Search This Blog

Thursday 29 December 2022

CODE X 5 N.G.S.S. (NEXT GENERATION SUPER SOLDIERS) - 1

  

Simulizi : Code X 5 N.g.s.s. (Next Generation Super Soldiers)

Sehemu Ya Kwanza (1)


"General Alex na Supreme Commando Jeff, tunawaomba mtoke nje. Nyumba nzima imezungukwa na vikosi vya wanajeshi wanaosubiria amri ya kushambulia. Hivyo kukaidi amri si jambo jema kabisa" sauti inasikika kutoka kwenye kipaza sauti nje ya nyumba ya Jeff. Alex na Jeff wakatoka nje mikono yao ikiwa juu wakiashiria kusalimu amri. Wanajeshi zaidi ya thalathini wakawasogelea huku midomo ya mitutut ikiwaelekekea na vidole vikiwa kwenye sehemu ya kufyatulia risasi.


"Jeff naona huu ndio mwisho wetu" General Alex akaongea, "kabisa, hatuna haja ya kupamba, tuiache sheria ifuate mkondo wake" Jeff akajibu na wote wawili wakapiga magoti na kuweka mikono nyuma ya vichwa vyao. "Malejendari hawa" akafika mtu mmoja aliekuwa ndani ya gwanda za kijenerali, "nilijuwa tu wewe ndio utakuwa nyuma ya jambo hili" General Alex akaongea. "Taratibu General, hawa unaowaona hapa wanasubiria amri tu wafyatue risasi" General Alfonse akaongea.


"Mkuu, ndani hakuna mtu mwengine" wanajeshi walioingia ndani kwa ajili ya ukaguzi wakarudi na kutoa taarifa. "Naomba munieleze vikosi vyenu viko wapi" General Alfonse akawageukia na kuongea. "Umechelewa sana Alfonse, vikosi vyangu vyote vimerudi chini ya raisi hivyo kuvipata sahau" Jeff akainuwa sura na kuongea. Gen Alfonse akakunja sura kwa hasira, "na kama unavyojuwa mimi nimestaafu na sina hata mtu mmoja aliekuwa chini yangu" Gen Alex akaongea.


"Sawa, kazi yangu basi itakuwa rahisi sana sasa, Mimi ni Gen Alfonse wa kikosi kazi maalum CIG (Crime Investigating Gorrillas). Kazi ilotuleta hapa imekamilika" akaongea kupiti kifaa maaluma, wanajeshi wakaanza kujikusanya. Ndege maalum za kivita zikatuwa eneo hilo. Gen. Alex na Sup Com Jeff wakafungwa pingu na kuingizwa ndani ya ndege kisha kikosi hicho kikatoweka eneo hilo.




Kitendo cha kuusukuma tu mlango walianza kushambuliwa kwa vurugu, “nilijuwa tu watakuwa wanatusubiri kwenye hiii koridoo” aliongea Jeff. Akaingiza mkono kwenye pochi alioichukuwa kutoka kwa zile maiti za wanajeshi na kutowa bomu la mwanga. Akalibonyeza juu na kulirusha, sekunde chache lile bomu likaripukana kuachia mwanga mkali sana uliowapofuwa kwa muda wale wanajeshi waliokuwa kwenye ile koridoo. Hapo sasa ikaanza kusikika milio ya bunduki iliofuatiwa na viliyo vya maumivu, na risasi wala hazikupigwa kwa fujo, ilikuwa ikitoka moja moja. Kila bunduki ilivyokohoa ndivyo yowe moja lilivyosikika. “Kazi nzuri partner” aliongea Alex, “hawa wala hawatii hamsha hamsha” aliongea Jeff na kurudisha bunduki ya mgongoni baada ya kuwamaliza wote kwenye koridoo hiyo, ndio yote hiyo ilikuwa ni kazi ya mtu na si mwingine bali na GHOST, hutamuona akija bali utahisi baridi akikupita.


“Ah! Wanaofata ni wa kwagu” aliongea Alex na kwa pamoja wakaanza kulekea mlango wa kutokea kwenye koridoo hiyo. “Hapo ndio mwisho wenu, huwo mlango unafungulia na nambari maalum za siri” ilisikika sauti kutoka kwenye spika zilzokuwepo eneo hilo. “Hivi unadhani tumefika katika vyeo unavyovisikia leo kwa bahati mbaya au” aliongea Alex kwa nguvu na Luteni jenerali Davidson akasikia. “Baada ya sekunde thalathini koridoo nzima hiyo itajaa gesi ya sumu” aliongea Lut jenerali Davidson. Alex akatabasamu na kusogea sehemu ya kuweka zile namba za siri kisha akafunga macho kwa sekunde kama kumi hivi “ti te ta too” sauti hizo zilijirudia kichwani mwake, akashusha pumzi na kubonyeza nambara zote kwa haraka sana ili kugunduwa mlio kwa kila namba.


Baada ya hapo akafuta ile milio na kubonyeza nambari ambazo milio yake iliendana na ile iliokuwa ikilia kichwani mwake “kwacha!” sauti hiyo ilisikika na loki za mlango huwo zikatoka na ukafunguka. “Siku ya pili musinifunge pingu tu, nizibeni na masikio” aliongea na kuonesha kidole cha kati kwenye kamera ya karibu. Lahaula! Kutoka tu wakakutana na jopo la wafungwa likiwasubiri, kila mtu alikuwa na silaha aliohisi itamfaa. “Pigania uhuru wako, ukimuuwa hata mmoja utaondoka humu” ilisikika sauti ya Luteni jenerali Davidson.


“Hivi munadhani mutaishi kutoka humu ndani, nawapa nafasi tu. Unganeni na sisi tutoke wote” aliongea Alex. “Nani aungane na nyie, kabisa munadhani kuwa mutatush…”, “shh! Wawili na nani?” alikatizwa na Alex. “Si wewe na mwenzako” aliongea yule alieongea mwanzo, “Kuwa na heshima bwana mdogo, nyinyi wote mutapambana na mimi. Yule muacheni tu maana tumekubaliana kuwa atakae kuja mbele yetu ni mali yangu” aliongea Alex na kutoa bunduki yake iliokuwa inaning’nia mgongoni na kumrushia Jeff. Aliidaka na kukaa kwenye kiti kimoja wapo kati ya viti vilivyokuwepo eneo hilo.


Wale jamaa wakacheka sana, Alex wala hakuwashughulikia. Alivua shati alilokuwa amevaana kuana kunyoosha misuli ilioanza kudata kutoka na kukosa kunyooshwa muda mrefu. Usoni alionekana kuanza kuzeeka lakini mwili wake ulikuwa ni kama kijana wa miaka thalathini hivi tena mwenye kufanya mazoezi ya kubeba vitu vizito. Kila msuli ulikuwa umekaa eneo stahiki, “KILLER” ni neno lilisomeka katika upande wa kulia wa kifuwa chake kilichojaa vilivyo. Alipohakikisha kuwa kila kitu kipo sawa baada ya kujinyoosha akawaangalia na kutabasamu. “Partner dakika tano tu” aliongea Jeff, “Tatu tu zinatosha, sijaona mtu wa kunitowa jasho hapa” Alex alijibu.


Jeff akachukuwa saa alioichukuwa kutoka kwa moja zile maiti na kuweka sehemu ya stop watch, akabonyeza na uliposikika mlio tu. Alex akafyetuka kama mshale kutoka kwenye upinde na kuwavamia, masikini hawakujuwa kiumbe huyo si binadamu wa kawaida. Kwa msaada kemikali iliokuwemo mwilini mwake, kasi yake ilikuwa mara dufu ile ya binadamu wa kawaida. Kila ngumu iliotuwa mwilini mwa mtu, ilifuatiwa na mlio wa mfupa kuvunjika. Aliporudisha ngumi lilisafiri teke na kushambulia, vilisikika vilio tu na mayowe ya maumivi pamoja na sauti za mifupa kuvunjika.


“Tafadhali nisamehe” ilisikika sauti ya mtu mmoja akiomba msamaha, alikuwa amebakia peke yake. “Nilikupa nafasi ukadhani nacheza, huwa sina tabia ya kumpa mtu nafasi mara ya pili.” Alikunja ngumi za mikono miwili na kuzishusha kwa wakati mmoja. Ngumi hizo zilituwa pande zote mbili kwenye kichwa juu ya masikio. Damu ziliruka kutokea puwani na mdomoni, alianguka na kupoteza maisha, “sekunde mbili na sekunde hamsini na tisa” aliongea Jeff na kusimama.


“Mi nilidhani watanipa angalau changamoto lakini hamna kitu” aliongea Alex na kuonekana kuchukizwa na watu kuwa dhaifu sana. “We dogo! Hakuna wengine angalau wenye uwezo kidogo maana hata jasho sijatoka. Kama hakuna acha kutupotezea muda, jitokeze nikuue niondoke humu. Nimechoka kuka kwenye hili danguro” aliendelea kuongea na alionekana kuwa na hasira kupita maelezo. Mwili wake ulikuwa umevimba mara mbili ya awali.

*******************************************************

“Hivi huyu ni binaadamu kweli” aliongea Luteni jenerali Davidson, “ulitegemea nini kutoka kwa mtu aloichezesha Marekani ngoma aliotaka yeye” alijibu jenerali Alfonse. “Hao wote wawili walishakwenda kuzimu na kurudi, ni miongoni mwa watu wanaotambulika kukitoraka kifo katika hatuwa za mwisho” aliendelea. “Kilichobaki hapa ni kutoroka tu, hatuwezi kupambana nao kwa sasa.”.

“Hapana ni lazima niwaue hawa wapuuzi”

“Davidson, huwezi kusimama hata kwa dakika moja mbele yao”

“Kwanini nisiweze?”

“Matvei ameanguka kwa mkono wa Jeff na Jenerali David ameanguka kwa mkono wa Alex. Ngoja nikuambie hasa vyeo vyao, Jeff ni Supreme general commando na Alex ni Gold Prime General. Kwa majina mengine wanajulikana; Jeff ni Supreme General Commando Ghost na Alex ni Gold Prime General Killer. Hata maraisi wa nchi zao wanawaheshimu kupita maelezo.”.


Vinyweleo vyote vilimsimama Luteni Jenerali Davidson na damu ikapowa ghafla. Alihisi mpaka moyo wake ukitaka kusimama. Aliwahi tu kusikia vyei hivyo vipo lakini hakutegemea hasa kama kutakuwa kuna watu ambao wanavimiliki. Kwa sekunde kadha alihisi ubonge wake kuwa mwepe kama wa mtoto mchanga aliezaliwa leo. Supreme General Commando Ghost, Gold Prime General Killer, majina hayo yalijirudia mara kadhaa kichwani mwake.


“Davidson” alishtuliwa na sauti jenerali Alfonse na ndio mawazo yake yakakaa sawa na ubongo ukarudi katika ya kawaida. “Kwanini hukunambia mapema, tumefanya kosa kubwa sana kuwaleta huku” aliongea Lut jen Davidson. “Kwani umesahau mpango kutoka kwa wakubwa wetu” aliongea jenerali Alfonse, “Sijasahau lakini tumewachukulia kiurahisi sana hawa” aliongea. “Hapana, kwa kuwachukuwa hawa. Kikosi kazi kitaondoka kambini kuja kuwaokowa. Wakifanya hivyo watu wetu watavamia kambi yao na kuiweka chini ya ulinzi” alifafanuwa.


Wakati wao wakindelea kuwekana sawa, Jeff na Alex walizidi kuwasambaratisha wtu huko walipo na kuzidi kusonga mbele. “Alex mi naungana na wewe, hawa wajinga dhaifu sana. Kweli walitegemea kufanya mapinduzi na wanajeshi wa aina hii. Hata kama tungeamuwa tusiingilie basi wangezuiwa na wanajeshi wa kawaida tu” aliongea Jeff. “Tumekuja kupoteza muda tu huku, la maana kubwa tulolifanya ni kunyonya taarifa tu” alijibu Alex baada ya kumvunja mtu. Wakati huwo wote wawili hawakuwa na mashati. Kila mmoja mgongoni alikuwa na maneno yaliosemeka “DANGEROUS DUO” (Wawili hatari). Ghost ilisomeka upande wa kulia wa kifuwa cha Jeff na Killer kwa Alex.

********************************************************

“Ndio, tumeshuhudia ndege nyingi zikiondoka kambini kwao” alitoa taarifa mwanajeshi aliekuwa akiichunguza kambi ya kina Jeff. “Sawa, chukuwa wanajeshi niliokupa na uende kushambulia, hakikisha unauwa kila aliokuwemo katika kambi hiyo isipokuwa watatu tu. Martina, Janeth na Talbot hawa nawahitaji wakiwa hai” aliongea mwanamke aliepewa taarifa hiyo. “Nahofia kama yule mwenda wazimu atakuwepo” aliongea alietoa taarifa, “Charlie! Ah, hawezi kubakia na kuacha utamu wote waupate wengine. Yule ni kama kichaa na anapenda sana kuuwa. Pia hawezi kutulia ikiwa Jeff atakuwa anahatarisha maisha yake. Hivyo usijali kabisa Frank” alifafanuwa mwanamke huyo.


Frank alitikisa kichwa na kuondoka, alichukuwa kikosi alichobakia na kuelekea ilipo Sector Zero Ghost Layer. Kikosi hicho kilikuwa na wanajeshi zaidi ya mia tatu waliopewa mafunzo maalum kwa ajili siku hiyo tu, na mipango yote ilikuwa inakwenda kama waasi walivyopanga. “Tayari kikosi kazi chetu kiko njiani kuelekea Sector Zero Ghost Layer, kesho usiku ile kambi itakuwa chini yetu Michael” alifikisha taarifa hiyo kwa kiongozi mkuu wa waasi ambae yeye tu ndie anaemjuwa kwa sura. “Kabisa Alice” aliitika Michael kisha akaendelea “tuone ukirudi utafikia wapi, nyumba yako itakuwa yangu na kila kitu chake ndani, Jeff.” Kisha akacheka kwa nguvu.



Frank alitikisa kichwa na kuondoka, alichukuwa kikosi alichobakia na kuelekea ilipo Sector Zero Ghost Layer. Kikosi hicho kilikuwa na wanajeshi zaidi ya mia tatu waliopewa mafunzo maalum kwa ajili siku hiyo tu, na mipango yote ilikuwa inakwenda kama waasi walivyopanga. “Tayari kikosi kazi chetu kiko njiani kuelekea Sector Zero Ghost Layer, kesho usiku ile kambi itakuwa chini yetu Michael” alifikisha taarifa hiyo kwa kiongozi mkuu wa waasi ambae yeye tu ndie anaemjuwa kwa sura. “Kabisa Alice” aliitika Michael kisha akaendelea “tuone ukirudi utafikia wapi, nyumba yako itakuwa yangu na kila kitu chake ndani, Jeff.” Kisha akacheka kwa nguvu.


Purukushani ziliendelea upande wa kina Jeff, kikosi cha waasi kilichokuwa pasifiki kilijikuta katika wakati mgumu sana kupambana mashujaa hao wa vita. Milio ya bunduki ilirindima kisawasawa, Alex na Jeff walikuwa wakibadilisha bunduki tu, “Chumba kile pale ndicho walichokuwepo wale wapuuzi wawili” aliongea na kusogea kwenye mlango kisha akajibanza ukutani. Akamfanyia Jeff ajaribu kufunguwa mlango, na jambo zuri ni kwamba mlango haukuwa umelokiwa.


Ulipofunguka tu Alex alibiringitia moja kwa moja mdomo wake bastola ukamuelekea jeneali Alfonse, “tulia hivyo hivyo” alifoka. Jenerali hakuwa na lakufanya alisimama kama nambari moja, “hivyo ndivyo unavyomaliza vita” alisikia sauti kutokea nyuma yake ikifuatiwa na kiti cha baridi kugusa kisogoni kwake. Hakuwa mwengine isipokuwa luteni jenerali Davidson, “Umesahau kama tupo wawili” na yeye akasikia sauti nyuma. “Sawa mimi nitakufa lakini na Alex atakufa, je uko tayari kumpoteza partner wako?” aliuliza.


“Hahaha!” alisikika jenerali Alfonse akicheka kwa dharau, “kwanza niwasifu kwa kuangamiza kikosi chetu kizima cha hapa lakini nasikitika kusema kuwa huu ndio mwisho. Hamtaishi kuliona juwa tena na taratibu watawasahau na kuendelea na maisha kama vile hamkuwahi kutokea” aliendelea. “Sisi hatuna haja ya kukumbukwa na mtu, lakini najuwa kabisa nyinyi waasi hamtatusahau hata tukifa leo” alijibu Alex. “Davidson wewe mmalize Jeff, mimi namaliza huyu kunguru” alitoa amri jenerali Alfonse.


“Nasikitika hilo halitawezekana jenerali Alfonse” aliongea Luteni jeneral Davidson, “Unaona bwana mkubwa, kuna kauli zinasema mchawi mpe mtoto wako amlee” aliongea na kuzidi kumchanganya jenerali Alfonse. “unamaanisha nini, Davidson” aliuliza.

“Kwanza nakukosoa, jina langu si Davidson na cheo changu sio Luteni jenerali”

“Unasema nini wewe?”

“Jina langu halisi ni Jason CJ Juniour, cheo changu ni Prime General. Au najulikana kama Prime General Shadow” alijitambulisha aliekuwa akijulikana Luteni Jeneral Davidson.


“Soldier, huwoni kama ni kosa kumuekea mkuu wako bastola kichwani” aliongea kwa nguvu, Jason CJ Jr akarudi nyuma na kufunga mguu. “Prime General Shadow reporting for duty” aliongea, “Jason, kamilisha kazi yako” aliongea Alex. Jason akamgeukia Jenerali Alfonse kumtandika shaba ya kichwa iliosambaratisha ubongo. “Mmoja tayari, wamebakia watano” aliongea Jason na kupiga saluti, Alex aliipokea kwa tabasamu zito kisha akafunguwa mikono. Jason alimsogelea na kumkumbatia, “natumai mama ako huko alipo anafurahia kazi ya mwanae kuendeleza kile alichokiacha yeye” aliongea Alex machozi yakimchuruzika.


“Baba acha kulia, unajitia aibu mbele komando” aliongea Jason, “Ah! Acha tu nilie kijana wangu, hujui ni kiasi nilikuwa nikisagika moyoni kwa kufahamu nimekupeleka kwenye moto mkali sana wa waasi” aliongea Alex kisha wakaachiana. “Kama tulivyokubaliana, ukikamilisa kazi hii nitakuonyesha picha ya mamaako” aliongea Alex, “tukirudi kambini nitakupa” alimaliza. “Ohaaa! Mbona mimi sielewi, mumeniacha kwenye mataa” walisikia sauti ya Jeff. “Ah! Partner kwanza naomba samahani kwa kukuficha juu ya hili, huyu unaemuona hapa ambae ulikuwa ukimtambuwa kama Luteni jenerali Davidson ni mtoto wangu wa pekee Jason CJ Jr.”. “Mpaka hapo nishajuwa, niachotaka kujuwa ametokea wapi na kwanini yumo humu ndani” aliongea Jeff. “Ni hadithi ndefu lakini nitakwambia kila kitu tukiwa kambini, kwasasa tupumzike tumuache Charlie afanye kazi yake.” Alijibu Alexna kuvuta kiti na kukaa.

**************************************************

Alice aliingia chumba cha Michael akihema, “tumetegwa” aliongea. “Kivipi?” aliuliza Michael, “tumekuwaa na mpelelezi ndani ya kambi zetu kwa muda wa miaka miwili sasa, Jason CJ Juniour. Ambae aliingia hapa kambini kama Luteni jenerali Davidson, ila sivyo na cheo chake ni Prime General katika medani za kivita anajulikana kama Prime General Shadow. Anachukuwa amri zake moja kwa moja kutoka kwa Gold Prime General ambae ni Alex. “Mi nilimwambia jenerali Alfonse awe makini na watu anaowateuwa kumsaidia lakini akajifanya anajuwa sana.” Aliongea na kuonekana kukerwa sana. “Mwambie Frank arudi na kikosi kizima, kazi imeghairishwa”, “hilo haliwezekani, wameshaingia kwenye non-communication zone (sehemu ambayo mawasiliano hakuna)” alijibu Alice na kukaa kwenye kiti akihisi kuishiwa nguvu.


Sector Zero Ghost Layer

Mita mia sita kutoka kwenye kambi hiyo, kikosi kazi kikiongozwa na Frank kilikuwa kikisonga mbele kwa umakini wa hali ya juu sana. Tayari walikuwa mita mia nne ndani ya eneo ambalo mawasiliano kutoka nje yote yalikuwa yamekatwa. Walikuwa gizani bla kujuwa kinachoendelea, wakiwa katika hali hiyo wakaanza kusikia milio ya ndege. Kadiri sekunde zilivyokatika, milio hiyo ilizidi kuwa mikubwa. “Mumeingia katika eneo lisilowahusu, mimi ni Supreme Commando Beast na hili ni eneo langu. Na kutoakana na sheria za Sector Zero Ghost Layer, yeyote atakaechanganya ambae hahusiki huku na kitoweyo changu” aliongea Charlie kupitia kifaa cha mawasiliano.


“Ndege zote zitashambulia kutoka na amri yangu, Shambulia” aliongea na kutoa amri papo kwa papo. Moto ukawashwa eneo hilo, milio ya bunduki ilisikika na damu zilisambaa eneo lote hilo. Baada ya dakika tano za mashambulizi hatimae milio ikanyamaza, wakashuka wanajeshi kadhaa na kukaguwa. “Kazi imekwisha” aliongea mmoja wao, wakarudi kwenye ndege na kuondoka eneo hilo. Baada ya hapo ikapita ndege nyingine na kumwaga mafuta na kwasababu moto wa uliowashwa na risasi bado ulikuwepo. Ukazidi kuwa mkali na kuchoma miili yote ya maiti zilizokuwepo eneo hilo.


Bahari ya Pasifiki.

Ndege nne ndogo na moja kubwa zilikuwa zikiikaribia ile meli ya waasi, na kwasababu kambi hiyo ndani ilishasambaritishwa mfumo wa ulinzi nao ulikuwa umezimwa. Alex, Jeff pamoja na Jason walikuwa juu juu wakisubiria usafiri wao. Ile ndege kubwa ilituwa kwenye uwanja uliokuwepo juu ya meli hiyo, Alfred akashuka na kupiga saluti. Jeff aliipokea na kutabasamu, Alfred alitaka kuongea kitu baada ya kumuona Jason lakini Jeff akamfinyia jicho asifanye hivyo. Alitabasamu na kuwapa ishara wapande, wote wakafuatana na kuingia kwenye ndege hiyo kubwa. “Kuna watu bado, tumewafunga kwenye chumba chekundu. Ndege mbili zitabakia mpaka kitapofika kikosi cha Alex, The Pirates, watawachukuwa na ndege zetu zitarudi kambini.” Aliongea Jeff na Albert akachaguwa ndege mbili kubakia eneo hilo.


Ikifuatana ndege ndogo mbili, ile ndege kubwa ikapotelea angani na safari ya kurudi Sector Zero Ghost Layer ikaanza. Kila mmoja alikuwa kimya ndani humo, Alfred aliwasha mziki laini uliowapoza magwiji hao na kusahau kwa muda kasheshe waliokuwa wakimbana nayo. Safari hiyo ilendelea kwa masaa mawili na hatimae ndege hizo zikawasili kambini. “Karibuni nyumbani” aliongea Martina, “tumekaribia” alijibu Jeff. “Ila Jeff ulichokifanya sicho, wewe utaniachaje huku ukaenda kufurahia peke yako huko” aliongea Charlie na kutabasamu. “Ah! Wala hakukuwa na furaha, wametupotezea muda tu. Jambo ambali lina faida katika kazi hii ni hizo taarifa tulizokusanya na si jingine. Pia mi nilidhani huku utakula utamu wote, kwani hawajakuchemsha damu hata kidogo” aliongea na kuuliza Jeff.


“Ah! Bora hata ningelala tu kuliko kwenda huko nje kuwasubiri watu ambao hata sura zao sikuziona” alisikitika sana Charlie. “Huyo mpuuzi anafanya nini huku” aliuliza Talbot baada ya kumuona Jason akishuka. “Ni hadithi ndefu ila huyo si adui yetu, Alex atatueleza vizuri baada ya mapuziko. Tunahitaji kuoga maana tokea tufike kula hatujaoga zaidi ya kunawa uso tu” alionea Jeff na kuelekea chumbani kwake.



“Ah! Bora hata ningelala tu kuliko kwenda huko nje kuwasubiri watu ambao hata sura zao sikuziona” alisikitika sana Charlie. “Huyo mpuuzi anafanya nini huku” aliuliza Talbot baada ya kumuona Jason akishuka. “Ni hadithi ndefu ila huyo si adui yetu, Alex atatueleza vizuri baada ya mapuziko. Tunahitaji kuoga maana tokea tufike kula hatujaoga zaidi ya kunawa uso tu” alionea Jeff na kuelekea chumbani kwake.

*******************************************

Miaka mitatu iliopita.

“Mkuu, kuna mtu anataka kukuona” Alex akiwa makao makuu ya jeshi, aliingia mtu na kumpa taarifa. “mwambie apite” alijibu na kuendelea alichokuwa anafanya, “habari ya saa hizi mkuu” aliingia yule mtu na kupiga saluti. “Nzuri, karibu ukae” aliongea na kuonesha mkono wake wa kulia kilipo kiti, yule jamaa alieingia, alishusha mkoba wake na kukaa kwenye kiti. Wakati wote huwo Alex hakumuangalia usoni mtu huyo, alikuwa ameshughulika na jambo fulani. Alipoliweka sawa ndipo akainuwa uso na kumuangalia, ghafla mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda kasi na kijasho chembamba kikaanza kumtoka.


“Mkuu” alishtushwa na sauti ya kijana alieingia, ndipo akazinduka kutoka kwenye mshangao wake. “E..h nikusaidie nini” alibabaika kidogo, “jina langu ni Jason CJ Juniour” alijitambulisha. Jina hilo lilizidi kumchanganya Alex, “nimeambiwa na Dr Nolan nikutafute ili niweze kupata majibu ya maswali yangu” aliongea Jason. “Dr Nolan” Alex alilirudia jina akijaribu kukumbuka ni wapi amelisikia, kwasababu lilionesha kugonga akilini mwake. “Dr Nolan wa hospitali St. Francisi Anamaria?” aliuliza, “ndio” alijibu Jason.


“Sawa Jason, ni maswali gani unahitaji majibu?” aliuliza tena, “niite CJ tu, inatosha” aliongea na kuendelea “nimelelewa kituo cha watoto yatima mpaka nilipofikisha miaka kumi na nane ndipo Dr Nolan ambae alikuwa kama mlezi kwangu alikuja na kunipa taarifa zako. Nilipomuuliza sababu, akaniambia nahitaji kukuuliza wewe sababu za yeye kunipa taarifa zako. Nilipomuuliza wewe ni nani kwangu, akanijibu kuwa ni baba yangu mzazi. Nilijaribu sana kutafuta uwezekano wa kuongea na wewe lakini ikashindikana, ndipo nikajiunga na jeshi nikiwa na miaka kumi na tisa.” Alinyamza kidogo na kuvuta pumzi.


“Hata hivyo haikuwezekana pia kuonana na wewe kutokana na utofauti wa vyeo na majukumu, na nliposikia kuwa wewe ndio Prime General nikaona njia pekee ya kukufikia ni kupanda vyeo na sasa mimi jenerali. Na ndio nimepata wasaa wa kuonana na wewe uso uso kwa uso, sasa maswali yangu ni mawili tu. Je ulikuwa unajuwa kama una mtoto na la pili mama yangu ni nani.” Ni kama alikuwa ametupa jiba kubwa moyoni kwa Alex na kutonesha kidonda ambacho kilivaa ngozi y kupona lakini ndani kilikuwa bado kibichi na kinavuja damu.


“Nitakujibu swali la kwanza tu kwa sasa, la pili inabidi tutoke mimi na wewe mpaka kwa Dr Nolan ili anifafanulie na ndipo nitakujibu.” Aliongea Alex na CJ akatikisha kichwa kuashiria kukubaliana nae. “Nilikuwa sifahamu kabisa kama nina mtoto, na kama sio kufanana na mama ako wala nisingekaa nikakusikiliza, labda ningekuwa nishakupiga risasi” aliongea na kuachia tabasamu. Gold Prime General Alex, miaka sitini lakini kama mtu miaka arobaini na kidogo. “Kwasababu kuna mambo mengi sana nataka kuyajuwa kutoka kwa Dr Nolan, ningeshauri tuelekee huko sasa hivi” aliongea Alex na kusimama.


“Dr Nolan kwa sasa ameshastaafu na yupo Denmark na familia yake, labda tuondoke kesho ila kwa leo sidhani kama tutawahi” Alijibu CJ. “Tutawahi, niambie anakaa mji gani tu”, “mjii mkuu, Copenhagen” alijibu CJ. Alex akanyanyua simu na kuongea kisha akampa ishara CJ amfuate, wakatoka ndani ya ofisi hiyo moja kwa moja mpaka kwenye gari iliokuwa inamsubiri. Waliingia kwenye gari na safari ikaanza, walielekea uwanja wa ndege wa kijeshi ambako ndege maalum ilikuwa ikiwasubiri. Waliingia na safari ya kuelekea Denmark ikaanza.


Copenhagen, Denmark saa chache baadae.

Walifikia katika hoteli ambayo iliandaliwa mapema sana wakiwa angani, walioga na kubadilisha nguo kisha wakapata chakula cha usiku. Japo waliondoka mchana Marekani, waliwasili mjini Copenhagen, Denmark usiku kutoka na saa kati nchi hizo mbili kupishana takriban kwa saa sita. Denmark iko mbele kwa saa sita, ikiwa Marekani ni saa tatu asubui basi Denmark ni saa tisa jioni. Na kwakuwa waliingia nchini humo usiku walipumzika ili siku ya pili mapema sana wakaonane na Dr Nolan.


Siku iliofuata waliilekea nyumbani kwa Dr Nolan ambako walimkuta akiwasubiri kwa hamu, CJ alimtaarifu ujio wao usiku walipofika tu Denmark. “Karibuni sana” aliongea, “ahsante” walijibu kwa pamoja wakiwa wamekaa kwenye makochi. “Alex, bado uko vizuri. Miaka yote hii tulioachana na bado unaonekana kama ndio umeanza kuzeeka” aliongea Dr Nolan. “Ni mazoezi tu ila nishazeeka ndani” alijbu Alex na wote wakacheka, “naona Jason umekuwa sana, na sasa ni jenerali kama sikosei. Kweli ullimwengu unabadilika, tufanye tena sisi wazee tuondoke tuwaachie vijana waendelee kutamba”.


“Najuwa Alex una maswali mengi sana, ulivyokuwa unaamini sivyo na unawaza ilikuwaje. Usijali nitakueleza kila kitu na naomba unisamehe ikiwa utakwazika” aliongea na kuendelea. “Miaka thalathini na moja iliopita, ulikuja na mpenzi wako hospitalini kwetu akiwa na hali mbaya sana. Wakati tunfanya uchunguz tukagunduwa kuwa alikuwa na mimba ya siku chache. Tuliongea nae na kumueleza hali aliyokuwa nayo, alilia sana alipojuwa kuwa anakupoteza wewe na hawezi kukuachia hata kumbukumbu. Ndipo nikamueleza kuwa tunaweza kumuokoa mtoto wake mtarajiwa kwa sababu kipindi hicho ndio nilikuwa nimetengeneza mashine ya kulea mimba changa kama yake lakini ilikuwa ni asilimia hamsini kwa hamsini”.


“Alikubaliana na hilo lakini aliniomba nisikwambie chochote kuhusu na jambo hilo, ili kusudi nisikupe matumaini ambayo hayakuwa na uhakika. Pia aliniomba hata likifanikiwa nisikwambie ili kukulinda kutoka kwa watu ambao wangemtumia mwanao kwa njia moja ama nyingine kukudhuru. Aliniambia pia nisimwambie mwanao chochote mpaka atakafikisha miaka kumi na nane ili afanya maamuzi binafsi kama ataamuwa kukutafuta au kuishi maisha yake bila uwepo wako. Kwa kweli alikupenda sana hakuwa tayari kuona janga lolote likikujia, alinifanya niape kuwa nitafanya yote alionambia. Nilikubaliana nae japo kwa shingo upande lakini nilielewa kusudi lake. Tulifanya operesheni ndogo kuondoa yai lilirutubishwa na kulihamishiwa kwenye mashine.” Alimalizia.


Machozi yalikuwa yakitiririka mashavuni mwa Alex, CJ alitaka kumgusa lakini Dr Nolan alimzuia. “Upendo wake haujapunguwa hata kidogo kwa mwanamke aliempenda, yuko kama siku aliokuja hospitali miaka mingi iliopita.” Alimwambia CJ. “Umenitoka na bado unanilinda, Rose. Laiti ningemjuwa mapema, nisingelimruhus aingie kwenye medani za kivita lakini sivyo. Endelea kutuangalia mpaka mwisho wetu” alijisemea mwenyewe kichwani mwake.


“Rose” alitamka jina hilo kwa nguvu kidogo, “Rose” CJ alilirudia. “Rose ndio jina mamaako, mwanamke mrembo, mwenye akili, nguvu na shujaa kuliko wanawake wote duniani” aliongea akitabasamu na mchozi yakiendelea kurowanisha mashavu yake. “Dr Nolan ahsante sana kwa kumuangalia mwanangu kwa kipindi chote ambacho sikuwepo kwa ajili yake. Sijui nikulipe nini?”, “umenipa kila ninachohitaji Alex, uwepo wako tu unayanufaisha maisha yangu na kuweka tabasamu usoni mwangu. Huwa napata amani na faraja moyoni ninaposikia duniani kuna Gold Prime General Alex ambae niliwahi kumhudumia kipindi ambacho hakuwa akitambulika kabisa. Hii ni hadithi nitaishi kuwasimulia wajukuu zangu na kuwasihi wawasimulie watoto wao na wawaambie kuwa katika ulimwengu ulojaa unyama, makosa na ushenzi wa aina zote, kuna watu wanaopigania haki na usawa na kuifanya dunia kuwa mahali pazuri pa kuishi” aliongea mzee huyo na kutabasamu, macho yake yalijaa machozi.”.



“Rose” alitamka jina hilo kwa nguvu kidogo, “Rose” CJ alilirudia. “Rose ndio jina mamaako, mwanamke mrembo, mwenye akili, nguvu na shujaa kuliko wanawake wote duniani” aliongea akitabasamu na mchozi yakiendelea kurowanisha mashavu yake. “Dr Nolan ahsante sana kwa kumuangalia mwanangu kwa kipindi chote ambacho sikuwepo kwa ajili yake. Sijui nikulipe nini?”, “umenipa kila ninachohitaji Alex, uwepo wako tu unayanufaisha maisha yangu na kuweka tabasamu usoni mwangu. Huwa napata amani na faraja moyoni ninaposikia duniani kuna Gold Prime General Alex ambae niliwahi kumhudumia kipindi ambacho hakuwa akitambulika kabisa. Hii ni hadithi nitaishi kuwasimulia wajukuu zangu na kuwasihi wawasimulie watoto wao na wawaambie kuwa katika ulimwengu ulojaa unyama, makosa na ushenzi wa aina zote, kuna watu wanaopigania haki na usawa na kuifanya dunia kuwa mahali pazuri pa kuishi” aliongea mzee huyo na kutabasamu, macho yake yalijaa machozi.”.

**************************************************

“Na hivyo ndivyo nilivyomjuwa mwanangu, Prime General Jason CJ Jr” alimalizia Alex, “Hilo moja, amewezaje kuwa katika vikosi vya waasi ni la pili” aliongea Jeff. “Nilitegemea swali kama hilo” aliongea Alex na kuendelea, “baada ya kujuana nilimhamisha kutoka kwenye kikosi alichokuwa anakitumikia BLACK HAWK SPECIAL OPS na kumuunganisha na kikosi changu. Kule alipokuwa akihudumu alikuwa jenerali peke yake lakini alishangaa kukutana na wimbi la majenerali katika kikosi changu na ndipo akaamuwa kuongeza cheo na kufikia cheo cha Prime jenerali, mafunzo yaliyochukuwa mwaka mzima. Lakini cheo cha prime jeneral hutunukiwi hivi hivi tu, ni lazima ufanye kitu cha pekee kabisa”.


“Kwa wakati huwo hakukuwa na jambo kubwa la kufanya, lakini akiwa mapunzikoni nchini Urusi alikutana jenerali Alfonce kuunda urafiki. Akiwa huko alitumia jina lake la bandia ambalo lilitambulika kipindi anahudumu katika kikosi cha Black Hawks ambalo ni Davidson. Baada ya wiki nzima kupita, urafiki wao ulikuwa mkubwa kiasi cha kuanza kumshawishi ajiunge na kikosi cha waasi kuleta mapinduzi. Baada ya jambo hilo alikuja kwangu na kunambia anataka kumalizia sehemu iliyobakiwa ili awe prime jenerali kamili kwa kuvamia kikosi cha waasi ili kukusanya taarifa muhimu kuhusu kikosi hicho”


“Nilifahamu kuwa ilikuwa ni kazi ngumu na kama baba sikuwa tayari kumpeleka mwanangu kwenye kifo chake kwa makusudi. Pia nilifahamu kabla ya kuwa baba kwa mwanangu nilikuwa baba kwa raia wote ninaowalinda hivyo sikuwa na budi zaidi ya kukubaliana nae japo iliuma sana na tulikubaliana itakuwa siri kati yetu.” Alielezea Alex. Kila mtu alishusha pumzi baada ya kumsikiliza gwiji huyo kwa makini sana, “CJ karibu kwenye kikosi kazi” aliongea Jeff na kutabasamu, “nimekaribia” CJ alijibu na kurudisha tabasamu hilo.


“Hawa jamaa tumewapata kwa kweli” aliongea Alex, “huwo unaitwa mtego ndani ya mtego mwengine ulioteguliwa” Jeff aliongezea. “Ukweli sikufikiria kama kazi ingeenda kama tulivyopanga japo tulikuwa mtoa taarifa wetu ndani ya kikosi chao” aliongea Alex na kumuangalia Janeth (Brain) ambae alikuwa kimya kwa muda kidogo.


Mwezi mmoja nyuma kabla ya kukamatwa kwa Alex na Jeff.

Wakiwa Sector Zero Ghost layer, Janeth (Brain) alionekana kufikiri kitu na kutokomea huko mawazoni. “Janeth unawaza nini” aliongea Martina, “unajuwa nilichokipanga kinaonekana kipo sawasawa kabisa bila kuwa upenyo wowote ule wa makosia” aliongea Janeth na kushusha pumzi kisha akaendelea “kuna jambo linanip wasiwasi sana, kama itawezekana naomba tufanye kikao cha dharura” alimalizia. Matina alikubaliana nae na kuandaa kikao cha dahrura.


“Janeth nenda kwenye kusudio tu, unajuwa kikao hichi kipo katikati ya kazi yetu” aliongea Alex, wengine wakatikisa vichwa kuashiria kukubaliana nae. “Sawa” aliitika na kuendelea, “nimejaribu kujifikiria mimi kama kiongozi wa waasi na hasa kuzingatia suala la silaha zitakazoniwezesha kukamilisha lengo langu. Na katika wakati huu ambao nafahamu kabisa nguvu yangu imevunjwa vya kutosha, seheu pekee ya kupata silaha ninazohitaji ni aidha serekalini au katika kambi za maadui zangu” aliongea na kuwachanganya wote walioko hapo.


“Najuwa mtakuwa na maswali lakini nitayajibu muda si mrefu” aliwatowa wasiwasi na kuendelea “munadhani ni kwanini watawakamata nyinyi wawili (Alex na Jeff), na sio wengine kama Martina, Talbot, Charlie. Ni kwasababu kufanya hivyo kutaiacha kambi uchi. Uchi nikiwa na maana kikosi kikubwa kitaondoka kambini kwenda kuwaokoa. Kufanya hivyo kutawapa wao urahisi wa kuivamia na kuichukuwa kambi hii ambayo kwa namna moja ama nyingine ndio wanaamini watapata silaha wanazozitaka. Mfano wakichukuwa mwengien yeyote isipokuwa nyie, mmoja wenu atakwenda kumrudisha aliechukuliwa na mwengine atabakia kuilinda kambi na hilo hawalitaki wao.”.


“Unajuwa hata mimi sikulifikiria hilo, na ukiangalia kwa umakini kuna uwezekano mkubwa likatokea” aliongea Jeff. “Hivyo ili kuepusha hilo umekuja na mpango gani” alihoji Alex, “mpango wetu wa awali uko pale pale na haujabadilika kitu” alijibu. “Ila kwenye swala la kuja kuwaokoa ndio mabadiliko yatakapotokea” aliendelea “nafahamu kuwa nyie wawili matosha kuiangamiza kamb nzima ya pasfiki, hivyo basi, badala ya Charlie kuja kuwasaidia yeye atafanya kama anaondoka kambini. Ila hatoondoka, katika hamsini zitakazoondoka kambini, ndege arobaini na sita zitazunguka kambi zikiw juu sana ili kuepusha kelele kusikika na ndege nne zikifutana na ndege mama zitakuja kuwachukuwa”.


“Kwasababu nina wasiwasi sana kuwa kuna watu wanatuchunguza, yeyote atakaeonekana anatanga tanga karibu na eneo la kambi huyo mali ya Charlie. Najuwa Charlie itakuuma lakini tunahitaji mtu wa kusukuma vikosi ikiwa kutatokea jambo lolote tusililolitarajia hapa kambini.” Alimaliza na kuwaangalia. Kila mtu alionekana kutafakari kwa kina juu ya kile alichokiongea mwanadada Janeth. Kwa wote kiliingia akilini lakini kwa Charlie kilimkoroga kweli kweli hasa ukizingatia alikuwa na hamu sana ya kwenda kupambana pamoja na mtu anaemkubali sana katika ulimwengu huu. Hata hivyo hakukuw na namna. Na hicho ndicho kilichotokea miezi kadhaa na kuwafanya waasi waangekie puwa.

************************************************

“Frank amerudi lakini amejeruhiwa vibaya sana” alifika mtu mmoja na kutoa taarifa kwa Alice, Alice akatoka ofisini kwake kuelekea alipo Frank. “Nilikuuliza mapema kuhusu yule kiumbe, ukanambia una uhakika hatakuwepo” aliongea kwa tabu sana alipomuona Alice. “Hilo lilikuwa kosa kubwa upande wangu na naomba unisamehe” aliongea Alice na kumuangalia Frank kwa macho ya huruma sana. “Kwa akili yao ya kawaida wasingeweza kutambuwa nilichopanga lakini inaonekana kuna mtu mwengine ukiachilia Jason CJ. Na huyo ndie alidadavuwa na kutambuwa hili” aliongea.


Wakati wakiendelea hali ya Frank ilizidi kuwa mbaya kutokana kupotoza damu nyingi sanakupitia majera aliyoyapata. “Mpelekeni maabara na mumuweke katika usingizi” aliongea Alice. Frank akabebwa na kukimbizwa maabara ambako alichomwa sindano ya usingizi iliofuatiwa na sindano nyingine iliokuwa na dawa ya kupunguza kasi ya mapigo ya moyo ili kupunguza kiasi cha damu kilichokuwa kinatoka. Baada ya maandalizi Alice nae aliekea maabara na kuanza kumfanyia opereshni za kumtoa risasi zilizokuwa mwilini mwa Frank.


Baada ya masaa mawili alifanikiwa kuziondoa risasi nyingi lakini hali ya Frank haikuimarika hata kidogo. Alipoona jitihada zake zimegonga mwamba, alitoka maabarana kuelekea chumba alichokuwa Michael. “Frank ana hali mbaya sana, nini msimamo wako” alimuuliza, “unajuwa nimefikiria sana lakini nahisi katika nlokuwa nayo sasa siwezi shinda hii vitu” hakujibu swali aliloulizwa badala yake aliongea kitu kingine. “Huu mwili wa bandia haunipatii virutubisho ninavyotaka, nahitaji mwili wa kweli na nahis mwili wa Frank utakuwa unafaa zaidi. Uingize kwenye jokofu X na uundae kwa ajili ya kuhamisha akili yangu” alimalizia Michael na kushusha pumzi.


“Lakini unafahamu kama huko nyuma tuliwahi fanya kitu kama hichi ikashidikana”, “Ndio lakini tulifanya katika miili ya maiti, huu wa sasa bado uko hai, nahitaji niuchukue kabla haujawa wa baridi. Nina uhakika wakati huu itawezekana”. “Sawa” aliitika Alice na kutoka kwenye chumba hicho na kuelekea maabara ambako alitoa maelekezo na Frank akahamishiwa kwenye jokofu maalum. Jokofu hilo likapelekwa chumbani kwa Michael ambako ni Alice peke yake ndie aliruhusiwa kuingia. Alifunga mlango na kutoa taarifa kuwa wasisumbuliwe. “Michael, natumai una uhakika na unachokifanya” aliongea Alice kionesha kuwa na wasiwasi, “usijali mpenzi wangu kila kitu kitakuwa sawa, nitakuwa na uwezo wa kuhisi, kucheka na kulia kama binaadamu wengine”alijibu Michael na kuvuta kopyuta ndogo kisha akaaza kufanya kile alichokiamini ni bora kwake.



“Lakini unafahamu kama huko nyuma tuliwahi fanya kitu kama hichi ikashidikana”, “Ndio lakini tulifanya katika miili ya maiti, huu wa sasa bado uko hai, nahitaji niuchukue kabla haujawa wa baridi. Nina uhakika wakati huu itawezekana”. “Sawa” aliitika Alice na kutoka kwenye chumba hicho na kuelekea maabara ambako alitoa maelekezo na Frank akahamishiwa kwenye jokofu maalum. Jokofu hilo likapelekwa chumbani kwa Michael ambako ni Alice peke yake ndie aliruhusiwa kuingia. Alifunga mlango na kutoa taarifa kuwa wasisumbuliwe. “Michael, natumai una uhakika na unachokifanya” aliongea Alice kionesha kuwa na wasiwasi, “usijali mpenzi wangu kila kitu kitakuwa sawa, nitakuwa na uwezo wa kuhisi, kucheka na kulia kama binaadamu wengine” alijibu Michael na kuvuta kopyuta ndogo kisha akaaza kufanya kile alichokiamini ni bora kwake.


Aliingiza nambari kadhaa mara kwa mara, tabasamu halikuacha kuonekana usoni mwake. “Uploading initiated” kompyuta ilonesha maneno hayo kwenye kioo na mstari mwekundu ukaonekana ukijaa. Baada ya hapo Michael akalala kwenye kitanda kikubwa cha chuma na kumuangalia Alice kisha akatikisa kichwa. Alice akabonyeza sehemu kikatoka kioo na kufunika kitana chote, moshi wa manjano ukaanza kutoka ndani ya kioo hicho na kusababisha aliekuwa ndani asioneka. Alice akasogeza lile jokofu alilokuwemo Frank pembeni ya kitanda ya Michael.


Akalifunguwa lile jokofu na kuvuta nyaya zilizotoka kwenye ile kompyuta ya Michael, Zilikuwa na ncha kali sana mbele. Akazichomeka katika maeneo tofauti tofauti kichwa mwa Frank. Kwa wakati huo kiyo cha kompyuta kilionesha “upload complete”. “Michael, natumai hili litafanya kazi kama ulivyokusudia, bila kuchelewa akabonyeza kitufe kwenye kompyuta. “Download initiated” kompyuta ilionesha ujumbe huwo kwenye kioo, Alice akachukuwa sindano yenye kemikali ndani na kuingiza kemikali hiyo kwenye mirija ya drip iliokuwa inapeleka dawa mwilini mwa Frank.


Saa tano zilikatika, hatuwa ya kusakinisha (download) ilikuwa imekamilika kwa asilimia tisini na tano. “Mpaka sasa kila kitu kinakwenda, hizi asilimia tano za mwisho ndio muhimu sana” alijisemea Alice na kuzidisha umakini. Mapigo ya moyo ya Frank yalianza kuongezeka kasi, asilimia tisini na saba zilikuwa zimekamilika. “Inakaribia kumalizika” alijisemea akiongeza ile kemikali kwenye mirija ya drip. Mapigo ya moyo ya Frank yalipunguwa kasi na kurudi katika hali ya kawaida. Asilimia tisini na tisa zilikuwa zimekamilika.


“Bado moja tu” alijisema Alice, ghafla mwili wa Frank ukaanza kutetemeka. Mapigo ya moyo yaliongezeka kasi mara dufu kuliko mara ya kwanza. Taa nyekundu ikaanza kuwaka na kuzima kuashiria hatari. Lakini mpaka wakati huwo Alice alipanga kukamiisha zoezi hilo chini ya hali yeyote ile, aliongeza ile kemikali japo haikusaidia sana. Baada ya mtetemeko wa dakika kama tano hivi, mwili wa Frank ulitulia na kompyuta ilizima kabisa. Mashine iliokuwa inaonesha mapigo ya moyo ilikuwa ikionesha mstari mmoja tu ulionyooka. Na hiyo ilikuwa na maana kuwa mwili wa Frank haukuwa na uhai tena.


Taratibu machozi yakaanza kumchuruzika, Alice hakuelewa afanye nini kwa wakati maana kuliko na uwezekano wa kuwapoteza wote wawili Frank na Michael. “Alice” alisikia akiitwa, lakini akadhani anasikia tu sauti akilini mwake. “Alice mbona unalia” alisikia tena sauti, lile jokofu lilifunguka na moshi mwingi ukatoka. “Frank” aliita Alice, “Michael” Frank alijibu. Ndio, hakuwa tena Frank bali alikuwa ni Michael. Alice alivuta taulo zito lililokuwa pembeni na kumpa Michael ambae kwa sasa anaonekana kama Frank kwa nje.


Nini kimefanyika mpaka Frank akawa Michael, turudi miaka kadhaa nyuma.

Michael akiwa katika ofisi yake alikuwa akichezea kompyuta yake, “hii ikifanikiwa itakuwa ugunduzi mkubwa sana, hapana! Itakuwa dawa ya kuishi milele” alijisemea na kucheka sana. Wakati huwo Michale alikuwa chini ya Matvei na ndie aliekuwa mtu wa mtandao katika kikosi hicho cha waasi kilichoongozwa na Matvei. Alikuwa akifanya uchunguzi juu ya uwezekano wa kusakinisha (dowload) akili ya mtu kwenye mashine na kuihamishia kwa mtu mwengine endapo yule mtu atakufa. Akiwa na maana anasakinish kumbukumbu na uwezo wa akili ya mtu.


Alifanikiwa kusakinisha akili yake kwenye kompyuta yake maalum, lakini kabla hajaanza majaribio alikutana na majanga na kuuwawa. Hiyo ilikuwa ni miaka mingi sana kipindi ambacho Matvei pia aliuwawa. Lakini kwasababu alifanikiwa kuhifadhi akili yake kwenye ile kompyuta, alikufa mwili tu na akili ikabaki katika ulimwengu wa wanaoishi. Na ndipo akaungana na mwanadada anaietwa Alice na kuanza majaribio ya kuhamisha akili hiyo kwenye ubongo wa tu mwengine.

*************************************************

Katika wakati ulokuwepo.

Frank alilipokea taulo kutoka Alice na kutoka kwenye lile jokofu, kisha akajifunga vizuri kiuononi. “Ni muda mrefu sana sijajisikia kama hivi” aliongea Michae na kusogea kwenye kiti na kukaa. “Karibu tena mpenzi wangu” aliongea Alice, “kweli umri umeenda Alice, ni miaka karibu thalathini na kitu. Si ndio” aliongea Michael. “Ndio Michael, japo wewe bado kijana ila mimi nazeeka tena” alijibu na kuonekana mwenye kusononeka. “Usijali Alice kila kitu kitakuwa sawa, hata hivyo tuna kazi kubwa ya kufanywa na mwili wako ulivyodhoofu hivyo itakuwa ni vigumu sana kutekeleza majukumu ipasavyo.”.


“Michael, lakini unafahamu binadamu amezliwa ili siku moja afe” aliongea Alice, “Alice mimi siamini hizo vitu, hainiingii akilini eti kwamba nimezaliwa ili kuna siku nife. Binaadamu tunatakiwa tuamuwe wenyewe tuishi kwa muda gani na pia tufe muda gani na sio jambo kama kuna kiumbe mwenye uwezo kuliko chochote kile katika ulimwengu huu. Na kwamba yeye ndie anaeamuwa tuishi kwa mfumo gani na kwa muda gani. Mimi naamini sayansi na siamini vitu vya kufikirikika kama uwepo wa Mungu, malaika na shetani sijui. Uwepo wangu hapa upo, ni kwasababu nilitakiwa kuwepo na kwasababu kuna mwingine alitaka niwepo na nitakufa siku nitakayoamuwa” alijibu kwa maelezo marefu.


Alice alihisi baridi ikimtambaa mwili mzima baada ya kusikiliza maneno hayo kutoka kwa mwanaume anaempenda kuliko wote duniani. Alitabasamu na kumkumbatia “Agh!” Michael aliguna kidogo, “si unajuwa bado nina vidonda vya risasi” aliongea Michael na kutabasamu, “nimepitiwa” alijibu Alice. Walicheka kwa pamoja na kuongea kwa muda mrefu. “Acha tuwaonyeshe nguvu ya mapinduzi, tutaiwasha dunia moto na kuwafanya wapoteane” aliongea Michael na kuachia tabasamu lililoonesha chuki ya wazi kwa walimwengu.


Sector Zero Ghost layer.

“Nahisi kwa sasa waasi hawatafanya lolote ukizingatia pigo walilopata” aliongea Alex na wote wakamuunga mkono. “Jeff unahitaji kwenda kumuona Christina maana nahisi atakuwa amekonda kwa kuwaza” aliongea Alex. “Damn! Nimesahau kuwa kesho na siku ya kuzaliwa ya Vincent” alongea Jeff na kuonesha hofu. “Sasa mbona unatoka jasho” aliuliza Alex, “ya mwaka jana sikuenda na nisipoenda ya mara hii. Amesema ataniangushia ndege kichwani kwangu” alijibu na kuwafanya wote wakacheka. “Ni muda mrefu sijamuona Vincent, tatizo nae hakai. Kila siku yuko nje ya ulimwengu huko, ndio shida ya kuwa mwanasayansi wa anga. Nawaza kama kuna siku tutakayopata watoto watakaoishi maisha kama raia wengine.” Aliongea Alex.


“Wewe hapo ulipo na miaka sitini, unategemea uzae tena. Labda ukaoe kizee mwenzako” Anita alijibu, wote wakaanguwa kicheko. Walisahau kabisa kama muda mchache uliopita walikuwa mpambanoni, na hiyo ndio ilikuwa kawaida yao. Hawakuishi kwa kujilimbikizia mawazo ya siku za nyuma, jambo likipita kwao linabakia kuwa kumbukumbu tu. Waliendelea kuongea mambo mengi na baada ya hapo walikubaliana kuwa siku itakayofuata wataondoka pamoja kwa ajili kuungana na familia ya Jeff na kusheherekea siku ya kuzaliwa ya Vincet, mtoto wa kwanza wa Jeff na mwanasayansi wa anga.


Baada ya hapo walitawanyika na kila mtu akarudi eneo lake kazi na kuendelea na majukumu yake. “Talbot, ikiwa tutakwenda vitani na hawa washenzi tutahitaji vifaa vyenye uwezo zaidi ya tulivyonavyo sasa, kuanzia silaha, mavazi na kila kitu kinachohusiana na vita. Tunahitaji kujipanga kupita maelezo” aliongea Jeff. “Usijali nilishaanza kuanda vitu vipya kabla hata hujanambia, nilielewa kutoka kwenye taarifa tulizozipata huenda vita ikawa ngumu kuliko zote tulizowahi kupigana, itatugharimu kila kitu tulichokuwa nacho mpaka roho.” Alijibu Talbot



Baada ya hapo walitawanyika na kila mtu akarudi eneo lake kazi na kuendelea na majukumu yake. “Talbot, ikiwa tutakwenda vitani na hawa washenzi tutahitaji vifaa vyenye uwezo zaidi ya tulivyonavyo sasa, kuanzia silaha, mavazi na kila kitu kinachohusiana na vita. Tunahitaji kujipanga kupita maelezo” aliongea Jeff. “Usijali nilishaanza kuanda vitu vipya kabla hata hujanambia, nilielewa kutoka kwenye taarifa tulizozipata huenda vita ikawa ngumu kuliko zote tulizowahi kupigana, itatugharimu kila kitu tulichokuwa nacho mpaka roho.” Alijibu Talbot.

*************************************************

Ndege kubwa ya shirika la Emirate iliachia ardhi ya nchi ya RDC na kupotelea angani, “jamani ee, tujitahidi kuwa kawaida. Tunakwenda kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Vincent na sio vitani” aliongea Alex na kuwaangalia wenzake. Maana wote walishasahau kuvaa sura za kawaida. Kila siku wao ni sura za kazi tu, “hakuna kubeba bastola yeyote ile zaidi ya pistol ndogo ya kawaida” aliendelea kusisitiza. Hasa alimuangalia Charlie aliekuwa amebeba bunduki yake ya udunguaji mgongoni.


“Charlie kwa heshima na taadhima hiyo mgongoni tutaiyacha nyumbani kwangu na hutakwenda nayo sehemu ya sherehe” aliendelea kuongea Alex. “Sawa, nitaiacha lakini sio kwako, bali nitaiyacha kwenye gari” alijibu Charlie. “Alex, huyo utakachomwambia hatokuelewa. Baada ya Jesca kitu pekee anachokipenda kutoka katika chemba ya moyo ni hiyo bunduki. Na hutamwambia chochote akakusikiliza” aliongea Jeff na kucheka kidogo.


Alex akashusha pumzi ndefu na kurudi kwenye kiti chake, ndiyo ndege hiyo waliikodi maalum kwa ajili ya kuwachukuwa wao tu na baadhi ya vijana wao waliokubali kuhudhuria na kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Vincent, mtoto wa kwanza wa Jeff. Wakiwa angani wengine walilala, wengine walikuwa wakiongea. Kila mtu alikuwa anafanya jambo lake analolijuwa mwenyewe. Ndege iliendelea kuchana mawingu kuelekea nchini Qatar.


Baada ya safari ndefu sana, hatimae ndege ilianza kushuka na mwishowe ikakanyaga ardhi ya Qatar. Walishuka kwenye ndege hiyo kubwa na kupitia mlango wa VIP, wakatoka nje ya uwanja ambako walikuta basi kubwa likiwasubiri. Waliingia na safari ya kuelekea kwa Alex ikaanza. Ikumbukwe kuwa Qatar ndipo Allen James alipokutana na mke wake wa pili, Tania. Waliwasili nyumbani kwa Alex, “karibuni” alitok mtu mmoja ambae kwa kumuangalia tu ana umri kati ya miaka thalathini na tano na arobaini.


“Ahsante” alijibu Alex, “Jeff” aliita Jeff. “Wajina” aliitika mtu huyo na kukumbatiana na Jeff, waliobaki wote walikuwa wamekodowa macho tu. “Inaonekana kuna mambo mengi hatuyajui kuhusu hii familia” aliongea Anitha. “Jamani musije mukatuchanganya majina, mimi naitwa Jefferson na Jeff wenu anaitwa Jeffery” aliongea Jefferson. “Jamani huyu ni mtoto wa pili wa Allen James” aliongea Alex na kuwafanya wote wazidi kushangaa. “Karibuni ndani jamani, tunatakiwa kujiandaa ili tuelekee shughulini” aliongea Jefferson Allen. Waliingia ndani kuoneshwa sehemu ya kuweka mizigo, kisha wakapelekwa kwenye chumba maalum ambacho kilikuwa na suti nyingi sana zilizokuwa zinaning’inia kwenye henga.


Na kila suti ilikuwa na jina la mtu husika, hivyo haikuwapa shida wakati wa kuchaguwa. Kila akabeba suti yake na kwenda kujiandaa, baada ya nusu saa walikutana katika sebule nyumbani hapo na kila mtu alikuwa kapendeza kweli kweli. Jefferson akafunguwa kabati na kutoa funguo kumi za gari aina ya FORD na kuwakabidhi. Wakaelekea sehemu ya kuhifadhia gari na kwasababu hawakuwa wengi sana. Gari hizo ziliwatosha. Jefferson, Jeff na Alex walipanda gari moja na wao wakawa ndio waongozaji wa msafara huwo.

*************************************************

“Mama! Hichi kibabu kiko wapi” aliongea Vincent akionekana kuwa na hasira, “Vincent nimekeambiaje kuhus kumuita babaako kibabu” alifoka Christina. “Tatizo mama unakipenda sana kibabu mpaka huoni kama kinazeeka” Vincent aliendelea. Alifahamu fika alikuwa akimuudhi mama ake lakini hakujali kabisa, “Mama, baba si atakuja” alifika vicky na kuongea. “Sijui kwakweli” alijibu Christina akishika tumbo lake kubwa. Watu wengi tayari walishahudhuria ukumbini hapo, ukiachilia kuwa na sherehe ya kuzaliwa kwa Vincent bali pia kulikuwa na jambo jingine kubwa siku hiyo.


“Halt!” wakati watu wakiendelea kupata vinywaji mbali mbali wakisubiria muda wa sherehe ufike, ikasikika sauti kali. Kila mtu aliacha alichokuwa anafanya na kuelekea ilipotokea sauti hiyo, mlangoni walikuwa watu wawili waliokuwa ndani ya suti nyeusi. Taratibu wakaanza kutembea kuingia ndani ya ukumbi huwo mkubwa. Haikuwa hao tu nyuma yao walifuata wengine wengi kiasi, walikuwa wakitembea kwa hatua zilizofanana na kufanya ukumbi mzima usike hatuwa moja kubwa kama zile za wapiga kwata.


“Vincent natumai sijakusubirisha sana” ilisikika sauti, na moja kwa moja Vincent akaitambuwa sauti hiyo. “Umenisubirisha sana, Commando” alijibu kwa nguvu, “Daddy” Vicky alipiga kelele na kukimbilia kule sauti ilipotokea, Jeff akatembea kwa mwendo wa haraka kuelekea upande aliokuwa anatokea Vicky. Vicky alipofika alirusha mikononi mwa babaake, “umekuwa mzito, bibi yako anakulisha nini” aliongea Jeff baada ya kumbeba. Christina alifuata na kumkumbatia mumewe, “taratibu bibie usije ukamuuza huyo wa tumboni” aliongea Jeff.


Jeff aliachiana na Christina na kumshusha Vicky kisha akaelekea alipo Vincent, “Heri ya siku ya kuzaliwa, Kido” aliongea. “Ahsante baba” Vincent aliitika na wakakumbatiana. “Kido, bado tu unakuwa” ikasikika sauti nyingine nzito, Vincent alichomoka mikononi mwa babaake na kutafuta sauti hiyo inatokea wap. “Heri ya siku ya kuzaliwa” Alex alitoka kwenye umati wa watu. “Anko Alex” Vincent aliongea na kumfata, wakakumbatiana. “Inaonekana una afya nzuri kijana” aliongea akimtikisa tikisa.


Baada ya kuwasili watu hao sherehe ikaanza rasmi, watu walikunywa na kula na kila alifurahi sana. Ulifika wakati wa zawaid, kabla zoezi hilo Vincent akaomba kipaza sauti. “Naombe muniazime masikio yenu” aliongea na watu wote wakamgeukia. “Ahsanteni”, “kwanza niwashukuru wote muliofika na kujumuika na familia yangu katika kuadhimisha siku hii muhimu sana kwangu, sio muhimu tu kwasababu ni siku yangu ya kuzaliwa. Laa kuna jambo jingine kubwa linaifanya siku hii iwe muhmu sana. Tarehe kama ya leo alizaliwa mtu muhimu sana, maana ya yeye kuzaliwa na mimi leo hii nisingekuwa hapa. Mama, najuwa utakuwa umesahau lakini nataka nikukumbushe kuwa leo si mimi tu niliezaliwa bali ni siku aliezaliwa babu yangu, Mzee Allen James” aliongea Vincent na Christina akajikuta akibubujikwa na machozi.


Jeff akampitisha mkono begani na kumvuta kwake kwa ajili ya kumpoza, “japo hatunae tena katika ulimwengu huu lakini ninaamini huko alipo anatuangalia na kutulinda. Ili kuadhimisha kwa ajili yake kila mtu anyanyue glasi yake juu” wote wakanyanyua. “Kwa mpendwa baba, babu na komred; heri ya siku ya kuzaliwa” aliongea na kumwaga kinywaji kilichokuwa kwenye glasi. Na wengine nao wakafanya hivyo, “humu ndani kuna mwanadada mmoja anaitwa MarryRose, MarryRose kama unanisikia naomba upite mbele” aliendelea kuongea. Binti mrembo akpenyapenya mpaka akafika mbele japo usoni kwake alionesha kuwa na aibu.


“MarryRose umekuwa na mimi kwa muda mrefu; katika shida na raha, dhiki na faraja. Mbele ya watu wote hawa kama mashuhuda. MarryRose will you marry me” aliongea na ukumbi mzima ukalipuka shangwe. Vincent akashuka alipokuwa amesimama na kuenda mpaka alipo MarryRose na kupiga magoti kisha akatoa kiboksi kidogo chekunde na kukifunguwa. Kilikuwa na pete ndani yake, MarryRose alinyoosha mkono kuashiria kukubali ombi la Vincent. Akamvisha kisha akasimama na kumbusu na kumkumbatia. Baada ya hapo akanyanyua kipaza sauti na kurudi alipokuwa amesimama awali. “Kabla hatujaendelea kusheherekea, napenda kuchukuwa nafasi hii kuwatambulisha wazazi wa MarryRose. Mr Adrian na Madam Scarlet naomba mpite mbele.” Alex na Jeff wakabaki wamepigwa na bumbuwazi kuachilia mbali Christina aliejikuta akichoka na kukaa kwenye kiti. 





“MarryRose umekuwa na mimi kwa muda mrefu; katika shida na raha, dhiki na faraja. Mbele ya watu wote hawa kama mashuhuda. MarryRose will you marry me” aliongea na ukumbi mzima ukalipuka shangwe. Vincent akashuka alipokuwa amesimama na kuenda mpaka alipo MarryRose na kupiga magoti kisha akatoa kiboksi kidogo chekunde na kukifunguwa. Kilikuwa na pete ndani yake, MarryRose alinyoosha mkono kuashiria kukubali ombi la Vincent. Akamvisha kisha akasimama na kumbusu na kumkumbatia. Baada ya hapo akanyanyua kipaza sauti na kurudi alipokuwa amesimama awali. “Kabla hatujaendelea kusheherekea, napenda kuchukuwa nafasi hii kuwatambulisha wazazi wa MarryRose. Mr Adrian na Madam Scarlet naomba mpite mbele.” Alex na Jeff wakabaki wamepigwa na bumbuwazi kuachilia mbali Christina aliejikuta akichoka na kukaa kwenye kiti.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog