Simulizi : Kiapo (Agano La Damu) (3)
Sehemu Ya Tano (5)
juu uliitwa upande wa dhahabu chini uliitwa upande wa silvar,
ilikuwa ni mbali kidogo na zilipo kambi yao
ivyo wapambanaji mida ya jion jumapil hiyo tayar walikuwa katika kambi zao zile za muda wa kijiandaa kwa dhana za kivita,wakisubiria saa sita kamil waanze pambana!
muda ausimami huwa unaenda,ndivyo ilivyokuwa hatimaye saa tano na nusu ikawadia!
wale walokwepo upande wa dhahabu wakawaambia wenzao kwa nin wasingewavamia silvar kabla ya muda wakawa angamiza na kuwateketeza kwa kuwa wenyewe muda huo watakuwa ndo wakijiandaa!
wakakubaliana,wakaianza safari,wakiwa bado njiani ghafla wakakutana na mwili wa mwanajeshi alovaa sare ya jeshi lao,mwanajeshi yule wala akuwa na kichwa alipasuliwa tumbo na kutolewa vyote vilivyopo ndani!
yalikuwa ni mauaji ya kutisha,awakuwa na shaka mtu yule ametoka upande wa Silvar,wakaachana Na Ule Mwili Wakazid Kusonga Mbele Yao Wakakutana Tena Na Miili Mingine Mitatu Ikiwa Imekufa Vifo Vile Vile,mbele Tena Wakakutana Na Wawili!
Je Ni Nani Aliyekuwa Akisababisha Mauaji Yale?,tena Akitoka Na Vichwa?,na Kula Mautumbo!,hali Ya Sintofahamu Ikazuka Kati Yao,mpaka wanafika kambini Silvar Watu Wote Kumi Walishakufa!...
"sasa Tufanyaje Tuwajulishe Wakuu?!"
"hapana Tutakosa Sifa,hawa Watakuwa Wamekufa Kwa Uzembe Wao Kikubwa Sisi Tujifanye Ndo Tumewaua,
Wakakubaliana,wakaikusanya Miili Yote,wakarudi Kambini Kwao Wakiwa Wanashangilia!
Kikaingia Kikosi Cha Jumanne,nacho Hivyo Hivyo,nawo Wakafanya Siri Upande Wa Silva Wakaliwa Kikaingia Kikosi Cha Jumatano Vivyo Hivyo Alhamisi,na Ijumaa!
Watu Wa Nne Wale Wakiongozwa Na Stanley Kwa Bahati Mbaya Au Nzuri Wote Walipangwa Upande Wa Dhahabu Ivyo Wote Walisalimika,na Ilibaki Ni Siri Yao Hakuna Alodiriki Kufungua
Mdomo wake na kuwaambia wenzake kuwa wenyewe awakupigana vita bali waliwakuta wa kambi ya Silvar Tayari Walishauwawa!...
Wote Walifanya Siri Mioyon Mwao!
"sisi Sote Hapa Tumekuwa Upande Wa Dhahabu Na Mara Zote Upande Wetu Huwa Ndo Unaoshinda...
Na Kesho Pia Jumapil Twaitaji Upande Wetu Huu Ushinde,na Kwa Bahati Nzur Zaidi Isack Hadui Yetu Yupo Upande Wa Silvar Kipi Sasa Kifanyike Sote Sis Watano Tutatoroka Na Kwenda Kuungana Na Kikosi Cha Dhahabu Kuakikisha Tunawaua Wote Wana Silvar!
Nimeshawapanga Wanaoenda Pambana Leo Wamekubali Tuwasaidie Kwa Siri Tuko Pamoja?!
Wote Wakakubaliana,pasina Kujua Ni Kitu gani kilichokuwa kikiua watu walokwepo katika hema au upande wa silvar!
usiku wakaungana kuelekea upande wa dhahabu wakawa kumi na tano huku Silvar Wakiwa Kumi!...
Silvar Wakiongozwa Na Isack Maskin Awakujua Ule Upande Walokuwepo Wao Ulikuwa Ni Upande Mbaya!,watu Walikufa Kimaajabu!
Ilikuwa Ni Tayari Sa Tatu Usiku Yakibakia Masaa Matatu Kabla Ya Kuanza Vita Wote Walikuwa Ndani Ya Hema Lao Wakipanga Njia Za Kupambana Na Jeshi La Dhahabu,
"duh Yani Vikosi Vyote Tisa Walosimamia Upande Huu Wameuwawa!,sisi Lazima Tuikomboe Silvar!..."
Isack Aliongea Kwa Unyonge Akijua Upande Wa Dhahabu Ndio Waliowaua Silvar,kumbe kuna siri nyuma ya pazia!,na silvar awakuuwawa kwa risasi!
mitaa kadhaa pembeni kidogo tu ya hema lile kulikuwa na pango kubwa!...
aikujulikana ndani ya pango lile waliishi viumbe gani!
vijana watatu wa silvar walitoka kule ndani ya hema wakazunguka nyuma ya hema lile nikama walikuwa wakitafuta kitu!
ghafla macho yao yakawatoka,ni baada ya kumuona binti mrembo,mrembo kupitiliza tena wa kiafrika!
pasina kujiuliza huyu binti kafata nin huku wakajikuta wanamfata binti akawa akiwaangalia kwa pozi huku akitembea kwa mwendo wa madoido kulifata pango lile akazama ndani!
nao walipofika pasina hata kujali nao wakazama ndani ya pango walichokikuta ndicho walichokikuta wenzao walioangamizwa kama wao!
ni mayowe tu yalosikika,mayowe yale yakawashtua walokuwa ndani wakijua tayari washavamiwa kina isack hao wakakurupuka na kubeba silaha zao mabomu wakatoka!
ila walichokutana nacho walipiga breki wakageuka na kuanza kukimbia!,kama walivyofanya wenzao!
nyuma lilionekana dubwasha la ajabu lilikuwa kama ng'ombe ila siyo yeye!,
Macho yake ya njano,mdomoni liliweza tema moto!,ila kwa pale alikutaka kuutumia,likawa likikimbia kwa kishindo,na alipomkamata alokuwa mbele yake alifunua domo lake kubwa na kumla kichwa kisha kumpasua na kula vyote vya tumboni sambamba na kunyonya damu kisha kuendelea kuwakimbiza!,muda mwingine lilitoweka lilipokuja kuibuka lilimuibukia wa mbele na kumdondosha kisha kumgeuza kitoweo,dubwasha lilitisha
Isack aliendelea kukimbia Kuja Kugeuka Nyuma,alikuwa Peke Yake Wenzake Walishauwawa Na Dubwasha Lile Lilikuwa Likimjia Kwa Kasi!
Ni Katikati Ya Pori Na Ni Usiku Wenye Kiza Kikuu!
ghaIfla alikuja kupigwa ile ya kusukumwa akaenda kudondoka kule!,dubwasha sasa likimjia kwa kasi huku limefungua domo lake kunyofoa kichwa cha isack
mguu wa kulia wa mbele akiwa kaunyanyua juu makucha yake yalikuwa yakikua,tayari kwa kurarua,tena Yule Ndo Alimtamani Zaidi!!...
Hii aikuwa ndoto wala si ndoto kama ndugu msomaji utakavyodhani
************* HAPO BAADAE ************
Hali Ya Mkanganyiko,kutoelewa Kinachoendelea Inazuka,watu Wasojulikana Wanamteka Isack,wanampeleka Kusikojulikana Na Kumlazimisha Aeleze Mahali Alipo Zidu,wakitaja majina yao halisi,jambo hilo linazidi kumshangaza Isack Anatambua Kashagundulika Je Nini Kiliendelea?!...
Songa Nayo Uendelee Kuburudika
Isack Alijua Sasa Mwisho Wao Umefika Ila Kwanin Watu Wale Walificha Sura Zao!
Hili Lilikuwa Ni Swali Gumu Ambalo Akulipatia Majibu!...
Akarudisha Kumbukumbu Hapo Awali Alipokuwa Katika Jumba Lake Usiku Akiwa Amelala,akahisi Kufunguliwa Kwa Mlango Na Watu Wale 4 Wakaingia Alijaribu Kupambana nao ila walimshinda na hatimaye alichomwa na kitu kama sindano!
Taratibu Akaanza Kuishiwa Pigo Moja Likampotezesha Fahamu Na Ndilo Lililo Mpeleka Pale Alipo!...
Akataka Kunyanyuka Akashindwa Ghafla Akasikia Mkwaruzo Wa Kufunguliwa Mlango Macho Yake Yakanata Mlangon Kumtazama Ajaye,mlango Ukafunguliwa Wakaingia Vijana Wawili Wakiwa Wamevaa Vilevile Kininja Mkononi Walishika Kioo Kikubwa Kama Kile Kiwekwacho Saluni!
Bado Isack Akujua Dhumuni Lao Ni Nin Hasa!...
Wakakiweka Mbele Yake,kisha Wakiwa Wametabasamu Wakakigeuza Sasa Isack Ajitazame!
Isack Alishtuka!...
Ni Baada Ya Kuiona Sura Yake Halisi,tofauti Na Ile Ya Bandia alovikwa na dokta silvestar loyer nchini marekani,kabla ya kuja Tanzania!...
"nadhani Hapa Utakuwa Umepata Picha Kuwa Sisi Atubahatishi Kwa Kile Tukifanyacho,ezian!"
"mkuu!" Ninjas Mmoja Akaitika,mwite Dokta Aje,jamaa Yule Akaitika Mkuu Na Kutoka Nje!
Cha Ajabu Sasa Na Kilichomshangaza Isack,dk Silvestar Ndiyo Aliyeingia,yule Yule Dokta Rafiki Yake Kipenzi Na Mh Rais Wa Marekani
Isack Akaduwaa
Hata Kama Ni Wewe Ndugu Msomaji ni lazima ungeshangaa na tena akuonekana kutekwa bali alionekana ana cheo fulan kwa vijana wale!
Akawekewa Kiti Akaketi,akamwangalia Isack Akashusha Tabasamu!...
"najua Ni Lazima ushangae,na pengine kutokuamin ukwel huu uonao,pengine unaweza ukahisi u ndoton hapana,nimefanya hivi kwa maana fulani!...
'Maana Fulani Ipi Hiyo?!'
Isack Akawaza,na Wazo Lake Ni Kama Lilisomwa Na Dk Silvester
"yapaswa Kazi Muifanyayo Muisitishe Kwanza Haraka Sana,au Wewe Uendelee Nayo Zidu Aachane Nayo Kuna Kaz Tena Nzito Imejitokeza Hapo Kati Na Mtu Muhimu Aloonekana Kuwa Anafaa Ni Yeye Hapo Ndo Kisa Cha Kukuforce,utueleze Mahali Alipo Zidu!...
Isack Ni Kama Akumuelewa Yani Waache Kumalizia Kulipa Kisasi Walichokula Kiapo Cha Agano La Damu Wafanye Kaz Nyingine?,akabaki Kamtumbulia Macho Dokta Yule akionekana wazi kumshangaa
"na kisa cha kunibandua sura? na kwa kifupi bado sijaelewa hasa dhumuni lenu ni nin hasa!"
Isack Aliwahoji Watu Wale Dokta Akatabasamu,"najua Ungeniuliza Swali Hilo,kazi Mnayoenda Kuifanya Inahitaji Mvikwe Sura Nyingine Kama Si Kutumia Sura Zenu Halisi,Isack akashtuka,
"ngoja nikueleze vizuri kwa ufupi tu nadhani unanijua kama dk Silvestar Ila Unijui Kiundani,mimi Kweli Ni Daktar Na Ni Waziri Wa Afya Nchini Kinte,nadhani Umepata Kusikia Machafuko Yanayoendelea Ndani Ya Kinte,taifa Lile Limegawanyika Upande Wa Ganyama Umejitenga Na Kuwa Taifa Jipya,ganyama Imekuwa Na Tabia Chafu inatuma wanajeshi wake Kinte Kuvunja Amani,wanaua Raia Wasiyo Na Hatia,rais Mernel ii Kamuona ZIDU anaweza Kuikomboa Kinte yeye Pekee Ndo Anayeweza Kuwa Mtetezi Wa Kinte,
Dk Silvestar Akaongea Kwa Uchungu,mpaka Isack Akabaki Anamuonea Huruma Si Kwamba Akupata Habari Zile Za Kugawanyika Kwa Taifa La Kinte La Hasha,ila Akutegemea Kama Zidu Angetafutwa!
"nimekubali Kuwapeleka Alipo Zidu!"
Isack Sasa Akajibu Kwa Kumaanisha,dk Silvestar Akatabasamu,akamchoma Sindano Ya Kumwongezea Nguvu!
Lisaa Limoja Badae Walikuwa Ndani Ya Ndege Wakielekea Katikati Ya Lile Pori Mahali Zidu K Alipofichwa!
Kwa Upande wa Zidu Katili,baada Ya Laptop Yake Kuingia Virus Na Kuzima,alibaki Ameduwaa Asijue Cha Kufanya!...
Wazo Alilokuwa Amelipata Katika Fikra Zake Aliliona Waziwazi Lilikuwa Likielekea Kufeli!,ni Vipi Angewasiliana Na Mh Alfonsor Kwani Alihtaji Jeshi,wafanye Mazoez Ndani Ya Pori Lile Kisha Wampindue Rais Max Malwale,wakati Akiwa Katika Mawazo Yale Ghafla Akasikia Mlio Wa Ndege!
Alijua Huyo Si Mwingine Ni Isack,na Baada Ya Dk Chake Ndege Ile Ilitua Akasikia Ikija,ghafla Kwa Mbali Ikajitokeza Kwenye Macho Yake,ikasimama,eneo Inaposimamaga,tofauti Na Mategemeo Yake Wakashuka Watu Zaidi Ya Watatu,Zidu alipomtumbulia macho alishangaa baada ya kumuona Isack Ana Sura Yake Halisi,
Kengele Ya Hatari Ikagonga Kwenye Ubongo Wake,alipo Mkazia Macho Aligundua Isack Hakuwa Na Khofu Yoyote Ila Hilo Alikumfanya Kutokuchukua Tahadhari Kwa Muda Ule Walokuwa Wakipiga Hatua Kumfata Akautumia Kuweka Risasi Katika Bastola Yake Ndogo
walipofika Isack Akamwambia Zidu Wageni Wake Wale Wana Kilichowaleta Akamkaribisha Daktari!
"komandoo Chaka Ujambo?!"
Dk Silvestar Alianza Kwa Kumsapraiz Zidu Kwa Kumuita Jina Alilokuwa Akilitumia Wakati Yupo Katika Mafunzo Ya Ukomandoo Aloenda Kuyasoma Ndani Ya Miaka miwili na miezi kumi na moja Nchini Marekani,wakati Isack Akichukua Kozi Ya Miaka Mitatu Ya Ujeda Kama Tulivyo Ona Katika Sehemu Zilizopita!...
Kuitwa kwa jina lile 'komandoo chaka' kukamfanya atabasamu,akikumbuka chanzo chake!
KAMBI YA UKOMANDOO SELVARY
Ni baada ya wanajeshi wanaoenda kuwa makomandoo kuwasili,akiwemo Zidu,hapo Awali Alijua Mafunzo Yake Yangechukua Miaka Mitatu,ila Mwez Mmoja Ulipunguzwa Makusudi Ivyo Mafunzo Yake Yalikuwa Ya Miaka Miwili Na Miez Kumi Na moja
'kikosi Silent Kiler Kila Mmoja Ataokota Kikaratas Chake Katika Box Ilo Hapo Atalifungua Na Jina Atakalolikuta Ndo Jina Atakalotumia Akiwa Hapa Kambini...
Hiyo Ilikuwa Ni Siku Ya kwanza
Kila Mmoja Akaenda Akaokota Kakikaratas Alipokutana Na Jina Ambalo Angepaswa Alitumie Pale Kambini!
Na Jina Lake Lisaulike Ndani Ya Miaka Hiyo Ya Mafunzo,zamu Ya Zidu Aliokota Kikaratasi Kilichoandikwa 'komandoo Chaka' Atherwise Ndo Jina Ambalo Angelitumia Akiwa Mafunzoni...
Mtu Yule,aloficha Sura Yake Kumuita Jina Lile Kuka Mpumbaza,jina Ambalo Hata Isack Mwenyewe Akulijua!
Zidu Katili,likaachia Tabasamu,tayar Alijua Yule Ni Mtu Wake Wa Karibu,dk Silvestar akajifungua uninja alouvaa,ZIDU akamtumbulia macho kumshangaa!
"dk ni wewe?!"
akamuuliza pasina kuamini!
dah haya tunaelekea mwishon Zidu Katika opereshen mpya ndani ya mtetezi wa kinte,jina akipewa komando Chaka,ataweza Kuikomboa Kinte?!,na Vp Isack Ataweza Kumalizia Kisasi Dhidi Ya Wazir Alex Na Rais Max Malwale!
Tuimalizie Safari Kwa Pamoja Na Tuanze Safar Mpya Mtetez Wa Kinte Zidu Aka Komandoo Chaka Kazini
Ni Baada Ya Kujikuta Akizama Katika Penzi La Mery,Isack anasitisha kuua!
Zidu anampinga vikali,na kuamua kutoka,Isack akijua Fika Zidu Anaenda Kulipiza Kisasi Ana Amua Kumfatilia Kimyakimya,tamati Ya Safari Yao Ni Katika Nyumba Yake Ya Zamani!...
Songa Nayo Kupata Mwendelezo
Isack Kwa Taratibu Sana Akaufungua Mlango,macho Yake Yakatua Sebuleni!...
"plz Beby Nakuomba Toka Niko Hapa Sebuleni Wacha Kunifanyia Hivyo..."
Isack Alishtuka,maneno Yale Yalisemwa Na Zidu Akiongea Na Simu!...
Mwanaume Akakata Simu!
Pale Sebuleni Aliwasha Taa Ilomuwezesha Isack Amuone Vizuri,
Akalitoa Lile Bushori Lake Alilokuwa amelivaa,akavua na miwani vyote akaweka mezani!
Isack Alishtuka,ni Baada Ya Kumuona Zidu Akiwa Katika Sura Yake Halisi!,mshangao Wake Aukudumu Sana,baada Ya Kumuona Mery Akiwasili Toka Chumbani Mwake!...
Zidu Alipo Muona Tu Mery Haraka Sana Akapiga Magoti Na Kuishika Miguu Ya Mkewe!
Cha Ajabu Sasa,wala Mke Akushangaa Kumuona Zidu Pale,akarudisha Miguu Nyuma,machozi Yalikuwa Yakimtiririka Zidu!,
Isack Pale Nje Alipokuwa Akipiga Chabo Aliuachama Mdomo Wazi Kwa Mshangao,akapikicha Macho Yake Kutoamini Kile Akionacho!
Waliyosema Mapenzi Ayana Ukomandoo Wala Awakukosea!...
"Nimekwambiaje Zidu,sikutaki kwenye maisha yangu mbona king'ang'anizi umekuwa mtu wa kujificha,kwa mwezi nakuona mara moja au sikuoni kabisa mapenz gani hayo sasa!..."
"najua nilikosea beby ila ilipaswa tutengane kwa muda nilikuwa nikisakwa,now nimerudi una budi kunisamehe!"
"umenikuta na mtu,sasa"
"ila Tambua Wewe Ni Mke Wangu Mery Tena Wa Ndoa,kumbuka Nilipokutoa Kwa Nini Wanisaliti Au Ni iko Kigari Hapo Nje Bwana Ako Alicho Kuonga!?"
"ishia Hapo Hapo Zidu Hiko Si Kigari Ni Gari Na Sijaongwa,bali Nimepewa,miaka Yote Hiyo Tumeishi Wote Mbona Ujawah Nipa!,mapenzi Gani Yale Naomba Uondoke Na Usinipigie Magoti,kampigie Mungu Wakko,mwanaume ni kujificha tu,maisha gani hayo!..."
"kumbuka mateso ulokuwa ukiyapata ndani ya ndoa yako (morose) kumbuka Mery,niliamua Kukusaidia Kwa Kuwa Nilikupenda,ulinihaidi Na ukala KIAPO mbele ya mashahidi utonisaliti Mery,utaishi na mimi kipindi cha shida na tabu,furaha na nderemo,iweje leo...
Zidu akashindwa kumalizia akawa akilia tu,bado alipiga magoti,mikono yake kaikunja kifuani,maneno aloyaongea hata Isack Mwenyewe Yalimuhuzunisha!
Mery alikumbuka mbali toka kijijini,alipopendwa na mwanaume Erick Sarjion akampeleka mjini shoga ake ambaye alikuwa mpz wa Zidu akaja kumsaliti na kutoka na mume wake,akaingia Katika Mateso Makali!,palepale Akajikuta Akimwinua Zidu Na Kumkumbatia!
"nimekusamehe Mume Wangu!"
Ilikuwa Ni Kauli Ya Faraja,pale Alipokuwa Amemkumbatia Mikono Yake Kaielekeza Mgongoni Ghafla Akagusa Kimiminika Kilichokuwa Kikimtoka Mery!
Sindo Akamuachia Kwa Ghafla Mery Akaenda Chini!
"mke Wangu,mke Wangu Umepatwa Na Nin?!"
Akauliza Kwa Mshangao Akiangalia Huku Na Kule Pasina Kuona Chochote!
"k..a..a..Na Mwa..nangu Gidion Viz..uri,acha Uja..mbaz Umlee Mwan..angu Ka..ti..ka Maz..ingira Maz..uri"
Palepale Mery Akakata Roho!
"nooooooo!"
Palepale Zidu Akaachia Ukunga,mkali
"uwezi kufa Mery!,nani Kafanya Hivi,hapana Mke Wangu Bado Nakuitaji Mamaa Amka Pls Usiende,ntamleaje Mwanangu Mimi!..."
Zidu Aliongea Kwa Uchungu Na Kwa Sauti Kali!,pale Pale Ghafla Mlango Ukafunguliwa Na Vijana Watatu Wakiwa Na Pistol Mkononi Wakaingia!...
Kwa Upande Wa Isack Bado Aliendelea Kuwachungulia Akimsikitikia Jamaa Ake Ghafla Akahisi Kuwekewa Kitu Puani,muda Ule Ule Akapoteza Fahamu Watu Wale Wakamuwah Kabla Ajadondoka Wakamnyanyua Juu Juu Mpaka Garini!
Wakarudi!,
Katika Dirisha Kulikuwa Na Mtu Mwingine Alokamatia Valvo Eight Seven Yenye Kiwambo Cha Kuzuia Sauti Huyu Si Mwingine Ni Mzee Alex mwenyewe,muda mrefu baada ya kuona kuwasili kwa Zidu Katika Simu Yake Kwani Aliisert Na Sebuleni Pale,haraka Sana Usiku Ule Ule Akaamka Na Kuwapigia Simu Vijana Wake,watatu,kutoka Jeshini Alokuwa Akiwatumia Kwa Shughuli Zake Haramu!
Mbiyooo,mpaka Mitaa Ile Wakashuka Mjeshi Mmoja Akaruka Juu Ya Geti Alipotua Ndani Akafungua Mlango Kwa Siri Sana Wakaingiza Gari! Wakashuka
Mmoja Akamnyatia Isack Pale Mlangoni Akamwekea Pistol Mwingine Akamziba Na Kitambaa Cha Madawa Ya Kulevya Wakamwingiza Garini
Mzee Alex Aliwachungulia Zidu Na Mery Pale Dirishani Akiwa Na Valvor Yake Alishughudia Walipokumbatiana Pale pale kwa kuwa mgongo wa Mery Ulikuwa Upande Wa Dirishani Akaachia Risasi Zisizo Na Idadi!
Watu Wake Wale Walishamfikisha Isack Garini Akawapa Ishara Waingie,wakamteke Zidu Pasina Kujua Kuwa Yule Si Mtu Wa Kawaida,yole Ni Komandoo!
Wakamuweka Chini Ya Ulinzi,
Muda Huo Mzee Alex alikuwa kaingia chumbani akatoka na katoto gidiony kakabeba shingo imedondokea upande mwingine tayari alishakanyonga masikini!
Zidu Akuamini Kile alichokuwa Akikiona,alihisi Ni Ndoto Mwili Wote Ulimlegea Ni Kama Alipatwa Na Koma Ya Ghafla,machozi Tu Yalimtiririka!
"hiki Ni Kiapo (agano La Damu) Nilichoweka Siku Nikimpata Muuaji wa namna hii,unamakosa mawili ambapo katika hukumu yangu utobaki hai!
kosa la kwanza ukaidanganya dunia ulishakufa!,sijui ulitumia njia gani!
kosa la pili kuua watu wangu wa karibu na kunitesa nikakosa amani ya kuishi!
Kwa Makosa Haya!,unastahili Kufa...
Ila Kabla Ajaendelea Ghafla Nguvu Za Ajabu Zikamvamia Zidu,wakakiamsha Kichaa Chake!
Kilichoendelea Hapo Ni Mauaji Ya Kutisha Kwa Watu Wale!...
Mwanaume Akaenda Mpaka Katika Gari Aliloifadhiwa Isack Akamtoa Na Kumuingiza Katika Gari Lake,wakarudi Nyumbani!,isack Akiwa Ana Ufahamu!
Na Hata Alipopata Ufahamu Zidu Akamsimulia Kila Kilichoendelea Alsack aliuzunika sana!,kifo kilikuwa ni haki yake! mwisho isack akamalizia!
TAMATI
Maafande watatu waliketi ofisini,kujadili jambo lile,ni juu ya vifo vile tata,ni afande Nurdini,afande Pusi Na Afande Saka!,
Wote Kwanza Walishangazwa Na Picha Za Kamera Walizozikuta Mule Ndani,kwamba Zidu Yupo Hai,walishughudia Jinsi Alivyokuwa Akimuomba Msamaa Mkewe,pia Walishughudia Jinsi Mh Alex Na Wenzake Walivyoingia Alex Akiwa Kakanyonga Katoto Ka Zidu Na Kukaua!
Pia Ripoti Ya Hosptalin Ilioanish Vidole Vya Mh Alex Ndivyo Vilivyo Mnyonga Mtoto Gidion Pia Na Mh Alex Ndio Aliyemuua Mke Wa Zidu Mery!
Ripoti Ile Ikafikishwa kwa waandishi wa habari na pia ikatangazwa kuwa Zidu Yupo Hai! Na Maelezo Yote Yakatolewa Kila Kitu Kilivyokuwa!
Miili Ya Marehemu Ikazikwa Na Serikali,Kwa heshima Zidu Na Isack Wakiwa Katika Sura Zao Za Bandia Bado Awakitaji Kujionesha!
Baada Ya Mazishi Watu Wote Waliondoka Makaburini Ila Walibaki Watu Wawili Tu Makaburini Mmoja Akilia Mwingine Akimpa Moyo Mwenzake!
Ghafla Nyuma Yao Ikasikika Sauti "pole Zidu,ni Kweli Ulikuwa Na Haki Ya Kumuua Baba Yangu..."
Wote Wakageuka Walipigwa Na Butwaa Baada Ya Kumuona Mery,alikimbia Akamkumbatia Zidu!
"pia Pole Sana Isack,kwa Mateso Baba Yangu Alokupa,alitaman ufe,leo hii yeye ndo kafa kakuacha naombeni mumsamehe apumzike salama uko aendako!"
WOTE WAKAJIKUTA WAKILIA!
MWISHO
0 comments:
Post a Comment