Simulizi : Kufa Tu Hakuna Namna
Sehemu Ya Nne (4)
"Kwa nini umehisi 'ZK' anaweza kuwa ni ZIDU?"
Madam 'S' akazidi kuhoji...
"Uwezo wa yule jamaa ni mkubwa sana na ni wazi huyu mwandishi hatakuwa pia si mtu wa kawaida,na kifupi cha ZK ni kirefu cha jina lake Z imesimama kama ZIDU na K imesimama kama katili"
"au Kite jina la baba yake,but katika ripoti nlotumiwa saivi na vijana wangu Zidu yupo katika matatizo,mke wake Katarina yupo gerezani na kesho Kutwa jumatatu ndo hukumu hivyo sidhan kama anaweza kuwa yeye ila tusiishi kwa fikra,kesho usiku huyo binti Sara auwawe katika msitu mnene mtatumia gari ya ofisi msipate usumbufu barabarani,hili sasa tukikutana tena kesho kutwa nguvu zetu kwa pamoja tuziwekeze kwa 'ZK' awe ni Zidu au nan tutamjua tu"
"mkuu"
Pizo akaita
"nakusikia"
Madamu akaitika
"Na ombi!,kuwa na gari moja ya serikali aitatupa usalama wa kutosha kufanya tusifatiliwe kumbuka siku za nyuma vijana wa jwtz waliwah kuzuia meli wa muheshimiwa pamoja na kwamba sisi tulikwepo tena na sare za jeshi,nimekukumbusha tu mkuu kuwa na gari la ofis si kinga tosha yapaswa tuwe na gari mbili moja tutakuwa wa nne ndani pamoja na maiti mtarajiwa wetu,nyuma watakuwa wawili ambao tutaachana umbali flani,hawa wanyuma watakuwa wakitulinda na ikiwa kuna yoyote atatufatilia hawa wa nyuma ndo watamdhibiti,tutakuwa tukiwasiliana"
"sawa amna neno,nyie pangen muwezavyo ila kesho usiku ndo uwe mwisho wa huyo binti"
Madam 'S' akafunga kikao...
wakatawanyika
*** *** ***
Siku hiyo Sara jamaa akumtesa kabisa,mchana alimletea chakula na kumlisha vijiko vitano,na maji,alilishwa hili aishi na si hili kushiba,
"nadhan leo ndo siku ya mwisho kuwa humu kesho usiku ndo tutaenda kukuua ikiwa tu utotupa memorikadi,"
Red deval aliongea kwa jeuri jioni ile ni baada tu ya kutoka katika kikao kile cha mwisho ambacho madam aliagiza kesho yake sara akauwawe...
Red d' akatoka akurudi tena,wala akuangaika kumfungulia pale juu alipo mfungaga
Usiku ukaingia,Sara alijua lazima yule mtu mvaa kininja angemtembelea na kweli giza lilipotawala kama mida ya saa nane akiwa kakata tamaa akahisi mlango ukifunguliwa taratibu...
Zikasikika nyayo za mtu
"shiishi akapewa ishara anyamaze,yule mtu alikuwa na tochi,Sara alimuona vizuri sana alikuwa niyule ninja akamfungua Sara akatua kama mzigo...
Akamfungua kamba alizofungwa mikononi na miguuni...
"toka juzi nimekupa nafas utafute njia ya kujiokoa umeshindwa sasa kesho unakufa,ila moyo umentuma nkusaidie twende..."
Akamnyanyua...
wakaelekea ulipo mlango wakatoka,Sara alishtuka kukuta maaskar wote wa nne walolinda jengo lile wamelala,ninja akawa akimkokota kwa kupitia nyuma watoke nje ya jengo lile,wakafanikiwa,
Sara alikuwa kaumia sana ivyo akuweza kutembea haraka haraka Ninja akambeba ila kabla awajasonga zaidi kwenye mti mmoja kitu kikatua,alikuwa ninja,
ikabidi mwokozi amwache Sara chini wakaanza kuzipiga,
Watu Wale Awakujuana,ila Yule alotua juu alo onekana wazi ni wakike kutokana na sauti yake mara kibao alimpa mapigo ya hatari mwokoz na kumdondosha,
Mwokozi alijitahidi kunyanyuka na kuendelea kupigana ila mwisho aliuwawa,ndipo yule mbambe akamfunua mwokozi,akuamini yule alomuona...
"Red deval ni wewe?!"
Mtu yule aliongea kwa sauti ya kike ambayo ilifanana vikubwa na sauti ya madam 'S'
Sara mwenyewe akuamini kama yule mtu alokuwa akimtesa,alombaka,alo mchanjachanja na kumpa makovu mwili mzima,ndo alohitaji kumuokoa,akuamin hakika...
Madam 'S' akabaki kaganda akiushangaa ule mwili,pasina kuamin akionacho...
Sara akiwa amebakisha siku moja tu ya kuishi anakuja kuokolewa na mtu alojifunga kininja,
Wanafanikiwa kutoka nje ya jengo lile lakin kwa bahati mbaya madam 's' naye akiwa kajifunga kininja anatua juu ya mti na kupigana vikali na mtu yule mwisho anafanikiwa kumuua anapomfunua sura anashtuka kumkuta ni Red Deval hakika madam aamin kwa jinsi alivyokuwa akimuamin kijana yule na ukatili alokuwa nao,hata Sara Mwenyewe anashindwa kuamini,kwamba yule alokuwa akimtesa ndo mkombozi wake,songa kujua kilichoendelea...
Madam 'S' muda ule ule akachukua simu yake na kutuma sms kwa watu alowajua yeye,kisha akamsogelea Sara akamnyanyua na kuanza kumkokota,akiuacha ule mwili pale,azikupita hata dakika tano vijana fulani wakiwa katika nyuso mficho waliwasili wakamnyanyua Red Wakamweka Nyuma ya buti ya gari yao wakaiondoka gari kwa kasi tayar kwenda kuuzika ule mwili kabla akujapambazuka
Madam akaurejesha ule mwili wa Sara katika kile chumba cha mateso,akiipita miili ya walinzi wake walokuwa wamelala wala akuangaika nao alijua wale watakuwa walinukishwa madawa akaubwaga mwili wa Sara kitandani na kutoka akafunga na kufuli kwa nje ufunguo akaondoka nao akaelea chumbani kwake kulala...
*** *** ***
Asubuhi ya siku ilofatia madam 'S' akaitisha kikao cha vijana wake Pizo,Chronic Killer,Veko,M'd, pamoja Na Green Cobro
"nasikitika kuwa ambia kuwa leo usiku tumempoteza mwenzeto Deval,alikuwa ni kijana niliyo muamini sana na wala sikufikiri wala kumdhania yeye kama anaweza kuwa ndiye msaliti
Nadhani sikuwahi kuwa ambia na sikuhitaji kuwa ambia kwa sababu nilijua mlikuwa mkijua ivyo sikutaka kuwajulisha kile ambacho nyinyi mnakijua,ila nimegundua kwamba sijui ni kiburi au amjui inanipasa niwa ambie...
Usalama wa taifa una vijana wengi sana tofauti na nyie na wala amtambuhani na nimewaeka kimakundi makundi,hilo sitoliongelea sana ninachoitaji kuwaeleza ni kwamba katika nyumba nzima hii katika kila chumba kuna kamera mahalum za dstv,ambazo naziona katika laptop yangu hii,siku nne nyuma wakati nikiwa nakagua kagua mazingira vyumbani nikashtushwa na tukio moja,akalitafuta lile tukio la siku ya kwanza kabisa Red deval alipo mtembelea usiku Sara na kumpa simu awasiliane na mtu awezaye kuwa mkombozi wake
...basi hapo ndipo nilipojua kati yenu kuna mtu mmoja msaliti japo sikumjua ni nani,jana pia nikashughudia jambo hilo,ndipo nilipoamua kuwa ambia huyu binti auwawe nikijua fika yule msaliti angeitaji kumtorosha,kwa kuwa sikuwa amini nyinyi hili swala nililivaa mimi kama mimi,nikaamua usiku wa jana nikae juu ya mti na kama mategemeo yangu nikamuona yule mtu akija akiwa kambeba Sara akihitaji kumtorosha sikujua ni kivipi aliwaekea madawa,pia sijajua mpaka sasa Red huruma yake ilitokana na nini!...
Je ni alimpenda yule binti au tusijiumize kichwa kwa jambo hili wakati kuna mambo mengi ya kufikiria huyu Sara usiku wa leo auwawe kama nilivyoagiza sitaki kujua mmejipangaje!,
"sawa mkuu" wote wakaitikia kwa majonzi kikao kikafungwa...
*** *** ***
JIONI YA SIKU HIYO
Ikiwa kesho yake ndo jumatatu ambaye angehitajika kwenda mahakamani jion hiyo akiwa kituoni akikagua baadhi ya mafaili ya kesi zinazoendelea pale makao makuu ghafla mlio wa msg ukaingia kwenye simu yake
'red' ndivyo ulivyosomeka hakupata tabu kugundua ni kipi ilipaswa afanye haraka sana kwa kuwa alikuwa ofisini mwenyewe akacho moa ile line na kuiweka line ingine,kabla ajaipiga akapokea sms
Akashtuka haraka sana Zena akafungua ile sms
"nenda chumbani kwangu ndani ya kiatu changu ndani ya sox zangu chini ya mvungu kuna memory kadi yenye ushahidi wa waziri"
Hakuwa na shaka ile sms atakuwa katumiwa na raisi akawaza,kuingia ikulu!,chumbani kwa rahisi mh,kabla ajazidi kutafakari ghafla simu yake ile ikapigwa na mheshimiwa waziri...
akaipokea
Nimepigiwa simu na kijana wangu ambaye ni dereva wa waziri kanambia usiku huu wa leo waziri hatakuwa giraffe hotel na kimwana ivyo ni muda wako sasa wa kwenda kupiga kazi,
"sawa muheshimiwa na vipi kuhusu meseji yako ulo ntumia kwamba kuna ushahidi wa waziri chumbani kwako kwenye kiatu"
"mimi?!,hapana asee sijakutumia meseji kama hiyo huo utakuwa ni mtego tu kuwa makini"
"sawa muheshimiwa"
Zena akakata simu,haraka sana akaichomoa ile line akiachana na ile meseji maskin akujua kuwa ni sms ya Sara,
USIKU WAKE MIDA YA SAA NNE
Zena tayari alisha wasili kwenye ile hoteli ya geraffe na kukaa pembeni punde tu gari ya waziri ikawasili,ni gari isotambulika na watu wengi sana,
Waziri akiwa katika nguo zake za kawaida na kapelo ilikuwa ni vigumu kumtambua akiwa kamshika yule binti kiuno kwa siri sana Zena akamtwanga picha kadhaa,wakiwa wanacheza tena alifanikiwa kumpiga picha kadhaa wakiwa wameshikana kimahaba,baada ya kuridhika na picha zile alizopata,akadandia pikipiki yake akaondoka kurejea nyumbani tayar ilikuwa ni saa saba za usiku...
Saa tano za usiku Sara alitolewa chumbani kule na kuingizwa ndani ya gari la ofisi ya waziri mkuu,
Pizo akakaa kiti cha dereva pembeni yake akaongezeka kijana mwingine alomuita chinja chinja,huyu akutofautiana sana na Red Deval kwa ukatili wake,nyuma wakakaa watu wawili wakimweka kati Sara ni Veko na Mudi,
Gari ya nyuma dereva alikuwa ni Chronic Killer pamoja na Green Cobra '
Gc'
Safari Ikaanza Kuelekea katikati ya msitu...
Zena naye njiani akielekea nyumbani..
Barabara Walokuwa Wakiitumia Ni Moja Ni Wazi Wangekutana...
'ZK' yeye alikuwa mbele akielekea nyumbani, ghafla nyuma yake akasikia muungurumo wa gari wakati akiwa njiani katikati ya usiku ule ghafla gari moja ikampita kwa spidi,
Akashawishika kuitazama namba ilosajiliwa katika gari ile alishtuka baada ya kuona ni namba za serikali,
Kwa mantiki hiyo gari Ile Ilikuwa ni ya serikali,
Hali ya udadisi ikamtawala mtu yule,
Kama mwandishi Na Pia Kama Mpelelezi Kwa Kazi Ilokuwa Siri yake aloifanya kupitia kivuli cha uandishi akatamani kujua juu ya gari ile ya serikali kumpita tena kwa spidi usiku mzito kama ule?!...,
'Inaenda Wapi,ndani yuko nan?!...'
Maswali kibao yakajijenga katika kichwa chake
Akakata shahuri liwalo na liwe wacha aifate pengine imeibiwa,kwa siri sana akaanza kuifatilia!...
Kadri alivyokuwa akiifatilia gari ile ndivyo alivyozidi kupatwa na wasiwasi,siyo wasiwasi wa uwoga!, la ashaaa!
hapana!...
Ila wasiwasi kwamba wale si watu wazuri,ilo akujali ndo kwanza damu ikazidi mchemka , akazidisha umakini, kiunoni alikuwa na bastola yake yenye risasi za kutosha,pia aliuamini uwezo wake wa kupambana,ivyo akutaka kuiruhusu hofu imtawale akazidi kusonga kuwafatilia...
Katu akujua kwamba nyuma alikuwa akifatiliwa na watu wengine hatari...
Muddy na Green Cobra
Akili zake alizishurutisha kufatilia mbele tu katu akujua nyuma pia kulikuwa na gari ilokuwa ikimfatilia na walokuwa kwenye gari hiyo ya nyuma walikuwa wakiwasiliana na wa mbele,naye alikuwa kawekwa kati...
Ndani ya gari ile ya serikali kulikuwa na watu watano, nyuma alikwepo msichana mmoja ambaye alikuwa kafungwa mikono yake na miguu kwa pingu uso wake wote ulikuwa umevimba kuonesha alipata mateso makali pia nguo zake zililoa damu,alikuwa akilia ila walokuwa ndani ya gari ile awakuonesha kujali kilio chake ndo kwanza walikuwa wakicheka huku wale vijana wawili walomuweka kati wakimchezea mwili wake kijinsia...
"oyaaaaa Veko Leo ana kwa ana na 'ZK' piga ua leo ndege wawili tunaua kwa jiwe moja"
Dereva alotambulika kwa jina la Pizzo aliongea akionesha wazi kufurahia kumuona "ZK" mbele yao...
Wao Kama wao Walimjua yule 'ZK' ni Mwandishi tu,na toka muda mrefu amri ilishatoka makao makuu ofisi ya waziri mkuu chini ya kitengo maalumu cha usalama wa taifa kuuwawa kwa mwandishi yule...
Hii ni kutokana na yeye kuvujisha siri nyingi za serikali,ivyo akawa akiichafua serikali,katu ofisi ya waziri mkuu aikujua kuwa yule kapandikizwa na Raisi makusudi ili akivujisha vile Raisi anapata faida fulani kivipi sasa?!.....
MTU HUYU NA RAISI WALIKUWA NA SIRI NZITO!
Mtu yule 'ZK' akiwa juu ya pikipiki yake alikumbuka siku wakiwa 'privet' na mh Rais,maneno rais alomwambia...
"kijana wangu naamin ufanyaji kazi wako, nimekutoa na kukusaidia hili nawe pia unisaidie,utafanya kazi chini yangu ila ripoti utonipa mimi,hapana...
Naitaji uwe mwandishi wa habari ila ficha sura yako isitambulike ovu lolote utakaloliona katika serikali yangu nilione katika televisheni!..
....na maana yangu na ipo siku utajua nini na maanisha...
...najua ni kazi ngumu nayokupa ila fanya kwa weledi utafanikiwa"
Mtu yule juu ya pikipiki yake alizidi kukumbuka,na kujikuta akizidi kukanyaga mafuta kuifatilia gari ile kujua hasa lipi lengo lao...
Gari ile ikazidi kuchanja mbuga kuingia maeneo ya porini, 'ZK' akazidi kuifatilia
Mbele kidogo gari ile ilisimama naye 'ZK' akasimamisha pikipiki yake milango ikafunguliwa vijana wawili wakashuka kutoka milango ya mbele wakafungua mlango wa nyuma kijana mmoja akashuka akamvuta mtu na kumtupa chini
Yule dada akaachia yowe,haraka 'zk' akashuka kwenye pikipiki yake aloipaki nyuma kidogo akijua ajashtukiwa akaanza kuwafata kwa kunyata silaha ikiwa mkononi,kwa kujificha akawa akisogea eneo lile,alijua giza lilimsaidia,
Wale watu wa tatu walokuwa na gari wakiwafata kwa nyuma nao walishuka kila mmoja akiwa na silaha yake wakawa wakisogea eneo alilopo 'ZK' kwa uangalifu kukwepa kumshtua...
"utatupa hiyo memory au utupi?"
Zk alisikia mtu mmoja akiuliza kwa ukali kabla dada yule ajajibu mtu yule akaunyanyua mguu wake na kuushusha kichwani kwa mwanamke yule ambaye aliachia yowe
ZK alimtambua yule mwanamke kama mwandishi wa habari sasa akawa akijiuliza ni memory gan wanayoitaka ambayo mtu yule anayo?!
Pili kwa pale alipaswa afanyaje,je aokoe au apige picha na siku inayofuata atoe habari zile kama Rais alivyo mwagiza?!
Palepale akatabasamu baada ya kukumbuka kuwa wale watu wanataka kitu kwa yule dada ivyo wasingemuua mpaka yule dada aseme ilipo hiyo memory kumleta kule ni kumtishia tu ivyo ilipaswa afanyaje?!
Afanye Kaz yake ya kuchukua tukio lile mpaka mwisho
Alijua mwisho baada ya kumtesa na kupoteza fahamu wangemrejesha na kesho kuendelea kumtesa mpaka aeleze ilipo hiyo memory card ivyo tukio la kuripoti lingemfanya mwandishi yule kuwa huru hapo 'ZK' akatabasamu kwa mara ya kwanza akamuelewa Rais Wake alikikuwa na maana gani kumpa kazi ile
Akavua Kibegi Chake Na Kutoa Kamera akaanza chukua tukio lile pasina kujua watu walokuwa nyuma yake walishughudia kila kitu alichokuwa akifanya...
"usemi siyo 'P' maliza"
'ZK' akuamini macho yake pale aliposhughudia risasi zikikishambulia kifua cha yule dada,mwili ulimlegea akajikuta akishindwa kuishika ile kamera na kuiachia ila ghafla kitu kizito kikatua kisogoni mwake,giza likatawala,akaenda chini!
Akapoteza fahamu!
Ilikuwa ni kazi nzuri ilofanywa na wale watu walokuwa nyuma yake bila yeye kujua mmoja alimpiga na kitako cha bunduki kisogoni baada ya yeye kupigwa na butwaa baada ya kushughudia binti yule akiuwawa mbele yake bila yeye kutarajia
Zena akaenda chini...
Hakuwa na ufahamu tena,
'Gc' wakamburuta mpaka walipo wenzao kilichofatia ni kumtoa ile mask waweze kuiona sura yake
Wote walishtuka
Kumbe ni mtoto wa kike
Siku zote walikuwa wakijua 'Zk' ni wa kiume ila kumbe....
Hakika kila mmoja alichoka
"Tumpigie mkuu saivi,kumjulisha kwamba tumempata ZK"
Veko akauliza
"Hapana aina haja saivi kakumbatiwa na mume wake siye tumsumbue ni vyema hii taharifa tumpe asbuh atafrah hakika"
"Amri ilitoka tumuue..."
"No,huyu lazima hatakuwa anatumiwa ivyo si vyema tukamuua mpaka tumjue anaye mtumia si yuko chini yetu lazima ateswe huyu"
Pale pale walimsachi wakakuta picha za waziri mkuu akifanya machafu,
"Dah hakika huyu dada ni mpelelezi hizi habari anazipata wapi"
pia katika ukaguzi walishtuka zaidi kukiona kitambulisho chake cha upolisi,kumbe ni askar yule tena wa makao makuu,
Jambo hilo likazidi washangaza watu wale,wakachimba shimo wakaufukia mwili wa Sara,wakauingiza mwili wa Zena ndani ya buti wakarejea kambini kwao...
Mwili Wa Zena ukaingizwa katika chumba alichokuwa Salome awali!...
Wakati mwanadada Zena akitoka katika miangaiko yake usiku anapitwa na gari ambalo anagundua ni gari la serikali,anajiuliza maswali mwisho ana amua kulifatilia,
Wanafika Katikati ya msitu ambapo anashushwa mwanamke na kuteswa,Zena anachukua video pasina kujua kuna watu wanaomfatilia kwa nyuma,
Mshtuko Unampata Pale Anaposhuhudia Sara akitandikwa risasi anapigwa na kitu kizito nyuma kina chopelekea kupoteza fahamu mwili wa Sara unafukiwa mabishano makali yanatokea wengine wakishahuri Zena auwawe Wengine wakipinga, upande wanaopinga unashinda Zena anawekwa kwenye buti na kwenda kuswekwa chumba alichokuwa Sara hapo awali,je unadhani nini kiliendelea?!
twendelee...
GEREZA LA SEGEREA
Kiza kilimeza taswira ya mwanga,ulikuwa ni usiku mzito majira ya saa saba mikoromo ya wafungwa kutokana na uchovu ilisikika...
Ghafla lango likafunguliwa, wakaingia maaskari wawili wa kiume na kwenda mpaka pale alipo madam mama,au big mama kama mwenyewe alivyopenda kuitwa,binafsi alikuwa kalala huku kamwekea mguu Happy mwanamke aliyedai mwenyewe ni mke wake,askar akamfikia na kumuamsha,big mama akashtuka na kukaa kitako akapiga mwayo mkubwa, mwayo wa uchovu...
"huyo binti yuko wapi?"
Yule askari akamnong'oneza big mama,naye nyapara yule akaangalia mahali alipokuwa amelala Scola akanyoosha kidole mahali alipo binti yule alolala kwa kujikunja...
Maaskari Wale Wawili wakamsogelea na kumnyanyua juu juu Scola
huku wakimziba mdomo kusudi asipige kelele wakamtoa nje
Kule Katika chumba cha mateso alicholazwa Katarina Usiku Ule Kikafunguliwa, maaskari Wawili Pia Wakaingia na kumtoa katarina uso wote ulivimba
wakampeleka mpaka ndani ya bwalo ambalo lilitumika na wafungwa katika kulia chakula,huko ndipo walipokuwa wakifanyia ufuska wao,
Ndani kulikuwa na maaskari takribani watano kila mmoja alikuwa na mfungwa mwanamke mwingine alikuwa akibaka,wengine walikuwa wakifanya kihiyari ili mradi ilileta picha isiyo nzuri machoni mwa Katarina,
Akawekwa Chini
"Mula wewe unaenda kuchukua wako au tupige hivi hivi,"
"huyu huyo tupige mande...
Hasira zikampanda Katarina,punde Maaskari Wengine Wawili Wakaingia Wakiwa Wamembeba Scola Wakambwaga Chini,
Katarina alijikuta akinyanyuka na kuruka double tik taka kila mmoja akimzawadia teke lake,maaskari wale wakasambaratika chini,akajirusha mpaka kwa wale walokuwa wamemkamata Scola akawashika kola zao na kuwa vuta nyuma kwa nguvu,
Wale maaskari wengine haraka wakavaa suruali zao na kutafuta silaha zao,lakini walishachelewa,jambo lililomshangaza Katarina
Scola hakuwa binti wa kawaida naye alikuwa ni mpiganaji,akimiliki mapigo tata,mabinti wawili wakawa wakipambana na wanajeshi wa magereza saba,wakaweza kuwadhibiti,na kuwazimisha wote,wakawafungia ndani ya lile bwalo,wakawaamuru mabinti wote wawafate wakaingia wote katika selo ile ya jimama,jimama alibaki kushangaa pasina kuelewa ni nini kilichotokea,Katarina alitamani sana kumjua mtu yule...
Ikabidi sasa yule binti awe muwazi...
"jina langu kamili naitwa kamanda alice mwashebaga ni afisa kutoka tahasisi maalumu iliyoko chini ya mkuu wa magereza Mheshimiwa Shedrack,miaka mingi tu nyuma ofisini tumekuwa tukipokea malalamiko ya maaskari kuwatesa wafungwa, kuwanyanyasa usiku kuwachukua na kuwabaka ndipo mkuu alipo nituma nije kama mfungwa katika gereza hili la Segerea Kuchunguza Jambo hili je ni kweli?!,na leo nimefanikiwa kugundua hawa wanawake watano ikiwepo wewe mtakuwa mashahidi na tutaanza na wale maaskari wa tano tulowafungia kule bwenini"
Si Katarina Pekee aloshtuka, hata Nyapara na wafungwa wote walokuwa ndani ya ile selo...
"kwa..kwa...hiyo ile stori uloniadithia kwamba ulimuua baba yako ni ya uongo?"
"yah,ile ni hili usinitambue na jina langu si Scola jina langu ni kamanda alice,Katarina alishangaa sana,
"ila sidhani kama naweza kuwa shahidi hiyo kesho"
"kwa nini usiweze Katarina?"
"kesho Mimi napandishwa kizimbani kwa mara nyingine"
"ahaaaa sory bhana sikujua asee.."
Usiku ule awakulala tena waliendelea na stori,jimama alikuwa mnyonge alinyong'onyea aliambiwa hili naye siri zake zifichwe za usagaji akubali kutoa ushahidi...
Big mama akakubali alibakisha mwaka mmoja tu kumaliza kifungo chake,alijua siri yake ingefuja kulikuwa na uwezekano wa kuongezewa miaka,miaka 24 alohishi gerezani ilikuwa mingi sana...
Alihukumiwa Miaka 25 kwa kosa la kumchoma mtu kisu kisa uwivu wa kimapenzi...
Kilicho muokoa ni kwamba yule mtu hakufa,alizeekea gerezani,aliingia bado binti mchanga,mwenye urembo wake...
huyo ndo big mama,madam mama,au jimama,mwanamke mtukutu mwenye cheo cha unyapara katika selo ile...
SIKU ILOFATIA
MAHAKAMANI
Mahakama ilijaa watu, waandishi wa habari pia walikwepo kuripoti chochote kitakachotokea,watu wote wakasimama hakimu akaingia akakaa sehemu yake,
Watu Wakakaa,
Zidu na Suzan walikaa pamoja, wakiwa na huzuni ya bandia,pia Paul alikwepo upande mwingine Isack na Mery pia walikwepo,Isack na Zidu awakuongea hasa ni baada ya Isack Kuchukia Kitendo cha Zidu kuwa tofauti na mkewe...
Zidu aliangaza macho yake kumtafuta Zena Ila akubahatika kumuona, hatimaye shahuri la Katarina likatajwa naye akiwa na pingu zake akapandishwa kizimbani akasomewa shtaka akakana,wakili wake alikwepo...
Shahidi namba moja kama mshtaki au mlalamikaji aloipandisha kesi ile mahakamani koplo Zena akaitwa...
...kimya...
Akaitwa mara ya pili pia kimya
...akutokea...
Kesi ile ikahairishwa mpaka mchana hili atafutwe,mahakama ikaendelea na kesi nyingine
Mchana Katarina alipopandishwa hali hilikuwa ile ile na hata pia alipoitwa aloshambuliwa kwa risasi Salome naye akwepo hiyo ikavunja nguvu ya walobakia, kutokana na kukosekana kwa ushahidi Katarina akaachiwa huru...
Zidu na Salome waliondoka bila hata kumchukua Katarina,wote Walijaa Simanzi Ndani Ya Mioyo Yao
Katarina alikumbatiana na shemeji yake Isack na mery hawa ndo walikuwa wafariji wake...
"upunguze sasa hasira mamy uishi kwa amani uraiani huku kutamu eti!"
Isack akampa ushahuri
'usihofu shem"
Akaingia ndani ya gari la Isack,tayari Kumpeleka nyumbani...
"mume wangu kama nilimuona mahakamani!..."
Katarina aliongea kwa sauti ya taratibu,aikujulikana ni swali au ni taharifa,
"ndiyo alikwepo,"
Isack alijibu kimkato akikunja mdomo ni kama akupenda swali lile,Katarina japo alilitambua hilo akujali akazidi kuongea..
"najua ajafrahia mimi kutoka,ajafrahia shem,alitaka nifungwe aendelee kuwa na yule mwanamke nitamuua tu,sina namna haiwezekani haipokonye furaha yangu"
"hapana kata yule binti hana makosa,"
"bali?,tumbo langu ndo lenye makosa?!,nimependa mimi kutobeba mimba nimependa?!...
Katarina akajikuta akianza kulia,alimpenda sana Zidu...
Kazi kubembelezana ndo ilofatia...
Hatimaye wakapiga breki nje ya geti ndani alilokuwa akiishi Zidu!...
Wakagonga,mlinzi akafungua, kwa muda mrefu sana ile nyumba aikuwaga na mlinzi ilikuwa ukipiga kengele Suzan ndo anayekuja kufungua...
Katarina alishtuka kukuta mlinzi,tena alipo muona Katarina alifurahi,akatoa picha na kuitazama, akamtazama na Katarina...
"yah Ndo Wewe, bosi kasema ukija nikupe mzigo wako uondoke nisikuruhusu uingie"
Akarudi ndani katika kibanda chake akatoka na begi la Katarina akalitupilia nje...
Akafunga geti kwa ndani...
Katarina alilia,ilikuwa ni kama kapata msiba
"nitaenda kuishi wapi mimi,kosa langu lipi hasa...
Kata alilia huku akigonga gonga lile geti,mwisho akawa akijigaragaza chini...
Ilikuwa Kama Kapandisha Mashetani,
Mambo yote yale yalokuwa yakiendelea nje Suzan aliyaona kupitia tv moja ilokwepo pale sebuleni ilounganishwa na camera ilokuwa pale getini...
Binafsi alikuwa akitabasamu kufurahia jambo lile...
Isack na Mery wakamwinua katarina pale chini na kumpeleka mpaka ndani ya gari,wakaanza mbembeleza upya...
"naomba nipeleke kazini kwake shem anambie nimemkosea nin hasa,nipeleke shem"
"katarina,tulia Kwanza Kapumzike Nyumban..."
"hapana Naomba Unipeleke Nikajue Naomba Shem"
"twende tu tumpeleke mume wangu"
Isack akatia gari mafuta kuelekea kazini kwa Zidu...
Hatimaye baada ya kukosekana kwa Zena Mahakamani Katarina anaachiwa huru,cha ajabu Zidu alokuwa kama mume wake anaondoka katika mazingira ya kutatanisha mahakamani katarina anapelekwa nyumbani ambapo mlinz anamwambia waz kapewa amri asiingie anatupiwa na begi lake nje,je nin kiliendelea?!...
Twendelee....
Isack alizidi kukanyaga mafuta baada ya dakika kadhaa wakafika katika jengo ambalo juu ndo ilikwepo ofisi ya Zidu,mwanaume ambaye Katarina alimpenda zaidi ya mwaume yoyote,
Kitendo cha Isack tu kulipaki gari lake Katarina akaushika mlango akiwa tayari kuufungua Isack akamzuia!
"hapana Katarina uwezi kwenda mwenyewe lazima mimi au Mery akusindikize,"
"ndiyo mume wangu wacha mimi nimsindikize"
Mery aliongea,Isack akaita kwa sauti ya upole
"Katarina shemeji yangu nakuomba punguza jazba,punguza hasira shem usitake kuleta vujo uko ndani,amin uvumilivu waitajika hakika mwisho wa siku kila kitu kitakuwa sawa,"
"sawa shem nimekuelewa"
Wakashuka Mery na Katarina wakaelekea lilipo jengo kubwa lile,maaskari wakawakagua wakaingia kwenye lifti mpaka ghorofa ya pili wakatoka wakaelekea ulipo mlango wa ofisi ya Zidu,wakafungua Ndani Kulikuwa Na Wafanyakaz Wengi tu wakaelekea eneo la mapokezi wakaonana na katibu muhtas mpya baada ya kuondoka Salome...
katarina akaomba ruhusa ya kuonana na Zidu,katibu akashika simu na kumpigia bosi wake,
"nimwambie nani?!"
"mwambie ni mkeo Katarina"
Katarina aliongea akionesha wazi dalili za kutaka kulia,dada yule akashika simu na kumpigia bosi wake...
"bosi kuna mdada kaja hapa anaitaji kukuona kasema ni mke wako"
"Sihitaji kumuona si mke wangu akileta ubishi ita security wamtoe ok?"
"sawa bosi,.."
binti yule mrembo akawageukia wageni wake wale,
"bosi kasema ahitaji kuwaona tafadhali naomba muondoke kabla sijahita ulinzi..."
Katarina akaangua kilio,...
Akawa aking'ang'ania kutaka kuingia kwa ulazima,Mery akawa kamshika kumzuhia
"hapana Katarina mtu kama kakataa kuonana na wewe wamlazimisha nini tuondoke dada yangu...
"hapana Mery,niache ni mume wangu hati,lazima nionane naye"
Katarina akawa akilia,huku aking'ang'ania kujitoa kwenye mikono ya Mery,
Zidu kila kitu alikiona akutaka Kuonana na mwanamke yule alimchukia sana Katarina,palepale akashika simu yake na kuwapigia walinzi,alijua asingefanya hivyo lazima Katarina angeingia tu,aliufahamu ubabe wake...
Wakati Katarina akilazimisha kujitoa kwenye mikono ya Mery ghafla maaskari wa nne wakaingia wakamkamata Kata Katarina na kumvuta nje,Mery alikuwa akimfata kwa nyuma...
Isack akiwa ndani ya gari lake macho yake yalikuwa mbele ya geti la jumba lile walipokaa walinzi,ghafla akaona walinzi wa nne wakipanda juu si ndo machale yakamcheza akashuka kwenye gari lake,ila kwa kuwa yeye alikuwa na silaha akuzuiwa getini kuingia hata baada ya kutoa kitambulisho,akaambiwa labda aache bastola pale getini...
Wakati mabishano yakiendelea lifti ilokuwa karibu na lile geti ikafunguka wale askari walomkamata Katarina wakamsukuma kwa nguvu katarina,Isack akawahi kumdaka,lau kama siyo kuwa pale Katarina lazima angeumia vibaya sana,ikabidi sasa Merry na Isack wapate kazi ya kumvuta mpaka kwenye gari,bado binti alilia,usingeweza kudhani ndo yule komandoo wa miaka kadhaa nyuma,komandoo ambaye ilikuwa ni nadra kuliona chozi lake...
Isack akaliondoa gari
****
Inspekta Nurdin alishtuka kutokumuona koplo Zena,
Hata alipoenda kwake alikutana na kufuli alipopiga pia namba zake pia azikupatikana
Alijua lazima koplo yule hatakuwa kwenye wakati mgumu,ila akujua angeanzia wapi kuanza kuchunguza jambo lile,alifikisha taharifa zile kwa mkuu wake,ambaye alimtoa khofu na kuahidi kulifatilia...
Wakati inspekta Nurdin akiwa katika hali ya sintofahamu upande mwingine ndani ya gari ya Danieli mtoto wa mh Raisi kulikuwa na kikao maalumu,
Ndani ya gari lile kulikuwa na watu wawili,wote walionekana kuwa na majonzi,ni muheshimiwa Rais upande wa dereva aliketi kijana Danieli
Rais alimweleza kila kitu Daniel Kuhusu Kukamatwa kwa 'Zk' usiku wa jana na khofu yake ya kuuwawa muda wowote,
Ilipaswa apatikane mtu wa kumuokoa Zena haraka sana maisha yake yalikuwa hatarini,
Je wangemtumia nani?,kimbembe kilikwepo hapo
"baba mimi naona bora tumtumie Isack naona huyu atafaa zaidi!"
ITAENDELEA
Simulizi : Kufa Tu Hakuna Namna
Sehemu Ya Tano (5)
"kwa nini umefikiria kumtumia Isack na si mtu mwingine"
Raisi aliuliza,Danieli aliwaza kwa muda kabla ajajibu swali lile,ndipo alipofungua mdomo wake...
"ni kijana anayejiamini,na pia uliwah kunipa sifa zake kwamba kuna mzigo wa muheshimiwa waziri mkuu na bilionea Stewart Greyson aliwah kuuzuhia bandarini japo ulilindwa na wanajeshi,ni kijana mpenda haki,tumtumie tu baba"
Mh Rais akatabasamu
"vizuri je una mawasiliano naye?!"
"hapana baba ila swala ilo naomba niachie nilishughulikie kila kitu kitakuwa sawa"
"ok mwanangu,kumbuka maisha ya yule binti yapo hatarini muda wowote anaweza kuuwawa ivyo fanya kwa haraka na umakini na usiri wa hali ya juu"
"sawa baba niamin mimi"
"ok twenzetu"
Palepale Daniely akaliondoa gari kumrejesha baba yake nyumbani...
Baada Ya Kumshusha baba yake Pasina Kupoteza Muda akaliwasha gari lake kuelekea mahali alipokuwa akiishi Isack,
kumfikishia ujumbe wa muheshimiwa raisi,ilikuwa ni kazi ngumu tena ya hatari ambayo lau kama angekubali kuifanya ingemwingizia kiasi kikubwa cha ela...
*****
Gari ya Isack Walifika nyumbani wakashuka, walimshika mmoja bega la huku mwingine huku,mwili wote ulimlegea,ilikuwa ni kama kapata msiba tena wa mtu wake wa karibu,machozi sasa yalishakauka,na hata sauti pia ila bado alilia kwani bado moyo wake ulikuwa ukiteketea,toka atoke gerezani,Katarina hakutia kitu mdomoni,na hata akuhisi njaaa
Kina Isack walimbembeleza mpaka wakachoka sasa walimwacha!...
Pengine kulia ndivyo kupunguza hasira zilizo usakama moyo wake...
Ghafla kengele ikalia Mery akaenda kufungua geti,akaingia mgeni,hakuwa mwingine zaidi ya Daniel,
Akakaribishwa Sebuleni,
Mery na katarina wakatoka,na kuelekea jikoni
Pale sebuleni Daniel akajitambulisha na kumueleza shida yake Isack!...
Juu ya kwenda kumuokoa "ZK" katika mikono hatari ya usalama wa taifa,Isack alizitambua izo namba,wale ni makomandoo walopitia mazoezi magumu kuliko hata yake,leo ajipeleke kwenye kambi yao kufanya uokozi,
"hapana asee sitoweza,japo ni kazi ya mh Rais lakin mmh,nataman kuendelea kuishi,"
Katakata Isack alikataa...
"labda kuna mtu naweza kukuunganisha naye akaifanya"
"ni nani mtu huyo?"
"ni komandoo Zidu!,huyu mtu ni komandoo tena mwenye uwezo wa ajabu ni mtetezi wa Kinte ambayo nchi hiyo kwa sasa yaitwa ganyakite..."
"staki maelezo mengi nahitaji nionane naye"
Basi Isack akamwelekeza Dani ilipo ofisi ya ZIDU,
Dani akaaga na kutoka zake,muda ule ule alikuwa akielekea mahali zilipo ofisi ya Zidu,
Daniel mtoto wa Rais Asamoye anajaribu kumshawishi Isack kumuokoa 'ZK',Isack anaingiwa na uwoga na kumshahuri Dani akaonane na Zidu pengine yeye angeweza kuifanya kazi ile,je Zidu atakubali na akikubali atafanikiwa?! twende pamoja kuzidi kuburudika...
Daniel alifika mpaka ilipo ofisi ya Zidu,akakaguliwa getini na kuruhusiwa kuingiwa ndani,akaikwea lift na kupanda mpaka ghorofa ya pili akatoka na kuchepuka kuelekea alipoelekezwa...
Akafungua mlango na kuelekea moja kwa moja mpaka mapokezi,
Akaruhusiwa kuonana na Zidu,baada ya salamu na kujitambulisha akapeleka ombi lake,kwamba anahitaji akamsaidie kwa ajili ya uokozi,tofauti na mategemeo yake Zidu alicheka kwa dharau,kisha akaufungua mdomo wake...
"miezi saba ijayo nategemea kuitwa baba natamani sana kumwona mwanangu kwa kuwa sijabahatika kupata mtoto,pia sijafanya mazoez siku nyingi na nadhani unavitambua vikosi vya usalama wa taifa si vikosi vya mchezo cha kukushahuri ukamshahuri Raisi achaneni na huyo binti ila undeni binti mwingine mbona wako wengi tu,"
Daniel aliishiwa nguvu akajaribu kumuomba sana,Zidu bila mafanikio,Zidu alikataa katakata hata baada ya kuhaidiwa kitita cha mamilioni ikiwa angefanikiwa kumuokoa mwisho akaaga na kuondoka zake
Daniel bado moyo wake ukumpa akarejea tena nyumbani kwa Isack Kwenda Kujaribu kumbembeleza...
"Zidu kakataa katakata kufanya hii kazi,nisaidie ndugu yangu nipo tayar tushirikiane kumsaidia huyu binti,"
"kwa nin akatae?!" Isack akahoji kwa mshangao akionekana wazi kutoamin swala lile,katu awakujua Katika Pembe ya sebule ile Katarina alikuwa akiwasikiliza kila kitu...
"anasema miezi saba ijayo anaenda kuitwa baba..."
"what!?" Isack Akauliza Kwa Mshangao alijua ile ni habari mbaya kama ingefika masikioni mwa Katarina,kwa udhaifu alo uonesha toka kuachwa na Zidu mwanaume alompenda hakutaman apate habari kama hii katu akujua Katarina alishasikia kila kitu,akaishia kutabasamu,
Mwanamke akilia sana,akiumia sana uzidi kupata ujasiri na ni vigumu kulia tena,ndivyo alivyokuwa Katarina,alilia Sana aliumia pia sana,mpaka maumivu yakafika kikomo ivyo hata aliposikia lile neno kwamba Zidu mumewe ni baba kijacho binafsi akujali,akachukulia kawaida ila ghafla akajitoa mbele yao akiwa siriazi pasina tabasamu
'Kwa moyo wangu mweupe, bila kushurutishwa na mtu,kwa kuipenda pia nchi yangu japo si niliyozaliwa nipo tayari kuifanya hiyo kazi ya kumuokoa huyo binti"
Si Daniel pekee alotoa macho ya mshangao kumshangaa binti yule hata Isack alomtambua fika,kwamba naye kwenye mapigano ana uwezo hata zaidi yake,ila mshangao wake kwa hali alokuwa nayo angeweza kufanya kazi kama ile?
Kazi iloitaji umakini wa hali ya juu,kazi ilohitaji hata kujitoa roho yako pale utakapodhibitiwa na kulazimishwa kumtaja alokutuma au alokuwepo nyuma ya mpango wote
"huyu ni nani?"
Daniel akamuhoji Isack swali hakiwa na uso wa mashaka wa akili za mtu alosimama mbele yao kikakamavu,
"naitwa komandoo Katarina,ni binti nilopitia mazoezi ya kiko mandoo na pia nimehusika katika operesheni mbalimbali,nipo tayari kufanya kazi hii ndani ya masaa 24 kumuokoa mtu huyo"
"huyu binti ni nani?!"
Daniel akarudia swali lake wakati huu akimkata jicho kali Isack,jicho lililo maanisha kutofurahia kitendo cha binti yule kuingiza utani katika swala lile nyeti,kuokoa maisha ya mtu!
"anaitwa kk,komandoo katarina,utambulisho wake alokupa ni wakweli mpe kazi kama kakubali kuifanya"
Daniel akacheka kwa dharau akapeleka mkono wake kibindoni ile anataka achomoe bastola akujua ni saa ngapi alinyakuliwa anachokumbuka ni wakati akitua chini binti akamuwah na kumpokonya bastola...
"nadhani ulitaka kujua uwezo nilokuwa nao hapo ulitaka chomoa bastola umwelekezee Isack"
Daniel alibaki pale chini kapigwa na butwaa kwanza wepesi wa yule binti pili uwezo wake wa kutambua hata kile ambacho akijatokea,
Katarina akampa mkono akamnyanyua pale,wakakaa kitako,
"kama upo tayari kufanya hii kazi tafadhal naomba tukafanye maongezi privet"
Katarina hakuwa na shida, hata Isack mwenyewe wakaingia ndani ya gari,na Daniel akaliondoa gari,ndani ya gari hakuna alomuongelesha mwenzake,gari ilielekea mpaka ikulu akamtumia meseji Rais,mh akatoka Dani akaliondoa gari mpaka mahali anapolipaki kando ya barabara na kufanyia mazungumzo!...
Daniel akamsimulia kila kitu,toka Isack kogopa ile kazi
kumuunganisha na Zidu,Zidu naye kumkatalia kwa kisingizio kuwa anaenda kuwa baba,wasichokijua ni kwamba yule binti ni mke wa huyo Zidu wenyewe wanayemzungumzia,ndipo aliporudi kwa Isack na kuendelea kumsihi akubali kwenda kumsaidia kufanya iyo kazi,
Isack alikataa katakata ndipo binti huyu ambaye hata naye ni komandoo alipojitokeza kukubali kuifanya hiyo kazi,
Rais alimshukuru sana Katarina
"nawe pia unatokea Ganyakinte?"
Rais Asamoye alimuuliza akitaka kudhibitisha kile mwanae alichomweleza,
"ndiyo mimi nilikuwa mke wa Zidu Ila tumeachana saivi naishi kwa shemeji yangu"
Rais akampa pole,
"kwa sasa ntakupa nyumba ya kifahari mbezi maeneo ya keko,gari kali ya kutembelea na ntakuunga katika kikundi changu cha usalama wa taifa (2) kuachana na icho cha waziri mkuu,fanya kwanza hii kazi mwokoe mwenzako muianze kazi rasmi kwa taharifa nilizozipata kwa sahivi huyo binti kaifadhiwa maeneo ya bunju b kulipo na kambi yao usiku sana ndo atapelekwa msitu pande kuuwawa ivyo wewe kabla awajafika pande utatakiwa uweke kambi mapema tu katika msitu wa mabwepande wakipita utajua jinsi ya kuwafatilia...
Sawa mkuu nimekuelewa nakuahidi kufanikisha jambo hili,pasina kufanya kosa hata dogo,kikubwa mida ya saa moja nifikishwe huko magwepande,
"hakuna tatizo,we utamwambia mwanangu vitu unavyohitaji atakupatia na usiku atakufikisha katika huo msitu,ukisha muokoa na kuwauwa wote utafata barabara ya vumbi ile inayoenda kutokea makabe then ukitokea makabe mtaelekea mpaka mbezi mwisho hapo mwenzako atakuelekeza nyumba ambayo unatakiwa ufikie,asubuh atakuja kuwachukua na kuwapeleka morogoro katika kijiji cha zinga eneo salama zaidi"
"sawa Mzee nimekuelewa,"
"ok binti kila la kheri naiman ni kazi ngumu ila utaishinda pia usisahau kusali Mungu Pia akupiganie na kukulinda pia"
"nimekuelewa muheshimiwa raisi nitashinda kwa hili"
"ok,kijana wangu nirejeshe ikulu!"
Daniel akalitia gari moto kumrejesha baba yake ikulu kwanza,ndipo ampatie vitu Katarina atakavyohitaji!
Katarina anaamua kubeba jukumu la kumsaidia 'ZK' pasina kujua kuwa binti huyu Zena ndiyo yule alokuwa amepania kumfunga siku chache nyuma,je Kk atafanikiwa kumuokoa "ZK" twendelee na sehemu hii ya 26 ya riwaya hii ya kusisimua...
USALAMA WA TAIFA
Asubuhi kama walivyokubaliana,vijana wa usalama wa taifa waliweka kikao ndani ya ofisi ya mkuu wao madam 'S' madam hakuwa na taharifa yoyote ya kukamatwa kwa "ZK" akafungua kikao kwa kutanguliza kumshukuru Mungu kwa kuwakutanisha tena
"kwa furaha zionekanazo ndani ya nyuso zenu zinanipa matumaini niamini kwamba kazi yangu mmeifanya vizuri pasina kosa lolote,"
Madam 'S' akaongea kwa sauti yake ya upole likipambwa na tabasamu dogo mdomoni mwake,
"ndiyo mkuu kazi imeenda vizuri na tunafurah kukwambia kuwa tumeua ndege wawili kwa jiwe moja"
Pizo akajibu kwa niaba ya wenzao,
"kivipi sasa?!" madam akahoji akikaa vizuri kwenye kiti chake,pizo akaendelea
"ZK yupo mikononi mwetu uwezi amin mkuu na tena kumbe ni mtoto wa kike?"
Madam 'S' akayatoa macho kwa mshangao,wakamueleza walivyo mkamata kirahisi tu,baada ya kuanza kuwafatilia pia wakamuonesha na picha walizomkuta nazo,Madam 's' aliwapongeza vijana wake kwa kazi nzuri,pasina kutambua Rais alisha zipata habari zile kupitia maiki alizozitegesha kisiri ndani ya ofisi ile kwa kumpa kijana wake aliyoko ndan ya kikosi chake cha siri mwenyewe alichokiita usalama wa taifa '2'
SIKU CHACHE NYUMA
Kwa Jina aliitwa Richard Mombi alishuka ndani ya gari lake taratibu na kuelekea ikulu,baada ya kukaguliwa aliingia ndani na kuonana na muheshimiwa Rais,Mombi huyu baada ya kufanya kaz muda mrefu Kinte,sasa aliamua kurudi nyumbani Tanzania kijana huyu pia ndo aliyewah kumsaidiaga Zidu kipindi kile alipotekwa na kutaka kuuliwa na Rais laizer,ni Mtanzania aliye enda Kinte Kwa ajili ya kulinda amani kule,baada ya machafuko kupungua sasa alikuwa karejea nyumbani,na siku hii Rais alimwita na kumpa kazi mahalamu ya kuhakikisha anaweka kamera ndani ya ofisi zote za usalama wa taifa,kwanzia pale ikulu na pia kule kwa waziri mkuu,
Pia Ilipaswa afanye juu chini kuingia usalama wa taifa (1) kama mpelelezi,kwa maana hiyo angelipwa mara mbili,alifanikiwa kufanya kama alivyoagizwa na habari zote za vikao walizokuwa wakifanya zikawa zikimfikia Rais moja kwa moja,
mpaka kikao kile cha kukamatwa kwa 'ZK' Rais alikisikia moja kwa moja ndipo alipo muita mtoto wake Daniel na kumpa taharifa,na kumwagiza akamtafute mtu awezaye kuwa mwokozi ndipo Dani alifanikiwa kumpata Katarina,baada ya Isack na mwenzake Zidu kupinga kufanya operesheni ile,
USIKU
Kama wenyewe walivyopanga kumtesa sana 'ZK' ndani ya msitu wa pande usiku wa manane na kumuua kikatili kwa kumkata kata vipande,usiku huu wakiwa ndani ya Gari lao,Zena alikuwa kaumia vibaya sana,ni baada ya kupata mateso yale makali,akilazimishwa aseme ni nani hasa anayemtuma,baada ya kukataa katakata ndipo Madam 's' alipoagiza kuuwawa kikatili kwa kumkata vipande vipande hawamu walijipanga kama ilivyokuwa kwa salome gari mbili ya mbele wakiwepo watu wa tatu na ya nyuma pia wakiwepo watu wa tatu ambao ni Richard Mombi,mudi,na Green Cobra huku gari la mbele likiendeshwa na Pizo siti ya nyuma alikaa veko katikati Zena na mwisho Chronic Killer Safari ilikuwa ni ndefu hatimaye wakaingia katika msitu wa mabwepande safari ikaendelea...
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment