Search This Blog

Friday, 30 December 2022

KIAPO (MTETEZI WA KINTE) (4) - 2

   


Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (4) 


Sehemu Ya Pili (2)



Yule dada mule ndani akijua pengine ni wahudumu akajongea kufungua mlango,ile anachungulia pasina huruma Chaka alimtandika ngumi,nyuma kishindo kikasikika,bibie alienda chini,kwa haraka chaka akamvua lile baibui akalivaa yeye juu ya nguo zake,alimtaman sana dada yule lakini akuwa na muda wa kufanya naye kitu akambeba mpaka kitandani na kufunika,akabeba begi lake mgongoni akatoka mpaka mapokezi akumsemesha kitu yule dada ambaye alikuwa bize na simu,huku macho yake yakitazama tv ilo endelea kutangaza juu ya kusakwa kwake,

alipofika kule nje,akaelekea chooni alipotoa zile nguo,alipotoka alikuwa Zidu,akaipanda Pikipiki Yake na kuondoka eneo lile,akujua anapokwenda ni wazi maisha yake yalizidi kuwa hatarini!



****



MAMBO KWAKE YALIANZA HIVI



Habari kuwa raisi Moreti ii alikuwa akituma mtu aje kumuua kilimuumiza sana rais wa Ganyama,haraka Sana Akaitisha Kikao na wanausalama wakubwa wa jeshi,kujadili swala lile,hapo ilikuwa bado Chaka ajawasili,"cha kufanya hiyo kesho viwekwe vizuizi mipakani,gari zote zikaguliwe,jeshi lote lizagae mtahani huyu Chaka akitua tu akamatwe!,

Rais Silvestar akatoa amri,waziri wa jeshi,ulinzi Na Usalama akadakia!



"pia pamoja na yote hayo kuna binti yupo ndani ya ndege kutoka mafunzoni cuba,muda wowote anaingia nchini,huyu binti anajulikana ufanyaji kazi wake huyu na lameck tutawakabidhi kazi hii kuakikisha wanamsaka mtu huyu kabla ajafika kwako nakuhaidi mheshimiwa ndani ya saa 24 watakuwa washamtia mkononi,



Waziri Wa Jeshi,ulinzi Na Usalama Mh Haruna akaongea kwa kujiamin na ni kweli muda huo mwanadada Katarina alikuwa ndani ya chopa tabasamu likipendezesha sura yake ya urembo,alikuwa akitokea nchini cuba kwa mafunzo na sasa alifuzu,alichoka mikiki mikiki ya porini sasa alifurah kurudi Ganyama Kupumzika,akiwa Ndani Ya ndege alikuwa akiifikiria familia yake alotengana nayo kwa zaidi ya miaka saba,

'Naipenda Ganyama,naipenda Afc' aliendelea kuwaza,



kumbuka hii ilikuwa ni siku moja kabla ya kuwasili Zidu!,



Nusu saa badaye mwanadada Katarina aliwasili Katika Uwanja Wa Ndege Wa Ganyama Na Kupokelewa na maafisa mbalimbali wa jeshi safari ya kuelekea ikulu ikaanza!,

alishangaa Ganyama Ilivyobadilika Siyo Ile alokuwa akiifikiria yeye,nyumba zilibomoka,miti ilianguka,huku na kule hali ilitisha,



Robo Saa badaye aliwasili ikulu kulipofanyika tafrija fupi ya kumpokea hata familia yake ilikwepo,alijua sasa muda wa kula raha,au kula bata umewadia,kusahau juu ya yale mateso aloyapata katika mafunzo huko cuba



Baada ya tafrija ile kumalizika aliitajika na Rais Wake Kwa Mazungumzo,alijua bado ni pongezi tu alizokuwa akipewa katu akufikiri wala kudhani kuwa kulikuwa na kazi ngumu kuliko hata ya kupigana vita ilokuwa mbele yake,kazi ya kumtia nguvuni jitu katili lenye roho mbaya *ZIDU* ilosemekana anakuja kesho yake,kwa kazi maalumu ya kumwangamiza rais wao,akawasili ofisini ambapo alielezwa hali halisi akakutanishwa na lameck!,kazi ikawa katika mikono yao!



"nahisi huyu jamaa atokuja na njia za kawaida atajia na njia za panya tuweke doria masanya pale!"



Kesho Yake Katarina Alipokutana Na Lameck Katika Ofisi Yao Ndogo Walopewa,wakipanga Jinsi Watakavyoianza Kazi akatoa pendekezo lake,lameck Akamuunga Mkono,kweli Wakaweka Kambi Eneo Hilo La Masanja,na Kwel Ilipotimia Mida Ya Saa Tatu Kasoro Za Usiku Wakaitilia Shaka Pikipiki Moja Ilopita,wakaamua Kuifatilia,na Kweli Pikipiki Ile ndo ilokuwa ya chaka,safar yao ikaishia katika club moja kama tulivyoona,lameck hapo ndipo alipo yaacha maisha yake,na hivi ndivyo ilivyokuwa!



TUENDELEE...



Macho yake madogo yalikuwa bize katika kalabrasha moja lililokuwepo juu ya meza yake,akisoma historia ya 'kc' Zidu,ili Kusudi ajue jinsi ya kumkabili,



Ghafla akashtushwa na mvurumisho wa simu yake ilokuwa mezan pale,haraka komando katarina 'kk' akapeleka mkono wake wa kushoto kushika mkonga huku wa kulia ukibonyeza batani ya kijani kupokea



"una uhakika ni yeye?!"

'kk' aliuliza kwa wahka huku akiyatoa macho pima,



ghafla akaweka mkonga ule chini,akisahau hata kukata simu akasimama na kutoka nje,ukumbuke ofis yake ilikuwa katika kambi ya jeshi!



Dakika moja badaye alikuwa ndani ya mandolini,ambayo nyuma kulijaza wanajeshi wenye silaha nzito,nyuma yao pia kulikuwa na gari mbili tena za jeshi,zote zikawa zikifata nyuma gari alokuwa akiendesha mwanadada 'kk'



Mwendo Walokuwa Wakitoka Nao Siyo Wa Kawaida!





Baada ya kutoka mafunzoni Cuba,mwanadada Katarina anapewa kazi nzito ya kuakikisha anamdhibiti Komandoo Chaka,



Komandoo alokuja Ganyama kwa kazi maalumu,ya kuakikisha anamwangamiza raisi wa nchi hiyo,Mh Goodluck Silvester



Baada ya kupewa kazi hiyo yeye na mwenzake Lameck wanaamua kuweka doria mpakani mwa Ganyama Na Kinte Katika Njia Ya Shortcut barabara ijulikanayo kama Masanja,mida Ya Saa tatu kasoro kweli wanamtilia Shaka,mtu Mmoja Alowapita Na Pikipiki Wanaamua Kumfata Na Mwisho Wanakuja Kugundua Ndiyo,Zidu baada ya kugundua amegundulika anaamua kuelekea chooni ambapo Lameck Anaenda Kwa Nia Ya Kumdhibiti,huo Ndo Unakuwa Mwisho Wa Maisha Yake,Zidu anatoweka na kuelekea katika gest ingine usiku ule ule ambapo hata ivyo mdada wa mapokezi anaonekana kumwangalia kwa macho ya matamanio,anachukua chumba,badae akiwa chumban anawasha runinga anaona picha yake,akisakwa,machale yana mshika,anahamua kutoweka eneo lile,katarina Usiku Ule akiwa ofisin kwake anafatilia historia ya 'kc' anapigiwa simu,haraka sana anakusanya jeshi,wanajeshi wa kutosha kuelekea huko,je watafanikiwa kumkamata ZIDU,tulisonge



NA HII NI SEHEMU YA TISINI NA SABA



Msafara ule wa gari zile za kijeshi uliishia katika hoteli kubwa mjini pale iitwayo Savena inn,hoteli ile ndiyo ilosemekana ndani yake alikwepo komandoo alotumwa roho ya rais,wanajeshi wale walishuka kijeshi na kuizunguka hoteli ile kama walivyofanya katika club masaa kadhaa nyuma,wateja wote walipigwa na butwaa ila ilo alikumzuia komandoo Katarina na timu yake kuingia ndani wengine wakiweka doria nje,wandani walifika kaunta walipopokelewa na mwanadada mrembo ambaye ndiyo aliyepiga simu polisi baada ya kuona tangazo la kusakwa kwa kc,ambaye yeye kama muhudumu ndiye aliyemkabidhisha chumba,katu akujua yule alompita dakika kadhaa akiwa kavaa nikabu na kutoka ndiye muhusika mwenyewe na alipita pale akamsikia jinsi akiitaharifu polisi juu ya uwepo wake,



"Umesema yupo chumba namba ngapi?!"



Aliuliza Katarina,binti Yule Mrembo akajibu



"no 15"



Polisi Wale Kwa Tahadhari Wakaanza Kunyata Silaha Zikiwa tayari kuelekea katika chumba hicho,



Nje pia ulinzi ulikuwa mkali kutoruhusu kutoka kwa kiumbe chochote,walipofika Katika Chumba Kile Kuingia Walishtuka Kukikuta kitupu,ikabidi waanze kusachi vyumba vya jirani,ambapo chumba kilichofatia waligonga sana bila mafanikio,walipoingia na kwenda kumfunua yule dada,walimkuta amevimba uso,akiwa uchi,nguo zake azikuonekana,badae wengine waloendelea na msako wa chumba kwa chumba waligundua juu ya nguo zilizokutwa chooni!,



"wakati nikiongea nanyi kwenye simu nilimuona huyu dada akipita sikumtilia shaka,ila akurejea sasa nashangaa nguo zake kukutwa chooni naye kuwa hivi!...



Machale yakamcheza 'kk' tayari yeye na wenzake walishagundua kile kilichotokea,kwa mara nyingine tena Zidu alishawatoka,Katarina alizidi changanyikiwa bado kazi ilikuwa ngumu kwa upande wake...



Kutazama Saa Yake Ni Saa Tano Kasoro Za Usiku...



Zidu Katili akiwa juu ya pikipiki yake akujua aelekee wapi,giza lilizidi kutawala,wasiwasi ukazidi kumvaa,ile ilikuwa ni siku ngumu kwake,toka saa mbili anaingia Bamala Alishakoswa Kukamatwa Mara Mbili Sasa,kivipi Sasa awe na amani,na angeendelea kupiga doria mpaka saa ngapi?!,angeelekea wapi sasa,kila mahali kwake kulikuwa kubaya alijihisi kuishi kama digidigi au swala kwa kuwindwa kila kona,maisha yake sasa yaligeuka dili,aliitaji lau angepata msaada wa kubadilishana mawazo,alijikuta sasa ubongo wake ukichoka,hapo ndipo alipomkumbuka,Isack yeye mwenyewe alimkataa,akajikuta akitaka kujilaumu,kwa kukataa msaada ule "Ni afadhali chozi langu limwagike mara moja kuliko lije kumwagika tena,likiambatana na chozi la mkeo Mery,tena mjamzito,tukiwa wote sitokuwa na furaha,kama nikiwa mwenyewe...



Alipokumbuka Maneno Yale akajikuta yakiuchoma moyo wake,furaha hiyo aloitegemea akiwa peke yake sasa iko wapi?,lau pengine wangekuwa wawili wangefarijiana,akajikuta mwili wote ukimloa jasho kwa uwoga



...nikiwa mwenyewe ntakuwa huru

ntafanya kazi kwa ufanisi,tukiwa wawili ntakuwa na khofu ya kukupoteza,nakuomba nipo chini ya miguu yako rudi Tz nakuhaidi nala *kiapo* kwako NITASHINDA vita hii



Akakumbuka maneno yale na *kiapo* cha ushindi alichomwahidi dogo yule walotokea kuwa marafiki japo aliwah kuwa adui yake mkubwa utotoni,*kiapo* kile kikamtia nguvu,ari ya kupambana kwa ajili ya taifa lake,alijua huku alionekana muuaji,katili,ila nchini kwake alikuwa ni shujaa!,ghafla kumbukumbu flani zikamjia akaachia tabasamu,tayari alishapata jibu ni nin afanye!...



Alikumbuka wakati tu ndo anaingia jeshini,yule aloonekana kuwa mwalimu wao,mwanadada lucy kwa mara ya kwanza ndo wakati wakianza mafunzo aliitaji kujua sababu ya kuingia jeshini,kambi ya mafunzo kipindi kile ilikuwa huku upande wa Ganyama kwani taifa la Kinte lilikuwa bado alijajitenga!



"naanza kwangu mwenyewe,sababu ilonifanya niingie jeshini mimi toka mtoto nilikuwa katili,mimi ni mtisyu ndo asili yangu,nikiwa kwetu tisyu niliwah kumuua mama yangu kikatili sana,baba yangu alikuwa jeshi na nilimpenda sana,wakati akiwa vitani mama alikuwa akimsaliti baba na kuja nyumbani na lijimwanaume jingine,siku moja mi nikaja wachomea ndani ya nyumba,sasa nikaanza kusakwa nilikimbilia katika kijiji kimoja hiki kinaitwa mzuva land kipo hapo mpakani mwa tisyu na huku ganyamakinte,kijiji iko nikama kimesaulika na serikali,hakina polisi,kipokipo tu,kila mwananchi na lake,mambo ya kufatiliana fatiliana wana mzuva hawana hili,niliishi miaka mitatu ndani ya kijiji iko mpaka niliposikia baba yangu amerudi ndipo niliporudi nyumbani,baba ndipo aliponileta jeshi na kunificha humu ganyamakite kwa kuwa kule tisyu bado nilikuwa nikisakwa!



Maelezo Yale Yalimsisimua Kila Mwanafunzi Pale,huyu Ndo Lucy Zidu Na Mwenzake Kijo Walombaka baada ya kumaliza mafunzo,wakafukuzwa jeshini na kukimbilia Tanzania Ambavyo Hata Ivyo Lucy aliwafata,ila Zidu alifanikiwa kumuua!...



leo hii maneno yake yamempa mwanga kipi afanye,akaingia sheli,akatia mafuta ya kutosha,akalipa ela mwanaume akawasha pikipiki kuelekea mzuva land,



katu akufikira ni miaka mingi imepita maisha yamebadilika,na pengine mzuva si ya miaka ile...

ni wazi akili yake ilikuwa imechoka na iliitajika aipumzishe



Kasheshe!!!







Mzuva land kilikuwa bado ni kitongoji tu kidogo cha watu masikini 'hoehae' walotengwa hata na serikali!

kitongoji hiki kilikuwa nje kidogo ya mji wa Bamala,mji ambao serikali yote iliweka akili zake kuwa mwanaume Zidu angeendelea kuwepo ndani ya kijiji hiko,



Vituo Vya Polisi ndani ya mzuva nzima vilikuwa viwili tu navyo polisi awakuangaika na wananchi wale,kesi walizimalizaga wenyewe kwa wenyewe kwa sheria zao za kikabila!,

Mauaji yalipotokea walimalizana wao kwa wao pasina serikali kuingilia!



Naaam hii ndo ilikuwa sehemu sahihi ya lijitu kama li Zidu kujifichia humo...



Ndio,ilikuwa ni gesti chafu ilokosa huduma mashuka yalikuwa machafu kama ya magereza,kunguni walijenga hifadhi katika vitanda vya gesti hiyo vitanda aina ya teremka tukaze,yani ukilala ukigeuka chumba cha pili na cha tatu watajua jirani kageuka,kwa kwacha!,kwacha ya kitanda,

usiniulize kama kugeuka tu inakuwa hivyo wapenzi wanalalaje!...



Sidhani kama serikali ingeweza kudhani wala hata kujaribu kuhisi kama lijitu kama Zidu lingeweza jificha humo,hata Zidu mwenyewe alitingisha kichwa kuafiki kwa pale alikuwa huru,nje gesti ile ilichakaa na kuzungukwa na bustani nzuri ya majani yalokuwa kama hifadhi nzuri ya mbu,hapa ndipo alipopata chumba komandoo huyu alomudu maisha ya popote pale,Zidu aliketi katika kile kitanda kilalamikacho pindi ukijigeuza laptop yake ikiwa mapajani aliingia google kuna vitu akawa akifatilia,



Ghafla akatabasamu akaandika tarehe 15/2 katika kakitabu chake,alisoma google kuwa siku hiyo ilitegemewa rais afanye mkutano mkubwa katika viwanja vya maili 6,akaandika google pale viwanja vya mail 6 akaletewa ramani,akaicheki vizuri ile ramani akatabasamu!...



Baada ya kuridhika akafunga laptop yake na kujaribu kulala,usumbufu wa kunguni ukamnyima usingizi,akaamua kujiondosha katika kile kitanda akalala chini,pia harufu mbaya chini ya kitanda kile ikamuogofya,ila badae sana akapitiwa na usingizi!...



Siku ya pili yake aliamka saa tatu,kutokana na kuchelewa kulala jana yake,siku ya kwanza ilokuwa na misukosuko,toka kuingia katika taifa lile,baada ya kujiamsha akaenda kuoga,sambamba na kujipatia chai,akutaka kutoka muda ule,akaenda mapokezi kuomba fagio,akarejea chumbani mwake na kuanza kufagia chini ya kitanda alitoa uchafu wa kila namna si masalama,pakiti za sigara,chupa za soda!



Akazidi Kustaajabu Maajabu ya kijiji kile,inamaana wahudumu huwa awafanyi usafi au?,akakumbuka pia harufu ya mashuka,akuwaza sana akabeba mashuka yake na kutoka nayo

nje akayafua!,na kuya anika,maisha katika gesti ile ilikuwa ni kama umepanga chumba,usafi wa chumba lilikuwa ni jukumu lako wewe mwenyewe!...



Wiki sasa ikawa imekata Zidu akiwa katulia kimya ndani ya ardhi ya Mzuva akista ajabu msako juu yake ulivyokuwa ukiendelea,raia wasio na hatia ndani ya jiji la Bamala walikamatwa maelfu kwa maelfu wakipimwa vipimo vya d.n.a



Hatimaye tarehe 14/2 ndiyo siku aloamua kurejea Bamala,kusudi Kesho yake akatekeleze mauaji,pembezoni mwa uwanja ule kulikuwa na hoteli kubwa,Zidu aliamini hapo ndipo ambapo angefikia,akatoa wigi fulani katika begi lake akalivaa,mtoto wa kiume akakaa kitandani akatoa vidubwasha flani begini,akaanza jipodoa,alibadilika akawa mfano wa joti ajigeuzapo mwanamke katika kipindi cha zecomedy,akatupia dela mtoto wa kike kutoka wanaume apishanao awakuacha kummezea mate,Zidu alibadilika hakika!...



akutaka kutumia pikipiki yake,akapanda boda boda mpaka stendi ambapo alipanda gari mchana akaingia Bamala alifikia katika hoteli ile,akafikia mapokezi alipopokelewa na muhudumu,



"nikusaidie nini dada?"



Muhudumu alimuhoji Zidu Akiogopa Kutambulika Niwa Kiume Na Kutiliwa Shaka Alijifanya Ni bubu akaanza kuongea kwa ishara dada yule kuelewa lugha ile ya ishara kwake ilikuwa ni kazi ngumu akampa karatasi na kalamu aandike,kwa mwandiko wa kike Zidu akaandika,'naitaj chumba'

utakaa kwa siku ngapi,akaandika pale mbili,jina lake,akatumia Katarina,akiwa na maana yake tayari alishang'amua kuwa anayemsaka anatumia jina ilo na kulitumia kwake alitumia kwa mawili moja kukwepesha ukaguzi wa begi lake naye mwenyewe kwani pale alikuwa na silaha 'born sniper' hii ni silaha itumiwayo na wadunguaji mara kwa mara ndani ikiwa na uwezo wa kukaa risasi 16,dada yule wala akuwa makini,akang'amua kuwa yule yu katarina akijisahau kuwa katarina hana sura ile,na alishasahau mara kadhaa katarina alionekana katika tv akiamasisha kukamatwa kwa Zidu Na Pesa,



Akamkaribisha adui pasina kujua,na mbaya zaidi akampa chumba cha ghorofa ya pili ambacho kilikuwa upande wa uwanjani ukifungua dirisha ungeweza kuuona uwanja vizur sana,vyumba hivi vilipata bei sana wakati wa mechi kwani mtu akuwa na ulazima wa kwenda uwanjani palepale aliweza kuiona mechi laivu laivu...



Zidu akalala kwa amani akipanga ili na lile,alikuwa tayari kwa kazi,na siku hiyo alikamia kuikamilisha kazi



****



Ulikuwa ni mkutano ulokusanya maelfu ya watu,ulinzi uliimarishwa kila mahali katika pande za kiwanja kile kikubwa



Kwa Siku hii komandoo katarina alipenda awe nyuma ya mh raisi na aliomba sana kwani machale yake alihisi kuna hatari ilokuwa ikimjia raisi,naye raisi akamkubalia,



Viongozi mbalimbali walisimama kuhutubia kabla ya Raisi kusimama kuhutubia,kila kiongozi alosimama akuacha kuisema vibaya Kinte kuwa ndiyo chanzo cha machafuko Ganyama na kuilaani vikali ambacho awakukijua mita kadhaa nyuma katika ghorofa ya hoteli alikuwa mlenga shabaha na komandoo mashughuri Zidu K,akisubiria rais apande kinarani naye aikamilishe kazi,



Rais sasa akakaribishwa, akasimama,kc,akamtazama kwa darubini akamvuta akamweka katika target akahesabu moja,mbili,tat



Akaachia Risasi...



Duh Zidu kafanikiwa kumuua Rais kirahisi ivyo!?,





Maisha ya Rais Wa Ganyama Goodluck Silvestar Yapo hatarini,pasina kujua akiwa katika mkutano mkubwa,katika jengo moja ghorofan yupo mzee wakazi,izraely wa kibinadamu Jitu Zidu,nia yake ni moja tu kumwangamiza Rais yule hii ikiwa ni kazi kutoka kwa Rais wake Mernel moreti ii wa Kinte,na sasa kashamuwekea silaha zile zitumikazo na wadunguaji,ka hesabu moja,mbil tatu akaachia silaha



TUSONGE



Sifa moja wapo katika sifa za kijeshi kama nilivyosema hapo awali ni kutozidharau hisia,'kk' akiwa nyuma ya Rais hakuwa katika hali ya utulivu,aikuwa hali ya kawaida ile,alijikuta mwenyewe 'automatic' mwili ukimsisimuka



macho yake yalicheza,alijua lazima kuna kitu kinachoenda kutokea,Wakati komandoo yule alipofikisha tatu na kubonyeza kifyatulio,bila ridhaa ya akili yake viungo vya 'kk' vilifanya kazi,kwani ghafla alijikuta tu akimkata mtama wa nguvu Rais, Rais akaserereka chini naye kijeshi mwanadada akajilaza akiachia tusi la nguoni kwa mfetuliaji risasi,risasi zile zikaenda mpaka katika mwili wa muheshimiwa Richard Bull waziri alokuwa kakaa nyuma ya Rais Silvestar katika kinara kile!"



"oh,shit!"



Mwanaume Kule Juu akabweka,baada ya kuona amemkosa mkusudiwa wake na kwa haraka akalikwapua begi lake,akaisweka silaha yake ndani ya begi lake lile akajitupa katika ngazi na kuanza kushuka chini,akiongozana na raia walokuwa nao wakishuka chini,tayari wanajeshi wenye silaha kali za moto walikuwa wakipanda kuelekea juu katika hoteli ile,wakiwazuia wanaume wote waloshuka,wakiruhusu wanawake pasina kujua hata ZIDU awamu hii lilikuwa katika sura ya mwanamke alojivisha dela,hali ilibadilika katika kiwanja kile raia walikimbia huku na huko kujiokoa



Zidu Akajipakia Kwenye Pikipiki,ilompeleka Mpaka Stendi Akamlipa dereva bodaboda yule akaingia ndani ya basi kuu kuu yaelekeayo mzuva land,katu hakukuwa na wakumtilia shaka kwani wengi walimuona kama yu mwanamke!,plan 'A' ikawa imeshindikana ya kumwangamiza raisi...



Mwanaume Wa Kazi akatulia chumbani kwake akitafakari kipi angefanya kukamilisha kazi yake,kwa pale alijua msako dhidi yake ungeongezeka mara kadhaa na ulinzi wa kumlinda raisi ungeongezwa zaidi ya pale!



ila kingine alichowaza ni juu ya mwanamke yule!,



*KATARINA*



Mwanamke huyu alionekana wazi kuanza kuwa kikwazo katika kazi yake,yeye kwa kiasi flani aliifanya kazi yake iwe ngumu!,ikabidi aanze kumtafakari kwa jicho la tatu!...



***



Wakati 'kk' yeye 'kc' akimfikiria kwa jicho la tatu,yeye binafsi moyoni mwake kulijaa furaha kwa kitendo chake cha kufanikiwa kumuokoa Rais Wake,baada Ya Rais Kuingizwa Katika Ambulance Ya Jeshi Kupelekwa Hospital Katika Ulinzi Mkali,sambamba Na Mh Richard alokufa palepale,'kk' akutaka kuondoka pale uwanjani,aliamua kuanzia upelelezi wake pale...



Aikumwia Ugumu Kugundua Chumba ambapo risasi ilitokea,akaelekea mapokezi ambapo alimkuta yuleyule dada alomkaribisha Zidu Akijua Ni Wakike!

"kwa Jina Naitwa Katarina Ni Afisa Wa Polisi Ninayefatilia Juu Ya Msako Wa Zidu"



Dada Yule Wa Mapokezi Akashtuka,hapo Ndipo alipooanisha sura ile na ile aionayo katika tv,sura zililandana,na yule!..



Mapigo Ya Moyo Yakaanza Kumwenda Kasi,ndiyo,alijua Muuaji Alikuwa Katika ile hotel yao,ila katu akufikiria kuwa muuaji anaweza kuwa yule 'bubu' 'lakini mbona alijitambulisha kwamba yeye ndo Komandoo katarina?,au yeye ndo...hapana aiwezekani...yule wa kike ati!'



Mwanadada yule aliwaza,ghafla akazinduliwa na swali kutoka kwa katarina!

"unaweza kunambia chumba namba nne ghorofa ya kwanza alikikodisha nani na kwa muda gani?"

Swali Lile Likazidi Mchanganya Muhudumu Yule Kwani Alitambua Chumba Kile Ndicho alichomkodishia bubu toka juzi mchana!



"alikodisha binti mmoja alokuwa bubu alojitambulisha kwamba ni wewe!,katarina akatoa macho kama kafumaniwa,



"ni mimi kivipi?!"



akahoji akiwa katoa macho vilevile,



"juzi jioni alikuja dada mmoja bubu mimi sikumuelewa alichokuwa akiongea hivyo akawa akiandika,nilipo muuliza yeye ni nani aliniandikia ni komandoo katarina anayesimamia msako wa Chaka,maelezo yake haya hapa!...



Dada yule akatoa daftari lile aliloandika Zidu,



"fackin blood inamaana uijui sura yangu?!"

Katarina akaongea kwa hasira akilaani uzembe wa yule binti,binti akujibu kitu,"utalipa kwa hili,embu mwekeni chini ya ulinzi huyu"



'kk' akatoa amri dada yule akawekwa chini ya ulinzi, "naitajika kwenda chumba cha cctv kamera kumjua mtu huyu,meneja wa hoteli ile akampeleka mpaka katika chumba cha cctv camera,ambapo alianza kufatilia kila kitu kwanzia mapokezi pale alista ajabu jinsi Zidu alivyojibadilisha,kwa yeye kuiona picha yake tu aligundua yule yu mwanaume akajikuta akimshushia Zidu tusi la nguoni kwa kumzidi kete!

"na wakati haya yote yakiendelea wausika wa ulinzi wa hizi kamera walikuwa wapi kutojua kinachoendelea?"



"Kisheria Kamanda,si Ruhusa Kuchunguza Vyumba Vya Wateja,kamera Hizi Ni Espesially Kumgundua Mwalifu Alivyo Ivyo Humu Amna Mtu Aloajiriwa Maalumu Wa Kufatilia Wateja Vyumban Mwao!"



"ooh comon bustard nyinyi,hiki ndo kilichowakost sheria uchwara hiyo unaona sasa matokeo yake?,nin maana ya camera hizi sasa,hoteli hii itafungiwa nawaambia,eti si sheria kufatilia wateja vyumbani mwao mtaona matokeo yenu sasa...,brown nsevie kila kitu katika flash yangu juu ya kakapoa huyo ntashughulika nae pumbavu zake na siku nikimtia mkononi naja mtafuna mzima mzima"



"kk" Aliongea Kwa Jazba!







Zidu 'K' alilala katika kitanda chake ndani ya hotel ile ya kimasikini,alishawazoea kunguni wale,ivyo hawakumpa tabu tena,kichwani kwake bado alimfikiria mwanadada Katarina,katika historia yake Jitu Lile alikuwahi kukosea shabaha,ila uwezo wa 'kk' ulimshangaza



'dah!,anavitu vya tofauti walah mshenzi yule!'



Aliwaza Zidu Na Kujiamsha Katika Kitanda Akabinua Mto Na Kuitoa Silaha Yake Ndogo Na Kuanza Kuifuta Futa Kwa Umakini,



Alitamani Usiku Wa Siku Hiyo Kurudi Bamala Kujirusha Kidogo,akutaka Kujificha Saana,Zidu lilikuwa ni jitu lisilo ogopa,lililojiamini kwa kila nyanja





*******



Magazeti mengi sana yalipambwa na habari juu ya Zidu kumkosa kosa raisi Silvester na risasi,tv zilitangaza,habari zikapenya na kufika mpaka nchini Kinte Rais moreti Merneli ii alifurahia kwa kumpata kijana Shujaa kama Zidu ndani ya wiki moja kashamkosa Raisi na risasi aliamini Zidu lazima angeshinda vita ile



Kwa upande wa Rais Silvester hali yake ilitengemaa akaendelea na shughuli zake za kawaida



Baada ya kupona ,akaelekea zake ikulu,kitu cha kwanza ni kumuita Katarina na Waziri wake Wa Jeshi la Ulinzi Na Usalama Mh Haruna Gozigozi,Raisi Akaanza Foka Pasina Kuona Fadhila Za Kuokolewa Kwake Na Mwanadada Yule!



"eti Ulisema Ndani Ya Masaa 24 binti huyu atakuwa kamkamata huyo Zidu yako wapi?,wiki ya pili sasa inaenda mwisho nitauwawa sasa!,ni kazi gani unayofanya kama umeshindwa kazi andika barua jiuzulu,unampa kazi msichana,msichana atafanya nini?,anaweza pambana na mwanaume huyu?,naona unataka kucheza na uhai wangu sasa natoa masaa 24 sijui utabadilisha mtu,sijui utafanyaje Huyu Mtu Apatikane tofauti na ivyo ndani ya masaa hayo uwasilishe barua ya kuomba kujiuzulu ofisini kwangu niteue mtu atakayeweza fanya kazi hii..."



Baada Ya Mheshimiwa Raisi kumaliza kuongea maneno yale makali,akajinyanyua pasina kutaka kusikiliza chochote akatoka zake mule ndani,sasa pale ofisini walibakia watu wawili muheshimiwa gozigozi na Komandoo Katarina,alofura Kwa hasira hakika maneno yale ya raisi yalimchoma moyo wake!,kumbe akuukubali ufanyaji kazi wake?! alikosa raha kugundua lile ila mh Gozigozi alijawa na hekima kistaarabu tu akaongea na 'kk'



"najua ufanyaji kazi wako nakuamini,sito mpa mtu kazi hii zaidi yako,ukiishindwa wewe limeshindwa taifa go ahead,kaendelee na kazi..."



Katarina alitoka ndani ya ofisi ile kichwa kilikuwa chamzunguka,hasira juu ya *ZIDU* iliongezeka mara dufu,sauti ile ya raisi ikawa ikijirudia rudia katika kichwa chake ni wazi usiku huo hata lepe la usingizi asingepata,wazo akatupie bia mbili tatu katika club ya jirani akili ikae sawa!...



Safari Yake Ikaishia Moisture King,ilikuwa Ni club ya watu maalumu,mafogo,watu wenye ela zao mziki laini ulipiga watu wakicheza taratibu wengine walitulia katika viti vyao wakitingisha vichwa vyao taratibu ishara ya kuukubali mziki ule,taa za rangi tofauti tofauti na zenye mwanga mdogo zilimulika eneo lile la waliocheza,ilikuwa ni vigumu kujuana usoni,



Maeneo Ya Counter aliketi dada mmoja mrembo,hapo mezani chupa tupu za bia zilikuwa pembeni,bado aliendelea kufakamia bia zile,



Tayari alikuwa bwiii kama si bwaaa,pembeni yake mita kadhaa aliketi 'sharo' mmoja alo onekana kummezea mate binti yule,sharo yule alivaa t shart nyekundu ilomkaa vyema na kuonesha mwili wake ulojengeka kimazoezi,



Kichwani alikuwa na nywele fupi alizozichana na katika paji lake la uso alipachika mawani myeusi iliyo muongezea umaridadi,kifuani alitupia cheni ya dhahabu,ilomtoa katika kundi la wenye dhiki na kumuweka kwa wenye nazo



Vidole vyake vitatu alivaa pete za dhahabu tupu,alichonga vizuri ndevu zake mtindo wa 'o',mkononi alikuwa na saa yake kubwa ya mshale ya rangi ya silvar



Alitupia jinsi na chini raba zilizo mkaa vyema,mdomoni alikuwa akitoa moshi wa sigara aloivuta kutokea katika sigara kubwa zilizotumiwa mara nyingi na nchi za magharibi,kishungi alikipangusia katika kakibakuli ka dogo kalichokuwepo pale mbele ya meza yake muda wote huo macho yake yalikuwa kwa binti yule aloonekana wazi kuvutiwa nae,kutokana na mwanga mdogo mule ndani akubahatika kuiona sura ya binti yule vizuri,si unajua walevi na mwanga vitu viwili tofauti



Muda kidogo ghafla dada yule akanyanyuka na kuingia kati,akaanza kukatika,si unajua pombe si chai,wanaume walijilamba mdomo kwa matamanio,bado sharo aliendelea kumcheki akiulamba mdomo wake!,



Ghafla Msichana Yule akazingirwa na wanaume sita,wote walishika visu hawa walitambulika kwa jina la 'watoto wa mbwa' pale mjini bamala,walikuwa wakimtaka msichana wamtakae umteka na kwenda kumbaka kwa pamoja ndio tabia yao hiyo!



binti yule akawa akicheka tu huku akibubuja maneno unajua mimi nani,ila akuweza kuwazuia wakamvuta kumtoa nje,binti alishindwa kujizuia akabebwa juu juu,akawa akipiga kelele aachiwe msaada,nani angeweza wazuia watoto wa mbwaa ajitafutie tiketi ya akhera?!...



Ni nani asiyependa kuishi ati?!,wakatoka nae mpaka mabaunsa wa getini awakuweza kuzuia kitu ila kabla awajapiga hatua kulifikia gari lao!,wakasikia sauti nyuma yao!



"hoya ma braza mwacheni basi hiyo kitu yangu mnaipeleka wapi?!"



kugeuka ni yule 'sharo' na kweli binti akajikuta akichoropoka pale na kwenda kumkumbatia 'sharo'



"nisaidie beby wanataka kwenda kunibaka"



dada yule akajikuta akiomba msaada kwani kilevi kilimzidia,wanaume wale wakamzunguka duara



'sharo wakimweka kati wote wakiwa wameshika visu,



"jamani wana,huyu binti kawakosea nini naombeni njia acheni izo!"



'sharo' akaomba,watoto wa mbwa wakacheka alo onekana kiongozi wao akakoroma



"oya dogo tupe mali yetu au unataka kwenda kumsaidia kutukatia kiuno geto maana nawe ni kama yeye tu!"



"ok!,mwenye kujiweza aje amchukue!"



yule kiongozi akiwa kashika kisu chake akajileta mzima mzima,alipokelewa na teke,sambamba na kuvunjwa mkono,kisu kule,ni pigo la nusu sekunde jamaa alikuwa chini pasina ufahamu!



wale wengine kuona vile wakamsogelea,kwa pamoja,mwanaume akaruka akambatiza kila mmoja teke lake,ngumi kuona vile watoto wa mbwa wakasepa!



"mh we shujaa asante mume wangu sasa utanipeleka mpaka kwangu gari yangu ileee!"



Sharo Akamshika Binti Yule Hata Kutembea Peke Yake Akuweza Mpaka Katika Gari Yake Akamweka!,akarejea Kukabidhisha Pikipiki Yake Kwa Walinzi Akihaidi Kuirudia Asb,akarejea Katika gari la binti,akakaa upande wa dereva,binti akamwelekeza sharo njia,mpaka katika jumba lake!



'Sharo' mwenyewe alishangaa binti yule kukaa katika jumba lile peke yake,akampeleka mpaka chumbani wakaoga pamoja wakazama kitandani!,



Kwao Ilikuwa ni mara ya kwanza kukutana ila ilikuwa ni kama wapenzi wa muda mrefu,dada yule japo alikuwa ni fundi lakini penzi lile alilopewa na kijana yule alikiri toka kabalehe kutowah kulipata!



*ALIJISAHAU KUWA ALIKUWA KATIKA SIKU ZAKE ZA HATARI*



Walichoshana,awakujua sangapi walipitiwa na usingizi mzito,tena wakiwa wamekumbatiana,kila mmoja alikuwa karidhika kwa penzi la mwenzake



Asb Wakwanza Kuzinduka Ni Yule Mdada,akajitoa Mwilini Mwa Yule Sharo Akistaajabu Kujikuta Ka Alivyozaliwa,huyu Ni Komandoo KATARINA,komandoo alokabidhiwa kesi ya kumsaka Zidu katili,kesi ilomchanganya na kujikuta akilewa na leo kalala na dubwasha la baa kitandani mwake,akajikuta hasira zikimpanda akahisi mwanaume yule kamchezea akisahau jana yake yeye ndo alomsaidia kwa watoto wa mbwa akavaa nguo zake vizuri akiadhimia kumpa kichapo yule mtu kwa kula tunda lake bila ridhaa yake,japo alikubali na kumpa ushirikiano nusu usiku mzima lakini zilikuwa si pombe akamwinamia kumuamsha



"we fala embu amka unambie usiku umenifanyia nini?!..."



Aliuliza 'Kk' huku akimwinua mwanaume yule ambaye akumtambua kwa sura vizuri toka jana usiku walipokutana



Kumwinua sindo akamuona vizuri,macho yakamtoka pima akumtarajia kama ndo mtu yule ni Mwanaume Wa Kazi Zidu katiti,izraeli wa kibinadamu,



"ni.ni..ni..wewe?!"



Katarina akajikuta akiuliza kwa kigugumizi,mwili wote kwa hasira ukimtetemeka,meno mdomoni yakigongana!...



Kwa upande wa Zidu naye akajikuta akiganda kama sanamu lile la polisi aloshika bunduki ymca mjin moshi,naye masikin muda wote toka jana akujua kama yule ndo KATARINA,binti hatari amsakae usiku na mchana leo hii mwenyewe kajilengesha katika anga zake!....







Ni baada ya kupokea maneno mabaya kutoka kwa mh Rais,ili kutuliza akili mwanadada Katarina anaamua kwenda clab uko anakunywa mpaka kulewa pasina kujua anajikuta akiingia katika ngono zembe na Zidu,asubuh Ndipo Wanapotambuana



Kizazaa!!



Tusonge...



SEHEMU YA MIA MOJA NA MOJA



Ghafla akili ya Katarina Ikazinduka, akajua Ilipaswa Afanye Nini,chini Ya Mto Wake Ndipo Alipoifadhigi Silaha Yake,ivyo muda ule ule akajirusha kitandani na kuikwapua silaha chini ya mto ile anakaa sawa anyooshe mkono wake mahali alipo Zidu,



Alichelewa,kwani akujua saa ngapi Zidu alijinyanyua pale kitandani,ile anaunyoosha mkono wake,akapokelewa na teke la mkono,bastola ile ikapaa hewani ilipotua ilikuwa mkononi mwa Zidu,lilikuwa ni tendo la ghafla eti,kama vile yake akaitwika kibindoni,kisha akitabasamu akamwangalia 'kk' "unayaweza?" Akamuoji Katarina akikaa mtindo wa kupigana mguu mmoja ukiwa nyuma ya mguu mwingine,Katarina akujibu kitu akaachia tabasamu la dharau akamwendea Chaka Kwa Spidi Na Teke kali,teke lililokwisha somwa na mtaalamu yule akajipinda kidogo kumpisha,Katarina akaenda moja kwa moja kujipiga ukutani na kuachia yowe la maumivu!...



Akajinyanyua,sasa alikuwa akiongozwa na hasira akamfata Zidu na kurusha ngumi zake kadhaa ambazo zote Zidu Alizikwepa,Zidu akutaka kumpiga binti yule ila kila alipomkwepa au kukinga yalikuwa ni maumivu kwa dada yule,baada ya kuendelea kukwepa ngumi zile ghafla akageuza mkono na kupokea ngumi moja ikaenda mpaka katika mkono wa Zidu,akawa akiubinya sasa ule mkono huku akimwangalia Katarina Usoni jinsi alivyokuwa akikunja sura,ishara ya kuyapokea yale maumivu!,



Aliendelea mpaka aliposikia binti yule akitoa miguno ya maumivu ndipo alipoamua kuuachia mkono ule!



"sikupigi!,ila tambua kila pigo lako kwangu ni maumivu kwako dada endelea..."



Akamsukuma Kwa Nguvu Kule,katarina Akaenda Kujigonga tena ukutani,ghadhabu zikiwa zimempanda,alijikunja na kuja tena kwa spidi kwa mtindo wa aikido,alojifunza japani,ambayo katu hata kama angetua chini kwa jinsi alivyojikunja asingeumia na viungo vyote alivilegeza ndani kwamba hata kama Zidu angerusha teke au ngumi isingemletea maumivu...



Zidu Akawa akimwangalia jinsi alivyokuwa akija ghafla alijibiringisha kwa mtindo wa gaichi kumpokea 'kk' alipotua alikuwa mkononi mwa Zidu bila ajizi 'kc' akaupeleka mdomo wake mdomoni mwa dada yule na kumnyonya mate 'romance',kwa mtindo wa kitaalamu mwenyewe alouita romance fantastic japo 'kk' alijaribu kujizuia lakini utamu

aloupata ndani ya mdomo wake,ulianza kulegeza maungo yake mkono wa Zidu ukaanza kuchezea chuchu zile kwani usiku wote si alicheza nae,aliujua udhaifu wake,kata akaanza kuhema kwa shida,Zidu akamtupia kitandani,akawa akimfata pale kitandani bastola akiitupia mezani kwani kwa vyovyote vile alijua wakati wakipapasana dada yule angeweza ichukua,alijua alisha mloga pale,asingeweza kukataa kwa pale alipofikia...



ile anajitupa kitandani katarina alijinyanyua kwa ghafla na kufyatua mguu wake teke likatua sehemu za siri za zidu!



Zidu Akajipinda Kuzishika Kosa Katarina palepale alimsweka kipepsi cha kongfu na wakati

huo huo akimzawadia na kipepsi cha tumboni kwa kutumia goti la mguu wake,



Bila Kupenda Zidu Akaenda Chini,kata akawa akimfata akipania akammalizie palepale chini ila Zidu Akajibiringisha Na Kunyanyuka,ile kata anamfikia zidu alimrushia ngumi moja katarina aliona nyota nyota hatimaye ngumi ile ikampeleka katarina chini,Zidu akamfata pale pale chini na kumwinamia akamnong'oneza,



"bibie nashkur kwa penzi lako tamu,"



Akaupeleka mkono wake shingoni kwa kata akawa kama vile anapapasa ghafla akawa kama akimnyonga, akamuachia, akajinyanyua "tutaonana" akamuaga na kuufata mlango akatoka zake...



Katarina Pale Chini akabaki akiwaza,'kwa nini Zidu Kamuacha Na Ajamuua?!,ila Alijua pengine labda akuona umuhimu wa kumuua ndo maana akamuacha,je akujua kuwa nitamfatilia?!...



palepale akanyanyuka na kuufata mlango akaufungua kwa mbali akamuona chaka,akilikaribia geti,akainyoosha silaha yake,na kuanza kufyetua risasi kadhaa ila zilimkosa,chaka akawa kashatoka nje,akakimbia kulifata geti silaha ikiwa mkononi!...



Kwa Upande Wa Chaka, alimwacha Katarina Kwa Makusudi,japo Hapo awali aliwaza kummaliza,ila kiukweli alijikuta tu akimpenda,penzi alilopata usiku lilimlevya,wakati akikimbia kabla ajalifikia geti akashtukia risasi ikigonga pembeni yake,ile kugeuka,akamuona Katarina akiwa kashika silaha,haraka sana akashika mlango wa geti na kujitoma nje!...



akafunga kitasa cha nje na kwa bahati nzuri pale nje palikuwa na kituo cha bodaboda,pasina kuongea kitu akamsogelea bodaboda mmoja aloiwasha pikipiki yake huku akitabasamu



"wapi unaelekea kaka!"



Pasina kujibu Zidu aliunyanyua mkono wake,akamtandika ngumi nzito jamaa akaenda chini,mwanaume akapanda juu ya pikipiki,akaiondosha,



"mwizi,mwizi,mwizi huyooo,mwizi!"



boda boda wale walobakia walitamka,kila mmoja akipanda pikipiki yake,tayari kuifukuzia pikipiki ya zidu!...



Mwanaume yule kufanya vile alikuwa na maana yake,kwanza ni ili kuwaondosha bodaboda wale pale,kwani alijua 'kata' kule ndani angefika getini na kukuta geti limefungwa kwa nje lazima angegonga kwa nguvu na ambao wangemfungulia ni wale bodaboda kwa kuwa kituo chao akikuwa mbali na ule mlango ina maana sauti ya ugongaji ule angeisikia!...



ila akujua kwa kufanya vile kaizalisha kesi ingine na bodaboda,kwani walizidi pigiana simu,kwani kituoni pale walikuwa watano tu ila mpaka muda ule walikuwa zaidi ya 20 nyuma yake,bahati nzuri alitumia njia ya vumbi isiyo na magari,

ghafla mbele yake boda boda kama 30 hivi zikatokea..



nyuma zikiwa 20 wakamuweka kati!...



akakosa pa kutokea!..



"auwawe,auwawe,achomwe moto moto mwiziiii"



kelele zikazidi kusikika...







Baada Ya Zidu kuona kazungukwa,na kuwekwa kati akaisimamisha pikipiki na kushuka chini,baadhi ya bodaboda nao wakashuka kwa wahka,wakamvamia Zidu,bila kuchukua tahadhari yeyote



Zidu K' Mtaalamu Wa Mapigano ghafla aliruka mateke na kuwatawanya akitumia aina ya taekwando!



mateke ya haraka haraka,baadhi ya bodaboda walipo ona kitendo kile wakaanza kurudi nyuma,zidu akaona pale atajichosha zaidi na mbaya zaidi anawezwa kutwa pale na wanausalama,ghafla akachomoa silaha yake na kufyatua risasi kadhaa hewani!,akajirusha juu ya pikipiki yake ile!



"kama mtu ni mwanaume kamili anifate"



akaongea kwa jeuri silaha ikiwa mkononi,hakukuwa na aliyesubutu kumfata mwanaume akatoweka!...



****



Baada Ya Katarina Kugundua Kwamba Amefungiwa akajaribu kugonga geti lake mara kadhaa,hili hata boda boda wale waloweka kituo nje ya geti lake,wamfungulie,aligonga mara kadhaa pasina mafanikio,akashangazwa na jambo hilo,ukuta mzima ulzungushiwa nyaya maalumu za shot huu ukiwa ni ulinzi maalumu,ivyo alijua asingeweza kurukia hapo...



Baada Ya Kimya Kile Na Kung'amua Nje Hakuna Mtu Alijua tayari Zidu alishamponyoka,na Akujua kwa nin akukuwepo na bodaboda pale nje kwani apakukosekanaga mtu hata mmoja pale...



Ghafla Akarudi Ndani Kwa spidi,akachukua simu yake na kupiga namba kadhaa!...



"aloo Saimon,nakuomba Uje Nyumbani Kwangu Mara Moja!"



Akakata Simu Na Kukaa Kochini,alichoka mwili na roho!...



Dakika tano badaye jamaa mmoja alikuja na gari yake kufika pale kabla ajashuka akaanza kupiga honi mfululizo 'fungua mlango nimefungiwa kwa nje'



meseji ikaingia kwenye simu yake,akaisoma palepale akashuka na kwenda kufungua geti!...



Tayari Katarina alikuwa hapo nje ya geti,haraka sana akajitoma nje,"twende,twende," huku akiongea kwa wahka,Saimon akiwa Na Uso wa mshangao akamfata,wakaingia kwenye gari,Katarina akakaa upande wa dereva!



"kitu Gani Kimetokea Katarina Mbona Sikuelewa?"



Saimon Akauliza Kwa Mshangao,



"dah,mmh Sijui hata nikwambie nin?"



Katarina aliongea pasina kujua aongee nini



"nambie hiko hiko kinachokuchanganya na huku tunaelekea wapi?!" Sai Akazidi Mbana Mwanadada Yule,katarina Akaanza Kumfungukia Pasina Kujua Atamuumiza Yule Kijana Kwa Kiasi Gani!,kwani Naye alishamuonesha chembe chembe za kumuhitaji na alishamwambia...



"dah unajua jana tuliitwa ikulu mimi na mh wazir..."



"yah taharifa hiyo niliipata makao makuu pale!,"



"basi Kufika Mkuu Kafoka,katoa masaa 24 Zidu Awe Amepatikana tofaut na ivyo mh waziri ajiuzulu,na mbaya zaidi ajaona ufanyaji kazi wangu,nimeumia sana,aliongea maneno makali kwa kwel nilishindwa vumilia nikaenda bar kutupia bia mbili tatu kichwa kikae vizur,punde watoto wa mbwa si wakanivamia,mbaya zaid mtoto wa kike nipo tung!"



"wacha weee,ukuwadhibiti?"



"nikisema nilikuwa tungi ni tungi kikwel kwel nayumba,hata kurusha teke sikuweza,hakuna aliyezuia mpaka walinzi getin wakatupisha njia,wakantoa nje..."



"khaaa wewe! kwa hiyo walifanikiwa ku.."



Kabla ajamalizia Kata Akamkatisha...



"wafanikiwe wapi kabla awajaniingiza katika gari yao si ndo yule bwege akatokea!" Kata Akaongea akiwa kakunja mdomo!



"bwege?,bwege gani tena?!" Sai akahoji kwa mshangao,



"Zidu!.."



"khaaa Umemuona Zidu?,ukumkamata? Mbona Ukutoa taharifa?"



"sikumtambua,nilikuwa nimelewa aswa Sai"



"kwa Hiyo Ukamuacha akaenda?"



"Hapana tukaja nae mpaka nyumbani,asb naznduka nipo kifuani mwake,akili ndo zikanirudi nimefanya ngono zembe,nikamvaa pale kumbe ndo yeye,tukaanza kupambana ila alifanikiwa kuniponyoka akakimbia na kunifungia nje!"



"Mungu wangu!..." Sai Akajikuta akiweka mikono kichwani,habari yake si tu ilikuwa niyamshangao kwake pia ni ya aibu,kichwan kwake akakiri mwanamke ni mwanamke tu,akafikiria msimamo wa Katarina,toka ametoka masomoni,akakaa katika kota za kambin mpaka sasa uraiani,amekuwa akimsumbua kumuitaji kimapenzi!,ila mara zote dada yule amekuwa akimwekea msimamo!,leo hii adui kirahisi tu anakuja kula kile alichoshindwa kukipata!...



akajikuta akikunja sura kwa hasira,kata haraka sana aliona badiliko lake lile, akaachia tabasamu,kumpa faraja!



"huku sasa tunaenda wapi?!"



Sai akauliza kwa hasira,



"pale club tulipo onana naye jana?!"



"khaaa sasa unadhani atakwepo hapo mpaka saivi?"



"no sina maana hiyo ila pale aliacha pikipiki yake!"



"atakuwa kashaichukua lakin!"

ITAENDELEA

Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (4) 

Sehemu Ya Tatu (3)





"twende tutajua mbele kwa mbele,ila Sai kuna Kitu Nataka Nikwambie!,"



Saimon akamkata jicho mwanadada yule,akakaa tayari kumsikiliza,kata akaendelea!...



"toka mara ya kwanza ulivyonambia kwamba unanipenda,sikutaka kukufungulia hisia zangu Sai,kutokana Na Kazi Iliyoko Mbele Yangu,ila Japo Sikukubalia toka ndani ya moyo wangu nilikupenda toka 'farst time' nilipokuona leo asb nilipogundua nimetoka na yule mweu,nilijihis hatia juu yako...



Wakati Katarina Anaongea Maneno Yale,kijana Yule Wala Akuamin Kama Yanatoka Mdomoni Mwa Katarina,mwanamke Alompenda Akakata tamaa hata ya kumpata!...



Akajikuta Mwenyewe Machozi Yakimchuruzika...



Na Wakati Huo Huo Zidu alikuwa ndani ya chumba chake kule mzuva land,mawazo yake,yalikuwa juu ya mwanamke yule!,moyo wake ulishampenda,sura yake ya urembo ilijinakili katikati ya ubongo wake!,alijikuja akiwa amekufa ameoza!...

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog