Search This Blog

Saturday, 24 December 2022

ULIMWENGU MZIMA KIGANJANI MWA CIA - 3

   http://pseudepigraphas.blogspot.com/2020/06/ulimwengu-mzima-kiganjani-mwa-cia.html

Simulizi :  Ulimwengu Mzima Kiganjani Mwa CIA

Sehemu Ya Tatu (3)


Baada ya uchaguzi mkuu wa Marekani wa November mwaka 1960, raisi Jonh F. Kennedy alishinda uraisi, hivyo Rais Eisenhower ambae alikuwa akiratibu uvamizi wa Cuba akasimamisha mipango kwakuwa hakuwa na nguvu tena ya kisheria ya kuinjinia uvamizi wa nchini Cuba, hivyo Raisi Eisenhower alimualika Rais Kennedy aliyechaguliwa katika uchaguzi wa mwaka huo katika Ikulu ya White House tarehe 6 Desemba, mwaka 1960, na tarehe 19 Januari, mwaka 1961 ili kumshawishi atakapoingia ikulu aendelee na mpango huo ambao mtangulizi wake alikuwa ameuanzisha, katika moja ya mazungumzo yao, Eisenhower alimwelez Kennedy kuwa toka mwezi Machi, mwaka 1960, serikali ya Marekani ilikuwa inatoa "mafunzo kwa vikundi vidogo vidogo lakini hatujafanya kitu chochote" kwasababu bado sija approve uvamizi, alimueleza pia Kennedy kuwa "baadhi ya mamia ya asikali ambao ni wakimbizi" wako huko Guatemala, na "wachache wako huko Panama, na baadhi jijini Florida."


Kama nilivyo elezea huko nyuma kuwa mara tu baada ya Fidel Castro kuchukua madaraka mwaka 1959, mwaka uliofuata yaani mwaka 1960, CIA kwa ruhusa ya Rais Dwight Eisenhower ambaye alikuwa anakaribia kuondoka madarakani walianzisha mikakati ya namna gani watamuondoa madarakani Fidel Castro, Fursa kuu waliyoitumia ulikuwa ni kutumia wahamiaji walioingia Marekani kutoka Cuba kukimbia utawala wa Fidel Castro uliokuwa "unafanya usafi" dhidi ya raia waliokuwa wanamuunga mkono Fulgencio Batista, Kwa hiyo CIA wakakusanya mamia ya raia hawa kwa siri kubwa na kuwapandikizia hari na ushaiwshi wa kutaka kumpindua Fidel Castro.


Mwezi March mwaka 1960 rais Dwight Eisenhower alipitisha bajeti ya dola milioni 13.1 kwa ajili ya mpango huu wa mapinduzi, Raia hawa wa Cuba waliokimbilia uhamishoni nchini Marekani ambao walifahika kama kikosi cha Brigade 2506, wakaanza mafunzo ya kijeshi kwa mwaka mzima nchini Guatemala, Mpango huu wa kuivamia Cuba na kumpindua Fidel Castro ulipangwa ufanyike mapema mwaka 1961 na ulikuwa umekamilika kila kitu lakini raisi Eisenhower hakuupa 'approval' na aliacha jukumu hilo la kuidhinisha uvamizi huo ifanywe na atakaye kuja kumrithi yaani Rais JF Kennedy.


Kwa hiyo mara baada ya uchaguzi mkuu mwezi November, 1960 na hatimaye JF Kennedy kuapishwa January 20 mwaka 1961, kitu cha kwanza ambacho alikabiliana nacho ni CIA kumkabidhi mkakati ulioandaliwa na wao CIA chini ya Rais Dwight Eisenhower kuhusu uvamizi wa Cuba na kumpindua Fidel Castro, hivyo mwezi February tarehe 13, mwaka huo, mpango wenye sura nzima ya utekelezaji operesheni hiyo ulitua mezani kwa Rais Kennedy.


Awali ni kwamba CIA walipowasilisha mkakati wao wa mapinduzi ya Fidel Castro kuna vitu vingi vya msingi walimficha Kennedy hii ni kwasababu Kennedy hakuonesha kuunga mkomo mpango huo toka alipotaalifiwa na maafisa usalama wa Marekani na hats Raisi Eisenhower walipokutana kwa mara ya kwanza ikulu december 10, 1960, hili ndio lilopelekea hata CIA kutompatia taarifa zote Kennedy kwakuwa waliona angekwamisha mpango huo, hivyo wakaamumu kumptatia taarifa chache, Na hii inaonekana kwamba walichukua 'advantage' kwa sababu ya ugeni wa Kennedy katika wadhifa wake huu upya wa Urais na kwa hiyo kutofahamu uhalisia wa vitu vingi kwa hiyo CIA wakatumia hiyo fursa 'kum-mislead' katika vitu muhimu kuhusu mkakati huo.


Mkakati ulikuwa ni mpana sana, lakini kwa ufupi ni kwamba, wavamizi hawa wa Brigade 2506 ilikuwa imepangwa wavamie Cuba wakitokea Guatemala na Nicaragua wakiwa na askari wa miguu pekee, Kennedy hakutaka Marekani ionekane ikihusika moja kwa moja kwenye uvamizi huo ili kulinda taswira yake katika jamii ya kimataifa na pia kuepuka kuamsha hasira za Urusi ambao walikuwa ni mshirika mkubwa wa Cuba, kwahiyo kukabiliana na hili, CIA walipendekeza kuwatumia makomando wake wa SAD, ntakuelezea kidogo kuhusu hawa SAD ni wakina nani?


SAD ni nini hasa?...


SAD ni kitengo malumu ndani ya shirika la CIA ambalo wao hufanya shughuri maalumu na zenye unyeti wa maswala muhimu, hivyo idara hii ni maalumu ndani ya shrika la CIA, ambayo hujulikana kama "Special Activities Division"


Watu wengi huzani kuwa CIA ndio kufanya shuguri zote za kijasusi, lakini ukweli ambao wengi hawauelezi ni kuwa umahiri na upekee wa wa shirika la CIA hufanywa na kikosi maalumu cha kipekee kwa ajili ya kazi nyeti maalumu na kazi hizo husamiwa na maafisa wa Idara ya SAD ndani ya CIA.


Upekee wa SAD ndani ya CIA ni nini?...


Kutokana kuongezeka kwa changamoto za kimataifa , ambazo nyingine zinatishia usalama au maslahi ya Marekani lakini marekani haiwezi kuchukua hatua zozote kutokana kujiepusha na lawama kutoka jamii ya kimataifa ndipo hapo ikaonekana kuna umuhimu wa kuwa na kitengo maalumu kwa ajili ya suala hili.


Ndipo hapa ambapo serikali ya marekani ikaagiza shirika la kijasusi la CIA kuanzisha kitengo maalumu ndani yake ambacho kitakuwa na maafisa (wanajeshi) ambao wanaweza kutekeleza oparesheni yoyote ya kijeshi kwa kujitegemea pasipo kuhusisha serikali ya marekani.


CIA wakaanzisha idara maalumu ndani yake na kuuita Special Activities Division au kwa kifupi SAD ambayo idara yenyewe ilikuwa na maafisa wa siri ambao hawabebi vitambulisho na majina yao ni siri kubwa hayawezi kupatikana hata kwenye orodha ya maafisa wa CIA.


Lengo kubwa la kuanzishwa kwa idara hii ni kutekeleza oparesheni maalumu za kijeshi au proaganda na iikitokea wakakamatwa au kushitukiwa basi serikali ya marekani wanawakana kuwa si maafisa wao (Plausible deniability).


Kwahiyo kitengo hiki kilikuwa kinafanya kazi kwa niaba ya serikali ya Marekani lakini kulikuwa hakuna uwezekano wowote wa adui kuunganisha uhusika wa kikosi hiki na serkali ya marekani.


Ndani ya Idara hii ya SAD kuna vitengo viwili;.......


Kitengo cha kwanza kinaitwa Political Action Group, kitengo hiki kazi yake kubwa ni kufanya ushawishi wa kisiasa (political influence), oparesheni za kisaikolojia (psychological operations) na vita za kiuchumi (Economic Warfares), Pia kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, kitengo hiki kimeongezewa jukumu la vita za kimtandao (cyberwarfares).


Tuchukulie kwa mfano, katika nchi fulani kuna serikali au mwenendo wa serikalin uatishia maslahi ya Marekani basi kitengo hiki kinaingia kwa siri kubwa na kufanya mojawapo ya mambo ambayo nimeyaorodhesha hapo juu.


Moja ya matukio ambayo kitengo hiki kimehusika sana na CIA wamekiri kwenye nyaraka zilizowekwa wazi mwaka 2004 ilikuwa ni kueneza propaganda ambayo ilichangia kupinduliwa kwa Rais wa Iran mwaka 1953, Pia kitengo hiki kilitumika kuzuia chama cha kikomunisti cha Italia kushinda uchaguzi mwaka 1960.


Pia kitengo hiki kimewahi kufanya oparesheni ya siri iliyoitwa Operation Mockingbird katika taifa la marekani, Oparesheni hii ilikuwa na lengo la 'kucontrol' habari zinazoandikwa na Vyombo vya habari nchini humo, Oparesheni hii imekuja kupingwa vikali siku za karibuni na baraza la seneti kwa kuwa sheria hairuhusi CIA kufanya oparesheni yeyote ndani ya ardhi ya marekani.


Kitengo cha Pili kinaitwa Special Operations Group (SAG) na kazi yake ni kama ifuatavyo......


Kitengo hiki kinajumuisha wanajeshi wenye weledi wa hali ya juu kutekeleza malengo ya kivita pasipo kujulikana uhusika wa serikali ya marekani, Ili kulinda utambulisho wao, wanajeshi wa kikosi hiki maalumu hawavai sare za jeshi wala kubeba vitambulisho, Inasemekana kuwa hiki ndio kikosi maalumu cha oparesheni za kijeshi chenye usiri mkubwa nchini marekani.


Maafisa wa kitengo hiki wanapatikanaje?...


Maafisa wote wanaojiunga katika kitengo hiki maalumu cha SAD wanachaguliwa kutoka katika vikosi vingine vya weledi vya jeshi la marekani mfano Army Rangers, Combat controllers, Delta Force, 24 th STS, US Army Special Forces, SEALs, Force Recon n.k.


Wakishakuchaguliwa wanapelekwa katika kituo maalumu cha mafunzo ya CIA kilichopo Virginia kinachojulikana kama Camp Peary (au maarufu kama 'The Farm') ambapo miezi 18 ya kwanza wanafundisha kuhusu intelijensia na ushushushu.


Baada ya miezi 18 hiyo wanapelekwa kwenye kituo kingine cha CIA kilichopo California ambacho kinajulikana kama 'The Point', Hapa wanafundishwa mafunzo ya hali ya juu ya kijeshi ambayo hayapatikani kwa kiwango hicho katika vikosi vingine vya marekani.


Mfano wanafundishwa; mapigano ya ana kwa ana ya kiwango cha juu zaidi (special hand to hand combat), kutumia karibia aina zote za silaha na milipuko ya jeshi la marekani na nchi za kigeni, ufuatiliajj adui (tracking), Kukabiliana na hali ngumu kwenye mamzingira ya kawaida na nyikani ( extreme survival and wilderness train ing), Kumkwepa aduia, kuzuia adui na kutoroka adui (evasion, Resistance and escape - SERE) na pamoja na mafunzo hayo anaongezewa kozi maalumu ya kutambua fiziolojia ya binadamu (Udaktari).


Afisa ambaye anafuzu mafunzo haya anakabidhiwa katika idara ya SAD ndani ya CIA na anatambulika kama "Afisa Mwenye Mbinu Maalumu" (Specialized Skills Officer), Katika oparesheni zao maafisa hawa huwa wanazitekeleza katika vikundi vya watu wachache sana wasiozidi sita na oparesheni nyingine zinatekelezwa na Afisa mmoja pekee.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog