Simulizi : Kiapo (Agano La Damu) (2)
Sehemu Ya Kwanza (1)
IMEANDIKWA NA : ZUBERI MARUMA
********************************************************************************
Simulizi : Kiapo (Agano La Damu) (2)
Sehemu Ya Kwanza (1)
Nikijana Mdogo Anayepitia Mambo Magumu, manyanyaso, mateso Ambayo Yanafikia Hata Kuhatarisha Maisha
Yake,
isack Ndo Jina Lake Kijana Mdogo Anayewapoteza Wazaz Wake Baada Ya Nyumba Yao Kuungua,
analelewa Na Jiran Yake Aitwaye Mzee Alex Ambaye Ndo Muhusika Wa Vifo Vya Wazaz Wake,
mzee Alex Kwa Kujua Ipo Siku Lazima Isack Angeitaj Kulipiza Kisasi Anamtumia Kijana Wa Kaz Zidu K
Kumuua Mtoto Yule!
Isack Anapona Kifo Mara Kadhaa Mwisho Anajikuta Akiingia Katika Ualifu Wa Kupora Akishirikiana Na
Machokoraa Wenzake,
kwa Bahati Mbaya Siku Hiyo Anamkwapulia Dada Mmoja Dada Yule Anapiga Kelele Wananch Wanakuja watoto
wale wanakimbia na Isack anadakwa!,
miongon Mwa Wananch Waliyokuwepo Ni Mwanaume Wa Kazi Zidu Katili Na Madam Jane Na Mwalimu Gibson,zidu K
Ana Amrisha Liletwe Tairi Na Petrol Mtoto Yule Achomwe Moto,
mwalimu Gibson Analeta Tair La Akiba Kutoka Kwenye Gari La Madam Jane Na Petrol Wanamvalisha Isack Na
Kummiminia Petroli Kwenye Tairi Lile! Wanamchoma Moto Na Kutawanyika! Je Nin Kiliendelea!,hapo Ndipo
Tulipoishia Katika Season One Na Hii Ni Season Two!
SEHEMU YA THALATHIN NA MOJA
Kwenye msafara wa mamba kenge ua akosekani,pia kwenye watu wabaya wazuri pia wapo ndiyo! niwakati mtoto
yule akipigwa mama mmoja wa makamo alishindwa kustahimili kuona vile,
alimuona yule ni kama mwanaye roho ilimsuta bila kutegemea akatoka eneo lile na kuchukua simu yake kwa
bahati nzuri mama yule alijuana na Mmoja Wapo Wa Maaskar Katika Kituo Kikuu Cha Polisi Ivyo
Alimpigia,kumjulisha Juu Ya Tukio Lile!
"samahan Afande Kiso Kuna Mtoto Mwiz Anauwawa Na Wananchi Huku Tafadhal Njoo Mumsaidie.."
"huyo mtoto ni mwizi! si ndo hao machokoraa wa hapo dampo?"
"ndiyo afande anapigwa sana,watamuua eti!..."
"hao watoto sasa wameshndikana acha wamuue itakuwa funzo kwa watoto wengine!"
afande Kiso Aliongea Kwa Jeuri Akakata Simu
"kwani Kuna Nini?!"
Afande Nurdin Alimuuliza Huku Macho Yake Yakiwa Bize Kwenye moja ya makalabrasha yake yaliyokuwepo
katika meza yake pale ofisini
"dah si huyu mama ananipigia simu ananambia kuna mwiz anapigwa na raia!"
"nawe ukamjibuje!?"
Nurdin Akauliza Akionekana Wazi Kuanza Kuchanganyikiwa! Tayari Alishasimama Akusubir Jibu La Kiso
Akampachika Swali Lingine
"ni Dampo Lipi?!"
"katikati Ya Jiji"
"poa Shtua Maaskar Wengine Chukua Jacket Proof first aid kit Gari Ndogo La Maji Tukamuokoe Huyo Mtoto
lazima watakuwa wanamchoma!..
Dakika Tano Zilizofuata Gari Ya Maaskari Ilikuwa Barabarani Ikitoa King'ora Cha Hatari
Wananchi Baada Ya Kusikia king'ora cha gari la polisi wakatawanyika,gari ya polis ile ikawasili maeneo
yale nakuanza kumwagia maji isack,
wakamtoa tairi lile alilovishwa haraka sana wakamfanyia huduma ya kwanza na kumuwaisha hospitalini!
moyo wa inspekta Nurdin Uliuzunika Sana,alimuonea Huruma Mtoto Yule Ambaye Alimtafuta Muda Mrefu Pasina
Mafanikio!,
mateso Ya Mtoto Huyu Ni Mpaka Lini?! Nurdin Alijiwazia Macho Yake Yakitazama Jinsi Mwili Wa Dogo Yule
Ulivyobabuka Na Kuharibika Vibaya!
Yeye Ndiyo Aliyejitolea Kusimamia Gharama Zote Za Matibabu Ya Mtoto Yule,hakika Alikuwa Bize Muda Wake
Mwingi Akiutumia Kumwangalia Mtoto Yule hali ile ikajenga hali ya sintofahamu kwa mke wake kipenzi
Saumu!
inspekta nurdin alijaliwa kuwa na familia yenye mtoto mmoja wa kiume walomwita Ramadhani,yeye Na Mke
Wake Na Mwanaye Walipendana,ila Ubize Wa Ghafla Wa Insp Yule Ulimshangaza Mkewe!,
mapema Tu Akaanza Kuingiwa Na Wasiwas Juu Ya Mtoto Yule,
mwanzo Kwa Kuwa Akuijua Istoria Kamili Ya Isack Saumu Alimtilia Shaka Mumewe Kuwa Mtoto Yule Amezaa Na
Madam Jane
Kutokana Na Ukaribu Waloujenga Katika Malezi Ya Yule Mtoto,wazo Ilo Akaja Akalifuta Baada Ya Mume Wake
Kumwambia Kuwa Madam Jane Kamtimua Yule Mtoto Kwa Tuhuma Za Wizi!
"mke Wangu Madam Jane sikamfukuza yule mtoto baada ya kumtuhuma uwizi?"
"kumtuhumu uwizi ama umeshindwa kupeleka mahtaji baba rama usinifanye mimi mtoto mdogo najua kabisa
yule ni mtoto wako na umempa yule mwanamke akulelee usinifanye mimi mjinga!"
"mbona ukawa na mawazo kama hayo mke wang?,"
"mawazo gan?,mbona watoto mtahani wako wengi tu kwanin umng'ang'anie huyo mmoja saiv unamtafuta ehe
ukimpata utamfanyaje?"
inspekta nurdin alishindwa kujibu kwa sir sana akaendelea kumtafuta yule mtoto mpaka ile siku
alipomuokoa katika tanuri la kifo na sasa alikuwa nae pale hosptalin alipanga akipona akaishi naye ila
je mkewe angempokea?!!....
Swala ilo ndilo lililo mkosesha raha ila mwisho akakata shauri itakavyokuwa na iwe ila lazima amsaidie
yule mtoto alisha amua!
basi siku zikasonga hatimaye isack akaruhusiwa hosptalin,
inspekta Nurdin Alifrah Akampakia Ndani Ya Gari Lake Safari Ya Kuelekea Nyumbani Ikafatia!
"mwanangu Isack!"
Inspekta Nurdin Akaita Kwa Upole
"naam Baba"
Isack Akajibu Kwa Uchangamfu
"pole Sana Kwa Yote Uyapitiayo Ila Tambua Kila Kitu Kina Sababu Yake Nadhani Unajua Kaz Yangu Ni Nin
Nimekuchukua Ukaishi Kwangu Ila Chonde Chonde Kama Kweli Wewe Ni Kidokozi Sitosita Kukufukuza Kama
Alivyofanya Madam Jane Acha Kabisa Hiyo Tabia"
"sawa baba"
"corect,kingine mwanangu mama yako ni kigeugeu na ana roho mbaya mvumilie kila atakalosema usiliweke
rohoni kikubwa we soma ufanikishe malengo yako nakuapia ipo siku maisha yako yatakuwa ya raha sawa
mwanangu?!"
"nimekuelewa baba"
Insp nurdin aliendelea kumpa wosia,isack kiumbo alikuwa bado mdogo sana mdogo kuliko hata rama alokuwa
darasa la saba
wakafika nyumbani inspekta akapak gari lake wakashuka wakaelekea ndani!,
"naona sasa umeamua kunletea mtoto wako nikulelee mwanaume una haya"
saumu akampokea mumewe kwa maneno
"shikamoo mama!" isack akasalimia
"nani mama yako? unaweza kuwa na mama kama mimi?"
"mama rama maneno gani hayo ya kumwambia mtoto?!,sasa utake usitake huyu mtoto atakaa hapa na ntamlea
kama mtoto wang!"
"kama mimi mke wako wa ndoa huyu mtoto atokaa hapa lasi ivyo unipe talaka yangu niondoke ubaki na mtoto
wako"
"hayo yote yanatokea wapi mama Rama?! Kwani Ukiishi Na Mtoto Huyu Utapungukiwa Nini?"
"kama Machokoraa Mtahani Wapo Wengi Basi Si Ungewachukua Wote Kwani Ubague Na Umchukue Huyu Kama Si
Mwanao! Plz Mpeleke Kwa Mamake Ila Si Hapa Kwangu Wewe Mtoto Sikutaki Naomba Uondoke!"
"nishasema Atakaa Hapa Hii Nyumba Ni Yangu Na Nsha Amua"
Inspekta Nurdin Alimaliza Akamshika Mkono isack na kumnyanyua pale chini,akamwonesha chumba cheke!
"hiki ndo kitakuwa chumba chako utakachokuwa unalala kama nilivyokwambia tulivyokuwa tunakuja shika
elimu ndo ufunguo wa maisha yako jumatat ntaenda kukuombea urudi shule sawa?"
"sawa baba"
"kwa sasa twende nkakununulie nguo tukirudi utamkuta mwenzako rama kashatoka shule mtaenda nae chuo
sawa?"
"chuo?! chuo ni wapi baba"
insp nurdin akacheka
"chuo ni madrasa huko utajifunza elimu ya din"
"lakini mimi siyo muislam!"
"utulub l ighlm wala ubiswii,hii ni hadithi sahihi yenye maana kwamba tuitafute elimu hata ikiwezekana
mpaka china na pia katika qur an tumeambiwa Iqra ikiwa na maana soma aijalenga muislam au mkristo ivyo
kuliko kukaa nyumbani nakugombana na mama yako nenda chuon na mwenzako ukajifunze mawili matatu! sawa?"
"sawa baba"
wakatoka
"tunatoka!"
inspekta nurdin akamuaga mkewe bi Saumu Ambaye Hata Ivyo Akuangaika Kuitika,moyo Ulimuhuma,mumewe
Nurdin Hata Siku Moja Akuwai Kutoka Out Na Mtoto Wao Ramadhan Ila Leo Anatoka Na Hako Ka Isack!
'lazima Nikaoneshe Haka Katoto Naapa Kataondoka Tu We Subiri Mfyuuu'
Bi Saumu Akajisemea Moyo Wake Ulishaweka Kutu Juu Ya Mtoto Yule!
****
Mzee Alex Alikaa Ofisini kwake Ila Mawazo Yalikuwa Mbali,bado Nia Ya Kumuua Isack alikuwa nayo!,moyo
wake ulimuuma sana baada ya afande kisogo kumpigia na kumwambia wazi kuwa insp nurdin kwa sasa ndiyo
anayeishi na mtoto yule!...
alishika simu yake na kumtafuta mzee wa kazi zidu katili!...
tayari kichwani kwake alishapata wazo
Tangu azaliwe ajawai kuwa na furaha,maisha yake yamekuwa yakiwindwa ajawai hata kutabasamu anaruka mara
Kadhaa Vizingiti Vya Kifo Toka Katika Mikono Hatari Ya Kijana Katili Asiye Na Roho Ya Kibinadamu Mwenye
Roho Ya Kinyama Pale Aoneshwapo Ela Zidu K Au Izrael Wa Kibinadamu!
Inspekta Nurdin Anamwokoa Toka Katika Tanuri La Moto Na Kumchukua Kuish Naye Hata Ivyo Mke Wake Bi
Saumu Anaonekana Kumpiga Vita Mtoto Huyo! Je Nini Kitaendelea Katika Maisha Ya Kijana Huyu Yatima
Twende Pamoja Katika Season Two Ya Riwaya Hii Ya Kusisimua Na Kuburudisha Pia Kwa Kila Silabi
Usomayo..!
*SEHEMU YA THELATHIN NA MBILI!*
Zidu K Akupoteza Muda Akawasili Ofisini Kwa Mzee Alex!
Kimya Kilitawala Kwa Sekunde Kadhaa Kila Mtu Akiwaza Lake,baada Ya Dakika Takribani Kama Tatu Hivi
Ndipo Mzee Alex Alipofumbua Mdomo Wake!
"kwa Sasa Kampeni Zinanifanya Nakuwa Bize Sana Ila Bahati Nzur Watu Wananipenda Japo Siyo Wote Na
Katika Wale Waso Nipenda Nawafyeka Mmoja Mmoja Nibaki Tu Na Wale Wanipendao,haka Katoto Mara Kadhaa
Kamepona Kifo Na na amin Ipo Siku Aka Katoto Kataniumbua Sina Aman Nako Kabisa Na Katika Watu
Wasonipenda Haka Nakaweka Cha Kwanza!
Sasa Kapo Mkonon Mwa Askar Wa Polis Aitwaye Inspekta Nurdin Kaz Nitakayo Kupa Mfyeke uyu inspekta"
Zidu Akaachia Tabasamu!
"nadhani Unazeeka Vibaya Mzee Toka Mara Ya Kwanza Hata Kabla Ajaish Na Huyu Mtoto Ulishapendekeza Insp
Huyu Auwawe Nami Nikakataa Nikisema Waz Sitaki Bifu Na Jeshi La Polisi Kwanza Huyu Jamaa Ananisaka
Kitambo Tu Leo Nijipeleke Kwa Hili Utansamehe Mheshimiwa!"
Mzee Alex Akaachia Kicheko
"ustake Kuniambia Leo Hii Zidu Unakataa Kaz,wewe Ulisha Acha Jeshi Unambinu Zote Za Kijesh Kivipi
Umuogope Polisi Alopitia Depo Ccp Ha Ha Ha Ha Unanchekesha Sana Kijana"
"umenielewa Vibaya Mkuu Sikwamba Sina Uwezo Wa Kumuua Uyo Jamaa La Asha Ila Pindi Ntakapomuua Jeshi
Zima Kupitia Idara ya polisi litansaka,sitopona mimi unajua madhara ya kumuua mwanausalama tena
inspekta kama yule mkuu?!,fikiria njia nyingine ya kufanya lakin siyo kumuua yule mtu ni hatari aisee!"
"yah! nshapata jibu umekataa hii milion 50 yupo ntakayempa na akaifanyia kazi,we endelea kutafuta njia
rais ya kukaua ako katoto au urudishe milioni kumi yangu"
"usijal mkuu hiyo milion hamsin mtafute mtu mwingine umpe sitak vita na jesh mimi ako katoto ntakawinda
na ntakaua siku si nyingi kama kamepona kwenye ule moto awamu hii akatapona kabisa"
"nshaizoea hiyo kauli yako na mara nyingi unamswii!"
"si una niamin?,ilo swala we niachie"
"kwa saiv sikuamin aisee"
mzee wa kazi akuongea kitu akanyanyuka taratibu na kuondoka zake,kichwan alitawaliwa na lindi la mawazo
kitendo cha kutokuaminiwa kilimkasirisha kisa katoto kadogo!
'nitakaua tu sioni raha kakiendelea kuish lazima kafe!'
akajiwazia akiwa ndani ya gari lake
****
UPANDE WA PILI WA SHILINGI
Mahusiano Ya Madam Jane Na Mwalimu Gibson Yalizidi Kukuwa Siku Hadi Siku!
Pia Mwalimu Gibson Akukata Penzi Lake Na Mke Wa Muheshimiwa Na Kwa Kipindi Icho Mheshimiwa Alex Alikuwa
Bize Na Kampen Na Kushindwa Kuisimamia Vyema Ndoa Yake!,bi Ney Akawa Akitoka Na Mwalimu Yule Vile
atakavyo!...
siku hiyo madam jane alijikuta akitaman kusoma msg za bwana wake yule kwan akuwa na tabia hiyo! muda
huo mwalimu gibson alikuwa bafuni akioga!
madam jane akashika simu na kuingia uwanja wa meseji
alishtuka baada ya kuona meseji za bi ney zilizoseviwa my love akujua huyo my lov ni nani ila taratibu
alianza kupata mwanga kila alivyozidi kuzisoma!
"beby mchana uje home mume bado yupo kweny kampen zake"
meseji hii ndo ilomfumbua kwa vyovyote akajua lazima atakuwa tu ni ney!,akazid kurudi nyuma! mwalimu
gibson hakuwa na tabia ya kufuta meseji!
"kale katoto tumekachoma moto"
madam jane alizid kushangaa kuona kuwa hata habar za yule mtoto mpz wake alikuwa akizituma!
akazidi kutiririka katika upande ule wa sent kusoma msg mpz wake alizotuma akipitia na inbox pia
"mpango gan mpz?" inbox akaenda sent
"kuna mpango nimeupanga!"
akashuka chini yake!
"nimemtuma yule mtoto dukani nikaiba simu za mwalimu so naenda tegesha katika begi lake lazima
ajulikane mwiz ni yey mpz huyu madam amfukuze ateseke mtahani!,"
madam jane alishtuka baada ya kuisoma meseji hiyo upande wa sent kumbe isack akumuibia ni njama za
mwalimu gibson?
akaenda mbele!
"nimefanikiwa na kafukuzwa hadi shule"
taratibu machozi yakaanza kumtoka madam jane alilia kwa uchungu kwa kitendo alicho mfanyia yule mtoto!
akakumbuka jinsi mwanaume yule alomkabidhi moyo wake siku ile alipokuwa akisisitiza begi likaguliwe!
madam jane bado alikumbuka jins alivyompiga kibao isack pindi alipompigia magoti!
madam jane akajikuta akilia kwa uchungu! moyo wake ulimuuma,akakumbuka pia isack usiku ule kulipokuwa
na mvua kubwa alipomtimua kwake na hata alipotoa tairi lake la gari kusudi mtoto yule asiye na hatia
achomwe moto
yote ni kwasababu ya yule mwalimu gibson
machoz yakazid kutiririka na sasa alilia kwa kwikwi!
akakumbuka mwanzo alivyokuwa akimpenda!
unyenyekevu alokuwa nao mtoto yule,ila mapenz upofu akajikuta mwalimu gibson akimzima yote yale!
pia alimkumbuka inspekta Nurdin Jins Alivyokuwa Akimuhusia!, akazidi Kulia...
Na Hata Mwalimu Gibson Alivyotoka Bafuni Madam Jane Akutaka Kumsikiliza Kabisa Alimtukana
Akamfukuza,akutaka Tena Maelewano Baina Yao!
Akapanga Kwenda Kituoni Kuonana Na Inspekta Nurdin Amuombe Radhi Apewe Yule Mtoto Tena Aishi Naye Safar
Ya Kwenda Kituoni Ikawadia Ila Alishachelewa...
***
Mapenz Alokuwa Nayo Kwa Isack Siyo Tu Yalimkasirisha Mama Hata Mwanaye Ramadhani Kitendo Icho
Kilimuuma!
Inspekta Nurdin Alionesha Kumpenda isack kupitiliza!
ilikuwa ni jumapil tulivu siku ambayo bi saumu alikata shauri lazima amuue mtoto yule tena kwa sumu ya
panya
siku hiyo mumewe alikuwa kaenda kazin sambili ile rama akashika vitabu vyake vya chuo wakati huo isack
alikuwa akifagia banda la kuku
"mama naenda chuo!"
"msalimie ustadh"
Rama Akatoka Pasina Kumuita Isack
Bi Saumu Akachukua Blue Band Ilokuwa Pale Mezani Akaitoa Na Kuchukua Kikopo Kingine Cha Blue Band
Akakorogea Ile Sumu! Kisha Akatoka
"isack Natoka Nenda Kanywe Chai Kwanza Na Mikate Usisahau Kupaka Na Ile Blue Band"
Baada Ya Maagizo Yale Akatoka Akutaka Kushughudia Isack Akifa
alitaka akirudi toka saluni akute mwili tu!
Maskin isack akuangaika kurudi kule bandani akaelekea sebulen akakaa kwenye kiti akachukua vipande vya
mkate na kuvipaka blue band baada ya kutosheka akamimina chai na kuiwekea sukari akakoroga!
Akabeba kipande cha mkate na kukipeleka mdomoni pasina kujua kina sumu ndani yake!
Baada ya kunusurika kuchomwa moto mtoto Isack anaokolewa na Insp Nurdin ambaye anamchukua na kuishi
naye ila tatizo linakuja kwa mke wake anamtuhumu Ins Nurdin kwamba yule mtoto ni Mtoto wake anaanzisha
Manyanyaso makali dhidi ya Mtoto Yule!.
Na kama hiyo aitoshi anapanga Kumuua kabisa na sasa Kamtegeshea sumu kwenye blue Band pasina kujua
Isack Anapaka Blue Band Ile Katika Vipande Vya Mikate Je Nin Kitaendelea Na Hii ni Sehemu ya thalathin
na tatu
"Ramadhan,..."
"Naam baba!."
"Hakikisha kila unapoenda chuo umwachi nyuma mwenzako isack nyuma sawa?,"
"Sawa baba!"
Rama Alikumbuka Maneno Yale aliyoambiwa na baba yake,siku ile walipokuwa njiani wakielekea chuoni pia
alikumbuka walipofika chuoni Baada Ya Nurdin Kumwandikisha Ustadh Alipomwambia...
"Rama Huyu Isack Ni Mdogo Ako Pindi Asipokuja Chuo Ntakuadhibu Wewe Iwe Isiwe Akikisha Unakuja Nae
Sawa?!"
"ndio Ustadh"
Ni Jana tu aliambiwa Maneno hayo leo anaenda bila Isack si Mwalimu wake atamuadhibu
Ghafla Kwa Wepesi Akageuka Na Kwa Kukimbia Akawa Akirudi Nyumbani Alikuwa Ajafika Mbali!
Alifungua Geti Lao Akaingia Mpaka Sebuleni Alishtuka Kumuona Isack Kashika Kipande Cha Mkate
Akikipeleka Mdomoni!
"Usije ukamruhusu akala mikate uyu mtoto si Ndugu yako chai atakunywa ile ya mwisho ilojaa machicha na
kitafunio atakula makoko na kile kitakachobaki kwenye sahan labda baba yako awepo sawa?!"
Rama Akakumbuka Agizo Lile Alilopewa Na Mama Yake Akazidi Kukunja Sura Alimfikia Isack Na Kumpiga Kibao
Akamnyang'anya Ule Mkate
"we Nan Kakwambia Ule Mikate Umesahau Mama Alivyosema?"
Rama Aliongea Huku Akimwangalia Vibaya Mdogo Wake Yule Wa Kufikia
"mama Kanambia Nile"
"mama Kanambia Nile!,una Share Yako Hapa Ukome!"
Rama Alijibu Akimgilizia Huku Akibana Pua
"mi Nakula Hii Mikate Na Hii Chai We Kajiandae Twende Chuo Baba Alinambia Nisikuache Nyuma Kabla
Sijakuzaba mavibao"
Rama Aliongea Akipeleka Kipande Cha Mkate Mdomoni,isack Kwa Unyonge Akakimbilia Ndani Kuvaa! Akimwacha
Rama Pale Sebulen Akifakamia Vile Vipande Vya Mkate!
****
Inspekta Nurdin Alisikitika Sana Kwa Kile Alichoambiwa Na Madam Jane!
"dah Ndo Maana Mi Nilikwambia Ule Ni Mchezo Tu Na Kama Umegundua Ilo Mi Sina Shida Tena Atafrah Sana
Maana Hata Pale Nyumbani Kwangu Si Salama Sana Mke Wangu Anamchukia Yule Mtoto Akisema Ni Wangu Bado
Yupo Katika Mateso"
"lazima Afikiri Hivyo Afande Una Roho Ya Kipekee Nataman Ningepata Mwanaume Kama Wewe!"
Inspekta Nurdin Akatabasamu Na Mwishoe Kuangua Kicheko!..
"usijal ipo siku utapata mwanaume kama mim...
kabla ajamalizia ghafla simu yake ikaita neno lililosomeka ni 'wife' katika screen ya kioo cha simu
yake! pasina wasiwasi wowote akapokea...
"m.m..me..wan..gu..mto.to..we.t.u"
mke wake yule alishindwa kumalizia sentensi yake kikaskika kishindo
"nin kimetokea mama Rama?! Hellow..Hellow"
Inspekta Nurdin Alijaribu Kuita Ila Upande Wa Pili Ulikuwa Kimya Akuwa Na Shaka Mkewe Atakuwa Kadondoka
Chini Na Kupoteza Fahamu Kwa Kishindo Kile Alichokisikia!
Haraka Sana Akanyanyuka Akiwa Kama Mtu Alochanganyikiwa! Akuongea Kitu Kilichoeleweka Akaingia Ndan Ya
Gari yake,madam jane akubaki nyuma naye akaingia kwenye gari yake na baadhi ya maaskari kuifata gari ya
Nurdin Kwa Nyuma!
Dakika Tano Walikuwa Wamefika Nyumban Kwa Insp Nurdin Chini Kulikuwa Na Miili Miwili Mwili Wa Rama Na
Mama Yake Saumu Alopoteza Fahamu Isack Alikuwa Pembeni Akilia
"ni Nin Kilichotokea Isack!"
Insp Nurdin Alimuuliza Isack Alokuwa Akilia Ikabidi Isack Asimulie Ilivyokuwa
"baada Ya Baba Kuondoka Saa 12 Mama Aliniamsha Akanambia Nifanye Usafi! Ilipofika Saa Mbili Nilipotak
Kwenda Kuoga Akanambia Nikafanyie Usaf Banda La Kuku Na Mim Ni Mkristo Naenda Chuo Kufanya Nin Bas Mimi
Nikaingia ndani kufanya usafi kama dak 3 hivi baada ya Rama kutoka mama naye akatoka akinambia nikanywe
chai na mkate nipake na blueband pale mezani nami nkafanya vyo ila kabla sijala Rama Alirudi Ghafla Na
Kunnyang'anya Ile Mikate
Akanambia Mi Sikustahil Kula Ilipaswa Nile Makombo Na Machicha Ya Chai Ivyo Nikajiandae Twende Chuo
Nikaondoka Nikimuacha Anakula Ile Mikate...
Niliporudi Nilimkuta Chini Mama Aliporudi Ndipo Alipokupigia Simu Akadondoka"
Nurdin Alishajua Kilichotokea Akapiga Simu Ambulance Ikaja Maiti Ya Mwanae Ikabebwa Na Mke Wake
Pia,vyakula Vile Pale Mezani Pia Vilichukuliwa Kwa Uchunguzi!
Pia Alifanikiwa kuiona ile blueband walokuwa wakiitumia,inspekta nurdin alikuwa na uchungu sana na mke
wake!
alimchukia na akumpenda tena!
palepale hospitalin aka amrisha apigwe pingu sambamba na kumuandikia talaka!
Saumu Alipozinduka Alilia Kwanza Kumpoteza Mwanae Kipenz Rama Pili Kuipoteza Ndoa Yake Na Tatu
Kuupoteza Uhuru Wake...
Kesho Yake Jumapili Sa Saba Wakamzika Rama Mama Yake Akiwa Lupango!
Moyo Wa Insp Bado Ulijaa Simanz Madam Jane Alijitahidi Kuwa Karibu Naye Kumtoa Katika 'stes' Japo
Ilikuwa Kaz Ngumu Ila Taratibu Alianza Kufanikiwa!
Kesho Yake Insp Nurdin Akaelekea Gulion Primary School Kumwombea Isack Msamaha! Kwa Walimu Baada Ya
Kuomba Sana Mwishoe Alifanikiwa Isack Kwa Mara Nyingine Akarudi Shule!
****
Jimbo Lile Lilitetema Shangwe Furaha Ilitawala Sasa Mr Alex Alikuwa Mbunge!
Ndiyo!,mbunge Wa Jimbo Lile
Alifanya Sherehe Kubwa Nyumbani Kwake Watu Walikula Na Kusaza!
Na Kizuri Zaidi Mwanaye Wa Kwanza Mery Alikuwa Katoka Masomon Nchini Marekani Miaka Saba Sasa Alikuwa
Akisomea Maswala Ya Sheria!
Si Mnajua Wenzetu Awanaga Cha Shule Ya Msingi Wala Sekondari Wenyewe Kwanzia Watoto Usomea Vipaji!
Akiwa Na Miaka 14 Urembo Wake Ulianza Kuonekana Waziwazi!,akukijua Kiswahili Zaidi Ya Kingreza,kwa kuwa
Mery Alikuwa Katoka safarini siku hiyo alitawaliwa na uchovu ikambidi Mery Amwombe Mdogo Wake Agnes
Wakapumzike,agy Akuwa Mbishi Wakaongozana Mpaka Chumbani Wakajitupa Kitandani!
"Can ask u something my young sister?!"
MERY akaongea kwa kingreza akimaanisha nikuulize kitu mdogo wangu?
"yes..."
Agnes Naye Akaitika Kwa Furaha Wakiwa Wamelalia Vimto
"Hey where is Isaack a child who used to play together with,he as a father,me as a mother and you as a
child!?"
(hivi Isack Yule Mtoto Jirani Tulokuwa Tukicheza Naye Cha Kimama Yeye Akicheza Baba,mimi Mama Na Wewe
Mtoto Kwa Saivi Yupo Wapi?)
Badala Ya Kujibu Agnes akawa akicheka,alicheka,akacheka!
" you make me remember those moments,long time,its a long story"
(umenikumbusha mbali sana dada ila ni storia ndefu)
Agnes Akajibu Huku Akiendelea Kucheka
" Tell me just in short"
(nielezee Hata Kwa Kifupi)
" his parents was died,their house fired with unknown people,so Isaack lived with us here for a long
time"
(yule Mtoto Wazazi Wake Walikufa Nyumba Yao Iliungua Moto Tukawa Tunaishi Naye Hapa Tumekaa Naye
Kitambo Sana Hapa!)
" Where he is gone now?"
(sasa Kaenda Wapi?!)
"His uncle took him "
(baba Mdogo Wake Alikuja Mchukua)
"You know where he lives with his uncle?"
(unajua Hata Anapoishi Na Huyo Ba Mdogo Wake Tukamtembelee?!)
Mery Akajaribu Kuomba
"no,no,i Don't Know"
(hapana Hapana Sijui) Agnes Akakana Kutopajua
Mery Aliridhika Kwa Jibu Lile,japo Moyoni Mwake Alionesha Kumpenda Isack!
"I will find,wanna talk to him before travelling"
(ntamtafuta Niongee Naye Kabla sijasafiri kuondoka!)
mery akawaza! mwenyewe
***
Jumatatu Ilofatia Asubuh Na Mapema Isack Alielekea Shulen Alkuwa Na Furaha Sana Kurudi Shuleni!
Moyo Wake Ulfarijika Zaidi Baada Ya Kurudi Kuishi Kwa Madam Jane!
Jion Kama Kawaida Aliingia Ndani Ya Gari La Madam Jane Safar Ya Kurudi Nyumbani Ikawadia!,katu Awakujua
Kama Wanafatiliwa Na Kijana Wa Kaz Zidu K
"nsubir Hapa Kuna Kitu Nkachukue Hapo Supar Market"
Madam Jane Alimwambia Isack Akipaki Gari Lake Akashuka,kitendo Tu Cha Kuingia Ndani Mwanaume Wa Kazi
Alishuka Kwenye Gari Lake Akachepuka Mp aka Kwenye Gari La Madam Jane!
Isack Alishtuka Kumuona Zidu ila zidu akamfunika puani kwa kitambaa alichowekea madawa! muda ule ule
isack akasinzia akamtoa na kumuingiza ndani ya gari lake!
Akalitoa gari kwa spidi kuelekea katika jumba lake safari hii akutaka kuharibu kazi tena alidhamiria!
Kijana wa kazi Zidu Katili.. Kwa mara nyingine, anafanikiwa kumteka mtoto Isack, lengo lake ni kumuua,
ikiwa ni oda aliyokwisha kupewa muda mrefu.
Pia tumemuona Mery, mtoto mkubwa wa Mh Alex akiwa kaingia nchini baada ya kutoka likizo huko nchini
marekani...
Na anaonekana kumuulizia Isack, Je.? Ni nini kilichoendelea..?
NA HII NI SEHEMU YA THELATHINI NA NNE
Gari ile aina ya Range iliendelea kukata mbuga, huku dereva akitamani hata apae kusudi afike mapema
nyumban,i mamba wake wakapate kufaidi, ni muda mrefu hakuwatupia chakula,... Alikabaki akitabasamu
mwenyewe kama mwehu.
Ghafla akapata wazo kichwani mwake,Aliona ni heri amjulishe kabisa mzee Alex ikiwezekana ashuhudie
tukio alilolipanga kulifanya dhidi ya Isack.
Akampandia hewani ambapo muda huo wa jioni, mzee Alex alikuwa katika sebule yake pana, iliyogawanywa
mara mbili.. Upande wa juu aliokaa yeye, mbele yake palikuwa na Tv, sofa za kupumzikia na meza ndogo ya
kioo, juu ya meza kulikuwa na chupa kadhaa za bia na Laptop yake ndogo.
Upande wa chini kulikuwa na kabati kubwa la vyombo, meza kubwa iliyozungukwa na viti sita vya kukalia
nyakati za kula chakula, kwa muda huo katika meza hiyo aliketi binti yake Agnes...
Macho yake yakiwa katika daftari zake, akijisomea somea.
Jikon alikuwepo Bi.Ney na mtoto wake Mery wakipika, huku akimfundisha fundisha baadhi ya maneno ya
kiswahili.. Kwani Mery hakuifahamu kabisa lugha ile kutokana na muda mwingi kuutumia marekani alipokuwa
anapata elimu yake... Hivyo lugha ya kishwahili ilimpa shida kidogo ingawaje, baadhi ya maneno
aliyaelewa.
Lakini alitaka kuifahamu kwa upana zaidi.
Wakati mzee Alex akiwa anapata mvinyo huku akitazama luninga, ghafla simu yake ikaita. Akaiangalia kwa
sekunde kadhaa na kushusha pumzi kidogo huku pumzi hiyo, ikisindikizwa na tabasamu pana usoni mwake.
"Niambie Zidu.''
"Ule mzigo nishaupataa, na baada ya dakika kadhaa hautokuwepo tena katika uso wa dunia hii.''
"Wacha bwana!! Nd'o maana mimi, nakuaminiaga ila Tafadhali! Tafadhali! Tafadhali sana, usikaue mpaka
nije tukaue wote.. Maana kametusumbua sana.''
Mzee Alex alibwabwaja kwa sauti kidogo bila kufahamu kama sauti yake inaweza kusikika na Agnes
aliyekuwa anajisomea kwenye meza kubwa ya chakula.
Agnes pale alipokaa akijisomea, alishtuka baada ya kusikia baba yake akizlzungumzia habari za kuua,
alipatwa na shauku ya kutaka kufahamu zaidi kile anachozungumza baba yake kwenye simu. Aliyatega
vilivyo masikio yake upande alipo baba yake.
"Yaah Yah! Ndio, dakika tano nitakuwa hapo.'' Mzee Alex baada ya kumaliza mazungumzo yake, akakata simu
na kuikwapua glasi iliyojaa kinywaji chenye kilevi na kugwida mafundo kadhaa, kabla ya kuitua juu ya
meza glasi ile.
Bado Agnes aliendelea kumfuatilia baba yake, pasina mzee yule kujua kama anafuatiliwa kisiri siri.
''Ha ha ha ha ha ha!!! Isack... Kwisha kazi yako, utakufa kifo kibaya zaidi ya walichokufa wazazi wako,
waliokufa kwa kuungua na moto... Ha ha ha ha.''. Mzee Alex aliendelea Kujitapa baada ya kuona mikakati
yake inaenda kutimia, akanyanyuka pale kwenye sofa huku akipepesuka, akatoka na kuelekea ilipo parking
ya magari na kuchagua gari atakayo itumia, aliingia ndani ya gari na kulitoa mazingiria ya pale
nyumbani kwake na kutokomea barabarani.
''Isack, i love you so much, I want hear something from you. Tell me Isack, do you love me.?''
(Isack nakupenda sana, nahitaji kusikia jambo fulani kutoka kwako, niambie Isack Unanipenda.?'')
Baada ya kushuhudia baba yake akiondoka, Agnes alikumbuka jambo fulani lililotokea usiku wa kuamkia
siku hiyo, jinsi dada yake alivyokuwa akimuota aliyemtaja kwa jina la Isack, alijaribu kuoanisha jina
alilolitaja dada yake kwenye njozi na jina alilosikia likitajwa na baba yake pindi alipokuwa
anazungumza na simu.
Pia alikumbuka wakati walipotoka kwenye sherehe jioni ya siku iliyopita.. Mery alimuulizia Isack, ni
wazi dada yake alimpenda sana kijana huyo, kijana ambaye kwa mazungumzo aliyoyasikia, hakuwa na shaka
baba yake alihitaji kumuua kijana huyo.... Baada ya kutafakuri kwa sekunde huku akiulazimisha ubongo
wake kuchanganua mambo kwa haraka zaidi, alipata wazo la kumfikishia dada yake taarifa ile.
Kwa haraka Agnes akajinyanyua pale alipokuwa anajisomea na kukimbia kuelekea jikoni, huku akiita jina
la dada yake kwa nguvu.
"Merry! Mery! Mery my sister , i need talk to you. Pleas follow me.''
(Mery! Mery! Mery... Dada yangu nahitaji kuongea na wewe, tafadhali nifate.'')
"Agnes!!! What wrong with you.?''."
(agnes!!! Tatizo nini wewe.?'')
Mery akauliza kwa wasiwasi baada ya kumuona mdogo wake akimhitaji huku akionekana ni mwenye kuhema kama
alitoka kukimbia mbio ndefu.
"Don't worry sweet, i need talk to you."
(''Usijali mpendwa, nahitaji kuongea na wewe.'')
"Kuna nini wewe Agnes, mbona mbio mbio.?''. Bi.Ney akauliza kwa wasiwasi huku akiacha shughuli
aliyokuwa anaifanya na kumgeukia Agnes aliyekuwa kasimama mlangoni.
''Don't worry mom, that's is import issue, I want ask her something.''
(''Usijali mama, hili ni jambo muhimu sana nataka kumuuliza huyu.''
Agnes akajibu, akijaribu kumtoa mama yao wasiwasi... Akamshika mkono dada yake na kumtoa jikoni,
wakaelekea moja kwa moja mpaka chumbani kwao kwaajili ya kuzungumza.
Katu hawakujua kama mama yao Bi.Ney aliwafuata kwa nyuma kutaka, kusikiliza ni kipi Agnes alitaka
kumweleza dada yake.
*******
CHUMBANI KWAKINA AGNES NA MERY.
"You can't believe it Sister! I got Isacks information dad want to kill him"
(Dada huwezi kuamini, habari za Isack nimezipata.. Baba anataka kumuua.)
Agnes alimwambia hivyo dada yake baada ya kufika chumbani kwao.
''What!!!'
(''Ninii.?'') Mery alitahamaki na kuuliza kwa mshangao kana kwamba hakusikia kile alichoambiwa.
''Habari niliyoisikia ndio hiyo na hivi sasa baba katoka kuelekea huko alipotekwa Isack.''. Kabla Agnes
hajaendelea kutoa maelezo vizuri, Mery akakurupuka na kuufuata mlango.
Bi.Ney alishtuka kusikia maneno yale, akajiuliza maswali lukuki yasiyokuwa na majibu, watoto wake
kwanini walikuwa wakifatilia maswala ya Isack.... Ghafla akamuona mwanae akiwa anaufuata mlango kwania
ya kutoka nnje.
Ili isijulikane kama alikuwa akiwasikiliza wanae, akaufungua mlango akijifanya nd'o anaingia kwenye
chumba cha wanae.
''Kuna nini nyie watoto.?". Akauliza huku akiwashangaa wanae, illa Mery wala... Hakutingishika kwa yake
kuingia chumbani mwao kwa kushitukiza namna ile, nd'o kwanza akampiga kikumbo na kutoka kwenye kile
chumba akimuacha Agnes na mama yao, kwa mwendo wa haraka alifanikisha kutoka nnje ya geti la nyumba yao
na kuliona gari la baba yake likichochea mafuta... Akaangaza kulia na kushoto na kufanikiwa kuona
bodaboda moja iliyokuwa imepaki kwenye mti mmoja uliokuwa kando na nyumba yao, aliikimbilia na
alipofika karibu na bodaboda ile. Akadandia kwa nyuma.
"Follow his car.''
(''Fata gari yake.'')
Ni kama dereva boda boda yule hakuelewa ile lugha. Maana baada ya kuambiwa vile, aliduwaa na kumtazama
abiria wake.
"Eeeee" Akajibu kama boyam
"I say follow him."
(''Nimesema mfuate.'')
Mery akarudia kwa ukali huku akilinyooshea kidole gari la baba yake lililokuwa limefika mbali kidogo,
dereva bodaboda yule hapo ndipo alipoelewa anaambiwa nini... Akawasha pikipiki na kuhitaji kuondoka,
lakini asita baada ya kusikia mlio wa geti likifunguka, alijua huenda kuna abiria mwingine anatoka.....
Mama yake na Mery pamoja na mdogo wake wakatoka kwenye geti na kutazama pikipiki iliyombeba Mery.
"Embu subirini"
"i say follow him. Don't waste time.''
(''Nimesema mfuate yeye, usipoteze muda.''l
Mery akaongea kwa ukali dereva wake akamtwii
"Huyu Mery kapatwa na nin lakini?!"
Bi.Ney akauliza akimtumbulia macho mtoto wake Agnes aliobakia nae pale nnje.
Agnes alijaaliwa umbea, saa ngapi asianze kuropoka.
"mama Ngoja Nikwambie Lakin Usije Kumwambia Dada Kama Mimi Ndo Nlokwambia"
"sema!" Bi Ney Akajibu Akionekana Kuwa Na Shahuku
"dada Anampenda Sana Isack?"
"anampenda Isack? Kivipi Nakamjuaje?"
"si Ndo Hapo Nami Nnaposhangaa Mama Ila Juzi Wakati Tulipotoka Kwenye Sherehe Tulipoingia Tu Ndani Dada
Akawa Akiniuliza Yule Mtoto Tulokuwa Tukicheza Naye Zaman Isack Yupo Wapi?"
"ehe Ukamjibuje?!" Bi Ney Akajibu Kwa Wahka
"nikamjibu Nyumba Yao Iliungua Tukaish Na Yule Mtoto Hapa Mpaka Alipokuja Chukuliwa Na Ba Mdogo Wake"
"vizur Sana naye akajibuje?!"
"akaniuliza napafahamu hapo kwa ba mdogo wake nimpeleke?"
"mh! makubwa ehe ukajibuje?"
"aku! nikamwambia mi sipajui"
"ehe"
"basi tukalala,usiku sasa alikuwa akimuota tu huyo kijana isack nakupend isack nakpenda"
"mmmh wewe!"
"ndiyo mama,sasa leo wakati nlpokuwa nasoma pale sebuleni sindo mara baba akapigiwa simu kumbe bab ndo
aliyechoma moto ile nyumba ya kina isack"
hapo kwa mara nyingine bi ney akashtuka ni kama akusikia wakati mtoto yule akimwambia mwenzake kule
chumbani
"we mtoto mpumbavu sana mmbeya kaz kuskia ya wakubwa nimeskia kila ulichomwambia mwenzako mtoto mdogo
una mambo yakikubwa ntamueleza baba yenu yote uone atakacho wafanya"
bi ney akamgeuka Agnes Akamshushua Na Kufungua Geti Lake Akarudi Ndani,agnes Akamfata Huku Akiomba
"hapana Mama!...Usimwambie Baba"
Bi Ney Akujibu Kitu Akafika Jikoni Akashika Simu Yake Akatafuta Namba Za Mumewe Na Kumpigia! Tayari
Kumwambia Juu Ya Kufatiliwa Na Mwanaye Mery,simu Ikaita...
****
Madam Jane Alitoka Ndani Ya Supar Market Ile Akiwa Na Kamfuko Alichoweka Vitu Alivyonunua!
Akalifikia Gari Lake Kwanza Akushtuka Kukuta Mlango Wazi Kwa Kuwa Alijua Isack Yupo Ndani!
Ila Alishtuka Baada Ya Kutomkuta Isack!,akaingia Ndani Ya Gari Lake Na Kuweka Vitu Vyake Akakaa
Kumsubir Akijua Pengine Kuna Mahali Alienda
Robo saa,nusu saa na hatimaye lisaa likakatika hakiwa pale
taratibu akaanza kuingiwa na wasiwasi
'au atakuwa karudi mtahani nin?!'
wazo hilo likapita katika kichwa chake akikumbuka ile siku usiku alipomkataa!
pengine isack naye alikumbuka akakosa iman naye!
'watoto wa mtahani daaah huyu alishazoea mtahani itakuwa karud mtahan nin!'
mawazo yakazidi kupandana katika kichwa chake!
wazo kwamba katekwa akuwa nalo kabisa!,akawasha gari lake tayari kurudi kituoni akaonane na inspekta
Nurdin Kwanza Ajue Wafanyaje!
*mambo Bado Ni Moto Mery Mtoto wa miaka 14 aingia kazid kumsaidia Isack ila mama yake agundua na
ampigia simu mumewe kumwelez kuwa anafatiliwa na mwanaye unahis nin kitaendelea?!,isack atapona kwenye
mkono wa zidu na vipi kuhusu mwalimu jane na insp nurdin watampata isack jibu ya swal hili endelea kuwa
nami ndani ya uwanja huu...
Zidu katili anafanikiwa kumteka mtoto Isack Anamjulisha Mh Alex Ambaye Anatoka Nyumban Kwa Furaha
Pasina Kujua Mtoto Wake Mdogo Mery Anamfatilia!
Pia Tuliona Madam Jane Kagundua Kutokuwepo Kwa Isack Ndani Ya Gari Ana Amua Kwenda Kuonana Na Insp
Nurdin Je Ninin Kitaendelea Twende Pamoja Kujua Mwendelezo Wa Riwaya Hii Yenye Mafunzo Tele Ndani
Yake!...
SEHEMU YA THALATHIN NA TANO
Bi Ney Aliendelea Kusikiliza Simu Ile Ikaita Mpaka Ikakata,
akashangaa!
iweje mumewe asipokee simu yake?
akapiga tena vivyo hivyo ikaita mpaka ikakata
tena na tena!
akachoka mwili na roho!
Wakati Simu Yake Ikiendelea Kuwepo Kwenye Masikio Yake Kwa Mbali Akaskia Simu Kama Ya Mume Wake Ikiita
Upande Wa Sebuleni
Haraka Sana Akajiondosha Kuelekea Sebulen Agnes Akimfata Kwa Nyuma!
Alishtuka Kuikuta Simu Mezani Kumbe Mzee Alex Kwa Furaha Aliisahau Simu Pale!
Bi Ney Alichoka Ndiyo! Alichoka Mwili Na Roho
Inspekta Nurdin Alimsikiliza Madam Jane Kwa Makini!
"yah Ni Kwel Mawazo Yako Ayajapishana Sana Na Mawazo Yangu Huyu Mtoto Lazima Atakuwa Karudi Mtahani
Itabidi tuingie mtahani tukamtafute! ila tuanzie kwanza nyumbani kwako pengine alitangulia!
madam jane hakuwa mbishi insp Nurdin Akajipakia Ndan Ya Gari La Madam,madam Akawasha Na Kuliondoa
Taratibu
Ndani Ya Gari Wote Walikuwa Kimya Nikama Kila Mtu Alikuwa Na Mawazo Yake!,kila Mmoja Alikuwa Na Hisia
Kwa Upande Wake!
Madam Jane Alijihis Kumpenda Inspekta Nurdin Hasa Ukarimu Wake,alitaman Awe Karibu Naye Kila Dakika!
Yeye Ndo Alozima Machungu Ya Mwalimu Gibson!...
Akabaki Akimwangalia Kwa Pembe Ya Jicho Kwa Macho Ya Matamanio!
'nataman Angekuwa Mume Wangu Na Isack Ndo Awe Mtoto Wetu Wa Kwanza I Think Ingependeza"
Wazo Hilo Likapita Kichwani Kwa Madam Jane Akajikuta Akitabasamu Mwenyewe!
Hata Kichwani Kwa Insp Nurdin Kwa Muda Alijikuta Akisahau Madhila Ya Mke Wake Ambaye Alishahukumiwa
Kifungo Cha Maisha Gerezani!
Alimchukia Sana Yule Mwanamke!,ila Kwa Sasa Alijikuta Moyo Wake Ukataman Aishi Na Madam Jane! Kiumbo
Kwanza Alikuwa Mzuri Ila Tatizo Kitendo Cha Madam Yule Kuadaika Na Mapenz Mpaka Kumfukuza Mtoto Yule
Kikatia Doa Upendo Wake!
Akajipa Muda Wa Kuendelea Kumchunguza Dada Yule!
Mawazo Yale Kwa Kila Mmoja Yakafanya Kimya Cha Muda Kikachukua Hatamu Baina Yao!
Hatimaye Wakaifikia Nyumba Ya Madam Jane hata ivyo awakukuta mtu ndani!
wakaingia mtahani kumtafuta wakipita dampo moja baada ya jingine!
ila awakubahatika kitu,wasiwasi ukawavaa!
*****
Bodaboda Ilombeba Mery Alizidi Kukata Mbuga Wakiifatilia Gari Ya Baba Yake Mzee Alex!
Mzee Alex Akujua Juu Ya Kufatiliwa Kwake Akazidi Kukanyaga Mafuta akakata Mitaa Kadhaa Hatimaye
akaifikia Nyumba Ya Zidu Katili!
Akasimamisha Gari Pale! Na Kuanza Kupiga Honi!
"Stop here don't proceed"
(simama Hapa!,usiendelee)
Baada Ya Agnes Kuona Baba Yake Kasimamisha Gari Lake Pale Akawa Akimwambia Dereva Boda Boda Yule
Asimamishe Lakini Ni Kama Akumuelewa Mpaka Mery Alipopayuka!...
"I've said stop here "
(nimesema simama)
boda boda yule akasimamisha na kumgeukia Mery!
"nini Sasa?"
Akamuuliza Kwa Kiswahili Kama Vile Anaijua Lugha Ile ,Mery Akujibu Kitu Akashuka
"How Much do you own me"
(unanidai Sh Ngapi?)
Bodaboda Akatoa Macho Akionekana Wazi Kujuta Kumpakia Mtoto Yule ,Mery akajiongeza akaingiza mkono
katika sketi yake aliyevaa akatoka na elfu kumi akampa!
kijana yule akiwa katabasamu akatoa pochi na kumrudishia elfu saba
"thanks"
"naweza kukusubiri?!" akamuuliza huku akiwa katabasamu
"what did you say?"
(eti unasema?)
"mh hapa kazi ipo"
bodaboda akajisemea na kuiwasha pikipiki yake
uyoo akaondoka zake!
Mery Akatabasamu Ila Ghafla Akakumbuka Kitu! Akamgeukia Yule Kijana Na Kumpayukia Akimwita
"Hey! Hey! Hey!"
Sauti Ile Ikapaa Mpaka Katika Maskio Ya Bodaboda Yule Ambaye Alikuwa Ajafika Mbali Akageuka Nyuma Alipo
Mshughudia Binti Yule Akimjia Kwa Kasi
Akasimamisha! Kumsubiri Mery Akamfikia
"please Go to the Police station and tell them that there is problem"
(tafadhali Nenda Kituo Cha Polisi Waambie Kuna Matatizo)
"nini?!" Bodaboda Akauliza Kwa Mshangao Kuonesha Kutokumwelewa
"i Say Go Police tell them there problem."
(nimekwambia Nenda Polisi Kawaambie Kuna Matatizo?)
"duh Hapa Kaz Ipo Sijui Hata Anaongea Nini naskia tu polisi sijui anasema nikaite polisi kitu kama icho
ila ntaenda kuwa ambiaje hao polis aaah watajua wenyewe'
dereva bodaboda yule akawaza na ghafla akajibu
"ok! ok"
kama vile alimwelewa,mery Akamtabasamia
"faster Fastar I Need Police there"
(haraka Haraka Naitaji Polisi Hapa)
Bodaboda Akaondoka,kurudi Kituoni Kwake Kwanza Hakuwa Na Element Eti Ajipeleke Polisi?!
Akaachia Tabasamu Pasina Kujua Laiti Kama Angefanya Vile Angemuokoa Isack!
FUNZO
Tusidharau kitu tusichojua uzito wake!,bodaboda kapuuza pasina kujua uzito wa jambo lile!
Baada Ya Bodaboda Yule Kuondoka Mery Akiwa Na Uhakika Baada ya dakika kadhaa polisi wangewasili akakaa
chini ya kamti kamoja kusubiri askar waje!...
Mzee Alex Baada Ya Kupiga Honi Getini Pale ndo kwanza Zidu Katili Alikuwa Kawasili Muda Huo Akashuka Na
Kulifata Geti
Akafungua Mzee Alex Akaingia Na Gari Lake Mpaka Parking Akashuka Garini Kwa Furaha Wakakumbatiana Na
Zidu Katili!
"hapo Sasa Kijana Umerudi Kwenye Ubora Wako!"
"ha ha ha ha fantastic zidu haaribug kazi"
Zidu Akajitapa Akifungua Mlango Wa Nyuma Wa Gari Yake!
Naam Akamtoa Isack Ambaye Kwa Muda Ule Mtoto Wa Watu Hakuwa Na Fahamu
"ha ha ha ha ha!"
wote wakaangua kicheko!,furaha kwenye nyuso zao zikatawala!
"ntakukata kiungo kimoja kimoja ntakitafuna kwa jinsi ulivyo ntesa tu ha ha ha ha"
Mzee Alex Aliongea Kwa Furaha! Wakakabeba Katoto Kale Na Kukaingiza Chumbani
"atakiwi Kufa Akiwa Hana Fahamu Uyu Tumzindue Kwanza"
Zidu Akaongea Akimkalisha Kwenye Kiti Kilichokuwa Katika Chumba Kile Akamfunga Asiweze Kufurukuta
Akawasha Swichi Flani Iliyokuwepo Mule Ndani!
Mbona Isack Aliamka Tena Kwa Yowe!...
Ni Shoti Alikuwa Akipigwa!
Zidu Na Mzee Alex Wakawa Wakicheka Chupa Za Pombe Zikiwa Katika Mikono Yao!
Zidu Baada Ya Kuridhika Akazima Swichi Ile Akamfungua Pale Mwili Wote Ndugu Msomaji Ulivimba, awakujali
Ilo wakamfunga juu!
wakaanza kumpiga ngumi kama gunia la mazoezi zidu akimpiga usoni!,mzee alex tumboni!
damu zilimtapakaa usoni,Zidu Alimuharibu Mtoto Wa Watu Uso! Naaam!
Ni Mateso Makali Alokuwa Akiyapata Mtoto Yule Mdogo,mateso Ambayo Ayalingani Na Miaka Yake,mbele Yake
Walikuwepo Viumbe Wawili Wenye Roho Mbaya,wote Walikuwa Na Chuki Kali Dhidi Yake!
"kanaonekana Haka Katoto Kagumu Sana Kufa! Embu Ngoja"
Zidu Aliongea Akitoka Ndani Ya Chumba Kile!
Aliporejea Alikuwa Na Mikanda Miwili Ya Kijeshi!
Mkumbuke Zidu Alishapitia Jeshi Ila Kwa Utovu Wa Nidhamu Alifukuzwa Tena Siku Ya Mahafali Amri Ikitoka
Auwawe,matokeo yake wanajesh wote walokuwa wakimsaka walikufa katika mazingira ya kutatanisha mpaka
muda huo alikuwa wanted ila cha ajabu alitumika na viongoz wa juu wa serikali!
mkanda ule kila ulipotua kwenye mwili wa isack ulitoka na nyama!
wakazidi kumshambulia ghafla akatulia tuli,
"atakuwa kashakufa huyu sasa ni muda wa mamba wangu kupata chakula!"
"nice! hata mimi na uakika huo sasa ni kumkatakata vipande vipande kusudi mamba watamfune nyama yake
vizur ngoja nkachukue visu"
muda ulizidi kuyoyoma masaa yakakata hatimaye mery alichoka kusubiri,wazo likamjia aingie ndani ya lile
jumba ila je geti litakuwa wazi?!
akajinyanyua na kulifata geti lile,akawaza kugonga ila kuna kitu kikamwambia asukume kwel akasukuma
akaingia nalo!
akatabasamu!
akanyata sasa kuelekea ndan ya nyumba ile akafungua mlango wa kuingilia ndan sasa kabisa ahmadi macho
ana kwa ana na zidu!
ndo kwanza alikuwa akielekea kuchukua visu!
"wewe ni nani na unataka nini?"
zidu aliongea kwa ukali akiwa kamtolea macho mery kwa uoga akageuka akimbie zidu akachomoa bastola yake
na kuachia risas kadhaa miguuni mery akaenda chini!
milio ya risasi ndiyo ilo mshtua mzee alex mbio akaja kuona kulikon akuamin alipomuona mtoto wake akiwa
chini damu zikimchuruzika!
"zidu umenipigia mwanangu!"
"mwanao?!" zidu aliuliza akimkazia macho mery alokuwa akiugulia chini kwa maumivu!
"huyu ni mwanangu what ar u doing here mery??."
(mery umefata nini huku)
"Dad,you are a marderer "
(baba wewe ni muuaji)
"Why do you say so my doughtar??"
(kwa nini unasema hivyo binti yangu?"
"You killed isacks parents and now you want to kill him also!"
(umewaua wazaz wa isack na bado unataka umuue na yeye)
kitendo cha kusema vile tu kikabadilisha mawazo ya mzee alex
"kaijua siri yangu anaonekana yupo tofauti na mimi kaja jana tu leo anaanza kunifatilia naye aungane na
mwenzake kukiona kifo nipo tayari afe zidu fanya kazi yako"
Isack Bado Yupo Mikonon Mwa Mzee Wa Kazi Zidu Katili,
Mwanamke Pekee Alotokea Kumpenda Mery Anajitolea Kumsaidia Pasina Kujua Baba Yake Ni Hatari Kwa Kias
Gani!
Naye Kwa Bahati Mbaya Anagundulika Na Mzee Anatoa Hukumu Wote Wauwawe Je Unajua Nin Kiliendelea?!
Endelea Kuwa Pamoja Na Mwandishi Akutanabaishe
NA HII NI SEHEMU YA THALATHINI NA SITA!
Bado Mery akuamini kile kinachoenda kutokea yani baba yake mzazi anataka kumuua?!
roho ilimuuma sana ila hapakuwa na jinsi akakumbuka enzi izo wakiwa watoto wakicheza cha kimama!
"isack hivi tukiwa wakubwa utanioa kweli?"
"yah ntakuoa mery kwel nakupenda"
Akaachia tabasamu,pembeni yao alilala agnes eti ndo mtoto wao,mery akaachia tabasamu tena macho Yake
Yakimwangalia Isack Alolala Pembeni Yake Pasina Ufahamu akiwa kama mfu alosubiria haki Yake ya kuzikwa
Mwili Wake Ulikatwakatwa Kwa Kipigo
ITAENDELEA
Simulizi : Kiapo (Agano La Damu) (2)
Sehemu Ya Pili (2)
Alitia Huruma,
"As long as I will still be alive I must help you Isac, I won't let you to be in trouble unless we are
together"
(kama ntakuwa hai lazima ntakusaidia isack sitokubali nikuache uangamie tuta angamia wote)
Mery Akajiwazia
Wakati Huo Baba Yake Na Mwanaume Zidu Walikuwa Sebuleni Wakinywa Bia Na Kuzidi Kujipongeza Kwa Kazi
Nzuri Waloifanya!
"na Wazo Bosi!"
"wazo Gani"
Mzee Alex Akaongea Kilevi!
"kwa Nini Usimwache Hai Mtoto Wako Kumbuka Ile Ni Damu Yako"
"hapana Mi Sina Damu Chafu Namna Ile Sina Kabisa lazima afe"
"basi haya"
"sasa tushamtesa vya kutosha naitaji nikashughudie maiti zao zikiliwa na mamba wako ha ha ha ha"
Zidu Hakuwa Mbishi Taratibu Aka Amka Huku Wakipepesuka Wakaelekea Varanda Ya Vyumba Vya Chumbani
Wakaingia Katika Chumba Kile Kwa Mshangao Chumba Kilikuwa Kitupu
Wameenda Wapi?!
Wote Wakajiuliza Pasina Kupata Majibu
Waliwa Acha Wakiwa Hoi Je Wamepoteaje Wakaanza Kusachi Mpaka Katika Vyumba Vingine Ila Si Isack Wala
Mery Alo Onekana
Wote Walichanganyikiwa!
Pombe Ikawatoka!
Kimuyemuye Kikatawala Baina Yao!
"kamera! Washa Kamera"
Ni Kama Mzee Alex Alimshtua
Zidu,mwanaume Wa Kaz Akaiendea kamera na kuiwasha wote wakawa wakiiangalia kwa makini!
watoto wakiwa wamelala
ghafla mlango ukafunguliwa na mtu mrefu alovaa kininja akaonekana akiingia,
akaichekea kamera na kuinyooshea dole gumba ni waz mtu yule alijua juu ya kuwepo kwa kamera zile
akainyanyua miili ile akaipachika begani na kutoka nayo!
ni nani ninja yule!
"nooh kijo sitokuacha mzima ma..ni.na"
Zidu Alijikuta Akiropoka Tusi La Nguoni Likimtoka
"ni Nani Huyo kijo?"
Mzee Alex Akauliza Kwa Ukali Ila Zidu Akuangaika Kujibu
Naam Alishachafukwa Naye Akaliendea Kabati Lake Akavaa Kininja Na Kuingia Ndan Ya Gari Yake Akatoka!
Naye Mzee Alex Akiwa katika hali ya sintofahamu akaingia ndani ya gari yake na kuondoka
wote sasa furaha ziliwatoka!
Kijo! xxx
****
SURA YA KUMI NA MOJA
TURUDI NYUMA MIAKA KADHAA
"KAMBI YA JESHI ISOGA
Ni Baada Ya Miaka Miwili Kama Sheria Ya Nchi Ile Ya Kinte Isemavyo Hatimaye Shamrashamra Zilishamiri,
ila zikiwa zimebakia siku mbili kufanyika kwa mahafali sambamba na kugaiwa vyeti kambini pale pakatokea
jambo lililosta ajabisha kila mwana jeshi alokuwepo katika kambi ile!
ni kubakwa kwa kamanda wa kike Jesca Na Watu Wasojulikana!
Vijana Hao Walombaka Wawili Walivaa Kininja Kuficha Nyuso Zao!
Ila Wengi Wa Wana Jeshi Walofuzu Walifurahia jambo hilo,kamanda yule alikuwa katili asiye hata na
huruma,
kubakwa kwake kukaongeza chuki kwa wanafunzi siku mbili zikageuka mwaka!
lakini kwa kuwa masaa ayasimami siku zile zikaisha na siku ya mahafali ikawadia!
mgeni rasmi alikuwa waziri wa ulinz Kipindi Hicho Alotambulika Kama Johnsohn Chaka
John Chaka Wengi Mnazifaham Kashkash Zake Katika Riwaya Ya Shujaa Wa Kinte!
Aligawa Vyeti! Mpaka Mwisho Vijana Wawili Awakupewa Vyetu Kutokana Na Uvunjaji Wa Nidhamu!
Si Wengine Ni Mzee Wa Kazi Zidu Katili Na kijo! Hawa Ndiyo Walosemekana Walimbaka Kamanda
Wakanyang'anywa Namba pamoja na Gwanda
wakafukuzwa rasmi kambini!
majuto ni mjukuu,waliingia katika gari ya jeshi kutolewa kambini pale!
"kamanda joice alikuwa na uchungu akukubaliana na hali ile adhabu ile aliiona ndogo kifo aliona ndo
halali yao!
akaamua kuwafatilia kwa siri sana!
Zidu Na Mwenzake Tijo Baada Ya Kuwasili Mjini Wote Awakuwa Tayari Kuelekea Katika Nyumba Zao Wakachukua
Hotel!
Na Baada Ya Kukabidhiwa Vyumba Wakaelekea Club Kunywa Kupunguza Mawazo!
Usiku Sana Ndipo Walipotoka,wakarudi Zao Katika Vyumba Walivyokodisha!
Wakwanza Kuingia Katika Chumba Chake Alikuwa kijo Alishtushwa Na Teke Lililompeleka Chini!
Alikuwa Kalewa Ivyo Hata Akuwa Makini,kwa upande wa Zidu Alipofika Chumbani Kwake Akaitoa Saa Ya Mkonon
Akaiweka Mezan,
akaingiza Mkono Mfukon Akajishangaa Kujikuta Na Simu Mbili Yake Na Ya Rafiki Yake Kijo
Akaachia Tabasamu Akaiweka Nayo Mezani Akajitupa Kitandani Vilevile Na Maviatu Ghafla Simu Ya Kijo
Ikaita Akaishika Baada Ya Kuiweka Silence Tayar Kumpelekea Bado Alipepesuka!
Alipofika Mlangon Kwa Kijo Sindo Akasikia Purukushani,wasiwasi Ukamvaa Akatoa Kisu Alichokinunua Mchana
Akajiweka Tayari!
Tayari kwa lolote!
Umakin Ukaongezeka Taratibu Akaanza Kuufungua Mlango Akuamin Alichokiona Ndo Kwanza Kamanda Joice
Alikuwa Kaishika Shingo Ya Jamaa Ake Tayar kuikunja,
Zidu Akakirusha Kile Kisu Kilichokuwa Mkononi Mwake Kikaenda Moja Kwa Moja Kifuani Na Kuondoka Na Uhai
Wa Kamanda Yule!
Kijo Akuamini Alimkumbatia Rafiki Yake Kwa Furaha Pombe Ziliwaisha
"tumeuwasha Moto Yapaswa Tuondoke Hapa Haraka Jeshi Zima Litatusaka Na Sasa Tutauwawa!"
Kijo Aliongea Kwa Wasiwasi Huku Akitetemeka!
"mi Nilijua Hili Kj Tota Lini Mwanajesh Akafkuzwa Na Kuachwa Hai?! Kwa Sasa Lazima Tuondoke Hapa Nchini
Si Sehemu Salama Tena!"
"swadakta!"
Usiku Ule Ule Wakaondoka Kwenye Ile Hotel Na Kutafuta Hotel Ingine Wakalala Kama Mizoga!
Walishtuka Mida Ya Sa Nne Wakiwa Wamevaa Masweta yenye kofia wakaelekea stendi ila walishtuka juu ya
ukaguz mkali walokutana nao!
bakabaka zilitapakaa mtahani wazo walokuwa nalo wakaingia katika maduka ya nguo wakanunua nikabu na
tasbih wakafunika nyuso zao!
walionekana kama wadada au wamama wa kiislamu wakapanda magari ya nnje ya nchi mpaka nchini Tanzania
Nchi Ilosifika Kwa Kuwa Na Amani!
"Kwa Sasa Hatuna Kitu Tutapiga Kazi Gani?!"
"tumefuzu Jeshi Wametufukuza Mbinu Zote Za Kijeshi Tunazo Tuzitumie Kupata Mali Au Unasemaje?"
"ukiwa Na Maana Tuwe Majambazi?"
"yes Ofcorse"
Kwanzia Hapo Kijo Na Zidu Wakawa Majambaz Walovaa Kininja!
Wakatajirika
ila ile tamaa ilo mponza fisi ikaja kumponza na zidu akataman amilik mali zote amilikazo kijo zibaki
chini yake!,wakapanga dili wakagawana chao ila akamuunguzia mwenzake polisi na hatimaye kijo akatiwa
mbaroni!
malizote za kijo zikabaki chini ya zidu kama alivyotaka!...
kijo yule leo hii ndo aliyemuokoa Mtoto Mery Na Isack Tena Kaingia Kwenye Nyumba Yake Bila Wasiwas
Wowote Tena Kwa Kujiamin!
Aliapa Kumuua Kifo Kibaya Sana Pasina Kujua Kijo Kajipangaje!
Vita Vitani! Wanaume Wakaz Wakutana!
Nani Zaidi?!
Wakati Akiwa Ndani Ya Gari Lake Ghafla Meseji Ikaingia Katika Simu Yake!
"una Sekundi 10 Tu Za Kuishi tazama kulia kwako!,ile zidu anageuza shingo kulia kwake akaliona bomu
tena likiesabu 7,6,5,4,...
Zidu Akazidi Changanyikiwa!
Mchezo Mchezon Zidu Atakufa?,vipi Watoto Isack Na Mery Kijo Kijana Wa Kaz Kawapeleka Wapi?!
Zidu Katili Akutana Na Mbabe Wake!,kijo!,ni Mtu Amjuaye Fika Anawatorosha Mateka Wake Mery Na Isack
Zikiwa Zimebakia Dakika Chache Kabla Ya Kuwaua!
Baada Ya Kumtambua Kijo Kupitia Camera Zilizopo Katika Jumba Lake Lile Anaingia Ndan Ya Gari Lake
Pasina Kuchukua Tahadhari Yoyote Akiwa Na Lengo La Kwenda Kumuangamiza Mtu Yule!
Ghafla Akiwa Ndani Ya Gari Anatumiwa Sms Inaye Mwambia Atazame Kulia Macho Yake Ayaamin
Anapolishughudia Bomu Likimalizikia 8,7,6,5...
Hizo Ni Sekunde
NA HII NI SEHEMU YA THALATHINI NA SABA
Pale pale akusubiri kuiona 4,ghafla alijirusha kupitia dirishani na nyuma yake kukafatia mlio mkubwa wa
bomu! gari yake ilikuwa ikiteketea!,taharuki ikazagaa eneo lile!
wakati akiwa bado katika butwaa ghafla mkono wake ukatetemeshwa macho yake yalofichwa na nikabu ile
alovaa yakautazama mkono wake!,akashtuka kumbe aliruka na simu yake!
watu walimzingira wakimpa pole wengine wakimshangaa Zidu alijua lau ange endelea kushangaa pale lazima
matrafki wangemkuta pale!
akatafuta njia akaponyoka!
Baada Ya Simu Yake Kuita Kwa Muda Mrefu Pasina Yeye Kupokea Ghafla Meseji Ikaingia Katika Simu Yake!
Akaifungua!
"bila Shaka Jaribio Langu La Kwanza Umelivuka Si Kwamba Umeshinda Sikutaka Ufe Naujua Wepesi wako! ila
nlikuwa nakuweka sawa karibu mchezoni"
meseji ile ilimtia hasira Zidu!...
moyo wake sasa ukawa ukimuenda mbio!
"karibu mchezoni"
Naye akaijibu ile msg!
Zidu akuwa Mtoto Alijua Pa Kuanzia,alijua Pa Kumkamatia Kijo
akaenda katika duka la mabegi akanunua begi lile la mgongoni suruali moja ya jeans tshart na raba!
hata wale walomuuzia walijua ni mwanamke! zidu aliweza mpaka kuigiza sauti ya kike!
baada ya kukabidhiwa mzigo wake akaingia chumba cha kujaribishia akavua ile nikabu akaitia ndani ya
begi lile alonunua akavaa ile tisheti jinsi akatoka akiwa mpya!
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment