Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (6)
Sehemu Ya Kwanza (1)
IMEANDIKWA NA : ZUBERI MARUMA
********************************************************************************
Simulizi : Kiapo Cha Mfungwa (6)
Sehemu Ya Kwanza (1)
Gambi hakuwa na uhai tena!
Laizar Nyoshi akaangua kicheko akausogelea mwili ule na kuukanyagia kanyagia chini kwa dharau.....
Ghafla mwili ule ukafumbua macho!
"Mamaaaaaa"
Laizar aka achia ukelele na ghafla akafumbua macho yake, naaam kumbe alikuwa ndani ya ndoto nzito
Ndoto mbaya!
Kufumbua kwake macho akapokewa na mlio wa simu yake ya mezani ambayo akujua ilianza kuita sangapi au muda gani!....
Mwili ukimlowa jasho
Akajiamsha na kupeleka mkono wake kushika mkonga wa simu ile akaupeleka sikioni!
"Kamishna wa jeshi la polisi Brown Stanley atunaye tena duniani"
"Whaaaaat!"
Laizar Nyoshi akuamini kile akisikiacho,kizungu zungu kikali kikamkamata akujua ni sa ngapi aliuachia mkonga ule na kwenda chini!
Fahamu zikamtoka!
Kishindo kile ndicho kilichomshtua mke wake alokuwa bado kalala
***
TANZANIA
KATIKATI YA USIKU!
Gari la kifahari ambalo ndani alikwepo Isack Lilizidi Kukata Mbuga Kuelekea Ndani Ya Msitu Ule,ni baada ya kufanikiwa kumpeleka Zidu Na Katarina Katika hosptali ya kcmc kwa matibabu alikuwa na uhakika ni lazima angekufa tu hali zao zilikuwa mbaya,kama si kwa Mpango Wa Mungu basi angemuulia palepale hosptalini kwa siri sana,
Usiku Ule walipiga kaz sana kijeshi mpaka panakaribia kupambazuka walifanikiwa Kuipata hazina hiyo!,wakaifadhi kwa mmoja wao waliyemwamin kila mmoja akarudi eneo lake la kazi...
Asbui wakati Isack aliporudi kwake,akipata chai na mkewe Mery Na Mtoto Wao ghafla simu yake ikaita kucheki namba niya nje ya nchi akapokea,ilikuwa ni namba ya Mh Rais Laizar Nyoshi alikuwa akimuulizia Zidu,
Isack akashikwa na kigugumizi,
"ndi..ndi..o ila yupo katika hali mbaya icu"
Laizar akishtuka,
"eti Nini?!" Anakumbuka Laizar aliuliza kwa amaniko naye kwa taratibu alimjibu
"ndio mh yeye pamoja na mkewe katarina"
"mbona amkunijulisha?!"
Isack alikumbuka hakuwa na jibu la kumpa,na ghafla kwa unyonge mh rais alisema "ooh shit tumekwisha"
Ni Wazi Rais alikuwa amechanganyikiwa,
'bila shaka anaitaji kumtumia kumwangamiza Gambi pole rais bila shaka muda huu anavuta pumzi zake za mwisho,Isack aliwaza akifurahia moyon mwake!
***
Rais Laizar japo aliongezewa ulinzi lakin akuwa na aman hata chembe,kila muda alikuwa akiwaza,ghafla akapata wazo,akashika simu yake na kupiga namba kadhaa akaweka simu masikioni...
"ubalozi wa kinte nchini Tanzania,mh Rais hapa naongea na baloz Mosweti Kaiguruki?!"
"ndio mh raisi unaongea na balozi wako Mosweti Kaiguruki!"
"vizur,unataharifa Kwamba Zidu Yupo Tanzania,naomba Mfanye Utaratibu leo hii hii muda huu huu asafirishwe india katika hospital kubwa juu chin atibiwe"
"sawa muheshimiwa Rais"
"jambo Ilo lifanyike haraka sana muda huu apakiwe katika ndege yeye na mkewe ok?"
"sawa muheshimiwa"
Raisi akakata simu,muda ule ule baada ya Raisi kukata simu balozi akawasiliana na hosptal kubwa Iliyopo Nchini India Kutoa taharifa,akaanzakushughulikia usafiri,akawasiliana Na hosptal ya rufaa kcmc,akapata na madaktar watakao msindikize,
Zidu Na Mkewe Wakasafirishwa, kwa nje Isack alionekana kufurahia ila moyon alikuwa na machungu kusafirishwa kwa Zidu Na Isack Kwake alikuwa jambo jema,ila aliapa kutumia vijana wake kuakikisha Zidu anauwawa huko huko india kuendelea kupumua kwa mtu yule kwake alikuwa jambo zuri!
Akashika Simu Yake Na Kupiga Namba Kadhaa,
"Rajey Khan Kuna Kazi Mumbai Hosptal kuna picha nakutumia akikisha unamuua kuna milioni miambili!"
Rajey Khan Muhindi Katili,akaduwaa Ni Kazi Nyingi alishafanya na Isack Ila akulipwa pesa nyingi kiasi kile,aliishia kulipwa milion tano mpaka saba,ila si kwa milion miambili,akaahidi kuifanya kazi hiyo siku hiyo hiyo!
***
INDIA
UWANJA WA NDEGE WA INDIA
Baada ya ndege ilo mbeba Zidu Katili Na Mkewe Katarina Kushuka Chini Ya Ardhi ya uwanja wa ndege haraka sana madaktari walisaidiana kumwingiza katika ambulance,ikatoka kwa spidi kuelekea Mumbai Hosptal,kijana Wa Kazi Rajey akiwa juu ya pikipiki yake aliifatilia kwa nyuma ile ambulance,hakuna alomtilia hofu,wengi wa wakazi wa Mumbai Walikuwa bize na mambo yao,wakafika hosptal Zidu Na Mkewe Wakashushwa Wakapakiwa Katika Machela Wakaingizwa Icu tayar kwa operesheni,kijana wa kazi akucheza mbali,kufatilia akitafuta mazingira sahihi ya kukamilisha kazi yake!
Baada Ya Masaa Kadhaa taa za icu zikawaka kuonesha opereshen imekamilika,madaktari wakatoka,
"vipi dokta mgonjwa!" Baloz Akaoji,
"opereshen Imefanikiwa Sasa Wanapelekwa Wodin Unaruhusiwa Kwenda Kumuona!"
'muda Wa Kazi Sasa'
Rajey akawaza,alishajua wodi ambayo Zidu alilazwa,akasubiri baloti katoka,naye akajikongoja kuelekea,pistor ikiwa kibindoni,akaufungua mlango akaingiza kichwa kuchungulia mkono wake ukiwa ndan ya mfuko wa surual yake tayar kuchomoa bastola...
Bado Mr X (Isack) anamuandama Zidu Kwa Siri lengo ni kumuua,kikiwa ni kiapo cha damu alichowah kula utotoni wakati Zidu alipokuwa akimtesa,na kutaka kumuua,
Zidu kwa msaada wa Rais Laizar Nyoshi anasafirishwa India Kwa matibaba pasina kujua 'Mr x' Isack naye anatuma mtu kwa siri hosptalin akimpa ela ya kutosha...
Na sasa Ragiv ndo anaingia wodi aliyelala Zidu Mkono Ukiwa Umeshika Silaha Mfukoni,je Nin Kitaendelea...
songa sasa kujua kitakachoendelea
Kitendo tu cha kuchungulia ndani mapigo ya moyo yakadunda,lengo la kutoa silaha akalisitisha
Kitandani Pale alikwepo nesi alokuwa akimchoma sindano,Ragiv akanywea ila kwa kuwa alikuwa kashaingiza kichwa chake,akukuwa na haja ya kutoingia akaingia tu kama rafiki yake,na mgonjwa alolala kitandani
"nesi mgonjwa wangu anaendeleaje?!"
"anaendelea tu vizuri kaka ndo kama unavyo muona si kama alivyokuja!"
Alipomtupia Jicho Zidu alilala kitandani japo alikuwa bado akihemea hewa ya oxygen lakini hali yake ilibadilika sana,
'milion miambil ni fedha nyingi sana na nilazima nizipate...'
Ghafla akapata wazo,amtumie yuleyule nesi kumuulia mtu yule 'nikimpa ela ya maana,atamuua kwa sumu na kitaalamu tofauti na mimi kumpiga bastola hali ya kuwa huyu ni shujaa wa taifa lake'
Kufkiria wazo lile akatabasasamu, akageuza shingo yake kumwangalia nesi yule,
"tunaweza kuzungumza privet nesi na mazungungumzo na wewe!"
Nesi yule akashtuka,'privet tena?!' ila akajua pengine mchizi kamzimikia,na kwa jinsi jamaa yule alivyo kwanza handsome boy,pili alionekana ni mtu mwenye fedha zake,
"privet kuna tatizo gani kaka?!" akajifanya kuuliza wasiwasi ukionekana kumvaa,Ragiv aliuona wasiwas ule,ikabidi amtoe wasiwas
"usijal dada,ni mazungumzo ya kawaida tu..."
"ok chukua namba zangu untafute jion kwanzia saa kumi ndo namaliza zamu!"
Rajiv akaandika hizo namba alipo maliza akaaga na kutoka,
'sijui ndo naenda kumsalititi mpz wangu Omykant ' Wazo hilo likapita katika kichwa chake,
Kwa Kuwa Yeye alidondokea tumbo,kwa mara nyingine tena mimba yake Katarina Iliharibika,yeye alisafishwa tumbo,akuwa na matatizo mengi,akarejewa na fahamu,ila bado alikuwa na dripu za maji ya lochanganywa na dawa ya kumwongezea nguvu,aliposhtuka tu akakumbuka simu alopigiwa na wifi yake Mery Na Kuambiwa Juu Ya Kupoteza Maisha Kwa Mume Wake,wakati Huo Yeye alikuwa hosptalin na akujua kama walishasafirishwa na sasa yupo nchini india...
Machozi yakaanza kutiririka,akawa akilitaja jina la mume wake Zidu,kwa bahati nzuri daktari hakuwa mbali,haraka akasogea katika kitanda chake akaanza kumpima mapigo ya moyo,kiasi cha joto,presure...
"usijal mumeo anaendelea vizuri,ukipata nguvu utaweza kwenda kumuona"
Daktar Kwa Sauti Ndogo Ya Kusihi Yenye Lengo La Kumwondosha Katika Wasiwasi akazungumza,Katarina akashtuka...
"ina maana mume wangu yupo hai?"
Akamuuliza yule daktari kwa mshangao,akuamini eti,daktari yule akamtoa wasiwasi wote akimwambia wazi mumewe yupo hai na anaendelea vizuri japo ajapata fahamu bado ila wanategemea muda wowote anaweza pata fahamu,Katarina akahema kutua mzigo aloubeba moyoni mwake simanzi ikamtoka,ila simanzi ile ilirejea alipokumbuka tumbo lake,alipojicheki kwa sasa tumbo lilikuwa flati,
'mtoto Wangu,mtoto Wangu Yupo Wapi?!'
Akapayuka,daktari Yule akimwangalia kwa huruma,akamjuza wazi alipodondoka aliangukia tumbo na mimba kuaribika kwa maelezo aliyoyapewa na kuyasoma katika file aliloletwa nalo,ivo alisafishwa tumbo,simanzi,majonzi Na Kilio Kikarejea Palepale,alitaman Kuitwa mama...
kwa mara nyingine tena mimba yake ilienda kuharibika...
***
Ilikuwa Ni hoteli ya kifahari,hotel yenye nyota kadhaa,amnishi kapoor binti wa kihindi na nesi katika hosptal kubwa ya Mumbai akuwahi kuwa na fikra hata kudhani kwamba ipo siku angeingia na kukaa katika hotel ile,achia mbali kula,ila leo hii ameingia...
Mbele yake alikuwa kijana mtanashati,aliyopo ndani ya suti ilo mkaa vyema,Ragiv kumar,baada ya kukaribishana na kimya cha muda baina yao Ragiv akaeleza kusudi la ombi lake,
"kwanza Samahani Kama Ntakuwa Nakukwaza dada yangu..."
Ragiv akaanza kwa kumtaka radhi,Amnish kapoor akujal sana akamtoa wasiwas kiukwel alijikuta tu akivutiwa nae,macho yake pekee yakaanza kuzungumza 'mh sitamwambia na mpz namwambia nipo singo ila ntamwambia anipe muda nimfikirie ni kijana mzuri,nikimkubali mapema ataniona malaya,atanihis wa bei rahisi,wazo hilo likapita katika kichwa chake,Kumbe Rajiv Yeye alikuwa na jambo jingine kabisa hata siyo ilo la kumtongoza!,akaendelea kumsikiliza...
"moja kwa moja nielekee katika point hasa la kukuita wewe hapa,kwanza angalizo naomba tuzungumzacho ikiwa utakubali au utakataa ibaki siri na ikiwa itavuja sitosita kukuua!...
Amnish akashtuka,kuna kuuana tena,wazo lake la kutongozwa haraka likayeyuka sura ya jamaa yule ya uhandsome boy ikajifuta katika ubongo wake,ikajileta upande wa pili kuwa aliyopo mbele yake ni mtu katili,jeuri,lengo la kumuita pale sasa ni nini,taratibu wasiwas ukaanza kumvaa
...ikiwa utakubali ombi langu ntabadilisha maisha yako,kwa kiasi kikubwa cha pesa ntakachokupa,pili na kuhaidi kukulinda milion amsin ndo mshahara wako,na naweza kukupa milion 20 kama advance ya kaz hiyo,mtu yule akatoa cheki akamuandikia fedha ile akamkabidhi...mrembo yule huku mikono ikitetemeka akaogopa kuipokea cheki ile,
"hapana nambie kwanza ni kazi gani hiyo utakayo niifanye!"
"vizuri,swali zuri naitaj ufanye chochote yule mtu kule hosptal afe kwa siri au kwa dhahiri,ufanye mwenyewe au tushirikiane!"
"mtu! mtu gani?"
"yule ndugu yangu"
Ragiv akajibu pasina kupepesa macho...
"mhmh sitoweza,hapana tafuta mwingine mimi hapana napenda kaz yangu,hapana kwa kwel,kwaheri!"
Kama Kachanganyikiwa dada yule aliongea maneno mengi akanyanyuka ila kabla ajaondoka Rajiv Akamkumbusha...
"hiki Nlichokwambia Iwe Siri kikivuja sitosita kukuua"
"sawa kaka yangu sitosema kwa mtu!"
Akaondoka!
Ragiv Pale Kwenye Kiti Wala akutingishika ni 'profesion' wa hizi kazi,ndo kwanza akaachia tabasamu la dhihaka...
'nimekuchagua wewe utaifanya tu hii kaz ngoja...'
Akanyanyuka,alishapata Wazo Jingine...
MAMBO YANAENDA KUWA MOTO KK APATA FAHAMU WAKAT HUO KIDUME RAGIV KINAPANIA KUMTUMIA NESI AMNISH KAPOOR KUIFANYA KAZI YA KUMUUA ZIDU ATAFANIKIWA?,
Ragiv pale kwenye kiti wala akutingishika ni profision wa hizi kazi ndo kwanza akaachia tabasamu la dhihaka
'nimekuchagua wewe utaifanya tu hii kazi ngoja...'
akanyanyuka,alishapata wazo jingine,
Ilikuwa Ni Lazima amfatilie yule dada,kujua mahali anapoishi,kwa muda ule akatoka,akazurura zurura,jioni alikuwa maeneo yale ya Mumbai Hosptal,na gari yake,na bahati ilikuwa upande wake,
Kabla ajashuka katika gari yake alishughudia yule nesi akitoka akaingia ndani ya gari flani,gari ile ikaondoka ilipopita pale alipo alishughudia dereva alikuwa ni mwanaume,akupata kutambua ni mpz wake au mumewe ila aliamua kumfatilia,
gari alopanda yule nesi ilielekea mpaka katika nyumba moja ilokuwa na geti wakapiga honi geti likafunguliwa gari ikaingia Ndani,
Ragiv Yeye alinyoosha na kwenda kusimama mbele,
'bila shaka hapa ni nyumbani kwake na yule alokuja kumchukua ni mume wake kumbe anamaisha mazuri sana huyu mtu'
Wazo hilo likapita katika kichwa chake,macho yake yakiwa katika said mirrow ya gari lake akitazama getini ghafla alishughudia geti dogo likifunguliwa na binti si chini ya miaka 18 akitoka,akawa akija kule upande wake,kwa sura alifanana na yule nesi hakuwa na shaka ni mtoto wake,Rajiv akatabasamu!...
Alishapata wazo ambalo kwake lilikuwa na faida kubwa sana,akashusha kioo chini...
"binti samahan naomba nikuulize kitu?"
Kitendo tu cha yule binti kusogea,ghafla akafungua mlango na kumvutia ndani,akaliondoa gari kwa kasi...
***
Hali Ya Katarina Sasa Ilikuwa Nzuri,aliketi Pembeni Ya Kitanda alicholala mumeme akutaka kwenda mbali naye,
Moyoni Mwake alimpenda sana Zidu na akujua ni nani aliyetaka kumuua,bado alikuwa na maswali mengi sana,
Hali Ya Zidu aikuwa mbaya sana naye taratibu matumaini ya kuwa vizuri yakaanza kurejea!,
Madaktari Walimwangalia Kwa Ukaribu,Rais Moreti alimuhitaji zaidi ya kitu chochote!...
Sekunde,dakika,hatimaye masaa Yakakatika Pasina Queen Kurejea Nyumbani,wazazi Wake Nesi Shree Na Mumewe Ajay Wakaanza Kuingiwa Na Wasiwasi,mtoto Wao atakuwa wapi walipojaribu kupiga simu yake aikupatikana,wazo lililokuwa katika vichwa vyao ni kuelekea kituoni ila kabla awajaenda simu ya shree ikaita kuangalia ni namba ya mtoto wake,haraka sana akapokea...
"Queen uko wapi tunakutafuta umeenda wapi wewe?"
Shree akahoji kwa wasiwasi upande wa pili ukajibu...
"ili kumwokoa mwanao huna budi kufanya kama nilivyokwambia,iwe siri yako kitendo cha kuijulisha polisi au mtu yeyote yule utampoteza mwanao
Baada ya maneno yale simu ile ikakata,nesi Shree alionekana wazi kuchanganyikiwa,akamweleza mumewe ambaye naye alimshahuri tu kuifanya hiyo kazi kuyanusuru maisha ya mwanaye huyo wa pekee! tena akampa wazo jinsi ya kuifanya hiyo kazi!,mumewe Ajay naye alikuwa ni daktari lakini katika hosptal ingine...
Ile dawa ambayo Zidu alikuwa akichomwa Ajay akatafuta kichupa kama kile ambacho alitia sumu ambayo ingemuua Zidu Kidogo Kidogo,ambapo Angekuwa Akimchoma Akampatia!...
Badae Rajiv alipiga tena kwa kutumia simu ya queen kujua wazaz wameamua nin,shree akajieleza,ragiv alifrah akahaid kuto mdhuru ila atamwachia huru pale tu Zidu atakapokufa...
Siku hiyo mume ajay na mke shree awakulala kwa raha mawazo juu ya mtoto wao,asb Nesi Shree alichukua ile dawa na kuitia katika begi lake,akaelekea zake kazini...
Asb Zidu tayari alishachomwa ivyo nesi shree ilipaswa aendelee kumchoma mchana na usiku,ambapo zidu lazima angefia usingizini,na ingesemekana amekufa kwa shinikizo la damu!...
Masaa Yakasonga hatimaye muda wa kwenda kumchoma Zidu Sindano Ukawadia...
Mwanadada Shree Akabeba Sinia Lake Lenye Pamba Sindano Na Vichupa Vya Dawa,akaelekea Mpaka Ilipo Wodi Alolazwa Zidu 'vip Room' akafungua mlango nusu aangushe sinia lake,kwani akutegemea kumkuta mtu kule ndani!
Katarina aliuona ule mshangao wa nesi,ila akapotezea, wakasalimiana, nesi akaweka zile dawa katika kimeza,
"naomba nafasi dada nimchome mgonjwa sindano"
Nesi Shree akaomba,Katarina akujali akosogea pale kwenye kitanda wakati huo nesi yule alikuwa akivuta dawa katika kichupa kile kwenda kwenye bomba la sindano!...
Macho Ya Katarina Yakatua Kwenye Kichupa Kile Cha Dawa,ambapo Nesi alizidi nyonya dawa ya kutosha akarudisha mezani na kumsogelea mgonjwa akamfunga mpira,akautafuta mshipa alipouona akaanza kuvuta bomba amchome...
"stooop!"
Ghafla akashtuliwa na sauti ya Katarina!,akageuza Shingo Kumwangalia
"nini?!"
"namashaka na hiko kichupa cha dawa,kile cha kawaida kilikuwa nusu iko kimejaa sijui inakuwaje na dawa ni dozi"
Katarina akauliza huku akisimama,na kusogea lile eneo kilipo kitanda cha mumewe mkononi akiwa kashika kile kichupa cha dawa alichokitoa pale mezani!
Nesi Shree akapigwa na butwaa,akutegemea kuulizwa swali kama lile,katarina alimcheki kwa macho makali tena ya hasira,ukumbuke katarina alipitia udaktar tena wa magonjwa ya akili,kumsoma mtu kwake ni rahisi,akafunua kile kichupa na kukinusa akakunja sura
"hii si poison?!"
akamkwida shingo,kwa ukali akamuuliza
"ni nani kakutuma umuue mume wangu"
Akaanza Mnyonga
"utanieleza Ukwel" Kk akaongea kwa ukali ila ghafla dada akatoa mguno wa maumivu mwil wake ukanyong'onyea kumwangalia vizuri damu katika nguo yake akamwachia kwa mshangao,
Nesi alipigwa risasi kwa mgongoni,katarina aliangaza macho kila upande ila palikuwa patupu,palepale akamgeukia nesi yule alokuwa bado akigugumia maumivu
"nnan alokut.."
akuweza kumalizia kauli yake palepale nesi akakata roho...
Katarina Akuamini...
Ragiv Kaamua Kumuua Nesi Shree Kupoteza Ushahidi,je Atafanikiwa Kumuua Zidu?! Je Nin Kitaendelea
ITAENDELEA
Simulizi : Kiapo Cha Mfungwa (6)
Sehemu Ya Pili (2)
Katarina anapata nafuu na kubeba dhima ya kumsaidia mume wake,siku hiyo anaitilia shaka dawa nesi shree anayotaka kumchoma anamzuia na kuinusa ile dawa anagundua ni sumu palepale anam'bana nesi yule aeleze ni nan alomtuma amuue mume wake lakin kabla ajamjibu kwa mgongon nesi anapigwa risasi na mtu asiye julikana,katarina anazidi changanyakiwa,tusonge sasa kujua kitakachoendele..
Rajiv akutaka kuwa mbali na eneo lile,kufatilia kila kitu kitakachoendelea,siku hiyo wakati sasa Shree akijiandaa kumchoma sindano Zidu,katarina akaingilia,Ragiv kila kitu alikishughudia...
Alipo ona nesi yule anabanwa zaidi,akachomoa bastola yake akachomeka kifaa cha kuzuia sauti,akabinjua kidogo kioo na kuachia risasi kadhaa ile anageuka kukimbia akapamiana na daktar,akampiga push na kuelekea panapo lift akaingia na kushuka chini,
Katarina akushangaa sana pale akauruka ule mwili hatua ya kwanza ya pili mlangoni nje akamshughudia mtu akimpushi dokta,hakuwa na muda wa kusubiri akaanza kukimbia kuelekea kunapo ngazi,akipania kuizuia njiani lift ili apande katika kituo cha chini,alishuka kwa kasi sana,
Muda huo yule daktari alicho moa simu haraka haraka na kupiga simu getini kuzuia mtu yoyote asitoke wala kuingia alipokata tu akapiga polisi...
Katarina alichechelewa ili lifti,ikamfikisha mwanaume chini akatoka akaingia ndani ya gari lake alipaswa atoke pale hosptal akajipange upya...
Ile anaondoka tu Katarina Naye Ndo akafika chini,aliangaza macho yake kumtafuta mtu yule alompush daktari sura yake aikuwa ngeni kwake mara kadhaa anakumbuka yule jamaa alikuwa akiingia na kumwangalia mumewe akisema ni rafiki yake na mara kibao mtu yule alikuwa akikaa pale nje,hali ilo mfanya Katarina Mapema tu kumtilia shaka mtu yule...
Katarina kwa hatua ndefu akazidi kupiga hatua kuelea getini,
Ragiv K' Katu akujua juu ya kuzuiwa kutoka kwa mtu yoyote nje ya hosptal wala kuingia kwa mtu yeyote tofauti na maaskar...
Kufika Karibia Na Getini Akakutana Na Foleni Ya Magari Akafanya Kosa La Kushuka Akajue Mbele Kuna Nini,katarina Naye taratibu akawa akiwasili eneo lile na kwa bahati nzuri akamwona akitoka katika gari yake,akaikazia macho ile gari kuna vitu akaviandika katika simu yake akaachana nayo,sasa akazidi kupiga hatua na kuzidi kumfikia mtu yule...
Ragiv Kabla ajafika getini,akahisi kuguswa nyuma kitendo tu cha kugeuka akapokelewa na ngumi nzito ilo mfanya akapepesuka akiona nyotanyota,mbele yake alikwepo mwanamke hatari ambaye akupata bahati ya kupata historia yake,watu haraka wakawazunguka kushughudia pigano lile la mtoto wa kike na mwanaume...
Wakati Wale Wakiendelea Kupigana Daktari Aliwasili,na Kuwanong'oneza Walinzi Kwamba Jamaa Ndiye yule anayepigana,palepale Ragiv akawekwa chini ya ulinzi,muda huo huo maaskar wakawasili na kumchukua akatoe maelezo...
ulinzi wa Zidu Ukaongezeka Mara Dufu Baada Ya kugundulika kuna watu wanayetaka kumuua,ila kitu kilicho muumiza Katarina Ni Kwa Nini Mume Wake Anawindwa,na Wanao Mwinda Lengo Lao Hasa Nini?
Katu akujua kikulacho kinguoni mwako,yule alojidai kumfariji,kumtia moyo Isack Ndo Chanzo cha yote yale,kikiwa ni kiapo cha damu alichowekeana agano kipindi iko akiwa mtoto,kwa mateso Zidu alompa,mara kadhaa alimpiga risasi,akuishia hapo alishamlaza na njaa na hata kusubutu kumtupia katika kisima chake cha mamba,kama ningekufa je,siwez msamehe wallah atailipa damu yangu...
Isack akazidi kuwaza baada ya kupata taharifa ya kukamatwa kwa kijana wake,muda ule ule akashika simu alijua alipopaswa kupiga,akapiga...
"kuna kijana angu,anashikiliwa na vijana wako naomba aachiwe!"
"nani mkuu?"
Isack akatoa maelezo...
"unajua itakuwa hatari kwa kuwa kesi yake inatangazwa sana na vyombo vya habari akitoka itapaswa ijulikane katokaje"
"andaa mpango wowote hata kama amekufa kijana awe mtahani naitaji uhuru wake zaidi ya kitu chochote mkuu nsaidie"
"ok,mr x kwa heshima yako ntalifanyia kazi ila yapaswa akitoka awe katika maficho"
Isack Akacheka "usijal Mkuu Kwanza Duniani Wawil Wawil ataonekana anafanana tu fanya ivyo mkuu naingiza chochote kwenye akaunt yako ya benk ya dunia"
Mtu Yule alo onekana kuwa ngazi za juu jeshini kama si waziri akakata simu,akapiga magereza alofungwa vijay,kuna mtu akaongea naye maneno kadhaa,akiomba wakutane,
Wakakutana Wakajadili Watu Wale Wawili Wakakubaliana,mzee Yule alokuwa ndiyo mkuu wa magereza baada ya kupewa maelekezo naye akaondoka...
Akaenda Kuwaita Vijana Kadhaa Ofisin Kwake Wakiongozwa Na Insp Amrishbabi alokuwa akiisimamia kesi ya yule mtu na makoplo wake kadhaa walokuwa nyuma yake...
"kutoka ngazi za juu yapaswa yule mfungwa aliyeua hosptalin aachiwe huru"
Vijana Wale Wakiongozwa Na Amrish Wakashtuka,kivipi Sasa Na Kesi Ile Inavyofatiliwa Na Waandishi?'
Mzee Yule Kwa Kuwa alijua ilo swali lazima vijana wake wale wangejiuliza akawapa 'mchongo' mzima sasa ulivyo...
"tutamruhusu mfungwa mmoja aondoke kwa kutoroka lakin na wakati akitoroka atapigwa risasi na kuuliwa mbali sura yake itaaribiwa na hatimaye tutatangaza Rajiv alikuwa anatoroka tukamuwah wakat tunatupiana risasi ndo tukamuua,hapo kijana tutamuachia huru kuna mtu anamwitaj kwa kaz zake!...
Na Ndivyo Ilivyokuwa...
Mfungwa Mwingi ne Usiku akatolewa akaambiwa kimbia akalimwa risasi,sura yake ikaharibiwa,usiku ule ule Ragiv akaruhusiwa,habari za kuuwawa kwa Ragiv Baada Ya Kutaka Kutoroka Zikazagaa Katika Vyombo Vya habari...
"HARAKA SANA ONDOKA HAPO UNAPOISHI NUNUA NYUMBA MPYA,KINGINE NIMEKUPA NAFASI YA PILI NA YA MWISHO ZIDU AFE SIJUI UTAFANYA NINI AWAMU HII UKISHINDWA UNAKUFA WEWE!"
Isack akampa maelekezo!...
Ragiv baada ya kukata simu sasa ubongo wake ukawa unachemka ni njia ipi aitumie kummalizia mbali Zidu,ambaye Kwa Sasa alikuwa na ufahamu,anakaa,anaongea...
Kazi Ilizidi kuwa Ngumu Zaidi...
Ila ghafla akatabasamu baada ya kupata wazo!
'kesho ndo mwisho wako ZIDU'
Akawaza akiendelea kutabasamu...
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment