Search This Blog

Friday, 30 December 2022

KIAPO (MTETEZI WA KINTE) (4) - 5

   


Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (4) 


Sehemu Ya Tano (5)



Ndani Lilikuwa Ni Jumba La Kifahari Uwezi Amini apakuishi mtu,palikuwa na bustan nzuri ya maua,ukoka wa kupumzikia bwawa la kuogelea,mandhari nzuri ilikuwa ni moja wapo ya nyumba za kifahari alizo miliki mwanadada yule nyumba yenyewe sasa ilikuwa na gorofa tano kwenda juu!,na yote ilikuwa safi,japo akuishi mtu,usiniulize usafi ulifanywa na nani!...



Akashuka,akafungua mlango wa nyuma akaanza na Isack akambeba juu juu mpaka katika lifti No 3 Akastopisha akatoka katika lifti mpaka katika chumba kimoja akabonyeza tarakimu fulani katika mlango,mlango ukafunguka,akaingia ndani!



chumba kilikuwa kimepigwa rangi nyeupeee kama chokaa hivi,kutoka juu ya singbord ukutan na mpaka sakafuni,kwa macho ya haraka haraka kilitisha!...



palikuwa pia na kakabati kadogo chenye sanduku tatu,na mwisho kilikwepo kitanda vile vya chuma akambwaga hapo kitandani!...



'teh teh teh isack,ntatoka na ushindi mkubwa sana,kukupata Wewe Ndo Mwanzo Wa Kumpata Zidu!',



Akawaza akashuka mpaka chini akambeba Mzee Lyayatuu Mpaka Katika Lifti akabonyeza no 5 lifti ikapanda juu ilipo 'stop' akatoka akaelekea katika chumba kingine chenye namba maalumu pia akabonyeza pale tarakimu kadhaa mlango ukafunguka,nacho hiki akikutofautiana na kile alicho muifadhi Isack,baada Ya Kumbwaga Chini akatoka akashuka ghorofa ya tatu,katika chumba kimoja wapo ni kama maabara fulani hivi



Akafungua kwanza kabati akatoa nguo nyeupe pee akazivaa na juu akajifunga nikabu kwa kitambaa cheupe macho tu ndo yalionekana alikuwa na maana yake kufanya vile....



Akachukua vipimo,ma dripu madawa katika kabaskel flani!...



akaelekea navyo kule alikolazwa Isack akaanza kumpima,kwanza alimtundikia dripu ya chakula...



Alishagundua Kitu Kikubwa Kilichokuwa Kinamsumbua Isack Ni Njaa,akamchoma Na Sindano Ya Usingizi...



Kitaaluma Pia Katarina Alikuwa Ni Daktari Mkubwa tu,hasa wa magonjwa ya akili kucheza na ubongo na Mwana saikolojia



Alipomaliza Akarejea kule alipo Zidu Akiwa Na Nguo Zake zile zile ,akaingia katika chumba kimoja kama maabara flan akachukua sindano akaweka katika kibaiskeli na dawa



dawa ile ukufanya kusema ukweli bila kujielewa! akaelekea mpaka katika chumba alichomlaza Zidu



Zidu bado hakuwa na ufahamu akanyonya kias cha dawa huku akiwaza



'ukutaka kunambia ukweli binafsi,utanambia sasa kwa ulazima'



Akamchoma ile sindano akiwa bado hana ufahamu kisha akakaa kama dakika tano hivi kusubiri dawa ichanganye ubongo wa komandoo yule



akatoka nje aliporejea alikuwa na ndoo ya maji! ya baridiii akamwagia nayo usoni palepale kitandani



Zidu Likashtuka!



Ila Mwili Wake Ukuwa Na Nguvu,akaangaza Macho Kutazama Chumba Kile,hakuwa Na Kumbukumbu Sahihi



'nipo akhera bila shaka!'



Akajiwazia Kutokana Na Weupe Wa Kile Chumba Na Mtu Alomsimamia,kk Akamsogelea Zidu alikuwa akitetemeka



"ulikuwa ukijifanya mjanja sana duniani!,muongo,tazama leo umelala kitandani huna nguvu nyanyuka sasa,umri wako mpaka umezeeka umeutumiaje?"



Kk Akaongea Kwa Nia Ya Kuzidi Kumuogopesha,na Kwel Zidu aliogopa,



"zidu yupo wapi?" kk akamuuliza,baada ya kumuona jinsi alivyokuwa akitetemeka



"ni..nipo hapa malaika"



Zidu Akajibu Kwa Kubabaika,dawa Ile Ilimpa Wenge! Na Mandhar Ya Kile Chumba,na Kukosa Kwake nguvu akajijua duniani alishakufa,alikuwa nusu mwendawazimu!,moyoni alikuwa tayari kueleza kila kitu! akaanza kuropoka mwenyewe...



..kaniombee msamaha kwa M/mungu niliongopa kwa ajili ya taifa langu nikajipa uzee,MUNGU anisamehe kwa uongo ule,



Kk Akaganda Kwa Mshtuko,sijui Ni Furaha Ilimzidi...





        "Zidu Yupo Wapi?" Kk akamuuliza baada ya kumuona jinsi alivyo kuwa akitetemeka 

"ni..nipo hapa malaika"

Zidu Akajibu Kwa Kubabaika,ni Wazi tayari dawa ile ilishampa wenge na mandhari ya kile chumba na kupoteza kwake nguvu akajijua tayari duniani alishakufa,alikuwa nusu mwendawazimu!,moyoni mwake alikuwa tayari kueleza kila kitu akaanza kuropoka mwenyewe...

...kaniombee msamaha kwa M/mungu Niliongopa Kwa ajili ya taifa langu nikajipa uzee,MUNGU anisamehe kwa uongo ule,

"embu ngoja kwanza!,ina maana wewe ni Zidu?!"

Kk Akaoji Pasina Kuamini,alipikicha Macho Yake Kama Ni Ndoto Azinduke,Zidu kidogo angeshtuka kwa swali lile,ila Kk Akamuwah

"mimi Kwa Jina Naitwa Malaika Tul Nafsi Mimi Ndo Nafs Yako,ila Si Kwamba Najua Kila Kitu Chako Ivyo Ili Nikakuombe Msamaha huna Budi kunielezea a to z ya maisha yako...

Usinidanganye Kitu hata kimoja! ok"

"ok,jina langu kamili naitwa Zidu Kite Ni Mzaliwa Wa Nchini Kinte japo sijaishi huko muda mrefu,baba yangu alikuwa ni mwanajeshi na alifia vitani mama yangu nilimuua kwa kuichoma nyumba alokuwa  na mwanaume mwingine baba yupo vitani mama anafanya ufuska nikamuulia mbali

Nikalelewa na mjomba angu!, awakujua kama mimi ndo niliye waulia dada yao baada ya kumaliza darasa la saba katika shule ya pampu mjomba aliona ni vyema nikajiunge na jeshi nikajiunga na jeshi,Siku Mbili Kabla Ya Kuhitimu Mimi Na Mwenzangu Kijo tulifanya tukio baya sana,sijui kama Mungu atansamehe,"

"tukio gani hilo?"

kk akaohoji,lengo lake ni ili kujidhihirisha yule ni Zidu Kweli au?

"mimi na mwenzangu Kijo tulimbaka kamanda wetu,kitendo hiko kilishtukiwa na uongoz wa jeshi ivyo siku ya mahafali sis tulifukuzwa rasmi jeshi...

Kwa akili yangu nilijua mambo yasingeishia pale,lazima tungetafutwa tuuwawe hivyo tukakimbilia mpaka Tanzania na kweli ilikuwa hivi yule Kamanda Alitufata Tanzania Nikamuua,Mungu ansamehe kwa kosa ilo ni kweli duniani nilikuwa na roho mbaya,sikuishia hapo tukaunda kundi la ujambazi tukawa tunaua na mwisho nika mgeuka hata na yule rafiki yangu nikamchomea polisi akakamatwa mali zote nikazimiliki mimi,ndugu malaika...

pamoja na kumiliki masupa maketi,maduka makubwa baadhi ya sheli bado ujambaz sikuuacha mwisho nikawa nawindwa na maaskari ni kaamua kukimbilia katika kijiji fulani kujificha mali zangu nikamuachia rafiki yangu niliye mwamin aziongoze!

Kijijin Kule Nltafuta Shamba Nkawa Mkulima Nikabadilisha Na Jina Nkawa Nikiitwa Gaspar Nilitokea Kuwa Na Rafik Yangu tulipendana sana japo maisha yake yalikuwa magumu nikaamua kumuunganishia mjini katika moja ya kampuni yangu akafanye kazi akawa akilipwa mshahara mnono!

Rose!...

"Rose Ndo Nani Huyo Rose?"

"tafuta kitabu cha morose (chuki) Kilichoandikwa Na Mtunzi ZUBER MARUMA utaipata stori yake yote!...

Kk Akashtuka,kisha Akatabasamu

"japo Malaika Huwa atusomagi vitabu vya hadidhi mimi ntaktafta nikisome,nielezee tu kwa ufupi!"

"Rose ni mwanamke nlitokea kumpenda,naye alikuwa ni rafiki na mwanamke mmoja alokuwa ni malaya sana pale kijijini MERY ndo jina lake,baada ya maisha kumwendea vizur Erick akarudi kijijin kuoa kwa bahati mbaya akampenda Mery Yule Malaya,nilimuonya Ila Akuelewa Akamuoa...

Sasa stori ile ikaanza kumvutia kk,

"ikawaje sasa?"

"pesa mwana haramu,kitambo sana kumbe mpz wangu alishampenda Erick,siku Ya Kuondoka Wakaondoka Wote Kisingizio Rose anaenda kuwa mfanyakazi...

Hapo Moyoni Mwangu Kukazalishwa Chuki Nami Nikarudi Mjini Ambapo Ktk Uchunguz Wangu Nilikuja Kugundua Erick Na Rose Wanamahusiano Na Wanamtesa Vibaya Sana Mery,nikaandaa majaribu kadhaa juu ya binti yule yote aliyavuka nikaamua kuish naye kama mke wangu Rose,Erick na yule rafik yangu waliishia rumande baada ya kupanga kunidhulumu,ila pamoja na yote bado nilikuwa nikiisha kwa kujificha mpaka kilipozuka kisa hiki cha kiapo(agano la damu) season 1

"una maana gani kusema hivyo?"

"siku moja niliitwa na waziri wa ulinzi mh Alex Kwanza Akanipa Uhuru Na Kunirudisha Jeshi,mwisho Akanipa Kaz Kumuua Isack!"

"eeh Isack Yule Rafiki Yako?"

"yah Of Corze,mara Kadhaa Nilijaribu Nikashindwa Mwisho Yule Dogo Tukijua Tumemuua tukamuuzia marekan kufika huko kumbe yu hai nami nikasafir kumfata huko kumbe yule mh anatembea na mke wangu bwana!"

"what pole sana!"

"nilikamatwa akuja kunitoa mpaka serikal ya marekani iliponitoa na kuniunganisha na Isack tukala Kiapo kulipiza kisasi na kwel tulilipa japo nilimpoteza mke wangu Mery na mwanangu naweza kuwaona?"

"usijal utawaona endelea!"

"baada ya opereshen ile kufanikiwa kwa asilimia 100 ndipo nikaitajika kinte kwa kazi hii ilo ondoka na roho yangu ila ukwel na aman alo uondosha moyo wangu ni mwanamke ni mpendaye nilikula kiapo kutokumuua,KATARINA nilimpenda sana,lau kama kaniua kwa manufaa ya taifa lake ni aman ya moyo wangu,nilisitisha kazi ilo nipeleka Ganyama Ya Kumuua Rais Wao Mshenzi Kwa Sababu Yake,nimejifanya Mzee Kusudi Niwe Na Muona Kila Dakika,japo Alikuwa Na Mpz Wake Nilivumilia Mateso Yote,ila Mwanangu...

Zidu Akajikuta Analia,hata Katarina mwenyewe maneno yale yalimsisimua akajikuta akienda na kumkumbatia!

Zidu Akaduwaaa

"nisamehe Zidu Natamka Wazi Hata Mimi Nakupenda!"..







Kazi ya moyo ni kusukuma damu lakin Zidu Moyo Wake Anaupa Kazi nyingine ya kupenda,tena mbaya zaidi anampenda mtu alopewa dhima ya kumsaka akashindwa,mwenye kiu ya kurudisha heshima yake kwa Rais Wake Kuwa anaweza!,je nin kiliendelea tusonge...



Moyo Wake Ulijawa Na Uzuni,penzi La Zidu Kwake Lilikuwa Ni Kubwa Akuweza Kulilinganisha Na Chochote!,



Akajikuta hata naye akishindwa zizuhia hisia zake na kumfungulia!,'Sai' hakuwa na mapenzi naye,kwanza alimuona mnafki wa mapenzi,kumchochea kwa raisi akanyang'anywa ile tenda akapewa yeye,kwake alikuwa ni mnafki!



"asante kwa kuufungua moyo wako juu yangu Zidu,pole kwa yote yalokukumba!"



akafungua kile kitambaa!



"katarina?!"



Zidu Akaita Pasina Kuamini

"ni Mimi babaa,ujafa Zidu,ila Nilifanikiwa Kukulevya Nikakuleta Katika Nyumba Yangu,mimi Ni Daktar Mtaalamu Wa Saikolojia Pia...



Ni Mzaliwa Wa huku ganyama historia yangu kwa ufupi,baada ya kumaliza kozi yangu ya udaktari jeshi lilinichukua kama daktar wa jeshi ila ilipaswa niingie katika mafunzo kidogo,uhodari wangu katika mafunzo ukanipa nafas nyingi zaidi mpaka kufanikiwa kuwa komandoo,nilipomaliza mafunzo kazi yangu ya kwanza ndo hii ya kukusaka wewe,ila kama wewe ulivyozama kwangu,nami vivyo hivyo nimezama kwako Zidu,nimegundua Una hisia nzito juu yangu nami vile vile kwa kugundua hilo nimezalisha hisia nzito juu yako *nakupenda Zidu* amini hili"



Hakika Zidu akuamini,kwanza furaha alokuwa nazo moja niya yeye kuwa mzima,akili ndo zilikuwa zikirudi,pili kumpata Katarina,kwa Nin asiwe na furaha!



"a..a...isack yupo wapi?!" akauliza huku mdomo ukimtetemeka kwa wasiwasi,ila ukuliacha tabasamu,Katarina naye akatabasamu,kutabasamu kwa mwanamke yule kukaiondosha hofu ilokuwa moyon mwa Zidu!



"Isack yupo salama kunywa kwanza haya maziwa uondoshe hii sumu Isack Utamuona Kesho Asubuh"



Zidu hakuwa tayari,akabugia maziwa kwa kuwa aling'ang'ania ikabidi tu Katarina ampeleke wakashuka mpaka ghorofa ya tatu!,



Walimkuta Isack Bado Kalala,hapo sasa moyo wa Zidu Ukawa Sawa,wakaelelekea Sasa Katika Chumba Kingine,hiki Kilikuwa Ni tofauti na vile vyumba viwili, hiki kilikuwa kizuri,kitanda cha sita kwa sita,meza aina ya dresing table,usiku huu akuna alokuwa na hamu ya kulala,kila mmoja alionekana kuwa na shahuku na mwenzake!



Wakazama Penzini!



"nala Kiapo Kwako Mpz,ntatupenda,ntakuwa Nawe bega kwa bega,ntaish nawe katika mazingira yoyote yale,yatabu ya shida,hata na raha pia,ntakusaidia pale utakapoitaji msahada wangu,nipo upande wako mpz,ntailea mimba yako,na nipo tayari kuwa mama wa wanao!"



Ni baada ya kufuraishana mioyo yao,na kila mmoja kuridhika na kukata kiu yake,Katarina akatoa ahadi kwa Zidu akiambatanisha na kiapo kutoka moyoni mwake!,kichwa Chake Alikuwa Kakilaza Kifuani Kwa Mwanamme Yule,naye Zidu akajibu...

"Nakupenda Katarina,nakupenda zaidi ya mwanzo nilivyokuwa nakupenda,nakupenda kwa kuwa umegundua kuwa nakupenda nala *KIAPO* kukupenda daima,kuish na wewe katika hali yoyote ulo nayo,dhiki,mateso na hata furaha pia...



Akamwomba Mdomo,Katarina akampa,wakazama tena penzini....



Hakika Usiku Ule Ulikuwa Ni Usiku wao



MASANJA ROAD



MPAKANI



Kulikuwa na maaskari wa kutosha wenye silaha nzito wote walikaa mafichoni,ndege ilotegemea kumchukua Isack tayari ilikuwa chini ya ulinzi walitegemea muda wowote Zidu angetokea,masaa,yakazidi kusonga,giza likazidi kutawala!



Wasiwasi Miongoni Mwao Ikazidi Kutawala,pengine Zidu alisha shtukia juu ya utekaji ule,mpaka panapambazuka Zidu Akuonekana,wakaondoka Wakiambatana Na Ndege Na Maaskar Wale Walokuja Kwa Ajili Ya Kumsaidia Isack!,

Kwa Mara Nyingine tena 'Sai' akawa kamkosa ZIDU K



asbuh,Katarina aliandaa chai,wakakaa mezani wawil wale,tayar walisha zoeana,walikuwa ni kama wapenzi wa muda mrefu,



"kinachofatia ni nin sasa mpz?!"



Katarina Akamuuliza Zidu akimwangalia kwa macho yalolegea,yalojaa hisia nzito!



"Nakusikiliza wewe mpz wangu!"



Zidu akajibu,mkononi akiwa kashika kipande cha mkate na kikombe cha chai,



"wewe ndo mwanaume,nakusikiliza!,"



"Katarina!"



"Rabeyka mume wangu!"



"Ni kweli unanipenda?!"



Katarina akashtuka,ina maana Zidu akumuamin au!?,naye akamuuliza!



"Kwa Nin Waniuliza Ivyo Mpz!?"



Zidu akakunja sura kutofuraishwa na jibu lile,akatasua mdomo wake!...



"Toka nimeishi Tanzania Nimegundua Sifa moja Kuu ya kumgundua m Tanzania pindi ukimuuliza swali uwa anakujibu kwa swali,wewe ni Mganyama Au m Tanzania niambie ukwel tafadhali!"



Katarina akaachia kicheko hafifu,kisha akajibu eti kwa aibu...



"Mimi NI Mganyama ila nimeishi sana Tanzania Kabla Sijaenda Cuba Kusoma,hivyo Nadhani Nimeiga tabia ya huko!"



"mh! yawezekana,ulikuwa kikazi au!,"



"yah,kuna kisa kimoja kimeandikwa na mwandish Zuber Maruma 'kufa tu' (hakuna namna) nilicheza kama muhusika mkuu,nilitumwa na taifa langu la Ganyama Nikamsake Suje Lion Mafia Mpumbavu Fulan alokimbilia Tanzania!,dah Nilikutana Na Mikiki Mikiki Kule,tafuta Icho Kitabu Soma Utajua Mengi tu nlopitia"



"ok! sawa,utansaidiaje katika kazi yangu ilo nleta huku!"



Ghafla Katarina Akabadilika,akakumbuka *Kiapo* Alichokula Jeshini,kulitumikia taifa lake,leo anasaliti?!,hapana *KIAPO* alichokula mbele ya rais,mbele ya mh wazir ambaye kwa sasa alistaafishwa,vikawa vikimsuta,haraka sana chuki ikaanza kujijenga moyoni mwake juu ya Zidu,akakumbuka Yule Ni Hadui Yake Na Si Rafik Yake!



Ghafla tu mawazo yakambadilika!...









Yah kuna kisa kimoja kimeandikwa na mwandish Zuber Maruma 'kufa tu' (hakuna namna) nilicheza kama muhusika mkuu,nilitumwa na taifa langu la Ganyama Nikamsake Suje Lion Mafia Mpumbavu Fulan alokimbilia Tanzania!,dah Nilikutana Na Mikiki Mikiki Kule,tafuta Icho Kitabu Soma Utajua Mengi tu nlopitia"



"ok! sawa,utansaidiaje katika kazi yangu ilo nleta huku!"



Ghafla Katarina Akabadilika, akakumbuka *Kiapo* Alichokula Jeshini,kulitumikia taifa lake,leo anasaliti?!,hapana *KIAPO* alichokula mbele ya rais,mbele ya mh wazir ambaye kwa sasa alistaafishwa,vikawa vikimsuta,haraka sana chuki ikaanza kujijenga moyoni mwake juu ya Zidu,akakumbuka Yule Ni adui Yake Na Si Rafik Yake!



Ghafla tu mawazo yakambadilika!...



TUSONGE



Lakini Kabla ajafikiria kitu cha kufanya akakumbuka kitu kingine!



Kama Ni Kiapo,hata Zidu itakuwa alikula nchini kwake,ila penz lake limefanya liyeyushe kiapo kile,ukishikwa shikamana,kwa nin yeye atake kusaliti kiapo walichokula jana na hata dakika chache zilizopita?!



"nala *kiapo* kwako mpz,ntakupenda,ntakuwa nawe bega kwa bega,ntaishi nawe katika mazingira yoyote yale yatabu,ya shida hata na raha pia *NTAKUSAIDIA PALE UTAKAPOITAJI MSAADA WANGU*,nipo upande wako mpz,ntailea mimba yako na nipo tayar kuwa mama wa wanao"



Ni Maneno Mazito aliyo mwambia Zidu Jana tu iweje leo atake kuyasaliti?,si ndo yeye aloyasema,roho yenyewe ikaanza kumsuta!



'kama wewe ulivyosaliti taifa lako ukaniangaikia mimi,nitakulipa kwa kukusaidia mpz!'



"Niliapa kukusaidia pindi ukihitaji msaada kwangu mpz,je ni msaada gani unaouhitaji nikusaidie!"



"mbinu za kufanya kumwangamiza Silvestar,"



Kk akatabasamu kidogo,akashika simu yake akaipekenyua pekenyua!,alikuwa akitazama ratiba za mikutano ya Raisi,

"wiki ijayo alhamis kama leo ndo utakapo mwangamiza rais?"



"kivipi?!" Zidu akaoji kwa shahuku,



"psiiii...



Katarina akamwekea kidole mdomoni ishara ya kumnyamazisha!,



....usiwe na haraka love umesahau mambo mazur huwa ayaitaji

uharaka?!,kuwa mvumilivu kwa saivi tumsafirishe kwanza Isack!,alafu Sijui Sai alipata habari gani usiku alitoka!,



"tunarudi kwake?!" Zidu akahoji,Katarina alimkata jicho,



"hivi wewe mwanaume unanipenda kweli?,"



"kwa nin waniuliza ivyo?!"



"sifa ya watanzania,kujibu kwa swal sivyo nilivyotaka unijibu we nambie nakupenda au sikupendi ila nataka nikutumie katika mipango yako mimi nimeamua kukusaidia kwa kuwa nakupenda,hata kama unipendi,kuwa muwaz kwangu usije badae ukaja niumiza!"



"yote hayo yanatokea wapi love?"



"Nijibu kwanza wanipenda au unipendi?!"



"nakupenda sana tu Katarina!,nadhan hata wewe mwenyewe walifahamu hilo"



"binafsi silifahamu ndo maana nikakuuliza!,lau kama ungekuwa unanpenda usingekuwa tayar turudi kule ukijua kwamba tukiwa kule natumika na yule Sai!"



Zidu Likacheka!



"ni Ndani Ya Kazi Mpz hiyo aina tabu!"



"ooh shit"



"hivi beby,ukumpenda yule mwanaume?"



"nilimpenda tena sana ila ni shoga,ana tabia za kike kike,mmbea mmbea ndo kitu kilichofanya nikamchukia, kaninyang'anya tenda ya kukukamata wewe kaichukua yeye,pasina kujali mi ntaumia kwa kias gani,huyo kwel alinipenda au alikuwa akicheza tu na hisia zangu?!"



"basi usijal mpz mi nipo kwa ajil ya kuzituliza,na kukufanya malkia ndani ya moyo wangu!"



"asante mpz!"



"kwa sasa tutaishi hapa,nataka urudi katika sura yako asilia siyo iyo,utakuwa ni wa ndan tu,mpaka maelekezo mengine yatakapotoka,hivi kule kijijin ulifanyaje fanyaje ukagundua siri za kule na kile kijiji ulikijuaje na ile familia ukaingiaje na mzee halisi wa ile familia yan mzee lyayatuu unajua mim nilikuwa nikikutilia mashaka toka mwanzo!"



Zidu Likacheka,"ha ha ha nami nilijua ulintilia shaka mapema ntakueleza sasa,baada ya kuja huku Bamala Na Kuona Msako Nisakwao,na Dau Lililotangazwa niliona hapa si mahali salama pa kuishi,nikakimbilia katika kile kijiji cha mzuva Land,na Kijiji Kile Nilikijua Kutoka Kwa Kamanda Wetu Lucy yule niliyemuua Tanzania,ndiyo alotuambia ishu ya kijiji kile,nilipofika nilikodi chumba gest,ile pale karibu na ile nyumba,sasa ile siku wakati naondoka kuja Bamala Kukuona Niliacha Nje Vurumai,wananchi Waliitoa Familia Yote Nje Wakawa Wakiipiga huku wakiilazimisha waseme mahal mzee lyayatuu alipokimbilia,



Hapo Nikakaririsha Lile Jina,nilijua Nikifika Kwenu Lazima Mngeitaj Kujua Natokea Wap Ni Sifa Ya Kijesh Hiyo nami niliijua! na si ndo ilivyokua!"



"dah! hakika wewe ni giniaz ulicheza mchezo asee,na ile nilivyokupa taharifa familia yako imeuwawa ulipopoteza fahamu,nilizitilia shaka sharubu na hizi ndevu zako nilipotaka kuzicho moa kichefu chefu kikanishika ni kaacha..."



"yah ile siku nilijifanyisha na ni liona ulivyo shituka,ila nikawai kuzibandika supa glu zikawa kama zangu vile!"



Wote Wakacheka...



Ghafla Simu Ya Katarina Ikaita Kucheki Mpigaji Ni My Husband Akakunja Sura Akapokea!



"nimeamua Niya anze maisha yangu,nawe fatilia maisha yako,kwa sasa mimi na wewe basi!" akakata,alipokea pasina salamu na akakata pasina maelezo,Sai akupiga tena!...



Sai asubuh alirejea nyumbani akiwa na hasira,alipofika nje ya jumba lake akakuta boda boda nyingi wakiwa wamevaa tshart za mwenzao alofariki,kwa mara ya kwanza si ndo Sai Akashtuka,akajua Kwamba Kijana Wa Pale Ndo Alouwawa Na Zidu,kivipi?!,na Kwa habar aloipata kijana yule alikuwa ni fbi kivip aje aweke kambi getin kwake!,



"hiv mteja wa mwisho kumpakia si huyu mzee wa hapa?"



Sai Alisikia Vijana Wawil Wakiulizana,ikabidi Akawahoji Vizuri,ndiyo,akapata Uhakika Mtu Wa Mwisho Kupakiwa Ni Yule Mzee Ambaye asbuh Katarina alimpa hela aende dukan akanunue nguo na ndani ya duka hilo hilo pia aliuwawa mtu,machale yakaanza kumcheza juu ya mzee yule!



Haraka sana akaingia ndan akamuulize baadhi ya maswal



ndani patupu!



Ndipo alipoamua kumpigia simu Katarina Naye Palepale Kumpa Makavu Kuwa Penz Lao Basi,jumlisha Na Zidu Jana Awakumkamata!...



Kichwan Akazidi Pata Picha



'usikute Muda Wote Hapa Nilikuwa Nikiishi Na Zidu Pasina Kujua,katarina Akimfuga! Dah embu Ngoja!'



palepale akatuma ile namba kitengo cha mawasiliano,kujua ile simu ilipigwa wapi,majibu yakaja ni



*MASAME HOUSE NO 5 UPANDE WA KULIA*



Palepale akaingia ndan ya gari yake mpaka kambini,gari nne zilizojaa makomandoo zikatoka kuelekea masame!



dakika nne nyumba ile ilizingirwa na jeshi,wakati huo sebuleni Katarina alikuwa akimnyoa ndevu Zidu ghafla wakasikia hodi,pasina kujal kwa kujiamin



KATARINA AKANYANYUKA TAYARI KWENDA KUFUNGUA MLANGO...



Ile kufungua tu,wanajeshi watano wakazama silaha nzito mkonon ZIDU NA Katarina Wakabaki Wameduwaa!,walikamatwa Patamu!



NJE KULIKUWA NA MAKOMANDOO KAMA ISHIRINI HIVI...







Mwanaume Wa Kazi Zidu K,Zidu katili anajikuta anaingia mikononi mwa makomandoo wa Ganyama,akiwa Pamoja Na Mpz wake Katarina Katika Nyumba hiyo hiyo yupo pia Isack Je Unahisi Wataokoka?!



Songa Nayo Kujua Ni Nin Kiliendelea!



Zidu Na Katarina Wakabaki Wamepigwa Na butwaa mitutu takribani minne ya silaha ilikuwa imemuelekezea yeye na mtutu mmoja wa mwanaume 'Sai' umemuelekezea katarina!



Moyoni Mwa Zidu Sasa alijua amepatikana,alijua akifanya 'mistake' kidogo angeyapoteza maisha yake,na wale ni makomandoo ni zaidi ya wanajeshi,akajitahadharisha,alipo mtupia jicho wa pembeni yake Katarina alishughudia chozi likimdondoka,akujua binti yule alompenda zaidi ya kitu chochote katika ulimwengu huu alikuwa akilia kwa kipi!,



Ila dakika ilofatia alijua,ni baada ya kumshughudia Katarina akienda mpigia magoti 'Sai' huku akilia akaanza kuomba msamaha,



"nisamehe Mpz Wangu,ni Tamaa tu,za kidunia mi si msaliti ni toe huku mpz!..."



Maneno Yale Yalimshangaza sana Zidu akuamin kama yanatoka mdomoni kwa mwanamke ambaye dakika chache tu alikula kiapo kumpenda,kuwa nae kwenye shida na raha kuto msaliti,mbona tena anamsaliti?!...



Hapana akutaka kukubali kirahisi akajua pengine ile ni janja tu ya komandoo lile la kike,



janja?!



Alikosea tena sana tu kuwaza hivyo,



Katarina alikuwa katika uoga ambao sio wa kawaida,isitoshe ndo kwanza hakuwa hata na muda mrefu toka ametoka mafunzoni afe kizembe,si kwa mwanamke asee!



Mwanamke Ua Na Moyo Wa Peke Yake,



Sai Alimtazama Kwa tabasamu baya tena la dharau,akaachia jicheko la kitajiri,la kuridhika!



"nilikuwa na mashaka na wewe mwanamke ulikaa na huyu mzee kumbe unajua ndo Zidu Ukamfuga Ukijifanya Umjui Kumbe Unacheza Na Akili Yangu Siyo?!,"



Ghafla Akamtandika teke la tumbo!,katarina Akashika tumbo!,



kosa,



Bora Uchezee Pengine Lakini Si Kwa Mtoto Wake,si Katika tumbo la katarina,mwanaume akujua kapata wapi nguvu ghafla akapanchu juu akiwazawadia wale watu wa nne teke aina ya 'double tik tak' teke hizi upigwa dabo dabo mmoja wapo akamnyang'anya silaha kufumba na kufumbua pipo zote nne zilikuwa chini pasina uhai,huku Sai Naye Akiwa Kalala Chini,mguu Wa Zidu Ukiwa Shingoni Kwake!



"nichezee Popote Lakin Si Mwanangu,si Damu Yangu,si Mrithi Wangu Kijana Umenikosea Sana Kabla Sijampeleka huyu hosptal nakuua kwa kifo kibaya sana k..m..nina 'akatusi' uso ulikunjika kwa hasira bado katarina alikuwa akigalagala maumivu,Sai Chini Pale Pamoja Na Kuwa Katika Maumivu Makali alikuwa akitabasamu!



"wachaaaa" ghafla nyuma yake ikasikika sauti,ni sauti ya mtu alo mfahamu,tena ilitoka katika hali ya maumivu makali,alipogeuka kumwangalia kujiakikishia ni Kwel Yule alikuwa ni Isack!,hakiwa chini ya ulinzi mkali



Point Ile Ya Kugeuka Nyuma 'Sai' aliitumia vizuri kwani alikusanya nguvu zake akaushika ule mguu kwa mikono miwili akaunyanyua na kuuweka pembeni sambamba na kunyanyuka akiachia teke jingine silaha ya Zidu Ikaenda kulee akapepesuka,mwanaume Akajirusha Akam'bambikiza Teke Lingine Zidu Kuleee Likajigonga Kwenye Ukuta Chini!...



Wanajeshi Wale Walo Mtoa Isack Wawili Wakachepuka Pale Alipozidu Kabla ajaamka wakamuwah na kumfunga pingu Mikononi Na Miguuni,hapo Ndo Wakawa Wamemuweza,sasa hata Sai akahema!



"niueni ila katarina mpeleken hosptal na isack mi nipo tayari kufa! niueni!"



Zidu akawa akipiga kelele auliwe tu!,kwani alijua pale asingepona tena!...



alijua ule ndo mwisho wa maisha yake,je angeuliwa kifo cha namna gani,masikini jitu katili alikujua!



'Uko Ninapoenda,nako Siyo Kwema hata bora na duniani kule nitaishi motoni milele,nimeua sana mimi tena bila huruma,wasio na hatia na wenye hatia,sijawai ingia mlango wa kanisani mimi,nilikuwa na mali sadaka sijawah toa nan hatarithi mali zangu,na tegemeo langu ndo huyo mtoto mama yake mwenyewe dah! sijui tutaenda nae au vipi'



Mawazo mabaya sasa yakaanza kumjia!...



Ndugu Msomaji,wewe Mwenyewe Unadhan hapo angeponaje?!,lazima akate tamaa!



Wakati huo kiongozi wa makomandoo wale mh "Sai" muda ule simu ilikuwa masikioni akisubiri tu mh Rais apokee,ampe taharifa ile nzur kwake,kwel Rais Silvestar akapokea...



"mh Raisi nimefanikiwa kumkamata Zidu,akiwa Na Isack Pamoja Na Msaliti Wetu Katarina!"



Maskini Pamoja Na Katarina Kuomba Kwake Kote 'Sai' hakuwa tayari kumsikiliza akamjumlisha,Rais akuamin alifurah,tunangoja idhini kwako tuwaue!



"ua! leta kwangu maiti!"



Rais Sili akatoa agizo,na kwa kuwa aliweka loud wote walisikia,maskin nan angemuokoa mwenzake,Zidu alibaki akimlilia mwanamke ampendaye KATARINA,



"msimuue Katarina Wangu,niueni Mimi,msiniulie Mwanangu Niueni Mimi,mwananguu"



Mwanaume Akawa Akilia!



"tukuue Kifo gani wewe mk..'tusi' kwa jinsi ulivyo ntesa leo tutakugeuza chekeche kwa matundu ya risasi mfungeni kwenye paaa



Wanajeshi Kadhaa Wakamnyanyua,jitu Katili Likafungwa Juu,



ISACK NA KATARINA NAO WALIKUWA WASHAPIGWA PINGU,



Usije ukakaa ukadhan hao ndo msaada



wanajeshi wakajipanga mstar mmoja mrefu nyuma nako wakajipanga,wote wakanyanyua silaha zao!



"nahesabu moja mpaka tatu nikimaliza tatu wote mnamshambulia mkikianza kichwa then mwili ok?!"



Wote wakajinyanyua juu kidogo ishara ya heshima mwanaume akaanza kuhesabu



MOJA....



MBILI.........



Kararina na Isack kwa uwoga wakayafumba macho yao hawakuwa tayari kuuona ubongo wa Zidu ukitawanywa hapo chini



Zidu pia kwa upande wake yeye Mwenyewe alikuwa naye kafumba macho yake tayari kukipokea kifo alijua sekunde inayofatia anaenda kuonana ana kwa ana na Izrael halisi akaanza kujuta na kujilaumu kwa kutofanya ibada hata siku moja sasa anaenda kujibu nini!



Mashaka yakazidi kujijenga moyoni mwake nilijiita izrael wa kibinadamu....



Ghafla akakatishwa mawazo yake baada ya kuanza kuisikia tatu ikianzwa kutajwa na vizuizo risasi vikianza kuachiwa



Tat....



TUONANE SEHEMU YA MWISHO YA SEASON HII







Hakuna marefu yasiyo na ncha,hatimaye mwisho wa Zidu unaonekana kufika,baada ya kukamatwa anafungwa juu na kugeuzwa shabaha,tumalizie episode hii ya mwisho kujua nin hatma yake!...



IKULU



Rais Silvestar akiwa na mke wake mezani wanakula chakula,ghafla simu yake ikaita haraka sana akapokea



"unasema?!" akauliza pasina kuamini macho kayatoa pima mkewe akabaki akimwangalia kwa mshangao



"kazi nzuri,kijana ninacho itaji kwangu iletwe miili yao tu"

Akakata,



"ni Nini Mume Wangu"



Mke Wake Alotambulika Kwa Jina La Jacklin Akamuoji



"wale Walokuwa Wakinikosesha Usingizi Mke Wangu Wamekamatwa!"



"unasema?!"



Hata Jack binafsi akuamini,akajikuta kamkumbatia mume wake,katika kumkumbatia kule akamnong'oneza kitu!



"ila umekosea kutoa amri waletwe kwako wakiwa maiti! mume wangu,wiki ijayo uhuru day wazo langu siku hiyo ya uhuru tuwanyonge atharani,kuwe na waandishi wa kitaifa na kimataifa,hili litakuwa onyo sidhani kama kuna mtu atakubali tena kutumwa kuja huku kukuua mfalme wangu!"



Rais akaachia tabasamu



"fact!,sikukosea kukuchagua wewe kuwa mke wangu,ngoja nizuie haraka...



Palepale Rais akashika simu yake tena,akampigia 'Sai'



Sai Kabla Ajamalizia Kutaja Nne Ghafla Simu Yake Ikaita,haraka Sana Akaipokea,



"msiwaue,watauawa siku ya uhuru juma tatu ya wiki ijayo!,katika kiwanja kikuu cha mashujaa



"sawa muheshimiwa"



Pale Pale Sai baada ya kukata simu akatoa amri Zidu afunguliwe,akatolewa chini ya ulinzi mkali msafara kibao wa magari ya kijeshi ukatoka katika nyumba ile!,safari yao ikaishia katika gerezaj kubwa la jeannamu jail,



Gereza hili lilikuwa la kijeshi kila mtu akawekwa katika chumba chake,tena pamoja na kwamba walifungwa pingu pia walifuwa miguu yao na minyororo mizito humo chumbani,



Siku Ile Ikapita Hakukuwa Na Watu Walowatembelea Hata Kuwapa Chakula,zaidi Ya Viongoz Mbalimbali Kuja Kuwa Angalia! Kwa Nje,lango alikufunguliwa,siku ya pili ikapita,njaa sasa zikawa zikishambulia tumbo zao,kila mmoja kwa upande wake!

Muda Wote Zidu Lilikuwa Likitaja tu jina la Katarina,mwanangu!...



Hawo Pekee Ndo Aliye Waonea Huruma,yeye Akujijal Kabisa Kufa Kwake Aliona Sawa Tu,ila Mrithi Wa Mali Zake,



Siku Ya Pili Yake Usiku Ndipo Geti Lilipofunguliwa,yakaingia Jitu Moja Lilokomaa Mkononi Lilishika Hotpot Ya Chakula!,ulikuwa Ni Wali Wenye Maharage Ya Kuhesabu Na Kijiko



"natokea Haki Za Binadamu,nipo Hapa Kukulisha,ukupaswa Kula Wewe Haya Fungua Mdomo!...



Zidu Ghafla Akafungua Mdomo Na Kumtemea Mate Usoni,jitu Lile Lilikasirika likaweka chakula Chini,na Kuanza Kumpiga,mateke Ya tumboni mdomoni pasina huruma, Zidu Maskin Alikuwa Goigoi alibaki tu kuita katarina,niitie katarina,katarina,niitieni katarina...



Damu mdomoni Zikawa Zikimtoka,kizunguzungu Kikali Kikamshika,jamaa Yule Alizidi Mpiga Mateke Mpaka Sasa Akawa Akitoa Mabonge Ya Damu! Ghafla Geti Likafunguliwa Wakaingia Makomandoo Wengine Watano



"chanto Unafanya Nini Utaua,muache Huyu Utajitafutia Kifo Tu"



Wale Makomandoo Waloingia Wakawa Wakimzuia Mwenzao Kuendelea Kumuadhibu Zidu!,ambaye Bado Alijilalia Akisema Niitie Katarina,akapoteza Fahamu!...



Wale Makomandoo wakatoka na mwenzao Chanto Alokuwa Akitusi Na Kulaani Eti Kwa Nin Akuachwa Aendelee Kumfundisha Adabu Zidu!



Upande Mwingine Wa Chumba Alicholala Isack Naye Kwa Upande Wake Alifungwa Mnyororo Hakiwa Katika Chumba Chake Peke Yake!...



Kichwa Kilimuuma Kwa Kulia,majuto Makuu Yalimwandama,alijuta Kwa Kuto Msikiliza Zidu,akamkumbuka Mke Wake Mery,akajikuta Akizidi Kulia Sasa Anaenda Kufa Kwa Kimbelembele Chake,nan Sasa Wa Kumuokoa,njaa Ilimuuma Siku Ya Pili Sasa Alikuwa Ajatia Kitu Mdomoni Ghafla Geti Likafunguliwa Na Jitu Likiwa Na Chakula Likaingia,alikumsemesha Kitu Likafungua Hotpot Na Kuchota Chakula katika kijiko isack akafungua mdomo wake,jitu lile lika weka kijiko chenye chakula katika mdomo wa Isack,alichota tu vijiko vitatu akafunga hotpot yake



"mzee sijashiba mzee,niongezee chakula na maji tafadhali!"



isack aliongea kwa kusihi,jamaa likageuka na kelbu moja matata ilotua vizur sana usoni!

Isack akawa kimya kiherehere kikamkata



"ujaja hapa kula hivyo vijiko vitatu si ili ushibe hapana bali ni ili uendelee kuishi mpaka siku ya muungano"



mtu yule akatoka!



upande wa wanawake katika chumba alicho binti Katarina,naye Hakuwa Tofauti Na Isack,yeye Alikuwa Akilia Huku Akilitaja Jina La Sai,huyu Pekee Ndo alimuona anaweza kumtoa katika mateso yale,alijuta kulisaliti taifa lake,katu akujua mwenzake Zidu Alikuwa Kafa Kaoza Kwake Na Mpaka Muda Ule Alikuwa Akilitata Tu Jina Lake...



Ghafla Naye Lango Likafunguwa Akaingia Bibi Mmoja Na Sahani Ya Chakula Kama Ilivyokuwa Kwa Isack Naye Akalishwa Vijiko Vitatu,

"naomba Niitiwe Sai"

Bibi Yule Akacheka,kwa Wakati Huo Sai Alikuwa Marekan Akistarehe,na Kwa Sasa Kapandishwa Cheo Kawa Kamishna Mkuu Aje Akuone Huku,unachekesha Sana Binti...



Katarina Akazidi Kulia Na Kukata Tamaa Hakika Zidu Alikuwa Kamponza!



Zidu Akiwa Kapoteza Fahamu Akalishwa Chakula Hivyo Hivyo

kuulinda uhai wake,alipo zinduka akajikuta ana nguvu zikapita tena siku mbili bila kula na chakula kilipoletwa Zidu alikuwa mjeuri,katarina na isack walikula!



Hatimaye Siku Ya Muungano Ikawadia,katika Uwanja Mkuu Wa Mashujaa Katika Mti Mmoja Mkubwa Kulifungwa Vitanzi Vitatu Chin Yake Kukiwa Na Viti,ambaye Juu Yake Alisimama Zidu,isack Na Katarina Huku Pembeni Ya Viti Vile Pakiwa Na Mtu Wa Kutengua



Uwanja Ulifurika Watu,waandishi Mbalimbal Walikwepo Kuripoti tukio lile,litangazwe dunia nzima iwe fundisho!



vitanzi vikavalishwa katika vichwa vyao,Rais akapewa maiki tayar kuruhusu unyongaji kwani kisemwacho na Rais Wa taifa flan kwa kosa lililotendeka katika nchi yake ni sheria!



"wametutesa sana,wameua wanajeshi wetu wengi sanna,na mwisho rais Moreti Katuma Ako Kajitu Hapo Eti Kaje Kaniue! Teh Teh Teh Leo Kanakufa kenyewe Bhana...



Umati Wote Ukaangua Kicheko,Rais Akajifuta jasho kidogo kisha akaendelea....



...tumeamua tuwanyonge adharani kila mtu aone hili iwe fundisho hata kwa mwengine yeyote atakayetumwa uhuru hoyee"



"oyeee"



"kidumu chama cha uhuru"



"kidumuuu"



"sasa ninacho semaa nitahesabu moja mpaka tatu,then killers mtafanya yenu wavisheni vitanzi"



WATATU WALE WAKAVALISHWA VITANZI!



Rais Akaanza kuhesabu,hali ya ulinzi mahali pale ilikuwa ya uhakika!



moja...



mbilii....



ta...



EMBU FANYA MPANGO WA MALIPO TUANZE SEASON 5 KUJUA JE ULE NDO MWISHO WA KINA ISACK,ZIDU NA KATARINA?!



KWA SEASON 4 TUISHIE HAPO





KARIBUNI TUSONGE SEASON 5


0 comments:

Post a Comment

Blog