Search This Blog

Friday, 30 December 2022

KIAPO CHA MFUNGWA (5) - 3

    

Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (5) 


Sehemu Ya Tatu (3)

"mume Wangu Zidu Kauwawa Na Jambaz Njoo Mume Wangu!"



Palepale Isack baada ya kupokea simu ile alinyanyuka akionekana wazi amechanganyikiwa Zidu Katekwa?,na Nani Na Kwa Nin,aliwaza Pasina Majibu Akaingia Ndani Ya Gari La Polis Na Mapolis Kadhaa,



"elekea Msitu Pande,akatoa Amri Kwani Simu Yake Alitegesha VCP na simu ya Zidu Kwa Usalama Ikiwa Mmoja Wapo atapatwa na tatizo alama ile itamjulisha mahali alipo au anapopelekwa



Baada Ya Mke Wake Kumpigia Simu Na Kumwambia Zidu Katekwa Akawasha Vcp Na Kunasa Eneo Mr Henry Alilokuwa Akielekea,nao Wakawa Wakielekea Huko Huko,moyon Mwake Akiwa Na Nia Moja tu kumuokoa ZIDU,rafiki yake wa kitambo



JE ISACK ATAFANIKIWA kumokoa zidu?,mr X Kashakamilisha Kazi Ni Kwel Zidu Kafa Na Mr X Na Zidu Wana Ugomvi Gani,je Baada Ya Mery Kumjulisha Katarina Kutekwa Kwa Mumewe Katarina Alifanyaje?,gambi Naye Rumande Kule Ndo Bas Tena? Majibu Yote Ni Kwendelea Kuwa Nami Katika Riwaya Hii Inayoumiza Kichwa Katika Utungaji Wake!









Ni Wakati akiwa hospitalin ghafla simu yake ikaita,akaingiza Mkono Kwenye Pochi Yake Na Kuitoa,



Aka angalia ni nani aliyempigia,



'Mery' ndo jina lililosomeka kwenye skrin ya simu yake pale pale Katarina akapokea simu ile,



Ghafla alitoa macho ya mshangao ni kama alipokea taharifa mbaya pale pale simu ikamponyoka naye chini,tena akidondokea tumbo maumivu mara mbili,haraka sana wauguzi wakamnyanyua na kumwingiza wodini,damu zilikuwa zikimtoka,ni wazi mimba yake kwa awamu nyingine ilikuwa imeharibika,habari aloipata kwamba mume wake Zidu Kauwawa Na Kisha Kutekwa Aikuwa habari njema hata chembe,



wakati hali ya Katarina Ikiwa Mbaya hosptalin baada ya kupokea taharifa mbaya,upande wa pili gari ilompakia Isack Na Baadhi Ya Wanausalama Ilizidi Kukata Mbuga Huku Macho Ya Isack Yakiwa Katika Kifaa Chake Cha Kumuelekezea Njia,taratibu Wakaanza Kuingia Msitu Pande,kichwan Kwake Akiwa Na Mawazo Kibao,



'naenda Kukichinja Kichwa Chake Katika Mvule Wa Ajabu Na Hapo Ndipo Ntakapoipata hazina ya mababu ilofukiwa humo muda mrefu'



Kumbukumbu hiyo ikajirudia katika kichwa chake mr x aliitaman ile hazina,swala la kumuua Zidu Akalisimamisha Kwanza Alishawah Kusikia Juu Ya Hazina Hiyo Katika Riwaya Ya Jini La Mapangoni



CHANZO CHA HAZINA HIYO KUTOKA KATIKA RIWAYA YA JINI LA MAPANGONI



KIPINDI CHA UKOLONI WA WAINGREZA



Baada ya waingreza kufanikiwa kuwang'oa mabepari wa kijerumani,taifa la Tanganyika Likawa Koloni La Waingreza,



Sir Horace Akiwa Gavana Wa Kwanza,baada Ya Miaka Kadhaa Kupita hatimaye katika kipindi cha gazana Wa Mwisho Richard Tunbull Waingreza Waliwah Kununua Hazina Ya Kutosha Kutoka Kwa Sultan Aliyeitawala Zanzibar Na Hazina Ile Waliifadhi Huko Mandaka Na Juu Wakapanda Mvule Ulokuwa Kwa Kasi,



Badae Baada Ya Baba Wa Taifa Kulipatia Taifa Uhuru Waingreza Waliondoka Pasina Kuchukua Kitu Ila Hazina Ile Ilibaki Katika kitabu Cha Kumbukumbu Katika Familia Ile Ya Gavana,



Miaka Ikasonga,hazina Ile Ikawa Ikilindwa Kila Alojaribu Kuifukua Alikufa,kutokana Na Kutokujua Masharti Ya Kuipata Hazina Ile,koo Za Gavana Walibaki Kusoma Kile Kitabu Kama Cha Stori Tu Na Kudharau Habari Zile Kizaz Kwa Kizazi Mpaka Kizaz Cha Henry Leyland,



Henry Akaamua Kuvalia Njuga hazina ile,na damu aloamua kuimwaga ni ya Zidu Katili



Katu Akujua Kitendo Cha Kumwambia Bosi Wake Ukwel Juu Ya Hazina Ile Naye Akaitaman Wazo La Kumwangamiza Zidu Akaliweka Pembeni,pesa Kwanza,na Kwa Kuwa Mr Henry Akumjua Kwa Sura Kazi Ile Angeifanya Vizur Sana,



Isack akazidi kumwambia dereva akanyage mafuta,

Langon Pale Wakapaki Gari Yao wakashuka na mitutu yao kuingia msituni kuelekea ulipo mvule,



Henry Leyland aliwasili katika mvule ule akamtoa Zidu ambaye bado akuwa na ufahamu akamtupa pembeni ya mvule ule aliitajika awe na shoka au pengine panga au kisu cha kumchinjia na pale akuwa navyo angepata wapi,akawaza ila ghafla akasikia mtu ni kama alikuwa akikata kuni akatoka pale kuelekea eneo alilosikia kuni zikikatwa,hapakuwa mbali sana na pale basi palepale akamtungua yule mtu juu kwa risasi yule mtu akadondoka na panga lake akabeba panga mtu akamuacha palepale chini, Wanajesh Wale Wakiongozwa Na Isack Walizidi Kusonga,ghafla Wakasikia Mlio Wa Risasi,



Moyon Mwake Isack Alizidi Kufrah Alitaman Amkute Zidu Kafa Lengo Lake Liwe Limefanikiwa alimchukia Zidu Zaidi ya kitu chochote yeye ndo alijiita 'mr x' naye ndiyo alikuwa kiongozi wa kundi la mafia,



Siku Zote Alicheka Na Zidu wakishirikiana katika maswala mengi ya hatari ila moyoni mwake alikuwa na chuki kali dhidi ya mtu yule



kiteso alichomtesa utotoni aliapa siku moja angekilipiza,tatizo Zidu Alikuwa Komando Naye Mwanajeshi Wa Kawaida,ivyo Asingeweza Kumfata Yeye Kama Yeye Na Kumuua Ilipaswa atume watu wenye uwezo wa kikomando, pesa alizolipwa na nchi yake pamoja na Kinte Kwa Kitendo Cha Kwenda Kumsaidia Zidu Akakusanya Na Fedha Zake Za Jeshini,akaungana Na Mwarabu Milionea Wa Pakistani Omari Al Watab Akafungua Kundi Lile La Mafia,



Likasambaa Ulimwenguni,akazidi Kuingiza Pesa Kwa Kazi Alizozipata,akanunua Makomandoo waloasi jeshi lao wakawa wakifanya kaz za kiuhalifu na kuzidi kujiingizia hela

yote Isack 'mr X' alifanya kwa siri tena katika usiri mkubwa,



Baada Ya Mr Henry Kubeba Shoka Lake aliwasili eneo la tukio mkononi pia alikuwa na kipande cha gogo,katu akujua kuwa tayari alishazingirwa na wanausalama,wakimtazama vile alivyokuwa akifanya,akaweka kile kigogo chini akamvuta Zidu Na Shingo Yake akaiweka juu ya kigogo akanyanyua shoka lake ila kabla ajaishusha,



Isack Kule Silaha Yake Ikacheua Risasi Kadhaa Zikakishambulia Kifua Cha Sir Henry Akatupwa Mita Kadhaa Shoka Likienda Kivyake Na Yeye Kivyake Palepale Akapoteza Maisha



'kwa Mr X Ni Kosa Kufanya dili juu ya dili'



isack akawaza,pale pale akawa amrisha dereva akalete gari,wamuwaishe Zidu hosptalin alijua awezi pona,

Wakati Dereva Ameenda Kuleta Gari Yeye Na Wale Wanajeshi Watano Aloshirikiana Nao Akawashirikisha Juu Ya Dili Lile,



Wakakubaliana



Haraka Wakamchukua damu ya Henry Na Kuinyunyuzia Mti Ule,



"tukishafika Mjini Kuwaleta Hawa Watu Sis Watano Itabidi Turudi Huku Kufukua Hii Hazina"



Isack Akatoa Wazo Lake,wenzake Wakakubal,dereva Akawasili Wakaipakia Ile Miili Mpaka Kcmc Kwa Matibabu,habar Zikafikishwa Marekani Kuuwawa Kwa Gaidi Wa Kundi La Mafia Alokuwa Akisakwa Kwa Muda Mrefu Nchin Tanzania...



Sifa Kwa Isack Zikazidi Mara Dufu Huku Akiandaliwa tuzo,muda huo Zidu Na Mke Wake Katarina Walikuwa Icu Mahututi,wakipumulia Mashine...

Kwa Kwel Hali Ilitisha







Hali Nchini Marekani Inazidi Kuwa Mbaya,hatimaye Mr X tunamtambua kama Isack,mwenye Malengo Ya Kumwangamiza Zidu Kutokana Na Mateso Aliyewah Kumpa Kipindi Cha Utotoni,



Kwa Siri Sana anamiliki kundi hatari la mafia linalopokea kaz mbalimbal za kiuhalifu,rais Mernel ii,pasina kujua analitumia kundi hili,ila vijana wote wanaotumwa wanauwawa mwisho Henry Akiwa Na Siri Nzito Anakuja Tanzania Kumwangamiza Mwenyewe Zidu anafanya kosa kumshirikisha bosi wake mr x dili lile,mr x anamgeuka Henry Na Kuchukua Jeshi,mpaka Katika Msitu Ule,anamwangamiza Kijana Ake Na Mwisho Zidu Anawaishwa Hosptal Akiwa Na Hali Mbaya,



Isack anajua Lazima Afe,katarina naye baada ya kupokea taharifa Ya Kuuwawa Na Kutekwa Kwa Mume Wake Anadondokea Tumbo Damu Zinaanza Kumvuja Naye Kupelekwa Icu Je Nin Kiliendelea Tusonge,tukiachana na Tanzania



TURUDI KINTE



GEREZA LA GOMOLE (JEHANNAM JAIL)



GOMOLE lilikuwa ni gereza kubwa lenye ulinzi mkali, Wanajeshi wenye silaha nzito walilizunguka gereza hilo kuzuia wafungwa kutoroka.



Milango ya chumba cha Mahabusu ilikuwa imezungukwa na minyororo na makufuli makubwa,



Askari walofuzu wakiwa na silaha nzito wakiwa pembeni ya milango hiyo.



Lilikuwa ni gereza la kijeshi, lenye mateso makali, wafungwa wote walikuwa wamelala chini, ubavu mmoja bila kuubadilisha.



Wakijaribu kupitisha nusu siku,



Ndipo jambo lisilotegemewa lilipotokea.



Muda huo huo kengele ya tahadhari ya gereza lile ikawa ikiita tena kwa fujo sana....



Souty goal...



Amri ilitolewa kila bweni milango ikifunguliwa na wanajeshi wafungwa wale kijeshi walitoka nje na kujipanga msitari mrefu taa za gereza lile zikawashwa.



Usiku ukageuka mchana.



Hekaheka zikatawala, tayari, vingora vya magari ya polisi vilishaanza kuskika,



Polisi wengine waliyokuwa na mbwa wakali walianza kutoka katika lango kubwa la gereza hilo;



Hali ya sintofahamu ilizidi kusambaa vichwani mwa wafungwa wale.



“Kuna nini?”



Ndilo swali walilokuwa wakijiuliza,



Ghafla askari kwenye spika akatangaza, popote alipo Laurent Gambi ajitokeze Huwezi kuukimbia mkono wa serikali, tayari jibu lilishapatikana kwa mara nyingine kidume roho ya paka kilishatoroka



§§§§§



Brown Stanley afisa upelelezi akiwa anajaribu kuutafuta usingizi simu yake ya kiganjani ikaita,



Ni mlio asioupenda, mlio wa tahadhari Katika simu yake,ni mlio kutoka idara ya upelelezi katika kitengo maalum cha Taifa.



Usingizi wote ulimpaa, miayo yote iliyeyuka, akanyanyuka toka kitandani kiuchovu na kuketi,



Akaichukua simu yake na kuipokea.



*“Laurenti gambi katoroka (…) na jeshi letu lazidi kumsaka (…) katoroka usiku huu kaua askari wetu wawili na katoroka na silaha zao na kamvua uniform mmoja,"*



Brown hakujibu kitu,



Hakupaswa kujibu kitu



Alivuta pumzi na kuzishusha kwa nguvu



“Gambi katoroka?”



Brown aliwaza akakumbuka shida alizozipata mpaka kumtia nguvuni mtu huyo hatari,ndipo akapandishwa cheo mpaka kuwa Kamishna afisa upelelezi



Japo kilikuwa ni kipindi cha baridi kali ghafla aliisi joto, harufu ya kifo chake aliiona katika mawazo yake.



Alimjua vizur gambi.



Kijana aliyekuwa akisubiria hukumu yake ya kunyongwa kwa kosa la kutaka kumtorosha baba yake,



Alirudi kitandani na kujitupa akizishusha pumzi ndefu, mke wake hakujua kinachoendelea yeye alikuwa usingizini pengine ndotoni.



Usingizi ulimpaa Brown ilikuwa ni lazima Laurent apatikane kwa njia yeyote ile akiwa mzima au maiti.



Aliendelea kuwaza huku akiutafuta usingizi bila mafanikio.



“Wakati huu tutasalimika kweli?”



Alihitimisha kwa wazo hasi.

Na akujua kwa nini aliwaza vile



§§§§§



Brown Stanley afisa upelelezi katika kitengo maalumu cha Usalama wa Taifa, aliingia ofisini kwake akiwa mnyonge akaenda kuketi kimya katika meza kubwa ilozungukwa na makabrasha mengi akipitia moja baada ya jingine



Aliishusha miwani yake chini kidogo akilitumbulia macho file moja akilisoma kwa umakini;



Ghafla tabasamu la faraja likaupamba uso wake alipata alichokihitaji,



Alibonyeza namba kadhaa na kuupeleka mkonga wa simu masikioni mwake akisikiliza upande wa pili,



simu iliita.



Macho yake yaliendelea kupitia wasifu wa mpelelezi wa kujitegemea,



Jonathan, ambaye alihisi ndiyo atakaye faa katika kazi ya kumsaka Laurent Mernel Gambi

.

“Makao makuu ya jeshi la polisi Ganyama inspecta Jonathan naongea,”



INS JONATHAN KIMARIO au JONA kama wengi walivyopenda kumwita alikuwa ni mpelelezi mashuhuri, na mwenye uchungu na nchi yake alikuwa ni kijana wa wastani mwili wake ulojengeka kimazoezi akiwa ni kijana mtanashati;



Kazi ya jeshi aliipenda tangu alipokuwa mtoto na alishaizoea mikiki mikiki,



serikali ilimtegemea kwa kila kazi ndo mahana nafasi nyingi za kusoma zilimwangukia yeye pia ilisemekana kuwa alikuwa ni mpelelezi wa fbi lakini hakuna mtu aliyedhibitisha,



Hakuna kesi aloishindwa iwe ya nguvu za giza, kigaidi, au ya kimafia ilipokuwa mkononi mwa Jonah kesi iliisha kwa muda mfupi tu.ndo mahana afisa upelelezi Brown alimteua yeye kuwa msimamizi mkuu wa kumrudisha LAURENT GAMBI kifungoni akiwa mzima au maiti jona alipanda ndege ya jeshi la polisi na safar ya kuelekea kinte ikaanza



Akitegemea masaa matatu mbele atakuwa mbele ya bosi wake akipata maelekezo.



§§§§§



Alikuwa ni bonge la mtu,



Pandikizi, aliyeenda hewani mwenye mwili wa mazoezi,



Alikuwa kavaa sare za maaskari wa jeshi la magereza mkononi alikuwa kashika mtutu aina ya gobore na mgongoni akiwa kavaa nyingine



Alikuwa akikimbia katikati ya pori huku jasho likimtoka japo halikuwa amechoka hakuwa tayari kusimama



Kitendo cha yeye kusimama ndo kingemaanisha kifo chake,naye hakuwa tayari kwa ilo.



Moyo wake ulijaa ghadhabu na hasira huku hakifikiria kitu kimoja tu kisasi kuuwa watu wote waliosababisha yeye kuwa mfungwa hakuwa na kosa heti abaki kusubiri siku ya kunyongwa ilo alikuwezekana,japo alionekana ni kijana mpole,mkarimu,ila sasa aliapa kuwa katili kwa wote waliomtenda kichwani mwake alikuwa na orodha ya watu aloitaji kuwaua.haraka sana,ni watu wenye vyeo,ni watu wenye pesa,yeye hakuwa na kitu,yeye alikuwa ni wanted hichi ndo kitu kilicho muumiza....



Ghafla akapiga magoti chini kwa hasira akawa analia, ghadhabu ,hasira zikampanda



HUYU NDO ALIKUWA GAMBI MFUNGWA ALIYETOROKA







kitendo cha yeye kusimama ndo kingemaanisha kifo chake,naye hakuwa tayari kwa ilo.moyo wake ulijaa ghadhabu na hasira huku hakifikiria kitu kimoja tu kisasi kuuwa watu wote waliosababisha yeye kuwa mfungwa hakuwa na kosa heti abaki kusubiri siku ya kunyongwa ilo alikuwezekana,japo alionekana ni kijana mpole, mkarimu, ila sasa aliapa kuwa katili kwa wote waliomtenda kichwani mwake alikuwa na orodha ya watu aloitaji kuwaua.haraka sana,ni watu wenye vyeo,ni watu wenye pesa,yeye hakuwa na kitu,yeye alikuwa ni wanted hichi ndo kitu kilicho muumiza....ghafla akapiga magoti chini kwa hasira akawa analia,ghadhabu,hasira zikampanda



Tuendelee....



Yeye hakuwa na kitu, yeye alikuwa ni "Wanted" ndiyo kitu kilichomuumiza akapiga magoti chini akiwa analia,


ITAENDELEA

    

Simulizi : Kiapo Cha Mfungwa (5) 

Sehemu Ya Nne (4)



uchungu ukiwa umemmeza dhidi ya watu walioua wazazi wake na kumweka yeye mahabusu;



Aliapa kuwafunza adabu hakupenda kuonewa ndo maana akaapa hata kutoroka gerezani,



Kila alipokumbuka ghadhabu zilimzidi, ghafla alianza kuachia risasi hewani akipiga kelele, kwa mbali akaanza kusikia sauti za mbwa wakibweka



Kwa ghafla na akashikwa na hamaniko,



Akajinyanyua pale chini na kuendelea na safari.



Safari hii akitembea ila kwa mwendo wa haraka.



Lilikuwa ni pori kubwa lililozungukwa na miti ilofungamana na kutawaliwa na giza,



Pori kubwa lililosifika na wanyama wakali na mauza uza kibao, kwa Gambi hilo hakulijali,



gobole alilolishika lilimlinda.



Huyu ndiyo Laurent Gambi, mfungwa aliyetoroka na kusakwa kwa udi na uvumba, ama awe hai au maiti.



Inspekta Jonathan aliingia makao makuu ya jeshi la polisi na kuelekea katika ofisi ya afisa mpelelezi na mapokezi alikaribishwa na msichana mrembo ambaye alikuwa ndiyo Mhudumu, mwenye haiba ya kimapenzi, uso wake muda wote ulijaa tabasamu na kichwani alitupia ushungi.



“Oooh Aisha sasa upo front office?”



aliuliza Jonathan. Bilhai kwamba alimtambua macho ya msichana yule mrembo yakaongea, akaelewa na kupotezea , kumbe naye alikuwa ni kachero mwenzake.



“Nahitaji kuonana na M...,” Jona aliendelea Aisha alitabasamu tena mwanya mdogo ukaonekana katikati ya meno, na mashavu yake yakajikunja na kutengengeza vishimo na kuongeza tashtiti ya urembo kwa msisichana yule aliyekuwa ni mrembo wa haja.



Mkono wake wa kushoto uliuendea mkonga wa simu na kuunyakua mpaka masikioni na mkono wake wa kulia kuzungurusha taakimu kadhaa.



“Kuna mtu anaitaji kukuona hapa,



kwa sauti ndogo dada yule aliongea.



Kisha akamgeukia Jonathan, “Eti nimwambie nani?” Aisha alihoji jina.



Jonathan akapatwa na mshangao akakodoa macho kama mjusi kabanwa na mlango kisha kwa sauti yake ya upole na kubembeleza iloanza kukata tamaa ikasikika



"Mh! ina maana mpaka jina umensahau Aisha?"



ila bado lugha ya macho iliendelea kusomeka machoni mwa mrembo yule ni lugha maalumu kwa wapelelez kama hao.



"Mwambie ni Jona!" Akatamka.



"Mheshimiwa, anaitwa Jona" Aisha alijibu kwenye simu.



"Ok ingia,"



hatimaye alimruhusu Jona alishangaa umakini wa yule dada mrembo ambaye ni wazi kuwa alimfahamu zaidi hata ya sisi tulivyomfahamu.



Jona aliingia huku kichwa chake kikiwa na maswali mengi yalokosa majibu juu ya binti yule ambaye ni wazi alikuwa pale kwa ajili ya kazi,



hilo hakulijua ila Aisha hakuwa Mkinte wala Mganyama, uwepo wake pale ulimtia shaka.



Akaachana nalo na kuingia katika ofisi ile.



Ilikuwa ni chumba kipana kilichozungukwa na makalabrasha pande zote,



katika kiti aliketi kijana mdogo si juu ya miaka 35 mtanashati, aliketi uso ukipitia ma file aloyapembua katika meza yake, moja baada ya jingine.



Jona alisaluti na kwenda kuketi baada ya kupewa ishara ya kufanya ivyo.



"Nimeitika wito afande" Jona alitamka baada ya kimya cha muda mfupi.



"Laurenti Gambi katoroka!" afisa yule alitamka neno lililomshtua hata JONA, mwenyewe



"Katoroka usiku wa kuamkia leo"



Kamishna Brown aliendelea kutanabahisha, sasa uso wa Jona hukuwa na mshangao tena bali sasa ulisoma fadhaiko na haminiko kwa kile alicho ambiwa,



kuwa kakimbilia katika msitu mnene uitwao Lwana,na kwamba maaskari wa anga na nchi kavu, wenye mbwa wameuzunguka msitu huo wakimsaka na mpaka wakati huo hakuna mafanikio na ya kuwa mtu huyo ni hatari kwa taifa.



"Aka!"



Jona alishtuka, ila Brown akaendelea,



“Amri imetoka Ikulu, idara ya Usalama wa Taifa kuwa mtu huyo apatikane akiwa mzima au maiti,”



bado Jona hakuelewa anacho ambiwa 'Laurenti katoroka? katoroka Gomole. gereza la kijeshi lenye ulinzi mkali katoroka kivipi?

au kuna njama?'



alijiuliza maswali, aikumwingia akilini,



“Kakimbilia msitu wa Lwana msitu na umezingirwa lakini hajaonekana kivipi?a”



Bado maswali yalizidi kutiririka kichwani mwake,



“Alivunja milango au alitorokaje?”



Akaitimisha mawazo yake kwa kushusha pumzi ndefu hakuwa na muda wa kumhoji bosi wake maswali alichohitaji muda huo ni kwenda kupumzisha akili yake kwanza ajue pa kuanzia kwake kesi za utata ndizo alizokuwa hakizihitaji zaidi,



Kesi zilizoshindikana



Baada ya kupokea file lile akatoka na kuelekea katika nyumba alokabidhiwa na jeshi la polisi kwa kipindi chote cha msako wa bedui Laurent Menel Gambi.



§§§§§



Akiwa ndani ya msitu ule mkubwa, kwa mbali alianza kuziona helikopta za kijeshi,



kwa sababu naye alikuwa na mafunzo ya kijeshi aikumuwia vigumu kujua ni kipi alichotakiwa kufanya.



Safari hii hakuwa na madawa ya kiganga ya kuto onekana ivyo ilimpasa ajifiche kijeshi kwa kulitambua hilo Kwa kasi ya ajabu alilala chini na kuanza kutambaa kama wanajeshi wafanyavyo,



Kutanabahi, sauti za mbwa kwa mbali zilianza kusikika zikija maeneo yale,



moyo wa Gambi ulianza kwenda mbio lakini aliuzuia woga na kuuvaa ujasiri,



yeye alikuwa ni mwanajeshi lazima akomae kama komandoo vitani, aghalabu, hakuwa kwenye eneo baya kwani vichaka vilivyofungamana vilimpa hifadhi ya kujibanza kwa umakini hilo alifanikiwa



Sauti za mbwa nazo zilizidi kusikika zikilikaribia eneo lile,



Gambi hakuwa tayari akutwe kama kondoo katika eneo lile,



alianza kutambaa chini kwa chini kwa minajili ya kusonga mbele katu hakuelewa kuwa msitu mzima nyigu walitapakaa,



akiwa anaendelea kutambaa kwa tumbo, mara alisikia muungurumo wa gari nyuma yake akajigeuza kutazama,



Lilikuwa ni Canter la kijeshi kwa mtazamo wa haraka ndani ya gari lile Gambi aliweza kuwaona wanajeshi wanne,



Akajibiringisha na kujificha katika kichaka kilichokuwa pembeni yake huku macho yake yakiliangalia canter lile likija kwa kasi.



Baada ya sekunde kadhaa Canter lile lilimpita, gambi alianza kutambaa akijificha na miti kuepuka kuonekana na helkopta zile.



Mwendo mfupi mbele lile gari lilisimama, Gambi aliliona na haikuwa mbali kutoka pale alipo aliongeza kasi kwa kutambaa na kulifikia, akakwea na kuingia nyuma kwa tahadhari kubwa ili asionekane



Nyuma ya kenta lile la kijeshi



Alijiamini huyu mtu...







Lilikuwa ni kenta la kijeshi kwa mtazamo wa haraka ndani ya gari lile Gambi aliweza kuwaona wanajeshi wanne,



Akajibiringisha na kujificha katika kichaka kilichokuwa pembeni yake huku macho yake yakiliangalia kenta lile likija kwa kasi.



Baada ya sekunde kadhaa kenta lile lilimpita, gambi alianza kutambaa akijificha na miti kuepuka kuonekana na helkopta zile.



Mwendo mfupi mbele lile gari lilisimama, Gambi aliliona na haikuwa mbali kutoka pale alipo aliongeza kasi kwa kutambaa na kulifikia, akakwea na kuingia nyuma kwa tahadhari kubwa ili asionekane hata kupitia kwenye vioo vya pembeni ilo alifanikiwa kuwapumbaza wale wanajeshi hata na kinachoendelea.



Insp Jona akiwa ndani ya gari aina ya BMW ya kisasa alokabidhiwa aitumie ndani ya kipindi hiki cha msako wa Laurent Gambi.



Alisimama katika gereza la kijeshi la Gomole, akashuka na kwa hatua zake fupi fupi akaelekea kwa mkuu wa Gereza



Wengi walipenda kumwita S.P Mkoloni ambacho kilikuwa ni kifupi cha jina lake Saimoni Patrick mzee mwenye miaka kama 60 na kuendelea aliketi katika ofisi moja akipekuwa mafaili;



Mlango uligongwa na kijana Jonathan akaingia, tayar S.P kwa kumtazama tu alijua yule mgeni wake ni mpelelezi.



"Karibu kijana!"



SP alimkaribisha, Jona akaenda kuketi baada ya salamu za hapa na pale na kujitambulisha kama Insp mpelelezi akaanza kumhoji maswali juu ya kutoroka kwa mfungwa huyo.



"Unasema milango haikuvunjwa, sasa Mheshimiwa unaweza kunambia huyu mfungwa alipitia wapi? au kuna alomtorosha?"



Jona alimtupia swali mkuu wa gereza macho yake ya kipelelezi akiwa kayakaza kumwangalia mzee yule ambaye hakukuwa na mtuhumiwa ambaye aliweza kutoroka katika gereza lile katika kipindi chote cha uongozi wake zaidi ya GAMBI kwa Mara ya pili sasa



Hata swali aliloulizwa hakuwa na jibu kwani mbinu alizotumia Gambi kutoroka yeye binafsi akuzijua zaidi ya kupata habari kuwa mwanaume katoroka na kusababisha mauaji ya wanajeshi wawili kivipi?!



Hilo hakulijua na yeye kama mkuu wa magereza aliitajika awe na maelezo yaliyojitosheleza!



Ilibidi Jona aende kuziona maiti zile huko zilikohifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi



Hawakuwa hata na jeraha!!



"Mh, shabash! ni nini kinachoendelea hapa? Mungu wangu!"



Jona alijiuliza. Kisha hapo akatoka na kurudi kwa Mkuu wake Kipara na kumuelezea ugumu wa kesi hiyo kwa jinsi alivyoiona mpaka hapo,



jinsi ilivyojaa utata na alishahisi bila shaka kuna wasaliti jeshini.

Aliapa kulivalia njuga kesi hiyo, kilichomuumiza kichwa ni juu ya kutoroka kwa Lau.



Akahisi katika maiti wale wawili kuna mmoja au wote aliwahadaa wakamtoa nje kisha akawauwa.



“Lakini ni kwa vipi na Gereza lile lina ulinzi mkali?” aliendelea kuwaza pasina majibu sahii



§§§§§



KATIKA IKULU ya nchi hiyo kikao cha watu watatu kikiongozwa na Rais wa mapinduzi Nyoshi, kati ya wajumbe akiwapo Mkuu wa upelelezi Brown Stanley na Waziri Mkuu.



Rais Laizer alitaka kujua walipofikia juu ya msako wa Mfungwa aliyetoroka



“Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu napenda kuiwasilisha taarifa hiyo kwa njia ya maandishi na kuifafanua kwa njia ya sauti,

Msako bado unaendelea na kesi ipo mkononi mwa kijana mchapakazi Jonathan japo amekiri kesi ni ngumu na yenye utata kwa jinsi alivyoiona haraka haraka, lakini ameapa kumtia nguvuni, na jeshi letu likiongozwa na Luteni Kanali Johnson bado lipo katika msitu mnene wa Lwana kwa msako mkali, inaaminika kakimbilia huko si ndo msitu ulioko karibu na gereza lile?"



alimalizia Brown akasimama na kusaluti akaikabidhi ripoti kwa waziri mkuu aloipitia naye akamkabidh rais wake naye aliisoma akatingisha kichwa kuafikiana na kilicho andikwa naye akafungua mdomo kusema machache.



"Itifaki imezingatiwa, tukiachana na hayo ni vizuri na inahitajika Gambi atiwe nguvuni haraka sana, na ikiwezekana auwawe kama tekelezo la hukumu yake ili kusiwepo na kizuizi katika uongozi wetu; si unajua yule atataka kulipiza kisasi kwa ajili ya wazazi wake! Kwa kuwa yeye pia ni mwanajeshi mbinu zote hatarishi anazo....."



Rais alieleza mjadala ukaendelea

Muda wote waziri mkuu alikuwa katika mawazo mazito na ghafla akaufungua mdomo wake!



"Nina shauri mkuu!"



Wote wakategaasikio kusikiliza



"Kwa inavyo onesha huyu Gambi ni tishio la taifa! Hasa kwetu sisi hofu yangu je jona kama mnavyomwita ataweza kupambana?! Na kumtia nguvuni na kwa nini asirejeshwe Komandoo Zidu toka Tanzania aje amuadibishe!"



Wote wakapigwa na butwaa,



Mshangao ukawavaa



Brown ambaye pia ni rafiki yake Mkubwa Zidu akaufungua mdomo wake!



" kwanza tutakuwa tunamdhihaki Gambi kafanya kazi kubwa sana mpaka sasa tupo hapa ni juhudi zake,tumuache Tanzania apumzike kwanza hata



GAMBI ni mwanajeshi mdogo sana ambaye kutokana na mafunzo aloyapata sina shaka naye



Hivyo tusimsumbue Zidu yule ni roho ya taifa,kazi zilizo shindikana ndo anapewa yeye ili la kumwangamiza GAMBI alijashindikana bado!"



Akamalizia Brown Stanley na wote wakaunga mkono! Swala lile

masaa kadhaa mbele kikao kikafungwa wakikubaliana Jonathan afatilie swala hilo.



§§§§§



Kambi ya jeshi Isonga ilikuwa kilomita chache upande wa mashariki kutoka katika msitu wa Lwana,



Gari la kijeshi, Gambi akiwa ndani yake liliingia na kuegeshwa mahala pake.



Wanajeshi walikuwa wakiendelea na shughuli zao za kawaida, wale wa tatu wakashuka kutoka katika lile gari.



Gambi kwa kutumia pembe ya jicho akichungulia, alipoona kila mtu anaendelea na yake kwa sekunde chache akaruka na kuingia chini ya gari lile na kutulia tuli akisubiri muda muafaka wa kutoka kule chini!



Giza kwa mbali lilianza kuingia, ndio muda alouhitaji



'Lazima niondoke eneo hili kwani si salama'



aliwaza



Hakujua atatoka kwa njia gani katika kambi hiyo ya jeshi ilikuwa ni kama kajiingiza mwenyewe katika mdomo wa mamba akitegemea kusalimika!



Kweli?!



Giza lilishika hatamu eneo lile wanajeshi wachache walikuwa nje ila wengi walikuwa kwenye mabweni yao iyo ndo ilikuwa nafasi ya pekee ya gambi kutoka eneo hilo alitoka chini ya gari lile na kuanza kuambaa na ukuta



“Nyoosha mikono yako juu, tupa silaha yako chini?”



ilikuwa ni amri iliyoingia mpaka katika ngoma ya masikio yake

Gambi hakuwa tayari kwa hilo alijigeuza haraka na teke kali lililotua katikati ya kifua cha adui na kumpeleka chini.



Gambi hakumpa muda zaidi alimfikia na kuikunja shingo yake na huo ndo ukawa mwisho wa mwanajeshi Yule kiherehere alojipeleka mzima mzima



Alipoangalia pembeni aliona shimo limefunikwa la kupitishia maji taka bila kuwaza zaidi alizivua nguo zile alizovaa za wanajeshi wa magereza akavaa zile za yule mwanajeshi akamburuza baada ya kufanikiwa kufunua mfuniko wa shimo lile akamtumbukiza ndani yake



hakukuwa na mtu aliyeshuhudia kitendo kile akiwa kama wanajeshi wa kambi ile akaanza kuondoka kuelekea getini hakuna aliye mtilia

Atatokaje pale getini?!



Hili ndilo swala lililomuumiza kichwa kwa wakati huo!







Gambi hakumpa muda zaidi alimfikia na kuikunja shingo yake na huo ndo ukawa mwisho wa mwanajeshi Yule.



Alipoangalia pembeni aliona shimo limefunikwa la kupitishia maji taka bila kuwaza zaidi alizivua nguo zile alizovaa za wanajeshi wa magereza akavaa zile za yule mwanajeshi akamburuza baada ya kufanikiwa kufunua mfuniko wa shimo lile akamtumbukiza


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog