Search This Blog

Thursday 29 December 2022

KUFA TU HAKUNA NAMNA - 5

   

Simulizi : Kufa Tu Hakuna Namna 

Sehemu Ya Tano (5)



Katarina akiwa juu kabisa ya mti akiwa kavaa mavazi kama ya 'zk' ayavaayo kibindoni kukiwa na pistol yenye kiwambo cha kuzuia sauti aliiona gari ikija kwa spindi mwasho wa taa ndo ulo mjulisha ujio wa gari hizo hakakaa tayari kule juu pistol ikiwa mkononi kitendo tu cha ile gari kufika usawa wake binti akajirusha na kupitia kioo cha mbele kwa kukivunja kupitia miguu yake miwili mkono ukiwa umeshika pisto,miguu ile ilovunja kioo cha mbele,mguu mmoja ukamtandika teke dereva huku risasi kadhaa zikicharanga vifua vya vijana wale wawili wa nyuma walokuwa pembeni ya Zena,lile teke alilopigwa dereva lika mpeleka nyuma naye akala risas kadhaa wakati ule gari lilikuwa bado kwenye mwendo,akakanyaga breki,kitendo tu cha gari kusimama tayari kulikuwa na maiti za watu wa tatu,ndani ya sekunde kadhaa hata dakika aikukatika,


huyo alikuwa ndo komandoo Katarina Mwanamke jasiri alowah kumtesa mara kadhaa Zidu katika riwaya ya kiapo 2 yeye akiwa kama mwanajeshi wa Ganyama Zidu akiwa Mkinte alotumwa ganyama akamuuwe raisi wa nchi hiyo...




Kitendo Kile hata Zena akuamini,binti tayari alikuwa kwenye mstelingi,




"pole sana binti,nimekuja kwa ajili ya uwokozi wako..."




Katarina aliongea huku akimtazama Zena ambaye alipoisikia tu sauti aliitambua kama alishaisikia mahali ila akuitambua kama ni ya yule alopania kumfunga siku chache nyuma!




Katu akujua kama ndo huyu leo kamuokoa kwenye mdomo wa kifo,




Zena akawa akimwoneshea binti yule nyuma,kwa furaha tu hata sauti aikumtoka,akimaanisha kuna watu wanaowafatilia nyuma,Katarina alielewa ila akujali tayar alishakuwa na maelezo...




Green Kobra na Mudy kule nyuma walilishughudia tukio lile ninja akitua kwenye kioo,kwa mtuo usio wa kawaida kabla awa jaamua kitu Richard alichomoa vifu viwili na kwa ghafla akamzawadia kila mmoja chake dereva cha mgongoni yule alokaa naye cha kifuani,baada ya kuwachoma wakati wakitapatapa akavitoa na kuondoka na uhai wao,akashuka kwenye gari na kuelekea gari la mbele wakaishusha ile miili kwa kutumia gari ile ile wakaendelea na safari kuifata barabara ya vumbi waloenda kutokea makabe wakaelekea mbezi mwisho Richard akamwelekeza nyumba alohitaji wafikie,waliingia katika nyumba hiyo Kwa kuwa katarina alishapitia udaktari na kila nyumba ya mpelelez au askar huwa aikosi madawa ya vidonda,Katarina akashika dhima ya kumtibu Zena,




Hakuna aliyelala mpaka saa tatu Dani Aliwasili akawa beba watatu wale na kuwapeleka ndani ya kijiji cha Zinga wakaweke kambi kwa muda kwanza hali ya hewa iwe shwari...




*** *** ***




SURA YA TANO




MASAKI




Ni katika eneo walilokuwa wakiishi watu matajiri,nyumba zote zilikuwa na geti na kuzungukwa na kuta zenye ulinzi wa shoti,pia nje ya geti kulikuwa na alama maalumu la vikosi vya ulinzi vilivyolinda nyumba hizo,




Pia tofauti na ulinzi huo nyingi ya nyumba hizo za kitajiri zilikuwa na kamera getini,katika moja ya majumba walokuwa wakihishi viongozi mbalimbali wa serikali ndani alikwepo mmama mmoja wa makamo alikuwa kakasirika vibaya sana,mbele yake alikwepo mwanaume kajiinamia chini kwa aibu,mwanamke yule alikuwa akiongea kwa aibu huku akiwa kashika picha kadhaa zilizo muonesha mwanaume yule na wasichana rika la mwanaye,




"mwanaume uoni aibu,mimi sikutoshelezi,mke wako akutoshelezi mpaka unatoka na watoto wadogo,tuna ua kukulindia heshima yako,tunamwaga damu za viumbe wasio na hatia kwa uzembe wako utaacha lini hii tabia baba Jimmy"




Mwanamke Yule alizidi kulalamika kwa uchungu,mzee akujibu kitu,angejitetea nini na ushahidi ulikwepo mbele yake,




"awali ulitoka na yule msanii wa bongo movie ukapigwa picha na waandishi tukafanikiwa kuzidhibiti,bado tena juzi umepigwa picha hizi mpaka lini lakini?"




Madam 'S' alizidi kulalamika huku akimuonesha zile picha zilizokuwa katika simu walo mnyang'anya 'ZK' usiku wa siku ilopita...




"nisamehe mpz wangu kosa hili alitojirudia tena,sitokusaliti na wala sitokuumiza niamin mpz"




Waziri John aliongea kwa kusihi,




Mwanamama Salma au madam S kwa jina atambulikalo kazini alitokea kumpenda sana John na katika mapenz yao walibahatika kumpata mtoto mmoja Jimmy,




Jemes John alikuwa kashaoa na ana watoto kadhaa,penzi lake na mmama yule mrembo lilikuwa ni siri sana wakiwa wamejenga eneo lile la Masaki,




Ndipo alipokuwa akiishi madam S wazir alikuwa akitaman kukutana naye ilimpasa atafute kisingizio chochote kwa mke wake kwa kuwa ni mtu wa serikalin mke wake hakuwa na shaka nae zaid ya miaka 15 sasa madam 's' na wazir walikuwa katika mahusiano pasina mama wawili mke halali wa waziri kugundua ilo




Salma hakuwa na budi kwa mara nyingine kumsamehe mwanaume yule akampa na taharifa njema ya kufanikiwa kumpata 'ZK' na usiku huu wa leo ndo vijana wake wangeenda kummaliza msitu wa pande,msitu umezao damu za viumbe visivyo na hatia,Waziri alifurah sana na kumkumbatia madam 'S' aki mzawadia mvua ya mabusu kilichoendelea ni kuiunganisha miili yao kupata burudani kama pongezi kwa jambo lile...




awakujua....




awakujua kinachoenda kutokea.....




Na laiti wangejua,wasinge jipongeza kabisa!...






Katarina anafanikiwa kumuokoa 'ZK' na kuwa angamiza vijana hatari wa usalama wa taifa,




Upande wa pili tumegundua kumbe mkuu wa kitendo cha usalama wa taifa madam 'S' sababu kubwa ya kumlinda waziri kwa kuwa wana mahusiano ya muda mrefu tu,na wamebahatika kupata mtoto Jimmy ambaye bado atujaelezwa yupo wapi!




Tuendelee na riwaya hii kujua kilicho endelea...




Ulikuwa ni usiku mzuri kwao wote wawili,habari ile kwao ilikuwa ni njema,wakazidi kujipongeza kwa kuiunganisha miili yao katika usiku ule awakujua ni sangapi walipitiwa na usingizi...




Asb walioga wakapata kifungua kinywa wakaelekea kazini pamoja,




Madam "s" alishtuka kutopata simu hata moja ya kijana wake na alipopiga simu ziliita mpaka zikakata,




Kengele ya hatari ikagonga kwenye kichwa chake, machale ya kamcheza, mpaka inatimu saa nne vijana wake awakurejea wala hakupokea simu yoyote kutoka kwao wala awakupokea simu yake,alijua lazima itakuwa walitekwa kama si kuuwawa, haraka sana akashika mkonga wa simu yake na kupiga namba kadhaa alizo zijua yeye




"ndani ya dakika tano nakuomba ofisini kwangu"




Madam 's' akakata simu,baada ya kukata akatoka,




"don akija kama sijarudi mwambie ansubirie ndani ofisini humo sitokawia kurejea"




"Ok,bosi"




Madam baada ya kumpa taharifa binti yule katibu muhtas wake,akatoka ndani ya ofisi ile na kuelekea upande zilipo ofisi ya waziri mkuu na watendaji wake,




"mzee yupo ndani?!"




"ndiyo,"




"ana mgeni?!"




"hapana"




Madam 'S' akuuliza tena swali lingine,akachepuka kuelekea mahali ulipo mlango wa kuelekea ilipo ofisi ya waziri akaingia,




"mambo vipi mpz,mbona ghafla hata simu?"




"kuna dharura imetokea nahisi hali si salama" Madam 'S' aliongea huku akionesha wasiwasi wa waziwazi,




"jambo gani alijakaa sawa mpz mbona wataka kuntisha tena?"




"kina Pizo toka jana usiku mpaka leo muda huu naongea na wewe sijapata simu yao,na si hivyo tu hata nikijaribu kuwapigia awapokei"




"watakuwa salama kweli?"


Waziri Mkuu aliongea kwa wasiwasi,naye akionesha wazi kuelekea kukata tamaa




"ni vijana katika usalama wataifa nilitokea kuwa amini hasa Veko na mwenzake Pizo,ZK atakuwa kawashinda nguvu na kuwadhibiti?,lakini mbona simu zao zinapatikana?"




Madam S alizidi kuongea wasiwas wake kwa waziri mkuu




"ni vyema ukatuma vijana wakafatilie jambo hilo,"




"yes lov,nimemwita don nahisi atakuwa kashakuja ntampa hii kazi ngoja niende kuwa na aman mpz,ila uache umalaya unaona unavyo nitesa mpz?"




Madam 'S' aliongea huku akijinyanyua pale alipokuwa amekaa akamsogelea mpz wake na kumpiga busu,akatoka alikuwa tayari kurejea ofisini kwake hakuwa na shaka don atakuwa akimsubiria




****




Gari la kifahari lilipaki eneo maalumu la kwa ajili ya kupakia magari,mlango ukafunguka na kijana mtanashati alovaa suti yake ilomkaa vyema akashuka ndani ya gari ile,




Akapiga hatua zake ndefu kuelekea nyuma ya jengo lile la waziri mkuu kulipokuwa na ofisi nyingine ikiwemo ofisi ya usalama wa taifa




Jina lake kamili ni Gaspar Kimario,ila akupenda jina hili litambulike akajipachika Don G,




katika vijana katili walotambulika usalama wa taifa ukimtoa red deval,Don alikuwa katili asee,ni vigumu kudhani kuwa alikuwa na moyo wa kibinadamu,ila pindi ungemkuta akifanya ukatili wake ungeweza kumweka kwenye kundi la kishetani usingekosea,




Pia alikuwa ni mzuri kwenye mapigano,usalama wa taifa aliitwa kwa kazi maalumu tena za hatari zenye hitimisho la kuuwa,naye alijua kuua kweli,




Alielekea upande zilipo ofisi za usalama wa Taifa wala akuangaika kubisha hodi akazama ndani,akaenda moja kwa moja mpaka alipo 'sekretary' wa Madam 'S'




"madam yupo?"




"kasema umsubiri ofisini"




Don akuuliza swali lingine akausogelea mlango na kuufungua akazama ndani,




Punde Madam 'S' akatokea,




"kashakuja?!"




Akamuuliza yule mfanyakaz wake,aliyetingisha kichwa kukubali,madam 's' akazama ndani...




Don kumuona aliinuka ghafla na kupiga saluti madam akaipokea na kumpa ishara aketi,




Ikabidi aanze msimulia mwanzo kwa toka waziri alipopigwa picha na Sudi (kama Wenyewe Walivyojua"




Sudi Kutaka ela mpaka wakamuua,siri ile ikavuja wakaendelea kuua ili kuificha kumlinda waziri kuibuka kwa "zk" mpaka walipo mkamata wakati wanaenda kumuua msitu wa pande mawasiliano yakapotea mpaka muda huu




Don akawa kashaelewa kila kitu,akamtoa khofu kufatilia na kumletea ripoti,




"kwa sasa ntautembelea huo msitu sitotumia gari ila ntatumia pikipiki walitumia gari gani?!"




Madam 'S' akamweleza ok tairi zake zile zinashika sana ardhi,pia ntatumia "kinasa alama cha tairi ardhini" ikiwa sito ona alama hizo kwa macho ya kawaida,kaz hiyo ntaianza saivi"




Madam 'S' akatabasamu, akampigia simu kijana wake mmoja akamwambia ampatie Don,pikipiki alohitaji yeye ahakikishe iwe full tank,pia kipima tair ardhini,bastola smg yenye risas za kutosha na pia risas za akiba kwenye kibegi,jacket proof ilo alilivaa palepale akatoa koti la suti,silaha akaiweka kwenye mfuko maalumu na kuifunga nyuma ya pikipiki




Kijana akaingia barabarani




Nusu saa alikuwa katika lango la msitu mabwepande akupata tabu kuziona alama za matairi ya gari alizoambiwa ndiyo walotumia kina Pizo akuangaika kutumia kipima ardhi akaitoa ile bunduki pale nyuma akaivaa akapanda pikipiki na kuingia msituni akafata sasa zile alama za gari,alienda mpaka akaikuta ile miili minne,akamjulisha madam "S"




Madam akamwambia aachane nayo atatuma askari wakaichukue yeye aendelee kufata njia...




ahakikishe anamwokoa Richard,alijua lazima Richard atakuwa katekwa,wazo lililokuwa vichwan mwao lazima 'ZK' atakuwa kaokolewa na watu,ila sasa watu hao wana nia gan hasa kwa serikali?




mbele kidogo akaikuta gari yao ya pili imetelekezwa ila akazidi kuzifata alama za gari alizozikuta hapo...










Madam "s" anashtuka kutopokea simu ya vijana wake alowatuma wakamwangamize 'ZK' ndani ya msitu wa pande anaamua kumtuma kijana wake mwingine Don 'G' kufatilia na Don anamtaharifu juu ya kuikuta miili ya watu wake katikat ya pori anamwambia achane nayo aendelee kufatilia je nin kitaendelea?!




Don G aliendelea kufatilia njia ya vumbi akatokea makabe hapo alikutana na barabara ya lami iloelekea mbezi mwisho hapo sasa zile alama za gari akawa azioni tena na kile kifaa chake akikuweza kupima lamini,palepale njiani akamjulisha madam alo muomba arudi wafikirie njia nyingine ya kutumia




Madam alirejea na kumueleza waziri juu ya kufa kwa watu wao,waziri akashauri wamwagwe askari wa kutosha vijiji vya karibu ni pori lile ufanyike ukaguzi mkubwa,madam 's' akampa kazi Don asimamie swala lile...




*** *** ***




Zidu alikuwa na furaha sana toka Suzan amwambie ni mjamzito alijikuta akimpenda zaidi,kila dakika hata akiwa kazini alikuwa akiongea naye,




Suzan alikuwa sebuleni, akiangalia tv,ghafla mlio wa simu ukaingia ndani ya simu yake akuwa na shaka ni Zidu akaachia tabasamu jepesi akielekea kuifungua...




"Suzan mdogo wangu nakuomba achana na mume wangu kama unapenda kuendelea kuishi"




Suzan aliyatoa macho ya mshangao mapigo ya moyo wake yakaanza kumwenda mbio ile namba aliijua fika,ni namba ya aliyekuwa bosi wake Katarina,




Je kajuaje ana mahusiano na aliyekuwa mume wake,hakupata jibu ya swali lile,akajikuta akishindwa kujibu...




Zidu alipoingia jioni aliona tofauti alokuwa nayo Suzan,akamuulizakwa sauti ya upole Suzan akampa simu asome ile sms,




"yani huyu mpuuzi,shetani alo laaniwa ndo wakukutisha wewe?!"




Zidu aliongea kwa hasira akapiga zile namba azikupatikana,akatoka pale nyumbani kwa hasira na kuingia ndani ya gari lake




"sasa namfata huko huko anapokaa atantambua mimi ni nani,"




Zidu akaongea akiwa kakasirika




Hata Suzan alipo msihi aache kwani kwa kitendo kile kingeyaweka maisha yake hatarini zaidi,




"hapana alisababisha Salome mfanyakazi wangu kwenda kusikojulikana,akaona aitoshi anataka akupeperushe na wewe haiwezekani lazima nikamwoneshe"




Zidu akawasha gari na kutoka,alienda moja kwa moja mpaka alipokuwa akiishi Isack,muda huo Isack alikuwa kazini akagonga Mery akafungua akaingia kama kwake vile...




"huyu mwanamke yupo wapi mpumbavu sana alokosa haya..."




Alikagua kila chumba huku akitukana,hakutaka kumpa nafasi Mery ya kuzungumza,au kumsikiliza,




"mi naondoka hakirudi mwambie aache kufatilia maisha yangu!




Zidu akaingia ndani ya gari lake na kuondoka akiwa bado kakasirika,alijua ujumbe utafika na ndo lengo lake katu akujua kwa saivi Katarina alikuwa aishi pale,tayari alishapewa nyumba ya kifahari maeneo ya Mbezi akiwa chini ya kikosi cha usalama wa taifa (2) hiki kilimilikiwa na muheshimiwa raisi,kwa siri sana kupambana na kikosi (1) kilicho milikiwa na muheshimiwa waziri kilichokuwa na wanajeshi wa kutosha




KIJIJI CHA ZINGA




Hatimaye wanausalama wakaingia katika kijiji kile walianza kutafuta nyumba moja baada ya nyingine




Msako ulikuwa ni mkali gari zote zikikaguliwa,




Katika nyumba moja iliyoko ndani ndani ya kijiji kile,nyumba ya kawaida asbuh asbuh aliwasili Dani,akawagongea,




"kwa taharifa nilizo zipata ni kwamba leo vijana wa usalama wa taifa watakivamia kijiji hiki ivyo si salama kwa sasa,picha walo nayo niyakwako Zena ila kk wala mimi na Rich awajatujua Rich Inajulikana ulitekwa wewe itabidi tukufungie hapa hapa Kk ntakupeleke nyumbani kwako huko utamtibu Zena mpaka apone"




"huko awawezi kagua?"




"hapana mbezi yote ishakaguliwa,"




Rich akapigwa kutengenezewa majeraha ya uongo akafungwa kwenye chumba kimoja hao wenyewe wakaondoka,




Maaskari wale wa usalama wa taifa walifika katika ile nyumba na kumkuta Rich walimsaidia Rich alisema walitekwa na vijana wasopungua kumi wote walivaa ninja waliwaua wenzao porini na mimi kunileta huku wamemuokoa "zk" na baada ya kusikia ujio wenu wamekimbia ila wameniacha hai wakisema wanahitaji vyombo vya habari vipate uhuru!




madam 's' akashtuka,awali alidhani pengine hao watu walosemwa walitokea chama cha upinzani ccm lakin kutajwa kwa neno uhuru wa vyombo vya habari vikaleta hali ya mkanganyiko katika mawazo yake!




au ni waasi kutoka chama cha waandishi wa habari,hapana akakataa wazo hilo chama kiwe na wanajeshi,kwa ufahamu wake alijua maninja alotajiwa lazima watakuwa ni wanajeshi,watu wa kawaida wasingeweza kuwa angamiza vijana wao!




Na walijuaje 'zk' anaenda kuuwawa usiku? wa siku ile,




Kichwa Cha Madam kikaanza kumuuma kwa ajili ya mawazo,unajua pamoja na wote kuiona sura ya Zena hawakutambua kama alishakuwa afisa wa polisi,




Na wao walipo mkamata na kumtoa mask akuna alosubutu kumpiga picha mawazo ya vijana wote yaliishia katika kutesa,ivyo hali ikarudi ile ile kumtafuta 'ZK' mvaa mask,japo kwa sasa walijua ni wa kike atumiaye mavazi na sauti ya kiume,




"na wazo kwa kuwa sura yake unaikumbuka tumtafute mchoraji umwelezee jinsi alivyo naye amchore picha,hiyo picha tuifikishe makao makuu,askar nao wakawaida watusaidie kumsaka,kwenye vyombo vya habari atangazwe kama jambaz sugu zawadi nono itangazwe kwa atakayefanikisha kumpata,watu hawatajua kama ni 'ZK' yule sura yake si aitambuliki? tutumie advantage hiyo kumpata huyu"




"wewe ni hazina Don unamawazo mazuri sana,fanya hivyo niletee mchoraji hii ni njia rahisi sana ya kumpata huyu mtu!"




Don G akatabasamu,akachukua simu yake na kumpigia mtu alomjua yeye,akamwagiza aje pale ofisini...




Wakaelewana akakata simu,




"nusu saa hatakuwa hapa"




Don akaongea kwa sauti ya taratibu,madam s akaishia kutabasamu tu.








Msafiri Patrick Stephano alitambulika pia kwa jina la Pms kijana huyu mdogo kiumbo na kiumri pia lakini alijaliwa kipaji kikubwa cha uchoraji,




Pms na Don G walikuwa ni marafiki wa muda mrefu,kiajira pms alikuwa ni kinyozi na mara nyingi tu Don alipenda kuwepo saluni ya jamaa huyo mchoraji kupoteza muda,tenda za kuchora zilipotoka alimwachia saluni Don naye kuingia kazini,




Katu hapakuwa na mtu aliyewah kudhani au hata kuhisi kuwa hawa watu ni wapelelezi hatari kutoka usalama wa taifa,kitahani walikwepo kama masela tena masharobaro,na vinyozi...




Don G baada ya kushika simu alimtafuta Pms na kumwelekeza aje ofisini kwa mkuu,pms akafunga saluni yake akaenda mpaka kwenye nyumba yake ya siri alipotoka alikuwa ndani ya gari yake,moja kwa moja mpaka ofisini




Alishuka na kuelea ofisin kwa madam 'S' akapiga saluti na kuketi




"kuna picha ya mtu 'p' tunahitaji uchore taswira yake tumsake huyu mtu kutumia polisi raia,kutumia trafki,migambo na hata jeshi pia"




Pms akujibu kitu akavua kabegi chake,akatoa daftari lisilo na mistari penseli na aina tofauti tofaut za rangi




Akafunua daftari na kuanza sasa kuchora kwa sifa alizopewa na madam alizo muona ile siku asbuh alipoambiwa na vijana wake kukamatwa kwake!




Alipomaliza akaipaka na rangi ile picha,kilikuwa ni kitendo kilichobeba dakika 22 na sekunde kadhaa kukamilika kwa picha ile madam alipoiona aliishia kutabasamu na kutingisha kichwa,




'ZK, mwanamke amnyimaye usingizi mpz wangu ndo huyu hakika'




Madam 'S' aliwaza akiitazama ile picha kwa chuki,




"kazi nzuri 'p' hii picha ntaipeleka makao makuu mtu huyu aswake,ntaipeleka katika vyombo vyote vya habari nahakikisha huyu binti anapatikana we ngoja!"




Madam 'S' aliongea kwa sauti ya uchungu,akutaka kupoteza muda akawaacha vijana wakaendelee na kazi kusudi yeye aelekee makao makuu ya polisi kuripoti mtu yule




UPANDE MWINGINE




MBEZI




Hatimaye Daniel alipiga breki nje ya geti ya jumba moja la kifahari akashika rimonti akalielekezea geti lenyewe likafunguka wakaingiza gari ndani,




Naaam,ilikuwa ni nyumba kubwa yenye eneo pana bustani nzuri miti,bwawa la kuogelea mahali pa kupumzikia,nyumba ilionekana ni safi kama vile paliishi mtu




wakaelekea mpaka eneo la 'parking' wakashuka




"hii ndo nyumba yako kk ulohaidiwa na rais na hii pia ni gari yako hapa ni sehemu salama kuna wafanyakazi wawili watu wa zima mtu na mkewe hawa ndo walikuwa waangaliz wa nyumba hii awana wa toto sasa maamuz yapo kwenu kuwafukuza au mbaki nao ni wafanyakazi wazuri tu,kwa upeo wako najua uwezi niuliza kwa nin nikachukua wazee,wazee ni tofauti na vijana,wazee ni wasiri wazee hawana tamaa ivyo kwa kuwa nyinyi ni wapelelezi msakwao ni vyema mkawa na wazee hawa wakawa wakiwasaidia kazi"




"sawa meja uko right fungua mlango mgonjwa angu atoke"




Daniel akabonyeza 'unlock' pemben ya msteling ghafla mlango wa upande wa pili ukafunguka, Zena akashuka, kutokana na matibabu mafupi alopewa alikuwa na unafuu aliweza tembea mwenyewe yalobaki ni majeraha huku magotini mapajani na kifuani kutokana na mateso alokumbana nayo,ila dawa alizopewa zilimsaidia sana,akashuka na kuelekea ndani Katarina akimfata kwa nyuma na Daniel akiwa nyuma kabisa,




Walipoufikia mlango wakasimama wakiwaza Dani akaongea kwa sauti 'gongeni' huku akizidi kuwafata,




Katarina akagonga,na kusikilizia,baada ya kama dakika mbili mlango ukafunguliwa na bibi wa miaka kama arobaini akuzeeka sana, akawakaribisha ndani sebuleni,bibi yule alikuwa ni mchangamfu na mwongeaji pia mwenye utani mwingi...




"wakasalimiana na kutambulishana bibi yule alitambulika kwa jina la bibi mkuu,na hata babu pia wakimwita babu mkuu ikiwa kirefu cha mkuu ni mkubwa hawakutaka kutambulika majina yao na hakuna alolazimisha kuwajua,wazee hawa walichukulia katika kambi ya wakimbizi miaka mingi wakati wenzao wakipandishwa katika magari kurudishwa kwao burundi wenyewe walilia wakitamani kuendelea kubaki Tanzania,




Walikataa Katakata Kurudi Kwao Burundi Kwani kila ambapo wangeona ardhi ile ndivyo ambavyo wangezidi kuumia kwa kuwapoteza ndugu zao,na hata watoto wao,ndipo Daniel alipowachukua akawapa uraia na kuwa ajiri katika nyumba moja ya baba yake kipindi hiko baba yake Asamoye akiwa katibu wa chama cha upinzani (demokrasia ya kweli)




Akawa ajiri kama wasimamizi wa nyumba hiyo,na kweli nyumba ile waliisimamia vizuri,utasema iliishi familia!




"bibi,babu mkuu yupo wapi?!"




"haaaa mjukuu wangu si yuko huko nyuma akata fensi!"




"ok,ngoja nkamwite aje awaone wageni!"




Palepale Dani akanyanyuka,akaenda nyuma ya nyumba ela aliporudi aliongozana na babu mmoja mwenye nguvu zake,




"babu na bibi mkuu,kila siku mmekuwa mkinisumbua mwataka mumjue mwenye nyumba wenu leo nimemletea ni huyu...




Dani aliongea huku akimnyooshea kidole Katarina,kisha Akaendelea




...na huyu mwingine ni mdogo wake"




Babu akaropoka




"alaaa,vizur ila angetoa ilo shungi huku kichwani tumjue mwali wetu sasa"




Babu aliongea kwa kuinjoyi wote wakacheka,




ikabidi sasa katarina atoe ile


shungi!,wote wakawa wakimtazama wakati akiivua...




"k.k.k.k.k.katarina?!!!....."




Zena alishikwa na kigugumizi,akataja lile jina kwa mshtuko baada ya kumgundua ni Katarina,binti alotokea kumchukia na kupania kumfunga na kama si shambulio lile usiku ule Katarina saivi angekuwa gerezani!...




ndo huyu alomsaidia?!,ni usalama wa taifa huyu mtu!!...




KWA KWELI ZENA AKUAMIN,




Muda Wote akumtambua,si alikuwa kajifunika,na pia alikuwa akiitwa 'kk' ikawa ni ngumu kumtambua...




Watu Wote,kwanzia Dani,na wale wazee wakabaki kumshangaa ZENA kwa jinsi alivyoshtuka,na kwa jinsi alivyokuwa akimshangaa KATARINA








(MWISHO SEASON ONE)




Hatimaye Zena anamtambua 'kk' kama Katarina mwanamke alomchukia na kupanga kumfunga kumbe ndo aliyemsaidia,




Zena hakuamin kwa kweli akabaki kamtumbulia macho kwa mshangao pasina kujua walokuwa pemben yake nao walibaki kumshangaa,je unajua nin kiliendelea?!




Twendelee na sehemu hii ya thalathini ya riwaya hii tuitimishe vipande 30 vya kwanza...tukisubiri 30 katika season 2




TWENDELEE...




Katarina alibaki mtazama Zena kwa tabasamu jepesi,kabla Zena ajaongea kingine chochote Katarina akamuwahi...




"ni mimi Zena,wala usiogope ya nyuma ulikuwa kazini,yale achana nayo tutaongea badaye"




"kumbe mnajuana?!"


Daniel akauliza huku akishindwa kuuzuhia mshangao wake,




"ha,mjukuu wewe si umesema ni mtu na dada yake..."




"mh,basi bibi wewe jua hivyo kwanzia sasa huyu Katarina ndo mwenye hii nyumba ni kiwa namaanisha huyu ndo bosi wenu,huyu ndo atakaye walipa"




"sawa baba tumekuelewa"




"Zena kwa kuwa hali yako ni nzuri kesho jumatatu unaweza kurudi kazin makao makuu au walokutambua sura wote si wamekufa au una khofu?"




Zena akatingisha kichwa kukubali alichoagizwa,Dani hakuwa na muda sana pale akaaga,




Akujua wala kuwa na kumbukumbu kuwa madam 'S alimuona na kwa muda huo alikuwa na picha yake akielekea makao makuu,wakiwa wenyewe sasa pale sebuleni Zena akaanza kwa kumuomba radhi katarina,




Katarina akamtoa khofu na kumwambia wazi amemsamehe asijali kuhusu swala lile kwake alichukulii kama kosa kwa kuwa ulikuwa kazini!




"je ni kwel ulimshambulia yule mwanamke?"




Katarina akacheka,"na nasikitika mdogo wangu yule mwanamke kuwa hai ila siku moja lazima ntamuua hakuna jinsi!"




"kwa nini?!,ni hatari kwa maisha ya Rais au usalama wa taifa kwa ujumla?"




"no,"




"kwa nini sasa unawaza kumuua?!"




"mapenzi Zena!"




"mapenzi?! Kivipi yani"




"nishaweka nadhiri kila mwanamke ntakayegundua anatembea na mume wangu Zidu nita mtahadharisha mara moja,asipo nisikia sitokuwa na maamuzi mengine zaidi ya kumuua...moyo wangu unajua ni kwa kiasi gani nampenda Zidu..."




Zena akakumbuka tabasamu la Zidu Ile Siku alipo mtembelea kwake,kumuhitaji mahakamani,tabasamu lililo mteka!,kumbe naye angekutana na kifo?,kimoyo moyo akajikuta akimshukuru Mungu...




Waliendelea na stori za kawaida Katarina akamuhadithia kila kitu Zena toka amekutana na Zidu akatumbukia katika penzi lake kipindi wakiwa Ganyama,heka Heka walizokumbana nazo,mpaka kuja Tanzania,atokee Mwanamke kula tamu yangu ntamuua,sitomuacha hai...




"ila utakuwa uwatendei haki kwa kuwa wengine unakuta mumeo ndo anayewataka"




Kwa Kujua hilo ndo maana nikawapa nafasi moja ya kuwaonya,ila akiendelea hapo ndipo atakapokuwa kakosea kitakachofuata ni kumwangamiza tu,wewe kwenye upolisi cheza sehemu yako ukintia hatiani sawa,ila usifanye kazi kama wanijua ikiwa dalaja la msako wangu likawa mkononi mwako,"




"sawa dada yangu"




Waliendelea Kubadilishana Mawazo,hili Na Lile,muda ukazidi kuyoyoma...




UPANDE MWINGINE




MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI




Madam 'S' aliingia eneo lile la makao makuu,na kusonga mbele kuelekea kwa kamishna Haruna Goziguzi,mkuu Wa Kituo Kile kikubwa cha jeshi la polisi...




Madam 'S' alitambulika sana eneo lile hivyo kila askari alopishana naye alimpigia saluti,




Safari yake ikaishia nje ya mlango wa ofisi ya kamishina,akasita kidogo na kufungua mlango akaingia...




"nimemkuta kamishna?"




Akamuuliza binti alomkuta eneo la mapokezi baada ya kupokea saluti yake,




"yupo ndani madamu unaweza tu kumuona"




Madam 'S' akaingia ndani ya kaofis kadogo,




Alimkuta mzee mmoja akiwa bize na mafaili yalojaa katika meza yake,




"mzee umechoka sasa yapaswa ukapumzike kazi uwaachie vijana unaacha mpaka unarundikiwa ma faili mengi hivi"




Madam 'S' akamtania hapo ndipo kamishna Haruna Gozigozi alipoinua kichwa chake kumtazama huyo mgeni alo mtembelea,




"na kweli mwanadada mrembo muda wa kustahafu sasa unaniamkia nami sina budi kuuitikia marhaba,lakini ujambo mjukuu wangu?!"




Madam akatabasamu, alikuwa akiyapenda sana maneno ya yule mzee,mara nyingi yalikuwa yanaladha katika masikio yake,




"sijambo babu ila ujio wangu hapa nina shida bila shaka utansaidia mkuu wangu,"




Kamishna akatabasamu,




"yah nipo hapa kwa ajili ya kukusikiliza hasa kama itakuwa inagusa usalama wa taifa letu!"




Madam akatabasam tena akijikaribisha kwenye kiti,muda wote alikuwa kasimama,akafungua begi lake na kuitoa picha,kabla ajampa akamjibu...




"ndio mkuu,inahusu usalama wa taifa,kwa kifupi huyu ni binti hatari mwenye malengo ya kuleta mvurugano katika taifa,naitaji kila askari awe na picha yake asakwe..."




Akamkabidhi Ile picha, kamishna akaipokea na kuitazama akayatoa macho ya mshangao,akauliza kwa kutoamini




"huyu si Koplo Zena?"




"koplo Zena?,unamjua huyu mtu?!"




Kamishna akazidi kuikazia macho ile picha,




"yah Huyu Ni Zena,embu ngoja..."




Akanyanyuka kwenda mpaka katika mafaili ya utambulisho wa maaskari waliyoko pale makao makuu




Yale ya mwisho mwisho ya maaskari wenye vyeo vya makoplo,hakupata tabu sana kulipata faili la Zena,akalicho moa na kumpelekea madam




"binti huyo si ndo huyu au?!"




Madam akalicheki lile faili akaridhika,




"huyu binti ni hatari yupo hapa?!"




"wiki ya pili sasa kapotea kwenye mazingira ya kutatanisha"




Kauli Ile ikazidi kumfanya amini yule ndo 'ZK' walokuwa wakimsaka muda mrefu kumbe ni polisi?!,




"kafanyaje huyu binti,tena katika idara yangu ni mfanyakazi mzuri tu,mchapa kazi alikuwa akishirikiana kwa ukaribu na insp Nurdin"




"huyu ndo yule mwandishi mkubwa atoaye siri za serikali akijiita 'ZK' kwa muda mrefu tu amekuwa akiichafua serikali hii ya mh Asamoye na kafanikiwa kuwaua vijana wetu kadhaa,asakwe huyu mtu likitangazwa dau kubwa kama nilivyosema awali picha yake isambazwe ni hatari sana huyu mtu"




'i..i...ina maana Raisi anajua kuwa huyu binti ni hatari kwa uongozi wake,na yeye si ndo alomleta hapa makao makuu'




Kamishna akajiwazia akikumbuka simu alopokea kutoka kwa raisi ikimuomba ampokee binti huyo kulitumikia taifa,au ni mchezo wa kisiasa? asije akawa anatumiwa na Rais?!




Akili ya kamishna ikachaji zaidi,wakati wakiwa katika mkanganyiko ule si ndo mlango ukagongwa na kabla Kamishna ajaruhusu mtu aingie mlango ukafunguka na mwanadada mrembo akiwa ndani ya sare zake za jeshi la polisi akazama ndani,alikuwa ni koplo Zena,Madam 's' akageuza shingo kumtazama ni nani aloingia tena bila nidhamu!




Macho kwa macho na Zena,akawaza kuomba radhi hatoke,ila alishtuka kumuona mama yule kamnyooshea silaha tena sasa alikuwa pembeni yake akujua aliinuka sangapi pale,




Kabla ajawaza afanyaje akahisi kitu kikichomoza begani maumivu makali yakafatia,niwazi alitandikwa risasi mkono ukawa kama unataka kuchomoka akatandikwa ya pili ile anageuka afungue mlango atoke akavutiwa ndani na kupokea konde zito 'ngumi' ilompeleka chini,






MWISHO WA SEASON 1, ENDELEA NA SEASON 2

0 comments:

Post a Comment

Blog