Simulizi : La Ultima Letra
Sehemu Ya Kwanza (1)
Katika wiki ambayo Taifa zima la Mexico likiwa limeingia katika hofu kuu kutokana na wafungwa 130 ambao wanatambuliwa na serikali kama "watu hatari kupindukia" (extremely dangerous) wakiwa wametoroka kutoka kwenye gereza lenye ulinzi mkali la Matamoros katika mji wa Tamaulipas, ndipo papo hapo ambapo pia Mwendesha mashitaka wa serikali Bw.Ricardo Castillo anapokea simu kutoka kwa askari waliopo eneo la Nuevo Laredo wakimtaarifu juu ya tukio lingine la kuogofya ambalo kwa hakika lazima nalo litalitumbukiza zaidi nchi ya Mexico katika hofu kuu.
Polisi walimtaarifu Bw. Castillo kuwa asubuhi hiyo wananchi wamekuta miili ya watu 9 ambayo kati yao wanne wakiwa wanawake ikiwa imening'inizwa darajani pasipo uhai.
Kitu cha kuogofya zaidi miili hii ilining'inizwa bila vichwa kuwepo katika viwili wili vyake. Pia miili ilikuwa imetobolewa tumboni pamoja na kukatwa katwa mabegani kiasi cha mifupa kutokeza nje.
Pia miili ya maiti hizo za wanaume ilikuwa imenyofolewa sehemu za siri.
Castillo akawauliza polisi kama kulikuwa na kitu chochote eneo la tukio kinachowawezesha kung'amua watekelezaji wa tukio hilo na polisi wakamjibu kuwa kuna ujumbe wa maandishi yameandikwa kwa damu katika kuta za daraja.
Kabla polisi hawajamueleza Kikichoandikwa kwenye kuta za daraja, Castillo anapigiwa simu nyingine na kamanda wa polisi kutoka eneo la Monterrey kumuarifu kuwa usiku wa kuamkia siku ya leo katika klabu maarufu ya usiku ya mjini hapo imevamiwa na watu 52 wameuawa kikatili.
Kamanda huyo wa polisi akaendelea kumueleza zaidi kwamba mauaji hayo ni ya kutisha na kuogofya kwani miili yote hiyo 52 imekutwa ikiwa imefungwa kamba mikononi na yote haina vichwa.
Castillo akakumbwa na mshituko na kuishiwa nguvu na akamuuliza kamanda wa polisi kama kulikuwa na chochote zaidi eneo la tukio, na kamanda wa polisi akamjibu kuwa kulikuwa na maandishi ukutani ndani ya klabu yameandikwa na damu. Lakini pamoja na hilo miili yote ilikuwa imechorwa kwa kisu kifuani herufi 'Z'.
Castillo akapigwa na bumbuwazi zaidi akakata simu akimuahidi kamanda wa polisi kuwa anampigia baada ya dakika chache.
Baada tu kukata simu Castillo akapiga simu kwa afisa wa kwanza wa polisi aliyeko Nuevo Laredo ambaye alimpigia simu ya kwanza.
Baada ya afisa huyo wa polisi kupokea simu akamuuliza haraka kwamba ukiachikia mbali maandishi yaliyoandikwa kwa damu kwenye kuta za daraja je kulikuwa na kitu kingine chochote kwenye miili ya maiti hizo. Afisa wa polisi akamjibu "ndio maiti zote zimechorwa kwa kisu kifuani herufi 'Z'"
Castillo akashikwa na hofu kubwa na mshangao na akamjibu kwa kifupi tu afisa huyo wa polisi "Niko njiani nakuja, nadhani nimeshafahamu waliotekeleza tukio", afisa wa polisi akamuuliza "ni nani?" castillo akamjibu kwa ufupi.. "Los Zetas
C:\Users\Tanga\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image003.jpg
zzzz 1.jpg
Moja ya maeneo ya tukio ambapo wapinzani wa Gulf Cartel waliuwawa kwa ukatili wa kutisha na kukatwa katwa kila kiuongo mahali pake.
1999: Tamaulipas, Mexico
Bw. Cardenas Guillen, miezi michache baada ya kukabidhiwa uongozi wa genge la mihadarati la Gulf Cartel lengo la kwanza alilo jiwekea ilikuwa ni kutwaa tena upya maeneo yao ya kibiashara katika miji yote ambayo hapo zamani yakikuwa chini ya himaya yao lakini wakapokonywa na genge la Sinaloa Cartel.
Ili kufanikisha azma hii Cardenas aling'amua wazi kuwa inahitaji kikosi maalumu cha Ulinzi kwa ajili ya kulinda viongozi wa genge lake, kulinda 'biashara' yao pamoja kusambaratisha mawakala wote wa Sinaloa Cartel katika miji ambayo atailenga.
Ni hapo ambapo aliwasiliana na Ruben Salinas Luteni mstaafu wa kitengo maalumu cha Operation za weledi wa hali ya juu cha Jeshi la Mexico kilichoitwa GAFE (Grupo Aeromovil de Feurzas Especiales).
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment