Search This Blog

Friday, 30 December 2022

KIAPO (AGANO LA DAMU) (2) - 3

 


Simulizi : Kiapo (Agano La Damu) (2) 

Sehemu Ya Tatu (3)





Isack Analia,kumuomba Msamaha,Zidu ilo ajal anabonyeza anahesabu moja lengo akifika tano ammalize mtoto 

yule asiye na hatia na sasa amefika nne akibakisha moja!



SEHEMU YA AROBAINI NA TATU



Bila Kutarajia Isack Akajikuta Akienda Chini Akampigia Magoti Zidu Huku Akilia!



"usiniue Baba Ntafanya Utakachotaka Lengo Uniachie Uhai Wangu"



Isack Alizidi Kuomba Huku Akiwa Kaishika Miguu Ya Zidu,izrael Wa Kibinadamu



"yaaaas!..."



Zidu Alifurahia Kimoyoni Huku Akiweka Bastola Yake Ile Mezani Lengo Lake Lilikuwa limekamilika!



lengo lake si kumuua mtoto yule kwa wakati ule la hasha!



ile ni kumtisha alijua lau angemuua na kesi ipo mahakaman kutokana na maelezo ya madam jane lazima 

angehisiwa vibaya lengo la kumuoneshea bastola ni kumtisha na ilo alifanikiwa sasa kilichobaki ni 

kutimiza kile kilichomfanya amtishe mtoto yule akaachia kicheko

"ha ha ha kwel maisha yana thaman hadi wewe mtoto unayalilia maisha bas siyo kitu nakuacha hai ikiwa tu 

utanikubalia ombi langu ukienda kinyume na mimi sitakupiga tena bastola bal ntakutupa katika kisima 

changu uliwe na mamba



jumatatu tutaenda mahakaman ukiulizwa unanijua kama nani sema bamdogo unaskia?"



huku akitetemeka isack akatingisha kichwa



"nilikutesa nkakutupa porini sema hapana sijawah kukutesa unaskia?"



Isack Akakubal Huku Bado Akiendelea Kulia



"pia Useme Madam Jane Huwa Anakutesa Anakunyanyasa Sawa?,ukienda Kinyume Na Mimi Nitakuua Wewe Na Huyo 

Mwalimu Wako Si Unajua Mi Naroho Mbaya Au Nikuue"



"hapana Baba! Usiniue"



"Bas Ufanye Ivyo Usimwambie Madam Kama Nilikuja Ukifanya Ivyo Utaish Vizur We Na Huyo Mwalimu Wako 

Sitowafatilia Tena Sawa?"



"sawa Baba!"



"hata madam wako akikwambia useme ukwel ili nifungwe ntatoroka ntaja kuwaua umenisikia?"



Isack Akaitikia Kwamba Ameelewa mwanaume akaondoka,



'baada ya haka katoto kukiri madam atafungwa hapo ndipo tutamtumia watu rumande akauwawe mimi 

nikikabidhiwa haka katoto nakaulia mbali natengeneza ata ajali ha ha ha huu mpango umeenda vizur'



Zidu aliwaza akiwa ndani ya gari lake akielekea nyumbani baada ya kutoka kule kwa madam jane



kizaazaa!



****



Madam Jane Alirudi Nyumbani Akiwa Amechoka Mwili Na Akili!

Hata Wewe Ndugu Msomaji Yangekukuta Haya Lazima Ungechoka Eti!...



Kesi Imefunguliwa Bila Kutarajia,pasina Kujipanga,mashahidi Wawili Alowategemea Wameuwawa hiyo hiyo 

siku aloenda kuwaona mwisho insp Nurdin Naye Apatikani!



tegemeo lake la mwisho lilibakia kwa isack maskin akujua kuwa mtoto yule naye alishatengenezwa!,kila 

mara alijitahidi kupiga namba ya Nurdin Lakini Aikupatikana!



"mwanangu Isack Baba Yako Apatikani Kilichobaki Jumatatu Useme Ukweli Wote Mahakamani Yule Ba Mdogo 

Wako Feki Afungwe Sawa?"



"sawa" Isack Aliitikia Huku Moyon Akiwaza 'laiti Ungejua Mama Kilichotokea Lazima Nidanganye Kuyalinda 

Maisha Yetu Yule Ba Mdogo Feki Si Mtu Mzuri Yule'

Isack Aliwaza Akimwangalia mama yake kwa huruma!

"usijal Isack tutashinda tu!"

madam jane bado alizidi mpa moyo mtoto wake yule



maskini! laiti angejua?!!!...



Ukumbi Wa mahakama ulijaa,watu walikuwa wengi kuliko siku zote siku hii hata mheshimiwa waziri 

alikwepo!



Waandishi Mbalimbali Wa Habari Walikwepo Kuripoti Tukio Lile!



Kesi Ikaanza Sikilizwa Kwa Madam Jane Kusomewa Shtaka Akakana Akaambiwa Apandishe Mashahidi Akasema 

Wale Walinzi Wa Msituni Amekuta Amekufa Ukumbi Wote Ukaguna Na Vipi Kuhusu Yule Askar Alomruhusu Kuishi 

Na Yule Mtoto Akasema Apatikani Ila Ushahidi Ulobakia Ni Isack Pekee Ndo Awezaye Kueleza Kila Kitu Na 

Ndo Shahidi Yake Akaruhusiwa Mtoto Yule Apande



"ehe Mtoto Unaitwa Nan?" Mwendesha Mashtaka Akamuuliza



"isack John" Isack Akajibu Baada Ya Kuapiswa!



"huyo hapo unamjua?!"



mwendesha mashtaka akauliza akimnyooshea kidole Jitu katili ZIDU K,Zidu akamkata jicho na kumkonyeza



"ba mdogo wangu!"



"ulishawah ishi naye?!"



"ndiyo!"



"ilikuwaje mpaka ukaishi naye?"



"alikuja kunichukua kwa jirani yangu mama mery"



"alishawah kukutesa?"



"hapana ajawah kunitesa!"



umati wote ukashtuka,madam jane akuamin kile alichokisikia alihisi anaota akapekecha macho pengine 

azinduke kwenye ile ndoto!



mwendesha mashtaka akaoji tena



"ba mdogo waku yule alishawah kukutesa?"



"hapana ajawai kunitesa"



"alishawah kukutupa porini na kujaribu kukuua"



"hapana ajawai"



"we mtoto muongo sema ukwel usiogope kitu isack!"

"dada hapa ni mahakaman na panataratibu zake kaa kimya"



hakimu akawa kimya,madam akanywea!,



"eleza mahakama ilikuwaje mpaka ukaenda kuishi kwa madam jane"



"ye aliniita tu niishi kwake"



"nawe ukaenda uliomba ruksa kwa bamdogo wako!"



"hapana niliogopa asingeniruhusu"



"sina jingine madam jane unaswali kwa mtoto"



madam jane akabak kimya alichoka mtoto wa watu ukawa sasa wasaa wa hakimu kutoa hukumu!



"kwa kuwa umeidanganya mahakama ukaiba mtoto kwa nzia sasa unanyang'anywa mtoto isack atarudi kwa ba 

mdogo wake nawe utaenda jela miaka saba au faini ya shilingi milioni kumi au kifungo cha miaka saba!



madam jane akajitolea kulipa faini benki alikuwa na hizo ela! akaongozana na baadhi ya maaskar kuelekea 

benk!



huku nyuma isack alitaka kumkimbilia madam akamuombe msamaha,Zidu akadamdaka

"unataka kuaribu siyo wakat tumemalza vizur kwa sasa tunaenda kwenye gari langu tunaelekea nyumbani kwa 

madam ntaenda kukuacha hapo sawa?!"

Isack Akatingisha Kichwa Ishara Ya Kukubali Wakaelekea Kwenye Gari!



Kama Zidu Alivyosema Ni Kweli Walielekea Nyumbani Kwa Madam Ila Moyon Mwa Zidu Alikuwa Na Nia Nyingine 

Na Madam Yule!

Isack Akamuelekezea Mahali Wanapoifadhigi Ufunguo Wakafungua Na Kuingia ndani Zidu likajikaribisha 

sebuleni kama lenyeji vile!



Madam jane Akuwa Vizur Kiakili Kila Alipopita Mtahani Alizomewa Vijana Walimkashifu Madam Akazid 

Sononeka,

Hatimaye Akafika Katika Jumba Lake Bado Kichwan Alikuwa Na Mawazo Ni Jinsi Gani Angewez Msaidia Mtoto 

Yule Na Alitaman Hata Kuonana Naye Ajue Alipatwa Na Shinikizo Gan Kumgeuka!



Alishtuka Kukuta Geti Liko Wazi Akashuka Akaenda Fungua Lote Akaenda Ingiza Gari Akafungua Mlango Wa 

Ndani Na Kuingia Huku Akijiuliza Ni Nan Aliyomo ndani?!



macho yalimtoka pima,akabaki kaganda!...



"we mwanaharamu umefata nin hapa kwangu?!"



Zidu Alishtushwa na sauti kali ya madam jane Zidu Akageuza Shingo Kumwangalia Atoaye Sauti!



Akaachia Cheko Lake Lile Baya



"nimefata Roho Yako Madam!"



Zidu akajibu kwa sauti ya upole akinyanyuka pale kwenye kochi aikujulikana ni sangapi alichomoa kisu

akawa akimsogelea madam



"niue! niue! kwa nin unachelewa?"



madam jane aliongea kwa uchungu huku akizidi msogelea Zidu Isack Akamkimbilia Zidu Na Kumshika Mguu 

Akimuomba Asimuulie Mama Yake ,Zidu Akajirusha Sambamba kuachia teke isack akaenda kule



akapiga hatua moja ya pili akamfikia madam,ghafla yowe likasikika

tayari Zidu Alishafanya yake!



mwili wa madam jane ulilala

katika dimbwi la damu! pasina uhai

zidu alifanikisha kumuua madam jane kikatil sana!



isack alidondoka chini akapoteza fahamu! pind Zidu Alipo Mchoma Tu Madam Jane Kisu



'madam Jane Kwisha Kazi Yako Bado Wewe Mtoto'



Zidu Aliwaza Akiuangalia Mwili Wa Madam Jane Kwa Dharau Pale Chini







Maisha yamejaa changamoto, mengi makubwa kijana huyu anapishana nayo ananusurika mara kadhaa 

kifo,anapata mapigo ambayo hata ayaendani na umri wake,anampoteza madam jane tegemeo pekee lililokuwa 

limebakia katika maisha yake!



SEHEMU YA AROBAINI NA NNE



Habari ya kifo cha madam jane ilipamba kurasa za mbele za magazeti karibia yote vichwa vingi vya habari 

vikiwa vya kuzalilisha!



"MWALIMU ALOSHINDWA KESI YA KUIBA MTOTO AJICHOMA KISU KUKWEPA AIBU"



Gazeti moja hapo liliandika!



"AJIUA KWA KUJICHOMA KISU KUKWEPA AIBU"

Chini pakaandikwa kwa maandishi madogo "ni yule mwalimu mwizi wa mtoto!,



lingine likaandika MWILI WA MWALIMU ALOIBA MTOTO WAKUTWA NYUMBANI KWAKE UMEOZA



hakuna alochunguza tukio lile!,wala akuna aliyedhani wala kuhisi kuwa madam jane aliuwawa!



mpango wa mazishi ukisimamiwa na ndugu zake ukafanyika hatimaye siku ya siku mwili wa madam jane 

ukafukiwa!



alikuwa ni mwanamke shujaa aliyekufa akipigania maisha ya mtoto mdogo isack!



Baada ya Zidu Kufanikiwa Kumwangamiza Madam Jane Akutaka Kupoteza Muda Mule Ndani,akambeba Isack Asiye 

Na Ufahamu Mpaka Parking Akamwingiza Ndani Ya Gari Na Kuliondoa Gari Kwa Spidi!



Siku Mbili Zilipita Pasina Madam Jane Kuonekana Shuleni Siku Ya Tatu mwalimu mwenzake alotambulika kwa 

jina la mwalimu Selina Aliamua Kwenda Kumtembelea Nyumbani Kwake Kusudi Ajue Kunani Alipofika 

Alishtushwa Na Harufu Kali



Alipozidi Kuingia Ndan Korido Ya Sebule Alikuta Kama Manyunyu Ya Damu Alipotupa Macho Yake Sebulen 

Alipatwa Na Mshtuko Baada Ya Kuuona Mwili Wa Madam Jane Haraka Sana Akaita Majirani! Sambamba Na Kupiga 

Simu Polisi! Kituo Cha Kati!



Kituo Cha Kati Katika Ofisi Aliyokuwa Akifanya Kazi Insp Nurdin Aliletwa Inspekta Mpya Huyu Aliitwa 

Inspekta Pusi!



Chanzo Cha Kupewa Jina Hili Ni Ulka Kipindi Mama Yake Alipokuwa Na Mimba Yake Alipenda Sana Paka 

Alomwita pusi!,



Kula alikula sahani moja na pusi wake, kulala wakati mumewe ambaye alikuwa ni polis akiwa kazin shift 

za usiku alilala na pusi wake kukaa alikaa naye yani mimba yake ilimpenda yule paka kupitiliza,ivyo 

alivyokuja kujifungua tu mtoto akapewa jina hilo "pusi"



pusi alikuwa na tabia za kipakapaka kweli hasa katika kuchunguza mambo alipomaliza four tu baba yake 

akamtupia ccp akasomea upolisi!



huyu ndo afande pusi,ambaye kipindi cha utawala ulopita aliwah mfatilia wazir akapewa uamisho na 

kutupwa ndani ya kijiji kile cha madongo kuinama!



utawala huu mpya pasina kumjua vizur mtu huyu wakimwona Nurdin Mbaya wanambadilisha Nurdin Anaenda Kule 

Pusi Anarejea Jijini,pasina kujua huyu ni mbaya zaidi hata ya yule...



Siku Ya Tatu Baada Ya Kuwasili Makao Makuu Pale Akiwa Ndani Ya Ofisi Ile Ile Pamoja Na Sajent Kiso Simu 

Iliita Kiso Akapokea!



Akapewa Taharifa Za Kukutwa Kwa Ule Mwili Wa Madam Jane!



Haraka Sana Kiso Na Pusi Wakaingia Ndani Ya Gari Wakati Wakiwa Njiani Ghafla Meseji Ikaingia Katika 

Simu Ya Sajenti Yule "aonekane Kajichoma Kisu Mwenyewe By Zidu" Kiso Akatabasamu Tayari Lile Lilikuwa 

Ni Dili La Ela,wakafika Eneo La Tukio Wakashuka Wakaanza Uchunguzi Kwa Kuvaa Gloves

Kabla Hata Awajaugusa Ule Mwili Ghafla waandishi wakatokea!



"kazungumze nao"



insp pusi akamnong'oneza kiso wakati yeye akiendelea kuvaa zile gloves kiso akujibu kitu akawasogelea 

wale waandishi



"mmegundua nin mpaka sasa?"



mwandishi mmoja akahoji



"yah marehemu kajichoma kisu kwa aibu"



Pusi Pale Alipochuchumaa Akashtuka Akageuka Kumwangalia Kiso!



Akuelewa Kwa Nin Kiso Alizungumza Vile Wakati Kwanza Ndo Alikuwa Akipima?



Na Hata Kipimo Chake Akikuonesha Alama Yoyote Ya Vidole Katika Kisu Kile Hii Ilileta Maana Madam 

Aliuwawa Na Muuaji Alitumia Kificha Vidole! Kivipi Kiso Aropoke?!



Akasimama Na Kwenda Mpaka Pale Waandishi Walipo



"samahanin Twawaomba mtoke nje watu wote uchunguzi bado unaendelea tutakuja kuwajuza kila kitu huko 

huko nje"



ndiyo jibu alowapa waandishi ambalo angetegemea kiso angewaambia hivo,waandish na watu wote wakatoka 

nje ndan wakabaki askari wale wawili



"kiso kwa nin umewajibu vile waandishi na unaona uchunguz ulikuwa ukiendelea!"



"no case niliamua"



Kiso akajibu kwa kiburi pasina kujua yule ni mkubwa wake! pusi akaja juu



"uliamua?!,utaamuaje na unajua hii ni kesi ya mauaji? umedanganya sasa yule kauwawa!"



"auwawe! ajiuwe shauri yake kafa kafa tu awezi rudi mambo ya kusema kauwawa na kujipa kaz za kuchunguza 

muuaji ni nani siyawezi askari tunakazi nyingi mjini...



ghafla askar wengine na madaktar wakaingia



"kwajina naitwa inspekta kikoti makao makuu ya jesh la polis kitengo cha mauaji kwanzia sasa kesi hii 

ipo chini yangu nikishirikiana na kiso waweza nambia ulipofikia ukanikabidhi kesi yangu"



Pusi akashusha pumzi ndefu mambo yalienda haraka sana damu ikaanza mchemka pua kumuuma ilihtaji 

ichunguze zaidi juu ya kesi ile! alipomtupia jicho kiso,kiso akamtupia tabasamu lenye kumnong'oneza 

yako wapi sasa?!



"nimegundua mtu huyu kauwawa na muuaji katumia gloves kuficha alama zake za vidole"



"nashkur unaweza kwenda ulichogundua kiishie hapahapa"



pusi akashtuka!



'kiishie hapa hapa kivipi?'



aaah akanyanyua mguu wake na kuondoka!



sasa madam alishazikwa na vyote vilisaulika!



ila si kwa insp huyu siku hii alikaa kwenye meza yake ndogo akishangazwa na vichwa vile vya habari vya 

magazeti yale! pua ikazidi kumtekenya!



'mtoto!...'



akataja jina hilo kimyakimya! huku akikumbuka yeye ndo alikuwa wa kwanza kukiona kisu na alijua yule 

madam akujiuwa iweje sasa magazeti yakazanie kajiua na yamzalilishe vile?!



'mh! hapana' akatingisha kichwa



"kuna siri gani kati ya ba mdogo,huyu dada marehemu na mh waziri?!"



akili ikazidi kujichanganya na kuzalisha maswali kibao!



'lazima nifatilie hili kuna siri nzito hapa katikati lazima niijue,'



akajikuta akizidi kujipa kazi



"anasema mtoto wazir na mke wake walikuwa wakimtesa,akaja chukuliwa na ba mdogo wake ambaye naye 

alipanga kumuua katikat ya pori akaokolewa na walinz wa msitu ambao nao wameuwawa kuna askar aliyekuwa 

akifatilia naye swala hili naye aliamishwa na apatikani ni nan huyo na kaamishiwa wap na kwanin 

aspatikane lazima naye atakuwa aliuwawa! nitaanzia wapi mimi?!'



insp yule alizidi waza kichwa sasa kilimuuma akajinyanyua na kuacha magazet yake pale akaelekea 

chumbani kwake kulala lakin hata ivyo akupata hata lepe la usingizi akaamka! na kwenda kuchukua priton 

akameza ndipo alipolala!



*****



Taratibu alifumbua macho yake,akapokelewa na ugiza totoro, kichwa kilikuwa kizito,akataka kunyoosha 

mikono akashindwa,miguu nako akashindwa,akagundua amefungwa!..,



akapekecha macho! hali ilikuwa ile ile akuona

ina maana amekuwa kipofu?!

ghafla taa zikawaka akahis kuburuzwa kwa kitu akaelekezea shingo yake kule aliposkia sauti akauona 

mlango taratibu ukifunguka

mtu akaingia!,mkononi kashika sahani ya chakula! akamkata zile kamba na kumpa chukula kile ale! pasina 

kumsemesha kitu taratibu akatoka!



kama dakika kumi baadaye alirejea! akafungua mlango na kuingia alishtuka kumkuta yule mtoto ajala kile 

chakula!



"we pumbavu mbona ujala icho chakula?!"



"sili kama utaki kunirudisha kwa baba yangu Nurdin Ntakufa Kwa Njaa Ila Sili"



"ha ha ha ha unataka kufa siyo huu sasa ndo mwisho wako bay bay toto..."



zidu akaongea kwa jeuri na kumkamata juu juu mpaka kwenye kisima cha mamba!



"nisameheee baba nakulaaa"



Safar hii Zidu akuwa na msamaha tena akamrushia hukooo



isack akadondokea ndan ya kisima chenye mamba wafugwao na zidu wakali na wenye uchu!



Naaam ISACK kisiman atapona kweli?!!



pusi naye aingia mchezon







Wengi Wa Wakombozi Wake Wamekufa,kwanzia Wazazi Wake Walichomwa Na Moto,madam Jane Akajitolea Kuishi 

Naye Naye Akachomwa Kisu Ikisemekana Eti Alimwiba Na Kajiua Kwa Aibu!...



Sasa Yupo Mkonon Mwa Jitu Lenye Roho Mbaya Zidu Katili Akiwa Ana Nia Dhabiti Ya Kumgeuza Chakula Cha 

Mamba Wake Kamnyanyua Juu Na Kumtupia Kisimani Je Nin Kiliendelea?...



Safari Bado Ndefu Ila Tuendelee Na Sehemu Inayofatia



SEHEMU YA AROBAINI NA TANO!



TURUDI NYUMA KIDOGO!



Zidu lilikuwa Jitu Lisiloua Kibudu Au Mtu Alopoteza Fahamu Yeye Alipenda Kuua Mtu Akiwa Macho,ivyo 

Baada Ya Kutoka Na Mtoto Yule Nyumbani Kwa Madam Jane Akamuweka ndani ya chumba chake kile chenye 

mamba!,



Uchu wa kuua ulimtawala!



Zidu Alikuwa Na Roho Mbaya,roho Chafu Alitaman Tu Isack Aamke Amuue Bas Roho Yake Iridhike!



Kwel Baada Ya masaa kadhaa akatamani kumuona dogo yule akawasha laptop yake ilounganishwa na kamera 

iliyokuwepo mule chumbani iloonesha Giza tu chumbani mule si palikuwa Giza akawasha swichi ilokuwa 

pembeni yake ilounganishwa mpaka katika chumba kile



Kwa bahati mbaya ndo muda huo huo Isack alikuwa kazinduka ivyo Zidu alimuona akiwa macho



Akanyanyuka Na Kuelekea Chumbani Mule akamfungua Zile Kamba Akatoka Pasina Kuongea Naye!



"sijaua Siku Nyingi Kwa Sumu Wacha Nikaue Kwa Hii Sumu Ya Pilipili"



Akachukua Unga Ule Wa Pilipili Ambayo Ilikuwa Ni Sumu Kali Akainyunyuzia Kwenye Nyama Akaziweka Kwenye 

Wali Na Kumpelekea Isack Mule ndani!,akamtupia nakurudi zake sebuleni! isack akachukua kile chakula ila 

kabla ajala akakumbuka!



"hivi kaka tarzan imekuwaje ukawa rafiki na wanyama?"



anakumbuka aliwah muuliza ivyo tazan kipindi kile kule porini kabla awajaja huku mjini



"ukarimu na kujipendekeza kwao,nawapa chakula,mfano simba nlikuwa nawawindia mpaka nkawa rafiki nao 

mchaw chakula ukimpa mnyama chakula bas anakuwa rafiki yako mkubwa!"



isack akatabasamu!



"najua ipo siku ili libaba litakuja kunitupia kwenye hiki kisima wacha nijenge nao urafiki hawa mamba 

wapo watatu hapa nyama zipo tano ntampa kila mmoja nyama yake! huu utakuwa ndo mwanzo wa urafiki 

wetu!,isack akawaza akanyanyuka na kukisogelea kile kisima akarusha nyama tatu kila mmoja akawa akila 

yake!



isack akawa akiwaangalia huku akiwachekea ghafla wakatulia isack akashtuka!



hapo akang'amua kile chakula kina sumu akakimwagilia mbali!



dakika tano baadaye Zidu akijua atakuta mfu akapiga hatua kurudi ndani alishtuka kuona yule mtoto 

kakimwaga kile chakula,alipo muuliza sababu isack akutaka kumwambia kuwa kina sumu akajifanya kuweka 

mgomo mpaka apelekwe kwa Ins Nurdin



Kwa Kuwa Zidu Alitaman Tu Mtoto Yule Afe Akamnyanyua Juu Juu Na Kumtupia Kisimani Pasina Kujua Mamba 

Wake Walishakufa sa nyingi!



aliposogelea kisima akuamin kile akionacho! mamba walikuwa wakielea elea pasina uhai!

mamba alowanunua kwa bei ghali sana!



"isack umeniulia mamba wangu?"



zidu akaongea kwa ukali akitafuta bastola ipo wapi!



******



Inspekta Pusi Asb Siku Ilofatia Aliamka Na Kuoga Akajiandaa Kuelekea Zake Kazini



Kabla Ajafikia Ofisini Alipitia Katika Restraunt moja iliyopo palepale katika kota za maaskar



katika restraunt ile katika kiti alichokaa ghafla alimuona Kiso!



Akashusha Tabasamu Akutegemea Kumuona Pale



Alikuwa Na Maswal Kadhaa Ya Kumuoji Akajinyanyua Na Kuelekea Pale Alipoketi Askari Yule



"habar Za Saizi Afande!"



Akaanza Salamu Kwa Kumpa Mkono



"salama Tu Nambie Za Tangia Majuzi"



Kiso Akajibu Akirudisha Tabasamu



"dah Salama Japo Moyo Unaniuma Sana!"



"moyo Una Kuuma Kwa Nin Tena?!"



"kwanza Embu Nambie Vipi Kuhusu Kesi Ya Yule Dada Mmefikia Wapi?"



"dada Yupi"



Kiso Akajibu Akianza Kuibadilisha Sura Yale



"haaaa Si Yule Mwalimu!"



Kiso Sasa Uso Ulikunjamana



Akakumbuka Pesa Aliyopokea Yeye Na Mwenzake inspekta kikoti Kutoka Kwa waziri wakiambiwa waache 

kufatilia ile kesi



"unaniuliza wewe kama nani hasa? na saiv sipo chini yako?"



Pusi Akashtuka,akutegemea Jibu Kama Lile Machale Yakamcheza!



"aaah Afande Kwan Kuna Ubaya Lakin Mimi Kujua?"



"ilo Alikuhusu Na Ikiwa Utajaribu Kufatilia Utaamishwa Mwisho Wa Dunia Kama Mwenzako Aliyekuwa Na 

Kimbelembele Kama Wewe Alipopelekwa Ukooo Madongo Kuinama Au Kupotezwa Kabisa Baybay"



Kiso Baada Ya Kumaliza Maelezo Yale Akaondoka Zake Akimwacha Inspekta Yule Katika Mshangao Ila 

Alishamfungulia Njia Pasina Mwenyewe Kujielewa Kama Kamfungulia!



'mh Makubwa Ina Maana Yule Alopelekwa Kule Nilipo Ndo

alikuwa akifatilia hii kesi?!

lazima nkaonane naye huyu ndo atanielezea kila kitu ngoja...'



akainuka kwenye kile kiti chake baada ya kumaliza kunywa chai akaelekea ofisini!



****



Koplo kiso alikuwa na furaha sana mkononi alikuwa na barua ya kupandishwa cheo toka ukoplo mpaka u 

inspekta sambamba na kwenda mafunzoni!



Akaishika Simu Yake Na Kumpigia Alofanikisha Kupata Nafas Ile



"nashkur Sana Mh Wazir Kwa Kunipigia Kifua Mpaka Kupata Nafas Hii"



"usijal Kijana Hiyo Yote Ni Kwa Msaada Ulonisaidia Ivyo Kaongeze Mafunzo Ukirudi Utakuwa Vizur Zaidi"



"bytharway Mkuu Kuna Mtu Nahis Anaweza Asiwe Mzur Ni Vyema kama mngemfyeka"



"nani tena huyo?"



"yule inspekta mlomleta badala ya Nurdin Anaonekana Kutaka Kuendelea Kufatilia Mauaji Ya Madam Jane 

Wakat Ulimstopisha"

"shabaaash Niachie Mimi Hiwo Kazi"

Hapo Hapo Akakata Simu!

Akampandia Hewani Zidu Tayari Kwa Kumpa Kazi Ile!



***



Zidu alikunja sura kwa hasira mkono wake ulitetemeka!



machoz ya isack japo yalimezwa na maji ila uso wa majonzi uliumbika katika uso wake!

kabla ajafyatua risas ghafla simu yake ikaita



ni mlio aliouheshimu!



akaweka mkono wenye silaha chini akatoa simu mfukoni akapokea



"nakuomba ofisini mara moja kuna kaz haraka sana achana na unachofanya ndani ya dakika 3 uwe 

umeshawasili"



"yes mkuu"



Zidu akaitika sambamba na kukata simu akashika silaha yake akamuelekezea isack kule chin ya kisima!



"paaa paaaa paaaaa paaaaaa"



milio kadhaa ya risasi ikasikika maji ndani ya kisima yakabadilika rangi!



kifuani kwa isack risas kadhaa zilikishambulia kifua chake



akayatoa macho kama vile anamshangaa izrael ambaye akupata kumuona toka amezaliwa ulim akaung'atia nje



alitisha hata kumwangalia



"ha ha ha ha ha kwisha kaz yako nkija ndo ntaenda kukutupa pumbav wewe"



Zidu Aliongea Kwa Furaha Akageuka Akafungua Mlango Na Kutoka!



Akaingia Ndan Ya Gari Lake Tayar Kuelekea Kwa Mh Wazir Alex



Duh Isack ndo Katuaga kwa kifo kibaya hivyo dah!



vipi kuhusu ins pusi atauweza mchezo Wa zidu?!



kisogo kapandishwa cheo kaenda mafunzon akija atakuwa na kazi gani



majibu ya swal hil na meng ujiulizayo endelea kufatilia riwaya hii inapoelekea kwenye kiini chake hasa!







Maisha ni songombwingo,maisha ni mtihani Isack Anajikuta Akifanya Mtihani Ambao Si Wa Kidato Chake! 

hilo linasababisha aingie katika mateso makal



yanayohatarisha maisha yake!



anakoswa koswa mara kadhaa kuuwawa na kijana mwenye uchu na roho yake huyu si mwingine ni Zid K'



Na Sasa Kamtupa Ndani Ya Kisima Cha Mamba Lengo Mamba Wamtafune Ila Pasina Kujua Nyama Alizowekewa 

Zinasumu Isack Anawapa Mamba Wale Kwa Lengo La Kuunga Nao Urafik Kama Alivyoambiwa Na Tartaz Tofaut Na 

Mategemeo Yake Mamba Wote Wanakufa,anamwaga Kile Chakula Zidu Kuingia Ndan Anakuta Dogo Kamwaga Chakula 

Chote Anamtupia Kisiman Kwa Hasira



pasina kujua mamba wake si wazima tena anapokuja kugundua hasira zinazidi mpanda na kumminia risas za 

kutosha isack,isack anatoa macho ulimi kaung'atia nje kama mfu je huu ndo mwisho wa isack? twende 

pamoja katika riwaya hii isiyoisha hamu katika usomaji



NA HII NI SEHEMU YA AROBAIN NA SITA



SIKU KADHAA NYUMA



NYUMBANI KWA INSPEKTA NURDIN



Sebuleni pale walikaa watu watatu kipindi icho madam jane alikuwa bado ajauwawa na Zidu,sebuleni Pale 

Alikwepo Ins Nurdin,isack Na Madam Jane!



Mezani Kulikuwa Na Ngoz Flan Ndo Kwanza Zilikuwa Zimeingia Nchini!



Ile Ngozi Kuna Jins Ulikuwa Ukiishonea Mwilini Ni Ulinz Tosha



ilikuwa na uwezo wa kuifadhi risasi bila kupenya katika ngoz ya ndani nayo ilikuwa na damu yake!



ule ulikuwa ni utaalamu wa mzungu!



"kesho ntamleta daktar lazima isack ushonelewe hiyo ngozi na ikiwa utatekwa ukipigwa risas yapaswa uekt 

umekufa ng'ata ulimi nje hivi!



isack akafanya kama vile alivyoelekezwa wote wakacheka haya ng'ata ulimi usifumbe macho usichezeshe 

icho kiini cheusi"

Wakazidi Kumpa Mafunzo Isack Jins Ya Kujifanya Mfu Wakafanikiwa!



Kesho Yake Dokta Yule Akaja Akamshonea Isack Ngoz Ile Ya Kuzuia Risasi!,



Na Siku Hii Ya Leo Isack Lile Zoez Ndipo Alipolifanya Baada Ya Zidu Kummiminia Risasi



kadhaa akayatoa macho pasina kuchezesha kiini,ulimi akaung'atia kama alivyofundishwa akamshughudia zidu 

likirudisha silaha kiunon na kutoka!



'dah sijapata kuona jitu lina roho mbaya kama hili kah'



Isack Akawaza Akistaajabu Roho Ya Kiumbe Kile 'zidu K' Izrael Wa Kibinadamu!



Baadaye Akasikia Muungurumo Wa Gari Nje Hakuwa Na Shaka Jamaa Lile Ndo Lilikuwa Likiondoka!



Akasubiria Dakika Tano Nyingine Zipite Kisha Akanawa Zile Damu Akajinyanyua Akasimama Juu Ya Mamba 

Mmoja Akashika Juu Akajivuta! Juu Ya Chumba



Akapiga Magoti Chini! Kumshukuru Mungu Wake



"asante Baba Kwa Kunipa Uhai Tena Naomba Usichoke Kunilinda Mungu Wangu Najua Sina Hatia Au Nimekukosea 

Mungu Wangu Mpaka Uruhusu Mateso Makal Namna Hii Najua Sijakukosea Baba Ndo Maana Bado Unanisimamia 

Amin"



Akainuka Pale Na Kuufata Mlango Kuufungua Mlango Ulifungwa Kwa Nje!



Isack Alichoka!



Je Angefanyaje Sasa,akabaki Kaduwaa Palepale Mlangoni Na Mara Akapata Wazo Ni Baada Ya Macho Yake 

Kuliona Dirisha Akatabasamu...



Akalikimbilia Dirisha Lile Na Kulifungua Ahmad Alichokiona Kikazidi Mkata Maini!



Dirisha Lile Lilikuwa Na Nondo Ndogondogo Ambazo Zilimzuia Kupita Kutoka Nje



Je Sasa Angetokaje?!



Sononeko,simanzi,huzuni,majonzi Vikamrudia!



Akakaa Chini



kama mzigo alijijua kwa Zidu Asingeweza Pona

Akabaki Tu Akisali Kumuomba Mungu Wake Amnusuru Katika Janga Lile!



***



Kwanza Alimuelezea Bosi Wake Jins Alivyomwekea Sumu Kwenye Chakula,akakimwaga Akamtupia Katika Kisima 

Cha Mamba Napo Kumbe Mamba Wake Wamekufa Mwisho Akamuulia Mulemule Ndani!



"yule Mtoto Nadhani Mizimu Ya Kwao Inamlinda Ila Siyo Ishu Kazi Nzur Kapona Mara Kibao Ila Hapo Ni Wazi 

Mwisho Wake Ulikuwa Umefika Sasa Ushaenda Kumtupa?!"



"hapana Bado Ndo Uliniita Mkuu"



"ok Huyu Usimtupe Porin Wala Wapi Yapaswa Ukamtupie Katika Kisima Chako Cha Gesi Ayeyuke Tena Nami 

Ntakwepo Kuhakiki Katutesa Sana isee"



mh alex akaongea kwa furaha



"kwel mkuu hakuna kaz iloniumiza kama hii aisee na jasho imentoa! ila nashkur nimeimaliza"



"ok! nice now kabla atujafanya ivyo kuna afande nataka umuondoshe duniani ni kimbelembele nimemtoa bush 

nikajua ni mshamba atofatilia maswala yangu imekuwa tofauti ananfatilia kes kaambiwa aache fatilia bado 

anafatilia ua zidu kes mi ntajibu"



"anaish wap huyo mtu!"



"palepale alipokuwa akiishi Nurdin"



"sawa Mkuu Esabia Hiyo Kaz Imekwisha kamilika"



"kwa Saiv Nakuaminia Jembe Langu"



Zidu Akaachia Tabasamu



"sasa Kumbe Kaz Yenyew Ya Usiku Now Twende Tukakateketeze Kale Ka Mfu Kule Nyumbani mkuu nikikafkiria 

napatwa kichefchef



"kijana wangu hiyo kaz ya kesho kwa saiv bak hapa kazin jion ukafanye hiyo kaz"



Zidu Hakuwa Mbishi Akaendelea Na Kazi Usiku Ule Akaelekea Mpaka Nyumbani Kwa Insp Pusi Kwanza 

Alishangaa Kukuta Mlango Umefungwa



'pengine Atakuwa Lindo'



Akawaza Akaamua Kujibwaga Kochini Kumsubiri!

Masaa Yakakata,hatimaye Akapitiwa Na Usingizi!

Alipokuja Shtuka Kumepambazuka!



'ina Maana Huyu Mfu Akulala Nyumban Jana?'



Akawaza Akijiinua Kochini Akajinyoosha Kidogo Akakaguwa Vyumba Viwili Vitatu Kujiakikishia Mtu Huyo 

Ayupo!



Akampigia Simu Bosi Wake Mh Alex Kumjulisha



"basi We Njoo Tukakazike kale katoto huku naongea na mkubwa wake nijue jana alifanya wapi kazi"



"sawa mheshimiwa"



Zidu Akakata Simu!



Mheshimiwa Alex Akampigia Simu Mkuu Wa Kituo Alichokuwa Akifanya Kazi Insp Pusi



"jana Kijana Wako Pusi Ulimpangia Kaz Wapi?"



"si Popote Mheshimiwa Alikuwa Ofisini"



"amkumpa Lindo La Usiku"



"hapana Muheshimiwa Yey Alikaa Ofisini Mpaka Saa 12 Akatoka Kuelekea Kwake Kwani Kuna Nin Mheshimiwa?"



"amna Kitu! Je Saivi Kashaingia Ofisini?"



"naona Ndo Huyo Anaingia Na Gari Mkuu"



"ok Poa Usimuulize Kitu Chochote"



"sawa Mkuu!"



Mh Alex Akakata Simu



"jana Kapona Alikuwa Kaenda Kulala Kwa Malaya Wake Ila leo utopona afande'



mh wazir alex aliwaza akiwa tayari kashapata jibu la kumpa kijana ake Zidu



Alimsubiria Kwa Hamu!



Jana Yake Baada Ya Insp Pusi Kutoka Pale Ristraunt Alipopewa Onyo Na Ins Mpya Kiso Akuweza Hata Kufanya 

Kaz Hamu Kubwa Kuonana Na Nurdin Ajue Hasa Kisa Cha Yule Mtoto Madam Jane Na Yeye Kuamishwa Na 

Kutokuudhuria Kesi Ya Madam



Saa Kumi Na Mbili Jion Baada Ya Kutoka Kituoni Akapanda Gari Yake Moja Kwa Moja Madongo Kuinama



Saa Tatu Usiku Alikuwa Ndani Ya Kijiji Kile Akuangaika Kuelekea Kituon Yeye Alielekea Nyumban Kwan 

Alipajua Si Ndo Alipokuwa Akiishi Akabisha Hodi Nurdin Akamfungulia



"naitwa insp pusi ndiyo ins ninayesimamia kesi ya kifo cha madam jane...



Nurdin Alishtuka...



"jane Kafariki?!"akauliza Pasina Kuamini



"yah Madam Jane Anasiku Ya Tano Alikutwa Nyumbani Kwake Kachomwa Kisu Na Mimi Ni Askar Wa Kwanza 

Kushughudia Mwili Wake Katika Uchunguz Wangu Wa Awal Niligundua Kachomwa Ila Baaday Waliwasil Maaskar 

Wengine Wakanambia Niache Kufatilia Kesi Ile Kilichonshangaza Habar Walizotoa Askar Ni Kwamba Jane 

Kajiua Kukwepa Aibu Ya Kuiba Mtoto"



Ins Nurdin Akazidi Kushtuka Habar Zile Zote Hakuwa Nazo Kule Palikuwa Ni Madongo Kuinama Kweli!



"kwa Hiyo Umenifata Mimi Ili Nikusaidie Nini



akiwa kachoka roho na akili insp Nur Akauliza Chuk Zake Akiziamishia Kwa Yule Askar Mwenzake Pale Mbele 

Yake!,aliona Waz Alitaka Mrejesha Kuonana Na Zidu Wakati Akutaka Ilo Litokee



"naomba Nieleze Unachojua Juu Ya Huyo Mtoto Isack,madam Jane Na Huyo Ba Mdogo Wake"



"sijui Chochote Nakuomba Uondoke Kwangu!"



Nurdin Akajibu Kwa Hasira!



Pusi Aliomba Na Kuomba Nurdin Mwisho Akaelekea Kulala,pusi Yeye Alilala Palepale Sebulen Asubuh 

Akajitahid Sana Kuomba Ila Nur Yey Alichomwambia Achana Na Hiyo Kesi Kama Unapenda Kuendelea Kuishi'

Maneno Hayo Yakazidi Mpa Ujasir Inspekta Yule Pasina Kumtambua Vizur Zidu! Katu



akujua usiku ule tayar oda ya kuuwawa yeye ilishatoka na mwanaume alikuwa ndani ya nyumba yake 

akimsubiri



AKANUSURIKA



saa kumi na mbil akaanza safar ya kurudi mjin pasina kuambiwa lolote hatimaye saa mbili alikuwa nje ya 

makao makuu ya jeshi la polisi! wakat huo mkuu wake wa kituo kile akimpa taharifa mheshimiwa kuwasil 

kwake kama tulivyo ona hapo nyuma



Ndan Ya Gari Yao Vicheko Vilitawala Ndo Walikuwa Wakielekea Nyumban Kwa Zidu Kumzika Mtoto Isack Ndan 

Ya Gar Walikuwa Wawili Tu Hata Dereva Awakumuitaj Safar Iliishia Katika Jumba La Zidu Katili Wakapaki 

Gari Na Kushuka



Isack Bado Alikuwa Nyuma Ya Mlango ghafla akaskia muungurumo wa gari kwa spidi akanyanyuka pale na 

kurudi zake kisimani



akaung'ata ulimi kama awali mlango ukafunguliwa Zidu Na Alex Wakaingia



"ingia Haraka Sana Ukamtoe"



Zidu Akaruka Kisiman Wakamtoa Isack Akamuweka Began Wakatoka Naye Na Kuingia Naye Katika Chumba Kingine



Hiki Kilikuwa Na Kisima Cha Ges Lau Angetupiwa Katika Kisima Kile Cha Tindikal Gesi Kali



Angeyeyushwa Hata Mfupa Wake Usingeonekana!



"Shika Mfuniko Hiv"



Mh Alex Akaushika,Zidu sasa akawa akimshusha isack taratibu chini ili sasa amdondoshee kisimani



akaanza sasa kumsukumia mtoto adondokee kisiman sasa ulibak msukumo mmoja isack kudondokea chini!...



"msukume sasa"



mh alex akaongea huku naye akiuvuta mguu wake kumsukumia mtoto yule



kisanga!!!...





Furaha Zinatawala Kwenye Mioyo Yao Thamira Ya Kuua Wakiona Imekamilika Wanajua Fika Washamuua Isack Na 

Sasa Ili Kufuta Ushahidi Ni Kumtupia Isack Kwenye Kisima Cha Gesi Huko Atayeyuka Hata Mfupa Auto 

Onekana



Je Nin Kiliendelea?!,ungana Na Muandishi Akujuze Kilichoendelea!



Kabla Zidu K Ajamsukumia Isack Kwenye Kile Kisima Ghafla Simu Ya Mzee Alex Ikaita,ikamlazimu Alex 

Aachie Mfuniko Ule Ulokuwa Mzito Ukaibana Miguu Ya Isack Ambapo Tayari Ilikuwa Kisiman Akakunja Sura!



Lau Kama Wangemuangalia Usoni Wangepata Kugundua Mtoto Yule Yuko Hai,ilimlazimu Avumilie Maumivu Yale 

Kwan Kulia Kungesababisha Agunduliwe yu hai auwawe!,nafsi yake nayo bado ilitaman kuishi



ndiyo!,



"ehe nambie muheshimiwa,..sawa sawa usijali mheshimiwa,yah yupo ndo tulikuwa tunamteketeza mida 

hii...sawa sawa muheshimiwa ni wewe tu,bloch d mianzin mkuu,yah kwa zidu! ok mkuu"



Baada Ya Maongezi Yale Mh Alex Akakata Simu Muda Wote Zidu Tu Alikuwa Akimtazama



"aina Aja Ya Kumteketeza Hiyo Maiti Imeshakuwa Dili Iweke Kwenye Kiroba Inakuja Chukuliwa Saiv 

Mheshimiwa Anaihtaji"



"mheshimiwa?! Mheshimiwa Yupi Na Anaitaji Maiti Hii Kwa Kaz Gani?"



Mh Alex Akakunja Sura!


ITAENDELEA

imulizi : Kiapo (Agano La Damu) (2) 

Sehemu Ya Nne (4)



"toka Lini Zidu Ukawa Na Jeuri Ya Kuniuliza Maswal Mimi?"



Mr Alex Akaja Juu! mr Zidu akanywea



"mkuu kwani kuna ubaya mi kujua!?"



"si lazima ujue kila kitu zidu we fanya kama nilivyokuelekez"



Basi Zidu Akutaka Kubisha Akatafuta Saflex Na Kumwingiza Isack Ndan Ya Saflet Ile Akaifunga Kwa Juu!



Baada Ya Dakika Kama Kumi Hivi Simu Ya Mr Alex Ikaita Tena Akapokea Na Kuitika Sawa Mkuu! Huyo Mkuu Ni 

Nan Asa? Ni Rais Wa Nchi Au? Zidu Akulijua Ilo



"kafungue Geti Kashafika"



Mh Alex Akatoa Amri



"nani Mkuu?!"



"sioni Aja Ya Kuuliza Uliza Maswali Badala Ya Kutekeleza Kile Ninachokwambia"



Zidu Akujibu Kitu Akaenda Fungua Mlango Gari Jeusi La Kifahari Likaingia!,lilikuwa Na Vioo Vya Tinted 

likajifunga!



gari ile taratibu ikaanza kuondoka isack akiwemo ndani yake!



"kwa sasa sahau kuhusu maiti hiyo kinachofuata akikisha yule mtu leo unamalizana naye!"



"mtu gani?!"



"ooh common Zidu Aupo Sawa?"



"im Ok Bosy Nshakuelewa Kila Kitu Kitakamilika"



"ok Mi Naenda Kaz Njema!"

Mr Alex Akalifata Gari Lake Akalipakia Na Kuondoka Zake



Huku Nyuma Zidu Akajipeleka Sebulen Kwake Akaelekea Kwenye Friji Na Kuchukua Pombe Kali Na Glasi 

Alijikuta Raha Tu Ikimtoweka!



Akagwida Ile Pombe Akili Ikae Sawa Maana Ilikataa Kabisa!



baada Ya Hapo Akaelekea Chumbani Na Kujitupa!



Jioni Ya Siku Hiyo Ndo Aliadhimia Kummaliza pusi!



Gari ile nyeusi ilisimama nje ya jengo moja la kifahari,

boneti ya nyuma ikafunguka akashuka mtu mmoja mwenye asili ya kizungu akaenda kukitoa kile kiroba 

akaingia nacho ndani ya jengo lile!



Baadaye Akarejea Na Kuingia Ndani Ya Gari Yake Ile! Boneti Ikajifunga Gari Ikaondoka!



Ni Nani Mtu Yule?!



Akuna Alokuwa Na Jibu Sahihi Ya Swali Hili



****



SURA YA KUMI NA TATU



MOTEL HOTEL



Ni ndani ya hotel ile Zidu Alijikelisha Bado Akili Yake Aikuwa Sawa! Aliamua Aende Katika Hotel Ile 

Akapumbaze Akili Kwa Kutazama Viuno Vya Wadada Wakikatika Na Ustad Wa Uimbaji Band! Akivuta Muda Usiku 

Akakamilishe kazi Yake Ya Kumfyeka Pusi!



"kaka Una Mtu Hapa?"



Akashtushwa Na Sauti Nyororo Ilomlazimisha Atoe Macho Kwenye Jukwaa Na Kumtazama Malaika Alosimama 

Mbele Yake!



Alikuwa Ni Mwanamke Mrembo,katika Warembo Ambao Zidu Aliwai Kukutana Nao Binti Yule Alikuwa Mmoja Wapo

Lakini Urembo Ule Aukumsukuma Zidu Kukubali Kukaa Na Binti Yule!



"yah Kuna Mtu Namsubiri"



Akajibu Kwa Mkato Binti Yule Taratibu Akajiondokea Na Kumpa Wasaa Zidu Aendelee Kugwida Kinywaji!



Ghafla Macho Yake Yakavutika Kuwa Angalia Wapenzi Wawili Kwenye Meza Moja!



Akuamini Kile Alichokiona!



'yule Si Mke Wa Mheshimiwa?'

Akajiwazia akajihisi yu ndotoni



akapikicha macho yake!,ile aikuwa ndoto,alichofanya akawapiga picha na kumtumia mh waziri



muda huo mh waziri alikuwa katika kikao ilikuwa ni mida ya saa kumi na mbil hiv jion ghafla simu yake 

ikaita akaomba radhi akaitoa kuicheki! akaikata na kuirudisha mfukoni! akaendelea na kikao!



ghafla ikaita tena,ikiwa na maana simu ile ilikuwa na umuhimu akaomba radhi akatoka kando kuongea na 

simu ile!



"nilikwambia nikikukatia simu Zidu Nipo Kwenye Kikao"



"najua Muheshimiwa Ila Dharura Ni Kwamba Nilazima Nikwambie Saiv Utoe Maamuz Ntekeleze Muda Huu Huu"



"upaswi Kupewa Maamuz Zidu Kama Umepata Nafas Ya Uyo Paka sijui nyau,pusi ua"



"siyo ivyo mkuu naomba washa data kuna picha nimekutumia whatsupp"



"kitu gani tena kijana wangu"



"usiwe na presha mzee we washa data then npe mchongo ok!"



Mr Alex Akujibu Kitu Akakata Simu Yake Ile!



Akawasha Data Na Meseji Za Whatsupp Zikaanza Kuingia

Simu Yake 'automatic' Picha Zilijidanload



Macho Akayatoa Pima,mshangao Ukamvaa Pasina Kuamini Kile Akionacho



"ney Mke Wang?!" Akajikuta Kaita Kwa Ukali Ghadhabu Zikampanda Akajikuta Akimpigia Simu Mke Wake!



Wakati Huo Bi Ney Bado Alikuwa Akiendelea Kujirusha Na Mwalimu Gibson Katu Awakumtilia Shaka Jiran 

Yao,Zidu sasa alijisogeza karibu yao na kuendelea kuwafatilia,ghafla simu ya bi ney ikaita!



"mume wangu huyo anapiga ngoja nikamsikilize hubby"



mwalimu gibson akamruhusu bi Ney Akajinyanyua Na Kuelekea Chooni Akapokea Simu Ile!



"nambie Mume Wangu?"



"uko Wapi Saiv?!"



Bi Ney Akashtuka!



"nipo Nyumbani Mume Wangu Kwani Kuna Nini?"



"una Uhakika Upo Nyumbani?!"



"ndiyo Mume Wangu Au Uniamin?"



"mpe Simu Mery Niongee Naye"



Mzee Alex Aliongea Maksudi Kumtega Mkewe



"yupo Mbali Kidogo Mume Wangu Ngoja Nimuite Mery?"



Akajifanya Kuita Kisha Palepale Akakata Simu Mwili Wote Ulimloa Jasho...



'atakuwa kashanigundua nin? embu ngoja!'



akawaza na palepale akampigia mwanaye mery ambaye alishajua lugha ya kiswahili na alishapoteza 

kumbukumbu akukumbuka vyote vya nyuma akumkumbuka

isack,wala akujua kama kuna binadam kama huyo mama yake akampanga! nakuunga na baba yako ongea naye 

ajue tupo wote nyumbani sawa?"



"sawa mama"



"aya uskate simu"



palepale akampigia mume wake!



"huyu hapa mume wangu haya ongea naye mery chukua simu baba yako anataka kuongea na wewe"



kule nyumbani Mery Kwa Kuwa Mama Yake Alishampanga Akajifanya Kupokea Simu



"shikamoo Baba"



Mh Alex Akaduwaa Akuelewa Mchezo Alochezewa



"marhaba Mwanangu ujambo?"



"sijambo baba"



"uko na mama yako hapo nyumbani eeh"



"ndiyo baba"



"basi nltaka nkujulie hali mwanangu bayii"



mr alex akakata simu katika line ile sasa wakabakia wawil mtu na mama yake wote wakaangua kicheko!



"nawe umezidi mama kutoka bila kuaga"



"mmmh mwanangu umensaidia ndo unansema?"



"siyo ivyo mama kiukwel umezid"



bi ney akaona atasemwa sana na mwanaye akakata simu



akiona ameshinda akarudi pale alipokaa mwalimu gibson



"duniani wawil wawil huyo si mke wangu mke wangu nimeongea nay nyumban na nimwemwambia anipe watoto 

wote nimeongea nao mfanyakaz,mery,agnes utanambiaje yey ndo anachepuk



mh Alex akaja Juu Zidu Akashtuka!



"bosi Mi Namjua Fika Shem Na Mida Hii Alitoka Ndo Nahs Alikuwa Akiongea Na Wewe Ayupo Nyumbani Huyo!"



"tusibishane Zidu Fanya Kazi Nilokupa Huyo Pacha Wa Mke Wangu Achana Nao!"



"si Pacha Bosi Ni Mke Wako Haaa"



"kama Ni Mke Wangu Basi Ua!"

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog