Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (6)
Sehemu Ya Pili (2)
Baada Ya Kukamatwa Isack anafanya mpango wa kumtoa gerezani Ragiv,na kumrudisha katika kazi ya kumwangamiza zidu,je Ragiv atafanikiwa?,songa nayo...
Wazo alilolipata lilifanya kazi yake iwe nyepesi,na kumtengenezea mazingira mazuri ya utekelezaji wa mauaji!...
Dokta Nurath Abdulhaziz Daktar mwenye asili ya kiarabu huyu ndiyo alokuwa akisimamia matibabu ya Zidu,binti uyu Daktar Bingwa alotokea katika moja ya familia kubwa nchini Saudia Na Kupendelea Kufanya Kazi India,alipenda Kuvaa Mabaibui Na Nikabu Kuficha Sura Yake,
Ragiv alipania kufanya linalowezekana kuingia wodini kama daktar yule na kutekeleza
mauaji,siku hiyo akukuwa na wagonjwa wengi akiwa kavaa kepu yake,kuficha sura yake kwa mara nyingine akawasili katika hosptal ile!...
Akakaa Upande Wa Wagonjwa Waloudumiwa Na Daktari Nurath akiwa mgonjwa wa mwisho hatimaye akaingia,bila kuchelewa alichomoa silaha na kumuweka daktar yule chini ya ulinzi akamwambia asimame kutoka kwenye kiti amfate,daktar akamtwii,alipo mfikia akampiga pigo moja shingon likamzimisha daktari yule,akamvua lile baibui akalivaa yeye,akavaa na ile nikabu,akachukua funguo akatoka,akafunga mlango kwa nje akaelekea sasa zilipo wodi alolazwa Zidu akipania siku hiyo kutokuaribu kaz
Alifika Mpaka Wodini,akampa Ishara Katarina Atoke Kusudi amuhudumie mgonjwa akutaka kutoa sauti yake akihofu kugundulika,
Katarina bila wasiwasi akasimama na kutoka nje...
Kitendo cha Katarina tu Kutoka Nje,haraka haraka Ragiv akatoa bastola na kuijaza risasi akaifunga kiwambo cha kuzuia sauti taratibu akamsogelea Zidu!...
Ile amefika kitandani anaunyoosha mkono wake pasina kutegemea mwanaume akainuka kwa kumkita teke risasi ikaenda kule!
Wakati akiwa katika butwaa Zidu alimbandika teke jingine akaangukia kitanda!
Katu akujua kama Zidu Yupo Fiti,na alishapona,na kuwa hosptal mpaka muda ule ni kumtega
Akijua tu lazima angejileta kiu yake kubwa ni kutaka kujua ni nan alomtuma na kwa nin atake kuuwawa?!...
Ndio,alijua Anakazi Ngumu Sana Kinte Ya Kwenda Kupambana Na Kidume Cha Kazi Gambi,na alijua fika maisha ya rais wake yalikuwa mashakani,na Rais Ndiyo Alompigania Na Kumleta India Kwa Matibabu Ila kiu yake aman ya moyo wake ni kuwajua wabaya wake ndo kisa cha kuendelea kujifanya mgonjwa mpaka muda ule japo hata rais akujua jambo lile alijua Zidu bado mgonjwa...
Na Sasa aduh Yake Alikuwa Mbele Yake akamsogelea pale kitandani alipodondokea akaunyanyua mguu na kuutua usoni,Ragiv akaachia bonge la yowe!.
Kwa Upande Wa Katarina Kitendo Cha Kutoka Nje tu macho yake yakatua parking mbele upande wa pili wa korido ile,akaikumbuka ile gari ya Ragiv Machale Yakamcheza,ghafla Akasikia Yowe haraka sana akarejea wodini,akuamin akionacho,mume wake alikuwa akipambana na alomjua ni daktari,akutaka elimu nyingi kung'amua kuwa yule akuwa daktari palepale akaingia kumsaidia mumewe sasa kimyakimya wakaanza kumchangia Ragiv!...
Wakimlazimisha aseme ni nan kamtuma,
Ragiv baada ya kuona anabanwa sana ghafla aliingiza mkono mfukoni alipoutoa akautupa mdomoni,muda ule ule akaenda chini povu mdomoni likaanza kumtoka,akukaa sana akakata roho,
Kimuyemuye Kikatawala Watu Wengi Walikuwa Madirishani Wakichungulia,na tayari simu ilishapigwa polisi kujulisha juu ya vurugu zile,Zidu alimfungua ile nikabu Ragiv Watu Wote Wakashangaa,muda ule ule maaskari wakawasili wakachukua maelezo,wakaenda ofisin kwa daktar Nurath wakafungua wakamkuta dokta akiwa kavuliwa nguo wakamsitiri,mwili wa Rajiv Ukawekwa Katika Chumba Kingine Polisi Wakafanya Uchunguzi Wao Walipotosheka Ukawekwa Mochwari,Zidu na Katarina hatimaye wakaruhusiwa wakapanda ndege kurejea Tanzania Kuchukua Vitu Vyao Na Kumuwaga Rafiki Yao Walomchukulia Kama Ndugu Yao Isack,siku Inayofatia ndiyo warejee Kinte!
Mioyon Mwao Wote Walikuwa Na Furaha,ila Zidu bado alikuwa akijiuliza ni nan hasa atakaye kumuua akuwa na jibu sahihi...
Baada Ya Kukata tiketi wote walikuwa ndani ya ndege kwa safari ya kuelekea Tanzania,na Kesho Yake Wasafiri Kuelekea Kinte...
Hali ndani ya ndege ilikuwa niya utulivu wakafunga mikanda yao vizuri ndege ikapaa na kuiacha ardhi ya india,kama nusu saa tu ndege ikiwa angani Zidu alihisi usingizi na si yeye tu mpaka mkewe Katarina,na Si Wao tu katika hali ya sintofahamu abiria wote wakalala,tena usingizi mzito hakuna alojua ni nin kilichotokea ila rubani alionekana kutabasamu,akaelekea alipo pajua yeye akaishusha ndege ile katikati ya msitu,kulikuwa na gari ikimsubiri Katarina Na Zidu Wakashushwa Na Kuingizwa Ndani Ya Gari Ile Ndege Ikapaa Na Kuendelea Na Safari,rubani Na baadhi ya wafanyakaz wake wakiwa na furaha,wakijua katika akaunti zao zimeshajaa...
***
Isack akiwa ofisini kwake,ghafla katika 'breaking news' ikatangazwa habari ya kufa kwa Ragiv hosptalin baada ya kutaka kumuua Zidu,habari Ile Ilimchanganya Sana Na Kumtia hasira,
Kabla ajaamua cha kufanya ghafla akapokea simu kutoka nje ya nchi,Zidu Ndo Alompigia alijifanya kusikitika kwa yalomkuta,akampa pole ila moyon mwake kulikuwa na chuki kali,dhidi ya mtu huyu
"kwa hiyo kesho nategemea kuja huko kesho kutwa nirejee Kinte"
"umekata Tiketi Ndege Gani Mkuu?"
Isack akauliza kimtego
"safiri Salama earway"
Hii Ilikuwa Ni Ndege ya Tanzania Itokayo Tanzania Kwenda India Na Kurudi,ivyo Zidu Ndo Aloikata,kumwambia Vile Isack akatabasamu akamtakia safari njema swaiba wake yule,akakata simu sambamba na kumpigia kijana wake alofanya kaz katika shirika lile akampa mchongo ule,na yule mtu akampigia rubani na kumpanga wakatafuta madawa ya usingizi!,mafia wakajipanga...
msitu wa zungu uliopo katika kisiwa cha maliyata kulikuwa na kambi ya mafia ndipo ndege ilipotua Zidu Na Katarina Wakashushwa,na Kuingizwa Ndan Ya Gari...
Isack akajulishwa naye akapanda ndege yake kuelekea kisiwani...
watenganishwe vyumba kila mtu awekwe chumba chake,kuwekwe mabomu mimi ndo ntakuja kuyalipua,nusu saa ntakuwa hapo...
mabomu yakategeshwa kwa siri Zidu Akafungwa Katika Chumba Chake Vivyo Vivyo Kwa Katarina Akasubiriwa Isack tu awasili!...
Kweli Isack Akawasili Akakaribia Katika Chumba Kimoja Macho Yake Yakatua Katika Tv Ilokuwa Ukutan Ambapo Zilionesha Zidu Na Katarina Vyumban Mwao Walipofungwa Pasina Fahamu Akapewa rimonti ambapo angebonyeza tu kitufe chekundu Kingeruhusu Kulipuka Kwa Mabomu Yale...
Akiwa Na tabasamu akapokea rimonti kidole chake kikagusa batan nyekundu tayar kuibinya macho ya vijana wote yakiwa katika runinga wakitegemea mlipuko mkubwa washangilie...
DAH ZIDU & KATARINA HATARINI WATAPONA KWELI?!
"bosi noooooooo!"
Watu Wote Wakamwangalia Yule alokuwa akimzuhia bosi wao kwa jina alitambulika kama Simion killer,kijana wa kituruki,katili asiye na chembe hata ya huruma!
"uzandiki huo bosi,unauaje kimama ivyo watu atujawatesa au nyinyi mwaridhika hawa kufia usingizini!"
"kwel simion upo sahii tuwatese mkuu,unawauaje hivyo"
Kijana Mwingine Alotambulika Kwa Jina La Ramtony akadakia Isack akaweka rimonti juu ya meza!
kwa uso wa tabasamu akaongea "hawa si watu wa kawaida wana uwezo wa ajabu na ukiwapa nafasi awatokuacha mzima,wangap wanaungana na simion pamoja na Ramtony?"
Vijana Wengine Wawili Wakanyoosha vidole,
"ni kwel bosi huu ni uduwanzi kuua ivyo,lazima wateme damu uongo pizo?" huyo jamaa alotambulika kwa jina la 'Kilimi' Akaungana Na Wenzake,
"basi Nawapa Kazi hii nyinyi Pizo,Kilimi,Ramtony na wewe Simion kumtesa na kumfyekelea mbali sisi tutatazama kila kitu hapa,"
Kwa Furaha Wa Nne Wale Wakiwa Na Silaha Nzito Wakatoka Katika Jumba Lile Kuelekea Katika Vyumba Vya Pemben Kule Walipoifadhiwa Zidu Na Katarina...
Huku Nyuma Isack Alibaki Kucheka Akiwasikitikia Vijana Wake Wale,akupenda Kubishana Na Mtu Kuliko Kubishana Alikuwa Radhi Hata Kupoteza,akupenda Kabisa Kitu Ubishi...
**************************
BAADA YA MASAA KADHAA
Zidu kule ndani alifumbua macho yake na kupokelewa na maumivu makali katika kichwa chake!
Akataka kupeleka mkono wake kugusa pale maumivu yalipotokea akapokelewa na ukinzani mzito katika mkono wake!
Akatanabahi kwamba mkono umefungwa na kamba ngumu ,na si mikono pekee mpaka miguu na tumbo katika kitanda kile alicholalia!
Rundo la maswali yakatiririka katika mawazo yake!
Alikumbuka mara ya mwisho alikuwa ndani ya ndege akielekea Tanzania akapatwa na usingizi mzito wa ghafla Je ni nini kilichoendelea mpaka kuwa pale?!
Na ni wapi pale?!
Katarina mke wake naye yupo wapi!
Akuweza kuendelea kuwaza zaidi maumivu makali yaka ambaa katika kichwa chake ilikuwa ni kama mtu alikigonga na nyundo!
Ndiii ndiii ndiii
Alijua yupo tena ndani ya mtihani mzito ilopaswa kwa vyovyote vile aufahulu
Ila kwa pale akukuwa na la kufanya zaidi ya kusubiri kitakachoendelea!
Muda ule ule Zidu alipofumbua macho yake upande mwingine wa vyumba vile mwanadada Katarina naye akafumbua macho yake!
Ndani ya sekunde ile ile ya ufahamu wake tayari akili yake ilishaisoma hatari ilokuwepo mbele yake na kuanza kufikiria mbinu za kujinasua mtego ule ambao akuitaji kujua kwa wakati ule amenasaje na ipi sababu ya yeye kuwa pale
Katika pembe ya macho yake upande wake wa kulia aliwaona vijana wawili walokuwa na silaha katika vifua vyao ,
Vile vile pia upande wa kushoto vijana wengine wawili walisimama wakiwa na silaha zao!
Vijana wale baada ya kuona Katarina kazinduka wakapeana ishara na vijana wawili wakatoka na kuwa acha wawili mule ndani!
Tayari walisha gundua masaa ya madawa ya usingizi kufanya kazi yalishapita hivyo wale wawili walikuwa wakirejea katika lindo lao kwani pale walikuwa kwa ajili ya stori!
Katarina tayari alishajua alipaswa kufanya nini!
Akaachia mguno hafifu!,ishara ya maumivu lakini mguno ule aliutoa kwa lengo flani!
Ulikuwa ni mguno wa kimapenzi naye aliutendea haki,na kwa kuwa alijua anatazamwa na uchovu wa Madawa Yale akajinyegesha zaidi!
Macho yake yaliiva,na kuwa mekundu akajilazimisha kunyanyuka lakini alishindwa akarudi chini!!!
"Mmmh jamani aaaaah ooooh nifungueniiii nimewakosea nini mimi chochote ntawapa ila msiniue"
Katarina akaongea kwa sauti nyembamba wale vijana wawili walobakia wakatazamana na kupeana ishara,mmoja akasogelea dirisha na kuchungulia kwa nje akashusha pazia na kuufunga mlango kwa ndani!
"Ikiwa utakubali kutupa hata kimoja kimoja tutakuacha huru sawa?!"
Kijana yule akaongea huku akimwangalia Katarina,nadhani akumjua vizuri dada yule!
Katarina akatingisha kichwa ishara ya kukubali!
"Ukienda kinyume na sisi atutosita kukumiminia risasi Ramtony naanza mchezo naitaji utuelekezee bastola ikiwa ataleta kujua I mean ujanja ujanja sambaratisha ubongo"
Kijana yule aliongea huku akivua koti na kumvamia Katarina katika kitanda chake!
Ram aliwaelekezea risasi!
"Shhhh aaaah mapenz gani hayo jamani raha ya penzi kuandaana nifungulie bwana nikupe kitu roho inataka mbona hujiamini?!"
Katarina akaongea huku akimkata jicho na kuzidi kujifanya ameshkika!
"Sasa hapa utaufaidije utamu wangu na miguu umefunga,nitakupapasaje na mikono umefunga siwez kuwageuka na kuna Alonshikia mtutu plzzz nifungulie"
Katarina akazidi kubembeleza,yule jamaa akamtazama mwenzake alomtingishia kichwa ishara ya kumruhusu amfungue akarudi nyuma hatua kadhaa bastola yake akiishika sawia!...
Je nini Kitaendelea hapo Katarina atasalimika?!
Vipi Zidu Kule!
Rais Laizer Nyoshi ataupona mkono wa Gambi?!
"Sasa hapa utaufaidije utamu wangu na miguu umefunga, nitakupapasaje na mikono umefunga siwez kuwageuka na kuna Alonshikia mtutu plzzz nifungulie"
Katarina akazidi kubembeleza,yule jamaa akamtazama mwenzake alomtingishia kichwa ishara ya kumruhusu amfungue akarudi nyuma hatua kadhaa bastola yake akiishika sawia!..
Kijana Yule akiwa na uchu na hamu ya kunongeka akamvamia Katarina na kumfungua kamba za mguu na za mkono!
Akianza za mguu na kumalizia za mkono!
Wote wale wawili walisha ama kihisia na Katarina ndicho alichotaka!
Awaweke katika mawazo mgando,ili awashugulikie vizuri
Ghafla akafanya kitu ambacho akikutarajiwa na wawili wale!,ambao walitoa mawazo katika ulinzi na kuyapeleka katika tamaa,
Akiwa pale chini Katarina jamaa yupo kwa juu akianza kumpapasa,ghafla alishtukia akitupwa , muda ule ule binti akajirusha hewani na kuachia teke kwa mshika silaha alokuwa ameganda kama sanamu!
Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana kama sekunde tano hivi
Sasa alikuwa katikati yao!,kakaa kwa style ya kimapigano!, akiwatazama wote kwa kupitia pembe ya macho yake!
Yule alokuwa ameshika bastola awali,akataka ageuke aifate silaha yake lakini alichelewa kwani Katarina alijirusha na kukikamata kichwa chake!!!
Akakikunja kidogo kikalia "kaaaa" tayari alisha kivunja akamwachia mwili ule ukaporomoka chini!,ukibadilik jina kuitwa maiti au marehemu!
ITAENDELEA
Simulizi : Kiapo Cha Mfungwa (6)
Sehemu Ya Tatu (3)
"Ramtony?!..."
Jamaa yule aliyebakia akaita akiuangalia mwili wa mwenzake
Macho yake akayatoa katika mwili ule na kuyapeleka kwa msababishaji , akapokelewa na tabasamu zito!...
"Je unaitaji kumfata mwenzako?!"
Katarina akaongea kwa dharau, lengo amkasirishe Jamaa apaniki akose umakini na ilo alifanikiwa jamaa akiwa sasa anaongozwa na hasira umakini akiuweka pembeni akajirusha kumuendea Katarina naye kwa hamu akamsubiri
alipomfikia akafyetua mateke mawili ambayo Katarina yote aliyapangua
Naye akaachia teke lake moja jamaa akapangua wakati anapangua msichana akarusha ngumi ilompata sawia katika jicho lake!
Jamaa akaachia yowe akipeleka mkono kugusa jicho lake muda huo huo Dada yule akapata mwanya sasa wa kumvaa kwa teke lingine
Teke lililomrusha jamaa na kujigonga ukutani akaporomoka!
Katarina akamsogelea!....
"Hapa ni wapi na kwa nini mlituteka na mmetumwa na nani,na mko wa ngapi, Zidu yupo wapi?!"
Akamuuliza Lundo la maswali kijana yule akujibu zaidi ya kuachia cheko lake la dharau!,
Katarina akauachia ule mdomo alokuwa ameushika na kumkamata katika koromeo!
Aliukamata mshipa mmoja na kuubana,jamaa akagugumia kwa maumivu!
"Utaki kusema siyo!"
Akamuuliza!,
"Nii ache na...na...sema"
Akaongea na Katarina akamuachia,ghafla zikasikika hatua kwa nje kama mtu alikuwa anakuja!
Katarina akakishika kichwa na kummaliza akausogelea mlango na kukaa tayari kumsubiri ajaye!
Kitasa kikatingishika na hatimaye mlango ukafunguka na jamaa aloshika bastola akazama mzima mzima,
pasina kujua kuwa kuna mtu nyuma Katarina akamuwai kwa kumrukia na kumdaka kwa nyuma alipomwachia akuwa na uhai tena sasa akili ilifanya kazi zaidi ya awali
Akuweza kuzitambua Mara moja uniform za wale waliozivaa lakini alitambua ni kundi la wanajeshi flani,
Hivyo alimfata mmoja na kuzivua nguo zake akazivaa yeye
Fulana nyeupe zenye mkato wa kijeshi katikati ya mikono miraba miraba na suruali za kijeshi akavaa na kulisogelea dirisha akachungulia nje!
Palikuwa kimya!, akausogelea mlango na kuufungua akachungulia na kutoka!
Ilikuwa ni nyumba kubwa kwa mbele kulikuwa na parking yenye gari tatu za kijeshi
Nje ya chumba kile chenye no 4 Kulikuwa na vyumba vingine vyenye no hivyo hivyo!
Lilikuwa ni eneo geni kabisa!....
Akulielewa...
Akawaza aanze na vyumba vya jirani namba tatu na namba tano kuvichunguza akiwa na lengo la kutambua chochote akalifata dirisha la chumba no tano ambacho chaka aliifadhiwa ndani na kuchungulia!...
***
Ilikuwa ni upande mwingine wa nyumba ile,chumba kile walichokuwepo Isack
Na watu wengine waliketi macho yao yakiwa katika runinga kubwa kufatilia kile kilicho oneshwa,wote walionekana kuridhika na jambo lile
Lilikuwa ni kundi la MAKOMANDOO WA MAFIA ( MWM) walianza kufatilia tukio lile kwanzia mwanzo viumbe wale walipopata ufahamu!
Isack muda wote wa matukio Yale alikuwa akitabasamu na mpaka Katarina anawauwa wale majamaa wawili kundi lile walipiga makofi kumshangilia
"Niliwa ambia huyu si mtu wa kawaida na si yeye tu hata huyo Zidu"
Isack kiongozi wa kundi lile aliongea akaweka tuo na kuendelea!...
"Nilipotoa wazo tuwalipue katika vyumba vyao kabla awajapata ufahamu wale wakabisha kwa kuwa nao ni makomandoo wakataka wawaue kishujaa sijui ni sifa au ni nini wanajua wenyewe na saivi atunao tena duniani wamwisho ndo anaenda kumaliziwa saivi ,....
Je wangapi wapo sawa na Mimi wanaoniunga mkono tuwamalize katika chumba chao au yupo anayetaka dau kama wale akajaribu bahati yake?!"
Kundi lile lote likabaki kimya ni wazi hawakuwa tayari na walikubali Isack awamalize mule mule ndani!
Ni kwamba chumba kile no 5 ambacho Zidu yupo ndani yake kilitegeshwa Bomu na Rimonti ya kulipulia alikuwa nayo Isack na mwanzo kama tulivyoona alipanga awauwe namna hiyo hiyo wale wa nne wakabisha na kuhaidi kuwaua macho kwa macho
Isack akakubali na ndicho walichokipata baada ya Katarina kuingia ndani ya chumba kile muda ule ule tayari bastola yake aloichukua mule ndani alipoua ilishacheua na risasi zisizo hesabika kumiminika kifuani mwa mtu yule alosalia katika wa nne wale
Akamkimbilia mumewe na kuanza kumfungua katika kitanda kile
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment