Search This Blog

Thursday 29 December 2022

CODE X 5 N.G.S.S. (NEXT GENERATION SUPER SOLDIERS) - 3

   

Simulizi : Code X 5 N.g.s.s. (Next Generation Super Soldiers)

Sehemu Ya Tatu (3)




Walimaliza kupata kifunguwa kinywa, wakatoka na kuelekea yalipo yale majokofu. “Kila kitu kitakwisha kabla ya ulimwengu kugunduwa ni kimewakuta” aliongea Michael na kutabasamu na kuangalia ukutani ambako kulikuwa na kitu kama saa kubwa sana. Juu kabisa ilikuwa na maandishi yaliosomeka “Majanga yatawakumba ndani ya miezi kumi na moja ijayo”.

Imesalia miezi kumi na moja mpaka siku ya vita.


BHGP HQ Base

Wanajeshi wote walijipanga katika mistari na kupita katika mashine maalum, mashine hiyo ilikuwa ikichukuwa vipimo vya nguo pamoja na uzito na urefu wa mwili. Zoezi hilo lilikamilika na wakaelekea katika sehemu ya huduma za afya na kuangaliwa afya zao. Baada ya hapowalikusanyika katika ukumbi wa matatngazo kwa ajili ya tangazo muhimi. Dr Anita pamoja na Dr Fred wakiwa na kikosi cha matabibu walikuwa mbele wakiongozwa jenerali wa kwanza Jeff. “Tunaokwenda kupambana nao, si wanajeshi wa kawaida. Na tulivyosasa tuna uwezekano mdogo sana kushinda. Ukiachilia hilo mpaka sasa hatujui idadi yao kamili, huenda wakawa wengi sana kuliko sisi kwasababu wamekuwa wakijipanga kwa miaka mingi sasa” alianza kuongea Jeff.


“Hivyo timu ya madaktari wetu ikishirikiana wanasayansi, wamefanikiwa kuipoza kemikali ya CODE X. Kemikali ambayo wengi munaifahamu na kuwatambuwa baadhi ya watu waliokuwa nayo katika miili yao. Kemikali hii haitafanya kazi milele, itatumika ndani ya muda maalum na baada ya hapo kila mtu atarudi kuwa kawaida” alimalizia na kumkaribisha Dr Anitha. “Kama alivyosema jenerali wa kwanza, kemikali ina lengo la kutusaidia kupambana katika vita hii ngumu iliyoko mbele yetu. Na tumeifanyia uchunguzi wa kutosha kama itakuwa na madhara kwa binadamu. Madhara tulioyabaini si ya kutiliwa maanani” alifafanuwa mpaka hapo na kusubiri kuona kama kutakuwa na swali lelote.


“Unaweza kutuambia madhara yake” aliuliza mwanajeshi mmoja, “madhara yake makubwa ni kuumwa na misuli kwasababu kemikali hii itaongeza kazi ya misuli na kuisukuma kufanya kazi kuliko ilivyozoea. Hivyo sio kwa wote ila wapo ambao watakutana na hali hiyo” alijibu na kukaa kimya kusubiria kama kutakuwa na swali jingine. “Kimya” alipoona hakuna tena swali akasafisha koo na kuendela, “Sio lazima kwa kila mtu atumie kemikali, kila ana uwezo wa kukubali au kukataa. Hatutakulazimisha kwasababu ni kinyume na misingi ya kibinadamu na kitabibu. Hivyo kabla ya kuanza huduma hii, kila anaetaka kushirikia atajaza fomu maalum ya makubaliano. Ambazo zinapatikana katika maabara zetu” alimaliza.


Mkusanyiko huwo ukatawanyishwa ila bada ya watu kuelekea mabwenini, wote wakaelekea maabara. Wanajeshi elfu moja na miasaba waliekea maabara kwa ajili ya kusaini fomu ya kujiunga na PROJECT CODE X. Jambo hilo lilipeleka tabasamu kwa viongozi wote waliokuwa wakishihudua tangazo hilo kwa mbali. “Wanaroho za wambanaji” aliongea Sup General Alex. Siku hiyo nzima ilikwishwa kwa watu kuchukuwa fomu na kurudisha.


Siku iliofuata wanajesho wote waligaiwa katika makundi matatu, makundi mawili yalikuwa watu mia tano na hamsini na moja likuwa na watu mia sita. Liliingia kundi la kwanza na kuanza taratibu, mawili yaliobakia yaliingia mazoezini kusubiri zamu yao. Baada ya mwezi mmoja lile kundi la kwanza lilitoka maabara na kuwafanya wenzao wote wakodoe macho. Walikuwa wamebadilika, miili yao iliongezeka na kuonekana kujengeka kisawasawa. Siku ilofuata kundi la pili likaingia maabara, nalo pia likatumia mwezi mmoja na kutoka na hatimae kundi la mwisho likaingia nalo likamaliza muda wake na kutoka. Miezi mitatu sasa ilikuwa imekata.


Mazoezi ya pamoja yaliendelea kuwa makali kadiri siku zilivyokwenda, majaribio ya silaha mpya zenye uwezo wa hli ya yalifanyika. Kila kitengo kilifanya kazi yake ipasavyo bila kutegea. Ndani ya mwezi mwingine mmoja katika kambo hiyo ilikuwa ni mchaka mchaka tu. Hospitali zilifurika watu waliouma mazoezini, mwezi huwo mmoja ulitosha kuwabadilisha wanajeshi na kuwa mashine za kuulia. “Sup general, nahisi sasa mazoezi ya pampja yanatosha, tuwagawe katika vikosi husika ili wazoeane kufanya kazi kwa ufasaha zaidi” alitoa wazo jenerali wa pili, Adrian. Alex akatikisa kichwa kuashiria kukubaliana nae, wakiongozana kwa pamoja, Sup general Alex na jenerali wa pili Adriana waliekea mpaka viwanja mvya mazoezi.


Jeff ambe ndie alikuwa akisimamia mazoezi hayo, alipowaona tu akajuwa kwamba kuna jambo. Akanyanyua firimbi na kupuliza, wanajeshi wote wakaacha mazoezi na kujipanga katika mistari ilionyooka. “Kwa siku ya leo mazoezi yatakuwa yamefikia kikomo, kesho tutakutana kwa ajili ya kuwatangaza makamanda na kugawana katika vikosi husika” aliongea jenerali Adrian. Baada ya tangazo hilo wakaruhusiwa kuelekea mapumziko.


“Hivi unadhani haya mazoezi alokuwa akitufanyisha jenerali wa kwanza tungekuwa tunafanya kila siku tokea tulivyoingia jeshini tungekuwaje”, “Mi nahisi ni kwasababu ya hii kemikali tu wengi tumefanikiwa, haya mazoezi ukimpa mtu wa kawaida bila shaka ataaga dunia”. “Kwani hukuwahi kusikia kama yule jamaa aliisambaratisha kambi kubwa miongoni mwa makambi ya waasi kwa usiku mmoja tu na kumuokoa mtoto wa raisi”, Kuna kamsemo fulani hivi kapachikwa wanasema, hutomuona akija bali utahisi baridi akikupita. Yaani kama mzimu vile”. “Acha utani wewe”, “mi nakwambia tena, akiwa katika mpambano utasema ni mtu mwengine kabisa” yalikuwa maongezi ya baadhi ya wanajeshi wakati wanaelekea mabwenini kupumzika.


Wakiw mabwenini waliendelea kuwachambuwa majenerali wao, “Oya! Nasikia jina la kazi Sup general ni Killer, amelipataje hilo jina” aliuliza mmoja wao akikaa kwenye kitanda. “Niliwahi kusikia kuwa kipindi yuko mdogo alipelekwa katika makambi maalum na kufanya panya wa maabara. Akiwa na miaka kati ya nane mpaka kumi na mbili, sikumbuki hasa ni miaka mingapi” aliongea mmoja wao alieonekana kuijuwa kidg historia ya Alex Jr. “Alipotoroka iliwachukuwa mwaka mzima kumkamata, na hapo aliuwa zaidi ya wanajeshi ishirini na tisa kwa mkono wake. Miaka michache mbele baada ya kurudishwa alitoroka tena na hapo ndipo alipozivuraga kambi nyingi sana za waasi. Kila alietumwa kumrudisha alirudi katika mfuko wa maiti. Na inasemekana baada ya kujiunga na jeshi la nchi yake, hakuna kazi alioshindwa kuikamilisa. Na kila alipopita aliacha mizoga ikiwa imetapakaa hovyo.”.


“Mwacheni aitwe Killer” aliongea mwengine, “na vipi kuhusu jenerali wa pili, General Adrian”. “Pia anatambulika kama Silver Fox” alidakia mtu mwengine na kuedelea, “yule ni rubani lakini pia mpelelezi aliewekwa kundi la wapelelezi bora zaidi duniani (Super Spy), akiwa katika kazi na akakamatwa anaweza kufa na asiseme kitu chochote. Inavyosemekana ndie mpelelezi aliteswa sana katika historia ya wapelelezo lakini zaidi ya kutaja jina lake na nambari ya kazi hawakuambulia kitu kingine. Alikuwa matesoni kwa zaidi ya miaka miwili lakini hakuthubutu kusema kitu. Kwa maneno mengine ni mtu mwenye kichwa kigumu kuliko yeyote duniani”.


“Yaani hii kambi imejaa watu wa ajabu kweli kweli, kuna yule Lut jeneral Charlie the beast mtu ambae hufanya sherehe akiona damu. Lut jenerali Jason CJ Jr, almaarufu kama Shadow. Kapenya kambi ya waasi kwa miaka mitatu bila kutambulika. Lut jenerali Mack, ubongo wa black hawaks. Yaani mimi hata nikifa katika hii vita nitahadithia huko kuzimu kama niliwahi kufanya kazi na majemedari wakubwa sana duniani” aliongea mwingine na kuwafanya wenzake wacheke.


Wakati wakiendelea kuongea, wakaanza kusikia minong’ono ikitokea nje. Kila mtu akataka kujuwa minong’ono hiyo ni ya nini hivyo wakaamuwa kutoka nje. Aliesababisha minong’ono hiyo alikuwa ni mwanadada, na mgongoni alikuwa na bunduki kubwa sana. Alikuwa amevaa vest yenye kombat ya kijeshi yenye mabaka baka ya aina yake. Jeff akiwa na Alex walikuwa wamesimama wakimsubiri, nyuma yao alikuwepo Charlie alionekana kutotulia. Yule bidada aliwasogelea viongozi wake na kufunga mguu kisha akapiga saluti, “Meja jenerali Jesca nimewasili baada ya kukamilisha kazi yangu” aliongea. “Karibu nyumbani Meja” aliongea Jeff. Baada ya kushusha mkno ndipo wengi wakashuhudua tattoo ya kichwa fulani cha mnyama chini kikiwa na maandishi yaliosomeka “She Beast”.

Miezi saba imebakia mpaka siku ya vita. 




Wakati wakiendelea kuongea, wakaanza kusikia minong’ono ikitokea nje. Kila mtu akataka kujuwa minong’ono hiyo ni ya nini hivyo wakaamuwa kutoka nje. Aliesababisha minong’ono hiyo alikuwa ni mwanadada, na mgongoni alikuwa na bunduki kubwa sana. Alikuwa amevaa vest yenye kombat ya kijeshi yenye mabaka baka ya aina yake. Jeff akiwa na Alex walikuwa wamesimama wakimsubiri, nyuma yao alikuwepo Charlie alionekana kutotulia. Yule bidada aliwasogelea viongozi wake na kufunga mguu kisha akapiga saluti, “Meja jenerali Jesca nimewasili baada ya kukamilisha kazi yangu” aliongea. “Karibu nyumbani Meja” aliongea Jeff. Baada ya kushusha mkno ndipo wengi wakashuhudua tattoo ya kichwa fulani cha mnyama chini kikiwa na maandishi yaliosomeka “She Beast”.

Miezi saba imebakia mpaka siku ya vita.


“Umemlea vizuri mwanangu” aliongea Charlie akimsogelea Jesca, “mbona yuko vizuri sana, amechukuwa roho kama hamsini hivi” alijibu Jesca na kuuvuta mbele mtutu uliokuwa unaning’inia mgongoni kwake. Akamkabidhi Charlie, “nambie eti ni kweli umechukuwa roho zote hizo peke yako” aliongea Charlie na kuusogeza mtutu huwo sikioni na kufanya kamavile anausikiliza. Kisha akatabasamu na bila kuongea kitu akaondoka eneo hilo. Jesca nae akafuata nyuma na kila mtu akatawanyika isipokuwa Jeff peke yake. Alikaa eneo hilo dakika kadhaa kisha akatikisa kichwa na kuondoka pia.

*********************************

Martina na kikosi chake cha wataalamu wa mtandao walikuwa katika chumba maalum, Talbot nae alikuwemo humo humo na muda wote alionekana akitabasamu. Dakika tano baadae; Alex, Jeff na Adrian wakiongozana na maluteni jenerali pamoja na meja jenerali Jesca waliwasili katika chumba hicho. “Baada ya hesabu nyingi sana na kazi kubwa, hatimae tumefanikiwa kutengeneza mfumo mpya wa ulinzi wa kimtandao” aliongea Martina na kutabasamu kisha akaendelea “unaitwa Octagonal Penta Case Cyber Shield (OPCCS)”.


“Mfumo huu ni wa kipekee duniani na utaizunguka kambii hii kwa umbali kilometa nzima katika pande zote. Hautakuwa mfumo wa ulinzi wa mtandao tu bali utahisi kila kitu kitakachopita katika kilometa hiyo” alimaliza kuongea na kuwaangalia wenzake saba waliokuwa wamesimama katika maeneo maalum. Kila mmoja alikuwa na ufunguo mkononi, “sasa tutachomeka funguo” aliongea na wote wakafanya hivyo. “Kwa pamoja tutazungusha funguo hizo ndani ya tatu, mbili, moja” kwa pamoja na usahihi wa hali ya juu funguo zikazungushwa. “OPCCS is online” kompyuta ikaongea, “All missiles are ready to fire” iliendelea.


Kwa pamoja wakapiga makofi na kupongeza kikosi hicho kilichofanya kazi kwa jitihada zote kuhakikisha hilo linafanikiwa. “Katika kila upande upande kuna vifaa maalum ambavyo vitakuwa vikinyonya sauti itakayosababishwa na mlipuko wowte ule. Hivyo hata raia hawatosikia mlipuko katika upande huu” aliongea Talbot. “Nitegemee nini tena kwa bingwa wa tehama ya kisasa” aliongea Jeff na kumpongeza. “Siku ya kesho kila mwanajeshi atapigwa muhuri ambao mfumo huu utamtambuwa na hivyo hautamshambulia” aliendelea, “Je, huu mfumo hauwezi kushambulia chochote badala ya binadamua” aliuliza CJ.


“Luteni jenerali umewahi kusikia mfumo wenye akili, basi ndio huu. Nimeuprogramu kwa kutofautisha binadamu na kiumbe mwengine yeyote, isipokuwa kama utahisi kuwa kiumbe amebaba kitu hatari” alijibu Talbot. Hakuna aliuliza tena swali maana majibu yote yalikuwa wazi na kila mtu aliamini katika uwezo wa watu hao. “Jeff, unajuwa serekali huko duniani zikitambuwa una watu hawa zitakufanyia vurugu” alitania Adrian. “Wasije wakanijaribu, hawa unaowaona hapa wote ni wapole”, “Acha utani Jeff, unataka kunambia Charlie pia ni mpole”. “Ndio” alijibu Jeff na kutoka katika chumba hicho, wengi walidhani ni utani lakini machoni mwa Adrian na Alex walitambuwa kuwa kuna mwengine ambae hata wao hawamtambui.


Siku iliofuata mapema wanajeshi wote walikusanywa kwa ajili ya mihuri, wakiwa katika uwanja huwo kwa ajili ya hilo. Katika vioo maalum kuliwashwa maruninga makubwa yaliyoonesha eneo la juu la kambi hiyo ambalo lilikuwa na mitambo mizito sana ya kivita. Wakati wakiendelea kupata mihuri, ghafla vioo hivyo vikaanza kumwesa mwesa rangi nyekundu huku vikionesha neno “Alert”. Alifika Martina akihema, “kuna mtu ameingia ndani ya kilometa moja” aliongea. “Hakuna haja ya kupeleka wanajeshi, jaribuni mitambo” aliongea Sup General Alex. “Ay” aliitika na kutoa kitu kama simu mfukoni, akabonyeza nambari kadhaa na kutuma.


Ghafla vile vioo vikaanza kumuonesha mtu aliekuwa kavaa kofia kama zile za cowboy, alikuwa amevaa vest ya kijivujivu na shingoni alikuwa na cheni iliokuwa na fuvu lenye mapembe ya ng’ombe. “Jitambulishe” alisikia sauti akiwa kasimama anashangaa, akashusha pumzi na kutabasamu na kuonesha kidole cha kati. Risasi zikaanza kumiminwa kwenye bunduki maalum, ajabu ni kwamba risasi hizo pamoja na kuwa na kasi zilimkosa. Mashambulizi yaliendelea kwa dakika kumi bila mafanikio yeyote yale, kila mtu aliekuwa anashuhudia jambo hilo alibakia kinywa wazi.


Kwa mbali wakaanza kusikia hatuwa zikija upande wao, wanajeshe kadhaa wakavuta mitutu yao na kujiweka sawa. “Tulieni” ilisikika sauti ya Jeff na wote wakatii, taratibu akaanza kupenya katikati ya wanajeshi hao huku akivuwa gwanda yake ya juu. Mwili wake mkubwa uliojengeka kisawasawa uliwashangaza wengi ambao hawakuwahi kumuona bila gwanda. “Unaonekana una kiburi sana kuingi hapa bila mualiko” aliongea na kusimama.


“Nipate mwaliko kwani hapa kuna sherehe” alijibu mtu huyo na kusimama mita kadhaa kutoka aliposimma Jeff. Bila kuchelewa Jeff akafyetuka kama mshale na kumvaa, yule jamaa akakwepa mashambulizi yote na kupiga sarakasi ya nyuma. “Inaonekana umejinowa vya kutosha” aliongea na kuvua begi lake. Akaliweka chini na kujipanga kwa kufanya mashambulizi, hatuwa tatu tayari alikuwa mbele ya Jeff jambo ambalo hakuwa amejiandaa nalo. Makonde kadha yalirushwa lakini Jeff pamoja na kutokuwa tayari aliyakwepa huku kadhaa yakimkosa kosa.


Baada ya dakika tano za mpambao huwo Jeff akajikuta akiingia kwenye anga za kijana na kuchezea makonde manne makali sana kwenye kifuwa. Hilo likawashtuwa wengi mpaka Charlie akataka kuingilia lakini akazuiwa na Alex. Yule kijana akarudi nyuma hatuwa kama sita hivi, akafunga mguu na kupiga saluti kisha akaongea, “Supreme commando Kelvin Bull, nimerudi baada ya kukamilisha mafunzo yangu”. “Karibu nyumbani komredi” aliongea Jeff na kuipokea saluti hiyo, “ila chief unazeeka sasa” aliongea na kutabasamu.


“Nina kitu nimeambiwa nikukabidhi” aliongea na kufunguwa begi lake akatoa kitu chenye rangi ya dhahabu, alitoa pia na bahasha. Aliifunguwa ile barua kwa ajili ya kuisoma ila Jeff akamzuia na kumgeukia Alex kuomba ruhusa. Alex akatikisa kichwa kuashiria kukubaliana nae, akamgeukia Kelvin kumwambia aisome.


“Ni kwa uzalendo na moyo wa kujitolea, umelitumikia taifa hili katika kila hali bila kuweweseka na kile unachokiamini. Umepitia vikwazo na misuko suko mingi, lakini hukuvunjika moyo ukaendelea kulitumikia taifa hili kwa moyo mkunjufu. Mimi Alfred Jackson ninavua cheo changu cha Chief Supreme General Commando na kukukabidhi, kitumikie mpaka mwisho wa uhai wako. Nawe ulieteuliwa utaandika kama hivi na atateuliwa mwingine baada ya kifo chako. Chief General Supreme Commmando Alfred Jackson, jina la kazi ni DEATH”


Kelvini alimaliza kuisoma baruwa hiyo na kumvisha Jeff cheni maalumi yenye mchoro wa dhahabu wa duni ulozungukwa na nyota tisa. Hapo sasa Jeff alipanda cheo na kufikia cheo cha juu kabisa cha jeshi katika nchi hiyo ambacho baada ya Alfred Jackson (Death) hakuna mwengine aliekichukuwa. Jeff aliwageukia wanajeshi na wote mpaka Alex wakafunga mguu na kupiga saluti. Akaipokea na kutabasamu kisha akamgeukia Kelvin ambae alikuwa amesimama kama mlingoti. “Kwa mamlaka ya jeshi niliokuwa nayo, Mimi Jeffery Alfred Jackson, Chief General Supreme Commando. Ninamuapisha Supreme Commando Kelvin Bull kushika cheo cha General Supreme Commando chini ya jina la GHOST. Hivyo kuanzia sasa atatambulika kama General Supreme Commando Kelvin, jina la kazi GHOST.” Alimaliza. 




Kelvini alimaliza kuisoma baruwa hiyo na kumvisha Jeff cheni maalumi yenye mchoro wa dhahabu wa duni ulozungukwa na nyota tisa. Hapo sasa Jeff alipanda cheo na kufikia cheo cha juu kabisa cha jeshi katika nchi hiyo ambacho baada ya Alfred Jackson (Death) hakuna mwengine aliekichukuwa. Jeff aliwageukia wanajeshi na wote mpaka Alex wakafunga mguu na kupiga saluti. Akaipokea na kutabasamu kisha akamgeukia Kelvin ambae alikuwa amesimama kama mlingoti. “Kwa mamlaka ya jeshi niliokuwa nayo, Mimi Jeffery Alfred Jackson, Chief General Supreme Commando. Ninamuapisha Supreme Commando Kelvin Bull kushika cheo cha General Supreme Commando chini ya jina la GHOST. Hivyo kuanzia sasa atatambulika kama General Supreme Commando Kelvin, jina la kazi GHOST.” Alimaliza.

******************************************

Sehemu isiojulikana.

Katika chemba iliokuwa na majokofu, Michael na Alice walikuwa peke yao wakiendelea na taratibu za kuiamsha miili iliokuwemo kwenye majokofu yaliokuwepo eneo hilo. “Hatua ya kwanza imekamilika” aliongea Michael na kuweko laptop yake mezani, “Vipi kuhusu dhana zetu za kivita” aliuliza. “Mpaka sasa hivi kuna karibu tani nzima ya silaha za moto, ziko njiani na kikois chetu maalum. Zitaingia kesho au kesho kutwa. Pia kikosi chetu za mafundi mekanika kinakamilisha kifaru cha hamsini pamoja na ndege sabini za kivita” aliongea Alice.


“Bado ni kidogo, vifaru hamsini na ndege sabini, wale wapuuzi nina uhakika wana vifaru zaidi mia mbili na ndege mpaka hawajui idadi” aliongea Michael. “Sio kama ni kikosi kizima, laa. Kambi hii tu, kuna kambi nyingine thalathini zinafanya kazi usiku na mchana kutengeneza vifaru na ndege ulimwenguni kote” baada ya kuona Michael amekereka akarekebisha kauli ambayo ilipokewa vibaya. “Ngoja, ukiachia hawa wanajeshi wa kwenye majokofu. Tuna wanajeshi wangapi kwa jumla” aliuliza Michael.


“Nilikuwa nakusubiri uniulize swali hilo, sisi tuko wengi sana kiasi kwamba itawabidi kila mwanajeshi wao mmoja apigane na wanajeshi wetu kama kumi hivi ili wajihakikishie ushindi” alijibu Alice. “Nipe namba kamili, sijasema unitabirie mwisho wa vita hii” alifoka Michael. Jambo hilo lilimshtuwa sana Alice maana hakuwahi kufokewa na Michael hata mara moja. “Tuna jumla ya wanajeshi elfu nane” alijibu kama swali lilivyotaka, “vizuri sana, nauona ushindi ukiwa mlangoni tu hapo” alifurahi Michael.


Wakiwa wanaendelea kujadili, simu ya Alice ilianza kuita. “Kuna nini? Nimesema nisipigiwe simu kama si jambo la msingi sana” aliipokea na kufoka. Lakini akajikuta akiishiwa nguvu baada ya kupokea taarifa zilizomshtuwa. Akakata simu na kuirudisha mezani kisha akavuta kiti na kukaa, “Alice mbona ghfla umepauka” aliuliza Michael. “Kambi zetu mbili zilizokuwepo jangwa la Sahara barani Afrika, kambi ya Madagascar, Antatika na ya visiwa vya Indiana Marekani zimesambaratishwa” aliongea kama vile mtu aliekuwa haamini alichokisikia. “Ah zisikuumize kichwa hizo, kambi tano tu si tatizo sana” Michael alionekana kutokujali.

“Michael, una nini lakini. Unajuwa hizo ni kambi kubwa na ndio zenye wanajeshi wengi zaidi kuliko kambi zozote zile. Taarifa ni kuwa hakuna hata mmoja alieokoka. Tumepoteza wanajeshi elfu tatu, unadhani ni jambo la kupuuza” alifoka Alice na kumfanya Michael aache alichokuwa anakifanya na kumgeukia mwanamama huyo ambae anaonekana ni binti mdogo. “Alice, wanajeshi elfu tano wanatosha kuifanya kazi hii hivyo usiwe na wasiwasi” aliongea kwa sauti ya kubembeleza. “Kwanini tusifanye mashambulizi na sisi” alifoka Alice na kuonekana kuwa na hasira kupira maelezo.


“Tunashambulia wapi sasa” aliuliza Michael, “si tunajuwa kambi yao ilipo” alijibu. “Unadhani wanakischaa kubakia pale, kweli umemdogosha Jeff. Miongoni mwa vilivyoshindikana duniani, hicho ni kimoja wapo. Kama sisi tunategemea jeshi kufanya mapinduzi, Jeff angefanya peke yake. Amepewa mafunzo ambayo binadamu wa kawaida hawezi hata kuyafikiria, yule ni mashine ya kuulia. Ukiachia huyo wana kichwa kingine Martina, leo nikipata nafasi ya kumuuwa kati ya Jeff na Martina basi ningeuwa Martina. Tukifanya mashambulizi sasa hivi, hii vita itakuwa imeisha kabla haijaanza. Na katika ile kambi walishahama kitambo sana, wako ziwa Tara. Na huko hayuko peke yake, yupo na Alex Jr pamoja na yule mwendawazimu Adrian. Kama mpaka sasa unadhani unawaweza nakuruhusu kafanye mashambulizi lakini usirudi hapa umefyata mkia katikati ya mapaja” aliongea Michael na kuendelea na kazi yake.


“Umejuaje kama washahama pale na umejuaje kama ameungana na hao wawili” aliuliza Alice kwa shauku ya kutaka kujuwa. “Kumbuka mimi ni Michael mwanadamu mwenye akili zaidi duniani na pia nina vyanzo vyangu vyaa taarifa ulimwenguni kote. Pamoja na kuungana kwao hawana idadi kubwa, sidhani kama wanafika hata elfumbili. Hivyo wanajeshi elfu tano wanatosha kuwaangamiza” aliongea kwa kujiamini. “Sawa kama ni hivyo lakini nahisi unawaangalia kwa jicho la kitoto, husema mtoto anacheza mpaka pale atakapokupiga teke katikati ya miguu ndio utajuwa kama alikuwa anajaribu kukuumiza kupitia sehemu ndogo usioitegemea” alingia Alice kwa mafumbo kidogo na kumuacha Michael.

*******************************************

“Kepten, amri imetoka tuelekee kambini” aliingia katika pango mwanajeshi mmoja na kuongea, “ah! Jenerali ana nini nae, ndio kwanza sherehe ilikuwa inanoga” alijibu kepten na kutema kijiti kilichokuwa mdomoni. “Tutaondoka kesho kutwa, amri imetoka kutoka kambi gani?” aliongea na kuuliza, “tumetumiwa kodi na nahisi ni kutoka nchini RDC” alijibu. “Oooh! Ukiona tu yuko huko ujue kuna jambo kubwa linakwenda kutokea, siwezi kusubiri kuona nini kitatokea” aliongea akimeza funda kubwa la mate kama mtu aliahidiwa chakula kitamu sana.


“Kepten, kwanini kesho kutwa wakati tunaweza kuondoka kesho”, “sasa tumekuja huku kufanya nini, tumesafiri kutoka Afrika mpaka huku halafu tuondoke bila kufanya chochote” aliongea na kukunja sura. “Lakini tumeangusha kambi nne tayari zinatosha”, “katika ulimwengu huu hakuna kitu kinachotosha, hata ukila unatamani uendelee kula mpaka uhisi kutapika. Na ikiwezekana unatapika tu unaendelea kula” alijibu mtu huyo alieonekana kuwa shetani katika mwili wa binadamu.


Full throttle Squad (FTS) kikiongozwa na kepten Ken kilikuwa visiwa vya indiana, kikosi hicho cha watu wa tano kutoka kikosi kikubwa cha The Pirates kilipewa kazi hiyo na Gold Prime General Alex. Kwa miaka sita sasa kimekuwa kazini kutekeleza amri ya mkuu wao, nayo ilikuwa ni kuzisaka kambi za waasi popote zilipo duniani na kuzingamiza. Ndani ya miaka hiyo wamevuruga kambi zaidi ya kumi na saba amabzo zilikuwa chini ya jenerali David.


Miezi minne nyuma walipata taarifa kuwa kuna kambi nyingine kubwa ambazo hazikuwa chini ya jenerali David. Waliamuwa kufanya uchunguzi na kuzibaini chache, na kwasababu hawakupewa masharti yeyo ya kazi yao wakaamua kuziangamiza. Walizitambuwa kambi tano kubwa zilizobeba nembo ya waasi na kuamuwa kufanya kile walichoagizwa miaka sita nyuma. Kambi walizovuruga mpaka wakati wanapokea ujumbe zilikuwa ni mbili za jangwa la Sahara, Madagascar na Antaktika, wakati huwo walikuwa visiwa vya indiana nchini Marekani kwa ajili ya kuiangamiza kambi ya eneo hilo.


Siku ya pili mapema waliingiakazini kumalizia kazi yao ya mwisho kabla ya kuelekea walipoitwa, “Gulam utakaa mita mia nane, hakikisha unaondoa vichwa ndio nitakulipa” aliongea kepten Ken. “Nimekusoma kepten, ila ujue kila kichwa dola mbili na mpaka sasa nishapasuwa vichwa thamanini” alijibu Gulam, mdunguaji wa kikosi hicho. “Sawa, wengine mtanifata kuelekea kambini. Utauwa kil kitakachopita mbele yako, ukisita nakuuwa wewe” aliongea kepten Ken a.k.a Hunter. Walivamia kambini humo na kuisambaratisha yote ndai ya nusu saa tu. Baada ya hapo walirudi katika pango walilofanya kuwa ni makazi yao ya muda mfupi na kuanza kujipanga na safari.


“Kepten, nimefikisha vichwa mia” aliongea Gulam na kumkabidhi kepten Ken maganda ya risasi alizotumia. Yalikuwa ishirini tu hayakuzidi wala kupunguwa, Gulam hakuwa kupoteza risasi. Kila risasi aliopiga ilifika ilipokusudiwa na kufanya kazi yake. Katika kazi zake zote ni watu wachache sana aliowatandika kifuani. Wengi alisambaratisha vichwa, hiyo ndio sehemu alioamini kuwa mdunguaji wa kweli anatakiwa kudunguwa. Kepten Ken alitoa dola miambili na kumkaidhi kama walivyokubaliana, Gulan alizipokea na kuonesha dole gumba. Siku ilofata walikusanya virago vyao na kutoweka katika visiwa hivyo wakiacha harufu za damu tu na mizoga.

Miezi minne mpaka siku ya vita





“Kepten, nimefikisha vichwa mia” aliongea Gulam na kumkabidhi kepten Ken maganda ya risasi alizotumia. Yalikuwa ishirini tu hayakuzidi wala kupunguwa, Gulam hakuwa kupoteza risasi. Kila risasi aliopiga ilifika ilipokusudiwa na kufanya kazi yake. Katika kazi zake zote ni watu wachache sana aliowatandika kifuani. Wengi alisambaratisha vichwa, hiyo ndio sehemu alioamini kuwa mdunguaji wa kweli anatakiwa kudunguwa. Kepten Ken alitoa dola miambili na kumkaidhi kama walivyokubaliana, Gulan alizipokea na kuonesha dole gumba. Siku ilofata walikusanya virago vyao na kutoweka katika visiwa hivyo wakiacha harufu za damu tu na mizoga.

Miezi minne mpaka siku ya vita.


Sehemu isiojulikana.

Taratibu majokofu yalianza kufnguka, watu waliokuwemo kwenye majikofu hayo wakaanza kuamka mmoja baada ya mwengine. Macho yao hayakuonesha kabisa kama watu hao walikuwa na uhai bali walikuwa kama mashine tu zinazongojea maelekezo. “Sasa ni muda wa kuwaamsha makamanda wa tano” aliongea Michael na kutabasamu, kisha akabonyeza kitufe kwenye kompyuta yake na yale majikofu matano yakaanza kufunguka. Ndani ya majokofu hayo walitoka watu watano waliojazia kisawasawa.


Wakati watu waliotoka kwenye majokofu wakiendelea kusimama bila kujuwa, “karibuni majemedari wangu” walisikia kutoka kwenye kipaza sauti na wote kwa pamoja wakageuka upande ambao kilikuwepo kipaza sauti. Juu kabisa kulikuwa na chumba kilichotengezwa kwa vioo tu na humo ndimo alimokuwa Michael na Alice. “Hawa wanapokea amri kutoka kwangu tu, katika akili zao nimeprogram kuwa mimi ndie kiongozi wao na watafuata amri zangu tu tena zitakazotoka kinywani mwangu” aliongea Michael. “Umewezaje kufanya hivyo?”, “Nimeweka kifaa maalum maalum katika bongo zao ambacho nimekitengeza kugundua muundo na mawimbi ya sauti yangu”.


“Umewezaje kuweka wakati muda mwingi tulikuwa pamoja?”, “mimi nimetengeza tu, kifaachenyewe ni kidogo sana kiasi kwamba hata kukiona kwa macho ni shida. Nimekipa jina la MIND NANOMICROBOT, kisha nikakiingiza kwenye mipira iliokuwa inapeleka kemikali katikaa miili yao. Na kila kimoja nimekifanya kiende kwa mtu mmoja hivyo hakuna mtu ambae amepata zaidi ya kimoja. Na vilipoingia katika miili yao nikaviwasha na kwasababu niliviprogramu viende kwenye ubong, baada ya kuviwasha vikahamia kwenye ubongo na kuweka makazi yake huko” aliongea kwa mapana zaidi Michael.


Hapo Alice sasa akaanza kuhisi kuwa anafanya kazi na mtu asie wa kawaida kabisa, Michael sasa alikuwa akianza kuonesha makucha yake. Michael ambae amekiuka sheria za asili na kuendelela kuishi hata baada roho yake kuachana na ulimwengu wa binadamu. Na swali lililokuwa likimtesa Alice ni kutojuwa sababu ya nini kilichomsukuma mwanaume huyo mpaka akafikia hapo. Michael ni nani, nini chanzo cha yeye kufika hapa leo, je ni kweli binadamu kama anavyosema au akili feki iliotengezwa kwa ajili ya kukamilisha kazi ambayo haikukamilika. Hayo yalikuwa ni baadhi ya maswali yaliokuwa yakizururra ndani ya kichwa cha Alice.


“Ukiacha nyinyi watano mlosimama pamoja, waliobaki wote elekeeni sekta A kwa ajili ya kuchukuwa gwanda zenu” aliongea Michael na wote isipokuwa aliowazuia wakaelelea upande waliombiwa na kuanza kuchukuwa na kuvaa. “Nyinyi watano elekeeni sekta B, huko myakuta nguo zenu” nao wakafanya hivyo na kuelekea walipoambiwa. Ni kama waliwahi kuwa katika eneo hilo lakini ukweli ni kwamba ramani nzima ya chumba hicho ilikuwa vichwani mwao na hiyo ilikuwa ni maajabu mingine ya Michael.


Wale watano walioelekezwa kuelekea sekta B walikuta nguo zilizokuwa kwenye mabeseni maalum yaliokuwa na majina. “Waangalie kwa makini” aliambiwa Alice nae akakaza macho, kwa sekunde kadhaa walisimama na kuyaangalia mabeseni hayo kama waliokuwa wakivuta kumbukumbu fulani. “Zangu zilie pale” aliongea mmoja wao na kunyoosha mkono kwenye beseni lililokuwa na jina la Matvei. Na kweli mtu hakuwa mwengine isipokuwa Matvei mwenyewe, japo alikuwa ni kivuli tu cha Matvei halisi lakini alikuwa na kumbukumbu zote. Alfred Jackson hakuongea bali alisogea mpaka kwenye beseni lililokuwa na jina lake na kuchukuwa nguo zake.


Na waliobaki kila mtu alifanya hivyo na hakuna hata mmoja aliekosea, “lakini hawa watu baadhi si wana uadui?” aliuliza Alice. “Alice nilipokwambi nitakuwa Mungu katika hii dunia ulidhani nakutania” aliongea Michael pasi na kujibu swali aliloulizwa na kumuangalia Alice. “Nilivumbuwa programu nyingine, inaitwa MEMORY OVERRIDE. Kupitia programu hii nimetengeneza kumbukumbu mpya na kuzisajili katika bongo zao. Pia kupitia programu hiyo hiyo nimefuta kumbukumbu zote za uhasama kati yao, si hivyo tu bali nimewafanya wasikumbuke chochote kuhusu familia zao wala maisha yao kabla ya vifo kuwakuta. Baada ya hapo nikawapa zawadi ya kifamilia na kuwafanya wajuane kama familia moja tu waliokuwa wakiishi tokea watoto na wote kuwa na ndoto moja tu. Ipo siku watafanya mapinduzi na dunia watanikabdhi mimi.” Aliongea na kucheka kwa nguvu.


Kama uliwahi kusikia kuwa shetani wapo miongoni mwa binadamu basi Michael alikuwa ni miongoni mwao. Katika maneno yake yote hakukuwa na la mzaha hata moja na alionekana kufanya mambo yake kwa umakini zaidi kuliko hata Alice alivyokuwa anafikiria. “Nimenyanyua mikono” alijisemea Alice na kumuacha nguli huyo ambae si tu alikuwa akiwapinga binadamu bali aliingilia mpaka majukumu ya kiungu.


Saa chache baadae.

“Matvei, umekamilisha mpango kazi” aliongea Alfred Jackson akikaa kwenye kiti chake, “ndio umekamilika na kila kitu kinakwenda kama tulivyokubaliana siku chache nyuma” alijibu Matvei. “Mimi baada ya kufanya uchunguzi wangu nimesikia kuwa kuna watoto wa juzi wanataka kutuzuia tusafanye kazi yetu” aliingilia Jason CJ Sr, “ah! Jeff na Alex au” na Alex Sr hakuwa nyuma. “Ndo hao nainavyoonekana wamejipanga kisawasawa kutukabili” aliongea Jason CJ Sr, “achana nao, hao paka wa juzi wanataka kujifanya wajuaji katika kiota cha chui. Pindi watakapotukabili tu watakuwa wameingia katika harakati za kuvisaka vifo vyao” Alfred Jackson aliwakatisha.


“Pia nimesikia kuna mdunguaji wao ana hatari, wenyewe wanamuita Beast” aliongea Alex Sr, “hahaha! Huyo niachieni mimi, nitamshuhulikia” aliongea Andrew Cross aliekuwa kimya muda wote. Ndani ya chumba hicho walikuwa watu watano hatari sana, walikuwa wakipanga mipango ya kivita kwa ajili ya kuwakabili wale wanaotaka kusimama katika njia yao. Alfred Jackson, jina la kazi Death; Matvei, jina la kazi Barseker (mwanda wazimu); Jason CJ Sr, jina la kazi Machine Gun (MG), Alex Sr, jina la kazi Mr Nobody na Andre Cross, jina la kazi Target.


Kila mmoja ndani ya chumba hicho alikuwa na historia yake ambayo ilimpatia jina alilokuwa nalo. Na pia kila mtu ndani humo alikuwa ni fundi wa kile anachokifanya. Watatu kati yao walikuwa katika kikosi kimoja enzi za ujana wao, kikosi hicho kiliitwa Tsunami. Kila kilipopita kiliacha maafa makubwa sana, watu hao ni Alfred Jackson aliekuwa nahodha wa kikosi hicho, Matvei aliekuwa mwanamipango na Andrew Cross aliekuwa akifanya kazi na Zack Smith kama wadunguaji wa kikosi hicho. Jumla kikosi hicho kilikuwa na watu watano. Ukiachia hao wanne hapo juu, watano alikuwa ni Abykin Dos Santos Jr au kifupi alitambulika kama Aby Jr na jina lake la kazi lilikuwa ni Chaos. Yeye alikuwa mvamizi wa kambi na kusababisha tafrani na wenzake walikuja kumaliza.


Jason CJ Sr alikuwa mpelelezi wa juu kabisa (first Grade Senior Investigator (1GSI)) katika kitengo cha siri cha FDP nchini Marekani. Na yeye ndie alikuwa mtu wa kwanza kugunduwa mbinu za waasi nchini marekani ambayo kwa namna moja au nyingine ilichangia kumsukumia kaburini kwake. Mbali na kuwa mpelelezi alikuwa bingwa katika mapambano ya karibu (close Combat), bingwa wa kutumia silaha za moto na mdunguaji wa masafa ya kati. Akiwa kazini alitambulika kama jeshi la mtu mmoja na hatimae akapichikwa jina la Machine Gun (MG). Mzunguko mmoja watu zaidi ya saba waliamguka na kuaga dunia, alikuwa ni nguvu ya kutambulika na siku zote alifanya kazi kwa umakini bila kucha ushahidi wowote umpite.

Mwezi mmoja mpaka siku ya vita.




Jason CJ Sr alikuwa mpelelezi wa juu kabisa (first Grade Senior Investigator (1GSI)) katika kitengo cha siri cha FDP nchini Marekani. Na yeye ndie alikuwa mtu wa kwanza kugunduwa mbinu za waasi nchini marekani ambayo kwa namna moja au nyingine ilichangia kumsukumia kaburini kwake. Mbali na kuwa mpelelezi alikuwa bingwa katika mapambano ya karibu (close Combat), bingwa wa kutumia silaha za moto na mdunguaji wa masafa ya kati. Akiwa kazini alitambulika kama jeshi la mtu mmoja na hatimae akapichikwa jina la Machine Gun (MG). Mzunguko mmoja watu zaidi ya saba waliamguka na kuaga dunia, alikuwa ni nguvu ya kutambulika na siku zote alifanya kazi kwa umakini bila kucha ushahidi wowote umpite.

Mwezi mmoja mpaka siku ya vita.


Kabla hatujaendelea, tumtazame Alex Sr na kwanini ameitwa Mr Nobody.

Turudi miaka mingi sana nyuma.


Alex Jr miaka minne na Alex Sr miaka sita, wote wakiwa ndani ya ndege pamoja na watoto wengine wakielekea wasipopajuwa. “Kaka mi naogoapa” aliongea Alex Jr, “unaogopa nini wakati kaka ako nipo” alijibu Alex Sr na kumfuta machozi mdogo aliekuwa akilia tokea mwanzo safari mpaka kamasi zikawa zinaning’nia puani. “Kwani baba yupo wapi” aliuliza Alex Jr, “sijui ila wametuambia ametoa maelekezo kuwa kama hatarudi tuchukuliwe na rafiki yake jenerali David”. “Kwa hiyo unamaanisha baba hatorudi tena” aliongea Alex Jr na kuanza kuanguwa kilio upya.


“Atarudi tu, inawezekana kazi ikachukuwa muda kidogo kukamilika” Alex Sr alijibu lakini moyoni alikuwa akilia. Alifahamu kabisa kuwa baba yao hatorudi tena maana barua aliopewa na jenerali David iliandikwa kwa herufi kubwa nyekundu “DIED IN ACTION” (amekufa kazini). Lakini kwa wakati huwo Alex Jr alikuwa mdogo sana kuelewa kilichotokea hivyo akaona njia ya kumtuliza ni kumdanganya tu. “Usijali, tena akirudi kasema atakulea ile bunduki unayoipenda kuliko zote” aliongea na kumfanya mdogo wake akenue meno na kuonesha mapengo kadhaa ya meni ya mbele.


Wakati wakiendelea kuongea jenerali Davidi alikuwa mbele yao na alisikia kila, alitabasamu na kuongea “usijali Alex mdogo, baba ako kasema mukae na mimi kwa kipindi kifupi tu. Akirudi kutoka kazini atakuja kuwachukuwa” na kutabasamu. Alex Sr alilazimisha tabasamu ili kumshawishi mdogo wake akubali uongo huwo. “Sawa” aliitika Alex Jr na kumuegemea kakaake, furaha ilionekana kurudi usoni mwake na ile hofu yote ilipotea. Baada ya safari ndefu hatimae ndege ilianza kushuka lakini kabla haijakanyaga ardhi, moshi mzito ulitanda ndani ya ndege na kuwafanya watoto wote walale.


Walikuja kushtuka wakiwa ndani ya vyumba maalum, na milango ilikuwa imefungwa. Alex mkubwa alimvuta mdogo na kumkumbatia maana alifahamu pasi na kufanya hivyo kianguka kilio kingine humo ndani ambacho ingekuwa kazi kukizima. Alex alikuwa mtoto wa kulia mno, jambo dogo alimwaga machozi kama maporoko ya maji. Alikuwa tofauti kabisa na Alex mkubwa ambae alionekana kuwa mkakamvu na mvumilivu zaidi japo umri wake haukuwa mkubwa.


Baada kama dakika kumi mlango ulifunguliwa na watu waliovalia nguo kama zile za zima moto waliingia mikononi wakiwa na mpira mnene kiasi wa maji. Alieushika mpira huwo, alifanya ishara fulani na ghfla mpira huwo ukaanza kurusha maji yaliokuwa ya baridi sana. Watoto wote waliokuwemo kwenye vyumba hivyo walirowesha na kutokana na maji hayo kuwa ya baridi mno. Hazikupita hata sekunde ishirini walianza kutetemeka. Kuna baadhi walianguka na miili kuonehsa kupauka kabisa. Baadi ya watu waliokuja na ndani ya chumba hicho walwasogelea na kuwagusa shingoni kisha wakafanya kwa kupitisha mkono kooni wakiwa na maana watoto hao wamefariki tayari.


Alex mdogo alitetemeka sana mwisho akaanguka chini na mwili wake ukaanza kupauka. Bila kufikiria mara mbili, Alex mkubwa alimvua viatu na kuanza kumsugua unyayoni. Aliendelea kumsuguwa unyayoni kwa takriban dakika tano. Taratibu Alex mdogo alianza kufumbuwa macho, baada ya zoezi hilo Alex mkubwa alishusha pumzi ndefu na kutabasamu. Watu waliokuja na mpira wa maji walitoka, waliingia watu wengine waliokuwa na mablanketi makubwa. Walifanika watoto waliobakia kuwatoa katika vyumba vilivyokuwa na maji ya barid.


Watoto wote wakahamishiwa ndani ya chumba kimoja tu, nacho kilikuwa kikubwa kupita maelezo. Kila mmoja humo alikuwa amejikunyata kutokana baridi ya maji waliomwagiwa awali. Lakini kadri muda ulivyoyoma joto ndani chumba hicho liliongezeka, baada ya nusu likawa kali sana kiasi kwamba watoto walikuwa wakichuruzika jasho vibaya sana. “Alex vua nguo zote” aliongea Alex mkubwa, Alex mdogo nae akafanya hivyo na kubakiwa na nguo ya kuzaliwa tu. Alex mkubwa nae akafanya hivyo, watoto walipoona wenzao wamevua nguo na wao wakaiga.


Hata hivyo hali ilizidi kuwa tete baada ya joto kuongezeka ndani ya chumb, “unakumbuka ule mchezo wa kubana pumzi” aliuliza Alex mkubwa, “ndio kaka, nakukumbuka” alijibu Alex mdogo. “Sawa, tushindane. Ukinishinda nitakupa viatu vyangu uvae” aliongea Alex mkubwa, hakuna jambo alilokuwa analipenda Alex Jr kama kuvaa viatu vya kakaake. Aliamini vinamfanya awe mtu mkubwa kama kakaake, “sawa” alijibu. Kwa pamoja wakahesabu mpaka tatu, wakavuta pumzi kwa nguvu na kuibana ndani. Kutokana na kucheza sana mchezo kipindi wako nyumbani, iliwafanya wawe na uwezo wa kubana pumzi kwa muda kuliko wawezavyo watoto wengine.


Dakika moja ilitimia na Alex mdogo akawa anafikia kikomo chake, lakini alipotaka kuiachia Alex mkubwa akavua kiatu chake na kumuonesha kisha akatikisa kichwa. Alex mdogo kuona hivyo akaamuwa kujikaza ili mradi avae viatu vya kakaake. Na kwasababu uwezo wa kubana pumzi ulikuwa umefikia kikomo, taratibu macho yakaanza kupoteza nuru na mwishoe akapoteza fahamu. Alex mkubwa nae hakuchukuwa muda akaanguwa na fahamu zikamuondoka.


Akiwa katika usingizi mziti, Alex mkubwa alihisi macho yakimuuma baada ya kumulikwa tochi machoni. Alikurupuka huku akihema kwa nguvu na jambo la kwanza alimuangalia mdogo wake aliekuwa bado kazima. Alijaribu kumtikisa lakini hakukuwa na muitiko wowote, wale watu waliokuja kukagua walimsukuma nyuma na kummulika Alex mdogo tochi ya macho. Hata hivyo kiini cha jicho hakikuonesha muamko wowte. Yule aliemmulika aliangalia pembeni na kutaka kupitisha mkono shingoni, lakini kabla hajafanya hivyo alijikuta akishtuka na kuiachia tochi yake baada kidole cha Alex mkubwa kuzama jicho.


Hata hivyo Alex mkubwa hakumjali mtu huyo, alimsogelea mdogo na na kukunja ngumi yake ndogo. Alimtandika mara kadhani kifuani upande wa kushoto kisha akambana puwa na kukutainisha mdomo wake na wamdogo wake. Alipuliza mara tatu na Alex mdogo alifunguwa macho na kuanza kukohoa kwa nguvu. “Nimeshinda eenh” aliongea, “ndio, umeshinda” Alex kubwa alijibu na kuvua kiatu kimoja kilichobakia mguuni. Akakiokota na kile kingine kisha akamvalisha mdogo ambae alionekana kufurahi sana.


Walitolewa kwenye chumba hicho na kuepelekwa katika chumba kingine. Chumba hicho kilikuwa na meza nyingi ambazo zilikuwa na vyakula. Watoto walivyoona hivyo walikimbilia mezani na kuanza kufakamia chakula. Lakini ilikuwa tofauti kwa kina Alex, japo Alex mdogo alitaka kukimbilia mezani akajikuta amenasa baada ya kushikwa mkono na kakaake. Alex mkubwa aliangaza huku na kule kama aliekuwa anatafuta kitu. Alipoona jagi la maji alitabasamu na kumvuta mdogo wake upande ambao lilikuwepo jagi hilo. Alitia maji kwenye gilasi na kumpa Alex mdogo ambae alikunwa kwa pupa, na yeye alikunywa pia.


Baada ya hapo ndio walisogea mezani kwa ajili ya kupata chakula, baadhi ya wale watoto waliokimbilia chakula walipaliwa na kwasababu kila mtoto alikuwa akijijali mwenyewe hakuna aliemtazama mwenzake. Baadhi ya waliopaliwa na chakula baada ya muda walikaa sawa na kuendelea na wengine bahati haikuwa ya kwao. Walipaliwa hadi kuaga dunia na hakuna mtu alieingia ndani ya chumba hicho mpaka watoto wote walipomaliza kula. Wale waliopaliwa hadi kufa walikuja kubebwa na machela, waliobaki walihamishiwa katika chumba kilichokuwa na vitanda na kuambiwa walale


Baada ya hapo ndio walisogea mezani kwa ajili ya kupata chakula, baadhi ya wale watoto waliokimbilia chakula walipaliwa na kwasababu kila mtoto alikuwa akijijali mwenyewe hakuna aliemtazama mwenzake. Baadhi ya waliopaliwa na chakula baada ya muda walikaa sawa na kuendelea na wengine bahati haikuwa ya kwao. Walipaliwa hadi kuaga dunia na hakuna mtu alieingia ndani ya chumba hicho mpaka watoto wote walipomaliza kula. Wale waliopaliwa hadi kufa walikuja kubebwa na machela, waliobaki walihamishiwa katika chumba kilichokuwa na vitanda na kuambiwa walale.

************************************************

Siku ilifata mapema walichukuliwa na kupelekwa maabara, juu ya mlango wa maabara kulikuwa na maneno makubwa ya rangi nyeusi yaliosomeka “PROJECT CODE X”. Waliingizwa ndani ya chumba hicho na kupokewa na watu waliokuwa ndani ya makoti meupe ya hospitalini. “Hamjambo na karibuni” aliongea mwanamama mmoja na kuendelea, “jina langu ni Dr Baby, na hao wengine mnaowaona ni wafanya kazi ambao wapo chini yangu. Katika chumba hichi tutwachoma chanjo muhimu kwa ajili ya ukuwaji wenu. Dawa hiyo tutawachoma kwa awamu tano, na kila awamu zitapishama wiki moja moja tu, baada ya hapo mtaungana na wenzenu katika nyumba zilizoandalia kwa ajili ya watoto kama nyie” aliongea Dr Baby na kuonesha tabasamu la uongo.


“Kaka mbona unatoka jasho wakati humu ndani kuna baridi” aliuliza Alex mdogo, “dawa… sindano” Alex mkubwa alishindwa kujibu. Pamoja na kujuwa mambo mengi sana kuhusu maisha, hakuna kitu alichoogopa katika uso wa dunia kama sindano. Hata ukimwambia achague kati ya kujimwa chakula siku nzima na sindano. Basi angechaguwa kujimwa chakula, adui yake mkubwa alikuwa sindano. Tofauti na Alex mdogo, yeye hakuogopa sindano wala dawa. Wote wakapangwa mstari mbele ya meza iliokuwa na vichupa na bomba za sindano nyingi tu.


Ilikuwa patashika nguo kuchanika ilipofika zamu ya Alex mkubwa, walitumia dakika kumi nzima kufanikiwa kumshika vizuri ili adungwe sindano. Baada ya zoezi hilo kukamilika walirudishwa katika chumba chao na kuambiwa wasubiri maelekezo. Kwa wiki walichomwa sindao kila baada ya wiki moja, ndani ya wiki hizo miili ya watoto wote walokuwemo humo ilikuwa imeongezeka lakini mwili wa Alex mdogo haukuonesha dalili yeyote ya ukuwaji. Tafauti na yeye, Alex mkubwa ndie aliekuwa na mwili mkubwa kuliko watoto wote waliokuwepo hapo.


Miaka miwili baadae.

Alex Jr, miaka sita sasa; na Alex Sr, miaka nane. Wakiwa katika chumba maalum cha mafunzo, Alex mdogo akiwa na mwili mkubwa kama wa kakaake akiwa na bastola ndogo mkononi. Mbele yake alikuwa kakaake aliefungwa pingu baada ya kukamatwa akijaribu kutoroka eneo hilo. “Adhabu yako ni kifo, umejaribu kutoroka na umeuwa walinzi wetu zaidi ya ishirini katika jaribio lako” aliongea mtu mmoja. “Ningejuwa kama ningekamatwa basi ningeuwa hata mia, wengine nimewaonea huruma kwasababu wameniomba nisiwauwe kumbe shukrani ya punda ni mateke. Wao ndio wametoa taarifa sehemu niliokuwepo” alijibu Alex mkubwa.


“Una kiburi si ndio?”, “nikuheshimi wewe kama nani, mbwa koko wee” alijibu Alex mkubwa na majibu yalikuwa ya kuudhi sana. “Unadhani hata ukiwa na kiburi utapona, na jambo baya zaidi atakaefanya kazi ya kukumaliza ni mdogo wako mwenye uliekuwa unamlinda tokea ulipofika hapa”. “Nilidhani nitanyingwa kumbe kifo changu kitapatikana kwa mikono ya mdogo wangu, sina tatizo na hilo na nitakufa natabasamu” alijibu. Jibu hilo lilimkera sana muulizaji na kuamuwa kurusha kofi zito sana, kwa kasi ya ajabu Alex mkubwa aliinama na kofi hilo likapita juu kisha akainukwa kwa nguvu na kumtandika kichwa cha kidevu. Aliweweseka kama aliekunywa pombe ingali tumbo halina kitu, bila mategemeo yake akajikuta akianguka chini kama gunia la mkaa.


“Alex muuwe kakaako” ilitoka amri, lakini Alex hakubonyeza kitufe. “Siwezi kumuuwa mtu aliekuwa familia pekee kwangu” alijibu kwa sauti ya chini. “Alex fanya kama walivyosema, ipo siku utakuwa muuaji mkubwa sana na utawarudia kuja kulipa kifo changu” aliongea Alex mkubwa. “Hapana siwezi kufanya hiviyo”, “Alex nimekwambia tandika risasi huyo mwehu” aliogea yule jamaa aliepigwa kichwa na Alex mkubwa. Wakati wakiendelea malumbano nyuma ya Alex mdogo akafika mtu akiwa na bastola mkononi. Alex mkubwa alimuona na akajikuta akiingiwa na hasira kupita maelezo, ila kabla haanza kufurukuta ukasikika mlio wa risasi. Tundu dogo la risasi likaonekana katika kifuwa cha Alex mkubwa, jambo lilitokea punde tu baada yule alietandikwa kichwa kumtikisa Alex mdogo. Hapo ikaonekana kama Alex mdogo bila mategemeo alifyetuwa risasi.


Tukio hilo lilitokea mbele ya macho yake lilituma shoti iliotoka kwenye ubongo na kusafiri hadi katika kidole kidogo cha mwisho cha mguu. Shoti ilifuatiwa na mwili kuingia ganzi na kuwa wa baridi kama mfu, ganzi hiyo ilidumu kwa sekunde kumi kisha taratibu ikaanza kurudi juu na yote ikahamia moyoni mwa mtoto huyo. Alijikuta akishindwa kupumuwa baada ya moyo kushindwa kuhimili uzito wa jambo lililotokea, “nimemuua kakaangu mpenzi” yalitoka maneno hayo kinywani mwake kwa sauti ya chini kabisa. Kiini chake cha macho kilitanuka kupita maelezo na badala ya kuwa cheusi kama ilivyokawaida, kilikuwa na rangi nyeusu iliopauka.


Kwa mbali sura yake iliingia giza na macho yalijifinywa kuwa madogo zaidi yakifuatiwa na makunyanzi makubwa sana usoni. “Aha…haa…heehee!” alianza kucheka kisha akamuangalia yule jamaa aliemtikisa na kumuoneshea mdomo wa bastola na bila kusita akabonyeza kitufe “koh” lakini hakikutoka kitu. Akatambuwa kuwa waliweka risasi moja kwa ajili ya kakaake, hata hivyo akili yake ilicheza haraka sana na bila kujuwa nini angefanya mtoto ambae kwa wakati huwo alionekana kupoteza akili. Alibonyeza kitufe kidogo kilichokuwepo pembeni juu kwenye mguu wa bastola, magazine ilichomoka. Akaidaka kwa mkono wa pili na kwa kasi ya ajabu akamavaa yule jama na kumkitia mara kadhaa shingoni mpaka alivyomtoboa na kuona damu “tabasamu jepesi likaupamba uso wake”.


“Damu damu damu nataka kuona damu” maneno hayo yalijiruidia mara kwa mara kinywani mwake. Aliinuka pale ulipolala mzoga wa yule jamaa na kuwaangalia wengine kisha akaramba midomo yake kama mtu alieona chakula kitamu sana na alikuwa na njaa ya kama wiki moja hivi. “Tunahitaji kumzuia bila kumuumiza” ilisikika sauti kutoka kwenye kipaza sauti. Wale jamaa waliokuwemo kwenye nyumba hicho wakachomoa virungu maalum vilivyokuwa vinapiga shoti na kumzunguka “zaidi zaidi zaidi, nataka kuona damu” aliendelea kuongea. Kwa kasi ya ajabu alianza kuwavamia, akafanikiwa kupata kisu kidogo kilichokuwemo kwenye mfuko wa mmoja wao.


Alikichukuwa na kuendelea mashambulizi, baada ya dakika kumi chumba hicho chote kilikuwa na damu kama vile machinjio. “Nahitaji zaidi, damu damu. Napenda kuona damu” aliendelea kuongea huku akiingalia ile miili iliolala pale chini kwa uchu. Alitamani iamke ili aiuwe tena, ama kwa hakika Alex Jr yule wa mwanzo alimezwa na chuki iliokwenda kujikita moyoni mwake. Akiwa bado anaiangalia ile miili, mlango ulifunguliwa na hilo ndilo kosa alilosubiria walifanye. Alielewa kuwa nje ya chumba kulikuwa na watu wengi sana kiasi kwamba angeuwa mpaka angetosheka.


Ulipofunguka na kupitisha mwanga tu, Alex aligeuka na kama risasi alimpita aliefunguwa huwo huku akizamisha kisu kitovuni na kumraruwa tumbo. “Tieni loki milango yote, na mumtafute” aliongea mtu mmoja aliekuwepo ndani ya chumba kile alichokuwemo Alex lakini alijibanza sehemu na kutulia tuli kama paka aliemwagiwa maji ya baridi. Milango yote ikafungwa kwa loki, vikosi vya askari waliokuwa wanasimamia eneo hilo vilisambazwa na kuanza kumsaka. Alex baada ya kutoka kwenye chumba hicho, akili yake ikamwambia aende moja kwa moja mpaka katika kile chumba walichokuwa wanalala. Huko walikuwepo watoto wengine na aliwachukia sana kwasababu walikuwa wakimcheka kila alipokosea.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog