Search This Blog

Thursday, 29 December 2022

KIAPO (AGANO LA DAMU) - 2

   

Simulizi : Kiapo (Agano La Damu) 

Sehemu Ya Pili (2)




Yeye ndiye aliyepika chai ile ya maziwa,aliwachemshia Yale mayai na kuwatengea




Ila akuruhusiwa kunywa wala kukaa katika meza ile!,ladha ya chai yeye alishaisahau!




Chakula chake alichokuwa akila ni cha shule alijua ilo ivyo icho sicho kilichompeleka pale!




"Unataka nini wewe Mwana wa haramu ulozaliwa na Malaya usiye na baba mgombanishi mpaka mashuleni"




Bi ney alimwambia kwa dharau,Matusi Yale Isack wala hakuyajali alishayazoea




"Daftari la hisabati mama!"




Isack akaongea kwa sauti ya taratibu,sauti ya unyonge




"Daftari la hisabati mama una hata haya umesikia ela tuna okota au baba yako waliacha ela hapa kwenda shule uko utajua utaandikia wapi"




Bi Neema akaongea kwa ukali,maneno yalomtisha mpaka Isack mwenyewe!




Kama mama yule kakataa kumpa daftari angeenda kumweleza nini mwalimu yule mnoko?!,akaona kuendelea kusimama pale ni kuendelea kuumizwa na maneno makali kutoka kwa walezi wake wale!




'Nitajificha chooni sitoingia kipindi cha Hitlar Mimi ataniua yule'




Isack akawaza akielekea zake shuleni tena akitembea kwa mwendo wa unyonge




Huku nyuma Bi Neema kwa kuwa alikuwa na namba za mwalimu Gibson ' Hitlar' alizochukua Jana alivyoenda shuleni akampigia muda ule....




"Alooh mwalimu nimeshamnunulia huyo mtoto daftar akija akuoneshe na kama asipokuonyesha mpeni adhabu kama ya Jana nisaidie mwalimu kumbadilisha tabia huyo mtoto anaelekea kunishinda eti...."




"Ni mtoto gani huyo?!"




Hitlar alikuwa ofisini kwa mwalimu mkuu asb ile wakijadili mambo baada ya bi Ney kumpigia simu Hitlar kuna kitu kikamtuma aweke 'loud speaker' ivyo ombi la Bi ney likasikika moja kwa moja mpaka kwa mwalimu mkuu




mwalimu mkuu alimkubali sana Hitlar ivyo akajikuta akiuliza kwa mshawasha




"Si yule mzazi alokuja Jana tukamuadhibu mwanae?!"




"Daaah inaonekana huyo mtoto ni mtundu"




Mwalimu mkuu akauliza akiangalia pembeni




"Haswaa mwalimu!,ila madam Jane anafuga ujinga"




"Najua mwalimu madam yule mpole sana ila naadhabu muwe mnaangalia zisizidi uwezo wa mtoto mia si mchezo ha ha ha ha"




Mwalimu mkuu akamalizia kwa kucheka




Maongez yakaendelea mida ilipotimia Hitlar akabeba fimbo zake na kitabu cha mwongozo kuelekea darasani




"Elimu ni ufunguo,wa maisha yetu,tusome kwa bidii,shkaaaaamooooo mwaaaaalim"




Mwalimu Hitlar alipoingia tu darasani akapokelewa na salamu wanafunzi wote wakasimama juu




Macho ya Hitlar yale makali yakatua kwenye dawati la Brayton


Isack akwepo




Pasina kuitika ile salamu akauliza kwa ukali....




"Isack yupo wapiiiiii"




Wanafunzi kimya




"Mstarini alikwepo?!"




"Ndiyoooo mwaaaalim"




Wanafunzi wote wakaitika




"Ananikwepa eeeeh! Johnson"



ITAENDELEA




Simulizi : Kiapo (Agano La Damu) 


Sehemu Ya Pili (2)




"Naaam mwaalim"




"Pita mbele" kijana mmoja ambaye alikuwa ni kiongoz akapita mbele




"William mbeleee na Ayubu pia mbele"




Wote walotajwa wakapita mbele




"Haya nyie wengine kaeni"




Wanafunzi wote wakaketi




"Zungukeni darasa a na b mumtafute Isack aletwe hapa mkimkosa muende nyuma ya madarasa na chooni"




Vijana wale wakatoka wakaanzia na darasani ,nyuma ya madarasa na mwisho wakaelekea chooni




****




Maskini Isack baada ya kutoka mistarin akaelekea zake chooni na akiwa chooni kule kichwani alikuwa na mawazo mengi sana juu ya Hatma ya maisha yake




Si kwamba hakupenda kusoma la asha alipenda sana asome aje awe hakimu ila vikwazo majaribu na mateso alokumbana nayo


Ghafla machozi yakaanza kumtoka kwa maumivu makali ilikuwa ni kama mtu kauchoma moyo wake na kitu chenye ncha kali




Mara ghafla akaskia harufu flani ya bangi akaelekea kule kule harufu hiyo ilipotokea




'Naskiaga hii kitu inapunguzaga mawazo'




Akajiwazia alipofika akamkuta mtoto wa darasa la sita akivuta mtoto yule alipomuona kwa kuwa alishatosheka akamkabidhi ye akatoka zake Isack akabaki mule ndani akivuta




Yule mtoto wa darasa la sita nje alipishana na viranja alishtuka ila alifrah kwa yeye kusalimika




Ndani viranja wale wakapokelewa na harufu ya bangi huku wakinyata wakaelekea choo cha mwisho




Ahmad ana kwa ana na Isack msokoto wa bangi mkononi




Wakaanza kumuongoza kumtoa nje na ushahid wake mkononi




Nje ya darasa lile mwalimu mkuu alikuwa na mwalimu Gibson akipewa baadhi ya maelekezo hatari kwa Isack ikiwa angefikishwa pale!...




Adhabu ni kufukuzwa shule!!!!!.....








Bado maisha ya kijana Isack yapo katika hatihati,mama yake mlez Neema amchongea kwa mwalimu wake wa hisabati mwalimu Gibson mwalimu huyo anapoingia darasani na kumkosa Isack anawatuma baadhi ya viranja waliomo kule darasani kumsaka Isack




Kwa bahati mbaya vishawishi vinamuingia Isack akiwa chooni anavutiwa na harufu ya bangi anaenda kuopoa baada ya kijana yule kutosheka anampa Isack naye kutoka zake nje ambapo anapishana na viranja wa shule anamshukuru Mungu wake kwa kumuokoa!




Isack anafumwa na sasa anatolewa nje ya choo kile kupelekwa kwa mwalimu kidhibiti chake kikiwa mkononi




Je unahis nini kilitokea?! Twende pamoja




*NA HII NI SEHEMU YA TISA*






Majuto ni mjukuu,methali hii ilitimia moyoni mwa kijana Isack,ila hakuwa na muda wa kurekebisha lile!




Pia akuwa na muda wa kurudisha muda nyuma arekebishe tatizo lile lililokwisha tokea akabaki akiongozwa kama mbuzi achungwaye machungi!




Badala ya kurekebisha tatizo sasa kaongeza tatizo jingine aliangalia chini kwa aibu




"Nyie mnampeleka wapi huyo mtoto embu njooni hapa"




Ilisikika sauti nyuma yao wote wakageuka ule upande sauti ile ilipotokea




Naaam mwalimu Janeth alikuwa kasimama akitokea upande wa vyoo vya walimu vyoo vya walimu na wanafunzi vilipakana kwa mita kadhaa




"Aingii darasani tukatumwa na mwalimu Gibson tumtafute tukamkuta chooni anavuta bangi!"




Mwalimu Jane alishtuka




"I..I..isack unavuta bangi?!"




Madam Jane akauliza kwa kigugumizi pasina kuamini kile alichokisikia




"Hapana mwalimu wanansingizia"




"Wanakusingizia?!! kwanini wakusingizie wewe tu?! Una nini mpaka wakusingizie Isack! Aupo kama nilivyokufikiria nilifanya makosa Mimi kukutetea ulistahili ile adhabu na sasa unaelekea kufukuzwa shule kwa hilo sina cha kukusaidia haya mpeleken"




Mwalimu Jane alionekana kukasirika waziwazi!




Isack akatupa ule msokoto wa bangi na kumkimbilia madam Jane akampigia magoti huku rundo la machozi yakimiminika kutoka katika pembe za macho yake




"Najua nimetenda kosa mwalimu nisamehe nisaidie nimeteleza tu bado napenda kusoma nikifukuzwa ntakua chokoraa Mimi ntaelekea wap sina baba sina mama sina wazazi Mimi wewe ndo mtetez wangu usintupe bado naitaj mchango wako mwalimu Wang....




Isack alilia machoz yalimchuruzika kama bomba la maji huku akishika miguu ya mwalimu wake




Madam yule dah!,alikuwa na moyo wapekee mwingi wa huruma mwenye moyo mwepes eti bila kutarajia kitu chenye ncha Kali kikaupasua moyo wake machozi nayo yakaanza kumchuruzika




Si yeye pekee hata na watoto wale viranja wa shule wakajikuta wakimwangalia Isack kwa simanzi




Uzuni ikatawala eneo lile!




Sasa wakati Yale yote yakiendelea ticha mnoko Hitlar aliyekuwa nje ya darasa lile la nne kwa mbali chooni kule si akaona lile tamasha palikuwa na umbali kidogo!




" he pale kuna nini embu twende tukaone"




Mwalimu mkuu akubisha wakashuka kwenye korido ile kuelekea eneo usika!




Madam Jane awakujua kama nyuma yao walimu walikuwa wanakuja




"Kuna nini hapo mwalimu?!"




Mwalimu mkuu akauliza kitendo kilicho washtua vijana wote wakageuka nyuma walichokiona kikazidi kuwaogopesha




Msokoto wa bangi ulikuwa chini tena karibu na miguu ya Isack




Ilikuwa ni kitendo tu cha kuangalia chini basi wangeiona bangi ile




Wote walichanganyikiwa pasina kujua wangefanyaje au wangejibuje




"Nauliza kuna nini hapa mwalimu mbona unijibu na una ukaribu gani na huyo mtoto?!"




Mwalimu mkuu akazidi kuuliza safari hii akiongea kwa ukali




Madam Jane hakuwa na cha kujibu angejibu nini sasa,alikuwa njia panda atetee au aeleze ukweli kumnusuru mtoto yule




Ghafla shingo ya mwalimu mkuu ikageuka taratibu nyuma kuwaangalia viranja wale




Ilikuwa ni hatari kwa Isack ikiwa mwalimu mkuu angeiona ile bangi pale chini kabla mwalimu mkuu ajageuka tena upande wao,bila kutarajia Isack kwa spidi akainama na kuichukua ile bangi akaiweka mfukoni




"Nyinyi nini kinachoendelea hapa!"




Baada ya mwalimu mkuu kushindwa kupata jibu kwa Madam Jane sasa akaamishia maswali kwa viranja




"Mwalimu!"




Isack akaita kwa sauti kubwa mwalimu mkuu na wote walokwepo pale wakamwangalia Isack wakitaka kujua ataongea nini




Isack akanyanyuka toka pale alipokuwa amepiga magoti kwa mwalimu Jane akajifuta kidogo magoti na kumsogelea mwalimu mkuu




"Nateseka sana mwalimu, nanyanyasika Mimi ni yatima nisiye na msaada wowote katika dunia hii tangu wazazi wangu wafariki nimekuwa nikizama katika Lindi la mateso pasina msaada wowote




Mwalimu nimekuwa nikinyanyaswa sana na walezi wangu wananipa kazi nyingi mpaka nachelewa shuleni juzi usiku baba kanchania daftar lang la hisabati asb namuomba mama anakataa naogopa kuingia darasani Mimi ndo nilikuwa namlilia mwalimu hapa aninunulie daftari niingie darasan...."




"Mwalimu je ni kweli?!"




Mwalimu mkuu akamuuliza madam Jane




"Ni kweli mwalimu mtoto huyu anateseka sana na kashanielezea kila kitu....




Madam Jane ikabidi aanze mtetea




" mwalimu swala hili tukaliongelee ofisini nyinyi rudini darasani"




Mwalimu mkuu akaitimisha viranja wale wakarudi darasani mwalimu Gibson,mkuu wa shule na madam Jane wakaingia ofisi ya mwalimu mkuu kuongelea swala lile na vipi wa msaidie mtoto huyo




"Mwalimu kwani amna uwezekano mi niishi naye huyu mtoto?!"




Madam Jane akapeleka ombi lake




"Inawezekana ikiwa walezi wake watakubali uishi naye"




Mwalimu mkuu akajibu




"Basi itabidi utaratibu ufanyike tumwite mzazi wao hapa shuleni na kumuomba juu ya hilo"




Gibson akadakia




"Na bahati nzur namba za mama yake nnazo ntamjulisha juu ya hili kesho naiman atakuja!"




"Vizuri sana ila kwa nini tusiandike barua tukampa mtoto akapeleka?!"




Madam Jane akashauri kitendo kilichomfanya Gibson amkate jicho la chuki




"Mi naona hilo ni jambo la msingi zaidi tofauti na kumpigia simu au unasemaje mwalimu?!"




Mwalimu mkuu akajibu akimwangalia Gibson




"Sawa tu!"




Gibson akajibu kimkato mwalimu mkuu akafungua kabati lake na kutoa daftar jipya akamkabidhi Isack




"Na hili ndo daftar la hisabati kuna daftar jingine lililoisha?!"




"Nashkur mwalimu!,hapana amna"




"Sawa ukiwa na tatizo usisite kunambia mimi au mwalimu yoyote yule atakusaidia sawa?!"




"Sawa mwalimu"




"Kaendelee na masomo baadaye ntakuletea barua umpelekee mzazi wako sawa"




"Sawa mwalimu"




Isack akajibu kwa furaha na kutoka katika ofisi ile akiwaacha walimu wale wakiendelea na maongezi




"Walimu mnaweza kwenda au kuna lingine?!"




"Hapana mwalimu"




Wote wakajibu na kutoka ofisini pale




"Habari mwalimu vipi maendelea ya mtoto kuandika kweli Leo?!"




Meseji iliingia katika simu ya mwalimu Gibson kutoka kwa bi Ney mwalimu yule akawaza kidogo na kumjibu!




"Hivi kwa nini mnamtesa sana huyu mtoto mnapata faida gani katueleza kila kitu na sisi tumeamua kumsaidia"




Bi Neema akayatoa macho kwa mshangao akarudia Mara mbili mbili ile meseji!




'Wameamua kumsaidia?!,kivipi?! Haiwezekani huyu pumbavu hatakuwa kaenda kuwatangazia walimu kwamba tunamnyanyasa sasa atajuta kuzaliwa ngoja aje!'




Dada yule mwenye roho mbaya aliwaza alikuwa ni mweupe ila kwa hasira alibadilika na kuwa mwekundu!




'Ntamuua Leo'




Akawaza akiwa bado mwingi wa hasira




Daaaaaah majanga tena kwa Isack nini kitaendelea?!,je atatoka katika mateso Yale ndani ya familia ile








Mateso yanaendelea kula sehemu kubwa ya maisha ya kijana Isack,walimu sasa wanabeba jukumu la kumsaidia na madam Jane anapeleka pendekezo la kumchukua kijana yule wa darasa la nne na kuishi naye




Je walezi wake wamtesao watakubali?! Twende pamoja kujua hatma ya chalii huyu




KATIKA SEHEMU HII YA KUMI




Moyo ulikuwa mzito,mwili ulimtetemeka,jicho lilimcheza ishara ya hatari!


'Kuna nini?!' Akajiuliza ila hakuwa na jibu alijua lazima nyumbani kutawaka moto ila je sababu kubwa ni nini!?




Je ni ile barua ilokuwa katika mfuko wake wa suruali?!,taratibu akaingiza mkono wake mfukoni na kuitoa bahasha akaiangalia na kuirudisha mfukoni!




'Mungu pekee ndo ajuaye hatma ya maisha yangu'




Akawaza akiendelea kutembea,maskini akujua mama yake mlezi bi Ney alikuwa akimsubiri kwa hamu baada ya kile wamfanyiacho kijana yule kugunduliwa na walimu!




Pasina kujua hilo kijana yule akazidi kusonga akiilazimisha furaha ilokwisha goma na kumezwa na hofu pamoja na woga




Wakati hayo yote yakiendelea kichwani kwa Mzee Alex alikuwa na wazo jingine kabisa juu ya kijana yule!




Kumuua!




Ndio alipaswa afanye jambo hilo haraka sana alijua ipo siku mambo yangemrudia kama angeendelea kumuacha hai kijana yule,lazima angechunguza vifo vya wazazi wake na si ivyo tu Bali pia angetaka kufatilia kuhusu viwanja vyao ambavyo kwa sasa vyote vilikuwa chini yake!




Sasa ilipaswa afanyaje kutotiliwa shaka kwa kile atakacho kukifanya?!,akazidi kupikicha ubongo ila bado hakuwa na jibu sahii ni njia ipi sahii alopaswa kuifanya kutekeleza lile alipangalo




Ghafla akamkumbuka mtu!




Kijana wa kazi




Zidu 'k' au zidu katili kijana katili 'profision' katika maswala hayo ya mauaji




muuaji wa kimataifa!




Mzee Alex akatabasamu ishara ya ushindi!,




'Nadhani sasa huu ndo utakuwa mwisho wako mtoto Isack ,Itabidi ufe!,kwa hili hakuna jinsi'




Mzee yule akiwa kwenye kiti chake ofisini kwake akawaza tabasamu likichanua katika pembe za mdomo wake!




Naaam akajinyanyua na kulifata kabati lililokuwa pale ofisini akalifungua kabati lile lilijaa faili mbali mbali




Kuna kitu alikuwa akikitafuta hakutumia muda mwingi sana chini ya faili zile akatoka na ka kitabu kadogo cha namba




Mzee Alex akatabasamu akarudi na kukaa kwenye siti yake




Macho yake yakasoma zile no na ghafla yakatulia katika no moja tena iloandikwa na wino mwekundu zkxxx




Akatabasamu!




Na kuishika simu yake akaenda uwanja wa meseji




'Nakuitaji ofisini kwangu'




Akaituma meseji ile katika namba zile akusubiri ipokelewe akawa tayari kashaifuta!




Alitegemea muda wowote kwanzia muda ule Zidu 'k' angekuwa mbele yake




Naaaam maisha ya mtoto Isack sasa yalikuwa hatarini!




*****




"Mamaaaaa nisamehe sitorudia mama nisamehe mimi unaniuaaaaa....




" kufa shetani wa miguu mitatu wewe usiye na haya mtoto mnafki eti unateswa wa kuteswa uwe wewe sasa Leo utaiomba mizimu ya wazazi wako ifufuke huko makaburini ije ikusaidie mpuuzi sana wewe.....




Ilisikika kilio cha mtoto mdogo huku vishindo vya kupigwa vikisikika naaaam alikuwa ni bi Neema akimuathibu mtoto Isack pasina hata chembe ya huruma huku akimsindikiza na maneno makali alimvua nguo zote na kumchapa na mkanda pasina kuangalia ni wapi apigapo!




Isack alilia akiomba msamaha ila Dada yule mwenye roho mbaya ndo kwanza alipandisha hasira na kumuongezea kipigo




"Nakuuliza hivi hapa nyumbani unateswaaaa"




Paaaa paaaaa paaaaa paaaa




"Ha...pana...ma..m.ma.."




"U nanyanyasika?!"




"Ha...pa...na...sijasema...chocho..te mi.mi"




Isack alizidi kujitetea Ila mwanamke yule akumuachia aliendelea kumtesa mpaka alipochoka akamuacha tena akiwa katika maumivu makali




"Na Leo uli utaenda kulala kwenye banda la mmbwa Malaya Mkubwa wewe"




Bi Ney aliongea kwa hasira huku akifikiria kazi gani ngumu ampe kama adhabu




"Na Leo utasugua huu ukuta mpaka ung'ae..."




Na wala mama yule akutania akampa sabuni ya unga ndoo Isack akaenda kuchota maji na kuanza kazi ile na hata alipomaliza alimwambia ujatakata arudie




Isack angefanyaje maskini!




Ikabidi afanye ivyo




Mpaka saa nne usiku ndipo aliporuhusiwa akalale tena katika banda la mbwa,




Isack akajikokota na kuingia ndani ya banda lile,hata mbwa walishangaa!,walimuonea huruma lakini hawakuwa na uwezo wa kumsaidia zaidi ya kukaa kimya na kutobweka kusudi mtoto yule alale




Ila usingizi ulikuwa mbali naye!,hata kama ni wewe sidhani kama ungepata usingizi katika maeneo kama Yale!,afadhali na kule stoo alipokwisha kupazoea mwenyewe kuliko katika kakibanda kale




Usiku alipigwa na baridi mtoto wa watu akitetemeka na meno mdomoni kugongana alijikunyata huku akifikiria hatma ya maisha yake ya hapa duniani




'Hivi kuna siku angelalia kitanda na kujifunika shuka kama walalavyo wengine?!'




'Hapana!' Aliwaza kwa kujiuliza na kukataa kwa kujijibu pia masaa yakazid kukatika akizama katika Lindi la mawazo




Hatimaye jogoo la kwanza likawika na kumjulisha wakti akajaribu kuusaka usingizi pasina mafanikio




Mpaka inagonga kumi na moja bi Ney anaenda kumfungulia mtoto yule akulala!,na hata alipomuamkia mama yake yule akuitikia




Akampangia kazi pasina kinyongo Isack akazifanya tena kwa moyo mweupe alipomaliza akaingia katika 'uniform' zake safari ya shule akiambatana na bi Neema ikafatia




Moyoni mwake alimuomba Mungu bi Ney akubali tu akakae nyumbani kwa madam Jane




Je angekubaliwa?!....




Hakuwa na jibu sahii ya swali hilo




Hatimaye walifika shuleni wakaongoza moja kwa moja mpaka ofisini kwa mwalimu mkuu dakika chache baadaye madam Jane na mwalimu Gibson wakaungana katika kikao kile kisicho rasmi




"Bila kupoteza muda kutokana na taaluma ya mtoto huyu kushuka kadri siku zinavyokwenda na baada ya kumpeleleza sana tumegundua anafanyishwa kazi nyingi sana mpaka anakosa muda wa kusoma , na si ivyo tu pia ananyanyasika huko nyumbsni....




Ghafla baada ya mwalimu mkuu kuongea maneno Yale uso wa bi Jane ukabadilika




Simanzi ikamvaa




" kweli tenda Wema usingoje shukran sisi tukunyanyase wewe Isack kwa nini tufanye hivyo?!




Mwanamke yule mwenye roho ya kishetani akaongea kwa hisia Kali huku machozi yakianza kumchuruzika....




"Ulitaka nini tukaacha kukupa Isack Leo hii unasema tunakunyanyasa?!....




Mama yule akashindwa kuvumilia machozi yakaanza kumchuruzika




" unnyanyasi mama Mimi sijasema!"




Kwa uoga Isack akajitetea katu akujua kuwa ndo anajiaribia




Walimu wale wakatazamana kwa mshangao!




"Unasemaje we mtoto huyu mama eti akunyanyasi?!"




Isack akatingisha kichwa kuafiki kuwa anyanyaswi kwani kitendo cha kumuona mama yake yule analia kilimtisha




"Nilishawaambia walimu huyu mtoto shetani tena mchonganishi mmeamini sasa mwambie aseme nilini Mimi nilishamtesa....




" basi mama yaishe lengo la kukuita ni tulikuwa tunaitaji kukuomba idhini aishi na madam wake hapa kwa kuwa huko nyumbani anateseka ila kwa kuwa amekiri mwenyewe kuwa anyanyasiki basi ni utoto mama tumsamehe tu!"




"Hapana baba! Bado sijashindwa kumlea huyu wazazi wake walituachia na tunaishi naye kama mtoto wetu ila kinachonshangaza ni icho cha kusema anateswa au kwa kuwa nilikuja kukuadhibu shuleni Isack?!"




Bi Neema akauliza akimtolea macho makali mtoto yule alotingisha kichwa kukataa




"Sasa tatizo nini au kipi nilichokukera mwanangu!"




Neema mbele ya walimu wale alijifanya mnyenyekevu akiificha roho mbaya yake na akafanikiwa kuwahadaa walimu wale na kujua maneno Yale alosema Isack ni utoto tu!




Swala lile la kumuamisha wakalitupilia mbali!




Wakamruhusu Dada yule aondoke na kumruhusu Isack aende darasani




Kabla ajaenda darasan Isack akaingia chooni




Tena choo cha mwisho pasina kujali uchafu ulotawala chooni mule,pasina kujali harufu Kali itokayo




Akiwa mwingi wa hasira akajitupa chini na kuangua kilio!




*NI NANI WA KUMUOKOA KIJANA HUYU?!*






Uchungu wake aliutoa kwa machozi yalotiririka katika pembe za macho yake!




Hakukuwa na wa kumbembeleza,akazidi kulia kwa uchungu ule ambao ulizidishwa baada ya bahati yake ya pekee kuyeyuka kama theluji ya barafu




Ghafla akaguswa nyuma! Akageuza shingo yake kumwangalia alomgusa




"Inatosha Isack usilie tena"




Sauti nzito ikatoka toka kwa kijana alokuwa nyuma yake!




Alimkumbuka fika!




Niyule ambaye Jana yake alimkuta mule mule chooni akampa bangi ambayo alinusurika kukamatwa nayo!




"Najua una mawazo mengi sana ila hii ni suluhisho la mawazo yako tumia kisha utanambia"




Kijana yule akaongea akimkabidhi Isack msokoto ule!, Isack akasita




'Pokea Isack usikatae hiyo!'




Nafsi yake moja ikamsihi na kujikuta akiipokea na kupiga pafu,kijana yule akamshushia tabasamu kisha pasina kuongea kitu akageuka kuondoka zake!




Isack akaendelea kuvuta bangi ile alipotosheka sasa akiwa yupo fit akaelekea zake darasani,mawazo yakiwa mbali naye!




Alichangamka aswaaaa!




***




Madam Jane akiwa ofisini mawazo yalikuwa juu ya mtoto yule




Isack




Akamkumbuka Brayton mtoto pekee alomwelezea juu ya manyanyaso ayapatayo kijana Isack na jinsi alivyomuomba amsaidie!




'Lakini kwa nini kama ananyanyaswa akatae na kusema anaishi vizuri tu au alimuogopa yule mama?!,inawezekana? Embu ngoja....'




Madam Jane akajiwazia na kujijibu mwenyewe akajiamsha na kushika kitabu chake cha kiswahili darasa la nne, kipindi hiko alikuwa na kipindi darasa la kina Isack




Akatoka kwa mwendo wa taratibu kuelekea darasani ila ghafla akamuona Isack akitokea chooni!




Kuna kitu kikamwambia asimame kumsubiri mtoto yule!




"Shikamoo mwalimu"




Isack alimsalimia madam Jane pasina kujua kuwa harufu ya bangi ilimfikia moja kwa moja mwalimu wake kutoka mdomoni kwake




"Mmmmmmh!!!!!..."




Badala ya kuitikia salamu ile Madam akaguna kwa mshangao Isack akashtuka!




"Umetoka chooni kufanyaje Isack?!"




Madamu Janeth Akauliza huku alionekana wazi usoni kuchukia




"Kujisaidia mwalimu!"




Isack akajibu wasiwasi ukianza kumvaa




"Unajua huwa sipendagi mtoto mwongo eeeh naomba niambie ulikuwa unafanyaje huko chooni?!"




Madam sasa akiwa anapandwa na jazba huku akimsogelea akazidi kumuuliza kwa ukali! Alijua Isack alikuwa akitumia bangi na hii ni Mara ya pili baada ya Mara ya kwanza kumsaidia baada ya kukamatwa na viranja




"Kweli madam natoka kujisaidia kwa nin uniamin?!....




Paaaaaaaaaaaaaaaaaa




Kilikuwa ni kibao kikali kilichotua katika shavu la mtoto yule,Isack aliona nyota nyota zikielea hewani




" huwa sipendi uongo Isack naomba nieleze ukweli kabla sijakupeleka ofisini ukapata adhabu kama ya juzi....




"Ntakueleza ukweli mwalimu usinipeleke ofisin..




" haya sema haraka...."




"Mwalimu sipendi Mimi kuwa hivi,kila siku nachapwa Mimi,nateseka nawe ndo ulikuwa msaada wangu si kwamba nyumbani siteswi hapana ila nilimuogopa mama ndo maana sikusema ukweli na kitendo icho kimenipa uchungu na ndipo nilipokimbilia chooni kulia ila nikiwa chooni mule nilitembelewa na rafiki yangu akanipa msokoto wa bangi na kunambia hii utoa mawazo....




" nawe ukaamini siyo?!..."




"Nisamehe mwalimu!..."




'Huyu mtoto anahitaji msaada zaidi ya msaada nlokuwa nikiufikiria embu ngoja!'




"Haya ingia darasani nikimaliza kipindi ntakuitaji ofisini tuzungumze"




"Sawa madam"




Isack akakimbilia darasani na kwenda kuketi!




****




Baada ya kipindi kweli kuisha Isack akamfata madam ofisini madam Jane akampa ishara aketi walimu wengine walikuwa bize na mambo yao isipokuwa kwa mwalimu Gibson




Hitlar! Kama wanafunzi walivyomtambua!




Alijikuta akitamani kufatilia mazungumzo Yale na kweli alifanikiwa




Isack alimweleza kila kitu mwalimu yule mpaka kulala kwenye banda la mbwa mikazi alokuwa akifanyishwa kusugua ukuta madam Jane alisikitika sana akahaidi kutafuta njia ya kumsaidia ila alimuonya kuhusu kutumia bangi




Isack akahaidi kuacha mara moja!,ila je angeweza?!...




Jambo hilo lilimfurahisha madamu yule ambaye alijitolea kuwa angempa ela jioni angempeleka kwake akale asb angempa chai katika Shea yake kwenye chai za walimu




Hakika Isack alifrah sana!




Ila furaha yake aikudumu!




Kwani alifurah siku moja na kulia mwezi mmoja!




Kivipi?!!!!




****




'Huu ni mwanzo lazima ateseke kwenye maisha yake yote ya hapa duniani Leo hii anaenda eti kuwa ambia walimu ananyanyasika bado ajanyanyasika kwanza embu ngoja....'




Bi Neema aliwaza akiwa kwenye kochi kubwa nyumbani kwake


Kitendo cha walimu kugundua juu ya wao kumtesa mtoto yule kilimkasirisha sana japo alisha kisahihisha ila alijua ilikuwa ni lazima awe makini kwani Isack kwa sasa alikuwa akitafuta suluhu ya matatizo yake!




Suluhu ya matatizo wampayo!!!!




'Lazima niwe karibu na mwalimu mmoja ambaye atakuwa upande wangu'




Mwanamke yule aliendelea kuwaza huku aliendelea kujipodoa juu ya kochi alolikalia sebuleni pale




Taswira ya sura ya mwalimu Gibson ikamjia katika ubongo wa kichwa chake!




'Tena kwa jinsi alivyo handsome jamani yule kaka daaah!'




Akajikuta akiung'ata mdomo kwa tamaa,ni wazi alimpenda mwalimu yule




'Ntamtega na lazima niwe naye kimapenz nikishamweka happpa mambo yangu yatakuwa mswano na hivi na namba zake embu ngoja'




Bi Neema akaweka kioo alichokishika juu ya meza na vipodozi kadhaa akaikwatua simu yake na kwenda uwanja wa majina!




Mwalimu!




Akastop katika jina hilo kwa sekunde kadhaa akiwaza alipige au,akabonyeza kitufe cha bluu na kuweka simu sikioni




Simu ikaita!




Mapigo ya moyo wa bi Neema yakaanza kwenda mbio




"Aloooh mama"




Mwalimu Gibson akapokea ila bi Neema mdomo ulikuwa mzito kuongea




"Aloooo"




Mwalimu akarudis Mara ya pili




"Aloooh"




Kwa sauti nyembamba imtohayo hata nyoka pangoni bi Neema akazungumza,sauti ilomuamisha hisia mwalimu Gibson na kubaki kayatoa macho kama mjusi alobanwa na mlango!




*kah mama wee! Roho mbaya kwa mtoto wa mwanamke mwenzio mpaka unafikia kutaka kumsaliti mumeo ili tu umfanye mtoto wa mwenzio aikose amani?! , binadamu wapi tunaelekea?!*




Kuna kipindi ufikiria mateso ameumbiwa yeye tu pale mateso yanapomzidi na kukosa wa kumfariji!




Likitoka hili linazaliwa hili tegemeo pekee lililobakia ni mwalimu wake wa kiswahili madam Jane anayetokea kuguswa na maisha yake na kujitolea kumsaidia!




Huku nyuma baba yake mlezi Mzee Alex anampangia njama za kumuua akimtumia kijana hatari Zidu katili




Kijana asiye hata na chembe ya huruma pale anapotengewa kiasi cha fedha




Je nini hatma ya maisha ya kijana huyu mdogo asiye na hatia?!




Twende pamoja!




*NA HII NI SEHEMU YA 12*




"Mwalimu tunaweza kuonana jioni hata tukapata moja moto moja baridi "




Bi ney akaomba kwa sauti ya upole sauti aloitoa puani na kuzidi kumchanganya mwalimu yule,




Mwalimu akapatwa na kigugumizi cha ghafla akashindwa kujibu!




"Jamani mwalimuuuu nakuomba plzeee"




Mwanadada yule akazidi kubembeleza kivipi sasa mwanaume yule shabab tena rijala angekataa kuonana na bi Neema ambaye kutokana na matunzo alionekana bado yu binti Mrembo?!




"S.s.sawa wapi...ssasa"




Mwalimu Gibson akauliza kwa kigugumizi bado akujielewa




"Aaaaaah mwalimu sema wewe bwana"




Mwanamke ni kiumbe kilichoumbwa kwa njia ya pekee ni kama sumaku inayoweza kuivuta hata chuma ilokwepo mbali




Ndio!,bi Ney alifanikiwa kuzivuta hisia za mwalimu Gibson zilizokuwa mbali naye!,mwalimu Gibson akajikuta akitamani kukutana na mwanamke yule kwa nia nyingine tofauti na mtoto Isack




"Alishampenda*




" nchagulie madam!"




"Ha ha ha ha wewe nawe basi Sheraton hotel"




"Haaaaaaaaaa!"




Gibson alishtuka,japo alikuwa ni mwalimu alo 'zovea' kwenye anasa ila hoteli ile yenye nyota tatu akuwai kuingia kutokana na gharama zake




"Mwalimu mbona unashtuka jamani!"




"Daaaaah gharama za hoteli hiyo tutazimudu kweli?!"




Gibson akajikuta akitahayati na kueleza wasiwasi wake bayana!




"Usijali mwalimu nipo kwa ajili yako gharama yote ni juu yangu mbona utafrah?!"




"Waoooooh kweli?!"




"Hakika we saa kumi kasoro uwe pale"




"Naona muda ni mrefu nataman hata ingekuwa saiv"




Mwalimu Gibson akajikuta akishindwa kuuzuhia ushamba wake na kuropoka bi Neema akaachia kicheko hafifu cha kimahaba kutoka katika tundu za pua yake




"Kama unaweza I means una muda njoo"




"True?! I don't believe it sina kipindi naja saiv"




"Waoooooh basi utankuta mpz"




Bi Neema akamalizia na kukata simu




"Kituuuuuu kwisha kazi yako Isack"




Bi Neema akashangilia akiruka hakika akumpenda mtoto yule na vyote alifanya kwa sababu yake




Huku nyuma si kwamba mwalimu Gibson hakuwa na kipindi kweli la hasha alikuwa na kipindi tena kwa bahati mbaya ni lile lile darasa la kina Isack kikiwa kipindi cha mwisho yani cha tisa




Akamfata madam Jane




"Madam Nina dharura la nne 'A' na kipindi kama vipi nenda kakimalizie"




"Usijali mwalimu ntafanya ivyo"




Mwalimu Gibson akasaini na kutoka zake tayari kwenda katika hoteli ile kuonana na bi Neema akisahau kuwa yule yu Mke wa mtu!




Na Mke wa mtu sumu!!!!




***




Wanafunzi wote walikuwa kimya kila dakika macho yao wakiyatupia dirishani wakitegemea kumuona mwalimu Hitlar akija!




Daftar za hisabati zilikuwa katika madawati wengi wakimalizia zoez lililotolewa asubuh wengine wakikariri tebo




Isack meno yaligongana kwa woga japo alisha andika kazi alirudia rudia Mara tano kuakikisha majibu yake




Hakika Hitlar aliogopwa katika shule ile,




Tofauti na mategemeo yao madam Jane akaingia




Woga,wasiwasi ukayeyuka katika nyuso zao




Tabasamu zikapendezesha midomo yao kwa furaha waka amka na Kwa pamoja wakasalimia....




"Elimu ni ufunguo,wa maisha yetu,tusome Kwa bidii,shikaaaamoooo mwaaaaalimuuuuu"




"Marhaba watoto wazuri haya kaeni"




Watoto wote wakakaa




"Tolu afute ubao"




Zuber kijana mrefu kuliko watoto wote katika darasa lile alokaa siti ya mwisho akainuka na kuifata dasta akaanza kufuta ubao alipomaliza akaenda kuketi!




Mwalimu akaandika ubaoni "kiswahili"




Hilo ndilo somo lake,na baada ya hapo chini yake akaandika "lugha"




Yah! Ni nyakati yani muda ulopita,uliopo na ujao




Chini akaandika sentensi




'Juma analima'




"Je ni nani awezaye kuandika katika wakati ulopita?!"




Wanafunzi wote kimya! Hakuna alokuwa na udhubutu hata wa kujaribu ila ghafla Isack akanyoosha kidole juu




Wanafunzi wote wakamshangaa




"Mwalimu naweza kujaribu?!"




Madam Jane akamnyooshea chaki Isack akaipokea na kwenda kuandika chini ya sentensi ile




"Juma halilima"




Katika wakati ulopita madamu Janeth alifrah "mpigieni makofi"


Wanafunzi wote wakampigia,Isack alikuwa na akili ya kuzaliwa mwenyewe tu "automatic" ubongo wake ulikuwa na uwezo wa kufikiri zaidi hata ya umri wake




Ila matatizo sasa ndiyo yaliyomshusha kiwango chake cha elimu, mwalimu akaendelea kufundisha na kutoa mifano mingi mpaka kipindi kilipoisha akatoka zake!




furaha ya Isack sasa ilirejea!!!




Ila je! Ingedumu?!!!!!!!!!!!!!!




******




*SURA YA NNE*




Ilikuwa ni nyumba ya kifahari iliyokuwa maeneo waishao watu wenye hadhi ya ukwasi




Nje kulizungukwa na kamera za cctv na juu ya ukuta kulizungushiwa nyaya maalumu za shoti ikiwa ni moja wapo ya ulinzi katika jumba ilo unaloweza kulifananisha na ekalu




Getini kulikuwa na walinzi wa vikosi mwalimu vya ulinzi kifuani wakiwa wamebeba silaha nzito za kivita




Ndani ya nyumba hiyo ambayo aliitumia kijana mmoja kwa kazi zake maalumu,ndani ya chumba kimoja alionekana mtu huyo mkononi akiwa na mkanda ule wa kijeshi akimuadhibu Mzee mmoja mwenye asili ya kiindi akiwa kamfunga kwenye kiti akimchapa kwa mkanda ule




Damu ziliruka ila ilo Jamaa yule wala akujali aliendelea kumchapa pasina huruma baada ya kutosheka akashika silaha yake ilokuwa kitandani akamnyooshea




Mzee yule alijaribu kunyoosha mkono ishara ya kuomba msamaa ila Jamaa yule wala akujali




Wala moyo wake ukuvutika kumwonea huruma Mzee yule ambaye alionesha dalili zote za kuonewa huruma



ITAENDELEA


Simulizi : Kiapo (Agano La Damu) 


Sehemu Ya Tatu (3)




Ila si kwa Zidu katili!!!




Baada ya sekunde chache bastola yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti ikacheua tena ikipiga kifuani eneo ulipo moyo


Na huo ukawa mwisho wa Mzee yule alomtapeli mwenzake madini na mwenzake huyo kumpa kazi zidu kumwangamiza muhindi huyo




Baada ya kufanikisha akashika simu yake na kumpiga picha kadhaa kisha akaubeba ule mwili na kwenda chumba kingine akasogeza kiti na kuufunua mfuniko akamtumbukiza Mzee yule na kufunika kwa haraka


Kule chini kulikuwa na gesi iliyouyeyusha ule mwili na kubakia maji maji ndani ya dakika mbili!




Kazi ikawa imeisha




Akaingia kuoga akavaa




Wakati akiwa anachana nywele zake ghafla mlio wa meseji ukaingia katika simu yake




Akauangalia na kuishia kutabasamu




'Mzee Alex anataka kunipa kazi gani?!'




Akawaza akiweka ile simu mfukoni na kutoka akaingia ndani ya gari lake tayari kuianza safari!




Aliingia katikati ya jiji na kuelekea katika kampuni kubwa ya ununuaji madini akapaki gari lake eneo usika na kushuka




Akaelekea mapokezi ambapo alikutana na katibu muhtasi




Alikuwa ni binti Mrembo Zidu akamwachia tabasamu jepesi




"Habari Mrembo?!"




"Salama tu kaka nikusaidie nini?!"




"Naweza kuonana na dairekta!"




"Una mihadi naye?!"




"Hapana ila mwambie Zidu yupo hapa"




"Sawa!"




Dada yule akajibu akishika mkonga wa simu akampigia bosi wake walomtambua kama Mr Dairekta




Upande wa pili ukaongea




"Ehe pili nakusikiliza!"




"Zidu anaitaji kukuona"




"M..mwambie....aingie"




Upande wa pili Mr dairekta ukaongea kwa kigugumizi kilichomshanga hata Dada yule




Akamwangalia Zidu kwa mashaka




"Kasema uingie"




Zidu akamzawadia tabasamu na kugeuka kuufata mlango


Huku nyuma yule Dada akimsindikiza kwa macho




Ghafla si akaiona bastola




Kiutani tu! Ikiwa 'kibindoni',mwa mzee wa kazi Zidu katili mwili ukamsisimuka Dada yule....




Zidu k huyu ndo Mzee Alex anataka kumpa kazi ya kumwangamiza Isack




Dah tunamfahamu vizuri na moto wake upo ndani ya riwaya ya Morose ( chuki) iliyopo katika kitabu cha Kisasi cha yatima




Unadhani Isack atapona kwa Zidu katili?! Nini hatma ya maisha yake!....




Bi Ney na mwalimu Gibson nin kitaendelea juu yao?!










Ni kijana katili asiye hata na chembe ya huruma pale anapotengewa ela




Huwa na roho mbaya zaidi hata ya mnyama pale linapotokea swala la kuua,kuua kwake ni jambo la kawaida na ni moja ya kazi zake zinazomuingizia kipato




Kwa jina alitambulika kama Zidu katili




Leo hii tunamuona Zidu k akitembelea kampuni moja ya uuzaji madini na kuomba kuonana na Mr Dairekta mmiliki halali wa kampuni ile je nini kiliendelea?!




Twende pamoja




*NA HII NI SEHEMU YA KUMI NA TATU*




Katibu muhtasi baada ya kuiona bastola ile kibindoni mwa mwanaume wa kazi Zidu 'k' mwili ulimsisimka,




Akakumbuka bosi wake alipopokea simu alipomtajia jina lile alivyobabaika je bosi wake alikuwa salama?!,hali ya sintofahamu ikazuka kichwani mwake umbeya na udadisi ukamvaa ila vyote vilifunikwa na woga!




Akakumbuka kuwa kama yule mtu ni mbaya akigundua yeye anamfatilia hatamuacha hai,akaona aache kama yalivyo kama anayapenda maisha yake!!!!




'Secretary' yule akaendelea na kazi zake za kawaida




Zidu katili baada ya kuingia ndani ya ofisi ile akapokelewa na tabasamu zito na mwenyeji wake alomkuta ofisini mule Mr Dairekta.




Zidu akalirudisha tabasamu lake Mr Dairekta akampa ishara aketi,Zidu akatii na kuketi,sasa Zidu akawa akitazamana na muhindi yule ambaye ndiye aliye imalizia kazi yake madakika kadhaa nyuma!




"Mr Dairekta kazi yako tayari na ushahidi huu nnachoitaji ni baki yangu ilobakia"




Zidu katili aliongea huku akimkabidhi muhindi yule simu kusudi azitazame zile picha alizozipiga wakat alipomuua yule mtu pale nyumban kwake na yule aliyopo mbele yake ndiyo alompa kazi ile ya kumwangamiza mwenzake mwenye asili moja baada ya kutapeliana madini




"Ooh nice kijana Wang iko Fanya kazi vizuri iko furahisha Mimi lipa Mara mbili wewe baki yako"




Muhindi yule aliongea kwa furaha huku akiangalia zile picha katika simu aliridhika moyoni mwake Zidu yeye alifurah kwa kuwa Mr Dairekta hakuwa na ela hapo alimuandikia hundi Zidu akachukue mwenyewe benki




Zidu akatoka hakiwa na furaha kwakuongezewa ela Mara mbili!




"Sasa Mrembo acha nikukatae ila ningependa hata uniachie no zako badae tuwe pamoja au unasemaje?!"




Zidu aliongea na katibu muhtas ambaye alionekana wazi kumuogopa mtu Yule




"Mi..mi!!!!?"




Dada yule aliuliza huku akitetemeka tayar Zidu alishajua Dada yule anaogopa nini akamsogelea huku akiwa na uso wake ule wa tabasamu na ghafla akaitoa bastola yake ile kibindoni Dada yule alishtuka!




"Najua unaogopa hii ila mi si mtu mbaya hii ni ya kujilindia si unajua tena sisi wana apolo nimeleta madini hapa nimeuza kitita cha maana mshua kaniandikia hundi hii ivyo badae ningependa niwe na mtoto mzuri kama wewe nijipongeze"




Zidu akaongea kwa kujiamini akimwonesha Dada yule ambaye mpaka muda huo akumjua jina Hundi ile Dada yule akaitupia macho na kwa ghafla tabasamu likachanua katika uso wake,akamwamini Mara moja kijana yule akaufunua mdomo wake kwa sauti nyororo ya kimtego...




"Usijali kaka Mimi sina shida ni wewe tu!"




Zidu akatabasamu tayari uzuri wa binti yule ulishamchanganya na kumsahau Mke wake Mery,Zidu akachomoa simu yake na kumpa Dada yule




"Tia namba zako huko!"




Bila kipingamizi Dada yule akapokea na kuziandika kisha akamrudishia mwenyewe Zidu!




"Nizisevu kwa jina gani Mrembo?!"




"Oooh sory mi naitwa Anita"

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog