Simulizi : Wauaji Walitumia, Chai, Miavuli Na Hata Sumu Kuwaangamiza Wapinzani
Sehemu Ya Tano (5)
Badala yake, habari zinasema kuwa alitiwa chuma cha moto katika tupu yake ya nyuma na hivyobasi kuchoma viungo vyake vya mwili bila kuwacha alama yoyote.
Habari hiyo huenda ilipingwa kuwa uvumi na wanahistoria wengi katika miaka iliofuata, lakini hatua hiyo haijawazuia wengine kuendelea kusambaza habari hiyo.
Njama ilopangwa ikapangika
Mara nyengine hata mipango iliopangwa vizuri inaweza kuharibika.
Na kuna wakati ambapo pia chombo cha usaidizi wakati mpango huo unapofeli kinaweza kufeli. Iwapo hilo linaaminika linaweza kutokea basi hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa watu waliopanga njama za kifo cha Grigory Rasputin 1916.
Inaonekana kuwa watu wachache hawakumpendelea mkulima huyo aliyependwa sana na kuamua kumuua. Lakini baada ya kumpeleka hadi katika jumba la mwanamfalme Felix Yusupov huko St Petersburg mambo yalianza kwenda mrama.
Grigory Rasputin, rais wa Siberia aliyedaiwa kuwa nguvu za kuponyesha watu aliuawa 1916
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Grigory Rasputin, raia wa Siberia aliyedaiwa kuwa na nguvu za kuponyesha watu aliuawa 1916
Wauaji wake ,mwanamfalme Yusupov na Vladimir Purishkevich, ambaye alikuwa mbunge kwanza walimlisha keki iliokuwa na sumu. Keki hiyo haikumuathiri na hivyobasi wauaji hao wakaamua kutumia bunduki zao. Risasi walizotumia zilishindwa kumuangusha na ngumi zao katika kichwa chake pia hazikufaulu.
Je aliuawa vipi?
Iwapo wauaji wake wanafaa kuaminiwa ilichukua risasi nyengine nne kufanikiwa kumuua Rasputin, ijapokuwa uvumi mwengine unasema kuwa walilazimika kumzamisha majini.
Lakini madaktari waliochunguza kifo chake wanasema kuwa alipigwa risasi moja katika tumbo na hivyobasi kupoteza damu nyingi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment