Search This Blog

Thursday 29 December 2022

C.O.D.EX 4 (A MISSING SOLDIER) - 1

  Simulizi : C.o.d.ex 4 (A Missing Soldier)

Sehemu Ya Kwanza (1)


Simulizi : C.O.D.EX. 4

Mwandishi: FRANK MASAI

Imeletwa kwenu na: BURE SERIES



“Tulikuwa ni watu kama watu wengine. Tuliwapenda wazazi wetu kama watoto wengine. Tuliishi na kufurahi kama watu wengine. Na tukapata malezi bora kama watoto wengine. Lakini mambo yalikuja kubadilika baada ya kuingia mikononi mwa Wanasayansi. Watu ambao hawajali uwepo wa nyama miili mwetu na mzunguko wa damu katika mishipa ya damu. Wakapandikiza kemikali zao kwenye damu zetu, wakatengeneza miili yao kwa kutumia nyama zetu. Na hatimaye tukaitwa wanajeshi. Na tena wanajeshi wenye uwezo wa kipekee duniani. Maisha ni kama upepo, ukiamua kubadilika, hubadilika bila kuambiwa ubadilike. Maisha yetu yakabadilikia hapo, na sasa tukaitwa wanajeshi hatari.”


NEW YORK, MAREKANI.


Kulikuwa ndani ya jengo kubwa na lenye mwanga mkali kila mahali. Watu mbalimbali walioenekana ndani ya mavazi ya kitabibu huku wamekamata Ipad za gharama ambazo walionekana wakizichezea chezea na wakati huohuo wakiangalia miili ya watu iliyokuwepo ndani ya majokofu yenye matirio ya kioo na ndani yake kulikuwa na maji yaliyojaa. Binadamu waliokuwepo humo, waliingiziwa mipira midomoni na puani na walibandikwa vitu fulani vifuani mwao kwa ajili ya kupima mapigo yao ya moyo.


“We called them, New Generation Soldiers, Sir (Tunawaita Wanajeshi wa Kizazi Kipya, Mkuu)” Aliongea bwana mmoja ambaye alikuwa nje ya maabara ile lakini aliweza kuona kila kinachoendelea kupitia kioo kikubwa kilichokuwa ndani ya jengo lile.


“Are you sure about your generation? (Unahakika na kizazi chako)” Bwana mmoja mwenye suti na mwenye asili ya Kimarekani, alimuuliza yule tabibu aliyekuwa kasimama pembeni yake akijinadi juu ya wale wanajeshi waliokuwa ndani ya majokofu zaidi ya hamsini.


“Yes Prime Minister. These are the best soldiers we ever created before. They can fight for so long without tired. (Ndio Waziri Mkuu. Hawa ni wanajeshi bora kuliko tuliyowahi kuwatengeneza hapo kabla. Wanaweza kupigana kwa muda mrefu bila kuchoka)” Akajibu yule tabibu ambaye alivaa kitambulisho kilichoonesha sura yake, jina na cheo chake. Bwana mmoja aliyekuwa na asili ya Kimarekani, na ilionekana kuwa kaongozana na Waziri Mkuu, aliangalia kitambulisho hicho kabla hajaongea.


“Tutegemee nini katika wanajeshi wako Dokta Ice Mujo.” Akauliza yule bwana aliyeongozana na Waziri Mkuu kwa lugha ya Kiingereza.


“Maajabu ya dunia. Wanajeshi watano pekee, wanaweza kuingamiza Urusi yote ndani ya saa moja. Tumewapachika uwezo wa kipekee na silaha nzito wanazo vichwani mwao.” Alijibu Dokta Ice.


“Silaha gani hiyo Dokta?” Akauliza tena bwana aliyeongozana na Waziri Mkuu.


“Nyuklia bombs. Kila mwanajeshi hapo, kabla hajaenda mapambanoni, tunampandikiza chip ndogo ambayo inaweza kuruhusu mabomu ya nyuklia yalipuke mahali ambapo yatapandikizwa. Kati ya wanajeshi watano tunaoweza kuwatuma, wawili ni lazima wawe na mabomu ya Nyuklia. Hawa ndio wanauwezo wa kipekee.” Alijibu Daktari.


“Wanauwezo gani?” Akauliza Waziri Mkuu.


“Angalia hii.” Akamsogezea Ipad. Kisha akabonyeza sehemu ya video na hapo wakaanza kuonekana wanajeshi wakifanyiwa majaribio. Picha ambayo iliwafanya wale mabwana waliokuja pale kushangaa, ni mlipuko mkubwa uliotoka kwenye mwili wa mwanajeshi mmoja, halafu baada ya mlipuko huo, yule mwanajeshi alitoka ndani ya moto akiwa anawaka lakini akitembea bila wasiwasi… Baadae moto huo unazima, na mwanajeshi anaoekana hana makovu yoyote ya moto licha ya nguo zake zote kuungua.


“Hatari sana hii.” Aliongea waziri mkuu huku katabasamu.


“Hiyo ndio C.O.D.EX improved chemical.” Daktari alijigamba kwa mbwembwe.


“Kwa hiyo ni ile C.O.D.EX ya wale wanajeshi wengine?” Aliuliza bwana yule aliyeongozana na Waziri Mkuu.


“Ndio Waziri wangu wa Ulinzi.” Kwa tabasamu pana alijibu Dokta Ice.


“C.O.D.EX ni nini?” Akauliza Waziri Mkuu.


“Ni kifupisho cha maneno haya, CINDREX OLTIVIASO DECA ENDROLINE X. Ni chemikali zilizobuniwa miaka kumi nyuma na walitengenezwa wanajeshi kadhaa ambao walisumbua sana CIA na FBI. Baada ya kujua kemikali hizi, CIA waliweza kuharibu maabara yote ya kutengenezea wanajeshi hawa. Sasa hivi ndio tumepewa kibali cha kutengeneza silaha kupitia kemikali hizi.” Alijibu Daktari.


“Kuna tofauti gani kati ya wanajeshi hawa na wale wa miaka kumi iliyopita? Hawawezi kuleta madhara kama yale?” Aliuliza Waziri wa Ulinzi.


“Hapana. Hawawezi fanya hivyo. Tatizo kubwa la wale waliyopita, hawakuwatoa kumbukumbu wale waliowatengeneza, hivyo ilikuwa rahisi kwa zile kemikali kurudisha kumbukumbu baada ya kuanza kuisha. Hilo likaleta tatizo kwa baadhi ya wanajeshi ambao kumbukumbu ziliwarudia.” Akajibiwa.


“Okay. Kwa hiyo hawa hawana kumbukumbu?” Akauliza tena Waziri wa Ulinzi.


“Ndio. Kabla hatujawaingizia C.O.D.EX, tulihakikisha kwanza tunafuta kumbukumbu zao zote za maisha yaliyopita. Tuna uhakika tumefanikiwa katika hilo.” Alijibiwa na daktari.


Waziri wa Ulinzi akaangaliana na Waziri Mkuu kisha kwa ishara fulani walipeana kuonesha kuwa wamekubaliana na ile kazi ya C.O.D.EX.


“Sawa Dokta. Ila kwanza ni lazima tufanye majaribio na silaha zako.” Waziri wa Ulinzi aliongea na kumpa nafasi dokta naye aongeze jambo kama analo.


“Mmepanga wapi kufanya majaribio yenu?” Akauliza Dokta.


“Iraq na Iran.” Akajibiwa na dokta akaonesha kukubaliana na majibu hayo.


“Ila kuna jambo moja ambalo tumelipandikiza kwenye miili yao.” Akakumbusha daktari.


“Lipi hilo?” Akaulizwa.


“Hawana huruma hata kidogo. Kitendo cha huruma kwao kimepita kushoto. Kwa hiyo hayo majaribio, tujaribu kuyafanya mbali na raia.” Akaongea dokta.


“Hamna shida.” Akajibiwa na Waziri wa Ulinzi kwa kifupi.


Baada ya maongezi hayo marefu, wale viongozi wa serikali ya Marekani, walianza kuondoka eneo lile huku nyuma wakifuatiwa na walinzi wao muhimu kabisa.


****


BAADA YA WIKI MBILI.


Vyombo vya habari duniani vilikuwa vinatangaza kuhusu Iran kuvamiwa na mitambo yake ya nyuklia kuharibiwa vibaya na wakati huo mateka wa Iraq walisemekana kuwa wamekombolewa na wanajeshi wa jeshi la Marekani lakini hawatambuliki ni wapi walipo. Habari zilikuwa zimezagaa na kuzusha maswali kadhaa kwenye vichwa vya habari na watu wote kwa ujumla.


Vyombo vya habari viliuliza kuhusu wanajeshi hao na Waziri Wa Ulinzi alithibitisha uwepo wa wanajeshi hao na kuahidi kuwa, Marekani itakuwa na nguvu kubwa kuliko nchi yoyote duniani.


Wakati hayo yanaendelea, daktari mkuu wa ile maabara alikuwa anatazama na kusikiliza vyombo vya habari kila kukicha. Jambo ambalo hakuwaambia wale viongozi, ni uwezo wa wale wanajeshi kuchukua matukio yote kwenye chipu iliyokuwa imepandikizwa vichwani mwao kwa ajili ya kuwatuma wafanye mambo fulani.


“Wajinga sana hawa. Niliwaambia wasifanye majaribio kwenye makazi ya raia wema. Matokeo yake wamewaua mateka wote. Washenzi sana. Natakiwa kufanya jambo moja muhimu sana kabla sijaondoka hapa.” Alijiwazia Dokta Ice na hapohapo akaifata kompyuta yake iliyokuwa katika ofisi ndogo kwenye chumba chake na kuanza kusoma mambo kadhaa kwenye mafaili yaliyokuwepo kwenye kompyuta hiyo.


Kesho yake ilikuwa Asubuhi ya Jumapili yenye bashasha nyingi sana. Dokta akiwa anajua wazi kabisa kuwa siku hiyo ni ya mapumziko kwake, alitoka ndani ya nyumba yake akiwa kakamata mkoba wenye makaratasi kadhaa, kisha akapanda gari lake la gharama na kuelekea zilipo ofisi zao.


Huko aliamrisha baadhi ya wafanyakazi waondoke kwa sababu alikuwa na kazi nyeti ya kufanya bila wao kuijua. Alipofanikiwa kuwatoa, akafungua jokofu moja ambalo lilikuwa tofauti na yale mengine. Lenyewe lilikuwa halioneshi na lilifanana na lile la kuhifadhia maiti. Alipolifungua, akaonekana muafrika mmoja aliyekuwa kafumba macho yake kama marehemu na mvuke ukimtoka kwa sababu ya kuganda kwa mwili wake.



Ice Mujo, akabofya vitufe kadhaa kwenye lile jokofu nalo likaanza kuvia maji ambayo yalikuwa ya moto. Maji hayo yakayayusha barafu iliyopo mwilini mwa muafrika yule na kumfanya awe laini na mwenye hali ya umoto.


Akabofya tena vitufe kadhaa kwenye ipad yake. Vitu fulani vikatokea angani na kisha vikashuka hadi kwenye lile jokofu. Vikazama ndani ya maji na kumkamata yule bwana, kisha vikatoka naye na kumuweka kwenye lile jokofu lingine ambalo lilikuwa linauwezo wa kujazwa maji pamoja mitambo ya kumuwezesha binadamu kupumua.


Dokta Ice, akambandika vile vifaa vya mapigo ya moyo pamoja na mipira maalumu kwa ajili ya kupumulia. Alipomaliza, akafunga lile jokofu na kufungulia maji yaliyoanza kujaa ndani yake.


Akasogea kwenye kompyuta inayoonesha hali ya yule binadamu muafrika. Akaanza kuruhusu kemikali aina ya C.O.D.EX ianze kuingia mwilini mwa yule bwana. Kilikuwa ni kitendo cha dakika kumi pekee kukamilisha tendo lile na lilifanikiwa kwa sababu muafrika yule alianza kupumua akiwa ndani ya jokofu lile.


Kwa haraka, akabonyeza tena vitufe kwenye kompyuta na hapohapo maji yakaanza kupungua na baada ya kuisha yote, yule bwana alijikuta akisogezwa nyuma kwa kasi na kisogo chake kikagota nyuma ya kidirisha kidogo ambacho kilifunguka na hapohapo mwanga fulani mwekundu ukaanza kupitia sehem hiyo ya kisogoni. Kisogo cha yule bwana kikafunuliwa kidogo kwa kutumia ule mwanga ambao ulitumika kukata sehemu hiyo.


Kiasi kidogo cha ubongo kikatolewa, na baada ya hapo, Dokta Ice alifungua mkoba wake na kutoa Diskette na kuchomeka kwenye sehemu maalumu ya kwenye komyuta aliyokuwa anaitumia. Ikaanza kusoma harakahara na baadaye ikaandika ‘loading succefully, 100%’. Dokta akashusha pumzi na kisha akabofya kitufe cha Enter. Hapo kule kwenye kisogo cha yule bwana, ikapandikizwa chipu na kisha ile ngozi iliyotolewa kisogoni, ikapachikwa na kupitiwa na mwanga ule mwekundu. Pakarudi vilevile.


Yule muafrika akatoka kule alipobananishwa na kusogezwa katikati ya lile jokofu. Dokta akabonyeza tena vitufe kadhaa kwenye kompyuta yake, yule bwana akaanza kuzunguka taratibu kwenye lile jokofu kw a dakika zipazo kumi. Aliposimama, kompyuta ikaongea kwa sauti ya kike, ‘upgrade complete’. Kisha maji yakajazwa ndani ya jokofu na dokta akawa kamaliza kazi ambayo alipanga kuifanya jana yake.


Dakika ishirini mbele, akamtoa mtu yule kwenye jokofu na kumuingiza kwenye mashine nyingine iliyoanza kuupembua mwili wa muafrika yule hadi ikaridhika na kutamka maneno mengine ya kiingereza, ‘Scan Complete’.


Dokta Ice akatabasamu baada ya kufungua mashine ile na yule muafrika kusimama mwenyewe na kumtazama Dokta.


“Nipo tayari kukutumikia mkuu.” Aliongea bwana yule kwa Kiingereza na kumfanya Dokta kuzidi kutabasamu.






Yule mwafrika akatoka kule alipobananishwa na kusogezwa katikati ya lile jokofu. Dokta akabonyeza tena vitufe kadhaa kwenye kompyuta yake, yule bwana akaanza kuzunguka taratibu kwenye lile jokofu ka dakika zipazo kumi. Aliposimama, kompyuta ikaongea kwa sauti ya kike, ‘upgrade complete’. Kisha maji yakajazwa ndani ya jokofu na dokta akawa kamaliza kazi ambayo alipanga kuifanya jana yake.


Dakika ishirini mbele, akamtoa mtu yule kwenye jokofu na kumuingiza kwenye mashine nyingine iliyoanza kuupembua mwili wa mwafrika yule hadi ikaridhika na kutamka maneno mengine ya kiingereza, ‘Scan Complete’.


Dokta Ice akatabasamu baada ya kufungua mashine ile na yule mwafrika kusimama mwenyewe na kumtazama Dokta.


“Nipo tayari kukutumikia mkuu.” Aliongea bwana yule kwa Kiingereza na kumfanya Dokta kuzidi kutabasamu.


ENDELEA.


“Nakutuma Tanzania. Nenda kaishi huko, usirudi tena Marekani. Nenda katende yaliyomema kwa walio wema. Usithubutu kuangamiza kilicho chema. Na watakaojaribu kuangamiza kile kilichochema, basi ni ruhusa kwako kuwaangamiza au kuwapoteza.” Aliongea Daktari Ice huku kakamata mikono miwili ya yule mwanajeshi.


“Kwa nini Tanzania?” Akauliza yule mwanaume aliyeundwa na Ice.


“Ni kwa sababu ni sehemu salama kwako kuliko sehemu nyingine yoyote duniani.” Akajibu Daktari kwa Kiingereza.




“Sawa. Nitafanya hivyo mkuu.” Akajibu yule bwana kwa heshima.


“Huko utatumia jina la Idris Iris,” Aliongea hayo huku anapekua mkoba aliokuja nao na kutoa passport kadhaa za bwana yule zikiwa na jina hilo alilolitaja. “Kuna nyumba ipo Arusha, ramani yake ipo humu.” Pia akamuonesha diskette ambayo alisema ndimo ramani ilimo. “Na hizi,” Akamuonesha mfuko fulani, yule mwanaume akauvuta. “Ni nguo zako.” Ilikuwa ni suti nyeusi na yule bwana alizivaa kwa haraka kwa sababu bado alikuwa hana kitu mwilini.


“Ahsante Mkuu.” Alishukuru Idris Iris baada ya kupendeza ndani ya suti ya gharama katika dunia ya leo.


“Wewe ni mwanajeshi. Hata kama utavaa vazi la namna gani. Kumbuka hilo Idris. Komboa waliokuwa wema na teketeza wabaya. Nakuamini sana, nimekutengeneza kwa uwezo wa kipekee, unauwezo mkubwa kuliko hawa wengine. Kaikomboe dunia dhidi ya waonevu.” Aliongea Daktari na hapohapo akaanza kupanga vitu vyake. Na kwa haraka, akaanza kutoka na Idris ndani ya maabara ile.


Alifanikiwa kufika nje na kukwea ndani ya gari lake akiwa na Idris lakini wakati anataka kufunguliwa geti ili atoke ndani ya jengo lile kubwa, alikutana na upinzani toka kwa walinzi wakitaka kumjua Idris ni nani, na kwa nini atoke mle ndani wakati hakuingia naye.


Dokta alipoona hali imekuwa tete, akakanyaga mafuta ya gari lake na kugonga geti huku akiwaacha wanajeshi waliokuwa wakilinda lango lile kufyatua risasi kadhaa nyuma yake. Lakini kwa bahati mbaya, risasi hizo ziliinshia kwenye kioo kisichoingiza risasi kwenye gari lile.


Kwa tukio hilo, haraka taarifa zikapelekwa makao makuu ya wanajeshi wale pamoja na CIA. Walipokuja ndani ya maabara, kweli walikuta kuna mwanajeshi mmoja aliyekuwa bado hajawekewa C.O.D.EX katoweka na ni wazi Dokta Ice ndiye alihusika kufanya hivyo.


“Ni lazima Dokta Ice atafutwe na haraka sana amlete yule mwanajeshi hapa kabla ya masaa ishirini na nne hayajapita.” Alibwata mkuu wa kitengo kile cha C.O.D.EX. “Tuma C.O.D.EX Soldier 0ne and Two. Aidha Dokta na mwanajeshi wake waangamizwe, au waletwe wakiwa hai.” Alitoa agizo haraka yule mkuu na bila kuchelewa, wanajeshi wawili toka kwenye jokofu lenye maji, walitolewa na kuvishwa magwanda ya kijeshi kabla ya kupewa silaha za kijeshi na misheni ambayo walipaswa kwenda kuifanya.


“Waleteni wakiwa wazima, hasa daktari, huyo mwanajeshi, mnaweza kummaliza tu.” Aliongea jamaa mmoja mwenye mamlaka juu ya ile maabara na C.O.D.EX kwa ujumla. “Mnaweza kwenda.” Baada ya maneno hayo, wale wanajeshi wawili ambao sura zao hazikuwa na tabasamu wala aina yoyote ya furaha, walitoka ndani ya maabara ile huku wanakimbia kama wachezaji wa mpira wanaopasha misuli yao joto kabla ya mechi.


Safari yao iliishia nje ya maabara ile kubwa na walikuta ndege maalumu ya kisayansi ikiwasubiria nje. Nao waliipanda kwa haraka na ndege hiyo ikachoma mafuta na kupaa kwa kasi toka ndani ya maabara ile.


Ikiwa ni saa tisa ya alasiri, kwenye nyumba ya Dokta Ice, wanajeshi wale wawili wanavamia nyumba hiyo kwa kuingilia madirishani. Ilikuwa ni kimuhemuhe kwa sababu waliingia kwa kupasua vioo kwa kutumia miguu yao ambapo kwa huku juu walikuwa wamekamata kamba iliyowawezesha kuning’inia na kuingia ndani ya jengo la Dr. Ice kwa mbwembwe hizo.


Wakatua ndani na macho yao yaliypokuwa yamevikwa mawani myeusi, yalianza kuangaza huku na huko. Japo ulikuwa ni muda wa alasiri, lakini ndani mle mlikuwa na giza linaloweza kumfanya yeyote asiweze kuona kirahisi.


“Scan the house.” Sauti ilisikika kwenye masikioni mwao kuwataka wale wanajeshi waweze kuitizama ile nyumba kwa kina zaidi. Wakashika kwenye mawani zao, nazo zikatoa mwanga wa kijani. Wakaanza kutazama huku na huko kuona kama kuna kiumbe chochote kitakachoonekana.


“Scanning Detected.” Mawani ya mmoja wa wanajeshi, ikaandika maandishi hayo ikimaanisha katika tafuta tafuta kwa kutumia teknolojia ile, iliewenza kung’amua kitu aina fulani ya binadamu au mnyama.


Miwani hizo ni kwa ajili ya kuwatambulisha kitu wanachokitafuta hasa ikiwa ni chenye damu, nyama, karatasi maalumu ambayo ni lazima wapewe taarifa zake ndipo waziseti hizo miwani kwa ajili ya msako.


Mwanajeshi mmoja anapewa taarifa kuwa miwani yake imeona kitu ambacho kinamaumbile sawa na wanachokitafuta.


“Easy soldier.” Ilisikika sauti ya aliyewatuma ikimwambia taratibu. Naye mwanajeshi akawa anaenda kama ananyatia kitu kilisikimbie angali alikwishaingia kwa fujo ndani ya nyumba ya Dokta Ice. Miwani yake ikazidi ikaonesha kuwa inakaribia hicho kitu, nayo mikono ya mwanajeshi yule ikajikaza kwenye bunduki hatari aliyoikamata. Alifika sehemu hiyo na kunyanyua meza kwa nguvu na kuitupa pembeni. Hapo paka fulani mwenye mabaka akatoka mbio. Si kiongoi wao wala wale wanajeshi ambao hakushusha pumzi kali waliyokuwa wameibana.



“Shit.” Kiongozi aliyewatuma alitukana baada ya kuona sicho wanachokitafuta. Yule mwanajeshi akageuka nyuma tayari kwa kuendelea na msako ndani ya jumba lile lakini kwa mshtuko mkubwa, kitu toka juu ya dali kilidondoka na kumvaa mwanajeshi yule hadi bunduki yake ikadondokea mbali na yeye. Pale alipojaribu kuifata, kitu kile kilijirusha kwa sarakasi ya chinichini na kuipigia mbali bunduki ile.


Mwanajeshi mwingine alipokuja kutahamaki, alikuwa karibu na mtu mweusi ambaye alikwishaikamata vema bunduki yake na tayari kwa kuitoa mikononi mwake kwa sababu alikuwa anaing’ang’ania kwa nguvu huku akiivuta. Alikuwa ni Idris Iris, mwanajeshi mpya toka kwa Dokta Ice.


Mwanajeshi wa pili aliyekuwa kakamata vema bunduki yake akiwa hataki kabisa kuiachia, alijikuta akisukumwa hadi ukutani na kufanya ukuta huo utikisike kutokana na mtikisiko wa miili ile iliyokumbana. Wakati huo mwanajeshi wa kwanza aliyevamiwa toka juu ya dari, alikuwa anaenda kwa kasi nyuma yao na alipokaribia, alijikuta akisimamishwa mwendo wake kwa teke zito la kifuani ambalo lilimrusha hadi kwenye kochi mojawapo lililopo kwenye ile nyumba.


Macho ya Idris yakamuangalia mwanajeshi aliyekuwa anang’ang’ania bunduki, wote walikuwa hawana chembe ya huruma ndani yao. Ni Idris pekee ndiye aliyekuwa anaweza kupambana nao. Naye hakumchelewesha sana huyu ambaye shingoni alivaa cheni yake ya kijeshi yenye jina C.O.D.EX Soldier 1. Idris akamtwanga kichwa cha puani, Soldier One bado akawa hataki kuachia bunduki, na badala yake, alimgeuza haraka Idris na kumbamizia ukutani. Ile bunduki akaanza kuisogeza maeneo ya shingoni tayari kumkaba nayo hadi kumyonga kabisa.


Idris na Soldier One wakawa wanashindana nguvu, huyu anataka kumkaba, na huyu mwingine anazuia tendo hilo. Mwisho wake ulikuwa Idris kupiga mguu mmoja wa Soldier One kwa mguu wake wa kulia, nao mguu wa Soldier ukakubali kulegea. Ile bunduki ikamtoka Soldier na kubaki mikononi mwa Idris ambaye alimpiga teke zito la uso yule mwanajeshi aliyelega-lega hadi mawani yake ikadondokea pembeni.


Soldier One akamtazama Idris kwa macho ya kithirani, na Idris kuonesha yupo vema, akatupa bunduki ile pembeni na kukaa sawa kimapambano. Soldier One akasimama wima, naye Soldier Two toka kule alipodondokea, akajizoa zoa na kujiunga na mwenzake, naam, wakawa wanataka kumuonesha Idris kuwa wao si wa mchezo.


“Ngoja tujue yupi ni mwanajeshi imara.” Aliongea mkuu wa C.O.D.EX ambaye alikuwa akishuhudia mpambano ule moja kwa moja kupitia skrini kadhaa zilizokuwepo mle mjengoni ambazo ziliundwa na kuungwa kwenye kompyuta.


Idris akiwa tayari kwa mpambano ule, alianza kusogelewa na wale mabwana ambao walijaa miili yao kama wanyanyuao vitu vizito. Walipomfikia, walianza kumshambulia kwa mateke na ngumi kadhaa ambazo Idris kwa ustadi mkubwa alikuwa anazikwepa na nyingine kuzitolea nje. Alipoanza yeye kucheza zake, wale mabwana walijikuta katika hali mbaya ambayo kiukweli hawakutegemea kama kuna mwanajeshi anaweza kupigana kulikoni wao.


Idris aliruka angani na kisha miguu yake miwili ikaibana shingo ya mwanajeshi mmoja na mikono yake ikakaba shingo ya mwanajeshi mwingine. Idris akawa juu kwenye vichwa viwili. Akajipindua kwa nguvu na kuwafanya wale mabwana nao kupinduka naye na kisha wakajikuta wanabamiza vichwa vyao kwenye sakafu.


Ilikuwa ni vita vya kimyakimya. Hamna ambaye alikuwa analia kwa maumivu kwa sababu miili yao iliondolewa kabisa hali ya kuhisi maumivu. Ni damu pekee ndizo zilizoweza kuwatoka lakini hawakuthubutu hata kulia au kugugumia kwa maumivu.


Baada ya kubwaga chini, Idris alisimama na kupanda juu meza kubwa iliyopo mle ndani, na kisha kwa nguvu zake zote, alijirusha kama mwanamieleka na mwili wake kudondokea tumboni kwa Soldier Two ambaye naye alikaza meno yake kuonesha lile pigo limemuingia haswa.


Idris alipomuangalia Soldier One, alimuona akijivaa vaa taratibu ili asimame na hilo likawa kosa lake kwani Idris alimchota ngwara nzito na jamaa yule alirudi chini akidondokea kisogo na kabla hata hajajua la kufanya, soli ngumu ya kiatu cha Iris ilikita kwenye mdomo wake na kuzidi kumpoteza kabisa.


Akiwa kasimama katikati ya wanajeshi wale wawili. Alisikia mlio wa simu toka mle ndani. Kwa haraka akaanza kukimbia kuelekea dirishani na kupasua kioo kilichokuwa kimebakia baada ya kupasuliwa mara ya kwanza na wale C.O.D.EX soldiers. Akajitupa nje na hapo helikopta kubwa ilitokea angani lakini helkopta hiyo ilijikuta inapoteza muelekeo wa Idris baada ya mlipuko mkubwa kutokea kwenye nyumba ya Dokta Ice.


Akili zao zikawaza kuwapoteza wale wanajeshi wawili na kumsahau kabisa Idris ambaye alidandia pikipiki moja kubwa iliyokuwa nje ya geti la Dokta Ice. Akaingiza gia, na kuanza kutokomea toka eneo lile akiwaacha wale wababe wengine wakihaha ndani ya jumba la Dokta Ice.






Idris alipomuangalia Soldier One, alimuona akijivaa vaa taratibu ili asimame na hilo likawa kosa lake kwani Idris alimchota mtama mzito na jamaa yule alirudi chini akidondokea kisogo na kabla hata hajajua la kufanya, soli ngumu ya kiatu cha Iris ilikita kwenye mdomo wake na kuzidi kumpoteza kabisa.


Akiwa kasimama katikati ya wanajeshi wale wawili. Alisikia mlio wa simu toka mle ndani. Kwa haraka akaanza kukimbia kuelekea dirishani na kupasua kioo kilichokuwa kimebakia baada ya kupasuliwa mara ya kwanza na wale C.O.D.EX soldiers. Akajitupa nje na hapo helikopta kubwa ilitokea angani lakini helkopta hiyo ilijikuta inapoteza muelekeo wa Idris baada ya mlipuko mkubwa kutokea kwenye nyumba ya Dokta Ice.



Akili zao zikawaza kuwapoteza wale wanajeshi wawili na kumsahau kabisa Idris ambaye alidandia pikipiki moja kubwa iliyokuwa nje ya geti la Dokta Ice. Akaingiza gia, na kuanza kutokomea toka eneo lile akiwaacha wale wababe wengine wakihaha ndani ya jumba la Dokta Ice.


ENDELEA.


Safari ya Idris iligotea kwenye hotel moja ya kifahari Jijini New York. Akaingia huko na kuchukua lift ambayo ilimpandisha hadi ghorofa ya juu kabisa na huko alikutana na Dokta Ice ambaye muda mwingi alikuwa kasimama kwenye dirisha la chumba alichopanga.


“Unajua ni sababu gani nimekuachia wewe huru?” Dokta Ice aliongea baada ya Iris kuingia na kusimama kiheshima nyuma ya Ice.


“Hapana Mkuu.” Akajibu kikakamavu kama wafanyavyo wanajeshi.


“Ni kwa sababu dunia haina usawa kabisa. Dunia hii inamambo ambayo ukiingia kiundani, haitendi vile tunavyotaka itende.” Akaanza kwa hasira kidogo Dokta Ice. “Wametengeneza….. Hapana, tumetengeneza wanajeshi, lakini wanajeshi hawa ni kama silaha. Hawana huruma hata kidogo. Kabla hatujaingia wazo la kuwawekea chipu za huruma, wamewachukua baadhi ya wanajeshi na kuwapeleka huko wanapopajua. Huko kuna baadhi ya mateka wakiwa watoto na wanawake wameuawa kikatili sana na hawa wanajeshi. Mwenye roho kama mimi, siwezi kuvumilia. Nimekutengeneza wewe ili kidogo wafahamu kuwa nyie si silaha za maangamizi bali pia ni wokovu kwa wasiojiweza.” Alitabanainisha Dokta Ice.


“Umeoa Mkuu?” Akauliza swali ambalo Dokta Ice hakulitegemea. Akamuangalia mwanajeshi wake kisha akatabasamu kwa masikitiko.


“Yeah! Nilioa na nilipata mtoto mmoja wa kike lakini niliwapoteza kwa ajali ya gari miaka kumi iliyopita. Toka hapo sikuwa na haja ya kuoa tena.


“Ilikuwaje ukawapoteza kwa ajali na wewe ukabaki?” Akauliza tena Idris Iris.


“Ni kama wewe navyotaka kufanya. Nilikuwa nawatorosha kwa sababu CIA walikuwa wananiwinda sana kwa ajili ya kutengeneza upya folmura ya C.O.D.EX. Sasa ili niepushe familia yagu kuingia matatizoni, nikataka kuwahamisha na kuwapeleka Afrika.” Alihadithia Dokta Ice.


“Afrika. Tanzania tena au wapi?” Akamuuliza swali lingine.


“Ndio. Nilitaka kuwapeleka Tanzania kwa sababu kule pana amani na wanaurafiki mkubwa na nchi zenye nguvu duniani hivyo kama Marekani wakiamua kuwapiga Watanzania, wajue watakuwa vitani na Cuba, China, Urusi na nchi zote za ujamaa.”


“Ajali ilikuwaje?” Akaendelea na maswali Iris.


“Mke wangu ndiye alikuwa dereva. Mimi nilimwambia akimbie na nikabaki nawazubaisha CIA kwa gari lingine. Walipogundua kuwa mke wangu anakimbilia uwanja wa ndege, ndipo wakatuma helikopta ambayo iliifutilia mbali familia yangu kwa kuizinga kwa taa zake na kisha kulipotezea muelekeo gari alilokuwa anaendesha mke wangu. Likaingia darajani na kupinduka huko. Likawaka moto na baadae kulipuka.”


“Mwanao alikuwa na miaka mingapi kipindi hicho?” Swali lingine toka kwa Idris. Dokta akamtazama kwa macho ya masikitiko kisha akamtaka mwanajeshi wake akae kwenye kitanda cha hotel ile.


“Alikuwa na miaka tisa pekee,” Dokta Ice akamjibu na kisha akaendelea. “ Hamna kitu kinachouma kama kumpoteza mtu au watu unaowapenda. Hadi leo inaniuma sana. Nilitaka kujivika roho ya kikatili na kulipa kisasi kwa watu ambao hawana hatia, lakini moyo umekataa kabisa baada ya kushuhudia mauaji ya kutisha ya kule Iraq kwa wale mateka.


“Samahani na pole kwa hilo mkuu. Lakini swali la mwisho, mkeo yeye alikuwa anafanya kazi gani?” Akaulizwa tena.


“Alikuwa ni daktari mwenzangu. Baada ya mimi ni yeye. Hata hii folmura ya C.O.D.EX ni mimi na yeye ndio tuliijenga lakini kulikuwa na kashikashi fulani ambazo zilinifanya nitake kumtorosha mke wangu. Hapo ndipo yakatokea yaliyotokea.” Akajibu swali kwa ufasaha kabisa Dokta Ice.


Macho ya Idris yakaonesha yanajambo la kutaka kuongea lakini hakutoa nafasi ya kuyatoa ambayo kayahisi toka moyoni mwake.


Japo Idris Iris alikuwa ni mwanajeshi wa kutengenezwa, lakini yeye aliumbwa kiufasaha sana na Dokta Ice. Yeye aliweza kuhisi yale ambayo kila binadamu anaweza kuyahisi. Lakini yeye hakuwa sana na binadamu kwa sababu alikuwa na kiruhusuji au activetor maalumu ya kulipua mabomu ya nyuklia. Mbali na hapo, yeye hakuwa sawa na wale wanajeshi wengine ambao wanaweza kuungua mavazi pekee. Yeye aliweza kuungua hadi kuisha kabisa mwili wake na kubaki vyuma fulani vilivyopandikizwa mwilini mwake kwa kemikali za C.O.D.EX ambazo ndizo zinamfanya aungue mwili mzima na baadae kemikali hizo, huanza kuujenga mwili wake kwa kutengeneza ngozi mpya. Tendo hilo huchukua dakika moja pekee.


“Unatakiwa kuondoka usiku huu Idris. Utashukia Dar es Salaam. Na hapo utakuta ndege maalumu kwa ajili yako, nayo itakupeleka hadi Arusha. Huko napo utakuta gari maalumu kwa ajili yako, nalo litakuchukua hadi kwako. Huko ishi kwa amani.” Aliongea Dokta Ice huku akikusanya baadhi ya vitu na kutumbukiza kwenye mkoba maalumu wa nguo.


“Kwa nini mimi lakini?” Akauliza Idris.


“Ukifika sehemu yoyote, fungua kompyuta hii, kisha tazama mafaili pamoja na video kadhaa ambazo zipo humo. Sina muda wa kukuhadithi kila kitu kwa sasa. Muda si mrefu C.O.D.EX wanatuvamia hapa.” Alijibu Dokta Ice na kulazimika kuanza kumzoa zoa Idris ili waondoke mle ndani.


Bomu lililolipuka nyumbani kwa Dokta Ice, ni bomu ambalo lilitegwa na dokta huyu mwenyewe. Ni bomu la kawaida ambalo halikuwadhuru wale wanajeshi. Hivyo baada ya kuokolewa, wale wanajeshi walipewa mavazi mapya tayari kwa kurudi kuwasaka Ice na Iris.


****


Saa mbili usiku, gari moja la kifahari lilisimama kwenye jiji la maraha nchini Marekani. Jiji la Las Vegas. Lakini kwa bahati mbaya gari hilo halikuwa limekuja kushangaa raha za Las Vegas na badala yake, alishuka Idris na Ice na kisha kuchukua treni ya umeme ambayo iliwapeleka hadi uwanja wa ndege. Huko Idris aliagana na Dokta Ice ambaye baada ya kuhakikisha kuwa mwanajeshi wake amekwishakwea ndege, akarudi haraka kwenye treni inayorudi mjini ambapo alliacha gari lake.


Idris akiwa katulia ndani ya ndege kabla haijaanza kuondoka, alichungulia nje kwa mara ya mwisho kabla ya kuanza safari ya kuiaga Marekani.


“America, Land of Opportunities. Godbless America. (Amerika, nchi/ardhi ya bahati/nafasi. MUNGU ibariki Amerika)” Idris aliongea maneno hayo akimaanisha kuwa Marekani ni nchi ya bahati au nafasi. Yaani alimaanisha kuwa, yeyote atayeishi Marekani basi anauwezo mkubwa wa kutoka kimaisha. Kifupi, nchi ya Marekani kama ukijishughulisha, basi unauhakika wa kuishi kama mfalme. Hamna ambaye anajishughulisha Marekani kisha awe fukara. Idris alilitambua hilo.


Baada ya nusu saa, ndege ilikuwa angani na Idris aliamua kutoa kompyuta mpakato aliyokabidhiwa na Dokta Ice. Akaifungua na kisha alianza kusoma mafaili kadhaa yaliyomo humo lakini kwa bahati mbaya, hakuwa akielewa ni nini hasa yalikuwa yanamaanisha. Akaamua kufungua video zilizomo humo, huko ndipo alipotulia na kuanza kuumia moyo wake.


“Happy Birthday to you… Happy Birthday To You…. Happy Birthday Dear Best, Happy Birthday To You.” Wimbo huo ulikuwa unaimbwa na watu kadhaa huku mwanaume mmoja mwenye nywele nyingi akiwa kakamata keki akielekea ilipokuwa meza kubwa.


Wakati anaelekea huko kwenye meza, mchukua video ile alianza kuwachukua watu waliokuwa wamehudhuria kwenye sherehe ile ya siku ya kuzaliwa.


Mama mmoja mwenye asili ya weusi, alionekana mwenye furaha sana na mchukua video alikuwa anamchukua kwa makini zaidi kwani mama yule alienda mahali hadi alipokuwa amekaa mtahiniwa wa sherehe ile. Hapo Idris akashtuka baada ya kumuona mtoto aliyekuwa anasheherekea miaka yake mitano ya kuzaliwa.


Alikuwa ni mtoto mweusi kama mama yake. Na kilichomfanya ashtuke ni ule muonekano ambao ulionekana kama yeye. Japo yeye alikuwa mkubwa kulikoni yule kwenye video, lakini hakutilia shaka kabisa kuwa yule kafanana naye. Akabonyeza stop na video ile ikasimama.


“Huyu ni mimi, lakini anaitwa Best, na mimi ni Idris.” Akajiwazi na kwa haraka akafungua mafaili ambayo hapo mwanzo aliyafunga kwa sababu hakuyaelewa.


“Best Boucher. Kazaliwa tarehe….” Akaanza kusoma yale mafaili kwa makini zaidi.


Baba yake Dokta Boucher, alikutwa kajinyonga ndani ya chumba chake baada ya kumuua mkewe. Mtoto wao alikutwa kajificha kwenye zizi la farasi na jukumu la kulelewa alipewa Dokta Ice ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Dr. Boucher.


Best alipotimiza umri wa miaka kumi na saba. Alipotea katika mazingira ya kutatanisha na baadaye taarifa zilitoka kuwa amekutwa kwenye fukwe za Miami amefariki.


Ni kifo cha utata sana kwa sababu Dokta Ice hakuwa tayari kufanya mazishi hayo wala kutaka maiti ionekane. Na yeyote aliyethubutu kuhoji kuhusu mwili wa Best, alipewa kilema cha maisha na watu wasiojulikana.


Katika vifo vya Dokta Bouncher na Mkewe ambaye alikuwa ni Mwanasheria, iligundulika kuwa mke wa Bouncher hakuuawa na mumewe na wala mumewe hakujinyonga. Mwili ulivyopimwa, kulikutwa na sumu kali sana ambayo leo hii wanaiita C.O.D.EX. Kemikali hii kwa maiti huwafanya wazinduke na kuwa watu wenye nguvu sana, lakini kwa wale wazima huwapotezea uhai wao haraka sana kwa kuwatoa damu kwenye kila tundu linalopatikana kwenye miili yao.


Mtu aliyefanya uchunguzi huo alikutwa maiti ndani ya ofisi yake na taarifa hizi zilizuka miaka mitano mbele kwa mtoto wa yule aliyefanya uchunguzi kuziweka hadharani. Naye hakuchukua muda, akapigwa risasi siku moja wakati anatoka mahakamani kusimamia kesi ya mtuhumiwa fulani huko Marekani.


Vifo vya familia ya Boucher vilijaa utata pekee na kila aliyejaribu kuvifuatilia alikutwa anakilema cha maisha au mfu. Hata mawakili wakubwa duniani, walikwishakataa kuzungumzia kesi ya Bouncher.


Idris akaendelea kuyasoma maelezo muhimu ndani ya mafaili yale ya kwenye kompyuta. Aliporidhika, akarudi kwenye video zilizopo. Akafungua video nyingine iliyokuwepo mbele ya kioo cha kompyuta.


“Dokta Ice. Tunakaribia kupotezwa. Mimi na familia yangu tunapotezwa muda si mrefu. Naomba umtunze mwana wetu. Nakuomba Dokta. Ukumbuke pia ile formula mpya C.O.D.EX.” Video hiyo iliongea hayo na picha ya Boucher ilionekana akiwa na wasiwasi mwingi sana, kwani aliangalia huku na huko wakati anayaongea hayo. “Nimemficha mwanangu kwenye zizi la farasi, utamkuta huko. Mlee vema kama…..” Hakumaliza maneno yake Dokta Bouncher, mlango wa nyumba yake ukafunguliwa kwa kishindo cha bunduki.


Kwa haraka akakimbilia kwenye kabati moja lililomo mle ndani na kufungua kisha akatoa gobole, lakini alikuwa amekwisha chelewa sana. Mwanajeshi mmoja mkubwa wa mwili alikuwa nyuma yake, na Bouncher alipogeuka tu! Akakuta na kabali nzito na kunyanyuliwa juu huku akiliachia gobole lake na kuanza kutapatapa.


Hayo yote yaliendelea kuonekana kwenye video ambayo ilikuwa inacheza kwenye kompyuta mpakato ya Idris.






“Dokta Ice. Tunakaribia kupotezwa. Mimi na familia yangu tunapotezwa muda si mrefu. Naomba umtunze mwana wetu. Nakuomba Dokta. Ukumbuke pia ile formula mpya C.O.D.EX.” Video hiyo iliongea hayo na picha ya Boucher ilionekana akiwa na wasiwasi mwingi sana, kwani aliangalia huku na huko wakati anayaongea hayo. “Nimemficha mwanangu kwenye zizi la farasi, utamkuta huko. Mlee vema kama…..” Hakumaliza maneno yake Dokta Bouncher, mlango wa nyumba yake ukafunguliwa kwa kishindo cha bunduki.


Kwa haraka akakimbilia kwenye kabati moja lililomo mle ndani na kufungua kisha akatoa gobole, lakini alikuwa amekisha chelewa sana. Mwanajeshi mmoja mkubwa wa mwili alikuwa nyuma yake, na Bouncher alipogeuka tu! Akakuta na kabali nzito na kunyanyuliwa juu huku akiliachia gobole lake na kuanza kutapatapa.


Hayo yote yaliendelea kuonekana kwenye video ambayo ilikuwa inacheza kwenye kompyuta mpakato ya Idris.


ENJOY.


Dokta Bouncher aliendelea kutapatapa pale alipokuwepo hadi akatulia kabisa ndipo lile bwana lilipomuachia. Baada ya hapo, likaanza kuangaza huku na huko na ndipo macho yake yakaelekea kwenye kompyuta ambayo bado ilikuwa inaendelea kuchukua tukio zima lililokuwa linaendelea ndani ya nyumba ya Dokta Bouncher.


Mwanajeshi yule alianza kwenda taratibu kwenye ile kompyuta na kisha akaanza kuikagua taratibu huku bado inaendelea kunakili kila kitu. Wakati anazidi kukagua, mara ukasikika mlio mkali wa bunduki na hapohapo yule mwanajeshi aliinama chini kwa maumivu na kitendo hicho cha kuinama, kikatoa nafasi kwa yule aliyefanya tendo lile kuonekana. Alikuwa Mama wa Best, Mke wa Dokta Bouncher akiwa kakamata gobole ambalo mumewe aliligwaya baada ya kupokea kabali nzito ya Mwanajeshi asiye na huruma. Mama yule akafyatua risasi nyingine na mwanajeshi yule alisikika akilia kwa uchungu zaidi.


“Mbwa wewe.” Mama yule aliongea kwa kithilani baada ya kufika chini alipolala yule mwanajeshi na maneno hayo yakafuata na mlio mkali mwingine wa bunduki. Kimya kikatanda.


Mama Best, mke wa Dokta Bouncher. Alijulikana kama Jesabel Amour. Ni raia wa Brazil. Kasomea sheria Marekani na baada ya hapo akaolewa na Dokta Ice ambaye alikutana na mwanamama huyu kwenye harakati za kuwakomboa waathirika wa tetemeko huko Haiti. Mmoja alikuwa Daktari wa Marekani, na mwingine alikuwa ni Mwanasheria aliyekuwa mafunzoni (field). Mapenzi yakawaka kuanzia hapo na siku hiyo, Jesabel, anapukutisha mwanajeshi aliyemuua mumewe.


Baada ya milipuko kadhaa na sauti ya mwanajeshi kupotea kwenye chumba kile, Mama Best, au Jesabel Amour. Anachukua kompyuta ile haraka na ikiwa vilevile bado inarekodi, anaiweka juu ya pambo moja ambalo lipo chumbani na lilikuwa limekamata taa zipatazo nne. Pambo hilo lilikuwa katikati ya dari, na alipoiweka kompyuta hiyo, ikakaa vizuri bila shida na kwa bahati nzuri, iliweza kumuelekea yule mwanajeshi ambaye alikuwa kapukutishwa na Jesabel. Alikuwa kafumuliwa kichwa vibaya sana na kifua chake kilikuwa kimelowana damu pekee. Ni wazi alikuwa kakiona cha moto toka kwa mwanamke jasiri wa Kibrazil.


Baada ya dakika kadhaa, sauti ya mwanamke ilisikika ikilia kwa nguvu nje ya chumba kile. Na baada ya muda kidogo, sauti hiyo ilisikika ndani ya chumba kilekile ambacho Dokta Bouncher na Mwanajeshi walikuwa maiti. Vishindo vya haraka vikasikika na mara watu wawili walionekana kuufuata mwili wa yule mwanajeshi na kuanza kuuchunguza.


Kwa hasira bwana mmoja alibwata na ghafla kwenye kitanda ambacho nacho kilikuwa kinaonekana kwenye ile kompyuta iliyokuwa inachukua tukio zima, Jesabel alirushwa na kudondokea hapo. Kisha yule bwana aliyebwata baada ya kuona mwanajeshi wake kauawa, akachomoa mkanda wa suruali kisha akaanza kumtandika mwanamke yule kwa hasira nyingi sana. Kilio kilikuwa kikubwa lakini hakukuwa na msaada wowote ule.


Damu zikawa zinamtoka mwanamama yule. Na yule bwana baada ya kuridhika na kipigo chake alichokitoa, alionekana akitoa ishara kule alipotekea kabla ya kwenda kumuona mwanajeshi wake.


Dakika moja mbele, yule bwana mwenye mkanda akatoka eneo lile, na hapohapo akatokea mwanajeshi mwingine mkubwa na huyu alikuwa anaasili ya weusi kwenye ngozi yake. Akasimama pembeni ya kitanda ambacho Jesabel alikuwa amelala. Yule mwanajeshi mweusi alijipekua nyuma ya mgongo na kisha akatoa panga moja refu kama yale wanayomiliki Yakuza (Kundi la Mafia la Japan). Mwanajeshi yule akiwa hana chembe ya huruma, alishusha panga lake kwenye shingo ya Jesabel na damu nyingi zikaruka na kuchafua mashuka ya kitanda chote. Mama yule alinyanyua miguu yake juu kabla hajaishusha na mwisho wake ukawa hivyo.


“Huyo Dokta mtoeni humu, kamtundikeni chumbani kwake.” Sauti ya yule bwana aliyemchapa Jesabel kwa mkanda, ilisikika na dakika hiyohiyo, mburuto ulisikika kabla ya yule mwanajeshi hajaja na kumchukua mwanajeshi wake na baadae kurudi tena na kuanza kusafisha damu za yule mwanajeshi Ili kupoteza ushahidi.


Video iliendelea kuonesha maiti ya Jesabel kwa dakika kama kumi. Na Idris aliendelea kuangalia sura ya mwanamke yule huku akiwa haamini kama kuna watu wakatili namna ile duniani.


Baada ya dakika hizo, ilisikika sauti ya mtu ikibishana na watu nje ya chumba hicho. Idris akashtuka na kuzidi kutega sikio lake.


“Nimesema sitaki mtu ndani ya chumba hichi. Nitafanya mlichoniambia lakini si kwa kupelekeshwa, hamtaki, na mimi niuweni tu.” Ilifoka sauti hiyo kwa lugha ya Kiingereza.


“Okay. Fanya unachoweza. Ila hakikisha hamna ushahidi.” Sauti ya bwana wa kuchapa kwa mkanda ikasikika.


Baada ya hapo, mtu akaingia kwenye chumba kile ambacho kilifanyika mauaji na sauti ya mlango kufungwa na baadae kusikika funguo nayo kufunga, vikasikika. Bado kompyuta iliendelea kuchukua matukio yote. Alikuwa kavaa suti nyeusi, na alipofika pembeni ya kitanda, alisimama kwa muda akiwa kainama jambo ambalo lilifanya ile kompyuta isiweze kuona uso wake vema.


“Jesabel dada yangu. Samahani sana dada yangu. Najua ulinipenda kama kaka yako, lakini nimeshindwa kukutetea dada yangu. Umeondoka na kaka yangu kipenzi. Hakika sitawasahau maishani mwangu. Ipo siku watakuja kulipa haya yote.” Maneno hayo aliyatoa yule bwana mwenye suti na yalikuwa yanasikika vema kwenye masikio ya Idris.


Sauti ile aliijua vema na alitamani sana mtu yule ainue uso wake aweze kumjua.


Bwana yule akafungua mkoba aliokuja nao na kutoa vitu fulani na kuvivaa mikononi. Kisha akachukua kitambaa na kuanza kufuta maeneo yote yaliyokuwa wazi. Kila kitambaa kilipokuwa kinalowa damu, alitumbukia kwenye kikopo kimoja ambacho kilikuwa na kimiminika kilichokuwa kinamwaga povu kila kitambaa kikiwekwa humo. Mwili wa Jesabel ukawa safi baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa wazi kama miguuni, mapajani, mikononi na usoni.


Baada ya zoezi hilo, yule bwana alitoa vitu vingine kwenye mkoba na kuanza kuvipaka kwenye mwili wa Jesabel kwa uangalifu zaidi.


“Nadhani hizo ni alama za Bouncher. Na ndio maana yasemekana yeye ndiye aliyemuua mkewe. Lakini yawezekana hiyo aliyomfutia ni kemikali ya C.O.D.EX na ndio maana ukazuka utata mwingine baadaye.” Aliongea peke yake Idris huku akiwa na shahuku ya kutaka kujua ni nini kiliendelea.


Baada ya kupakapaka sehemu za mwili ambazo alizifuta, yule bwana aliyetumwa kufanya hivyo, akatoa kichupa kingine na kukiminya. Damu zikaruka maeneo yale aliyoyafuta. Akameza funda kubwa kukubaliana na kile alichokifanya.


Akasimama pembeni kuangalia kazi yake. Akaona ipo sawa. Akainama kuonesha kutoa heshima yake ya mwisho. Na baada ya hapo akageuka na kuanza kuangaza huku na huko na kwa bahati mbaya au nzuri, uso wake ukatizama juu ya pambo ambalo ile kompyuta iliwekwa na Jesabel.


“Dokta Ice?” Akajiuliza kwa mshangao mkubwa Idris Iris.


****


Baada ya kutoka Jijini Vegas kumsindikiza Idris, Dokta Ice anaamua kurudi kwenye nyumba yake ya siri iliyopo Los Angeles. Alichukua siku moja tokea usiku aliomsindikiza Idris hadi usiku uliofuata, ndipo anafika Los Angeles kwa kutumia gari lake lililokuwa linauwezo mkubwa wa kusafiri kwa umbali mrefu bila kupoteza ubora wake.


Nyumba aliyokwenda, ni nyumba ambayo alikuwa anapenda sana kwenda kuvinjari na mkewe siku za mapumziko na sherehe mbalimbali. Aliweka mlinzi mmoja ambaye aliishi kwenye nyumba mojawapo ya nje lakini akiwa na mitambo kadhaa ya kuangalia watu wanaokuja na kutoka.


Dr. Ice anakwenda katika nyumba hiyo na kumkuta mlinzi wake akiwa katika uangalizi mzuri kabisa. Wanasalimiana na Dokta anaingia ndani kwake na kuanza kufanya uchunguzi mdogo hasa wa usafi. Anaona pako sawa, anawasha runinga iliyopo humo kabla hajachukua jukumu la kwenda kuweka mwili wake safi na kisha kurudi sebuleni ambapo anapata wasaha mwanana wa kupata chakula cha usiku.


Saa nane usiku akiwa kalala, anasikia kurupushani nje ya nyumba yake jambo linalomfanya ainuke na kwenda kuchungulia dirishani upande ule ambapo anasikia kurupushani hizo. Hapo anashuhudia mlinzi wake akivutiwa gizani akiwa kalegea na baadae wanajeshi wenye mavazi meusi na pua na midomo yao ikiwa imezibwa na maski, wanaonekana na mitutu yao ya bunduki ikiwa mbele.


Dokta Ice anawahi kwenye kabati lake na kuchukua maski ambayo kwa pembeni kulikuwa na vichupa viidogo vya gesi ya oksijeni. Anavaa haraka kabla hajasikia kioo cha dirisha lake kikivunjwa na bomu la machozi kudondokea ndani. Moshi wa hatari unaanza kutapakaa mle ndani.


Dokta Ice anaenda chumba kingine na kufungua kabati moja kubwa la nguo. Huko anapekua hadi nyuma ya nguo zilizopo na kushika kitasa ambacho anakiminya na kufunguka. Anaingiza kichwa chake na baada ya dakika kadhaa, anatoka na bunduki moja kubwa na boksi la risasi ambazo zilikuwa na kimiminika ndani yake.


“Pumbavu hawa, nimewaunda mwenyewe, hawanizuii kuwafanya lolote. Ngoja niwaoneshe.” Akaongea kwa hamasa Dokta Ice huku akiijaza bunduki yake zile risasi zenye kimiminika cha rangi ya kijani.


Baada ya tendo hilo, Dokta Ice, anaelekea sebuleni huku bado akiwa na maski yake na moshi ukizidi kutumwa toka kwa wale wanajeshi waliopo nje.


Anafungua mlango fulani ambao upo kwenye ‘silling board’ ya sebuleni, mlango ule unafunguka na ngazi moja inashuka ambayo Dokta Ice anaipanda na kuingia juu ya paa la nyumba yake. Anaelekea sehemu moja ambayo ilikuwa na dirisha dogo kiasi lakini lenye uwezo wa kuona eneo kubwa lililopo pale nje. Anashuhudia wale mabwana wakiwa wamejipanga kwa mstari na bunduki zao za mabomu ya machozi.


Anaikoki bunduki yake na kuipitisha kwenye dirisha lile dogo. Anachukua shabaha kwa kumlenga mmoja wa wanajeshi wale kwenye jicho. Anaachia risasi na inamkuta yule bwana kwenye jicho kama alivyodhamiria. Mwanajeshi anadondoka chini na kuanza kulia huku taratibu ngozi yake ikianza kuchubuka na nyama kuanza kumwagika ardhini. Ilikuwa ni picha ya kutisha pale wanajeshi wengine walipokuwa hawaamini kama mwenzao anakufa. Sekunde pekee zilitosha kumgeuza yule bwana majivu kwani kemikali za risasi zile zilikuwa harari sana.


“Nadhani mmeshuhudia kifo cha mwenzenu, nanyi mtakufa vivyo hivyo.” Dokta Ice aliongea na kuachia risasi nyingine ambayo ilimbabatiza mwanajeshi mwingine pembeni ya kichwa chake.








Anaikoki bunduki yake na kuipitisha kwenye dirisha lile dogo. Anachukua shabaha kwa kumlenga mmoja wa wanajeshi wale kwenye jicho. Anaachia risasi na inamkuta yule bwana kwenye jicho kama alivyodhamiria. Mwanajeshi anadondoka chini na kuanza kulia huku taratibu ngozi yake ikianza kuchubuka na nyama kuanza kumwagika ardhini. Ilikuwa ni picha ya kutisha pale wanajeshi wengine walipokuwa hawaamini kama mwenzao anakufa. Sekunde pekee zilitosha kumgeuza yule bwana majivu kwani kemikali za risasi zile zilikuwa harari sana.


“Nadhani mmeshuhudia kifo cha mwenzenu, nanyi mtakufa vivyo hivyo.” Dokta Ice aliongea na kuachia risasi nyingine ambayo ilimbabatiza mwanajeshi mwingine pembeni ya kichwa chake.


ENJOY.


Naye aliweza kufa kwa kifo sawasawa na cha yule mwenzake. Mwanajeshi aliyebakia akawa hana la kufanya zaidi ya kuangalia kule risasi zinapotoka. Kwa macho yake ambayo yalikuwa na kitu kama darubini, yalieweza kumuona Dokta Ice akibonyeza kifyatulio cha bunduki yake. Naye bila kupoteza muda, risasi ya kichwa pia iliingia kwenye paji lake la uso. Kifo kibaya kikashirikishwa kwenye maisha yake.


Kosa kubwa ambalo Dokta Ice alilifanya, ni kumuachia yule mwanajeshi amuangalie kwani baada ya kuonekana kwenye macho ya yule bwana, taarifa zilifika haraka makao makuu ya C.O.D.EX Soldiers na hapohapo kupitia satelaiti, walituma taarifa hizo kwa wale waliowaleta wale wanajeshi. Ndipo mwanajeshi mwingine aliweza kutuma mionzi mikali ya bunduki yake na kusambaratisha nyumba ya Dokta Ice. Wakati mwanajeshi yule amesimama tayari kwa kutuma mionzi yake ambayo ilikuwa ni hatari sana. Ni mionzi iliyotengezwa kwa madini ambayo yanapatikana chini ya bahari. Dokta Ice aliweza kumuona na alijua tayari yupo kwenye hatari. Hali hiyo ikimfanya Ice kutoka kule juu na kujitupa hadi chini na kulala ili mlipuko ule uliokusanyika na moto mkubwa usiweze kumfikia.


Baada ya kimya kidogo. Dokta Ice aliinua kichwa chake na kutaka kusimama lakini alishindwa kusimama kwa sababu ya kuhisi maumivu makali kwenye miguu yake. Tokea kule juu aliporuka hadi chini, ulikuwa umbali mrefu sana japo yeye mwenyewe aliona kawaida sana kwa sababu alikuwa anajitahidi kuokoa roho yake.


“Upo chini ya ulinzi.” Mwanajeshi mmoja aliongea huku kamuelekezea Dokta Ice bastola yake.


“Usimuue. Tunamuhitaji.” Sauti ilisikika kwenye masikio ya yule mwanajeshi na bila mchecheto, akarudisha bastola yake kiunoni na kumnyanyua Dokta Ice kwa nguvu na kuanza kwenda naye kwenye gari ambalo sasa lilibakiwa na dereva tu.


Akamsukumia Dokta Ice nyuma ya gari lile na kufunga mlango vema ili mtuhumiwa wao asitoroke wala kuleta shida njiani. Safari ya kuanza kurudi New York ikaanza.


****


“Dokta Ice, karibu tena New York.” Sauti ilisikika na bwana mmoja mwenye suti matata sana alioongea baada ya Dokta Ice kufumbua macho yake na kujikuta yupo kwenye kiti ndani ya ile maabara aliyokuwa anafanyia kazi.


“We’ ni mjinga Uzo. Ni mjinga sana. Unadhani unaweza kusimamisha nilichokiwaza?” Dokta Ice aliongea na wakati huo mtu aliyemuita Uzo, alikuwa anakagua jeshi lake lililokuwa kwenye jokofu. Alikuwa kakamata Ipad yake ya kufanyia kazi.


“Si hivyo Dokta Ice. Na wala siwezi kukukwamisha ulichoanza, ila….” Uzo aliongea kwa kejeli huku anaenda pale alipokuwa amekalishwa Dokta Ice. “Wapo ambao watafanya hivyo.” Akaongezea huku uso wake akiusogeza karibu kabisa na Dokta Ice.


“Unajidanganya. Mimi ndiye alpha na omega kwenye kutengeneza hiyo kemikali na kuifanya iwe bora zaidi. Nilioshirikiana nao, wote mliwaua. Bado mimi ni jiwe la pembeni.” Akaongea pia Dokta Ice.


“Una uhakika Ice?” Akauliza Uzo huku ametabasamu.


“Unauliza maembe Tanzania mwezi wa kumi mbili?” Naye akajibu kwa kejeli.


“Inaonekana unapajua sana Tanzania. Hamna kitu wale, tukiamua kuiangamiza ni dakika tano tu. Ila sipo huko, nilikuuliza kama unauhakika na kauli yako. Tatizo ni kwamba hujui unalolizungumza. Hamna alpha wala omega duniani. Labda Shetani na MUNGU. Napo vita yao ni lazima mmoja akubali kupigwa. Je ni nani? Shetani au MUNGU. Na wewe upo upande gani hadi sasa? Kwa MUNGU ama Shetani?” Akatulia kidogo huku bado macho ya Dokta Ice yakimtazama kwa uchu. “Hata hivyo sipo huko, nataka nikutambulishe kwa mrithi wako.” Baada ya maneno hayo, akaoneshea mkono kwenye mlango wa kuingilia ambao ulikuwa nyuma ya Dokta Ice. Nao mlango ukafunguliwa jambo lililofanya Dokta Ice kugeuka kuona anayeletwa.


Macho yakamtoka pima akiwa haamini kile anachokiona nyuma yake kinakuja pale mbele.


“Simeria?” Akaita kwa sauti ya chini Dokta Ice.


“Ndiye Simeria. Mkeo wa zamani, Ice.” Uzo akamwambia Dokta Ice wakati mwanamama aliyeitwa Simeria akisogea upande wake wa kushoto na kusimama. “Lakini sasa, si mkeo tena.” Akamgeukia Simeria, naye yule mwanamke akamgeukia na kupeana ndimi zao kwa sekunde kadhaa kitu kilichomfanya Dokta Ice kutaka ardhi ifunguke naye aingie, kisha ijifunge naye afie huko.


“Nini kimekubadilisha Simeria?” Akauliza kwa uchungu Dokta Ice.


“Hamna. Ni maisha tu! Nilitakiwa kuwa nawe ili yatimie haya. Umenifundisha folmura nyingi sana. Na sasa ni muda wangu kwenda nazo.” Akajibu Simeria.


“Kwa hiyo mapenzi yote yale, yalikuwa ni maigizo?” Akauliza tena na Uzo alikuwa kimya wala hakutaka kuingilia ule ugomvi.


“Heri yawe maigizo ya kutisha ama ya mapenzi, tunaweza kukumbwa na hisia za kweli. Lakini hayakuwa maigizo hayo, bali yalikuwa maigizo ya vichekesho. Yaani unaweza kufa, mtu asiamini kama umekufa kwa sababu ni ucheshi.” Akajibu Simeria na kumfanya Ice kusikitika. “Una swali lingine kabla hujafa?” Akauliza tena Simeria lakini Dokta Ice alikuwa kimya kainamisha kichwa chake asijue aulize nini. “Baby,” Simeria akamuita Uzo.


“Naam, honey.” Akaitika yule mwanaume mwenye umri kati ya miaka arobaini hadi arobaini na sita.


“Huyo ni wenu. Naomba nianze kazi yangu.” Akaongea yule mwanamama ambaye naye si haba. Licha ya kuwa na umri kati ya miaka thelathini na sita hadi arobaini, lakini alikuwa kama msichana wa kileo kutokana na mavazi pamoja na mikwatuo aliyokuwa anajikwatulia.


“Okay baby.” Uzo alimuitikia na kisha mwanamke yule akajipeleka na kukutanisha ndimi zao tena kwa mahaba makubwa hadi baadhi ya walinzi wakawa wanaona aibu kuwaangalia. Walipomaliza tendo hilo la aibu, Simeria akaanza kuelekea kule ilipo mitambo.


“Simeria.” Akaitwa na Dokta Ice. Mwanamke yule akageuka na kurudi tayari kwa kumsikiliza.


“Merice….” Akalitaja jina hilo kwa kigugumizi. Ni wazi alitaka kuuliza lakini hakutaka kupata majibu anayoyafikiria.


“Merice nini? Mbona humalizii sentensi?” Akauliza kwa ngebe Simeria.


“Merice, mtoto wetu. Naye yuko wapi?” Ikambidi amuulizie mwanaye pekee wa kike ambaye inasemekana alikufa kwenye ajali mbaya ya gari akiwa na mama yake, lakini mama yake kaonekana, je mwanaye?


Simeria akamsogelea Dokta Ice hadi wakakaribiana nyuso zao.


“Si mwanao tena.” Akaongea maneno hayo na kuchapa vidole vyake na kutoa sauti kama ya kuita kitu fulani kije. Ndipo mlango ukafunguliwa na akatokea mwanamke mmoja mrefu na mwenye nywele mwanana akiwa kavalia mavazi ya kijeshi. Dokta Ice akawa kakodoa macho yake asiamini kile anachokiona.


“Umemuharibu hata mwanao wa kumzaa Simeria?” Aliongea Dokta Ice baada ya kushuhudia uso wa Merice ambaye naye alikuwa katika muonekano wa kutocheka wala kutambua lolote kuhusu wazazi na watu wengine.


“Ni wako huyu Uzo.” Simeria badala ya kuongea na Dokta Ice, akamruhusu Uzo, yule mwanaume wake mwingine afanye anachoweza kumfanya Dokta Ice. Naye Uzo bila haya, wakati Simeria anaondoka eneo lile, akampiga kofi kwenye makalio yake na mwanamke yule alitabasamu kana kwamba kile ni kitendo cha kawaida sana.


“Watakuua tu siku moja Simeria. Kama ulivyoniua mimi.” Dokta Ice aliongea lakini Simeria hakujibu lolote bali kupotea kabisa eneo lile.


“Turudi kwenye biashara yetu Dokta.” Aliongea Uzo huku anaanza kusogea mbele ya Dokta Ice.


“Sina biashara na wewe Uzo.” Akajibu mapigo Dokta Ice.


“Unayo. Na tambua hata kama huwezi kuongea sasa, tutakufanya utapike yote. Nadhani unalitambua hilo vema sana.” Uzo alibwabwaja. “Nachotaka kujua, ni huyu mwanajeshi uliyemtorosha, anaubora gani na ulitumia folmura ipi?” Akauliza.


“Hahahaaaa.” Dokta Ice akacheka kwa sauti kabla ya kutulia na kumuangalia Uzo. “Unamuogopa sana eeh! Ni hatari sana huyo, mara mia na hawa niliyowatengeneza.” Akaongea kwa furaha Dokta Ice.


“Sijakuuliza uhatari wake. Nimekuuliza kitu kingine kabisa.”


“Unajua sheria za udaktari, huruhusiwi kutoa siri za ugonjwa au mbinu za kutibu ugonjwa. Nipo hapa kama daktari. Kwa hilo hutopata.” Akajibu Ice.


“Okay. Na kuna risasi ulikuwa unazitumia kule kwako….” Uzo ni kama alikuwa kasahau kitu. Akakatisha yale maneno. “Na nilitaka kusahau, ni mkeo ndiye alituambia nyumba yako ya siri.” Akaongea maneno hayo baada ya kujishtukia.


“Si mke wangu. Ni malaya wetu.” Akaongea Dokta Ice na kumfanya Uzo acheke.


“Leo ni malaya?” Akauliza kwa mshangao.


“Kama unaweza kumpiga matako na akacheka tu, unadhani yupo salama akilini huyo?” Maneno hayo yakamfunga mdomo Uzo.


“Hayakuhusu.” Mwishowe akaongea. “Nachotaka sasa ni kujibu nachokuuliza.” Akaongea kwa ukali zaidi.


“Oooh! Umekuwa mbogo pia? Napenda ukiwa na hasira kuliko ukijidai mwema.” Akaongea huku katabasamu Dokta Ice. “Hata hivyo, hutaambulia lolote.” Akaongeza na kumfanya Uzo amfate pale kwenye kiti na kumchapa ngumi moja ya nguvu.


“Nahitaji majibu. Na siyo porojo zako.” Akaongea Uzo kwa hasira.


“Uzo rafiki yangu. Umesahau kuwa tulisomea wote upelelezi? Umesahau yale mateso yote tuliyoshiriki kwa pamoja ili tuseme kambi yetu iko wapi? Hivi tulisema kweli?” Akamuuliza lakini hakumpa nafasi ya kujibu. “Nadhani unaelewa unachokifanya ni kujisumbua tu kwani sitosema lolote.” Akamaliza.


“Ipo njia ya kusema.” Uzo alipoongea hayo, akafanya ishara ya mkono wake na Dokta mmoja alifungua mlango ule aliotokea Simeria na aliingia eneo lile akiwa kabeba sahani iliyofunikwa kwa bakuli la bati.


Akaenda hadi kwa Uzo na kuifunua sahani na hapo ikaonekana sindano ambayo muhimili wake uliundwa kwa chuma na ulikuwa na muonekano kama wa bastola. “Pinnacle.” Akaongea Uzo akiwa kakamata ile sindano huku anaingalia. “Nadhani jina la sindano hii uliipa wewe kwa sababu ya maumivu yake na ulevyaji wake. Ni muda wa wewe kuelewa maana ya pinnacle.”


“Kama niliitengeneza mimi, basi najua jinsi ya kuihimili.” Akajibu Dokta Ice na kabla Uzo hajasogea pale alipokuwa kakalishwa, Dokta Ice akarusha teke lake na kumpiga sehemu za siri Uzo na kwa taharuki ya hatari, akajirusha kwa nyuma huku kiti bado kikiwa mgongoni kwake, akadondokea mgongo na kukifanya kiti kile kivunjike na wakati huo karibu yake kulikuwa kuna mwanamaabara mmoja aliyepigwa mtama wa kushtukiza jambo lililofanya adondoke na kumpa nafasi Dokta Ice asimame naye huku kamkaba.


“Mkileta papara tu! Navunja shingo ya huyu mbwa wenu.” Akawachimba mkwara na wakati huo wanajeshi wawili, mmoja aliyekuja na Dokta Ice na mwingine Merice, mtoto wake wa kumzaa, wote walikuwa wamemuoneshea bastola.


“Msifanye lolote.” Aliongea Uzo kuwaelekeza wale wanajeshi lakini kitendo cha kushtukiza sana






“Kama niliitengeneza mimi, basi najua jinsi ya kuihimili.” Akajibu Dokta Ice na kabla Uzo hajasogea pale alipokuwa kakalishwa, Dokta Ice akarusha teke lake na kumpiga sehemu za siri Uzo na kwa taharuki ya hatari, akajirusha kwa nyuma huku kiti bado kikiwa mgongoni kwake, akadondokea mgongo na kukifanya kiti kile kivunjike na wakati huo karib yake kulikuwa kuna mwanamaabara mmoja aliyepigwa mtama wa kushtukiza jambo lililofanya adondoke na kumpa nafasi Dokta Ice asimame naye huku kamkaba.



“Mkileta papara tu! Navunja shingo ya huyu mbwa wenu.” Akawachimba mkwara na wakati huo wanajeshi wawili, mmoja aliyekuja na Dokta Ice na mwingine Merice, mtoto wake wa kumzaa, wote walikuwa wamemuoneshea bastola.


“Msifanye lolote.” Aliongea Uzo kuwaelekeza wale wanajeshi lakini kitendo cha kushtukiza sana alikifanya Uzo, kitendo ambacho hamna aliyekitegemea, hata Dokta Ice.


ENJOY.


Wakati anawasihi wanajeshi wake wasifanye lolote, kwa kasi ya ajabu alichomoa bastola yake na kugeuka alipo Dokta Ice na kumpiga risasi ya bega Dokta yule na kumfanya amuachie yule mwanamaabara na kugugumia kwa maumivu.


“Ulisahau kuwa nilisomea usalama wa taifa, Dokta Ice. Ina maana umesahau?” Aliuliza huku ametabasamu Uzo wakati huo yule mwanamaabara alikuwa anapepesuka huku akitoka eneo lile la Dokta Ice.


Macho ya Dokta Ice yakawa yanamuangalia Merice, mwanaye pekee wa kike. Kisha akatabasamu na kukumbuka miaka kumi na tisa nyuma walipompata mwana yule.


Yeye na mke wake, Simeria walikuwa wanagombania jina la kumpa. Dokta Ice alitaka kumpa jina la ukoo wao na Simeria alitaka kutoa jina toka ukoo wao, hivyo ikawa vurugu na patashika japo kulikuwa hamna gomvi bali utani na masikhara mengine.


“Basi tufanye kitu mke wangu.” Aliongea Dokta Ice baada ya mvutano mdogo.


“Nataka kiwe kitu cha maana.” Naye Simeria akaongea.


“Unaonaje tukaunga majina yetu, kisha tukapata jina moja la kumpa huyu mtoto.” Akatoa wazo ambalo halikupingwa kabisa na Simeria kama yale mawazo ya mwanzo.


“Tumuitaje sasa kwa majina yetu?”


“Icemeri?” Jina hilo likapingwa vibaya na Simeria. Dokta Ice akaendelea kutoa majina na majina kupitia muunganiko wa majina yao lakini Simeria alikataa. “We’ unataka jina gani?” Ikabidi Ice amuulize Simeria.


“Merice. Yaani Meri la kwanza ni langu na Ice la mwisho ni lako. Hiyo ‘i’ ni yangu na yako pia. Unaonaje?” Simeria akatoa wazo na kumfanya Dokta Ice atabasamu.


“Limepita hilo, sina la kusema wala kuongeza.” Akaongea Dokta Ice na wote wakawa wamekubali kumpa Merice hilo jina. Leo anamtazama Merice mwingine kabisa, Merice aliyeathiriwa na C.O.D.EX.


“Utasema tu ni folmura gani imeitumia na zile risasi zako ni kemikali gani zile.” Sauti ya Uzo ikamtoa mawazoni Dokta Ice ambaye alikuwa anaenda pale alipokuwa kakaa huku mkono wake mmoja ukiwa umeshika jeraha alililopigwa risasi.


“Uzo Buzzin,” Akaita Dokta Ice na kumfanya Uzo amuangalie mtu anayemuendea huku kakamata sindano yake. Macho yake yalimtazama vema Dokta Ice na yaling’amua jambo fulani la hatari. “Umesahau kuwa tumefundishwa na njia za kumshinda adui ambaye ameshindikana.” Akaongeza maneno yake Dokta Ice.


“Usifanye huo ujinga Dokta.” Akaonya Uzo huku akiongeza kasi ya kwenda pale alipokuwepo Dokta.


“Merice. Wewe ni mtoto mwema, kumbuka hilo.” Maneno hayo yalitoka wakati huo Merice naye alikuwa anamtazama baba yake. Kabla Uzo hajafika alipokuwa kakaa Dokta Ice, Dokta yule aliikunja shingo yake upande wa kushoto, kisha kwa nguvu sana akaizungushia upande wa kulia na kuifanya ilie kama kipande cha mti kilichovunjika.


Uzo akasimama ghafla na kumtazama Dokta Ice aliyekuwa kakodoa macho yake. Tayari alikuwa kajinyoga bila kamba wala mikono. Ni mbinu walizowahi kufundishwa wakiwa usala wa taifa, hivyo ndivyo alivyosema.


“Mjinga sana Dokta Ice. Umeona bora ufe kuliko kusema ukweli. Hongera sana. Wewe ni shujaa wangu wa mwisho.” Uzo akageuka nyuma na alimuangalia Merice ambaye naye alikuwa kama hajielewi baada ya kuona tukio lile. Alikuwa kama kapatwa na mshtuko baada ya kushuhudia kile kifo. Macho yake bado yakawa kwa Dokta Ice lakini hajui ni kwa nini hali ile ilimtokea.


“Merice.” Akaitwa na Uzo na Merice akamtazama yule bwana. “Chukueni hiyo maiti na kuipeleka maabara. Yawezekana ubongo wake tukaupandikiza kwa mtu mwingine na kugundua alichotuficha.” Maneno hayo hayakusubiriwa na wale wanajeshi wawili bali mwili wa Dokta Ice kubebwa na kupelekwa maabara.


****


Macho ya Idris Iris yalibaki kwenye kioo cha kompyuta yake akiwa haamini kama Dokta Ice ndiye Yule aliyekuwa anashiriki upuuzi wa kuwaua watu ambao yeye hakuwafahamu lakini kwa asilimia fulani aliamini wale walikuwa wazazi wake.


“Haiwezekani.” Idris alibwata kwa sauti ya juu kidogo na kumfanya muhudumu wa ndege ilea je na kumtuliza kwa sababu kwenye ndege hakuhitajiki kelele za namna ile. “Sawa mkuu.” Alijibu kiuanajeshi baada ya kuuambiwa kuwa haihitajiki kelele ndani ya ndege.


Muhudumu wa kike alitabasamu baada ya kugundua kuwa yule ni mwanajeshi na kamjibu kwa heshima ya jeshi.


Idris akaachana na ile video ambayo iliishia Dokta Ice anachukua kompyuta iliyokuwepo juu ya pambo moja lililozungukwa na taa mule chumbani. Akafungua video nyingine ambayo ilionekana pale kwenye kompyuta yake. Ilipofunguka, Dr. Ice ndiye alionekana na alikuwa anaongea mengi sana kwa lugha ya Kiingereza.



“Iris. Kama bado hujaelewa video za mwanzoni, basi naomba uelewe sasa. Dokta Boucher na Jesabel walikuwa ni marafiki zangu sana. Walikutana nyumbani kwangu kwenye siku ya kuzaliwa ya mke wangu. Ilikuwaa maraya pili, hapo wakaanza mahusiano yao ambayo yalipelekea hadi ndoa kufungwa. Baadaye wakapata mtoto wa kiume ambaye kwao alionekana kaja kwa mengi na ndipo wakamuita Best.” Video ile ilianza kueleleza kwa maneno hayo. Ikazidi kuendelea huku Iris akiweka umakini wake zaidi ya mwanzo. “Walipouawa, mengi yalionekana lakini hakuna ambaye alikuwa tayari kushuhudia maafa yakimtokea. Walinyamaza wote.


Lakini sasa nataka ulimwengu ujue ni nini kilitokea na ni siri gani waliyonayo hadi wanadiriki kuua madaktari wazuri baada ya kupata wengine. Lakini kabla sijakupa siri hiyo, tambua kuwe Best ni wewe na Bouncher na mkewe ndio wazazi wako.” Idris akavuta pumzi kabla hajaendelea kuangalia.


“Sasa nakupa siri,” Hapo Idris akatega mwili na akili vyote kwa pamoja. “C.O.D.EX ni sumu moja matata sana katika mwili wa binadamu. Hapo mwanzo waliwekewa watu wenye akili zao kabisa. Ilikuwa inambadilisha binadamu na kuwa kama Shetani. Maumivu ambayo alikuwa anayapata huyu mtu anayeingiziwa hii kemikal, hamna ambaye aliweza kuyavumilia. Wengi walikufa na hata waliopona, nao walikuwa si watu bali ni silaha za hatari. Baadaye makao makuu ya C.O.D.EX, yalivunjwa kwa sababu yalikuwa kinyume na haki za binadamu. Miaka kumi mbele ndipo yakafunguliwa tena na kuna baadhi ya wanajeshi tayari tumekwishawajenga. Mimi, baba yako na mke wangu ndio tulipewa jukumu la kutengeneza kemikali hizi na badala ya kuwamiminia binadamu, tuliwawekea maiti au wafu.” Manenno hayo yakamfanya Idris ajihisi kufa tena baada ya kusikia kuwa waliwekewa wafu.


“Ina maana nilikufa?” Akajiuliza lakini hakuwa na jibu zaidi ya kuendelea kuangalia ile video.


“Lakini siyo marehemu wote ambao walikuwa wanatengenezwa kwa hii kemikali na si wote waliweza kuhimili hii kemikali, na ndipo hapo tulipoamua kuwa tunaua wale watu imara katika mapambano na wenye akili nyingi sana. Hao tuliowaua tuliweza kufanikiwa sana tena sana tu. Kipindi hicho wewe ulikuwa mdogo sana. Baada ya C.O.D.EX kufanikiwa kwa asilimia nyingi sana, ndipo waliamua kumuua Baba yako na Mama yako na baadae kumuua mke wangu na mtoto wangu. Wewe nilikabidhiwa mimi lakini pia walikunyweshwa madawa ya kukukata uhai wako ukiwa na miaka kumi na saba.” Iliendelea kuelezea video ile huku Idris akiwa makini sana. “Sikutaka uwe kundi la wanajeshi wale makatili, nikakutenga kabisa. Miaka minne mbele ndipo tukaanza kuwajaribu wanajeshi wetu, tukafanikiwa na mwaka huu tukawaita Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi, wakaanza kuwafanyia majaribio lakini wanajeshi hawa yaonekena wameumbwa kwa ajili ya kufanya maangamizi na si kuokoa. Hapo ndipo nikapata wazo la kukutumia wewe kwa kukuwekea hizo kemikali lakini ukiwa na uwezo wa kuwa na huruma na kutunza kumbukumbu. Kwa sasa huna kumbukumbu zako, lakini jinsi unavyokwenda, utakuja kukumbuka yote ya nyuma, tangu ukiwa mtoto.” Aliendelea Dokta Ice kuongea mengi ya muhimu kuhusu C.O.D.EX lakini kubwa zaidi alimsisitiza Idris ajifiche sana huko aendako.


“Kwa hiyo umeamua kunipoteza?” Akaiuliza ile video kana kwamba yaweza kumjibu. “Kwa hiyo mimi ni mwanajeshi mwenye huruma, na ni mwanajeshi mwenye kumbukumbu na kibaya zaidi, mimi ni mwanajeshi niliyepotezwa?” Akajiuliza tena. “Sawa. Acha nipotee. Kama nitapotea, basi mimi si mwanajeshi niliyepotezwa bali mwanajeshi aliyepotea. I am A Missing Soldier, they have to find me..” Akamaliza hayo huku anafunga kopyuta yake na kutulia.


****


Saa saba mchana ndani ya Jiji la Dar es Salaam ndege ya Shirika la Ethiopia ambayo iliwachukua baadhi ya wateja walioshuka na ndege toka Marekani, ilitua katika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere. Idris Iris alionekana akishuka taratibu huku kakamata mabegi yake mawili, moja likiwa la kompyuta na lingine la nguo chache. Aliitazama ardhi ya Tanzania kwa makini na kutafakari machache kabla hajachukua jukumu la kwenda sehemu ya ukaguzi.


“Idris Iris. Karibu sana Tanzania.” Sauti ya kike ilimuongelesha Idris huku mwanadada huyo akimkabidhi ‘passport’ yake Idris.


“Ahsante sana…..” Idris alionesha kidole chake akitaka mwanadada yule ajitambulishe jina lake baada ya yeye kuishia njiani. Aliongea Kiswahili fasaha sana. Dokta Ice aliweza kumpachika chipu inayoweza kumbadilisha mwanjeshi yule na kuongea lugha yoyote ile.


“Naitwa Miss Timasi.” Akamjibu mwanadada huku tabasamu pana likiwa limepamba uso wake.


“Sawa Miss Timasi. Nadhani kuna ndege yangu ambayo napaswa kuipanda hadi Arusha.” Akaongeza Idris.


“Ipo tayari Idris. Nenda mlango ule na kisha utawakuta walinzi ambao utapanda nao ndege hadi Arusha. Huko nenda kaishi salama. Na hapa nilikuwa nasubiri ujio wako tu. Kesho, nami nitaanza kuhudumia wakazi wa Arusha.” Akaongea Timasi huku bado tabasamu lake likiwa bado limekamata namba.


Timasi alikuwa ni mwanamke wa makamo, miaka kati ya ishirini na tisa hadi thelathini na tatu, ndio ilitosha kumkadiria. Alikuwa na rangi ya kahawia, na nywele nyeusi huku macho yake yakiwa yanapendeza kwa rangi kali ya udhurungi. Alipendelea kupaka midomo yake rangi ya damu ya mzee na kuzungushia wanja mweusi na kuufanya uso wake uzidi kupendeza kama malaika wa duniani.


Siku hiyo yeye ndiye alikuwa anawagongea mihuri ya wasafiri mbalimbali wanaoingia na kutoka Tanzania, na ndiye yeye aliyetoa mamlaka ya Idris kwenda ambapo ndege yake binafsi inamsubiria.


“Ahsante sana dada. Na karibu Arusha.” Alishukuru Idris na kuanza kwenda kwenye mlango alioelekezwa na Timasi. Baada ya kutoka, aliweza kuelekea ilipokuwepo ndege aliyoandaliwa, nayo ilimchukua na kuanza kwenda katika Jiji la Arusha.






Timasi alikuwa ni mwanamke wa makamo, miaka kati ya ishirini na tisa hadi thelathini na tatu, ndio ilitosha kumkadiria. Alikuwa na rangi ya kahawia, na nywele nyeusi huku macho yake yakiwa yanapendeza kwa rangi kali ya udhurungi. Alipendelea kupaka midomo yake rangi ya damu ya mzee na kuzungushia wanja mweusi na kuufanya uso wake uzidi kupendeza kama malaika wa duniani.


Siku hiyo yeye ndiye alikuwa anawagongea mihuri ya wasafiri mbalimbali wanaoingia na kutoka Tanzania, na ndiye yeye aliyetoa mamlaka ya Idris kwenda ambapo ndege yake binafsi inamsubiria.


“Ahsante sana dada.” Alishukuru Idris na kuanza kwenda kwenye mlango alioelekezwa na Timasi. Baada ya kutoka, aliweza kuelekea ilipokuwepo ndege aliyoandaliwa, nayo ilimchukua na kuanza kwenda katika Jiji la Arusha.


****


ENDELEA


Uwanja wa kawaida sana uliopo Jijini Arusha, uliweza kumpa tofauti kubwa sana Idris. Alipotoka, huko Marekani, kulikuwa na maisha matamu sana na yenye utajiri mwingi kuliko Tanzania. Lakini hayo yote hayakumfanya Idris Iris kukataa kuja kuishi katika Jiji lile ambalo yasemakana kwa Tanzania, ndilo lenye gharama za juu katika maisha yake hasa kwenye vyakula na malazi.


“Tanzania. Kwa nini nimekuja huku?” Akajiuliza Idris wakati anatoka uwanja wa ndege na kuelekea sehemu ambayo aliona gari aina ya Audi nyeusi na ya gharama ikiwa imepaki kwa ajili yake. “Kwa sababu ni sehemu ya amani na naweza kufanya mambo yangu huku bila wasiwasi.” Akajijibu mwenyewe na wakati huo gari ile iliyokuwa inamsubiri yeye, ilijifungua mlango yenyewe ile sehemu ya abiria, na Idris alikwea ndani yake tayari ya kupelekwa maeneo ambayo atakuwa anaishi.


****


Baada ya kifo cha Dokta Ice, huko Marekani pakazuka mtafaruku mkubwa kati ya mashirika ya kijasusi na kipelelezi pamoja na serikali ambayo iliingilia yale mambo na kuyafanya kuwa kama kisasi. Kitendo cha Dokta Ice kufa akiwa anakataa katukatu wale wanajeshi wasitumiwe kwa ajili ya kuangamiza wasiyokuwa wana hatia, kiliweza kuyafanya mashirika ya upelelezi kukubaliana naye na walisikitika sana kuona mtetezi yule amekufa na kapewa mamlaka mtu mwingine ambaye naye hana huruma hata chembe. Mwanamama Simeria, mke wa zamani wa Dokta Ice na sasa ni kimada wa Uzo, akapewa jukumu la kuunda wanajeshi wengine kama wale wa Dokta Ice tena wakiwa bora Zaidi na wenye roho mbaya sana.


“Nasema sisi kama FBI, hatuwezi kuona huu ufilauni wenu unafanyika bila kuupigia kelele.” Alilalamika Afisa mmoja wa FBI wakati wa kikao chao na serikali ya Marekani.


“Bwana Bastian, hatupo hapa kubishana na wewe. Tupo hapa utuambie upo ndani au nje, kuhusu hawa wanajeshi. Huna mamlaka ya kukataa ambacho tumekianza. Kwanza wewe ni mpelelezi tu, mambo ya jeshi ni ya serikali.” Akaongea Waziri wa Ulinzi ambaye ndiye alikuwa muongeaji mkuu wa serikali ya Marekani.


“Sasa mliniita hapa ili iweje?” Akauliza Mkuu wa FBI ambaye kitambulisho chake kilisomeka kwa jina la Bastian Winch.


“Kukupa heshima yako tu! Usijekuona kama tunakutenga. Na kama hutaki hii heshima, tutatuma C.O.D.EX mmoja tu nyumbani kwako. Atatafuna hadi kale kachanga kako.” Maneno yalimtoka Uzo, mkuu anayesimamia projekti nzima ya C.O.D.EX.


Bastian akagwaya baada ya maneno hayo. Akamuangalia kwa macho makali sana yule bwana anayeitwa Uzo.


“Bwana Ally. Upo nasi au nawe hadi tukwambie kama tulivyomwambia Bastian.” Swali hilo likamgeukia mkuu wa CIA ambaye yeye alijulikana kama Ally Ahmed Ally. Bwana yule akamtazama Bastian, akatikisa kichwa kushoto na kulia, kasha akawaangalia wale wachimba mkwara.


“Nitakuwa nanyi japo Bastian yupo sahihi Zaidi.” Akawajibu wale mabwana na hapo hapo kwa pamoja wakasimama na kupeana mikono ya kheri kwenye kazi yao ya kushirikiana kuua na kushambulia mataifa mengine kwa kutumia wanajeshi waliyoundwa kwa kemikali za C.O.D.EX.


“Mi nadhani tumekubaliana kwa pamoja japo kwa kutumia nguvu kidogo.”Akaanza tena Uzo baada ya kukaa kwenye sehemu zao. “Hilo halina shaka, mtatuelewa baadae maana yetu. Hii ni Marekani, lazima tudhihirishe nguvu zetu hapa duniani. Na moja ya kufanya hivi, ni kuunda jeshi ambalo litapigana vita kwa nguvu na kushinda vita hiyo.” Akaongeza.


“Lakini kuna tatizo nimelipata Uzo.” Bastian, kutoka FBI akakatisha maelezo ya kibabe toka kwa Uzo.


“Tatizo gani Bast…” Akataka kujua.


“There’s a missing soldier.” Akajibu akimaanisha kuwa, kuna mwanajeshi kapotea.


“Ni kweli Bast… Mwanajeshi huyo aliyepotea, aliundwa na Dokta Ice na ni yeye ndiye anajua yupo wapi. Na tulipofatilia ni wa aina gani, tukagundua ni kama binadamu tu! Yeye anahuruma na pia hayupo kama hawa anaowatengeneza Simeria. Kwa hiyo sidhani kama ni tatizo kwetu.” Akajibu kwa kujiamini.


“Siyo tatizo?” Akauliza kwa mshangao Ally, mwana CIA.


“Ndio. Kwani yeye kaumbwa kama binadamu tu.”


“Lakini ni zao letu lile. Veje leo awepo mahali kwingine na hatushtuki na tunaona hamna tatizo kabisa.” Akaongeza Ally.




“Unataka ushauri nini Ally.” Ikabidi Uzo aulize baada ya kukabwa sana mbele ya Waziri wa Ulinzi ambaye alionekana kuwa upande wa Ally na Bastian.


“Tumtafute, na tumrudishe eidha awe mfu au hai. Silaha kama ile ikiingia China, Urusi au Korea, hakika wataiboresha Zaidi na watatisha sana.” Akajibu Ally.


“Hiyo ni kazi yako wewe CIA, kumtafuta.” Akajibu Uzo.


“Hapana. Mwanajeshi hutafutwa na wanajeshi wenzake. Sisi kazi yetu ni kuwatafutia mahali alipo tu! Kumkamata ni kazi yenu.”


“Unataka kumaanisha nini?”


“Tutakuonesha alipo, kasha utatuma C.O.D.EX wako.”


“Hawa si kazi yao. Hawatafuti mtu mmoja bali hawa ni wa kupambana vita tu.”


“Wale mateka mliowaua walikuwa ni vita?” Akauliza Bastian.


“Naomba hayo usiyaingize hapa Bast..” Akang’aka Uzo.


“Sasa usikatae na kutetea mambo ambayo hayana makalio wala kucha.” Bastian naye akatuna mbele ya Uzo. Uzo naye akabaki anamtazama Bastian kwa macho ya hasira.


“Tutatuma C.O.D.EX endapo tutajua wapi alipo huyu mwanajeshi.” Ikabidi Waziri wa Ulinzi akubali jukumu hilo ambalo Uzo alikuwa kama anataka kulikimbia.


“Ahsante Muheshimiwa.” Akanena Ally kwa furaha.


“Lini mtakuwa mmempata?” Akauliza Uzo.


“Wiki moja tu.” Ally wa CIA akajibu na kwa majibu hayo, yakawafanya wote walidhike na habari zingine zikaanza kujadiliwa hasa katika kuvamia nchi mbalimbali na majaribio ya silaha zao.


*****


Siku tatu nzima, Idris alikuwa anashinda ndani bila kwenda sehemu yoyote. Chakula na kila kitu vilikuwa ndani ya jumba kubwa na la kifahari lililopo Jijini Arusha. Sura yake haikutawaliwa na tabasamu hata kidogo, kila muda alitaka kujua mengi ya dunia. Aliangalia taarifa za habari na vipindi vya burudani kila siku ili kujifunza kuishi sawa na maisha ya binadamu wa leo.


Pia kila mara alikuwa anasoma nyaraka nyingi ambazo aliachiwa na Dokta Ice. Aliweza kugundua mengi sana ambayo yalikuwa nyuma ya pazia. Aligundua mtandao mzima wa mauaji ya watu huko Marekani na aliweza kujua jinsi gani Jeshi la C.O.D.EX linavyotengenezwa. Ndani ya nyaraka hizo, pia kulikuwa na madhumuni chanya na hasi ya C.O.D.EX na pia watu pekee ambao wanaweza kusimamisha mpango huo, ni UN.


“Hawa UN nawapataje? Na wataelewa kweli nia yangu? Au wanaweza kunifanya kitoweo hawa na kuniletea matatizo zaidi.” Akaendelea kujiwazia kisha macho yake yakarudi kwenye runinga ambayo ilikuwa sebuleni kwake. Akajikuta anaitazama kwa muda kabla ya kufanya maamuzi. “Ila kwani mimi na shida gani? Nina kila kitu humu ndani, kwa nini nisifurahie maisha haya badala ya kuanza kuwaza mambo yatakayonifanya nipotee duniani kabisa au kufanywa muuaji baada ya kurudishwa tena Marekani. Acha nifurahie utamu wa Tanzania.” Maneno hayo ndio yakawa mwisho wa kusoma mafaili mengi aliyoachiwa na Dokta Ice, akayakusanya na kuyahifadhi mahali na kisha taratibu akaanza kujifunza mambo mengi ya kidunia.


Aliangalia video mbalimbali za starehe kama kucheza muziki, kuimba, kufanya mapenzi, na pia aliendelea kujifunza mengi ambayo hakuyajua kwa kupitia video hizo. Ndani ya wiki moja, tayari aliamini kuwa yupo tayari kuanza kuyatumia mambo aliyojifunza.


Shauri la kwanza alitaka mtu ambaye anaweza kumsindikiza katika kufanya mambo yake. Idris alihitaji rafiki wa karibu ambaye wangeweza kufurahi kwa pamoja na kutumbua mali ambazo alikuwa kawekewa na Dokta Ice.


Akiwa kakaa sebuleni kwake, akawa anawaza na kuwazua ni nani anaweza kuwa rafiki yake wa karibu? Dereva wake au nani? Dereva hakumtaka kabisa kwa sababu si kazi yake kumtambulisha jiji. Yeye alitaka rafiki ambaye kidogo anaijua dunia na mambo yake hasa anasa.


“Timasi.” Akajikuta anataja jina hilo baada ya kumkumbuka mwanadada mrembo aliyemuona uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, na kisha kumgongea visa ya kuishi Tanzania, kabla hajaenda Arusha akitokea Marekani.


Haraka baada ya mawazo hayo, akachukua koti lake la leiza na kutoka nje haraka ikiwa ni mchana wa saa saba. Akabonyeza rimoti ndogo iliyokuwa imeungwa na funguo za nyumba, mlango mkubwa wa bati ukaanza kufunguka kwenda juu na hapohapo ukaonekana uzio mkubwa ambao ulikuwa na magari yapatayo nane na yote ni ya kifahari.


Gari nyekundu aina ya ferrarri, ndiyo ilimvutia siku hiyo. Akaingia ndani yake na kuitoa nje. Akabofya rimoti yake na ule mlango wa varanda, ukajifunga, naye Idris akachoma mafuta yaliyomo kwenye gari lake hadi uwanja wa ndege.


****


“Hellow mrembo.” Sauti ya Idris ilichombeza mbele ya Timasi ambaye hakumuona kama amekuja pale uwanja wa ndege ambapo alihamishiwa. Uso wa Timasi ukanyanyuka na kisha kupambwa kwa tabasamu mwanana.


“Wapi leo Idris.” Akauliza Timasi akitaka kujua Idris anataka kwenda safari ya wapi.


“Oooh! Leo nataka kwenda na wewe mahali.” Akajibu mwanaume kwa bashasha. Timasi akamuangalia kwa mshangao na kisha akatabasamu kama kawaida yake.


“Unataka kwenda wapi na mimi?” Akauliza Timasi.


“Popote pale tulivu tukajiliwaze.”


“Hahaaa. Am sorry my dear.” Maneno hayo ya samahani yalimtoka Timasi huku kanyanyua mkono wake na kumuonesha pete aliyovaa.


“Ouch. Sorry too my dear. Sikujua hilo. Kwa hiyo wewe ni Mrs nani?” Akauliza Idris.


“Mrs. Sema.” Akajibu Timasi huku bado tabasamu mwanana likiendelea kuupamba uso wake.


Wakati wote huo wanaongea, kulikuwa hamna wateja wa kuwahudumia lakini wakiwa katika maongezi, mara walisikia kelele kali ya mshangao na ya kike. Wote wakageuka kwa haraka kuangalia kule sauti ile kali ilipotokea.


Macho yakamtoka Timasi baada ya kumuona mtoto wa kike ambaye alipiga kelele zile. Idris naye akawa kwenye kizungumkuti akiwa haamini kama anaona jini au anaangalia filamu ya maigizo na muda ukifika itakwisha na kugundua kuwa yalikuwa maigizo. Wote watatu na wafanyakazi wengine wakawa katika mshangao wa aina yake.








“Mrs. Sema.” Akajibu Timasi huku bado tabasamu mwanana likiendelea kuupamba uso wake.


Wakati wote huo wanaongea, kulikuwa hamna wateja wa kuwahudumia lakini wakiwa katika maongezi, mara walisikia kelele kali ya mshangao na ya kike. Wote wakageuka kwa haraka kuangalia kule sauti ile kali ilipotokea.




Macho yakamtoka Timasi baada ya kumuona mtoto wa kike ambaye alipiga kelele zile. Idris naye akawa kwenye kizungumkuti akiwa haamini kama anaona jini au anaangalia filamu ya maigizo na muda ukifika itakwisha na kugundua kuwa yalikuwa maigizo. Wote watatu na wafanyakazi wengine wakawa katika mshangao wa aina yake.


ENDELEA.


“Timasi?” Sauti ileile iliyopiga kelele na kuwafanya watu wapigwe na butwaa, ndio pia iliita jina la Timasi kwa nguvu.


“Limasi?” Naye Timasi akaita kwa nguvu na kuanza kutoka sehemu ile ya dawati la kuhudumia wateja na kuanza kwenda kule ambapo yupo mtu aliyemuita Limasi. “Ooooh! Dada huyoo.” Akawa anamfuata Limasi huku katanua mikono yake kwa kutaka kumkumbatia.


Bado macho ya Idris yalikuwa hayaamini yanachokiona. Katika kumbukumbu zake hakuwahi kuwaza kuwa kuna watu wanaweza kufanana namna ile. Limasi na Timasi walikuwa wanafanana kila kitu, hadi aina ya nguo na vipodozi wanavyopaka, walikuwa wanaendana sana. Idris akatikisa kichwa na kufuta macho yake ili aone kama amelala au yupo macho, lakini alipoangalia, aliweza kuona picha ya wawili wale wakiwa wamekumbatiana kwa furaha kubwa.


“Mbona unakuja kimyakimya dada?” Timasi akamuuliza Limasi baada ya kuachiana.


“Nilitaka nikusapraizi dada yangu. Yaani hapa siamini kama ni wewe. Shemeji yangu, handsome langu, mzima?” Limasi aliyeonekena wa maneno mengi, alianza uchokozi wake.


“Mzima, ndio sababu ya mimi kuhamia Arusha toka Dar. Ila twende kwanza nyumbani. Maana wewe ulivyo chiriku, sitamaliza hapa.” Maneno hayo yalienda sambamba na Timasi kuchukua baadhi ya mizigo ya dada yake na kuanza kuivuta hadi pale kwenye dawati analofanyia kazi. Wakati huo Idris bado alikuwa anawatazama asiweze kuamini kama kweli duniani kuna watu wa aina ile.


“Idris. Huyu ni pacha wangu. Yeye ni Doto na mimi ni Kulwa. Anaitwa Limasi. Alikuwa India miaka saba sasa. Kasomea huko elimu yake ya juu.” Timasi akamtoa mawazoni Idris ambaye alikuwa bado anamtazama Limasi.


“Nimesomea Sheria, na nimesoma hadi ‘School of Law’ na nina muhuri na naweza mengi tu.” Aliongea kwa tambo Limasi. Idris akawa mtu wa kutabasamu kwa mbwembwe za Limasi.


“Limasi. Huyu anaitwa Idris. Alitokea Marekani wiki iliyopita. Kaishi sana huko na sasa kaamua kurudi nyumbani. Leo kaja kunitembelea kwa sababu mimi ndiye nilimpokea na kuthibitisha passport yake ya kusafiria.” Timasi akamtambulisha Idris kwa Limasi.


“Nafurahi kukufahamu Limasi.” Sauti nzito ilimtoka Idris.


“Mmmmh! Gentleman. Nafurahi pia kukufahamu.” Akaongea Limasi kwa pozi nyingi sana.


“Ngoja niage kwa sababu muda wangu umekwisha pia. Nataka twende nyumbani. Idris unaweza kutupeleka?” Akauliza Timasi huku anaelekea ofisini kwa mkuu wake ili amuage.


“Sure. Naweza.” Akajibu Idris wakati huo Timasi alikuwa ameingia ndani ya ofisi.


****


Huko makao makuu ya CIA wiki ilikatika na hakuna matokeo yoyote ambayo yalionekana kuhusu Idris Iris. Walitumia mitambo yao yote ya Satelite na camera za CCTV ili kuona kama watampata mwanaume huyo, lakini hawakufanikiwa hata chembe. Nchi zote za Ulaya zilitazamwa. Asia na mabara yote makubwa pamoja na baadhi ya nchi za Afrika, yalipitiwa na msako mkali wa CIA na mashirika mengine ya kipelelezi, lakini hawakuweza kumuona Idris.


“Nipe maendeleo Ally.” Uzo alikuwa anawasiliana na aliyepewa jukumu la kumsaka Idris.


“Hamna kitu Uzo.” Akajibu Ally.


“Afrika umeangalia au umepuuzia.” Akauliza tena Uzo.


“Nimeangalia Afrika Kusini, Nigeria, Ghana, Morocco, Tunisia, Algeria lakini sijaona kitu.” Akajibu Ally.


“Sasa atakuwa wapi? Kama Afrika, hatuwezi kuwafuata sana. Najua hawezi kuwa nchi za kipumbavu kama zile. Hapo atakuwa amepelekwa nchi zenye uwezo wa kutengeneza silaha tu!” Akaongea Uzo.


“Sasa kama ataingia mikononi mwa hao, huoni kama ni hatari?” Akauliza swali ambalo ndio sababu ya yeye kupewa jukumu la kumtafuta Idris. Badala ya Uzo kujibu swali lile, akakata simu.


****


“Idris. Yaonekana unapesa sana. Umetoa wapi?” Limasi akamuuliza Idris ambaye alikuwa anawapeleka nyumbani kwao kwa gari yake aina ya Ferrarri.


“Baba yangu alikuwa Daktari huko Marekani. Baada ya kufa, akaacha mali nyingi sana huku na kule ili baadae nichague niishi wapi. Nikaona bora nije kwetu tu ili niendeleze biashara zangu nilizokuwa nafanya huko.” Akajibu.


“Kwa hiyo unafanya biashara gani?” Limasi akachimbua.


“Aaagh na wewe mwanasheria embu tulia mwenzako aendeshe gari.” Timasi akaingilia baada ya kuona maswali yanazidi kipimo.


“Sasa dada si nataka kumjua rafiki yetu?” Akadeka Limasi.


“Hamna shida Timasi. Mimi na kampuni ya usafirishaji wa kwenye maji. Nasafirisha mizigo pamoja kupokea pia, huko Mtwara na Mombasa.”


“Ohoo! Hiyo safi sana. Na umeoa?” Akauliza tena Limasi. Timasi akashusha pumzi ya nguvu na ni wazi swali lile aliliona la ajabu.


“Bado sana.” Akajibiwa kwa kifupi. Limasi akakaa kitako na kumshangaa Idris.


“Kivipi handsome kama wewe, tajiri kama wewe na mtaalamu kama wewe, uliyeishi Marekani na msomi mwenye kampuni kubwa ya usafirishaji, usiweze kuoa?” Maneno yakamwagika toka kinywani mwa Limasi. Bado Timasi alikuwa anatamani afike nyumbani ili maongezi yale yaishe, lakini haikuwa rahisi.


“Hamna Limasi. Kila kitu huenda kwa mipango tu. Nadhani nitaoa sasa.” Akajibu Idris na kumuangalia Limasi ambaye alikaa upande wake wa kushoto na Timasi akiwa nyuma kafura kwa tabia za dada yake.


“Utamuoa nani?” Akauliza kwa hamasa Limasi. Kabla hata Idris hajajibu, akazidi kuendeleza maswali yake na maneno mengi. “Kama dada yangu nitafurahi sana. Lakini naye kaolewa ila nina rafiki pia anapenda kuolewa na Mtanzania. Au tayari wifi tunaye, nisijekuwa najipendekeza hapa.”


“Jamani Limasi, si utulie dada?” Kwa unyonge Timasi akamuhasa dada yake ambaye alikuwa bingwa wa kuzogoa ndani ya Ferrari.


“Dada, siongei na wewe. Hapa naongea na shem wangu mpya. Eti Idris, shemeji langu, utamuoa nani?” Akazidi kuonesha ujuaji wake.


“Natamani wewe ndiye nikuoe.” Akajibu Idris. Mshtuko wa moyo ukampata Limasi. Mapozi yakamuisha. Akatazama pembeni ya kioo na aibu fulani ya kike ikamchukua.


“Eheee! Endelea sasa. We’ si kiboko ya kuungia wenzako, linywe hilo sasa.” Timasi akaongea huku akicheka.


“Vipi. Mbona kama umepoa ghafla? Kuna tatizo?” Akauliza Idris. “Au nimekukwaza Limasi.” Maswali yakaendelea bila kikomo lakini Limasi alikuwa kimya na hakuongea tena hadi anafika nyumbani walipopanga kufika.


“Idris, ahsante sana kwa kutufikisha nyumbani. Hapa ndio kwetu na dada yangu karudi, unaweza kuwa unakuja kumchukua.” Aliongea Timasi huku katabasamu lakini Limasi alimtazama kwa macho ya ghadhabu baada ya kusikia maneno yale.


“Dada naomba uniteme.” Limasi aliyeoonekana ni mjanja mjanja, alimbwatukia Timasi kwa hasira.


“Linywe mama. Umeyataka mwenyewe. Idris, mchumba huyu, nakuachia.” Timasi akazidi kupamba maongezi na wakati huo akifungua mlango tayari kwa kutoka ndani ya gari. Lakini badala ya Limasi kumuaga Idris Iris, naye alifungua mlango wa Ferrari ile matata na kwa hasira akabamiza mlango wake na kwenda anapopaswa kuishi. Idris akabaki anamshangaa mrembo yule matata.


“Idris. Mzowee dada yangu kwa leo tu. Namjua mimi.” Dada mtu ikabidi amtetee Limasi kwa kile kitendo.


“Usijali Timasi. Kawaida tu!” Akaonesha urijali wake.


“Okay. Karibu basi nyumbani kwangu. Mbona hutoki humo?” Akauliza Timasi akiwa anachungulia kwenye kioo cha gari, upande aliokuwa kakaa Limasi.

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog