hao wanaichambua sheria ya kila wizara na kuichanganua kuangalia mapungufu na kuyapatia ufumbuzi, hapa huibuka hatari ambayo itawafanya watu wenye nguvu duniani kuingilia kati na kumpinga kiongozi huyo kwa dhana tofauti tofauti. Wapo watakaosema kuwa kiongozi huyo anajichumia mali na kujinufaisha yeye na familia yake, wapo watakaosema kiongozi huyo ni dikteta hana huruma na wananchi, wapo watakao muita muuaji na asiye na huruma kwa wananchi wake vilevile hata hivyo pia wapo watakaoanzisha kampeni za chinichini ambazo zitasukumiwa kwa wananchi wenyewe wenye uchu na madaraka kisha kuwapandikizia chuki yenye kuleta uhasama nchini....wapo watu wa namna hii kwenye mataifa mengi ya ki-Afrika na watu wenye mpango mbaya na Afrika yetu huko ughaibuni wanawajua watu namna hiyo na wanawatumia ipasavyo.








Wapo watakaosema kuwa kiongozi huyo anajichumia mali na kujinufaisha yeye na familia yake, wapo watakaosema kiongozi huyo ni dikteta hana huruma na wananchi, wapo watakao muita muuaji na asiye na huruma kwa wananchi wake vilevile hata hivyo pia wapo watakaoanzisha kampeni za chinichini ambazo zitasukumiwa kwa wananchi wenyewe wenye uchu na madaraka kisha kuwapandikizia chuki yenye kuleta uhasama nchini....wapo watu wa namna hii kwenye mataifa mengi ya ki-Afrika na watu wenye mpango mbaya na Afrika yetu huko ughaibuni wanawajua watu namna hiyo na wanawatumia ipasavyo.




SONGA NAYO SASA




Wako radhi kuwasaidia kwa kiwango kikubwa cha pesa, kuwadhamini silaha kali za kivita na hata kuwapa mafunzo makali ya kijeshi kwa usiri mkubwa ili ikiwezekana waibue hata machafuko ambayo yatawarahisishia wao kuingia nchini na kuchota wakitakacho kwa fujo na kuwaachia nchi yenu ikiwa mfano wa fuvu lisilo na chochote ndanimwe. Itazame Libya ya sasa, itazame Kongo ilivyojaa uasi, itazame Burundi na Rwanda wababe wa ughaibuni wanavyotumia fimbo ya ukabila kwa mataifa haya na kuwafanya iwaumize wenyewe huku wao wakicheka mbele ya runinga zao zinazorusha habari hizo kama wanaangali picha ya ngo mpya iliyoingia sokoni, itazame Sudan. Zitazame nchi za Afrika....zitazame...? Hatuandikii mate maono na shahidi hizo zipo kwa mataifa ya wenzetu hapa Afrika. Hili ndilo linaloendelea hapa nchini Catherine." Alieleza kwa mapana AKM. Nilimuelewa kwa kina sana na alinifumbuwa mengi mno. Nilijikuta nikifungua ukurusa mpya wa matukio kupitia maelezo yake na kuibua kitu kipya kabisa akilini mwangu.




"Unataka kuniambia kuwa huu ni mpango wa nje?" Nilimuuliza.


"Haswaa..!" Alijibu akatulia kwa jozi ya sekunde kisha akaendelea.


"Mpango huu ni hatari sana Catherine yaani unakupiga kimyakimya na kukuangamiza. Mnakufa pasipo kujua kinachosababisha mfe ni nini. Unaweza kung'amua ya usoni kwamba labda ni ugonjwa ama hata ukosefu wa dawa kama hili la hapa nchini lakini je, nini chanzo kilicholeta ugonjwa huo. Hapa ndipo kwenye shida.....shida kubwa...shida ndiyo,"


"Nimekuelewa Luteni hata hivyo katika uelewa wangu lipo la kushauri...!"


"Nini..?"


"Huu mpango uko na watu wachache na hao ndio kauzibe. Sina imani kama mpango huu uko wazi, wapo watu wenye nguvu sana na wanazuia huu mpango ilimradi kumlazimisha muheshimiwa Rais afanye wanachokitaka...wanachokitaka eeenh...! Kwa sababu gani nimesema wanachokitaka...? Ni matukio tu jinsi yanavyojiunga mkuu...!"


"Akha...! Kumbe uko na wazo sawa na mimi, nilimshauri mkuu na kumwambia kuwa matatizo huwa hayaishi milele maishani mwetu, kuna wakati huwa yanakwisha. Hili litakuwa ni pigo kwake na fimbo kwa wapinzani wake. Nikamshauri aweke pamba masikioni kwa muda bila kutoa majibu wala kusikiliza chochote hadi pale ambapo ataona hakuna namna. Nikamwambia kwa hilo ni lazima funyo aliyeuvundisha mwili na kuufanya unuke ni lazuma ajitokeze na hapo litakuwa si tatizo tena maana ni rahisi kumuua funyo aliyoko nje ya kidonda kinachooza na kukinyunyizia dawa kidonda kuliko kutafuta ufumbuzi wa tiba ya kidonda, kwa kumchokonoa na pamba isiyo na dawa. Funyo hatatoka ataendelea kukusumbua kidondani hata hivyo utakuza kidonda. Akanielewa japo yeye alitaka aende mbali zaidi ikiwezekana kuomba msaada nje ya taifa hili. Nikamwambia kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuwafungulia njia hawa wajinga wapite kwa urahisi.


Akanielewa zaidi. Tukaufunga mjadala ule kwa makubaliano ya uchunguzi wa kweli na maadhimio ya kuhitimisha huku tukiwahimiza waliokabidhiwa jukumu hili la kuwatafuta hawa waharakishe kisha kuwasafisha.


Mjadala ukafungwa.


"Nataka nijue kwa upande wako kuna nini..?" Aliniuliza. Nikamtazama kwa tuo kisha nikaisogeza pembeni sahani ya chakula na kujifuta midomo tena kwa mikono yangu. Nilishakinahiwa na kile chakula tayari na sikuwa na hamu nacho tena. Maelezo ya Luteni mstaafu yalikuwa yameanza kuichemsha damu mwilini mwangu na kunipa ari mpya ya kurudi mchezoni....nilikuwa naenda kumaliza kazi kabisa.


"Naweza kusema kuwa nimepiga hatua fulani japo sijui kama ndiyo njia ya kumfikia Musa ama la!"


"Mmnhu...!" Akaonesha hamasisho kwangu la kunitaka niendelee mara baada ya kuona nimeweka tuo. Nikaendelea.


".....katika uchunguzi wangu nimeweza kumgundua mtu mmoja ambaye sina hakika kama ndiye atanifikisha kwenye hitaji langu."


"Mtu gani..?"


"Amsuni Bhehe...!"


"Amsuni Bhehe....? Amsuni Bhehe ndiye mtu uliyemnasa kwenye uchunguzi wako? Umemgunduaje..?"


"....ni baada ya kuchunguza kwa kina na kukutana na mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Welason, nilipombana na mtu huyo vizuri ndipo aliponitajia huyu mtu...!" Nilimueleza namna iliyopelekea mimi kukutana na huyo marehemu Welason hadi kunitajia Amsuni Bhehe.


Nilimueleza kinagaubaga hadi mtu ambaye naye niliamini ni mpelelezi.


"Shiit...!" Akang'aka AKM huku akiyatembeza macho yake pale sebuleni.


"Amsuni Bhehe hilo si jina geni kwangu Catherine, huyo ni mtu hatari sana na alishapigana vita kadhaa akiwa jeshini kabla ya kustaafu. Ana weledi mkubwa wa kutumia silaha za aina mbalimbali, anazijua vizuri medani za kivita, ana roho ngumu kama ya paka isiyokubali kushindwa, ana shabaha kali." Alisema AKM akiwa ananitazama moja kwa moja usoni. Wazo juu ya anayoyazungumza ni kama lilikuwa likiniletea jazanda fulani usoni mwangu nalo moja kwa moja likanipeleka kwa yule mdunguaji ambaye alikuwa akianiandama ndani ya lile pori zito.


Atakuwa ni yeye.


"....inawezekanaje? Kwanini mwanajeshi mstaafu afanye mambo kama haya na yeye aliishi miaka mingi akiwa ni wa kulitumikia jeshi kwa nidhamu ya haki huku akiwa tayari kufa kwa ajili ya taifa lake...hii ni mpya kwangu Luteni...?"


"Inawezekana." Alinijibu Luteni Abdallah Mapande huku akivuta subira kidogo na kupachika sigara mpya kinywani mwake kishapo akaendelea baada ya kuiwasha kwa kiberiti cha gesi.


"Unamaanisha nini unaposema inawezekana?" Nilimuuliza hata hivyo hakunijibu, alinikata jicho kali sana ambalo liliashiria kuwa sikutakiwa kumkatia kwa mbele wakati akiwa bado anaendelea kuzungumza. Alijawa na zile kanuni za kijeshi. Nikatulizana kimya kabisa. Akaendelea.


"....wapo wanajeshi ambao ni wasaliti yaani hawana chembe ya uzalendo na watu wa aina hii wakaishi jeshini kwa misingi hiyo hadi kustaafu kwao, watu wa namna hii ni wepesi sana kuendeleza upuuzi wao wakiwa out of the job....unashangaa...?"


"Mh! Mh!... Nimekuelewa na unanileta kwenye maana halisi. Naamini kwa asilimia kubwa nikimtia mikononi Amsuni basi kuna uwezekano mkubwa wa kumpata mtu anayeitwa Musa?"


"Naamini hivyo kwa sababu siamini kama mtu mwenye uwezo mkubwa kama yeye asizijue siri za anaowafanyia kazi...haiwezekani." Aliongea Abdallah Mapande. Nilijikuta nikipata morali mpya ya kazi sasa nilisimama wima na kujiweka sawa. Mwanajeshi yule mstaafu alinitazama usoni akiwa bado amekaa kitako kisha akasimama na kunitazama kwa ukaribu zaidi.


"Unaondoka na giza hili likiwa limekwisha anza?" Aliniuliza.


"Lazima niende na usiku huu ikiwezekana nimjue huyo mjinga au ikishindikana basi iwe ni kesho mapema nikichelewa huyu mpuuzi ataharibu kila kitu." Nilimwambia huku nikielekea chumbani, nilipotoka nilikuwa nimebeba begi moja dogo mbalo lilikuwa na silaha kadhaa ambazo mzee huyo alinitaka niondoke nazo kama akiba ikiwa sitafika kwenye ile nyumba ambayo nilikuwa nikiitumia ambayo ilikuwa na silaha za kutosha. Nilichukua bastola moja niliyoipenda kutoka mule begini kisha nikaifutika mafumichoni. Nikakagua kama visu vyangu vipo sawa niliporidhika kuwa vilikuwepo, nililikamata lile begi vizuri. Nilitoka mule ndani na kufika maegeshoni.


"Lazima nikakuache mjini ili uwahi kwenye harakati zako. Hali ni mbaya ya kiusalama na pia ukifika huko mjini ndiyo utajua watu wanaishi wakiwa katika hali gani, watu wanakufa hovyo hakuna tiba...hakuna tiba ndiyo...! Unadhani kutakuwa na tiba bila dawa? Watu wanakufa Catherini kuna watu wana roho za plastiki nyie acheni...khaa!" Alisema huku akinipita na kuingia upande wenye usukani nami nikajifungulia mlango na kuingia upande wa abiria. Aliendelea kuvuta sigara huku akiendesha gari. Sikuhitaji kutumia kilevi chochote kulingana na hali halisi ilivyo. Kimya kilikuwa kikubwa mule ndani ya gari hadi tulipoikamata barabara iliyokuwa ikielekea kijiji cha Bantu.Tuliongea mengi sana na mzee huyo ambaye kubwa zaidi hadi hapo alinipongeza kwa ukakamavu wangu kama mwanamke alinitazama huku akitabasamu na kukosa kunipa jina zuri. Tulitazamana akacheka nikacheka.


Hakika tulicheka.


"Hakika wewe ni shujaa?" Akamalizia. Sikumjibu kwani tulishafika mahali alipotaka kuniacha. Tulisimama kwenye njia panda ya kutokea bantu na barabara kubwa ya lami. Akaniacha hapo huku akinitakia safari njema yenye mafanikio. Nikamuaga.


Akaondoka, nikaondoka.




________




Kwa upande wa Malfrey Kobra hali yake ilikuwa si ya kuridhisha hata kidogo bado alikuwa amepotelewa na fahamu tangia hali ile ilipomtokea hapo awali. Walimfikisha nyumbani kwake akaingizwa kwenye chumba ambacho ndicho chumba maalumu chenye kutolewa matibabu dhidi yake. Alikwenda kuitwa daktari wake ambaye alikuwa ni dokta Lumoso Papi Mmbai. Alichoka sana dokta huyo, uzee ulikuwa umechukuwa nafasi kubwa kwake, bado mwili wake ulikuwa na afya japo, huwenda ni kutokana na kuyazoea maisha halisi aishio. Alifuatwa chumbani kwake alipokuwa akipenda kushinda na kujisomea vitabu mbalimbali vya saikolojia, sayansi na hata riwaya za kijasusi. Hiki ndicho kilichokuwa kilevi chake kikuu na mara nyingi umkutapo jua utamkuta akiwa na kitabu mkononi. Alitimiziwa vitu hivyo kwa kadiri alivyokuwa akiviagizia lakini si kupewa uhuru wa kutembea au kufanya chochote ambacho kingeleta hisia za kutaka kutoroka. Taarifa ya kuwa Malfrey Kobra alifikia katika hatua mbaya kiafya zilimshtu. Alikurupuka kutokea alipokaa na kukimbilia mahali ambapo alimkuta bwana huyo akiwa ametokwa na fahamu.


"Amepatwa na nini huyu?" Aliuliza akiwa ametuliza akili vizuri akimtazama mgonjwa wake wa muda mrefu. Nywele zake za pembeni zilizokoswa na uwaraza mkubwa uliotawala katikati ya kichwa chake hadi karibia na kisogo, zilikuwa zimetawaliwa na weupe kwa asilimia kubwa sana. Ndevu zake nyingi pia vivo hivyo. Alimtazama Tally Man na wauguzi wengine wawili waliyopo hapo kutoa msaada akisubiri jibu la swali alilouliza.


"Mshtuko....alikumbwa na mshtuko mkubwa ambao ulitokana na shughuli zake za kibiashara." Alijibiwa hata hivyo jibu hili lilikuwa na mashaka makubwa ndani yake.


Haya mambo hayakuwepo kwa muda wa miaka kumi sasa iweje yarudi leo....? Tangu kupoteza maisha kwa kaka yake Maleley Kobra hakukuwa na purukushani hizi. Kwa akili yake ya kiutu uzima alijua fika hapo ni lazima kutokee kitu ambacho kingeweza kuirejesha faraja iliyopotea.




Pamoja na kwamba alithaminika na Malfrey lakini hakupenda kuishi katika imani na furaha ile ya ndani kwa ndani, pia hata siku moja hakupenda kuwa na imani na watu hao ambao upendo na mapenzi yao makubwa huja pale wawapo na shida ya msingi. Kifo cha dokta Omary Maboli Siki bado kilikuwa kikiishi moyoni mwake kwa chuki kubwa dhidi ya watu hao. Kuna wakati alijishauri kufanya jambo baya kwa huyo aliyesalia hata hivyo wazo hilo alilipuuzia mara baada ya kufikiri mengi ikiwemo uhitaji mkubwa nchini kwake. Akazidi kuvuta subira ambayo nayo ilimchosha hivyo pia hakuwa na namna nyingine. Alimtazama Malfrey kwa kitambo kirefu huku akijaribu kushika hiki na kile akijaribu kumpima. Hadi pale alipokuja kupata ufumbuzi wa tatizo lile kwa ujumla wake. Afya ya mtu huyo aliifahamu vizuri na alijua fika muda na wakati wowote huyo bwana angeweza kupoteza maisha. Hadi hapo kwa tathmini yake alijua fika asingepoteza muda mrefu bila kurudiwa na fahamu. Aliacha dripu la dawa liendelee kumuingia mwilini huku akiwa pembeni yake akiyaruhusu masaa na dakika zake yasogee.




Nusu saa baadaye, Malfrey alianza kwa kutikisa miguu yake kisha mikono kuisogeza na kuitupa kwa awamu. Dokta Lumoso akamtazama mgonjwa wake kwa tuo na udadisi zaidi kwani alikaa pembeni ya mgonjwa huku akiwatoa wauguzi wote akiwa na sababu zake binafsi. Dokta Lumoso Mmbai alitaka kujua kilichomtokea huyo bwana ni kipi. Alikuwa na uhakika kuwa bwana huyo angeropoka tu baada ya kurejewa na fahamu na kwa kawaida ya wagonjwa wa namna hiyo kwa ujuzi na uzoefu wa taaluma yake ni kwamba mgonjwa huropoka kile ambacho kimemletea masaibu hayo ya kumpotezea fahamu.


Alitaka kukisikia.


Usukumwaji wa mikono uliendelea taratibu, mara akaanza kuongea maneno yasiyoeleweka.




"Mnashindwa vipi na mwanamke...mwanamke...hasara...hapana lazima atafutwe, auawe...afe, afe...eenh! Ndiyo, afe....a...aa....aaaghr.....!" Malfrey alizidi kuongea mambo yasiyoeleweka alizidi kubwabwaja tu huku dokta Lumoso akiwa kimya tayari akiwa wima. Hakutaka Malfrey afumbue macho na amkute yuko hapo.


Hata.


Kwa watu wenye mambo mabaya kama hao huwa hawaamini pale walipopotewa na fahamu hatimaye fahamu hizo kuwarudia halafu wakakutana na mtu ambaye si wa kusikia siri zao. Hawana msamaha na maamuzi yao huwa ni magumu hawataki siri zao kuota mbawa hata iweje.


Dokta Lumoso alifahamu yote hayo labda ni kutokana na kupenda kusoma riwaya za saikolojia za watu mbalimbali.




".....aaaagh....! Aaaa....Musaa....akijua, akijua...ni hatari akijua muu....!" Dokta Lumoso Papi Mmbai hakusubiri Malfrey amalize alichokuwa akikiropoka. Alishafika mlangoni na kupiga macho kulia na kushoto kisha akarudi kwenye chumba chake ambacho hukitumia kama ofisi. Akajiweka kitandani na kujishika shavu akiingia kwenye tafakuri nzito. Alisikia neno Musa.






Dokta Lumoso Papi Mmbai hakusubiri Malfrey amalize alichokuwa akikiropoka. Alishafika mlangoni na kupiga macho kulia na kushoto kisha akarudi kwenye chumba chake ambacho hukitumia kama ofisi. Akajiweka kitandani na kujishika shavu akiingia kwenye tafakuri nzito. Alisikia neno Musa.




SONGA NAYO SASA....




Musa...naona kitu kwenye hili jina na huwenda...huwenda nikawa sahihi juu ya mawazo yangu....! Fikra zilipita kichwani mwake namna hiyo dokta Lumoso. Ile dalili ya kuwa huwenda anakombolewa kutoka mikononi mwa watu wabaya ilikuwa ikienda kutimia. Alilijua hilo jina tangu mara ya kwanza anapewa vitisho na kuambiwa aandae ripoti. Hata kuamua kuificha ripoti ile isionwe ila akiamini ingekuja kuonwa na watakaotaka njia ya kujua ni wapi walipelekwa. Hakuna mwingine anayejua kuhusu Musa ila yeye na kama ni yeye basi yapo matumaini ya kukombolewa na kurudi nyumbani. Chozi la uchungu liliwamba kwenye mboni ya jicho lake la kushoto. Aliivuta pakiti ya sigara na kuchomoa sigara moja akaibana kwenye kingo za midomo yake na kuiwasha kwa msaada wa kiberiti cha gesi akavuta kwa nguvu huku akiliruhusu lile chozi kumdondoka baada ya kuyafinya macho yake sambamba na mtoko wa moshi kinywani mwake.


".....aaa! Dokta...dokta! Sauti iliita. Alikuwa ni kijana mmoja miongoni mwa vijana walioongezwa kwa ajilj ya kuimarisha ulinzi baada ya hali kuonekana mbaya. Dokta alifuta machozi na kujipa utulivu kisha akaivuta ile sigara kwa pafu zito kisha akaisiga kwenye kikombe cha majivu na kuiweka karibu na kiberiti cha gesi akasimama na kuzitupa hatua zake kufuata wito.


"Aisee! Amerudiwa...amerudiwa na fahamu tayari." Ilitoa taarifa kwa fujo ile sauti. Dokta Lumoso akazidi kuzirusha hatua zake huku akitabasamu kwa muda.


Wapuuzi sana hawa, wajinga kabisa hawa vichwa maji..!


Akatoka mbio na kuwahi kwenye chumba alicholala Malfrey.


"Unajisikiaje sasa..?"


"Mwili...kichwa na mwili naona vimekuwa vizito sana...nini kilitokea..?"


"Ulipoteza fahamu mkuu...!" Yule kijana alidakia. Kumbukumbu mbaya ikaanza kumnyemelea Malfrey akaanza kuona macho yakiwa mazito huku mbele yake akiwa amesimama Amsuni Bhehe.


Wewe ni mwanajeshi Amsuni....Amsuni fanya linalowezekana...hasara aaa...! Laana kum! Ilikuwa balaa.




Pamoja na kujiwazia kote bado aliona namna hali ivyokuwa ngumu kwa upande wake. Akakurupuka na kutaka kutoka kitandani hata hivyo alishindwa baada ya kujikuta miguu ikimuwia uzito.


"....aaaaaaghrr....!" Alibwatuka kwa ghadhabu kubwa alipoona miguu yake ikiwa imefungwa kwa mikanda maalumu pale kitandani. Akafiri kwa muda kisha akatabasamu huku akimtazama dokta japo tazamo hilo lilikuwa limeficha kitu kizito ndani yake.


"Mwambie Tally Man aniunganishe na Mr. Polgeo sasa hivi." Alitoa amri kisha akabaki akitweta utadhani akili yake ilikuwa katikati ya marathon.


Aliiona dunia ikija kama jiwe usoni mwake kisha kumtazama na kumcheka ikiwa inaning'inia karibu na paji lake la uso.


Si kifo hicho?




Punde Tally Man alifika akiwa na simu mkononi akamkabidhi, Malfrey akaiweka sikioni hata hivyo kabla ya kuongea chochote aliishusha ile simu na kumtazama dokta Lumoso na yule kijana kwa macho makali. Wale wawili wakaelewa, wakatoka nje mule ndani akiachwa Tally Man.


"Nimepata hasara Mr. Polgeo...hasara...hasara kubwa. Helkopta yangu imelipuliwa vijana zaidi ya ishirini eti...eti, nao wame...wameangamizwa...kuna nini sasa hapo..?"


"Nimezipata hizo taarifa na zimenichanganya hata mimi na mbaya zaidi huyu mjinga Rais Backa hataki kutoa maamuzi yoyote kuhusiana na onyo nililotoa licha ya wananchi wake kufa kama kuku mdondo...!"


"Tumepoteza...!" Malfrey akaropoka hata hivyo hakufika mwisho akaitoa ile simu sikioni kama iliyokuwa ikimuunguza akaitazama na kuiweka tena sikioni akiendelea. ".....nini tunafanya kwa hatua ya mwisho...?"


"Ni kuwaacha wananchi wake waendelee kufa kwa kuwa ameridhika wafe lakini wewe ukipanga vijana tena huku wakihakikisha wanamuwinda au kuwawinda hao wasumbufu ikiwezekana hadi kesho tuwe tumefunga hii kazi ya hao wasumbufu na tubakiwe na huyu Rais na mzagao wa maiti mitaani--unasemaje?"


"Ninalo sasa..!" Aliropoka tena. Alikuwa amechanganyikiwa waziwazi.


Alipatwa.


"Kingine ni kwamba kuanzia sasa sote hasa wewe Malfrey uhakikishe tunakubaliana kuua 'MU' na kubakiwa na 'SA' kuanzia sasa...narudia tena kuanzia sasa Malfrey yaani wewe usibakie kwako na hapa Samiado bali uanze kuishi kwenye jumba la makutano yetu ili kuzuia kuwavuta hawa wajinga wasije wakamfikia Musa mapema, kila kitu kitamalizikia huko kwa upande wako kuanzia ulinzi na kadhalika...!"


Yaani MUSA inatenganishwa 'MU' inaondolewa na kubakiwa na 'SA' kwa kipindi gani sasa...? Hiki au..? Mbona isingeleta maana...!


"Haya sawa..!" Alikubali kwa shingo upande Malfrey kwani kuondoka Samiado na kwenda kuishi Muavengero ilikuwa ni hatari sana kwake, hali si hali, zote zikiwa pamoja ndiyo zilileta maana kubwa kabisa ya jina hilo lakini kufika hatua hiyo ya kutenganishwa ilikuwa ni hatua mbaya. Maji yalimfika ama yaliwafika shingoni hivyo hawakuwa na namna nyinge zaidi ya kukubaliana iwe hivyo.




Angefanyaje.


_________




Marietha na Mabule walikuwa wakibishana sana sebuleni wakiwa kwenye jengo ambalo walikabidhiwa kwa ajili ya operesheni hiyo. Mabishano hayo yakiwa ni kuhusiana na mienendo ya Sembuyagi Mpauko kwani hadi hapo kila mmoja alikuwa akiamini kuwa huyo si mwenzao katika kazi.


"Ilikuwaje akawa ni mamluki na usijue au mko pamoja?" Aliuliza Marietha akiwa amechanganyikiwa. Akamtazama Mabule aliyekuwa ameikunja sura yake kwa ghadhabu.


"Nimetoka Tanzania na huyu mtu Marietha hata hivyo sikujua kama anakuja kunitia aibu huku ugenini...nashindwa kuelewa ni kipi hasa kilichosababisha awe hivyo....sijui kilichompumbaza."


"Unakubali kuwa Sembuyagi ni mamluki?"


"Hadi hapa tulipofikia na kwa kile nilichokiona kule msituni, jamaa ni nyoka tena nyoka mwenye sumu ambaye alikuwa akisubiri tuzubae atumalize kama kuku tu bandani." Alisema Mabule akiwa amechoka akili na mwili.


"Nisikilize?" Alisema Marietha akimtazama Mabule usoni. Akavuta pumzi na kuendelea.


"....nilijua hili mapema na nilijua jamaa yupo kwa ajili ya kutuzuga tu. Jamaa alikuwa akitoka usiku bila kutuaga na hasemi anakwenda wapi...kumbukumbu zangu zinaniambia ni mara mbili Sembuyagi Mpauko alikuwa akitoka usiku. Nilianza kumzoea kuanzia mavazi yake lakini siku ya kwanza alipotoka usiku na kurudi usiku huo huo wa manane asubuhi alibadili mtindo wa mavazi na si kawaida yake, hata kama alikuwa akijaribu kubadili muonekano lakini si kwa namna ile....ilikuwa hivi; jamaa alidhani labda mimi na wewe tulikuwa tumelala lakini haikuwa hivyo kwani sikuwa na uwezo wa kulala hasa ninapokuwa na kazi kubwa ya kulisaidia taifa langu. Ilikuwa ni saa sita kama sikosei. Jamaa alinyata kutoka chumbani kwake hadi kwenye chumba changu akachungulia nilimuona ila sikutaka kumuuliza wala kumshitua. Alitoka na kuufuata mlango akatia ufunguo na kutoka nje, sikuwa na papara ya kujua ni kwanini alifanya yale. Nilisubiri nione huwenda hata akifanyacho kilikuwa na faida kwa upande wetu. Alirudi usiku mkubwa akaingia kama alivyotoka. Alipojifungia chumbani kwake ndipo nilipochukua jukumu la kuchunguza anachokifanya. Nikatoka hadi kwenye mlango wa chumba chake ambako nilichungulia kwenye tundu la funguo sikuweza kuona kitu kwani jamaa aliacha ufunguo kwa upande wa ndani. Kama pia ulikuwa hujui jamaa hakupenda kuacha mlango wake wazi kama ilivyo kwa mimi na wewe. Nikachungulia kwa shida sana kupitia nafasi za wazi za mlango ndipo nilipoona akijitibu jeraha dogo la mchubuko juu kido ya uso wake. Siku iliyofuata jamaa akaanza kuvaa miwani myeusi na kofia ya chepeo ambayo ilikaribia kuufunika uso wake. Hapo mimi nilikuwa nikijua nini anachokifanya na huwenda hakikuwa chema kabisa....hakuishia hapo tu hata na siku iliyofuata ilikuwa ni hivyo na kila akirudi jamaa anakuwa anaugulia maumivu....!"


"Kwanini uliamua kumfuatilia Sembuyagi Mpauko namna hiyo?." Hatimaye Mabule aliuliza akiwa anamtazama Marietha usoni kwa makini zaidi.


"Si Sembuyagi Mpauko Haufi tu bali hata wewe na hii ilikuwa ni oda niliyopewa na mkuu wangu wa kazi kwanza kuwachunguza ninyi kabla ya kuridhishwa na kufanya kazi pamoja. Ni vigumu kumuamini mwanadamu moja kwa moja hasa mwanausalama kwasababu mwanadamu mwenyewe hataki kuaminiwa, nilifanikiwa kwa kiwango kikubwa sana na nilibakisha ushahidi wa mwisho ambao hata wewe mwenyewe umekufunulia sababu yangu ya kumfuatilia huyo jamaa....jamaa si mtu mzuri na nia yake kubwa ni kumuondoa yule binti duniani maana kwake ndiye anayeonekana kikwazo kikubwa." Aliweka tuo Marietha kisha akamtazama Mabule usoni kwa macho yake mazuri ambayo yalimfanya Mabule ameze mate ya uchu.


"Siku nyingine alipotoka na kurudi aliteguliwa bega...!" Akaendelea kusema Marietha.


".....sikutaka kuamini kama huyu bwana anachokifanya ni chema, nikawa makini zaidi na ndipo nilipogundua pia alikuwa akifanya....!" Hakumalizia alichokuwa akikizungumza. Mlango ulisukumwa na Sembuyagi Mpauko aliingia kwa haraka akawasalimia kwa furaha kisha akaingia chumbani kwake. Hawakuonesha tofauti yoyote kwake kila kitu kilikwenda kama awali walionekana wakipiga soga za kawaida tu huku wakitazamana kwa mahaba kiasi mtu yeyote angeweza kuhisi kulikuwa na kitu kati yao kilianza kujichipua.




Sembuyagi alipitiliza moja kwa moja chumbani kwake na kutulia akiwa amesimama dirishani. Alikuwa na kazi kubwa mbili na zote alitakiwa kuzifanya kwa weledi. Moja ilikuwa ni kuhakikisha anazijua nyendo za yule mwanamke aliyewaletea shida kule porini na nyingine ikiwa ni kucheza na akili za akina Mabule. Aliwajua hawa watu vizuri hasa huyu mwanamke kwake alikuwa ni mtu wa kupaswa kuangaliwa kwa umakini mkubwa sana. Akili yake ilimwambia kuwa huwenda wenzake wanamhisi vibaya kutokana na maamuzi ya kutaka yule binti ashambuliwe au kuwatoroka kule porini wakati wanakimbia na kwa mtazamo wa kawaida tu ilionesha kuwa alikuwa upande sahihi. Hili lilimuumiza kichwa sana na inavyoonekana alitakiwa kutumia akili ya ziada kuwaweka sawa.


Ni akili gani?




Hapa ndipo palipokuwa na mtihani mzito. Akawaza na kuwazua kwa kitambo kirefu pasipo mafanikio ya kuamua ni nini afanye. Alisimama kwa muda kisha akakigeukia kioo kilichopo mule ndani na kulitazama jazanda lake kiooni. Akajitazama begani ambako kulikuwa na mchubuko wa kupapuzwa na risasi ya mtu aliyehisi ni mdunguaji kwa asilimia kubwa. Akameza mate ya chuki dhidi ya watu hao wanaomzibia nafasi ya yeye kupata pesa nyingi. Akalifunika lile jeraha vema kisha akajitathmini kwa awamu nyingine. Akajiridhisha. Akatoka na kwenda kuungana na wenzake.


"Ulikuwa wapi kiongozi..?" Aliuliza Marietha huku akimtazama usoni Sembuyagi Mpauko.


"Tulipotezana kule porini na hatukujua wewe ulikwenda wapi hadi sisi tunafika hapa?" Mabule alidakia. Sembuyagi Mpauko alijiweka sawa kitini akawatazama kwa pamoja na kusema.


"Nilijua lazima mngeniuliza swali la namna hiyo ndugu zangu. Unajua wakati napambana na yule mshenzi muuaji, kuna risasi ilinikosa na huwenda aliyeshuti hakuwa na shabaha kamili yaani kashuti pasipokujua itamkusudia nani. Yule alikuwa ni mdunguaji. Na kwa kuona vile ikanibidi kujiepusha na kutimua mbio hata hivyo nikiwataka na ninyi muweze kuondoka maana ilikuwa ni hatari sana. Sikupenda tuongozane tukiwa sambamba hii ingekuwa ni hatari zaidi na ingemrahisishia adui kutumia mbinu ya kutupa jiwe kwenye kundi la ndege. Ikanibidi nitafute njia nyingine na kujikuta nimetoke mbali mno kiasi kwamba iliniwia ugumu kuweza kufika nje ya ule msitu." Akawatazama baada ya kuweka tuo huku akiomba Mungu swala la yeye kujificha sura kwa maski lisiwekwe hadharani.


Tulikuona ukiwasiliana na mtu mwingine kupitia kisafirisha sauti kwanini hapo husemi hivyo? Marietha alitaka kumuuliza hivyo ila hakuona haja ya kufanya hivyo ikambidi kuwa mpole na kuichukua ile hoja ya kiongozi wake huku akijipa utulivu hakutaka kuchukua maamuzi ya haraka, pia hata kumuuliza kuhusu mask walijionya wasimuulize kwani waliamini angekuwa na uhakika kuwa wamemshtukia na angefanya kitu kisichosahihi kwa kukurupuka ikiwa bado walitaka kumkamata akiwa mahala pazuri, akamtazama Mabule kwa haraka kisha akahamisha macho yake kwa kiongozi wake.


"Nini kinafuata?" Mabule aliuliza ni kama akili yake ilikuwa sawa na Marietha.


Mmnh! Mbona kama kuna hisia za tofauti zipo kwa hawa watu.....? Mawazo hayo yalikuwa yakipita kwenye kichwa cha Sembuyagi japo hakuwa wazi kuwaonesha kuwa alishaanza kuwahisi vibaya.


Lakini kwanini nawaza hivi...? Akazidi kuzungumza na nafsi yake.


"Kinachofuata....kinachofuata ni...ok, kwa sasa ni lazima tufanye jambo moja la msingi sana ambalo kwa asilimia kubwa tutafanikiwa kumdhibiti huyu muuaji ambaye hadi sasa hajajidhihirisha anataka nini...lazima tuanzie pale tulipoanzia awali, lazima turudi pale kwenye ile nyumba ya waziri ambapo huyu mwanamke alisababisha mauaji. Tunaweza kupata kitu cha ziada tukifika pale na kinaweza kutufikisha mwisho wa hili." Aliongea Sembuyagi huku akiwatazama kwa zamu.


"Kwanini huyu mwanamke zaidi?" Alihoji Marietha.










"Kinachofuata....kinachofuata ni...ok, kwa sasa ni lazima tufanye jambo moja la msingi sana ambalo kwa asilimia kubwa tutafanikiwa kumdhibiti huyu muuaji ambaye hadi sasa hajajidhihirisha anataka nini...lazima tuanzie pale tulipoanzia awali, lazima turudi pale kwenye ile nyumba ya waziri ambapo huyu mwanamke alisababisha mauaji. Tunaweza kupata kitu cha ziada tukifika pale na kinaweza kutufikisha mwisho wa hili." Aliongea Sembuyagi huku akiwatazama kwa zamu.


"Kwanini huyu mwanamke zaidi?" Alihoji Marietha.




SONGA NAYO SASA...




"Yeye ndiye mshukiwa namba moja wa matukio haya ya mauaji yanayoendelea hapa nchini kwa kuwa tulimkuta eneo la tukio na wakati ninyi mnafika pale niliona akiwa anatoka mbio kwenye ile nyumba ya muheshimi waziri. Hivyo harakati zote zile zilikuwa ni za kumkimbiza yeye kama tutaendelea kumuacha apumue ni wazi kazi iliyotuleta huku Mabule itatushinda kamwe hatutaweza kuwarudisha madaktari wetu nyumbani."


Kama mwanadamu wa kweli anavyoongea huyu mpuuzi kumbe ni mnyama mwenye sumu. Aliwaza Mabule huku sura yake ikiachia tabasamu la matumaini ingawa ndani ya moyo wake kulijaa chuki dhidi ya mtu huyo.


"Inabidi tuelekee huko sasa hivi kwani ni hatari sana kama tutachelewa, hamuoni kama tutampa nafasi ya kujificha zaidi?" Aliuliza Mabule huku akimtazama Marietha kwa jicho la matumaini kisha akayahamishia macho yake kwa Sembuyagi wakasimama. Walitoka kwenye mlango kwa kasi na kukimbilia kwenye maegesho ya magari ambako waliingia kwenye gari yao na kuondoka eneo hilo kwa kasi ya ajabu.




__________




Ni kama dakika tano zimepita tangu niingie ndani ya nyumba niliyokabidhiwa na luteni mstaafu AKM ambayo ndiyo niliyokabidhiwa hadi kumalizika kwa kazi iliyonileta nchini Ungamo. Nilikuwa na utajiri mkubwa wa nilichokivuna kwa AKM hivyo sikuwa na shaka lolote. Nilikuwa na mambo mawili makuu na muhimu kuanza nayo ambayo la pili liko ndani ya la kwanza. Na la kwanza hilo likiwa ni kuanza kumfuatilia Amsuni Bhehe huyu ndiye ambaye niliamini angeweza kuzalisha jambo la pili muhimu ambalo ni kuhakikisha Musa ananikabidhi watu wangu mkono kwa mkono bila purukushani. Sikuwa na haja ya kukawia kuwa hapo nilichokifanya ni kuweka mambo sawa ikiwemo kujimwagia maji na kujiandaa kwa ajili ya kutoka na kuanza harakati zangu. Ilipata kuwa ni saa mbili na dakika thelathini na tano za asubuhi. Bado nyumba hii ilikuwa mpya kwangu na kila niwapo ndani yake najihisi unyonge sana hata hivyo asubuhi hii nilijiona mwingi wa mawazo sana. Nilifikiri ni muda gani niliweza kupata wasaa wa kuweza hata kumtumia ujumbe mkuu wangu wa kazi kamanda Daniel Matia Okale au Mwalimu Dao kwa jina lake la kificho, sikukumbuka na haikuniingia akili kila nilipokuwa nikijipa uhakika kuwa niliwasiliana naye. Nikaonelea kuwa huo ndiyo ulikuwa muda pekee wa kufanya maamuzi kwani sikuona nafasi nyingine ya kufanya hivyo na vilevile nisingependelea kufanya kazi kienyeji pasipo kumpa taari yoyote.


Haikuwa kwenye taratibu zangu za kazi.


Nilivuta tarakilishi na kuiwasha kisha nikaingia moja kwa moja kwenye mfumo wa mawasiliano yetu na kutuma ujumbe wa kieletronic ukiwa umebeba maelezo yote kwa ufupi kuanzia nilivyoingia nchini hadi nilipofikia. Nilimueleza vyote vya msingi huku misukosuko niliyoipitia ikiwa ni sehemu yangu ya majumu. Nilipokwisha kuhakikisha kuwa ujumbe ule umekwenda, nikaizima na kuirudisha kwenye begi langu la siri ambalo lilikuwa likibeba vitu vidogovidogo vingi vya kazi kama hiyo tarakilishi na silaha nyingine za kijasusi. Nikaviweka kwenye kiti kilichopo nyuma ya meza hapo sebuleni tayari kwa kuvibeba wakati wowote ule. Nikiwa naelekea chumbani ili nipunguze nguo, akili yangu ikanigonga kwa nyuma na kuufanya ubongo wangu kuwa mzito kufanya kazi. Akili iliniweka katika hisia mbaya mwili ukawa mzito wenye kusita kufanya jambo.


Nikashangaa.


"Hii ni nini?" Nilijiuliza kwa sauti kama kwamba yupo wa kunisikiliza. Nilikuwa kwenye sintofahamu. Wazo la kuingia bafuni kuoga likaingilia kati ya majibizano ya sintofahamu zangu ikaichangamsha akili yangu huku mapigo ya moyo wangu yakikimbia kwa kasi nisiyoitarajia. Nikajionya. Sikuwa sahihi kupingana na mawazo yangu hata kidogo.


Lile wazo la kwenda kuoga likayeyuka taratibu kama bwimbwi kwenye upepo.


Nilipaswa kuwa makini....makini tena sana. Haukuwa wasaa mzuri wa kufanya maamuzi ya haraka wakati akili yangu ikiniweka katika u-machale. Hapana, huu ni muda wa kufikiri juu ya hii hali sipaswi kupingana na mawazo yangu.


Ngojea...nini hiki ambacho...ambacho kinanizuia kufanya....!


Nilichelewa kuamua. Kishindo kikubwa kikasikika niligeuka kwa haraka kubwa pale mlangoni ambako kishindo kile kilisikika.


Lo! Mlango ulifumuliwa ukanyanyuliwa juu na kutupwa ukutani huku vipande vidogovidogo vya mbao ya mlango vikirushwa huku na huko na kutengeneza uchafu usio na jina kwenye maandishi. Mitutu ya bunduki kwa idadi nisiyoijua kutokana na kuhamanika ikiwa inanimwagia mvua ya risasi si kawaida. Zilikuwa nyingi na wapigaji walikuwa kama waliyochanganyikiwa kiakili.


blood Saramanda...blood Kenge....! Niliwatusi nilivyoona inafaa.


Nilijirusha kutoke pale niliposimama kwa mruko wa kulala kiubavu kisha kwa kasi isiyotarajiwa nikapita na lile begi langu lilolokuwa pale kwenye kiti, sikutaka kuacha taarifa zangu hata kidogo. Nikabingilia chini kama mpira hadi ulipo mlango wa kuingilia chumbani nikaupiga kikumbo ukafunguka, nikajitoma ndani na kuujinyanyua kwa haraka nikaufunga mlango nyuma yangu kisha kitendo bila kuchelewa nikakimbilia ukutani palipo na swichi. Nikaminya mara nyingi hadi kapeti zilipojiachia pale chini. Nikakimbilia pale kwenye ule uwazi wa kuelekea chini ya aridhi kabla shabaha zao hawajazielekeza pale kwenye ule mlango na kusababisha kunipa ugumu wa kufanya maamuzi. Nikaingia kule chini kwa haraka sana nilipofika moja kwa moja nikataka kukimbilia mahali swichi ilipo hata hivyo sikufika nilisikia sauti za risasi kutokea juu huku nyingine zikinikosa kwa hatua chache sana za kuhesabia.


Oough shiit!


Hali ilikuwa tete na sikuwa na namna ya kuweza kufanya. Nilipokuwa nikizidi kushangaa, nikasikia kitu kama jiwe kikija kwa mvumo kutokea juu, nikahaki sikupoteza wakati nilitimua mbio kali sana kutokea pale, nilikuwa mjuvi wa vitu hivyo nilikimbia kwa hisia kutokana na giza na kwa kuwa nilishaijua njia na nilijua ilikuwa ikielekea wapi. Kumbukumbu zangu hazikusahau kunikumbusha kuwa njia ile sikuwa nimekwenda nayo hadi mwisho. Nilifika kwenye mlango mmoja mkubwa nikausukuma kwa kuwa sikuwa nimeufunga siku ile zaidi ya kuurudishia. Nilipofika ndani yake nikauacha mlango ambao wakati naingia kwa mara ya kwanza niligundua kuwa ilikuwa ni stoo ndogo ya kuhifadhia silaha. Sikuwa na muda wa kuchukua chochote hivyo nilicho nacho mgongoni ndicho ambacho ningeweza kutumia kama albaki yangu ya silaha.


Nilitakiwa kujiokoa na si kushangaa.


Niliufuata ujia mmoja mwembamba ambao baada ya hatua tatu nilikutana na ngazi ambazo zilikuwa zikipanda juu.


Mungu wangu!


Nilitikiswa na mtetemeko mkubwa sana huku nyuma biwi kubwa la moto likaibuka na kusababisha kuta za jengo lilo upande huu wa chini kuvunjika. Biwi lile la moto likawa linakuja kwa kasi kubwa kunifuata niliko huku likiburuza kila kitu kilichokuta njiani. Japo kulikuwa na muinuko hata hivyo niliongeza kasi, sasa ule mwanga wenye joto kali la mauti uliozaliwa na moto ule wa mlipuko wa bomu kama mawazo yangu yalivyohisi baada ya kuusikia ule mvumo mithili ya jiwe, ulikuwa ukija kwa sifa ya kutaka kuniangamiza kabisa na kunifanya nisionekane kwenye ramani ya dunia. Niliwatukana watu hao waliyofanya hivyo kila tusi lililokaa mbele yangu huku nikikimbia kwa kasi isiyo mithilika, niliweza kuzihesabu ngazi nyingi zilizokuwa zikielekea juu kwa kuzipanda. Sikuwahi kupita njia hiyo hivyo sikujua nilikuwa nakwenda kutokea wapi kwa awali nilipoingia niliishia kuitazama tu na sikupata wasaa wa kujaribu kuichunguza muishilizio wake. Sasa nilitakiwa kuitumia ili initoe kwenye hili sekeseke.


Umeona hatari ilivyo?




Nilizidi kujiwazia na kusema kweli kama mbele yangu kuna ukuta basi ni wazi kuwa kifo changu kingekuwa ni humo chini ya ardhi tena kifo kibaya sana cha kuungua kwa moto. Nilizidi kukimbia huku nikijitahidi kuyapotezea maumivu ya uzito mdogo wa begi langu mgongoni lililosheheni zana mbalimbali. Niligeuka nyuma na kukutana na lile biwi la moto likija kwa hasira ileile ya kuuwa, matumaini ya kutoka salama hayakuwapo kwani moshi nao ulianza kuniletea shida kubwa sana ya kushindwa kuvuta hewa vizuri. Sikuchoka kukimbia japo nafsini nilijilaumu kwa kuchukua maamuzi ya kuingia kwenye jengo hili ya chini ya aridhi.


Ningekwenda wapi wakati mbele kulikuwa na mitutu ya bunduki si chini ya sita.


Hilo lilikuwa ni wazo la kipumbavu. Joto lilizidi kuwa kali huku moshi mzito ukifukuta, mwili ulianza kuchoka huku jasho jingi likinimwagika kutokea sehemu mbalimbali za mwili wangu, moyo wangu nikauhisi kama ufao ganzi sasa. Niliomba dua ya hatua zangu za mwisho. Mbele niliona mlango mgumu sana wa chuma. Nilipoteza matumaini kabisa ya kutoka salama. Nilisogea karibu zaidi ndipo nikaona kufuli zito likiwa limefungwa kwenye ule mlango mzito wa chuma. Nilijipapasa haraka kiunoni mwangu katika kuitafuta silaha yangu.


Ilikuwepo.


Moyo ukachanua kwa tabasamu la matumaini. Niliichomoa na kulilenga lile kufuli kisha nikaachia risasi moja ambayo ililichangua lile kufuli na kulidondosha chini nilivuta kipete kizito na kuufungua. Huku nyuma moto ulizidi kunikaribia zaidi huku ukizidi kufanya uharibifu mkubwa zaidi. Sijui hata walitumia silaha gani yenye hatari namna hii au huwenda humu ndani hasa huku chini ya hili jengo kulikuwa na mfumo wa gesi au mitungi ya gesi. Yote hayo nilikuwa nikiyafikiria maana huu moto haukuwa wa kawaida. Hata hivyo sikutaka kuamini kama kulikuwa na gesi au mfumo wowote wa gesi kwani AKM asingesita kunifahamisha hilo. Hisia zangu zilibaki kuniambia huwenda walitumia silaha yenye mlipuko mkubwa waliohakikisha unaondoka na uhai wangu.




"Wapumbavu sana hawa!" Niliwatusi zaidi kisha nikauvutia kwangu ule mlango katika namna ya kuufungua, ukafunguka nikatoka na kuurudisha kisha nikafunga kwa kipete kingine kilichopo upande ule wa pili wa mlango. Nilitafakari ukubwa na madhara ya ule moto, nilijua hapo sikufanya kitu. Hata hivyo sikuzubaa nilianza kutafuta uelekeo wa kwenda kushoto, kulikuwa na ukuta, kuumeni ndiyo kulikuwa na ngazi. Nikazifuata bila kukawia. Baada ya hatua kumi za mbio, huku nyuma ule mlango ulifumuliwa na kupigizwa kwenye ukuta wa kingo za ule ujia. Ilinishtua vibaya mno na ulikuwa karibu kunifikia. Nikaongeza kasi ya mbio zangu huku pumzi zikianza kunisaliti.




Mbele niliona mwanga hata hivyo bado moto ulizidi kunifuata kwa kasi ileile. Nikajivuta kwa nguvu zangu za ziada na kufanikiwa kutoka nje kwa kujirusha mara baada ya kukuta uwazi wa kuniwezesha kupita bila shida. Nilipotoka akili yangu ikafanya kazi ya ziada ya kutafuta namna ya kuuchelewesha ule moto kuonekana kwani kama ungeonekana kwa haraka ni wazi wangejua kuwa hapa palikuwa na njia hivyo wangefika hapa kabla hata sijafika mbali. Kulikuwa na mfuniko mzito wa chuma ambao ulikuwa umesimama kuonesha kuwa ulikuwa wazi muda wote hivyo niliusukuma kwa nguvu na kujifunga pale nikachomoa bisibisi nene fupi nikaivuta kutokea kwenye mpini wake na kubaki yenyewe kisha nikaichomeka kwenye kipete cha mfuniko ule hivyo kuufanya usifunguke kwa urahisi. Nitazama huku na huko kwa wakati huo mwili wangu ukianza kupata nguvu nyingine. Upande wa magharibi mwa hiyo nyumba kulikuwa na kibanda kama cha ulinzi. Nilikifuata kwa kasi nikiwa nimeinama kutokea kiunoni huku bastola yangu Baretta 8000 ikiwa mkononi madhubuti. Kibandani pale palikuwa kimya, utulivu ule uliniwezesha kutafakari kwa haraka na kujishauri nitazame upande wa mbele wa nyumba hii. Niliona vijana kama watatu wakiwa wamekamata bunduki aina ya AK 47 wakielekeza kwenye mlango wa ile nyumba. Walijua bado nipo ndani na walikuwa na uhakika kuwa nisingechomoka pasipo kuingia mikononi mwao. Niliwatukana moyoni tusi baya kisha nikautazama upande huo wa magharibi. Ambako ndiko niliigesha gari yangu na sikujua kwa nini nilipenda sana kuegesha gari eneo hilo.


Sasa nilijua kuwa huo ndiyo wakati pekee nilikuwa nikiihitaji gari yangu zaidi.




Nilichomoka tena mbio huku nikiwa nimeinama ila sikufika mbali baada ya kusikia kelele za kunitaka nisimame. Sikusubiri niingie mikononi kipumbavu. Nikageuza jicho la chonjo kutazama sauti ilipotokea, ulikuwa ni upande ule wa nyuma ya kibanda kile ambacho punde nilikuwa hapo. Nikastaajabu kwani sikuwa najua kama upande wa nyuma wa kile kibanda kulikuwa na watu. Walikuwa ni vijana wawili wakiwa wamekama bunduki aina ileile kama waliyokamata washirika wenzao waliyoko mbele ya nyumba hii iliyozingirwa. Bahati ilikuwa kwangu kwani nilipokuwa nikitafuta namna ya kufanya. Sauti ya mlipuko ikasikika huku kile chuma ambacho nilikuwa nimekifunga pale kwenye ile njia niliyotokea kikirushwa juu na kupiga juu ya kile kibanda na kuwafanya wahahe kwa hofu waliyoitengeneza wenyewe. Niliitumia nafasi hiyo kuweza kuwachabanga kwa risasi kutoka kwenye bastola yangu yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Mmoja nilimchapa risasi kwenye paji la uso na mwingine risasi ya kisogoni mara tu alipogeuka kutazama moto ulipotokea.




"Kule kuna njia ya siri...kuna njia ya siri ona...ona yule kule anatoroka!" Niliisikia sauti ikipayuka, akili yangu ikakaa sawa na kunifanya nitambue kuwa pale hapakuwa salama tena kwangu. Nilikimbia kwa hatua chache kabla sijalifikia Peugeot 404. Nikaliwasha na kuliondoa kwa kasi huku risasi za hao mabwana zikiacha matundu kwenye gari yangu sehemu tofauti tofauti.


Sikujali.


Niliizungusha kama nipigaye misele kisha nikalitoa kwenye barabara.


Mungu wangu!




Nilikosea. Mbele yangu kulikuwa na Land Rover ya kizamani juu yake upande wa nyuma kukiwa na watu wane wakiwa wameshikilia bunduki aina ilele. Nikatazama upande wa kushoto tena kulikuwa na gari kama hiyo zote zilikuwa na sura mbaya. Nilikotoka niliona watu kama wane wakiwa na vunduki zenye mitutu mirefu. Kulia kulikuwa kutupu. Nikalizunguusha gari langu na kukanyaga mafuta.


Kosa.






Nikatazama upande wa kushoto tena kulikuwa na gari kama hiyo zote zilikuwa na sura mbaya. Nilikotoka niliona watu kama wane wakiwa na vunduki zenye mitutu mirefu. Kulia kulikuwa kutupu. Nikalizunguusha gari langu na kukanyaga mafuta.


Kosa.




SONGA NAYO SASA...




Risasi zisizo na idadi ziliniandama kwa fujo zikiwa na lengo la kunitahadharisha kuwa ujinga wowote wa kutaka kuwatoka utayagharimu maisha yangu, nikasimama ghafla na kulala kwenye kiti huku nikiupiga mlango kwa teke mlango ukafunguka nikatoka na kudondokea nje upande ule ambao ulikuwa shwari.


"Acha kuleta ujanja binti mrembo...usilete ujanja kabisa. Ulipo ni mahala pabaya...mahala pabaya mno. Jisalimishe!" Sauti iliongea kwa majigambo. Nilitulia kimya kama si mimi niliyekuwa nikionywa. Akili iligoma kufanya kazi kwa haraka na sikujua nifanye nini kwa wakati ule. Kimya cha muda kikatanda kisha risasi kurindima tena. Gari yangu ilikuwa si gari tena. Ilijaa matundu ya risasi ile mbaya na gurudumu zake kutobolewa, zikatokwa na uhai.


Nilipatwa.


"Bado unakaidi niruhusu risasi zaidi?" Sauti ile yenye mamlaka ilizungumza tena. Nikalitazama gari nikaona jinsi lilivyokuwa limetobolewa kwa risasi kiasi cha kuwa wazi kila upande. Mlango wa upande wa kushoto uling'olewa na kutupwa chini, kioo cha mbele hakikujulikana kilipo kabisa mlango wa upande nilipo mimi ambapo nilikuwa nimechutama, niliudondosha mimi kwa kuusukuma kwa guu langu wakati wa kujiokoa na shambulio lile na vioo vyote vilikuwa vimechanguliwa vibaya sana. Lilikuwa ni skelepa kamili.


"Naona uko kimya wacha tumalizane na wewe kwa risasi za mwisho." Ilisema tena ile sauti kwa mamlaka makubwa.




Wamalizane na mimi....wamalizane na mimi kwa risasi za mwisho...? Hapana wata...wataniuwa hawa, lazima nitumie mbinu...ndiyo, lazima nitumie mbinu za mwisho za kijeshi....!


"Moja...wacha tukuhesabilie hadi tatu mrembo kisha hatuna msalie mtume...mbili....je, bado unakaidi..? Ta...!"


Sikutaka kuwaruhusu washambulie tena, wangenimaliza. Nilinyanyua mikono yangu juu huku mkono mmoja ukiwa umekamata bastola na nikigeuka taratibu kuwatazama.


Loh!


Walikuwa wengi na nisingefanya kitu kwa haraka. Macho yangu yakatazamana na silaha zilizopo. Nilikubaliana na wazo langu kuwa nisingefanikiwa kwa kupambana zaidi ya kutumia mbinu ya mwisho ya kijeshi japo ni hatari sana kutumia mbinu hii ya kujisalimisha kwa maadui.


Wataniauwa..? Hili la kuniuwa sikuliafiki kwani wasingeniuwa bila kujua kwanini niko hapa nchini lazima watake kujua hilo na ili wajue ni lazima waondoke na mimi kwa ajili ya mahojiano zaidi. Huko ndiko nitajua namna ya kufanya zaidi.


Nilikamatika.


"Hatuendi hivyo mrembo...hatuendi hivyo kabisa. Tupa chini hiyo silaha yako..!" Sauti ile yenye mamlaka iliniamrisha, sikuwa na namna zaidi ya kufanya hivyo. Niliitupa chini bastola yangu kisha nikamuona aliyekuwa akitoa amri hiyo akiagiza mtu kuja kuichukua ile silaha na kutoa amri nyingine ya wawili kunisogelea nikajua nini kinafuata.


Kudhibitiwa.




Yule mmoja aliokota ile silaha huku akinitazama kwa macho ya kutoamini kama ni mimi ndiye niliye zungukwa na kundi kubwa la wao wenyewe. Nilikuwa mrembo niliyetafsirika vingine kabisa mbali na kutwaa silaha mikononi mwangu na kuwa tishio. Wale wawili waliivuta mikono yangu nyuma na kuifungia kwa nyuma pamoja kwa kamba za malighafi ya plastiki, waliikaza kiasi nikahisi maumivu yakianza kuninyemelea hata damu kushindwa kutembea vizuri kwenye mishipa yangu. Nilimtazama yule mtoa amri nikamuona kwa jinsi alivyokuwa akinitazama kwa dharau kubwa huku akikenua tabasamu. Nilijitikisa kwa kuwashtukiza waliyokuwa wakinifunga na kuwafanya watetereke. Nilipigwa ngumi mbili za mbavu kabla sijajipinda kuyafuata maumivu, nilipigwa kwa buti nyuma ya magoti yangu na kukita magoti chini bila kupenda.


"Tulia mwanamke, mbona bado halafu unataka kuharakisha. Mume yupo kwa ajili yako sawa mrembo?" Sauti ya mmoja aliyekuwa akininong'oneza sikioni ilikita kwa chuki ndani ya ngoma za masikio yangu. Nikageuza macho kumtazama. Alikuwa anatabasamu japo tabasamu lake sikulipenda kwa kuwa jino moja la mbele halikuwepo, nilijikuta nikikereka na kuzidisha hasira kwa maneno yake, nilipogeuka kwa huyu mwengine, yeye alikuwa akihangaika na kumalizia kunifunga. Walinisimamisha kwa nguvu mmoja akiwa huku na mwingine huku. Nilimtazama tena yule wa mbele ambaye ndiye kiongozi. Macho yetu yakakutana. Akatoa meno yake ambayo sikutaka kuyazungumzia sana maana hata yangekuwa masafi kiasi gani bado yangenikera. Sikuwapenda wanaume wapumbavu kama yeye hata kidogo asiyejua nini anapaswa kufanya kwa ajili ya maisha yake hata hivyo sikuacha kumtazama kwa chuki. Nikamuona akigeuza macho yake taratibu akinionesha upande ambao nyumba ile niliyokuwepo punde ilivyokuwa ikiteketea kwa moto baada ya mlipuko mwingine wa nguvu kukita eneo lile, hii ilimaanisha kuwa kulikuwa na bomu jingine lilitegwa mule ndani kuhakikisha wanasambaratisha kila kitu na mimi kuangamia kama ningekuwemo. Niliitazama nyumba ile kwa uchungu mkubwa sana. Ule mlipuko wa kule chini ya ardhi ulikuwa mkubwa kupitiliza kwa kuwa bomu lile lilipolipuka lilikutana na silaha nyingine ambazo zilihifadhiwa kule chini zenye kusababisha milipuko. Akili yangu sasa ilipata kufahamu hilo.


Shiit! Nilikuwa naelekea kufa kama nisingekuwa makini hasa. Niliwaza. Yule kiongozi akatoa ishara kwa watu wake kuwa niingizwe garini kisha nikamuona akipokea simu aliyopewa na kijana mmoja. Aliongea maneno ambayo mimi sikuweza kuyasikia kwa kuwa nilikuwa nikisukwasukwa na wale watu wakiniingiza garini huku mitutu ya bunduki ikiendelea kunitazama.


Nilipatikana hasa.




_________




Punde gari ziliondolewa kwa kasi kubwa sana kiasi kwamba wingu zito la vumbi lilinyanyuka na kuifanya ile sehemu kuwa kama uwanja wa mashindano ya magari. Sikuweza kuona nje kwani kila upande nilikuwa nimezingirwa na mtu huku kasiba za bastola zao zikiwa kwenye mbavu zangu. Mwendo ulizidi kuwa wa kutisha tukipita barabara hii na ile, ukimya ndani ya gari ulikuwa ni mkubwa mno sauti iliyokuwa ikisikika ni injini ya gari pekee na mbwembwe za dereva katika kutoa na kuingiza gia. Wakati ukimya ukiwa mkubwa hivyo, akili yangu haikuacha kutazama namna ambavyo ningeweza kujiokoa na wale watu ambao hadi muda huo sikujua ni wapi wananipeleka.


"Mnanipeleka wapi?" Niliwauliza kwa lengo la kuona watajibu nini na watafanya nini. Nilikuwa nikipima uwezekano wa kuweza kuwatoroka.


"Tulia mwanamke, tulia...ni hapahapa mjini si mbali na utapokelewa vizuri." Alijibu kwa utulivu yule mtu ambaye alikuwa ndiye kiongozi, sauti yake ilitokea nyuma ya gari ile. Sikuwa nimewekwa kwenye gari ya wazi, ilikuwa ni Noah ya rangi nyeusi huku vioo vyake vikiwa vyeusi pia. Niliyazungusha macho yangu kila upande baada ya jibu lile hapo ndipo nilipopata idadi kamili ya watu waliomo ndani ya gari. Nikimtoa dereva, gari nzima ilikuwa na watu wane. Wawili ubavuni mwangu na mmoja nyuma ambaye ni mwenye mamlaka na mwingine mbele ambaye alikaa akinigeukia mimi huku akiwa amekamatia mtutu wa bunduki. Sikuona sababu ya kusombwa msobemsobe kama jambazi sugu namna ile. Watu wane wasingeweza kunifikisha popote na ingekuwa ni aibu kama ningeshindwa kuwaacha solemba barabarani. Nilijitahidi na nikafanikiwa kutazama mbele kupitia kioo cha upande wa pembeni. (Side mirror). Nikaona gari zile zenye sura ya kutisha zikiwa zinaongozana katika hatua za kutokuachana sana na gari niliyopo mimi.




Wanaweza....wanaweza kuniua kweli...? Hapana, huwenda kuna mtu amewatuma kuja kunikamata na kama wameamua kunibeba ni wazi walitakiwa kunifikisha nikiwa hai hata hivyo ni lazima wangetaka kujua tuko wangapi kwenye sekeseke hili lililoanza kuwatoa jasho. Niliwaza huku nikiona namna ambavyo nitawaacha.


Hata hivyo inawezekana wakawa wamepewea amri mbili mosi ikiwa ni kuniangamiza kama ningeleta ujuaji na ya pili ikiwa ni kunifikisha nikiwa hai kama ningekuwa mpole. Niliendea kuwaza nikijionya mwenyewe. Ile kauli ya mtu mwenye mamlaka nyuma yangu ilinifanya nichanganue zaidi na kuona ni jinsi gani huyo aliyewatuma atakavyofurahi baada ya kuuona uwepo wangu mbele yake


Ujinga.


Niende ili nikaijue ngome ya maadui au niwaache solemba? Nilijiuliza kwa kadiri niwezavyo. Nilimtazama mtu mwenye mamlaka nyuma yangu kupitia kioo kilichopo kwenye paa la gari juu ya kichwa cha dereva. Nilimuona akiwa anabofya namba fulani kwenye simu yake. Nikawatazama kwa macho ya pembeni hawa wawili waliyoniwekea silaha huku na huku, hawakuwa makini japo silaha zao zilikuwa macho kwenye mbavu zangu. Huyu wa mbele alikuwa makini hata hivyo nilitathmini namna atakavyo hamanika nitakapofanya shtukizi la ghafula. Nikahamisha macho yangu pale kwenye kioo cha juu ya dereva nikamuona jamaa akiweka simu sikioni.


Hapa hapa. Nikawaza huku nikitazama kwenye kioo cha pembeni zile gari tatu zilikuwa zikiendelea kufuata huku nyuma wale watu waliyokuwa wamenizingira kwa silaha kule kwenye ile nyumba, walikuwa wameficha silaha zao chini ya bodi bila shaka wasiweze kuwashangaza watu mjini hapo. Mara mwendo ukapungua na kuwa wa kusuasua. Nilipotazama kwenye kioo cha mbele nikaona foleni kubwa ya kutisha nikajua kuwa tupo kwenye mataa kwenye makutano ya barabara ya Haika na ile ya Mtoni. Nikayarudisha macho yangu tena kwenye kioo cha pembeni, kisha cha juu ya dereva na kwa macho ya kuibia nikiwatazama hawa waliokaa ubavuni mwangu. Nyuma gari zilikuwa nyingi pia kulikuwa na msongamano wa nyumba nyingi kwenye mtaa wa hilo eneo. Nikatathmini namna nitakavyoweza kujichanganya kwenye hizo nyumba na kuwapotea pia sikuacha kutathmini namna nilivyofungwa mikono yangu nikajua kuwa nilikuwa na uwezo wa kuipindua mikono yangu na kuiweka mbele. Hii ni michezo niliyokuwa nikiipenda tangu nikiwa mdogo.


Nilijigeuza pale kwenye kiti na kumlalia huyu wa kuumeni kwangu nikakunjua miguu yangu yote miwili baada ya kuikunja na kuniwezesha kuzunguuka kwa makalio pale kwenye siti. Lilikuwa ni tukio la ghafla sana sililotegemewa nao.




"Hallo! Ndiyo tupo kwenye fo...!" Aliishia kuongea maneno hayo yule kiongozi nyuma yangu na kuastaajabu nilivyokuwa nikifanya mchezo ule wa hatari na haraka huku nikiwa kwenye kasi asiyoitaraji. Nguvu zangu za miguu zilimtupa huyu kijana wa kuumeni kwangu nje baada ya mlango kufunguka kwa kishindo. Nilijipindua kwa sarakasi ya mbele huku nikimsukuma na huyu nileyekuwa nimemlalia na kumbabatiza na mlango wa upande wa kushoto. Risasi kadhaa zikarindima, nilipotazama vizuri nikagundua mpigaji alikuwa kahamanika kwani hakuwa na shabaha tambulifu. Nilipofika chini nilimrukia yule niliyekuwa nimemsukuma kwa guu langu na kumtandika kichwa cha mdomo akapiga kelele hovyo nikajizungusha kwa haraka huku nikikwepa shabaha za waliokwenye gari, nikamtandika teke baya sana la shingo na kuangukia pembeni. Nilijiviringita hadi kwenye uvungu wa gari kubwa la mizigo nikiepuka wale wengine wasije kutoka garini na kunikuta nikiwa palepale, nikajipindua kwa kujikunja hadi mikono yangu ilipohamia mbele nikiwa pale chini ya uvungu wa gari hilo kubwa la mizigo.




"Msipige risasi hovyo ni hatari, mtafuteni kimyakimya na mumshuti yeye tu. Bora afe!" Niliisikia sauti ikifoka. Nilishatokea upande mwengine ambako kulikuwa na pikipiki ikiwa nayo imesimama mwenye pikipiki akiwa anajiandaa kuondoka baada ya taa ya utayari kuwaka. Nilibandika zile kamba zilizonifunga mikononi kwenye bomba la kutolea moshi la ile pikipiki ambalo lilikuwa likifuka kwa joto kali sikujali kuungua na mimi mwenyewe nilochojali ni kuiweka mikono yangu huru. Kamba zile hazikuyeyuka lakini zililainika hivyo kunirahisishia kuzivuta na kuzitakata huku nikisikia sasa mhemko wa hasira kutoka kwa kiongozi wa lile kundi. Nilimama na kumtandika yule jamaa mwenye ile pikipiki teke moja matata la kuzunguka akatupwa mbali nikiwa na lengo la kuipora pikipiki yake na kutokomea mbali na hatari hiyo hata hivyo sikufanikiwa kuipanda ile pikipiki kwani nilikoswa na risasi kama tatu ambazo zilichangua vioo vya magari yaliyopo mbele yangu. Nikajipenyeza kwenye uwazi wa gari na gari nikaanza kutimua mbio nikiwa nimeinama. Nilipoona nimefika mbali nilisimama na kuruka mtaro mmoja pembeni ya barabara na kupotelea kwenye majengo mengi marefu na mafupi. Bado nilikuwa na begi langu mgongoni ambalo lilikuwa na silaha. Wale wapuuzi hakuwa wamenivua. Nilikimbia bila kusimama na nilipoona bado hawakati tamaa nilizidisha mbio na kuwapoteza kwenye kona hii na ile hadi nikaja kutokea kwenye nyumba nyingi za hali ya kawaida ambazo zilikuwa zimesongamana kiasi kwamba kulijaa vichochoro vingi. Hapa nilipunguza mwendo na kutembea kabisa kwa mwendo wa kawaida. Nikaitoa simu yangu na kutafuta namba ya Jamali Maigwa yule kijana tuliyekutana kwenye gari la abiria nilipokuwa nikienda kijiji cha Asumile. Nilipoipata niliipiga na kuweka simu sikioni, haikuita sana na mpokeaji akapokea.




"Ndiyo ni mimi....ni mimi umesema uko wapi hapa mjini maana leo nina hamu sana ya kukuona...!" Nilimwambia nikiwa najitahidi kuiweka sauti yangu kwenye utulivu.


"Kama uko hapa mjini ni karibu siko mbali sana...wewe uko wapi kwani?" Aliniuliza Jamali Maigwa.


"Nipe tu maelekezo siwezi kupotea....! Siwezi kupotea bwana mimi si mgeni wa hivyo". Nilimjibu huku nikiwa naangalia huku na huko kuona kama kulikuwa na mtu anayenifuatilia.


"Ukiwa...ukishafika kwenye makutano ya barabara ya Haika na Mtoni fuata barabara ya mtoni...mbele kidogo utakuta yadi kubwa ya magari inayomilikiwa na wahindi, ukifika hapo nipigie," aliniambia. Nikakata simu kisha nikatazama mahali nilipo maana hata akili yangu ilikuwa imeshapoteza utaratibu wake wa ufanyaji kazi sikuwa na ramani yoyote, nilitumia akili ya ziada. Nilikuwa nikiufuta uelekeo huo huo wa barabara ya Mtoni hivyo nilitazama usalama wangu nilipoona utulivu nikaanza tena kukimbia nikifuata zile chochoro za katikati ya nyumba na nyumba. Mbele kidogo nilipokuwa nikitaka kuvuka barabara ndogo ya vumbi, nikasikia sauti ya muungurumo wa gari na nilijua ni gari ya aina gani. Nikajibana kwenye ukuta wa makuti wa nyumba moja kisha nikawa nachungulia kutazama mahali muungurumo huo unapotokea. Ni ile gari miongoni mwa zile zenye sura za kutisha nikajibana zaidi baada ya kuona watu waliyoko kwenye bodi wakiwa wamezikamata imara silaha zao. Nilishangaa sana kuona watu wasio askari kuzionesha silaha mitaani bila hofu.










Nikajibana kwenye ukuta wa makuti wa nyumba moja kisha nikawa nachungulia kutazama mahali muungurumo huo unapotokea. Ni ile gari miongoni mwa zile zenye sura za kutisha nikajibana zaidi baada ya kuona watu waliyoko kwenye bodi wakiwa wamezikamata imara silaha zao.




SONGA NAYO SASA...




Nilishangaa sana kuona watu wasio askari kuzionesha silaha mitaani bila hofu. Nikiwa hapo nikawaona watu wengine wakiwa wanatokea mahali nilipokuwa naelekea. Walivaa suti nyeusi na walikuwa wako watatu bastola zao zikiwa mikononi.


"Shiit!" Niling'aka kisha nikaachana na njia ile niliyokuwa nataka kuifuata na kuchukua chochoro jingine. Nilizidi kusonga mbele huku umakini ukiwa mkubwa zaidi. Sasa mbele yangu niliiona hiyo yadi ya magari na nilitakiwa kuvuka barabara ndipo niwe upande ule. Niliitia simu yangu mfukoni na kutazama usalama wa eneo lile kwa kulitazama kwa namna ya kulipeleleza nilipoona kimya nikavuka baada ya kuruhusu magari mawili yapite. Nilipokuwa upande ule na kujiandaa kupiga simu, nikaguswa mgongoni. Moyo ukapiga konde. Mapigo yakibadilika namna ya upigaji baada ya kusimama kwa muda. Woga ukanivaa.




"Kumbe haukua mbali sana mrembo wangu..?" Nilipumua kwa nguvu sana nilipogundua kuwa alikuwa ni Jamali Maigwa.


"Nimechoka sana sikujua kama unakaa mbali hivi unajua nilikuwa matembezi sasa aagh!...nahitaji hata kuoga kwanza maana mwili umemwaga sana jasho," nilimwambia huku akili yangu ikiwa haiko kwenye utulivu japo nilifanikiwa kuyadhibiti macho yasiangaze huku na huko na kubaki nikimtazama kwa hitaji hasa la kuupoza hata mwili kwanza.


"Sawa twende si mbali sana na hapa," aliniambia huku akinishika mkono. Nilikuwa mpole maana nilikuwa nikihitaji kujificha kwa muda kabla sijaanza tena mbio zangu za kumtafuta Amsuni Bhehe. Haukuwa mwendo mrefu mara tukafika kwenye nyumba moja tulivu ambayo ilikuwa na vyumba kama vitatu hivi kwa makadirio. Akausukuma mlango tukaingia ndani. Niliingia kwa woga kidogo huku nikisita.


"Ingia usiogope kuwa huru!" Aliniambia. Nikamtazama usoni kwa muda kisha nikamuuliza.


"Huna mke kwani Jamali?"


"Ha...hapana, mke bado mrembo labda niwe mbioni sasa kumtafuta." Alinijibu huku akinitazama kwa tabasamu la kuomba jambo. Alikuwa akinichombeza. Nilimpenda huyu kaka kwa maongezi yake, alikuwa muongeaji sana na sijui kwanini nilivutiwa na tabia hiyo. Tuliingia moja kwa moja chumbani kwake huku nikiwa sijaitazama vizuri hata sebule yake. Chumba chake kilikuwa sawa na vijana wengine wa kawaida wa kileo. Kulikuwa na kitanda cha chuma cha kisasa cha futi tano kwa sita, godoro kubwa lilipanda juu huku likiwa limetandikwa safi kwa shuka la manjano lenye urembo katikati sambamba na mito yenye foronya laini zenye kuendana na rangi ya shuka. Kulikuwa na meza kubwa ya kioo katikati ambayo haikuwa imetandikwa kitu chochote kulikuwa na pakiti ya sigara ya Embassy na kiberiti cha kuni, simu iliyoonekana kuchoka ambayo ilitolewa betri yake ilikuwa imetelekezwa juu ya meza ile. Akaitupia simu yake ya kisasa hapo hapo mezani na kunikaribisha. Akili yangu bado ilikuwa kwa wale watu waliokuwa wakinifukuza kama jambzi sugu japo macho yangu yalikuwa yakikichunguza kile chumba kwa kificho. Hakikuwa na vitu vingi sana. Akawasha feni ili liweze kupunguza angalau joto la mule ndani. Nilikuwa bado nimesimama huku nikitazama jazanda yangu kupitia kioo cha kabati la kunguo lililokuwa kwenye ukuta unaotazamana na mimi upande wa magharibi mwa chumba kile.


"Karibu sana Jamila sijui ungependa kutumia kinywaji gani?" Akanikaribisha. Akili yangu ikarudi mule chumbani na kutazama kama kulikuwa na friji. Halikuwepo. Nikatabasamu baada ya kujua kuwa taarifa zangu kwa jamali zote zilikuwa za uongo, kuanzia jina hadi utambulisho mwengine kwake, sikuwa na namna.




"Nahitaji kuoga kwanza Jamali mwili unafukuta joto sana." Nilimwambia huku nikimpa tabasamu lililomfanya ajione mwenye bahati sana kuwa na msichana mrembo kama mimi ndani ya chumba chake. Ilikuwa ni bahati ya mtende kuota kwenye misitu ya mvua nyingi. Alisimama na kutoka bila kuniambia chocho nami nikapata wasaa wa kukitazama chumba chake vizuri huku nikikaa kwenye kochi moja lenye uwezo wa kubeba watu wawili angalau hapo feni likaniliwaza kwa kunipa hewa mwanana huku kidogo nikijipa amani ya kuwa hai, kulikuwa na seti moja ya makochi humo ndani. Niliwakumbuka wale watu waliokuwa wakinifukuza ambao walikuwa wakiongozwa na yule mtu ambaye bado tabasamu lake lilikuwa likiendelea kuzisumbua kumbukumbu zangu. Sikulipenda lile tabasamu kwa kuwa lilijaa dharau kuliko kawaida. Nilipokuwa nikikumbuka hilo mara picha ya wale watu watatu wenye suti niliyowaona pale uchochoroni ikanijia tena.


Wale walikuwa ni akina nani...? Walikuwa watatu na miongoni mwao alikuwapo mwanamke...yaa ndiyo, alikuwapo wa kike...! Walivaa suti na ikiwa waliokuwa wakinifukuza walivaa kila mmoja na jezi yake vile alivyopenda.


Inamaana wao pia wamo kwenye mpango unaohusiana na wale...? Kama sivyo ni nini sasa hadi wakawa pale...? Kama wanahusiana je, kwanini sikuwaona tangu kule msituni.


Si hatari hii sasa! Mbona nachanganyikiwa...? Niliwaza.


Akili yangu ilisumbuka sana kuhusiana na watu wale kwa kweli na bado ilitaka kuwajua ni akina nani hata hivyo nilikuwa ni kama ninayejifariji tu maana nisingeweza kuwajua kamwe nikiwa hapo naendelea kuwaza bila kufanya jitihada zozote za kukaa.


"Choo changu ni cha nje Jamila hivyo nifuate nikakuonyeshe." Jamali alinirudisha tena mule ndani baada ya akili yangu kutoka masafa ya mbali kabisa ikitoka kuyazuru mauzauza ya kufukuzwa kama mwizi au Mbwa aliyepatwa na kichaa.


"Hakuna...hakuna shida." Nilimjibu huku nikifuatana naye. Alinionesha choo na bafu vilipo kisha akaondoka. Niliingia kwanza chooni kwenda kuweka mambo sawa maana shughuli ile ya kukimbizwa na kuokoka kwenye mdomo wa mamba, ililichafua tumbo langu. Nilipotoka nikiwa mwepesi ndipo nikaingia bafuni ambako nilipoteza dakika nane kwa kujimwagia maji kwa kiwango cha kutosha kwani Jamali aliniwekea maji mengi tu. Nilipotoka nilikuwa mwepesi huku akili yangu ikiwa inafanya kazi vizuri, moja kwa moja nilirudi ndani. Nilipoingia nilikwenda kukaa palepale kochini.




"Pole kwa uchovu..je, utatumia nini sasa?" Hatimaye Jamali aliniuliza. Nilimtazama huku nikionesha tabasamu.


"Chochote chenye kuondosha kiu?"


"Unatumia kilevi?"


"Hapana, sitahitaji kutumia kwa sasa."


"Ooh! Ingefaa sana kuweka mwili wako sawa Jamila na angalau kukuondolea uchovu."


"Unadhani ni dawa ya huu uchovu nilionao?" Nilimuuliza huku nikimtazama kwa utulivu mkubwa, nilimuona jinsi alivyokuwa akinitazama kwa uchu wa kunitafuna kama Fisi atafunavyo mifupa.


"Haswaa!" Alinijibu kwa hamasa.


"Sawa." Nilimjibu na ni kama aliyekuwa akilisubiria jibu langu kwa hamu kubwa kwani muda huo huo alinyanyuka na kuelekea sebuleni aliporudi alikuwa amekamatia chupa nne za pombe akazitua juu ya meza ya kioo akafungua na kunikaribisha pasipo kutumia bilauri.


"Asante sana." Nilimshukuru huku nikiinyanyua ile chupa na kupiga tarumbeta refu na kuitua chini. Alinitazama kama aliyekuwa akizungumza na moyo wake katika namna ya kuniteta labda nilikuwa na kiu sana, sikujali kama ni kweli ana niteta ni juu yake. Nilitabasamu tabasamu baya sana katika kutongoza hisia mbaya kwa mwanaume yeyote yule rijali, naye nikamuona akitabasamu kisha akanyanyua chupa na kuigandisha hewani nikajua anataka nini, nami nikanyanyua ya kwangu na kuzigongesha kuleta urafiki wetu ama cheers. Tulikunywa huku kila mmoja akimtazama mwenzake kwa mtindo wa kuibia hadi chupa zile zilipokata. Nikamzuia asiende kuleta nyingine kwani sikutaka kulewa sana kwa kuwa akili yangu haikuwa na utulivu kabisa hasa nikikumbuka kuwa bado natafutwa. Tulikuwa tumesogeleana sana kiasi pumzi zetu zikawa zimezalisha joto lenye kutufanya tuzidi kukabiriana zaidi. Jamali nilianza kumuona ni kijana wa pekee sana kwani kwa wakati huo ambao nilikuwa nikitafutwa huko nje, ni yeye pekee ambaye ameweza kunificha kuepuka karaha hiyo pasipo yeye mwenyewe kutambua. Sikutaka kumuonesha ukaidi wowote hata pale mikono yake ilipokuwa ikipita kwenye mwili wangu kwa mtindo wa kunipapasa. Macho yake malegevu yaliyozidiwa na hisia za kuhitaji jambo fulani mwilini mwangu yalizidi kuniinulia hisia za ajabu na kujikuta nikitoa ushirikiano kwa kila kitu alichokitaka. Ni muda mfupi akawa ameweza kunilegeza kabisa na kunilaza kwenye lile kochi na kunifanyia utundu mkubwa. Aliweza kuninyonya na kunilamba kifua changu chenye matiti mazuri ya mviringo yaliyobeba chuchu imara nyeusi. Yalikuwa ni matiti makubwa kiasi ambayo yalizidi kumpa wazimu wa kufanya kila anachokijua. Alikuwa akitoa sauti za kimahaba huku na mimi nikiwa katika hali mbaya zaidi. Macho yangu yalipoteza nguvu kabisa na nilikuwa nikihisi raha ya ajabu. Mikono yangu haikuwa nyuma kupapasa kila mahali mwilini mwake huku ulimi wake ukiwa unatalii kwenye kinywa changu nikiifurahia ladha ya ubaridi ya ulimi wake. Mikono yangu ikawa inaelekea kwenye mkanda wa suruali yake nikaufungua kisha nikaivuta kidogo na kutaka kuingiza mkono wangu kwenye nguo yake ya ndani. Mara hisia mbaya zikaniingia mwilini pale alipokuwa akiishusha suruali yangu ya jeans ambayo sikujua alinivua muda gani mkanda wa suruali yangu. Sasa alikuwa akiuachezesha mkono wake kwenye mapaja yangu malaini na makubwa meupe ambayo yalizidi kumpa uchu wa kunitafuna. Alipokuwa akipandisha mkono wake kuufikisha kwenye chupi yangu ya rangi ya pinki hapo ndipo jina la mmiliki halali wa mwili wangu liliponijia kichwani. Roi.




"Ha...hapana Jamali na...nahisi haja ndogo...niruhusu nikajisaidie...!" Nilimwambia huku mkono wake nikiwa nimeuzuia kwa mkono wangu.


"Ok, usijali...usijali Jamila mpenzi ne..nenda tu!" Alisema Jamali akiwa na hamu hasa na mimi lakini mimi hamu iliniisha ghafla na sikuwa nikihisi chochote kwa wakati huo. Jamali alisogea pembeni na kuniacha nikisimama. Niliweka sidiria yangu vizuri baada ya kuivuta atakavyo ili kuyapata matiti yangu vizuri kisha nikaiweka sawa fulana yangu nyeusi nikiwa tayari nimeipandisha suruali yangu juu. Nilipomtazama usoni nilimuona alivyokuwa akinitazama kiunoni kwa matamanio. Nilifunga zipu ya suruali yangu na kufunga mkanda kisha nikatoka nje kwa haraka mithili ya mtu aliyekuwa amebanwa sana na haja ndogo. Niliingia bafuni na si chooni kisha nikaigamia ukuta na kujilaumu juu ya kitendo nilichokuwa nikitaka kukifanya. Nilimhurumia Jamali na kuona jinsi nilivyomkatili kunifaidi. Alinificha kutoka kwenye mikono ya wale manyang'au hivyo kwa namna moja ama nyingine nilitakiwa nimtunukie zawadi ya penzi ili niendelee kukaa kwake kwa muda fulani bila kunitilia mashaka kwanini sasa sijafanya hivyo. Upande mwingine nilijiona nafanya kitu cha ajabu sana.


Mungu wangu nini kile...angeni...angenivua nguo kweli yule mwanaume. No, nampenda sana mpenzi wangu na siwezi kufanya hivi bila sababu za msingi.


Amenikosa.


Hata kama huwa nafanya ngono wakati mwingine kwenye hizi harakati zangu hata hivyo si kirahisi namna ile kama ambavyo Jamali alitaka kuufaidi mwili wangu. Hali hii huwa inatokea kikazi kwelikweli na inatokea pale ninapotaka kumtia mikononi adui hapo ndiyo huwa sina budi kumpa mwili wangu na kumlegeza. Hizi ni mbinu za kijasusi hasa kwa sisi majasusi wa kike na ni mbinu ambayo inatumia akili nyingi sana ili adui aje ajutie kuufaidi mwili wako bila malipo. Si kipumbavu na kizembe hivi kama kwa Jamali Maigwa. Never.


Nilikataa kabisa.




__________




Niliushika ukuta kwa takribani dakika moja nzima nikipanga mbinu mbadala ya kumkatalia Jamali kushiriki nami mapenzi. Nilipoipata nilijitoa pale ukutani na kwenda kwenye sinki la kunawia nikanawa mikono na uso wangu huku nikijitazama kwenye kioo kidogo kilichopo juu ya sinki hilo. Sura yangu ilikuwa imebadilika sana kutokana na matukio ya ajabu yalivyokuwa yamenizonga. Nilikuwa na michirizi ya michubuko kwa mbali ambayo ilianza kukauka. Nilinawa haraka kisha nikajifuta maji na kutoka nikiwa na mbinu mpya ya kukaa mbali naye. Nilipofika sebuleni, akili yangu ikanifinya. Nikasita kupiga hatua hata hivyo nilipuuza hali ile na kuzirusha hatua zangu hadi kwenye mlango wa kuingia chumbani. Niliusukuma mlango na kuingia ndani.


Tobaa!


Jamali Maigwa alikalishwa katikati ya chumba na kuwekewa bastola kichwani na inavyoonekana alikuwa akihojiwa maswali fulani. Sura yake ilikuwa kwenye hofu kubwa sana na alikuwa akinitazama kwa namna ya kunifukuza mule ndani ili kuwaepuka wale watu.


Hakujua masikini.


"Huwezi kutukimbia wewe mwanamke mpuuzi...huwezi, unajidanganya tu!" Sauti ya mamlaka iliniambia na nilipomtazama yule mtu aliyekuwa akitoa mamlaka niligundua alikuwa amenipa mgongo na alivaa mavazi ya kujiziba hadi uso wake. Akili yangu ikalipuka kama bomu lipu! Na kukumbuka mtu huyo ni wapi niliwahi kukutana naye. Sikupata tabu kukumbuka alikuwa ni yule niliyepambana naye kule porini na huyu ndiye yule niliyekuwa nikipambana naye kwenye giza la siku mbili, kwanza ikiwa ni nyumbani kwa jaji hayati Kiago Mathias na vilevile nyumbani kwa aliyekuwa mwendesha mashtaka wa serikali kipindi hicho marehemu Masuka Mvungi. Aligeuka na kunitazama. Mboni zake za macho nilizitazama vizuri na katika kumtazama huko ndipo nilipogundua kupitia macho yake kuwa alikuwa na chuki kubwa sana na mimi.


Kwanini? Nilijiuliza pasipo kuwa na majibu mazuri.


"Sasa hatuwezi kukuachia ni lazima ujibu maswali yetu machache kisha tukuuwe!" Alizidi kunitisha yule bwana anayejificha sura. Jamali Maigwa alinitazama kwa macho ya hofu na hakujua nini kilichokuwa kikiendelea baina yangu na watekaji wale.


"Muacheni huyo asiyekuwa na hatia basi...!"


"Hatuwezi kumuachia hivi hivi kwani hii inamhusu aliyekuwemo na asiyekuwemo huwa hatuna kawaida ya kumuamini mtu. Siju kwanini umemnyima uroda huyu jamaa na alibakiza hatua ndogo tu kukufaidi kahaba mrembo kama wewe." Aliongea yule mtu wa kujificha sura sikuwa nikimjua bado. Nilighadhibika kwa kuitwa kahaba na ghadhabu zangu zilizidi pale nilipogundua kuwa mchezo ule ulikuwa ukishuhudiwa nao.








Siju kwanini umemnyima uroda huyu jamaa na alibakiza hatua ndogo tu kukufaidi kahaba mrembo kama wewe." Aliongea yule mtu wa kujificha sura sikuwa nikimjua bado. Nilighadhibika kwa kuitwa kahaba na ghadhabu zangu zilizidi pale nilipogundua kuwa mchezo ule ulikuwa ukishuhudiwa nao.


Inawezekana walifika muda tu hapa?




KWA USALAMA WA KAZI HII HAPA NI UKOMO WAKE. ANAYETAKA KUIMALIZIA AFUATE MAELEKEZO MWISHO WA POST HII.


SONGA NAYO...




Nikajiuliza huku nikilitazama dirisha lililokuwa upande wangu wa mbele kisha nikamtazama yule mtu wa kujificha sura akanikonyeza kwa namna ya kunidhihaki.


"Ohoo! Hata hivyo wewe ni mwoga sana maana unaficha sura tangu awali nikufahamu na sijaijua sababu ya kufanya hivyo?" Nilimwambia huku nikijidhatiti nisioneshe ghadhabu zangu mbele yao.


"Haikuhusu hii hali...!"


"Muachieni huyo aende hana hatia...!" Nilifoka.


"Haiwezi kuwa hivyo kahaba...!"


"Mpuuzi utajuta kuniita mimi kahaba wewe, pengine kahaba anaweza kuwa mama yako...!"


"AAAAAGHRR...!" Baada ya mimi kuzungumza vile nilimshuhudia yule mtu akirusha teke na kumpiga Jamali mbavuni na kumpindua kisha yule aliyekuwa amemulekezea bastola akamfuata na kumrudisha pale juu kwenye kiti.


"Jibu tu ujinga halafu maumivu yahamie kwa mpenzi wako." Niliumia sana kwa kupigwa Jamali Maigwa kwani maumivu yale yaliyomkuta hakukuwa na mwingine wa kulaumiwa isipokuwa mimi. Nilighadhibika mno na nilimtazama kwa jicho baya yule mtu wa kujificha sura.


"Kwanini unatusumbua wewe...!" Aliniuliza yule mtu wa kujificha sura.


"Namtaka Amsuni Bhehe." Nilijibu huku nikiyatazama macho ya yule mtu wa kuziba sura. Niliziona nyama za pembeni ya macho yake zikijikunja nikajua wazo langu limefanikiwa kuwa kweli.


Huyu mpuuzi anamfahamu Amsuni Bhehe. Nilizidi kumtazama kwa kumdadisi japo nilikuwa nikiyatazama zaidi macho yake.


"Niliwaambia mimi huyu ni wa kumuua tu, ona...ona sasa anaongea nini si amechanganyikiwa huyu na nahisi kilichomchanganya ni mauaji aliyokuwa akiyafanya tangu mwanzo." Aliongea yule mtu wa kujificha sura. Hata hivyo niliigundua janja yake, alikuwa akijaribu kunipoteza maboya kwa kunihusisha na mauaji ambayo mimi sikuhusika nayo.


Yapi sasa?


Nikawatazama kwa umakini hasa yule aliyekuwa akimuelekezea silaha Jamali Maigwa kisha yeye. Nilipoona kuwa uwepo wao usinge nishinda kuwamudu, nikajiandaa kuwashambulia kwa shambulio la ghafla hata hivyo yule wa kijiziba sura alikuwa makini na hisia zangu na hatua za mwili wangu kwani kwa kasi ya ajabu alirusha teke jingine na kumpiga Jamali Maigwa kwenye upande wa sikio la kushoto, ukelele wa uchungu ulimtoka Jamali huku akitupwa mbali na kiti chake. Damu zilianza kumtoka masikioni na puani.


Nilimhurumia.




"Usijaribu kufanya jaribio lolote la kijinga wewe kahaba." Sauti ya yule wa kujiziba sura ilinionya tena baada ya kujiweka sawa.


"Ukimuona huyo Amsuni Bhehe unamjua?" Aliniuliza tena yule wa kuziba sura.


"Wewe ndiye utakayenipeleka kwa huyo Amsuni Bhehe." Niliwaambia hata hivyo niliwashuhudia wakicheka cheko kubwa sana wote wawili kisha, cheko la kebehi. Nilipandwa na hasira na kutaka kuwafuata nilishaanza kupiga hatua moja mbele.


"AAAAAGH...AAAH!" Ukelele ulimtoka tena Jamali Maigwa baada ya bastola ya yule kijana aliyekuwa amemuelekezea hapo awali kukohoa kidogo na risasi yake kulichangua goti lake la kulia. Nilijikuta mwili ukiiniisha nguvu ghafla na damu ikinichemka mwilini kisha nguvu zikarudi na wazo la kufanya kitu cha ajabu mbele yao kikiniingia mwilini kama mzuka. Nikakunja ngumi huku nikiuma kingo zangu za midomo ya juu. Hapo hapo mwili ulipoteza muhimili baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani. Macho yangu yakapoteza uangavu. Nilijitahidi kugeuka ili kumtazama mtu akiyeniadhibu kichwani. Nilikutana na tabasamu baya sana na mtu niliyekuwa nikimfananisha na yule aliyekuwa akitoa amri ya kufungwa kamba. Nilitaka kunyoosha mkono wangu kumuendea yeye kama ninayemuomba radhi hata hivyo mkono uliniwia mzito kiasi nikajikuta nikishindwa kutimiza lengo.


"....anamtaka Amsuni....Amsuni Bhehe...huyu...huyu ni mpuuuu...puuuzi..........!" Nilisikia kwa mbali maneno mengi mengi yakipita kichwani mwangu. Sasa macho yakawa yanagubikwa na giza zito huku kichwa changu kikiwa chepesi kama ubua. Mwili ukawa mzito miguu yangu ikashindwa kuuhimili. Nikajikuta kwenye giza zito sikujua kitu kingine.


Nilidondoka.




_________




"NIKO MBIONI KUMALIZANA NA HII OPERESHENI MKUU, NIMESHAJUA NINI KINAENDELEA NA HAPA NIKO NAMSUBIRI HUYU BINTI ARUDI TENA." Frank Matiale Bambi alikuwa akiongea huku simu yake ikiwa sikiono. Akatulia kidogo na kuongea tena.


".....wanahusiana, mwanzo walikuwa wakinichanganya sasa kule msituni ndiyo nimejua kuwa wako kwenye kundi moja mkuu. Kwa kushirikiana na huyu binti sasa huu mpango ni lazima tuumalize japo sijamjua huyu binti ni nani na kwani ameingia kwenye hii operesheni Safisha....!" Aliongea tena Frank kisha akatulia tena.


"Ndiyo, nataka kushirikiana naye...!" Alisema tena kisha akaendelea baada ya kutua kidogo.


".....hana madhara na pia kwa kufanya hivyo nitajua yeye ni nani na kwanini yuko ndani ya hii operesheni...!" Akatulia akiwa makini kusikiliza upande wa pili kisha;


"Najua mkuu kuwa ukiachilia mbali ofisi yetu ya ujasusi, pia kitengo maalumu cha usalama wa taifa kiko humu hata hivyo sina imani kama atakuwa ni huyu binti. Huyu binti ni jasusi hatari sana mkuu kwani mapambano yake kule msituni hayakuwa lelemama hata kidogo na pia sikujua alinipotea kwa namna gani. Sina imani na eti, ni mtu kutoka kitengo maalumu cha usalama wa taifa hapa nchini....ilaa...!" Alisema tena Frank Matiale Bambi kisha mtu wa upande wa pili wa simu akaonekana kuingilia katikati ya mazungumzo yake hivyo akatulia.


"....ndio, nilitaka kusema kuwa nina mashaka na uyasemayo mkuu...ninamashaka kabisa kwani kule porini niliona makundi mawili tofauti na huwenda hili kundi la pili liko na namna na hisia zangu zinakataa kuwa liko upande wa kuimaliza hii operesheni...!" Akatulia tena kisha akasema.


"Sawa nitakujuza kila hatua kutokea hapa.!" Alimaliza kuongea kisha akairudisha simu mfukoni.




Alipotoka kule Porini Frank wazo lake la kwanza lilikuwa ni kuhakikisha anaifuatilia ile gari Peugeot 404 ambalo ndilo aliloliacha Catherine mara tu alipofika eneo lile wakati yeye akiwa juu ya jengo lililokuwa likitazamana na jengo la marehemu Abdallah Juma Kimbo aliyewahi kuwa waziri wa nishati na madini. Hivyo aliamini fika kuwa ni lazima binti yule angerudi tena mahala pale. Alikuwa na dhamira kuu ya kuhakikisha anashirikiana na binti yule. Kitu ambacho hakukijua ni kwamba. Yalipofika majira ya saa tano usiku, kuna watu wengine watatu walifika kuweka kambi hilo eneo ila hawakuweza kuonana. Waliendelea kusubiri hapo kila mmoja kwa wakati wake na watu wale watatu alikuwapo Sembuyagi Mpauko Haufi, Marietha na Mabule ambao nao baada ya kushauriana waliamua kufika hapo kumsubiri Catherine arejee kulifuata gari lake. Waliendelea kuvumilia kadhia ya Mbu wenye hasira kali hadi yalipotimu majira ya saa tisa usiku.


"Unadhani atafika hapa huyo mwanamke?" Aliuliza Mabule akimtazana Sembuyagi.


"Ninauhakika lazima afike hapa kwani bado kwa shughuli zake atalihitaji sana hili gari." Alijibu Sembuyagi akiwa anatazama mahali gari lilipo huku akiwa hajui kuwa ukali wa macho yake ulikuwa sawa na Frank Matiale katika namna ya kulitazama gari hilo kwa kulichunguza kama linasogelewa na mtu ama lah! Kichwa cha Marietha kilikuwa kinawaza mambo yake na hadi hapo alijua fika anafanya kazi na adui anayetaka kumuua mtu mwenye haki ila alichokuwa akikifanya ni ile inayoitwa uvumilivu wa mwisho kabisa hadi kumkamata adui yake akiwa ni mwenye ubaya wake mikononi.


Wakaendelea kuwa wavumilivu wao sambamba na Frank pia huku wakiwa hawaonani. Ilipotimu saa tisa ndipo walipokiona kivuli cha mtu kikiwa kinapiga hatua kulisogelea lile gari. Haraka sana Frank akavaa miwani ambayo ilikuwa na uwezo wa kumuonesha gizani. Naam, aliyemuona alikuwa ni yule binti amtakaye. Wakati huo huo Sembuyagi naye akichukua darubini ya kuona gizani.


Hakika alikuwa ni yeye.




Walimuona mtu huyo akiangaza macho yake huku na huko hadi alipohakikisha kuwa hakuna alichokiona ndipo akaanza kulikagua gari kama alivyoliacha ndivyo alivyolikuta. Akaingia garini na kuliwasha akawasha taa kali na kuliondoa eneo hilo taratibu. Frank alijua fika binti huyo ni hatari hivyo aliweka umakini katika ufuatiliaji wake vivo hivyo Sembuyagi na wenzake. Alianza kutangulia Frank kisha wakafuata akina Sembuyagi. Umbaliwa waliyokuwa wameachana haikuwa rahisi kwa yeyote kugundua mbinu mbaya ya adui ya kuungiwa mkia si kwa Catherine, Frank wala Sembuyagi na wenzake. Walizidi kufuatilia hadi walipofika kwenye mji tulivu wa Ashura ambako ndiko nyumba ile aliyokabidhiwa Cathereine ilipokuwa. Frank alipitiliza akaenda mbele zaidi ya nyumba hiyo huku Sembuyagi na wenzake wakiingii kwenye njia nyingine upande wa mashariki mwa nyumba ile kisha wakaegesha gari yao hatua kadhaa kutoka nyumba hiyo ilipo. Frank alirudi kimya kimya akiwa tayari amefanikiwa kuitelekeza pikipiki yake. Hadi wakati huo hakukuwa na mtu hata mmoja aliyefanikiwa kugundua uwepo wa mwingine eneo hilo. Majira yalikuwa yametimu saa kumi na robo usiku. Wakati Mabule na Marietha wakiwa wamejibana mahali wakifuatilia mwenendo wa Catherine ndani kwa kutumia darubini yenye nguvu, Sembuyagi alikuwa amewaacha kwa usiri na kupiga simu mahali kisha kuanza kuongea na mtu wa upande wa pili akiwa kwenye wasiwasi mkubwa.




"Shiit! Mabule tazama hii...hii ni nini Mabule? Huyu jamaa ni hatari sana na hapa anatufanya sisi ni wapumbavu kwa kutuburuza akidhani hatuja mshtimukia!" Aliongea Marietha akiwa amepigwa na mshangao mkubwa. Mabule akatazana alichokuwa akioneshwa, ilikuwa ni simu ikionekana kupokea maongezi ambayo yalikuwa yakifanyika upande mwingine karibu na hapo. Wakaikaribia ile simu kwa kutega masikio yao kwa umakini mkubwa.


"Hakikisha umeandaa vijana wa kutosha ili huu uwe ni wakati wa mwisho wa huyu kahaba." Sauti ambayo ilijulikana kuwa ni ya Sembuyagi ilikuwa ikiongea.


"Vijana wako tayari cha kufanya ni kuhakikisha hao uliyokuwa nao unawadhibiti kabla hawajawa miiba mikali yenye sumu kwetu." Sauti iliyokuwa ikipewa taarifa ilijibu huku ikitoa maelekezo. Ilikuwa ni nzito sana.


"Hawa ni kama kuku ninaowafuga ndani kwangu hawana madhara nitawauwa muda wowote nikitaka. Huyu niliyetoka naye Tanzania nitamuua punde baada ya kumtia mikononi huyu jasusi kisha huyu mwanamke naye atakufa kwa wakati mwingine mzuri na tulivu zaidi." Alijibu Sembuyagi, sauti yake ilikuwa ikipenya vema kwenye masikio yao mane. Miili iliwachemka haswa huku wakipandwa na ghadhamu kali sana. Sasa walijua kuwa nini kilitakiwa kufuata dhidi ya mwenzao. Mabule alikuwa na hasira sana pia akijiona anafedheheka ugenini kwa kuwa na mtu asiye mwaminifu kisa tu ni pesa.


"Hakuna shida wacha wazidi kunisaidi kumtia mfu mwenzao mikononi mwangu." Kauli ya mwisho ilisikika kisha mawasiliano kukatika. Marietha haraka sana aliitia simu mfukoni na kutulia kimya akiwa macho mbele usawa wa ilipoelekezwa darubini ya kuonea gizani.


"Anafanya nini sasa?" Aliuliza Marietha.


"Anaonekana amepitiwa na usingizi." Alijibu Mabule.


"Lazima, shughuli aliyonayo siyo ndogo." Aliongea Marietha akiwa macho mbele kama awali.


"Unafikiria nini? Aliuliza Mabule.


"Hatuwezi kufanya hila yoyote ni hatari kwetu na kwa huyu dada. Lazima....!" Aliiacha kauli yake katikati baada ya kusikia hatua za mtu zikiwa zinakaribia eneo hilo. Ukimya ulikuwa mkubwa sana baada ya Sembuyagi kufika eneo hilo.


"Nipeni matokeo." Akauvunja ukimya huku akiwatazama kwa umakini mkubwa.


"Amepitiwa na usingizi." Alijibu Mabule maana yeye ndiye aliyekuwa akimuona kupitia lenzi ya darubini iliyopo machoni mwake.


"Endelea kumfuatilia tu asikupotee machoni mwako, anakamatika kama Kondoo leo." Alisema Sembuyagi kwa kujitapa. Mabule akamtazama Marietha kwa kificho macho yao yakakutana kisha wakaachana na ile hali.




Kwa upande wa Frank Matiale Bambi, muda ulikimbia sana na miwani yake haikutoka machoni, alikuwa akiendelea kumfuatilia yule binti kupitia uwazi wa kioo dirishani upande ule aliyoko yeye. Alimhurumia sana baada ya kumuona ndiyo alikuwa akishtuka kutokea usingizini. Ilikuwa imetimu saa moja na dakika thelathini tayari na bila shaka kilichomkurupusha kutokea usingizini kilikuwa ni miale ya jua iliyoanza kupenya kupitia dirisha maana alionekana akiyakinga macho yake kwa mkono. Alijinyoosha pale kochini kisha akaangaza macho yake kama vile ni mgeni ndani ya sebule ile. Frank Matiale Bambi alizidi kumfuatili. Akiwa pale kuna kitu cha ajabu alikiona ila alishindwa namna ya kufanya kwani alijiona akiwa amechelewa tayari. Kulikuwa na kundi kubwa la watu waliokamata silaha kali aina ya AK 47 huku wakiwa wamejipanga nje ya ile nyumba. Akahamaki akipigwa na butwaa asijue watu wale wamefikaje pale na muda gani. Watu wale walikuwa pale karibu na mlango wakiwa wametulia kimya wakionekana kusubiri amri kutoka kwa wakuu wake. Frank alipotazama vizuri kuna mtu alimvutia sana naye alikuwa akizungumza kitu na mtu mmoja aliyekuwa amevaa suti nyeusi. Mtu huyo alikuwa akimfahamu japo hakuwa na ukaribu nae. Huyu akimfahamu kwa jina la Amsuni Bhehe. Alikuwa ni mwanajeshi mstaafu wa kikosi namba 17 cha mapambano ya silaha aliyekuwa na cheo cha Meja.




MWISHO


0 comments:

Post a Comment

Blog