Search This Blog

Thursday 29 December 2022

MIKONO YA JASUSI - 4

  

  Simulizi : Mikono Ya Jasusi 

Sehemu Ya Nne (4)





"Huyu mtu ni mpuuzi na hawezi kufika mahali popote najua ni lazima atakuwa amemuhoji yule marehemu kupata kitu kuhusu sisi hivyo huu ni mpango mzuri maana ni lazima atakuwa mbioni kututafuta. simu ya yule marehemu aliichukua na nilipompigia marehemu alipokea yeye...!" Binti mmoja kuzungumza. Huyu alikuwa ni yule mwana dada mwenye mrefu na mrembo awaye karibu na Mohammed Saloom muda wote ambaye alitambulika kwa jina la Maria.


"Ulimsikia sauti ili kumjua ni wa jinsia gani?" Akadakia Mohammed.




"Hapana hakuwa mjinga kujitambulisha kwangu nilikuwa nikimtegea naye akawa ananitegea pia hivyo nikaamua kukata simu na kuiharibu kabisa ile laini ili asinipate daima." Maria alizungumza. Na huyu ni yule mwanamke ambaye alikuwa akionekana mara kwa mara na Dokta Lumoso Papi Mmbai katika viunga vya Hospitali ya Bombo. Na huyu ndiye alikuwa akizungumza lugha za mafumbo na yule jamaa ambaye alipambana na Alan kule kwenye wodi namba nne ndani ya jengo la Cliff.




"Umefanya vema Maria hii itampa shida kidogo hata hivyo bado ninamashaka na kauli yako kuwa inawezekana alipata kumuhoji yule marehemu na kupata chochote kutuhusu kweli...!"


"Si rahisi Bosi...!"


"Kwanini isiwe rahisi...?" Aliuliza kwa hamaki Mohammed.




"Nimeongea na Dokta Robinson Mango na akaniambia kuwa kifo cha yule jamaa hakikuwa na shaka ya kuhofia siri zetu kutoka kabisa na alikufa akiwa anapambana na jambo hili. Alisema kuwa ilivyoonekana ni kwamba jamaa alikuwa akilazimisha kuchota siri zetu pale kwa kumjeruhi na kumpa mateso alimradi afanikishe lengo na dhamira yake hata hivyo yule jamaa alikuwa mkaidi na alikuwa yuko tayari kufa lakini si kutoa siri zetu nje. Kifo kimemkuta akiwa kwenye 'movement' ya kutaka kufanya jambo fulani la kujihami na kwa uthibisho wa hicho walichokigundua ni kisu ambacho kilikutwa mikononi mwake." Alieleza Njorinjori au Mathew Bangile. Huyu alikuwa ndiye mpokea taarifa wa pande zote na kuzifikisha mahali husika. Alikuwa makini sana.




"Namuamini sana Dokta Robinson Mango ni mshirika wetu mzuri na anatenda kazi yake vema nadhani ilifanyika busara kubwa sana kumvuta huyu mtu na kumfanya kuwa upande wetu...unataka kuniambia aliwahi mapema mahali pa tukio?" Aliuliza mwishoni yule mzee au Bosi. Zayd, faraja ikianza kuinawirisha sura yake kwa kasi kubwa.




"Alifika kule baada ya kupokea taarifa za kuhitajika na yule jamaa kama ambavyo Maria alisema, hivyo akawa mtu wa kwanza kulishuhudia lile na yeye ndiye aliyehakikisha hakuna kitu kinajulikana kwani haraka aliweka mazingira sawa kama kufuta damu zilizokuwa zikianza kusambaa sakafuni na kwenye mwili wa yule mgonjwa kisha akamfunika shuka jeupe akaita machela akatolewa mule ndani na kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti huko akafanya shughuli zote akiwa makini huku akimtahadharisha mlinda jengo lile la kuhifadhia maiti kuwa ile ibaki kuwa siri kwake. Alifanikisha hata hivyo baada ya muda kidogo baadaye alimchanganyia sumu yule mlinzi wa chumba cha maiti na kumuua ili siri ile ya mwili ule kupigwa risasi ibaki kuwa yake. Akautelekeza mwili wa yule jamaa kule kwenye masanduku ya kuhifadhia maiti huku mwili ukiwa hauna taarifa wala kadi lolote."


"Safi sana Mathew, nimependezwa mno na utendaji wa huyu Dokta na umakini wake unanifurahisha mno kwani hata ikija kugundulika baadae kuwa kuna mwili mule ndani una majeraha ya risasi hautajulikana umetokea wapi na pia hakuta kuwa na taarifa zake kwa kuwa hazipo na hazitokuwepo na mlinzi hakuona. Huyu mjinga ana akili za ziada sana na madaktari kama hawa wangekuwa saba tu kwenye taifa hili Waallah! Kusingekuwa na sababu ya kusafirisha wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi." Akamaliza kuongea Mohammed akionekana kuwa na furaha sana huku akifurahishwa zaidi na ufanyaji kazi wa vijana wake.




"Watapata taabu sana kufika wanapotaka kuja na tutawaua hadi tufanikishe lengo letu la kuimaliza hii idadi ambayo tumepanga kuifyekelea mbali." Akaongezea Zayd.






Huyu mjinga ana akili za ziada sana na madaktari kama hawa wangekuwa saba tu kwenye taifa hili Waallah! Kusingekuwa na sababu ya kusafirisha wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi." Akamaliza kuongea Mohammed akionekana kuwa na furaha sana huku akifurahishwa zaidi na ufanyaji kazi wa vijana wake.




"Watapata taabu sana kufika wanapotaka kuja na tutawaua hadi tufanikishe lengo letu la kuimaliza hii idadi ambayo tumepanga kuifyekelea mbali." Akaongezea Zayd.




"Si hilo tu Bosi, Dokta Mango ameniambia kuna kitu kisicho cha kawaida amekiona na anakwenda kukifanyia kazi na majibu yake yapo muda mfupi mbele. Anachotaka ni kuhakikisha hakuna siri inayokuwa wazi." Mathew akazungumza na kumfanya Mohammed na Mohammed kufurahi zaidi na wala hawakuuliza ni jambo gani hilo bali alichokifanya Zayd ambaye ndiye kiongozi mkuu wa jopo hilo ni kutoa maagizo kwa Maria.




"Maria hebu waambie watunza pesa wetu wamuingizie huyu Daktari kiasi cha shilingi milioni tatu kwenye akaunti yake ananifurahisha sana halafu naomba niunganishwe naye sasa hivi." Alipokwisha kusema hayo Zayd Aboushariff, Maria alisimama na kutoka mule chumbani akizitikisa nyama zake za nyuma kwa maringo makubwa. Akapotelea kwenye mlango wa chumba kingine. Alipoteza muda wa kama dakika mbili kisha akarejea akiwa anatabasamu.




"Zoezi linafanyika Bosi nadhani ndani ya masaa mawili baadae kiwango hicho cha pesa kitakuwa kikiogelea kwenye mifuko yake ya benki." Alisema Maria huku akiisogelea meza ndogo iliyoko pembeni ya kiti cha Zayd Aboushariff na kunyanyua kiwambo cha simu akaminya namba kadhaa kisha akauvuta mkonga wa simu ile na kumkabidhi kiwambo kile Bosi wake.




"Dokta Mango?" Aliita Zayd Aboushariff akiwa na bashasha usoni mwake.




"Ndiyo mkuu...!" Sauti ya upande wa pili wa simu ile ilisikika.




"Tunakwenda vizuri na hapo ulipofikia ni hatua ambayo haina ubaya. Kuna kiasi cha pesa ya maji ya kunywa kwenye akaunti yako ya benki umewekewa." Alizungumza Zayd.




"Asante sana Bosi kwa hilo, nimefurahi mno na naahidi kuwa bega kwa bega nanyi."


"Ok, sawa 'make sure every thing is ok,' nataka kuona unafanya kazi kwa kiwango kile nilichokitegemea." Akamaliza na wala hakusubiri majibu, akakata simu akairudisha mikononi mwa Maria huku akiwa anazungumza.




"...watu kama hawa hutakiwi kupata nao shida, wape pesa uone kazi itakayofanyika si mmeona wenyewe jinsi alivyofurahi na ameshajua ni kwanini nimempa hii pesa." Kikao hiki kilifika tamati kwa kila mmoja kuwa na imani kubwa kuhusiana na mipango yao namna inavyokwenda vema, walikuwa na uhakika kuwa huyo mtu ambaye ameingia na kuanza kuleta hofu kwao hawezi kuchukua muda mrefu atakuwa amenasa kwenye maua waliyoyatega kwenye kila pembe jijini.




Kikao hiki wakati kinatawanyika, simu ya Alan ilikuwa ikiita kutokea mezani, aliinyakuwa na kuiweka sikioni na ni baada ya kujua mtu aliyempigia.




"Maisara habari yako?" Alisalimia.




"Salama Mr. Jabir, vipi hali yako?" Akajibu salamu Maisara.




"Salama haya nijuze?"


"Niko nje hapa Maua Inn nimeshafika tayari." Alisema Maisara. Alan akanyanyuka tokea kitandani na kuelekea hadi dirishani akavuta pazia kidogo na kuchungulia upande wa chini. Chumba chake kilikuwa kikipeana ubavu na sehemu ya mbele ya hii Hoteli hivyo haikumpa shida kumuona huyo msichana upande wa chini. Alivalia sketi fupi nyeusi na viavu virefu, akiwa amesuka nywele zake kwa mtindo wa rasta.




"Ohoo! Ni vema kama uko chini hapo naweza kukuelekeza sasa...njoo ghorofa ya pili chumba namba 16."


"Ok, hakuna shaka." Aliitikia Maisara kisha akakata simu. Aliingia hadi mapokezi ambako alijitambulisha na kusema kuwa kulikuwa na mwenyeji wake ghorofa ya pili chumba namba 16, akataja hadi jina la mwenyeji wake hata hivyo idara ya mapokezi ilichukua jukumu la kujihakikishia hilo kwa kuamua kumpigia mtu aliyeuliziwa, walipojiridhisha na majibu hakuzuiwa akaruhusiwa kuingia. Akazipanda ngazi taratibu hadi ghorofa husika. Aligonga mlango akafunguliwa na kukutana na tabasamu la aina yake lililomkaribisha kwa kumchombeza. Walikumbatiana na kubusiana walipokuja kuachiana, Alan alimkaribisha mgeni wake kwenye kiti kisha akafungua friji na kutoa mvinyo ambao aliuagiza mapema kwa ajili ya mgeni wake huyo.




"Karibu sana mrembo?" Alikaribisha kwa mara nyingine Alan.




"Nimeshakaribia!" Alijibu Maisara akiwa kwenye sura ya aibu. Walipiga hadithi hii na ile hadi pale mvinyo ulipoanza kuwakolea ndipo maswali ya hapa na pale yalipoibuka.




"Utaendelea kuwepo hapa Tanga kwa muda gani Mr. Jabir?" Lilikuwa swali la kwanza kuuliza Maisara.




"Niko kwenye likizo kama nilivyokuwa nimekueleza awali. Hivyo nitakuwa hapa mjini kwa mwezi mzima nadhani." Maisara akamuangalia Alan kuanzia usoni hadi kifuani alipofika kifuani akayatuliza macho yake kwa kitambo kifupi kabla hajayahamishia pembeni huku tabasamu la mahaba likijitunga usoni mwake. Alipendezwa sana na kifua cha huyo kijana na pia kilimpa maswali mengi sana kwani kilikuwa tofauti sana na vijana wengine ambao walionesha kuridhishwa na maisha. Pengine alitaraji kukutana na kifua cha kawaida huku kitambi cha mridhiko wa maisha mazuri kikionekana kikitunga hata hivyo haikuwa hivyo, kifua kipana kilichojichora kwenye singleti nyeupe na misuli iliyotutumka kuonesha kuwa kijana huyo alikuwa na ratiba nzuri ya mazoezi kilimvutia sana na kutamani hata kukiweka kichwa chake kifuani hapo.




"Nitakuwa ni mtu mwenye bahati sana Mr. Jabir kuweza kuwa nawe kwa mwezi wote huu." Alisema Maisara baada ya kutoka kumtazama kijana huyo kwa kitambo kirefu.




"Nadhani huu ni wasaa wangu wa kufurahi maisha ya kimapenzi japo si kwa muda mrefu...!" Aliongezea kisha akatuama na kutazama pembeni kwa jozi ya sekunde akarudisha tena macho usoni mwa Jabir na kuzidisha tabasamu hata hivyo akazidi kudadisi.




"Umenibamba...najua uko na familia kama sikosei; mke na watoto si ndiyo...?" Jabir akajipa utulivu kabla ya kukurupuka kujibu. Alikuwa akimtazama usoni mrembo huyo huku akimchunguza kwa ukaribu zaidi na kuzidi kumtongoza kwa tabasamu lake la mahaba. Hata hivyo hakuwa ameupata wasaa wa kujibu kwani binti huyo alishaomba makazi kinywani mwa kijana huyo na kuuhifadhi ulimi wake. Walipeana radha ya mate kwa takribani dakika tatu pasipo kuachiana ni miguno tu ya kuzidiwa na utaku waliokuwa wakipeana ndiyo iliyokuwa ikihanikiza eneo hilo. Simu ile ambayo alikuwa na hakika kuwa yule muuguzi anayefahamika kwa jina la Zaituni angepiga, alikuwa ameizima ili kuepusha mkanganyiko wa maswali kwa Maisara. Masara alikuwa amevaa kimtindomtindo sana kiasi kumuacha Alan akiwa na shauku kubwa ya kutaka kumtafuna. Mapaja yake malaini yaliyonona yalikuwa wazi kwa kiasi kikubwa kutokana na kashikashi ile ya kunyonyana ndimi. Mikono yake laini haikuacha kukipapasa kifua kipana cha kijana huyo ambacho kimekuwa kikipitia mazoezi ya mara kwa mara. Aliivua singleti ya kijana huyo na kuitupia mbali kisha akamalizana na bukta aliyokuwa ameivaa kwa wakati huo wa usiku. Muda mfupi mbele, wote walikuwa wakifanana. Maisara alikuwa ni mrembo wa haja sana hasa akiwa katika kipindi ambacho nguo zake zote zimetolewa mwilini mwake. Matiti yake makubwa ya mviringo yaliyotuna na kubeba chuchu nyeusi tii! Macho yake malegevu sambamba na kingo zake pana za midomo ndizo hasa zilizommaliza nguvu Alan. Alikuwa akimnyonya binti huyo kwa utaratibu maalumu huku akihakikisha anamtaabisha ipasavyo. Miguno ya kimahaba ilikuwa haikomi hata kidogo na muda mfupi mbele kelele za mahaba zikaongezeka kasi baada ya kuingia kwenye mtanange wa awamu ya kwanza, ilipokwisha wakaunganisha awamu ya pili na walipoimaliza walikuwa hoi na kila mmoja akajitupa upande wake huku wakipongezana kwa kuoneshana uhodari.




_____________




Saa kumi na mbili juu ya alama Maisara anashtuka akitokea kwenye usingizi mzito. Alan yeye alikuwa ameshtuka muda sana na alikuwa akimtazama mrembo huyo huku akiwa haamini kama amemtafuna kweli. Walitabasamu kwa kitendo kile cha kutazamana kisha kumbukumbu ya kile walichokifanya usiku kikajirudia tena. Maisara aliuma kingo ya juu ya mdomo wake kwa hisia kali na kujikuta akimvamia tena Alan.




"Please Mr. Jabir give me once agan." Alisema Maisara huku akipanda juu ya kifua cha Alan na kujipimia mwenyewe na kuanza tena misukosuko ya kusafiri safari ya asubuhi huku miguno ya kimahaba ikiwa imenoga kwelikweli. Alionekana kuufurahia mchezo ule kwa kiwango kikubwa sana kwani alikuwa akiongea lugha za ajabu ambazo hazikuwa zikieleweka hata kidogo. Dakika arobaini zilitosha kumaliza mchezo ule. Maisara aliitazama saa ya ukutani na kujikuta akishangaa sana baada ya kuona zilibakia sekunde chache kufikia saa moja kamili ya asubuhi. Alikurupuka na kukamata taulo ambapo alijifunga imara kabisa na kupotelea bafuni. Alioga kwa muda wa dakika kumi akatoka na Alan naye akazivuta hatua kulekea huko. Alipofika kwenye mlango wa bafu akageuka nyuma kumtazama Maisara ambaye kwa wakati huo alikuwa amempa mgongo. Loh! Kitu asichokitarajia ndicho alichokiona kwenye macho yake. Alijikuta akikumbwa na mshangao mubwa sana mara baada ya kuona kitu kile. Aliingia bafuni akiwa ni mwingi wa maswali mengi mno. Lilikuwa ni Ua kubwa lililokuwa likifanana kila kitu na lile lililokuwa limechorwa kwenye ile karatasi na kufichwa ndani ya moja ya droo za kitanda kile cha Hospitali ndani ya wodi namba 04 kwenye jengo la Cliff. Mawazo mengi yalipita kichwani mwake huku jazanda la yule mwanamke likijengeka upya kichwani mwake. Hawa wanawake wako wangapi? Akawaza hata hivyo hakuwa na jibu la kujipa. Hakika lilikuwa ni lile Ua la Bee Balm. Akafikiria sana maana ya mchoro huu kukaa kwenye mwili wa mwanamke mrembo kama Maisara tena mgongoni kisha uchorwe kwenye karatasi. Hawa watu walikuwa na mpango gani hapa mjini.




HATIMAYE ALAN KWA MACHO YAKE ANASHUHUDIA UA LA BEE BALM LIKIWA MGONGONI MWA MAISARA. SWALI LA KUJIULIZA HAWA MA BEE BALM WAKO WANGAPI HAPA JIJINI JE, NI MMOJA? NA KAMA NI MMOJA, MARIA NI NANI, ISABELA NI NANI? NA JE, NI HAWA HAWA AU KUNA WENGINE. HUU NI MTITI AISEE.






Mawazo mengi yalipita kichwani mwake huku jazanda la yule mwanamke likijengeka upya kichwani mwake. Hawa wanawake wako wangapi? Akawaza hata hivyo hakuwa na jibu la kujipa. Hakika lilikuwa ni lile Ua la Bee Balm. Akafikiria sana maana ya mchoro huu kukaa kwenye mwili wa mwanamke mrembo kama Maisara tena mgongoni kisha uchorwe kwenye karatasi. Hawa watu walikuwa na mpango gani hapa mjini. Jambo hili likamfanya hata kumfikiria yule bwana aliyempa simulizi ya kifo cha Luteni Jenerali Leous Mipango. Kuwa mwanamke ndiye aliyehusika na kifo cha mwanajeshi huyo. Kwa namna fulani matukio yalikuwa yakiungika hata hivyo hakuweza kumuhusisha Maisara moja kwa moja kwani jina la mwanamke aliyehusika kuyaondoa maisha ya yule mwanajeshi hakuwa akiitwa Maisara na badala yake aliitwa Isabela. Kichwa kiliimuuma hata kuoga hakuoga ipasavyo. Alirudi chumbani mule na kumkuta Maisara akiwa amekaa kitandani akimsubiri baada ya kuwa ameshavaa nguo zake tayari. Alipoingia alibadili nguo tofauti na alizokuwa nazo siku iliyopita na kuvaa suruali ya jeans nyeusi na fulana ya rangi nyekundu isiyo na maandishi wala michoro ya aina yoyote. Alivaa buti ya ngozi; safari buti. Maisara alinyanyuka tokea kitandani na kumsogelea Alan na kumuweka sawa kola ya fulana ile sambamba na kumshika hapa na pale kama kujihakikisha kuwa alivaa vizuri.




"Leo utakuwa wapi mpenzi...?" Aliuliza Maisara akiwa ameegemeza mkono kifuani mwa Alan. Alan alimtazama kidogo na kukamata nywele zake katika mtindo wa kumpapasa. Wazo lake kuu lilikuwa likimsukuma kumuweka chini ya ulinzi mkali huyo mwanamke na ambane kuhusiana na Ua lile lilikuwa na maana gani mwilini mwake hata hivyo alipingana vikali na wazo lake hilo. Aliona ni bora ajipe kwanza utulivu ili aweze kuzisoma nyendo za Maisara huwenda kufanya hivyo kungempa mengi.




"Leo kuna safari fupi fupi naweza kuzifanya hapa mjini au naweza kwenda hata Muheza kuna jamaa yangu nilisoma naye hapa mjini shule ya Sekondari ya Galanosi kipindi hicho cha nyuma." Alijibu Alan hata hivyo sidhani kama alikuwa sawa juu ya majibu yake. Akili yake ilikuwa ikifikiria vitu vingi kwa wakati mmoja. Waliagana kwa mabusu mazito kisha Alan alimsindikiza binti yule hadi nje ya Hoteli akamuacha akiondoka. Wakati anarudi chumbani kwake akiwa anazipanda ngazi taratibu, yale maneno aliyokuwa akiyasikiliza kule kwenye wodi ya Cliff yakajijenga tena upya. Akawa anayakumbuka maneno mawili tu ambayo yalikuwa yakimtatiza sana 'Ua, nyuki; nyuki, Ua,' yakawa ni maneno yasiyo kwenda mbali kimafikirio yake. Akayaundia matukio na mwisho wa yote alikuja kugundua kuwa huwenda hawa wanawake wakawa ndiyo maua mahususi kwa ajili ya kuwavuta karibu maadui. Amemjua adui ambaye ni miongoni mwa maua yaliyopandwa kila upande wa mji huu ili tu aweze kuingia mtegoni mtu kama yeye au wale ambao waliwakusudia kuwaingiza kwenye himaya yao. Hapa sasa akawa amepata maana ya Bee Balm jina la Ua ambalo ni kivutio kikubwa cha nyuki na viumbe na viumbe wengine wavutiwao na maua mazuri. Hawa ndiwo wanaohusika na kifo cha Luteni Jenerali Leous Mipango. Akajihakikishia nafsini mwake ingawa alitamani sana kukutana na huyo aliyetwa Isabela. Aliingia chumbani kwake akapanga zana zake za kazi katika mpangilio mzuri kisha akaficha zile ambazo hakutaka kuzitumia kwa wakati huo na kufikiria nini cha kufanya. Kwanza aliikumbuka simu yake ambayo ilikuwa na namba za watu wasio wa muhimu, ilikuwa bado imezimwa hivyo akaiwasha, kitendo kile cha kuiwasha tu kukawa kumeingia jumbe kama mbili, moja ilikuwa ikimjulisha kuwa namba fulani ilimpigia mara nyingi wakati akiwa amezima simu na ujumbe mwingine ulikuwa ni wa lawama kutoka kwenye namba ileile ambayo ilipiga mara nyingi ukimuuliza sababu ya kutokuwepo hewani kwa wakati ule. Hakujisumbua kuujibu kwani hakuona sababu ya kujibu ujumbe wakati alikuwa na salio la kutosha. Alishamjua mtu huyo ni nani. Akaipiga hiyo namba.




"Habari yako?" Akasalimia Alan baada ya simu ya upande wa pili kupokelewa.




"Sitaki unatabia mbaya kaka Abasi, ndiyo nini mimi nakupigia simu jana uje nyumbani na hukupatikana...?" Alilalamika Zaituni yule muuguzi.




"Hapana Zaituni, unajua kazi zetu hizi za uandishi wa habari ni ngumu sana. Hatuna muda mahususi wa upataji wa habari zetu mara nyingine huwa tunapewa taarifa ya tukio hata usiku wa manane. Utanisamehe sana mpenzi." Akajitetea kwa uwongo mwingi Alan huku akitabasamu kwa namna alivyoweza kuyatumia majina yake ya kughushi vema bila kutetereka.




"Sawa hata hivyo ungeniambia tu." Alilalamika Zaituni.




"Uko nyumbani kwa sasa?" Akauliza Alan huku akiyapuuza malalamiko yale.




"Ndiyo niko nyumbani."


"Nitafika hapo kwako saa sita kamili mchana napenda uniandalie chakula kizuri kama huto jali."


"Usijali kaka yangu...!"


"Niite mpenzi bwana Zaituni...!" Alidakia Alan na kumfanya Zaituni aangue cheko la haja kisha akasema;




"Mmh! Haya kama unapenda iwe hivyo...!"


"Kwani wewe hupendi iwe hivyo?"


"Mimi sijui...!" Akajibu kwa aibu Zaituni. Wakamaliza maongezi yao kwa utani wa hapa na pale na kuagana kwa minajili ya kukutana muda wa saa sita mchana.




_________




KIJANA IDDIALAN SIMION ALIKUWA KATIKA MATEMBEZI YAKE NDANI YA MITAA ILE NA HII HAPO JIJINI TANGA. Matembezi haya yalikuwa ni ya kawaida sana na alitaka kuyapa macho yake kitu cha ziada. Ni muda mrefu sana aliondoka hapa mjini na kwenda ughaibuni kabla ya kurudi nchini akiwa ni kijana mwingine kabisa. Hakuwa amepata wasaa wa kufika hapa jijini kwa kitambo hicho kirefu hivyo kila alichokiona machoni mwake ni kama kilikuwa kipya. Alikuwa akitokea Chumbageni, alikamata barabara ya Chumbageni Polisi akiwa kwenye mwendo wa kawaida kabisa akaja kukutana na barabara iendayo Tanesko akaiacha barabara hiyo na kuingia kulia akiifuata Taifa road. Aliambaa na barabara hiyo akiipita barabara ya kwanza, pili tatu na nne kabla ya kuupita uwanja wa Tangamano. Alipofika barabara ya kumi na sita akaingia kushoto na kuifuata barabara hiyo taratibu akiyapita maduka mengi ya nguo, vifaa vya umeme na ya vipodozi. Alipofika mtaa wa Makoko, hakunyoosha na hiyo barabaraba, alikunja kulia akiifuta barabara ya kumi na saba kumi na nane. Akaupita mtaa wa Lumumba. Akatazama kwenye kioo cha pembeni yake kuona kama kulikuwa na gari au mtu aliyekuwa akimfuatilia. Hadi hapa hakukuwa na mtu wala gari yoyote iliyomjengea hisia mbaya akilini mwake. Ila wakati anauvuka mtaa huu wa Lumumba kuingia mtaa wa Usambara, kuna gari nyeupe Toyota Noah ilichepuka ikitokea barabara ya kumi na sita ikionekana kuja upande aliyopo. Akaitazama kwa umakini ile gari ili kuona kama kuna namna yoyote ya hatari aliyoundiwa hivyo akapunguza mwendo katka namna ya kulitegea. Lile gari nalo lilipunguza mwendo. Machale yakamcheza na damu kumkimbia mwilini, alikuwa kwenye hali ya hatari na hakutakiwa kujisahau. Akaongeza mwendo akiupita huu mtaa wa Usambara. Ile gari nayo ikaongeza kasi ikiwa nyuma yake. Hadi Alan anafika msikiti wa Markaz Tabligh Tanga, ile gari ilikuwa karibu mno. Hakukuwa na namna nyingine zaidi ya kutafuta namna ya kuikimbia. Akakunja kona kwenye mitaa hii na ile alikuwa katika mwendo wa kasi kidogo. Alipofika mtaa wa Swahili akatazama tena nyuma na hakuiona tena hii gari. Hakutaka kujihakikishia usalama bado alijiona yu katika wakati mgumu sana hivyo alikuwa kwenye kasi ile ile akaja kutokea kwenye kanisa la Protestant. Hali ya hewa ya ufuatiliwaji wake uliridhisha na hakuona haja ya kuongeza tena kasi. Akaingia barabara ya Jamhuri. Hakutaka kuifuata hii barabara na badala yake alirudi nyuma hadi mzunguuko wa barabara wa Mabanda ya papa. Akaikamata barabara ya kwa mkuu wa mkoa. Ni punde tu wakati anamaliza huu mzunguuko ndipo alipoona tena hii gari ikiwa hatua kadhaa nyuma yake. Loh! Ilikuwa ni hatari ya wazi wazi. Alijiuliza sana kuhusiana na hiyo gari hata hivyo hakuwa na kumbukumbu nzuri kama kulikuwa na chanzo cha yeye kufukuziwa namna ile. Hakujua ni wapi aliweza kuonekana na maadui hadi kuanza kumfuatilia. Hakuwa na namna hata hivyo zaidi ya kuongeza kasi mara dufu. Alikanyaga pedeli ya mafuta kabla hayapunguza mwendo mtaa wa viwanda. Akaifuata barabara hiyo na kukipita kiwanda cha Foma. Hapa ile gari ilikuwa mbali kiasi hivyo alikuja kuigesha gari yake kwenye karakana moja ya magari iliyopo nyuma ya hiki kiwanda cha Foma. Akateremka na kujibana kwenye pembe upande wa reli akitazama kule alikoiacha gari yake. Gari ile iliyokuwa ikimfuatilia ilisimama nyuma hatua chache kabla ya kufika chini ya mwembe nyonyo ambako ndiko Alan alikoiacha gari yake. Loh! Waliteremka watu watatu wakiwa kwenye mavazi ya suti kali huku mmoja kati yao akiwa amevaa miwani ya jua na mwingine akiwa amevaa kofia ya kukinga jua aina ya pama, huyu mwingine wa tatu akiwa hajaongeza ziada yoyote ya mavazi yake. Wakatazama mahali gari ya Alan ilipo kisha wakapeana ishara kuwa waifuate. Wakapiga hatua kuisogelea. Wakati wakiwa wanaisogelea pasipo shaka, Alan alikuwa akiendelea kuwachungulia huku mkono mmoja ukiwa kwenye kiuno chake akihakiki uwepo wa silaha yake. Wale watu walipolifikia gari lake mmoja akalisogelea na kulikagua kisha akatoa ishara kuwa hakukuwa na mtu ndani. Wakawa wanaangaza huku na kule na wasione mtu. Wakagawana mmoja akaingia ndani ya ile karakana huku wawili wakifuata uelekeo ambao Alan alikuwapo. Ilikuwa ni hatari sana kwa upande wa Alan kwani kila alipowatazama watu wale hakika hawakuwa watu wazuri hada kidogo. Alijitoa pale na kukifuata kidaraja cha maji machafu ya povu la sabuni yatokayo kiwandani akaingia chini ya kile kidara na kutulia. Kimya kilimzunguuka huku pumzi za hofu ndizo zikiwa pekee ambazo alizisikia. Hakuacha kutazama huku na kule kuangalia kama kulikuwa na dalili zozote za kuwepo kwa mtu. Hakuwa amejua kama watu wale waliku wamekwenda upande wa juu wa ule mfereji wakitafuta kama adui yao alikuwa mahali hapo. Ilikuwa ni bahati sana Alan kutazama upande ule kwani alikutana macho kwa macho na yule jamaa aliyevaa miwani ya kukinga mionzi mikali ya jua akiwa amesimama kando ya ule mfereji.




"Yule pale mpuuzi...!" Yule jamaa aliyevaa miwani ya jua alipayuka. Wakaanza kuchomoa bastola zao na kuanza kumuelekezea huku wakimkimbiza. Alan kuona hivyo ikambidi kukimbia kwa kasi kulifuata kona moja ndani ya ule mtaro. Risasi zikaanza kuvurumishwa ambazo zilikuwa zikimkosa kwa kiasi kidogo sana.




"Anakimbia mtokee kwa juu...muuweni tu...!" Jamaa mmoja aliongea huku akimimina risasi ambazo zilikuwa zikichimba udongo na nyingine zikipiga kwenye kingo za kile kidaraja na kuifumua vibaya sana zege yake. Alan alikuwa akitokwa na jasho jingi sana, hofu ya kupigwa risasi kisha kufa kipumbavu ilimtawala. Hakutaka aibu hiyo ya kushindwa kupambana na maadui waliyopo ndani ya taifa lake. Alidhamiria kuhakikisha anapambana hadi tone la mwisho la uhai wake. Hivyo aliikamatia bastola yake vizuri mkononi na kupiga mahesabu ya haraka, akajirusha kutokea pale chini mferejini na kubingilia juu ya ule mtaro. Lahaula! Ilikuwa ni chupuchupu sana kichwa chake kiweze kufumuliwa na risasi kwani kabla hajafika kwenye reli. Risasi ilipita pembeni kidogo ya ubavu wake na kujikita kwenye chuma cha reli. Kelele kali za mgongano wa chuma cha reli na ile risasi ilikwenda kuziumiza ngoma zake za masikio hata hivyo hakuacha kuhakikisha shabaha za adui zinakuwa maboya. Alipoivuka ile reli, alimuona yule jamaa aliyevaa pama akiwa ndiye anayemsulubu kwa kumkosa kwa risasi. Shabaha zake kali hazikufanya makosa. Yule jamaa alisukumwa nyuma huku mguno mdogo wa maumivu ukimtoka baada ya kupokea risasi ya kifua. Alan hakuridhika akaachia risasi nyingine ambayo ilipenya upande wa moyo ikampeleka yule jamaa chini mazima akiwa hana uhai.






Alipoivuka ile reli, alimuona yule jamaa aliyevaa pama akiwa ndiye anayemsulubu kwa kumkosa kwa risasi. Shabaha zake kali hazikufanya makosa. Yule jamaa alisukumwa nyuma huku mguno mdogo wa maumivu ukimtoka baada ya kupokea risasi ya kifua. Alan hakuridhika akaachia risasi nyingine ambayo ilipenya upande wa moyo ikampeleka yule jamaa chini mazima akiwa hana uhai.




SONGA NAYO....




Alan hakutaka na wale wawili wamkute pale, alisimama na kutimua mbio akiufuata ujia mdogo wa watembeyao kwa miguu akiwa anaranda pembeni ya uwanja wa mpira wa miguu wa eneo hilo. Wale jamaa walipotoka mtaroni walimuona Alan akiwa anatokomea kuwakimbia hivyo wakamuungia mkia. Walimkimbiza kwa kasi kubwa hata hivyo hawakuambulia kitu kwani Alan alishafika kwenye jengo moja lililotelekezwa na kuingia ndani yake kwa kuwa jengo hilo halikuwa na mlango. Wale jamaa walipofika hapo wakazikamatia bastola zao imara na kuingia ndani wakiwa kwenye tahadhari kubwa.




Alan alipokuwa ameingia mule ndani alijua fika watu wale asiyowajua ni lazima wangefika eneo hilo. Hivyo alitafuta mahali pazuri ndani ya chumba kimoja pembeni ya mlango akajibanza. Wale jamaa walipofika kwenye jisebule kubwa la jengo lile wakagawana na kila mmoja akaelekea kwenye upande wa vyumba vyake huku wakiwa na wasiwasi mkubwa. Huyu mmoja ambaye yeye hakuwa amevaa ziada ya vazi lolote zaidi ya suti yake nyeusi na kiatu kirefu kigumu cha ngozi, alikuwa akijongea taratibu upande ambao Alan alikuwa amepangisha kwa muda. Silaha yake ilikuwa mbele kwa lolote lile. Alichunguza hapa na pale bila tahadhari ya dhati akaingia kwenye chumba alichomo Alan. Pigo moja la karate, likaitupa mbali ile silaha kisha akamvamia kwa mapigo mengi hata hivyo jamaa alikuwa yuko vizuri akawa analeta upinzani mkubwa kwa kijana huyo. Alan alijua kwa kuwa hilo jengo lilikuwa wazi hivyo ni lazima jamaa aliyepo upande wa pili ameweza kusikia vutumai zile hivyo hakutaka kupoteza muda na kujikuta akizidiwa ujanja na watu hao. Alimbadilishia mapigo huyo jamaa hata hivyo bado alikuwa yuko vizuri. Jamaa huyo aliyatoka mapigo ya Alan na kuvurumisha ya kwake ambayo yalimletea shida Alan katika namna ya kuyatoka. Mapigo machache yakamkuta na kumrudisha nyuma jamaa afurahi na kuja kwa kasi kubwa. Alan alimpisha kwa kumkwepa kama aliyekuwa akimkimbia akadandia ukuta kwa namna ya pekee sana kisha akageuka kwa pigo kali sana la teke aina ya flying kick lililompata jamaa nyuma ya shingo. Lilikuwa ni pigo baya sana ambalo lilikwenda kuivunja kabisa shingo ya yule jamaa na kumtupa chini. Muda huo huo risasi zikarindima zikielekea katika chumba alichopo yeye. Hakuwa na njia ya kuweza kukwepa risasi na mpigaji hakuwa akitania hata kidogo. Alijua kama atachelewa kufanya maamuzi basi atakuwa mwenyeji wa risasi za huyo jamaa aliyesali hivyo alirudi nyuma kwa tahadhari na kukimbia kwa hatua zenye malengo, akadandia dirishani kisha kuurukia ukuta kwa upande wa chumba kile kisha akajigeuza kwa sarakasi safi akatua upande wa pili hata hivyo bado alikuwa akiandamwa na zile risasi. Alipofika chumba hicho pia alifanya kama alivyofanya alikotoka. Jamaa kuona hivyo akawa anakuja kwa kasi kubwa kuifuata ile korido ambayo ilibeba milango ya vyumba vile. Alan alimsomea ramani yule jamaa hivyo wakati yule jamaa akiwa anaingia kwenye kile chumba kilichofuata, Alan akawa ametua chini kwa namna ya pekee na kuzunguka kwa mzunguko wa hatari, akamchota mtama yule jamaa. Jamaa akapinduka mwereka hata hivyo alikuwa fundi sana akasimama lakini Alan akawa tayari ameuadhibu ule mkono ambao ulibeba silaha wakabaki wakitazamana kishujaa zaidi.




"Wewe ni nani kwani?" Aliuliza yule jamaa mwenye miwani ya jua ambaye ndiye aliyesalia huku akiwa anatweta vibaya mno kutokana na zile mbio za muda mfupi.




"Nikuulize wewe ninyi ni akina nani ambao mnanifuatilia namna hii bila sababu za msingi." Aliuliza Alan huku akiwa anatabasamu.




"Hii ni oda ya kukuondoa duniani...!"


"Aliyewapa oda hii ya kuniangamiza ni nani...?" Akahoji Alan hata hivyo jibu halikuja, jamaa alirusha ngumi tatu za maana zilizopigwa kitaalamu zaidi hata hivyo Alan alizikataa na kurusha za kwake jamaa akazitoa kiufundi zaidi. Mapambano hayo makali na ya aina yake yalikwenda kuwafanya kila mmoja kuamini kuwa hakuwa na mtu mdogo kimapambano. Jamaa alikuwa fundi sana na alikuwa na uwezo wa kutumia mitindo mingi ya kimapigano. Aliitumia vizuri judo hata hivyo alimkuta Alan akiwa amelalia huko na kuleteana upinzani mkubwa. Mguno wa maumivu ulimtoka Alan baada ya kupokea ngumi nzito ya kifua ambayo ilimteteresha, ile nafasi ya kutetereka ikapelekea kupokea ngumi mbili nyingine za uso akayumba zaidi. Jamaa yule mwenye miwani ya giza alizunguuka na flying kick matata sana ambayo ilimpata Alan na kumtupa chini. Hakika alikiri moyoni kuwa alikutana na mtu fundi sana. Alijizoazoa pale ukutani ambako ndipo aliposukumiwa na kukaa sawa.




"Lazima ufe, hii ni oda nimeambiwa unafuatilia mambo yasiyokuhusu." Aliongea yule jamaa kwa tambo kubwa sana huku akiwa anasogea taratibu. Alan alikuwa akimtazama jinsi yule jamaa alivyokuwa akimsogelea, alimtazama miguu, mwili wake na hata macho. Kwa jinsi hii ni kwamba alikuwa akiusoma mwili mzima wa huyu jamaa. Hii ilikuwa ni mbinu ya pekee sana kuweza kutumiwa na wapiganaji. Jamaa alipomkaribia Alan akatupa ngumi iliyokuwa na lengo la kupiga usoni hata hivyo Alan alikuwa tayari ameshapata jibu la namna gani anaweza kufanya. Alibonyea kidogo na kuhama lile eneo. Mbavu za yule jamaa zilipata dhoruba kali sana baada ya Alan kuzungumza nazo kwa ngumi tatu safi. Kwa kasi kubwa isiyoweza kukaa kwenye maandishi, baada ya ngumi hizo tatu kutua mbavuni mwa jamaa huyo, ngumi moja pekee yenye ujazo ndiyo iliyotumika kukichakaza kidevu cha yule jamaa kiasi kwamba meno matatu ya mbele yakatoka na kurukia mbali huku ute mzito uliochanganyikana na damu ukimwagika sakafuni. Alan aliruka juu na kumpiga teke kali la tumbo yule jamaa na kumtupa mbali sana, jamaa akahisi kutapikatapika tu. Alan akasogea karibu na kusimama karibu yake.




"Ni nani aliyewapa oda ya kuniangamiza?" Akauliza huku akitweta.




"Nakuuliza wewe ni...!" Hakufika mwisho wa swali Alan, alijikuta hewani baada ya kupokea mtama wa maana akatua chini huku mguno wa hofu ukimuingia, jamaa aliweza kumtega Alan vema na kumpa adhabu ile kisha kwa kasi ya ajabu. Akamtwisha Alan kiatu cha kisogoni Alan akaguna tena huku akihisi kizunguzungu na maumivu makali yakimtambaa kichwani mwake. Jamaa aliruka kama nyanda na kumpiga Alan kabali ya maana sana. Ilikuwa ni kabali nzito ambayo ilianza kumpa maumivu makali. Alianza kuona nyota zikiwa zinatembea mbele ya macho yake akaanza kutapatapa kutokana na pumzi kuanza kuwa nzito na mwenyewe kuzitafuta kwa shida kubwa. Jamaa alikuwa akizidisha nguvu ya kabali yake. Sasa Alan alikuwa akifa, alijiona waziwazi kuwa sasa alikuwa akielekea kupoteza maisha akatazama huku na huko kwa taabu kubwa huku akiwa ameitawanya mikono yake sakafuni mithili ya mpiga mbizi. Hakuona kitu cha kumfanya kuweza kujinasua na jinamizi lile la kifo. Akageuza macho yake upande mwingine wa mbele ndipo akaona bastola ile ambayo alifanikiwa kuitoa mikononi mwa huyo jamaa mwanzoni. Lengo lake kuu likahamia kwenye ile bastola ila hakujua namna ambayo angeweza kuitumia ili kuipata basotola ile. Sasa alifikia hatua ya mwisho kabisa ya uvulimilivu. Akairukia ile bastola hata hivyo jamaa alikuwa makini sana kwani alimzuia na kuzidisha nguvu zaidi ya kabali yake. Alan akajua hana namna ya kuweza kujinasua kutoka kwenye ile mikono yenye nguvu hivyo akawa tayari ameshajikatia tamaa maana jamaa alimdhibiti kila sehemu. Mishipa ya shingo ilikuwa imemsimama sana na macho yakiwa yameanza kubadilika rangi huku yakiwa yamemtoka pima. Alibakiwa na mbinu moja nayo ni kukubali kuwa amezidiwa ujanja na ajilegeze kuwa sasa alikuwa amesha kufa, wazo hili lilikuwa ni gumu sana kwake kwani kufanya hivyo ingeirahisisha kabali ya huyo jamaa mwenye miwani ya jua kuweza kuzama kooni na kusababisha kukosekana kabisa kwa hewa. Ilikuwa ni bora hata na vile alivyokuwa akiipata pumzi kwa shida kuliko kama ataruhusu kutokuipata kabisa. Kitu pekee alichobakiwa nacho ni kujituliza kimya na kuipa akili yake mafikirio nini afanye ili kujinasua. Hali ilikuwa mbaya zaidi na sasa uvumilivu ule ukaenda kubadilisha hata mpango wake wa kutaka kuleta mafikirio akaanza kutapatapa akiitafuta pumzi ya mwisho huku akiwa anajiona yupo katika ile hatua ya sakaratul mauti. Ni hapa katika kutapatapa ndipo alipohisi kitu, nacho kilikuwa kidogo sana ambacho kiliweza kumkwangua kwenye mkono wake. Alipotazama akaona damu ikianza kumtoka. Akatazama vizuri na kuona ulikuwa ni msumari wa nchi sita ukiwa umejaa kutu sana. Hili lilikuwa ni tumaini jipya katika kujikomboa kwake kwani kwa hatua ile aliyofikia hata kama angeona kibanzi cha kipande cha ukuni kilikuwa ni silaha hatari na kingeweza kumponya na kifo lile, ule msumari haukuwa mbali hivyo ilikuwa ni rahisi kuuvuta na kuutumia kama silaha. Akatumia nafasi ile ya mwisho kutafuta nguvu chache tu. Akabana pumzi zake kwa nguvu japo zilikuwa ziko mbioni kwisha, akapata nafasi ya kukaza mishipa yake ya shingo na kuvuta nguvu. Alipima mahali jicho la jamaa huyo lilipo na kufanikiwa kujua kuwa lilikuwa karibu sana pembeni ya sikio lake la kushoto. Alijisukuma kwa nguvu na kuuzamisha ule msumari kwenye jicho la kuume la yule jamaa. Jamaa alipiga yowe kali sana huku akimuachia Alan, akaanza kuhangaika huku akilizuia jicho lake. Msumari ule ulizama kwa juu kidogo ya jicho kutokana na ile miwani hata hivyo lilikuwa si jicho tena kwani Alan aliukita ule msumari kwa utaalamu mkubwa sana. Miwani haikuwa na faida tena aliitoa na kuitupia mbali huku kwa wakati huo Alan akihangaika pale chini akilishika koo lake na kukohoa hovyo huku ute mzito wa mate ukimtoka. Jamaa lile lilipandisha ghadhabu na kumfuata Alan kwa kasi kubwa kisha akampiga teke ambalo lilitua tumboni mwake, kwa kuwa Alan alikuwa amekita magoti na mikono yake chini mithili ya mnyama wa miguu minne, teke lile lilitua sawia na kumtupa mbali. Alan alipiga yowe kali la maumivu na kugeuzwa kisha kukalishwa ukutani. Ilikuwa ni hatari isiyoelezeka, bado alikuwa hoi bin taaban jamaa nae alikuwa amepandisha mori haswa. Zile damu zilizokuwa zikitoka jichoni mwake ni kama zilimpa wazimu. Alimfuata tena kama awali Alan akaona kifo bado hakikuwa mbali naye hivyo kulihitajika namna ya ziada ya kujinasua. Alikuwa akimtazama jamaa anavyokuja kisha kujivuta kama anayetaka kubutua mpira wa adhabu. Teke lile kali lilishia mikoni mwake kwa kuwa alijiandaa kulipokea. Hakukawia alijipindua na kumpisha jamaa ambaye teke lake la pili liliuvaa ukuta. Mapigo ya nguvu kutoka kwa Alan yakamchosha yule jamaa kwa vile yalipigwa kwa lengo maalumu.




"Nataka uniambie wale waliokutuma muje kuniangamiza mimi na kupelekea kunifuata kama mkia wangu." Alisema Alan huku akimsogelea yule jamaa.




"Wewe ni mjinga sana...Aaaoogh! Siwezi...siwezi kusema eti kwa kuwa umenizidi ujanja hata hivyo iko namna...!" Alisema kisha akatumia kuvu zake za mwisho akasimama na kumfuata adui yake kwa kasi na kumkumba kwa kikumbo kizito kisha akakimbilia ukutani na kuudandia ukuta kama aliyekuwa akitaka kutoroka kwa kuangukia upande wa pili hata hivyo haikuwa hivyo, alipofika katikati ya ule ukuta alijigeuza kichwa chini miguu juu na kukikita kichwa chake chini sakafuni. Tukio hili lilikuwa ni la kipekee sana na lilimuacha Alan kinywa wazi.




"Aisee! Hawa jamaa ni wa namna gani mbona wanajitolea uhai kiasi hiki. Ni siri gani ambayo wanafichiana?" Alijiuliza maswali mengi sana Alan pasipo kuwa na majibu yenye kueleweka. Alimsogele yule jamaa pale chini na kumkuta akiwa anatokwa na damu za masikioni, puani na kinywani akachutama Alan na kumuuliza.




"Ni nani aliyewatuma?" Jibu hakupewa na badala yake yule jamaa alikuwa kama hasikii chochote kile zaidi ni kwamba alikuwa akipambana na wakati mgumu sana wa maumivu huku akikoroma vibaya sana kama nguruwe pori aliye lala. Alitapika damu nyingi sana kisha akanyoosha miguu yake na kutulia. Alichanganyikiwa Alan, hakujua hawa watu ni wa dizaini gani na pia hakujua kwanini walikuwa wakimfuatilia. Akaanza kumpekua mmoja baada ya mwingine. Kwenye mfuko wa suruali wa huyu jamaa mwenye miwani ya jua ndiyo alikuta simu ndogo lakini kwa wale wengine kama huyu aliyemuua chumba cha tatu kutoka chumba alichopo na yule aliyemuangamiza kule relini, hakukuta chochote. Akajaribu kuipekua hii simu kuanzia sehemu za kuhifadhia majina na sehemu za kupiga na kupigiwa kote huku hakuna alichoambua.




HAPA NDIPO NINAPOWAHOFIA HAWA JAMAA, LINAPOKUJA SUALA LA KUTOA SIRI WAKO RADHI KUJITOA UHAI KULIKO KUSEMA.








Akaanza kumpekua mmoja baada ya mwingine. Kwenye mfuko wa suruali wa huyu jamaa mwenye miwani ya jua ndiyo alikuta simu ndogo lakini kwa wale wengine kama huyu aliyemuua chumba cha tatu kutoka chumba alichopo na yule aliyemuangamiza kule relini, hakukuta chochote. Akajaribu kuipekua hii simu kuanzia sehemu za kuhifadhia majina na sehemu za kupiga na kupigiwa kote huku hakuna alichoambua.




SONGA NAYO.....




Alipofika kwenye sehemu ya jumbe fupi za maneno, kuna ujumbe ulimvuta, ujumbe huu ulikuwa mfupi na wa maneno machache. 'MKILIPATA KONTENA HILO NENDENI MKAZIMWAGE BIDHAA ZOTE SHIMONI KB NA MLITEKETEZE.' Ujumbe huu ulisema maneno hayo. Alan akayafikiria na kushindwa kung'amua kitu kwenye hili kwani ilikuwa ni sentensi iliyojaa mafumbo sana. Kontena? Kontena la nini? Na litakuwa limebeba bidhaa gani? Aliwaza Alan hata hivyo ilikuwa ni kazi bure maana hakuwa akijua kitu akaamua kuondoka.




Alifika pale ambako alilitelekeza gari lake na kupanda kisha akachukua uelekeo wa njia ile aliyojia. Dakika chache alikuwa amefika mjini tayari na alipotazama saa yake ya mkononi muda ulikuwa ni saa sita na dakika tano. Alikuwa ndani ya muda wa miadi ya kukutana na Zaituni. Aliigeuza gari yake na kurudi kwenye mzunguuko wa barabara wa mabanda ya papa kisha akachukua barabara ya Jamhuri. Alitembea kwa mwendo wa kasi akiwa makini na matuta ya barabarani. Alifika Makorora ndani ya muda mfupi sana akawa anapita mitaa hii na ile aliitafuta nyumba namba 120. Hakuwa na papara pia alijitahidi kuweka umakini mkubwa kwa vile tayari alishaiona hatari inayomnyemelea, alianza kuzihesabia nyumba alipoikuta nyumba yenye namba 116. Mwendo wake ulimfikisha nje ya nyumba hiyo aliyokuwa akiihitaji, aliyasoma mazingira ya eneo hilo yalivyo yalikuwa tulivu sana yasiyo na purukushani zozote, hakukua na mtu aliyekuwa akimfuatilia na kila alipozitazama sura za watu wachache wa eneo hilo hakuona sura ambayo angeweza kuitilia shaka. Alitafuta mahali pa kuegesha gari akaona mti mmoja ambao ulikuwa na kivuli kizuri. Palikuwa na gari nyingine ndogo ya rangi nyekundu. Akaisogeza gari hapo na kuiegesha akateremka na kuzirusha hatua zake taratibu kuelekea kwenye mlango wa nyumba namba 120.




Alan alibisha hodi mara ya kwanza, pili na tatu kisha akatulia kwa jozi ya sekunde alipotaka kubisha tena hodi, mlango ulifunguliwa na msichana mrembo akachungulia.




"Oooh! Karibu sana ndani mgeni, nilijua na leo usingeweza kufika...?" Alisabahi yule msichana. Alikuwa ni Zaituni.




"Hapana leo nisingeweza kufanya hivyo kwa kuwa nilidhamiria, nisingefanya busara kutokukuona kisura wangu." Alijibu Alan huku akiwa anaingia ndani mbele akitanguliwa na Zaituni. Vazi ambalo alivaa huyo binti lilikuwa matata sana kiasi cha kumfanya kidume huyo kumeza mate ya tamaa. Hakuwa amevutiwa sana na Zaituni kimapenzi bali kilichomfanya kuweka ukaribu wa namna hiyo ni kuhusiana na kile ambacho huwenda alikuwa akikifahamu binti huyo hasa kuhusiana na yule jamaa aliyejifanya mgonjwa kiasi cha kulazwa kabisa kwenye wodi zile za Cliff. Zaituni alikuwa mrembo sana na aliyejaaliwa umbo lenye kuleta mvuto wa kumvuta mwanaume yeyote rijali hata hivyo Alan hakuwa amevutiwa sana na binti huyu.




"Karibu sana nyumbani Abasi, hapa ndipo ninapoishi na nimeshangaa sana kwa kuweza kupafahamu kwa wepesi kiasi hicho."


"Asante sana Zaituni, unajua maelekezo uliyonipa yamejitosheleza sana hivyo sidhani kama kuna mtu angeweza kupotea hata kama angekuwa ni mgeni wa huu mji." Alijibu Alan akiwa anajikalisha kwenye kochi moja sebuleni pale. Nyumba hii ilikuwa na ukubwa wa wastani, ilikuwa ni ya vyumba vitatu vya kawaida, sebule, sehemu ya kulia chakula, choo cha ndani na jiko. Sebuleni hapo kulikuwa na makochi ya kisasa yenye rangi hudhurungi ya kuvutia, pia katikati kulikuwa na meza kubwa ya mbao safi ya mti wa mwembe iliyotandikwa vizuri huku kukiwa na viti vitatu kuizunguuka meza hiyo.




"Unatumia kinywaji gani kaka?" Akauliza Zaituni na jibu hili likamtoa Abasi kwenye tafakari aliyonayo na kumrudisha sebuleni pale.




"Maji yanatosha mrembo wangu niko na kiu sana." Zaituni alizitupa hatua zake zilizokuwa zikitikisa nyama zake za nyuma kwa kiwango kikubwa sana ni wazi ungesema kuwa hakuwa amevaa nguo ya ndani kwa jinsi nyama zake za makalio zilivyokuwa laini. Alan alibaki kuwa mtazamaji wa macho akiburudika kwa kile kilichokuwa kikioneshwa na binti huyo. Aliletewa maji kwenye birauli, akapiga funda moja kubwa na kuishika vema birauli ile mkononi.




"Ulikuwa na mtu ndani?" Akauliza Alan huku akitazama mahali kilipo chumba ambacho huwenda ndicho alichokuwa akikitumia Zaituni kwa mapumziko ya usiku. Zaituni alitabasamu pasipo kutoa jibu la aina yoyote kisha akamsogelea kijana huyo na kukaa pembeni yake.




"Kama angekuwepo wala nisingekuruhusu ufike nyumbani kwangu, nimekuruhusu kwa kuwa sikuwa na mtu mwingine na hayupo. Ni wewe pekee kwa sasa humu ndani harufu yako inanukia."


"Kumbe...! Asante sana kwa nafasi ya upendeleo." Alijibu Alan kisha akapiga tena kupuo la maji na kuishika tena birauli mkononi.




"Nimeandaa chakula kizuri kwa ajili yetu Abasi naomba nikaoge ili tuingie mezani." Aliongea Zaituni kisha akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake hasa kule ambako Alan au Abasi alihisi.




Kumbukumbu mbaya zikajiunda kichwani mwake. Alikuwa akikumbuka mengi sana hasa ilikuwa ni kuhusu kule Hospitali. Aliyakumbuka yale maneno ya wale watu wawili yule mwanamke na yule jamaa aliyemuondolea uhai. Kulikuwa kukizungumzwa lugha za mafumbo sana na kikubwa kilichokuwa kikimuumiza kichwa kila mara yalikuwa ni yale maneno ya kuwa hakuna nyuki aliyelikaribia Ua hadi unafika wakati ule. Maneno hayo yakamfanya aweze kuvuta picha nyingine hasa pale alipoliona Ua la Bee Balm kwenye moja ya droo za kitanda, Ua hili liliwekwa pale kwenye zile droo kwa minajili gani maana kila akikumbuka kama kulikuwa na sababu zozote za kuwepo kwa Ua lile pale ndani hakuziona. Kwanini Ua lile lilifanana kila kitu na lile ambalo lilichorwa mgongo mwa Maisara? Aliwaza Alan kisha moja kwa moja akajipa imani na alama ya tahadhari kuhusiana na hawa wanawake wawili. Huyu Maisara na yule ambaye alitoweka katika mazingira tatanishi kule hospitalini, aliona namna wanawake hawa walivyobeba hatari kubwa, na alivyotakiwa kuwa makini zaidi kwani kama akiwa mtu wa kupuuza hisia zake huwenda jambo hilo likamgharimu. Alipanga kumchunguza Maisara ili ajihakikishie kama kweli ni dereva teksi au alikaa pale kijiweni siku ile kwa makusudi maalumu hivyo aliapa usiku wa siku hiyo ni lazima afike pale kwenye kituo cha teksi cha Kwaminchi. Hata hivyo aliendelea kuwaza zaidi. Vipi kuhusu wale ambao waliokuwa wakimfuatilia na kumuandamisha hadi kwenye mtaa wa viwandani. Hawa nao walisema kuwa wametumwa waweze kumuangamiza hata hivyo hawakusema wametumwa na nani, mtu pekee ambaye alipaswa kumwambia alikuwa ni yule ambaye alijitoa uhai kwa kujirusha kisha kutanguliza kichwa chini miguu juu na kukifanya kichwa chake kupata dhoruba kali sakafuni. Hii kazi alikiri kuwa ilikuwa ni ngumu na hakutakiwa kuwa mtu wa kujionesha hovyo hovyo kwani huwenda kibarua kikamshinda mapema sana. Hapa sasa akaukumbuka na ule ujumbe alioukuta kwenye ile simu ya yule jamaa mwenye miwani ya jua. KB. KB ni wapi? Akawaza Alan hata hivyo jibu hakuwa nalo.




"Karibu mezani mgeni?" Sauti ya Zaituni ikamrudisha tena Alan pale ndani, akatazama kule sauti ilikotokea loh! Hii ilikuwa ni zaidi ya mitego, Zaituni alivaa kijisketi kifupi sana ambacho kiliishia juu ya magoti na kuacha sehemu kubwa ya mapaja yake wazi. Juu alivaa fulana nyepesi yenye kuonesha kila kitu cha ndani. Chuchu zake imara na nyeusi zilikuwa zimesimama wima huku midomo ya binti huyo ikiwa imetegwa katika mtindo wa kuvutia sana. Alan hakuelewa nini sababu hasa ambayo imepelekea mabinti kujirahisisha sana kwake hasa akutananapo nao kwa mara ya kwanza. Alimeza funda la mate ya uchu Alan kwa kile akionacho mbele yake hata hivyo alijifanya kutokutamani kile na kunyanyuka kuelekea mezani.




Chakula kilikuwa kitamu sana na alikula kupita kiasi kwa kuwa alikuwa akihisi njaa mno.




"Asante sana kwa chakula kitamu namna hii mrembo." Alisifia Alan.




"Kula kwanza ukishamaliza ndipo usifie." Alijibu Zaituni.




"Hapana, naweza kusifia hata nikiwa bado sijamaliza kula kwani kuna ubaya wowote."


"Hakuna ubaya." Alijibu Zaituni huku akikitua kwenye sahani kijiko cha chakula na kuvuta birauli ya sharubati ya parachichi akapiga funda dogo na kuirudisha mezani, akamtazama Abasi kwa macho malegevu kabisa yanayoweza kuamsha hisia nyingine kabisa. Alan akaona huo ndio ulikuwa wasaa mzuri wa kuweza kuuliza maswali yake kuhusiana na jambo ambo limetokea kule hospitalini.




"Vipi kuhusu mwenendo mzima wa majukumu ya kazi yako Zaituni?" Alianza namna hiyo Abasi.




"Namshukuru Mungu anasaidia Abasi, tunazidi kupambana na hali zetu."


"Hakika na kazi zenu ni ngumu sana na ni zenye kuhitaji ujasiri sana."


"Hakuna kazi nyepesi my love kazi zote ni ngumu na zinahitaji uwe na moyo wa kujitoa sana."


"Najua Zaituni hata hivyo hukujua kwanini nimeongea hivi, nimeongea hivi nikiwa na maana ya kuwa kazi ya uuguzi ni zaidi ya hata mwalimu kwa kuwa wewe unakutana na watu waliojikatia tamaa kwa hali mbaya za kimaradhi waliizokuwa nazo ambazo eidha zimetokana na ajali ama matukio mengine. Wote hao wanahitaji huruma yako wewe muuguzi ili kuweza kumrejeshea matumaini mapya ya kuishi hata kama hana miguu kabisa."


"Ni kweli uyasemayo Abasi hata hivyo kuna nyakati huwa tunakutana na mambo ya kuogopesha sana tunapoingia kwenye wodi mbalimbali ila hakuna namna ni majukumu yetu na hakuna njia nyingine...!"


"Ila siamini kama wanaolazwa wodini wote ni wagonjwa...?" Akadakia Alan huku akimkazia macho Zaituni tabasamu akiwa ameliweka kwa uchache tu. Zaituni akamtazama kijana huyo kwa mshangao hata hivyo haukudumu sana kwa kuwa alishaelewa nini ambacho Alan anamaanisha.




"Hili unalolizungumzia kwangu naona ni jambo jipya na tukio la kushangaza sana. Tokea nimeajiriwa kazini hapa hadi sasa natimiza miaka miwili hata hivyo sijawahi kukutana na tukio ambalo limetokea, yule anayesemekana ni mgonjwa halafu asiwe mgonjwa...!"










"Ila siamini kama wanaolazwa wodini wote ni wagonjwa...?" Akadakia Alan huku akimkazia macho Zaituni tabasamu akiwa ameliweka kwa uchache tu. Zaituni akamtazama kijana huyo kwa mshangao hata hivyo haukudumu sana kwa kuwa alishaelewa nini ambacho Alan anamaanisha.




"Hili unalolizungumzia kwangu naona ni jambo jipya na tukio la kushangaza sana. Tokea nimeajiriwa kazini hapa hadi sasa natimiza miaka miwili hata hivyo sijawahi kukutana na tukio ambalo limetokea, yule anayesemekana ni mgonjwa halafu asiwe mgonjwa...!"




SONGA NAYO....




"Unamaanisha nini unaposena inasemekana...!" Akadakia Alan.




"Sikiliza Abasi Mgizu, yule jamaa hakuwa mgonjwa hata kidogo, kwanini nasema hakuwa mgonjwa. Ni mara nyingi sana nimekuwa nikikutana naye nyakati za usiku nikiwa zamu...!"


"Wee! Usiniambie...!"


"Amini nikwambialo...!"


"Unakutana naye akiwa mzima kabisa."


Ndiyo, unajua subiri nikuweke wazi labda. Wakati naingia kazini siku moja, tuliitwa katika kikao wauguzi watatu na bosi akatuambia kuwa tumeteuliwa sisi watatu kuwahudumia wagonjwa waliyoko kwenye jengo lile la Cliff hakutakuwa na muuguzi mwingine na pia tukaambiwa kuwa tutakuwa na mataktari bingwa wawili ambao wapo pale Hospitali kwa kazi maalumu hivyo hata hao tunaweza kuwa nao. Ila kitu cha kushangaza ni kwamba tulizuiwa kabisa kuingia kwenye wodi namba 04 na tukaambiwa kuwa mgonjwa aliyeko mule atakuwa akihudumiwa na daktari maalumu." Alieleza Zaituni. Alan akatafakari sana jambo hilo. Hili lilikuwa si kwamba haliwezekani lah! Kilichokuwa kikimchanganya ni namna jambo hilo lilivyo la kushangaza na kuchanganya.




"Umesema alikuwa akitoka usiku huyo jamaa...?"


"Sema marehemu Abasi kwa kuwa sasa si hai tena!"


"Wee! Ameuawa...?" Alijifanya kushangaa sana Alan kwani hakutaka kujulikana kama ni yeye ndiye aliyefanya tukio la mauaji.




"Sina hakika kama ameuawa ila muda ule wakati wewe unatoka pale kwenye lile jengo, dakika thelathini mbele ndipo tulipokea taarifa za kifo cha yule jamaa na tulipofika wodini kwa amri ya bosi tulimkuta akiwa tayari ameshahifadhiwa kwa shuka safi na kupakizwa kwenye machela akapelekwa chumba cha maiti." Hapa Alan alikuwa akifunguliwa masikio yake na kuona namna ambavyo mambo yalivyokuwa yakiendeshwa kwa usiri mkubwa. Alitegemea kuambiwa kuwa jamaa aliuawa kwa kupigwa risasi lakini kinachomshangaza eti, haikujulikana jamaa ameuawa au amekufa kama wagonjwa wengine wanavyokufa. Hakika haya yalikuwa ni makubwa na madogo ndiyo yenye nafuu. Akiwa anawaza hivyo Alan akakumbuka kile kinachosemekana kuwa Zaituni alikuwa akikutana na huyo jamaa kabla ya kifo chake na ni nyakati za usiku. Hili lilimvutia sana na lilikuwa na maana kubwa sana kwake. Akaisogeza sahani ya chakula pembeni kisha akamtazama Zaituni usoni.




"Ulikuwa ukikutana na huyo jamaa akiwa anaelekea wapi?" Akauliza.




"Mara ya kwanza nilishtuka sana nilipomuona na nilijua labda ni kibaka kwa kuwa alikuwa amevaa mavazi ya ajabu ya kujifunika. Nikiwa nataka kutoka ofisini na kwenda kuwapa wagonjwa dawa na kuwachoma wengine sindano zao za masaa, ile nafungua tu mlango nikamuona naye akitoka kule kwenye wodi aliyolazwa. Niliogopa sana. Alivaa sweta la kofia iliyokaribia kuuficha uso wake. Alikuwa ameitumbukiza mikono yake kwenye mifuko ya suruali akiwa anatembea kwa hatua za haraka hata hivyo hakukuwa kukisikika sauti zozote za soli yake ya kiatu. Niliweza kumuona vema hasa niliporudi ndani na kujibana nyuma ya mlango, alipita na alikuwa akitazana huku na huko hii ikanipa mashaka sana na nilikuwa nikitetemeka mno. Mwanzoni nilijua kuwa huwenda ni mtu ambaye alikwenda kumtembelea mgonjwa yule hata hivyo alipopita karibu kabisa na mimi nilijikuta sehemu zangu zote mwilini zikikosa ushirikiano. kikomo na miguu ilikufa ganzi na nikashindwa kuelewa nini cha kufanya...!"


"Kwahiyo hukujua ni wapi alipokuwa akielekea?" Akahoji Alan akiwa mtulivu sana.




"Nilijua...nilijua na hii ilikuwa ni siku ya tatu kwani siku ya pili hakuwa ametoka...!"


"Unauhakika hakuwa ametoka siku iliyofuata?" Aliuliza Alan na lengo la kuuliza kwake lilikuwa ni kujua ni hatua gani ambayo binti huyo aliichukua mara baada ya kumuona jamaa huyo kwa siku ya kwanza.




"Ndiyo, hakutoka...!" Akasema akaweka tuo kidogo Zaituni kisha akaendelea.


"...unajua baada ya kumuona kwa siku ya kwanza, nilipatwa na shauku ya kutaka kumjua anaelekea wapi na kufanya nini. Wazo hili lilikuja baada ya kumuona msichana mrembo sana siku iliyofuata akiwa ameingia kwenye ile wodi namba 04. Nikajiuliza sana na kufikiri hivi ni mgonjwa gani ambaye anaweza kuwa katika hali ya ugonjwa mchana na usiku akawa mzima na kutoka. Hili ndilo lililonipa msukumo wa ufuatiliaji. Siku hii ambayo yule binti mrembo alikuja kumuangalia mchana, hakutoka; siku ya pili sasa ndiyo alitoka na muda ulikuwa ni uleule. Alipotoka mlango huu wa mbele, mimi nilivua viatu vyangu na kutoka hadi kwenye mlango aliotokea yeye na kuchungulia kwa kificho sana. Huwezi amini Abasi. Yule jamaa alikuwa akielekea kwenye lile gofu ambalo zamani lilikuwa likitumika kama ofisi za madaktari. Ile ilikuwa ni ofisi ya zamani sana tangu enzi za ukoloni na kwa kipindi hiki lile jengo halitumiki kabisa. Nilimuangalia hadi alipopotelea ndani kabisa ya jengo lile ndipo nikaondoka pale mlangoni hata hivyo sikuwa katika hali nzuri kabisa na sikuwa hata na hamu ya kumuelezea mtu yale niliyoyaona ikabaki kuwa siri yangu tu, leo ndiyo nakuambia." Alimaliza kuelezea Zaituni na alieleza kwa urefu sana. Alan alimtazana huyu binti na kuangalia kama kwenye maelezo yake kulikuwa na chembe za uwongo. Hakuona. Aliamini kile alichokuwa akiambiwa kilikuwa ni ukweli mtupu. Hisia zake kuhusiana na kundi hili la watu, zilikuwa zikimwambia ukweli na sasa zinakwenda kumfungulia njia ya safari yake ya kuwakamata waliohusika na kifo cha Luteni Jenerali Leous Mipango.




"Hakuna mlinzi yeyote anayelinda lile gofu maana liko ndani ya uzio wa Hospitali?" Akauliza Alan. Zaituni akafikiria kwa tuo kidogo kisha akasema;




"Hakuna...mlinzi hakuna, ila karibu na ofisi ya bosi kipo chumba ambacho kinatumiwa na mganga mmoja bingwa wa magonjwa ya akili na saikolojia. Mzee huyu kama ukikutana nae anaweza kuwa na mengi ya kukusaidia kwa kuwa muda wote anakuwa hapo ofisini kwake na karibu sana na ofisi ya bosi...!"


"Mambo hayo huwa yanafanyika usiku sana sasa inawezekana vipi huyu Dokta bingwa wa magonjwa ya akili na saikolojia ahusike?" Akakatisha Alan akizidi kuweka utulivu.




"Nimesema hivi kwa sababu maalumu Abasi mpenzi, mzee huyu huwa anaingia kazini kuanzia saa nne usiku si kwamba hii huwa ndiyo ratiba yake ya kikazi la hasha! Aghalabu sana huwa anapenda kufanya tafiti zake nyakati hizo pia naweza kusema miongoni mwa wafanyakazi wote wa ile Hospitali, ni huyu mzee pekee ndiye anayeongoza kwa kuwa eneo la kazi muda mrefu. Tumempa jina la mzalendo. Wakati yule jamaa akiwa anatoka majira yale ya usiku, huyu mzalendo alikuwepo majira hayo na niliona kivuli chake kwa ndani kupitia dirisha." Alijibu Zaituni. Huu ukawa ni mwanzo mzuri wa Alan kuweza kumchunguza huyu mganga mkuu. Akaridhika kwa mahojiano hayo aliyoyafanya hata hivyo alikuwa na la kuuliza kuhusiana na bosi huyo.




"Bosi wako ni nani?" Akakumbuka kuuliza Alan.




"Mganga mkuu Richard Bango." Alijibu Zaituni, Alan akalihifadhi hilo jina kwenye kitabu cha kumbukumbu ubongoni mwake. Akatafakari mengi ubongoni mwake kisha akayapoza kwa sharubati ya parachichi akatulia kitini akimtazama Zaituni. Binti huyo aliondoa vyombo kisha akarudi mezani akiwa anatazama saa iliyopo ukutani. Ilikuwa imetimu saa saba na nusu. Muda wote huu Alan alikuwa ameanza kumfikiria mganga mkuu Richard Bango. Huwenda haya yote yalikuwa yakipewa ulinzi mzuri na huyu mganga mkuu ili hawa watu waweze kupenyeza watu wao kukamilisha waliyoyapanga kuyakamilisha. Aliwaza sana Alan kisha akauliza.




"Unapajua nyumbani kwake?"


"Hapana sijawahi kufika na sijawahi kumsikia akipazungumzia hata siku moja."


"Huwa anaingia muda gani kazini na anatoka muda gani?"


"Kwa kawaida hadi ifikapo saa mbili na nusu asubuhi anakuwa tayari ameshafika ofisini kwake na ifikapo saa kumi na mbili na nusu jioni anakuwa anajiandaa kuondoka."


"Anatumia usafiri gani?"


"Gari yake ni Land Crusser ya rangi ya maziwa mara nyingi inapakiwa nje ya ofisi yake ambayo ipo karibu na jengo la Cliff pia ikiwa imepakana na jengo la zamani ambalo ni gofu kwa sasa." Alijibu Zaituni. Maelezo haya yakawa yameweza kuunda picha nyingine kichwani mwake hasa pale alipoweza kuunganisha maelezo ya Zaituni kuhusiana na yule jamaa aliyekuwa akitoka nyakati za usiku. Akawa ana kazi mbili za kuhakikisha anazifanya usiku wa siku hiyo, moja ikiwa ya kumfuatilia Maisara masikani anayotumia kupakia gari yake na nyingine ikiwa ni hiyo ya kumfuatilia mganga mkuu.




"Muda unakimbia sana my love." Alisema Zaituni huku akijikalisha kwenye mapaja ya kijana huyo, aliweza kuyapeperushia mbali mawazo ya Alan kwa muda huo.




"Ni kweli muda umekimbia sana na muda wa wewe kuingia kazini unawadia kwa kasi mno...!" Alijibu Alan hata hivyo hakufika tamati ya maongezi yake akashtukia akipewa kinywa na Zaituni, hakuwa na ajizi zaidi ya kukipokea. Walinyonyana mate kwa kitambo kifupi na walipoacha zoezi hilo wakabaki wakitazamana usoni huku Zaituni akiwa amelegeza macho yake kwa kiasi kikubwa sana akiashiria kuwa kuna kitu alikuwa akikihitaji toka kwa kijana Alan. Vyote hivi vilifanyika kwa haraka ya pekee sana hakika mrembo huyo alikuwa katika uhitaji mkubwa mno wa kushiriki tendo na Alan. Akalegeza Khanga yake nyepesi aliyotoka kuivaa punde akikiacha kifua chake kichanga kikiwa wazi kabisa. Matiti imara yaliyosimama wima yakamfanya kijana huyo kumeza mate ya uchu kwelikweli. Alan alikuwa mzito sana kufanya mapenzi kwa wakati huo na huyo binti ijapokuwa kila akimtazama alishindwa kuzizuia hisia zake hata hivyo moyo wake ulikuwa ukimtuma mahali na si kufanya mapenzi na msichana huyo. Akamtoa kwenye mapaja yake kisha akasimama, kitendo kile kikapelekea khanga ya Zaituni kuporomoka kabisa chini na kumuacha akiwa na nguo ya ndani pekee. Zaituni hakulaza damu alimkumbatia Alan huku akilalama kwa hisia kali kabisa akisema yuko kwenye uhitaji mkubwa na alihitaji kuipata huduma yake.






Alan alikuwa mzito sana kufanya mapenzi kwa wakati huo na huyo binti ijapokuwa kila akimtazama alishindwa kuzizuia hisia zake hata hivyo moyo wake ulikuwa ukimtuma mahali na si kufanya mapenzi na msichana huyo. Akamtoa kwenye mapaja yake kisha akasimama, kitendo kile kikapelekea khanga ya Zaituni kuporomoka kabisa chini na kumuacha akiwa na nguo ya ndani pekee. Zaituni hakulaza damu alimkumbatia Alan huku akilalama kwa hisia kali kabisa akisema yuko kwenye uhitaji mkubwa na alihitaji kuipata huduma yake.




SONGA NAYO.....




Alan alikuwa akisumbuliwa na matukio fulani fulani kichwani mwake na kila akitazama namna matukio yale yanavyomjia ndivyo hamu ya kufanya mapenzi inapoyeyuka moyoni mwake. Aliikumbuka picha ya yule mwanamke kule Hospitali akiwa chumbani kwa yule jamaa mgonjwa wa kutengeneza. Akakumbuka mazungumzo yao. Hasa pale walipokuwa wakizungumzia nyuki. Kisha akakumbuka lile Ua la Bee Balm lililodondoka toka ndani ya droo pembeni ya kile kitanda alicholala yule jamaa kisha kumbukumbu ikahamia hotelini chumbani kwake alipokuwa amefikia. Alimkumbuka Maisara, Ua lililopo mgongoni mwake, Ua lile lile la Bee Balm halafu hapo hapo akakikumbuka kifo cha Luteni Jenerali Leous kipango. Kifo chake kilisababishwa na mwanamke, hii ilikuwa ni kwa maelezo ya mtu aliyejinasibisha ukaribu na Leous Mipango. Hapa jina Ua likatawala ubongoni mwake akapuuzia uwepo wa Zaituni mbele ya macho yake ambaye alikuwa akijipindapinda kama funyo mikono yake laini ikiupapasa mwili wake. Wakati akiwa anawaza haya huko nje mvua kubwa ilikuwa imeshaanguka na ilikuwa ikinyesha kwa kishindo kikubwa sana.




"Muda umesonga sana mpenzi siwezi kufurahia nawe kwa muda huu, jiandae uende kazini mimi nitakuja kesho asubuhi kwa ajili yako." Aliongea Alan huku akiiokota nguo iliyoanguka na kumvisha Zaituni.




"Siwezi kuchelewa mpenzi, niko katika uhitaji mkubwa sana na nashindwa kuvumilia nina muda mrefu sana sijaguswa mwili wangu...!"


"Najua hata hivyo muda huu si muafaka napenda kuwa nawe kwa muda mrefu sana." Alijibu Alan baada ya malalamiko ya mtoto huyo wa kike. Alan alitoka huku Zaituni akiwa haamini kama ameachwa kwenye hamu kubwa kwa kiasi hicho. Alijishika kifuani huku akiwa amefumba macho kwa hisia kali mapigo yake ya moyo yalikuwa kasi sana huku damu yake ikimchemka kwa kiasi kikubwa hakika hakuwa kwenye uhitaji mdogo wa kufanya mapenzi. Alikimbia mbio hadi mlangoni na kuiona gari ya Alan ikiondoka kwa mwendo wa kawaida hapo nje. Alirudi ndani kwa hatua za taratibu huku akiwa ameghadhibika, ghadhabu za kukosa akitakacho; mapenzi.




____________




Zaituni hakuona haja ya kuendelea kupoteza wakati akaingia moja kwa moja maliwatoni na kwenda kujimwagia maji ya baridi ili kuweza kuuweka sawa mwili wake. Alipokuwa anatoka maliwatoni akiwa amejifunga Khanga nyepesi iliyoloana maji, akiwa anatembea kwenye korido nyembamba ya kumpeleka chumbani kwake huku akiyatikisa mapambo yake ya nyuma kwa kiwango cha kimataifa, akausukuma mlango wa kuingia chumbani kwake na kuzama ndani. Loh! Ndani kulikuwa na mgeni ambaye hakuwa akimtarajia kabisa na huyu aliingia pasipoutaratibu maalumu. Mshtuko wake ulikwenda kumuibulia hofu kubwa sana kwa kuwa mgeni mwenyewe hakuwahi kufikiria hata kidogo kama angekuwa hapo.




"Bosii!" Alitahamaki kwa kiwango cha juu sana huku mshtuko ule ukiwa umemuacha akiidondosha chupi yake aliyotoka nayo bafuni baada ya kuifanyia usafi.




"Zaituni...karibu sana chumbani kwako Zaituni au unataka nikupishe ubadilishe nguo." Aliongea huyo mgeni kwa upole wa hali ya juu huku anachokiongea kikizidi kumuacha Zaituni kwenye mshangao mkubwa sana. Chumba chake mwenyewe, ndani ya nyumba yake mwenyewe, anakaribishwa na mgeni ambaye mbali ya kuingia pasipo utaratibu hata hivyo hakuwa na miadi naye ya kukutana naye hapo nyumbani kwake. Hakuwa mtu wa kufika nyumbani kwake na pia hakuwa na uhakika kama mtu huyo aliyemuita bosi alikuwa akipajua hapo nyumbani kwake. Hali ile ikamfanya Zaituni kuingiwa na mashaka makubwa sana ndani ya moyo wake, aliogopa sana na woga wake ukamfanya mwili kumtetemeka.




"Zaituni, leo nimependa kukutembelea nyumbani kwako au hupendi?" Akauliza Richard Bango. Alikuwa ndiye mganga mkuu wa Hospitali ya rufani ya Bombo. Huyo ndiye aliyekuwa bosi wa Zaituni.




"Si kawaida hii bosi na inashangaza...!" Akaonesha wasiwasi wake Zaituni. Richard Bango mganga mkuu aliyekubali kuwa mnyama mara baada ya kupewa mafunzo maalumu ya kimapigano alipokuwa kwenye masomo maalumu nchini Uingereza. Akiwa huko kwa muda wa miaka miwili, mwanzoni kabisa mwaka wa kwanza Bango aliweza kupenyezewa ujumbe uliomtaka kuingia makubaliano ya kukubali kuingia kwenye mafunzo maalumu ya kujilinda kama alivyoelezwa. Alijiwa na bwana mmoja wa kizungu akiwa amevaa kofia ya kapelo na mkononi mwake akiwa amevaa glovu nyeusi. Bwana huyo alimpa huo ujumbe na kumwambia kuwa utakuwa ni wenye manufaa makubwa kwake. Alikubali kwa kuwa alipenda mafunzo hayo hasa alipofikiria kujilinda mwenyewe. Akafunzwa mafunzo hayo yaliyodumu kipindi chote cha masomo yake. Aliporudi nchini, akafikia kituoni kwake katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kipindi hicho akiwa kama Dokta bingwa wa magonjwa ya moyo. Hakudumu sana ndipo alipohamishiwa jijini Tanga akiwa kama mganga mkuu wa Hospitali hiyo ya rufani Bombo. Mwaka mmoja tu pekee ulitosha kumpa uzoefu na ndani ya mwaka huo akapokea ujumbe wa kumtaka awe chini ya wale waliyomfunza mapigano. Lilikuwa ni ombi la kuchekesha sana na hakuwa na uelewa wowote juu ya ombi hilo na pia aliliona ni ombi la kitoto hivyo akakataa na kusema wakae mbali naye. Hakujua kuwa watu hao walikuwa ni makini kiasi gani. Siku asiyoikumbuka jina, yule bwana ambaye alikuja kwake siku moja akiwa nchini Uingereza. Akiwa anevaa kapelo na glovu nyeusi, alimuibukia tena nyumbani kwake nyakati za usiku tena akiwa anajiandaa kulala. Ugeni huo wa ghafula ulimuweka katika taharuki kubwa akataka kuingia kwenye mapambano mara baada ya kuvamiwa na mtu ambaye bado alikuwa hajamtambua. Yule jamaa wa kizungu alipojionesha kwa muonekano ambao Dokta Bango alikuwa akiuelewa, akapoa na kuwa mdogo sana. Aliambiwa;




"Ulipokea mafunzo yetu kwa mikono miwili basi huna budi kupokea ombi letu kwa mikono miwili pia."


"Ninyi ni akina nani...?"


"Leo hii sisi ni akina nani? Mbona hukuuliza mwanzoni hadi tukapoteza muda wetu bure kwa ajili yako. Ulijua waliimu waliokuwa wanakufua walikuwa wanakufua bure, hasha! Tulitumia gharama ili kuhakikisha unapata mafunzo mazuri na unatoka pale ukiwa umeiva. Hukuuliza...nashangaa hukuuliza kwanini tunatumia gharama kwa ajili yako wewe mtu mweusi tusiyekuwa tukikufahamu. Au waalimu waliokuwa wakikufua walikuwa weusi kama wewe?"


"Hapana...!"


"Ulikuwa ni mpango...ule ulikuwa ni mpango madhubuti sana wa kuhakikisha unakuja kuwasaidia watu weusi wenzako katika mapambano. Najua hujui ni mapambano ya aina gani hata hivyo hutakiwi kuwa na wasiwasi sana kwa kuwa ni mapambano ya amani. Si bure utakuwa ukiingiza pesa nyingi sana kwenye hili na hautakuwa ukipambana kwa muda mrefu. Wewe kazi yako kubwa itakuwa ni kuwapatia huduma wapambanaji hasa wanapopata majeraha makubwa wakati wa mapambano vile vile kuhakikisha unawapa hifadhi nzuri pale wanapopoteza maisha mapambanoni." Haya ndiyo yalikuwa mazungumzo yao na hata alipotajiwa kiasi hicho cha fedha hakuweza kupinga kwa kuwa hakuwa na njia ya kupinga. Akakubali na kuanza rasmi kuwatumikia watu hao ambao hakuwa akijua wanapambania nini. Hakuwa amewekwa wazi na alikuwa pale kama njia japo alitakiwa kuwa msiri sana kwa jambo lile. Huyu ndiye aliyemhifadhi yule jamaa kule kwenye wodi ya Cliff na ilihali si mgonjwa hata hivyo inasemekana jamaa yule alikumbwa na majeraha makubwa sana kama ambavyo alitakiwa kufanya. Hata alipopoteza maisha maiti yake haikutolewa kwa utoaji wa kawaida na badala yake alitolewa kwa siri kubwa na yeye mwenyewe nyakati za usiku huku akihakikisha hakuna anayemuona. Mwili ule ulitelekezwa kwenye jengo la kuhifadhia maiti ukiwa hauna taarifa yoyote huku akimsababishia kifo kibaya sana mlinzi wa jengo lile kwa kumuwekea sumu kwenye kinywaji. Huyu ndiye Dokta Richard Bango alikuwa akiifanya kazi yake kama vile alivyoelekezwa.




Leo hii yuko kwenye nyumba ya Zaituni akiwa kama mgeni asiyeeleweka.




"Zaituni nimekuja kwako kwa sababu moja nayo ni kukuuliza machache kisha niondoke...!" Akasema Richard Bango kisha akatulia kidogo kabla ya kuendelea.




"...kwanini ulikuwa ukimhudumia mgonjwa niliyetoa maelezo ya kutokuhudumiwa?"




"Hapana Dokta sijawahi kutoa huduma kwa yule mgonjwa hata siku moja...?"


"Unauhakika na unachokizungumza Zaituni?"


"Asilimia mia moja Dokta...!"


"Wewe ni mwongo Zaituni na uwongo ni dhambi au hujui...?"


"Sijawahi kweli Dokta na sikuwa nikikikaribia kabisa kile chumba." Alizidi kulalama Zaituni alipokuwa akiambia kuwa alikuwa akitoa huduma kwa yule mgonjwa. Hakukubali hata kidogo kwani hakuwa akitoa huduma kweli.




"Aliwahi kuniambia kuwa ulikuwa ukienda kumpa huduma...!"


"Ni mwongo Dokta...huyo mgonjwa wako ni mwongo siku...!"


"Wewe ndiye mwongo na si mgonjwa wangu. Mgonjwa wangu alikuwa na majeraha makubwa sana kiasi kwamba hata kutembea alikuwa hawezi muda wote yupo kitandani." Dokta Richard Bango alizungumza lakini akiwa makini na macho ya Zaituni. Zaituni alikumbwa na mshtuko wa wazi kabisa baada ya kusikia kuwa mgonjwa yule alikuwa ni mgonjwa asiyeweza hata kutembea tena alikuwa na majeraha makubwa. Hakujua kama mshtuko ule ulikuwa ukidhihirisha jambo kwa Daktari yule.




"Umekumbuka kitu?" Akauliza Dokta Bango baada ya kuona ule mshtuko. Zaituni akatikisa kichwa kwa namna ya kukataa akiwa amechanganyikiwa waziwazi.




"Unazidi kuniongopea Zaituni. Mgonjwa wangu aliniambia kuwa siku ya kwanza saa saba usiku ulikwenda kumuhudumia hata hivyo huduma yako iliishia njiani, siku ya pili hukwenda japo yeye alikuwa akitaraji huduma yako na siku ya tatu ukaenda na ulimpa hudua hadi ulipojua anaendeleaje ndipo ulipoondoka...hapa pia hukumbuki au unajitia tu hamnazo?" Aliuliza Dokta Bango huku akiwa amebadilika kwa kiasi kikubwa sana. Zaituni akawaza kwa kina sana kuhusiana na maneno yale, akakumbuka kitu na hiki kilimpa hofu zaidi.






Mgonjwa wangu aliniambia kuwa siku ya kwanza saa saba usiku ulikwenda kumuhudumia hata hivyo huduma yako iliishia njiani, siku ya pili hukwenda japo yeye alikuwa akitaraji huduma yako na siku ya tatu ukaenda na ulimpa hudua hadi ulipojua anaendeleaje ndipo ulipoondoka...hapa pia hukumbuki au unajitia tu hamnazo?" Aliuliza Dokta Bango huku akiwa amebadilika kwa kiasi kikubwa sana.




SONGA NAYO....




Zaituni akawaza kwa kina sana kuhusiana na maneno yale, akakumbuka kitu na hiki kilimpa hofu zaidi. Akajua kuwa alikuwa akionekana wakati akiwa anamfuatilia yule jamaa usiku ule kwa kuwa hakuna muda ambao yule jamaa alitoka zaidi ya usiku wa saa saba. Aliogopa sana na akawa anatikisa kichwa chake hovyo kwa namna ya kukataa huku akiwa anarudi nyuma.




"Zaituni uko pale Hospitali kwa ajili ya kazi na si kufuatilia mambo yasiyokuhusu. Niliweza kukuona mwanzo mwisho ulivyokuwa ukimfuatilia yule mgonjwa wangu. Mara ya kwanza uliishia kuchungulia lakini mara ya pili ulitoka kabisa nje. Sikujua unamadhara gani na sikuwa nimekujengea sana mashaka, ila kilipotoke kile kifo cha mgonjwa wangu ambacho kwa imani ya kawaida tu wewe ndiye umehusika na uhusikaji wako moja kwa moja ukanitanabaishia kuwa kuna mtu nyuma yako." Aliongea Daktari, hapa Zaituni akaanza kumfikiria Abasi Mgizu aliyejitambulisha kwake kama mwandishi wa habari. Akakumbuka siku alipomuibukia ofisini na kumuuliza maswali mawili matatu kisha kuondoka wakiwa wamepeana ahadi ya kukutana. Akakumbuka kuwa siku ile ndipo ilipotambulika maiti ya yule jamaa kule wodini. Akapata hofu zaidi na kuona huwenda kweli Abasi amehusika kwa kiasi kikubwa kwa tukio lile mauaji.



ITAENDELEA


   


Simulizi : Mikono Ya Jasusi 


Sehemu Ya Tano (5)




"Ni nani aliyekuwa anakutuma umfuatilie mgonjwa wangu?" Akauliza Dokta Bango. Zaituni akakataa kuwa hakukuwa na mtu aliyemtuma. Kitendo hicho kikaibua hasira za wazi kabisa kwa Bango akachomoa bomba la sindano toka kwenye koti lake la suti. Alikuwa amevaa suti nyeusi sambamba na miwani ya kusomea huku kichwani akiwa amevaa kofia ya pama. Huu ulikuwa ndiyo muonekano wake akiwa nje ya kazi. Akatoa kifuniko cha kuikinga sindano na kukitupa kisha akavuta hatua kumsogelea Zaituni. Zaituni alikumbwa na hofu na akajua tu kile ni kifo kwani kimiminika kilichopo kwenye lile bomba la sindano hakuwa amewahi kukiona. Akatoka mule chumbani mbio na kukimbilia sebuleni. Akili yake ilikuwa ikimwambia kuwa hakuna mtu aliyepaswa kumpa msaada zaidi ya Abasi Mgizu. Akakumbuka simu yake ilikuwa kochini sebuleni hivyo aliikwapua mara tu alipofika. Wakati akiwa anatafuta namba, Bango alishafika. Zaituni akakimbia hata hivyo hakuwa ameachwa umbali mrefu. Alikuwa kwenye ile korido akielekea mahali choo kilipo huku akiipiga ile namba na kuiweka sikioni. Aliufungua mlango wa choo na kuingia hata hivyo Dokta Bango alikuwa ameshafika na kumtazama kwa macho ya kikatili.




"Choooniiiii...PAAH...! AAIIII!" Alipiga kelele Zaituni, mara baada ya simu kupokelewa na alikuwa na lengo la kueleza mahali alipo ili kama mtu huyo yupo karibu basi awahi na kuweza kumuokoa. zaituni aliyekuwa ameishikilia Khanga yake, alipopiga lile yowe la taarifa akapokea kofi zito ambalo lilibadili yowe lile na kuibua la uchungu simu ile ikadondoka na kutumbukia kwenye sinki la choo ikapotelea ndani. Dokta Richard Bango alimchapa Zaituni makofi matatu kisha akamcho na ile sindano kwenye mbavu. Akawa anamtazama kwa macho ya kinyama zaidi.




"Hii ndiyo safari yako ya mwisho huyo basha wako hawezi kufanya kitu juu yako." Aliongea Dokta Bango huku akiwa anamtazama mrembo huyo kifedhuli. Macho ya Zaituni yakawa yanapoteza uoni wake huku akianza kukakamaa kwa kasi sana hatimaye akadondokea kwenye sinki la choo cha kukaa huku kichwa chake akikipigiza ukutani. Dokta Richard Bango alilichomoa lile bomba la sindano na kuchukua ule mfuniko wake akaurudishia kisha akamtoa ile khanga Zaituni na kuitupia pembeni.




"Ulikuwa ni mrembo sana na uliyejaaliwa kila kitu hata hivyo kwa sasa huna ladha tena." Akasema huku akimtemea mate na kutoka mule ndani.




__________




Ile ilikuwa ni sauti ya hofu na muongeaji alidhihirisha kuwa hakuwa katika kipindi chenye usalama. Alan alichanganyikiwa baada ya sauti ile kisha kusikika kishindo cha kipigo. Hakuona haja ya kuendelea na safari yake tena. Alikuwa ameshaanza kuukaribia mzunguuko wa Mabanda ya papa, kasi aliyoongeza ikapelekea kuunzunguuka ule mzunguuko kwa namna ya kufurahisha sana watu waliokuwa pembeni mwa barabara walibakia midomo wazi kwani halikuwa jambo la kawaida. Bodaboda walikuwa wakipiga honi vibaya sana huku mayowe machache yakiibuliwa, alirudi kwenye barabara ile ile ya jamhuri akiwa kwenye kasi ile ile. Alikuja kufika nje ya nyumba ile yenye namba 120 inayomilikiwa na muuguzi Zaituni. Aliteremka garini kwa haraka kubwa huku mvua kubwa ikiwa bado inaendelea kunyesha akauelekea mlango kwa haraka akijikinga na ile mvua kwa kuiwahi baraza ya nyumba iliyopakana na ya Zaituni huku akiwa makini mno. Eneo lile lilikuwa kama alivyoliacha hakukuwa na gari yoyote wala chombo chochote cha usafiri ambacho labda angekijengea mashaka ni ile gari nyekundu tu ambayo ilikuwa chini ya mti hata alipoitazama vizuri aligundua kuwa haikuwa nzima kwani gurudumu zake zilikuwa hazina hewa. Akausukuma mlango huku akiichomoa bastola yake kutokea mafichoni. Alitembea kwa tahadhari kubwa akiifuata korido moja baada ya kuipita sebule. Hakutaka kukimbilia chooni ambako mtu aliyepiga yowe ndiko alikosema yupo, kwanza alihakikisha anakagua vyumba vyote kisha akishajihakikishia usalama ndipo aelekee upande wa chooni. Aliingia chumba kimoja baada ya kingine na hakukuwa na kitu alichoambua, vyumba vilikuwa vitupu. Akaingia chumba cha mwisho ambacho Zaituni alikuwa akikitumia, huku nako hakukuwa na mtu wala kiumbe chochote akiwa anataka kutoka akavutiwa na kitu kimoja nacho ni alama za viatu. Alama hizi zilikuwa bado mbichi kabisa kuashiria kuwa mtu huyo hakuwa ameingia muda mrefu. Lilikuwa ni buti kubwa. Akarudi nyuma huku akiendelea kuzichunguza zile alama za viatu hadi zilipokomea kwenye mlango wa kuelekea maliwatoni, akagundua mtu huyo alishatoka kutokana na alama zile zilivyomuonesha, akausukuma mlango huo na kuingia. Loh! Hakuamini kwa haraka alichokiona, mwili wa Zaituni ulikuwa uchi wa mnyama ukiwa umelala juu ya sinki la choo cha kukaa. Hakuwa hai tena kwani mwili wake ulikuwa umekakamaa na ngozi ya mwili wake ilikuwa ikibadilika rangi na kuwa nyeusi kwa kasi kubwa. Akatoa glovu zake mfukoni na kuzivaa kisha akausogelea ule mwili, hakukua na majibu tofauti zaidi ya yale ya mwili huo kuwa hauko hai tena. Alihuzunika sana moyoni mwake, alijilaumu sana kwa kuondoka mapema kwani huwenda ile hali ya Zaituni ya kubembeleza na kumtaka aendelee kuwapo pale ilikuwa na maana kubwa sana na pengine angekuwa msaada kwa binti huyo hata hivyo hakujua mtu aliyevamia humo ndani alikuwa na hatari kiasi gani hivyo hata yeye kuweza kuondoka ilikuwa ni ponyaponya yake ya kukaa mbali na kifo. Aliiokota ile khanga na kuufunika ule mwili mara baada ya kuutoa kule chooni na kwenda kuulaza sebuleni chini. Alitoa kifaa kidogo kama cha kukatia kucha kisha akataka kukata nyama ndogo sana kutoka kwenye ule mwili ili aweze kutafuta namna ya kuufanyia uchunguzi. Alishajua kilichotumika kumuondoa Zaituni Duniani kilikuwa ni sumu alichotaka kujua Alan je, ni sumu ya aina gani? Alisita kufanya hivyo kwanza kisha akasimama na kutafakari kama lingekuwa ni jambo la msingi kufanya vile. Akafikiria kuukabidhi mwili ule mikononi mwa polisi kisha waupeleke Hospitali na kuusimamia hadi majibu ya uchunguzi yatakapokuwa tayati ndipo ayafuatilie. Wazo hili halikuwa na maana kwake kwa vile hakupenda kuwa karibu na askari polisi katika kazi yake hii ya kijasusi hivyo akalipuuzia akawaza tena na kuona ni bora auache huku akitoa taarifa polisi kutokana na kuwa alishajua kifo cha Zaituni kilitokana na sumu. Wazo hili halikuwa baya hata hivyo hakukubaliana nalo kwa asilimia mia moja. Kikubwa alichokiibua kichwani mwake mara baada ya kuwaza na kuwazua ni kupata muunganiko mzuri wa matukio hivyo wazo la kuondoka na kipande cha nyama lilikuwa ni la maana zaidi. Aliinama na kukata kipande kisha akatoa mfuko wa nailoni na kukifunga vizuri akakitumbukiza kwenye moja ya mifuko yake ya suruali, akavua zile glovu na kuzirudisha mfukoni kisha akatoka mule ndani. Alipofika garini aliitoa simu yake na kupiga polisi akatoa taarifa ya mauaji yale na kutoweka lile eneo.




Alan alikuja kuisimamisha gari yake maeneo ya barabara ya kumi na nne ikiwa ni baada ya kuisogeza gari yake pembezoni mwa barabara na kuiegesha. Akatazama usalama wa eneo lile alipoona sura za watu wa eneo hilo si za kutilia mashaka, akateremka na kuingia ndani ya maabara moja ya hapo mtaani. Hakutaka kuuliza bali alikwenda moja kwa moja hadi kwenye chumba kilichoandikwa 'Doctor', akausukuma mlango na kuzama ndani. Chumba hicho cha ofisi kilikuwa na makabrasha mengi ya kiofisi kama zilivyo ofisi nyingi za kitabibu. Juu ya meza kulikuwa na kila aina ya vifaa ambavyo vilistahili kuwa juu ya meza ya ofisi kama hiyo, nyuma ya meza ile kulikuwa na mzee mmoja wa kihindi akiwa amejikalisha kwenye kiti chake cha kiofisi akiwa amevaa shati la mirabamiraba huku koti lake la suti akiwa ameliegemeza nyuma ya kiti chake alichokalia. Mzee yule alinyanyua uso wake mpana uliovalishwa miwani ya kusomea akiwa hana wasiwasi hata kidogo.




"Karibu sana...karibu kiti...!" Alikaribisha yule mzee wa kihindi.




"Asante sana Dokta." Alijibu Alan huku akiwa anatazama kila kona ya ofisi ile kwa kificho.




"Naweza saidia veve...?" Akauliza yule Daktari. Alan akamtazama yule mzee kwa tuo kisha akasema.




"Ndiyo, Dokta kuna jambo nataka ulifanyie uchunguzi wa kitaalamu ili niweze kujua." Akaweka tuo Alan kisha akatoa ule mfuko wa nailoni na kuuweka juu ya meza akaufungua na kutoa kile kipande cha nyama. Dokta yule alishtuka sana na kumtazama mteja wake kwa macho ya mshangao.




"Usiogope Daktari," akaendelea Alan.


"...mimi ni mpelelezi kutoka kwenye jeshi la polisi hapa mjini. Kuna mauaji yametokea na mauaji hayo yamekuwa ni tata sana hivyo nikaona mbali na uchunguzi wa madaktari unaofanywa na Hospitali kubwa ya hapa jijini, mimi nifanye uchunguzi wangu ili baadaye niweze kuoanisha majibu toka pande zote mbili." Akahitimisha Alan huku akiambatanisha na kitambulisho kinachomtambulisha kama askari polisi ambacho hiki alikuwa nacho muda wote na aghalabu hutembea nacho akiwa na umuhimu nacho mkubwa. Dokta akawa kama anauzito fulani wa kuikubali kazi ile, Alan akavuta waleti yake akahesabia noti nne za shilingi efu kumi na kuziweka mezani.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog