Simulizi : Kufa Tu Hakuna Namna (2)
Sehemu Ya Tatu (3)
Jane alipofika hapo akawa anapandisha kulia ila akajitahidi kuendelea hivyo hivyo kwa shida...
...baada ya madam kuingia muda huo huo akatoka akanifata na kuanza kuniuliza nani kaingia kabla yake!,nani kamuua kamishna si ndiyo nikashtuka kwenda kuchungulia ofisini kweli nilishughudia mkuu akiwa na damu kifuani! nikarudi na kumuuliza madam kwanin kamuua kamishna si ndo akanikaba akizidi kuniuliza ni nani aliyeingia kabla yake"
"na hapakuwa na mtu aliyeingia kabla yake?"
Inspekta Nurdin akahoji akionekana kuwa mtu aliyekuwa akitafakari jambo!
"angekwepo ningemuhisi yeye?,madam ndiye aliyeua na kama kungekuwa na mtu mwingine nilivyo mpigia mkuu asingepokea ila mkuu alipokea akaniruhusu madam aingie kuingia nashangaa heti kanatoka na kuniuliza nani kamuua kamishna kateswe katasema tu"
Jane akazidi kuongea kwa hasira,
Inspekta Nurdin aliandika maelezo yote aliyeona yanafaa,hata yeye katika kichwa chake alijua lazima madam 'S' hatakuwa ndiyo muhusika kwani katika upelelezi wake alishagundua Mombi anatoka usalama wa taifa chini ya madam yule na ndiye aliyemteka kamishna kabla wenyewe awajamuokoa, kama sheria inavyosema akamrudisha Jane katika 'lock up' zilizokuwepo pale makao makuu...
Akaenda Kumtoa Madam tayari kwa kumohoji ila kabla ajamuhoji kitu ghafla simu yake ikaita alipocheki alompigia alishtuka akaipeleka haraka masikioni
"ndiyo mkuu"
"sawa mkuu!"
Akaitikia na kuikata, akamwangalia madamu kwa sekunde kadhaa kisha akamwambia
"madam unaweza ukaenda"
Madam 'S' akujibu kitu, akaondoka zake,wala akutaka kujua ni nani aliyeongea na Nurdin akampa amri amwachie...
Haraka sana inspekta Nurdin Akaelekea eneo aliloitwa...
***********************
SURA YA SITA
Assistant Commissioner of polisi (acp) Kurwa Haji akiwa ndani ya ofisi yake ghafla simu yake ikaanza kuita kupokea ni DSP Maliyamungu
Huyu alikuwa ni msaidizi wa cp Haruna gozigozi,kamishna wa jeshi la polisi,
DSP Maliyamungu akaanza kumgombeza ACP Kurwa kwa kitendo cha kijana Nurdin kumweka 'lock up' Madam 'S' akamuomba Kurwa ampigie Nurdin Na Kumwagiza amwachie haraka sana Madam 'S' kwani kila kazi afanyayo ni kwa ajili ya taifa na eneo alilopo anaruhusiwa kuua hata kama ameua Nurdin ana idhini ya kumuhoji,
Alipokata Simu Ndipo Acp Kurwa alipo mpigia Nurdin na kumwambia amwachie madam 'S' haraka sana,
Inspekta Nurdin hakuwa nabudi kumsikiliza mkuu wake, akamwachia madam S,pamoja na Jane,kesi Ile Ikaishia Juu Juu
Familia ikiambiwa polis bado wanaendelea na uchunguzi, kiongezi mkubwa katika idara ya polisi kamishna!...
akazikwa kiheshima idara ya polis ikijua madam 's' ndiyo aliyemuua
MASAKI
Wapenzi wale wawili,ambao wote walikuwa na familia zao walikutana tena katika jumba lao lile la siri,Safari hii madam hakuwa na raha kabisa,
"kwa nini umemuua kamishna?"
Waziri John alimuhoji madam 'S',madam aliachia tabasamu japo lilionekana wazi si tabasamu la furaha! waziri akaendelea
"kama si kumpigia DCP nikamlalamikia wewe kushikiliwa na idara ya polisi tena ka inspekta tu naye Maliyamungu naye kumpigia acp Kurwa unadhani ungetoka wewe?!..."
"yule inspekta ni mtu mdogo sana najua labda hakujua wadhifa wangu,tofaut na msaada wako kikawaida mimi kama mkuu wa usalama wa taifa yule inapaswa anipigie saluti,aipaswi anihoji chochote kile nilimshangaa sana yule mtu!"
"ha ha ha mpz msamehe pengine alichanganyikiwa na kujisahau ila kwanini umemuua kamishna?!"
"hapana si mimi niliye muua kamishna,ichi kitu ndo kinacho nitatiza,kamishna alikuwa anajua kila kitu juu ya wanaokuchafua na hivi unajua yule mwandishi ZK yupo idara ya polisi?!,lengo la kwenda pale nimteke nikamtese anieleze yule mtu 'ZK' ni nani na anatumwa na nani ila cha ajabu nilipofika pale,yule secretary wake alimpigia simu sijui ni kwel alimpigia au ni uongo kunizuga akaongea naye si ndo akaniruhusu niingie kufungua mlango kuchungulia nikaiona maiti,hivyo kwa vyovyote vile kamishna kauwawa kusudi hili mimi nisimteke,ina maana ma adui zetu tayari walishagundua kwamba nataka kumteka kamishna ndo maana wakamuua na yule binti lazima atakuwa anamjua muuaji,mtu atapita wapi akaonane na kamishna bila kupitia kwake?!,yule msichana lazima ni dili naye kujua kila kitu mbinu yao ya kunipandikizia mimi nionekane muuaji imegoma sasa atanieleza kila kitu mwanaharamu yule........
Yule binti lazima atakuwa anamjua muuaji,mtu atapita wapi akaonane na kamishna bila kupitia kwake?!,yule msichana lazima nidili naye...
Madam 'S' aliongea kwa hisia,sauti yake ilimaanisha kile anacho ongea,
Aliona wazi ule mchezo alokuwa anaucheza ilipaswa awe siriaz vinginevyo angezidi kuwa katika hali ya sintofahamu!
je ni nani kwake msaliti?,avujishaye siri zake?!
au ni Don G?
Hapana alipinga wazo hilo vikali baada ya kutokea kumwamini kijana huyo japo alijua aikupaswa kumuamini anaweza kuwa msaliti kama Red deval,kijana aliyemwamini kwa kuwa na roho mbaya,ukatili wa hali ya juu ila siku ya siku akaja msaliti na kutaka kumtorosha Sara,
"hali ni mbaya na kwel yule binti hatakuwa anajua kila kitu dili naye ukimtesa kidogo atakueleza ukwel wote"
Waziri John aka afikiana naye! huku akiupapasa mkono wa mwanamama yule jasiri na kumpa muemko,kilichoendelea hapo ni kukifanya kilichowafanya wakutane kwenye jengo lile,kuifuraisha mioyo yao...
********
MAWIO STREET
Ni katika mtaa mpya waloamia Zidu na mpz wake Suzan,ambaye tayari mimba yake ilishafikisha miezi mitatu kama mwenyewe alivyodai!
Zidu na Suzan waliamia mtaa huu baada ya Suzan kumshawishi mpz wake akisahau kwamba yule ni mume wa mtu,wahame pale walipokuwa wakikaa awali kwa hofu kwamba lazima ipo siku Katarina angekuja,
Mtaa wa mawio ulikuwa nje kidogo ya jiji la Dar es sallam ndani ndani ya mkoa wa pwani,
Kule Waliona ndo eneo zuri la kujificha,
Baada ya siku mbili tatu Katarina kuwatembelea kwenye ile nyumba yao ya zamani na kukuta kufuli nje awali alihisi pengine watakuwa wamesafiri,ila alipoweka windo kazini alifanikiwa kumuona Zidu akajua lazima pale watakuwa wamehama!
Kwa Siri sana akaanza mfatilia Zidu mpaka akagundua mahali walipokuwa wakiishi kule pwani! ndani ya mtaa wa mawio,mtaa waishiwayo matatiri au watu wenye hali ya juu kiuchumi!
Pembezoni mwa jumba lile la Zidu na Suzani palipokwepo na ka grosary waliketi watu mbalimbali wakipata bia
Ghafla ikapaki gari,akashuka mtu aloficha sura yake dizaini kama ninja avaavyo, akaelekea mpaka ndani ya bar ile akiacha watu wakimtazama kwa mshangao...
Pengine walikuwa wakijiuliza inakuwaje binti wa kiislamu tena mwenye imani thabiti kuingia bar?,wakisahau kwamba lile ni vazi tu la kumsitiri mtu lipendwalo kuvaliwa na wale wamuogopae Mungu na kufata sunna za wake na watoto wa mtume japo siyo wote wavahao ni waumini wa dini ile,
Dada yule kule ndani ya bar macho yake yalikuwa makini kutazama geti la jumba lile ambalo ndani yake aliishi Zidu na aliyekuwa mfanyakazi wao Suzani,
Ghafla alishughudia lango lile likifunguliwa ikatoka gari ya Zidu lango likajifunga palepale wala akuangaika kuendelea na kile kinywaji alichokuwa nacho, mwanadada akajinyanyua tena akiwa na ghadhabu
'nilikuonya Suzan uachane na mume wangu ukajifanya mkahidi sasa itakupasa *KUFA TU HAKUNA NAMNA* kifo umekitaka mwenyewe najua namkosea Mungu ila sina jinsi nafanya hivi kuupa moyo wangu amani!,"
Katarina aliwaza akizidi lisogelea lile geti,kabla ajalifikia ghafla akaanza kusikia king'ora,tena kikali,kabla ajakaa vizuri na wala hata akujua wapi wametokea vijana wa nne wakamzunguka,
Katarina akajirusha na kuwatandika rasharasha ya mateke lakini watu wale waliyakwepa katarina akatua chini,mmoja akawa akimfata kwa spidi alipo mfikia akajirusha katarina akamkwepa mtu yule akaenda chini akajigeuza kwa wale wawili walokuwa wakimfata na kuwabambikiza double tik tak wote wakasambaratika chini,
Sasa Katarina akaanza kukimbia kwa mtindo wa zig zag kulifata gari lake risasi zikimfata nyuma kutoka kwa watu wale mapigo ya moyo wake yalipiga kwa kasi,kwani akuamini kile kilichotokea, akaingia ndani ya gari lake na kuliondoa kwa kasi, akijitukana matusi yote kwa kushindwa kuifanya kazi yake vizuri!...
Suzan akiwa ndani ya nyumba yake ile alonunuliwa na Zidu kama zawadi ya kumbebea mimba,aliketi mezani akiendelea kunywa chai nzito ya maziwa pembeni pakiwa na mikate ilopakwa blueband,mayai chapati na vikorombwezo vyote vinavyopaswa kuwa mezani kwa staftah ya asubuh,wakati akiendelea kunywa chai ghafla akasikia alamu ilo maanisha kuna mgeni alokuwa akilikaribia geti la nyumba yake si ndo atupie macho kwenye runinga,
Alishtuka!,japo Katarina Alikuwa Katika Mavaz Ya Suruali Nyeusi Ilompwaya Kidogo Kutomchora Umbo Lake Na Juu Alivalia Hijabu ambalo hata hivyo akulifunga vifungio vya mbele ndani akiwa kavaa tshart nyeupe...
Usoni akiwa kajifunga shungi kichwa kizima kaacha macho tu kusudi ili aone
Hivyo Kwa Mavazi yale aliweza kuruka teke,na ku tamba awezavyo,
Pamoja na kuvaa vile Suzan Alimtambua fika yule ni Katarina!
Katarina walomkwepa toka Dar amewafata mpaka huku,
ITAENDELEA
Simulizi : Kufa Tu Hakuna Namna (2)
Sehemu Ya Nne (4)
Katika Jumba lile lilikuwa likilindwa na wanajesh walotoka jkt walikuwa wakilinda kwa zamu,asbuh mpaka usiku wakilinda wa nane,usiku mpaka asubuh wakilinda pia nane vilevile wa nne ndani,wa nne nje,
Wa Nje waliketi nyuma ya jengo lile,kusudi kuto onekana kwa urahisi,jumba lile lililindwa kama kasri la kifalme kutokana na hatari Zidu aliyo iona,
Binafsi Zidu alimjua vizuri mke wake,huwa anasimama katika kile akitakacho hivyo alijua lazima tu angemfatilia na kuhitaji kumuua yule aliyeweza kumbebea mimba!...
Aliapa Kumlinda zaidi ya kitu chochote ndo maana akamwekea ulinzi ule,
Akuona Shida kutumia pesa kwa ajili ya ulinzi huo...
Baada ya Suzan kumtilia shaka Katarina haraka sana akaenda kwenye ile tv na kubonyeza kitufe chekundu si ndo alamu nje ika anza kuita,walinzi walokuwa nyuma haraka wakawah mbele ya geti lile wakamzunguka Katarina,mkono Ukatembea Kabla Katarina ajakimbia na kujiingiza ndani ya gari lake
'mshenzi sana wewe unadhani utaniua kirahisi'
Suzan aliwaza huku akicheka kwa dharau ghafla simu yake ikaita kuangalia ni ile namba ya Katarina haraka sana akaipokea
"we malaya embu acha kufatilia maisha yangu mwanaume kwani ni mmoja tu kama hakutaki si umuache kwani kuna ulazima wa kumng'ang'ania we umeshindwa kumbebea mimba sijui huna kizazi mwanaume kakumbimbia mimi nimem'bebea niache na sasa ukiendelea kunifatilia nitakuua KATARINA sitojali umenitoa wapi ok"
Suzan aliongea kwa hasira baada ya Katarina Kumpigia,KATA akuamini kama maneno yale yalitoka kwa binti yule,akabaki na butwaa pasina kuongea chochote,machozi ya hasira yakimchuruzika...
Binti alomsaidia tena anakumbuka hapo awali alipowasili nyumbani pale Zidu alimkataa na hata wakagombana na kununiana aliikumbuka vizur siku hiyo,
ILIKUWA HIVI
Ni Wakati Wakiwa Wanatoka kazini,kabla Katarina ajasimamishwa kazi na mumewe kufika katika jumba lao nje pale getini wakamkuta msichana akiwa na kamalboro, nguo zimechanika chanika,achilia mbali kuchafuka...
Binti baada ya kuiona ile gari akaikimbilia na kuanza kuomba msahada wa kazi!
"embu toka hapa umesikia tuna shida ya mfanyakazi?!"
Zidu akaongea akiwa kakunja sura,jamaa huyu alikuwa na roho mbaya,ila moyo wake ulikuwa ni tofauti na wa Katarina,labda kutokana na maisha magumu Katarina alopitia nchini Ganyama mpaka kujikuta akiangukia jeshini tena ukomandoo na hatimaye usalama wa taifa wa nchi ile,
"haaaa mume wanguu!,si unajua hapa hatuna mfanyakazi,nyumba inabaki peke yake tumchukue tu nakuomba mume wangu"
Zidu alimkata jicho kali Katarina,akashuka na kumsukumia kule yule binti akaenda fungua geti akarudi na kuliingiza gari
"mume wangu tumsaidie yule msichana"
Katarina akaendelea kum'bembeleza mumewe
"ishia hapo hapo unamjua wewe yule?,tunapambana na kesi ngapi sisi kama yule ni explorer tutajuaje,hata kama siye sihitaji kuishi na mtu mwingine zaidi yako na ndo maana hata walinzi sijataka kuweka
Kazi yetu ni ya hatari wanaweza kutumika na mahadui zetu wakipewa pesa sihitaji mfanyakazi hapa!"
"hapana Mume Wangu me naenda kumchukua"
Katarina akashuka kwenye gari,akarudi cha getini, akalifungua na kumkuta yule binti bado yupo pale nje,kajiinamia
Akaenda kumwamsha na kumshika mkono akamwingiza ndani,
Akamwonesha bafu akaoge, akamtolea nguo zake nzuri nzuri akampa avae akimwahidi wikiendi kwenda kumnunulia mpya madukani,wakat huo Zidu akawa aongei na mke wake kamnunia,
Wakati anatoka kazini akawa akimsaidia kazi wakipika pamoja,wikiendi alimpeleka kwenye duka kubwa la nguo akamnunulia nguo za gharama,kwa kuwa Zidu alimkataa yeye akashika dhima ya kuwa anamlipa kutoka kwenye mshahara wake tena mshahara mnono,
Mpaka Zidu alipo muachisha kazi ndo Zidu akawa akimlipa mwenyewe,anakumbuka ile siku ya kwanza tu alipo muuliza anatokea wapi akamjibu anatokea Gongo la mboto mwisho wa lami,na siku ilofatia kweli alimpeleka kwao ambapo ilikuwa ni nyumba ya udongo tena iliyolala upande mmoja
Yeye Suzan akiwa mtoto wa kwanza chini akiwa na wadogo zake watano vimefatana fatana,
Chakula walikuwa wakigombania,
Walikuwa wakihishi maisha ya dhiki,
Katarina yeye akabeba dhima ya kurepea nyumba ile kwa kutoa pesa yake mfukoni!,
Akawatengenezea nyumba ya tofali za kuchoma,wazee wale walifurah,Suzan alilia machozi akimshukuru!
LEO HII YEYE WA KUMWAMBIA MANENO YALE?!,
'we malaya embu acha kufatilia maisha yangu mwanaume kwani ni mmoja tu kama hakutaki si umuache kwani kuna ulazima wa kumng'ang'ania we umeshindwa kumbebea mimba sijui huna kizazi mwanaume kakumbimbia mimi nimem'bebea niache na sasa ukiendelea kunifatilia nitakuua KATARINA sitojali umenitoa wapi ok'
Maneno yale yakazidi kugonga kwenye ubongo wake na kuuchoma moyo wake
Suzan yuleyule aliyetaka aifute huzuni yake na kumjengea furaha,sasa anamkaribisha katika huzuni baada ya kumpatia furaha!
Yale maneno yakajirudia tena kwenye ubongo wake,yakauchoma moyo wake,akajikuta akiuinamia mstelingi wa gari yake na kuanza kulia,
Alilia Kwa uchungu,palepale akalitia gari lake moto kuelekea Jijini Dar,lengo afike gongo la mboto kwa wazazi wake Suzan akawaelezee pengine wanaweza wasiliana na mtoto wao na kumuonya amwachie mumewe,akazidi kanyaga mafuta...
Huku machozi yenyewe yakitiririka,jemedari,komandoo moyo wake ulijeruhiwa akawa akilia,
Baada ya masaa kadhaa alikuwa akiingia gongo la mboto,akazidi kukanyaga mafuta mpaka katika nyumba alowajengea wazazi wake Suzan,
akapaki gari lake nje ya nyumba ile,akashuka macho yalivimba nakuwa mekundu kwa sababu ya kulia,
Akapiga hatua kuelekea kwenye ile nyumba ghafla akasikia mlio wa simu upande wa nyuma wa nyumba ile akazunguka kufika akamkuta mama yake Suzan akiwa anachuma mboga akapiga hatua taratibu kumsogelea
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment